Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Upendo Nkone kumsindikiza Rose Muhando

$
0
0

MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone ni miongoni mwa wasanii watakaosindikiza uzinduzi wa albamu ya Rose Muhando.Muhando anatarajia kuzindua albamu hiyo Agosti 3, mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuendelea katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba, Agosti 10.
 
 Akizungumza na gazeti hili,  Muhando alisema Nkone tayari amekubali kushiriki katika uzinduzi huo na ana matumaini litakuwa tamasha la aina yake.Nkone ametamba na albamu mbalimbali ikiwemo Mungu Baba, Hapa Nilipo, Zipo Faida na Uniongeze Yesu.

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

MHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI,MDAU DISMAS LYASSA ACHUKUA FOMU KOGOMBEA URAIS WA TUCTA

$
0
0
 Mhariri wa masuala ya Biashara wa gazeti la Mwananchi na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU-T) Tawi la Mwananchi Communications Limited, Dismas Lyassa (kulia) akirudisha fomu ya kugombea Urais  wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kwa Katibu Mkuu wa COTWU Kanda ya Dar es Salaam, Musa Mwakalinga, jana ofisini kwake (kwa Mwakalinga). Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 4-5, mwaka huu mkoani Dodoma. Picha na Khamis Tembo.

WATU NANE WAJERUHIWA VIBAYA NA BOMU JIJINI ARUSHA

$
0
0

 mmoja wa mtu alielipuliwa na bomu katika mgahawa wa
Traditional Indian Cusine aliyejukilana kwa jina la Deepak Gupta (25)
akiwa amelazwa  katika hospitali ya seliani ndani ya  chumba cha
mahututi (ICU) mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto
kutokana na mguu huo kuumizwa sana na bomu hilo.


 Mtoto   Manci  Gupta akiwa amelala anasikilizia maumivu ya miguu  aliyoumia mara baada ya kulipukiwa na bomu yeye na familia yao wakati wameenda kupata chakula cha usiku katika mgahawa huo
 mama Munisha Gupta (42) pamoja na mme wake Mahush
Gupta (42) akiwa wameegemeana wote wamezurika katika mlipuko wa bomu hilo wakati wameenda kupata chakula cha usiku
 picha ikionyesha askari wa jeshi la wananchi  kitengo cha mabom wakiwa
katika eneo la tukio ambalo bumu lilirushwa  ndani ya mgahawa wa
ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine  ulipo pembeni ya
hotel ya gmkana.
 muonekano wa eneo la tukio.


 SEHEMU ambayo inasemekana bomu  lilitua mara baada ya kutupwa.


Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza,Arusha.


Mlipuko unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha  katika mgahawa wa  Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane.

Akithibitisha kupokea wagonjwa walioathiriwa na bomu hilo,  Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga  alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na saatano .

Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.



"kati yawagonjwa hao nane,mmoja alikutwa akiwa mahututi ,kwani mguu wake ulikuwa umeathiriwa sana na bomu hilo ,ivyo ikatulazimu  kumkata mguu mmoja wa kushoto ,mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa  Deepak Gupta (25) mwanaume,na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupo katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani"alisema Kisanga



Alisema kuwa  katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari



Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na  Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25)  wote wakiwa na asili ya kiasia.
Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio  waliofika hapo hospitali walidai kuwa   bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.

WAZIRI WA UJENZI DKT MAGUFULI AZINDUA KIVUKO BUNDA-MARA

$
0
0
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA BUNDA NA MAJITA MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MWIBARA ALPHAXAD KANGI LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISHI MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIBONYEZA KITUFE CHA KIVUKO CHA MV MARA KUASHIRIA KUKIZINDUA RASMI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA NA MAJITA KATIKA WILAYA MBILI ZA BUNDA NA MUSOMA VIJIJINI.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAKIFURAHIA JAMBO NA MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA BALOZI HERBERT MRANGO HUKU MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO ALIYESSIMAMA KULIA NA MBUNGE WA MWIBARA KANGI LUGORA WAKWAANZA KUSHOTO WAKIANGALIA.

MFUMUKO WA BEI NCHINI UMEPUNGUA - OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kupungua kwa  mfumuko wa bei nchini.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini  kwa mwezi Juni 2014 umepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma za jamii katika maeneo mbalimbali.
 
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2014 umepungua na kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.5.
 
Amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi Juni 2014 imepungua ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Mei kutokana na hali ya kupungua kwa bei  kwenye  bidhaa na huduma
 
 Ameeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Juni umeongezeka hadi asilimia 8.5 kutoka asilimia 7.9 za mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi imeongezeka hadi asilimia 7.8 kutoka asilimia 7.2 za mwezi uliopita huku badiliko la fahirisi za bidhaa zisizo za vyakula likipungua hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Aprili 2014 kutoka asilimia 7.2 iliyokuwepo mwezi uliopita.
  
Kwa upande wa  mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi Bw. Kwesigabo amesema kuwa umepungua kwa asilimia 0.6 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.4 kama ilivyokuwa kwa mwezi Mei mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 148.98 kwa mwezi Juni 2014 kutoka 140.00 za mwezi Juni 2013.
 
Amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini  kuwa ni pamoja na mchele, mahindi,unga wa Muhogo, Viazi vitamu, dagaa, matunda jamii ya machungwa,mbogamboga na vitunguu maji.
 
Kuhusu mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula zinazotumika nyumbani na migahawani amefafanua kuwa kwa mwezi Juni umepungua hadi kufikia asilimia 8.7 kutoka asilimia 9.3
 
 Aidha, amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma  za jamii kutoka mwezi Septemba 2010 hadi Juni 2014 umeongezeka hadi shilingi 67 na senti 12 kutoka shilingi 66 na senti 72 za mwezi Mei mwaka huu.
 
“Kupungua kwa bei ya bidhaa kwa mwezi Juni kunamaanisha kwamba, uwezo wa fedha yetu umeongezeka,hii inamaanisha mfumuko wa bei unaposhuka, thamani ya shilingi nayo inapanda” Amesema.
 
Kuhusu ulinganifu  mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 7.39 kwa mwezi Juni 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.30 za mwezi Mei ,  huku  Uganda ikiwa na mfumuko wa asilimia 4.9 kwa mwezi huu ikilinganishwa na 5.4 za mwezi uliopita.

KILA LAKHERI WATU WANGU WA KAZI......!

$
0
0
'' Siku yangu ya kwanza katika ‪#‎BBCSwahili‬. Miongoni mwa walionipokea ni dada yangu Regina Mwalekwa. Hapa tukiwa na ndugu yetu Baruan Muhuza (kushoto). Picha nikiwa na wanafamilia wengine itafuata hivi punde.'',Si maneno yangu hayo,bali ni maneno murua kabisa kutoka kwa Mtangazaji mahiri niliyekuwa nikimfahamu kutoka Clouds FM,Arnold Kayanda.

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AZINDUA NEMBO MPYA YA AMREF HEALTH AFRICA TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania Dr. Festus Ilako (wa kwanza Kushoto) Akimkaribisha Waziri wa Afya Dr. Seleman Seif Rashid kuzindua Nembo Mpya.
Waziri wa Afya, Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya Amref Health Africa Mr. Omari Issa, Dr. Festus Ilako na wafanyakazi wa Amref Health Africa Tanzania katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi.
wadau na wageni waalikwa katika uzinduzi huo
Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau wa Amref Health Africa baada ya Uzinduzi.
SHIRIKA la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Afrika Medical and Research Foundation (Amref) limezindua rasmi jina na nembo yake mpya ambapo sasa litajulikana kama Amref Health Africa Tanzania.
Uzinduzi huo ulifanywa jijini Dar es Salaam Ijumaa ya tarehe 4/7/2014 na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid ambapo Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Festus Ilako, alisema imebidi kubadili jina na nembo yao ili kuendana na majukumu yao ya sasa ambayo yamekuwa ni zaidi ya utafiti na utoaji wa huduma za tiba.
“Kwa sasa tunajikita pia katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya, mafunzo, mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na mtoto, ukimwi, kifua kikuu, malaria, huduma za madaktari bingwa na maabara.“Mabadiliko ya jina na nembo yetu hayataathiri aina ya walengwa wetu wakuu; tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa,” alisema Dk. Ilako.
Alitoa mfano kuwa kila siku wanawake 22 wanapoteza maisha nchini wakati wa kujifungua na kwamba mpango wa Amref ni kupunguza vifo hivyo.Waziri Seif katika hotuba yake ya uzinduzi, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa taasisi hiyo na kwamba wamesaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, mimba za utotoni na upatikanaji wa majisafi na salama.

MBUNGE MAGIGE ALAANI VIKALI TUKIO LA BOMU ARUSHA

$
0
0
bom 1Mbunge viti maalum Mhe.Catherine Magige kupitia chama cha mapinduzi CCM akimjulia hali Deepak Gupta (25 aliyepoteza mguu wake ) mmoja wa majeruhi wa bomu lililolipuka jana usiku majira ya saa 4 usiku  katika mgahawa wa VAMA Traditional Indian Culture jijini A rusha na majeruhi hao  kukimbizwa katika hospital ya Selian
bom 2Mhe. Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mmoja wa majerui katika hospital ya Selian,kushoto ni Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali hiyo kulia ni Dk.Afizay Mkufya.
bom 4Mhe.Mbunge Catherine Magige akiangalia  kwa uchungu namna Deepak Gupta (25 )mmoja wa majeruhi katika bomu ambapo alipoteza mguu wake wa kushoto .
bom7
Mhe.Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mtoto Ridtwaik Lwal (13)aliyejeruhiwa mkononi kwa bomu

Mbunge wa viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh.Catherine Magige amelaani vikali  tukio la Bomu lililotokea katika mgahawa wa VAMA Tradition Indian Culture  jijini Arusha huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo

Mh.Magige aliyasema hayo leo katika hospitali ya Selian wakati alipowatembelea majeruhi nane Raia wa Asia waliolazwa katika hospitali hiyo ambapo wengi wa majeruhi waliumia katika maeneo ya miguu,mikono na tumboni hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi kupoteza mguu wake wa kushoto

Magige alisema kuwa kutokana na matukio ya aina hiyo kutokea kwa mfululizo, hali hiyo imesababisha jiji la Arusha kupoteza amani ili hali Tanzania ni Nchi ya Amani'

"Inasikitisha sana kwa kweli matukio kama haya kujirudia rudia inatia hofu sana kwa wakazi wa Arusha pamoa na wageni wanaokuja katika jiji letu"alisema

Aidha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo vya dola kufanikisha kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na matukio ya uvunjifu wa amani.(Pamela Mollel wa Jamiiblog)

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 25 ZA KUCHIMBA KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MAKUBURI, DAR

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni,Joseph Nicholous 9kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,  ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 ikiwa ni msaada uliotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati hiyo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya Makuburi.James Ngoitanile.
 Jengo la zahanati ya Makuburi
 Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni,viongozi na wahudumu wa zahanati hiyo pamoja na Wajumbe wa kamati ya maji ya mtaa huo Mwongozo wakifurahia kupata msaada huo kutoka TBL.

Wabongo wamtaka Rose Muhando amlete Rebecca Malope

$
0
0
MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando amesema mashabiki wengi nchini wameomba malkia wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, awepo kwenye uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Agosti 3, mwaka huu.

Uzinduzi huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali nchini wameshaalikwa kushiriki.

“Nimekuwa nikipokea simu nyingi za mashabiki wangu wakitaka nimualike Rebecca, najua kuna gharama zake kubwa, hivyo kwa kushirikiana na wasaidizi wangu tunalifanyia kazi.“Napenda mashabiki wangu wafurahi, lakini pia itategemea ratiba yake naye inasemaje, hivyo kazi kubwa itafanyika,” alisema Rose.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook. Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

DKT SHEIN AFUTARISHA WANANCHI KASKAZINI PEMBA

$
0
0
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) akiwakaribisha Mashekhe katika futari  aliyoiandaa kwa Wananchi  waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba huko Viwanja vya Ikulu ya Wete jana.
  Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na akinamama   na Viongozi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana.
  Baadhi ya  akinamama mbali mbali wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari aliyowandalia na Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana.
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (aliyesimama) alipokuwa akitoa shukurani pamoja na kuomba dua baada ya kumaliza kufutari wananchi waumini wa Dini ya kiislamu,futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana.
  Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiitikia Dua iliyoombwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiagana na  akinamama   mbali mbali na Viongozi waliohudhuria katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

RAIS KIKWETE ALIPOKABIDHIWA KITAMBULISHO NAMBA 1 CHA USHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA (DITF) KUTOKA MAXMALIPO .

$
0
0
Rais  Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akabidhiwa kitambulisho Maalumu cha kielektoniki kwaajili ya Kuingia katika Maonesho ya 38 ya biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kutika Kwa bwana Ahmed Lussasi Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo

Rais. Jakaya Mrisho alipata Nafasi ya kuzungumza na Maafisa wa Maxmalipo Juu ya Mfumo wa Kieletroniki wa Ticket (e-Ticketing System) uliofungwa na Maxmalipo Katika viwanja Vya Sabasaba. Pia Mheshimiwa Rais alijionea Jinsi Mfumo huu unavyodhibiti na kuboresha Ukusanyaji wa Mapato katika msimu huu wa Maonesho ya sabsaba. Mfumo huu wa kisasa pia Unauwezo wa kusimamia mapato katika nyanja mbalimbali kwa kutumia Barcode technology pia na Facial detection.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lusasi akifafanua Jambo kwa Mh. Dr. Jakaya Mrisho wakati alipo Tembelea Banda la Maxmalipo ndani ya Viwanja vya sabasaba.
 Mh.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (Rais) Akitizama kwa Umakini na kupata maelekezo Juu ya mfumo wa kielektoniki wa Ticket unavyotumika sabasaba na unavyowezakutumika sehemu Mbalimbali.

viwalo vipya vya Michuzi Media Group kutoka kitaa wear

$
0
0

 Baada ya kuvutiwa na ubunifu wa wajasiriamali vijana wa Kitanzania wanaokwenda kwa jina la KITAA WEAR Michuzi Media  Group chini ya Ankal imeona ni vyema kuwaunga mkono kwa kuweka oda kubwa ya T-shirts kwa ajili ya timu yake pamoja na wadau wa Globu ya Jamii na Michuzi TV. Wadau wengi wanavaa Kitaa Wear wakiwemo Diamond, Fid Q na mastaa wengine kibao. Kama umependezwa angalia maelezo hapo chini. Jamaa wako sharp na very professional. Siku nne tu mzigo tayari... KAZI KWAKO!

KITAA WEAR In Store Today
We got variety of T-Shirts its your choice
You choose we deliver 
Make your choice now and contact us:

WhatsApp / Viber: +255 754 310 202
BBM CHAT: 22696DDA
Skype: mwakatundu.m 
Twitter ; Mike_Tee1

Available colors for T-Shirts are (Brown,Black,Red,Blue and White)
Sizes Available ( Small, Medium,Large, Free Size, and Xtra Large)

KAMPUNI YA MEGATRADE YATOA MSAADA YA VYAKULA MASHULENI

$
0
0

CMeneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway kulia, akimkabidhi msaada wa vyakula  diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo kwaajili ya shule za msingi katika kata hiyo ambazo ni shule ambazo  zinaukosefu mkubwa wa chakula cha wanafunzi hali inayopeleka masomo kudorora na wanafunzi kuzimia ovyo kwa ajilii ya njaa mashuleni hali hiyo ilipelekea kampuni hiyo kujitolea msaada uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni moja,msaada huo ni Magunia ya mahindi,maharagwe na mafuta ya kula, jana jijini Arusha
DMeneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway kulia akimkabidhi gunia la maharagwe diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo jana jijini Arusha kwaajili ya shule za msingi katika kata hiyo,shule zilizonufaika na msaada huo ni shule ya Sokoni 1,Sinoni,Ukombozi,Engosengiu na Sinoni
BDiwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ukombozi Bi.Fatuma Mashombo gunia la mahindi kwaajili ya wanafunzi wa shule yake
ADiwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sinoni Bw.Eliud Mainoya gunia la mahindi kwaajili ya wanafunzi wake
FWanafunzi wakishusha magunia ya mahindi,wanafunzi hao walifurahia msaada huo kutoka kwa kampuni hiyo nakudai kuwa wataondokana na tatizo la njaa mashuleni na kuhaidi kuwa watafanya vyema katika masomo yao
GDiwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sinoni Bw.Eliud Mainoya gunia la maharagwe kwaajili ya wanafunzi wake
H
IDiwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sinoni Bw.Eliud Mainoya dumu la mafuta kwaajili ya wanafunzi wake
KDiwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ukombozi Bi.Fatuma Mashombo dumu la mafuta ya kula kwaajili ya wanafunzi wa shule yake(Pamela Mollel jamiiblog)

MBUNGE MAGIGE AHIDI KUWAINUA AKINAMAMA KIUCHUMI KUPITIA CATHERINE FOUNDATION

$
0
0
MA7Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha aliyevalia ushungi mweupe katikati Catherine Magige,akiwa na kikundi cha  akinamamalishe baada ya kuwawezesha vifaa vya upishi kwaajili ya kuendeleza biashara yao ya chakula katika eneo la kilombero jijini Arusha leo ambapo aliwawezesha wanawake wajasiliamili 150 wa jijini Arusha wanaojishughulisha na uuzaji wa mbogamboga,mama ntilie,machinga.
1.Wakina mama wakiwa wanamsikiliza Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha Mhe.Catherine Magige
2Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha Mhe.Catherine Magige akiwakabidhi kikundi cha akinamama kiasi cha shilingi laki mbili kwa kila kikundi ambapo alichangia jumla ya shilingi Milioni Moja na nusu kwa vikundi hivyo vya akina mama kwaajili ya kuwaezesha kuendeleza vikundi vyao vya vikoba.
3Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha  Mhe.Catherine Magige akiwa anamkabidhi mamantilie vyombo vya kuendeleleza biashara yao ya chakula katika eneo la kilombero jijini Arusha.
 
5
MA6Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha Ctherine Magige akiwa anaongea na akina mama wajasiriamali ambapo aliwachangia kikundi cha sombetini jijini Arusha shilingi Laki tano nakukubali kuwa mlezi wao
MA4Katibu wa mbunge huyo Lucy Bongole akiwa anazungumza na akinamama kabla ya zoezi kuanza
MA5Wanavikundi wakiwa wanasikiliza kwa makini
MA3
MA2
MA 1MA84Waandamizi katika pozi,Jamilah Omary wa chanel ten pamoja na devid Rwenyagira wa Redio 5
MA9MA10Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha aliyevalia ushungi Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya akina mama
MA 11
MA 12Muonekano katika soko la kilombero ambapo Mhe.Catherine Magige alikwenda kuwatembelea vikundi hivyo
MA13Picha ya pamoja na baadhi ya kikundi cha wamachinga na Mhe. Mbunge
MA14MA 15Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha Mhe.Catherine Magige akiongea na akinamama ntilie mara baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wanavikundi hao na kujionea namna wanavyoendesha biashara zao
 
MA 16Soko la kilombero jijini Arusha Mhe.Catherine Magige akiwatembelea wauzamatunda na mbogamboga
MA 18Kinamama wa soko la kilombero wakimsalimia Mhe.Catherine Magige mara alipofanya ziara ya kuwatembelea katika biashara zao za uuzaji wa mbogamboga

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Mhe Filipe Nyusi alipowasili leo jioni Julai 9, 2014, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania, kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.
Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana.

Rais Kikwete Ziarani Kilindi mkoani Tanga

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Pikipiki mmoja wa maafisa watendaji kata Wilaya ya Kilindi Bi.Elizabeth Mwita muda mfupi kabla ya Rais Kuhutubia Mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi jana.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kombe katibu wa TFF Wilaya ya Kilindi Bwana Omari Javu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songe Kilindi jana.Kombe hilo lijulikanalo kama Kikwete cup litashindaniwa katika ligi ya wilaya ambapo mshindi atakabidhiwa kombe hilo na zawadi nyinginezo .(picha na Freddy Maro). 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi Mkoani Tanga jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi mkoani Tanga.

MGOMBEA WA URAIS MSUMBIJI KWA TICKET YA FRELIMO ATUA NCHINI

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege ,jijini Dar es salaam.
  Katibu NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege ,jijini Dar es salaam.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusiakiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo atakuwa na ziara ya siku 4 nchini Tanzania.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusia akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana nyumbani kwa Mwalimu Nyerere ,Msasani Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani,jijini Dar es salaam.
 Mama Maria Nyerere akisalimiana na Samora Machel Jr nyumbani kwa Mama Maria Nyerere,Msasani Dar es Salaam.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akiondoka nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam baada ya kupita kumsalimia mara baada ya kuwasili nchini.(Picha na Adam Mzee).

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA BONDIA SADAT MIYEYUSHO KINONDONI DAR

$
0
0
Baadhi ya mabondia Makocha pamoja na wadau wa mchezo wa ngumi wakiungana pamoja wakati wa msiba wa bondia Sadat Miyeyusho aliezikwa leo katika makaburi ya FM Kinondoni Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia wa siku nyingi Koba Kimanga akiwa amemeba jeneza lenye mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho kwenda kuzika katika makaruri ya FM Kinondoni Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyeyusho wakiwa katika msiba wa bondia mwenzao Sadat Miyeyushopicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Ngumi Cristopher Mzazi akiwa kabebwa kwenye poikipiki tayali kwenda kuzika
Mamia ya waombelezaji wakiupereka mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho kuzika

Waombelezaji wakiwa wanazika mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho katika makaburi ya FM Kinondoni
Baadhi ya waombelezaji wakiwa makaburini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza katika maziko ya bondia Sadat Miyeyusho yaliyofanyika katika makaburi ya FM Kinondoni Dar es salaam ,bondia huyo aliefariki kwa ajali ya pikipiki juzi amezikwa jana katika makaburi hayo ya Kinondoni

Historia fupi ya marehemu inaonesha kuwa alianza ngumi mwaka  2006 ambapo mpambano wake wa kwanza katika ulimwengu wa masumbwi kacheza na Adam Yahya  na kushinda kwa point mpambao uliofanyika katika ukumbi wa  DDC Mlimani Parkmpambano wake wa mwisho katika maisha yake ya mchezo wa ngumi ni mwaka 2012 alipopambana na Issa Nampekecha katika ukumbi wa  Friends Corner Hall na kupoteza kwa pointbondia huyo ameshacheza na mabondia wanaotamba kwa sasa kama Ramadhani Shauli na Juma Fundi ambao alisha wai kuoneshana nao umwamba katika uringo


Bondia huyo ameacha mke na watoto
mungu awape subra familia ya marehemu pamoja wa wafiwa wote katika kipindi hiki cha msiba wa mpendwa wetu Sadat Miyeyusho
mbele yake nyuma yetu

Mahojiano na Mtunzi wa Vitabu vya Utaalamu wa Mapishi Benn Haidari, kutoka Stockholm nchini Finland.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images