Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 314 | 315 | (Page 316) | 317 | 318 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge)akitembelea leo  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia  ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
   Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge)akipata  maelezo  leo   kuhusu bidhaa  mbalimbali  kutoka kwa Bi mkubwa  Juma kwenye banda la Zanzibar  katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kushoto  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
   Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge) akipokelewa  na Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa  wakati alipotembelea leo  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
   Mama  Salma Kikwete  akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea leo  banda la  Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa  kwenye  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana akifungua rasmi mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara mjini Dodoma leo.
   Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Sera - Utumishi ambaye pia ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara Bw.Mathias Kabunduguru akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.Pindi Chana (hayupo pichani) kufungua mkutano wa Baraza hilo lilozinduliwa rasmi mjini Dodoma leo.
   Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo mjini Dodoma leo.
   Mkurugenzi Msaidizi - Utumishi Bi. Hilda Kabisa akiwasilisha mada baada ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara mjini Dodoma leo
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo mjini Dodoma leo.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakijaribu kufanya mazoezi katika mashine zilizo ndani ya Gym ya mazoezi ya timu ya Azam Fc, wakati walipotembelea Gym hiyo kujionea leo baada ya hafla ya uzinduzi wa Msikiti wa ‘Masjidil Huda’, kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, leo Julai 4, 2014.
   Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, wakati walipokuwa wakitembelea kujionea Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya Azam Fc, leo Chamazi. Picha na OMR
   02:- Wakitembelea Uwanja wa Chamazi, kujionea maendeleo ya timu ya Azam Fc , leo.
   Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (kulia) akitoa maelezo kwa viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  wakati walipokuwa wakitembelea kujionea Uwanja Gym ya mazoezi ya timu ya Azam Fc iliyopo kwenye Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya hiyo, leo Chamazi. 
   Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  wakati walipokuwa wakitembelea kujionea Uwanja Gym ya mazoezi ya timu ya Azam Fc iliyopo kwenye Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya hiyo, leo Chamazi
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akijaribu kufanya zoezi katika moja ya mashine zilizo ndani ya Gym ya mazoezi ya timu ya Aazam Fc, kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, wakati walipotembelea Gym hiyo leo. Picha na OMR

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea  Waziri wa Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan Ikulu jijini Dar es salaam leo
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika  mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa China Jenerali Chang Wanquan  Ikulu jijini Dar es salaam leo
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa China  Ikulu jijini Dar es salaam leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan Ikulu jijini Dar es salaam leo. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (mstaafu) Mhe Abdulrahman Shimbo pia walikuwepo

  0 0

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda lao,kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
  Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania,Happy Iteba (kushoto) akitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la Posta kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
  Maafisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania Happy Iteba na James Musyaji wakiwahudumia wateja waliotembelea banda hilo.

  0 0

  Mteja akipata maelezo ya Kina kutoka kwa wafanyakazi wa Access Bank katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni ya Channel 10, Meshack akifanya mahojiano na Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Muganyizi Bisheko na kueleza huduma wanazozitoa  katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ambapo Bisheko alisema kuwa huduma zinazotolewa ndani ya banda lao ni ufunguaji wa akaunti kwa bei rahisi ya shilingi 1,000 huduma ya utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali 
   Mtangazaji wa Azam Tv, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza machache ndani ya banda la Access Bank mara baada ya kutembelea  katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa benki hiyo, Muganyizi Bisheko akiwa pamoja na wafayakazi wenzake.
  Wafanyakazi wa Acces Benki wakipata pozi mbele ya kamera ya Kajunason

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Monica Mwamunyange akibadilishana kadi na Profesa Liu Xueyi kutoka Chuo kikuu cha Southwest Jiatong, wakati mkufunzi huyo na wanafunzi wa chuo hicho walipotembelea wizara ya Uchukuzi leo mchana kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya reli hasa reli ya mwendo kasi.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange, akifafanua jambo kwa Wakufunzi na wanafunzi wanaochukua shahada za Uzamili na Uzamivu katika Reli kutoka Chuo Kikuu cha Southwest Jiatong, wakati walipotembelea Wizarani hapo kujifunza na kubadilishana uzoefu hasa kwenye usafiri wa Reli, leo mchana.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi, wanafunzi na sehemu ya wakurugenzi wa Wizara ya Uchukuzi, wakati wanafunzi hao wanaochukua shahada za uzamili na uzamivu katika Eneo la Reli kutoka chuo kikuu cha Southewest Jiatong walipotembelea Wizarani hapo leo mchana ili kubadilishana uzoefu hasa katika treni za mwendo kasi. Aidha chuo hicho kimeahidi kubadilishana uzoefu na Chuo che Reli Tabora ili kujenga uwezo katika masuala ya Reli. (Picha na  kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)


  0 0

  Sehemu ya muonekano wa banda hilo ndani ya viwanja vya Mwalimu JK Nyerere kunakofanyuika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya saba saba.
    Wadau mbalimbali wakipita kwenye banda hilo kujipatia maelezo ya hapa na pale
  Wageni wote wanakaribishwa kwenye banda hilo.

  0 0

   Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, leo Julai 5, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Mbogamboga aina ya Kabeji ilivyostaawi katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.  
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kiatu aina ya Buti ambacho kimetengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga Moshi, Kiwanda hicho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza. Rais Kikwete ametembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014  katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  Jijini, Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

   Waziri wa Ardhi na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akitoa mchango wake katika Mada ya Ushirikiano wa Vijana katika vyama vya Siasa Kimataifa wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
   Mwakilishi wa Mgeni Mualikwa Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Vijana waliohudhuria Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto,upande wake wa kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk.Telephory Kyaruzi,Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.(Balozi Joseph Sokoine alimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Bernard Membe ambaye alikuwa na hudhuru)
   Wadau wakifuatilia kwa makini michango ya Mada zinazotolewa wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
   
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam akizungumzia suala la kukuza na kuendeleza Umoja wa Afrika na kukuza Umoja wa Kiuchumi ikiwa pamoja na kuunga mkono sera ya kutofungamana na upande wowote na kuwataka Vijana wasomi kusimamia na kuchangia maoni yao katika upatikanaji wa Itikadi ya nchi.
   Mtumishi wa Mungu Askofu Isaya Joseph akifuatilia kwa makini Mada mbali mbali wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
   Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia waliohudhuria.
  Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
   Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk Telephory Kyaruzi akiagana na Mwakilishi wa Mgeni mwalikwa Balozi Joseph Sokoine kwenye Viwanja vya Karimjee mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto.

  0 0

  MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando anatarajia kutambulisha kwa mashabiki wake albamu ya Kamanda Pindo la Yesu Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

  Albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.

  Taarifa ya mwimbaji huyo kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa tayari mkoa wa Mwanza umekuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa Dar es Salaam.“Nitazindua Diamond Jubilee Agosti 3, baada ya hapo nitaenda Mwanza Agosti 10 Uwanja wa CCM Kirumba, naomba mashabiki wangu wajiandae kupata vitu vizuri sana.“Nimejipanga kuhakikisha nawapa burudani ya nguvu, najua nini wanakitaka, pia najua waimbaji gani wanawapenda, nipo katika utaratibu wa kuhakikisha wanafurahi,” alisema Muhando.

  Kwa mujibu wa Muhando, nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

  Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

  Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

  0 0

  Diamond Platnumz na DMK kwenye utoaji tuzo za BET Los Angeles
  Photo Credits: DMK Global Promotions' facebook page
  Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Damond Platnumz. Msanii mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Tanzania
  Amejiunga nasi kwa njia ya simu punde baada ya kuhudhuria utoaji tuzo za BET ambako yeye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania tuzo hizo.
  Kazungumza mengi kuhusu TUZO HIZO.

   
  Alipopokea na alivyopokea uteuzi wake, aliloliona kwenye tuzo hizo, ulinganishaji wake katika utoaji tuzo hizi na za Tanzania / Afika, alichojifunza, faida ya kuja kushiriki hili na hata mikakati yake ijayo kuhakikisha kuwa muziki wa Tanzania unafika mbali zaidi.

   
  SWALI jingine alilojibu ni kuwa....ni kweli kuwa ili muziki wa Tanzania ushinde tuzo ni lazima uwe na mahadhi ya Afrika Magharibi (kama muziki wake wa Number One) ama Afrika Kusini 
  Amejiunga nasi kwa msaada wa promota Dickson Mkama almaarufu DMK ambaye pia ndiye meneja wa msanii huyo hapa nchini.
  KARIBU  0 0

  2Rais Jakaya Kikwete akielekea ofisini kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE leo, katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara na kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje TANTRADE Bi. Anna Bulondo5Rais Jakaya Kikwete akiangalia majiko ya mkaa katika moja ya mabanda ya Kenya6Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Ofisa Mauzo Mwaandamizi wa kampuni ya Gold Finger Investiment Bi.Beatrice Kibanya wakati alipoteaembelea banda hilo. 8Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na baadhi ya vijana kwenye banda lao la Forever Living12Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw.Babar Hussain wa kampuni ya kuteneneza viatu ya Zubair Shoes.13Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. Edwin Wekefield wa kampuni ya Mimic Craftis kutoka nchini Afrika kusini inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano.14Mshauri wa jeshi la Magereza Bw. Alferio akitoa maelezo kwa Rais jakaya Kikwete kuhusu kofia bora za kujikinga waendesha pikipiki wakati alipotembelea katika banda la Mafereza 15Rais jakaya Kikwete akipiga picha na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje wakati alipotembelea katika banda hilo leo Mh. Rais Jakya Kikwete aliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa. 3Rais jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN)wakati alipotembelea banda hilo leo na kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini.4Rais jakaya Kikwete akizungumza na vijana waliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa katika mafunzo ya ujasiriamali wa tatu kutoka kulia nji Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa Mawasiliano wa umoja wa Mataifa (UN)
  17
  Rais jakaya Kikwete akimsalimia mtoto ambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati akitembelea katika mabanda mbalimbali kwenye viwanja vya Sabasaba leo.

  0 0

  Baadhi ya Watoto wakionyesha ujuzi wa kucheza sarakasi kwenye uwanja wa Kasulu, Mburahati kwa Jongo wakati wa onyesho la kuhitimisha warsha ya sarakasi na ngoma za samba regge iliyoandaiwa na kituo cha Baba Watoto kupitia mradi wa Fit For Life.
  Ngoma za samba regge kutoka Brasili zikichezwa kwenye uwanja wa Kasulu, Mburahati kwa Jongo
   Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akitoa hatuba yake kwa wananchi na wapenzi wa muziki na sarakasi waliofika kwenye onyesho hilo
  Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani cha Goethe Institut ambaye pia ni Mkurugenzi wa mradi wa fiti for life, Eleonore Sylla akisema machache wakati wa onyesho la kuhitimisha warsha ya sarakasi na ngoma za samba regge kupitia mradi wa Fit For Life
  Mratibu wa kimataifa wa mradi wa Fit for life, Daniela Titze akisema machache wakati wa onyesho la kuhitimisha warsha ya sarakasi na ngoma za samba regge kupitia mradi wa Fit For Life
  Meneja Mradi wa Fit fr life, Habiba Issa akitoa maelezo kuhusu mradi huo wakati wa onyesho la kuhitimisha warsha ya sarakasi na ngoma za samba regge kupitia mradi wa Fit For Life
   Kutoka kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA, Godfrey Mngereza, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani cha Goethe Institut ambaye pia ni Mkurugenzi wa mradi wa fiti for life, Eleonore Sylla, Mratibu wa kimataifa wa mradi wa Fit for life, Daniela Titze na Meneja Mradi wa Fit fr life, Habiba Issa wakifurahia jamb wakati wa onyesho hilo
   
  Mkurugenzi wa Kituo cha Baba watoto, Mgunga Mwa Mnyenyelwa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani cha Goethe Institut, Eleonore Sylla ambaye pia ni Mkurugenzi wa mradi wa fiti for life na Mratibu wa kimataifa wa mradi huo, Daniela Titze.

   

  Watoto hao wakionyesha upigaji wa ngoma za samba regge wakati wa kuhitimisha warsha ya muziki wa samba regge na sarakasi inayofanyika kupitia mradi wa fit for life ambayo imewashirikisha watoto walio kwenye mazingira magumu kati ya umri wa miaka 10 hadi 25 imefadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) na kusimamiwa na kituo cha Utamaduni cha Ujerumani Goethe-Institut kwa ubia na Ufa-Fabrik ya Ujerumani na Parapanda Theatre.
  0 0

   Baadhi ya washiriki kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na kampuni ya Max- Malipo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya  kuanza kwa maonesho.
   Mtaalamu kutoka  Tanzania Gemmological Centre (TGC) Bw. Prosper Tingo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TANSORT.
  Mjiolojia kutoka Idara ya Nishati Bw. Habass Ng’ulilapi akielezea sera ya nishati kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara.

  0 0

  Sehemu ya muonekano wa banda hilo ndani ya viwanja vya Mwalimu JK Nyerere kunakofanyuika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya saba saba.
    Wadau mbalimbali wakipita kwenye banda hilo kujipatia maelezo ya hapa na pale.
  "Wageni wote wanakaribishwa kwenye banda la Diaspora..."anasema Bi Lucy Naivasha, ambaye ni meneja wa Tanzanite Account ya CRDB ambayo imeboreshwa kuhudumia vyema walio ughaibuni na hata wa hapa nyumbani. Banda lao lipo ndani ya banda kuu la Tanzania

  0 0

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington (kulia) akikabidhi tiketi kwa mawakala waliochaguliwa kwenda kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Brazil ambapo anaemkabidhi ni Hasham Lardhi wa kampuni ya  SS Hassan, huku nyuma yake ni Al-Farham Dewji wa kampuni ya Regal Solar na anaengali mwenye fulana ya bluee ni Jacob Mwalyolo wa kampuni ya Maranatha Electronics ya Mbeya
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington (kulia) akimkabidhi tiketi Hasham Lardhi wa kampuni ya  SS Hassan ambae ni mmoja kati ya washindi waliochaguliwa kwenda Brazil kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.

  MAWAKALA watatu wanaojishughulisha na mauzo ya visimbuzi vya AzamTV wamesafiri kuelekea Brazil kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.

  Mawakala hao ni pamoja na Hasham Lardhi wa kampuni ya SS Hassan, Al-Farham Dewji wa kampuni ya Regal Solar ya Dar es Salaam na plus Jacob Mwalyolo wa  Maranatha Electronics ya Mbeya.

  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Operation Mkuu wa Azam Media alisema kuwa kampuni hiyo inatambua mchango wa mawakala wake katika kuendeleza biashara ya visimbuzi hivyo.

  Alisema kuwa watakaa Brazil kwa siku kumi kuanzia tarehe 4 mwezi huu na watapata nafasi ya  kuangalia mechi hiyo ya nusu fainali itakayofanyikia  Belo Horizonte, Julai 8.

  Alisema kuwa tangia kuanza kwa biashara ya visimbuzi vya AzamTV mawakala hao wamefikia kiwango cha juu cha mauzo ya huduma kwa wateja wa Azamtv. Casse alisema kuwa wakiwa nchini humo watatembelea miji kadhaa kama vile Rio de Janeiro na Belo Horizonte.

  Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington alisema kuwa kwa kipindi hiki cha michuano ya kombe la dunia mauzo ya visimbuzi vyake yamekuwa makubwa.

  Alisema kuwa kwa kutambua mchango wa mawakala katika kufanikisha mauzo ya visimbuzi vya AzamTV kampuni hiyo itaendelea kuwazawadia mawakala wote watakaokuwa wakifanya vema.

  “Mafanikio yamekuwa makubwa kabisa tangu tumeanza biashara hii ya kuuza visimbuzi mnamo Desemba mwaka jana na kutokana na mchango wa makawala tumejitaidi kufanya vema sokoni”.
   
  “Tunawashukuru sana  Azam Media pamoja na mtandao mzima wa biashara ya Bakhresa bila kumsahau Eric  Casse ambae tumekuwa tukifanya kazi naye bega kwa bega kuhakikisha tunafikia malengo yetu kwa ujumla"; kwakweli hii ni safari ya kipekee katika maisha yetu na tumefurahi sana kupata nafasi ya kwenda kushuhudia kombe la dunia nchini Brazil, hakika hii ni ndoto iliyokamilika”…kwa pamoja walisema mawakala hao waliobahatika kupata nafasi hiyo.

  0 0
 • 07/05/14--13:24: Article 3 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI
                                                                          
                                                                        
                                                                    
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI (Mb) KUZURU MIKOA YA MWANZA NA MARA
  Wizara ya Ujenzi napenda kutoa taarifa ka umma kuwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kukagua miradi  mbaimbali ya Maendeleo katika  mkoa wa Mwanza na Mara.

  Mheshimiwa Waziri Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Mwanza tarehe 06 Julai ambapo atakagua mradi wa Ujenzi wa barabara ya Usagara – Kisesa (by pass) yenye urefu wa km. 16.7 inayojenga kwa kiwango cha lami. Siku inayofata tarehe 07 Julai, Mheshimiwa Waziri ataelekea mkoani Mara kukagua  mradi wa barabara ya Makutano – Natta – Mugumu (sehemu ya Makutano – Sanzate km 50). 

  Siku hiyo hiyo mchana Dkt. Magufuli  atazindua rasmi kivuko cha MV. Mara kitakachotoa huduma kati ya Iramba na Majita. Aidha, baada ya uzinduzi huo  Mheshimiwa  Waziri wa Ujenzi atafanya  mkutano wa hadhara na kuongea na wananchi wa eneo la Mwibara ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa mradi wa Barabara ya  Nyamuswa – Bunda – Kisorya – Nansio (sehemu ya Bulamba – Kisorya km 51).

  Mheshimiwa Magufuli ataendelea na ziara yake tarehe 09 Julai Mkoani Mwanza ambapo atazindua kivuko cha MV. Temesa katika eneo la Nyegezi(Sweya). Kivuko hicho kimefungwa mitambo ya kukiwezesha kusafiri kwa mwendo wa kasi ili kukiwezesha kutoa huduma katika mwambao huo wa ziwa Victoria. Aidha, Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba Tani 65 ambazo ni sawa na abiria 80 na magari madogo matano kwa wakati mmoja. 

  Kivuko hicho kitakuwa kinafanya kazi kutoka Luchelele kupitia Sweya, Butimba, Mkuyuni, Igogo hadi Kirumba ikiwa ni mkakati wa kupunguza foleni katika jiji la Mwanza.

  TAARIFA HII IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI
  05/07/2014

  0 0  Licha ya elimu ya kampeni za tohara  katika wilaya ya kilolo kupokelewa na    kuwa na  mwamko wa kujitokeza  kwa watu kwa kiwango kikubwa katika zoezi la kufanyiwa tohara  bado kunachangamoto zinazowakumba watoa huduma katika kituo cha kutolea huduma hiyo.

  Akizungumza mwelimishaji rika wa kampeni za tohara zinazoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la JPIEGO kutoka katika kituo cha afya cha nzihi SCOLASITIKA MKWEMWAamesema kuwa watu kuanzia 98 mpaka 99 hujitokeza kwa siku.

  Amema kuwa,kuna wakati wamekuwa wakishindwa kuwahudumia na kulazimika kusitisha huduma kutokana na kuwa jengo husika halina umeme, kwani huduma hizo hufanyika hata nyakati za usiku.

  Amesema kuwa wengi wao wanapenda kupewa huduma hiyo mida ya usiku kwa ajiri ya usiri huku akiitaja  changamoto nyingine kuwa ni watu wanashindwa kujitokeza kutokana na kuwa huduma hiyo inaambatana na zoezi la upimaji vvu.

  Akizungumza meneja wa eneo hilo DOLIC KADETE amesema kuwa huduma ya tohara kwa kituo hicho huanza saa 2 asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

  Ameongeza kwa kutaja changamoto nyingine inayowakabili ni kuwa asilimia kubwa ya watoto wanaorudishwa kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo ya vidonda huwa haviko katika hali nzuri.

  Akizungumza mmoja wa  wanaume ambao wamefanyiwa tohara KASIANI SAFARI amelishukuru shirika la jpiego kwa huduma hiyo huku wakiwashauri wanaume wengine ambao hawajafanyiwa tohara kujitokeza kupata huduma hiyo kwani itawasaidia kuwakinga na magonjwa ya zinaa.

   Kampeni za tohara zinafanyika katika mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya vvu kiko juu na katika mikoa ambayo tohara inafanyika kwa kiwango kidogo kuanzia miaka 10 na kuendelea Lengo likiwa ni kusaidia kupunguza maambukizi ya vvu kwa asilimia 60.

  Aidha kampeni za tohara ambayo ni kuanzia mwezi wa tisa mwaka jana hadi mwezi wa tisa mwaka huu shirika la jpiego lilipanga kuwafikia watu laki moja na ishirini na tano elfu na kufikia mwezi huu wa saba tayari wameshafikia lengo.

  0 0

  IMG-20140705-WA0001Rais wa asasi ya Ladies circle  kwa hapa Tanzania ,Julieth Anthony akizungumza katika uzinduzi rasmi wa asasi hiyo uliofanyika jijini Arusha katika hotel ya Naura springs.
   
  IMG-20140705-WA0000Mshereheshaji wa shughuli hiyo akifanya yake
  IMG-20140705-WA0002Janeth Julius ambaye ni mwenyekiti wa Ladies circle Tanzania
  IMG-20140705-WA0003Meza kuu wakati wa uzinduzi
  IMG-20140705-WA0004Picha ya pamoja
  IMG-20140705-WA0005Mgeni rasmi katika uzinduzi huyo,Mbunge wa bunge maalumu la katiba, Yasmin Aloo
  IMG-20140705-WA0006
  ZAIDI ya watu  60 wenye  uhitaji  wamewezeshwa na asasi  isiyo ya kiserikali ya Ladies Circle International katika mahitaji mbalimbali ikiwemo elimu, matibabu ,malazi pamoja na mitaji  .

  Hayo yalisemwa  na Rais wa asasi hiyo  hapa Tanzania ,Julieth Anthony wakati akizungumza katika uzinduzi rasmi wa asasi hiyo uliofanyika mjini hapa hivi karibuni.

  Alisema kuwa , asasi hiyo ilianza kufanya kazi hapa nchini mwaka 2012 ambapo ina jumla ya matawi matatu kwa nchi nzima ,huku asasi hiyo ikiwa kwenye nchi 37 hapa duniani.

  Alisema kuwa, lengo hasa la kuanzishwa kwa asasi hiyo ni kuhamasisha wanawake kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, kusaidia kuhimiza elimu na masomo ya sayansi kwa watoto wa kike wakiwemo yatima .

  Aidha lengo lingine ni kuboresha huduma ya mama na mtoto ili kuzuia kifo cha mama na mtoto ,na kuendeleza ujasirimali kwa vijana wanawake pamoja na kufadhili elimu kwa watoto yatima na kuwapatia mahitaji yao.

  Julieth alisema kuwa, kuwepo kwa asasi hiyo hapa nchini ambayo inaundwa na wanawake wenyewe kutasaidia sana kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani zinazowakabili wanawake na watoto wa kike kwa ujumla.

  Naye Katibu Mkuu wa shirika la Love for all people Tanzania na Mratibu wa uanzishwaji wa asasi hiyo, Anthony Musani alisema kuwa,kuanzishwa kwa asasi hiyo hapa nchini ni baada ya kutembelea nchi za nje na kukuta wakiwa na asasi hiyo ambayo wamekuwa wakisaidia jamii zenye uhitaji ndipo alipoguswa na kuomba kuanzishwa hapa nchini .

  Musani alisema kuwa,watu wengi wana uwezo mkubwa sana wa kusaidia jamii zenye uhitaji ila changamoto kubwa inakuja katika kupata wawezeshwaji wa miradi ama vikundi vyao watakavyoanzisha.
   
  Aidha Musani aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuhakikisha wanaitumia asasi hiyo ipasavyo kwa kusaidia jamii mbalimbali zenye uhitaji wakiwemo wajane, yatima na hata wenye mahitaji maalumu.

  Naye Mgeni rasmi katika uzinduzi huyo,Mbunge wa bunge maalumu la katiba, Yasmin Aloo aliunga mkono uanzishwaji wa asasi hiyo sambamba na kuanzisha mfuko wa kuwezesha asasi hiyo ili kuendeleza mipango yake ya kusaidia jamii.

  Aidha aliitaka asasi hiyo kutumia chombo hicho kwa malengo yaliyowekwa ikiwemo kuanzisha kituo cha afya kijiji cha ndani mkoani Dodoma na kuanzisha kituo cha ushauri nasaha na mafunzo ya ufundi kwa watoto wa mitaani waliotelekezwa baada ya kupata mimba katika umri mdogo mkoani Arusha.

older | 1 | .... | 314 | 315 | (Page 316) | 317 | 318 | .... | 1904 | newer