Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

NAFASI ZA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MASHINE ZA KUTOTOLEA VIFARANGA VYA KUKU.

$
0
0

Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia  MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINJI  inatangaza  nafasi  za   MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI  WA  MASHINE  ZA  KUTOTOLEA  VIFARANGA  WA  KUKU.
Mashine   zitakazo fundishwa  kutengeneza  ni  INCUBATOR   ( MANUAL & AUTOMATIC) ZENYE  UWEZO  WA  KUTUNZA  JOTO  KWA  SAA  48 PAMOJA  NA  KUTOTORESHA  MAYAI   KUANZIA  240  HADI  5000.
Vile  vile  yatatolewa  mafunzo  ya   UTENGENEZAJI  WA  MAJIKO  SANIFU  NA  NISHATI  MBADALA.
ADA   YA   MAFUNZO   :
Ada  ya  mafunzo  haya  ni  SHILINGI  ELFU  ISHIRINI  NA  TANO  TU. (Tshs.25,000/=)
TAREHE  YA  KUANZA  KWA  MAFUNZO
Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  siku  tano  kuanzia  tarehe    01  SEPTEMBA  2014  hadi  tarehe  05 SEPTEMBA  2014
FOMU   ZA   KUJIUNGA   NA   MAFUNZO :
Fomu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya  zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU  ( Tshs.15,000/=).
MWISHO  WA  KUCHUKUA  FOMU  :
Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe   28  AGOSTI 2014.
Ofisi  zetu  zinapatikana  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.
JINSI   YA   KUFIKA   OFISINI   KWETU:
Kufika  ofisini  kwetu, panda  daladala za  UBUNGO- CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia utaona  ofisi  imeandikwa   RAEFO  TANZANIA.
Kwa  maelezo  zaidi wasiliana  nasi  kwa  simu 0784406508.
Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  mafunzo  ya  utengenezaji  wa  mashine  za  kutotolea  vifaranga, tembelea :
www.rafikielimu.blogspot.com

SERIKALI WILAYANI NGORONGORO YATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA REDIO ZA KIJAMII

$
0
0
DSC_0010
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwakaribisha wadau wa maendeleo ofisini kwake Loliondo walioongozwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa tatu kushoto) aliyefuatana na Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania , Bw. Slyvester Nteere (wa pili kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Eric Kalunga (kushoto) wakiwa na mwenyeji wao Diwani wa kata ya Ololosokwani, Yannick Ndoinyo (kushoto kwa DC).

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.

Serikali na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa ushirikiano kwa redio za kijamii wilayani humo kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM, Joseph Munga, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na wadau wa maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa Uswiss hapa nchini.

‘Redio za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na jamii katika suala zima la kujiletea maendeleo’ alisema Joseph Munga.
DSC_0019
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwa kwenye mazungumzo na wadau wa maendeleo waliofika wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).


Munga aliongeza kwa kusema kuwa redio hiyo iliyoanza kurusha matangazo mwezi Oktoba 2013 imekuwa ni kichocheo cha kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii wilayani Loliondo na kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii huku akiitaka serikali na halmashauri wilayani humo kuisaidia katika kufikia malengo ya kuitumikia jamii na kuwashukuru wadau mbali mbali wanaoiwezesha redio hiyo ikiwemo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambayo imetoa mnara wao kurushia Matangazo ya redio Loliondo.

“Suala hapa ni ushirikiano hasa kwa halmashauri kuelewa na kuona umuhimu wa kutumia redio hii katika matukio mbali mbali yanayofanyika kwenye halmshauri vikiwemo vikao vya baraza la madiwani ili wananchi walioshindwa kufika waweze kujua baraza lao limepitisha nini sanjari na huduma kwenye sekta za afya na elimu”, alisema Munga.

Redio Loliondo ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani humo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya RAMAT kwa kufadhili miradi ya Maktaba,kutoa elimu kwa jamii ya kifugaji yenye malengo ya kuinua uelewa na ufahamu kwa jamii hizo zilizopo pembezoni hasa katika suala zima la kujiletea maendeleo.
DSC_0049
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kushoto) ambaye pia ndio mkuu wa msafara huo akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo hayo. Kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.

Nae Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, alisema kuwa misingi ya redio hiyo inalenga kuikomboa jamii ya Loliondo kwa kutoa elimu ya kifugaji na elimu kwa wananchi wilayani humo ambao hapo awali hawakupata fursa ya kupata taarifa na matukio mbalimbali yanayoendelea wilayani humo. 

Akifafanua faida za redio hiyo kwa jamii ni kupata taarifa mbali mbali zinazoendana na shughuli zao za ufugaji hususan taarifa za chanjo ya mifugo na madawa na kupata taarifa nyingine kuhusiana na masuala mbali mbali ya kijamii ndani na nje ya wilaya hiyo ambayo hapo awali yalikuwa vigumu kupatikana kwa wakati kutokana na jiografia ya wilaya hiyo.

“Pamoja na kwamba malengo ya mradi huu yameanza kuonekana dhahiri machoni petu,wafadhili kutoka UNESCO pamoja na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ambayo mnara wake umekuwa ukitumika kurusha matangazo ya redio hii, tunataka kuhakikisha kwamba mnaweza kujiendesha wenyewe hapo baadae ili mradi kama huu uweze kuwanufaisha na wenzenu sehemu zingine”, alisema Al Amin.
DSC_0156 Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo juu mradi waliobuni wa kituo cha utamaduni wa Kimasai ambao uko mbioni kuanza ujenzi wake wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika hilo.
 
Akizungumzia miradi inayoletwa na wafadhili wilayani humo Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha vijana ambao wana shauku ya kuishi mijini kurudi nyumbani na kuendeleza jamii hali ambayo imetafsiriwa kutoa uelewa kwa wanajamii na hivyo ni faraja kubwa kwa wananchi wilayani Loliondo.

Ameyataka mashirika na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuingalia Ngorongoro kwa ukaribu na kuwa wadau wazuri wa kuiletea maendeleo wilaya hiyo kwani miradi iliyopo itachochea ukuaji wa uchumi na kusaidia uelewa wa wakazi wilayani Loliondo katika dhana nzima ya kujileta maendeleo na kukuza uelewa wa wananchi wa kupata taarifa mbalimbali kwa wakati.
DSC_0179 
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili lulia) akitoa ushauri kuhusu kituo hicho kuwa kitakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa jamii hiyo ya kifugaji pindi kitapokamilika huku akisisitiza kuwa mipango iliyopangwa kama walivyopewa maelezo iendane na wakati.
DSC_0310
Mmoja wa wadau wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga akisoma moja ya vitabu ndani ya maktaba hiyo inayofadhiliwa na UNESCO, Maktaba hiyo inayotumiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo.
DSC_0361
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) ambaye pia ni mkuu wa msafara huo wa kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO akiteta jambo na Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere ndani ya maktaba hiyo. Anayefuatilia mazungumzo hayo kwa karibu ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (katikati).
DSC_0294
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akitoa maelezo baada ya kutembelea Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO nje ya maktaba hiyo.
DSC_0392
Kikundi cha ngoma ya Kimasai kilichowatumbuiza wageni waliotembelea mradi wa redio ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO wakitumbuiza wakati wa ziara hiyo.
DSC_0412
Afisa Miradi wa kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko, akijumuika na kinamama wa kikundi cha ngoma za kimasai kutoka kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0432
Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwemo maktaba, redio na ugawaji wa vitabu vya masomo ya Sayansi na hesabu vinavyoafadhiliwa na UNESCO kwenye kata hiyo.
DSC_0441
Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akitoa pongezi kwa redio Loliondo FM kwa kuweza kuihamasisha jamii inayoizunguka kwa kuburudisha, kutoa elimu na habari kwa ujumla hiyo sio kazi nyepesi kutokana na uchanga wenu wa redio yenu.
DSC_0476
Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akikabidhi zawadi kwa kikundi cha ngoma cha kinamama wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi inayofadhiliwa na UNESCO kwenye kata ya Ololosokwani.
DSC_0478
Wanakikundi cha ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia taarifa mbalimbali za mitandao kwenye “Tablet” inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara hiyo.
DSC_0488
Mmoja wa wanakikundi akitumia Tablet kupiga picha wanakikundi wenzake pamoja na wadau wa maendeleo (hawapo pichani).
DSC_0509
Wanakikundi cha ngoma za kimasai wakiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni huo huku wakionyesha furaha baada ya kupokea zawadi ya fulana kutoka kampuni ya Samsung.
IMG-20140807-WA0024
Meneja wa redio jamii ya Loliondo FM, Joseph Munga akiwa kwenye studio za redio hiyo wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi inayoifadhili.
DSC_0516
Meneja mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (aliyeketi) akiwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph ndani ya studio za kurushia matangazo za redio ya Loliondo FM inayorusha matangazo yake kwenye mnara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuifika jamii kubwa kwenye maeneo hayo.

FLAVIANA MATATA FOUNDATION NA PSPF WAKABIDHI VIFAA VYA SHULE LINDI

$
0
0
Mwanamitindo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation. katika mradi wa Back to school project /FMFstationarykit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni PSPF,
Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja nashule za msingi Litingi na Mnengulo ziliyopo Lindi.

bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine "hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli".

Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.
2G2A8196
Add caption
2G2A8156
Add caption
2G2A8088 Flaviana Matata ameongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
Martin2G2A81742G2A82342G2A82482G2A82792G2A8299IMG-20140811-WA0044IMG-20140811-WA0023IMG-20140811-WA0029

Castle lite Yazindua Promosheni ya Lite up the wekeend.!

$
0
0
 Meneja masoko wa bia ya Castle lite Vimal Vaghmaria  kushoto mwenye miwani,Meneja wa Castle lite  Geofray makau   katikati na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania Victoria kimaro wakionyesha chupa ya bia hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ya shindano la kuwapata washindi wa Castle lite VIP Yacht Party ambapo washindi watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.
 Meneja masoko wa bia ya Castle lite Vimal Vaghmaria kushoto mwenye miwani,Meneja wa Castle lite  Geofray makau   katikati na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania Victoria kimaro wakionyesha chupa ya bia hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ya shindano la kuwapata washindi wa Castle lite VIP Yacht Party ambapo washindi watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo katika Hotel ya Slip way washindi wa Castle lite VIP Yacht Party watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.


BBC yazindua studio zake nchini,kipindi cha asubuhi cha Amka na BBC kuruka moja kwa moja kutokea dar es salaam

$
0
0
Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu, Bi. Nikki Clarke akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, katika Jengo lao lililopo Mikocheni jana jioni. Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,  Bw. Ali Saleh.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bw. Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, Bw. Hassan Mhelela (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu yake.
Taswira za Studio za BBC jijini Dar es salaam.
Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar es salaam.
Picha na Othman Michuzi.

MEMBE ,NAPE WATOA POLE MSIBANI MTAMA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akisalimiana na Salum Said Mchora ambaye amepoteza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23 Said S. Mchora  mkazi wa Masasi,Majengo.Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akititoa  mkono wa pole kwa Ndugu Said Mchora ambaye amepoteza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23 Said S. Mchora  mkazi wa Masasi,Majengo kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama karibu na stendi ya mabasi ya Masasi,Katikati ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye ambaye alitoa salaam za rambi rambi kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi.
Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akiongozana na  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye kwenda kutoa salaam za rambirambi kwa familia zilizopoteza jina wao kwenye agari ya gari iliyotokea Mtama,kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini,Richard Kasesela .Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye wakimsikiliza Mzee Halfani Libaba ambaye ameondokewa na mtoto wake wa kiume Rajab Halfani kwenye ajali mbaya ya gari lililoacha njia wakati dereva akijaribu kumkwepa mbuzi na kusababisha vifo vya watu 8.

 Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe  na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wa CCM Mkoa na Wilaya ya Lindi wakionyeshwa eneo ambalo ajali ilitokea.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye wakimpa pole mpiga picha maarufu Mohamed Selemani ambaye amelazwa kwenye hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akimjulia hali na kumpa pole Ndugu Shaaban Issa mmoja wa majeruhi watatu wa ajali ya a gari iliyotokea Mtama na kusababisha vifo vya watu 8.

Hotuba fupi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank kwa DIASPORA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Charles Singili alipokuwa akizungumzia huduma za benki yake kwa waTanzania jijini Washington DC
PICHA ZOTE KWA HISANI YA IKULU
Hotuba fupi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Charles Singili alipokutana na waTanzania waishio nchini Marekani usiku wa Agosti 2, 2014. Hotuba hii ilitolewa kwenye mkutano kati ya waTanzania wa Marekani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Jakaya Kikwete Karibu umsikilize


BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA INDIA DESK

$
0
0
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja huduma mpya ya India Desk  inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.

Wadau wa Benki ya CRDB.
Wadau mbalimbali wa Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya India Deski.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya India Deski uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi mpya ya India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakisakata rhumba wakati wa hafla hiyo.


Airtel yazindua huduma mpya ya mitindo kwa njia ya simu kwa kushirikiana na Mbunifu Mahiri Afrika Mustafa hassanali.

$
0
0
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, imeshirikiana na mbunifu wa mitindo Afrika ,Mustafa Hasanali katika kusheherekea miaka 15 ya mafanikio yake makubwa katika sekta ya mitindo.

 Mustafa Hassanali amefanya maonyesho katika miji 27 katika nchi 18, na kugusa maisha ya watu mbali mbali  kwa njia tofauti. Na anaendelea kuwa maarufu katika sekta ya mitindo nchini na Afrika kwa ujumla.

Ushirikiano huo kati ya Airtel na Guru wa mitindo  Tanzania na nje ya Tanzania, utawezesha wateja wa Airtel na washabiki wa mitindo kuwa karibu  zaidi na ulimwengu wa mitindo kwa kupata habari mbali mbali na za kisasa kupitia simu zao za mikononi.

Akiongea kuhusu muungano huo Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba, alisema “mitindo ni moja kati ya vipengele muhimu katika maisha yetu, zikiwemo nguo, vifaa na vyombo mbalimbali. 

Kila mtu anataka kupendeza na kujihusisha na mitindo ya kisasa. Ila , hivi sasa upatikanaji wa habari na huduma za mitindo ni mgumu sana. Hivyo Airtel tumekuwa wa kwanza katika kuwapatia wananchi huduma hii kupitia simu zao za mkononi itakayowasaidia kupata habari mbali mbali za mitindo kwa ujumla . Huduma hii inajulikana kwa jina la “Airtel Fasheni”. 
Tunaamini kuwa , huduma hii itawasaidia wateja wetu wote ambao wangependa kupata habari mbali mbali na kuwafikia wabunifu wa mitindo ili kupata ushauri na pia kununua bidhaa zao.”

Mustafa Hassanali, mbunifu mitindo mahiri Afrika alisema , “ Airtel fasheni ni huduma ya kipekee ambayo wateja wa Airtel wanaweza kuipata mahali popote na wakatii wowote kwa kupiga *148*82#. Huduma hii ni Tsh.90 kwa siku.”

NSSF YAPELEKA VETERANI TANGA

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Kombaini ya Tanga, Kassim Jumaa (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Survey veterani, Ahmad Rasuli (katikati), wakati wa mchezo maalum wa kusherehekea Sikukuu ya Wakulima Nanenane uliofanyika kwenye viwanja vya Disuza mjini Tanga. Mchezo huo ulidhaminiwa na NSSF. Kuilia ni Amir Athuman wa Kombaini ya Tanga.

Na Elizabeth Kilindi, Tanga

Timu ya Survey Veterani ya jijini Dar es salamu imeifunga timu ya Kombaini vijana  Veterani ya Jiji la Tanga 2-1 katika mchezo wa kuazimisha sherehe za wakulima nane nane viwanja vya Disuza vilivyopo Mkoani Tanga.


Mchezo huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ulikuwa na lengo la kukutanisha timu za maveterani ili kujenga mshikamano na kuhamasisha michezo.


Katika mchezo huo wachezaji wa savey Carlos Mdinga alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na wapinzani hatua ambayo ilisababisha gori hilo Dakika ya pili.


Aidha katika mchezo huo timu ya Savey ilionyesha makali yake ambapo dakika ya 40 walisawazisha goli kutoka kwa kiungo wake  Silyvester Malango.

Hata hivyo bahati nyota ilizidi kungaa kwa timu ya veterani baada ya Dakika ya 70 kupata goli la pili lililotiwa nyavuni namshambuliaji wake David  Emanuel.

Katika mchezo mwengine ni kati ya Timu ya Best point veterani imeibuka na ushindi wa goli mbili dhidi ya  Kombaini ya wazee Veterani ya Jijini Tanga.

Magoli  ya Best point yalifungwa na Sadiki Salumu dakika ya saba na goli la  pili lilifungwa na Miraji Paulo dakika za lala salama.

Baada yakumalizika kwa mchezo huo kocha Seleman Mgaya ambaye ni Katibu wa Survey Veterani ya Dar es salaam amesema wamefurahishwa ushirikiano unaotolewa namfuko wa hifadhi ya jamii NSSF hasa kwa kuonyesha mchango wao katika michezo.

“Tunaishukuru sana  NSSF kwa moyo wa kutukutanisha pamoja kimichezo hatua ambayo tunajivunia kwaniwao wametambua umuhimu wetu hivyo hatuna budi kutoa ushirikiano”amesema Mgaya.

Review Class for the 13th December 2014 CISA & CISM Exams

$
0
0

                             




Registration is NOW open for CISA & CISM Review Class for the forthcoming CISA & CISM exam on 13thDecember, 2014. Our Reviews are due to begin on Monday 25th August, 2014 to Thursday 22nd October, 2014 (Monday to Friday) .Both the weekday and the weekend options will be for a total duration of more than 90 hours.
The review classes focus exclusively on the essential areas covered in both CISA & CISM exam. A series of sample exam questions that provide participants with a "feel" of the format and the types of questions encountered on the exam.

Our trainers are qualified Professionals with technical experience, skills and knowledge of specific domain(s). Participants will gain an overall understanding of the relevant CISA & CISM Examination DOMAINS.

Study Materials
Our Courses utilize official ISACA presentations and study materials provided by ISACA. We will inform you about recommended materials upon your enrolment.
Fees- 1,000,000 Tshs.  Per Participant

For more details about the course and online registration visit Click the Link!! or contact - info@isaca.or.tz

BI VAILET MAKAZI WA MTANANA WILAYANI KONGWA AOMBA MSAADA ILI AKAFANYIWE UPASUAJI

$
0
0
Na John Banda,Kongwa.
Bi Vailet Sekwao (40) mkazi wa kijiji cha Mtanana Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, anaomba msaada wa kifedha kiasi cha shilingi million mbili (2) ili aweze kufanyiwa upasuaji wa jicho lake ambalo lina uvimbe.
Akizungumza na mwandishi wetu katika kijiji cha Mtanana alisema kuwa anaomba msaada huo ili umwezeshe kugharimikia gharama za kumfikisha katika Hospitali ya Mhimbili na kufanyiwa upasuaji  wa uvimbe ulioko kwenye jicho.
Sekwao alisema kuwa uvimbe huo ambao ulinza kama kipele pembezoni mwa jicho hilo mwaka 2013,uliazidi kuongezeka na kufikia hatua ya kuvimba na kulifanya jicho hilo kutokuwa na uwezo wa kuona.
Alisema pamoja na juhudi za kwenda hospitali mbalimbali ikiwemo ya Mvumi, hali jicho hilo limezidi kuvimba na waatalam wamenishauri nikafanyiwe upasuaji kwa hatua iliyofikia.
“Kwa kweli ninapata maumivu makali sana hivyo ninawaomba wasamaria wema,taasisi na mashirika kunisaidia kiasi hicho cha fedha ikibidi hata kama kuna uwezekano wa kuweza kunitibu mimi nitakuwa tayari tu ,kwani hivi sasa nimeuza kila kitu ikiwemo nyumba,shamba na kiwanja,kwa ajili ya kupata fedha za kujitibu”alisema.
Bi Sekwao hata hivyo alisema kwa wale wote watakaogunswa na kilio changu kwa lengo la kunisaidia ninawaomba watumie namba zifuatazo za simu 068752216007881077530682400989 

I: DIASPORA NA URAI PACHA

$
0
0

Ndugu Kagutta N.Maulidi





Tunapoendelea kufuatilia majadiliano  ya wajumbe maaluum wa bunge la katiba si vibaya tukaweka msisitizo au kuwakumbusha wajumbe wetu kuhusu mada iliyopo katika rasimu ya katiba sura ya tano inayozungumzia  urai pacha.

Nchi yetu bado haitambui uraia wa nchi mbili, kwa maana kuwa ukichukua uraia wa nchi nyingine unapoteza haki ya Urai wako  wa Tanzania. 

Tunashukuru kuwa swala hili limeingizwa katika rasimu ya pili ya katiba,ili liweze kujadiliwa .Sisi Watanzania tunaoishi nje ya nchi   ni matumaini yetu kuwa wajumbe wa bunge maalumu wataliangalia swala hili kwa mapana zaidi na kulikubali kwa faida ya watanzania na nchi yetu kwa jumla.

Wengi wa watanzania wanaoishi nje(Diaspora) wamelazimika  kuomba uraia wa nchi wanazoishi ili kupata haki zao baada ya kuishi na kufanya kazi kati katika nchi hizo kwa muda mrefu.

Watoto:
Zipo nchi zinazowatambua moja kwa moja wanapozaliwa kuwa ni raia lakini pia bado zipo nchi hawatoi uraia kwa watoto wanapozaliwa mpaka wanapofikisha miaka 18. 

Kwa wale ambao wanapewa urai kwa kuzaliwa, moja kwa moja wanakuwa hawawezi tena kuchukua urai wa wazazi wao, na kuendelea kuwa wageni katika nchi  ya asili yao Tanzania. 

Watoto ni hazina kubwa ya taifa letu ,kwa kuwapa uraia wa nchi ya asili yao inawapa fursa ya  kuliwakilisha taifa letu katika michezo ya kimataifa na kuliletea sifa na maendelleo taifa letu. Watapata fursa ya kuutumia ujuzi wao katika kuchangia maendeleo ya taifa letu kiuchumi.
Watoto wa watanzania pamoja na kuwa wamezaliwa ughaibuni lakini wana mapenzi makubwa kwani wanajua wazi  Tanzania ndio kwao kiasili.
Faida za Uraia pacha:

Kwa maoni ya wengi na hivyo ndivyo ilivyo ,sheria ya urai pacha itawapa msukumo diaspora katika kushiriki zaidi katika kuchangia maendeleo ya taifa letu,kiuchumi,kisiasa na kijamii. Watanzania watakuwa wamepata fursa nzuri ya kuwekeza nyumbani na kuongeza ushawishi kwa wawekezaji wa nje kutoka sehemu wanazoishi kuwekeza Tanzania.

Ni imani yangu kuwa asilimia 100% ya watanzania hawakuondoka nchini kwa kuto ipenda nchi yao bali wametoka katika kutafuta,kusaidia familia zao na wazazi wao nyumbani,bado wana mapenzi makubwa na nchi yao,kutokuwepo sheria ya urai pacha ni kuwabana watanzania hao na kuwasababishia kukosa haki na huduma muhimu  katika sehemu wanazoishi.

Mkiangalia katika mitandao utaona jinsi watanzania hawa walivyo na mapenzi na nchi yao,wanajionyesha wazi kabisa hasa wanapo sherehekea sikukuu za kitaifa kwa pamoja na kujaribu kuwa karibu na nchi yao katika siku zenye kumbukumbu kubwa kwa taifa letu. Wanapo pata likizo inawagharimu  kulipia visa ambayo pia ina muda wa kukaa nchi ambayo ndiko kuna kila kitu chake ,wazazi,ndugu,marafiki nk.

Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imetoa kipaumbele na kutambua mchango wa diaspora kwa taifa. serikali imeona umuhimu wa kuwashirikisha diaspora katika ujenzi wa nchi yao na kuwapa nafasi za kuchangia maendeleo kiuchumi,kisiasa na kijamii,hivyo ili kuongeza kuwapa nafasi diaspora kutoa ushirikiano zaidi katika maendeleo ya nchi yetu,Sheria ya uraia pacha ipite,tunaomba ndugu wajumbe mkumbuke kwamba wapo watanzania wengi nje ya nchi wenye ujuzi mbalimbali ambao wangeweza kulitumikia taifa lao kama raia na kupunguza gharama za kuajiri wageni ambao wengine wana ujuzi hata chini ya watanzania hawa.

Wakati umefika wa kufanya hivyo,bila kuangalia tu kuwa eti diaspora wanataka huku na kule. Tuchukue mifano ya mataifa mengine ambayo sheria hii ipo siku nyingi katika nchi zao,hakuna hasara wala madhara kabisa ya kupisha sheria ya urai pacha , zaidi ni faida kwa raia na nchi kwa jumla. 

Mpaka sasa kuna jumuiya nyingi za watanzania zilizoundwa nje ya nchi,lengo na madhumuni ni kuwakusanya watanzania kuwa pamoja na kushirikiana kwa kila hali,kushauriana na kuweza kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.Watanzania hawa pamoja na michango yao mikubwa kwa familia zao (remittance),lakini  wana lengo la kupanga mikakati ya pamoja na kubuni mbinu za kushiriki katika maendeleo ya taifa. Kongamano za diaspora ni ishara ya wazi inayoonyesha jinsi gani wazalendo hawa walivyo na nia ya maendeleo na mapenzi ya nchi yao .

Wajumbe wa Bunge maalumu la katiba pamoja na kujadili vipengele vyote muhimu vya rasimu ya katiba ambavyo ndio msingi na muuongozo wataifa letu,tunawaomba mlijadili kwa kina suala hili kwani tunaolipigania tuko nje lakini sio sababu ya kutotiliwa makazo. Ni matumai yetu suala hili mtalipitisha katika katiba mpya ya nchi yetu kwa faida  yetu,nchi yetu na vizazi vijavyo.

Kwa kufanya hivyo tunaamini kuwa haki ya kidemokrasia ambayo tumekuwa tukinyimwa watanzania ughaibuni itapatikana.Uwekwe utaratibu mzuri ili na sisi tuweze kushiriki katika kuchagua viongozi wetu hasa uchaguzi mkuu wa rais kuanzia 2015.

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU LIBARIKI BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Kagutta N.Maulidi
Mwenyekiti
Tanzanian Diaspora Committee in Italy.
e-mail: tanzaniaitalia.sc.coop@gmail.com 
Tel/fax +39 081 0200142  cell. +39 398 85 83370
 

MWANALIBENEKE DOTTO KAHINDI NA ELIZABETH NGUMA WAMEREMETA

$
0
0
Baada ya kuwa marafiki kwa zaidi ya miaka minane Dotto Paul Kahindi (Mandolin) na Elizabeth Riziki Morris Nguma, Agosti 9, 2014 Mungu amewajalia kufunga pingu za maisha kwenye kanisa la Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Assis, mjini Biharamulo, Kagera.
Dotto Paul Kahindi (Mandolin) na mkewe Elizabeth Morris Nguma katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera.
Mr&Mrs Dotto na wapambe wao Mr&Mrs Frank katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera.
Bibi Harusi akiwa na mpambe wake katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera
Mr&Mrs Dotto, wapambe wao Mr&Mrs Frank, pamoja na wasimamizi wa ndoa hiyo Mr&Mrs Wema Rusasa katika pozi muda mfupi baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera
 
Bibi Harusi na Mameid

Mr&Mrs Dotto (Mandolin) na wapambe wao Mr&Mrs Frank katika picha ya pamoja na wazazi wa pande zote mbili
Maharusi wakiwa na wapambe wengine
Bwana harusi ni Baunsa sana tu
Mr&Mrs Dotto Paul (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya ndugu zao, kutoka kulia ni Mdogo wa bwana harusi Samweli, Kaka wa bibi harusi Deogratius, kaka wa bwana harusi Peter Kulwa na kaka wa bibi harusi Raygan
Bwana Harusi Dotto Paul na Bibi Harusi Elizabeth Riziki wakila kiapo wakati wa misa ya ndoa iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Francis wa Asis, Biharamulo, Kagera
Tumepokea vyeti

Mr&Mrs Dotto Paul wanameremeta
Mr&Mrs Dotto Paul katika picha ya pamoja na kamati ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Rest mjini, Biharamulo, Kagera
Utambulisho
Wakati wa chakula
Mama wa bwana harusi Mary Charles Kahindi

Wakati wa zawadi

Meet The NGOMA AFRICA BAND, the popular and most wanted band based in Germany

$
0
0

 Soulful Vocals,Hypnotic Guitars and the driving Extraordinary rhythm of the "Bongo Dance" from East Africa

The NGOMA AFRICA BAND; known as the (Golden Voice of East Africa) or " FFU- Field force unit" is one of the few amongst african bands in Germany to have touched hearts and left audience dancing and week in the knees.

 Founded in 1993 and led by Tanzanian musician borned Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja - "King of Anunnaki".Every concert is unique, uniting the audience after a few minutes on the dancing floor.

Bongo Dansi –meaning Dance able east african dance, is the "Extraordinary Rhythm" that describes the NGOMA AFRICA BAND and makes the band the people´s choice.Baptized under different names by excited fans – the Annunaki empire, FFU –Field Force Unit.

The NGOMA AFRICA BAND has succesfully written and released several hits amongst others the latest "Bongo Tambarare", repertoires mostly in the native Tanzania and east african Kiswahili language.

Under the leadership and great visionary-Ebrahim Makunja AKA -Kamanda Ras Makunja; the NGOMA AFRICA BAND comprises of africa´s young and most talented musicians, drummers,guitarists bassist,percussionist, dancers amongst others multi-talented  soloist –Christain Bakotessa aka "Chris-B"  Mo Benda,Jessy Ouyah, Flora William, Jonathan Sousa aka "Jo Jo" ,Aj Nbongo making the NGOMA AFRICA BAND a complete travel party of eight vibrant musician and dancers.

Book The NGOMA AFRICA BAND and experience the extraordinary sensational Bongo dansi from East Africa´s best dancable music, best for indoor and outdoor festival and events of all kinds! Give your audience the best of Africa this season with the NGOMA AFRICA BAND

Click here for more and listen www.ngoma-africa.com

El-Maamry afunga ARS ngazi ya taifa

$
0
0
 Mkurungenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akitoa hutuba yake wakati wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars ngazi ya taifa uwanja wa Karume jana.
 Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Said El-Maamry akisalimiana na wachezaji wakati wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars ngazi ya taifa uwanja wa Karume jana.
 Mshambuliaji wa timu ya wasichana ya Amina Ally (jezi nyekundi) akichuana vikali na mlinzi wa Zanzibar Sarah Hashimi katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa Karume jana. Temeke ilishinda 6-1.

MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKUTANO WA DUNIA KUHUSU AMANI NA USALAMA JIJINI SEOUL,KOREA KUSINI

$
0
0
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda  (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese (kulia) na mkewe Bibi Filifilia Tamasese  (Agosti 12, 2014). Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad ambao wameandaa mkutano huo.
    Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda  (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad (kushoto) ambao wameandaa mkutano huo. Kulia ni Dk. Amalberga Kasangala kutoka Tanzania ambaye pia anashiriki mkutano huo
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda  akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na wajumbe wengine wanaoshiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini.
  Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda  akiwa na wajumbe wengine kutoka Afrika Kusini, Japan na Marekani ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).
 Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya, Tanzania na Lesotho ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifuatilia matukio kwenye ukumbi wa Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini.  Wa pili kulia ni Rais mstaafu wa Mali, Prof. Dioncounda Traore. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese na mkewe Bibi Filifilia Tamasese.

TBL YAKAGUA UJENZI WA KISIMA CHA MAJI CHA ZAHANATI YA MAKUBURI KILICHOJENGWA KWA MSAADA WAO

$
0
0
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitanile (wa tatu kushoto) wakiangalia kisima kipya cha maji kikisafishwa katika Zahanati ya Makuburi Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kiwanda hicho Kimejengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 25.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitanile (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Fundi Mkuu wa Kampuni ya Drima Drilling  & Civil Works, Rashid Abdallah walipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kisima cha maji kikisafishwa katikaZahanati ya Makuburi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kiwanda hicho Kimejengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 25..
  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitanile (wa tatu kushoto) wakiangalia kisima kipya cha maji kikisafishwa katika Zahanati ya Makuburi Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kiwanda hicho Kimejengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 25.

Mahojiano ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan

$
0
0
JhikoMan akitumbuiza kwenye Tamasha la Majahazi 2013
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Helsinki Finland mwishoni mwa mwezi Julai 

Amezungumza mengi kuhusu ziara yake ya Ulaya iliyoanza mwezi wa nne, maonyesho aliyofanya, kazi alizorekodi na pia watu aliowashirikisha kwenye albamu yake mpya ijayo. Amezungumzia IMANI ya RASTA na pia MUZIKI WA TANZANIA kwa ujumla Ameongea mengi mema
KARIBU UJIUNGE NASI

SEMINA YA UTHAMINISHAJI MADINI KUFANYIKA BAGAMOYO

$
0
0


 
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
  

TAARIFA KWA UMMA

 SEMINA YA UTHAMINISHAJI MADINI KUFANYIKA BAGAMOYO

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Uthamini wa Madini ya  Almasi na Vito (TANSORT)  inatarajia kufanya  semina ya siku mbili ambayo  itahusisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa  Kanda na   Afisa Madini Wakazi yenye lengo la  kujadili   utendaji kazi, mafanikio pamoja na maboresho ya  tasnia ya vito na almasi nchini.

Semina hiyo itakayofunguliwa na  Katibu Mkuu wa Wizara  Bw. Eliakim Maswi, inatarajiwa kuanza Agosti 14, 2014 na kumalizika  Agosti 15, 2014.


TANSORT itaendesha  semina hiyo  ili kuboresha  shughuli za uthamini wa almasi na madini  ya vito kwa lengo  la kukokotoa mrabaha, kutayarisha miongozo ya bei  za madini  zinazotumika kukokotoa mrabaha, kutoa huduma  za kijemolojia (  Gemological Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati, kusimamia mauzo ya almasi na madini ya vito ndani na nje ya nchi.

Semina hiyo itawawezesha washiriki kutoa maoni yatakayowezesha Kitengo hicho kuboresha  huduma za kutoa ushauri wa masoko, ukataji na ukadiriaji thamani  kwa wachimbaji wadogo  na wa kati, kufanya utafiti wa masoko na bei za almasi na madini ya vito, kutunza takwimu  za uzalishaji  na mauzo ya almasi na madini ya vito na  kusimamia tasnia ya almasi na madini ya vito nchini.

Kitengo cha TANSORT kilianzishwa mwaka 1966 malengo yake yakiwa ni pamoja na kusimamia mrabaha stahiki unaokusanywa na kulipwa serikalini na kuhakikisha madini ya almasi na vito yanayozalishwa nchini yanapata  bei bora.

Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

12 Agosti, 2014
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>