Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 345 | 346 | (Page 347) | 348 | 349 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Vuga kuhusu Ugonjwa wa Ebola na mikakati ambayo SMZ inaendelea kuichukuwa ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari, hadi sasa hakuna mgonjwa alieyegundulikana na ugonjwa huo Zanzibar.
  NA/JAMILA ABDALLA –MAELEZO ZANZIBAR.

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imeanza kuchukua hatua mbali mbali za kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Ebola ambao unazidi kusambaa katika nchi mbali mbali Barani Afrika.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar kuhusiana na mikakati ambayo SMZ inaichukua ili kukabiliana na ugonjwa huo.

  Waziri Aboud amesema licha ya kwamba Zanzibar hakuna Mgonjwa aliyegundulika kuwa na Ebola lakini mazingira yanaonesha kuwa Zanzibar inaweza kupata maradhi hayo kutokana na kuwa na muingiliano mkubwa na nchi nyingine ambazo tayari zimethiriwa na Ugonjwa huo.

  Ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari juu ya maradhi ya Ebola na namna ya kujikinga.

   Mh: Aboud amesema kuwa pia serikali itaimarisha taratibu za ugunduzi ,ukaguzina ufuatiliaji wa washukiwa wa ugonjwa huu katika bandari ,viwanja vya ndege,vituo vya afya na jamii kiujumla.

  Akiendelea kufahamisha mikakati hiyo waziri huyo amesema kuwa Pia serikali imeandaa maeneo maalumu kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Ebola ambapo wizara ya Afya watayatangaza hivi karibuni.

  Pamoja na mikakati hiyo waziri Aboud amewaomba waandishi wa habari kusaidia katika kusambaza elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huo.

  Akitaja dalili za ugonjwa huo Waziri Aboud amesema kuwa dalili kuu ni homa, maumivu makali ya kichwa, misuli na viungo vya mikono na miguu pamoja na koo.

  Dalili nyengine ni kukosa nguvu za kiwiliwili na kufuatiwa na vipele katika ngozi,macho kuwa mekundu na kutokwa na damu katika tundu mbalimbali za mwili ikiwemo pua ,masikio mdomo na ngozi.

  Kwa upande mwengine waziri ametaja njia zinazotumika kusambaza ugonjwa huo kuwa ni kugusana mojakwa moja na mtu aliyeambukizwa ,kugusa majimaji yanayotokana na mgonjwa kama vile damu,jasho, mate ,mkojo na makohozipamoja na kutumia vifaa vilivyotumiwa na mgonjwa mwenye maambukizi bila kusafisha vizuri.

  0 0


  0 0

  Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela.
  Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

  Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo.

  Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

  Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

  “Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema Mkurugenzi huyo.

  Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.

  0 0

   HUAWEI Technologies (T) Limited Channel Executive, Mr. Moses Hella (left) explains to the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya Kikwete on the company’s latest introduced latest smart phone called Ascend P7 when he visited the company’s booth during a two-day Tanzania Diaspora Initiative conference held in Dar es Salaam recently. Second left is the Prime Minister, Mizengo Pinda and Huawei Terminal Marketing Manager Lydia Wangari (third left).
  HUAWEI Technologies (T) Limited Channel Executive, Mr. Moses Hella (left) explains to the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya Kikwete on the company’s latest introduced technology called Enhanced LTE (eLTE) when he visited the company’s booth during a two-day Tanzania Diaspora Initiative conference held in Dar es Salaam recently. Looking on second left is the Prime Minister, Mizengo Pinda.

  HUAWEI Technologies (T) Limited, a leading global information and communications Technology (ICT) company, has introduced in the Tanzania market a new technology called enhanced LTE, which will boost the government’s anti-poaching campaign as well as critical communication and video trunking or video surveillance for enterprises.

  Speaking during a two-day Tanzania Diaspora Initiative conference held in Dar es Salaam recently, Huawei Technologies Channel Executive, Mr. Moses Hella said the new device enables fast restoration of communication at critical times, having a video trunking (WALKI-VIDEO) for quick and accurate dispatch decision making, which can be effective in the current Tanzania anti-poaching campaign. 

  “We have introduced into the Tanzania market our latest technology called ‘enhanced LTE’ which is a state of the art mobile solution for critical communication as well as mobile video surveillance especially in transporting of important goods or people.

  “With this device, problems like illegal poaching in the country can be minimized if not eradicated. We believe that by installing this device in areas where illegal poaching is rampant will boost the ability of game wardens to monitor and track activities going on in the game parks/national reserves. 
  “Installing wireless cameras and deploying mobile surveillance system in different national game reserves will greatly support the government’s anti-poaching campaign,” said Mr. Hella.

  He reiterated that the eLTE technology has been deployed in more than 30 countries mostly in Armies, Police, Power Grids, Ports, Airports, Oil and Gas fields as well as Security Companies. Mr. Hella said that Huawei being the main sponsor of the fast Diaspora conference; it helped the company showcasing several other latest technologies such as smart-phones, modems and home devices that helps Tanzanians to catch up with technological advancement.

  “We have also introduced our latest smart phone called Ascend P7 which is an outstanding artwork with 5.00-inch 1080x1920 High Definition display powered by 1.8GHz processor alongside 2GB RAM and 13-megapixel rear camera, the gadget was also handed over to the President who visited our Huawei booth making him to be among the first Huawei Ascend P7 user in Tanzania,” he added.

  Commenting on Huawei’s eLTE technology President Jakaya Kikwete said; “this is good technology, did you show to Kova, the Special Zone Police Commander?”

  Meanwhile, during the meeting the president encouraged the Tanzania Diaspora to bring technologies in Tanzania.  The President urged for the Tanzania Diaspora to bring technologies in Tanzania. He said "Today Huawei gave me their latest smart phone P7, this shows Huawei is keeping up with competition and innovations, so Diaspora have to cooperate with these giants to bring technologies in Tanzania."

  Likewise, Mr. Hella mentioned that Huawei for more than ten years in Tanzania has been working hand in hand with the community to bridge the digital gap through ICT training to subcontractors and telecom operators.

  “We hope we can cooperate further with the Government and Diaspora society in bridging digital gap in Tanzania especially in the area of capacity building,” he said.

  Huawei is the leading telecommunication solution provider in the world with operations in more than 170 countries. The company has 150,000 staffs globally, and they have more than 120 staff in Huawei Tanzainia company, in which more than 65% are Tanzanians.

  0 0

   Salma Moshi akizungumza na Mubelwa Bandio kwenye mahojiano haya

  Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.

  Mmoja wa wagombea hao, Salma Moshi amaketi nasi kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014 chini ya utayarishaji wa Vijimambo Blog.Karibu uungane nasi kusikia anachopinga

  0 0
 • 08/18/14--21:28: BUSINESS SEMINAR

 • 0 0

  Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano
  Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu. Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.

  Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014.
  Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga


  0 0

   Vimwana wa Miss Temeke 2014 wakiwa kwenye pozi la picha,ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya kuelekea kwenye kinyang'anyiro chao kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa TCC klabu Chang'ombe jini Dar es Salaam Agosti 22,2014.Jumla ya washiriki 17 watapanda jukwaani siku hiyo kuwania taji hilo huku Globu ya Jamii ikimzawadia kitita cha Sh. Mil 1 Mrembo atakaeonekana ana mvuto wa picha (Miss Photogeni 2014).
  Wakiwa wamepozi wenyewe.
  Wakitembea kwa mwendo wa madaha mithili ya Twiga mbugani.


  0 0
 • 08/19/14--05:17: NISSAN PATROL INAUZWA
 •  Nissan Patrol ipo sokoni.
  Nissan Patrol, Engine TD42, 4200CC,Diesel, Manual, Make 1997.

  Wasiliana kwa namba 0752 753 309

  0 0
 • 08/19/14--07:15: HEPAUTWA CUP YAZINDULIWA
 •  Mdhamini wa mashindano ya Hepautwa cup 2014,Nuru Hepautwa akikagua timu ya kata ya Gangilonga katika uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Samora.
   Mdhamini wa mashindano ya Hepautwa cup 2014,Nuru Hepautwa akikagua timu ya kata ya Makorongoni katika uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Samora.
  Sehemu ya heka heka zilizofungasha virago vya Gangilonga kama inavyoonekana pichani
  Na Denis Mlowe,Iringa

  KINYANG’ANYIRO cha kugombea kombe la Hepautwa limezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki kwa mpambano kati ya kata ya Gangilonga na Makorongoni kwa kushuhudiwa Gangilonga kushushiwa kipigo cha aibu kwa kufungwa magoli 6 -0 katika mtanange ulioshuhudiwa na mamia ya mashabiki wa soka mkoani hapa na kufanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa.

  Mechi hiyo ya upande mmoja mchezaji Michael Gabriel kuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga magoli manne pekee yake na magoli mengine yakifungwa na Leonard Geka na David Mhanga katika mchezo ambao ulichezeshwa vema na refarii Bakari Makupa

  Mvua ya magoli kwa kata ya Gangilonga ilianza mnamo dk.11 kwa mchezaji David Mhanga kufunga goli kwa mkwaju mkali baada ya kuelewana vema na Michael Gabriel aliyeisumbua ngome ya kata ya Gangilonga walionyesha mapema kuzidiwa katika mchezo huo.

  Nyota wa mchezo huo Michael Gabriel alianza kuishushia mvua ya magoli Gangilonga katika dk ya 28 kwa kufunga goli la pili na katika dk 38 alifunga goli la tatu na kuwapa matumaini kata ya Makorongoni kujihakikishia nafasi ya kuingia katika makundi ya nane bora.

  Mnamo dk. 42 Michael Gabriel kwa kutumia juhudi binafsi alimzidi kete beki wa Gangilonga Abdalah Adebayo kwa kumpiga chenga ya maudhi na kuipatia kata ya Makorongoni goli la nne na kuwakatisha tamaa ya kata ya Gangilonga ‘watoto wa geti kali’ na kufanya hadi kwenda mapumziko wakiongoza kwa magoli 4 kwa sifuri.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kata ya Gangilonga kutaka kurudisha lakini bahati haikuwa yao na mnamo dk 47 ya kipindi cha pili mchezaji Leonard Geka aliipatia kata ya Makorongoni goli la tano na dk ya 79 Michael Gabriel alifunga goli la sita na kuwahakikishi timu ya Makorongoni nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi.

  Awali wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mgeni rasmi Nuru Hepautwa ambaye ndiye mdhamini wa mashindano hayo alisema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuibua vipaji vipya katika kata 16 zinazounda halmshauri ya manispaa ya Iringa na kupiga vita janga jipya la maambukizi mapya ya virus vya ukimwi.

  Alisema alisema mashindano hayo yatasaidia kukua kwa soka ndani ya mkoa wa Iringa na  kukuza viwango vya vijana na kuwezesha ajira na pia kuepukana na ugonjwa wa Ukimwi na kuwaweka katika afya njema vijana ambao kwa sasa wamekuwa wakikiuka maadili kwa wengi wao kujiingiza katika makundi hatarishi yakiwemo ya watumiaji wa madawa ya kulevya.

  Katika mechi nyingine za mtoano zilizoendelea juzi na jana kata ya Mlandege iliumana vikali na kata ya Ilala na Mlandege kufanikiwa kuwaondoa Ilala kwa bao 1 - 0

  Mchezo mwingine ulikuwa kati ya kata ya Isikalilo dhidi ya kata ya Ruaha ambapo Ruaha imeaga mashindano baada ya kufungwa magoli 5 – 4 hivyo Isakalilo imesonga mbele na kusubiri kuingia katika makundi ya timu nne nne.

  Katika mashindano ya Hepautwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kombe na sh.1,000,000  na sh.600,000 kwa mshindi wa pili na sh 300,000 kwa mshindi wa tatu na mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka mkoani hapa.

  0 0


    Katibu Mtendaji Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa  Jukwaa la Wadau watakaoangalia mazao ya mikunde na nafaka litakalofanyika Agosti 20 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo na Ofisa Programu wa Women & Youth Development Foundation, Luke Daniel Kifyasi.
  Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo  akizungumza wakati wa mkutano huo.

  Na Clezencia Tryphone


  Waziri Mkuu Pinda, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la wadau watakaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara baada ya kuvunwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge amesema katika uzinduzi huo utafanyika katika hoteli ya Golden Tulip Agosti 20 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi.
  Alisema lengo la kufanya uzinduzi huu ni kutokana na changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.
   
  Miongoni mwa changamoto hizo, ni utuzwaji wa mazao hayo baada ya kuvunwa, hasa kwa wakulima wadogo wadogo na wale wa kati na wafanya biashara huku changamoto nyingine ikiwa ni upotevu wa Mbegu pamoja na matumizi ya tekinolojia ya utunzaji na takwimu.

  “Tunatarajia kufanya uzinduzi wa jukwaa la wadau wanaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara tu baada ya kuvuna, na lengo kubwa ni kuwaamasisha pia watunzaji wa nafaka hizo, ili kuepuka upotevu, na tumefikia hatua hii baada ya kufanya utafiti,”amesema Rukonge.

  Amesema, mara baada ya kufanywa kwa takwimu wamegundua kuwepo kwa upotevu mkubwa wa mbegu za mazao hayo na hiyo ndiyo sababu iliyowafanya kuzindua jukwaa hilo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (kulia ) akizungumza na balozi wa China nchini Tanzania Dr. LU Youqing (kushoto) aliyemtembelea ofisini kwake leo kwa ajili ya maandalizi ya kongamano la China – Afrika linalotarajiwa kufanyika mkoani Arusha, Tanzania mapema Machi, 2015.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dr. LU Youqing (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (kulia) juu ya hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya kongamano hilo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (kulia ) na Balozi wa China nchini Tanzania Dr. LU Youqing (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
  Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 08/19/14--07:25: KAAZI KWELI KWELI


 • 0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius B. Likwelile akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu, kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kuisaidia sekta ya Elimu nchini, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius B. Likwelile na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
  Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa akichangia wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome.
  Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa (kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome (wapili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius B. Likwelile (wapili kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier (kulia) wakijadiliana wakati wa kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kuisaidia sekta yaElimu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM

  Na Rose Masaka - MAELEZO

  Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu wa shilingi bilioni 203 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mpango wake wa matokeo makubwa sasa(BRN).

  Mkataba huo umesainiwa na Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dk. Servacus Likwelile huku ukiwashirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elinu na Naibu Katibu Mkuu kutoka TAMISEMI leo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya kusaini mkataba Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Servacus Likwelile ameishukuru Benki ya Dunia kutoa mchango huo kusaidia sekta ya elimu nchini na kuwataka TAMISEMI na Wizara ya Elimu kusimamia vizuri pesa hizo ili kuleta mafanikio zaidi kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa.

  Aidha Dk. Likwelile amewataka waajiri wote katika sekta ya elimu kutoa kipaumbele kwa walimu ili waweze kuboresha elimu nchini na kuwataka kupeleka majina na akaunti namba za walimu wote Hazina ili Hazina iweze kuwawekea mishahara yao katika akaunti zao kwa wakati.

  Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome amesema kuwa Wizara ya Elimu kwa sasa imepiga hatua kubwa katika kufanikisha lengo la matokeo makubwa sasa linalolenga kukuza na kuendeleza elimu katika ngazi ya shule za msingi na sekondari hivyo fedha hizo zinatumika kutatua matatizo katika sekta ya elimu ambapo kwa sasa shule nyingi zimeanza kuonesha matokeo mazuri.

  Akitoa mchango wake wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier amesema kuwa Benki ya Dunia imeona kuna umuhimu wa kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu ili kuleta ujuzi na kuvumbua vipaji kwa vijana wadogo watakaosaidia kuleta maendeleo hapo baadae.

  Naye Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa ameahidi kusimamia fedha hizo kwa ufanisi na kuhakikisha kuwa zinawafikia walengwa wote hadi ngazi ya chini waweze kufaidika na pesa hizo.

  0 0

  Frank Mvungi_ Maelezo.


  Serikali  imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.


  “ Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya Juu.”Alisema Mwaisobwa.


  Akifafanunua, mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini . Aidha Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo  yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.


  Pia Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi  ambayo ni www.heslb.go.tz.na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.


  Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa.

  WAKATI HUO HUO  

   


  Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya fedha za malipo ya mafunzo kwa vitendo kwa mwaka wa masomo 2013 2014.
  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Mwaisobwa alisema kuwa jumla ya wanafunzi  9946 kutoka vyuo vikuu vitano hawajapatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ambao wengi wao tayari wako katika maeneo waliyopangiwa.
  “Bodi tayari imeandaa malipo yao na yanatarajiwa kutumwa mwishoni mwa juma hili, ambapo vyuo vikuu vitano  ikiwemo Tumaini Makumira (TUMA) wanafunzi 1 715, Stefano Moshi (SMMUCO) wanafunzi 1 191, Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM)wanafunzi 2 578,  Mt. Augustino (SAUT) wanafunzi 2639 na Teofilo Kisanji (TEKU) wanafunzi 1823.
  Akijibu swali la waandishi wa Habari Mwaisobwa alisema kuwa sababu zilizopelekea kuchelewa kwa fedha hizo ni mchakato wa upatikanaji wa fedha  zilitarajiwa kupatikana mapema zaidi.
  Aidha, Mwaisobwa alitoa rai kwa wazazi na walezi wenye uwezo wa kuwalipia watoto wao wafanye hivyo ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa kunufaika na mkopo mkopo wa Bodi.


  0 0

   Afisa Mnadhimu namba wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Japhet Lusingu akitoa ufafanuzi wa mada mbalimbali zilizojadiliwa kati ya Jeshi hilo na wadau wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Bwalo la Afisa wa Polisi (Police Officers Mess) mwishoni mwa wik
   Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Francis Duma akitoa elimu ya Polisi Jamii katika kikao kilichowajumuisha viongozi wa Jeshi la Polisi na Wadau wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha.
    Katibu wa kikao cha Viongozi wa Polisi na Wadau wa Polisi Jamii ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Arusha Bw. Adolph Olomi akitoa mwongozo kwa wadau juu ya uendeshaji wa kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi mwishoni mwa wiki.
   Mdau wa Polisi Jamii ambaye pia nin Mwanasheria wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Kiomoni Kibamba akisisitiza jambo wakati anachangia mada ya Usalama mkoa wa Arusha katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi mwishoni mwa wiki iliyopita
  Picha ya pamoja kati ya baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha na wadau wa Polisi Jamii mkoani hapa mara baada ya kikao cha kujadili usalama kilichofanyika ukumbi wa Bwalo la Polisi habari picha na woindeshizza blog

   
  Wadau wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha kutoka kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka sekta binafsi na za kiserikali wamedhamiria kufungua Akaunti benki kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu.


  Hayo yalielezwa na wadau hao wakati wa kikao cha kujadili usalama wa mkoa huu kilichofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi (Police Officers Mess) mwishoni mwa wiki kati yao na Viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa. Wadau hao walisema kwamba wawezeshaji wa Jeshi hilo ni wana Arusha wenyewe hakuna mtu yeyoye atakayetoka mkoa mwingine kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi la Polisi mkoani hapa.


  “Tunataka Arusha iwe mfano na mikoa mingine iige, bila kuwawezesha Polisi hatuwezi kukomesha uhalifu na tunatakiwa tuwawezeshe ili tupate nafasi ya kuwalaumu, hivyo basi nashauri iundwe Kamati ndogo itakayowajumuisha Polisi na Wananchi ambao watafanya harambee kwa watu mbalimbali”. Alisema Kiomoni Kibamba ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya jiji la Arusha.


  Wadau hao walisema pamoja na Mfuko huo kutumika kuliwezesha jeshi la Polisi katika kuongeza bajeti ya mafuta na vifaa vingine lakini pia utakuwa unatumika kuwapa motisha wale wote watakaokuwa wanaliwezesha Jeshi hilo kuwapa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuonyesha kuwa wanathamini mchango wao.


  Mbali na mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa siku hiyo pia wadau hao walilishauri Jeshi la Polisi Mkoani hapa kuwa makini na waendesha pikipiki yaani Boda Boda na ikibidi kila pikipiki inayotumika kusafirisha abiria iwe na makazi ya maegesho yanayojulikana ili tukio la uhalifu linapotokea askari wawe wanapata pa kuanzia katika suala zima la upelelezi.


  Walisema kwa sasa pikipiki hizo zinafanya kazi mpaka usiku hivyo kama kuna uwezekano wangewekewa ukomo hasa muda wa usiku badala ya kufanya biashara hiyo mpaka asubuhi kwani baadhi yao wanatumia mwanya huo na kujiingiza katika vitendo vya kihalifu.


  Awali  akifungua kikao hicho Katibu wa kikao hicho Bw. Adolph Olomi ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Arusha, alisema kwamba pamoja na mambo mengine lakini pia lengo la mkutano huo ni kufahamiana ili kupunguza kama si kuondoa kabisa pengo kati Jeshi hilo na wananchi hali ambayo itasaidia kuwa na ukaribu utakaosaidia kushughulikia matatizo ya kihalifu kabla hayajatokea.


  Kwa upande wake Afisa Mnadhimu namba moja wa Jeshi hilo mkoani hapa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Japhet Lusingu aliwataka wadau hao watoe taarifa za wahalifu na uhalifu kupitia kwa viongozi wa Jeshi hilo ili kupunguza malalamiko juu ya uvujaji wa taarifa hizo.


  (ACP) Lusingu aliongeza kwa kusema kwamba, hata watoa taarifa mara baada ya kutoa taarifa Polisi wanatakiwa wakae kimya bila kumshirikisha mtu yeyote kwani  hali hiyo inasababisha majirani kumfahamu mtoaji wa taarifa hizo na baadae wahalifu kumfahamu kisha lawama kuliangukia jeshi la Polisi hivyo akasisitiza kwamba usiri unatakiwa kuanzia kwa mtoa taarifa mwenyewe.


  Akitoa mada katika kikao hicho Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi (SSP) Mary Lugola alisema kwamba, umefika wakati muafaka kwa Jeshi la Polisi na wananchi wote kufanya kazi kwa ukaribu zaidi ili kuweza kuimarisha usalama. Alisema kikao hicho ni moja ya mpango mkakati  wa kuhakikisha mkoa wa Arusha unakuwa salama hasa ikizingatiwa pia ni kitovu cha shughuli za kitalii.


  Naye Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Francis Duma alisema kwamba, Falsafa ya Polisi Jamii ilikuja baada ya kuona kuna pengo kubwa kati ya Polisi na Jamii hivyo kuondoshwa kwa pengo hilo kumesaidia pande hizo mbili kuwa karibu.


  Alisema Polisi pekee bila kushirikiana na wananchi haiwezi kukomesha uhalifu ikizingatiwa kwamba, kutokana na sensa ya mwaka 2012 uwiano unaonyesha kuwa, Polisi mmoja anatakiwa ahudumie kaya 1300 kwa masaa 24 bila kupumzika, hivyo ukomeshaji wa matukio ya uhalifu utafanikiwa endapo wanajamii nao watajitoa ipasavyo katika suala zima la kuimarisha usalama

  0 0

  Kuluthum Sagamiko akihojiwa na waandishi wa habari
  mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo 


   Eva Mwingizi akihojiwa na waandishi wa habari mara
  baada ya kufungua warsha hiyo.

    viongozi hao wakisikiliza watoa
  mada (hawapo pichani) wakati wa warsha hiyo
  DIWANI wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko ameandaa warsha kwa ajili ya wenyeviti na makatibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya mafunzo ya kujiimarisha kichama na ujasiriamali
  kwa wanawake.

  Warsha hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, ambapo jumla ya viongozi
  hao kutoka kwenye kata 34 za wilaya hiyo walishiriki na kuweka
  mikakati ya pamoja. 
  Akifungua warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bara, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Eva Mwingizi, aliwataka  kuwa mstari wa mbele na kusimama katika nyanja zote ikiwemo siasa na biashara bila woga.
  Alisema uwiano sawa wa asilimia 50 kwa 50 katika uongozi hauwezi
  kufikiwa endapo  wanawake wenyewe watasita kujitokeza kugombea nafasi
  mbalimbali.
  "Nimefurahi leo kuwaona wanawake wamekutana pamoja, kwa sababu warsha kama hizi zinawajengea uwezo,kina mama wanaweza na wakijengewauwezo basi wanafanya vizuri katika nyanja zote.
  "Kina mama ni mtaji mkubwa popote pale, ni tegemeo kwenye maeneo
  mengi, hawa ni jeshi,ukitaka kufanikisha jambo, na kuwatumia kinamama
  basi jambo hilo lazima lifanikiwe, kwahiyomafunzo ya kufanya
  wajitambuezaidi ni muhimukwao,"aliongeza.

  Alisema  ingawa UWT ipo kisiasalakini walifikiria kuwainua kina mama
  kwa kuanzisha kitengo cha miradi, ambapopamoja namambomengine
  kinawaunganisha na taasisi mbalimbali za mikopo ilikuinua biashara
  zao.
  Naye muandaaji wa warsha hiyo, Diwani wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko,alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanawake  hao wanaotoka katika kata, kwakuwandiowenye watu .
  "Pia wajitambue nakujipanga nachangamoto hususan  cha uchaguzi na
  maisha kwa ujumla, hasa wakati huukuelekea katikachaguzi za
  kitaifa,"aliongeza.
  Licha ya kupata mafunzo ya kisiasa,Kuluthum  alisema pia kunamkufunzi  wa mamboya biashara, ili kuleta msukumozaidi,kwa kuamini kuwa mwanamke mwenye uchumi ananguvu  zaidi.
  "Kwenye wilaya yetuyaKinondoni, tumepoteza majimbo mawili na kata 11,
  kupitia wanawake hawa, wenye nguvu nauelewa itakuwa rahisi kurudisha
  maeneo tuliyopoteza kwa upinzani,"alisema.

  0 0

    Naibu Meya wa jiji la Helsinki nchini Finland akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa wa Kalasatama nchini Finland kwa viongozi wa Tanzania walioko katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania
    Baadhi ya majengokatikamji wakisasa wa Kalasatama nchini Fnland
    Baadhi ya majengokatikamji wakisasa wa Kalasatama nchini Fnland

  Baadhi ya viongozi wa Tanzania walipotembelea kanisa lilijengwa kwa mbao katika jiji la Helsiniki nchini Finland Kutoka kushoto ni Godfrey Nyamurunda kutoka taasisi ya Uongozi, Athanas Kapunga ambae ni meya wa jiji la Mbeya,Wilson Kabwe ambae ni mkurugenzi wa jiji la Dar na Lisa Tervo wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania (picha zote na Vedasto Msungu)

  0 0

   Mr. Shrima of Innocent hardware receiving 4th category award Bajaj Boxer motorcycle from Mr. Alpesh Patel CSMO(Chief Sales & Marketing)
  Mr. Dilip on be half of Aim Steel Arusha receiving 4th category award Bajaj Boxer motorcycle from Mr. Alpesh Patel CSMO
  Mrs. Elizabeth of Lazy Shop receiving for 6Th category award Samsung S4 Mini from Genesis Mushi Sales executive of Silafrica.
   Bi Fatma Wahenga akitoa shukrani za dhati kwa uongozi mzima wa kampuni ya SIMTANK baada ya kupokea zawadi ya gari aina ya Suzuki carry kama motisha baada ya kuibuka mnunuzi mkubwa wa SIMTANK eneo la buguruni DSM, kushoto ni Afisa masoko na mauzo wa SMTANK Alpesh Patel Kulia ni msherehashaji wa hafla hiyo iliyo fanyika serena hotel DSM havi karibuni.
  Mkurugenzi mtendaji wa Silafrica SIMTANK Bw. Shah akimkabidhi mfano wa funguo wa gari aina ya Suzuki Carry kwa bi. Fatma Wahenga baada ya kuibuka mnunuzi mkubwa wa SIMTANK eneo la buguruni DSM ambapo washindi wengine walijishindia gari aina ya noah, pikipiki na sim za mkononi.
  Wasanii kutoka Kundi la THT wakitoa burudani katika sherehe hiyo
  ZAWADI ZA PIKIPIKI NA MAGARI ZITAKABIDHIWA SIKU CHACHE ZIJAZO BAADA YA KUKAMILIKA KWA USAJILI.

  Simtank inatambua mchango mkubwa kutoka kwa wateja nwake hivyo imejiwekea utaratibu wa kurudisha sehemu ya faida zake kwa wale walioweza kununua kwa kiasi kikubwa SIMTANK kwa mwaka.

  Kampuni ya SilAfrica ambao ndio watengenezaji na wauzaji wa matanki ya Kuifadhia majii aina Ya SIMTANK wafanya sherehe kwaajili ya kuwakabidhi zawadi wateja wao wanaonunua matank yao kwa idadi kubwa. 

  Kampuni hiyo imekua ikifanya hivyo kila mwaka ikiwa kama njia ya Kuwapongeza na kuboresha uhusiano wao baina ya kampuni na Wateja wao vilivile sherehe za kuwapongeza na kuwapa zawadi hufanyika kila mwaka kwaajili pia ya Kutambua mchango wao kwa kampuni hiyo ya SilAfrica ambao ni watengenezaji wa Matanki ya kuhifadhia Maji ya SIMTANK

older | 1 | .... | 345 | 346 | (Page 347) | 348 | 349 | .... | 1898 | newer