Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WAZAZI JIJINI DAR WATAKIWA KUPELEKA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5 KUPATA MATONE YA VITAMINI A NA DAWA ZA MINYOO.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 
Wito umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan wazazi wenye watoto  walio na umri chini ya miaka 5 kuhakikisha kuwa  wanashiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za Minyoo kwa kuwapeleka watoto wao katika vituo mbalimbali vya afya ili waweze kupatiwa dawa hizo kabla ya terehe 20 mwezi huu.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam kufuatia zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za minyoo  kwa vituo vyote vya kutolea huduma vya Serikali, binafsi na mashirika ya dini  vilivyoainishwa katika  manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni kuelekea mwisho.

Amesema  zoezi hilo lililoanza tarehe 7 mwezi huu  ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati  wa Lishe wa Taifa  uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2013  kwa lengo la kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kuongeza hali ya lishe nchini.

“Zoezi hili sio geni kwani ni utaratibu ambao sote tunaufahamu kuwa Serikali yetu kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa Afya huendesha zoezi huendesha zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za Minyoo kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5 nchi nzima  kila mwaka”

Amesema zoezi la utoaji wa dawa hizo ni muhimu kutokana na  miili ya watoto hao kuwa katika mahitaji makubwa ya vitamin A kutokana na mchango wake  katika ukuaji wa miili na akili kwa kuimarisha uwezo wa kinga zao dhidi ya magonjwa pamoja na kuimarisha uwezo wa macho.

Kwa upande wake mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Magembe akizungumza kuhusu zoezi hilo ambalo linafikia kilele chake tarehe 20 mwezi huu amesema kuwa ni vema jamii ikawa na mwitikio chanya kwa zoezi hili kutokana na umuhimu wake  kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5.

Amesema kuwa zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A huokoa maisha ya watoto kwani huwalinda na dhidi ya maradhi hatari kama vile Kuharisha, Surua na maradhi ya mfumo wa hewa.

“Kila mzazi anatamani kumuona mtoto wake anakua akiwa na afya njema, watoto wenye upungufu wa Vitamini A wapo katika hatari ya kuugua maradhi,kupata upofu na hata kupoteza maisha” Amesisitiza.

Aidha, amesisitiza kuwa dawa zinazotolewa katika zoezi hilo ni salama kwani tayari zimepitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Nawasihi wananchi mjitokeze kwa wingi katika zoezi hili kwa siku zilizobaki kwa kuwa zoezi hili tunaloliendesha ni salama”

UONGOZI WA HOTELI YA NAURA SPRINGS WAKANUSHA TAARIFA ZA KUWAKA MOTO KWA HOTEL HIYO

$
0
0
SEHEMU YA JENGO LA HOTEL HIYO LIONEKAVYO KWA NJE.
MENEJA WA HOTEL HIYO BI.BEATRICE DALLARIS AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI,JUU YA  TAARIFA ZA UZUSHI ZILIZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMI KUWA HOTEL HIYO IMEUNGUA MOTO MAPEMA LEO JIJINI ARUSHA.

UTAWALA NA WAFANYAKAZI WA HOTELI YA NAURA SPRINGS IMESIKITISHWA KWA TAARIFA ZILIZOSAMBAA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII KUHUSU KUWA HOTELI YETU INAWAKA MOTO NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATU WA MKOA WETU, NDUGU NA JAMAA WA WAFANYAKAZI WA HOTEL ,VIONGIOZI MBALIMBALI, VYOMBO VYA USALAMA, IDARA YA ZIMA MOTO, WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALI MBALII VYA HABARI NA PIA KUSABABISHA WASIWASI NA KUTOWESHA UTULIVU NA AMANI WA MJI WETU.
TUMESIKITISHWA SANA NA TUMEOMBA UONGOZI WA MKOA WETU WALISHUGHULIKIE SWALA HILI KIKAMILIFU KWANI HILI SIO LA KUCHUKULIA MZAHA NA TUNGEOMBA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA HARAKA SANA KWA ALIE TOA TAARIFA HIYO YA UONGO.

TUNAWASHUKURU WATU WOTE WALIOFUATILIA SWALA HILI NAPIA TUNATOA TAMKO KUWA HABARI HIZI ZA KUWA HOTELI YETU INAUNGUA NI ZA UONGO.

BEATRICE DIMITRIS DALLARIS
HOTEL MANAGER

SUPER D AWAKUTANISHA MABONDIA WAKE NA WADAU KATIKA FUTARI

$
0
0
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akifuturu pamoja na mabondia na wadau wa mchezo huo wa pili kushoto ni Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Birali Ngonyani, Shomari Mirundi, Raymond Mbwago wakati wa futari iliyoandaliwa na kucha huyo nyumbani kwake Rozana Dar es salaam 
Baadhi ya waumini wa dini ya kislam wakiomba duwa baada ya kufuturu katika futari iliyoandaliwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' mwenye kibagarashia na kanzu
Mabondia na wadau mbalimbali wakifurahia futari iliyoandaliwa na kocha Super D. Picha zaidi BOFYA HAPA

KUMBUKUMBU

$
0
0
MWALIMU JANE GRACE SUFIANI

Ni miaka 12 sasa tangu ulipoiaga dunia tarehe 19.07.2002. Upendo, ukarimu na wema wako havitasahaulika kamwe. Unakumbukwa na watoto wako Elizabeth, Sofia, Lucy, Robert na Michael; wajukuu zako Rodgers, David, Joel, Bernice na Ellyson. Unakumbukwa pia na ndugu, jamaa na marafiki wote.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE!

BARAZA LA HABARI WAMUAGA BALOZI WA NORWAY

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ndugu Kajubi Mukajanga akizungumza wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach. Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari alimsifia Balozi wa Norway kwakuwa rafiki wa kweli kwa Baraza la Habari la Tanzania.
Rais wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
 Bakari Machumu akiwakilisha Chama Cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Jukwaa la Wahariri  wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
 Mshehereshaji wa shughuli hiyo ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Dk.Ayoub Rioba
Wasanii wa Dar Creators Group wakitumbuiza wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach,Julai 18,2014.
  Meneja wa Rasilimali Watu Baraza la Habari Tanzania Ziada Kilobo akimsaidia Balozi kufunga kilemba ikiwa sehemu ya zawadi ya vazi la asili la Kiafrika alilozawadiwa Balozi,kulia ni Meneja Uthibiti na Viwango  Pili Mtambalike wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
 Rais wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ndugu Kajubi Mukajanga wakiangalia picha ya Balozi ambayo alipewa kama zawadi wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga  Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik akizungumzwa wakati wa tafrija ya kumuaga iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach. Balozi pia amesifia Baraza a Habari kwa kukuza weledi na maadili katika tansnia ya Habari.
 Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Profesa Ruth Meena wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi huyo Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
 Rais wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari Rose Haji wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga  Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
 Dk.Ayub Rioba(kulia) akizungumza na Mhariri wa Baraza la Habari Tanzania Hamisi Mzee wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga  Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Baraza la Habari,Wahariri na wadau wengine wa Habari kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
(Picha kwa Hisani ya kamerayangublog.com)

INTRODUCING KOBA FT DULLY SYKES - KIZUNGUMKUTI OFFICIAL MUSIC VIDEO HD

(TWA) NA BENKI YA WANAWAKE TANZANIA (TWB) WAFANYA MAFUNZO KITUO CHA KINAMAMA WENYE WATOTO WENYE UGONJWA WA MTINDIO WA UBONGO NA MGONGO WAZI CHAWAWAKI KIGAMBONI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Bi. Margaret Chacha akizungumza na kikundi cha kinamama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha kigamboni(Chawawaki), wakati ya mafunzo ya ujasiriamali na kuwaelimisha juu ya fursa zinazotolewa na benki ya TWB, Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Tanzania Women Of Achievement(TWA)
  Mwenyekiti wa Tanzania Women Of Achievement(TWA) Bi.Sadaka Gandi akizungumza na kinamama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha Kigamboni(Chawawaki) pembeni yake ni Bi. Margaret Chacha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania na Bi. Hellen Kiwia Katibu Mkuu wa Taasisi ya TWA.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Bi. Margaret Chacha akifurahia jambo na Katibu mkuu wa Tanzania Women Of Achievement(TWA) Bi. Hellen Kiwia wakati mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa kwenye kituo cha Chawawaki Kigamboni.
Bi Blandina Sembo akiongea na kinamama wa Chawawaki
  Mshauri nasaha na mtoa mafunzo wa CCBRT Bi. Mgaya Mhamanda na Bi Suzane Mrema wakiongea na kinamama hao.
Kinamama wa Kituo cha watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi wa Kigamboni(Chawawaki) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake (TWB)Bi. Margaret Chacha(hayupo pichani)wakati wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Women Of Achievement(TWA).

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 LIVE: YEMI ALADE, SHILOLE KUONYESHANA KAZI AGOSTI 8, 2014


RAIS KIKWETE AFUNGUA DARAJA LA RUHEKEI LINALOUNGANISHA WILAYA YA MBINGA NA WILAYA YA NYASA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli wa kwanza kulia wakifanya ishara ya kuweka jiwe la msingi na kufungua Daraja la Ruhekei linalounganisha kati ya Mbinga na Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akifurahia kikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma katika sherehe ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika barabara Mbinga –Mbamba bay mkoani Ruvuma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salma Kikwete pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakipita juu ya Daraja la Mto Ruhekei baada ya kulifungua mkoani Ruvuma. Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya mpya ya Nyasa pamoja na Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya (Mb) kabla ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) katikati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Mto Ruhekei mkoani Ruvuma.

KAMPUNI YA MONTAGE YAFUTARISHA WAOTO YATIMA WA KITUO CHA SOS VILLAGE

$
0
0
4a
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Montage ya jijini Dar es salaam akiwagawia watoto yatima wa kituo cha kulelea watoto cha SOS Village kilichoko Sinza barabara ya Sam Nujoma alipowakaribisha kwa futari kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Kindondoni juzi ikiwa ni moja ya maelengo ya kampuni hiyo kuwakumbuka watoto yatima na kuwakarimu wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
5a
Anitha Pangani mfanyakazi wa kampuni ya Montage akiwagawia watoto chakula wakati wa futari hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Montage.
6a
Watoto wakiendelea kupata chakula
7a
Watoto wakifuturu
8a9a
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho wakishiriki katika futari hiyo pamoja na watoto.
11a
Mtoto Naijo Nestor Mapunda akifuturu pamoja na watoto wenzake wa kituo cha SOS Village Sinza.
13a
Watoto wakipaku chakula

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO; JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI TAMKO KUHUSU KUONDOKA KWA WALIOKUWA VIONGOZI

$
0
0


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Kigoma Kaskazini tunapenda kutoa taarifa kwa umma kutokana na sintofahamu inayotaka kulazimishwa mbele ya jamii kuhusu uimara wa chama chetu mkoani Kigoma.

Tangu jana na leo kumeenea taarifa zinazowahusu watu watatu, Jaffari Kasisiko, Msafiri Wamarwa na Mama Malunga Masoud, ambao vyombo mbalimbali vya habari vimeandika kuwa wamehama chama chetu cha CHADEMA na kukimbilia wanakojua wao (maana CCM inafanya kazi zake katika sura mbalimbali).

Katika hatua ya awali, sisi CHADEMA Jimbo la Kigoma Kaskazini tungependa kusema machache juu suala hilo la watu hao kuhama;

1.      Kwanza watu hao mbali ya kwamba walikuwa ni viongozi wa chama ngazi ya mkoa, kwa uhakika kabisa walikuwa ni kikwazo kama si kizuizi cha muda mrefu sana kwa chama chetu kustawi na kuwa imara zaidi katika mkoa mzima wa Kigoma ili kiweze kukimbizana na wenzetu wa maeneo mengine nchi nzima. Badala yake walikikumbatia na kukiatamia chama. Wakati maeneo mengine wenzetu wakiongeza wabunge majimboni, Kigoma chini ya uongozi wao ikauza majimbo.

2.      Tunaweza kusema kuwa viongozi hawa pamoja na wengine wachache ambao tunajua wako mbioni kuondoka kati ya leo na kesho, walikuwa ni sawa na KOTI LILILOTUBANA. Kwa muda wao wote wa uongozi hawakuwahi kufanya kazi yoyote ya kioganazesheni na kukieneza chama mkoa mzima. Wao walikuwa watu wa mikutano ya hapa na pale Kigoma mjini pekee au pale ambapo kunakuwa na uongozi wa kitaifa au wabunge.

3.Kwa muda mrefu saa wamekuwa viongozi ‘waliotubana’ kwa sababu walifanya kazi kwa kuangalia zaidi maslahi yao. Sasa kuondoka kwao, ni nafuu kwa chama. Pia ni fursa iliyokuja kwa wakati mwafaka kwa wanachama makamanda waaminifu na watiifu waliofungiwa milango kwa muda mrefu, kusonga mbele kukijenga chama chetu kwa imani kubwa ya kuendelea kubeba matumaini ya Watanzania wanyonge. 

4.Upo ushahidi wa wazi katika hili. Kwa muda mrefu sasa viongozi hao na wengine wenzao waliopangwa kuondoka kwa awamu nyingine, wamekuwa wakilalamikiwa kufanya kazi ya chama kingine cha siasa kwa maslahi na maelekezo ya CCM. 

5.      Katika madai yao ya kuhama chama watu hao wamesema wamefikia hatua hiyo eti kutokana na chama chetu kuwa cha kibabe eti kwa sababu tu Zitto Kabwe alivuliwa nafasi Naibu Katibu Mkuu ndani ya chama! 

6.      Madai hayo yanashangaza kwa sababu mbali ya chama kuwa na sababu nzito za kumvua Zitto (na wenzake akina Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba) cheo hicho kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu, pia tunaamini hakuna mwanaCHADEMA amejiunga na chama hiki kwa ajili ya cheo. Ndani ya chama chetu tunaamini katika kugawana majukumu si vyeo.

7.      Katika hali ya kushangaza zaidi wanasema eti Zitto amezuiwa kugombea uenyekiti. Sasa tunajiuliza hiyo nia ya kugombea ambayo hatujawahi kuisikia ikitangazwa kwa kufuata katiba, kanuni, maadili, miongozo na itifaki za chama, waliambizana wao wenyewe na mtu wao? Lakini kwa wanachama wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma tunaelewa Jafari Kasisiko analipa fadhila za misaada binafsi ikiwemo kupelekwa nje ya nchi. 

8.      Ninaomba kutoa wito kwa viongozi wenzangu wa wilaya na majimbo ya Kasulu Mashariki, Muhambwe, Buyungu, Kasulu Magharibi, Manyovu, Kigoma Kaskazini, Kigoma Kusini na Kigoma Mjini, tukutane kwa ajili ya kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa ili sasa tuchukue hatua zingine za muhimu na haraka za kuhakikisha tunasafisha chama chetu kwa kuwaondoa vibaraka na wasaliti wote waliosalia.

9.  Pia tunaomba katika hali ya dharura Chama Makao Makuu pia kiingilie kwa kutumia kifungu cha Katiba 6.1.3, ili kupata chombo cha kuendelea kuwaunganisha wanachama wakati mkoa ukijiandaa kuchukua hatua hiyo kupitia Baraza la Mashauriano.

10.Sisi wa CHADEMA Kigoma Kaskazini tunawataka wale wengine waliosalia katika mkakati huo wa kuhamisha watu wachache lakini kwa makundi ili eti kujenga taswira ya CHADEMA kubomoka, wakiwemo viongozi kadhaa wa Kanda wasisubiri. Chama chetu kitajengwa na watu wenye imani watakaoweka maslahi na matakwa ya wananchi mbele kwa kuzingatia misingi yetu kama inavyoelezwa katika Katiba ya Chama, kanuni, maadili na miongozo.

Kwa niaba ya Wanachadema imara na makamanda watiifu na waaminifu kwa mabadiliko yanayobeba matumaini na haki za Watanzania wanyonge, naomba kutoa taarifa hii.

Ally Kisala
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kigoma Kaskazini
Mjumbe wa Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Kigoma

TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2014 ' NDONDI ZA MWAKA'

Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KOICA/KAAT) yapata uongozi mpya

$
0
0
 Rais Mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT), Bw. Stephen Katemba (Kulia) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa. Anayemsikiliza ni Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Kushoto).
 Viongozi wapya KAAT na viongozi wa zamani wakipongezana mara baada ya uchaguzi huo.
 Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Katikati) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Kushoto ni aliyekuwa Muweka Hazina wa KAAT, Bibi Emilia Maingu na kulia ni Bw. Stephen Matee ambaye ni Muweka Hazina mpya.
 Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Wapili Kulia) akikabidhi nyaraka za KAAT kwa uongozi mpya. Kutoka kushoto pichani ni Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara), Bw. Bukheti Juma (Wapili kushoto) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar). Wengine ni Rais Mpya Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Stephen Matee (Kulia)ambaye ni Muweka Hazina mpya.
 Uongozi mpya wa KAAT wakizungumza na Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Wapili kulia).
Wakiwa katika picha ya pamoja ni uongozi mpya wa KAAT na baadhi ya viongozi wa zamani wa Jumuiya hiyo.


*Wadhamiria kuitangaza Tanzania kibiashara kimataifa

Na Saidi Mkabakuli.

Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea imefanikiwa kupata uongozi mpya, utaongoza umoja wa Watanzania hao kwa muda wa miaka miwili.


Waliochaguliwa kuongoza KAAT ni pamoja na Bw. Stephen Katemba ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya. Bw. Katemba atasaidiwa na Bw. Bukheti Juma (Makamu wa Rais, Zanzibar) na Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara). Katika nafasi ya Uweka Muweka Hazina, aliyechaguliwa ni Bw. Stephen Matee, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ulio chini wa Mama Anna Mkapa.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Jumuiya hiyo, Bw. Katemba ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Biashara za Kimataifa, amesema kuwa Tanzania ina fursa kubwa katika eneo la biashara za kimataifa kuwa kuzingatia rasilimali zilizopo nchini na kuchagiza kuwa fursa hizo zinaweza kutumiwa ipasavyo kwa kujitangaza tu.


Bw. Katemba aliongeza kuwa kama Watanzania tukiwa na uzalendo wa dhati na kuwa mabalozi wazuri, Tanzania itakuwa na uhakika wa kukamata masoko makubwa ikiwemo Korea na Bara la Asia kwa ujumla. 


“Kwa mfano kwa mujibu wa hali ya uchumi wa Taifa, kwa mwaka 2013, mwenendo wa biashara ya bidhaa na huduma nje haukuwa wa  kuridhisha ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilipungua kwa asilimia 1.7 kutoka Dola za Kimarekani milioni 8,675.6 mwaka 2012 hadi Dola milioni 8,532.0,” alisema.


Kwa mujibu wa Bw. Katemba kuwa ili kufikia malengo ya kimkakati ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulio chini ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao umelenga kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi, Tanzania haina budi kufikia malengo ya kikao cha tisa cha Shirikisho la Biashara Ulimwenguni (WTO) ambalo linalenga kuziwezesha kibiashara nchi wanachama kuboresha biashara zao.


“Katika kikao cha tisa cha WTO, Mawaziri wa nchi wanachama 159 wa Shirikisho walikubaliana kuwa na “Mpango wa Bali” ambao unalenga kuziruhusu nchi zinazoendelea kuwa na fursa zaidi ya kuzalisha chakula cha akiba, kuinua kiwango cha biashara kwa nchi changa na kusaidia maendeleo ya nchi changa kibiashara. Hivyo, tunaweza kufikia malengo haya kwa kutangaza bidhaa zetu hasa za vyakula kwa mataifa yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” alifafanua.


Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim alisema kuwa Tanzania ina bidhaa nyingi ya kuziuza kwenye soko la Korea na kutolea mfano mchele wa Kyela kuwa ni bidhaa nzuri kwenye soko hilo.

Mtandao wa Wanawake na Katiba Wazungumzia Katiba Mpya

$
0
0
Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari. 
Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada katika mkutano huo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada katika mkutano huo.Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 

Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.

 MTANDAO wa Wanawake na Katiba umevitaka vyombo vya habari kuacha kuyumbushwa na upepo wa kisiasa katika suala zima la kupigania mambo ya msingi kwa jamii ambayo yanaitaji kuingizwa kwenye Katiba mpya kwenye mchakato unaoendelea hivi sasa wa kuandika katiba mpya. 

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wajumbe wanaounda mtandao huo jijini Dar es Salaam walipokuwa wakizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuelezea msimamo wa wajumbe hao kwenye mchakato wa uandikaji katiba mpya. Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu aliviomba vyombo vya habari kuwaunga mkono wanamtandao hao ambao pamoja na mambo mengine wamejipanga kupigania kero za wananchi kuhakikisha zinapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya hivyo kuwataka wanahabari kuwaunga mkono. 

Alisema vyombo vya habari visikubali kupelekeshwa na wanasiasa kwa kupaza sauti kwenye maslahi ya wanasiasa zaidi na kushindwa kujadili masuala ya msingi ya jamii, ambayo endapo yatapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya wananufaika ni wananchi wote tofauti na masuala ya utawala (madaraka). "Waandishi wa habari msikubali kuchezeshwa ngoma za wanasiasa, ambao mara zote wanapigania maslahi yao kiutawala...tupiganie maslahi ya jamii, jamii inaitaji kuona huduma bora za afya, elimu na mgawanyo sawa wa rasilimali," alisema Dk. Semakafu. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari alisema vyombo vya habari vina nguvu za kipekee katika kuleta mabadiliko kwenye jamii na mamlaka hivyo kuwaomba watumie fursa hiyo ipasavyo katika kupigania maslahi ya umma. 

"...Hivyo vyombo vya habari, kama msingi wa kupatikana kwa taarifa yoyote, na kuongoza katika ushawishi vina sehemu muhimu sana katika kuongoza kuleta mabadiliko yawe ya sera, tabia au utamaduni," alisema Bi. Msoka ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba. Hata hivyo alivitaka vyombo vya habari kuwaunga mkono wanawake kwani licha ya kuwa na mchango mkubwa katika jamii wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kusahaulika kwenye fursa anuai zilizopo. 

"...Wanawake ni asilimia 80 ya nguvu kazi vijijini na ni asilimia 60 ya wazalishaji wakuu wa chakula...lakini tunachangamoto nyingi," alisema Bi. Msoka. Mtandao wa Wanawake na Katiba ni muunganiko wa asasi za kijamii na kitaaluma zipatazo hamsini zilizoungana kudai katiba inayozingatia masuala ya kijinsia na inayotokana na mchakato ulioshirikisha sauti za makundi yote. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

MH.BALOZI MULAMULA AZUNGUMZA NA WAGOMBEA WA DMV PAMOJA NA KAMATI YA UCHAGUZI

$
0
0
IMG_8020Balozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Washington Dc na Mexico Liberata Mula mula akiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea uongozi DMV, wajumbe wa bodi na wajumbe wa tume ya uchaguzi kwenye ofisi za ubaloi Washington Dc Ijumaa Julai 18,2014. IMG_7900Mh.Balozi akifungua kikao hicho. IMG_7881Wajumbe wa bodi ya DMV Bw.Ulotu na Mama Kimolo wakifuatilia kikao hicho. IMG_7894Mjumbe wa tume ya uchaguzi Asha Haritz katika kikao hicho. IMG_7896Mgombea wa nafasi ya rais wa Jumuiya Bw.Liberatus Mwang'ombe akifuatilia mkutano. IMG_7895Mgombea nafasi ya makamu rais Harriet Shangarai akifuatilia kikao hicho. IMG_7891Rais aliyepo madarakani na anayetetea nafasi yake Bw.Iddy Sandali akifuatilia mkutano huo. IMG_7886Wagombea wa nafasi ya katibu Bw. Mwilima kushoto na Bw.Mwamende. IMG_7888Mgombea wa nafasi ya kaimu katibu Bi.Bernadetta Kaiza akiwa na katibu wa tume ya uchaguzi Bi.Asha Nyag'anyi. IMG_7985Anti Asha kushoto akmuendorse mgombea wa nafasi ya makamu rais Bi.Salma huku wakipata futari. IMG_7904Bw.Eliudi Mbowe kushoto akipata futari baada ya kikao na mgombea wa nafasi ya kaimu katibu Bw.Solomon Cris.Kwa piocha zaidi ungana na Sundayshomari.com

HOFU YATANDA KWA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS, HUKU WENGINE WAKITAMANI WIKI IJAYO ISIFIKE.

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa mbele ya Majaji tayari kwa kupewa maoni yao na hatimaye kutaja watakaotoka chomwa na jua la utosi kwa Wiki hii. Kutoka Kulia ni Tishi Abdallah, Katikati ni Mtawa Kapalata na Kushoto ni Joshua Wambura.
Anneth Peter (katikati) akiwa mwenye huzuni kubwa kutokana na Mshiriki mwenza kutoka kanda ya Kaskazini Kareb John (hayupo pichani) kutoka kwenye shindano mara baada ya kuchomwa na jua la utosi.
 Washiriki wawili waliondolewa katika Shindano kwa wiki hii wakiwa mbele ya Jukwaa mara baada ya kutangaziwa kushindwa kuendelea kutokana na kuwa na idadi chache ya kura kutoka kwa watazamaji.Wa kwanza kushoto ni Kareb John na Malima Deogratius ambao wameaga mashindano
  Kareb John na Malima Deogratius mara baada ya kutangaziwa kuyaaga mashindano..
 Mara baada ya Kareb John Kuaga mashindano Mshiriki kutoka kanda ya Kaskazini Annet Peter alionekana mwenye huzuni kubwa.

 
 Washiriki wakiwa na huzuni kutokana na wenzao kuaga mashindano.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions, Dar Es Salaam
 Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Ni wiki ya Pili sasa ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki wengine wawili wamechomwa na Jua la Utosi na hatimaye kuaga shindano. Mchujo huo ni muendelezo wa Mchujo ambao kila wiki washiriki wawili watachomwa na jua la utosi na hatimaye kupelekea kuaga shindano la TMT.
Mpaka sasa Washiriki wanne tayari wameshayaaga mashindano na kupelekea washiriki 16 kubakia katika mchujo unaofuata.
Mpaka sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekua ni shindano lililoteka hisia za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na ubora, Uhalisia na Ubunifu wa hali juu kutoka kwa Waandaaji na waendeshaji pamoja na washiriki kuonyesha Vipaji vyao.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki wako asichomwe na Jua la Utosi unachotakiwa ni kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumfanya abaki ndani ya Nyumba ya TMT.
Mara baada ya washiriki wa wiki hii kuondolewa katika shindano hali imezidi kuwa ni simanzi kwa washiriki kutokana na kutokujua ni zamu ya nani kutoka wiki ijayo.
Washiriki waliotoka wiki hii ni Kareb John ambae alikua mmoja kati ya Washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha huku Mshiriki Malima Deogratius akiwa ni Mshindi kutoka KAnda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda namba 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678. Piga kura kadri uwezavyo ili kumnusuru mshiriki wako kutochomwa na Jua na Utosi wiki ijayo.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano lililobuniwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo inahusika na utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa filamu za Kitanzania huku ikiwa na malengo pia ya Kuibua vipaji vya Kuigiza na Mpira wa Miguu kwa Wanawake. Shindano hili Pia linaendeshwa na Kusimamiwa pia na Kampuni bora ya Usambazaji wa Filamu nchini ya Proin Promotions Limited
Huzuni na Simanzi zaendelea kutawala ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki hao wawili kuondoka lakini Pia Hofu Yaendelea Kutanda ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki kwa kutokujua ni zamu ya nani sasa kuchomwa na jua la utosi litakalompelekea kuaga shindano kwa wiki ijayo.

Msondo, Sikinde uso kwa uso Iddi Mosi TCC Club

$
0
0
Magwiji wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra “Sikinde” siku ya Iddi Mosi watachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa Nani Mtani Jembe ni kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Id El Fitr na pia litaamua ni bendi ipi kali kati yao.Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga amesema pambano hilo litaanza saa nane alasiri hadi majogoo. 
 
Kapinga alisema bendi zote mbili ziko msituni kujiandaa na mpambano huo.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kulinda upinzani wao.
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera  alisema jana watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaisambaratisha Sikinde.
 
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera,  Eddo Sanga, Juma Katundu, Roman Mng’ande `Romario’  na Hassan Moshi.Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
 
“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Sikinde ni Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Abdala Hemba, Musemba Waminyugu.
 
Ramadhani Mapesa, Adofth Mbinga, Kelvin Mausi Mjusi Shemboza, Tonny Karama, Bonny Bass, Habibu Abass Jeff , Juma, Juma Choka, Mbaraka Othman, Hamisi Mirambo, Ali Yahaya, Yusuph Benard na Ali Jamwaka.Pambano imedhaminiwa na Konyagi na Saluti5.

Rais Kikwete azindua rasmi stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma, Barabara ya Peramiho -Mbinga

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa jiwe la Msingi kuzindua rasmi stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Ruvuma Katika ziara ya Kikazi kukagua miradi ya maendeleo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi kufungua rasmi Barabara ya kilometa 78 ya Peramiho –Mbinga mjini  Julai 19,2014.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Wairi wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bwana Servasius Likwelile, mwenyekiti  wa mfuko  MCC Tanzania Bwana Bernard Mchomvu. Picha na Freddy Maro
 Sehemu ya Barabara ya Peramiho -Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78 iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78Km huku akiwa  na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali na balozi wa China nchini.

 Mamia ya wakazi wa Mbinga wakifurahia wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anamshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Utendaji wake mzuri wa kuwajali wakazi hao kwa kuwajengea miundombinu bora.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza kulia akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli kabla ya uzinduzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78km .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katikati akimshukuru balozi wa China nchini aliye kushoto kwake kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mkandarasi kutoka China Kampuni ya Synohdro. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria ufunguzi wa barabara hiyo.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Mawaziri waliohudhuria katika ufunguzi wa barabara ya Perahimo-Mbinga. Picha na Jackson Msangula

MABONDIA WAKUTANA NA KUUNDA UMOJA WA KUSAIDIANA KATIKA MAMBO MBALIMBALI

$
0
0
Bondia Japhert Kaseba kushoto akizungumza katika mkutano wa kwanza wa umoja wa kusaidiana katika mambo mbalimbali kwa mabondia wengine ni Habibu Kinyogoli 'masta' Fransic Miyeyusho na Thomas Mashali .

mmoja wa wapiganani wa kick boxing Mkali Kaizum akichangia mada
Mmoja wa mabondia Crispian Kisinini akichangia mada
mmoja wa mabondia akichangia mada.
Bondia Japhert Kaseba akizungumza kabla ya kufunga mkutano huo aliouitisha kwa ajili ya kuunda umoja wa mabondia kusaidiana kwa mambo mbalimbali picha nawww.superdboxing coach.blogspot.com

TAPELI LILILOJIDAI KISHOKA WA TANESCO LADAKWA LIVE MLIMANI CITY

$
0
0
10500539_819006161445574_7780628803053090260_n
Pichani juu na chini ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.

TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
10417599_819006198112237_2101442257557265538_n 
Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images