Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

Kinana azungumza na Filipe nyusi

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi kwenye hotel ya Golden Tulip ambapo alikuwa na mazungumzo naye .
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, kabla ya kuanza mazungumzo kwenye hoteli ya Golden Tulip.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu mahusiano yao na CCM pamoja na namna Demokrasia inavyoendeshwa nchini Msumbiji,Mheshimiwa Nyusi alisema mahusiano yao na CCM ni mazuri na ya kihistoria Tangia wakati wa mapambano ya Ukombozi,alipoulizwa kuhusu uwezo wake wa kuongea Kiswahili vizuri alisema wakati wa mapambano ya Ukombozi aliwahi ishi Tunduru na Nachingwea nchini Tanzania.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa Chama Cha Mapinduzi kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.

Tanzania, Algeria kuanzisha Kampuni za Ubia

0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Muhongo  Wa kwanza kulia), akiongea  jambo  na wataalamu wa masuala ya gesi na umeme wa Algeria wakati walipokwenda  kutembelea Mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa HAMMA ,Mtambo huo wenye uwezo wa kuzalisha mewagati za umeme  418 unamilikiwa na Serikali ya Algeria  kwa asilimia 100.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo (Kushoto), akiongea na Waziri wa Viwanda na Migodi wa Algeria, Mhe. Abdessalem BOUCHOAREB.(Kulia)  Mawaziri ambapo wamejadili maeneo ya ushirikiano katika sekta ya Madini. Katikakati ni mkalimani.
 Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuanzisha kampuni za Ubia za ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme na ujenzi wa Mtambo wa kusindika gesi ya “Liquefied Petroleum Gas’ (LPG) ambayo itauzwa kwa wananchi kwa kutumia mitungi. Walio upande wa kulia ni Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Mhe. Youcef Yousfi, Algeria (wanne kutoka kulia) na ujumbe wake.

=======  ========  ========
Tanzania, Algeria kuanzisha Kampuni za Ubia
·        Ni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme
·        Kujenga mtambo wa kusindika gesi ya LPG, na kuuzwa kwenye mitungi.
·        Sekta ya madini pia yaguswa

Na Asteria Muhozya
Tanzania na Algeria zinakamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya Ubia itakayohusika na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza  umeme na Kampuni ya Ubia ya kujenga mtambo wa kusindika gesi ya “Liquefied Petroleum Gas” (LPG) na kuiuza gesi kwa wananchi kwa kutumia mitungi.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika ziara ya kikazi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wake nchini Algeria, ambayo inalenga kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya awali ya kushirikiana katika kubadilishana uzoefu kwenye masuala yanayohusu sekta za Nishati na Madinikufuatia Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa nchi hizo uliosainiwa tarehe 2 Disemba, 2013 nchiniAlgeria.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkutano  baina ya Mawaziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa  Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi,mawaziri haowameyaagiza mashirika ya Umeme ya Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme la Algeria (KAHRIF) kukamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya ubia ya ujenzi wa miundombinu   ya  kusambaza umeme.

Mkutano huo wa mawaziri,ulitanguliwa  na kikao cha awali cha wataalamu wa nchi zote mbili, ambacho  kiliongozwa na   Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme , Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga,  ambacho  kilijadili maeneo ya ushirikiano yanayohusu umeme, mafuta, gesi na madini.

Katika hatua nyingine, Mawaziri hao wameziagiza kampuni za mafuta na gesi likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni za mafuta na gesi za Algeria za NAFTAL na SONATRAC kukamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya ubia ya  kujenga mtambo wa LPG na kuuza gesi hiyo kwa wananchi kwa kutumia mitungi, ambapo  kampuni zote za ubia zimetakiwa kuanza kazi ifikapo Januari, 2015.

Wakati huo huo, Waziri Muhongo amekutana na Waziri wa Viwanda na Migodi wa Algeria Mhe. Abdessalem BOUCHOAREB ili kujadili maeneo ya ushirikiano katika sekta ya Madini ambapo wamezielekeza taasisi zinazohusika na madini za nchi hizo, kuandaa mpango wa utekelezaji wa ushirikiano katika kuwajengea uwezo wataalamu wa madini  kubadilishana uzoefu na teknolojia, utafutaji na uendelezaji wa madini ya dhahabu, chuma, almasi, phosphates na utunzaji wa taarifa za jiolojia na madini (Management of geological and mining database).

Katika ziara hiyo, Waziri Muhongo na ujumbe wake wamepata nafasi ya kutembelea Mtambo wa kufua umeme wa kutumia gesi asilia  wa HAMMA ambao unamilikiwa na serikali ya nchi hiyo kwa asilimia 100 na una uwezo wa kuzalisha megawati  za umeme 418, na uwezo wa kutumia mafuta ya dizeli na gesi kwa nyakati  tofauti.

Vilevile, ujumbe huo wa Tanzania umepata fursa ya kuona mashine za kuzalisha umeme zinazotembea (mobile generators) ambazo hufungwa kwa dharura sehemu inapohitajika na kuhamishiwa sehemu nyingine, ambapo mashine moja ina uwezo wa kuzalisha megawati za umeme 20.

Katika ziara hiyo, Mhe. Muhongo ameongozana na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme, Mhandisi Innocent Luoga na wataalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), TPDC na TANESCO.

Mkataba wa Makubaliano (MoU) ya ushirikiano  wa Tanzania na Algeria, ulisainiwa na Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Mhe. Youcef Yousfi.

Wakazi wa Mtwara na Lindi kushuhudia fursa za Utalii na Uchumi kupitia Tamasha la Utamaduni la Mtwara,Waziri mkuu pinda kuwa mgeni rasmi.

0
0
 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Tamasha la Mkoa wa Mtwara, ‘Mtwara Festival’, linatarajia kufungua milango ya fursa kwa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi katika kuziona fursa kadhaa kwenye sekta ya Utalii na Uchumi.Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia mwezi Agosti 16 na 17 mwaka huu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona  ulipo Mtwara mjini. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Fursa Zimefunguka, Tuzitambue, Tujiandae, Tuzichangamkie.

Tamasha hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania Creative Industries Network (TACIN) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) huku likisaidiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumzia Tamasha hilo Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN, Anic Kashasha alisema kuwa mikoa hiyo inautajiri mkubwa katika utalii, uchumi na vivutio vingi mbalimbali.

"Mikoa hiyo ina utajiri mkubwa tena sana katika rasilimai zake mbalimbali kama vile fukwe nzuri na za kuvutia, utajiri mkubwa wa historia yake utamaduni na hata ubunifu wa aina mbalimbali hivyo matamasha kama haya yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utajiri huo," alisema Kashasha. Aliongeza kuwa, "Kwa sasa mikoa hiyo imeghunduliwa kuwa ina utajiri mkubwa wa gesi na hivyo kuna watu mbalimbali wameshaajiliwa ikiwa pamoja na kupatikana kwa fedha nyingi tayari kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na taifa zima kwa ujumla."

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu  ya TTB, Devota Mdachi alisema kuwa utalii umekuwa kwa kiasi kikubwa ukisaidia maendeleo ya uchumi wa nchi. Anasema kuwa katika tamasha hilo ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali za kiutamaduni, sanaa na nyinginezo ni nafasi kubwa ya kukuza utalii pia hasa utalii wa ndani au utalii wa kiutamadunia. "Ni nafasi kwao katika kutangaza mengi kuhusiana na masuala ya Utalii, hapa nchini au hata utai wa shughuli za kiutamaduni pia ni muhimu na hii ndio nafasi ya kipekee kwao na kwa wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono Tamasha hili la aina yake," alisema Mdachi.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Ofisa ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkuu wa Wilaya wa Mtwara na Mikindani Baraza la Wilaya la Mtwara Vijijini, Baraza la Biashara, KIlimo na Viwanda (TCCIA). Wengine ni Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Pride FM, Radio of Mtwara pamoja na Kampuni ya Mawasiliano ya Strictly Communications.

RINO SALOON AND SPA YAWANG'ARISHA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT)

0
0
 Mshiriki wa Fainali ya TMT akihudumiwa katika Saloon ya Rino Saloon & SPA iliyopo Msasani Karibu na Capetown Fish Market jijini Dar Es Salaam.
 Mshiriki Kutoka Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha Anneth Paul akipata Huduma ya kutengenezwa Nywele kutoka kwa Mmoja wa Wahudumu wa Saloon Nzuri na Ya kisasa kabisa ya Rino ambapo washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) walipoenda kupendezeshwa kwaajili ya Show ya Mchujo.
 Steven Mapunda mshiriki kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) akihudumiwa katika Saloon ya Rino iliyopo Msasani Karibu na Cape Town Fish Market
Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa ndani ya Saloon ya Kisasa Kabisa ya Rino iliyopo Msasani karibu na Cape Town Fish Market kwaajili ya kupatiwa huduma zote muhimu za saloon zikiwemo Kutengenezwa Nywele, Kucha, Uso na Nk kabla ya kwenda kushiriki kwenye Onyesho la Mchujo ambalo litafanyika jioni ya leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ambapo leo kuna washiriki wataaga Mashindano hayo.

Saloon ya Rino iliyopo Msasani karibu na Cape Town Fish Market ndio saloon pekee ambayo imewapedezesha Washiriki wote 20 wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kabla ya washiriki hao kwenda kushiriki kwenye Show ya Mchujo ambapo leo washiriki wawili wataaga Mashindano hayo ambao fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents itafanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane
.
Kila wiki kutakuwa na Show ya mchujo ambapo washiriki wawili watatolewa katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo fainali yake itafanyika mwisho wa mwezi wa nane ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania na Washindi kumi bora watafanya filamu ya pamoja na Kunufaika na Filamu hiyo.

Ili kuweza kuwabakisha washiriki uwapendao unachotakiwa kufanya ni Kuwapigia kura washiriki kwa Kuandika ujumbe Mfupi wa Maneno kupitia Simu yako kwa Kuandika neno "TMT" halafu ikifuatiwa kwa namba ya Mshiriki na kutumwa kwenda 15678. MFANO: TMT00 tuma Kwenda 15678
Vilevile Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa katika Kituo Cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku na Kurudiwa Siku ya Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 Usiku.

Ili kuweza Kupata taarifa kuhusiana na Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) nenda kwenye simu yako ya Mkononi andika neno "TMT" halafu tuma kwenda 15678

Rais Kikwete afungua ukumbi wa mihadhara CHUO cha SEKOMU, aagiza wilaya zote nchini zijenge maabara katika kila shule

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Mkuu wa Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU  Askofu Dr.Stephen Munga(kushoto)Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Dr.Anneth Munga(watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa wilayani Lushoto 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu chA Sebastian Kolowa Memorial University mabapo alifungua ukumbi wa mihadhara na kuhutubia wananchi.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga na kulia ni makamu wa chuo Dr.Anneth Munga.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasililiza kwa makini wanafunzi kutoka Irente school for the Blind wakati walipoimba shairi maalumu wakati wa sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa katika  chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi wa wageni waliohudhuria sherehe ya ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa uliofanyika katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU huko Lushoto Mkoani Tanga

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Wananchi kuhakikisha kuwa ifikapo Mwezi Novemba Mwaka huu,  kila Shule ya Sekondari katika maeneo yao, ina  maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.

Rais Kikwete amesema hayo Mkoani Tanga katika nyakati tofauti Wilayani Kilindi na Lushoto ambapo yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Tanga tangu tarehe 8 Julai hadi tarehe 12 Julai,2014.

"Nataka ifikapo Mwezi Novemba, Mwaka huu vyumba vya maabara viwe vimekamilika, tulipeana miaka miwili, imetimia" Rais amesema na kuongeza kuwa lazima tusahihishe makosa tuliyofanywa ya kutojenga maabara wakati tunajenga shule za sekondari nchini kote.

Mwaka 2006, Serikali ilihamasisha ujenzi wa Shule za Sekondari nchini kote na muitikio ni mzuri, lakini hakukuwa na uhamasishaji wa kujenga maabara. “Tumeamua kushughulikia suala la maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya Sayansi kote nchini." Rais amesisitiza.

Rais amesema ameridhika na upanuzi wa Elimu katika ngazi za Msingi na Sekondari kote nchini na Serikali inaendelea na hatua ya kutatua changamoto za ubora wa Elimu, kuongeza Walimu, kuongeza Vitabu, ujenzi wa Maabara na Nyumba za Walimu kote nchini.

 Akihutubia katika mkutano wa hadhara Wilayani Lushoto Rais ameahidi kuboresha na kushughulikia suala la ujenzi wa barabara ya kwenda Bumbuli na zaidi kuhakikisha anaweka barabara ya lami katika mji wa Lushoto na mji mdogo wa Bumbuli.

Rais anaendelea na ziara Wilayani Lushoto na Mkinga ambapo anaendelea kuzindua miradi na kukagua miradi ya maendeleo.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.

10 Julai,2014

JAPANI YASAIDIA WAKIMBIZI TANZANIA

0
0
DSC_0069
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe (katikati) akibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili kwenye Bandari ya Dar na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada.
Alifafanua kuwa msaada huo utasadia watu 70,000, wakiwemo watoto chini ya umri wa miaka mitano ambao idadi yao inakadiriwa kufikia 14,000 na akina mama wajawazito wanaokadiriwa kufikia 3,150.

Alisema kuwa pesa hizo zitasaidia pia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwani Maharage zaidi ya tani 400 yatanunuliwa humu nchini. Alibainisha kwamba kwa mwaka uliopita shirika hilo limetumia zaidi ya dola milioni 10 za kimarekani kununua chakula kwa ajili ya wakimbizi hapa nchini.
DSC_0078
Mshereheshaji wa hafla hiyo Afisa Habari wa WFP, Fizza Moloo akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye halfa hiyo iliyofanyika jana jijini Dar kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mathias Chikawe aliwashukuru wafadhili wote ambao wamekuwa wakisaidia wakimbizi kwa miaka mingi. “ninawashukuru wote kwa pamoja kwa misaada yenu kwa kusaidia tatizo la wakimbizi nchini kwetu kwa roho moja jambo linalomaanisha tunasaidiana katika kuubeba huu mzigo” alisema Chikawe.

Hata hivyo Chikawe alisema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jumuiya za kimataifa imekuwa ikitoa misaada ya kuwarejesha Wakimbizi makwao hali ya vita ikitulia na kwa kipindi cha zaidia ya miaka kumi serikali imewarejesha wakimbizi zaidia ya laki sita.
Aliahidi kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kutafuta suluhisho la kusaidia Wakimbizi, huku akiwahakikishia wafadhili kuwa milango ipo wazi waendelee kutoa ushirikiano kwa mujibu wa tamko la Geneva la mwaka 1951.
DSC_0170
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akisoma hotuba yake kwenye sherehe fupi ya kukabidhiwa msaada wa Chakula kwa ajili ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma uliotolewa na Serikali ya Japan.
DSC_0109
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akisoma risala wakati sherehe fupi za kukabidhi msaada wa Chakula kwa Serikali ya Tanzania zilizofanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam jana.
DSC_0083
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati hafla fupi ya makabidhiano ya Chakula cha msaada kilichotolewa na Serikali ya Jaapa kupitia Balozi wake hapa nchini.
DSC_0185
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akikabidhi msaada huo kwa Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan (kulia) kwenye hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar.
DSC_0056
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) mara baaada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada wa dola za kimarekani milioni 1.4, kwa shirika la Chakula duniani (WFP) kwa ajili ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma. Kulia ni Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)

Na Mwandishi wetu
Serikali ya Japan imetoa msaada wa dola za kimarekani milioni 1.4, kwa shirika la Chakula duniani ili liweze kuwasaidia wakimbizi zaidi ya 70,000 wakiwemo watoto 14,000 wanaohitaji Chakula katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Akikabidhi msaada huo, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, aliwashukuru wafanyakazi wa shirika la Chakula duniani wanaofanya kazi Tanzania kwa kusaidia hali ya maisha ya Wakimbizi katika kambi zao.

Akizungumza katika halfa hiyo, Okada alisema nchi jirani na Tanzania zimekuwa katika vita zilizosababisha machafuko, lakini Tanzania kwa upande wake imekuwa ikiwapokea kwa wema Wakimbizi hao hivyo inapaswa kuungwa mkono kusaidia tatizo hilo la Wakimbizi
Balozi Okada alikabidhi pia tani 91 za mafuta ya kupikia, tani 367 za Unga wa nafaka, tani 400 za Maharage na tani 444 za Mahindi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani hapa nchini Richard Ragan aliishukuru serikali ya Japan kwani imekuwa ikisaidia Wakimbizi kwa miaka mitano iliyopita.


DSC_0178
Kaimu Meneja wa Bandari Bw. Nelson Mlali (kulia), Kaimu Afisa Mkuu wa Mawasiliano Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Peter Millanzi 9katikati) na Bw. David Mbonika wa WFP (kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0143
DSC_0147
Sehemu ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Bandari waliohudhuria halfa hiyo.
DSC_0193
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo kwenye hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada na Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan.
DSC_0010
Afisa Uhusiano na Siasa Ubalozi wa Ujerumani, Bw. Benedict Kikove (katikati) akijadiliana jambo na Afisa Habari wa WFP nchini, Bi.Seetashma THAPA (kulia) na Mtafiti na Mshauri wa masuala ya uchumi wa Ubalozi wa Japan nchini, Bi. Tamaki Yoshida mara baada ya tukio hilo.
DSC_0019
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan (kushoto) akifurahi jambo na Bw. David Mbonika wa WFP (kulia) pamoja na Brian Mahemba wa African Marine Surveyors and Consultant Ltd. (katikati) mara baada tukio hilo.
DSC_0214
Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari wakiandaa msaada huo tayari kupakiwa kwenye gari kupelekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
DSC_0243
Forklift ikiingiza sehemu ya msaada huo kwenye Lori maalum lililoandaliwa kusafirisha mzigo huo.
DSC_0009
Pichani juu ni sehemu ya msaada huo uliokabidhiwa jana jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyofanyika Bandari ya Dar.
DSC_0004

STEVE NYERERE AWAANDALIA CHAKULA CHA JIONI WASANII WA FILAMU NA WADAU

0
0
   Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere akizungumza machache wakati wa hafla aliyowakaribisha chakula cha jioni wasanii wa Filamu na wadau mbalimbali wa filamu Bongo ikiwa ni kuungana na wenzao waliokatika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilifanyika ndani ya Great Wall Restaurant iliyopo Osterbay jijini Dar esa Salaam.

 Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini maneno yaliyokuwa yakitolewa na Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere.
 Wasanii wakipata maakuli...
 Wolper na Kajala wakila chakula wakati wa hafla hiyo.…
 Mazungumzo ya hapa na pale hayakukosa...
Kila mmoja aliona ni wakati mwafaka kuongea na mwenzake aliyepotezana nae miaka kadhaa.

 
 Ilikuwa ni furaha maana wasanii wengine kuonana huwa ni mara chache chache.
Jini Kabula, Mariam Mndeme na Isabela Mpanda wakijumuika katika hafla hiyo.
 Meza ya waheshimiwa...
Ester akiwa na rafiki yake Zilpa.
 Jose Mara nae hakuwa nyuma...
 Samaki aina ya Kaa.
Chaz Baba akipakua chakula.
 Zungu wa GPL akiwa na Mkurugenzi wa Kajunason blog, Cathbert Angelo pamoja na msanii Rich.
 Msanii Nguri wa Muziki wa Bongo Fleva, Profesa J akipata chakula....
 Msanii Haji akimsurubisha samaki aina ya Kaa.
 Mshereheshaji wa hafla hiyo akieleza machache. 

 Msanii JB akiwasisitiza wenzake suala la upendo miongoni mwao.
    Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere akizungumza machache wakati wa hafla aliyowakaribisha chakula cha jioni wasanii wa Filamu na wadau mbalimbali wa filamu Bongo ikiwa ni kuungana na wenzao waliokatika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilifanyika ndani ya Great Wall Restaurant iliyopo Osterbay jijini Dar esa Salaam. 
 Malkia wa Mipasho, Bi. Khadija Kopa akilto nasaha kwa wasanii wenzake pamoja na wadau waliojumuika katika hafla hiyo.
 Wasanii na wadau wakitafakari kwa pamoja.
 Msanii Nguri wa Muziki wa Bongo Fleva, Profesa J akitoa machache. 
 Wasanii wakipongeza Msanii Nguri wa Muziki wa Bongo Fleva, Profesa J mara baada ya kutoa neno zito.
 Mwandishi Sauda Mwilima nae alikuwa ni miongoni mwa wadau walialikwa. 
 Chaz Baba nae hakuwa nyuma kutoa shukrani zake za pekee.
 Mwalimu Julio alikuwa ni miongoni mwa wageni waliofika na kutoa maneno/wosia mzito kwa wasanii.
 Mboni Masimba akieleza machache na kutoa shukrani zake kwa Rais wa Bongo Movie Steve kumutambua kuwa yeye mdau muhimu katika tasnia hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo na kuwakaribisha wasanii hao mkoani kwake ili waweze kufungua milango ya uwekezaji.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda akiwasisitiza vijana namna ya kufanya sanaa yao ikawaletea matunda mema.
 Zamaradi akizungumza machache na wasanii.
 Mboni akipata ukodak na Zungu wa GPL.
Furaha za hapa na pale nazo zilitanda. 
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

WINGU JEUSI LATANDA MSIBA WA SISTA ANNA, DAYOSISI YA KUSINI KATI YATANGAZA KUENDELEA KUENZI KAZI ZA MAREHEMU

0
0
Sista Anna Enzi za uhai wake.
Msiba wa sista Anna Peterson umeibua simanzi si kwa familia yake tu bali kwa wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe alipokuwa akifanya kazi za kijamii tangu ujana wake. 

Hayo yamebainika wakati wa ibaada maalum ya kumkumbuka iliyofanyika hii leo katika kanisa la KKKT usharika wa Amani Bulongwa, ibaada iliyoongozwa na baba askofu wa dayosisi ya kusini kati Levis Sanga, Askofu Mstaafu Dkt. Solomon Swallo na Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa pamoja na msaidizi wa askofu Philemon kahuka. 

Akihubiri katika ibaada hiyo maalum Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa amesema marehemu alikuwa akifanya kazi zake kwa mkono wa dayosisi ya kusini kati tangu enzi za ujana wake bila ubaguzi ingawa yeye alikuwa mzaliwa wa nchi ya Sweeden. 
Askofu mstaafu Manyiewa akihubiri ibadani hapo.


Amesema amemfahamu toka 1969 na hadi anafikwa na umauti alikuwa akisaidia watoto yatima, wajane, wagane na walemavu wote na hata wasiojiweza na kusisitiza kuwa kanisa haliwezi kumsahau kamwe.

Akielezea historia ya marehemu Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo amesema Sista Anna alikuwa akifanya kazi zake kwa kujituma bila kujali ugumu wa kazi uliokuwepo kwa kipindi hicho hasa ubovu wa barabara na ugumu wa kuwafikia wananchi kutokana na tabu ya usafiri. 

 
Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo.


Dkt Swallo amesema alikuwa akisisitiza kuwa Mungu ndiye aliyemtuma kufanya kazi Bulongwa Makete na si Binadamu hivyo haoni shida kutumikia jamii ya Makete toka ujana hadi uzee wake. 
Dkt Nicodemas Kikoti.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu hospitali ya Bulongwa Dkt Nicodemas Kikoti amesema marehemu pia alikuwa akifanya kazi na hospitali hiyo pamoja na jamii ikiwemo kusomesha watoto yatima kutoka shule ya awali mpaka vyuo, kuwajengea nyumba wasiojiweza, kuhudumia wajane, kusaidia vifaa vya umeme pamoja na kujenga makao ya kituo cha watoto yatima Bulongwa.
Mch. Dkt Phares Ilomo.

Naye Mch. Dkt Phares Ilomo kutoka chuo Kikuu cha Iringa amesema yupo tayari kuandika kitabu cha kuelezea historia ya marehemu Sista Anna kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kanisa na washarika kuchangia gharama ili kitabu hicho kichapishwe na kuzalishwa kwa faida ya vizazi vijavyo ikiwemo kukiweka katika maktaba ya chuo chake. 

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi amesema marehemu alikuwa akifanya shughuli ambazo kimsingi zilitakiwa kufanywa na serikali hivyo wema wake kwa jamii ya Makete hauna mfano. 
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi.

Amesema njia pekee ya kumuenzi ni kufanya yale aliyoyapenda huku akisisitiza kuwa serikali itashirikiana na kanisa kuendeleza kazi zote alizoziacha Sista Anna. 

Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga.

Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga ametangaza tarehe 26 Juni kila mwaka kuwa ni siku maalum kikanisa ya kumkumbuka marehemu sista Anna hivyo jamii inashauriwa kufika kwenye kituo cha watoto yatima Bulongwa kwa ajili ya kuwatembelea na siku hiyo itakuwa ikifanyika ibaada maalum kwa ajili ya marehemu.

Sista Anna Peterson amefariki Juni 26 mwaka huu nchini Sweeden alipokwenda kwa ajili ya matibabu na amezikwa leo hii nchini humo, na hapa Makete alikokuwa akiishi toka ujana wake imefanyika ibaada maalumu ya kumkumbuka.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Sista Anna Peterson, Amen.

Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete

WAZIRI WA MAZINGIRA DKT. BINILITH MAHENGE AKANUSHA KUTUMIA FACEBOOK YENYE JINA LAKE

0
0
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge amewataka wananchi kupuuza taarifa zozote zinazotolewa kwa jina lake kupitia mtandao wa facebook kwa kuwa yeye hatumii mtandao huo. 

Waziri Mahenge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wetu wilayani hapo na kusema kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mitandao hiyo vibaya kwa kufungua akaunti yenye jina lake ilihali yeye hajawahi kujiunga na facebook na hana mpango huo. 

Amesema kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali wapo watu wanaoziamini taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia mtandao huo wakidhani zimetolewa na yeye lakini imekuwa tofauti na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa zinatolewa na mtu ama watu fulani na si yeye.

 "Ukiangalia pale pana picha yangu kweli, lakini taarifa zingine ni uongo mtupu, kwa mfano tarehe yangu ya kuzaliwa iliyoandikwa hapo sia ya kweli, hii inaashiria wanavyoviweka ni vya uongo" amesema Waziri Mahenge.

 Aidha ametoa rai watu kuitumia vizuri mitandao hiyo kwa kuisaidia jamii huku akiwataka waliofungua akaunti hiyo kuifunga na kuacha kuwapotosha watu kwa kutumia jina lake kwani ni kinyume cha sheria na atakayebainika sheria iko wazi dhidi yake. 

Hivi karibuni kumekuwa na watu fulani kufungua akaunti kwnye mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya viongozi mbalimbali kwa lengo la kuwahadaa watu na kuwapa taarigfa ambazo si sahihi

Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete

MAMA SALMA KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO WA MWAKA WA TAASISI YA SEGAL FAMILY HUKO NGURDOTO- ARUSHA.

0
0
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Segal Family uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto huko Arusha tarehe 10.7.2014.
  Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Segal Family wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye ukumbi wa Ngurdoto 
  Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Segal Family wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye ukumbi wa Ngurdoto
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Mwanaidi Maajar ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Segal ya nchini Marekani. Viongozi hao walikutana huko Arusha katika hoteli ya Ngurdoto unakofanyika mkutano huo ambao Mama Salma alialikwa kuuhutubia (keynote addres) tarehe 10.7.2014.
  Mwanzilishi wa Taasisi ya Segal Family Bwana Barry Segal akimpongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kutoa hotuba ya kusisimua kwenye mkutano wa mwaka wa Taasisi hiyo

VIONGOZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE MAPAMBANO DHIDI YA MAABUKIZI MAPYA YA VVU.

0
0
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam mara baada ya kukamilisha ziara ya siku nne mkoani Dar es salaam. Dkt. Fatma ameeleza kuwa maabukizi yameendelea kupungua kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akitoa mchango wake kuhusu namna viongozi wanavyoweza kusaidia kupunguza vitendo hatarishi vinavyochangia maabukizi mapya ya VVU katika maeneo wanayoyaongoza, wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya ziara ya watendaji wa TACAIDS katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuangalia hatua iliyofikiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam. 
==========  ========  ========
VIONGOZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE MAPAMBANO DHIDI YA MAABUKIZI MAPYA YA VVU.
Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
10/7/2014,Dar es salaam.

Serikali imewataka viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele na kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na vitendo vyote vinavyochangia maambukizi mapya ya VVU katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam. 

Amesema viongozi na watendaji wa jiji hilo ndio wenye dhamana na jukumu la kusimamia na kuongoza mipango yote ya mapambano ya maambukizi mapya ya VVU wakishirikiana na wananchi katika maeneo wanayoyaongoza na kufafanua kuwa janga la Ukimwi lisipodhibitiwa katika ngazi zote litaendelea kupoteza nguvu kazi na kuiongezea serikali mzigo wa kuwahudumia wagonjwa wapya.

“Nawaagiza viongozi wa manispaa zote tatu za mkoa wa Dar es salaam kulipa kipaumbele kikubwa suala hili la mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa kuweka msukumo katika kutoa elimu ili tuweze kuokoa rasilimali zetu” Amesema.

Amesema serikali, vyombo vya habari na Taasisi zilizo kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU zimekuwa zikifanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya namna ya kujikinga na janga hili na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kwa hiari ili kujua kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Ameeleza kuwa licha ya mkoa kukabiliwa na changamoto mbalimbali umeendelea kuchukua hatua  za kupunguza maabukizi mapya ya VVU kwa kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu, kupiga marufuku ngoma hatarishi za usiku zinazokesha, kutekeleza sheria mbalimbali kupitia jeshi la Polisi ambalo huendesha operesheni mbalimbali za kuwakamata wananchi wanaovunja sheria hususan waendesha biashara za madanguro,watumia madawa ya kulevya na biashara ya ngono kwenye majumba ya starehe. 

“Tunaendelea kutoa elimu ya kujikinga na maabukizi mapya ya VVU ili kusaidia hata operesheni mbalimbali tunazofanya katika jiji letu kuzaa matunda na kuwafanya wale wote waliokuwa wakijihusisha na vitendo vinavyochangia kueneza VVU kuachana navyo” Amesisitiza. 

Aidha, Bw. Meck Sadiki amegiza kupatiwa orodha ya maeneo yote ya jiji la Dar es salaam ambayo yanaongoza kwa kuwa na vihatarishi vya VVU ili aweze kuyafanyia kazi na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kutoa ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi za serikali na kuwafichua wanaoendesha vitendo vinavyochangia maambukizi hayo ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kisheria.

Kwa upande wake Mkiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho akizungumza wakati wa majumuisho hayo amesema kuwa  hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam yameendelea kupungua kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

“Ni kweli hali ya maabukizi ya VVU kwa mkoa wa Dar es salaam imeendelea kupungua  mwaka hadi mwaka toka asilimia 10.9 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 6.9 za mwaka 2012 jambo linalotufanya tuendelee kuongeza juhudi zaidi ili tufikie malengo ya kitaifa na kimataifa ya kufikia sifuri tatu”. Amesisitiza.

Amesema ili kuhakikisha kuwa vita dhidi ya maambukizi mapya ya VVU inaendelea kufanikiwa , Serikali inashirikiana na taasisi mbalimbali, Baraza na mitandao ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi  nchini katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tatizo hilo.

Ameongeza kuwa serikali inawathamini na inaendelea kuwajengea uwezo Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi waliojiunga katika Vikundi vya Kuweka Akiba na Mikopo (VICOBA) katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mwamko mkubwa wa kujiletea maendeleo waliouonyesha. 

Ametoa wito kwa WAVIU kote nchini kuendelea kujiunga na mifuko mbalimbali  ukiwemo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kunufaika na huduma za afya zinazotolewa kupitia mfuko huo.

Dk.Shein ziaraNI Kusini Pemba

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mshauri wa Rais Uwekezaji Bw.Abrahman Mwinyi Jumbe (kushoto) akipotembelea shamba la ufugaji wa samaki la kikundi cha Hakiliki Mwambe kusini Pemba jana. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi wa  wanakikundi cha Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki Mwambe kusini Pemba jana,wa Pili (kulia) Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilahi Jihadi Hassan
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Watoto wa Kijiji cha Mwambe  mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa  wanakikundi cha Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki  jana,alipofanya ziara katika Mkoa wa Kusini Pemba.
 Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Chake Chake  Pemba jana.
  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Kusini Pemba katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Chake Chake
 Baadhi ya akinamama wa Mkoa wa kusini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari waliyoandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Ikuu ya Chake chake jana, [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Pemba Mwanajuma Majid katika futari iliyowaandalia wananchi wa Vijiji mbali mbali vya mkoa wa Kusini Pemba hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Ikulu ya Chake Chake.

Rais Kikwete azindua nyumba za bei nafuu Mkinga

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi nyumba za bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa( National Housing) huko Wilayani Mkinga,Mkoa wa Tanga jana.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Cha Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing) Bi.Susan Omari(kushoto) akitoa maelezo na kisha kukabidhi kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mshine za kutengeneza matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Tanga ili kuwawezesha kuanzisha vikundi vya ujenzi vya vijana.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Galawa.Mashine hizo zilitolewa wakati wa Uzinduzi wa nyumba za bei nafuu Wilayani Mkinga(Picha na Freddy Maro)

KAMATI YA MAJI KING'ONGO DAR WAKAGUA UJENZI WA MRADI WAO WA MAJI ULIOFADHILIWA NA TBL

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MO Resources Limited,Onesmo Sigalla (kulia), akitoa maelezo kwa kwa wajumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo,  Kata ya Salanga, Kimara, Dar es Salaam,  kuhusu hatua aliyofikia ya usafishaji maji katika ujenzi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kamati hiyo iliyokwenda kukagua maendeleo ya mradi huo jana, iliongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo, Demetrius Mapesi (kulia). Wajumbe wengine ni Anna Kibwana (wa pili kulia) na Emannuel Isimbula.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MARY NAGU MGENI RASMI KONGAMANO LA NNE LA KITAIFA LA MAKATIBU MUHTASI TANZANIA LEO JIJINI MWANZA

0
0
 Pichani kushoto ni Waziri wa Uweshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu,Mh.Mary Nagu ambaye ndiye mgeni rasmi wa Kongamano la nne laKitaifa la Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh.Angela Kairuki akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa TAPSEA wakati alipokuwa akiwasili kwenye ufukwe wa hotel ya Malaika,ambako Kongamano hilo linafanyika leo jijini Mwanza.
Pichani kushoto ni Waziri wa Uweshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu,Mh.Mary Nagu akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa TAPSEA,Mh.Angela Kairuki wakati alipokuwa akiwasili kwenye ufukwe wa hotel ya Malaika,ambako Kongamano hilo linafanyika leo jijini Mwanza,pichani kati Mwenyekiti wa Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Bi.Pilly Mpenda wakiwa wamezungukwa na washirki wengine mbalimbali wakiwasili kwenye ufukwe wa hotel ya Malaika,ambako Kongamano hilo linafanyika leo jijini Mwanza. 
Ngoma ya asili ya wasukuma ikipigwa kuwakaribisha washiriki mbalimbali waliokuwa wakiendelea kuwasiliasubuhi hii kwenye kongamanno hilo jijini Mwanza
Washiriki mbalimbali wakiendelea kujiandikisha kwa ajili ya ushiriki wa kongamano hilo
Mazungumzo ya utaratibu wa washiriki wa Kongamano hilo ukiendelea kuwekwa sawa na waandaaji .
Waandaji wa Kongamano hilo wakiendelea kujadiliana jambo
Washiriki wa kongamano hilo wakiwa katika picha ya pamoja
Washirii wa kongamano hilo wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Washiriki wa Kongamano hilo wakitabasamu mbele ya Camera ya Globu ya Jamiii
Wadau wa TAPSEA wakiwa katika picha ya pamoja
Washiriki wakendelea kuwasili kwenye ufukwe wa hotel ya Malaika,ambako Kongamano hilo linafanyika leo jijini Mwanza.

PICHA ZIARA YA VIONGOZI WA TANZANIA SINGAPORE

0
0
 Kutoka kushoto ni mkurugenzi wa taasisi ya biashara ya kimataifa iliyo chini ya wizara ya viwanda na biashara Singapore, Rahul Ghosh akibadilishana mawazo na Denis Rweyemamu na Linda Manu kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania ambayo ndiyo iliyoandaa ziara ya mafunzo kwa makatibu wakuu na vionzoi waandamizi wa serikali ya Tanzania nchini Singapore.
 Baadhi ya makatibu wakuu walioko kwenye ziara ya mafunzo nchini Singapore yaliyoandaliwa na taasisi ya uongozi Tanzania, kutoka kushoto ni Dk Shabn Mwinjaka- Katibu mkuu wizara ya uchukuzi, Dk Ffolens Turuka- Katibu mkuu ofisi ya Waziri Mkuu,Dk Philip Mpango- Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Mipango na Dk Sivvacius Likwelile- Katibu Mkuu wizara ya Fedha.
Ujumbe wa makatibu wakuu na viongozi waandamizi wa serikali ya Tanzania wakiwa katika mafunzo nchini Singapore, kuhusu uendeshaji wa shughuli za serikali kwa ushirikiano na sekta binafsi PPP mfumo ambao umeisaidia kimaendeleo nchi ya Singapore, Ziara hii inaratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania- Uongozi Institute. (Picha zote na Vedasto Msungu Singapore)

GARI AINA YA FORD EXPEDITION V8 INUZWA

0
0
 MAKER: FORD
MODEL: FORD EXPEDITION V8
YoM: 2000
CC: 5400
COLOR: SILVER
MAWASILIANO: 0713327106/0756673327








Attention- Weruweru Alumni in the Diaspora

0
0
 Now, we have been receiving lots of inquiries on how the Weruweru Alumni community living outside of Tanzania, can get access to the Khanga, Tshirts and Mugz of Weruweru Alumni?! ...Today,let me help you all with the answer.
 Our Alumni Association leaders and Steering Committee will be traveling in different countries for their personal and official duties... What they will be doing is, CARRYING a number of Khanga, Tshirts and Mugs for those Alumni who will be ready to buy them. How would you get them?
 Get in contact with ME through missiepopular@gmail.com and place your order. Your email should include the number of pairs of Khanga you need and the city you are from and I will do the needful to ensure the package reaches you!
 Yes...it is as simple as that!... Don't let the movement pass you, grab your memorabilia and feel the Weruweru love wherever you are!

 Oooooh I love these women! My Weruweru family...
 The Prices for these items are GPB 5 for those in UK and 10$ for the rest...
Share the Weruweru experience with the world ....Grab your memorabilia Today

PINDA ASAFIRI KWA TRENI KWENDA READING KUZUNGUMZA NA WATANZANIA

0
0






Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipanda treni kutoka Reading kwenda London Uingereza baada ya kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI NYALANDU AMWAGA MSAADA WA MILIONI 10 WA MABATI 420 SHULE ZA SEKONDARI KWA AJILI YA MAABARA

0
0
diwani
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Lazaro Nyalandu.
mwenyekit
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.

Na Hillary Shoo, SINGIDA.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.

Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa za mitaani.
kinyeto
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akizungumza kwenye shule ya sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
“Nataka niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo, haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu wanajipitishapitisha wakitukana.” Alisema Hanje kwa hasira.

Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
“Mimi inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani ya Chama Willaya hii.” Alisema Hanje kwa kujiamini.
 
elia
Katibu wa Mbunge Lazaro Nyalandu , Elia Digha, msaidizi wa Mbunge Ellen Mutalemwa wakimsikiliza Mwenyekiti Hanje Kinyeto.
ellen
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Mtinko.
hanje
Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini, Narumba Hanje akizungumza na wananchi wa Kata ya Mtinko wakati wa kukabidhi mabati 220.
kabidhi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini, Narumba Hanje (kulia) akimkabidhi mabati 220 yenye thamani ya shilingi milioni tano Afisa Mtandaji wa Kata ya Mtinko Jimbo la Singida Kaskazini, Eliufoo Mkanga katika hafla fupi iliyofanyika jana katika shule ya Sekondari ya Kata ya Mtinko , mabati hayo yametolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe,Lazaro Nyalandu.
maabara
Hili ni jengo la maabara ya sekondari ya Kinyeto likiwa katika hatua ya lenta.
kibao
Kibao kikionesha shule ya sekondari Mtinko.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images