Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA SRI LANKA, POLAND NA ROMANIA LEO

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Sri Lanka nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya,  Dkt Velupilai Kananathan kwenye sherehe fupi zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Balozi wa Sri Lanka nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya, Dkt Velupilai Kananathan  baada ya kupokea hati yake ya utambulisho  kwenye sherehe  fupi  zzilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa  Poland nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya, Mhe.  Marek Zial Kowski  kwenye sherehe fupi zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe Balozi wa  Poland nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya, Mhe.  Marek Zial Kowski  kwenye sherehe fupi zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Balozi wa  Poland nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya, Mhe.  Marek Zial Kowski baada ya kupokea hati yake ya utambulisho  kwenye sherehe  fupi  zzilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi wa Romania nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya, Mhe Julia Pataki kwenye sherehe fupi zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Balozi wa  Romania nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya, Mhe.  Julia Pataki baada ya kupokea hati yake ya utambulisho  kwenye sherehe  fupi  zzilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.PICHA NA IKULU

MAENDELEO HAYANA CHAMA- ASEMA MAGUFULI

0
0

WAZIRI WA UJENZI AMBAYE PIA NI MBUNGE WA CHATO MHESHIMIWA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA NCHANKIMA KUHUSU MAENDELEO YA KATA HIO JANA KATIKA SHULE YA SEKONDARI ICHWANKIMA, WILAYA YA CHATO MKOANI WA GEITA


WAZIRI WA UJENZI AMBAYE PIA NI MBUNGE WA CHATO MHESHIMIWA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKITOA MAELEKEZO  KWA MKUU WA WILAYA YA  CHATO RODRICK MPOGOLO WA PILI KUTOKA KUSHOTO PAMOJA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO NDUGU CLEMENT BEREGE WAKWANZA KULIA. WAKWANZA KUSHOTO NI NDUGU IBRAHIM BAGURA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA CHATO.

UMATI MKUBWA WA WATU WALIOKUSANYIKA KATIKA KATA YA KASENGA WAKIMSILIZA WAZIRI WA UJENZI AMBAYE PIA NI MBUNGE WA CHATO MHESHIMIWA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKIWAHUTUBIA KUWAELEZA KUHUSU UTEKELEZAJI WA 
========  ========  ======
MAENDELEO HAYANA CHAMA- ASEMA MAGUFULI

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa Wananchi Jimbo la Chato Mkoani Geita kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano bila kujali itakadi zao za kisiasa.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana katika mikutano yake ya kuhamasisha maendeleo katika kata za Kasenga, Ichwankima na Kachwamba wilayani Chato katika mkoa wa Geita.

“Ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii, maendeleo hayaji hivi hivi, tuache malumbano na itikadi zetu za vyama ili tujenge jimbo letu vizuri” Alisema Waziri Magufuli.

Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali ya CCM haina ubaguzi ndio maana inapeleka maendeleo katika maeneo yote na hata yale yanayongozwa na wapinzani.

“Mnatakiwa kushirikiana na Serekali na sio kubeza kama watu wengine wanavyofanya. Serikali yetu imefanya mambo mengi mazuri ya kuwaletea maendeleo” alisisitiza Mheshimiwa Waziri.

Katika hatua nyingine Waziri Magufuli alimtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ndugu Peter Ngunula kuhakikisha kuwa ndani ya miezi miwili wananchi wa kata ya Kasenga waanze kupata maji kama awali.

“Mhandisi naomba baada ya miezi miwili wananchi hawa waanze kupata maji kama awali, na wananchi mtunze miundombinu ya maji haya ili tuweze kutatua kero hii kwa pamoja” alisema Waziri Magufuli.

Katika kusisitiza jambo hilo Waziri Magufuli alichangia shilingi milioni moja ili zisaidie katika tatizo hilo la maji.

Katika hatua nyingine, waziri Magufuli aliwaahidi wakazi hao kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuwaletea umeme na wajiandae na fedha kidogo tu Shilingi elfu ishirini na saba 27000/= kwa ajili ya uunganishaji.

Serikali imedhamiria kuwasaidia na kushusha gharama za uunganishaji umeme ndio maana kipindi kile  tunaunganisha umeme pale Chato gharama zilikuwa shilingi laki nne na nusu.


 

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG’ARA KWENYE MAONESHO YA SABA SABA

0
0
Mjiolojia Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Mwara Shoo akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonesho ya kimataifa ya Saba Saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Utaalam Elekezi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Wataalam kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mstaafu wa Shirika hilo Bw. Gray Mwakalukwa mara alipotembelea banda hilo.

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA

0
0
Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena.
Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. 
Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka.

MATUKIO NDANI YA MAONYESHO YA KIMATAIFA UA BIASHARA YAENDELEA JIJINI DAR

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas Tarimba akitoa maelezo ya uendeshaji wa michezo ya kubahatisha kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uchumi , Viwanda na Biashara leo ilipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jiji ni Dar es salaam. Picha na HAZINA


Mazishi ya Mwanahabari Nguli nchini, Mzee Nkwabi Ng’wanakilala

0
0
Mzee Nkwabi Ng'wanakilala enzi za uhai wake.
Mwanahabari wa Reuters nchini Bw. Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo  (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. 

Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI.
Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba.
Mkurugenzi Msaidizi  wa Idara ya Habari MAELEZO  BW. Raphael Hokororo  (kati) akiwa na wadau wa habari waliokuwepo mazishini

Nafasi za Masomo University of Oldenburg,Germany

0
0
Kwa wale wanaohitaji kujiunga na elimu ya juu nchini Ujerumani.
 
Kuanzia B.A,Bsc,M.A mpaka Phd Watanzania tumieni nafasi hizi,
chuo kinapokea wanafunzi hata kwa vijana wa Kitanzania walio maliza kidato cha sita wana nafasi ya kujiunga na chuo hiki,maelezo zaidi,
Tafadhali wasiliana na anuani hii hapa chini:

 International Student Office
 Carl von Ossietzky Universität Oldenburg
 Ammerländer Heerstr. 114-118,
 26129 Oldenburg
 Germany
 
 
Pia fomu za maombi zinapatikana online katika link hii chini:

Mitambo ya IPTL yaanza kuzalisha megawati 100

0
0
·        IPTL kuongeza uzalishaji hadi megawati 200 mwakani
·        Kushusha zaidi bei ya umeme hadi chini ya senti nane za marekani

UZALISHAJI umeme katika kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) umefikia megawati 100 ambayo ni kiwango cha juu cha uwezo wa mitambo yake, kiwango kilichofikiwa tarehe 15 Juni, huku uongozi wa kampuni hiyo wakiahidi kutekeleza mipango mkakati yake yote ya utanuzi kwa awamu.  

Hayo yalibainishwa na Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za viongozi wa kampuni hiyo kwa umma na mamlaka za serikali tangu PAP iliponunua IPTL.

“Tarehe 15 mwezi wa sita mwaka huu, mitambo ya IPTL iliyopo eneo la Tegeta, ilianza kuzalisha megawati 100 za umeme, ambazo ndiyo uwezo wa mitambo hiyo. Hii ni moja ya ahadi zilizotolewa na uongozi wa PAP wakati wa ununuzi wa mitambo ya IPTL,” alisema Makandege .

Alisema IPTL ambayo inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Pan African Power Solutions Tanzania Limited, inaendelea na jitihada zake za kutimiza ahadi yake ya kuwapunguzia wateja/walaji adha ya gharama ya umeme Tanzania.

“Tumepanga kuzalisha megawati 200 kwa kutumia mitambo inayoendeshwa kwa kutumia gesi ifikapo Desemba 2015, ambapo tutauza umeme wake kwa chini ya dola nane za kimarekani, ikiwa ni awamu ya kwanza ya utanuzi. Katika awamu ya pili ya utanuzi, tumepanga kuzalisha megawati 300 ifikapo Desemba 2017.

“Tuliahidi kupunguza bei zetu, kuongeza uzalishaji mpaka kufikia kiwango cha juu cha mitambo yetu na kuendelea kutanua mitambo yetu ili kuweza kuzalisha megawati 500 baada ya kibadilisha mfumo yake iweze kutumia gesi. Hatua hii itawezesha IPTL kupunguza zaidi bei zake hadi kufikia kati ya senti sita na nane za kimarekani kwa kila unit. Ndani ya kipindi hiki kifupi, tumeweza kudhihirisha uwezo wetu wa kutimiza ahadi zetu zote,” alisema Bw. Makandege.


Alisema kuwa ingawa bei ya umeme kwa kampuni yao kwa sasa zimesimama kati ya senti 26 na 30 za kimarekani kwa unit, wateja wajiandae kuanza kufurahia bei zilizopungufu hivi karibuni baada ya kampuni kubadilisha mashine zake na kuanza kutumia gesi kuzalishia umeme.
Kwa sasa, wazalishaji umeme wengine katika soko wanatoza kati ya senti 38 na 60 za kimarekani kwa kila unit. Bw. Makandege aliongeza kuwa mitambo yote ya IPTL imefanyiwa marekebisho makubwa baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya miaka karibia sita bila matengenezo.

Alisema uongozi mpya unaendelea na uboreshaji wa barabara zote za ndani ya kiwanda kwa kiwango cha lami, pamoja na marekebisho mengine ambayo yatabadilisha muonekano mzima wa IPTL.
“Tukiwa kama kampuni ya ufuaji umeme, tunatambua faida za kiuchumi za kutumia umeme wa bei rahisi kwa mteja na kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi kwa ujumla.
“Hii ndiyo maana tunafanyakazi kwa jitihada zote ili kuweza kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha umeme wa bei rahisi ambao utasaidia kuboresha uchumi wa nchi hii,” alisema Makandege.

Bw. Makandege alisema kuwa kampuni yake imeamua kutafuta njia bora za uzalishaji wa umeme wenye gharama nafuu, ikilinganishwa na washindani wengine katika soko, sababu inaamini uwepo wake utasaidia katika kuboresha maisha ya wateja wake na jamii inayoizunguka.

“Uongozi mpya wa IPTL/PAP unaamini katika kuwapatia wateja wake matokeo yaliyo chanya. Njia pekee ya kufanya hivyo ni kutoa
bidhaa/huduma zilizo na gharama nafuu kwa wateja, licha ya utofauti waliokuwa nao katika viwango vyao vya mapato,” alisema.


KILA LAKHERI BI REGINA MWALEKWA NDANI YA KITUO CHAKO KIPYA CHA KAZI BBC

0
0
Wakiwa wenye Nyuso za Furaha.Watangazaji mahiri wa Radio na Televisheni,Bi.Regina Mwalekwa aliyekuwa mtangazaji wa Radio One na baadae akahamia Clouds FM/TV na sasa amejiunga na Shirika la Utangazaji la BBC akiwa na mtangazaji mwenzake kutoka kituo cha televisheni cha ITV/Radio One Bi.Fatma Almas Nyangasa,kama walivyonaswa na Camera ya Globu ya Jamii ndani ya viwanja vya maonyesho ya Saba saba yanayoendelea hivi sasa jijini Dar.Bi Regina Mwalekwa kwa sasa sauti yake itakuwa ikisikika rasmi ndani ya BBC.Globu ya Jamiii inamtakia kila lakheri katika kituo chake kipya cha kazi.
Bi.Regina Mwalekwa akifanya mahojiano na mmoja wa washiriki wa maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya Saba saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwal.Julius Nyerere,jijini Dar.

WANAHABARI KILIMANJARO WAPIGWA MSASA JUU YA MATUMIZI YA INTERNET KWA SHUGHULI ZA UANDISHI WA HABARI

0
0
Mratibu wa Mafunzo ya Internet ,Andrew Marawiti akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo kwa makini.
Mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo Seif Jigge akitoa maelezo kwa wanahabri wanaohudhuria mafunzo ya Internet  yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi VETA mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.
Darasa likiendelea.
Kila mshiriki alikuwa na kazi ya kufanya kipindi chote cha mafunzo.
Baada ya kujifunza kwa muda mrefu darasa lililazimika kusimama na kunyoosha mwili kidogo.
Ukafika Muda wa chakula kwa wenzetu ambao hawako katika mfungo.
Washiriki wakapata picha ya pamoja.

kibonzo cha Nathan Mpangala

TTCL YAFURAHIA KUIBUKA NA TUZO YA USHINDI KATIKA SEKTA YA MAWASILIANO

0
0
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota akionesha tuzo ya ushindi katika sekta ya mawasiliano.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba. Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo katika sekta ya Mawasiliano.Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba. Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.

KAMPUNI ya Simu Tanzania, TTCL imeshinda tuzo katika kundi la kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo,  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota katika uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere. 

Ushindi wa TTCL unatokana na ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo katika upande wa mawasiliano ya simu na pia mawasiliano ya intaneti "DATA". TTCL imesema ushindi huo umeipa hamasa ya kuendelea kubuni bidhaa ambazo zitakuwa chachu ya ukuaji uchumi nchini.

Airtel Divas yatembelea kikundi cha Sauti ya walemavu kwenye Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba

0
0
Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kushoto), Afisa Uhusiano, Jane Matinde (wa pili kushoto), na Afisa mauzo, Rachael Mboya (kulia), wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Mwanachama wa Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, Adelina Mluge (kulia), akitoa maelezo kuhusu bidhaa zinazouzwa na kikundi hicho kwa Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, (kutoka kushoto), Afisa Mauzo, Rachael Mboya, Afisa Uhusiano, Jane Matinde na Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kulia), na Afisa Uhusiano, Jane Matinde (kushoto), wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na kikundi SWAUTA katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba, ambapo Airtel Divas imekiwezesha kikundi hicho kuwa na banda katika maonyesho hayo.
Afisa Mauzo wa Airtel , Rachael Mboya,akiangalia kazi ya kikundi cha ulemavu ikiwemo kushona na uwezo wa kusoma vitabu mbalimbali vilivyopo katika banda lao wakati wanawake wa Airtel Divas walipotembelea banda lao katika maoenyesho ya sabasaba.

Umoja wa kikundi cha wanawake cha Airtel Divas leo kimetembelea kikundi cha sauti ya wanawake walemavu Tanzania (SWAUTA) katika banda lao lililopo katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Saalam

Airtel Divas wamefanya hivyo hivyo ikiwa ni muda mfupi tu tangu walipofanya harambee ya kukiwezesha kikundi hicho kupata fedha za kulipia banda katika viwanja vya maonyesho ya 38 ya kimataifa maarufu kama Sabasaba ili nao kuonyesha bidhaa zao kwa watanzania

Akiongea wakati wa ziara hiyo, mwanachama wa Umoja wa wanawake wa Airtel na Meneja Huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema” Airtel Divas tunayofuraha kuona tumeweza kuwasaidia kina mama wenzetu kutimizia lengo lao na kuwapa nafasi yakuweza kuonyesha ubunifu wao uwezo wao na kazi zao za mikono kwa washiriki na wateja wa ndani na wanje wanaotembelea maonyesho haya ya Sabasaba.

Ni matumaini yetu kuwa fulsa hii ya kuonesha na kujitangaza hapa saba saba itawawezesha kufikia malengo yao ya kutanua wigo wa biashara zao na kupata masoko na kuuza bidhaa zao kwa wingi zaidi. Tunatoa wito kwa watanzania kujitokeza na kuwaunga mkono kina mama hawa katika banda lao lililoko Benjamini Mkapa.

Kwa upande wake Mwanachama wa Umoja wa sauti ya walemavu Tanzania Bi Adelina Mluge Alisema “Tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuwepo katika mazingira mazuri ukilinganisha na ilivyokuwa na miaka iliyopita. mpaka sasa tumeweza kupata wateja wengi wakipita hapa kuona na kununua bidhaa zetu kwa wingi. Tunategemea kufanya vyema katika maonyesho ya mwaka huu kutokana na maboresho haya na hivyo basi tunaishukuru sana kampuni ya Airtel kwa kujitolea kutusaidia.

Airtel kupitia huduma zake za jamiii imeweza kuwafikia jamii na kuwawezesha kupata huduma muhimu hususani katika elimu, Airtel kwa kupitia Divas Airtel inaendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo kina mama hawa wa umoja wa sauti ya walemavu Tanzania.

MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF, MH. RAMADHAN KIJJAH AVUTIWA NA UTENDAJI KAZI WA PPF KATIKA MAONYESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA MAARUFU KAMA SABASABA

0
0
Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh Ramadhan Kijjah akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea banda la PPF ili kujionea utendaji kazi wa Wafanyakazi wa PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba
Mmoja wa wateja waliotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam akijaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba.Anayemuelekeza Pembeni ni Afisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, BwMohamed Siaga
 Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwahudumia baadhi ya wateja waliofika katika banda la PPF kwenye maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Katika Barabara ya Kilwa, Jijini Dar Es Salaam
Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka akitoa ufafanuzi kwa mteja aliyefika katika Banda la PPF kwaajili ya kupenda kufahamu hatua za kisheria zinazochukuliwa pindi pindi mwajili au mwanachama wa PPF anaposhindwa kuwasilisha Michango kwa Wakati kwenye Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Afisa Mafao wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Mercy Sammy akimuhudumia mmoja wa wateja waliofika katika banda la PPF kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam kwaajili ya Kujipatia huduma mbalimbali kutoka PPF.
 Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akiwauhudumia wateja waliofika katika Banda la PPF kwaajili ya kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam.
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel (kushoto) akitoa ufafanuzi wa maswali aliyoulizwa na mmoja wa wateja waliotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA JIJINI ARUSHA

0
0

Na woinde shizza,arusha.
 JESHI la polisi mkoani hapa limewaua majambazi watatu waliokuwa wamepanga njama ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso  mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa,majambazi hao watatu  waliuawa jana tarehe 3 eneo la TBL -Njiro  wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora fedha hizo.

Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba  fedha zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100  huku wakiwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.

Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo  polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika  eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.

Ambapo majibizano yalianza kati ya majambazi hao na polisi huku wakirushiana risasi hadi eneo la TBL njiro ndipo majambazi walipofika eneo hilo waliamua kutelekeza gari na  kushuka chini  na kumimina risasi kwa askari polisi  hao.

Kamanda Sabas alisema kuwa,hatimaye polisi waliweza kuwauawa majambazi hao  na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya  Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.

Aidha Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea kuongeza juhudi hizo zaidi.
 


DHAMIRA YETU NI KUKIDHI MAHITAJI YA WATEJA YA KIBENKI NA YA KIFEDHA.

0
0
Pichani ni  Meneja wa Tawi lililopo ndani ya  maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar,Bi. Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki hiyo.Bi.Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na huduma bora kabisa katika soko  kwa bei inayowezekana kulipa na viwango  vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa mwanahisa.

Amesma benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH,ambapo zaidi ya ATM 180 na mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa.
 Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bwa.Adalbert Alchard akizungumza na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar.Pichani kushoto ni  Afisa wa Benki hiyo,Bi Tuddy Lutengan.

SHUKURANI

0
0

Familia ya Bibi Mary Singano wa Sahare Tanga, inapenda kumshukuru Mungu kwa baraka na rehema zake katika kipindi cha msiba wa Marehemu Lt. Col(Rtd) Maurice Noel Singano kilichotokea tarehe 31/05/2014 Chennai, India .

Tunawashukuru Wizara ya Afya kwa msaada Wakati wa ugonjwa ,tunatoa shukrani  za kipekee kwa Mganga Mkuu wa Serikali Dr Donan Mmbando,Dr Goloka Muambata wa Tanzania nchini india na wote waliojitoa kuokoa maisha ya mpendwa wetu .

Tunamshukuru Dr. Jayashree ,Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Apollo Chennai kwa matibabu katika kipindi cha ugonjwa

Tunawashukuru father Maurusi, Jerome na father Francis  kwa huduma za kiroho, Watanzania waliokwepo Apollo katika kipindi Chote Cha  ugonjwa. Tunawashukuru Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Mathias Mlumba ,Jumuiya ya Mt Mathias Mtume wa Mikocheni DSM,Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Martha DSM na Mathias Mulumba Tanga. Baba Askofu jimbo la Tanga .Jumuiya ya Mt Yuda Thadei Sahare, Wawata na Walei Tanga.

Tunamshukuru Mkurugenzi wa St. Christina Bwana Gabriel Kessy, Mwenyekiti wa bodi ,Walimu,wafanyakazi na wanafunzi.Menejimenti na watumishi wa MSD,TFDA na Airtel kwa ushirikiano na kutufariji katika kipindi hiki kigumu. Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa huduma ya mazishi.

Tunawashukuru Ndugu jamaa,majirani na marafiki walioshirikiana nasi katika kipindi chote cha ugonjwa na msiba.Tumefarijika sana kwa upendo mlio tuonyesha na Mungu awabariki sana.

Kutakua na mkesha tarehe 25/07/2014 utakaohitimishwa na misa siku ya tarehe 26/07/2014 nyumbani kwa Bibi Mary Singano- Sahare Tanga. Wote mnakaribishwa

“Raha ya Milele umpee ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie,apumzike kwa AMANI”

“Nimepigana Vita vilivyo vizuri,nimeimaliza safari, imani nimeilinda” Timotheo 4:7

Dk. Shein Akutana na Mwana Mfalme wa Japan

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akifuatana na Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino mara walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuonesha kitu Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino baada ya mazungumzo yao alipotembelea Ikulu Mjini Zanzibar leo na Mkewe Princess Akishino.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino alipowasili Ikulu mjini Zanzibar leo akifuatana na Mkewe Princess Akishino na baadae kufanya mazungumzo.

NIDA IMEUNDWA KWA MUJIBU WA SHERIA NA MAJUKUMU YA NIDA YAPO WAZI HIVYO NEC WAACHENI NIDA WAFANYE KAZI KAMA WALIVYOPANGIWA :WAZIRI CHIKAWE ALONGA

0
0
 Waziri wa mambo ya ndani ya  nchi Mathias Chikawe  akiwa anafunga mkutano wa wafanyakazi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa  uliokuwa unafanyika ndani ya hotel ya snowcrest jiji Arusha.
  washiriki  katika mkutano wa Wafanyakazi wa  Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIda wakiwa wanamsikiliza waziri wa mambo ya ndani ya nchi kwa makini wakati akifunga mkutano wao katika hotel ya snowcrest
 waziri akiwa anapena mkono na mkurugenzi mara baada ya kutoa  risala ya kufunga mkutano huo
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) , Dickson Maimu akiwa anatoa shukurani kwa  waziri kwa kuja kufunga mkutano  wao
 washiriki  katika mkutano wa Wafanyakazi wa  Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIda wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi waziri wa mambo ya nchi Mathias Chikawe   nje ya jengo la hotel ya Snowcrest sehemu ambayo mkutano ulikuwa unafanyika

 washiriki wakipongezana mara baada ya waziri kufunga mkutano huo

washiriki wakiwa wanasikiliza kwa makini risala ya mgeni  Rasmi

JERRY SILAA AFUNGUKA KUHUSU SIASA - THE SPORAH SHOW

0
0
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images