Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

PUB BUSINESS FOR SALE @ KINONDONI MANYANYA

0
0
Best located at the Busy-Business-Hub ‘Kinondoni’ along Kawawa (former Morocco) road, near NBC Bank Kinondoni Branch, Puma (the former famous ‘Mwanamboka’) Filling Station and Casablanca Bar; the Lounge is uniquely designed, walls well decorated with modern ‘crazy colours’.  Night Club lighting is well done to suite today’s market. It is fully air-conditioned, very well furnished with modern and durable local made furniture which will last many years to come. 

The indoor lounge is fully tiled; the counter is fitted with marble top, plus beautiful paintings on the walls. Three (3) 40’ (inch) flat plasma TV sets fitted on different walls of the indoor lounge. Indoor lounge also has an almost brand new Fully-Equipped-DJ-Music-System in its own DJ room, while the outdoor bar has its own music system. There is a small outdoor counter and a big kitchen fully tiled.

The business is on-going with a good customer base with good sales 7 days a week. The place is rented for Tshs. 550,000/= per month, now already paid up to 31st December, 2014. Existing contract is valid until 2017, renewable.


Phone: 0788 893364

Email: tinogobba2002@yahoo.com

TTCL YAZINDUA HUDUMA YAKE MPYA YA BWERERE.

0
0
 Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
 Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
=======  ======= =======
Bwa.Peter alisema kuwa siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promosheni inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la  BWERERE   yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.

''Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na maofisini ambao wanatumia  huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe,

Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA)  kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo''.Alisema Bwa.Peter Ngota.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA PETER MUTHARIKA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika aliyemtembelea kumjulia hali kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambapo wote walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akisalimiana na Mama Salma Kikwete alipomtembelea kumjulia hali Rais Kikwetev kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo marais hao walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akiomngea na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, alipomtembela kumjulia hali Rais Kikwete. Viongozi hao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akisalimiana kwa furaha na mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika walipokutana kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika, wakiongea kwa furaha walipokutana kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. 

Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili. PICHA NA IKULU

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 KESHO NDIYO KESHO TAIFA

0
0
SIKU iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali imewadia ambapo kesho Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa patakuwa hapatoshi wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua nafasi.
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli.
Akizungumza na Centre Spread, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kuwa maandalizi yote yameshafanyika na tayari mkali wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na ngoma ya Johnny, Yemi Alade ameshatua nchini, kinachosubiriwa ni burudani mwanzo mwisho.

“Kila kona ya burudani imeshakamilika hivyo kama wewe ni mpenzi wa ndondi kuna ngumi kati ya mabondia Mada Maugo dhidi ya Thomas Mashali, JB dhidi ya Cloud 112, Said Memba dhidi ya Khalid Chokoraa na wengineo.
Navy Kenzo.
“Wapenzi wa Bongo Fleva, kutakuwa na mfalme wao, Ali Kiba akiwa sambamba na mastaa kama Shilole, Madee, R.O.M.A, Meninah, Navy Kenzo, Scorpion Girls, Juma Nature na wengine kibao,” alisema Maloto na kuongeza:“Kwa wale wapenzi wa soka basi watakutana na mechi kabambe kati ya Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga, Azam Fc dhidi ya Mtibwa, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na wengine wengi.”
Ally Kiba.
Maloto aliongeza kuwa jukwaa litashambuliwa pia na wanamuziki wa nyimbo za Injili kama Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Angel na wengine wengi. Tamasha la Usiku wa Matumaini linatarajiwa kuanza kesho saa 5 asubuhi hadi saa 6 usiku ambapo wapenzi wa burudani watainjoi mambo yote kwa kiingilio cha shilingi elfu 5 tu.

MBUNGE JOSHUA NASSARI AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO WA BARA LA AFRIKA

0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Jesse Jackson, Mwanaharakati wa siku nyingi wa Haki na Usawa.Kushoto ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani Afrika Kusini (Democratic Alliance) Mbali Ntuli.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na Waziri mkuu wa Mauritius, Ramgoolam.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na rais wa Uganda Yoweri Mseveni .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiteta jambo na Seneta Christopher Coons ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Marekani anayesimamia maswala ya Afrika.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiteta jambo na Balozi Suzan Rice ,mshauli wa Rais Obama maswala ya Usalama..
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo,Joseph Kabila.

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA BARA LA AFRIKA,JIJINI WASHINGTON DC

0
0
o3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.o6 o7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014o8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014
o2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.

Sikiliza Mahojiano na Mtaalamu wa Uchumaji Asumini Bi Kijakazi Hassan

0
0
Blog ya Swahilivilla Siku ya Jumamosi July 19 2014 ilifanikiwa kufanya Mahojiano na mtaalamu wa uchumaji wa mauwa ya asumini Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa, a.k.a (Kijakazi) ambae alielezeaa mengi kuhusu umuhimu wa Asumini pamoja na utunzani wake.
Mtaalamu wa uchumaji asumin Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa akiwa katika harakati za uchumaji wa mauwa ya yenye harufu nzuri asumin
Katika Mahojiano haya na mtaalamu wa utunzaji wa Miasumini Kijakazi Hassan Mustafa ambae ni mkaazi wa Mwembetanga Zanzibar atuelezea mambo mbali mbali kuhusu umuhimu wa ujumaji na utuzaji wa mauwa ya Asumin, ya kiwemo kusingwa kwenye sherehe za harusi na hata kutengezea uturi pamoja na vikuba vyenye harufu nzuri ya kunukia.
Asumini ni BUSTANI ya mapenzi yenye mauwa madogo yenye kutoa harufu nzuri, huchumwaa kwa kuwekewa kitandani ili bwana asitoke ndani wakti muwafaka wajioni.
Kwa mawazo zaidi wasiliana nasi kwa njia ya Email: swahilivilla@gmail.com
Ungana nasi taratibu kusikiliza mahojiano haya.

MFUKO WA UTT WATOA ELIMU KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA WAKULIMA JUU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI MKOANI LINDI

0
0
Ofisa Masoko wa UTT, Rahim Mwanga akitoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuhusu, mifuko ya uwekezaji inayoendeshwa na UTT. 
 Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Ofisa Masoko wa UTT, Rahim Mwanga.
 Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, wakimsikiliza Ofisa Masoko wa UTT, Rahim Mwanga wakati akitoa mafunzo kwa watumishi hao juu ya mifuko ya uwekezaji inayoendeshwa na UTT. 
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusino wa UTT akitoa elimu kwa wakulima wa wilaya ya Tandahimba juu ya mifuko ya uwekezaji inayoendeshwa na UTT kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayofanyika mkoani Lindi. (Picha kwa Hisani ya UTT).

TTCL YAZINDUA HUDUMA YAKE MPYA YA BWERERE

0
0

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI NCHINI

0
0
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai 2014 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa-MAELEZO.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa ongezeko dogo la mfumuko wa bei nchini kutoka asilimia 6.4 za mwezi June hadi asilimia 6.5 za mwezi Julai 2014 linatokana na kupanda kwa bei za baadhi ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo Bia, Sigara, mavazi kwa wanaume na yale ya watoto zimechangia ongezeko hilo.

Aidha, huduma na bidhaa nyingine zilizochangia ongezeko hilo ni gharama za udobi, kodi za pango, mazulia na mkaa wa kupikia Bw. Kwesigabo amefafanua kuwa hali ya mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Julai umepungua hadi 7.9 kutoka asilimia 8.5 kutoka asilimia 8.7 za mwezi Juni huku badiliko la fahirisi za bidhaa zisizo za vyakula likiongezeka hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Julai 2014 kutoka asilimia 4.8 iliyokuwepo mwezi uliopita.

Kuhusu mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi amesema kuwa umeongezeka kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.6 kama ilivyokuwa kwa mwezi Juni mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 149.16 kutoka 148.98 za mwezi Juni 2014.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kutoka mwezi Septemba 2010 hadi Julai 2014 umefikia shilingi 67 na senti 04 kutoka shilingi 67 na senti 12 za mwezi Juni mwaka huu.

“Kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa na huduma kwa mwezi uliopita kunamaanisha kwamba, uwezo wa fedha yetu katika kununua huduma na bidhaa hizo unaupungua hii inamaanisha mfumuko wa bei unapopanda thamani ya shilingi nayo inashuka” Amebainisha.

Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 7.67 kwa mwezi Julai 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.39 za mwezi Juni huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 4.3 mwezi huu ikilinganishwa na asilimia 5.0 za mwezi Juni.

WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA WAMIMINIKA KWA WINGI NA KUJIUNGA NA MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU WA GEPF

0
0
p2Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko kutoka katika Mfuko wa GEPF akifafanua jambo kuhusu  mafao yatolewayo na Mfuko wa GEPF katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arusha.p1Mwanachama mpya akipata maelekezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa GEPF kutoka kwa Afisa wa GEPF Bi Jane Rutashobya katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arushap4Afisa Masoko Clement Oningo akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF kwa wakazi wa jiji  la Arusha waliofika katika banda la GEPF.DSC_4775
DSC_4826Muonekano wa banda la GEPF katika viwanja vya nane nane jijini Arusha.Meneja Masoko Aloyce Ntukamazina ,   Alitoa wito kwa wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya nane nane ili kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huo. “Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika maonyesho haya na kuja kutembelea katika banda letu na kuweza kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huu”alisema Ntukamazina.

WANAFUNZI WA SEKONDARI YA WASICHANA MAKETE WATAKIWA KUWA MFANO BORA KIELIMU NA KITABIA

0
0
Wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa Makete Girls Sekondari (hawapo Pichani)
Maktaba ya shule hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (wa tatu kushoto) akiwa na walimu wa shule hiyo, wa kwanza kulia ni Afisa Taaluma sekondari wilaya hiyo.
===
Wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule pekee ya wasichana iitwayo Makete girls secondary School iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuzingatia masomo na kuwa mfano bora wa kuigwa toka shuleni hadi sehemu wanazotoka

Aidha kwa kufanya hivyo kutapelekea wafaulu vizuri masomo yao na kuhakikisha lengo la serikali kuanzisha shule hiyo linafikiwa hasa kuinua kiwango cha ufaulu kwa wasichana katika wilaya hiyo

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro wakati alipofanya ziara katika shule hiyo hii leo kwa lengo la kujionea maendeleo na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ili zitafutiwe ufumbuzi ikizingatiwa shule hiyo ni mpya, ambapo akiwa shuleni hapo pamoja na mambo mengine amekula chakula cha mchana na wanafunzi hao

Akizungumza na wanafunzi hao Mh. Matiro amewataka wanafunzi hao kuepuka wanaume walaghai ambao hutumia njia mbalimbali kuwarubuni hasa wanaporudi majumbani mwao wakati wa likizo na kusema kuwa hategemei tatizo la ujauzito kuwakumba wanafunzi hao endapo watakuwa msimamo wa kuzingatia masomo tu

"Tunategemea shule hii iwe ya mfano na ninyi ndio wenye uwezo wa kuifanya hivyo, hii shule ni mpya na ninyi ndio wanafunzi wa kwanza kusoma hapa, tunategemea mfaulu vizuri, sisi tunajitahidi kwa kila namna kuboresha shule hii, ninyi kazi yenu ni kusoma tu, acheni mzaha someni kwa bidii, kila jambo na wakati wake, wakati mlio nao sasa ni wa kusoma tu na si vingine" amesema Matiro
 
Kwa upande wa wanafunzi hao akiwemo Prisila Haule, Jema Kyando na Florida Ngogo wametaja changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa vifaa vya michezo, ukosefu wa waalimu wa sayansi, shule kukosa gari, pamoja na shule kukosa matroni.

Mkuu wa shule hiyo Bi. Sayuni Sanga amesema ni kweli shule ina wajibu wa kumuajiri matroni lakini kwa sasa haiwezi kufanya hivyo kwa kuwa shule hiyo ni changa na haina uwezo wa kumlipa ila kwa sasa mwalimu mmoja amejitolea kuwa matroni hadi hapo atakapopatikana matroni halisi

Kuhusu michezo mwalimu wa michezo shuleni hapo Bw. Japhet Mwile amesema wanashindwa kuainisha maeneo ya viwanja vya michezo kutokana na maeneo hayo kuwa na mazao ambayo hayajavunwa na kwa sasa wanasubiri yakishavunwa waanze kuandaa viwanja kwa kuwa walikubaliana na wazazi kuwa wakishavuna mazao yao hawatalima tena mashamba hayo kwa kuwa kwa sasa ni mali ya shule

Shule hiyo imeanza rasmi Aprili 22 mwaka huu na ina wanafunzi 36 na walimu wanne, huku changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni ukosefu wa mabweni ambapo serikali imeahidi kupambana kuitatua changamoto hiyo kwani kwa sasa wanafunzi hao wanalala madarasani.

Habari/picha na Edwin Moshi.

BODI MPYA YA BARAZA LA HABARI YAZINDULIWA

0
0
Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila akihutubia katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania kwa niaba ya Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, Agosti 7,2014.
 Rais  wa Baraza la Habari aliyemaliza muda wake  Jaji Mstaafu Dk. Robert Kisanga  akihutubia katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania ambapo alisisitiza umuhimu wa Baraza la habari na kutaka liungwe mkono kufanikisha malengo yake .Dar es Salaam, Agosti 7,2014.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga akizungumza wakati wa kutambulisha Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania kwenye Hoteli ya Blue Pearl Dar es salaam,Agosti 7,2014.
 Baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania.

 Meneja wa Udhibiti na Viwango wa Baraza la Habari Tanzania Pili Mtambalike (Kushoto) akifuatiwa na Meneja wa Rasilimali Watu wa Baraza la Habari Tanzania Ziada Kirobo, Meneja wa Fedha wa Baraza la Habari John Nguya na Mjumbe mpya wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Profesa Bernadetha Killian wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.
 Rais wa Baraza la Habari Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akipokea cheti cha kumaliza muda wa kutumikia Bodi iliyomaliza muda wake kutoka kwa Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila .
 Rafii Haji Makame mjumbe wa Bodi iliyomaliza muda wake akionyesha cheti alichokabidhiwa katika sherehe za kuaga bodi ya zamani na kuzindua bodi mpya ya Baraza la Habari, kulia ni Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila na kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga.
Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila akimkabidhi cheti Mjumbe wa Bodi iliyomaliza muda wake Ussu Mallya wakati wa sherehe za kuzindua Bodi Mpya na kuiaga ya zamani kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es salaam.
 Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania Ndugu Badra Haji Masoud wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi mpya ,wajumbe waliomaliza muda pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa Bodi hiyo .
 Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania.
Wajumbe wa Bodi Mpya na iliyomaliza muda pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi mpya Jaji Shaban Ally Lila (wa tatu kusoto walioketi).Picha kwa Hisani ya Adam H. Mzee wa kamerayangublog.com

DKT. Fenela Ziarani China

0
0
Waziri wa Habari,  Vijana,  Utamaduni na Michezo Dkt.  Fenela Mukangala yuko nchini China katika ziara ya kuangalia maendeleo ya Sekta ya Utangazaji na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Utangazaji kati ya Tanzania na China.Katika ziara hiyo ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga,  Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw. Clement Mshana na Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Bwana Habbi Gunze.

Pichani ujumbe wa Waziri ukitembelea sehemu mbalimbali zikiwemo studio na vivutio mbalimbali vya Utangazaji katika kituo cha Tv cha Jimbo la Sichuan nchini China.

tazama hii kuhusu sanaa ya tanzania


shule ya msingi kibamba yapata kitengo cha wenye ulemavu wa akili

0
0
Kitengo (madarasa) cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili, shule ya msingi kibamba. Kitengo kimejengwa na Bw Rupin Rajani wa Rajani Group kupitia DSM Mentally Handicapped Children Support Group.
Kibao kinacho onesha wafadhili wa kitengo hiki.
Bw. Rupin Rajani na wanachama wa DSM Mentally Handicapped Children Support Group nje ya darasa moja wapo.
Bw. Rupin Rajani ndani ya darasa lenye wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika shule ya msingi Kibamba, pamoja na waalimu wa elimu maalum na Mama Evelyne DSM Mentally Handicapped Children support Group.

NIGHT OF HOPE 2014: UPENDO NKONE AKITOA MATUMAINI NDANI YA UWANJA WA TAIFA DAR

0
0
Mwimbaji wa Injili, Upendo Nkone akiwapa matumaini wananchi waliohudhuria Usiku wa Matumaini muda huu ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Upendo Nkone akiwapa burudani wapenzi wa Gospel ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
Umati wa watu ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
Nkone akizidi kufanya yake pamoja na vijana wake.
Baadhi ya wanahabari na wadau wakifuatilia tamasha hilo.

WAKULIMA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI MAZA

0
0
 Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia (kulia) akiwa na baadhi ya wakulima wa ufuta wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana, katika banda la Farm Afrika kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha.
Watanzania wenye asili ya bara Asia wakipewa maelezo ya ubora wa mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha.
 
Wakulima wametakiwa kutumia fursa ya kuongeza thamani mazao yao ili waweze kunufaika zaidi kiuchumi kuliko kuuza mazao yao yakiwa ghafi kwani watakuwa wanayonywa na kuzidi kuwa masikini.
Wito huo umetolewa jana na Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane, kanda ya kanda ya kaskazini yanayoendelea jijini Arusha.  
Alisema kupitia Farm Africa wakulima wengi wa ufuta wa mkoa huo wamenufaika kiuchumi kutokana na kuongeza thamani mazao yao na kutouza yakiwa ghafi hivyo kujiongezea kipato zaidi kinachowaletea maendeleo.
“Farm Africa inawataka wakulima nchini waje wajifunze kupitia wakulima wetu wa ufuta,

MAKAMU WA RAIS AIPA TUZO VETA KWA KUIBUKA WASHINDI WA KWANZA NANE NANE KITAIFA

0
0
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharibu Bilali akikabidhi tuzo ya Ushindi wa kwanza Kitaifa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kuibuka washindi wa jumla katika Kundi la Taasisi za Utafiti na Mafunzo. Anaepokea ni Mkurugenzi Masoko, Mipango na Maendeleo,  wa VETA - Tanzania, Enock Kibendera
Wafanyakazi na wanafunzi wa VETA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka washindi kitaifa hii leo katika siku kuu ya Nane Nane iliyofanyika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

KONGAMANO LA KWANZA LA TANZANIA DIASPORA INITIATIVE KUFANYIKA AUGUST 14 - 15,2014 JIJINI DAR

0
0
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images