Mkuu wa kitengo cha Oparesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugen Massawe (wapili kushoto) akikata utepe kuzindua mafunzo maalum kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa kituo cha mafunzo cha Exim Academy, Bi Priti Punatar na Kushoto ni Beatus Temba, mkufunzi katika kituo hicho.
Meneja Mafunzo na Maendeleo wa Exim Academy, Japheth Oyugi akiwafunza baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wanaopata mafunzo hayo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo maalum yatakayotolewa na kituo hicho cha mafunzo jijini Dar es Salaam jana.
Benki ya Exim Tanzania imezindua mafunzo maalum, yakiwa na lengo la kuwapatia maafisa wake wapya na wa zamani wa matawi mbali mbali wa benki hiyo ujuzi katika shughuli a kibenki za kimihamala na juu ya sera za udhibiti ili kuimarisha tija kwa wafanyakazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.
Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa kwa wastani wa, masaa 56 ya mafunzo kwa maafisa mpya wa matawi mbali mbali ya benki, pamoja na masaa 160 kwa mafunzo yatakayokuwa yakiendelea ya darasani kwa maafisa wote wa matawi ya benki hiyo, kila mwaka.
Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika kituo cha mafunzo ya benki ya Exim cha 'Exim Academy' jijini Dar es Salaam jana, Meneja Mwandamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya Exim, Bi Priti Punatar alisema mafunzo hayo yanalenga katika kuboresha shughuli za matawi katika mazingira yaliyo salama na kupima ujuzi wa utatuaji wa matatizo mbali mbali bila kuwepo kwa viashirio vya majanga ambayo taasisi za kifedha ukumbana nayo katika dunia halisi ya masuala ya kibenki.
"Leo tunazindua mafunzo maalum ambayo yatawapatia maafisa wetu wa benki katika matawi mbali mbali ujuzi katika shughuli za kibenki za kimihamala na juu ya sera za udhibiti.
"Wafanyakazi wetu watapewa mafunzo juu ya majukumu mbalimbali katika tawi ili kuwajengea uelewa zaidi juu shughuli za kibenki na kuboresha za ujuzi wao katika biashara za masuala ya kibenki. Tunatarajia kuwa njia hii mpya itasaidia kuon geza ufanisi wetu katika shughuli zetu na kutuwezesha kufikia lengo la kufikia matakwa ya mteja, "alisema.
"Mafunzo haya yataongeza ufanisi kwa wafanyakazi wetu na tija, na hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja," alisema Bw Eugene Masawe, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji katika Benki.
Alibainisha kuwa, mafunzo hayo yatawawezesha wafanyakazi kujifunza kwa vitendo, mbinu za kuthibitika zitumikazo katika sekta kwa kutumia vifaa vya kipekee, ikiwa pia inalenga katika kuboresha na kurahisisha taratibu mbali mbali za kibenki katika benki.
"Tumeanzisha mafunzo haya tukiwa na lengo si tu kuongeza jitihada za kufikia matakwa ya mteja bali pia kutoa msaada bora wa huduma kwa wateja wetu wote na kuongeza ufanisi na kupunguza makosa yanayojitokeza ya kibenki katika shughuli zetu za kila siku.
"Kupitia mafunzo haya, wafanyakazi wetu pia watakuwa na uwezo wa kutathmini na kukabiliana na majanga yanayohusiana shughuli za kimihamala za kibenki, kukidhi mahitaji ya udhibiti, kuhakikisha wafanyakazi wanatumia fursa zote za kimauzo zinazojitokeza, hivyo kuboresha utoaji huduma kwa wateja," aliongeza Masawe.
Pia alisema kuwa mafunzo hayo yataiwezesha benki yake kufikia malengo ya kuendeleza wafanyakazi wa benki hiyo kwa kuwa na ujuzi wa uhakika katika masuala ya kibenki na utoaji wa huduma.
Exim Academy ni kituo cha mafunzo kilichothibitishwa kikiwa na cheti cha ISO 9001:2008 kilichoundwa kwa ajili ya wafanyakazi wa Benki ya Exim ambacho utoa mafunzo tofauti yakiutendaji, uongozi na utoaji wa huduma bora, na kujenga uhusiano nzuri na mteja kwa ujumla.