Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Sumaye kubariki uzinduzi wa Rose Muhando

$
0
0
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa albamu ya mwimbaji mahiri wa Injili nchini, Rose Muhando iitwayo Kamata Pindo la Ye`su.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Agosti 3 mwaka huu, ambapo waimbaji mbalimbali wa muziki wa kiroho watatumbuiza siku hiyo.Baadhi ya waimbaji mahiri ambao hadi sasa wameshathibitisha kushiriki uzinduzi huo ni Upendo Nkone, John Lissu, Bonny Mwaitege na Ephraim Sekeleti.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, ambao ni wadhamini na waratibu wa uzinduzi huo, Alex Msama, ilisema maandalizi muhimu kuhusiana na uzinduzi huo yanaenda vizuri.

“Tumekubaliana tumuombe Waziri Mkuu mstaafu Sumaye aje atupe baraka kwenye uzinduzi huo, nafurahi kusema ni mtu wa watu, amekubali kujumuika na wadau wengine siku hiyo. Hili ni jambo la furaha kubwa kwetu.

“Wasanii mbalimbali tunaendelea kuzungumza nao kuhakikisha wanashiriki katika uzinduzi huo, ambao utakuwa moto wa kuotea mbali,”  alisema Msama katika taarifa yake.

Sumaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005, akiwa ndiye Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu katika wadhifa huo kwa historia ya Tanzania.

Alisema hamasa kuhusiana na uzinduzi huo imekuwa kubwa pengine kuliko hata matamasha mengine ambayo Kampuni ya Msama Promotions imewahi kuyaandaa, kwani waimbaji wanatamani siku ifike wafanye mambo, mashabiki nao wanatamani siku ifike waone mambo.

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ni Kamata Pindo la Yesu, Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema na Facebook.

Baadhi ya albamu zilizompa umaarufu Rose Muhando ni Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo.

Baada ya uzinduzi wa Dar es Salaam, Muhando ataendelea kuitambulisha albamu yake mkoani Mwanza Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba.

KAA TAYARI KUSHUHUDIA KIVUMBI CHA PEPSI KOMBE LA MEYA 2014.

$
0
0
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuelekea kuanza kwa Michuano ya kandanda ya Pepsi Kombe la Meya 2014 , kutoka kushoto katika picha anaonekana meneja wa Kampuni ya SBC watengenezaji wa kinyaji cha Pepsi Nicolas Coetz, Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, na meneja mauzo wa kampuni ya Pepsi Sharif Taki. 
MASHINDANO ya Pepsi Kombe la Meya Jiji la Mwanza 2014 kuanza kutimua vumbi Agosti 2 mwaka huu na Bingwa kujinyakulia mzigo wa kitita cha Sh. Milioni sita, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Mwaka huu jumla ya timu 22 zitashiriki ambapo timu 12 zitatoka katika Kata 12 za  Jimbo la Nyamagana na timu nyingine 12 zitatoka katika vikundi na asasi mbalimbali za kijamii zilizopo jimboni humo.
Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, Albert G. Sengo akizungumza na wanahabari kuhusiana na taratibu za michuano hiyo zitakavyokuwa.
Mashindano haya yanafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo chini ya udhamini wa Kampuni ya SBC inayotengeneza vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha Pepsi ambapo kwa mwaka huu yameboresha zaidi kwa kuhakikisha vifaa vitakavyotolewa vinakuwa na ubora ikiwa pia na ongezeko la ukubwa wa zawadi za washindi. “Lengo kubwa la mashindano haya ni kuwezesha vikundi vya vijana wajasiriamali, kuleta umoja, hamasa, kuendeleza vipaji vya soka, mshikamano na burudani, lakini pia kuviwezesha mitaji ya kuendesha shughuli zao kupitia mashindano ya soka ili kuvijengea uwezo,”

Zawadi kwa washindi mwaka huu zimeongezeka ambapo bingwa atajinyakulia Bajaji ya kisasa ya kubeba mizigo na watu wanne yenye thamani ya milioni 4.5 na fedha tasilimu milioni 1.5 (jumla milioni sita), mshindi wa pili milioni 2, mshindi wa tatu milioni 1 huku mfugaji bora, timu yenye nidhamu na mwamuzi bora kuzawadiwa Sh. Laki mbili.
Awali meneja wa kamati ya mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, Bitegeko (wa kwanza kulia) alieleza kwamba timu zitakazoshiriki michuano hiyo zimegawanywa katika makundi manne ambapo kundi A litakuwa na timu sita, kundi B, C na D kila moja litakuwa na timu tano, mzunguko wa kwanza utachezwa kwa mtindo wa ligi katika makundi na hatua ya robo fainal timu zitacheza kwa mtoano hadi kupata timu mbili zitakazo cheza fainali ili kumpata bingwa kwa mwaka 2014.


“Viwanja vitakavyotumika katika michuano ya Kombe hilo ni Nyamagana, Nyegezi Kona, Mabatine Polisi, Buhongwa, Igoma Mnadani na Mkolani na waamuzi watakaochezesha mashindano hayo ni vijana wanafunzi kutoka katika Kituo cha Michezo cha Alliance cha jijini hapa,” alieleza.

 
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (wa pili toka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuelekea kuanza kwa Michuano ya kandanda ya Pepsi Kombe la Meya 2014 , kutoka kushoto katika picha anaonekana meneja wa Kampuni ya SBC watengenezaji wa kinyaji cha Pepsi Nicolas Coetz, Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, na meneja mauzo wa kampuni ya Pepsi Sharif Taki. 
Moja kati ya kanuni za mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, zinaeleza kuwa timu itaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi 25 kwa fomu zilizotolewa, Wachezaji wa Ligi kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza hawataruhusiwa katika mashindano haya.

Ni kosa kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa. Timu itakayo mchezesha mchezaji ambaye hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa itapoteza michezo yote ambayo mchezaji huyo aliichezea.

Mchezaji hatoruhusiwa kusajiliwa kwenye timu zaidi ya moja. Iwapo mchezaji huyo akibainika ataondolewa kwenye mashindano na timu hiyo haitoruhusiwa kuweka mchezaji mwingine mbadala, timu itanyang'anywa pointi kwa michezo aliyo cheza mchezaji huyo.
Pepsi Kombe la Meya 2014 itafuata sheria zote 17 za soka. Kubadili wachezaji (substitution) mwisho watano. Mchezaji akipewa kadi nyekundu hatoruhusiwa kucheza mechi moja inayofuata. 

Mashindano yatasimamiwa na Kamati ya Mashindano ambayo inamamlaka ya kuifuta katika mashindano timu yoyote ambayo wachezaji wake watakuwa ni chanzo cha vurugu katika mashindano.
"Matayarisho yako safi kwa asilimia 100" says Nicolas Coetz.
*    Kila timu ina wajibu wa kutunza nidhamu ya wachezaji na washabiki wake ndani na nje ya mchezo.
*       Maamuzi ya refa yatakuwa ya mwisho katika mchezo.

*      Ni kapteni wa timu pekee ndiye anaruhusiwa kupeleka malalamiko kwa muamuzi ndani ya mchezo.

*    Timu itakayogomea mchezo itakuwa imepoteza mchezo husika na Kamati ya mashindano itakaa kuijadili timu hiyo kwa adhabu nyingine kama itaona inafaa.

*     Mchezo utaanza saa 10:30 jioni. Kila timu inatakiwa kufika uwanjani saa moja kabla ya mchezo kuanza.

*  Viongozi wa timu watatakiwa kusaini kwenye nakala ya kanuni itakayobaki kwa muandaaji wa mashindano ikiwa ni ishara ya kuwa wamezielewa na wataziwasilisha vyema kwenye timu zao ili kuboresha mchezo.


Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya SBC Sharif Taki alisema kwamba tangu kuanza kudhamini mashindano hayo kwa sasa yamepanua wigo na kuwa na sula ya kitaifa  na tayari yamefanyika Morogoro, Mbeya, Dodoma na wanategemea Arusha kufanyika baada ya kumalizika haya ya Jiji la Mwanza huku pia wakianda ya kukutanisha timu za bingwa kwenye Majiji ya Mwanza, Tanga, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA QUR-AN JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi kukabidhi Tuzo za washindi wa mashindano ya kuhifadhi qur-aan, yaliyofanyika leo Julai 20, 2014, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Hatham Sadar, kutoka nchini Kenya wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

IPTL VS KAFULILA

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi)
Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL) na Pan Africa Power Solutions (T) Ltd, Joseph Mwakandege akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la ununuzi wa IPTL. Kushoto ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi.
  Habari na Mwene Said 
wa Blogu ya Jamii. 
 KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), imewasilisha maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ya kutoa zuio la muda kwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) la kutoendelea kutangaza maneno ya kashfa juu yake. 
Imeiomba mahakama hiyo kutoa zuio hilo, hadi shauri la msingi walilolifungua mahakamani hapo dhidi ya mbunge huyo kwa kuwatuhumu kuchota fedha katika akaunti ya Escow isivyo halali litakapoamriwa. 

IPTL kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP) na Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Harbinder Sign Seth, wamewasilisha maombi hayo mahakamani hapo chini ya hati ya kiapo cha dharura na yameungwa mkono na Seth.Maombi hayo namba 306 ya mwaka huu, yalitajwa mahakamani hapo Alhamisi iliyopita, mbele ya Jaji Rose Teemba, ambapo aliyaahirisha hadi Agosti 28, mwaka huu, kwa kutajwa. 

 Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, wadai hao kwa kupitia wakili wao Augustine Kusalika, wanaiomba mahakama hiyo itoe zuio la muda kwa Kafulila kwa kutoendelea kutangaza maneno ya kashfa kwa IPTL, PAP na Seth hadi shauri lao la msingi litakapoamuriwa.  Pia, wanaiomba mahakama kutoa zuio la muda kwa Kafulila kutoendelea kutangaza maneno ya kashfa kwa IPTL na PAP na aamuriwe kulipa gharama za maombi hayo. 


 Hivi karibuni IPTL, PAP na Seth kwa kupitia wakili wao Kusalika, walimfungulia kesi ya madai Kafulila, mahakamani hapo wakiiomba aamuriwe kuwalipa fidia ya jumla ya sh. bilioni 310 kutokana na kutangaza taarifa za kashfa dhidi yao. 

 Katika kesi yao ya msingi, wadai hao wanaiomba mahakama kuu katika hukumu yake, imwamuru Kafulila awalipe sh. bilioni 210 kama fidia kutokana na kashfa hizo na hasara ya taswira ya biashara na hadhi yao. Aidha, aamriwe kuwalipa sh. bilioni 100 kama fidia ya madhara ya jumla kutokana na usumbufu walioupata kutokana na taarifa za kashfa zilizotolewa dhidi yao na awaombe radhi kutokana na taarifa hizo, gharama ya kesi, riba kwa kiasi cha fedha yote wanayodai kwa kiwango cha asilimia cha mahakama kutoka tarehe ya hukumu hadi tarehe ya mwisho wa malipo hayo. 
 Pia, wanaiomba mahakama kutoa amri nyingine itakazoona zinafaa. Kwa kupitia hati yao ya madai ya kesi ya msingi, wadai hao wanadai kwa nyakati tofauti ndani na nje ya Bunge na kupitia mitandao ya kijamii, Kafulila ametoa maneno ya kashfa dhidi yao kwamba wamejipatia fedha katika akaunti ya Escow iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa njia zisizo halali. 
 Wadai hao wanadai IPTL iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuisambazia umeme na imekuwa ikitekeleza majukumu yake kama walivyokubaliana. 

 Inadaiwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited na TANESCO ambapo sh. bilioni 200 zilihifadhiwa katika akaunti ya Escrow iliyofunguliwa BoT, kusubiri kumalizika kwa mgogoro huo uliokuwa mahakama kuu.  Kwa kupitia hati hiyo inadaiwa kuwa baada ya kumalizika na kuhimitishwa kwa mgogoro huo, mahakama ilitoa amri ya IPTL kukusanya fedha hizo na BoT kutakiwa kuziachia. 

 Wadai hao wanadai katika hali ya kushangaza na bila ya uhalali wowote, Kafulika katika shughuli mbalimbali nje na ndani ya Bunge na kupitia mitandao ya kijamii  alimua kusambaza taarifa za kashfa kwa IPTL na Mkurugenzi Mtendaji wake. 

 Inadaiwa Juni, 2014, Kafulila alichapisha taarifa za kwamba IPTL na Seth walijipatia fedha kutoka katika akaunti ya Escrow isivyo halali, wakati si kweli na imehusika katika vitendo viovu vya kuchukua fedha katika akaunti hiyo. 

 Kwa kupitia hati hiyo, inadaiwa Kafulila amekuwa akitoa taarifa za kashfa, kwa kumtaja Seth kwa jina la singasinga, jambo ambalo si sawa na hivyo kumharibia sifa yake na kumsababishia uendeshaji wa biashara zake zinazotekelezwa na IPTL na PAP kudorora. 

 Inadaiwa kutokana na taarifa zilizotolewa na Kafulila, ameisababishia jamii kuamini kuwa ni kweli IPTL imejipatia fedha hizo katika akaunti ya Escow bila uhalal na zimesababisha hasara au kupungua kwa hadhi ya kampuni hizo. 

 Hata hivyo, wadai hao wanadai Kafulila akiwa mbunge ana kinga ya kutochukulia hatia za kisheria kwa masuala ambayo ameyasema bungeni, lakini amekuwa akitoa taarifa za kashfa dhidi ya wadai ndani na nje ya shughuli za bunge. 

 Wadai hao wanadai taarifa zilizosambazwa na Kafulila mbali ya kuwashushia hadi pia zimesababisha hasara ya kibiashara na ameendelea kufanya hivyo licha ya kupewa taarifa ya maneno na ya maandishi. Inadaiwa kutokana na taarifa hizo, Kafulila amesababisha hadhi ya kampuni hizo kushuka sio tu nchini bali hata kimataifa, hivyo kuwasabishia hasara kibiashara na madhara ya kisaikolojia na usumbufu kwa menejimenti. 

 Wadai hao wanadai kitendo cha Kafulila kuelezea mambo yaliyotokea katika mahakama za kisheria kuhusu maombi baina ya IPTL na kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited kimesabaisha si tu kuingilia uhuru wa mahakama bali pia hasara kwa IPTL, wakati alikuwa akijua kilichoendelea mahakani. 

Inadaiwa IPTL inatoa huduma ya kuisambazia umeme Tanesco, hivyo kutokana na taarifa za mdaiwa zimehatarisha uhusiano baina yake na shirika hilo hivyo kusababisha kudorora kwa uchumi na biashara yao.

NACTE Public Notice on Expired Status of Registration and Accreditation OF TECHNICAL INSTITUTIONS

Rais Kikwete amteua Jaji Shabani Ally LILA kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu

TAIFA STARS YATOKA SARE NA MSUMBIJI

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 


Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
 Thomas Ulimwengu  akichuana na beki wa Msumbiji, Josemar Machaisse.

 Huniwezi...Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior.
 Mshambuliaji wa Stars, Khamis Mcha akiwa katika harakati za kufunga goli.
 Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la 
Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka 'Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete'.

WAZIRI DK. KAMANI ATEMA CHECHE BUSEGA

$
0
0
NA MWANDISHI WETU, BUSEGA
MWENYEKITI wa CCM mkoani Simiyu, Dk. Titus Kamani, amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Madiwani, Makatibu wa Chama na Jumuia zake, kujiwekea ratiba ya kutembelea wananchi ili watambue kero zinazowakabili.
 
Dk. Kamani, ambaye pia ni Mbunge wa Busega na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama katika Kijiji cha Lamadi wilayani Busega.
 
Alisema huu sio wakati wa kukaa na kubweteka ofisini kusubiri wananchi wapelekea kero, bali ni wakati wa kuwatembelea na kufanya mikutano na kuwajulisha utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo ambayo yanatekelezwa kutokana na Ilani ya CCM.
 
“Madiwani wenzangu, wenyeviti, makatibu wa Chama na jumuia zetu ikiwemo ya vijana, msiwasahau wananchi, jiwekeeni utaratibu wa kuwatembelea ili mfahamu kero zao, msidhani mikutano ya mbunge pekee ndiyo njia ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi,” alisema.
 
Aliwataka viongozi hao kamwe wasibweteke wala kusuasua katika kufanya mikutano na kutembelea wananchi, ambao kimsingi ndio wanaowatumikia.
 
“Ndiyo maana tumewapa baiskeli makatibu watendaji wa Chama na UVCCM wa kila Kata ili ziwasaidie kuwafikia wananchi na wanachama kwa wakati muafaka, nao wana wajibu wa kuwatembelea wananchi na kukiimarisha Chama,” alisema Dk. Kamani.
 
Hivi karibuni, Mwenyekiti huyo wa Chama wa mkoa wa Simiyu alitoa baiskeli 39 zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 5.8 kwa wenyeviti na makatibu Kata wa CCM na Makatibu wa UVCCM kwa ajili ya kuwasaidia usafiri wa kuwafikia wanachama na wananchi kwa urahisi.
 
Awali, mwishoni mwa wiki, Dk Kamani alitembelea na kukagua ujenzi wa wodi ya Wazazi unaendelea katika Zahanati ya Kata ya Lamadi Kijijini Lukungu, inayojengwa kwa thamani ya sh. milioni 75 zilizotolewa na AMREF mkoani Simiyu, chini ya kampeni ya Uzazi-Uzima.
Mbunge wa Jimbo la Busega, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, akishuhudia maji yakitiririka baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kijiji cha Manala Kata ya Badugu wilayani Busega. Kulia ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Busega, Agatha Magonela.
 Dk. Titus Kamani, akimtwisha ndoo ya maji mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Manala, baada ya kufungua mradi huo.
 Dk. Kamani akikagua msingi wa Kituo cha kulelea walemavu wa ngozi (albino) kinachojegwa katika Kijiji cha Lukungu Lamadi wilayani humo, mbele yake ni Mratibu wa kituo hicho, Mudy Gimonge.
 Dk. Kamani akishiriki na baadhi ya wananchi wa Lukungu kusomba tofali za ujenzi wa kituo cha kulelea walemavu wa ngozi (albino).

WALIMU WANAOTAKIWA KUJIUNGA NA JKT WATAJWA

$
0
0
Hatimaye jeshi la kujenga taifa limetangaza majina ya walimu ambao wanatakiwa kupitia jkt kwa ajili ya mafunzo MAALUM kama ilivyo kwa kidato cha sita,yajulikanayo kama mafunzo kwa  mujibu wa sheria.


Walimu waliochaguliwa ni wa ngazi ya cheti ambao wamepangiwa vikosi vya kwenda.
Kuangalia majina hayo tafadhali BOFYA hapo chini;

TAARIFA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kukanusha habari zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa kesho Jumatatu Benki ya FBME itafungwa na shughuli zote za benki hiyo zitakuwa chini ya Benki Kuu.

Habari hizi si za kweli na kwamba benki hiyo haipo chini ya usimamizi wa Benki Kuu na itaendelea kutoa huduma kama kawaida.

IMETOLEWA NA
 IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI, BENKI KUU YA TANZANIA.

TIMBER LAND JOGGING AND SPORTS CLUB YOMBO KILAKALA WAFUTURISHA NA KUTOA VYAKULA KWA WATOTO YATIMA

$
0
0



TIMBER LAND JOGING AND SPORTS CLUB YOMBO KILAKALA.
Baadhi ya wtoto wakifuturu wakati wa futari iliyoandaliwa na klub ya jogging ya timber land iliyopo yombo kilakala
Baadhi ya kina mama na watoto nao wakipata futari
BAADHI YA WANACHAMA WANAWAKE WA KLUB YA TIMBER LAND YA YOMBO KILAKALA WAKIPATA FUTARI YA PAMOJA 
Mlezi wa klabu ya Timber land sports club ya yombo kilakala ,bi

Carren-Flora Mgonja wa pili kushoto akiwa na baadhi ya wanachama mara baada ya kumaliza futari

Mlezi wa klabu ya Timber land sports club ya yombo kilakala ,biCarren-Flora Mgonja  akizungumza wakati wa futari hiyo
Makamu Mwenyekiti wa Timber Land Chorai JAohn akizungumza
Kanali Mstaafu Iddi Kipinguakitoa nasaha zake


Diwani wa kata ya yombo kilakala bi, Elizabeth Magwaja akiongea

Balozi wa Palestina awaomba wanahabari Tanzania kupaza sauti

$
0
0
Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. 
 Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff akiwasilisha mada katika mkutano huo. 
Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff akiwasilisha mada katika mkutano huo.Sheikh Jalala (katikati) akizungumza katika mkutano huo. Sheikh Jalala (katikati) akizungumza katika mkutano huo.Meza kuu ikifuatilia majadiliano katika mkutano huo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. Meza kuu ikifuatilia majadiliano katika mkutano huo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina. Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina. Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.


BALOZI wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish amevitaka vyombo vya habari nchini Tanzania kusaidia kupaza sauti dhidi ya vitendo vya uonevu na mauaji yanayofanywa kwa raia wa Palestina na taifa la Israel ili vitendo hivyo vikomeshwe mara moja. 

Balozi Abu Jaish ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokutana na ubalozi huo kuzungumzia hali halisi ya mgogoro wa Palestina na taifa la Israel unaoendelea hadi sasa. "...Mi naomba waandishi wa habari Tanzania andikeni ukweli juu ya uonevu huu wanaofanyiwa raia wasio na hatia, sitaki muandike kwa kupotosha semeni ukweli ili umma ujue nini kinachoendelea kwa Wapalestina ndani ya taifa lao...," alisema Balozi Abu Jaish akizungumza na wahariri hao. 

Pamoja na hayo Balozi Abu Jaish aliiomba Tanzania na mataifa mengine yanayopenda amani kuungana kwa pamoja na kupaza sauti kukemea uonevu wanaofanyiwa raia wa Palestina ndani ya ardhi yao, kwani sauti za wengi zinaweza kukomesha hali hiyo na hatimaye mauaji kwa raia wasio na hatia kukoma mara moja. Aidha alisema kitendo cha taasisi za kimataifa kukaa kimya huku raia wasiokuwa na hatia wakionewa na wengine kupoteza maisha ni sawa na kubariki vitendo hivyo viendelee.

 "...Makosa yanayofanywa na taifa la Israel yanaweza kuwa ya ulimwengu mzima endapo tutaendelea kukaa kimya huku watu wakionewa na kuuwawa nchini mwao...kama kweli hatupendi haya yaendelee kwanini tunakaa kimya," alihoji Balozi Abu Jaish. Awali akiwasilisha mada kwa wahariri Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff alisema mgogoro wa Palestina na Israel unachochewa na ukandamizaji ulioanza kufanywa katika mgawanyo wa ardhi ya mataifa hayo tangu mwaka 1947. 

Alisema chanzo cha Tatizo la Palestina lilianza tangu mgawanyo wa ardhi kati ya Wayahudi na Waarabu; katika mgawanyo huo waarabu ambao walikuwa wengi walipewa sehemu ndogo ya ardhi huku Wayahudi ambao walikuwa ni wachache walipewa sehemu kubwa ya ardhi. Alisema mpango wa Mgao wa Palestina uliofanywa na Umoja wa Mataifa, UN mwaka 1947 uligawa nchi ya Warabu milioni 1.2 walipewa ardhi kwa asilimia 43, huku idadi ya Wayahudi milioni 0.6 wakipewa ardhi asilimia 56 mgao ambao haukuwa sawa kimtizamo.

 "...Israel ilipoiteka ardhi ya Kiarabu, pamoja na Palestina mwaka 1967, Baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere alikemeasema; “The establishment of the state of Israel was an act of aggression against the Arab people…Israel must evacuate the areas … - without exception- ...we cannot condone aggression on any pretext, nor accept victory in war as a justification for the exploitation of other lands, or government over other peoples.“Huu ndio uliokuwa msimamo wa TZ 1967. 

Tulivunja uhusiano na Israel, na tulikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuipokea ubalozi wa Palestina." Alisema Pref. Sheriff akihoji ukimya wa sasa. Waandaaji wa mkutano huo pia walitangaza kufanya maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Quds Duniani yanayotarajiwa kufanyika Julai 25, 2014; kwa Tanzania maandamano yataanzia Ilala Boma jijini Dar es Salaam kwenda Uwanja wa Kigogo na baadaye Karimjee ambapo kutakuwa na mada anuai.

AZANIA BANK LTD YAFUTURISHA WATEJA WAKE NA YATIMA KITUO CHA MITINDO HOUSE FOUNDATION

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Bwa.Singili alisema kuwa Benki ya Azania ni kama sehemu ya jamii, watajitahidi kutoa msaada kwa jamii katika Nyanja za elimu,afya na kusaidia yatima kila nafasi na uwezo unaporuhusu.Benki ya Azania pia iliwaalika Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa  benki ya Azania imekuwa sasa na kufikia matawi 15 ikilinganishwa na matawi matatu waliyokuwa  nayo mwaka 2007,alisema kwa Dar es salaam pekee wana jumla ya matawi 05. ''tunawashukuru wateja wetu,kwani bila uwepo wao tuingefika hapa,tunapenda kuwahakikishia kuwa tunaendelea na juhudi zetu za nia ya kutaka kuwa na teknolojia ilio sahihi'',alisema MKurugenzi huyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo pamoja na waalikwa wengine kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
 Afisa mkuu maendeleo ya biashara kutoka benki ya Azania,Bwa.Othman Jibrea akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
 Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania sambamba na wadau wengine wa benki hiyo,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
Sheikh Abdulrahman Ali Issa akitoa shukurani za dhati (kwa niaba ya sheikh wa Mkoa Dar Es Salaam),kwa uongozi wa benki ya Azania kwa kutoa mwaliko wa futari kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo watoto yatima kutoka kituo cha Mitindo House Foundation..
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakipakua ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
 Wageni waalikwa wa benki hiyo ya Azania wakiendelea kuchukua futari tayari kwa futuru.
 
 Mazungumzo ya hapa na pale yalikuwepo pia .

KOMWETA HEMED MANETI A.K.A CHIRIKU WA VIJANA JAZZ AFUATA NYAYO ZA MAREHEMU BABA YAKE HEMEDI MANETI ULAYA

$
0
0
1970462_1454799778083088_1638018053_n
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
1486871_1427285270834539_2027172492_n
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
......................................................................................................
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.
Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa (Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.
 
Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad. 

Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo.
 
hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi. Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa 

"Nashukuru Mungu sana kwa hilo na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..." Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".

Rais Kikwete akagua kilimo cha Kahawa Mbinga

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
 Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma

 Sehemu ya  Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma..(picha na Freddy Maro).

NAPE : CCM HAIKATAZI MWANACHAMA WAKE KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Channel 10.

Nape  alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema "Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda".

   Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
Chanzo: kamerayangublog.com

Anne Kansiime kuburudisha Dar August 2.

$
0
0
 Mkali wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki, Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kali hapo August 2, katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
                      
Tukio hilo linaloandaliwa na kituo cha Radio 5 litaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band, pamoja na mchekeshaji Fredi Omondi kutoka Kenya na Pilipili wa Tanzania.

Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis alisema kuwa wameamua kumualika Kansiime kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu katika uchekeshaji na ana mashabiki wengi Tanzania.  

“Kansiime ni mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa uwezo wake wa kuweka utani kwenye maisha ya kawaida’ alisema Francis.

Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

Burudani hii ya Kansiime, ambayo itakwenda kwa jina la Cheka Kwa Nguvu, itaanza saa moja usiku na tiketi zitauzwa shilingi elfu 90,000 kwa mtu mmoja, na shilingi 700,000 kwa meza ya watu nane. 

‘Kama ambavyo mwandishi wa vitabu, Maya Angelou alivyowahi kusema, “Simwamini mtu yeyote asiye cheka” tukio hili linalenga kuonesha umuhimu wa kucheka katika maisha yetu ya kila siku” alihitimisha Francis. 


TFF yaitaka Airtel kudhamini U-20

$
0
0
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Rebeca Mauma akizungumza wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya washiriki wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars wakifutilia kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisisitiza jambo wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiteta na Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo. 

==========   -==========  -========
Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Selestine Mwesigwa amesisitiza umuhimu wa programu za vijana kwa maendeleo ya soka nchini na kuitaka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuangalia uwezekano wa kuwa wadhamini wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20. 

Akifungua semina elekezi kwa makatibu wakuu wa mikoa inayoshiriki mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars (ARS) iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 19, 2014 Mwesigwa alisema hali halisi inaonyesha kwamba miaka michache ijayo wachezaji wengi watakaounda timu ya taifa ya U-20 watatokana na ARS hivyo ni vema kampuni ya Airtel ikawa mdhamini mkuu wa timu hiyo. 

Alisema kuwa suala la programu za vijana ni agenda namba moja ya TFF na kuzitaka timu za ligi kuu kuzingatia maagizo ya shirikisho hilo la kuwa na timu za vijana. “Klabu ya Simba imefanikiwa sana katika suala hili na ni vema timu nyingine za ligi kuu zikaiga mfano huo”, alisema Mwesigwa na kuipongeza Airtel kwa kuwekeza katika soka la vijana. 

“Wachezaji wanapolelewa na klabu tangu wakiwa wadogo inakuwa ni rahisi kwao kuendana na maadili ya klabu hiyvo kuwa na wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu tofauti na wachezaji waosajiliwa kutoka sehemu mbali mbali wakiwa na umri mkubwa”, alisema. 

Aliwataka makatibu hao wa mikoa kuzingatia kanuni ikiwa ni pamoja na umri ili kuwafanya vijana watakaoshiriki mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa na ushindani ulio sawa. Mashindano ya ARS yanashirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17. 

Mwesigwa aliungwa mkono na Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi aliyesema kuwa programu za vijana e.g. ARS ndiyo mkombozi wa kweli wa soka popete pale duniani. 
 
 Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa Julai 27 na kushirikisha mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ilala, Kinondoni na Temeke kwa upande wa wavulana huku timu za wasichana zikitoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Zanzibar, Ilala, Kinondoni na Temeke. 

Akiongea katika semina hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza viongozi wa mikoa kwa kazi nzuri iliyoiwezesha Tanzania kutwaa ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya ARS (wasichana) yaliyofanyika Nigeria na kuzawadiwa USD 10,000, medali na vikombe. 
“Vile vile timu ya wavulana ilifanya vizuri sana na ni imani yangu kwamba mwaka huu Tanzania itashinda vikombe kwa wasichana na wavulana”, alisema na kusisitiza nia thabiti ya Airtel kuendelea kuboresha mashindano hayo. 

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi aliwataka makatibu hao kufanyakazi kwa karibu na kamati ya vijana ya TFF inayosimamia mashindano hayo.

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YATANGAZWA, KUONA BOFYA LINK HAPO CHINI

1st DEATH ANNIVERSARY OF JOHN SHILATU

$
0
0

The late John Shilatu

It is exactly one year since you passed away, the way we miss you, and the way we remember you, the gap is clearly shown, we exactly know how much you meant to us. We still think about you everyday, we just love and miss you in our own special way.

Deeply missed by your Wife Bernadina; Your Children Benigna, Emmanuel, Geofrey, Gerald & Digna; your only grandson Jayden; Your Sisters Laura & Clara; Your Sisters inlaws, friends, neighbours, relatives and clans of Shilatu & Makere.

May GOD rest your soul in peace wherever you are. Deeply Missed John Shilatu.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images