Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 328 | 329 | (Page 330) | 331 | 332 | .... | 1897 | newer

  0 0

   
   Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya soka ya vijana wa TFF Ayoub Nyenzi  kwa ajili ya mashindano ya Airtel Rising Stars yanayotariwa kuanza kutimua vumbi ngazi ya mkoa Jumapili ijyayo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana jijini Dar-es-Salaam.
  ·          
  Saidi Meck Sadiki mgeni ramsi ufunguzi Jumapili.

  Airtel Tanzania Jana Alhamis Julai 24, 2014 imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 18 za wavulana zinazoshiriki michuano ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam Jumapili 27 Julai 2014.

  Dar es Salaam inajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Washiriki wengine wa mashindano hayo ya kubaini na kuendeleza vipaji watatoka katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Morogoro. Akizingumza katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa iliyofanyika kwenye uwanja cha Kumbu Kumbu ya Karume, Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi amesema maandalizi yamekamilika.

   “Tunatajia kuwa na mashindano yenye ushindani mkali na ya kusisimua. Napenda kuchukua fursa hii kuwataka viongozi wa soka ngazi ya mkoa kuhakikisha wanakuwa makini ili kuchagua vijana wenye vipaji kuunda timu zao za mikoa zitakkazoshiriki fainali za taifa zitakazofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao”, alisema Nyenzi.

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars katika mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni utakofanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Jumapili ijayo.

  Mkoa wa Mwanza utafungua rasmi michuano yake Agosti 3, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya ambao umepangiwa kuanza mashindano yake Agosti 4 wakati mkoa wa Morogoro utaanza mechi zake Agosti 5. Wakuu wa mikoa husika wanatarajiwa kuwa wageni rasmi kwenye hafla za ufunguzi wa michuano hiyo.

  Mbali na timu za wavulana, mashindano hayo pia yatashirikisha timu za wasichana katika ngazi ya taifa na kufanya fainali hizo kuwa na jumla ya timu 12, sita za wasichana na sita za wavulana. Timu za wasichana zinatoka mikoa ya Ilala, Kinodoni, Temeke, Mbeya, Mwanza na Zanzibar. Huu ni mwaka wa tatu tangu mashindano ya Airtel Rising Stars yalipoanza kushirikisha timu za wasichana.        

  Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde amesisitiza nia thabiti ya kampuni ya Airtel ya kuendelea kudhamini programu hii ya vijana na kulipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, wizara inayosimamia michezo na wadau wengine wa soka kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel kusaidia maendeleo ya soka la vijana. 

  Michuano wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.

  Airtel Rising Stars itahitimishwa kwa mashindano ya kimataifa ambayo yatashirikisha wachezaji nyota kutoka nchi 22 barani Afrika ambapo kampuni ya mawasiliano ya Airtel inafanya biashara.  Mashindano hayo ya kimataifa yamepangwa kufanyika nchini Gabon kuanzia Agosti 25 hadi 30.
     0 0


  0 0

  DSC_0084
  Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  Tafiti zimebaini kwamba Vijana hawatumii Kondomu na hutoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kutopata ladha wakati wa tendo la ndoa na kwamba inapunguza nguvu na visingizio vingine vingi vinavyopelekea kuashiria hatari ya maambukizi.

  Hayo yameelezwa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias wakati akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio.

  “Asilimia 40 ya Wasichana na Asilimia 47 ya Wavulana ndio wenye ufahamu wa kina juu ya maambukizi ya VVU huku asilimia kubwa wakiwa hawana elimu ya kutosha na hawajui afya zao kwa kuwa hawana utamaduni wa kupima VVU ”, amesema Bw. Mathias.
  DSC_0184
  Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akiwapiga msasa washauri wa Vikundi vya Vijana kwenye warsha ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa.

  Katika warsha hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNICEF katika kituo cha Redio cha Nuru FM Iringa, Bw. Mathias amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu sahihi kwa Vijana ya kujikinga na maambukizi ya VVU na Mimba kutokana na uelewa mdogo wa Vijana katika matumizi sahihi ya Kondomu.

  Wakichangia mada kuhusu masuala muhimu yanayowahusu vijana katika maambukizi ya VVU vijana wamesikitishwa na mimba za utotoni kwa wasichana zinazochangia vifo vya Mama na Watoto na wasichana kuacha masomo.

  Washiriki wa warsha hiyo wametaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha kuwa sheria za mtoto zinazoruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo zinafanyiwa marekebisho ya haraka kulinda haki ya mtoto wa kike.
   
  DSC_0139
  Mmoja wa washiriki akihoji jambo kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.
  Wakijadili mada hiyo washiriki wamesema mila na tamaduni pia zinachangia kwa kiasi kikubwa kumkandamiza mtoto wa kike katika masuala mbalimbali ya maendeleo yake.
  Wakitoa mifano ya baadhi ya mila zilizowafanya wapaze sauti kuhusu mabadiliko ya sheria za mtoto ni ile sheria ya ndoa na mila inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi. Umri huo unakinzana na haki za mtoto kufurahia maisha yake na kupata elimu.
  Mifano mingine ya kitamaduni ni pale mwanamume anapochumbia mimba wakati akijua wazi mtoto ana haki zake za msingi za kuishi.
  Wamezitaja pia asasi za dini kutoa elimu kwa vijana ili kusaidia hali iliyojitokeza ya wazazi kutokuwa na muda na watoto wao kuwaelimisha kuhusu mabadiliko ya miili na afya zao.
  DSC_0089
  Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akifafanua jambo kwa washiriki.
  Akitoa mada kuhusu mbinu mbalimbali za kuwezesha majadiliano katika vikundi vya wasikilizaji, Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdul Mfuruki amewataka wawezeshaji kutotumia nafasi walizonazo ili kuendesha mjadala wenye tija.
  Amesema washauri wa vikundi hawana budi kuweka mizania kutumia busara, kusoma mazingira na kutoingiza imani au itikadi itakayopelekea kuharibu mjadala unaoendeshwa wa kufuatilia vipindi vya SHUGA Redio, kuwa wavumilivu, kusoma na kuheshimu mawazo ya wengine na kutofungamana na upande wowote ili kumweleza mshiriki wa majadiliano kufunguka zaidi.
  Bw. Mfuruki amesema vijana wa vikundi vya wasikilizaji kuwaza mambo mengi ni vyema kuwasikiliza kwa uvumilivu, kupata ushauri wa wengi kwa lengo la kufanya maamuzi sahihi bila kulazimishana na vile vile kuwa wabunifu kwa kutumia mbinu mbadala ili kupata habari iliyojificha.
  DSC_0114
  Mkufunzi Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akiwaelekeza jambo washiriki wakati wa mazoezi ya vikundi kazi kwenye warsha hiyo.
  DSC_0075
  Pichani juu na chini ni baadhi washauri wa vikundi vya vijana wakifuatilia kwa umakini warsha hiyo kwa ajili ya kutekeleza Mradi mpya wa SHUGA Redio wenye lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU kupitia Redio za Jamii nchini.
  DSC_0091
  DSC_0120
  Pichani juu na chini ni Washiriki wakijidiliana kwenye vikundi kazi wakati wa warsha hiyo.
  DSC_0124
  DSC_0182
  Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akitoa mwongozo wa kazi za vikundi kwa staili ya aina yake kwa washiriki wa warsha ya siku mbili katika utekelezaji wa Mradi mpya wa SHUGA Redio.
  DSC_0203
  Pichani juu na chini washiriki akitolea maelezo ya picha aliyoichora ikimaanisha nini wakati wa warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa.
  DSC_0221

  0 0

  IMG-20140725-WA0006 
  Katika kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali barabarani wakali katika muziki wa bongo fleva Mr Blue, Amini, Banaba Boy na Dyna Nyange wamerekodi wimbo wa pamoja kuhamasisha uzingatiaji wa usalama barabarani na kwenye vyombo vya usafiri. Wimbo unaitwa Dereva Makini umetayarishwa na katika studio za C9. Kampeni hiyo ya dereva makini imeandaliwa na Transevents Marketing ambao ndio wamiliki wa tovuti ya Kariakoo Digital kwa lengo la kutoa hamasa kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuwawezesha abiria kufika salama waendako.

  0 0
 • 07/25/14--05:58: kibonzo cha Nathan Mpangala


 • 0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila leo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Shaban Ally Lila (kulia) akitia saini hati ya Kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuapishwa kwake  leo jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye miwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akishuhudia tukio hilo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Kiapo cha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi  hati ya Kiapo  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) akimpongeza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
  : Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahaka Kuu Tanzania mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman.Picha zote na Frank Shija- MAELEZO

  0 0

   Usu Millya Mwanamtandao wa Ulingo wa Katiba na wanawake ambaye alikuwa ndiye mwezeshaji wa Mkutano huo ambao  ulikuwa ni wa siku mbili akiendelea kutoa mwongozo wa mkutano huo.
   Doreen E. Maro kutoka TAMPRODA ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akiwakilisha Wafugaji Akileta Mrejesho wa walichokuwa wakikijadili katika Kundi lao juu ya mapendekezo ya kuimarisha Masuala muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
   Dkt. Macca A. Mbalwa  Mkurugenzi wa Giyedo Tanzania akiwa anatoa Mrejesho wa kile ambacho walikuwa wamekijadili na kutoa mapendekezo yao ya Kuboresha masuala muhimu katika Rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
   Salama Aboud Talib Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba  na Naibu Katibu Mkuu wa UWT akizungumzia makosa mbalimbali ambayo yapo katika Rasimu ya Pili ya Katiba mpya na kutoa mapendekezo kuwa Iboreshwe ili kuweka usawa.
   Executive Director wa  Women Fund Tanzania Mary Rusimbi akizungumza juu ya Majumuisho ya pomoja na Kupanga mikakati ambayo yatasaidia Kuimarisha Masuala Muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.

   
   Mgeni Hassan Juma Mwenyekiti wa Wawakilishi  Wanawake Zanzibar akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria kwa muda wa siku mbili katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la  Katiba, Mtandao wa wanawake na TAMWA
   Profesa Ruth Meena  Akitoa Majumuisho pia kutoa Shukurani kwa wale wote waliohudhuria katika Mkutano huo uliochukua siku mbili.
   Valerie Msoka akifunga Rasmi Mkutano huo.
   Fredrick Msigala Mjumbe Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mlemavu wa Miguu akielezea masikitiko yake ya Jinsi watu wenye ulemavu wakiwemo wanawake na wanaume ambavyo wametengwa na kukosa haki zao, amesisitiza Serikali katika Rasimu Mpya ya Pili ya Katiba wawaangalie walemavu kwa umakini na ukaribu maana wanahaki sawa na watu wengine. Pia amesisitiza walemavu wajaliwe katika huduma za Afya mana ni Muhimu kwao. Mwisho amesisitiza kuwa wanawake wenye ulemavu wanahaki ya Kuolewa na kuto nyanyaswa pindi wanapokuwa katika ndoa zao.
   Modesta Mpereme ambaye ni Kiziwi hasikii lakini anaongea vizuri pia ni Mwenyekiti kutoka  Sauti ya Wanawake  wenye Ulemavu Tanzania, Ameiomba serikali iwe na vitendea kazi vya kutosha ambavyo vitawasaidia walemavu katika secta mbalimbali Mfano katika Mabenki kuwe na vifaa maalum vya kuwasaidia walemavu, Katika Upande wa Afya amesisitiza kuwe na hata watu wanaoweza kutoa msaada wa kutafsiri mambo mbalimbali mfano kwa Viziwi, wasio ona na ambao Hawawezi kuongea.
   Siti Ally Mwanasheria na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar akisisitiza umuhimu wa usawa kati ya haki za wanawake na wanaume katika jamii , Pia alisisitiza juu ya mabinti wanaopata Mimba za utotoni wakiwa mashuleni na kusisitiza kuwa wanaruhusiwa kusimama masomo mpaka kipindi mtoto atakapokuwa mkubwa anaruhusiwa kuendelea na masomo,  Mwanaume aliyesababisha Mimba anaweza akashtakiwa .
   Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba pamoja na Wadau mbalimbali waliofika katika Mkutano huo.

  0 0

   Afisa Uhusioano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Wapili kulia), akimsalimia Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima, (CHAKUWAMA), kilichoko Sinza jijini Dar es Salaam jana, baada ya wafanyakazi wa Mfuko huo kukab idhi misaadsa ya vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Idd. Mfuko huo pia umekabidhi misaada kama hiyo kwa vituo vingine sita vya yatima jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd. Kulia ni Afisa wa fedha wa Mfuko huo, Mohammed Madenge, na kushoto ni A\fisa Masoko, Magire Werema
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Kulia), akikabidhi msaada wa vyakula ikiwemo Mbuzi, kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea yatima cha Mwandaliwa kilichoko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. PSPF, imetoa misaada kama hiyo kwa vituo sita vya yatima jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd.
   Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema, (Kulia), akikabidhi Mbuzi na vyakula kwa watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Chakuwama, Sinza jijini Dar es Salaam jana. Mfuko huo umekabidhi misada kama hiyo kwa vituo vingine sita jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki.
  Chakuwama_Said Hassan
  Afisa anayeshughulikia masuala ya fedha, wa Mfuko w aPensheni wa PSPF, Mohammed Madenge, (Wakwanza kjulia), akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamkizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, (Katikati), na afdisa masoko, Magira Werema, wakikabidhi msaada wa vyakula ikkiwemo Mbuzi, kwa kituo cha kulea watoto hyatima cha Mwandaliwa kilichoko Bunju nje kidogo ya jiji jana. PSPF, imekabidhi misaada kama hiyo kwa vituo vinghine sita jijini kwa ajili ya khjusherehekea sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa wiki.

  0 0

   ??????????????????????
  Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kilolo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Gerald Guninita akiweka ngao ya jadi katika sehemu inayotarajiwa kujengwa Mnara wa Mashujaa wa Jeshi la Mkwawa waliopigana vita dhidi ya dhuluma za Wajerumani, Mnara huo upo karibu na walipozikwa askari wa kijerumani 300 wakati wa vita na chifu wa wahehe Chifu Mkwawa mnamo mwaka 1891 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo mkoani Iringa.
  1
  Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita kwa gwaride la heshima katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo mkani Iringa leo.
  3
  Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita(Kushoto) akiwa pamoja na mwenyekit wa Halmashauri ya wilaya hiyo
  Joseph Muhumba wakitoa heshima  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo.
  5
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya,Pudenciana Kisaka (mwenye pinki) sambamba na wakuu wa wilaya ya Mufindi na Iringa wakitoa heshima wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo.
  ??????????????????????
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP, Ramadhani Mungi akiweka silaha ya jadi (mkuki) kwenye mnara wa mfano wa mashujaa. Mnara wa mashujaa wa askari wa Chifu Mkwawa utarajia kujengwa mahali hapo karibu na mnara wa wajerumani 300 waliozikwa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa.
  9
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo. (Picha zote na Denis Mlowe)

  0 0

  Regional retailer, Nakumatt Holdings, will on Sunday morning officially open the doors to its 48th branch located at Mlimani City Mall, Kinondoni District in Dar es salaam.
  The new branch, will also be aptly known as “Nakumatt Mlimani” and will provide a convenient shopping spot for shoppers in Dar es Salaam.

  What:                         Nakumatt Mlimani branch opening
  When:                        Sunday, July 27th, 2014
  Where:                       Mlimani City Mall
  Time:                          10:00am

  Attendees:                 Hon. Janet Mbene,
  Deputy Minister, Ministry of Industry, Trade and   Marketing
  Mr. Atul Shah,
  Managing Director Nakumatt Holdings
  Mr. Thiagarajan Ramamurthy,
  Regional Director, Operations and Strategy at Nakumatt Holdings

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
    Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwela ngao kwenye mnara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo. Wengine ni
   Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Waziri Mkuu Mzengo Pinda leo Julai 25, 2014
    Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.Wengine toka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe omar  Othman makungu leo Julai 25, 2014
    Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiamkiana na wazee wa Tanzania Legion waliopigana katika vitra kuu ya dunia ya pili  waliohudhuria  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani  ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014.

  0 0

  PG4A6139
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na  makamu wa Rais wa Sudan, Hassabo Mohamed Abdel Rahman katika mkutano maalum wa nchi za maziwa makuu wa kujadili ajira kwa vijana uliofanyika jijini Nairobi Julai 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PG4A6141
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza  na  makamu wa Rais wa Sudan, Hassabo Mohamed Abdel Rahman katika mkutano maalum wa nchi za maziwa makuu wa kujadili ajira kwa vijana uliofanyika jijini Nairobi Julai 24, 2014.
  PG4A6075
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Mtanzania  Nancy Kairagi ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa  Rais wa Umoja wa Vijana wa Nchi za maziwa makuu, wakati alipokutana nae jijini Nairobi Juai 24, 2014 kwenye mkutano maalum  wa nchi za maziwa makuu  wa kujadili tatizo la ajira kwa vijana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PG4A6086
  Waziri mkuu, Mizengo Pinda  na Waziri wa kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kushoto)  wakizungumza na Mtanzania Nancy Kairagi ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa Nchi za Maziwa  Makuu katika Mkutano Maalum wa nchi za Maziwa Makuu wa kujadili swala la ajira kwa vijana uliofanyika Nairobi Julai 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  2
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Moroco jijini Dar es salaam wakati akielezea kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya uzinduzi wa albam ya mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando inayojulikana kama "Kamata Pindo la Yesu" maarufu FACEBOOK utakaofanyika kwenye ukumbi wa VIP Diamond Jubilee Agosti 3/ 2014 jijini Dar es salaam na kufuatiwa na maonesho mengine katika mikoa ya Tabora, Geita na Mwanza mara baada ya uzinduzi wa Dar es salaam, Msama ameongeza kuwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wamethibitisha kushiriki katika uzinduzi huo ambao ni John Lisu, Upendo Kilahiro, Upendo Nkone , Ephraim Sekereti na wengine wengi, Tiketi zinapatikana katika vituo vifuatavyo Maduka yote ya Msama Promotion Kariakoo na Posta, Bestbite Namanga, vituo vya mafuta Puma Mwenge na Airport. Watu wote mnahimizwa kuwahi kununua tiketi ili kujihakikishia nafasi katika uzinduzi huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  3
  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu baadhi ya mapato yatakayopatikana kuelekezwa kwenye vituo vya watoto yatima.
  4
  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kuhusu tikaeti ambapo amesema zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi ambayo ni Maduka yote ya Msama Promotion Kariakoo na Posta, Bestbite Namanga, vituo vya mafuta Puma Mwenge na Airport watu wote mnahimizwa kuwahi kununua tiketi ili kujihakikishia nafasi yake katika uzinduzi huo.
  5
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumza ya Mkurugenzi ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wakati akielezea mambo mbalimbali kuhusu uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pino la Yesu ya mwimbaji Rose Muhando.

  0 0

  IMG-20140725-WA0004
  Pichani ni Mtangazaji anayeongoza Kipindi cha 'Mimi na Tanzania' Hoyce Temu aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 akiwa nje ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili ambapo alimua kufunga safari kwa ajili ya kufanya mazungumzo maalum na Balozi wetu wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula.
  IMG-20140725-WA0006
  Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
  IMG-20140725-WA0005
  Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema ...Naipenda Tanzania yangu!
  IMG-20140725-WA0003
  Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang'anyi na Balozi Ombeni Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na Balozi wa sasa Mh. Liberata MulaMula.
  IMG-20140725-WA0007
  Mheshimiwa Balozi Liberata MulaMula ndani ya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC, Marekani!
  Mahojiano hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.
  IMG-20140725-WA0009
  Na wale waliokuja kuomba Visa wakapiga picha na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania na muongozaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu.
  IMG-20140725-WA0008
  Hoyce Temu akipata picha ya ukumbusho na mpiga picha Iska JoJo aliyerekodi kipindi hicho.Hoyce Temu anatoa shukrani za pekee kwa Blogger Mzee wa VIJIMAMBODJ Luke Joe kufanikisha mahojiano ya Hoyce Temu na Balozi Liberata Mulamula.

  0 0

  WAKATI hamu ya mashabiki kila kona kwa sasa ni Agosti 8, mwaka huu katika tamasha kubwa la kihistoria la Usiku wa Matumaini litakalofanyia Uwanja wa Taifa jijini Dar, mashabiki wengi wanatamani kuwaona wakali kibao wakipanda jukwaani na kupiga nyimbo zao kali.
  Diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade
  Good newz ni kwamba Zuwena Mohamed ‘Shilole’ atapanda jukwaa moja na diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade kudondosha shoo ya kihistoria.

  Uzuri wa wasanii hao wawili ndiyo unashawishi watu wengi kufika katika tamasha hilo lenye lengo ya kuchangia mfuko wa elimu nchini. Unataka kujua sifa za wasanii hao? Hizi hapa:

  Shilole ambaye wengi wamezoea kumwita  Shishi Baby, amekuwa habahatishi jukwaani kwa jinsi anavyojua kuwapagawisha, hivyo mashabiki wategemee sapraizi kibao kutoka kwa bidada huyo kwenye sekta maalum ya kukata mauno na kuacha watu midomo wazi.

  Kwa upande wake, Yemi Alade anatisha balaa. Staili ya Johnny ndiyo atakayoinesha siku hiyo huku akichungulia kwa kumtafuta Johnny uwanjani mpaka atakapofanikiwa kumuona na kurudi naye Nigeria kama alivyoahidi.


  NGOMA ZAO
  Pata picha kwa Shilole atapopanda na kupiga nyimbo zake kali kama Chuna Buzi, Lawama, Nakomaa na Jiji, Paka la Baa na Namchukua inayotamba kwa sasa, hakika patakuwa hapatoshi kwani Shilole amesema hatabakisha kitu siku hiyo.
  Zuwena Mohamed ‘Shilole’
  Bidada Yemi Alade atashuka na ngoma inayotamba Afrika, Johnny kisha atazidondosha kali nyingine ambazo zimetokea kuiteka Afrika kama GhenGhenLove, Bamboo, Show Me na Tangerine.
  MADANSA
  Shilole ameahidi kudondoka na madansa wake ambapo watakuwa naye sambamba jukwaani katika kukamua siku hiyo.
  “Mashabiki wategemee kuona mpangilio na staili tofauti kutoka kwa masteji shoo hao ambazo zitakuwa funika bovu,” alisema Shilole.
  Yemi naye hatakuwa nyuma katika eneo hilo, ameahidi kucheza sambamba na madansa wake siku hiyo. Kama ilivyo kwenye makamuzi yake kupitia video ya Johnny na Tangerine ambapo madensa wake wanaonekana wakikamua mwanzo mwisho.
  WENGINE
  Mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto amefunguka kuwa mbali na shoo hiyo kali, utamu zaidi utakolezwa zaidi na mastaa wakali wa Bongo Fleva wakiongozwa na mfalme, Saleh Ally ‘Ali Kiba’, Meninah, Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Scorpion Girls, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.
  “Kila msanii atakayepanda jukwaani atahakikisha anapiga nyimbo zake zote ndipo ampishe mwenzake, itakuwa ni jiwe baada ya jiwe,” alisema Maloto.
  Aidha, tamasha hilo litapambwa na mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge mashabiki wa Simba na wenzao wa Yanga, Bongo Fleva na Bongo Movie pamoja na mapambano kibao ya ndondi, burudani zote hizo mashabiki watazipata kwa kiingilio cha shilingi elfu tano.
  Tamasha hilo limedhaminiwa na E.FM, Clouds FM, Times FM, Vodacom, Pepsi, Azam TV na SYSCORP.
  JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

  0 0
  Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bahati Bukuku akiwa kwenye moja ya kazi zake ya uimbaji.

  Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Gari lenye namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia ikiendeshwa na EDSON S/O MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa Tabata – Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeruhi kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari lingine linalosadikiwa kuwa ni Fuso.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 majira ya saa 03:00 alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.

  Kamanda MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON s/o MWAKABUNGU ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI D/O BUKUKU, Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20, Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam yeye ana michubuko usoni na mkono wa kulia. Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

  Aidha Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

  Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.


  0 0

  Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. 


  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaa wa vyakula kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuvisaidia viweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr. 

  Msaada huo wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 3 umekabidhiwa na Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, ambaye alisema utaratibu huo ni wakawaida kwa kampuni yao kusaidia makundi na taasisi na idara anuai kwa masuala ya kijamii. 

  Bi. Mwakalebela alivitaja vituo ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza vyote vya jijini Dar es Salaam. 

  “…Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, jambo hili la leo ni utaratibu wa kampuni ya TTCL kusaidia makundi, taasisi na idara mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii,” alisema Bi. Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura. Msaada uliotolewa kwa vituo hivyo ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga, unga wa sembe, maharage pamoja na katoni za juisi za maboksi.

   Kwa upande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru Kampuni ya TTCL kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine  majumbani.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowassa akizungunza na waumi wa dini ya kiislam (hawapo pichani), katika hafla aliyofuturisha katika Msikiti Mkuu wa Monduli mjini.
   Shekh wa Wilaya ya Monduli Shekh Mwinshehe Mwinyi akizungumza na waumini wakati wa futari iliyoandaliwa na Mh. Lowassa.
   Baadhi ya waumini wakipata futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa.
   Mke wa mbunge wa jimbo la monduli Mama Regina Lowassa akizungumza katika ghafla ya futari  iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa iliyofanyika katika msikiti wa monduli.
   Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiwa na Shekh wa Wilaya ya Monduli Shekh Mwinshehe Mwinyi wakati wa futari aliyoiandaa kwa ajili ya waumini wa dini ya kiisalamu wilaya Monduli. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

  SERIKALI imepongezwa kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari za kujenga nyumba za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo Mwenge wa Uhuru ulifika na kuweka jiwe la msingi Julai 22 mwaka huu.

  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib katika risala aliyosoma mbele ya Kiongozi wa Mwenge kitaifa, Rachael Kassanda alisema Serikali kukitambua kijiji hicho kumeongeza ari ya wasanii kujenga nyumba za kisasa na kuongeza kasi ya maendeleo.

  Alisema kijiji cha wasanii kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya kuwakomboa na kuwapatia makazi ya kudumu wakisha staafu au kupotea kwa umaarufu wao katika fani zao.

  Katika sherehe hizo ambazo wasanii zaidi ya 1,500 waliofurika kupokea mwenge wa uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge, Rachael Kassanda aliwatoa wito kwa wasanii kuwa kioo halisi cha jamii kwa kuiga mema na kupiga vita mabaya katika jamii zinazowazunguka.

  Awali Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila aliwaasa wasanii kutumia vipaji vyao kuwaelimisha jamii kuhusu maadili mema na kuiga yanayostahili kwa mila na desturi za Mtanzania.

  Katika sherehe za kuweka jiwe la msingi zilizofanywa na kiongozi wa mbio za Mwenge,SHIWATA ilimsimika balozi wa kijiji hicho kuwa ni msanii maarufu na mtangazaji wa kituo cha Redio Times FM, Suzan Natasha ambaye aliahidi kukitangaza kijiji hicho katika mipaka ya ndani na nje ya Tanzania.

  Sherehe hizo zilizoambatana na burudani mbalimbali zilizongozwa na Bendi ya Polisi, wanamuziki maarufu Kikumbi Mwanzo "King Kikii", Siza Mazongera "Wana Segere" na wasanii mbalimbali walitumbuiza.

  Wengine walioshudia kuwekwa jiwe la msingi katika kijiji hicho baadhi yao ni wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, George Lucas,Thom Kipese na kwa upande wa Yanga ni Abeid Mziba, Ramadhani Kampira, Bakari Malima, Omari Husein na wengineo.

  Pia katika kusherekea mwenge wa uhuru SHIWATA ilitoa ofa bure kwa wanachama wapya kupimiwa viwanja vya kujenga nyumba bure katika kijiji hicho ambapo wanamichezo, wasanii na waandishi wa habari walipata fursa ya kuoneshwa viwanja watakavyotakiwa kujenga.

  0 0


older | 1 | .... | 328 | 329 | (Page 330) | 331 | 332 | .... | 1897 | newer