Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 344 | 345 | (Page 346) | 347 | 348 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
   Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
   Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
   Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.

   Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kushoto) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
  Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (kulia kwake) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
    Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto mbele) akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kushoto mbele) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
   Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (kushoto) akimuonyesha waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) moja ya sehemu za ndani ya mradi wa nyumba wa NSSF wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, unaondelea kujengwa, wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofsdhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.

   Waziri Mkuu Mizengo Pinda (watano kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa nyumba za NSSF wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500 wa nyumba zenye gharama nafuu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
   
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata maelezo juu ya jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa ziara yake alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani  544, 530, 562 unafadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 45 ya hisa na Azimio Housing Estates Co. Ltd kwa asilimia 55 ya hisa.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata maelezo juu ya jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa ziara yake alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani  544, 530, 562 unafadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 45 ya hisa na Azimio Housing Estates Co. Ltd kwa asilimia 55 ya hisa.  Serikali imesema itajipanga ili kuona namna ya kukabiliana na changamoto mbali mbali ambazo zitaweza kukwamisha miradi mikubwa yanayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) yatakayo badilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam..

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyasema hayo baadaa ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) amayo ni pamoja na daraja la Kigamboni, mradi wa nyumba za gharama nafuu inayojengwa Mtoni Kijichi na mradi wa nyumba Zaidi ya 7000 uitwao  ‘Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.

  Akizungumza wakati wa kukamilisha ziara yake huko Dege Kigamboni katika mradi wa nyumba Zaidi ya 7000 uitwao  ‘Dege Eco Village’ Jumamosi , Pinda alisema Kigamboni inendelea kwa kasi kubwa kiasi kwamba miundombinu iliyopo haitoshi kuhimili idadi ya watu watakaohamia.

  “Tunahitaji kujipanga kwa dhati kuhakikisha barabara na vivuko vinafanya kazi. Changamoto kubwa hapa ni barabara za viuongo kutoka Mandela upande wa Kurasini na upande wa Kigamboni pia. Barabara hivi zote sita za darajani zitatakiwa kufika Kigamboni, Mjimwema, Mbagala na kwingineko,” alisema.

  Pinda alisema daraja litakapo kamilika, watumiaji watatozawa tozo la barabara ili kuweza kulihudumia. Alisema serilaki inafikiria pia namna ya kuipanga Kigamboni ili iendane na maendeleo yanayokuja.

   Kuhusu Mradi mkubwa wa Dege Eco Village wenye uwezo wa kuchukua nyumba za gorofa Zaidi ya 7000 na za kawaida (villas) 300, Waziri mkuu alisema mradi huo utaleta msukumo mkubwa kwa maendeleo ya taifa kwani hakuna mji utakao fanafana na ule kati ya miji mingi aliyofika.

  Aliitaka Manispaa ya Temeke kuangalia idadi ya watu kule Kigamboni  ili serikali iangalie uwezekano wa namna ya kupanga usimamizi kiutawala.

  Pinda alifurahishwa na kitendo cha NSSF kuwapa kipaumbele wanachama wake kupata nyumba ambazo zimejengwa katika mradi wa Mfuko huo uliopo Mtoni Kijichi. Tayari nyumba 85 zilizojengwa katika awamu ya kwanza zimeshachukuliwa na wanachama. Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Novemba 2008 na kukamilika 2010.

  Nyumba 215 zilizojengwa katika awamu ya pili nazo zimeshachukuliwa na wanachama na baadhi ya wadau wengine. Nyumba hizo kwa mujibu wa Meneja Miradi, Mhandisi John Msemo, zilianza kijengwa mwaka 2011 na kumalizika mwaka 2013 ikiwa ni awamu ya tatu.

  Mhandisi Msemo alisema awamu ya tatu ndio inaendelea kwa sasa ya ujenzi wa gorofa na nyumba za kawaida (villas) jumla yake ikiwa ni nyuma 820, mradi ambao ulianza mwaka jana 2013 na unatarajiwa kumalizika 2015. Tayari nyumba 300 zimeshalipiwa kabla hazijamalizika.

  Akiongea na waandhishi wa habari baada ya ziara ya waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK Ramadhani Dau alisema miradi yao ilikuwa inapata changamoto kubwa hasa upande wa barabara.

  “Tukimaliza ujenzi wa daraja tunategemea barabara zote jijini ziwe zimeisha ili kupunguza msongamano katika daraja. Itakuwa haina maana kumaliza daraja wakati maungio hayajakamilika,” alisema.

  Aliongeza pia kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza wa miradi hiyo ikiwemo ya kutopata ardhi toka kwa wananchi kwa muda unaofaa, serikali kuchelewa kutoa asilimia 40 ya sehemu yake katika mradi na pia masuala ya kitaalamu katika ujenzi wa daraja.

  Kuhusu mradi wa nyuma Mtoni Kijichi, alisema walikuwa wanahitaji sana daraja litakounganisha Mtoni Kijichi na Mbagala kwani nirahisi sana kuvuka sehemu hiyo na kuingia kigamboni kiurahisi kuliko kutumia Zaidi ya kilometa 20 kuzunguka katika daraja ili mtu afike Kigamboni au Mbagala.

  Tatizo la maji alisema walilazimika kuchimba visima wakati DAWASA waki jiandaa kufanya taratibu za kuweka maji.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo.Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na  Dkt Stergomena Tax [katibu mkuu wa SADC] na kwa upande wake wa kushoto ni Nkosazana Dlamini-Zuma  (Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika)

  Mtoto wa Kitanzania, msichana Neema Steven Mtwanga, ameibuka kinara katika Mashindano ya Utunzi wa Insha katika nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa washindani 39 waliowania Tuzo ya Utunzi wa Insha hiyo kwa Mwaka 2014. 

  Msichana Neema Steven Mtwanga, 16, kutoka Shule ya Sekondari ya Naboti, Mkoa wa Njombe, ametunukiwa Tuzo ya ushindi huo katika Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC ulioanza leo katika Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe. 

  Nafasi ya pili imeshikwa na Kudzai Ncube kutoka Shule ya Sekondari ya Mazowe nchini Zimbabwe na nafasi ya tatu imeshikwa na Manxoba Msibi kutoka Shule ya Sekondari ya Etjendlovu katika Swaziland. 

  Kwa ushindi huo, Neema Steven Mtwanga ambaye yuko kidato cha nne, amezawadiwa hundi ya dola za Marekani 1500 ambayo ni sawa na shilingi milioni 2.3 na amelipiwa gharama zote za kumwezesha kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC na kukabidhiwa zawadi hiyo. Aidha, Neema amepewa zawadi ya ipad kwa ajili ya matumizi yake ya teknolojia ya mawasiliano na habari. 

  Mashindano hayo ya Insha ya Mwaka 2014 yalianzishwa rasmi Oktoba, 2013 ambako washindani walitakiwa kuandika Insha kuhusu mada: “Climate Change is having adverse effect on the socio-economic development in the Region. What should the Education Sector do to mitigate the impact on the youth” – Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kanda ya SADC. Nini Sekta ya Elimu ifanye kupunguza athari hizo kwa vijana? 

  Insha 39 zilipokelewa kutoka nchi 13 kati ya nchi 15 wanachama wa SADC ikiwa ni Insha tatu kwa kila nchi. Insha zilipokelewa kutoka Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. 

  Majaji wa kupitia na kuamua washindi wa Insha hizo walitoka Tanzania, Zambia na Zimbabwe na walikutana mjini Gaborone, Botswana, Julai, mwaka huu kupitia Insha zote na kutoa uamuzi wa nani washindi. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa SADC umepokea kwa furaha ushindi wa msichana Neema ukieleza kuwa ushindi huo umeiletea Tanzania heshima kubwa katika eneo la SADC na nje ya eneo hilo. 

  Imetolewa na; 
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
  Ikulu – Dar es Salaam. 
  17 Agosti,2014  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi,Abdallah Bulembo (katikati) akiwasili katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na wasanii kwenye dua maalum ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki.Kulia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere.
  Msanii wa vichekesho ambaye pia ni muinjilisti kwa sasa Emanuel Mgaya Maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiongoza dua kwa upande wa wakristo huku Msanii Jacob Stephen JB akiwa ameishikilia Biblia.Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum ambaye aliongoza dua kwa upande wa waislam,katika shuguli hiyo ya kuwaombea Wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya wadau wa Filamu nchini wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuwaombea Dua Wasanii wote waliotangulia mbele ya haki (waliofariki) iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam jana.
   Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum akijadiliana jambo na baadhi ya wadau walioshiriki kwenye dua hiyo.
  Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere akipeana mkono na watu mbali mbali baada ya kumalizika kwa dua ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Paulina Nyoni (Mama wa mtoto Fatuma Msuya) akiwa amembeba mwanaye ambaye anahitaji msaada wa matimabu .

  ----------------------
  Paulina nyoni mkazi wa kijiji cha Hanga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma anaomba msaada kwa yeyote atakaye guswa na tatizo la mwanaye  aitwaye Fatuma Msuya ili aweze kupata matibabu katika hospitali ya KCMC moshi.

  Paulina ni mama mwenye watoto wa tano anayejishugulisha na kilimo , Mume wake aitwaye  Jafari Msuya amemtelekeza baada ya kujifungua mtoto mwenye tatizo hili na kukimbia kusikojulikana hivyo kumfanya mama wa mtoto huyu kutokuwa na msaada wowote ule,

  Fatuma Msuya (1) amezaliwa tarehe 24/2/2013 katika Hosptali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na tatizo la kutokuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji tumboni ambapo kwa sasa anatolea haja kubwa,awali kabla ya kupasuliwa alikuwa akitolea haja kubwa sehemu ya aja ndogo.

  Upasuaji wa awali alifanyiwa katika Hospitali ya Mission Peramiho iliyopo wilaya ya songea tarehe 19 04/ 2013.Na kwa sasa mtoto huyu anakabiliwa na tatizo jingine la kutokwa na vidonda sehemu anayojisaidia  hali inayomsababishia maumivu wakati wote na anapojisaidia haja kubwa hutokwa na damu.

  Gharama za matibabu zinazohitajika  ni shilingi milioni tatu, Yeyote atakayeguswa anaweza kutoa msaada kwa Mpesa no 0767 710 113 .
  “Kutoa ni moyo”

  0 0

   Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamed Ligora , akizungumza kwa niaba ya  Wazee wenzake  wa mkoa wa Dar es salaam walipoongea na waandishi wa habari leo ambapo amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema  UKAWA na wenzao  wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia.
    Mzee Alhaji Sheikh Bakari Chiwaka (kulia) akisisitiza umuhimu wa maridhiano katika mchakato wa Katiba Mpya na kuwa Katiba bora itapatikana kwa uongozi bora na wa kidemokrasia nchini. Kushoto ni Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamed Ligora.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akiwasikiliza
  Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mara baada ya mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

   Immaculate Makilika –MAELEZO_DAR ES SALAAM 
  WAZEE wa Mkoa wa Dar es salaam wamewaomba Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) kurudi Bungeni ili kuendelea na mchakato wa majadiliano ya Rasimu ya Katiba Mpya yanayoendelea.

   Wazee hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini pamoja na Bunge la Katiba Mpya linaloendelea mjini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Wazee wenzake Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamedi Ligora , amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema UKAWA na wenzao wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia. 

   Amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawataki kufananishwa na nchi zingine zilizofanya makosa na kupata matatizo kutokana na mambo kama haya ambayo yalisababisha wananchi wao kuzikimbia nchi zao kwa mambo ambayo wangeweza kukaa chini na kumaliza wenyewe kwa ajili ya maslahi ya umma. Kapteni Mstaafu Alhaji Ligora amesema kuwa suala la mchakato ni suala la kidemokrasia, hivyo ni vyema UKAWA wakatumia fursa hiyo waliyonayo kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Rasimu ya Katiba hali itakayosaidia kupatikana kwa Katiba Mpya ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wa Tanzania. 

   Aidha, amewaomba wajumbe walio Bungeni na wale walio nje ya Bunge kuacha kuwazomea UKAWA badala yake wawasihi warudi katika chombo rasmi cha kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya. 

   Naye Mzee Ali Bakari Muki, amewataka UKAWA kuheshimu misingi ya demokrasia lakini pia amewapongeza wabunge walioitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Katiba kwani ndio Jukwaa pekee la kuwapatia wananchi Katiba bora. 

   Kwa upande wake Mzee Yahaya Ngoma amewataka viongozi wote hasa UKAWA kuheshimu na kudumisha jitihada zilizofanywa na waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuzingatia misingi na kanuni za uongozi bora kwa kutumia njia ya majadiliano pale panapokuwa na mawazo tofauti baina yao. Halikadhalika, Alhaji Sheikh Bakari Chikawa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza ni moja ya tunda la uongozi bora na demokrasia nchini. 

   Aidha, ameongeza kuwa UKAWA ni vema wakatumia fursa hiyo ya demokrasia kwa kuwawakilisha vema wananchi wa Tanzania ili kuhakikisha wanapata Katiba Bora. Alhaji Chikawa amewaomba UKAWA kurudi Bungeni kwani kunyume na hivyo ni watakua wametenda dhambi na madhara yake ni makubwa sana, na kusisitiza kuwa mazungumzo ni muhimu na yakipuuzwa basi kuna madhara.


  0 0


  Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe akimkabidhi Bi. Sheila Hashim Mbita, binti yake Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita Tuzo ya Juu ya Taifa la Zimbabwe ya Nishani ya Royal Order Of Mwanamutapa kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa Taifa la Zimbabwe na nchi nyingine kusini mwa Afrika. Rais Mugabe alikabidhi tuzo hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe. Picha na Fred Maro
  ---------------------------
  Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeishukuru na kuipongeza tena Tanzania kwa mchango wake mkubwa na wa hali na mali uliofanikisha jitihada za mapambano ya ukombozi yaliyoleta uhuru kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
  Aidha, SADC imemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Afrika, Brigedia Hashim Mbita wa Tanzania, kwa mchango wake na uongozi wake wa mapambano ya ukombozi, iwe katika nyanja ya kuviwezesha vyama vya ukombozi kwa hali na mali, raslimali na ushauri.

  Pongezi hizo kwa Tanzania zilitolewa usiku wa jana, Jumamosi, Agosti 16, 2014, na Kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC – SADC Troika- kilichofanyika kwenye Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe, chini ya Uenyekiti wa Rais Hifikepunye Phohaba wa Namibia.
  Mkutano huo wa SADC Troika ulihudhuriwa na wanachama wa Asasi hiyo – nchi za Namibia, Lesotho na Tanzania. Nchi za Afrika Kusini, Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilishiriki kama waalikwa maalum wa kikao hicho.

  Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya nwenzake, Rais Pohamba alisema: “Tunawashukuru wananchi wa Tanzania kwa mchango wao wa kiuchumi, kijeshi na kimkakati katika kuunga mkono kwa hali na mali jitihada za mapambano ya ukombozi wa nchi zetu.”

  Aliongeza Rais Pohamba: “Sote tunaijua Tanzania, sote tunawajua Watanzania.  Kwa pamoja walitoa jasho na damu na sisi wenyewe katika kutafuta ukombozi wa nchi zetu. Tutaendelea kukumbuka na kuenzi mchango wao mkubwa na usiosahaulika kwa ustawi wa nchi zetu.”

  Kuhusu Mzee Mbita, ambaye Ripoti yake ya shughuli za ukombozi ilitarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC, Rais Pohamba alisema: “Brigedia Mbita alifanya kazi mchana na usiku kufanikisha shughuli za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tunamshukuru sana kwa uongozi wake na mchango wake mkubwa katika kuleta uhuru wa nchi zetu.”

  Aliongeza: “Brigedia Mbita ni raia wa Tanzania na alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika iliyokuwa na makao makuu yake mjini Dar es Salaam. Alichapa kazi kweli kweli na chini ya uongozi wake, vyama vya ukombozi vilipata misaada ya hali na mali, misaada ya kiroho na ushauri wa kijeshi kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mtu wa shughuli za jeshi.” Mzee Mbita aliongoza Kamati ya Ukombozi tokea mwaka 1974 hadi ilipomaliza shughuli zake.

  Akizungumza kwa ufupi sana katika kikao hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimpongeza sana Brigedia Mbita akisema kuwa alifanya kazi nzuri na kubwa na “tunampogeza kwa kazi nzuri sana ya kuandaa Ripoti hiyo.”

  Ripoti hiyo inayojulikana kama Mradi wa Hashim Mbita iliongozwa na Meneja wa Mradi, Profesa Arnold Temu wa Tanzania na imechapishwa na Kampuni ya Mkuki na Nyota, pia ya Tanzania, ambayo Mtendaji Mkuu wake, Mzee Walter Bgoya ameandamana na mwakilishi wa Mzee Mbita kwenye mkutano huo.
  Imetolewa na;
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.

  17 Agosti,2014

  0 0

   
   Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana,leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro.Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele
   Malkia wa Taarab hapa nchini,Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele,pichani nyuma ya Afande Sele ni guli wa muziki wa Reggae hapa nchini ,Innocent Nganyagwa.
   Afande Sele akifarijiwa na mkali wa hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Joh Makini
    Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana,wakiwa katika picha ya pamoja na Afande Sele mara baada kupitia nyumbani kwa msanii huyo na kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro.
   Pichani ni mmoja Wanahabari kutoka gazeti la Mwananchi na Efm,Henry Mdimu,Joh Makini pamoja na Ben Paul wakiwa katika picha ya pamoja.
  Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumfariji Afande Sele.Picha zote kwa hisani ya Dj Choka aliyekuwepo kwenye msafara huo,Afande Sele aliwashukuru Marafiki,washabiki wake ndugu jamaa na Marafiki kwa umoja na mshikamano waliouonesha kwake katika kipindi hiki kigumu ambacho hakikuwahi kumtokea katika maisha yake ya kuondokewa na Mpendwa Mke/mzazi mwenzake. '' sina maneno yanayoweza kuelezea kwa wepesi faraja,upendo na ushirikiano nilioupata kutoka kwenu,nawashukuruni sana ndugu zangu'' ,alimaliza kusema Afande Sele huku akionekana kuwa mwenye simanzi kubwa

  0 0

   Washiriki  wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na Viwanda wakiwasili katika  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Washiri hao wanatoka katika Wizara za Uwekezaji na Biashara ambapo washiriki 15 kutoka katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini wanashiriki mkutano huo. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Nordic Africa Institute (NAI) kwa kushirikiana na Trans African University Partnership (TANUP/PUTA), huku ikisaidiwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweeden (SiDA) na FAO.
   Mkurugenzi wa Fedha Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Job Chacha akiwakaribisha washiriki  wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki  wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, wakisaini kitabu cha wageni walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati), akizungumza na baadhi ya washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali ili waweza kupata uwezo wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati), akizungumza na baadhi ya washiriki  wa mkutano huo.
   Baadhi washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wakimsikiliza Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo walipotembelea  Ofisi za Chuo hichoMikocheni jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya washiriki.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wakimsikiliza Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo.
   Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Uchumi na Usimamizi (UB) Dk. Lenny Kasoga na Mkurugenzi wa Fedha UB, Dk. Job Chacha.
   Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoaj na washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF,  Cresentius Magori akifafanua jambo kwa washiriki wa kongamano la Maofisa Rasilimali watu wa Taasisi za Kifedha lililofanyika Morogoro Hotel.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maoafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi za Kifedha wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano hilo.

  Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Rasilimali watu  NSSF ,Chiku Matessa akizungumza na maafisa Rasilmali watu wa mabenki na taasisi mbali mbali za kifedha wakati wa uzinduzi wa kongamano la maafisa rasilimali watu wa mabenki.


  0 0

  DSC_0069
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kushoto ni Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga na kulia ni Mtaalamu wa Programu za Vijana kutoka UNFPA, Tausi Hassan.( Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

  .Siku ya vijana duniani na ujumbe wa “Vijana na Afya ya Akili”
  .Takwimu zinaonyesha nusu ya idadi ya watu nchini ni vijana

  SERIKALI Kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeahidi kukuza na kuboresha misingi ya kuwashirikisha vijana katika utekelezaji wa sera mbalimbali, programu na mikakati ya maendeleo.

  Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bibi Venerose Mtenga amesema kwamba lengo la kuwashirikisha vijan ni kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi.

  “Katika kutekeleza eneo hili Tanzania inalenga kuweka fursa zitakazowawezesha vijana kukuza utaalamu na ujuzi utakaowawezesha kufanikiwa katika kipindi cha mpito kutoka ujana kwenda katika utu mzima,” amesema Bibi Mtenga.

  Amesema kwamba Tanzania kama sehemu ya dunia inatambua changamoto maalum zinazowakabili vijana walioko katika mazingira hatarishi pamoja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kikamilifu katika malengo ya maendeleo.
  DSC_0096
  Bi Mtenga aliongeza Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vijana pamoja na wadau wa maendeleo ili kuunga mkono programu za elimu ya afya kwa vijana walioko ndani na nje ya shule.

  Alilisitiza kwamba Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wataendelea kuunga mkono taasisi za mafunzo rasmi na zisizo rasmi ili kukuza uwezo na uelewa miongoni mwao katika masuala ya afya ya akili na mwili kwa ujumla.

  “siku ya vijana duniani inatambua na kuthamini kuwa kipindi cha ujana kinaambatana na mabadiliko makubwa na ya haraka na safari ya kutoka utotoni kufikia utu mzima,” “Safari hiyo inaweza kuwa ngumu na yenye changamoto nyingi na hivyo kuhitaji utulivu na ukomavu wa akili, hapa Tanzania, kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya vijana, kijana ni mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 35,” aliongeza
  Amesema kwamba katika takwimu za kitaifa hapa nchini nusu ya idadi ya watu ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.
  DSC_0133
  Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya vijana duniani, kushoto kwake, ni Mwakilishi wa UNFPA, Dkt. Natalia Kanem.
   
  Bibi Mtenga aliendelea kusema kwamba msisitizo mkubwa unawekwa katika kuhakikisha vijana wanakuwa na fikra chanya ambazo ni za kimaendeleo na zinazoleta mabadiliko chanya kwa jamii.
  Kwa Upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem amesema kwamba siku ya vijana duniani ni nafasi nyingine kwa vijana kukutana pamoja na kujadiliana matatizo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
  Amesema kwamba vijana kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa katika kupambana na changamoto za matumizi ya pombe kupita kiasi, dawa za kulevya na mimba za utotoni.
  “kwa pamoja serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa wana wajibu wa kushirikiana na vijana katika kuwasaidia kufikia malengo yao mbalimbali katika harakati za kujiletea maendeleo,” amesema Dkt. Kanem.
  DSC_0041
  Baadhi ya timu za mpira wa kikapu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
  Dkt Kanem aliongeza kwamba ni muhimu kwa vijana kutambua kwamba bila kuwa na afya nzuri ya akili ni vigumu kupiga hatua za kimaendeleo na kuondokana na umaskini wa kipato.
  Amesema kwamba katika mkutano unaokuja wa viongozi duniani watatumia nafasi hiyo kuwakumbusha viongozi wa dunia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana kama taifa la kesho.
  Dkt.Kanem alifafanua umuhimu wa vijana na jamiii kwa ujumla kutumia mitandao ya kijamii katika kupashana habari za afya ya uzazi na mambo yanayowahusu vijana kwa ujumla.
  Wakati huo huo, Katika mashindano ya mpira wa kikapu timu zilizoshiriki ni timu saba kati ya hizo tano ni za wanaume na pili za wasichana.
  DSC_0061
  Kwa upande wa wasichana mshindi wa kwanza ni Don Bosco Lioness na washindi wa pili ni Tanzania Prisons Queens na kwa upande wa wavulana, washindi wa kwanza Lord Baden-Powell Memorial High School, washindi wa pili Makongo High School, washindi wa tatu ni Kizuka Sekondari school.
  Timu zilizoshiriki ni Tanzania Prisons Queens, Lord Baden-Powell Memorial High School, Makongo High School, Don Bosco Lioness, Kizuka Sekondari School, Tabata Segerea na Bahari Beach.
  DSC_0157
  Mgeni rasmi, Venerose Mtenga akirusha mpira wa kikapu kuzindua rasmi mashindano ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana wa shule za sekondari nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
  DSC_0150
  Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem akirusha mpira wa kikapu kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
  DSC_0161
  Mgeni Rasmi na Mwakilishi wa UNFPA wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya timu za mpira wa kikapu.
  DSC_0183
  Mgeni rasmi, Venerose Mtenga akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wasichana ya mpira wa kikapu wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
  DSC_0175
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama (kulia) na Mgeni rasmi, Venerose Mtenga (kushoto) wakimuonyesha jambo Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem (katikati) mara baada ya kupata picha za kumbukumbu na timu zilizoshiriki bonanza hilo la mpira wa kikapu katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
  DSC_0201
  Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem akisalimiana na msanii muziki wa bongo flava Domokaya (wa pili kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
  DSC_0636
  Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza akipata u-selfie na msanii wa bongo flava Domokaya wakati wa maadhimisho hayo.
  DSC_0639
  Phillip Musiba kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akipata picha na msanii wa muziki wa bongo flava nchini Domokaya.
  DSC_0228
  Timu za Kizuka sekondari kutoka Morogoro, (Nyeupe) na Makongo Sekondari (Njano) wakitoana jasho katika mchezo wa ufunguzi wa mpira wa kikapu, Makongo walishinda vikapu 30 dhidi ya 14 ya Kizuka sekondari kutoka Morogoro.
  DSC_0235
  DSC_0245
  Mgeni Rasmi, Bibi Venerose Mtenga akifafanuliwa jambo kutoka kwa Mshauri wa vijana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNNFPA), Bw, John Kalimwabo alipotembelea banda hilo.
  DSC_0271
  Mgeni Rasmi, Bibi Venerose Mtenga akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Tatu Mwakifuna na Mwanafunzi wake, Zawadi Salehe wote kutoka KIWOHEDE. Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mtaalamu wa Programu za Vijana kutoka UNFPA, Tausi Hassan.
  DSC_0294
  Mgeni rasmi akipata maelezo kutoka kwenye banda la Tanzania Network Against Alcohol Abuse kwenye moja la shirika lake la Tanzania Girl Guides Association, anayetoa maelezo ni Fadhia Khamis Ally na kushoto kwake ni Shadya Soud Milanzi wasichana hao wanatoka Girl Guides ambacho ni chama kisicho cha kiserikali na ni chama cha kujitolea, madhumuni yake ni kuwaendeleza wanawake pamoja na motto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.
  DSC_0304
  Mgeni rasmi, Bibi Venerose Mtenga akimsikiliza kijana kutoka Kituo cha Vijana UMATI, Temeke, Kassim Abdallah alikuwa akimweleza mgeni rasmi jinsi wanavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa kutumia vipeperushi na ushauri nasaha.
  DSC_0343
  Wawakilishi kutoka Marie Stopes Hospital Tanzania, Bibi Zayana Nuhu na John Basso Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wakimweleza jambo mgeni rasmi jinsi hospitali hiyo inavyofanya kazi hapa nchini.
  DSC_0352
  Mgeni rasmi akipata picha ya kumbukumbu na mmoja wa wahudumu wa banda la Marie Stopes wakati wa maadhimisho hayo.
  DSC_0518
  Joynes Ashery kutoka Marie Stopes Hospital Tanzania akifafanua jambo kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi kwa Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ambao ni wameshiriki kuratibu maadhimisho hayo, Stella Vuzo.
  DSC_0392
  Mshauri wa vijana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNNFPA), Bw, John Kalimwabo akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya Kondomu za kike kwa kutumia kiungo bandia cha mwanamke kwa vijana waliohudhuria maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani.
  DSC_0398
  Vijana wakiendelea kumiminika kwenye banda ya UNFPA kupata maelezo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  DSC_0489
  Mratibu wa uzazi wa mpango kutoka shirika la PSI, Hadija Ameir akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa vijana wakati wa maadhimisho hayo katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
  DSC_0545
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na baadhi ya watoto walioshiriki mashindano ya kuchora picha mbalimbali zikiwemo za kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya baada ya kuvutiwa na kazi zao.
  DSC_0549
  Mtoto Tarzan Iddy akionyesha picha yake aliyoichora ikizungumzia uvutaji wa Bangi kwa vijana.
  DSC_0738
  Mgeni rasmi, Bibi Venerose Mtenga na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama wakikagua baadhi ya picha hizo na maudhui kabla ya kutangaza washindi.
  DSC_0742
  DSC_0755 
  Mgeni rasmi, Bibi Venerose Mtenga akikabidhi nyenzo za sanaa ya uchoraji zilizotolewa na UNFPA kwa mtoto Lawrence Dennis wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani.
  DSC_0765
  Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akimkbidhi mmoja kati ya tatu bora wa mashindano ya uchoraji Aziza Iddy nyenzo za sanaa ya uchoraji kutoka kwa zilizotolewa na UNFPA sambamba na ufadhili wa kusomeshwa kulipiwa ada ya darasa la uchoraji kwa siku tano.
  DSC_0835
  Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akiwavalisha medali timu zilizochukua ubingwa wakati wa maadhimisho hayo.
  DSC_0867
  DSC_0801
  Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akimkabidhi zawadi Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Maluwe kama shukrani ya kuratibu bonanza la mpira wa kikapu kwa vijana wakati wa maadhimisho hayo.
  DSC_0944
  Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kwanza wa bonanza la mpira wa kikapu timu ya Lord Baden-Powell.
  DSC_0948
  Timu ya wasichana ya mpira wa kikapu ya Don Bosco Lioness kwenye picha ya pamoja na Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga.
  DSC_0935
  Timu ya waichana ya Don Bosco Lioness wakijipiga u-selfie baada ya kuibuka kidedea kwenye maadhimisho hayo.

  0 0

   
   Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania na baadhi ya wateja wakionyesha fataki kusheherekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
   Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugene Masawe (wa kwanza kulia) naMeneja Mwandamizi wa Tawi la Samora, Nancy Huggin (wa kwanza kushoto) pamoja na wateja wa benki hiyo wakikata keki kusherehekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997. (Picha na mpiga picha wetu).
  Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania (wa kwanza kulia) Anita Goshashy akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997
   Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugen Masawe (Aliyenyanyua mikono) akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
  Baadhi ya wafanyakazi wakongwe wa Benki ya Exim Tanzania katika picha ya pamoja iliyopigwa wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.

  IKIJIKITA katika safari yake tangu mwaka 1997 ikiwa na tawi moja na kupanua wigo wake mpaka matawi 27 nchini na nje ya nchi, Benki ya Exim imepiga hatua ya kipekee katika sekta ya kibenki nchini Tanzania. Ikidhiirishwa na miaka 17 ya historia ya Benki iliposheherekewa Ijumaa Agosti tarehe 15 na wafanyakazi wa benki pamoja na wateja nchi nzima. 

  Benki ya Exim imekuwa na mpango kazi madhubuti wa 'upanuzi na ugunduzi' tangu kuanzishwa kwake kama benki ya kitanzani, mali zake kwa jumla zikiwazimevuka shilingi tilioni moja ilipofika mwezi Juni 2013.  Bw. Eugene Masawe, Mkuu wa Idara ya Uendeshaji na mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu alisema; "maadhimisho ya miaka 17 ya benki yanaashiria mafanikio makubwa kwa miaka mingi, yaliyodhiirishwa na utendaji wake mzuri wa kuwa na dhamira ya kuwa "benki bora zaidi ya wengine".

  Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ya Exim hayaonyeshi tu mafanikio yaliyopatikana katika miaka hiyo lakini pia uongeza hari ya utendaji mzuri kwa wafanyakazi wote. Wakati faida ghafi ya benki ikikua kwa asilimia 80 (shilingi bilioni 9.6), pato la jumla litokanalo na riba likikua asilimia 36 (shilingi bilioni 14.3) na pato kupitia biashara ya fedha za kigeni liliongezeka kwa  asilimia 33 kuanzia mwaka jana ni viashirio thabiti kwamba benki hiyo itafikia malengo katika miaka michache ijayo.

  Utendaji huo wenye mafanikio wa Benki ya Exim umetokana jitihada za benki hiyo kutoa huduma za kipekee zikiungwa mkono na wafanyakazi mahiri pamoja na wateja waaminifu na kuifanya benki kuwa ya kwanza katika Huduma kwa Wateja (Customer Care) nchini Tanzania mwaka 2012 (Ripoti ya KPMG).

  Ikiwa na zinazomlenga mteja za rejareja, mikopo mbali mbali na kuanzisha huduma za kibenki za kisasa vimekuwa na  umuhimu mkubwa kwa kuendana na kauli mbiu ya benki ya, 'ugunduzi ni maisha.’

  Naye Nancy Huggin, Meneja Mwandamizi wa tawi la Samora akasema, "sasa tumejikita katika mpango wa kibunifunifu ujulikanao kama innovative retail model utakao tusaidia kuboresha mawasiliano na wateja na uratibu wa matawi katika maeneo tunayofanyia kazi."

  Kwa upande wake, Issa Hamisi, kaimu Afisa wa Fedha Mkuu aliongeza; “kipaumbele chetu kikubwa kinabaki kuendelea kuimarisha nafasi yetu katika soko na kuboresha ufikiwaji wa matakwa ya mteja kupitia utendaji ulio na ufanisi.”

  Katika siku hiyo maalum, Benki ya Exim iliwaalika baadhi ya wateja wake kusherehekea maadhimisho hayo katika matawi yote nchini Tanzania kwa wafanyakazi wa jijini Dar es Salaam wakisheherekea katika Tawi la Samora ambapo Benki ya Exim ilizaliwa.

  Wakati wa tukio hilo la kukumbukwa, Bw. Masawe aliongeza na kusema, "Baada ya kumaliza miaka 17 ya shughuli zenye mafanikio Tanzania, tutaendelea kusimama imara, na kuendelea na kuwa na mpango wa ukuaji  tukijikita zaidi na utoaji wa huduma zenye ubora zaidi na vile vile bidhaa na huduma zilizo na ubunifu zaidi."

  0 0


  KAMPUNI maarufu ya filamu Swahilihood ya Safina Movies imeandaa nafasi za bure kabisa kwa msanii yoyote mwenye kipaji kujiunga na kampuni hiyo kwa ajili ya kuonyesha kipaji chake, msanii chipukizi atakayejiunga na kundi hilo atafundishwa na kushiriki katika kazi za kampuni hiyo.

  Akiongea na wanahabari mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Mshindo Jumanne amesema kuwa kampuni hiyo imekusudia kukuza vipaji vya wasanii chipukizi waliokosa fursa hiyo pamoja na kuwa na uwezo wa kuigiza kwa vitendo na si maneno.

  “Wasanii wenye vipaji ni wengi sana mitaani lakini hawapewi fursa kuigiza na kushiriki katika filamu na tamthilia, ndio maana kampuni yetu ya Safina Movies imeliona hilo na kuwapa nafasi za kuonyesha vipaji vyao bila gharama,”anasema Mshindo.

  Mkurugenzi huyo amedai kuwa kutokana na ugumu wa ajira nchini Tanzania baadhi ya wasanii chipukizi wamejikuta wakitapeliwa kwa kuchangishwa fedha na kuuziwa fomu kwa gharama kubwa na kuishia kupigwa picha bila kupewa kazi.

  Aidha kampuni ya Safina Movie yenye maskani yake Kijichi Mbagala inasajili wanaohitaji kuwa wasanii nyota Bure kabisa kama msanii anahitaji anaweza kuwasiliana na uongozi kwa namba hizi 0658 010 100/ 0752 132 347 utakuwa umeingia katika tasnia ya filamu.

  Safina movie inahitaji wasanii zaidi ya 400 kwa ajili ya tamthilia inatayorushwa katika moja ya televisheni kubwa za Afrika Mashariki, kampuni hiyo ambayo ni watengenezaji na wasambazaji wa filamu nchini imesema pia wasanii hao pia watashiriki katika filamu za kampuni hiyo.

  0 0


  MWIGIZAJI wa kike wa filamu Aisha Bui, amedai kuwa alijitoa maisha yake kutoka na filamu yake ya Mshale wa Kifo, kutokana na sinema hiyo kutengeneza porini katika msitu hatari wenye wanyama wakali.

  Msanii huyo amedai alifanya hivyo kufuatia maoni ya wapenzi wa filamu ambao kila siku wanalalamika kwa kusema kuwa filamu zetu nyingi zimekuwa za mijini tu, huku baadhi ya matukio yakirudiwa kila katika sinema hizo jambo ambalo limekuwa likiongelewa mara kwa mara.

  “Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, lakini najua na deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema Asha .

  Filamu ya Mshale wa Kifo Imetengenezwa na Yuneda Entertainment na imewashirikisha wasanii nyota kama Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Asha Bui, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ na wasanii wengine.

  Sinema hiyo imerekodiwa Mkoani Morogoro Vijijini ikiwa ni hatua nyingine kwa watayarishaji wa filamu kwenda kucheza filamu nje ya jiji la Dar es Salaam kama ilivyozoeleka, Aisha anasema kuwa maeneo yanayotumika yanarudiwa sana hata baadhi ya watazamaji wameyashika kwani yanaonekana kila filamu.

  0 0

  Baadhi ya wana bongo dansi wakiwa katika picha ya pamoja na bendi ya vijana jazz wakati wa kusherehekea mwaka mmoja wa kundi hilo tangia lianzishwe kwenye mtandao wa kijamii wa fecebook ambapo kundi hilo mpaka sasa lina wanachama 3,086 mashabiki wa bendi mbalimbali wa mziki ya dansi nchini .
  Baadhi ya wanachama maarufu wa bongo dansi kushoto ni Abdulfareed Hussein ,  Senetor Mwinyi na William Kaijage walipokutana katika sherehe za mwaka wa kundi hilo zilizofanyika vijana kinondoni Dar es salaam picha na www.burudan.blogspot.com
  wafulumusha magitaa wa bendi ya Vijana Jazz wakiwajibika wakati wa sherehe za kutimiza mwaka mmoja kwa kundi la Bongo Dansi ambao ni mashabiki wa mziki wa dansi nchini wanaokutanishwa katika mtandao wa kijamii wa fecebook kushoto ni Shomari Ally na Said Kizunga picha na www.burudan.blogspot.com.
  Wasanii wa bendi ya Vijana Jazz wakiserebuka.
   
  Mpiga tumba wa bendi ya vijana jazz Ally Rajabu kushoto na Mpiga drams wa bendi hiyo Samata Hassani waki wajibika wakati wa onesho lao
  Waimbaji wa bendi wa Vijana Jazz wakiimba kutoka kushoto ni Saburi Athumani,Julius Mwesiwa,Abdallah Mgonahanzeru na Husein Boom wakitoa burudani wakati wa kundi la mashabiki wa mziki wa dansi nchini la bongo dansi lilipokuwa linatimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kweke katika mtandao wa kijamii wa fecebook lina wanachama 3,086 mashabiki wa bendi mbalimbali wa mziki ya dansi nchini picha na www.burudan.blogspot.com

  Waimbaji wa bendi ya vijana Jazz wakitoa burudani kwa kundi la Bongo Dansi kutoka kushoto ni Julius Mwesiwa na Komweta Maneti picha na www.burudan.blogspot.com
  Baadhi ya wana Bongo Dansi wakiwa katika meza wakiendelea kupata burudani za vijana jazz

  Mwana familia wa Bongo Dansi William Kaijage akisema chochote wakati wa sherehe hizo kulia ni mwimbaji wa bendi ya vijana jazz Abdallah Mgonaanzeru
  Wasanii wa Vijana Jazz wakimkaribisha Miraji Shakashia katikati
  Wana bongo Dansi wakimkaribisha mwenzao Rajabu Zomboko katikati kushoto ni William Kaijage na kulia ni
  Senetor Mwinyi wakati wa kundi hilo lilipotimiza mwaka mmoja kamili tangu lianzishwe kwake kwenye mtandao wa kijamii wa fecebook

  Mwimbaji wa bendi ya Vijana Jazz Komweta Maneti kushoto akiserebuka na wana bongo Dansi wakati wa onesho lao

  0 0

  signing deal
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.

   Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300. Mkataba huo umetiwa saini nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.

  Akizungumza kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.

  “MeTL na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013, uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100.

  Dewji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini amesema kampuni yake imekuwa na mafanikio makubwa kibiashara mpaka kuaminiwa na benki mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Pamoja na mkopo huo kwa MeTL hivi karibuni kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd, ilipata mkopo wa sh. bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

  “Mwaka 1999 wakati najiunga katika kampuni hii ya kifamilia biashara yetu ilikuwa ni ya dola za marekani milioni 26 na sasa tumejiongeza mara zaidi ya 60 kwani sasa pato letu litafikia dola za Marekani bilioni 1.5 ifikapo mwishoni mwa mwaka”, alisema Dewji.

  Alisema mafanikio yalkiyopatikana ya kulipa mikopo husika yamewezesha yeye kusaini mkataba wa mkopo wa dola za Marekani milioni 200 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu wafikie uwezo wa kukopa dola milioni 100 za Marekani. “Ninataka kusema kwamba maendeleo makubwa ya MeTL yasingelifikia hapa bila RMB kutuamini katika hatua za awali” alisema ofisa mtendaji huyo ambaye pia alielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na MeTL.

  Alisema kampuni yake inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara, petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na masuala ya simu.
  Toast
  Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane wakinywa shampeni baada ya kufanya "Toast" kama ishara ya kutakiana kheri na mafanikio kwenye biashara zao.


  Akisaini mkopo huo, Dewji aliwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ya kusaini kati ya kampuni yake MeTL na RMB huku ikijivunia kufanya biashara katika nchi za Ethiopia, Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan Kusini na Kenya.

  Alisema kwamba kampuni hiyo inataka kujiimarisha zaidi katika sekta mbalimbali.MeTL kwa sasa ina viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee; huku ikiwa imetawanyika katika nchi 11 zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara. "Tumejitanua katika nchi mbalimbali barani Afrika, nashukuru kwa ushirikiano mzuri ambao umechangia mafanikio makubwa ya kampuni yetu", alisema Dewji.

  Dewji maarufu kwa jina "MO" anasema elimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani ndio iliyomfumbua macho na kuona umuhimu wa kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani. “Nia yetu ni kuwa na nguvu kubwa ya kibiashara Afrika Mashariki na Kati tukipania MeTL kuwa na pato la zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 kwa mwaka ifikapo mwaka 2018 na kutengeneza ajira za watu 100,000.” Alisema Dewji.

  Alisema katika hotuba yake hiyo kuwa siri ya mafanikio ya kampuni ya MeTL ya kukua kwa zaidi ya mara 60 katika kipindi cha miaka 15 tangu alipojiunga nayo kuwa ni kutumia vyema fursa zilizopo na pia hamu yangu ya kuwatumikia na kuboresha maisha ya watanzania.“Falsafa yangu kama mfanyabiashara sio kuridhika na mafanikio niliyonayo bali kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kufanikiwa zaidi.” Alisema.
  Chat
  Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (kulia). mara baada ya kutiliana saini mkopo wa Bilioni 300 za Kitanzania.
  speech
  Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (MB) akisoma risala yake kwenye hafla ya utiliaji saini wa mkopo wa Bilioni 300 za kitanzania kutoka Benki ya Rand Merchant ya Afrika Kusini (RMB) iliyofanyika kwenye hoteli ya Saxon jijini Johannesburg Afrika Kusini.

  0 0

   
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini pamoja na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwa ajili ya viongozi wa SADC wanaohudhuria mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akiwakaribisha viongozi wa KAAT walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba na Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akifurahia jambo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
   Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
   Bw. Bukheti Juma (Kulia) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba akiwasikiliza.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akitilia mkazo umuhimu wa jamii kusaidia wazee wasiojiweza, wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
  Baadhi ya wanachama wa KAAT wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Katikati).

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na KilimoTanzania Bw. Daniel Machemba akiongea na waandishi habari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa waandishi kuhusu maonyesho ya bidhaa za Kichina, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Uchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu China nchini Tanzania Bi.Wang Fang, na kulia kwake ni Bi Rehema Mtingwa Afisa wa Mawasiliano kutoka TPSF.
   
   Baadhi wa washiriki waliohudhuria kwenye mkutano wa waandishi kuhusu maonyesho ya bidhaa mbalimbali  za Kichina yatakayoanza tarehe 21 hadi 24 mwezi huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

   Mwakilishi wa Uchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu China nchini Tanzania Bi.Wang Fang akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani).
   Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na KilimoTanzania Bw. Daniel Machemba akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya mkutano na Waandishi.

  0 0

   Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari ,utamaduni na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa timu ya wasichana ya Temeke Fatuma Issa baada ya kuibuka mabingwa. naeshudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso. 
   Makamu mwnyekiti wa chama cha soka cha wanawake Tanzania Rose Kisiwa akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa timu ya mkoa wa kisoka Kinondoni Fred Mazuri  Baada ya kuibamiza Ilala 5 – 3, Jumapili jijini Dar-es-Salaam. 
  Wachezaji wa timu ya mkoa wa kisoka ya Kinondoni wakishangilia ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 baada ya kuifunga timu ya Ilala 5 – 3, Jumapili jijini Dar-es-Salaam.

  Kinondoni yatwaa ubingwa ARS 2014
  Timu ya Kinondoni wavulana imetwaa uchampioni wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ngumu ya Ilala 4-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

  Mechi hiyo iliyotanguliwa na shamra shamra za maandamano na halaiki, ilikuwa yenye upinzani mkali na baada ya kosa kosa za hapo na pale Kinondoni walipata goli katika dakika ya 31 kupitia kwa Kassim Kitwana kwa shuti kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Ilala Sulum Siasa. 

  Goli hili lilibadili kasi ya mchezo huku Ilala wakitafuta goli la kusawazisha na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 40 baada ya kutoke piga ni kupege golini mwa timu ya Kinondoni na mchezaji hatari Juma Yusufu kufunga kwa huti la karibu.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliamba kwa zamu lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata goli la kuongoza hadi dakika ya mwisho. Ndipo refa akaamua kumaliza ubishi kwa penati.Katika penati tano, Kinondoni walifunga kupitia kwa Abdul Malangali, Milaji Gwangaya, Omri Rashid na Abubakari Nuru wakati Kassim Kitwana alipaisha. Kwa upande wa Ilala waliofanikiwa kufunga ni Abdul Bitebo na Rashid Mohamed wakati Maisala Adam na nahodha wa timu Shaban Zuberi walikosa.

  Akifunga fainali hizo za taifa za Airtel Rising Stars, mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Professor Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mheshimiwa Juma Nkamia, aliipengeza kampuni ya Airtel kwa kujitokeza kusaidia maendeleo ya soka hapa nchini.

  Alitoa wito kwa vijana kuzingatia nidhamu katika michezo na kujituma ili kupata mafanikio na kusema kuwa katika dunia ya leo soka ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi. Pia alisema kuwa kufanikiwa kwao kutaiwezesha Tanzania kufahamika zaidi kimataifa. Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendelea kudhamini mashindano ya vijana ya Airtel Risig Stars.  

  0 0

  Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.

  WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ameipongeza Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kuandaa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF ikiwa ni fursa itakayowainua kiuchumi wastaafu hao. 

  Waziri Kabaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa rasmi mpango wa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF, mpango utakaowawezesha wastaafu sasa kuchukua mikopo na kuendelea kukidhi maitaji yao kipindi hicho. Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Waziri Kabaka alisema Benki ya Posta na Mfuko wa Penseni wa LAPF hauna budi kupongezwa kwa hatua ya kulikumbuka kundi la wastaafu ambalo kimikopo lilikuwa limesahaulika.

   “…Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru Benki ya Posta Tanzania pamoja na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa kubuni mpango huu maalum wa kuwasaidia wastaafu kimaisha na kuwawezesha kumudu gharama za mahitaji yao na kukabiliana na ukosefu wa muda mfupi wa fedha wanazohitaji kwa kuwapatia mikopo,” alisema Waziri Kabaka. Aliongeza kuwa mpango huo utawasaidia wastaafu kipindi cha maisha yao mapya ya kustaafu kwani licha ya muda huo wengi kuwa na kipato kidogo cha mapato lakini gharama za maisha kwao hazipungui na badala yake huendelea kupanda, jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwao.

   “…Ninafarijika kuona kwamba Benki ya Posta pamoja na LAPF mmeliona hili na kulifanyia kazi, na hatimaye kuja na huduma hii ya mikopo. Lengo mahususi la mpango huu ambao kwa kiasi fulani umeanza kutekelezwa ni kuwapa faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali, ili kuweza kuboresha maisha yao na maslahi kwa ujumla,” alisema waziri huyo. 

  Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla hiyo, alisema mkopo huo ni wa kwanza na wa aina yake katika soko la mabenki nchini hivyo wanaamini utatoa hauweni kwa wastaafu wa LAPF. 

  Akifafanua zaidi alisema mstaafu anayehitaji kuwa na dhamana huku riba inayotozwa kwa mkopo huo kuwa ni ndogo yaani asilimia 12 tu kwa mwaka ukilinganisha na mikopo mingine. “…Mkopo huu umewekewa bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea kudaiwa. Hivyo wastaafu wote wa mfuko wa LAPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu,” alisema Moshingi. 

  Alisema huduma za mikopo hiyo ni za haraka na bora na zitatolewa kwa matawi yote ya Benki ya Posta Tanzania hivyo kuwataka wahitaji wote wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF kwenda katika matawi hayo popote nchini kupata maelezo ya nini cha kufanya kabla ya kupata mkopo huo. 

  Hata hivyo TPB kwa kushirikiana na LAPF wamezishauri taasisi za fedha nyingine zikiwemo Benki kuangalia namna ya kuweka mipango ya kusaidia wastaafu nchini kwani kundi hilo lina kiasi kikubwa cha fedha ambacho kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchango mkubwa katika uchumi wan chi ya Tanzania. 

  Hafla hiyo pia iliyohudhuriwa na viongozi waandamizi na wafanyakazi wa TPB na Mfumo wa Penseni wa LAPF ilishirikisha pia baadhi ya wastaafu ambao baadhi walieleza wameanza kunufaika na mpango huo wa mikopo kwa wastaafu. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

older | 1 | .... | 344 | 345 | (Page 346) | 347 | 348 | .... | 1897 | newer