Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA WAPYA 20 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda,  Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose Migiro, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu,  Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu Jaji  Frederick Werema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein kattanga  katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama kuu ya Tanzania baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Kuu Tanzania na Majaji  wapya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  majaji wapya 
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa na Majaji wapya 
 Rais Kikwete na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro wakiwa wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wanawake wapya
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa katika pic ha ya jumla na Majaji wapya na wa zamani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WACHEZAJI WA SIMBA KAMILI YAENDA ZANZIBAR KUWEKA KAMBI YA MAZOEZI

$
0
0
 Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe (wa pili kushoto) akiwa na wachezaji wenzake.
 Wachezaji wa Simba wakiwa wamepozi kwa picha.
Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa katika boti kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda kuweka kambi ya Mazoezi Zanzibar.
 Baadhi ya wachezaji wa Simba wakielekea kupanda boti katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya safari ya kwenda Zanzibar kwenye kambi ya mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanzai hivi karibuni. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa wamepozi kwa picha.

KIONGOZI WA NGOMA AFRICA BAND KAMANDA RAS MAKUNJA AFUNGUKA !

$
0
0
KUHUSU HAKI YA URAIA NA URAIA PACHA ! 
SI SWALA LA WENGI WAPE BALI NI HAKI YA BINADAMU NA PIA URAIA!
WENGI WANAHITAJI KUELIMISHWA!

MTAZAMO WA KATIBA MPYA NA MTANZANIA KWANZA

Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mtunzi,mwimbaji kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma africa band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, amefunguka na machache yafuatayo kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania na haki za raia wa Tanzania:

Akizungumza kutoka katika makao yake mjini Oldenburg,Ujerumani.
Kamanda Ras Makunja wa kikosi kazi FFU-Ughaibuni alisema
Kuwa: MCHAKATO WA KATIBA MPYA UMEWAFANYA WATANZANIA
WENGI KUSOMA KATIBA YA ZAMANI ! MWANZO WALIKUWA HAWAISOMI NA KULIELWA VEMA ! 
Kwa sasa ! WATANZANIA HATUNA HAJA YA KUOGOPA  MAUMIVU YA 
MABADILIKO YA KATIBA LAZIMA TUENDE KUFUATANA NA WAKATI,
LAZIMA TUWEKE MASALAHI YA TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA,

Ras Makunja,alichambua zaidi kwa kusema kuwa watanzania tumekuwa tunatabia za uwoga wa maumivu ya mabadiliko linapokuja swala la kujadili masilahi ya kitaifa na mtanzania,mara nyingine bila ya kujijua tunawapigania
watu ambao sio walengwa katika katiba "Nina maana walengwa wa kunufahika katika katiba hii lazima wawe watanzania wote wa bara na visiwani ambao wanaishi popote pale duniani" bila kujali dini,jinsia au
vyama vyao vya kisiasa.

SWALI: NINI ? MTAZAMO WAKO NA UNATARAJIA NINI ? KATIKA KATIBA MPYA ?

RAS.MAKUNJA: Mtazamo wa wangu katika kulijadili hili la katiba mpya ningewaomba kwanza wale wabunge walio katika bunge maalumu la katiba
kwamba : WAFANYE KILA HALI KATIKA MJADALA HUU KUPATA KATIBA
YENYE MASILAHI 99% TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA

Mfano: Haki za kumiliki Ardhi,tunapoongelea swala la Haki ya mtanzania
basi Ardhi na maslahi yanayo patikana katika Ardhi lazima yamilikiwe na
raia wa Tanzania kwanza,kwa sababu Ardhi ndio msingi au ubongo wa nchi yetu,kwa maana hii asilimia kubwa ya ardhi kama haipo katika miliki ya raiawa Tanzania ,uhuru wetu unatakuwa umepungua maana.
 
ARDHI NA RAIA WA TANZANIA NDIO MOYO WA TAIFA NA UTAWALA
WA TANZANIA,asilimia 50% ya Adhi ikiwa mikononi mwa watu ambao sio
watanzania,au watu ambao wana offer za kukaa au kufanya jambo katika
ardhi kwa mktaba wa miaka mingi ,wananchi tutajikuta tupo ugenini katika ardhi yetu.HII HAINA MAANA KUWA TUNAWAFUNGIA MILANGO WAWEKEZAJI BALI TUNAWEZA KUINGIA NAO MIKATABA YA MUDA MFUPI .

SWALI:  KUHUSU URAIA PACHA UNALIONAJE HILI?

RAS MAKUNJA: SIO SWALA LA WENGI WAPE ! NA WACHACHE WANYIME BALI SWALA LA HAKI YA BINADAMU NA URAIA

WATANZANIA LAZIMA TULITAZAME SWALA URAIA PACHA KWA FAIDA YA TANZANIA NA PIA TULICHAMBUE HASARA NA FAIDA ZAKE.
Ras Makunja aliingia kwa kina kwa kusema kuwa kuhusu uraia pacha
walio wengi wanahitaji kuelemishwa faida na hasara zake,pamoja na haki
za msingi kwa watanzania wanaomba hili liwemo katika katiba mpya.
Kwanza tunapolizungumzia hili lazima tujue nini ?maana uraia na nini maana Pasipoti.
 
Historia inaonyesha kuwa matumizi ya PASIPOTI yalianza mapema mwaka
1910 SOVIET UNION (URUSI) ndio walioanzisha kwa nia ya kuwathibiti raia
wao katika mfumo wa kikomunisti,baada ya hapo ndipo madola mengine yakafuata;Leo tunapoongelea uraia pacha wengine wanachanganya pasipoti tu za kusafiria na kusahau haki za uraia na binadamu kwa ujumla.
Katika kanuni za haki za binadamu hairuhusiwi mtu kunyang'anywa uraia wake,Mimi ningeshauri kuwa katiba mpya iruhusu raia watanzania waweze kuwa na pasipoti zaidi ya tatu,kwa sababu zitawasaidia katika maswala la maendeleo,kama vile uchumi,elimu n.k
 
MFANO HAI KUNA WATOTO WALIOZALIWA NJE YA NCHI  WAZAZI WAO WOTE NI WATANZANIA LAKINI WANAKOSA HAKI KATIKA NCHI WALIOZALIWA KWA KUWA SI RAIA WA NCHI HILE,NA WANAPOTIMIZA MIAKA 18 WANASHINDWA KUUKANA URAIA WA TANZANIA NA KUOMBA WA NCHI WALIOZALIWA JAPO NCHI WANAYOISHI WANAWEZA KUWA RAIA PACHA.
 
Watoto hawa wanasulubiwa kwa kuhukumiwa makosa ambayo hawajafanya ! kwani awakuomba wazaliwe ughaibuni,watanzania katika katiba mpya lazima tuwafikirie watoto hawa wasio na hatia.
Hata katika kanuni za haki za binadamu zinasema kuwa "Si ruhusa kwa binadamu yeyote yule kunyanga'nywa uraia wake.Sasa mtoto wa kitanzania
akiwa hana haki ya kuwa mtanzania kwa kuwa kazaliwa nje ya nchi ! hii si haki.
 
(B) Muwekezaji wa Kigeni anapokaribishwa Tanzania kwa maneno ya "Jisikie upo Nyumbani ! na mtanzania hakubaliki kwao hapa kidogo pana utata lazima patazamwe upya.

Kwa sasa kuna nchi nyingi duniani ambazo katika katiba zake zinasema kuwa raia wa nchi hizo harusiwi kuny'angwa uraia wake ata kama anaomba uraia wa nchi nyingine,sisi bado tunaogopa kulijadili kwa visingizio vya usalama.
Kwa Sasa hatuna adui kama ilivyokuwa zamani tuliofu makaburu n.k
Adui wetu wa sasa ni NJAA NA UMASIKINI na Uraia pacha unaweza kuwa silaha kubwa ya kupiga vita adui zetu hawa NJAA,UMASIKINI.

TUNAWEZA KUWEKA MASHARTI KWA WALE WATAKAO KUWA NA URAIA PACHA(Ras Makunja alisisitiza)
Mfano: Mtu akiwa na uraia pacha hawezi kugombea nafasi za juu ya uongozi wa taifa kama vile mbunge,diwani,rahisi.
Au kufanya kazi katika sekta ya usalama na mambo nyeti yanayo husu taifa.
huu ni mfano tu. Uraia pacha si swala la kuliogopa bali kuelimishana.

SWALI : MATEGEMEO YAKO ? KUHUSU KATIBA MPYA.

Ras Makunja: Ni mategemeo yangu kuwa wabunge katika bunge maalumu la katiba wataweka maslahi ya Tanzania na watanzania kwanza na kuondoa itikadi zao za ki-vyama kama tunanyoona sasa. Tunategemea watatuletea rasimu ya mapendekezo ya katiba yenye masilahi ya Taifa na watanzania kwanza
si vinginevyo. mwanamuziki huyo alimalizia.

TANZANIA MWENYEJI WA MASHINDANO YA 8 YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
 Mkuu wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya Majeshi Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkuta huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.

 Waandishi wa Habari kutoka vyombo tofauti wakimsikiliza Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman (hayupo pichani) katika Mkutano wake na wandishi leo.
 Mkurugenzi wa ufundi wa mashindano hayo upande (JWTZ) Luteni  Kanali Joseph Bakari akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo.

 
==========  ==========
Na Miza Othman Makame   Maelezo- Zanzibar .
      
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Michezo ya nane ya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 18 mwezi  huu.  

Akitoa Taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  Makao Mkuu ya Brigedi Migombani kwa waandishi wa Habari, Mkuu wa Brigedi hiyo Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman amesema lengo la michezo hiyo  ni kujenga  mashirikiano kati ya Majeshi na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema katika Michezo hiyo kutakuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa na wote watakuwa washindi, lengo ni kujenga uweledi na nidhamu ndani ya majeshi yetu.

“Hii ni fursa ya wanajeshi wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana pamoja kama tunavyofanya katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi”, alisema Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman. 

Amezitaja Nchi za Jumuiya hiyo zitakazoshiriki  Michezo hiyo kuwa ni wenyeji Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya  na Uganda.  Amesema Michezo itakayochezwa na wanajeshi hao ni  Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu  na Mbio za nyika  na ameelezea viwanja vitakavyofanyika kwa ajili ya michezo hiyo  Polisi ziwani ,Vyuo vya Mfunzo Kilimani, JKU Saateni, Pamoja na Viwanja vya Zimamoto na Uokozi.

Brigedia Jenerali Sharif Sheikh ambaye pia ni Makamo  Mwenyekiti wa Michezo hiyo, amewataka  Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuona vipaji vitakavyoonyeshwa na wanajeshi kutoka Nchi hizo .

 Akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo Leftinenti Kanali Joseph Bakari amesema pamoja na micheo hiyo kutakuwa na Burudani ya Ngoma za Utamaduni kutoka Vikosi vya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema jumla ya wanamichezo 505 wakiwemo Viongozi kutoka Nchi hizo watashiriki michezo hiyo itakayodumu kwa muda ya wiki mbili.                                                                 

INTRODUCING NEW SONG MAUMIVU -BOB JUNIOR AND ROMA

NEWS ALERT: MOTO WATEKETEZA KITUO CHA KUPOZEA UMEME CHA MJINI MOSHI ASUBUHI HII

$
0
0

Askari wa kikosi cha Zimamoto wakifika eneo la tukio asubuhi hii
Wananchi wakishuhudia juhudi za kuzima moto huo
Moto ukiendelea 
Juhudi zikiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
Transforma zinazosambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro zilizoko eneo la Bomambuzi zimewaka moto asubuhi hii muda mfupi baada ya kutokea shoti ambayo haijafahamika chanzo chake ni nini. 

 Moto huo umetokea majira ya saa 1:10 na kusababisha maeneo kadhaa ya mji wa Moshi kukosa umeme hadi sasa. 

 Globu ya jamii imeshuhudia kikosi cha zimamoto kutoka manispaa ya moshi kikijaribu kuzima moto huo ambao hata hivyo ulikwisha teketeza sehemu kubwa ya  kituo hicho cha kupozea umeme.

MAZOEZI REDD'S MISS TEMEKE YAPAMBA MOTO

$
0
0
 Warembo wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd's Miss Temeke, wakipozi wakati wa mazoezi  katika Klabu ya TCC, Chang'ombe, Dar es Salaam. Mashindano yatafanyika kwenye klabu hiyo, Agosti 22,mwaka huu.




marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la kiwengwa

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (wakatikati) katika ziara ya kutembele mabaa na mahoteli ya kitalii, kutokana na wananchi kulalamikia vitendo vya upigwaji wa ngoma na vitendo viovu, (kulia) Mkuu wa Wilaya Kaskani (B) Unguja Khamis Jabir Makame na kushoto ni Sheha wa Kiwengwa Bw. Maulid Masudi Ame huko Kiwengwa.
 Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Khamis Jabir Makame wakipapa maelezo kutoka kwa mmiliki wa Baa ya Vision Pub Francis Vicoguga juu ya undeshaji wa kazi zake katika Baa hiyo.
 Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk,akizungumza na wananchi na wamiliki wa mahoteli na baa katika kijiji cha Kiwengwa mara baada ya ziara yake ya kutembelea hoteli hizo.
 Mratibu wa Wanawake na Watoto Bi Mtumwa Rashid Khalifa ,mkaazi wa Kiwengwa akizungumzia kero wanazozipata kutokana upigwaji wa madisko katika mabaa kijijini hapo.(Picha na Jamila Abdalla – Maelezo Zanzibar).
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar. 15/8/2014.
Waziri wa Habari,Utamaduni , Utalii na Michezo Saidi Ali Mbaruok amepiga marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la kiwengwa mpaka pale Serikali ya wilaya itapo toa maelekezo maalumu ya upigaji wa disko hilo kwa utaratibu unao faa.
Agizo hilo amelitoa leo huko kiwengwa Mkoa wa kaskazini “A”wilaya ya kaskazini B Unguja katika Ofisi ya umoja wa maendeleo wa kijiji cha kiwengwa wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa mikahawa,na kumbi na starehe juu ya kukithiri wa upigaji wa magoma kucha.
Amesema amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji wa madisko usiku kutokana na kutokua na  utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku  haliambayo inapelekea wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa usingizi na kusumbuliwa wagonjwa wenye shindikizo la damu.
Amsema hali hiyo haiwezekani kuona inaendelea katika hali kama hiyo kwani inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wanchi na  raia kwaujumla.
 “Nimepokea messsege ya kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko,hili hiliwezekani liendelee”lisema Waziri.
Aidha alisema haiwezekani kuona utamaduni wa burudani unavurugwa kituambacho ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibuzao selka zao.
“kuazia leo napiga marufuku mpaka sheha wa shehia hii aridhie hata kama kuna kibali ,kwani sheha yeye ndio anae jua hali za raia wake kuna wagonja,na wenyemaradhi ya kuhitaji kupumzika hatutaki kuona masuala yasio na utaratibu.”aliongeza Waziri.
 “mimi kazi yangu ni kuutangaza utalii nasio utalii uharibiwe ,tufahamu kua ulalii Zanzibar ndio uchumi unao tegemewa kwa sasa kwa hivyo tulinde,”aliongeza Waziri Said.
Hata hivyo waziri huyo alichukia vitendo vya uwasharati vilivyo tapakaa katika kijiji hicho na kujenga mabaa karibu na nyumba za ibada kitu ambacho aliagiza kwa mkuu wa wilaya kuyafanyia kazi.
Nao wazazi wa kiwengwa Othumani mnyanja na mtumwa Rashidi walisema kiwengwa hivisasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko na kukosa masoma kitiambacho ni hatari kwao.
Aidha walisema kua watoto wao wakiwa na umri mdogo na kujishughulisha na masuala ya kimapezi jambo linalo wafanya nialama ya kupotea na kuacha mila za kislamu.
Wakitaja maeneo ya nayopigwa miziki na watoto wao kwenda ni pamoja na  maeneo yanayo pigwa madisko hayo ni pamoja na ,kigorofani, vishani wazalendo pub, Kamili View,Obama Baa na kigorofani eneo la mafarasi.
 Nae miliki wa ukumbi wa Disko wa PERUU B, Peruce Osward Buhoma  akiulizwa swali na waziri kwanini anafanya mazogo usiku alikiri kwa kusema hufanya hivyo kwaajili ya kuvuta wateja na kufanya ushindani kila mmoja kwajili ya  kusikika zaidi kuliko mweziwe.
Bibbi huyo na wezake walisema wanaweza kujirekebisha lakini pawe na utaratibu wa kupiga madisko kwa zamu na utaratubu mzuri utakao wekwa na uongozi.

Wahamiaji haramu 21 wanaswa wakiwa ndani ya roli la saruji

$
0
0
 
 Naibu Kamishna uhamiaji mkoa wa Njombe Bi. Rose Mhagama akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.


  Baadhi ya wakazi wa mjini Makambako Mkoani Njombe waliojitikeza kuwaangalia wahamiaji hao( kulia) na waliokaa ni raia wa Ethiopia mara baada ya kukamatwa na kufikishwa katika ofisi za uhamiaji za Makambako.


Na James Festo, Njombe.

IDARA ya Uhamiaji Mkoani Njombe, imefanikiwa kuwanasa wahamiaji haramu 21 walioingia nchini kwa kutumia roli la kubebea mifuko ya saruji ambalo lilikamatwa na maofisa uhamiaji katika eneo Mashujaa kwenye Halmashauri ya Mji wa Makambako.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Mkoani Njombe, Rose Mhagama alithibitisha kukamatwa na kushikiliwa kwenye kituo cha polisi Makambako wahamiaji hao ambao ni raia wa kutoka nchini Ethiopia.

Mhagama alisema askari wa kikosi cha uhamiaji mnamo Agosti 14,mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni wakiwa kwenye doria katika barabara kuu ya kutoka Makambako kwenda Songea walilishuku na kulisimamisha roli namba T587 CSN likiwa na tela namba T780 CHM lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Nyange na kuanza kulikagua.

Pasipoti Nne za Baadhi ya Wahamiaji Hao Waliokamatwa Mjini Makambako

 Alisema roli hilo aina ya IVECO mali ya Everest Flight LTD,  S.L.P 77004 DSM baada ya dereva huyo kusimamisha, askari hao walianza ukaguzi kwenye gari hilo, na baadaye walibaini kulikuwa na watu kadhaa wamefichwa.

Kufuatia kubaini kuwepo kwa watu hao, dereva wa roli hilo alipohojiwa alikiri kubeba watu hao, na kuwaeleza askari Uhamiaji kuwa alikuwa akiwasafirisha kwenda nchini Malawi kupitia mkoani Ruvuma.

"Dereva alipohojiwa alisema alikuwa anakwenda kukutana na mtu ambaye anahusika na watu hao akiwa mjini Njombe, ili aweze kuwashusha pale Njombe na waweze kuendelea na utaratibu wao walioupanga wa kwenda nchini Malawi," alisema Mhagama.

Naibu Kamishna huyo wa Uhamiaji alisema baada ya kuendelea kufanya upekuzi, askari wa uhamiaji waligundua kuwepo na watu 10 waliokuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo ya saruji, na ndipo dereva huyo aliamuliwa kulipeleka lori hilo kituoni.

"Baada ya kufika kituoni, askari wakiwa wanaendelea kuwashusha watu hao idadi yao iliongezeka na kufikia 21, dereva wa roli hilo alifanikiwa kutoroka na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumsaka ili aweze kufikishwa mahakamani," alisema Mhagama.

Mhagama alisema kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji hao, walipohojiwa walisema wameingia nchini wakitokea Mombasa nchini Kenya kupitia mkoani Tanga na kwamba walikuwa wakielekea nchini Malawi.
 
Orodha ya majina ya wahamiaji hao. 

Naibu Kamishna huyo wa Uhamiaji alitoa mwito kwa raia wema mkoani hapa kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwafichua wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia njia za panya. Alisema kuanzia kipindi cha Januari hadi Agosti, mwaka huu jumla wa hamiaji 25 walikamatwa na kuhukumiwa vifungo vya, ambapo  wahamiaji 24 walikuwa ni kutoka nchini Ethiopia na raia mmoja alikuwa akitoka nchini Congo.

Wakati huo huo, Mnadhimu wa jeshi la Polisi mkoani Njombe, SSP Yahaya Rajabu  alithibitisha kukamatwa na kushikiriwa kwa wahamiaji hao 21 kutoka Ethiopia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rajabu alisema wahamiaji hao walikamatwa katika mtaa na kata ya Mjimwema uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako majira ya saa mbili usiku.

MARIA SHILA NDIYE REDD'S MISS KINONDONI 2014

$
0
0
Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya  kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. 

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.
  Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (klatikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. PICHA ZAIDI: FATHER KIDEVU BLOG

TANZANIAN QUEEN MILLEN MAGESE SPEAKS KINDLY ABOUT LIVING WITH ENDOMETRIOSIS.

SUMATRA MKO WAPI?ABIRIA HAWA WAMETESEKA ZAIDI YA MASAA 6 BILA MSAADA

$
0
0
 Abiria wakwama njiani zaidi ya masaa 6  abiria ambao walikuwa wanaelekea mwanza na gari la princes shabaha  wamezidi teseka  huku  hawajui hatima yao ya safari.

 Gari hilo lenyenamba za usajili T102 AVX  Wamekwama maeneo ya kibamba jiji dar es salamu  huku kina mama na watoto wakizidi teseka


 Mama Huyu Akiteseka na mtoto mdogo
 Abiria wakiwa nje ya basi


 Baadhi ya abiria wakijadiliana nini cha kufanya ili wapate usafiri mwingine
 Hizi ndio namba za basi hilo




KANISA LA YESU CHRISTO LA WATAKATIFU WA SIKU ZA MWISHO WAFANYA UKARABATI JENGO LA YATIMA GROUP TRUST FUND MBAGALA CHAMANZI

$
0
0


Baadhi ya waumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakipaka rangi bweni la kituo cha watoto yatima cha yatima group trust fund kilichopo mbagala chamanzi ambapo waumini hawo walitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira mbalimbali ikiwemo kukata kuni pamoja na kucheza na watoto wanaoishi katika kituo hicho kama njia moja ya kuwafariji
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakipaka rangi bweni la kituo cha watoto yatima cha yatima group trust fund kilichopo mbagala chamanzi ambapo waumini hawo walitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira mbalimbali ikiwemo kukata kuni pamoja na kucheza na watoto wanaoishi katika kituo hicho kama njia moja ya kuwafariji
Muhumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho Charles Nyamuhanga akikati kuni kwa mashine kwa ajili ya watoto yatima wa group trust fund kilichopo mbagala chamanzi ambapo waumini hawo walitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira mbalimbali ikiwemo kukata kuni pamoja na kucheza na watoto wanaoishi katika kituo hicho kama njia moja ya kuwafariji
kuni zikikatwa.
Baadhi ya waumini wakinamama wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakimenya viazi kwa ajili ya kupika na watoto wa kituo cha Yatima group trust fund cha mbagala chamanzi Dar es salaam
waumini wakinamama wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakijadiliana mambo mbalimbali
Baadhi ya watoto yatima wanaoishi katika kituo hicho wakiimba na kucheza.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakiwa wamebeba kani kwa ajili ya shughuli za kituo cha watoto yatima cha
Yatima group trust fund cha mbagala chamanzi Dar es salaam

Watoto wa wahumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakicheza mpira wakati walipotembelea kituo cha watoto Yatima group trust fund cha mbagala chamanzi Dar es salaam.
Watoto wakicheza
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakiwa katika picha ya pamoja walipo tembelea kituo cha Yatima group trust fund cha mbagala chamanzi Dar es salaam

Wajumbe wa Bunge la Katiba waaswa kurejea Bungeni

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo.

Na Rose Masaka-MAELEZO
Viongozi wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  Jijini Dar es salaam.
Jaji Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.

“Sheria inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji Werema.

Pia Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.

Aidha, Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.

Rais Kikwete ahudhuria Mkutano wa 34 wa SADC Victoria Falls

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maua kutoka kwa watoto leo muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe ambapo atashiriki katika mkutano wa 34 wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika hoteli ya Elephant Hills, mjini Victoria Falls nchini Zimbabwe leo(picha na Freddy Maro).

shindano la Tanzania Movie Talents lafikia hatua ya mwisho.

$
0
0
Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakifuatilia Filamu fupi iliyochezwa na baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie talents (TMT) wakati ilipokua ikionyeshwa kwenye runinga kubwa katika Ukumbi wa Makumbusho. Kutoka Kulia ni Single Mtambalike au Rich Rich katikati ni Vyonne Cherry au Monalisa na Kushoto ni Jaji Mkuu wa Shindano hilo Roy Sarungi.
 Mahosti wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwajibika katika Jukwaa la Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea alhamisi iliyopita.
 Mmoja kati ya Washindi kutoka Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar Es Salaam katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Shiraz Ngassa (wa Kwanza Kushoto) akiongea na Msanii Joti mara baada ya Kuaga rasmi shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya alhamisi.
 Fredy Kiluswa ambae pia alikuwa mmoja kati ya Washindi watano kutoka Kanda ya Pwani katika Hatua ya kuwatafuta washindi wa Kanda akitoa maneno ya Shukrani mara baada ya kuaga shindano hilo kutokana na uchache wa kura alizopata.
 Baadhi ya washiriki wa kundi la Kwanza wakiwa mbele ya Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mara baada ya Filamu yao fupi kuonyeshwa.
Mwinshehe Mohamed ambae alikua mmoja kati ya Washindi wa Tatu kutoka Kanda ya Kati mkoa wa Dodoma akitoa pongezi na Maneno ya Shukrani kwa Timu nzima ya TMT mara baada ya kuaga shindano alhamisi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) waliofanikiwa kuingia hatua ya Fainali ambapo mshindi wa Shindano hilo linalotarajiwa kufikia Tamati Mnamo mwisho wa Mwezi wa Nane kwa Mshindi Kukabidhiwa Kitita Cha Shilingi Milioni hamsini za Kitanzani.Picha Zote na Josephat Lukaza - Proin Promotions ltd.

 
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limefikia hatua ya Mwisho kabisa mara baada ya washiriki kumi bora kupatikana katika Show ya Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Alhamisi.
Show hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda Mbili za Tanzania yaani Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika Kinyanganyiro hiko na Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao wameingia hatua ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.
Washiriki waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko ni Mwinshehe Mohamed ambae alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kati ambapo anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati kuondolewa na Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika Fainali hiyo. Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam. Kanda ya Pwani walichukuliwa washindi watano huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya Washiriki wanne kuondolewa katika kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani, Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati ya washindi watano kutoka kanda ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani katika Fainali kubwa ya Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika Mashariki na Kati la Tanzania Movie Talents (TMT).
Mpaka Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake wote watatu ndio wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi wote kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja na Hatimaye kuanza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Hivi Karibu.
Vipindi vya Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) vitaendelea kurushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku huku marudio yake yakiwa siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Siku ya Jumatano saa 5 usiku.
Ili Kuendelea kumuwezesha Mshiriki wako kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kwa Mwaka 2014 unachotakiwa ni kuendelea kumpigia kura kwa wingi kadri uwezavyo kwa Kuandika Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) Neno TMT acha nafasi ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 halafu tuma kwenda 15678 au unaweza kupiga kura pia kupitia Ukurasa wetu wa Facebook kwa kufungua kiunganishi hiki https://www.facebook.com/tztmt/app_316963748468949

MKURUGENZI REDIO 5 AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUANDIKA NA KUANDAA VIPINDI VYA KILIMO

$
0
0
IMG_0085
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kufanya hafla fupi iliyofanyika mjengoni kwao ,ya kuwapongeza kwa kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya mawasiliano na habari kwa ukanda wa kaskazini maonyesho ya nane nane, Pamoja na  David Rwenyagira aliyepata Tuzo za Tanapa hivi karibuni
IMG_0073
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis  akiwa anampongeza Mfanyakazi wa kituo hicho David Rwenyagira kwa kupata Tuzo na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na   Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni.

???????????????????????????????
Meneja masoko wa Tan media Bi.Sarah Keiya akiwa ameshikilia kikombe kabla ya halfa kuanza.
IMG_0088
???????????????????????????????
David Rwenyagira akiwa anatoa pongezi kwa Mkurugenzi wao kwa kuweza kuona mchango wao katika kampuni hiyo ambapo pia aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari hapa Nchini  kutoa ushirikiano kwa wanahabari wao katika kuibua habari za kijamii ikiwa nipamoja na kuwaezesha kufika vijijini
 
IMG_0024
IMG_0028
Bw Robert Francis akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari kuandika na kutangaza habari zinazohusu wakulima vijijini hali itakayosaidia kupatikana kwa  wataalam wa kuwasaidia katika kilimo ikiwa nikukuza ajira katika upande wa kilimo

Pia amewaomba  waandishi wa habari Tanzania kupeleka kazi zao katika mashindano mbalimbali hali itakayosaidia kujipima na kuongeza ujuzi zaidia huku akimtolea mfano mtangazaji wa kituo hicho David Rwenyagira aliyepata TUZO na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na   Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni
IMG_0017
Watangazaji wa kituo hicho wakiwa katika halfa
IMG_0014
IMG_0011
 
IMG_0003
IMG_0030
Ulaji ulikuwa hivi..
IMG_0037
IMG_0036
IMG_0034
IMG_0032
IMG_0031
IMG_0038
IMG_0042
Mtangazaji Clara Moita akiwa anajipakulia katika halfa
IMG_0048
IMG_0049
Semio Sonyo wa kipindi cha Love cuts akiwa anafanya yake
IMG_0055
IMG_0078
IMG_0076
Wafanyakazi wakiwa katika nyuso za furaha baada ya halfa
IMG_0060
IMG_0082
IMG_0080
IMG_0090
(  Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Watafiti Afrika waelezwa kutoa tafiti zenye uhusiano na jamii

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, akihutubia wakati akifunga Kongamano la 25 la Wajiolojia Barani Afrika lililofanyika tarehe 14-16 Jijini Dar es Salaam. Wakati akifunga Kongamano hilo, Waziri Pinda amewataka watafiti barani Afrika kufanya tafiti ambazo zina mahusiano ya moja kwa moja na jamii ili tafiti hizo zitumike katika kuwazesha wananchi kufaidika na rasilimali zilizopo barani Afrika
 Baadhi ya Wajilojia kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanaohudhuria Kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika wakifuatilia hotuba ya kufungamano hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajiolojia waliohudhuria kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Sadik Meck Sadik na Rais wa Wajolojia Afrika Profesa  Aberra Mogassie.
 

Watafiti Afrika waelezwa kutoa tafiti zenye uhusiano na jamii

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Wajiolojia barani Afrika wametakiwa kufanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii na kuzionesha tafiti hizo ili ziweze kutumiwa  kama ufumbuzi wa  matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la hilo, jambo ambalo litaiwezesha  Afrika  kunufaika  na rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi , maendeleo ya watu na mapato ya mataifa yao.

“Najua watafiti wanaweza kusema serikali zetu hazitumii tafiti zetu, lakini mkifanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii, mkazitoa kwa jamii tutazitumia msizifungie makabatini,” amesisitiza Pinda.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda  leo jijini Dar  es Salaam wakati akifunga kongamano la 25 la Wajiolojia barani Afrika  na kueleza kuwa, ili Afrika  iweze kuendelea na kufaidika na rasilimali zake, inahitaji kuzalisha wataalamu wengi  katika taaluma ya sayansi ikiwemo wajiolojia.

“Hapa nchini Tanzania Profesa Muhongo anapambana sana na taaluma hii, jambo hili litasaidia kuzalisha wataalamu wengi katika sekta za mafuta na gesi. Lakini na ninyi, mnahitaji kuzalisha wataalamu ili tuisogeze mbele Afrika,” alibainisha Pinda.

Ameongeza kuwa, serikali ya Tanzania tayari inajipanga katika kuhakikisha inazalisha watalaam wengi wa sayansi kupitia programu za Vyuo Vikuu ambapo tayari imeanzisha masomo ya mafuta na gesi katika baadhi ya vyuo vikuu nchini, hususani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ikiwemo kampeni ya kuhakikisha kwamba kila shule ya sekondari inakuwa na maabara ambazo zitachochea kizazi cha wanasayansi.

Vilevile, amezungumzia  tatizo  la Afrika kutokufaidika na rasilimali  zake zilizoko ardhini  na kuongeza  kuwa,  linatokana na matumizi kidogo ya sayansi  yanayofanywa na nchi nyingi za Afrika,  hivyo,  amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanatoka na njia ambazo zitasaidia na kuliwezesha bara hilo kuitumia sayansi kwa maendeleo ya nchi zao kwa sasa na kwa kizazi kijacho.

Aidha, amewataka wataalamu hao kutumia kuitumia taaluma hiyo zaidi ya inavyotumika sasa ikiwemo kuhakikisha kwamba afrika inasimama imara kupitia rasilimali zilizopo na kuiondoa katika matatizo ya kiuchumi, kiafya na kimazingira.

Halikadhalika, amewataka wataalamu hao, kufikiria namna ambavyo nchi za afrika zitasimamia suala la uthaminishaji madini katika nchi zao kwa kuhakikisha kwamba, shughuli za uthamini madini zinafanywa ndani ya Afrika tofauti na sasa ambapo nchi nyngi bado zinasafirisha madini nje bila kuyathamini  jambo ambalo linachangia katika kuzikosesha nchi hizo mapato stahiki yanayotokana na rasilimali hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini,  Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika mkutano huo, amewataka wajilojia Afrika kufanya tafiti nyingi za kutosha ili kujua kiasi cha mafuta na gesi ambacho bado  kipo Afrika lakini bado hakifahamiki ili rasilimali hizo  zisaidie kubadilisha taswira ya afrika.

Ameongeza kuwa, Afrika inatakiwa kujikita zaidi katika kuzalisha wataalamu wa kutosha na kujua namna ya kuziendelea rasilimali hizo wakati huo huo ikihakikisha kwamba, zinchangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi, kuvutia uwezaji na kuchangia katika maendeleo ya watu.

Ameongeza kuwa, bado afrika inazalisha kiasi kidogo cha nishati ya umeme wakati dunia inahitaji nishati hiyo kwa kiasi kikubwa hivyo, amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanasaidia katika kuwezesha upatikanaji wa rasilimali hiyo kupitia taaluma zao.

Vilevile, amewataka wajiolojia afrika kuipa kipaumbele miradi ya umeme vijijini katika nchi zao, na kuhakikisha kwamba, miradi hiyo kama ilivyo miradi ya REA nchini, inafanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwemo kufanya tafiti kuhusu miradi hiyo.

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo amekitaka  Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Dodoma kulifanyia kazi suala la ukosefu wa wahadhiri katika vyuo hivyo  katika fani za mafuta na gesi na wizara imehaidi kuhakikisha kwamba inawezesha upatikanaji wa wakufunzi katika masomo hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Naye Mhadhiri wa  Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam Profesa Nelson Boniface,   ameeleza kuwa, kongamnao hilo la siku tatu la wajiolojia barani Afrika limewawezesha washiriki kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu taaluma hiyo yakiwemo kyanayohusu  nishati mchanganyiko, namna ya namna jilojia inavyoweza kusaidia matatizo ya umaskini, maji, afya na mengineyo yalijadiliwa katika kongamano hio.

Profesa Boniface ameongeza kuwa, washiriki wa kongamano hilo walijadili na kuona kwamba, uwepo wa  wataalamu waliobobea katika taaluma hiyo ni  jambo la msingi kutokana na nafasi na mchango wao katika kuendeleza , namna ya kutumia  Afrika na dunia zinavyoweza kufaidika  na rasilimali hizo.

Akielezea kuhusu mkutano wa Tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani  ambao ulitangulia kabla ya kongamano hilo, ameleza kuwa,  mkutano huo uliweza kuwapa nafasi vijana kujadili masuala mbalimbali kuhusu namna jiolojia inavyoweza kuchangia kuondoa umaskini na kuwezesha maisha bora kwa jamii ya Afrika inavyoweza kunufaika na rasilimali asilia na masuala mengine muhimu.

Kongamano la 25 la Wajilojjia Afrika limewakutanisha wajiolojia  waliobobea katika taaluma hiyo kutoka nchi zaidi ya 42 Afrika na duniani . Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imewezesha kufanyika kwa kongamano la wajilojia uliokuwa ufanyike nchini Brazil.

Aidha, mikutano yote miwili imedhaminiwa na taasisi na makampuni mbalimbali, ambapo pia kampuni inayofanya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta ya BG-Tanzania ilikuwa ndio mdhamini mkuu wa kongamano hilo.

kongamano lingine la Wajiolojia Afrika linatarajiwa kufanyika nchini Afrika kusini.
 


TANZANIA HAINA UGONJWA WA EBOLA, UDHIBITI VIWANJA VYA NDEGE NA MIPAKANI WAIIMARISHWA.

$
0
0
Mtaalam wa ufuatiliaji wa magonjwa ya binadamu wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vida Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu historia ya ugonjwa wa Ebola, Virusi vyake , dalili na namna unavyoenea wakati wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo jijini Dar es salaam. 
 .Mkurugenzi wa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Binadamu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Janeth Mghamba akifungua  wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa ugonjwa wa Ebola jijini Dar es salaam.
Afisa Afya Mkuu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anayeshughulikia maeneo ya Bandari, Viwanja vya ndege na mipakani Dkt. Chacha Mung’aho  akizungumza namna walivyojipanga kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola  kupitia wasafiri wanaoingia nchini Tanzania.
 Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo.
 
 
TANZANIA HAINA UGONJWA WA EBOLA, UDHIBITI VIWANJA VYA NDEGE NA MIPAKANI WAIIMARISHWA.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
17/8/2014.Dar es salaam.

Imeelezwa kuwa Tanzania kwa sasa haina  raia yeyote  aliyeingia nchini kutoka mataifa mengine aliyebainika kuwa na maabukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Ebola kufuatia zoezi linaloendelea la uchunguzi wa wasafiri wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege na maeneo mengine.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na wataalam wa ufuatiliaji wa magonjwa ya binadamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanaoshughulikia magonjwa ya milipuko wakati wa mafunzo kuhusu ugonjwa  wa Ebola kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Wamesema kuwa ugonjwa huo licha ya kuleta madhara na maafa makubwa katika maeneo ya nchi za Afrika Magharibi kama zinavyoonyesha taarifa za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) bado haujaingia nchini Tanzania na kuongeza kuwa tayari Serikali kupitia wizara ya Afya imechukua  hatua za udhibiti  kupitia timu ya wataalam wa afya walio katika maeneo mbalimbali nchini.

Dkt. Chacha Mung’aho ambaye ni Afisa Afya Mkuu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anayeshughulikia maeneo ya Bandari, Viwanja vya ndege na mipakani akizungumzia namna walivyojipanga kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola  kupitia wasafiri wanaoingia nchini Tanzania amesema kuwa  tayari Serikali imetenga maeneo maalum, vifaa vya uchunguzi na huduma kwa wasafiri watakaobainika kuwa na dalili za maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema kuwa wataalam waliopo kutoka Wizara ya Afya wanaendelea  kushirikiana na wenzao wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege, Uhamiaji na Wizara ya Kilimo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuendesha zoezi la uchunguzi wa afya ili kupata taarifa za wasafiri kulingana na mataifa wanayotoka.

“Kwa sasa tunafanya kazi kwa kushirikiana na tunapata taarifa sahihi za abiria kutoka kwa mashirika ya ndege wanayotumia kusafiria jambo linalotusaidia kuwabaini wasafiri waliotoka katika nchi za Liberia, Ivory Coast na Guinea zilizoathiriwa na ugonjwa huo” Amebainisha Dkt. Chacha.

Amesema tangu kugunduliwa kwa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka huu huko Afrika Magharibi mataifa  mbalimbali duniani kote yamekuwa katika mapambano kudhibiti ugonjwa huo kuendelea kusambaa na kuleta maafa katika maeneo mengine duniani ambako haujafika.

Naye Dkt. Vida Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu historia ya ugonjwa wa Ebola, Virusi vyake , dalili na kuenea kwake amesema kuwa kwa mara ya kwanza uligunduliwa mwaka 1976 nchini Zaire maeneo ya mto Ebola ukihusishwa binadamu kula nyama ya wanyama jamii ya Sokwe, Nyani na Popo.

Amesema kuwa katika nchi za Afrika ya Magharibi ambako sasa ugonjwa huo umeshika kasi chanzo kimetajwa kuwa ni binadamu kula nyama ya wanyama jamii ya Sokwe na Popo huku wengine wakiambukizana kupitia kugusana na mgonjwa, majimaji, kushika damu ya mgonjwa, mate, mavazi au mwili wa mtu aliyekufa kwa Ebola.

Kuhusu kipindi cha mgonjwa kuanza kuonyesha dalili za kuambukizwa ugonjwa huo kinaazia siku ya 2 hadi ya 21 na kufafanua kuwa dalili hizo huambatana na kutokwa na damu zehemu za wazi, maumivu makali ya mwili na kichwa na kuongeza kuwa mgonjwa asipopatiwa tiba ya dalili hizo mapema hupoteza maisha.

Amesema serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari juu ya namna ya kujikinga na kuchukua tahadhari na  endapo watabaini uwepo wa mtu mwenye dalili za Ebola pia kuratibu mipango yote ya vifaa tiba,matibabu na mazishi endapo ugonjwa huo utaingia nchini kupitia kamati ya maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu .

Aidha, amesema licha ya ugonjwa huo kuibuka na kupotea katika vipindi tofauti katika mataifa mengine ya bara la Afrika na nchi jirani  za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda , wataalam hapa nchini wanaendelea kufanya utafiti juu ya chanzo kinachohifadhi Virusi hao kutokana na tabia yao ya kupotea katika kipindi fulani na kuibuka tena.

JAJI BWANA NDIYE MWENYEKITI MPYA BARAZA LA CHUO KIKUU HA BAGAMOYO (UB)

$
0
0
BODI ya Wadhamini ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), imemteua  Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini, Dk.Stephen Bwana Kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Mikocheni Dar Es Salaam, Dk.William Kudoja alisema  Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho ambayo Inaongozwa na Professa Paramaganda Kabudi Ndiyo ilimteua Jaji Bwana kushika wadhifa huo mpya baada ya kuona Ana sifa za vigezo Vya kushika wadhifa huo.

Dk.Kudoja ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Taaluma, alisema jaji Bwana ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa  ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia.

Jaji Bwana aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Kama Jaji wa Mahakama Kuu  Seychelles 1994-1999, Jaji wa Mahakama Rufaa ya Seychelles 2004-2009 , Kaimu wa Rais wa Mahakama hiyo ya Rufaa ya Seychelles kuanzia  Mwaka 2006-2008.

Mbali na kushika nyadhifa hizo Jaji Dk.Bwana  pia aliwai Kuwa Mshauri wa Benki ya Dunia kuhusu  Uboreshaji  wa Shughuli za Mahakama Afrika Kati ya Mwaka 2003-2008, Msajili wa Mahakama ya rufaa nchini Mwaka 1989-1994 na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania  Mwaka 1989  na Hakimu na Hakimu Mkazi Mwaka 1974.

Dk.Kudoja alisema Mwenyekiti huyo wa Baraza la UB, Jaji Bwana atawaongoza wajumbe  wajumbe 19 wa Baraza Hilo kutekeleza majukumu hayo ambao nao wanapitishwa na Bodi ya Wadhamini wa chuo hicho na watatekeleza majukumu waliyopewa.

Mbali na Jaji Bwana  Alisema wajumbe wa Baraza Hilo ni Profesa Esther Mwaikambo kutoka Taasisi ya Vyuo Vikuu Binafsi(IES), Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya juu nchini, Dk.Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Emmanuel Ole Naiko, Vicent Jonas, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, George Simbeye, Wakili Mwandamizi wa Serikali Malata Gabriel , Mhadhiri wa Sheria wa chuo hicho, Baraka Mkami, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, Makamu Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Costa Mahalu, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila, Dk.William Kudoja.

Aidha Alisema wajumbe wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine  anayeshughulikia Taaluma Profesa Peter Gillah, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Johnson Lukaza, Mathias Massawe, Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Katika Wizara ya  ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Evelyn Mbede, Balozi na Wakili mwandamizi nchini Mwainaidi Sinare Maajar, Wakili wa kujitegemea Vulfrieda Mahalu na Mkuu wa Shule ya Elimu ya UB, Profesa Elias Bayona.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images