Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

PUB BUSINESS FOR SALE @ KINONDONI MANYANYA

$
0
0
PUB BUSINESS FOR SALE @ KINONDONI MANYANYA: PRICE TSHS. Mil.45
Best located at the Busy-Business-Hub ‘Kinondoni’ along Kawawa (former Morocco) road, near NBC Bank Kinondoni Branch, Puma (the former famous ‘Mwanamboka’) Filling Station and Casablanca Bar; the Lounge is uniquely designed, walls well decorated with modern ‘crazy colours’.  

Night Club lighting is well done to suite today’s market. It is fully air-conditioned, very well furnished with modern and durable local made furniture which will last many years to come. 

The indoor lounge is fully tiled; the counter is fitted with marble top, plus beautiful paintings on the walls. Three (3) 40’ (inch) flat plasma TV sets fitted on different walls of the indoor lounge. Indoor lounge also has an almost brand new Fully-Equipped-DJ-Music-System in its own DJ room, while the outdoor bar has its own music system. There is a small outdoor counter and a big kitchen fully tiled.

The business is on-going with a good customer base with good sales 7 days a week. The place is rented for Tshs. 550,000/= per month, now already paid up to 31st December, 2014. Existing contract is valid until 2017, renewable.

Contacts:
Phone: 0788 893364
Email: tinogobba2002@yahoo.com

KIKAO CHA MKAKATI WA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI ZA KUDUMU KATA CHAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu Meya Manispaa ya Kinondon,Songoro Mnyonge (katikati), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), Agosti 12, 2014 jijini Dar es Salaam mara bara baada ya kufungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha za kujenga zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu (kushoto), Afisa Uhusiano Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera, na kulia. Diwani Kata ya Kawe Othmani Chipeta.
 Mchumi, wa Manispaa ya Kinondoni, Bw.Salm Hamisi Msuya akielezea mchakato wa uchangiaji wa ujenzi wa maabara katika shule 18 za sekondari zilizokuwa na maabara za kudumu wakati wa kikao hicho.
 Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw.Sanga Omari akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
 Diwani kata ya Manzese, Mhe.Eliam Manumbu akichangia mada.
 Wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule wakiwa kwenye kikao chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha za kujenga maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.  HABARI PICHA- NA PHILEMON SOLOMON


MANISPAA  ya Kinondoni inahitaji jumla ya kiasi cha Sh Bilioni 1.3 ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.

Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge  wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha hizo.

Huku akiwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia upatikanaji wa fedha hizo, Songoro alisema ushirikiano wao katika suala hilo utaipa  faraja manispaa hiyo kutokana na umuhimu wa elimu kwa taifa.

“Tunawaomba mjitokeze kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete anayetaka kuona shule zote za sekondari zinakuwa na maabara za kudumu ili kusaidia kupanua wigo wa ufundishaji kw wanafunzi mashuleni, jitihada zetu pekee hazitotuwezesha kufikia malengo hayo kutokana na ufinyu wa bajeti” alisema Mnyonge.

Aidha alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 114 kukidhi mahitaji katika kata 32 huku sekondari 14 ndizo pekee katika zilizo na maabara hizo kati ya 46 zilizopo katika manispaa hiyo suala alilosema linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.

Alisema kila chumba kimoja cha maabara ya kudumu ujenzi wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Sh Milioni 75 na kwa jumla ya vyumba vote 114 inahitajika kiasi hicho cha zaidi ya Sh Billioni 1,suala alilosema haliwezi kufanikiwa bila nguvu za wadau mbalimbali.


Alisema malengo ya baadae ya manispaa hiyo ni kujenga vyumba vitatu vya maabara ya fikizia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016 hatu aliyosema kwa kiasi kikubwa itamaliza tatizo la ugumu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi sambamba na kuongeza wataalam wa baadae wa Taifa hili.

michuano ya Airtel Rising Stars Yaendelea kurindima uwanja wa karume jijini dar

$
0
0
 Nahodha wa Timu ya Ilala, Maisala Adam (kulia) akimiliki mpira asinyang'anywe na mshabuliaji wa Kinondoni, Ibrahimu Chuli wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.
 Mchezaji wa Timu ya Ilala, Hussein Rashid (kulia) akipimana ubavu na Beki wa Timu ya Kinondoni, Miraji Kwangaya wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.
 Mabeki wa Timu ya Kinondoni Fredy Mazuri (Kushoto) na Miraji Kwangaya wakimzuia mshambuliajai wa Timu ya Ilala,Hussein Rashid wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.
Naodha wa Timu ya Kinondoni, Fredy Mazuri (aliyeanguka) akijaribu kumzuia naodha wa Ilala,Shabani Ally (Aliyeruka) asipite wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.

Article 10

KIBONDE, GARDNER WAPANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0

Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani.
Watangazaji hao wakiongozwa na maofisa wa polisi kuelekea mahakamani.
...Wakiingia mahakamani.
MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.

Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.

Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena. (Picha na Shakoor Jongo / GPL)

Airtel na GSMA waandaa semina kuhamashisha matumizi ya Nishati mbadala rafiki wa mazingira Dar es Salaam - Green Power Energy

$
0
0
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa  (wa pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya mbadala kwa wadau wa Mawasiliano ya simu ya GSMA, inayofanyika jijini Dar es Salaam leo.  Kulia ni Meneja wa Programu wa GSMA Mobile, Ferdous Mottakin na Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa Towers Services Ltd, Prakash Ranjalkar.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa  (kushoto), akijadiliana jambo na  Mkurugenzi  wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya Kijani kwa Mawasiliano ya simu ya GSMA, inayofanyika jijini Dar es Salaam jana. 

Bharti Airtel, kampuni ya mawasiliano ya kimataifa yenye shughuli katika nchi 20 mbalimbali Asia na Afrika, leo imeshiriki kuandaa semina ya GSMA inayofanyika Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo tarehe 12 na 13 Agosti 2014 katika hoteli ya Serena. 

 Semina hiyo ya kimataifa ya GSMA inalenga zaidi kutazama maendelea ya sekta ya Mawasiliano kwa kuangalia Zaidi mipango, mafanikio na fursa ya baadaye ya mawasiliano ya nishati mbadala rafiki kwa mazingirana yaani –green telecoms, pia itaendesha majadiliano juu ya mikakati inayowezekana kuongeza maendeleo katika sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira (green power energy). 

 Semina hiyo inahudhuriwa na makampuni kutoka mataifa yapatayo 60 ikiwemo Tanzania, ambapo wanajadiliana na kubadilishana mawazo katika sekta ya mawasiano. Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel alisema, “tunajisikia fahari sana kushiriki katika mabadiliko ya nishati ya kijani yenye lengo la kutunza mazingira ambayo yataleta faida kubwa katika jamii yetu. 

Ushirikiano wetu na GSMA katika kuandaa tukio hili kutatuwezesha pia kuanzisha na kuleta technolojia mpya ambapo tutachangia kwa kutoa mawazo yetu katika mijadala inayohusiana na mawasilano endelevu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla sehemu yetu ya kwa jamii (CSR)”. 

 “Mjadala iliyoandaliwa itajikita zaidi katika mambo yanayohusu teknolojia na maendeleo yake kama vile ufahamu kwenye teknolojia ya nishati ya jua, yaani (solar hybrid technologies) au fuel cell technology na nyingine nyingi. 
Baadaye, wasemaji mbalimbali wataangazia fursa za uwekezaji na miundombinu ya biashara ambazo zitaweza kunufaika na uvumbuzi huu wa matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala–rafiki wa mazingira kutumika kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania”.aliongeza Colaso.

  Akiongea katika ufunguzi rasmi wa shughuli hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa aliwapongeza GSMA na Airtel kwa kazi yao nzuri katika juhudi za kuleta maendeleo kwa jamii kwa kupitia teknolojia ya mawasiliano. vile vile alishukuru sana GSMA kuipa nafasi nchi ya Tanzania kuwa muandaaji wa semina hiyo muhimu kwa mwaka huu. 

Pia kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano hasa kwenye swala la nishati ya kuwezesha minara nchini Tanzania, Prof. Mbarawa alifurahishwa sana na mtazamo wa fulsa hiyo ya utumiaji wa teknolojia ya nishati mbadala rafiki wa mazingira. “kunachangamoto kubwa katika Kuanzisha na kuendeleza miundombinu kwa kizazi kipya hasa kwa nchi zetu zinazoendelea. 

Hivyo, tuna kila sababu ya kukaa na kushirikiana jinsi ya kutumia teknolojia mbadala ili kwa pamoja kupunguza changamoto za ukosefu wa nishati, na kuendeleza ufanisi wa huduma na uhifadhi wa mazingira utakaofaidisha Afrika katika miaka ijayo” , aliongea Mheshimiwa Mbarawa.

Mama Tunu Pinda atunukiwa Cheti cha Ubalozi wa Amani Duniani

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa UPF, Dk. Charles Yang mara baada ya kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja viongozi wenzake 10 waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja viongozi wengine waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini. Walioshika vyeti kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa visiwa vya Samoa, Bibi Filifilia Tamasese , Mke wa Rais wa visiwa vya Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak na Mke wa Rais wa Fiji, Bibi Koila Nailatikau. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).

Mkurugenzi Idara ya Habari( MAELEZO) atembelea vitengo vya Mawasiliano Serikalini

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambeneakiwaonesha Maafisa Habari wa Wizara ya Maji (hawapo pichani) namna Matumizi ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter unavyofanya kazi hasa katika nguvu na kasi ya upashaji habari kwenye jamii, wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelazaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Maafisa Uhusiano Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kutoka kushoto ni Neema Mbuja, Salama Kasamalu na Henry Kilasila wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (hayupo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Dennis Kiilu akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (hayupo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bi. Fatuma Malende.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Adrian Severin akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (hayupo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelzaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akieleza jambo kwa Maafisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) (baadhi hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini yenye lengo la kuangalia utendaji kazi na ufanisi wa vitengo hivyo katika utekelzaji wa majukumu yake ya kila siku leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Adrian Severin na katikati ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Henry Kilasila. [PICHA NA HASSAN SILAYO]


Breking Newz:Msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni unateketea kwa moto hivi sasa.

$
0
0
Msikiti wa Mtambani,uliopo Kinondoni jijini Dar,hivi sasa umeteketea kwa moto na  kusababisha hasara kubwa ya mali zilizokuwemo, Globu ya Jamii baada ya kutaarifiwa kwa tukio hilo  la moto,iko kazini na punde itakuarifu kilichokuwa kikijiri eneo hilo ikiwemo pia na kutaka kufahamu nini hasa chanzo cha moto huo,uliowashtua wakazi wengi wa eneo hilo la Kinondoni na kwingineko. 

Juu na chini ni sehemu tukio hilo la kuteketea kwa moto kwa msikiti huo
wa Mtambani, likiendelea hivi .


Rais Kikwete afanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya 20

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama, amewateua wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.

WATUMISHI WA MAHAKAMA

(i)                 Bw. Penterine Muliisa KENTE, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.

(ii)               Bw. Benedict Bartholomew MWINGWA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.

(iii)             Bw. Edson James MKASIMONGWA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.

(iv)             Bw. David Eliad MRANGO, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Baraza la Ushindani, Dar es Salaam.

(v)               Bw. Mohamed Rashid GWAE, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam.

(vi)             Dkt. John Eudes RUHANGISA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha.

(vii)           Bw. Firmin Nyanda MATOGORO, ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Mwenyekiti, Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam.

MAWAKILI WA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI

(i)                 Dkt. Eliezer Mbuki FELESHI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Mashitaka, Dar es Salaam.

(ii)               Bi. Barke Mbaraka Aboud SEHEL, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

(iii)             Bi. Winfrida Beatrice KOROSSO ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam.

(iv)             Bi. Lilian Leonard MASHAKA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,                      (TAKUKURU), Dar es Salaam.

(v)               Bi. Leila Edith MGONYA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.

(vi)             Bw. Awadhi MOHAMED, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mchunguzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKURURU), Dar es Salaam.

MAWAKILI WA KUJITEGEMEA

(i)                 Bw. Lugano J.S. MWANDAMBO, kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam.

(ii)               Bw. Amour Said KHAMIS, kutoka AKSA Attorneys, Dar es Salaam.

(iii)             Dkt. Paul KIHWELU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemeana na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam.

(iv)             Bi. Rose Ally EBRAHIMU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga.

(v)               Bi. Salma MAGHIMBI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.

WATUMISHI WA VYUO VIKUU

(i)                 Dkt. Mary Caroline LEVIRA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha.

(ii)               Dkt. Modesta Opiyo MAKOPOLO, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe, Morogoro.

Wateuliwa wote wataapisha tarehe 15 Agosti, 2014 Saa 05.00 asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.

Imetolewa na Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo
13 Agosti, 2014

HIVI NDIVYO MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI JIJINI DAR ULIVYOKUWA UKITEKETEA KWA MOTO JIONI HII.

BREAKING NYUUZZZZZZ: MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA MIVUMONI ILIOPO KWENYE MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI YATEKETEA KWA MOTO JIONI HII

$
0
0
 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.

Eneo hilo ambalo lilikuwa likitumika kama Mabweni ya Wanafunzi wa Shule hiyo,Maabara na Ofisi za Walimu limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna kitu chochote kilichoweza kuokolewa.

Jitihada za kuuzima moto huo zimekuwa zikiendelea hadi hivi sasa,huku sehemu ya Waumini wa Kiislam wakijitokeza kwa wingi kusaidia juhudi hizo za kuuzima moto huo zilizokuwa zikiendesha na Kampuni ya Kuzima moto ya Ultimate,japo baadae gari hilo liliisha maji,hali iliyowapelekea Waumini hao kulijaza maji gari hilo kwa kutumia ndoo huku kazi ya Uzimaji moto huo ikiendelea.

Chanzo cha Moto huo,inadaiwa ni hitilafu ya Umeme iliyokuwepo kwenye Bweni la Wasichana Wanafunzi wa Shule hiyo.Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.Picha zote na Othman Michuzi. 
 Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
 Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.
 Sehemu ya Waumini wa Kiislam wakishirikiana kusombelea maji ili kuuzima moto huo. 
 Jitihada zikiendelea. 
  Gari la Zima Moto mali ya Kampuni ya Ultimate Security likijazwa maji kwa ndoo ili kuendelea na zoezi la uzimaji w amoto huo. 
  Likafika na gari hili kwa ajili ya kusaidia kuzima moto huo.
Mashuhuda wakiwa nje ya eneo hilo.

UFAFANUZI WA MADAI TUME YA OPERESHENI TOKOMEZA KUKWAMA

Rais Kikwete, Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Diaspora jijini Dar es salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) ambao umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014. 

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Diaspora Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi. 


Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, wenye kaulimbiu “Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza” (Connect, Engage, Inform and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za uwekezaji na ajira zinazopatikana Tanzania.


Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje 
na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam. 
13 Agosti, 2014

washindi wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” wapatikana jijini dar

$
0
0
 Mshindi wakwanza wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” Laurent Dyanko kutoka chou kikuu cha kilimo, Sokoine University of Agriculture (SUA) akikabidhiwa zawadi wa shilingi milioni moja na cheti cha ushindi
 Mshindi wapili wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” George Firimini kutoka chuo cha usimaniza wa fedha, Institute of Finance Management (IFM) akikabidhiwa zawadi wa shilingi laki sita na cheti cha ushindi
 Mshindi watatu wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” Godlove Kellya kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akikabidhiwa zawadi ya shilingi laki nne na cheti cha ushindi


Washindi watatu bora shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” Laurent Dyanko, George Firmini na Godlove Kellya katika picha ya pamoja na mwakilishi kutoka benki ya NMB, mkuu kitengo cha njia za huduma mbadala.



Afisa mtendaji mkuu wa Dar es Salaam Stock Exchange akiongea na wanafunzi walioshiriki katika shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” wakati wa hafla ya kuwatambua wanafunzi hamsini bora na uandaaji wa mchakato wa kutafuta washindi watatu bora wa shindano hilo. Katikati ni bwana George Kivaria  mwakilishi benki ya NMB (wadhamini wa mashindano) kushoto ni Sosthenes Kewe  Mkurugenzi wa taasisi ya uendelezaji wa huduma za fedha.

 Baadhi ya wanafunzi hamsini bora wakikabidhiwa vyeti vyao na wageni rasmi, wa kwanza kotoka kushoto ni George Kivaria mkuu wa kitengo cha huduma mbadala Benki ya NMB, wapili Sosthenes Kewe Mtendaji mkuu taasisi ya uendelezaji wa huduma za fedha.
 Wanafunzi wa vyuoni wakijiandaa kujibu maswali (kuhojiwa) katika mchakato wa kumtafuta mshindi wa shindano la uzekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014”
 Majaji wakifatilia majibu ya wanafunzi jinsi namna walivyofanya maamuzi ya uwekezaji katika shindano la uwekezakaji “DSE Scholar Investment Challenge”
 wadau wa soko wa soko la hisa la Dar es Salam “Dar es Salaam Stock Exchange” wakifuatilia mchakato wa kutafuta washindi watatu bora.


MH. LOWASSA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati alipo mtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada akifafanua jambo wakati wa Mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimtambulisha Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada pamoja na Ujumbe wake alioambatana nao.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akielezea jambo kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada na ujumbe wake alioambatana nao wakati wa kikao chao kilichofanyika leo ofisini kwake Mwenge,jijini Dar es saalam.Kulia ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) na Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine (kulia) wakimsikiliza Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na namna Ubalozi huo utakavyoweza kufanisha Mradi wa Ujenzi wa Shule na Hospitali katika Wilaya ya Monduli.Wa pili kulia ni Katibu wa Balozi wa Japan,Bw. Sato Firgt.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada mara baada ya kufanya nae mazungumzo ofisini kwake Mwenge,Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada

MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL ATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA UMEME WA GESI NA KUTUNZA MAZAO RIELA NCHINI UJERUMANI

$
0
0
photo
Bw. Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa wanafunzi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013 Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.

Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni Tanzania pekee tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya kilimo Tanzania.

Dorice Mollel amesema “ hichi ni kitu cha muhimu sana nikiwa kama mrembo nikirudi nyumbani na kuieleza jamii inayonizunguka ili kutuletee faida baadae nchini kwetu”.
photo (1)

JUMA KASEJA AWA BALOZI MPYA WA NSSF

$
0
0
Golikipa wa timu ya Yanga, Juma Kaseja, ambaye ni mwanachama wa Hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akikabidhiwa mkataba kutoka kwa  Mwanasheria wa NSSF, Chedrick Komba kuwa Balozi rasmi wa Shirika hilo katika Huduma Mbalimbali zitolewazo na NSSF.
Golikipa wa Yanga, Juma Kaseja, ambaye ni mwanachama wa Hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akisaini mkataba wa kuwa balozi wa NSSF katika huduma mbalimbali zitolewazo na Shirika hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Kulia ni Mwanasheria wa NSSF, Chieldric Komba.

WAZIRI KAMANI ANG'ARA KIMATAIFA, APEWA TUZO

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani (Pichani), amepewa Tuzo ya Utawala Bora katika kipengele cha Watendakazi Bora Serikali barani Afrika kutokana na wizara yake kuonyesha utendaji kazi wa hali ya juu.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Kampuni ya CEO Titans Building Nations ya Afrika Kusini, ambayo imejikita katika kutambua watu na viongozi wanaofanya kazi kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Hilton jijini Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam, juzi jioni mbali na Dk. Kamani, mwingine aliyepata tuzo hiyo ni Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu, aliyenyakua tuzo ya Uongozi Thabiti katika Vyombo vya Habari vya Tanzania.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dk. Kamani alisema hiyo ni ishara ya kuwa serikali na watendaji wa wizara yake wanawajibika kikamilifu.

Alisema wizara yake ina jukumu la kusimamia maendeleo ya mifugo sekta ambayo, imekuwa mkombozi mkubwa wa Watanzania wengi na kuwa, amefarijika kuona utendaji wa wizara yake ukitambulika kimataifa.

“Wakati naalikwa kuhudhuria hafla hii nilijua ni masuala ya utendaji ila sikufahamu kama kuna tukio hili la jitihada za wizara yangu kutambuliwa. “Nimefarijika kuona kazi yetu inatambulika hivyo, tutaendelea kuongeza bidii zaidi ili kutimiza azma yetu ya kuwainua wafugaji na wakulima kwa ujumla kiuchumi,” alisema Dk. Kamani.

Washiriki 100 kutoka taasisi mbalimbali barani Afrika walichaguliwa, ambapo wawakilishi 28 waliingia fainali kuwania tuzo katika nyanja tofauti.

Benki ya Diamond Trust (DTB) yatangaza mafanikio yake makubwa kwa nusu mwaka wa 2014

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB),Bwa.Viju Cherian akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Mapema leo ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano Serena Hotel jijini Dar kuhusiana na ripoti ya nusu mwaka wa 2014 kuhusu utendaji wa benki hiyo kwa ongezeko kubwa la faida kabla yakodi (profit before Tax (PBT) ya sh.billioni 10.3 ikiwa ni  asilimia 38 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2013 sambamba na mafanikio makubwa iliyoyapata benki hiyo.

Bwa.Viju alisema kuwa mwaka 2014 unatoa matumaini ya kuwa mwaka mwingine mzuri kibiashara kwa DTB,alisema kuwa mafanikio yalipatikana katika maeneo yote muhimu ya urari wa mahesabu ya mwaka.''Benki yetu inajivunia kwa mara nyingine kupata faida kubwa ikilinganishwa na benki zingine shindani ikiwa na ongezeko la asilimia 44 katika biashara ya fedha za kigeni na ongezeko la asilimia 30 katika mikopo.Pichani shoto ni Mkuu wa kitengo cha Fedha na Utawawala Bwa.Joseph Mabusi pamoja na mwisho kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Bwa.Sylvester Bahati.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images