Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 316 | 317 | (Page 318) | 319 | 320 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Watumishi wa TMAA wakiwa tayari kuwaelimisha na kuwahudumia wananchi waliotembelea Banda lao kwenye viwanja vya Saba Saba.

   Baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la TMAA wakishuhudia mchanga wa dhahabu uliokuwa ukioneshwa banda hapo.

  Na Saidi Mkabakuli
  Mamia ya wakazi ya jiji la Dar es Salaam na vitongoji vya wamejitokeza kujionea mchanga wa dhahabu unaoneshwa kwenye Banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Mmoja wa wakazi hao Bw. Shabaan Charahani, amesema ameshawishika kuja kujionea mchanga huo na kupata ukweli juu ya kutoroshwa kwa mchanga huo kama inavyovumishwa na watu wengi nchini. “Nimekuja kujifunza masuala ya ukaguzi wa madini na kujua ukweli juu ya mchanga wa dhahabu unaozalishwa hapa nchini,” alisema Bw. Charahani.

  Akitoa maelezo kwa wananchi hao waliojitokeza bandani hapo, Afisa Habari wa Wakala huo, Mhandisi Yisambi Shiwa alisema kuwa mchanga wa dhahabu ni zao lenye madini ya shaba na fedha lipatikanalo mara baada ya kuchenjua mawe yenye dhahabu kwenye mtambo wa kuchenjulia mawe hayo uliopo kwenye migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi.

  Aliongeza kuwa kuna mkanganyiko wa matumizi sahihi ya neno mchanga wa dhahabu, ambapo kiusahihi mchanga wa dhahabu ni makinikia ya shaba (copper concentrate). “Kutokana na madini ya shaba kuwa mengi kwenye huu ‘mchanga wa dhahabu’ kuliko madini mengine, jina rasmi linalotumika na kutambulisha zao hili ni makinikia ya shaba,” alifafanua.

  Kwa mujibu wa Mhandisi Shiwa, kwa sasa, uzalishaji wa makinikia ya shaba unafanyika katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi tu. Akiitaja sababu ya kuwepo na aina ya mashapo ya dhahabu ya migodi hiyo kuwa na sifa tofauti na migodi mingine mikubwa ya dhahabu hapa nchini.

  Akitaja sababu za kusafirishwa nje ya nchi mchanga huo, Mhandisi Shiwa kwamba kutokuwepo kwa teknolojia ya kutenganisha madini hayo, pamoja na gharama kubwa za kuendeshea mtambo wa kufanya kazi hiyo. “Gharama za mtambo wa kuchenjulia madini hayo ni wastani wa dola za kimarekani milioni 500. Gharama hizi ni kubwa ukilinganisha na hali halisi ya mapato ya migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi yatokanayo na ‘mchanga wa dhahabu’,” alisema Mhandisi Shiwa.

  Mhandisi Shiwa aliongeza, “kutokuwepo na umeme wa uhakika na uzalishaji duni wa makinikia hayo ndo sababu kuu za kutofanyika kwa kazi hiyo hapa nchini,” aliongeza. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kiasi cha makinikia kinachozalishwa hapa nchini ni wastani wa tani 45,000 ilhal kiasi kinachotakiwa ni wastani wa tani 150,000 za makinikia ya shaba.

  TMAA ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 362 la tarehe 6 Novemba, 2009. 

  Lengo la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni Mama Asha Bilal. Picha na OMR.
    Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe, Malawi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06,  2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake 
  Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06,  2014.


  ========  =========  =========

  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA MALAWI
  Julai 06, 2014 Lilongwe

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumapili Julai 06, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Malawi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Civo jijini Lilongwe.

  Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia alihudhuria Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Waziri Mkuu wa Msumbiji na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika.

  Sherehe hizo zilianza kwa ibada ya misa asubuhi na kisha kuhamia katika 
  uwanja wa Civo mchana ambapo Rais wa Malawi Prof. Athur Peter Mutharika  alikagua gwaride na kisha kuwasha Mwenye wa Jubilee ya miaka 50 na baadaye kulihutubia taifa.

  Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Mutharika alisisitiza kuhusu umuhimu wananchi wa Malawi kuwa wamoja na akaeleza nia yake ya kujenga umoja kwa nchi zinazoizunguka Malawi pamoja na zile za Kusini mwa Afrika. Baada ya  hotuba hiyo, sherehe hizo ziliendelea na mchezo wa soka baina ya timu ya taifa ya Malawi na Msumbiji.

  Malawi ilipata uhuru wake mwaka 1984 ikiongozwa na Rais wake wa kwanza Dkt. Kamuzu Banda hadi mwaka 1994. Baada ya mwaka huo alifuata Rais Dkt. Bakili Muluzi aliyetawala kuanzia mwaka 1994 hadi 2004. 

  Baaada ya mwaka huo alifuata Rais Profesa Bingu wa Mutharika aliyetawala hadi mauti yalipomkuta mwaka 2012. Dkt. Joyce Banda aliyekuwa Makamu wa Rais wa Mutharika alichukua madaraka na kukaa hadi mwaka huu 2014 ambapo Malawi iliingia katika uchaguzi mkuu na kisha Rais Profesa Arthur Peter Mutharika aliposhinda uchaguzi huo na hivyo kuwa Rais wa nne wa Malawi.

  Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim na Mheshimiwa Makamu wa Rais amerejea nyumbani Tanzania Julai 07, 2014 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Julai 06, 2014 Lilongwe: Malawi

  0 0

   Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda lao mapema leo ,kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam.
   Mama Mjasiliamali wa kampuni ya Tree of Life,Bi.Jessica Msamba akifafanua jambo kwa  Afisa Masoko wa Twiga Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard mapema leo mchana kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam.Bi Jesca ni mmoja wa wateja wakubwa wa benki hiyo na amekuwa akiendesha biashara zake za ujasiliamali kupitia mikopo mblimbali ya benki ya  Twiga Bancorp.
   Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa Twiga Bancorp,Bwa.Richard Kombole akielezea jambo kwa baadhi ya Wanahabari hawapo pichani,mapema leo kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam,waliotaka kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao,kulia ni Meneja wa Tawi wa benki hiyo Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Sigisbert  Komba na nyuma ni Msimamizi wa Usalama wa Majengo benki ya Twiga Bancorp.
   Afisa Masoko wa Twiga Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard akihojiwa na moja ya chombo cha habari,mapema leo mchana kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam,kuhusiana na huduma wazitoaza kwa wateja wao,Bwa.Adalbert amesema kuwa benki yao,Twiga Bancorp inatoa huduma mbalimbali kama vile Akaunti ya Akiba,Akaunti ya Biashara,Akaunti ya Amana,Huduma za Kibenki za Kimataifa,mikopo,utumiaji wa fedha na nje ya nchi,''Dira yetu kubwa ni kuwa taasisi ya kifedha inayoongoza kutoa huduma bora za kibenki nchini'',alisema Bwa.Adalbert.
   Baadhi ya Wateja walipatiwa vipeperushi vilivyosheheni huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo ya Twiga Bancorp.

  0 0  0 0

   Afisa uendeshaji wa Mfuko wa PPF kanda ya Ziwa, Bi Grace Balele akirufahia jambo pamoja na wateja waliofika katika Banda la PPF kwenye Maonyesho ya Sabasaba leo kwaajili ya kujipatia huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko huo wa Pensheni
    Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel  akimsikiliza kwa umakini wa hali ya juu mmoja wa wateja waliofika katika banda la PPF kwenye maonyesho ya sabasaba leo tarehe 7-7-2014 kwaajili ya kutaka kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko wa Pensheni wa PPF
   Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akiwahudumia kwa umakini wa hali ya juu wateja waliofika katika meza yake kwaajili ya kutaka kufahamu ni namna gani PPF inavyowekeza kwa kutumia michango ya wanachama wake
   
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba leo kwaajili ya kupata maelezo ya huduma mbalimbali za PPF na jinsi ya kuweza kujiunga na mfuko huo kwa wafanyakazi wasio katika sekta isiyo rasmi.
  Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye meza ya Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati walipotembelea banda la PPF kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo, Dr. Shukuru Kawambwa, jana Tarehe 7 July-2014, alitembelea maenesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE) , yajulikanayo kama maonesho ya Saba Saba, na kutembelea Banda la Shule ya Sekondari Imperial, Dr. Kawambwa ametoa pongezi kwa uongozi na waalimu wa Shule ya Sekondari Imperial, kwa Jinsi ilivyojipanga kuhakikisha inatoa Elimu Bora Nchini, inayokidhi viwango vya Kimataifa, kwa gharama nafuu.

  Shule ya Sekondari Imperial, iko Msolwa-Chalinze.

  Shule imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 27, lililopo Plot No. 1, Block C, Msolwa-Chalinze.

  Shule inafundisha na kutoa mtaala "Curriculum" wa hapa hapa nyumbani, yaani NECTA na Mtaala wa IGCSE "Cambridge Curriculum"
  Wanaopenda kujiunga au kuandikisha watoto wao kwa mwaka wa Taaluma unaanza Tarehe 5 Januari,-2015, fomu ni chache na zinapatikana kwa anuani zifuatazo:

  www.imperial.ac.tz principal@imperial.ac.tz 0758 50 51 52
  IMG_9373
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa akipokelewa na Mabalozi wa shule ya sekondari ya Imperial wakati alipowasili kwenye banda la shule hyo jana na kupata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo na waalimu.
  IMG_9377
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa akiingia katika banda la shule ya sekondari Imperial.
  IMG_9391
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa akisaini kitabu cha wageni wakati apotembelea banda la shule ya sekondari ya Imperial Kushoto ni Mama Iryna Kanyoko Mkuu wa shule hiyo.
  IMG_9406
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Imperial Mama Iryna Kanyoko alipotembelea katika banda lao kwenye viwanja vya Sabasaba
  IMG_9411
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Imperial Mama Iryna Kanyoko akimtambulisha Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa baadhi ya walimu wa shule hiyo.
  IMG_9445
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa akizungumza na baadhi ya wakuu wa idara za shule ya sekondari ya Imperial iliyoko Msolwa Chalinze mkoani Pwani.
  IMG_9472
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari ya Imperial Mama Iryna Kanyoko, kutoka kulia ni Mwalimu wa taaluma Bw. Juma na Dr. Mwingira Daktari wa shule ya sekondari Imperial.

  0 0

   
   Meneja wa Biashara Kubwa na Uwekezaji wa kibenki wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Justin Wambali (Kushoto) akiwaelezea wateja watarajiwa juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo walipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba. Wapili kushoto ni Afisa Mauzo, Irene Joachim na Afisa Uhusiano, Cosmas Nade (watatu kushoto).
  Meneja wa Biashara Kubwa na Uwekezaji wa kibenki wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Justin Wambali (Kushoto) akimpa maelezo mtoto, akiwa kama mmoja kati ya wateja watarajiwa juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo walipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba. Wapili kushoto ni Afisa Mauzo, Irene Joachim na Afisa Uhusiano, Cosmas Nade (watatu kushoto)
  Afisa Uhusiano wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Cosmas Nade akisambaza vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbali mbali zitolewazo na benki hiyo kwa wanafunzi waliopita katika banda la benki hiyo wakati wa maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam ya Saba Saba mwishoni mwa wiki

  0 0

  DSC_0772
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akipata maelezo ya sabuni mpya ya MO BEAUTY kutoka kwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi (kushoto) mara baada ya kuwasili katika banda hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.
  DSC_0784
  Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaabaadhi za Vitenge na Khanga (hazipo pichani) vinavyozalishwa na kiwanda cha 21st CENTURY Textile Ltd chini ya MeTL GROUP alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
  DSC_0050
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kushoto) akipewe maelezo ya ladha za aina tofauti za soda zinazotengenezwa na kampuni hiyo kutoka kwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi (wa pili kulia) kabla ya droo maalum kwa wateja wanaotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.
  DSC_0759
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akipata maelezo ya sabuni mbali mbali za unga kutoka kwa Mfanyakazi wa Royal Soap Detergent Industries, Aneth Masesa alipotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
  DSC_0797
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) akipata maelezo ya aina tofauti za kamba na magunia yanayotengenezwa na kampuni hiyo kutoka kwa Mtaalamu wa Mkonge wa MeTL GROUP, Bw. Iddi Omari (wa kwanza kulia) wakati alipotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
  DSC_0140
  Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Mrisho Millao (kushoto) akichanganya boksi lenye majina ya wateja waliotembelea Banda la kampuni ya MeTL GROUP na kujaza kuponi za kushiriki kwenye droo ya Bahati nasibu ambayo imechezeshwa jana kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia), Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi (wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
   
  MBU_2699
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza kwenye droo kubwa ya Kampuni ya MeTL GROUP kwa wateja waliokuwa wanatembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali na Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi.
  DSC_0111
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kulia) akimtangaza mshindi wa droo maalum kwa wateja wanaotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Na Mshindi huyo ameshinda Zawadi ya Pikipiki aina ya A1 ambayo imesajiliwa na seti mbili ya Vitenge,Wa kwanza kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu Bwana Mrisho Millao.Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi na Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (wa Kwanza kulia).
  DSC_0863
  Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna washindi kumi waliopatikana watakavyochukua zawadi zao mara baada ya kupigiwa simu na wahusika kwa ajili ya kukabidhiwa zawadi hizo.
  DSC_0191
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akipokea zawadi ya soda za MO Cola kutoka kwa Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi.
  DSC_0202
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiondoka kwenye banda la MeTL GROUP mara baada ya kumaliza shughuli ya kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa wateja wanaotembelea banda la MeTL Group kwenye maonesho hayo.
  DSC_0728
  Mtaalamu wa kutembea juu kamba nchini Hassan Mkenjula a.k.a SPIDERMAN akitoa burudani ya kupiga danadana kwa kutumia mdomo kwenye banda la MeTL GROUP.
  DSC_0552
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiwasili kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
  Na Mwandishi wetu
  Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ameipongeza makampuni yaliyochini ya Kundi la METL kwa kuhakikisha ajira kwa watanzania na soko la mali ghafi kwa wakulima wa bidhaa mbalimbali nchini.
  Silaa alisema hayo jana wakati alipotembelea banda la METL na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na makampuni yake mbalimbali zikiwemo bidhaa za michikichi na katani.
  Alisema kwa kutengeneza sabuni, mafuta na mali ghafi nyingine kutokana na michikichi kampuni za Metl zinawezesha wakulima kujiendeleza na pia kuwa na uhakika wa soko.
  METL yenye makampuni zaidi ya 25 sehemu kubwa ya bidhaa zake zinatokana na mali ghafi inayozalishwa nchini na nyingine ni zile zinazotumika kwa ajili ya wakulima kama matrekta.
  Aidha katika banda hilo kubwa ambapo kulijaa aina mbalimbali ya bidhaa kuanzia Sabuni,Vitenge, mafuta ya Mawese,vinywaji baridi, Matrekta na bidhaa za nyumbani, Mstahiki meya huyo alichezesha bahati nasibu za watu waliotembelea banda hilo.
  DSC_0556
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba mara baada ya kuwasili.
  Akizungumzia uwekezaji wa METL, Silaa alisema kwamba anafarijika na jinsi bidhaa za kampuni hizo zinavyoimarika ubora kila mwaka na kusema wakati umefika kwa serikali kuangalia wawekezaji wazawa.
  Alisema kwa maoni yake serikali ione jinsi ya kuwasaidia wawekezaji wanaoagiza mitambo toka nje ili kodi wanaoyotakiwa kulipa wailipe baada ya kuanza kazi za uzalishaji.
  “Hii itasaidia sana kuwa na wawekezaji wa ndani ambao wataweza kutoa huduma kama soko la mali ghjafi na pia kuongeza thamani ya bidhaa zinazoalishwa kutoka Tanzania” alisema silaa.
  Aidha Silaa alipongeza MeTL Group kwa kuweza kutoa ajira kwa watanzania wazawa huku bidhaa zake nyingi zikiwa kimbilio la watanzania wote, hasa wa kipato cha chini.
  DSC_0571
  Afisa Mwandamizi wa TANTRADE, Fidelis Mugenye, (kushoto) akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ratiba ya ziara kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho ya Sabasaba yanayokaribia kufikia ukingoni.
  “Naipongeza MeTL Group, kwa kuzalisha bidhaa bora ambazo ni kimbilio la wananchi wengi… hasa bidhaa zake za mafuta, sabuni, unga, vinywaji na bidhaa zingine kibao” alisema Silaa
  Pia aliipongeza MeTL kwa upande wa kutoa ajira na kukuza uchumi hapa nchini, ikiwemo kuzalisha bidhaa nyingi na zenye ubora ikiwemo za kamba ya mkonge ambayo alisema ni majibu ya utunzaji wa mazingira kutokana na vifungashio vya plastiki kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.
  Katika bahati nasibu iliyochezeshwa mkazi wa Kijitonyama Jijiji Dar es Salaam, Irene Manamba amejishindia zawadi ya pikipiki mpya.
  Aidha, katika droo hiyo, washindi wengine waliojishindia zawadi mbalimbali katika droo hiyo majina yao na wanakotoka ni Victoria Charles ambaye alikuwa mshindi wa pili mkazi wa Temeke, Julius Kamele (Tabata), Irene Mushi (Kijitonyama), Semi Anderson ((Dar es Salaam), Happyness Kalokola (Kitunda), Noel Kalenga (Sinza Kumekucha), Adam Mkwaya (Mabibo), Mery Msangi (Dar es Salaam) na Aisha Abeid (Tabata).
  DSC_0574
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ndani ya ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE.
  DSC_0604
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akiongozwa na vijana wa skauti kuelekea kwenye mabanda mbalimbali huku akiwa ameambatana na msaidizi wake Anthony William (kushoto).


  0 0

  Wafanyakazi wa shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao ndani ya  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
   Mmoja wa Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania,akimuelezea mmoja wa wateja wao aliefika kwenye banda lao kwa ajili ya kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo,kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam
   Wateja wakiendelea kudodosa mambo mbalimbali kuhusiana na huduma zitolewazo na shirika hilo hapa nchini
    Mmoja wa Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania,akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja wao aliefika kwenye banda lao kwa ajili ya kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo,kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam
  '' Karibu tena Mzee kwa huduma mbalimbali za Shirika la Posta'',ndivyo aonekanavyo akiambiwa na mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo

  0 0

  DSC_0017

  Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa mada inayohusu mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha matumizi rafiki ya huduma za kuzuia VVU na Huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana wakati warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU iliyofanyika hivi karibu katika kituo cha Habari na Mawasiliano Sengerema, Mwanza chini ya mradi wa SHUGA unaoendeshwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa UNICEF na UNESCO kwa kuzishirikisha redio jamii nchini.

  Na Mwandishi wetu Sengerema
  Licha ya jitihada za serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kupambana na mambukizi ya Virusi Vya Ukimwi hapa nchini, baadhi ya madhehebu ya dini nchini yameelezwa kuchangia kukwamisha juhudi hizo kutokana na imani zao .

  Hayo yameelezwa na washiriki wa mafunzo ya siku tatu kwa vyombo vya habari vya jamii Tanzania juu ya kuendesha mradi mpya wa SHUGA unaolenga kutumia vyombo vya habari kutoa elimu na hamasa kwa vijana kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

  Washiriki hao kutoka redio mbalimbali za jamii hapa nchini wamesema kuwa kumekuwa na baadhi ya viongozi wa dini ambao kwa namna moja au nyingine hawakubaliani na matumizi ya kondomu kama njia sahihi ya kuzuia sio tu maambukizi ya VVU bali pia magonjwa ya ngono na kama njia ya mpango wa uzazi kutokana na itikadi zao kidini kwa kile wanachokiita kuzuia mimba ni dhambi.
  DSC_0025
  Pichani juu na chini ni Baadhi ya waandishi wa Habari na Mameneja kutoka vituo mbalimbali vya redio za jamii walioshiriki warsha hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasishwa kwenye warsha hiyo.
   
  Yamekuwepo pia madhehebu mengine ambayo yamediriki kuzuia watu wanaoishi na VVU kuachana na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU na badala yake maombi ndio njia pekee ya uponyaji jambo ambalo linaonekana kuwa imani potofu kwa sababu ya kuchanganya imani na utaalamu wa kisayansi uliofanyiwa utafiti wa kina na sahihi.
  Matokeo yaliyotajwa na washiriki baada ya ushawishi huo wa imani za kidini kwa watu wanaoishi na VVU kuacha matumizi ya dawa zenye kupunguza makali ya virusi ni kudhoofika kwa haraka, kushambuliwa na magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na ukosefu wa kinga mwilini na hatimaye kufa.
  “Dini ina nguvu kubwa katika kukuza maadili ya kawaida hasa juu ya heshima na utakatifu wa maisha ya binadamu, upendo, huruma na uvumilivu na ina mengi ya kuchangia katika mapambano dhidi ya VVU / UKIMWI hususan huduma za kujitolea na kutoa sadaka kuwasaidia waliopatwa na maambukizi na walioathirika, kuhamasisha watu na makundi mbalimbali kwa kutumia maeneo ya maombi na kuchangisha rasilimali kwa ajili ya kuwajengea vituo vya malezi watoto, wagane na wajane ni muhimu kwa waandishi wa habari kuzitangaza na kuzipa umuhimu wake”.
  DSC_0040 
  Majadiliano hayo yalitokea baada ya mwezeshaji Bi Rose Haji Mwalimu kuwasilisha mada yake iliyohusu ‘Mchango Wa Vyombo Vya Habari Katika Kuhamasisha Matumizi Rafiki Ya Huduma Za Kuzuia Maambukiziya VVU,’ na kusisitiza kwamba hadi sasa bado hakuna chanjo wala tiba sahihi kutibu VVU na UKIMWI. Njia sahihi ni kuzingatia na kufuata maagizo ya kitaalam katika kuthibiti na kupunguza maambukizi mapya hasa kwa vijana hususan matumizi ya kondomu.

  Wakati huo huo waandishi wa habari wamehimizwa kuzingatia maadili na lugha mahsusi katika kuandika habari zinazohusiana na VVU pamoja na watu wanaoishi na VVU na kuacha kuandika habari ambazo zina mwanga mdogo, ni za mfumodume, kejeli, na zinakosa ujumbe mpya.
    DSC_0022 Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akiendelea kuwapiga msasa Mameneja na waandishi wa Habari kutoka redio za jamii zinazoshiriki mradi mpya wa SHUGA.
  “Kuna changamoto kubwa katika kuandika na kutayarisha vipindi vya VVU kwa sababu mara nyingi lugha zinazotumika katika taarifa au zinanyanyapaa, kubagua, kuhukumu na kulaumu, vyombo vya habari havitendi haki”, alisema Bi Rose Haji Mwalimu ambaye ni Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii nchini kutoka UNESCO katika warsha hiyo.
  Warsha hiyo ya siku tatu imefanyika katika kituo cha Habari na Mawasiliano Sengerema, Mwanza chini ya mradi wa SHUGA unaoendeshwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa UNICEF na UNESCO kwa kuzishirikisha redio jamii nchini.
  DSC_0152 Mshiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA kutoka Sengerema FM Redio, Peter Marlesa (kushoto) na Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu wakifutilia kwa umakini kazi zilizokuwa zikiwasilishwa na vikundi kazi. DSC_0165
  Mmoja wa washiriki kutoka redio ya jamii FADECO ya wilayani Karagwe mkoani Kagera akiwasilisha kazi ya kikundi chake ya kutengeneza jedwali la Message Matrix mbele ya washiriki wenzake.
  DSC_0030
  Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akifuatilia jambo kwa umakini wakati wa warsha hiyo.
  DSC_0300
  Meneja wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa (kulia) akimshukuru Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu kwa kuwapiga msasa kupitia mradi wa SHUGA unaolenga kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU mara baada ya warsha hiyo ya siku tatu.

  0 0

   Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) Bw. Harbinder Singh Sethi (wa pili kulia) akimwonyesha kitu Fadha Gerald Kamina (wa pili kushoto) mara baada ya kukabidhi hundi ya Shilingi milioni 14.5 kama msaada kwa jumuiya ya Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Kushoto ni Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo na kulia ni Rajiv Bhesania, msaidizi wa Mwenyekiti mtendaji wa IPTL.
   Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) Bw. Harbinder Singh Sethi (wa pili kulia) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 14.5 kwa Fadha Gerald Kamina (wa tatu kilia), kama msaada kwa jumuiya ya Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Pamoja nao ni Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo (wa tatu kushoto), Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL Bw. Joseph Makandege (wa pili kushoto), Mwanasheria wa IPTL Melchisedeck Lutema (wa kwanza kushoto) na wa kwanza kulia ni Rajiv Bhesania, msaidizi wa Mwenyekiti mtendaji wa IPTL.
  Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL Bw. Joseph Makandege (wa pili kushoto),  akimpongeza Fadha Gerald Kamina (wa tatu kilia), mara baada ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL Bw. Harbinder Singh Sethi (wa pili kulia) kukabidhi hundi ya shilingi milioni 14.5 kama msaada kwa jumuiya ya Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Pamoja nao ni Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo (wa tatu  kushoto), Mwanasheria wa IPTL Melchisedeck Lutema (wa kwanza kushoto) na wa kwanza kulia ni Rajiv Bhesania, msaidizi wa Mwenyekiti mtendaji wa IPTL.

  =========   ======  =======   =====


  KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imetoa msaada wa shilingi milioni 14.5 kwa jumuiya ya Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo.


  Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi kwa jumuiya hiyo, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Bw. Harbinder Singh Sethi alisema kuwa IPTL imetoa msaada huo ili kusaidia katika ujenzi wa Kanisa hiyo ya Mtakatifu Petro.   


  “Hizi milioni 14.5 tulizotoa kwa Kanisa la Mtakatifu Petro, ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kuwezesha miradi mbali mbali za kijamii ambazo zinagusa maisha ya watu wengi. Tuna imani kwamba kwa kuchangia fedha hizi zitasaidia kusukuma mbele ujenzi wa kanisa hili ili liweze kukamilika mapema na kutumika kwa ajili ya ibada. 


  “Jitihada hizi ni moja kati ya mkakati wetu wa utekelezaji wa mpango wetu wa kutumia sehemu ya faida tunayopata kutokana na shuguli zetu, kwa kuiwezesha jamii katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo kiuchumi. Misaada kama haya hayalengi tu kusaidia vijana wa kitanzania kuendelea kiuchumi lakini pia misaada kwa taasisi za kidini itasaidia katika kujenga jamii inayo mcha Mungu na hivyo taifa kuwa katika mazingia mazuri ya kupiga hatua kubwa kimaendeleo,” alisema Sethi. 


  Bw. Sethi alisema kuwa kampuni yake ina mpango madhubuti unaolenga kusaidia mashule, makanisa, misikiti na mashirika mengine yasiyoyakibiashara yanayofanyakazi ili kuwawezesha vijana kuwa wachangiaji wakubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi Tanzania. 


  Naye Katibu na Mshauri Mkuu wa IPTL, Bw. Joseph Makandege alisema kuwa IPTL ikiwa na mpango wake wa kuunga mkono jitihada mbali mbali za kimaendeleo na kijamii, itaendelea kushirikiana na jumuiya mbali mbali ili kwa pamoja kuona kwamba fursa mbali mbali za kiuchumi zinazojitokeza zinapewa msukumo kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwa ujumla. 


  “Kama IPTL, tumeona kuwa ni jukumu letu kuisaidia jamii inayotuzunguka. Nina imani mchango wetu kwa Jumuiya ya Mtakatifu Petro leo hii utasaidia kuongezea nguvu ujenzi wa Kanisa unaoendelea. Lengo letu ni kuona kwamba tunachangia maendeleo ya kiuchumi lakini pia bila kusahau jamii yetu inayotuzunguka zikiwepo jumuiya mbali mbali za kidini,” alisema Bw. Makandege.  


  Kwa upande wake, Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, aliishukuru IPTL kwa msaada wake na kusema kuwa fedha iliyotolewa itasaidia kwa kiasi kikubwa kusukuma mbele ujenzi wa kanisa hilo ambao bajeti yake ni zaidi ya shilingi milioni 600. 


  “Naishukuru IPTL kwa kuona umuhimu wa kukubali ombi letu na kuja kutuunga mkono katika jitihada za ujenzi wa kanisa letu. Fedha hizi zitasaidia kusukuma mbele zaidi ujenzi wa kanisa letu, huu ni mfano mzuri wa kuigwa na makampuni mengine na watu binafsi,” alisema Bi. Rupia.

  0 0

  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (MP) welcomes Prince Akishino and his wife Princess Kito from Japan at Manyara Airstrip ready for their visit to Ngorongoro Crater and Serengeti National Park over the weekend.
  Princess Kito of Japan receives a bouquet of flower from Ms. Lilian Sukhe of Tanzania Tourist Board during their arrival at Manyara Airstrip ready for their visit to Ngorongoro Crater and Serengeti National Park over the weekend.
  Maasai Cultural Troupe entertains Prince Akishino and his wife Princess Kito when they arrived at Loduare Gate, Ngorongorto Conservation Area.
  Prince Akishino and his wife Princess Kito making a short walk in the plains of the Serengeti National Park.
  Prince Akishino and his wife Princess Kito pose for a picture in the Serengeti National Park.
  Prince Akishino was also good in taking pictures from his personal camera.
  The couple enjoying hippo pool in the Serengeti National Park.
  Taking a closer shot!
  Acting Mara Regional Commissioner Angelina Mabula presenting an elephant carving to Prince Akishino soon before their departure at Serengeti National Park.

  0 0

    Pichani ni Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana jijini Arusha,aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa watu nane wamejeruhiwa vibaya na mlipuko huo .
   Picha ni majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25),akiwa amelazwa katika hospitali ya Selian,katika chumba cha watu mahututi (ICU),mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mhuu huo kujeruhiwa vibaya na bomu.
   Sehemu ya baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Selian,jijini Arusha kwa matibabu.


  0 0

  DSC_0401
  Watoto wa shule ya Ojays Kiddies Zone iliyopo maeneo ya Kinondoni Block 41, wakiwa kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kuanza kwa mahafali ya Kaka na Dada zao wa Laura Class kuanzia miaka 4-5 (T-shrits za kijani) yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Regency Park jijini Dar mwishoni mwa juma.
  DSC_0406
  We are happy to Graduate....! Wanafunzi wa Laura Class wakipata Ukodak.
  DSC_0640
  Mkurugenzi wa Shule yaawali ya Ojays Kiddies Zone iliyopo Kinondoni -Block 41, Bi. Debbie Ndulla akiwakaribisha walezi/wazazi na wageni waalikwa kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
  DSC_0434
  Baadhi ya walimu wa madarasa wakitambulishwa kwa wazazi kwenye mahafali hayo.
  DSC_0484
  Walimu na wanafunzi wa Ojay Kiddies Zone wakitoa burudani kwa wazazi/walezi na waalikwa kwenye sherehe za mahafali hayo.
  DSC_0723
  Wazazi/walezi wakichukua Ukodak wa watoto wao kwenye mahaali hayo.
  DSC_0494
  Darasa la awali la Lilies Class wa miaka 1-2 wakitoa burudani ya kuimba kwa wazazi/walezi na wageni waalikwa kwenye mahafali ya kaka na dada zao.
  DSC_0595
  Mwenyekiti wa Bodi wa shule ya Ojays Kiddies Zone, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wazazi/walezi kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo ambapo aliwashukuru wazazi kwa kuonyesha kuwaamini na kuwapa fursa watoto wao kusoma kwenye shule hiyo yenye maadali bora na kuzingatia ustawi wa mtoto pindi awapo katika mazingira ya shule.
  DSC_0623
  Mwanaharakati wa Haki za Watoto, Zubeida Masabo akitoa nasaha kwa wazazi/walezi juu ya kuwalinda na haki za msingi ambapo aliwaasa kutenga muda wa kufuatilia maendeleo ya mtoto kila siku, amewashauri wazazi kuwa na taratibu za kutenga muda wa jioni kuzungumza na watoto wao kutokana kukithiri vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hali itakayosaidia kubaini vitendo vya uovu.
  DSC_0619
  Mmoja wa wazazi Dr. Isaac Maro akifafanua jambo kwa wazazi/walezi likiwemo suala la afya kwa watoto hasa magonjwa ambukizi kama Tetekuangua (chicken pox) ambapo wazazi wengi wamekuwa na hofu endapo kunatokea mlipuko wa ugonjwa huo kwenye mazingira ya shule wasihofu na kushauri watoto kuendelea kuhudhuria masomo kwani wakiumwa utotoni ni nafuu zaidi kutibika kuliko kuugua ukubwani.
  DSC_0502
  Watoto wa Lantana Class kuanzia miaka 3-4 wa shule ya awali ya Ojays Kiddies Zone wakijitambulisha mbele ya wazazi/walezi kwenye mahafali hayo.
  DSC_0534
  Kwa picha zaidi bofya hapa

  0 0

  Mijadala ihusuyo maswala ya usalama mtandao imeendelea katka ngazi mbali mbali. July 6 ya Mwaka huu wa 2014 Yusuph Kileo alipata kushiriki na wataalam wengine wa ndani kujadili maswala mbali mbali yahusuyo usalama mtandao nchini.
   Mjadala ulihusisha mkusanyiko wa taarifa mbali mbali za kiusalama mitandao kutoka katika mataifa mengine pamoja na mwelekeo wa kukabiliana na uhalifu mtandao katika mataifa mbali mbali Duniani.

  Kipindi kilihusisha wageni walio alikwa Katika studio pamoja na mjumuisho wa simu kutoka kwa wasikilizaji ili kupata mawazo mchanganyiko yahusuyo maswala ya usalama mtandao. Kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio kilikua na lengo la kutoa elimu kwa umma, hali halisi ya uhalifu wa kimtandao duniani ilivyo na hapa nchini Tanzania.
  Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na hali halisi ya uhalifu mtandao ambapo takwimu na baadhi ya makosa mapya ya kimtandao yalipata kujadiliwa.  Mifano, uhalifu mtandao unaoweza kutoa fursa ya kuua mtu kwa msaada wa mtandao bila ya kuwa karibu na mlengwa pamoja na makosa mengine yalipata kuangaliwa kwa karibu.
  Aidha, paligusiwa namna ambavyo sheria za mtandao na uhalifu wa kimtandao zilivyo hivi sasa nchini Tanzania na faida zake endapo zitaanza kutumika rasmi. Maswala makubwa matano ambayo yanategemewa kupewa nguvu katika mataifa mbali mbali ili kupunguza uhalifu mtandao pia yalijadiliwa.

  Maswala hayo ni pamoja na elimu ya ulewa kwa wananchi ( awareness), Kupatikana kwa sharia madhubuti zitakazoweza kuto uwezo wa kuwadhibiti wahalifu katika mataifa mbali mbali, Kujengea uwezo wa wataalam wa ndani katika maswala ya usalama mitandao, Kuwa na framework ya pamoja kama bara ( Bara Ulaya tayari limesha fanyia kazi hili) pamoja na uwazi wa takwimu za uhalifu mtandao katika ngazi za kitaifa ili kuwezesha wataalam kugundua maeneo hatarishi zaidi na hatimae kuunganisha nguvu kudhibiti maeneo hayo hatarishi.

  Pakizingatiwa, kundi kubwa la watu ni la vijana kati ya Umri wa miaka 15 hadi 30 na vijana hao ndio wanao onekana kuathiri zaidi mitandao (Uhalifu matandao) pamoja na aina nyingine za uhalifu. pameendelea kuwa na mbinu mbali mbali zenye malengo ya kuwawajibisha vijana ili kupunguza uhalifu ikiwa ni pamoja na uhalifu mtandao.
  Jitihada hizo ni pamoja na za wakala wa umoja wa mataifa inayojihusisha na maswala ya teknohama (ITU) kupitia Young innovators ambapo Yusuph kileo aliteuliwa kuwa miongoni mwa mabalozi wapya anaetegemewa kuungana na wengine wote wakiwa na malengo ya kuwashughulisha vijana kifikra kutoka maeneo yote duniani.
  Vijana wanashirikishwa katika kubuni maswala mbali mbali yahusuyo Teknohama ambapo zawadi za fedha taslim pamoja na kuwezeshwa kufanikisha kilicho buniwa kuingia katika uhalisia ni miongoni mwa faida zinazo patikana.
  Wito umetolewa kwa vijana wa kitanzania kuchangamkia fursa hii hasa ukizingatia Mtanzania (Yusuph kileo) ni miongoni mwa mabalozi katika hili. Kwakushiriki kwenye hili patawezesha vijana wa kitanzania kuweza kutambulika zaidi uwezo wao na kupeperusha bendera yataifa kimataifa pamoja na kujumuika na vijana wengine kutoka maeneoo mbali mbali (Network building).
  Ilikupata Kuona na kujua zaidi juu ya shindano linaloendelea chini ya mpango huu wa Young innovators iliyo chini ya wakala wa umoja wa mataifa inayo jihusisha na maswala ya teknohama (ITU) tembelea "HAPA"
  Walio shiriki katika mjadala uliohusisha maswala ya usalama mitandao ni pamoja na Yusuph Kileo,Josephine Safiel,Kevin Chungu,Mahadhi Juma na Mtangazaji Maduhu wa Morning Star Radio.

  0 0

    "MUZIKI WA DANSI " NI SALIMALI INAYOPENDWA KIMATAIFA

  TFF Rudolstadt 2014 kwawashwa Moto na muziki wa dansi kutoka Tanzania
  tarehe 4 Julai 2014

  Muziki wa dansi wa Tanzania umezidi kufungua ukurusa mpya katka tufe la dunia,baada ya wasananii na wanamuziki wa Tanzania kutumbuiza katika onyesho la TFF Rudolstadt 2014,yaliofanyika kuanzia tarehe 3 adi 6 Julai 2014 mjini Rudolstadt,Ujerumani,ambako vikundi mbali mbali vya sanaa na bendi za muziki kutoka Tanzania zilishiriki,zikiwemo bendi ya Black Warriors ikiwashirikisha jukwaani na wakongwe wa muziki akina Mafumu Bilal,Hassan Bichuka,Cosmas Chidumule na wengine,pia Mchiriku ulikuwapo,bila kukosa Kikundi cha ngoma ya Kaya Baikoko kutoka mkoani Tanga, kikundi cha Qwasida ".
   
  Tarbiyya Islamiyya" kutoka Zanzibar, Kikundi cha kinamama cha Ngoma za Wagogo kutoka Dodoma, Mambo moto moto band na Segere lao walikuwapo  hayo yote yalikuwa mjini Rudolstad, nchini Ujerumani nchi ambayo ndipo makao makuu ya "FFU-Ughaibuni".

   

  0 0

   Mwana wa mfalme wa Japan Prince Fumihito Akishino na mkewe Kiko, wakifurahia ngoma za makabila la Wadatoga (Barbaig) na ile ya Wamasai, katika eneo la mlango wa Loduare kwenye hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro, pamoja nao wapo pia maafisa wa mamlaka hiyo, Bruno Kawasange na Adam Akyoo pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu, Felix Daudi Ntibenda.
   wakiwa wanafurahia ngoma za wamasai pamoja na wabarabaigi
   Katika picha nyingine Mwana huyo wa mfalme wa Japan akipewa maelezo kuhusu shughuli za uhifadhi ndani ya mamlaka hiyo katika kutuo cha habari cha Loduare Gate


  0 0

  Ndugu wanajumuiya, mabibi na mabwana.
  Familia ya marehemu (Bondia)  Iraki Hudu,inapenda kuwajulisha maadhimisho ya arobaini ya marehemu Iraq Hudu itayofanyika siku ya 19 Julai 2014 Shughuli hii itafanyika jioni
  wakati kufutari nyumbani kwa marehem huko Buguruni ,Rozana,Dar-es-salaam .

  Shughuli hii ya arobaini kwa kuwa imengia katika mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan,familia ya marehem imeamua kutimiza shughuli hii kwa kufuturisha na
  kisomo.

   Kwa heshima na taazima tunawaomba ndugu na jamaaa wote kushiriki katika shughuli hii. Marehemu Iraq, alitutoka tarehe 13.Juni 2014 na kuzikwa siku ya 14.Juni 2014 .
   
  Hivyo hatunabudi kutekeleza wito huu wa kuadhimisha siku ya kisomo chake. Kwa maelezo na habari zaidi, unaweza kuwasiliana na ndugu (Mtoto) wa marehemu kupitia simu hii 0717795070  kwa wanaopiga kutoka nje ya nchi +255 717795070
  Asanteni sana.
   
  Wenu, mwakilishi wa familia ya marehemu  Dani Huddu.

  0 0

  SEMINA    SEMINA   SEMINA  !!!
  Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia MRADI  WA  WANAWAKE  SALAMA  TANZANIA  inapenda  kuwaalika  wanawake  wote  waishio  jijini  Dar  Es  salaam  kushiriki  katika   SEMINA  YA  UTENGENEZAJI  WA  VYAKULA –LISHE.

  Mafunzo  yatakayo  tolewa  katika  semina  hii, ni  pamoja  na  UANDAAJI, UTENGENEZAJI  NA  UTAYARISHAJI  WA  VYAKULA-LISHE  MAALUMU  KWA  WAGONJWA  NA  WATU  WANAO  SUMBULIWA  NA  MATATIZO  MBALIMBALI  YA  KIAFYA.

  Washiriki  wa  semina  hii  watasaidiwa  kuanzisha  na  kuendesha  biashara  ya  kutoa  huduma  ya  vyakula –lishe  kwa  watu  wanao  sumbuliwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  waliopo  katika  maeneo  mbalimbali  jijini  Dar  Es  salaam.

  Vile  vile, wataingizwa  katika  MTANDAO  WA WATOA  HUDUMA  YA  VYAKULA-  LISHE TANZANIA.

  ADA  YA  KUSHIRIKI : Ada  ya  kushiriki  katika  semina  hii  ni  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU ( Tshs.15,000/=).

  TAREHE   YA KUFANYIKA   KWA SEMINA :
  Semina  hii  itafanyika  siku  ya  Alhamisi  ya  tarehe  31  JULY  2014  kuanzia  saa  4  kamili  asubuhi  katika  ukumbi  wa  SINZA  CHRISTIAN  CENTRE  uliopo  katika  eneo  la  SINZA  PALESTINA, JIJINI  DAR  ES  SALAAM.

  JINSI  YA  KUJIANDIKISHA  :
  Kujiandikisha  katika  semina  hii, fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.
  JINSI  YA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
  Kufika  ofisini kwetu, panda  daladala  za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kwenye  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  RAEFO  TANZANIA.
  Kwa  maelezo  zaidi wasiliana  nasi  kwa  simu 0784406508

  0 0

   Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni, Lulu Mengele (kushoto) akimkaribisha Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji, Mh Dodorius Kamala (kulia) wakati alipotembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayomalizika hivi leo.
   Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji, Mh Kamala juu ya wanachama wanavyonufaika na mafao wakati wanapostaafu kazini, Wa kwanza Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko, Lulu Mengele
  Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akimpa maelekezo Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji, Mh Kamala namna PPF wanavyotumia michango ya Wanachama wao katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ambayo baadhi ya miradi hiyo tayari ishaanza kufanya kazi.
  Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji, Mh D.Kamala akiagana na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele mara baada ya kumaliza kutembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayomalizika hivi leo.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

older | 1 | .... | 316 | 317 | (Page 318) | 319 | 320 | .... | 1897 | newer