Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 326 | 327 | (Page 328) | 329 | 330 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
  Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibarkilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi yadharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. 

  Mradi huoambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
  Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa  kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
  Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
  Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
  Mwonekano wa Bara barabara hiyo.
   
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.Picha Zote Na Dj Sek Blog.

  0 0

  KAMA BADO HUJALIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KULIKE UKURASA WETU KWA KUFUATA KIUNGANISHI HIKI
  https://www.facebook.com/tztmt ukishalike ukurasa wetu fuata hatua hizo chini
   Ukurasa wetu ukifunguka Unaonekana kama Picha inavyoonyesha juu hapo Utafata hatua ya Kwanza kama ilivyoonyeshwa kwenye picha hizo.
  Ukishamaliza kumpigia kura mshiriki umpendae kwa kubofya kitufe kilichoandikwa VOTE utapokea ujumbe mfupi kwenye kioo chako na utakuwa tayari ushampigia kura.
  Hatimae Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) hapo Jana  limezindua huduma ya kuwawezesha Watazamaji wa Vipindi vya TMT pamoja na wapenzi wa Shindano hilo huduma ya kumpigia kura mshiriki au washiriki wanaowavutia kupitia ukurasa wa facebook wa TMT.

   Hatua hiyo imekuja mara baada ya kuona kuwa Shindano hili limetokea kuwa kivutio kikubwa cha Watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchini ambao wanafuatilia kwa Ukaribu sana shindano hili na hatimaye wengine kukosa nafasi ya kuwapigia kura washiriki wanaowavutia kutokana na Kushindwa kutumia huduma ya SMS. 

  Kwa kuona umuhimu wa watazamaji wetu TMT ikaamua kuleta huduma hii karibu ili kuwawezesha watazamaji na wapenzi wengi wa TMT kuweza kuwapigia kura washiriki wawapendao. Sasa Watazamaji wa TMT wanaweza kuwapigia Kura washiriki kwa Kufuata Hatua hizi Hapo Juu

  0 0

  1
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHCBw. David Shambwe akisoma taarifa ya shirika hilo kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku na mitandao ya kijamii kuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu Kyando ameundiwa zengwe na baadhi ya wabunge ili aondolewe katika shirika hilo, wanaofuaia katika picha ni Muungano Saguya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii, Bw. Martin Mdoe Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki
  2
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHCBw. David Shambwe akisoma taarifa ya NHC kulia ni Mpnda Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi .
  ....................................................................................
  Utangulizi: Jumatatu na Jumanne ya wiki hii, kumekuwa na taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya gazeti la kila siku zikieleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu ameundiwa zengwe na Bodi ya Wakurugenzi ya NHC kwa nia ya kuhakikisha kuwa harejeshwi tena katika wadhifa huo, hasa baada ya Bw. Mchechu kumaliza muda wake wa kuliongoza Shirika hili. 

  Aidha, gazeti hilo liliwaaminisha umma wa watanzania kuwa mizengwe hiyo inaungwa mkono na vigogo wa Serikali wakiwemo Wabunge ambao kuwepo kwa Bw. Mchechu katika Shirika kumewanyima ulaji ikiwemo kupangishwa nyumba za Shirika. 

  Gazeti lililienda mbali zaidi likidai kuwa Bw. Mchechu amewekewa masharti magumu na Bodi hiyo ya kumtaka apunguze idadi ya Wakurugenzi wa Menejimenti ya sasa ya Shirika.

  Kwa kuwa habari hizo zimeleta mtafaruku katika Shirika na zimesababisha umma kuwa na mijadala mbalimbali juu ya jambo hili, tungependa kuwataarifu umma kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, na Shirika la Nyumba la Taifa linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-

  1. Kwanza, ifahamike kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC ina miezi miwili tu tangu iteuliwe na Mamlaka husika na haijawahi kukaa katika kikao chochote kujadili suala la kumuondoa Mkurugenzi Mkuu na kupunguza Menejimenti ya Shirika iliyopo sasa.

  2. Tunapenda kuwafahamisha kuwa Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya Shirika bado wana mikataba halali ambayo haijamalizika muda wake, hivyo hoja ya kuwa Bwana Mchechu na Menejimenti yake wanaundiwa zengwe baada ya kumaliza muda wao haina ukweli wowote.

  3. Kwamba kutokuwepo kwa Mkurugenzi Mkuu kwenye ufunguzi wa miradi hakukutokana na kuwepo mizengwe kama ilivyoripotiwa na Gazeti hili. Bw. Mchechu alikuwa katika likizo yake ya mwaka iliyooanza tarehe 30 Juni na kumalizika Julai 18, 2014. Likizo hii ni stahili halali ya Bw. Mchechu kama walivyo watumishi wengine wa umma, na hakuichukua likizo hii kutokana na kuwepo mizengwe ya kumuondoa kama ilivyoripotiwa na Gazeti hili. Kuanzia tarehe 21 Julai, 2014 Bw. Mchechu yupo kikazi nje ya nchi na anatarajiwa kuwa ofisini kwake tarehe 28 Julai, 2014.
   
  4. Mwisho, tunapenda kuwatanabaisha wanahabari kuwa kama ilivyo kawaida yetu, NHC imekuwa na itaendelea kuwa mstari wa mbele kutoa habari makini kwa vyombo/chombo chochote cha habari bila kuficha jambo lolote. Hivyo, tunawaomba muendelee kuitumia vyema fursa hii kupata habari zenye ukweli na zilizo sahihi kwa jambo lolote mnalohitaji kuufahamisha umma wa watanzania. 

  Kwa kufanya hivyo, tutaendelea kuwa washirika wakubwa wa vyombo vya habari, tukizingatia kuwa vyombo vya habari vina dhima na dhamana kubwa katika kuleta tija kubwa kwa Shirika na Taifa letu. Aidha, tunawafahamisha wateja wetu kuwa hakuna mtafaruku wowote uliyopo ndani ya Shirika la Nyumba la Taifa na kwamba tunaendelea kuwapa huduma zetu zilizo bora katika sekta ya nyumba tuliyoaminiwa na Taifa kuisimamia.

  IMETOLEWA NA: BW. DAVID SHAMBWE, KAIMU MKURUGENZI MKUU,

  0 0

   Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Damian John wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 zilizotolewa kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Wengine ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba (mwenye miwani) na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
   Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu, Arusha, wakati wa hafla ya kuwakabidhi mfano wa hundi ya sh. mil. 45 za kugharamia uchimbaji wa kisima cha maji kijijini hapo, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba na aliyekaa ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu, Moses Mabula.
   Wananchi wa kijiji hicho wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Moses Mabula na Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maji ya Kijiji cha Kambi ya Simba pamoja na watalaamu watakaochimba kisima hicho cha maji, baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 na TBL.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uzalishaji soda Bw. Louis Coetzee ( wa kwanza kulia), akielezea jinsi kiwanda hicho kinavyotumia maji taka kulinda Mazingira ya kiwanda.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Dkt. Injinia Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake na kuwaambia kwamba nchi inahitaji wawekezaji wanaotunza na kulinda Mazingira yetu. Viwanda alivyovitembelea ni kiwanda cha kuzalisha Mafuta ya kula na sabuni (BIDCO), M.M.I steel mill kinachozalisha Nondo na Mabati pamoja na kiwanda cha Coca Cola vilivyopo Mikocheni  jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge, akizungumza na Menejimenti ya kiwanda cha Coca Cola (hawapo pichani)  kuhusu kiwanda hicho jinsi walivyoweza kutunza Mazingira na kuwataka waendelee kuboresha zaidi Mazingira ya kiwanda na kuwa mfano wa kuigwa kwa viwanda vingine.
   Maji machafu yenye kemikali  yanayotiririka kutoka kwenye kiwanda kinachozalisha Nondo na Mabati (M.M. I steel mill ) kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam ambayo si salama kwa wananchi na mazingira kwa ujumla.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano  Mahenge ( wa pili kulia)  pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu (wa kwanza kushoto), wakiwa katika ziara  fupi ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha Coca Cola kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Wakiwa pamoja na mkurugenzi wa uzalishaji soda katika kiwanda hicho Bw. Louis Coetzee (wa kwanza kulia).

  ========== =======   ========

  Wawekezaji wote Nchini wanatakiwa kuhakikisha wanaacha kutumia magogo katika uzalishaji badala yake watumie tekinolojia ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya tabia ya nchi  na uchafuzi wa Mazingira yanayotokana na ukataji miti. 

  Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Mh.Dkt. Injinia Binilith Mahenge wakati  alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia (BIDCO) kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam.

  Amekiagiza kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya magogo kwani inaathari kubwa sana kwa jamii.  Hata hivyo amesema kuwa atatembelea tena kuangalia kama wameacha kutumia magogo ndani ya miezi sita, endapo watabainika wanaendelea kutumia magogo,hatua kali itachukuliwa juu ya Kiwanda hicho endapo watakiuka masharti waliyopewa  Kiwanda kitafungwa mara moja.

  Hata hivyo Mh. Mahenge amewaomba wawekezaji wa viwanda vingine kuiga mfano wa kiwanda cha Coca Cola katika utunzaji wa Mazingira, kwani wao ni mfano mzuri kwa viwanda vingine kwa kuanzisha technolojia nyengine ya kuchunguza maji taka kama ni salama kwa viumbe hai.

  Amemalizia kwa kusema "Tunapenda wawekezaji lakini ni wale wanaotunza na kuyaenzi mazingira kwa usalama wa wananchi na nchi yetu kwa ujumla".


  0 0

  Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi.

  Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.

  Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea. Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.

  Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa  ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati  utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.

  Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
  Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli.
  Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli yaliyoteketea kwa moto, akiongozana na mkuu wa shule hiyo mwalimu Agnes Nyange.
  Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
  Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.

  0 0

   
  Warembo 14 wanaowania taji la Kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014) watashindania taji la vipaji (talent award) lililopangwa kufanyika siku ya Idd Pili kwenye ukumbi wa Maisha Plus, Kibaha, Mkoa wa Pwani.
   
  Akizungumza jijini leo, mratibu wa mashindano hayo, Alex Nikitas alisema kuwa kutokana na mashindano hayo ya vipaji, kambi ya warembo iliyopangwa kuanza Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge, sasa itaanza Julai 28 kwenye hotel ya Precision mkoani Pwani.
   
  Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekwisha kamilika na warembo hao mbali ya kushindana katika vipaji, pia watatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima cha mkoa wa Pwani na baadaye kurejea mkoani Morogoro tayari kwa mashindano yaliyopangwa kufanyika  Nashera Hotel Agosti 8.
   
  Alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo  14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
   
  Warembo  hao ni Lucy Julius Diu, Prisca  Mengi, Tarchisia Noback Mtui na Angel  Shio ambao wanatoka Morogoro.  Warembo wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian  Andrew na Leila  Abdul  Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni  Nidah Fred Katunzi, Lightness  Mziray na Nelabo  Emmanuel.
   
  Pia warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary  Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya mashariki mwaka jana,  Diana Laizer.

  0 0
  Mtaalamu kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Nyaso Makwaya akisisitiza jambo wakati alipokuwa  akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya Wizara katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi


  Na Greyson Mwase, Morogoro

  Wizara ya nishati na madini inatarajia kuanzisha mpango wa taifa wa matumizi bora ya nishati  unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mara baada ya maandalizi yake kukamilika.

  Akizungumza katika  kongamano la mabadiliko ya tabianchi lililokutanisha wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam linaloendelea mjini Morogoro, Mhandisi Nyaso Makwaya kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini alisema kuwa mpango huo uko katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.

  Mhandisi Makwaya alisema kuwa maandalizi ya mpango huo yalianza mwaka 2013 na kuongeza kuwa lengo la mpango huu ni kuweka malengo ya kitaifa kwa kila sekta kwa ajili ya matumizi bora ya nishati, kuzichanganua changamoto zilizopo za matumizi bora ya nishati na kuzitafutia utatuzi na kuandaa miradi ya matumizi bora ya nishati.

  “ Nishati ya umeme ni muhimu sehemu yoyote, inahitaji usimamizi  bora hivyo mpango huu  unalenga kuboresha matumizi ya nishati katika sekta zote nchini, iwe viwanda, kilimo, ujenzi,mawasiliano n.k, mpango huu unatoa dira sahihi kwa kila sekta” Alisema Mhandisi  Makwaya Mhandisi Makwaya aliongeza kuwa  mpango huu utapelekea  uanzishwaji wa  sheria na kanuni katika usimamizi wa matumizi bora ya nishati.

  Aliongeza kuwa  wadau na watekelezaji wakuu wa mpango huo ni Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Taifa la Viwango (TBS) ambao watajengewa uwezo na mradi huu.

  Akizungumzia changamoto zilizopo katika usimamizi wa matumizi  bora ya nishati   Mhandisi Makwaya alieleza kuwa  ni kutokuwepo kwa kanuni  zinazosimamia matumizi  bora ya nishati  katika ujenzi  na matokeo yake ni wajenzi kujenga majengo  yasiyokuwa na uwiano kati ya ukubwa wake na kiasi cha nishati ya umeme  kinachohitajika.

  Mhandisi Makwaya alisisitiza kuwa  changamoto hiyo ilipelekea Wizara kubuni mkakati huo ambao utaisaidia nchi kuokoa kiasi cha nishati kinachopotea na kuongeza kuwa katika utekelezaji wa mpango huo  elimu kwa umma itatolewa ili wananchi wawe na uelewa wa kusimamia vyema matumizi bora ya nishati .

  “Wananchi wengi hususani wafanyakazi maofisini na viwandani hawana uelewa juu ya matumizi sahihi ya nishati ya umeme, mpango huu utakuwa ni mkombozi na hii itachangia uchumi wa nchi kukua kwa haraka kwa kuokoa gharama zisizo za lazima. “ Alisisitiza Mhandisi  Makwaya.

  0 0

  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO. 

  Rais mstaafu wa awamu ya pili , Ali Hassan Mwinyi ,amewataka watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao.

  Kauli hiyo ameitoa jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

  Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.

  “Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu” Amesisitiza.

  Amewashukuru viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.

  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa mvua jijini Dar es salaam.

  Bw. Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.

  Amezitaka mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika maeneo hayo.

  Katika hatua nyingine Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.

  Amezitaka mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi. Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na kuendelea kuvumilia.


  0 0

      Gavana  wa  Benki   Kuu  ya  Tanzania,  Prof.  Benno  Ndulu   akichangia   hoja   wakati  wa mkutano  wa  kupitia  taarifa  ya  mwaka mmoja ya utekelezaji  wa  Mpango  wa  Matokeo  Makubwa  sasa (BRN) uliofanyika  leo  Jumatano   Julai  23,  2014  katika  ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere  Jijini  Dar es  Salaam.  Kulia  ni  Katibu   Mkuu  wa Wizara  ya Maji  na  Umwagiliaji  Mhandisi  Bashir Mrindoko
  Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi   Ombeni  Sefue  akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa  ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji  wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam. Kulia  ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Asha- Rose  Migiro   na (katikati)  Mtendaji  Mkuu  wa  Ofisi  ya  Rais-  Usimamizi  wa  Utekelezaji  wa  Miradi  (PDB),  Bw. Omari Issa.
   Naibu  Waziri  wa Viwanda  na Biashara, Mhe. Janet Mbene akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam. Kushoto  ni Katibu  Mkuu Ofisi  ya Waziri Mkuu Tawala  za  Mikoa  na Serikali  za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini.
   .       Naibu  Waziri  wa  Katiba  na  Sheria, Mhe. Angellah Kairuki (katikati)  akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam.
  1.       Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe  (kulia) akichangia akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam. Kutoka  kushoto  ni  Waziri  wa  Elimu na Mafunzo  ya Ufundi,  Mhe. Shukuru  Kawambwa,  Naibu  Waziri  wa Fedha  na Uchumi, Mhe.  Mwigulu Nchemba,  na Katibu  Mkuu wa  Wizara  ya Nishati  na Madini,  Eliakim Maswi.

  (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
   Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
  =========  =========  =========
  RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI  SIKU YA MASHUJAA.
  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
  23/7/2014. Dar es salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya  Mashujaa  itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo yamekamilika na kuongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu kihistoria  yanalenga kuwaenzi wote waliojitoa muhanga katika jitihada za  kuikomboa ardhi ya Tanzania, kuilinda na kudumisha amani na utulivu uliopo.

  Amesema  maadhimisho  hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Gwaride la Kumbukumbu litakaloonyeshwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

  Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na uwekaji na silaha za asili, maua kwenye mnara wa kumbukumbu pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoa dua na sala kuliombea taifa.

  Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja huo.

  Aidha, katika hatua nyingine ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo  barabara ya Lumumba, Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo.

  0 0

  Kijana aliyetambulika kwa jina la Musa Mbeko(24) anayedaiwa kuwa ni mwandishi wa habari mkoani Tabora akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kujifanya kuwa ni afisa kutoka idara ya usalama wa taifa (TISS).kijana huyo inadaiwa aliwahi kufanya kazi kituo cha radio cha Voice of Tabora (VOT) kinachomilikiwa na mbunge wa Jimbo la Tabora mjini,Ismail Rage,hata hivyo Uongozi wa VOT umekana kijana huyo kuwa ni mwandishi wao na kwamba ulikwisha mfukuza kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya Utapeli
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni Afisa Usalama wa Taifa.
   . 
  Kitamburisho alichokuwa akitumia kijana Musa Mbeko.
  Kijna Musa Mbeko akiwa mbele ya kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzana Kaganda.
  Kijana Musa Mbeko akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Polisi.

  0 0
 • 07/23/14--07:05: GARI INAUZWA
 • ?????????????????????????????????????????????????????????????? 
  Toyota Celica, ya mwaka 2001. CC 1780

  Inauzwa, ipo kwenye hali nzuri, service inaenda kama kawaida.

  Bei 7,500,000

  0713303305

  0 0

   
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, wakiweka saini mkataba wa “wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014. Chini ya Mkataba huo, zaidi wa wafanyakazi 400 wa MSD wamejiunga na PPF. 
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, baada ya kusaini mkataba wa mpango wa “Wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014
   Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, (Kushoto), akikabidhi kadi mpya ya uanachama kwa mwanachama mpya ambaye ni mfanyakazi wa MSD, mara baada ya PPF na MSD kusaini makataba wa mpango wa 'Wekeza" kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014
   Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, (Kushoto), akikabidhi kadi mpya ya uanachama kwa mwanachama mpya ambaye ni mfanyakazi wa MSD
   Viongozi wa PPF na wenzao wa MSD, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutiliana saini mkataba ambapo MSD na PPF zimekubaliana kuanzisha mpango wa "Wekeza" ambapo wafanyakazi wa MSD sasa watakuwa wakichangia kwenye mfuko huo ili kujiwekea akiba na kujipatia mafao mbalimbali
  Viongozi wa PPF na wenzao wa MSD, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa MSD waliokabidhiwa kadi za uanachama wa Mfuko huo, mara baada ya kutiliana saini mkataba ambapo MSD na PPF zimekubaliana kuanzisha mpango wa "Wekeza" ambapo wafanyakazi wa MSD sasa watakuwa wakichangia kwenye mfuko huo ili kujiwekea akiba na kujipatia mafao mbalimbali

  0 0

  Bondia Ibrahimu Maokola akipiga beg zito wakati akijifua katika GYM ya okaido iliyopo Mbagala Charambe  kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakala pambano litakalofanyika agost 9 katika ukumbi wa amenya pub uliopo mbagala.
  Bondia Ibrahimu Maokola akijifua Okaido GYM iliyopo Mbagala Charambe kwa ajili ya kujitaharisha na mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala Agosti 9. 
  Bondia Ibrahimu Maokola akijifua Okaido GYM iliyopo Mbagala Charambe kwa ajili ya kujitaharisha na mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala Agosti 9. .
  Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakala litakalofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala siku ya ya augoust 9 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


  Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Ayubu Tezikoma wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Selemani Mkalakali mpambano wa ubingwa raundi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub Augost 9 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Ayubu Tezikoma wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Selemani Mkalakali mpambano wa ubingwa raundi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub Augost 9 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Ibrahimu Maokola
  Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akipiga beg kubwa kwa kusimamiwa na Athumani Magambo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakali litakalofanyika Augoust 9 katika ukumbi wa Amenya pub mbagala Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

   Baadhi ya wananchi wa Bagamoyo wakiswali swala ya Magharibi wakati wa  futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.
   Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akichota futari pamoja na  wananchi wa Bagamoyo walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.
     Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akijumuka  na wananchi wa Bagamoyo walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.
    Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukurani kwa wananchi wa Bagamoyo waliohudhuria  katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.
     Sehemu ya kinamama  wa Bagamoyo waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.

   Baadhi ya wafanyakazi wahudumu katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.
   Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na wananchi wa Bagamoyo walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Jumatano jioni Julai 23, 2013. Rais Kikwete, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, aliwakilishwa na Mhe Ridhiwani.PICHA NA IKULU.


  0 0

  10514673_338168816341103_5043683657096333091_n
  Bendi Mahiri na Machachari Jijini Dar Skylight Band wametoa wimbo wao wa Tano ikiwa ni muendelezo wa kutoa nyimbo tofauti tofauti kupitia Studio yao ya kisasa ya Skylight Production.

  Akiongea na Mtandao huu Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK47 amesema wimbo huo unaitwa “Pasua Twende” ambo umetungwa na Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo Dk. Sebastian Ndege akishirikiana na wanamuziki wa Bendi hiyo.

  Aneth akaongezea kwamba wimbo huo ni wa tano kutolewa katika mtiririko wa nyimbo zao zilizokwisha kutoka na imetengenezwa ndani ya studio yao ya Skylight Production chini ya Produzya Joobanjo.

  Isikilize hapa chini na Ijumaa hii utapa fursa ya kusikiliza ikipigwa LIVE ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

  0 0

   
   Ujumbe kutoka Bill & Melinda Gates Foundation umefanya ziara Tanzania na kuitembelea pia TFDA kwa lengo la kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya wanayoifadhili Tanzania. 

  Ujumbe huo unaoongozwa na Mkurugenzi katika Mfuko huo Bw. Michael Poole, umesifu maendeleo ya Mradi wa ADDO na Uwianisho wa mifumo ya udhibiti wa dawa kwa nchi za Afrika Mashariki, miradi ambayo TFDA imekuwa ikisimamia utekelezaji wa ADDO hadi mwaka 2012 na kushiriki Uwianisho wa mifumo ya udhibiti wa dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki toka mwaka 2012 hadi sasa. 

  Hivi sasa ADDO inasimamiwa na Baraza la Famasi kufuatia Sheria ya Famasi ya mwaka 2011.Wenyeji wa ujumbe huu ni Shirika la Menejimenti ya Sayansi ya Afya (MSH) ambao ni wadau wakuu wa mradi wa mpango wa ADDO nchini.
    Picha ya kikao cha ueasilishaji wa taarifa za maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko huo

   Picha ya pamoja ya ujumbe kutoka Mfuko wa Bill & Mellinda Gates, Maafisa wa TFDA, MSH na Baraza la Famasi mara baada ya ziara ya TFDA.
  Picha ya Kaimu Murugenzi Mkuu TFDA, Dkt. S.S Ngendabanka, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bill & Mellinda Gates Bw. Michael Poole katika viwanja vya TFDA

  0 0

  Mhandisi Donart Makingi (Kushoto) kwa niaba ya Meneja wa Usalama kazini akitoa maelekezo kwa wahandisi namna ya kuzingatia usalama katika eneo la kazi ikiwa ni pamoja na kuto kupanda kwenye nguzo, ama kugusa vifaa vya kazi bila kupata muongozo.
  Wahandisi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) wakiwa katika mazoezi mbalimbali ya kubaini nguzo bora yanayofanyika katika Kiwanda cha Sao Hill, mkoani Iringa.
  Bw. John Mwaura Njenga ambae ni Meneja wa Poles and Timber Implementation akitoa maelezo kwa Wahandisi wa TANESCO namna kiwanda kinavyofanya kazi.
  Wahandisi wakiwa maabara wakifanya majaribio ya namna kiasi cha dawa kilivyoingia ndani ya nguzo wakipata na maelekezo kutoka kwa Boniface Mwansatu ambae ni Mdhibiti Ubora kutoka Kampuni ya SGS.
  Wahandisi wa TANESCO wakifuatilia maelekezo ya namna mtambo wa kuwekea nguzo dawa inavyofanya kazi katika kiwanda cha Sao Hill. Picha zote na Henry Kilasila.

  Wahandisi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wanaonolewa katika kutambua nguzo bora za kusambazia umeme wameanza mafunzo ya vitendo ya ukaguzi na utambuzi wa nguzo bora na salama katika baadhi ya viwanda vya kuzalishia nguzo hizo mkoani Iringa. 

  Ziara ya wahandisi hao wa TANESCO inalenga katika kuwawezesha katika kukabiliana na matumizi ya nguzo zisizo na ubora na ili kuongeza ufanisi na usalama katika zoezi la kusambaza umeme nchini.

  Wahandisi hao wamepata fursa ya kutembela kiwanda cha Sao Hill kilichopo Mafinga mjini Iringa ikiwa ni mafunzo kwa vitendo juu ya utambuzi wa nguzo bora.

  Washiriki waliweza kuona namna uzalishaji na utayarishaji wa nguzo unavyofanyka ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa nguzo kabla haijawekewa dawa na ukaguzi wa nguzo baada ya kuwa ya kuwekewa dawa.

  Akivitaja vitu vinavyoangaliwa kabla nguzo haijawekewa dawa Bw. Emmanuel Simkoko ambae ni mkaguzi kutoka Kampuni ya Ukaguzi wa Ubora ya SGS ya jijini Dar es Salaam, alisema vitu vya kuzingatia katika zoezi la utambuzi wa ubora wa nguzo ni pamoja na aina ya mti unaotumika katika kuandaa nguzo hizo, ukubwa, pamoja na kimo cha nguzo husika.

  “Kuna vitu vya kuzingatia wakati wa kuchambua aina ya ubora wa nguzo, ni muhimu kujua aina ya mti ili kubaini hali ya unyevunyevu, na masuala mengine ya utaalamu ikiwamo vipimo vya nguzo husika,” alisema Bw. Simkoko.

  Kwa mujibu wa Bw. Simkoko, nguzo bora haitakiwi kuwa na hali ya unyevunyevu kuvuka 25%, pamoja na ukubwa wa kitako cha nguzo kisipungue milimita 20 na juu ya nguzo isipungue milimita 20.

  Wahandisi hao walielimishwa sifa nyingine ya nguzo bora kuwa ni pamoja na kuangalia nguzo kama imeliwa na wadudu, umbo la nguzo iliyo panda haifai kwa kuwa haitoweza kukidhi kazi husika.

  Bw. Simkoko alihitimisha kwa kuwaelimisha wahandisi hao namna ya kuwekea dawa nguzo zilizo bora, “Baada ya nguzo kuwekewa dawa huwafanyiwa majaribio kuangalia dawa kama imewekwa ipasavyo, na tuna utaratibu wa kuzifanyia majaribio kila mwezi,” aliongeza Bw. Simkoko.

  Wahandisi wa TANESCO wapo mkoani Iringa kwa mafunzo ya wiki mbili yenye lengo la kuwawezesha wataalamu hao kuwa na weledi wa hali ya juu katika kutambua nguzo zenye sifa na umadhubuti na salama katika zoezi la usambazaji umeme nchini.


  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI
  WAKALA WA UFUNDI NA UMEME(TEMESA)


     
  Telegrams TEMESA DSM                                                             S.L.P  70704
  Simu: +255-22-2862796/97                                                             DAR ES SALAAM
  Fax:   +255-22-2865835                                                                  TANZANIA


  TAARIFA KWA UMMA  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) anawatangazia wananchi wote kuwa kivuko cha MV. Kigamboni kinatarajiwa kwenda kwenye matengenezo makubwa wakati wowote kuanzia leo.

  Hivyo huduma za uvushaji zitaendelea kwa kutumia vivuko vya MV. Magogoni pamoja na MV. Lami katika kipindi chote cha matengenezo husika.
  Uongozi wa TEMESA unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakao jitokeza.
  Imetolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu
  TEMESA

older | 1 | .... | 326 | 327 | (Page 328) | 329 | 330 | .... | 1898 | newer