Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 354 | 355 | (Page 356) | 357 | 358 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
   Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
   : Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
   Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha  Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
  Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa  Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi hiyo. Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo.

  0 0

  Asasi ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na mbegu zake imeadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.

  Maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya ‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo biashara.
  picha 1
  Afisa ufundi wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima kuhusu mbinu bora za uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
  Wakulima wakimsikiliza Mtaalamu wa masuala ya mbolea na viuatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi. Baby Nkossa wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viuatilifu kwenye mazao
  Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa  wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
  picha3
  Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi, akisiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Giliard Daniel katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
  picha 6
  Shamba mfano lililotumika kuwafundishia wakulima siku hiyo.

  0 0

  Mr. Elihuruma Ngowi has joined Serengeti Breweries Ltd. as Brand Manager with a profound experience in Customer Care, Marketing and Sales after having spent over eight (8) years at Vodacom Tanzania Ltd.

  At Vodacom, he worked in various departments from Customer Care to Marketing and finally with Sales & Distribution Department where he held key positions, most notably as Product Marketing Manager, Devices & Alternative Channels Manager and Franchise Operations Manager respectively. He is also the Vice President and co-founder of CIBN Tanzania Ltd.

  Mr. Ngowi holds a Bachelor of Business Administration (Marketing) degree from the University of the Western Cape, Cape Town, South Africa. He also expects to graduate his master’s degree in International Business (Investment in Emerging markets) from the University of Dar es Salaam Business School later this year.

  He is a strong believer on strong performance. He believes that one has to over deliver and outshines their performance. He also believes that people have to network with the right people, have a positive pride on your performance and be able to sell your results, successes and achievements and celebrate. Always treat people with high integrity and honesty and learn to hold courageous discussions. Spiritual powers should not be forgotten. Remember to say your prayers at all times.

  0 0

  Legendary Music-Tanzania is taking this opportunity to thank everybody from the Artists, media, other stakeholders to the Fans for a massive wonderful support that was showed on the event BEAUTY AND MUSIC NIGHT.We have had a very successful event the past weekend and its all due to your support. We thank you indeed, and please keep supporting LMEP
  Best regards.
  0 0

  1 
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi Kamishna wa Polisi wa Namibia Bw.Schalk Meuwesen ofisini kwake jana.Kamishna huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tatu akiwa na maafisa wengine kutoka Namibia kujifunza jinsi Jeshi la Polisi Tanzania lilivyofanikiwa katika kutekeleza Maboresho yake.
  2 
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki akimfafanulia namna maboresho ya Polisi yalivyoanza Kamishna wa Polisi wa Namibia Bw.Schalk Meuwesen ofisini kwake jana.Kamishna huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tatu akiwa na maafisa wengine kutoka Namibia kujifunza jinsi Jeshi la Polisi Tanzania lilivyofanikiwa katika kutekeleza Maboresho yake.
  3 
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki akiwafafanulia namna maboresho ya Polisi yalivyoanza Makamishna wa Polisi kutoka Jeshi la Polisi la nchini Namibia Bw.Schalk Meuwesen na Bw.Abed Kashihakumwa ofisini kwake jana.makamishna hao pamoja maafisa wengine wapo nchini kwa ziara ya siku tatu kujifunza jinsi Jeshi la Polisi Tanzania lilivyofanikiwa katika kutekeleza Maboresho yake.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi).

  0 0


  MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel  Sitta amewahakikishia Watu wenye Ulemavu nchini kuwa wanatendewa haki katika Katiba Mpya itakayopatikana.

  Mhe. Sitta ameyasema hayo leo Septemba Mosi, 2014 katika mkutano wake na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) ambalo lilikuja katika Bunge Maalum kwa lengo la kuwasilisha hoja zenye msisitizo kuhusu haki za watu wenye ulemavu katika mchakato Katiba Mpya.

  Mhe. Sitta amesema kuwa kazi wanayoifanya ya kuyapokea makundi mbalimbali Bungeni hapo haina lengo la kuja na hoja mpya  na kuziwasilisha katika Bunge hilo, bali ni mawasiliano ya kawaida yanayohusu safari kutoka Rasimu Mpya ya Katiba mpaka kufikia katika Katiba Mpya inayopendekezwa ipatikane.

  “Jambo lolote lililoandikwa na binadamu halikosi kasoro, katika Rasimu hii ya Katiba tumegundua inayomapungufu kadha wa kadha, kuna baadhi ya maoni ambayo hayakuzingatiwa ndiyo maana tunayafanyia kazi ili yawemo katika Katiba Mpya itakayopatikana,”.alisema Mhe. Sitta.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Inclusive Development Promoters and Consultants kutoka  Dar es Salaam, Bw. Kaganzi Rutachwamagyo ambaye pia ni mwanachama wa Shirikisho hilo,amesema kuwa Kikosi cha Ushauri kuhusu masuala ya watu wenye Ulemavu kimeweka kipaumbele cha msisitizo wao ambao unajielekeza katika hoja za kuongeza masuala ya mambo ya Muungano ambapo wamependekeza kuwa kwenye orodha ya Mambo ya Muungano kuongezewe suala moja zaidi la Nane kwa mujibu wa Rasimu ya Pili ya Katiba ambalo ni uratibu wa masuala ya haki, usawa na fursa na uwajibikaji kwa watu wenye ulemavu kama jambo la Muungano.

  Bw. Rutachwamagyo  ameongeza kuwa hoja nyingine ya msisitizo inahusiana na suala la uanzishwaji wa chombo cha uratibu wa haki, usawa wa fursa na uwajibikaji wa haki za watu wenye ulemavu ambayo hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 33 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu na Mkataba mwenza wa nyongeza iliyoridhiwa kwa pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amesema kuwa wanataka chombo hiko kijulikane kama Tume ya Kitaifa Juu ya Haki, Usawa wa Fursa na Uwajibikaji kwa Watu wenye Ulemavu.

  Aidha, Bw. Rutachwamagyo  amegusia pia juu ya hoja nyingine inayohusu suala la Uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwenye Bunge la Tanzania, Baraza la Wawakilishi, Mabaraza ya Madiwani utamkwe na Katiba na ukokotolewe kwa misingi ya asilimia badala ya kuweka idadi mahsusi. “Mathalani, tunapendekeza kifungu 113 kisomeke kuwa asilimia 5% ya Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakuwa ni watu wenye ulemavu wakiwakilisha kundi hili na watapatikana kwa kuchaguliwa na wahusika wenyewe,” alisema .

  Aliongeza kuongeza kwa kuzitaja hoja nyingine ikiwemo suala la matumizi ya lugha sanifu kwa muktadha wa watu wenye ulemavu na amesema kuwa kuna hali ya matumizi ya misamiati na islahi ambazo zinakinzana na dhana za walemavu kimataifa hivyo ni vema kukawa na tafsiri sahihi ya majina kwa watu hao ili kuepuka kukinzana huko, aidha amegusia pia suala la Hifadhi ya jamii huku akifafanua kuwa wadau wenye ulemavu nchini wanadai kuwepo kwa ibara maalum ndani ya Katiba inayoelekeza masharti ya upatikanaji wa hifadhi ya jamii kwa watu wenye Ulemavu ikiwa ni pamoja na kulipwa gharama ama kupewa unafuu ya kupunguza makali ya walemavu kwa mujibu wa ibara ya 28 ya Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu ya 2006.

  Akiongea kwa niaba ya watu wenye ulemavu, Mhe. Amon Mpanjo ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo amemuomba Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuunga mkono sio kupokea maoni mapya, bali kuyaboresha yale yaliyokwisha wasilishwa hapo awali. “Tukuombe Mwenyekiti ulisisitizie Bunge letu Maalum la Katiba liweze kuzingatia haki za watu wenye Ulemavu ili nao wapate kuwa na maisha bora,” alisema Mpanjo.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Bi. Amina Mollel amesisitiza juu ya hitaji la wanawake la hamsini kwa hamsini na kati ya hizo, asilimia 5% wawe ni wabunge walemavu na ameitaka Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa kutoa nafasi nyingi za uongozi  kada mbalimbali kwa walemavu. “Hii iwe chachu katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapewa nafasi kwa uwezo walionao na sio kubaguliwa,” alisema Amina.

  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
  01/09/2014.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Usuluishi na Ushauri wa Sheria (katikati) akisisitiza jambo kwa wanahabari alipokuwa akitoa tamko kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka. Kushoto ni Mwanasheria wa Tamwa, Loyce Gondwe na kulia ni Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba. Mkuu wa Kitengo cha Usuluishi na Ushauri wa Sheria (katikati) akisisitiza jambo kwa wanahabari alipokuwa akitoa tamko kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka. Kushoto ni Mwanasheria wa Tamwa, Loyce Gondwe na kulia ni Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba. Mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa TAMWA wakisoma tamko lao juu ya umuhimu wa jamii kuwajali watoto. Mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa TAMWA wakisoma tamko lao juu ya umuhimu wa jamii kuwajali watoto.Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba (wa kwanza kulia) akizungumza katika semina kwa baadhi ya wanahabari juu ya uandishi wa habari za kuwatetea watoto.  Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba (wa kwanza kulia) akizungumza katika semina kwa baadhi ya wanahabari juu ya uandishi wa habari za kuwatetea watoto. 


   CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimeitaka Serikali na jamii kwa ujumla kuwekeza katika kumuandaa mtoto kwani licha ya kuwa zawadi kubwa, watoto pia ni tumaini na uhai wa taifa kuendelea. 
   
  Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka katika taarifa iliyosomwa kwa wanahabari jijini Dar es Salaam kuhamasisha jamii kwa ujumla kuwajali watoto hasa kwenye mchakato unaoendelea hivi sasa wa uundaji wa Katiba Mpya. TAMWA ilisema mabadiliko ya sera za siasa na uchumi kwa kiasi kikubwa yameathiri namna taasisi za kijadi na kidini zinavyofanya kazi na kujikuta zikijiondoa kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwasaidia pamoja na kuwalinda watoto.

   "...Leo hii mzigo mkubwa wa malezi umeachiwa Serikali kwa kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na ile ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Ajira na Kazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, taasisi za kidini, asasi zisizo za Kiserikali, Televisheni, sinema, wasanii na hata majambazi nao wanalea watoto," ilisema taarifa hiyo. Alisema kwa sasa Wizara nyingi zinaamini hazihusiki na watoto hivyo kujikuta sera na sheria zao nyingi kuwasahau watoto. 

  Alisema suala la watoto ni mtambuka hivyo kula kila sababu ya kufanya mabadiliko yoyote ya sera na sheria kuwa na manufaa zaidi kwa watoto hasa katika kipindi hichi cha mabadiliko ya katiba. Aliongeza kuwa suala la malezi ya mtoto ni jukumu la kila mmoja na sio kuwaachia baadhi ya watu tena wawalee watoto hao wanavyojua wao kwa maslahi yao pekee. Watoto ni zawadi kubwa na tumaini la taifa kuendelea hivyo kuna kila sababu ya kuwekeza katika kundi hilo. 

   "...Tujipange ili tusiendelee kudharauliwa kuwa hatuna uwezo wa kuwapenda na kuwalea kwa ajili ya ufukara. Ni dhabi kusikia kuwa umemchoma moto mtoto kwa kuiba shilingi mia kwa ufukara. Au wengine kunajisi watoto wadogo kwa kisingizio kuwa ufukara ndio umekusababisha utende hayo. Tunasema huo ni zaidi ya unyama...tuache kuvumilia aina yoyote ya ukatili unaowafanya watoto wakose furaha, upendo na matumaini," alisema katika taarifa yake. 

  Mkurugenzi huyo wa TAMWA alisema zamani enzi za bibi na babu taasisi za jamii zilisaidia kumtayarisha kijana juu ya nmna ya kuishi na watu, majirani, wenzi wake huku suala la malezi ya watoto likiwa ni jukumu la jamii nzima jambo ambalo kwa sasa limekoma baada ya kuingia utandawazi. Alibainisha kuwa kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza katika dhana nzima ya malizi kwa watoto hatuwezi kurudia kama ilivyokuwa enzi za mabibi na mababu bali inaweza kutumika falsafa zao na kujikuta tunaendelea kuendesha maisha yetu kwa sasa. 

  Alisema ipo haja ya kuchambua jinsi gani shule na hata malezi ya nje ya shule yanavyoweza kuwa pahala pa kunoa na kumpiga msasa mtoto ili afikie umri wa miaka 18 awe amehitimu, anaheshimu haki zake na za wengine, aweze pia kuishi kwa kujitegemea na kutumia elimu na ujuzi alioupata kwa faida ya jamii. Hata hivyo aliitaka jamii kuunga mkono juhudi zote chanya zinazowekwa ili kujenga mazingira mazuri ya kumfanya mtoto aweze kuishi kwa amani, furaha, upendo na matumaini. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0


  0 0

  Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Leonard Ishengoma akisoma hotuba ya ufunguzi (kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara, Eliakim Maswi) wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, juu ya mpango kazi wa mazingira wa sekta za nishati na madini, Septemba 1, 2014.
  Afisa Misitu Mkuu kutoka Kitengo cha Mazingira – Wizara ya Nishati na Madini, Theodory Silinge akisisitiza jambo wakati wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza.
  Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Gideon Kasege akizungumza na Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, Septemba 1, 2014 jijini Mwanza, wakati wa semina ya mafunzo kwa wanamazingira hao.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiraia ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km70.9) huku akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA, Ndugu Kuniaki Amatsu kulia huku Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km 70.9) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine 
   Taaswira ya mkeka mpya kutoka Dodoma hadi Fufu wa Kilomita 70.9 aliouzindua Rais Kikwete
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakimtazama Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero walipokuwa wakipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Fufu(Kilomita 70.9)
   Waziri wa zamani wa Ujenzi Mzee Job Lusinde akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa rasmi wa barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya Dodoma-Fufu (Kilomita 70.9) huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge wakishuhudia tukio hilo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli  pamoja na viongozi wengine wakitaifa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma-Iringa sehemu ya Dodoma- Fufu Kilomita 70.9. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini –Wizara ya Ujenzi

  0 0

  Tunaleta  camera aina kama hizi Sony pd175,nikon na canon na nyinginezo kwa special order,pia vitu kama lens,flash,charger,batteries etc.Pia tunaleta used plotter's,used cd printer's etc,kwa mawasiliano waweza piga number hii 0767410763 ama kwa email macamaca97@outlook.com.
    

  0 0

  WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWELI KUTOKA USA, @AK CLASSIC COSMETICS  WAMEWASHUSHIA TENA MZIGO MUPYAA KABISA!! 

  KAMA KAWAIDA BIDHAA ZOOOTE  KUANZIA PRODUCTs ZA KUONDOA MICHIRIZI, MAKE UPS,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI ,MAFUTA YA KUKUZA NA KUJAZA NYWELE (T444Z) NA INGIZO JIPYA JAMAICAN BLACK CASTROL OIL(JBCO) ,BODY SHAPERs,..NA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..
  KWA MAELEZO YA KINA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE BLOGUNI
  www.akclassic.blogspot.com.

   KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.
  WAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.

  PIA UNAWEZA KUWAFOLLOW INSTAGRAM @ak_classic_cosmetics

  KARIBUNI SANA.
  0 0

  1 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wenye nyumba 150, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)
  2 
  Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wengine wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Nehemia Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wenye nyumba 150, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye.4Majengo ya Nyumba za Makazi za Medeli Mjini Dodoma kama yanavyoonekana pichani.5 
  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji huku Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene wakishuhudia wakati wa ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma. Mradi una jumla ya nyumba 150. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)6 
  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Bulla Boma wakati wa ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma.7 
  Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mara baada ya ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma.

  0 0

  1384142_505866609511143_1668869613_n
  Awin Williams Akpomiemie.

  MY PEOPLE FIRST OF ALL, I WOULD LIKE TO EXPRESS MY HEART BY TELLING THE GENERAL PUBLIC AND THE FANS OF DIAMOND PLATNUMZ, THAT WE FROM BRITTS EVENTS MANAGEMENT IS VERY SORRY FOR WHAT HAPPENED LAST NIGHT, DURING THE CONCERT OF DIAMOND PLATNUMZ. IT WAS NEVER PLANNED FOR THE CONCERT TO BE DELAYED OR FOR THE ARTIST NOT TO PERFORM. 

  HERE I WOULD TELL YOU ALL THE TRUTH OF WHAT REALLY HAPPENED ABOUT THIS EVENT FOR YOU ALL TO KNOW THE TRUTH.

  THE PROJECT OF DIAMOND CONCERT WAS A VERY EXPENSIVE PROJECT,
  BECAUSE THE BRITTS EVENTS MANAGEMENT WANTED EVERYTHING TO BE PROFESSIONAL, AS A COMPANY WE DECIDED TO LOOK OUT FOR INVESTORS WHO WOULD INVEST IN THIS PROJECT, THEN WE APPROACHED THREE INVESTORS WHO INVESTED BUT ONE OF THEM DID’NT INVEST TOO MUCH AS HE SAID HE WONT BE IN THE COUNTRY.

  THE TWO INVESTORS ARE WELL KNOWN PEOPLE LIVING IN STUTTGART
  ONE WORK WITH THE USA MILITARY THE SECOND ONE OWNS A SHIPPING COMPANY IN STUTTGART, THESE WERE THE TWO MAJOR INVESTORS THAT WE GOT, WE GAVE THEM A CONTRACT TO SIGN AND ONE OF THEM SIGNED BUT THE SHIPPING GUY REFUSE TO SIGN THE CONTRACT OF THE PROJECT THAT HE WANTS TO HAVE A PRIVATE CONTRACT WITH THE USA GUY, THEN I TOLD MR.USA THAT WAS A WRONG MOVE BUT MR.USA SAID BRITTS DO NOT WORRY,ALL WILL BE FINE, 

  MY PEOPLE THE PROJECT STARTED AND THEN THE TWO INVESTORS THEN NOTICE THAT DIAMOND IS A BIG ARTIST AND HE WOULD PULL LOTS OF CROWD AND PEOPLE LOVE HIM, THEN THEY TEAMED UP AGAINST BRITTS WHO INVITED THEM AS INVESTORS ON THIS CONCERT AND WANTED TO TAKE THE PROJECT AWAY FROM BRITTS BECAUSE THEY ARE THE ONE WHO BRINGS PART OF THE MONEY FOR THIS PROJECT WHILE BRITTS IS THE ONE WHO OWNS THE ARTIST AND THE PROJECT,.

  JUST BECAUSE BRITTS IS A NEW COMPANY IN STUTTGART MR. SHIPPING GUY DECIDED TO TEAM UP WITH THE USA GUY AND DJ -WANTED, TO TAKE OVER THE PROJECT, WHEN BRITTS SITS DOWN AND HOLD MEETINGS WITH THEM, THEY WOULD DO THEIR OWN MEETING AND THEN,CHANGE ALL THE PLANS BEHIND BRITTS MANAGEMENT, SO THEY WERE OPPRESSING AND PUSHING THE PROJECT BEHIND BRITTS.


  , BRITTS HAVE AGREEMENT WITH THEM THAT WHEN THE ARTIST ARRIVE GERMANY THEY WOULD GIVE HIM THE BLANCE OF 3.250 EUROS, AND THEY AGREED TO THIS TERM BECAUSE DIAMOND MADE IT CLEAR THAT WITHOUT THE MONEY HE WOULD NOT FLY, THEY ASKED ME TO TALK TO DIAMOND THAT THEY WOULD GIVE HIM THE MONEY RIGHT AT THE AIRPORT, BUT DO YOU KNOW WHAT? BEFORE DIAMOND ARRIVED, MR.USA AND MR.SHIPPING GUY TOGETHER WITH DJ WANTED, ARRANGED FOR THUGS TO STEAL THE ARTIST FROM BRITTS EVENTS BUT BRITTS WAS SMARTER AND TOOK AWAY THE ARTIST BEFORE THEY COULD MAKE ANY MOVE, THAT WAS WHERE THE TROUBLE STARTED FROM, IN ESSEN BEFORE BRITTS ARRIVED THERE, USA GUY AND SHIPPING GUY ,ALREADY BRING IN NEW WORKERS AND
  SECURITY TO TAKE OVER THE SHOW, AND DROVE AWAY THE ORIGINAL WORKERS .
  THEN BRITTS WAS FIGHTING WITH THEM THAT THEY ARE JUST INVESTORS AND NOT THE COMPANY MANAGER, WHY DO YOU WANT TO STEAL THE EVENT BECAUSE YOU WANT TO MAKE MONEY AND NOT CARING ABOUT THE PEOPLE, BRITTS THEN NOTICE THAT THE WORKERS THEY BROUGHT WERE THEIR EX-GIRL FRIENDS AND RELATIVES.
  10649568_792593844095765_1264697582686012878_n
  THE REASON WHY THEY DID THIS WAS TO STEAL THE MONEY AND NOT TO FOLLOW THE CONTRACT WITH BRITTS, SO WHEN DIAMOND ARRIVED STUTTGART LATE NIGHT AT 11.PM, HE WAS NOT TOO FINE BUT THE TWO INVESTORS DO NOT CARE.
  THEY WERE ONLY THINKING ABOUT HOW THEY WOULD GET THEIR MONEY BACK,DIAMOND SAID HE NEEDS HIS MONEY BUT SHIPPING GUY REFUSE USA GUY TO GIVE DIAMOND THE MONEY , THINKING THAT BRITTS EVENTS WANTS EXTRA MONEY .
  THEN WHEN IT WAS ALREADY TOO LATE THEY MANAGED TO BRING OUT 3.000 EUROS THEN IT WAS 3.30AM ALREADY , BUT DIAMOND REFUSED TO STILL PERFORM BECAUSE HE SAID THEY MUST GIVE HIM HIS BLANCE OF 250 EUROS , WHICH IS RIGHT CAUSE THAT WAS THE AGREEMENT.
  BY THE TIME MR SHIPPING GUY AND MR USA GUY REALISED THAT BRITTS WAS DOING THE RIGHT THING BY ASKING THEM TO PAY UP THE MONEY TO DIAMOND IT WAS ALREADY TOO LATE CAUSE PEOPLE HAVE STARTED FIGHTING,WHILE DIAMOND WAS RIGHT INSIDE THE CAR IN FRONT OF THE VENUE,IF I LET HIM OUT THEY WOULD KILL HIM, AS WE ARE TALKING RIGHT NOW, MR. USA SAID THE MONEY WE MADE FROM THE WHOLE EVENT WAS STOLEN BY THE PEOPLE, SO BRITTS EVENTS CAN’T GET MONEY FROM THE EVENT WE ORGANISED AND OWNED .
  THESE WHERE THEIR PLANS TO TAKE OVER ANOTHER MANS BUSINESS DUE TO GREED.

  BRITTS EVENTS LOVE YOU GUYS, BRITTS EVENTS WANTED EVERYONE TO BE HAPPY, BRITTS EVENT HAVE NEVER PROMISED ANY ARTIST AND THE ARTIST DID’NT COME,.
  AND TRUST ME WHEN WE DID BRACKET EVENT WE HAD THE SAME EXPERIENCE THE SAME THING FROM THE INVESTORS , AS SOON AS THEY SEE THAT THE EVENT WOULD BE A SUCCESS THEY STARTED ASKING FOR 50% OF THE COMPANY.
  WELL AM NOT SUPPOSE TO SAY ALL THESE HERE AS ITS A MANAGEMENT ISSUE,BUT I DECIDED TO CLEAR THE AIR I CAN’T KEEP IT ANY MORE , WE HAVE LOTS OF GREEDY AFRICANS OUT THERE WHO WANTS TO TAKE AWAY PEOPLES BUSINESS JUST BECAUSE OF GREED.

  OUR AIM IS TO MAKE YOU ALL HAPPY, NOT TO WASTE YOUR TIME AND MONEY , WE KNOW THAT YOU ALL CAME FROM FAR PLACES, LEFT YOUR KIDS AND FAMILY . BRITTS EVENTS MANAGEMENT IS REALLY VERY SORRY ABOUT THIS.
  SO DO NOT BLAME THIS ON BRITTS EVENTS BUT BLAME IT ON THE GREED OF MR USA GUY AND MR. SHIPPING GUY. WE LOVE YOU AND WE PROMISE YOU A FREE SHOW EVENT WITH DIAMOND VERY SOON…. JUST LOOK OUT.

  0 0
 • 09/02/14--00:55: Taarifa ya Msiba
 • ‎Familia ya Kairuki inasikitika kutangaza kifo cha Bibi Ma Angelina Kairuki kilichotokea usiku wa kuamkia jumanne tarehe 2 Septemba 2014 katika Hospitali ya Kairuki. 

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Mama Kairuki Mikocheni, Dar es salaam.

   Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na Marafiki wote wanaohusika na Msiba huo popote pale walipo.

  0 0

  IMG_9800Fr. Shao wa kanisa la Katoliki Balktimore anayeongoza Parokia hiyo pamoja na misa za Kiswahili DMV akiwa na Padre anayechukua nafasi yake Fr.Honest Munishi Jumapili katika ibada maalum ya kumwaga Padre Shao iliyofanyika huko Baltimore Maryland, Fr.Evoda Shao baada ya kuhudumu kwa miaka 9 sasa anarudi kuendelea na huduma nyumbani Tanzania. IMG_9827Mapadre wakiongoza ibada. IMG_9927Balozi wa Tanzania Washington Dc na Mexico Mh.Liberata Mula mula akitoa maneno ya kumuaga Fr.Evod Shao. IMG_9917Mwakilishi kutoka ofisi ya Meya wa Baltimore akitoa hotuba ya kumuaga Fr.Shao. IMG_9939Mwambata wa jeshi Washington Dc na Canada Kanali Adolph Mutta na mkewe wakifuatilia ibada hiyo. IMG_9793Baadhi ya Watanzania waliohudhuria ibada. IMG_9791Harriet Shangirai makamu rais wa Jumuiya ya watanzania -DMV akiwa na mumewe Bw.Dan, kushoto ni Brian Daudi. IMG_9836Kulia Mzee Safari akiwa na mkewe. IMG_9941Kulia ni katibu wa Jumuiya ya watanzania Bw.Said Mwamende. IMG_9951Mwenyekiti wa jumuiya ya wakatoliki DMV Bw.Pius Mutalemwa nyuma yake ni naibu katibu wa jumuiya ya watanzania Bi.Bernadeta Kaiza na mwanae.Kwa picha zaidi ungana na http://sundayshomari.com/

  0 0

  Matron wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.
  Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati) akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwaajili ya kununua zawadi Kwaajili ya Wazazi wake.
  Mfanyakazi wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa katika matembezi Kariakoo.
  Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi kwaajili ya wazazi wake
  Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi kwaajili ya Wazazi wake
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao.

  0 0

   Rais wa Serikali ya Visiwa vya Comoro Ikililou Dhoinine akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia
   Rais wa Serikali ya Visiwa vya Comoro Ikililou Dhoinine akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Seychels James Michel  walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana   na Rais wa Seychels James Michel  baada ya mazungumzo walipokutana kwa   jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia.
   Wajumbe wa  Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa na Maafisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini michango inayotolewa katika mkutano huo unaoendelea huko Nchini Samoa katika ukumbi wa jengo mkutano huo,
   Wajumbe wa  Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa na Maafisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini michango inayotolewa katika mkutano huo unaoendelea huko Nchini Samoa katika ukumbi wa jengo mkutano huo,
   Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Bibi Fatma Fereji akiwa mwenyekiti katika sehemu moja ya Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa unaoendelea katika jengo ya Ukumbi wa Apia nchini Samoa,(kulia) Kaimu Sekretary (UN)  Bibi Erner Herity na (kushoto)Marrio Barthelemy  Mkurugenzi wa Uchumi na Mambo ya Kijamii,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
   Wajumbe wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa wakiwa katika ukumbi  wa jengo la Apia wakati michango mbali mbali ikitolea jana na Vingozi wa Nchi zilizoshiriki mkutano huo.

  0 0

  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller Muller (kulia) akikabidhi kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na masuala ya uzazi wa mpango kwa Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady jaydee' katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano hayo katika ofisi za MST, jijiji Dar es Salaam jana.

  Lady Jaydee, mwana muziki mashuhuri wa kizazi kipya nchini Tanzania, aliibua shangwe na chereko kwenye hospitali ya uzazi Marie Stopes iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.  
   
  Uwepo wa Jaydee ulitokana na kuungana kwa nyota huyu na Marie Stopes kwenye kampeni ya “Chagua Maisha” ambayo inalenga  kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii.
   
  Akiongea na waandishi wa habari punde baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Msimamizi wa MST nchini Tanzania, Bi Uller Muller, Lady Jaydee aliwaambia waandishi : “Nina furaha kubwa kuchukuka nafasi hii ya kipekee kama Balozi wa Marie Stopes kwa sababu wanafanya mengi kuwawezesha wakina mama kusimama na kujitegemea. 

  Lengo kuu la Kampeni hii ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana haki ya kuchagua mfumo wa uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na kutimiza malengo yao ya kimaisha, hususan mabinti wadogo”.
   
   Akitafakari sababu zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza: “siku zote nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha Tanzania kimaendeleo. Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo kuwa Wanawake wengi hupoteza maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa kuacha masomo kutoka na ujauzito. Mimi nimeamua kusaidiana na Marie Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili fikra na hatima zao, kwa kutumia uzazi wa mpango”.

  Takwimu zinaonyesha  kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwenye idadi ya vijana,  54% wakiwa chini ya umri wa miaka 20. Vijana hawa wana uwezo wa kubadili na kukuza hali ya kiuchumi ya Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo iwapo watapata msaada.

  Akiwa amesimama Pamoja na Lady Jaydee, Bi Muller alikuwa na haya ya kusema: “Leo hii nchini Tanzania, mmjoa kati ya kila Wanawake wane chini ya umri wa miaka 19 wamekwisha kuwa wazazi na asilimia 20% ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 wamo katika ndoa za kulazimishwa. 

  Zaidi ya hayo, kama binti akipata ujauzito hata kwa kubakwa, anafukuzwa shule na huo ndio unakuwa mwisho wa elimu yake. Haya siyo mazingira mazuri ambayo vijana wetu wanahitaji iwapo wana matumaini ya kukuza uchumi wa taifa letu na kuliweka kuwa katika kipato cha kati (middle income). Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuchangia kukua kwa taifa letu, hivyo ni jukumu letu kuwapa fursa hizo”.

  “Nina imani kubwa kuwa tutafanikiwa”, aliongeza Lady Jaydee, “tunataka kila mmoja atambue kuwa ana haki ya kuchagua muda na wakati wa kupata watoto, na pia idadi ya watoto wanaowataka. Marie Stopes na taasisi nyingine zinaweza kukusaidia kumaliza masomo yako na kuhakikisha kuwa una maliza elimu na kuwa na mwanzo mzuri wa maisha, kabla hujaamua kuwa mzazi. Name nitaanza kueneza ujumbe huu Jumamosi hii kwenya Nyama Choma Festival, Dar es Salaam!”.
   
  Tukio hili la Lady Jaydee kutembelea Hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es Salaam litaonyeshwa jumapili tarehe 07 Septemba kwenye East Africa TV. Kituo hiki kilichopo Mwenge ni miongoni mwa hospitali 11 za Marie Stopes nchini Tanzania. Zote hizi zinatoa huduma za uzazi wa mpango kwa Wanawake bure kabisa bila malipo yoyote.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe mkoani Tanga, litakalowashirikisha wanamuziki nyota, Mzee King Kikii (wa pili kushoto) na Banana Zorro (kushoto), litakalofanyika kesho Septemba 03, katika viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba.
  Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe mkoani Tanga, litakalowashirikisha wanamuziki nyota, Mzee King Kikii (wa pili kushoto) na Banana Zorro (kushoto), litakalofanyika kesho Septemba 03, katika viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
  Mwanamuziki nguli nchini, King Kikii akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu ushiriki wake katika onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe mkoani Tanga, litakalofanyika kesho Septemba 03, katika viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (wa pili kulia), ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba na Mwanamuziki nyota, Banana Zorro.

  Kampuni Airtel Tanzania leo imetangaza kuanzisha mpango wa huduma kwa jamii utakaowashirikisha wafanyakazi wake kujitolea na kushiriki katika kuchangia na kusaidia jamiii nchini.

  Mpango unategemea kuanza wiki hii unashirikisha wafanyakazi kutoka katika vitengo mbalimbali utawawezesha wafanyakazi hawa kuandaa shughuli zitakazowawezesha kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia shule mbalimbali ambazo zina mahitaji muhimu katika maeneo mbalimbali nchini.

  Mradi huu umezindulia rasmi na Kitengo cha huduma kwa wateja ndio kitakuwa cha kwanza kushiriki ambapo wameandaa burdani ya musiki itakayowashirikisha magwiji mahiri wa muziki nchini King KKii and Banana Zoro inayotegeme kufanyika siku ya jumatano tarehe 3 septemba 2014 katika viwanja vya ofisi ya Airtel. Wafanyakazi wa Airtel na watu mbalimbali kutoka nje wamealikwa kushiriki na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum Tanga.

  Akiongea kuhusu mpango huu Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema” katika kushiriki kutatua changamoto mbalimbali zinazozikumba jamii wafanyakazi wa Airtel wameona ni muhimu kuanzisha mpango huu maalumu wa kusaidia jamii. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii umeonelea ni vyema kutenga siku 14 mahususi kwa wafanyakazi kupata muda wa kusaidia jamii.

  Hivyo tutakuwa na shughuli mbalimbali kuanzia sasa zitakazofanya na wafanyakazi katika kukusanya fedha na kisha kufatiwa na siku 14 za kutoa misaada wa jamii zinazotegemea kuanza rasmi mwakani mwezi wa tatu. Lengo letu ni kuhakikisha tunazifikia shule 10 na kuzisaidia kwa sasa na leo tunachukua nafasi hii kuwaalika wafanyakazi wetu na jamiii kutuunga mkono na kushirikiana nasi”.

  “Baadhi ya shule zitakzofaidika na mpango huu ni pamoja na shule ya Msingi Pongwe Tanga itakayojengewa darasa, shule ya msingi ya kumbukumbu Dar es salaam itapatiwa msaada wa viti na meza kwa darasa la watoto wa masomo ya awali, shule ya sekondari Ndala watapewa vifaa vya ofisi kwa wafanyakazi , uhuru mchanganyiko watanunuliwa mashine ya Braile pamoja na vifaa vya kufundishai na shule ya msingi kimara watapatiwa tanki ya kuhifadhi maji.

  Nia yetu ni kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi na jamii kwa ujumla “aliongeza Mmbando.Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya elimu nchini mpaka sasa zaidi ya shule 1000 zimeweza kufaidika na vitabu kupitia mradi wa Shule yetu” wiki iliyopita

  Airtel imetangaza zaidi ya shule 30 zitakazofaidika na misaada ya vitabu kwa mwaka huu wa 2014 na leo kupitia wafanyakazi wake Airtel inaendelea kuwafikia watu wengi zaida na jamii nzima kwa ujumla nchini.

older | 1 | .... | 354 | 355 | (Page 356) | 357 | 358 | .... | 1897 | newer