Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Mh. Zitto atikisa Mwidau CUP Pangani

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Mwidau CUP leo mjini Pangani.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiingia uwanjani kuzindua mashindano ya Mwidau CUP .Kushoto ni mdahamini wa mashindano hayo ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiwa ameshika ngao ya hisani ambayo iliwania katika mchezo wa ufunguzi wa Mwidau CUP, ambapo timu ya Torino iliibamiza APL ya Mwera bado 2-0.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema hatua ya Tanzania kutofanya vizuri katika michenoa ya kimataifa ni kukosekana misingi imara wa kuinua vipaji kuanzia ngazi ya chini.

Hayo alisema leo mjini Pangani alipokuwa akizindua mashindano ya Mwidau CUP, ambapo asema hatua ya Tanzania kutoka patupu katika mashindano ya Olimpiki ni kielelezo tosha cha kuhitaji maandalizi ya kina.

“Nchi yetu haijapata bahati ya kufanya vizuri kwenye michezo kwani hivi juzi timu zetu zilikuwa katika michuano ya Olimpiki nchini Scotland lakini hatukupata medani hata moja.

“Wiki iliyopita tulikuwa Maputo Msumbiji timu yetu ya Taifa imetolewa kwenye mashindano ya Mataifa huru. Tanzania kwa mara ya mwisho ilishiriki mashindano ya mataifa huru tangu mwaka 1980. Hatujawahi kushiriki tena na sababu kubwa tumesahau kujenga vipaji,” alisema Zitto.

Alisema ni vigumu kumnenepesha ng’ombe siku ya moja ya mnada ila kinachotakiwa ni juhudi kama zilizonzishwa na Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini. Alimtaka mbunge huyo kuhakikisha mashindani yajayo yakuwa na timu za chini ya miaka 17 ambazo zinatasaidia katika kuibua vipaji zaidi.

“Hii itatusaidia kuwajua watoto bado wadogo kwani hapa Pangani wapo kina Ulimwengu na kina Mbwana Samatta. Ninatoa wito kwa mashirika ya umma kuwa na timu zao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwani hii itasaidia kuinua soka letu na hata michezo mingine katika Taifa letu,” alisema.

Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidau (CUF), alisema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na maboresho makubwa ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh 500,000 wa pili 400,000, wa tatu Sh 300,000 huku mshindi wa nne akijinyakulia Sh 100,000.


Timu ya Que Bac Yatwaa Ubingwa wa Mbagala Cup, Yazawadiwa..

$
0
0
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi.  
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindiMgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi. Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi.Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo. Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo.
 
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo. Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo.Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akisalimiana na wachezaji kabla ya kipute kuanza. 
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akisalimiana na wachezaji kabla ya kipute kuanza.[/caption] [caption id="attachment_49509" align="aligncenter" width="640"]Picha ya pamoja kati ya wachezaji na mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John. Picha ya pamoja kati ya wachezaji na mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John.Mashindano ya Mbagala Cup Mashindano ya Mbagala CupKaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi.[/caption] [caption id="attachment_49511" align="aligncenter" width="467"]Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi. Kushoto ni Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John. 
Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi. Kushoto ni Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel JohnMashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia. Mashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia.mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa bora. mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa boraMchezaji bora akipokea kitita cha shilingi laki moja toka kwa mgeni rasmi Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa. Mchezaji bora akipokea kitita cha shilingi laki moja toka kwa mgeni rasmi Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares MagesaTimu kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi. 
Timu kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi.

 TIMU ya Vijana ya Mpira wa Miguu ya Que Bac ya Mbagala Kipati jijini Dar es Salaam jana imeibuka bingwa wa Mashindano ya Mbagala Cup baada ya kuibugiza timu ya mpira wa miguu ya Kipati magoli 2 kwa bila. Que Bac imetawazwa mabingwa na kukabidhiwa Mbuzi, seti moja ya jezi pamoja na mpira. Que Bac ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Kipati ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji wao hatari, Yahya Tumbo (9) alikwamisha mpira katika nyavu za wapinzani baada ya kuunganisha pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake. 


Lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Que Bac walikuwa mbele kwa goli moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo wachezaji wa Kipati waliongeza mashambulizi kwa wapinzani wao kutaka kusawazisha goli lakini goli kipa wa Que Bac pamoja na walinzi wake walikuwa makini na kuondoa hatari zote mara kadhaa langoni mwao. Jahazi la Kipati lilizamishwa zaidi na mshambuliaji wa Que Bac, Shine Duu jezi namba 17 ambaye alifanikiwa kuifungia timu yake goli la pili na kuongeza matumaini ya kutangazwa Mabingwa wa Mashindano hayo (Mbagala Cup). Hadi kipenga cha mwisho Que Bac 2 na Kipati 0. Akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali, Mratibu wa Mashindano hayo, Musa Hemed (Kibwetele) alisema mashindano hayo yalianza rasmi Aprili 5, 2014 ambapo timu 16 zilishiriki katika mashindano huku zikiwa katika makundi mawili, yaani A na B na kila kundi lilikuwa na timu nane. Alisema mshindi wa pili katika mashindano hayo amefanikiwa kupata seti moja ya jezi pamoja na mpira, huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa wachezaji na timu yenye nidhamu. Alisema lengo la mashindano hayo ilikuwa kuwakuza vijana katika vipaji vyao kwenye fani ya mpira wa miguu pamoja na kuwaunganisha vijana kushiriki katika michezo kwa pamoja. "...Sisi eneo letu tumezoea kuona mashindano ambayo yanaanzishwa labda na diwani lakini tena mara moja kwa muda mrefu. Sasa mimi nikakaa na kufikiria nasie vijana tunaweza kujipanga na kuanzisha mashindano kama hayo,...nikazialika timu tukachangishana ada kidogo na hatimaye tukapata mlezi wa mashindano na yamefanyika," alisema Kibwetele. Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi, mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa ameahidi kuyafadhili mashindano hayo kuanzia sasa na atakuwa akiwezesha kufanyika kwake. Mbali na kiongozi huyo kuyafadhili liongeza zawadi kwenye mashindano hayo ambapo alitoa shilingi laki moja moja kwa mchezaji bora, kipa bora na waamuzi na kamati ya maandalizi wa mashindano hayo. Naye Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John alisema lengo la mashindano hayo ni kutaka kuwaleta vijana karibu, kuleta upendo dhidi yao na kudumisha umoja na amani kwa vijana wote. Alisema mashindano kama hayo yanawatoa vijana kutoka katika mtizamo ya wao kukaa vijiweni na kujishughulisha na michezo zaidi ambayo inamanufaa kwao kuliko kushinda wakipiga soga kwenye makundi vijiweni. 

Zimeshiriki Kata tano za Kata ya Mbagala, Kata ya Kiburugwa, Kata ya Kijichi, Mbagala Kuu "Unajua vijana wengi mitaa yetu wanakaa vijiweni si kwamba wanapenda kufanya hivi, wanafanya tu kwasababu wanakosa cha kufanya...sasa kuna kila sababu watu wenye nafasi kujitokea na kuwawezesha ili kuwatoa walipo, nimetokea mimi nimedhamini mashindano yamefanyika, wameshindana na vijana wamepata burudani, upendo na amani pia mshindi kapatikana," alisema. 

Aidha alisema wapo vijana wengi wenye vipaji ambao wanaitaji kupewa nafasi za kushiriki katika mashindano kama hayo na hatimaye vipaji vyao kuonekana na kuendelezwa katika mashindano ya juu. "...Tumeona leo hapa vijana wameondoka na zawadi mbalimbali wachezaji bora wamezawadiwa, timu bora, golikipa bora kapatikana, timu zimejishindia jezi na mipira vyote vyao...timu hizi awali zilikuwa zikicheza na jezi za kukodisha lakini leo wamepata za kwao baada ya kushinda," alisema.

 Kijana huyo alisema anajivunia kuwa sehemu ya kupunguza maovu kwa vijana kwani katika kipindi chote cha mashindano hayo vijana walielekeza nguvu zao nyingi kwenye michezo kimashindano jambo ambalo anaamini limepunguza baadhi wenye nia ovu kubadili mienendo yao kutokana na mashindano hayo. Pamoja na hayo aliishauri Serikali na vyama vya soka kushuka ngazi ya chini mitaani kusaka vipaji vya michezo anuai kwani zipo vingi lakini vinakosa fursa ya kuonekana.

WANAWAKE WOTE DUNIANI TUNALILIA AMANI - MAMA PINDA

$
0
0
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akitoa mada ya ufunguzi kwenye Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama ulioanza leo (Agosti 10, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini
 Mama Tunu Pinda akishiriki katika mjadala wa mkutano huo
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda  (wa nne kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wakuu wanaohudhuria  Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama ulioanza leo
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa tatu kushoto) akiwa na watoa mada wenzake mara baada ya ufunguzi kwenye Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama ulioanza leo (Agosti 10, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini. Kutoka kulia ni mwana wa Mfalme wa kisiwa cha Maori kilichopo New Zealand, Whatumaona Paki; Mke wa Rais wa Fiji, Koila Nailatikau; Mke wa Rais wa visiwa vya Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak, aliyekuwa Balozi wa UN katika Nchi zinazoendelea, Balozi Anwarul Chowdhury na Katibu Mkuu wa UPF, Bw. Tageldin Hamad. Chini ni picha ya pamoja baada ya ufunguzi.
Picha zote na habari na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu
MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wote duniani wanalilia amani na hawapendi vita wala machafuko kwani husababisha amani kutoweka kwenye familia na vifo vya watu wasio na hatia.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumapili, Agosti 10, 2014) wakati akitoa mada kama mzungumzaji mkuu (keynote speaker) kwenye Mkutano wa Dunia wa siku tano ulioanza leo jijini Seoul, Korea Kusini.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na taasisi ya Universal Peace Federation (UPF) ambayo inatoa ushauri kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uchumi na Kijamii unajadili masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo.

Akiwasilisha mada yake kuhusu usalama, amani na maendeleo barani Afrika, Mama Tunu Pinda alisema: “Ninaiomba jamii ya Kimataifa duniani kote tusimamie amani na usalama kwani kinyume na hapo ni kuleta machafuko na vita. Wanawake hatupendi vita wala machafuko...,” alisema huku akishangiliwa.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo wasimame katika nafasi zao kama baba na mama, kama kaka na dada na kuhakikisha kuwa dunia inakuwa ni mahali pazuri pa kuishi. “Ninawasihi tuendeleze maono ya Muumba wetu, tuweke utu mbele kwa kuwajali wengine na tuache kutanguliza maslahi yetu binafsi,” alisema.

Mapema, akiwakaribisha wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi 68 wanaoshiriki mkutano huo, Rais wa UPF, Dk. Thomas Walsh alisema taasisi hiyo inasimamia misingi ya amani, usalama na maendeleo ya jamii kwa nia ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa mbalimbali.

Alisema anatumaini uwepo wa wakuu wa nchi mbalimbali na viongozi mashuhuri, utasaidia kupata majibu ya changamoto inayoikabili dunia juu ya upatikanaji wa amani ya kudumu.

Naye, Mfalme Letsie Mswati III kutoka Lesotho, akizungumza katika mkutano huo alisema dunia inakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa amani kubwa ikiwa ni uharibifu wa mazingira. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanahimiza utunzaji wa mazingira kama njia ya kupunguza matatizo yanayojikeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Alionya kwamba kuna haja ya kuweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha kuwa dunia haiendelei kuwa na matukio ya kigaidi na matumizi ya silaha za maangamizi. “Kama tutakubali vita viendelee kutokea, na migogoro isiyokwisha barani Afrika na nchi za Uarabuni, ni lazima tukubali kuwa hakutakuwa na maendeleo katika mabara haya,” alisema.

MASHIRIKA MBALIMBALI YAOMBWA KUDHAMINI PIA MATAMASHA YA MUZIKI WA INJILI

$
0
0
1
Meya wa jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba. 

 Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula  ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba. Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe aliouwakilisha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba,Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kushawishi makampuni ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili ka ambavyo yamekuwa yakifuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa mfungo wa ramadhan.

'' kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii itasaidia kupunguza gharama za uandaaji, jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika jamii'',alisema Mabula.
01
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pindo la Yesu uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia.
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
6
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo. 
2
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.

Benki ya Exim yaunga mkono kongamano la Badilisha Fikra

$
0
0
 
Wafanyakazi wa idara ya mauzo wa Benki ya Exim Tanzania (kulia) wakizungumza na baadhi ya vijana waliotembelea banda la benki hiyo juu ya huduma zitolewazo na benki wakati wa kongamano la ‘Badilisha Fikra’ lililoambatana na maonyesho mbali mbali iliyoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Vijana (International Youth Fellowship) jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha na mpiga picha wetu).

UNESCO KUPITIA READ INTERNATIONAL WATOA MSAADA WA VITABU VYA SAYANSI KWA SHULE YA SEKONDARI MWEDO ARUMERU

$
0
0
.DSC_0308
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
DSC_0313
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo, Martha Sengeruan.
DSC_0315
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
DSC_0332  DSC_0356
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakishusha maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.


Na Mwandishi wetu, Arumeru
Wanafunzi wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru wamelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Read International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika masomo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara Meijo alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali za masomo ya Sayansi wanalishukuru Shirika la Read International kwa kuweza kuwapatia vitabu hivyo tulivookabidhiwa na UNESCO.

Meijo alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwashirikisha wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji.
DSC_0026
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisalimiana na Mwalimu Clara Meijo mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Aidha alisema kuwa wanafunzi hao ni wale waliokuwa kwenye maeneo ambayo upatikanaji wa elimu yalikuwa mbali, shule hiyo inayomilikiwa na Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) lenye makao makuu yake jijini Arusha huku shule hiyo ikiwa imejengwa kwa michango mbalimbali ya wafugaji kwa kutoa mifugo yao.
“Changamoto kubwa inayoikabili shule yetu ni upungufu wa mabweni, maji na umeme wa kudumu ikisababisha wanafunzi kushindwa kujianda kwa mitihani yao kwa kujisomea nyakati za usiku hali inayoangusha ufaulu kwa wanafunzi hao” alisema Meijo.
Ameiomba Serikali na wafadhili kuwasaidia kupata umeme kwa haraka ilikuweza kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi huku akiomba pia kusaidiwa upatikanaji wa maji safi kwenye shule hiyo na kuongeza kuwa msaada huo wa vitabu umekuja wakati muafaka kwao na utasaidia kukua kwa ufaulu shuleni hapo.
DSC_0037
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo. Kulia ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko aliyeambatana na Bw. Al Amin.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph alisema kuwa wanaimani kubwa kuwa vitabu hivyo vitatumika kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kuwa vitabu hivyo vinatambuliwa na Wizara ya Elimu katika kufundishia masomo ya Sayansi hivyo ni wajibu wenu kama wanafunzi kujifunza kwa bidiii ili muwe mabalozi wazuri katika ujenzi wa taifa.
Bw. Al Amin aliongeza kuwa wanampango wa kuiboresha maktaba ya shule hiyo kwa kuongeza matumizi ya Tehama kwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa ajili ya masomo.
Shule hiyo inawafanyakazi 18 wakiwemo walimu kumi na idadi ya wanafunzi wakiwa 153 huku wanafunzi kumi ni wakutwa na waliobakia ni wa bweni.
DSC_0041
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari ya wasichana ya Mwedo iliyopo wilayani Arumeru jijini Arusha.
DSC_0057
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akizungumza na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes (wa pili kulia) wakati akikagua maktaba ya shule hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolea na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kutoka kushoto ni Mwalimu Clara Meijo, Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo Martha Sengeruan na Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
DSC_0065
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa maelekezo ya namna ya upangiliaji wa vitabu kwenye maktaba hiyo kwa Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes.
DSC_0162
DSC_0101
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akipitia rekodi za uhifadhi wa maktaba hiyo kabla ya kuwaahidi kuleta Kompyuta itakayokuwa "Software" ya kisasa zaidi na kuweza kuwarahisisha kuhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za maktaba hiyo.
DSC_0141
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisikiliza maelezo ya mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shuleni ya sekondari ya wasichana MWEDO anayesaidiana na Mwalimu wake katika kutoa huduma za maktaba ya shuleni hapo.
DSC_0129
Sehemu ya mashelfu ya kuhifadhia vitabu kwenye maktaba ya shule hiyo.
DSC_0386
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) na fisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko wakipata maelezo ya maabara ya shule y sekondari ya wasichana MWEDO kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Sayansi shuleni hapo Bw. Edickiel Mturi.
DSC_0231
Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes akiutambulisha ugeni wa UNESCO kwa wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana MWEDO wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu shuleni hapo.
DSC_0248
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO ambao aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii kuweza kukomboa familia zaidi hapo baadae kupitia elimu

DSC_0019
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akipolewa na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes alipofika shuleni hapo kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.

HITIMISHO LA SHINDANO LA ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WANAZUONI (DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE) KUFANYIKA AGOSTI 13 2014

$
0
0
Soko la Hisa Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange), kwa udhamini wa benki ya NMB, Selcom na FSDT, linapenda kuwajulisha wanafunzi wa elimu ya juu nchini walioshiriki katika shindano la elimu ya uwekezaji kwa mwaka 2014 (DSE Scholar Investment Challenge 2014) kuwa maandalizi yote ya kuhitimisha shindano hili kwa sasa yamekamilika.

Mchakato wa kutambua nafasi ya kila mshiriki wa shindano umemalizika. Majina ya wanafunzi 50 wanaoongoza katika shindano hilo yamebandikwa katika mtandao wa DSE (www.dse.co.tz) kwenye kipengele cha Investment Challenge.

Sherehe za kuwatambua washindi na kuwapatia vyeti na zawadi zitafanyika tarehe 13 August 2014 jijini Dar es Salaam. Mialiko ya kuhudhuria sherehe hizo inaendelea kutumwa kwa njia ya simu.
 (sehemu ya umati wa wanafunzi walioshiriki katika elimu ya uwekezaji kwenye hisa na masoko ya mitaji nchini iliyoendeshwa na DSE kwa wanazuoni).

Shindano la elimu ya uwekezaji kwa wanazuoni (DSE Scholar Investment Challenge) lilianza tarehe 01/04/2014 na kumalizika tarehe 30/06/2014. Wanafunzi washiriki walipewa nafasi ya kutumia simu zao za mkononi ili kununua na kuuza hisa zinazouzwa katika soko la hisa (DSE) la Dar es Salaam. Kila mshiriki alipewa mtaji (virtual capital) wa shilingi milioni moja. Ushiriki kwa shindano hili ulikuwa ni bure na huru kwa yeyote aliyependa.

Nia kubwa ya shindano hili ni kuwapatia vijana walio katika vyuo vya elimu ya juu nchini fursa ya kuwekeza katika soko la hisa kwa majaribio na kuangalia mitaji yao ikikua. Elimu hii pia ni muhimu katika kujenga utamaduni wa utunzaji fedha na uwekezaji miongoni mwa vijana walio vyuoni (ambao ni viongozi, wawekezaji, wahasibu, wachumi, na washauri watarajiwa).

Washiriki walitegemewa kushindana kukuza mitaji waliyopewa kwa kipindi cha miezi mitatu. Mafanikio ya shindano na elimu hii ni makubwa sana. Mwanafunzi anayeongoza amekuza mtaji wake kutoka shilingi milioni moja aliyopewa na kufikisha shilingi milioni nne (kwa kipindi cha miezi mitatu tu).
DSE inawapongeza zaidi ya wanafunzi 5,000 walioshiriki katika shindano na elimu hii muhimu kwao na taifa kwa ujumla.

Shindano na elimu hii imepangwa kufanyika tena mwakani na kuwahusisha wanafunzi wengi zaidi ya elfu tano walioshiriki mwaka huu. DSE imepanga kuwawezesha wanafunzi na vijana nchini kutumia simu pamoja na intaneti mwakani ili kuwapa uwanja mpana zaidi wa kushiriki. Mipango ya baadaye ni kuwashirikisha wanafunzi walioko kwenye shule za sekondari pia.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA MITAALA KWA VYUO VYA KIISLAM, MJINI MOROGORO

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana wakati akiwasili katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake  wakati akiwasili wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, wakati akiwahutubia kwenye ufunguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti matunda aina ya Shokishoki, kwa kumbukumbu baada ya kufungua rasmi  Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Professa wa Chuo cha Sokoine, Ally Aboud, kuhusu ufugaji wa njia raihisi na gharama nafuu wa Samaki baada ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF. Picha na OMR.
Picha ya pamoja.

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2014 LAZINDULIWA KWA KISHINDO JIJINI MWANZA.

$
0
0
Nyota wa  muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho  la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki.
 Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. 
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Diamond na Ney wa Mitego wakioneshana umwamba wa kuwateka mashabiki kila mmoja kwa staili yake,huku miluzi na Shangwe ikiwa imtawala ndani ya uwanja.
 Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Vanessa Mdee a.k.a V Money akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo,tamasha hilo limefanyika mwishoni mwa wiki.

HATIMAYE MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014 AKABIDHIWA ZAWADI YAKE WILAYANI UKEREWE MWANZA

$
0
0
 
Mama Shujaa wa Chakula 2014  Bahati Muriga akitoa neno la Shukurani Baada ya Kukabidhiwa zawadi rasmi zawadi zake Wilayani kwake Ukerewe
Eluka Kibona kutoka Oxfam akimkabidhi ufunguo wa Pikipiki Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula.
Bahati Muriga akijaribisha kuiwasha Pikipiki yake Mara baada ya Kukabidhiwa.
 
 Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akisaini kupokea zawadi zake kutoka OXFAM kupitia Programu ya GROW, Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo Inalipa.
Bwana Hamis Kombo muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe akitoa salamu za pongezi kwa Mama Shujaa wa Chakula 2014 pia kuwashukuru OXFAM kwa kutoa zawadi hizo.
 Bahati Muriga akifurahia zawadi zake

 Kulwa Kizenga wa kwanza kushoto  na Eluka Kibona kutoka OXFAM  wakimkabidhi zawadi Bahati Muriga
 Mkamiti Mgawe wa kwanza kushoto kutoka OXFAM akiwa na Mama shujaa wa Chakulaa
Zawadi alizopokea Mama Shujaa wa Chakula.

***************

Mshindi wa Maisha Plus/Mama shujaa wa chakula msimu wa tatu 2014 Bahati Jacob Muriga jana alikabidhiwa zawadi nyumbani kwake  Ukerewe. Zawadi hizo ni vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi milioni 20 ambapo Bahati Muriga alichagua kununua shamba lenye ukubwa wa ekari 7, pikipiki yenye miguu mitatu aina ya TOYO, vifaa vya kulimo kama vile mbegu, mbolea, mipira ya kumwagilia, watering cane, water pump, spray pump, koleo na dawa za kuondoa wadudu na ukungu, majembe, mundu, engine oil lita 2  na petroli lita 96. 
Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2014 lilifikia tamati mnamo  tar. 18 May, 2014 ambapo Bahati Jacob Muriga ndiye  aliyeibuka kidedea  wa shindano hilo. Mama shujaa huyu ni mkulima kutoka Nansio, Ukerewe mkoa wa Mwanza na pia ni mwalimu mkuu shule ya Msingi Mhozya. Ni mjane mwenye watoto watatu na hutumia kilimo kama nguzo ya kuhakikisha mahitaji ya kifamilia yanatimizwa.

Hafla fupi ya kumkabidhi zawadi zake Bahati zilifanyika katika Ukumbi wa Afro Beach ambapo watu na wawakilishi mbali mbali kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile Kivulini, EMEDO walihudhuria ili  kushuhudia jinsi anavyokabidhiwa zawadi. 

Bw. Kombo, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ukerewe alionesha furaha yake kwa mama shujaa kutoka Ukerewe alisema” Ninayo furaha kubwa na kama kiongozi kijana kuona wilaya yetu imetoa mshindi wa shindano kubwa kama hili na kuiweka ukerewe katika historia na  ramani ya nchi kuwa, kumbe nasi tunaweza, najisikia furaha pia kwa ushindi huu kwani toka anaanza huu mchakato wa kuchukua fomu na kuelekea kijiji cha maisha plus nilikua miongoni mwa niliotoa ushirikiano mkubwa kwa kutoa  ruhusa na araka zangu za yeye kushiriki katika shindano hili kwani ni mwalimu huyu”.

KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS LIMITED YASAINI MKATABA NA MZEE YUSUPH KWAAJILI YA KUSAMBAZA FILAMU YAKE IITWAYO "NITADUMU NAE"

$
0
0

Mzee Yusuph (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa filamu yake ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo imeingia sokoni leo Jumatatu na inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampun ya Proin Promotions Limited, Evans Stephen.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kwa Makini Mzee Yusuph wakati akiongelea Ujio wa Filamu yake Mpya iitwayo NITADUMU NAE ambayo imeingia sokoni leo na filamu hiyo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.

 
 Mzee Yusuph (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Meneja Wake Said Mwangushi (kulia) na Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Evans Stephen (Kushoto) mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Kampuni ya Proin Promotions Limited zilizopo Mtaa wa Ursino Mikocheni
Mzee Yusuph akibadilishana Mkataba na Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Halima Mara baada ya Kumaliza kutiliana saini katika Mikataba.Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited
Hatimaye Mzee Yusuph atambulisha rasmi ujio wake katika Tasnia ya Filamu leo mara baada ya kuitambulisha filamu yake mpya na ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo ni moja ya filamu ambazo zimetoka katika nyimbo zake.
Akiongea na Waandishi wa Habari Mzee Yusuph alisema "Filamu hii nimeitengeneza muda mrefu sana na imetoka katika nyimbo zangu lakini nilishindwa kuisambaza kutokana na kukosa Msambazaji ambaye anaweza kukubaliana na vigezo vyangu lakini Kwa bahati nzuri Proin Promotions imeweza kuwa na vigezo ambavyo mimi nimekubaliana navyo na nimeridhika navyo ndio maana nimeona wanaweza kusambaza filamu yangu" .
Na Pia ameelezea sababu kubwa ya yeye kuamua kufanya kazi na Proin Promotions ni kwamba "Kampuni ya Proin Promotions hainunui hakimiliki za wasanii ndio maana nimeona nifanye nao kazi" 

Vilevile Filamu ya Mzee Yusuph ishaingia sokoni leo na inasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Limited ambapo filamu hiyo inapatikana Nchi nzima kuanzia leo.
Mbali na hiyo pia Mzee Yusuph amesema kuwa sasa anabadili nyimbo zake kwenda kwenye filamu kwasababu nyimbo zake zote zina uwezo mkubwa wakuwa filamu ndio maana kwa kuanza ameanza na Nyimbo yake ya Nitadumu Nae.

TAASISI ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA UZAZI

$
0
0
 Kina mama wakionyesha mfano wa kuwanyonyesha watoto wachanga katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa
 Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
 mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania  Paul Edwards akizungumza. (picha zote na Denis Mlowe)
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akizundua kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto) ni kaimu mkurugenzi wa mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe tanzania Dk. Joyceline Kaganda na katibu tawala mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akionyesha kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo mara baada ya kukizundua rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto)ni katabu tawala mkoa wa Iringa na kulia nimwakilishi wa Unisef tanzania Paul Edwards.
 Wanajeshi wa KJ Mafinga wakiigiza kuhusu janga la Ukimwi katika wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
 
 Wanajeshi wa KJ Mafinga wakiimba kwa hisia kali kuhusu janga la Ukimwi katika wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.

 Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
 Msanii wa marufu nchi Emanuel Mgaya 'Masanja' akiongoza maandamano ya kuadhimisha kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi.

Na Denis Mlowe,Mufindi.

SERIKALI imewataka waajiri katika taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kuzingatia na kulinda sheria zinazowalinda wanawake wanaojifungua kwa kuwapa likizo za uzazi kwa kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake.
 
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa juzi, mgeni rasmi Katibu wa Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo, mwanamke aliyejifungua mtoto mmoja anatakiwa kupewa likizo ya uzazi ya siku 84 na aliyejifungua watoto mapacha anapewa likizo ya siku 100.
 
Alisema likizo hizo zinaambata na malipo kamili ya mshahara na mama aliyejifungua anaweza kuchukua likizo yake ya mwaka akihitaji na mzazi aliyerudi kazini baada ya likizo ya uzazi anapewa ruhusa ya saa mbili kwa siku kwenda kumnyonyesha mtoto.
 
Pallangyo aliwaasa wadau wengine wanaojishughulisha na uuzaji wa maziwa mbadala ya watoto, mikoa na halmashauri zote kujua na kufuata kanuni za kitaifa zilizotungwa chini ya sheria za mamlaka ya chakula dawa na vipodozi sura ya 219 kudhibiti uuzaji na usambazaji wa maziwa mbadala ya watoto pamoja na bidhaa zinazoambatana na vyakula vya watoto.
 
Aidha alivitaka vyombo vya habari kuelimisha wanafamilia na wanawake hasa wanawake wanaojiita wa kileo ambao wanaiga tamaduni za kigeni za ulishaji watoto ambazo mazingira yake ni potofu.
 
“Tungependa kuwaona hawa wanawake wa kisasa wanabadilika na kuelewa kuhusu umuhimu wa kunyonyesha watoto hasa katika miezi sita ya mwanzo ili kuwajengea watoto msingi mzuri kimwilina kiakili hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo kamati za lishe za mikoa na wilaya ili kuhakikisha kwamba elimu inatolewa kwa wanawake wote” alisema Pallangyo
 
Awali Mkuu wa mkoa wa Iringa Christine Ishengoma katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Ayubu Warioba, aliitaka jamii kuelimishana kwenye kaya na jamii kuhusu unyonyeshaji na ulishaji sahihi wa watoto katika ustawi na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema jukumu la kuboresha afya na uhai watoto wa kitanzania ni la wananchi wote likianzia na mtu binafsi na familia kwa ujumla.
 
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania  Paul Edwards alisema shirika hilo na wadau wengine linalenga kuimarisha unyonyeshaji  wa maziwa ya mama kama njia ya ufanisi na kuokoa maisha ya mtoto.
 
Alisema shirika hilo litawajengea uwezo watoa huduma za afya kwenye vituo na wahudumu wa afya vijijini pamoja na watu wengine ambao ni muhimu katika kufanikisha mipango ya kuboresha lishe kwa watoto.


RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA KISIMA CHA MAJI, LAMBO KATIKA KIJIJI CHA JAMII YA WAFUGAJI CHA MBALA,CHALINZE

$
0
0
 Ridhiwani Kikwete akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho. Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana.
 Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua kisima hicho.
 Ridhiwani Kikwete akifungua maji ikiwa ni ishara ya kuzindua lambo la kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Mbala kinachokaliwa kwa asilimia kubwa na jamii ya wafugaji

 Mama mwingine wa Jamii ya Kimasai akitwisha ndoo ya maji na Ridhiwani Kikwete.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akiongozana na akina mama wa jamii ya kimasai waliobeba maji waliyoyateka baada ya mbunge huyo kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani jana. Kisima hicho pamoja na lambo la kunyweshea mifugo vimejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. Kushoto ni Kiongozi wa mradi huo, Joseph Chagama na nyuma yake ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)


 Ng'ombe wakitoka kunywa maji kwenye lambo hilo
 Watoto wa kimasai waonja maji ya kwenye lambo baada ya uzinduzi
 Kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Wasabato la Mbala, ikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, mkoani Pwani jana. Kanisa hilo limejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia) akishiriki katika maombezi
Kwaya ya Kanisa la Wasabato la Manzese wakimwimbia bwana wakati wa hafla hiyo

Kinondoni kutoa Redd’s Miss Kinondoni

$
0
0
KUMEKUCHA! Miss Kinondoni anayemaliza muda wake, Lucy Tomeka, ametamba ni lazima mrembo wa Redd’s Miss Tanzania mwaka huu atoke Kinondoni.

Lucy alisema ana uhakika huo mkubwa kutokana na kuwaona washiriki wa Redd’s Miss Kinondoni na kuona wana vigezo vyote vya kulitwaa taji hilo. Mrembo huyo ambaye atakabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni mwishoni mwa wiki alisema, ana uhakika huo kutokana na uzoefu alioupata wakati akishiriki Redd’s Miss Kinondoni.

“Taji lazima lirudi nyumbani, warembo wa Kinondoni kusema kweli wana sifa zote, wana kila aina ya sifa. Tena mwaka huu naona upinzani ni mkali zaidi kuliko miaka yote, kutokana na sifa ya warembo hao,” alisema Lucy.

Naye Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni, Husna Maulid, alisema warembo 20 wanatarajiwa kuchuana Ijumaa wiki hii ili kumpata mshindi kati yao. “Ijumaa fitina yote inaisha, kinachosubiriwa ni siku tu na warembo 20 wapo katika mazoezi makali kwa ajili ya shindano hilo.”

Shindano la Redd’s Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Escape 1 uliopo Mikocheni, Dar es Salaam huku kukiwa na burudani kali toka Malaika Band inayoongozwa na Christian Bella.  Taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.

Warembo wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti maalumu.

Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s Original, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo, Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu, Greaters Salon, EFM na Mseto.

Temeke yaanza Airtel Rising Stars kwa kishindo

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Omary Rajabu (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya Philipo Edson katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa Karume.
 Mshambuliaji wa wa timu ya vijana ya Temeke, Siaba Salehe (jezi nyekundu) akiwania mpira na kipa  wa timu ya vijana ya Mbeya, Kelvin Dismas (kulia) na beki Yusufu Hongoli katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

 Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Haruna Ally  (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya,Yusufu Hogoli  katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

 Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Haruna Ally (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya, Yusufu Hogoli  katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

 Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Temeke, Haruna Ally (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya vijana ya Mbeya, Yusufu Hogoli katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

Mshambuliaji wa wa timu ya vijana ya Temeke, Siaba Salehe (jezi nyekundu) akiwania mpira  na beki wa timu ya vijana ya Mbeya,Yusufu Hongoli (jezi namba 6) katika mchezo wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa huku mwenzake Elia Salengo (jezi namba 13) akijiandaa kumsaidia.

Timu ya wavulana ya Temeke jana imeyaanza vyema mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa kwa kuifunga Mbeya 2-1 katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja wa kumbu kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. 
Baada ya kosa kosa za hapo na pale kutoka pande zote mbili, Temeke walifanikiwa kuandika bao lao la kwanza katika dakika ya 27 kupitika kwa mshambuliaji machachali Siaba Selehe. Bao hilo lilipokelewa kwa nderemo na vifijo na mashabiki wa Temeke. 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila upande ukitafuta goli na Mbeya waliweza kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Mantony Malewa aliyefanya kazi ya ziada kupangua ngome ya Temeke na kuweka mpira kimiani. 
Goli hilo liliongeza kasi ya mchezo huku Temeke wakisaka goli la kuongoza kwa udi na uvumba na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 70 kupitia kwa Said Mussa. Katika mechi ya wasichana ya fungua dimba ya wasichana, timu ya Ilala ilifanya mauji ya kuungamiza baada ya kuifunga Mwanza 6-0. Dalili za kupoteza mchezo huo kwa vijana wa Mwanza ilianza kuonekana mapema ambapo Ilala walipata goli la kwanza katika dakika ya sita kupitia kwa Rehema Abdul ambaye alifunga manne peke yake. 
Abdul alifunga magoli mengine katika dakika za 38, 47 na 67 huko magoli megine yakigungwa na Arasa Abdul katika dakika za 56 na 65.
 Kwa ujumla Ilala walitawala mchezo katika kila idara. Mechi nyingine zilizotarajiwa kuchezwa jana ni kati ya Zanzibar na Temeke (wasichana) na Ilala dhidi ya Mwanza (Wavulana). 
Mashindano hayo ya kubaina na kuendeleza vipaji ngazi ya Taifa yalitarajiwa kufunguliwa rasmi na Mjumbe wa Heshima wa shirikisho la soka la Afrika (CAF) Said El Maamry. 
Wachezaji 32 watachaguliwa katika mashindano haya ili kuunda timu za wasichana na wavulana ili kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars itakayofanyika nchini Gabon baadaye mwezi huu.

Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala yakaribishwa rasmi Soko la Hisa la Dar es Salaam

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Alhaj Ali HAssan Mwinyi akigonga kengele kuashiria kuingia rasmi kwa kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. David Mestres akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukaribishwa rasmi kwa kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. Ernest Massawe akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukaribishwa rasmi kwa kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar Es Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Alhaji Ali HAssan Mwinyi akipozi kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala Bw. Ernest Massawe(kushoto) na Mkurungenzi wa Swala Bw.Abdullah Mwinyi kwenye sherehe za kukaribishwa rasmi kampuni ya Swala kwenye soko la Hisa la Dar es salaam.
Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi na Mh.Joseph Mungai wakimsikiliza Rais Mstaafu Mh.Alhaj Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa kukaribishwa kwa kampuni ya Swala kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

mama pinda katika mkutano wa Dunia wa masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo jijini Seoul, Korea Kusini.

$
0
0
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wakuu wakifuatilia mada kwenye mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Shirikisho la Wanawake na Amani Duniani  (WFWP) kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho la Kimkoo, jijini Seoul, Korea Kusini leo mchana (Agosti 11, 2014). Kutoka kushoto ni Balozi wa Uruguay nchini Korea, Alba Rosa Legnani, Mke wa Rais wa visiwa vya Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak na wa kwanza kulia ni mke wa Rais wa zamani wa Uruguay, Bibi Mercedes Menafra de Batlle.
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Shirikisho la Wanawake na Amani Duniani (WFWP) pamoja na wake wa Marais mara baada kumaliza mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Shirikisho hilo kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho la Kimkoo, jijini Seoul, Korea Kusini leo mchana (Agosti 11, 2014).
PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA WANASAYANSI VIJANA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta na Gesi.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya sanamu la mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akipokea zawadi ya picha ya mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya ramani ya Afrika, Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR

WAREMBO REDD'S MISS TEMEKE WAJIFUA VILIVYO RIO GYM & SPA EXTRA

$
0
0
 Warembo wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd's Miss Temeke, wakifanya mazoezi ya viungo katika ukumbi wa mazoezi wa Rio Gym & Spa Extra Jengo la Golden Jubilee, Dar es Salaam. Mashindano hayo yatafanyika TCC Club, Chang'ombe Agosti 22, mwaka huu.
 Ni mazoezi kwa kwenda mbele.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.



 Rebecca na Neema Mollel wakiendelea na mazoezi hayo




'HAKUNA DINI YA KWELI INAYOCHOCHEA MAUAJI'

$
0
0

MJUMBE wa Baraza la Uendeshaji la UNESCO linalosimamia ukuzaji wa utamaduni, Dk. Mary Mbiro Khimulu amesema machafuko na mauaji hayana uhusiano wowote na dini ambayo ni ya kweli.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Agosti 11, 2014) wakati akishiriki mjadala wa jinsi ambavyo bara la Afrika linakabiliana na migogoro inayotokea barani humo kwenye mkutano wa Dunia unaojadili masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo jijini Seoul, Korea Kusini.

Dk. Khimulu ambaye ni raia wa Kenya, alisema: "Dini ya kweli haiwezi kuruhusu umwagaji wa damu, hakuna dini ya kweli inayochochea mauaji wala kuruhusu mapigano. Ninawasihi wote mliopo hapa, msiruhusu dini zenu zitumike kufanya mambo mabaya."

Dk. Khimulu alisema ili kuepuka migogoro ya dini, anashauri diplomasia ya utamaduni (cultural diplomacy) itumike kuleta amani, usalama na maendeleo barani Afrika. "Kwa kuitumia diplomasia ya utamaduni, tuangalie ni kwa njia gani mijumuiko ya pamoja ya kidini (inter-faith communities) inaweza kutumika kuleta amani, upendo na mshikamano kwenye jamii tunazoishi," alisema.

Vilevile, Dk. Khimulu alisema kwa kutumia diplomasia ya utamaduni tunaweza kuvunja chuki na kuleta mshikamano na umoja miongoni mwa watu wetu, watu wakatembeleana kupitia michezo, nyimbo au matamasha, na wakajenga mahusiano ya kuheshimiana kidugu.

Alisema kwa kuwa vita huanzia akilini mwa mwanadamu, ni humo humo ambamo mawazo ya kuacha mapigano ama machafuko yanapaswa kuingizwa. "Kwa hiyo tuitumie diplomasia  ya utamaduni kama njia pekee ya kujenga mahusiano ya karibu kwenye jamii zetu na itusaidie kufikia malengo yetu ya kupata amani na usalama kwa watu wetu,"aliongeza.

Mapema, Balozi wa Kudumu wa AU kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Antonio Tete alisema wakati Umoja wa Afrika unaanzishwa mwaka 1963, baadhi ya wakuu wa nchi walikuwa na ndoto ya kuwa na jeshi moja barani  Afrika ambalo lingekuwa na kazi ya kukabili migogoro yote barani humo.

"Kutokana na mabadiliko ya wakati na kadri muda ulivyosonga mbele, matarajio yao hayakutumia. Viliundwa vikosi vya muda navyo havikudumu. Tumeshuhudia miaka ya 90 kwenye migogoro ya Rwanda na ya Somalia. Hakuna jeshi lilipelekwa wala hakuna askari waliokuja kutoka nje," alisema.

Alisema Umoja wa Afrika unakabiliwa na changamoto ya kukosa fedha za kujiendesha kubwa likiwa ni la kusimamia amani na usalama wa nchi wanachama. “Tunayo programu ya ulinzi na usalama lakini asilimia 90 ya mpango huu inachangiwa na wafadhili kutoka nje ya nchi. Hii siyo kazi rahisi... huwezi kujiendesha namna hii,” alisema.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni kuwepo kwa vikund vya kigaidi. “Hawa wanaendesha mambo yao tofauti na kwa teknolojia ya hali ya juu, hata ungekuwa na jeshi la aina gani si rahisi kuwashinda... huwezi kutumia njia za kawaida za kupambana na uhalifu unapokabiliana na makundi ya aina hii,” alisema.

Katika hatua nyingine, Balozi Tete aliwaomba baadhi ya washiriki wafikirie kuwekeza barani Afrika kama njia mojawapo ya kuleta amani ya kudumu katika bara hilo. “Kwa muda mrefu bara hili limetumika kama chanzo cha malighafi kwa viwanda vya Ulaya na Amerika. Ni wakati sasa tubadili muelekeo na tufikirie kuwekeza katika bara hili kwani kwa kufanya hivyo mtasaidia kutengeneza ajira nyingi kwa vijana wa Afrika kupitia viwanda ambavyo mtavijenga.”

“Kukiwa na ajira za kutosha, mtaleta maendeleo na mtaleta amani kwa vile mtapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro na machafuko yanayotokana na kugombea rasilmali haba zilizopo,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 11, 2014
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images