Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDIUA MSIMU WA FIESTA 2014

$
0
0
Mmoja wa wasanii watakaotoa burudani katika matamasha ya mwaka huu ya Serengeti Fiesta, Vanessa Mdee akizungumza wakati wa uzinduzi wa  tamasha la muziki la mwaka huu la Serengeti Fiesta litakaloanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapo. Kushoto kwake ni Meneja wa Bia ya Serengeti, Rodney Rugambo na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Sebastian Maganga . 

Fiesta ya mwaka huu inadhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la leo ni, Diamond Platinum, Ommy  Dimpos, Linah, Chenge, Temba, Shilole, Ally Kiba, Mr. Blue, Mwana FA, Young Killer, Ben Pol, Christian Bella, Roma, Ney wa Mitego, Mkubwa na wanae, Barnaba, Belle 9, Rachel na Madee.

NIGHT OF HOPE 2014: BONGO FLEVA 1, BONGO MOVIES 0

$
0
0
Mchezaji wa Bongo Fleva, Ali Kiba akimtoka msanii wa Bongo Movies, Issa Mussa 'Cloud 112'.
Mwanamuziki H-Baba akijaribu kuwatoka wachezaji wa Bongo Movies.
Nyomi ndani ya Uwanja wa Taifa ikifuatilia mechi hiyo.
Kikosi cha Bongo Movies.
Kikosi cha Bongo Fleva.
Bongo Fleva wakisalimiana na Bongo Movies kabla ya mechi.
Bongo Movies kabla ya kuanza mtanange dhidi ya Bongo Fleva.

Bongo Fleva wakisali kabla ya mechi.

Kikosi cha timu ya Bongo Fleva kimeibuka kidedea katika mtanange wao dhidi ya Bongo Movies kwenye Tamasha la Usiku wa Matumanini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mfungaji wa bao pekee la Bongo Fleva ni mwanamuziki Ali Kiba.

MARAIS WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA WA WAWEKEZAJI MAREKANI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wa nchi za Jumuiya ya Mashariki, Mhe Paul Kagame wa Rwanda, Mhe Yoweri Museveni wa Uganfda, Mhe Uhuru Kenyatta wa Kenya na MhePierre Nkurunzinza wa Burundi wakati wa mkutano wao na wawekezaji wa Kimarekani uliofanyika katika makao makuu ya chama cha wafanyabiashara (US Chamber of Commerce) jijini Washington DC. PICHA NA IKULU

AJALI ENEO LA AFRIKANA, MBEZI BEACH MCHANA WA LEO

$
0
0
 Gari aina ya Nissan Hard Body yenye Namba za Usajili T 524 ALW likiwa limetupwa mtaroni na trela la lori (halipo pichani) ambalo lililigonga gari hilo na kutumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach Mchana wa leo. Katika Ajali hiyo iliyohusisha Lori na gari aina ya Nissan Hard Body hakuna mtu yoyote aliyepoteza Maisha
 Wananchi wakisaidia Kulifunga minyororo gari aina ya Nissan Hard Body ambayo imetumbukia mtaroni mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo katika Eneo la Mbezi Afrikana
Wananchi wakisaidia kuligeuza gari ndogo aina ya Nissan Hard Body iliyotumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo, katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha. Picha zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

WABUNGE WA YANGA WAISAMBARATISHA SIMBA TAMASHA LA MATUMAINI 2014

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ni shabiki wa Yanga, Ridhiwan Kikwete akivua jezi yake kwa ajili ya mashabiki mara baada ya ushindi wa timu yake wa mabao 3-2 dhidi ya Simba leo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akishangilia na shabiki wake baada ya ushindi wa Yanga.
Mwigulu Nchemba akiwarushia skafu yake mashabiki wa Yanga.
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba.
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
Mashabiki wakifuatilia mtanange huo.
Timu zikiingia uwanjani.
Ridhiwan akiwapa hi mashabiki.
Waamuzi wakiingia uwanjani.
Kikosi cha Yanga kilichokwaana na Simba na kuibuka na ushindi wa 3-2.
Kikosi cha Simba kilichopigwa 3-2 na Yanga.
Mwamuzi Othman Kazi akiongea na manahodha wa Yanga na Simba (Wabunge). Mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 imemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2. Wafungaji Simba: Maji Marefu na Yusuf Gogo. Yanga: Idrissa Kitwana, Ahmed Ngwali na Mark Tanda.

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE KITAIFA MKOANI LINDI

$
0
0
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wakulima Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Watoto waliotembelea Banda lka WQizara ya Viwanda na Biashara.
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wakulima Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mmshiriki akionesha bidhaa za Ngozi ndani ya mabanda ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akizungumza na Waandishi wa habari.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akiwa anatembelea mabanda ya maonesho.


Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akipiga picha ya pamojanaViongozi mbalimbali waserikali katika maonyesho ya Nanenane 2014, Lindi.

Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akipokea zawadi baada ya kutembelea mabanda.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akiwa anatembelea mabanda ya wadau.

HAFLA YA MEET AND GREAT YAFANA NDANI YA UFUKWE WA CLUB YA JEMBE NI JEMBE JIJINI MWANZA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga a.k.a Joe sambamba na Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions ,Bi Juhayna Kusaga ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Ephraim Mafuru  ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo wakiwa ndani ya hafla ya Meet&Great ya Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya (watakaoshiriki tamasha la fiesta) na wadau wengine ndani ya Ufukwe wa Club ya Jembe ni Jembe,ilioko nje ya mji wa Jiji la Mwanza.

Tamasha la Serengeti Fiesta linatarajiwa kuzinduliwa leo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba,huku Wasanii mbalimbali wakiwa wamekwishawasili tayari kwa onesho hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na Wakazi wa jiji hilo la Miamba.
 Baadhi ya Wasanii bongofleva na Wadau wengine mbalimbali wa muziki wakiwa wamujumuika kwa pamoja kwenye hafla ya meet&great iliyofanyika usiku wa kumkia leo kwenye kiota cha maraha cha Jembe ni Jembe,jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,pichani kulia Sebastian Maganga akiwa na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM,kwenye hafla hiyo ya Meet&Great.Pichani shoto ni B Dozen,Nikson pamoja na Millard Ayo.
Baadhi ya Wasanii watakaoshiriki tamasha la Fiesta wakiwa wamejichanganya na wadau wengine wakibadilishana mawazo na kufahamiana pia.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MAKAMU WA RAIS DR. MOHAMMED GHARIB BILAL ALIPOTEMBELEA BANDA LA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

$
0
0
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr.Mohamed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi wakati alipokuwa akitembelea katika banda hilo jana mini Lindi kushoto ni Waziri wa Kilimo na Chakula Mh. Christopher Chiza na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Ludovick Mwananzila.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr.Mohamed Gharib Bilal akimuelezea jambo Meneja masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi wakati alipokuwa akitembelea katika banda hilo jana mini Lindi.
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akisikiliza kwa makini huku Meneja mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi akisisitiza jambo wakati alipokuwa akitembelea katika banda hilo jana mini Lindi katika maonyesho ya Nanenane yaliyofungwa jana.

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr. Gharib Bilal akikaribishwa na Meneja masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi wakati alipotembelea banda la shirika hilo katika maonyesho ya Nanenane kitaifa yaliyofungwa jana mjini Lindi na Mh. Makamu wa Rais Mh. Dr. Mohammed Gharib Bilal .
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi wakati alipokuwa akitembelea katika banda hilo jana mini Lindi.
3-1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akipata maelezo kutoka kwa Meneja masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi wakati alipokuwa akitembelea katika banda hilo jana mini Lindi.


MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL NDANI YA TAMASHA LA MATUMAINI 2014

$
0
0
Mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal akitoa hotuba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Eric Shigongo naye akitoa neno la matumaini kwa maelfu ya Watanzania waliofurika Uwanja wa Taifa, Dar.
Mgeni rasmi Dk. Ghalib Bilal akikakua timu ya wabunge wa Simba.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wabunge wa Yanga.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo na refa wa mchezo wa mechi ya wabunge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global, Eric Shigongo.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mohamed Ghalib Bilal amelipongeza wazo la Tamasha la Usiku wa Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, jana kuwa ni zuri.
Alimpongeza Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwa kuandaa tamasha hilo kwani linaunganisha Watanzania wote.

MADA MAUGO ALIPA KISASI CHA KUIPIGWA NA THOMASI MASHALI

$
0
0
Bondia Thomasi Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mada Maugo wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Maugo alishinda kwa point mpambano huo .
Bondia Thomas Mashali kulia akimrushia konde la mkono wa kulia bondia Mada Maugo wakati wa mpambano wao uliofanyika juzi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Maugo alishinda kwa point mpambano huo
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com.
Mabondia Mada Maugo kushoto na Thomas Mashali wakipambana ulingoni
Bondia Said Memba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Khalid Chokoraa wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Chokoraa alishinda kwa point.
BondiaKhalid Chokora kushoto akirusha konde kwa saidi Memba wakati wa mpambano wao chokoraa alishinda kwa point
 

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKTABA YA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI GEORGE W.BUSH

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) iliyo katika Taasisi ya Bush (George W. Bush Institute) mjini Dallas, Texas, na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani. 
Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na mawasiliano. Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo katika Tanzania. 
 Rais Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
 b1: Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani ya Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office*
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembeleana kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewakama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kiraisya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *
 *b3, b4, b5: *Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiondoka baada ya kutembelea Maktabaya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library)

WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI JUU WALIOFADHILIWA NA TBL WAPATA MAVUNO MENGI

$
0
0
 Mkulima (wa pili kulia) wa Shayiri katika mashamba ya Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha akiendelea na uvunaji wa Shayiri kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wameweza kuvuna hadi gunia 1o kwa hekari moja. Wakulima wa Monduli Juu wameanza kuvuna mazao yao, baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) iliyowapatia mafunzo, mikopo ya mbolea na dawa. Pia shayiri hiyo hununuliwa na TBL kwa ajili ya kutengenezea kimea katika kiwanda kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

 Afisa Ugani wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Monduli Juu na West Kilimanjaro, Editha Temu akipima kuangalia ubora wa Shayiri iliyoanza kuvunwa katika mashamba ya Monduli Juu. Kushoto ni  ni Mwenyekiti wa wakulima wa Shayiri Monduli Juu Bariki Kivuyo.

 Mkulima wa Shayiri Goigoi Kivuyo akionyesha sehemu ya shamba linalotarajiwa kuvunwa Shayiri eneo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha, baada ya kulima kwa kufuata maelekezo na mkopo  wa mbegu na dawa kutoka Kampuni ya TBL
: Mkulima wa mfano Mepoloo Lolosi aliyelima hekari 180 za Shayiri katika eneo la Monduli Juu wilayani Monduli, mkulima huyo alikuwa akionyesha baadhi ya zana za kilimo ambazo aliwezeshwa kuzipata kwa njia ya mkopo ili kufikia malengo yake ya kulima kisasa.  Tayari amekwisha kumaliza kuzilipia zana hizo pamoja na nyingine.
Meneja wa Barley kutoka  Kiwanda cha Bia nchini (TBL) Dk. Bennie Basson akiwaonyesha waandishi wa habari hawao pichani namna Kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima wa Shayiri katika kulima kilimo bora chenye tija.

TEKNOLOJIA YA MIWANI YA KISASA YAWA TISHIO

$
0
0

Kumekua na wimbi la ukuaji wa teknolojia kila kukicha, Ukuaji huu wa teknolojia umepelekea matumizi makubwa ya mitandao maeneo mengi na hili linaenda sambamba na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao hivi sasa. Mbali na "MIWANI" pamoja na "MAGARI YASIYO NA DEREVA" kutoka Google, pia kumekua na aina nyingine ya miwani maarufu kama “Spy glasses” ambayo awali iliaminika inatumiwa zaidi na wahalifu ( wadukuzi) wa taarifa za watu.

Miongoni mwa maswala yaliyo umiza vichwa wataalam wa maswala ya usalama mitandao katika mijadala ni pamoja na kupima athari za miwani hii ya kisasa ambayo inakua imeambatanishwa na kifaa chenye uwezo wa kuona, na kusafirisha taarifa upande wa pili huku pande zote mbili kuweza kusafirisha sauti kupitia mawani hiyo.

Aina tatu za mawani hizi za kisasa ziliweza kuangaziwa macho na wataalam wa maswala ya usalama mitandao ili kujua ni athari kiasi gani zinaweza kuleta kwa jamii na badae katika kampeni ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa msaada wa tasnia ya uigizaji, Hollywood kupitia Tamthilia ya "NIKITA" kwenye kipengele chake cha mwisho sehemu ya kwanza naya tatu walitolea ufafanuzi aina mbili za miwani na uwezo wake.

Aina hiyo ya mawani sasa imeonekana kuchukua sura mpya pale Polisi nchini uchina kukamata wanafunzi waliyokuwa wakitumia miwani hiyo wakati wakifanya mitihani ilikuwasiliana na walio nje kupatiwa majibu ya mtihani. Uchunguzi huo uliambatana na tahadhari kuwa miwani hiyo iko kawaida sana na kwa haraka haraka si rahisi kuitambua hivyo wasimamizi mitihani kutakiwa kuwa makini sana kwa wavaaji miwani.

Aidha, aina hii ya miwani pia imehofiwa kuenea zaidi ambapo inaaminiwa kwa kushirikiana na teknolojia ya simu zinazo tumiwa na wahalifu kufatilia watu kwa pamoja zinategemewa kutumiwa vibaya na hatimae kusababisha wimbi la uhalifu mtandao lililoboreshwa zaidi kuleta madhara makubwa kwa mataifa mbali mbali.

RPC NJOMBE APATA AJALI NA MLINZI WAKE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.
Na James Festo, Njombe.

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.

Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi  limesema kuwa  katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George  Stephano  Matiko (24)

 H580 Pc George  Enzi za uhai wake.
Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058  alisema kuwa kutokana  gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.

"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari  na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.

Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".

Kwa upande wake  Afisa muuguzi wa hospitari hiyo  Bw. Denis Haule alisema kuwa majeruhi wawili  walipokelewa majira ya saa tano usiku na mwingine  alikuwa amekwisha fariki dunia na kubainisha kuwa hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri na  Kamanda wa Polisi anaweza kuruhusiwa muda wowote.

"tumewapokea jana usiku  majeruhi  wawili na mmoja  akiwa amekwisha fariki dunia , hali yao kwa sasa inaendelea vizuri  na kamanda anaweza kuruhusiwa wakati wowote....lakini dereva wake anatakiwa kuendelea kupewa matibabu kutokana na maumivu mbalimbali katika mwili wake.

MABONDIA MANENO OSWARD NA ABDALLA PAZI WAPIMA UZITO KUZIPIGA KESHO JUMAPILI MWANANYAMALA CCM MWIJUMA

$
0
0

Mabondia Maneno Osward kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumapili katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala jijini Dar es salaam picha na WWW.SUPESDBOXINGCOACH.BLOGSPOT.COM
 bBondia Juma Biglee akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake kesho
 Bondia Abdallah Pazi akipima uzito kushoto ni Maneno Osward

AZANIA BANK ILIVYOSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE JIJINI ARUSHA

$
0
0
Afisa Masoko wa Kanda ya kaskazini wa Benki ya Azania ,Bhoke Makore akizungumza na baadhi ya wananfunzi waliotembelea banda la Azania Benki katika maonesho ya Nane nane kanda ya ksakazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi jijini Arusha.
Mmoja wa Staff wa Azania Bank tawi la Arusha Jovin Joseph  akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja waliotembelea banda la Bank hiyo katika viwanja vya Nane nane.
Afisa Masoko wa Kanda ya kaskazini wa Benki ya Azania ,Bhoke Makore akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo walipotembelea banda la Azania Benki katika maonesho ya Nane nane kanda ya ksakazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi jijini Arusha.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS UHURU KENYATTA MJINI DUBAI WAKIWA NJIANI KUREJEA NYUMBANI

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama.
 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia  ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
 Balozi wa Tanzania  katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe.Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na balozi wa Kenya katika UAE Mhe Mohamed Gello katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai ambapo mabalozi hawa walifika kuwapokea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta waliosimama kwa muda mjini hapo wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi za Afrika ulioandaliwa na Rais BArack Obama wa Marekani. Picha na IKULU

WANAWAKE WOTE DUNIANI TUNALILIA AMANI - MAMA PINDA

$
0
0
MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wote duniani wanalilia amani na hawapendi vita wala machafuko kwani husababisha amani kutoweka kwenye familia na vifo vya watu wasio na hatia.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumapili, Agosti 10, 2014) wakati akitoa mada kama mzungumzaji mkuu (keynote speaker) kwenye Mkutano wa Dunia wa siku tano ulioanza leo jijini Seoul, Korea Kusini.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na taasisi ya Universal Peace Federation (UPF) ambayo inatoa ushauri kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uchumi na Kijamii unajadili masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo.

Akiwasilisha mada yake kuhusu usalama, amani na maendeleo barani Afrika, Mama Tunu Pinda alisema: “Ninaiomba jamii ya Kimataifa duniani kote tusimamie amani na usalama kwani kinyume na hapo ni kuleta machafuko na vita. Wanawake hatupendi vita wala machafuko...,” alisema huku akishangiliwa.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo wasimame katika nafasi zao kama baba na mama, kama kaka na dada na kuhakikisha kuwa dunia inakuwa ni mahali pazuri pa kuishi. “Ninawasihi tuendeleze maono ya Muumba wetu, tuweke utu mbele kwa kuwajali wengine na tuache kutanguliza maslahi yetu binafsi,” alisema.

Mapema, akiwakaribisha wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi 68 wanaoshiriki mkutano huo, Rais wa UPF, Dk. Thomas Walsh alisema taasisi hiyo inasimamia misingi ya amani, usalama na maendeleo ya jamii kwa nia ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa mbalimbali.

Alisema anatumaini uwepo wa wakuu wa nchi mbalimbali na viongozi mashuhuri, utasaidia kupata majibu ya changamoto inayoikabili dunia juu ya upatikanaji wa amani ya kudumu.

Naye, Mfalme Letsie Mswati III kutoka Lesotho, akizungumza katika mkutano huo alisema dunia inakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa amani kubwa ikiwa ni uharibifu wa mazingira. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanahimiza utunzaji wa mazingira kama njia ya kupunguza matatizo yanayojikeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Alionya kwamba kuna haja ya kuweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha kuwa dunia haiendelei kuwa na matukio ya kigaidi na matumizi ya silaha za maangamizi. “Kama tutakubali vita viendelee kutokea, na migogoro isiyokwisha barani Afrika na nchi za Uarabuni, ni lazima tukubali kuwa hakutakuwa na maendeleo katika mabara haya,” alisema.

KITUO CHA REDIO 5 CHANYAKUA UBINGWA MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KASKAZINI

$
0
0
r1
Wafanyakazi wa Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Manyara Erasto Mbwilo na viongozi wa Taso mara baada ya kunyakua  ubingwa katika maonyesho ya kanda ya kaskazini kwa upande wa Sekta ya Mawasiliano na habari katika viwanja vya nane nane Themi jijini A rusha
 
b
Meneja masojo wa Tan Communication media Bi.Sarah Keiya akiwa na timu yake kutoka Redio 5 wakiwa wamebeba zawadi ya mbolea kwa washindi katika maonyesho hayo ambapo  pia walitoa baskeli mbili
aMtangazaji wa Redio 5 Hilda Kinabo wa kipindi cha mishe mishe akiwa anafurahia kikombe  walichoshinda baada Redio hiyo kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya mawasiliano na habari kwa ukanda wa kaskazini
s1Meneja masoko wa Tan media Bi.Sarah Keiya akiwa na baadhi ya timu yake wakifurahia kikombe katika banda lao la kudumu katika viwanja hivyo vya nane nane jijini Arusha
s2Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa katika nyuso za furaha,nyuma ni washabiki wao waliokuwa wakiwashangilia mara baada ya kushinda katika sekta ya mawasiliano na habari
 

-r3Godfrey Thomas mtangazaji wa kipindi cha Usiku wa Moto akiwa anaendesha baskeli kwaajili ya washindi wa maonyesho hayo

cMohamed ambaye pia ni Dj mkali sana wa Ataun city akishow love na kikombe walichokinyakua katika maonyesho hayo
 
s5Mtangazaji wa Africa ngomaa Ernest Matundiro kushoto ni Geofrey Stephen wakifanya yao
s6Mtangazaji Mwanaisha Suleiman akiwa ameshikilia kikombe
s7Watoto nao walipata mda wa kuonyesha vipaji vyao….ilikuwa balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
s8Watatu kushoto ni Mtangazaji maafu Semio Sonyo wa kipindi cha Love cuts kilichompa umaarufu mkubwa kinachoruka jumatatu hadi ijumaa saa nne hadi saba usiku

TAHA ILIVYOSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MBEYA

$
0
0
Mtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambaniMtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambani katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Chainizi iliyopandwa kwa ustadi wa hali ya juuChainizi iliyopandwa kwa ustadi wa hali ya juu.


Afisa kilimo Mkoa wa Mbeya (Aliyevaa tai) akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHAAfisa kilimo Mkoa wa Mbeya (Aliyevaa tai) akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHA  katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Afisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa MkulimaAfisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa Mkulima katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
 
Hema maalumu(greenhouse) la kuoteshea mazao yanayohitaji joto ili yaweze kustawi vizuriHema maalumu(greenhouse) la kuoteshea mazao yanayohitaji joto ili yaweze kustawi vizuri
Plot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika pichaPlot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika picha
Mazao ya mboga yaliyopandwa kwa utaalamu wa hali ya juu kwenye vitalu vya mboga vya TAHAPlot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika picha
Karoti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane MbeyaKaroti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane Mbeya
Wananchi wakipokea elimu kutoka kwa mtaalamu wa TAHA namna ya kuotesha nyanya kwenye hema maalumu ya kuoteshea mazao ya mbogaWananchi wakipewa elimu lishe kuhusu umuhimu wa matumizi ya mboga kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi. Lawrencia wakati wa maonyesho ya Nanenane Mbeya
Mtaalamu akimuelekeza jambo Mkulima aliyetembelea Banda la TAHAMtaalamu akimuelekeza jambo Mkulima aliyetembelea Banda la TAHA
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images