Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 327 | 328 | (Page 329) | 330 | 331 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi lilopo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala bw. Abdon Mapunda (wa pili kushoto) alipotembelea bwawa la maji taka la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa kiwanda cha Murza Oil Mills Limited Bw. Dinesh Kana (wa tatu kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kushoto) kuhusu mfumo wa maji taka ambao wanautumia katika kiwanda hicho.

   Maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali vilivyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ambayo hutiririsha maji yake katika mto wa msimbazi, maji ambayo yanahatarisha afya ya binadamu
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Bw. Richard Matari ambaye ni msimamizi wa dampo la Kinyamwezi lililopo Pugu jijini Dar es Salaam, baada ya waziri kuwasili katika dampo hilo na kutaka kujua utendaji wa kazi zao katika kulinda Mazingira.

   Na Rashda Swedi- VPO.

  Viwanda vitakavyokiuka masharti na kanuni za kulinda mazingira havina budi kufungiwa mpaka vitakapofuata taratibu na sheria za utunzaji wa Mazingira, ameseme jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mzingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Mahenge alipofanya ziara fupi ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta (Murza Oil Mills Limited) kilichopo Vingunguti. 

  Dkt Mahenge alisema hayo baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho na kuwaambia waboreshe zaidi mfumo wa maji taka kwa lengo la kulinda mazingira kwa sababu wasipofanya hivyo Serikali itachukua hatua ya kukifunga kiwanda hicho. 

  Wakati huo huo, mwanasheria wa NEMC Bw.Manchale Heche amesema kuwa, kutokana na ziara waliyoifanya pamoja na Mh. Waziri wamegundua mengi na hawatafumbia macho suala la viwanda vinavyotumia magogo, kuni na wale wasiokuwa na mfumo mzuri wa majitaka endapo hawatafuata masharti waliyokubaliana nayo viwanda hivyo vitafungiwa.

  Waziri alitembelea pia bwawa la maji taka lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam na kugundua kuwa kuna uharibifu mkubwa wa Mazigira, kutokana na maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali karibu na eneo hilo kutiririsha maji yao kwenye mabwawa hayo.

  Kutokana na hilo amewataka Manispaa kushirikiana na NEMC kuvijua viwanda vinavyopitisha maji machafu moja kwa moja bila kufuata utaratibu uliowekwa.

   "Ni wajibu wa kila mtu kulinda mazingira na sio wajibu wa Ofisi ya makamu wa Rais tu kwani Mazingira ni yetu sote na ni muhimu kuyalinda" Mh. Mahenge alisema.Alisisitiza kuwa, huo hautakuwa mwisho wa ukaguzi wa viwanda utaratibu wa kukagua viwanda utaendelea kuangalia Mazingira rafiki kwa wananchi.


  0 0  0 0

  DSC_0092
  Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akitoa mada kuhusu tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ua VVU kwa Vijana katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.

  Idadi kubwa ya Vijana hususan wa kike wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wanaanza kufanya mapenzi katika umri mdogo jambo ambalo linaashiria hatari ya maambukizi ya VVU ikilinganishwa na idadi ya Vijana wa Kiume.
  Akitoa mada kuhusu tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ua VVU kwa Vijana katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, amesema hadi sasa kuna Asilimia 3.9 ya wasichana wenye umri huo wamepata maambukizi ya VVU ikilingaishwa na asilimia 1.7 ya wavulana.

  Kufanya mapenzi pia katika umri mdogo kunachangia kwa kiasi kikubwa mimba za utotoni na kuathiri ustawi wa maisha ya wasichana. Wastani wa watoto wa kike 6,000 huachishwa masomo kila mwaka kutokana na mimba za utotoni.
  DSC_0269
  Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akichangia mada iliyotolewa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (hayupo pichani) katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.

  “Wasichana wengi wamekatishwa masomo kwa ajili ya kupata Mimba za utotoni zinazochangiwa na kufanya mapenzi katika umri mdogo tabia ambayo pia inachangia maambukizi ya VVU”, alisema Bw. Mathias. Amezitaja tabia nyingine hatarishi zinazochangia maambukizi ya VVU kuwa ni kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja, kuwa na wapenzi wenye umri mkubwa na ngono wenzi.

  Nyingine ni matumizi duni na yasiyoendelevu ya Kondomu, kufanya ngono wakati umelewa, ngono kinyume na maumbile na ngono ya jinsia moja.
  Akichangia suala hilo Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu amesema tamaduni zinazoendelezwa katika jamii pia zinachangia kumuweka msichana katika kundi hatarishi la kupata maambukizi ya VVU.
  DSC_0066
  Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akitoa mada ya Afya ya Uzazi kwa Vijana na mahusiano yake na maambukizi ya VVU wakati wa warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.

  Amezitaja tamaduni hizo ikiwa ni pamoja na kumbagua Mwanamke katika majukumu mbalimbali Kijinsia kutokana na tabia inayofundishwa na kutolewa kwa mtu kulingana na jinsi yake.


  “Jinsia, Utamaduni na VVU ni masuala yenye mahusiano yanayomuweka Mwanamke katika hali ya hatarishi kupata maambukizi ya VVU, na kubadili tabia si jambo rahisi kwa sababu limejikita katika tamaduni zetu zinazoelekeza majukumu mbalimbali ya mwanamke na mwanaume kijinsia na hivyo kuchangia maambuki ya VVU” amesema Bi. Mwalimu.
  Amesema ni jukumu la Wanahabari Vijana kuhakikisha kuwa wanahamasisha kubadilisha tabia hatarishi zinazochangia maambukizi ya VVU ambazo zimemzunguka mwanamke.
  Baadhi ya mifano halisi ya kijinsia kwa wanaume na wanawake katika Afrika ikiwemo Tanzania ni kumuona mwanamume kama kiongozi katika kaya, jamii na kuwajibika kufanya maamuzi yote wakati mwanamke huonekana ni mlezi na kulinganishwa na mtoto mdogo.
  DSC_0037
  Mfano mwingine ni mitala. Mahusiano ya kimapenzi hata katika jamii isiyokumbatia mitala kutoka na tamaduni zilizojikita katika jamii inakubalika kwamba mwanaume ana haki ya kuwa na wapenzi wengi wakati wanawake wanatakiwa kuwa waaminifu kwa mtu mmoja ambao ni waume zao.
  “Wanawake pia wanatarajiwa kuwa watiifu kwa waume zao lakini utiifu huo hautegemewi wapewe wanawake kutoka kwa waume zao. Wanawake watakaokwenda kinyume na kanuni hiyo hunyooshewa vidole na kuambiwa kuwa wazinzi na wanaweza kuadhibiwa na jamii kwa namna yoyote ile hususani kupigwa, kutolewa maneno makali na kupewa talaka lakini wanaume hawafanyiwi hivyo”.
  Kutokana na tamaduni hizo yanajengwa mazingira ambayo mwanamke anakuwa hana uwezo wa kujadili masuala ya ngono salama au ya kuridhisha kwa sababu kunakuwa hakuna mawasiliano katika nyumba kuhusu ngono kati ya mume na mke.
  DSC_0227
  Mshiriki wa warsha hiyo Veronica Mtauka kutoka Kitulo FM Redio Makete akishiriki kuchangia mada wakati wa warsha hiyo.
  Mradi wa SHUGA Redio unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Kimataifa moja linaloshughulikia Huduma za Watoto (UNICEF), Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Redio Jamii 10 nchini Tanzania una lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
  Redio hizo ni kutoka Karagwe, Kahama, Kyela, Kitulo na Kwanza Jamii. Nyingine ni kutoka Iringa, Simanjiro, Ifakara, Sengerema na Uvinza.
  DSC_0091
  Mtangazaji wa Uvinza FM Redio, Mwinyi Mtulla akichangia hoja wakati wa warsha hiyo ya siku tatu inayoendelea mjini Iringa.
  DSC_0200
  Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akiwaelekeza jambo baadhi ya washiriki wakati wa warsha hiyo inayoendelea kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa.
  DSC_0027
  Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa inayolenga kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
  DSC_0047
  DSC_0016
  DSC_0182
  Baadhi ya washiriki kutoka Redio za Jamii mbalimbali watakaotekeleza Mradi wa SHUGA Redio wakiwa kwenye vikundi kazi.
  DSC_0198

  0 0

  Na Hassan Silayo-MAELEZO
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Eid- ElL-Fitri.
  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Suleiman Lolila baraza hilo litafanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa kumi kamili alasiri.
  Aidha taarifa hiyo imesema kuwa Sikukuu ya Eid-EL-Fitri inatarajiwa kuwa tarehe 28 au 29 julai 2014 kulingana na mwandamo wa mwezi.
  Sikukuu hiyo itaadhimishwa kitaifa  katika Mkoa wa Dar es Salaam na swala itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa moja na nusu asubuhi.
  Mufti na sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba anawatakia waislam wote na Wananchi kwa ujumla Eid-EL-Fitri njema

  0 0

   Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.
   Baadhi ya misaada iliyotoa mbunge wa Iringa mjini mch. Peter Msigwa kwa kituo cha  chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.  (Picha zote na Denis Mlowe). 
   
  Na Denis Mlowe,Iringa
   
  MBUNGE wa Iringa Mjini(Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzani Islamic Center msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.
   
  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila, Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga mkono Waislamu katika  mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote wanaoishi katika mazingira magumu.
   
  Mchungaji Msigwa alisema ni jukumu la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.
   
  Mchungaji Msigwa alikabidhi tambi katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia, kilo 250 za unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani zaidi ya shilingi milioni 1.5.
   
  Alisema ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
   
  Akishukuru kwa msaada huo Kwa niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120 ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa, Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge asiyechagua itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu wote bila kubagua watu wake.
   
  “Namshukuru sana Msigwa kwa kuweza kutoa msaada huu na  utafikishwa kwa wale wote waliolengwa kupewa na hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa iringa mjini.” Alisema |Chalamila
   
  Chalamila aliwataka wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia.

  0 0


  Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki,Ibrahim Mwangalaba (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa UAP,Nick Itunga kwa pamoja wakifunua pazia kuashiria uzinduzi wa huduma hiyo.
   Wakurugenzi wakifuatilia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
   Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki,Ibrahim Mwangalaba (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa UAP,Nick Itunga kwa pamoja wakifunua pazia kuashiria uzinduzi wa huduma hiyo.
   Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa UAP,Nick Itunga kwa pamoja wakipeana mikono baada ya Uzinduzi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa UAP,Nick Itunga akizungumza na waandishi  wakati wa Uzinduzi.
   Viongozi wa Maendeleo Banki wakifuatilia jambo wakati wa Uzinduzi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akizungumza wakati wa Uzinduzi.


  DAR ES SALAAM, Tanzania

  Maendeleo Bank PLC ni benki iliyoanzishwa na kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisya Mashariki na Pwani ambapo uanzishwaji wa benki hii ni utekelezaji waagizo la Mkutano Mkuu wa Dayosisi wa 2008. Mara tu baada ya benki kuanzishwa, mwezi Septemba mwaka 2013, ilisajiliwa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kupitia dirisha dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) ikiwa ni pekee na ya kwanza Tanzania kuanzishwa na kusajiliwa na DSE.  Kusudi kubwa la kuanzishwa kwa Maendeleo Bank PLC ni kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwani hao ndio walio wengi na upatikanaji wa huduma za kibenki kwao ni changamoto kubwa. Benki hii imebuni huduma mbalimbalia mbazo zinawalenga wananchi wa kada mbalimbali, ikiwemo akaunti mbalimbali, kutuma na kupokea pesa kutoka nje na ndani ya nchi, huduma za ATM kupitia mitandao ya ATM za UMOJA Switch zaidiya 180 sehemu nyingi Tanzania na kutoa mikopo ya aina mbalimbali, ikiwemo kwa wajasiliamali wadogo ambayo haina dhamana, yaani mikopo ya vikundi.  Leo hii tunashuhudia Maendeleo Bank ikizindua huduma ya bima ikiwa ni lengo la kuwapatia wateja huduma zote muhimu ndani ya dari moja. Pia inachangia juhudi za serikali kuboresha na kufikisha elimu na huduma za bima kwa wananchi wengi ambao hawajafikiwa. Maendeleo Bank Insurance Agency imeanzishwa ili kuunga mkono mkakati wa Serikali wa huduma za kifedha jumuishi ambazo zitahamasisha wananchi wengi watumie na wafikiwe na huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na bima.  Katikahudumazabima, Maendeleo Bank Insurance Agency imejipanga kutoa huduma zote za bima isipokuwa za maisha. Huduma zifuatazo zinapatikana Maendeleo Bank Insurance Agency: Bima za binafsi na za biashara zikiwemo bima za moto na wizi, bima za magari ya aina zote pamoja na mitambo, bima za nyumbana vitu vya majumbani, bima za wafanyakazi, bima za maofisini, bima za biashara, bima za wakandalasi, bima za vitu vinavyosafirishwanabimazaafya.  Akizungumzawakatiwauzinduziwa ‘’Maendeleo Insurance Agency ‘’ MkurugenziMtendajiwaMaendeleo Bank Ndugu Ibrahim Mwangalaba alisema ‘’Kwa kuungana na kampuni ya kimataifa ya Bima yaani, UAP Insurance nifaida kubwa kwa wateja wa Maendeleo Bank Insurance Agency kwani UAP Insurance inauwezomkubwawakubebabimazotezitakazopelekwakwaonaiwapoitatokeatatizolinalohitajikugharimiamadharayakilichowekewabima, basimtejawetuhatasumbukakwaniMaendeleo Bank Insurance Agency itafuatilia mambo yotekwamudamfupiiwezekanavyoilimtejaasisumbuke. 

  Mwangalaba aliongeza ‘’ Bimabinafsi au zabiasharanimuhimumnokatikakulindakipatonamalizawatejawetu, uanzishwajiwahudumazabimanikuishikwavitendokatikakaulimbiuyetuyapamojanawekatikamaendeleo, kwanitunapendakuonamaendeleoyawatejawetuyakiendambelesikurudinyumakwamatukioyanayowezakuzuilikakwakuwanabima’’  DirayaMaendeleo Bank PlcniKuwabenki bora zaidi Tanzania ambayoinaendeshwakwakukidhimahitajiyawatejahukuikirudishafaidakwawanahisa.  Maendeleo Bank ilifunguamilangotakribanimieziminaneiliyopitanatangiakufunguamilangoyabenki, tumepatawatejawenyeakauntizaainambalimbalizaidiya5000 natumetoamikopokwawatejazaidiya2000 ikiwanimikopoyavikundi, wafanyakazinawafanyabiasharawadogonawakatiinayofikiatakribaniTshs. 4.60bn.  MAENDELEO BANK PLC.  0 0

  SIKU chache baada ya kusajiliwa rasmi chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Taasisi inayojulikana kama Handeni Kwetu Foundation, imepangwa kuzinduliwa August 5 mwaka huu, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutafuta namna ya kusaidiana na serikali katika mambo mbalimbali, ikiwamo Kujenga uwezo kwa jamii kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha utawala.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, alisema taasisi hiyo imeanzishwa na itafanya kazi zake bila kuvunja masharti yaliyowekwa na serikali ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yanapatikana.

  Alisema kuwa taratibu za kuelekea kwenye uzinduzi huo zinaendelea kuwekwa katika hali ya kukutana pamoja kwa wageni walioalikwa kushuhudia uzinduzi huo wa aina yake.

  “Kwa miezi kadhaa sasa taasisi ilikuwa kwenye mchakato wa usajili wake, hivyo baada ya kukamilika, kinachofuata sasa ni kuzindua ili ianze kazi zake kama ilivyokusudia.

  “Taasisi hii itakuwa na Makao yake Makuu wilayani Handeni, lakini itafanya kazi zake nchi nzima na huko mbele itakuwa na ofisi katika kila eneo itakaloona inafaa,” alisema.

  Sababu nyingine za kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuleta ustawi kwa jamii katika njanya mbalimbali, kutoa mafunzo kuhusu kilimo bora na jinsi ya kutafuta masoko, kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha misingi ya utawala bora, kutoa elimu na ushauri kuhusu mbinu bora za kuimarisha  afya na elimu ya msingi kuhusu Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.

  Malengo mengine ni kutoa elimu kuhusu makundi rika katika elimu ya uzazi, kuhamasisha na kushawishi jamii kuzingatia ustawi wa mtoto katika jamii, kufanya utetezi kwa makundi maalum ambayo haki zao zinakiukwa na kufanya tafiti mbalimbali zenye malengo ya kuboresha maisha ya jamii, kiuchumi na kijamii.

  0 0

  Na Rose Masaka-MAELEZO-Dar es Salaam.

  Serikali imewataka  wananchi       kujihadhari na wizi ambao hufanywa na Taasisi za Fedha hewa ambazo zimekuwa zikidai kutoa mikopo kwa njia ya simu.

  Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

  Amesema kuwa Taasisi hizo zimekuwa zikitumia  mitandao ya simu za mkononi kutapeli wananchi kwa kuwaraghai kuwa watawapatia mikopo.

  Mwambene ameongeza kuwa Taasisi hizo zimekuwa zikitumia majina ya viongozi wakubwa mbalimbali wa vyama na Serikali kuwatapeli wananchi kwa kuwachukulia fedha zao.

  Amesema kuwa baadhi ya taasisi hizo zinatumia namba za uongo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwaibia wananchi.

  Mkurugenzi huyo amezitaja baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni pamoja na Social credit Loans ambayo inadai  imesajiliwa na TRA kwa namba Reg.No.33/SCC/REG/7894 na namba ya utambulisho wa mlipa kodi ni TIN:203-344-6789.

  Taasisi nyingine ni Saving Foundation na Quicken Loan ambazo zote hizo zimekuwa zinawatapeli wananchi.

  Amesema kuwa baada ya kuwasiliana Mamlaka ya Mapato Tanzania, imebainika kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu Taasisi hizo.

  Mwambene amesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia uchunguzi ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

  Aidha , Mkurugenzi huyo amewakumbusha wananchi kutokubali maombi ya fedha, fadhila au maelekezo yanayodaiwa kutolewa na uongozi wa juu bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika.
   

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na balozi mdogo wa Japan nchini Kazuyoshi Matsunaga (wa tatu kushoto) wakishirikiana kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA.Wengine pichani toka kushoto ni ni Mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa,Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kapten Mstaafu Joseph Simbakalia,Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Wairi wa Ardhi nyumba na mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa TAMISEMI,Hawa Ghasia.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza balozi mdogo wa Japan Kazuyoshi Matsunaga muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA.Kushoto ni mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa, wapili kushoto ni Waziri wa ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Wairi wa Ardhi nyumba na mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua maji katika kisima kuashiria kuzindua rasmi mradi wa maji katika kata ya Nalasi wilayani Tunduru.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Bakari Nalicho,Wapili kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Nalasi Rehema Kassim Yakubu wakati alipokwenda kuzindua mradi wa maji katika kata hiyo iliyopo katika wilaya Tunduru leo.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa CPA na Spika wa Ufalme wa Lethoto, Enoch Sephir Motanyane, wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, jijini Arusha kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC jijini Arusha baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania, Azan Zungu, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha kufungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wabunge baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Picha na OMR

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwila akimkabidhi msaada wa Madaftari na vyakula mbalimbali Samson Ali (12) ambaye ni mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu ambao hivi sasa wanalelewa katika Kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki.watoto hao wanapatikana kwa kukusanywa mitaani.
  Mwalimu wa Kituo cha Kulea watoto waishio katika mazingira Magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, Martin Modest akipokea Msaada wa Vyakula na Vifaa vya Shule yakiwemo Madaftari kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila ,Watoto hao wanapatika kwa kukusanywa kutoka mitaani na kulelewa hapo ambapo wanapatiwa ushauri kabla ya kuanzishwa shule.
  Watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleya watoto waishio katika mazingira magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, wakifurahia madaftari waliyokabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwila ambaye ndiye aliyekabidhi msaada huo.
  Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu ambao wanalelewa katika kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, kikiwa chini ya Kanisa Katoliki wakibeba mizigo ya vyakula mbalimbali na vifaa vya shule baada ya kukabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd.

  0 0

   
   Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sanaa Chamwino 'CAC', Dr. Kedmon Mapana (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa utambulisho wa tamasha la saba la muziki wa cigogo 2014. Kushoto kwake ni Katibu wa CAC, Sospeter Elisha Mapana na wa upande wa kulia ni Nason Mazengo, Kaimu Mkurugenzi.
   =========  ==========
  Na   Andrew Chale, Dodoma
  SHAMRA shamra za tamasha la Muziki wa Cigogo zitatarajia kulipuka hiyo kesho Julai 25, kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa kwa kushuhudia vikundi zaidi ya 30, vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni  hu ku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi  akitarajiwa kulifungua rasmi.
   
  Katika kukuza na kuendeleza sanaa nchini, tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la msimu wa  Saba (7) likifahamika kama (Wagogo music festival 2014)  lenye kauli mbiu  ‘Utamaduni na Amani’ linatarajia kulindima kwa siku tatu, Julai 25 hadi 27, Kijijini hapo  Chamwino Ikulu.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari  katika mkutano uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana,  wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center-CAC) alisema jumla ya vikundi  31 vinatarajiwa kushiriki tamasha hilo.
   
  “Tamasha la Wagogo mwaka huu ni la saba, ambapo shamrashamra ya tamasha hilo zinatarajia kuanza majira ya saa nane mchana Mkuu wa Mkoa atakapolifungua rasmi huku tukitaraji pia kuwa na wageni wasiopungua 1000” alisema Dr. Kedmon Mapana.
   
  Na kuongeza kuwa, kituo hicho cha CAC  kimekuwa kikiandaa tamasha hilo kila mwaka huku lengo kuu likiwa ni kudumisha mila na tamaduni za Wagogo.

   
  Aidha, alisema jumla ya wasanii 750 wanaotoka kwenye vikundi hivyo 31,  wanatarajia watawasha moto wa aina yake kwa kuonyesha sanaa ya muziki wa kabila hilo.
   
  “Miaka ya nyuma tulikuwa na vikundi vya kutoka hapahapa Chamwino na baadae kutoka ndani ya Mkoa wetu pekee, lakini kwa sasa tumeamua kualika na makabila jirani.. wapo wanaotoka Dar es Salaam, Pwani, Singida na Visiwani Zanzibar hivyo wote kwa pamoja tutadumisha utamaduni wetu” alisema Dr. Kedmon Mapana.
   
  Dk. Mapana  pia alipongeza wafadhili wakuu wanalioliunga mkono tamasha hilo wakiwemo, Chamwino  Connect  na Schweizerische Eidgenossenschaft  (German).
   
  Tamasha hilo pia uhudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka mataifa ya nje, ikiwemo nchi za Ulaya, America, Asia na bara la Afrika, ambapo pia kunakuwa na warsha na makongamano katika vijiji vya Chamwino.Aidha, alivitaja vikundi vitakavyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na kutoka Dodoma kuwa ni New Pendo, Yelusalem, Inueni mioyo, Yeriko, Nyota njema, Ushirikiano, Nyerere na Ebenezer.
   
  Vikundi  vilivyo vijiji vya Wilaya ya Chamwino ni  Upendo (Kijiji cha Dabalo),  Imani, Sinai  (Kijiji cha Membe).  Mchungaji mwema, (Kijiji cha Nzali), Juhudi, Muhubiri (Kijiji cha Kawawa), Nyota njema, Safina, Ndagwa (Kijiji cha Msanga).
  Msifuni (Kijiji cha Mlimwa), Nyota, Ufunuo (Kijiji cha Majeleko), Simba (Kijiji cha Mbele zungu) na Inueni mioyo (Kijiji cha Mgunga).
   
  Vikundi kutoka Wilaya ya Kongwa imani ( Kijiji cha Mkutani), Faru (Kijiji cha Songambele) na  Safina (Kijiji cha Chigwingili), Pia  kikundi cha Uvuke na Upendo  (kutoka  Manispaa ya  Dodoma mjini).
   
  Vikundi vingine ni Mandoo/Tasuba kutoka Bagamoyo  Mkoa wa Pwani, Nazareti (Dar es s Salaam), Muungano (Manyoni, Singida) na  Zanzibar.

  0 0

  Makamu mkuu wa shule ya sekondari Iwawa Fadhili Dononda akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake hii leo.

  Ikiwa zimepita siku chache tangu kutangazwa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete mkoani Njombe imetoa siri ya mafanikio ya wanafunzi wake kufaulu na kushika nafasi ya nne kitaifa. 
   
  Akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake Makamu mkuu wa shule hiyo Mwl. Fadhili Dononda amesema miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na wanafunzi hao kuwa na utayari wa kusoma hivyo wanafunzi hao hawakuwa walevi wala watoro bali walikuwa wakizingatia masomo. 
   
  Amesema kutokana na wanafunzi hao kutopenda utoro wala ulevi na kuwasikiliza walimu wao na kufuata taratibu za shule kumepelekea wao kutumia muda mwingi katika masomo. 
   
  Mwalimu Dononda amesema pia nidhamu baina ya wanafunzi wenyewe kwa wenyewe pamoja na kwa walimu wao kumesababisha walimu kuwa na ari ya kuwafundisha na kutumia jitihada za hali ya juu kwa wanafunzi hao ili waweze kufaulu vizuri jambo ambalo limefanikiwa. 
   
  "Unajua kila mzazi anamleta mtoto wake shule ili afaulu, sasa ukiwakuta wanafunzi wana ari kwa kweli hata mwalimu unapata moyo wa kufundisha kwa bidii, wanafunzi hawa waliofaulu walikuwa wamechujwa ipasavyo toka wakiwa o'level (kidato cha i-iv) kutoka kwenye shule walizosoma, hivyo kila mmoja alikuwa na moyo wa kuhakikisha anafaulu, na pia wenyewe walikuwa na mshikamano pia" amesema mwalimu huyo. 
   
  Ameongeza kuwa katika mtihani wa utamirifu (mock) ambao ulifanywa na wanafunzi 39 pia ulionesha dalili njema za matokeo ya mwisho kuwa mazuri kwa sababu wanafunzi 29 walipata daraja la I, 9 wakapata daraja la II, na mmoja alipata daraja la III.
   
  Kwa upande wake mwalimu Jitahidi Sanga ambaye alikuwa akifundisha masomo ya Jiografia na General Studies kwa wanafunzi hao na pia mwalimu wa darasa, amesema siri ya wanafunzi hao kufaulu vizuri ni pamoja na walimu kufundisha kwa muda wa ziada na wikiendi bila malipo yeyote. 
   
  Amesema utayari waliokuwa nao wanafunzi hao ulipelekea kufundishwa muda wa ziada bila kusukumwa. 
   
  "Kwa mfano likizo ya mwezi Juni mwaka jana wanafunzi hao wengi wao hawakwenda likizo, na mimi mwenyewe nilikuwa nikiwafundisha kwa muda wa ziada bila kudai malipo yeyote, na pia kwa kuwa nilikuwa mwalimu wa darasa nilikuwa nikiwasihi wazingatie masomo pamoja na yale waliyoaswa na wazazi wao" amesema mwalimu Sanga.
   
  Bi Anita Sanga ni mzazi ambaye amezungumza na mwandishi wetu na kusema kuwa matokeo hayo wameyapokea kwa furaha na hawakutegemea kama shule hiyo ingefanya vizuri kwa kiasi hicho. 
   
  Amesema wanafunzi wote wazingatie masomo kama walivyofanya hao waliomaliza kidato cha sita ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri na hatimaye iwe ya kwanza kitaifa kwa kidato cha nne na cha sita. 
   
  Shule ya sekondari Iwawa ni miongoni mwa shule tatu za serikali zenye kidato cha tano na sita wilayani hapo.

  Na Edwin Moshi

  0 0
 • 07/24/14--13:30: Article 10


 • 0 0

  Baadhi ya wahariri wa vyombo anuai vya habari wakiuliza maswali kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo anuai vya habari wakiuliza maswali kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.

   MTANDAO wa Wanawake na Katiba nchini Tanzania umewakutanisha baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba kujadili namna ya kushinikiza masuala ya haki za wanawake kuingizwa katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya. 

   Semina hiyo iliyoshirikisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wanahabari imeanza leo katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam na itafanyika kwa siku mbili yaani Julai 24 na 25, 2014. Akizungumza kukaribisha washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka alisema wajumbe katika mkutano huo watajadili umuhimu wa kuimarisha masuala ya haki za wanawake katika Katiba.

   Alisema kuwa wajumbe pia watajadili namna ya kutetea na kulinda masuala muhimu ya haki za wanawake yaliyojitokeza katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na masuala ya katiba yenye maslahi ya wanawake na taifa. 

   Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi ambao ni moja ya taasisi zilizoratibu mkutano huo, alisema pamoja na mambo mengine madhumuni ya mkutano huo ni kuwawezesha wabunge wanawake kwa wanaume katika Bunge Maalum la Katiba na wanaharakati wa jinsia na haki za wanawake kuimarisha hoja zao. 

   Katika mkutano huo wahariri wa vyombo anuai vya habari kwa nyakati tofauti waliwataka wajumbe hao kuvitumia ipasavyo vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano ili hoja zao ziingie katika vyombo hivyo na kuifikia jamii. Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la Katiba wakizungumza kujibu baadhi ya maswali ya wahariri wa habari walisema wamejipanga kupaza sauti kuhakikisha hoja zao wanazozipigania zinaingizwa katika Katiba Mpya. 

  Naye Mjumbe wa Bunge Maalum, Dk. Avemaria Semakafu alivitaka vyombo vya habari kuendelea kuwaunga mkono wanamtandao hao ili kupigania kero za akinamama na wananchi kwa ujumla na kuhakikisha zinapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya

  Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa mkutano. 
  Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa mkutanoMkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi akiwasilisha mada katika katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
  Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi akiwasilisha mada katika katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Ruth Meena akiwasilisha mada. 
  Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Ruth Meena akiwasilisha mada.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (kulia) akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (kulia) akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo. 
   Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo.Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo. 
  Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo.Baadhi ya wahariri wa vyombo anuai vya habari wakiuliza maswali kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo anuai vya habari wakiuliza maswali kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo. 
  Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huoBaadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba katika mkutano huo. Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba katika mkutano huoBaadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba katika mkutano huo. Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo.
   *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0
 • 07/24/14--13:39: Article 8


 • 0 0


  0 0


   Mafundi wakiwa kazini katika chumba cha Independent Power Tanzania Limited (IPTL) cha uendeshaji mitambo. 
   Moja kati ya karakana za kampuni ya ufuaji umeme za IPTL
   Malori yakisubiri kushusha mafuta mazito yanayotumika na kampuni ya kufua umeme ya IPTL, ambayo umeme wake huingizwa katika gridi ya taifa
   Sehemu ya mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya IPTL
  Sehemu ya kituo cha kusambaza umeme kutoka katika mitambo ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL 

  MAKAMPUNI ya Songas Tanzania na Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ni makampuni pekee ya binafsi yazalishayo umeme ambayo kwa sasa uzalisha umeme kwa ajili ya gridi ya Taifa wakati mengine yaliyobaki Aggreko na Symbion Power Tanzania yakiwa yanatumika tu wakati wa dharura. 

  Uwezo ulioongezwa katika mitambo ya gesi asilia ya Songas iliyopo Ubungo ni ya megawati 189, wakati kampuni ya IPTL inatumia mafuta mazito na uwezo wake ni kuzalisha megawati 103, ingawa uzalishaji huo ubadilika mara kwa mara kutokana na mahitaji katika gridi ya Taifa. 

  Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Bw. Adrian Severin alisema hii ni kutokana na ukweli kuwa  nchi kwa sasa inazalisha umeme kutoka katika vyanzo vingine vyenye gharama nafuu ambavyo ni maji na nishati ya mvuke (thermal power).
  “Mitambo ya uzalishaji umeme kupitia maji kwa sasa inazalisha kati ya megawati 450 hadi 500 toka katika mitambo yenye uwezo wa megawati 561.84 wakati mitambo mitatu ya gesi inayomilikiwa na Tanesco katika eneo la Ubungo na Tegeta inazalisha jumla ya megawati 252. 

  “Hii inafanya jumla ya uzalishaji kutokana na maji na nishati ya mvuke kuwa megawati 752 ambayo inatosheleza mahitaji katika gridi ya taifa. Mahitaji makubwa ya umeme Tanzania mara ya mwisho yalirekodiwa kuwa megawati 898.5,” alibainisha Bw. Severin. 

  Uzalishaji wa pamoja kwa Symbion ni megawati 120 ambapo uzalisha megawati 60 toka katika mafuta aina ya Jet – 1 na nyingine  megawati 60 kupitia gesi asilia, wakati Aggreko inazalisha megawati 100 kwa kutumia mafuta mazito katika mitambo yake iliyopo Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Bw. Severin alisema kuwa mitambo ya Symbion na Aggreko kwa sasa itatumika tu katika hali ya dharura itakapotokea.

  “Katika hali ambayo kina cha maji katika mitambo yetu inayozalisha nishati kupitia maji kimepungua au pale ambapo mitambo yetu inayozalisha nishati ya mvuke inafanyiwa ukarabati, uwa mara nyingi tunawaomba Aggreko na Symbion kuingiza umemewao katika gridi ya taifa ili pasiwepo na adha ya mgao,” Alisema Bw. Severin.  

  Akizungumza kwa njia ya simu jana juu ya kwa nini anadhani kampuni yake inaendelea kuzalisha umeme katika gridi ya Taifa, licha ya mitambo yake kutumia mafuta mazito ambayo imeongeza gharama za uzalishaji, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Bw. Harbinder Sethi alisema IPTL chini ya uongozi wa Pan Africa Power Solutions (PAP) imejitoa katika hali ya kupata faida kubwa ya kupindukia, kwa kuanza kufanya uendeshaji wa gharama nafuu ikiwa na lengo la kuipatia nchi (wateja) umeme wa bei nafuu. 

  “Ni kweli kuwa uzalishaji wa nishati kwa kutumia mafuta mazito ni ghali na ndiyo sababu tuna mpango wa kuweka mitambo ya gesi ya megawati 200 pembezoni mwa IPTL katika awamu ya kwanza ya mkakati wetu wa upanuzi. Majadiliano yanaendelea na mamlaka zote zinazohusika. Lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata nishati ya bei rahisi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati na kuwafikia watu wengi zaidi hivi karibuni,” alisema. 

  Bw. Sethi alionyesha kuwa na matarajio kwamba mabadiliko yaliyoletwa na PAP ndani ya IPTL, itaisaidia kampuni hiyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko ya hali ya umeme iliyopo na unafuu wa gharama zake nchini. 

  Vyanzo vya nishati kupitia nguvu ya maji nchini ni pamoja na Kidatu megawati 204, Kihansi megawati 180, Mtera megawati 80, Nyumba ya Mungu megawati 8, New Pangani megawati 68 na vile vile Hale megawati 21.  
  Kwa upande mwingine, Tanesco inaendesha mitambo miwili ya gesi iliyopo Ubungo kwa pamoja ikizalisha umeme wa megawati 207 pamoja na mtambo mmoja wa gesi uliopo Tegata wenye uwezo wa kuzalisha megawati 45 na mtambo mwingine ukitumia mafuta ghafi mazito uliopo Nyakato, Mwanza wenye uwezo wa kuzalisha megawati 63.

  0 0

  U.S. Embassy Public Affairs Officer Ms. Marissa Maurer (left)  presents a ticket to Clouds Media Presenter and Brand Manager Ms.  Louissa Babbie Kabae, who will participate in the U.S. Department of State sponsored U.S. Commitment to Africa Reporting Tour to be held from July 26 through August 8 in the United States. 

  Kabae will join more than 20 other African journalists in a working tour of Washington DC and the City of Atlanta to cover the U.S – African Leaders Summit and Young African Leadership Initiative (YALI) Forum hosted by President Obama.  

  These two initiatives build on, and seek to further strengthen partnership between United States and Sub-Saharan Africa  in strengthening democratic institutions, accelerating economic growth,  promoting trade and investments, advancing peace and security and investing in the next generation of African leaders. For more information about the events visit  https://youngafricanleaders.state.gov/http:/ and www.whitehouse.gov/us-africa-leaders-summit  (Photo courtesy of the American Embassy).

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha ya Mashirikiano baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa iliyo jirani na Hifadhi za Taifa .
  Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, (TANAPA) Allan Kijazi akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya  Mashirikiano kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa inayopakana na Hifadhi za Taifa. Mkutano unaofanyika katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro.
  Mmoja wa washiriki katika Warsha ya Mashirikiano baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama na TANAPA,  Mrakibu wa Polisi, Mary Lugola akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera mara baada ya kufungua warsha ya viongozi hao. 
  Mgeni Rasmi katika Warsha ya Mashirikiano kati ya TANAPA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Mororgoro Joel Bendera (wa tatu toka kulia) akiwa na viongozi wengine,toka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP, Leonard Paul, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo, Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Allan Kijazi. Wengine baada ya RC Bendera ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
  Viongozi wa ngazi ya juu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kwa mikoa iliyo jirani na Hifadhi za Taifa wanakutana Nashera Hotel kujadili ushirikiano baina yao na Hifadhi za Taifa,(TANAPA) katika kupambana na uhalifu unaolenga Maliasili.


  Baadhi ya washiriki katika warsha hiyo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alipokuwa akifungua warsha hiyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakichukua matukio muhimu wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Vitalis Uruka akitoa mada juu ya Changamaoto za Uhifadhi katika Kanda ya Kusini na hali halisi.
  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Stephen Qoli akitoa mada juu ya Changamaoto za Uhifadhi katika Kanda ya Kaskazini na hali halisi.
  Meneja Mawasiliano, TANAPA Pascal Shelutete akitoa mada ya Utaratibu wa kutoa Taarifa kwa Umma juu ya masuala ya Ulinzi na Usalama wa Maliasili na Watalii.
  Mshiriki wa warsha hiyo, Franco Kibona akichangia mada katika warsha hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo akichangia mada wakati wa warsha hiyo.
  Mshiriki Abdulla Suleiman akichangia mada katika warsha hiyo.
  Mshiriki Faustine Masalu akichangia mada katika warsha hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Allan Kijazi akichagia mada katika warsha hiyo.
  Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP, Leonard Paul mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo.
  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini aliyeko Morogoro.

older | 1 | .... | 327 | 328 | (Page 329) | 330 | 331 | .... | 1898 | newer