Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 310 | 311 | (Page 312) | 313 | 314 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Joseph Mwaisango
  ******

  TONE MULTIMEDIA GROUP Ambao ni wamiliki wa Mtandao huu wa Mbeya yetu Blog , Tunapenda Kuungana na wadau wetu wote Kumpongeza Bwana Joseph Mwaisango ambaye ndiye Mwandishi Mkuu wa Blog hii ya Mbeya yetu  na Mmoja wa wakurugenzi wa Tone Multimedia Company Limited (TMCL)  ambao pia ni wamiliki wa Blogs za Mikoa TanzaniaTone Radio-Tz , This Day MagazineStay In Tanzania(Tanzania Tours) , Tone Tube Tz  , Matukio na Wanavyuo na Watanzania waishio nje ya Nchi kwa kutimiza miaka yake kadhaa siku ya Leo.

  Tunapenda kumpa Hongera sana kwa kazi nzito ambazo anazifanya ili kuwaletea wadau habari zilizo sahihi na za uhakika zaidi kutoka pande zote za Mkoa wa Mbeya, Pia tunamuombea kwa Mungu ampe siku nyingi zaidi , Afya Njema na aendelee kuchapa kazi zaidi na zaidi bila kusahau kuongeza Ubunifu zaidi.

  Pia katika Hili tunapenda kuwashukuru wadau Mbali mbali wa Habari wakiwemo Bloggers wote wa Tanzania, Magazeti, Radio na TV kwa kuendelea kuonesha ushirikiano mkubwa ili kazi ziendelee kwa ufanisi mkubwa

  Mwisho tunapenda kumshukuru kila mmoja wetu ambaye ni mdau mkubwa wa Blog ya Mbeya yetu,  wote tupo pamoja katika kusherekea siku hii ya leo.

  0 0

  Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
   Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wadau wa mchezo wa Riadha waliojitokeza kuwapokea wachezaji wa mchezo huo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
  Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.Picha na Frank Shija, WHVUM


  Na Frank Shija, WHVUM
  Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.

  Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.

  Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake. “Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.

  Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia. Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.

  Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo. Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand.


  0 0

   Waziri wa Nchi wa Mazingira wa Uganda, Flavia Namugere (katikati) akiwakabidhi tuzo ya ushindi wa jumla ya RECP Afrika Mashariki ya usimamizi bora wa matumizi ya maji na nishati kwa Mhandisi wa Huduma za Kiufundi wa Kiwanda cha Mwanza cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sunday Kidolezi (kushoto), na Mhandisi wa Mitambo wa kiwanda hicho, Erick Ernest ambayo kampuni hiyo ilituzwa katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Entebe, Uganda.
   Tanzania Deputy Permanent Secretary for Environment in the Vice President’s Office  (Left)  presenting one of the three                Resource Efficient & Cleaner Production (RECP) awards won by TBL Mwanza Plant to TBL Mwanza Plant Process Engineer, Erick Ernest (center) and TBL Mwanza Plant Utilities Engineer, Sunday Kidolezi (Right)
  TBL Mwanza Plant Utilities Engineer , Sunday Kidolezi (Left) and TBL Mwanza Plant Process Engineer, Erick Ernest (right) showing off all three regional awards they won on Resource Efficiency & Cleaner Production at the dinner gala awards ceremony at the Imperial Botanical Resort Beach hotel in Entebbe , Uganda earlier this month.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akipongezana na Balozi Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB mara baada ya kuzindua rasmi SITE ya Maonyesho ya Kimataifa Utalii ya Tanzania yanayojulikana kama Swahili International Tourism Expo (SITE) kwenye hoeli ya Serena Mwisho ni mwa wiki, Maonyesho hayo yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devotha Mdachi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)4a 
  Wageni wlikwa mbalimbali wakiangalia jinsi mabanda yatakayotumiwa na washiriki wa maonyesho yatakavyokuwa.6a 
  Msanii Wanne Star kushoto na kundi lake wakitoa burudani katika hafla hiyo.13aBurudani kutoka kundi la Wanne Star ikiendelea wakati wa hafla hiyo14a 
  Meneja wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena Katikati, Emmanuel Okware Meneja wa mauzo kutoka Quatar Airways kulia na mdau Juma Mabakila wakiwa katika hafla hiyo.15a 
  Baadhi ya wanahabari wakiwa katika hafla hiyo18a 
  Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo20a 
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Bw. Goefrey Tengenea wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na maofiza wenzake wa TTB wakati wa hafla hiyo.
   
  ................................................................................................
  (HOTUBA YA MH. WAZIRI RAZALO NYALANDU WAKATI WA UZINDUZI WA SITE)
  Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati, kwa wageni wote mliofika katika tukio hili muhimu ambapo nitatambulisha kwenu kuanzishwa kwa onesho jipya la utalii la kimataifa litakalojulikana kwa jina la Swahili International Tourism Expo (S!TE).

  1. Sekta ya Utalii ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hasa kwa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama vile usafirishaji, viwanda na biashara, kilimo, sanaa za mikono na kadhalika. Sekta ya utalii ina uwezo wa kuongeza ajira kwa haraka zaidi na inatambulika kwamba kila mtalii mmoja anapokuwa nchini huchangia takribani nafasi 12 za ajira za aina mbalimbali. 

  Aidha, Utalii ni tasnia muhimu katika kuongeza kipato na kupunguza umasikini, kukuza mahusiano ya kijamii na vile vile katika kutunza na kuendeleza maeneo ya kihistoria na maliasili. Hapa nchini, katika kipindi cha kati ya mwaka 2002 na 2013, utalii wa kimataifa umekuwa kwa zaidi ya asilimia 50%, kutoka watalii 575,000 mwaka 2002 wambao waliliingizia taifa Dola za Marekani milioni 730 hadi kufikia watalii 1,135,884 mwaka 2013 ambao waliingizia taifa Dola za marekani Bilioni 1.81.

  2. Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya maliasili na utamaduni vya kipekee. Kutokana na kuwepo kwa vivutio hivi, taasisi ya Kimataifa ya World Economic Forum katika taarifa yake ya ushindani kwenye tasnia ya Utalii (Travel and Tourism) imeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) duniani ikiongozwa na Brazili kwa kuwa na mazingira asilia yenye Urithi asilia wa kimataifa, wingi wa wanyamapori na ardhi kubwa iliyo hifadhiwa. 

  Hakika, ni ukweli usiopingika kwamba katika vivutio saba vya maajabu ya asili katika bara la Afrika, vitatu vinatoka Tanzania. Huu ni ushuhuda kwamba juhudi zetu za kuhifadhi mazingira zinazaa matunda. Hivi sasa Bonde la Ngorongoro; hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Mlima Kilimanjaro ni vivutio ambavyo vimeorodheshwa katika Maajabu saba ya asilia barani Africa.
  3. Hata hivyo, hatuwezi kutegemea tu uwingi na ubora wa vivutio hivi vya utalii peke yake. Ni muhimu kuongeza juhudi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili kujenga uelewa wa utajiri huu kidunia. Kama taifa, tunahitaji juhudi na mikakati zaidi ili kutangaza vivutio vyetu.

  4. Kwa kuzingatia umuhimu wa kuendelea kutangaza utalii wetu na kuifaya Tanzania iweze kushindana kimataifa, mnamo mwezi Februari, 2013, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), iliingia makubaliano na kampuni inayojulikana kama Pure Grit Project and Exhibition Management LTD, hapo mwanzo ilijukana kama Witch & Wizard Creative (Pty Ltd) ili kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa nchini Tanzania yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo -S!TE), ambayo yataanza rasmi Mwezi Oktoba, 2014. Pure Grit Project and Exhibition Management LTD ni kampuni inayoendesha maonesho ya utalii ya INDABA ambayo ni maonesho ya tatu kwa ukubwa duniani. 

  Onesho la S!TE litafanyika hapa Dar es salaam, mwezi Oktoba kila mwaka katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na kujikita zaidi katika kuvutia washiriki kutoka ndani nan je ya nchi.

  5. Mkoa wa Dar es Salaam umechaguliwa mahsusi kuwa eneo la kufanyika kwa onesho la S!TE kutokana na sehemu ulipo Mkoa huo kijiografia, na uwepo wa miundombinu bora na huduma nzuri zinazofaa kwa kuendesha au kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa.
  6. Hadi kufikia Juni 2014, hali ya maandalizi ya onesho hili ni kama ifuatavyo.

  6.1 Mwenendo wa idadi ya washiriki hadi sasa: Zaidi ya asilimia 50% ya nafasi za maonesho hayo tayari zimejazwa kwa kuchuliwa na makampuni binafsi na Bodi za Utalii za nchi mbalimbali. Aidha, kuna idadi kubwa na ya kuridhisha ya maombi ya washiriki inayoendelea kuandaliwa. Lengo ni kwamba ifikapo katikati ya mwezi Agosti, 2014 tuwe tumetumefikia asilimia 100.

  6.2 Programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii: Katika kuhakikisha kuwa onesho hili linakuwa ni fursa ya kuwaunganisha wafanyibiashara ya Utalii wa Tanzania na masoko ya Utalii, S!TE itakuwa na programu maalum (Hosted buyer and travel writer programme) ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii na waandishi wa habari za utalii (Tour Operators, Wholesalers, Packagers and Travel Agents and Travel Writers) na kuwapangia ratiba maalum ya kuonana na washiriki wa maonesho hayo ili kuwawezesha kuanzisha uhusiano wa kibiashara. 

  Mawakala hao wapatao ishirini na wandishi wa habari kumi watagharimiwa (hosted) na S!TE.Hadi kufikia Juni 2014,mawakala 13 kutoka Marekani, Australia, Ujerumani, Uholanzi, India, Mexico, Norway na China wamethibitisha ushiriki wao.

  6.3 Utangazaji wa Onesho la S!TE: Onesho la S!TE lina tovuti ijulikanayo kama www.site.co.tz. Tovuti hii imeandaliwa ili kukidhi maudhui ya onesho lenyewe ambapo inataarifa nyingi zinazoweza kumfanya yeyote anayetembelea tovuti hiyo kupata taarifa zote muhimu kwa muda mfupi. Kwa mfano tovuti inatoa taarifa za ukumbi wa onesho, mabanda ya maonesho yatayojengwa na kumruhusu mteja kuchagua eneo kulingana na uwezo wake. Aidha, tovuti hii ambayo pia imeunganishwa na ukurasa wake wa Facebook, inapatikana kwa lugha mbalimbali

  7. Pamoja na kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, S!TE ina lengo la kuunganisha wafanya biashara wa Utalii wadogo na wa kati wa Tanzania (Small and Medium Tourism Enterprises - SME’s), na masoko ya utalii ya kimataifa. Ni ukweli kwamba SME’s za kitanzania zina uwezo mdogo wa kimtaji wa kuweza kufikia masoko ya utalii ya kimataifa. Kupitia S!TE, hasa kupitia programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii, itasaidia katika kutatua changamoto hii.
  Naomba watanzania kuchangamkia fursa hii muhimu katika kukuza biashra ya Utalii nchini.

  0 0

   Afisa Michango kutoka PPF Makao Makuu, Bi Glory Maboya (kulia) akimpatia maelezo ya Huduma mbalimbali mmoja wa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipotembelea Banda la PPF katika Viwanja vya Mwl Nyerere maarufu kama Sabasaba.
   Mkazi wa Jiji la Dar Es Salaam akipatiwa maelezo juu ya huduma ya Fao la Kujitoa kutoka kwa afisa uendeshaji wa Mfuko wa PPF kanda ya Ziwa, Bi Grace Balele wakati mteja huyo alipotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba.
  Mchambuzi wa Mfumo wa Teknolojia (System Analysist) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Makao Makuu, Bi Irene Togolai akimpatia fomu ya Kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF mmoja wa Wakazi wa Jiji la Dar aliyetembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Kibiashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba
  Mchambuzi wa Mfumo wa Teknolojia (System Analysist) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Makao Makuu, Bi Irene Togolai akijibu maswali ya wateja wa PPF waliofika katika banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara za Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl Nyerere Barabara ya Kilwa, Jijini Dar Es Salaam.
   Happiness Mmbando , Afisa Rasilimali watu Utawala na Ushauri kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF akiwasikiliza kwa makini baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar waliotembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara za Kimataifa.
  Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam wakiuliza maswali kuhusiana na mfuko wa Pensheni wa PPF wakati walipotembelea katika banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar Es Salaam, Kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF kanda ya Temeke, Bi Jacquline Jackson

  0 0

  Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akifungua mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Malimu Nyerere Conference Centre jijini Dar es salaam kuzingumzia mambo mbalimbali kuhusu huduma hiyo ya bima ya afya, wadau waliohudhuria katika mkutano huo n kutoka wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni mkoani Dar es salaam, Lengo kuu likiwa kuhamasisha na wananchi kujiunga na mfuko huo na kufikia asilimia 30% ifikapo mwaka 2015, Pia kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa malengo hayo na kuzitatua.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)2 
  Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya Bw. Khamis Mdee akizungumza na kuelezea mikakati ya mfuko huo kwa wadau waliohudhuria katika mkutano huo leo.3Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Taifa Afya ya Jamii NHIF Balozi Ally Mchumo akimkaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wadau wa mfuko huo.4 
   
  Anjela Mziray (kushoto) Meneja masoko kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akisoma taarifa za mkutano huo ulipokuwa ukiendelea.11Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na viongozi wa mfuko huo wakipig picha na wadau mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo.12131415 

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dr. Eng. Binilith Satano Mahenge wa (kwanza kushoto) akizungumza na Balozi wa Ujerumani Mr. Hans Koeppel alipomtembelea ofisini kwakwe mtaa wa luthuli jijini Dar es Salaam, kuhusu mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaotarajia kufanyika julai mwaka huu mjini Berlin Ujerumani.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dr. Eng. Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Julius Ningu (wa kwanza kulia) wakiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani Mr.  Hans Koeppel kwa ajili ya Mazungumzo jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji kwenye makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwa Mkurugenzi Mkuu, ni Meya wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, Bakari Beji.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji kwenye makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwa Mkurugenzi Mkuu, ni Meya wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, Bakari Beji na Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Gabriel Silayo.
   Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (Kulia), akitoa maelezo kwa madiwani wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo, Bakari Beji, (Wanne Kulia), walipotembelea makao makuui ya PSPF jijini Dar es Salaam jana. Wasita kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Gabriel Silayo.

  0 0

  IMG-20140629-WA0000kikosi cha timu ya mpira wa miguu kutoka cho cha AJTC

  IMG-20140629-WA0001Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL akiongozana na meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Mega Trade Investment Godluck Kway kukagua timu ya netball ya chuo cha uandishi wa habari AJTC.IMG-20140629-WA0002

  IMG-20140629-WA0003Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa AJTC Bw. Alli Ahmedi akikabidhiwa kombe la ubingwa na Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL

  IMG-20140629-WA0004

  Timu za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, lililofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

  Katika bonanza hilo, ambalo mgeni rasmi alikuwa, Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto  jumla ya timu  10 zilishiriki na  liliandaliwa na Taswa Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique.

  Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha  uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.

  Mgeni rasmi Pinto ambaye pia ni Mjumbe wa bodi vya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa  soka alipewa kikombe, pamoja na fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.

  Mshindi wa pili wa soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe na fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.

  Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (TBL), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel,

  Timu zilizoshiriki ni Radio 5, timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na  Taswa Arusha  ambayo iliibuka na ushindi katika kukamata kuku.

  Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi  nzuri waliofanya.

  “Nachukuwa fursa hii kuwapongeza sana Taswa Arusha kwa kuandaa bonanza hili kwani halifanyiki sehemu nyingine nchini”alisema

  Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi TBL kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.

  Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kuendelea kulidhamini.(Pamela Mollel wa jamiiblog)


  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu yanaendelea japo kwa kiasi kikubwa hatma yake inategemea kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya. 

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Juni 30, 2014) wakati akizungumza na Mameya wa Majiji, Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya Tanzania katika kikao cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga. 

  Waziri Mkuu yuko Tanga kwa ajili ya sherehe za Serikali za Mitaa ambayo kilele chake kitafanyika kesho Julai mosi kwenye uwanja wa Tangamano jijini hapa. Ameamua kukutana na viongozi hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kukutana nao aliyoitoa Mei 14, 2014 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa ALAT. 

  "Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni kitendawili kwa sababu kwa kiasi kikubwa inategemea sana kukamilika kwa Mchakato wa Bunge la Katiba," alisema na kuongeza:"Kama Wizara tunaendelea na maandalizi tukiamini uchaguzi upo, kama hiyo fursa isipotokea bado tutakuwa tumekamilisha maandalizi kwa upande wetu.Tunaendelea kuandaa kanuni kwa kushirikisha wadau wote," alisema. 

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kusisitiza suala la ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali. Kuhusu mapato, Waziri Mkuu alisema katika mwaka wa fedha wa unaoisha sasa, hali ya ukusanyaji mapato haikuwa nzuri. 

  Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu alisema amewaandikia barua Wakuu wa Mikoa akiwataka waweke utaratibu wa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu juu ya makusanyo ya kila Halmashauri zilizo kwenye mikoa yao. 

  "Katika taarifa hizi itabidi kila Halmashauri ieleze ilipanga kukusanya kiasi gani, je imefikia lengo na kama sivyo ni kwa nini. Nia yetu ni kutrack down makusanyo na kuona yamekwama wapi na yamekwamishwa na nini," alisema. 

  Kuhusu udhibiti wa matumizi, Waziri Mkuu aliwataka Mameya na Wenyeviti hao kuendelea kuwabana wahusika ili kudhibiti matumizi yasiyofaa. "Lazima muendelee kuwabana na kuwasimamia wakurugenzi na wataalaam wa kwenye Halmashauri zenu. 

  Fanyeni kazi kwa ufanisi, msiwachekee wale wanaoharibu," aliongeza."Ili muweze kuwabana vizuri, ni lazima mdai kupatiwa taarifa za fedha kutoka kwa Mkaguzi wa Ndani (Internal Auditor)... kuna baadhi ya watendaji wanadai kuwa hizi taarifa ni siri wakati siyo siri," alisema.Aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kwamba taarifa hizo ni muhimu kwao kuzipata na zitawasaidia kuonyesha mapungufu yoyote kama yapo. 

  Aliwataka kila mmoja wao kwa nafasi zao za Meya na Mwenyekiti wahakikishe wanalenga kupandisha pato la wananchi wanaowaongoza.
  (mwisho)
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, JUNI 30, 2014

  0 0

  Na Hariet Shangaei Washington DC .
  Ndugu WanaDMV, kwa heshima na taadhima nachukua nafasi hii kujitambulisha kwenu rasmi kama Mgombea wa Nafasi ya Makamu wa Raisi wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
  Hariet Shangarai, Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Raisi wa Jumuiya ya Watanzania DMV alipokuwa katika kampeni.
  Nikiwa na mapenzi ya dhati kwa jamii,nimekuwa mtetezi wa haki za watoto yatima toka utotoni mwangu. Binafsi, nilijitoa kwa kidogo nilichokuwanacho na pia, nimekuwa muhamasishaji wa misaada ya elimu,chakula mavazi na malazi kwa watoto yatima. Kwa ufupi nimeona mafanikio ya kina, japo bado wahitaji ni wengi.
  Vile vile, nilikuwa mstari wa mbele katika uanzishwaji wa Kikundi cha Wanawake cha Kupambana na Ukimwi “KIWAKUKI”.Chombo hiki kimedumu takribani miaka 25 na kinaendelea kusaidia wengi nchini Tanzania kikishirikina na mashirika mbali mbali duniani. 
  Nikiwa Mwanadiaspora nimepitia changamoto nyingi za afya na huduma zake. Jambo ambalo lilinishawishi kuingia taaluma ya afya ili niweze kuwa msaada kwa jamii. Jitihada hizi zimenipelekea kuanzisha blog yenye kutoa elimu afya kwa jamii kwa lugha ya kiswahili“NesiWanguBlogspot.com”. Nia ni kuleta mwamko katika uwanja wa afya na huduma zake.
  Hariet Shangarai (NesiWangu Mynurse) mtowaji wa huduma za afya DMV, alipokuwa akipata picha ya pamoja na mhudumiwa baada ya maangalizi ya afya bureDMV siku ya Jumamosi April 12, 2014.
   
  Zaidi, nimejihusisha na zoezi la utafutaji wa Maangalizi ya Afya kwa wanaDMV. Zoezi hilo lilikuwa jaribio la ufumbuzi wa matatizo ya fya kwa Wanadiaspora. Nashukuru kwa mchango wa kila mmoja wenu na ninaomba Wanadiaspora wa vitengo vya afya kuwa mstari wa mbele katika kujali afya za jamii yetu.

   
  SERA ZA MGOMBEA;
  Jumuiya na Watoto;
  Jumuiya iwe ni chombo cha kuunganisha watoto wa Kitanzania kwa kuweka taratibu za shuguli endelevu zitakazowakutanisha watoto wetu kupitia michezo na vipaji vyao mbali mbali, ili kuwapatia uwanja wa kujitambua na kung’ara katika jamii yao
  Kuhamasisha watoto wetu kushiriki katika vikundi mbali mbali vinavyotoa mafunzo ya lugha, tamaduni na historia ya nchi kama “Dasara la Lugha ya Kiswahili”, “Tanzania Youth Diaspora & Friends” na vikundi vingine mbali mbali.
  Kushirikisha Wazazi na Wakufunzi wa vijana ili kutoa mafunzo na mwongozo kwa watoto wa kiume na wakike pale wanapoingia katika umri wa ujana (Adolescence). Lengo ni kuwaelimisha na kuwatahadharisha vijana wetu kuhusu changamoto mbali mbali za ujana na matokeo ya maamuzi yasiyo sahihi .
  Jumuiya na Vijana;
  Kutoa mwongozo na msaada kwa vijana wetu, ili waweze kusimama Kielimu na Kiuchumi, na kuishi katika Maadili yanayokubalika na sheria za nchi.
  Kufuatilia upatikanaji wa nafasi za udhamini (scholarship) kwa vijana, ajira, misaada na mikopo inayotolewa kwa wajasiriamali wadogo wadogo hapa nchini.
  Kuwakilisha na kuhamasisha wanaDMV kushiriki mikutano inayohusu sauti za wahamiaji watokao bara la Afrika kama vile “African Affairs Advisory Group” (AAAG),Montgomery county, “Office on African Affairs”( OAA), DC nk. Hii itawezesha sauti zetu kuwakilishwa kwa County Executive na DC Mayor ambao wana malengo ya kuimarisha jumuiya za Waafrika katika maswala ya uchumi,elimu ,afya na utamaduni. (Tutambue kuwa, mchango wetu wa uchumi ni mkubwa na unatambulika na serikali ya nchi)
  Kuhamasisha vijana kushiriki katika mikutano na fursa za elimu zinazosimamiwa na utawala wa Rais OBAMA kwa maendeleo ya Afrika kupitia “Young African Leaders Initiative” (YALI). 
  Kutafuta ufumbuzi na msaada kwa wanaDMV walio katika mazingira magumu; kama vile, wajane na dada zetu wanaojikuta katika mahusiano gandamizi hapa nchini.
  Jumuiya na Wazee;
  Kuwa na siku maalum ya kuwaenzi wazee wetu DMV na kuwapa uwanja wa kutoa hoja zao ili kuzitafutia ufumbuzi. Kutambua mchango wa wazee waliotutangulia na kuwa wa msaada pale wanapotuhitaji
  Kuwashirikisha katika shughuli zote na kutambua nafasi yao kama walezi wa jamii
  Jumuiya na Afya;
  Kushirikiana na wanaDMV wa kitengo cha afya ili tuweze kutoa msaada endelevu kwa wanaDMV.Kutoa taarifa na mafunzo endelevu ya elimu afya kwa jamiiKufahamisha WanaDMV kuhusu huduma msingi za jamii zipatikanazo hapa nchini.
  Kuhamasisha wanaDMV kupata bima mbali mbali zitakazo wawezesha kukabiliana na mabadiliko mbali mbali ya maisha kama magojwa,majanga, uzee na kifo
  Mwisho, kukumbushia wanaDMV umuhimu wa kuandika wosia (Advance directives), ili kuondoa msuguano endapo kifo kitatokea.
  Jumuiya na Sheria;
  Kupata Mwanasheria atakayehudumia wanaDMV kwa bei nafuu na kutoa ufafanuzi wa sheria katika maswala ya uhamiaji, ajira, mahusiano na ndoa.
  Jumuiya na Tabaka;
  Jumuiya iwe ni chombo kisichofungamana na upande wowote kwa kuwaunganisha wanaDMV na kuwashirikisha bila upendeleo katika fursa mbali mbali zinazojitokeza katika jamii yetu.
  Wapendwa wanaDMV, nipo tayari kutoa ushirikiano wangu kwa Viongozi woote watakaochaguliwa na kushirikiana na makundi yote bila kujali jinsia, dini,itikadi za vyama au kabila
  Tukiweza Kufanikiwa Ugenini , Tutafanikisha na Nyumbani pia.
  Naombeni Kura Zenu !.
  Asanteni sana

  0 0

  With a big live concert the Zambian Afro-Jazz songstress Yvonne Mwale released last Saturday her latest record "Ninkale – Let It Be" in Frankfurt (Germany).

  Though still new to Germany Yvonne Mwale managed to mobilise a large crowd of people to attend at 'Das Bett', a popular place for live concerts in Frankfurt. After one of Germany's biggest entertainment magazines featured Yvonne with a full page article a good number of locals became curious to see what the African Star had to offer. 
   
  Those who joined were not disappointed: for two and a half hours Yvonne Mwale rocked the place and kept the crowd dancing all night long, cheered by an excited audience. To maintain the African originality Yvonne had 'Sir' Jones Kabanga from Zambia and 'Twaba' from Tanzania on stage. Since the concert was a record release concert the new album 'Ninkale' was for the first time on sale that night. Most visitors decided to go home with their own copy after watching a convincing performance of the whole band. Many of them queued up the get their copy signed by the artist.

  When asked about how she feels about her new album Yvonne had to say: "Working in such a studio with only professional musicians was a new experience for me. But it helped me to extend my limits further. It's great after all that work to see the album finally out and selling. Now, after performing my first major concert here in Germany after the 2010 tour I'm excited to see all the people here. It's good to see that even in Europe the audience loves our Africa music and I will give my best to reach a wider audience with it."

  The album was previously recorded in the Art Of June Studios, one of the major german recording studios that allows to record full bands live. The 14 tracks of the album feature besides the Zambian guitar legen 'Sir Jones' also the Tanzanian percussionist Twaba, the danish saxophonist Bobby Ricketts as well as musicians from Germany that usually perform with German superstars like Xavier Naidoo and Glashaus. To get the final polish, the album was after mixing sent to Switzerland for mastering.

  With her latest album Yvonne Mwale is further establishing her position in the global World Music scene. First reviewers have been excited about the artistic and technical quality that take Zambian music to a whole new level. The album is available in all popular music stores and streaming services around the world (e.g. iTunes, Amazon, Google Play, Spotify, Deezer and many more).

  In July Yvonne will perform at the Africa Festival in Stuttgart (Germany). Further shows later this year are in preparation.


  A short video documentary about the making of the album is available here: https://www.youtube.com/watch?v=OB5siXT6iUY  0 0


   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Kituo cha Taifa cha Utunzaji  Kumbukumbu (NRC) Dodoma leo (jana).
   Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue  (hayupo pichani) katika Kituo cha Taifa cha Utunzaji Kumbukumbu (NRC) Dodoma.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (wa kwanza kulia) katika moja ya sehemu za kuhifadhi kumbukumbu katika Kituo cha Taifa cha Utunzaji Kumbukumbu, kushoto kabisa anayetoa maelezo  ni Mkurugenzi Msaidizi Utumishi Bw. Joseph Ndauka.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (kushoto), pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi wakipitia moja ya jalada lililofunguliwa mwanzoni mwa miaka ya 60.

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu Mradi wa Chuma Liganga kutoka kwa Nie Zhiyan (kulia), ambae ni Makamu Afisa Muendeshaji Mkuu wa Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL). Hili  ni eneo ambalo kiwanda cha chuma chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kitajengwa. Kutoka kushoto, wengine ni Bw. Ramson Mwilangali, Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama - NDC , Bw. Erasmus Masumbuko, Mchumi - Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, anaeshughulikia Sekta za Uzalishaji, Bw. Israel Mkojera Makamu Meneja Utawala - TCIMRL, Bi. Florence Mwanry Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anaeshughulika na Huduma za Jamii na Idadi ya Watu na Bw. Mlingi E. Mkucha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC.
   Kilima  chenye madini Ya chuma, ambapo  shughuli ya uchimbaji wa chuma unategemea kuanza kutekelezwa. Uzalishaji wa chuma unatarajiwa kuanza mwaka 2016.
   Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika eneo ambalo uchimbaji wa chuma utatekelezwa. Pamoja nao ni Viongozi kutoka National Development Corporation (NDC) na Tanzania China International Mineral Resources Ltd. Nyuma ni kilima ambacho kimejaa utajiri wa mawe yenye madini ya chuma ambapo jiwe linakadiriwa kuwa na chuma kwa 52%.
   Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), National Development Corporation (NDC) na Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMR) wakiwa pamoja na viongozi wa kijiji cha Mundindi ambapo ni eneo ambalo Mradi wa Uchimbaji wa Chuma utatekelezwa. Viongozi hawa pamoja na wanakijiji wameonyesha ushirikiano mzuri na mwekezaji katika kufanikisha utekelezaji wa mradi.
   Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wa kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd kuhusu Iron Ore Samples zilizopatikana wakati wa utafiti kuhusu wingi na ubora wa chuma kitakachopatikana katika eneo la Liganga.
  Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Dkt. Philip I. Mpango (aliyesimama) akiongea na Viongozi wa Kijiji cha Mundindi pamoja na viongozi na wataalam wa kampuni ya Tanzania China International Mineral Resorces Ltd. Picha na: Thomas Nyindo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma  Pinto akiwa akiwa anakagua timu ya mpira wa pete kutoka AJTC kabla ya mechi ya fainaili kuchezwa katika Uwanja wa Kumbukumbun ya Sheikh Amri Abeid, Arusha.
  washabiki wa timu ya AJTC wakiwa wanashangilia mara baada yakukabidhiwa kombe katika bonanza la Taswa.
  Kwa picha zaidi na Woinde Shizza BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   hawa ndio washindi wa redd's miss kanda ya kaskazini kwa mwaka 2014

   hawa ni wadhimini wa shindano hilo kutoka minjingu.

  LEMUTUZ nae alikuwemo ndani ya Redd's miss kanda ya kaskazini  bila kumsahau mwenyekiti wa Taswa Juma pinto.


   mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na mkuu wa mkoa wa Manyara waliuthuria katika usiku huo wa kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini ambapo katika shindano hilo warembo wanne wamwanzo watakingia katika kambi ya Redd's miss Tanzania
   Mh hashimu Lundenga akiwa anatangaza washindi wa tatu bora
   warembo wakiwa wameingia ukumbini wakicheza wimbo wa ufunguzi.

   papa mwandago akimwaga maneno akiwa kama muandaaji mkuu wa shindano hili.
   hawa ndio warembo walioingia tano bora.
   waandaji wa shindano hilo wakiwa wamekaa kwa mapozi wakifuatilia shindano.PICHA zote na libeneke la kaskazini blog


  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Oparesheni wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Eugen Massawe (kushoto) akikabidhi moja ya tuzo zinazotolewa kila mwaka na AIESEC kwa Rais wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) Bw. Abubakar Ahmed (kulia) wakati hafla ya kila mwaka ya wadau wa taasisi ya wanafunzi ya AIESEC iliyofanyika jijini mwishoni mwa wiki.

   Mkuu wa Kitengo cha Oparesheni wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Eugen Massawe (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Majanga na Udhibiti wa Benki hiyo Bw. David Lusala (kulia) katika picha ya pamoja wakati hafla ya kila mwaka ya wadau wa taasisi ya wanafunzi ya AIESEC iliyofanyika jijini mwishoni mwa wiki
  Mkuu wa Kitengo cha Oparesheni wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Eugen Massawe (kushoto) akikabidhi moja ya tuzo zinazotolewa kila mwaka na AIESEC kwa Rais wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) Bw. Abubakar Ahmed (kulia) wakati hafla ya kila mwaka ya wadau wa taasisi ya wanafunzi ya AIESEC iliyofanyika jijini mwishoni mwa wiki. Wakishuhudia ni wanafunzi wa chuo cha IFM, Hafifa Bahfif (katikati), Said Yusuf (wapili kulia) na Erick Justice (wa kwanza kulia).

  0 0

  Mzazi wa mtoto Idda Baitwa,Bw Respcius Baitwa akifanya maandalizi na mwanae ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya
  kupanda Mlima Kilimanjaro
  Mtoto Idda Baitwa akiwa na baba yake mzazi Bw Respcius Baitwa pamoja na ndugu zake wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya
  kupanda Mlima Kilimanjaro.
  Mtoto Idda Baitwa akijiandikisha katika lango la Umbwe la kupanda mlima Kilimanjaro kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.nyuma yake ni Bw Respicius Baitwa akshuhudia.
  Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtoto Idda Baitwa ikaanza.
  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

  MTOTO wa miaka tisa(9) Idda Baitwa ameanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na umri mdogo zaidi huku akitumia njia ya Umbwe ambayo inaaminika kuwa ngumu zaidi kwa watalii wakati wa kupanda mlima huo.


  Msichana huyo mwanafunzi wa darasa la nne, katika shule ya msingi Mnazi iliyoko Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro alianza safari hiyo Juni 28, mwaka huu ambapo ikiwa atafanikiwa kufika katika cha mlima huo atakuwa amaeweka rekodi mpya.


  Akizungumza na Globu ya jamii wakati akianza safari ya kupanda mlima huo, katika lango la kupandia la Umbwe-Kibosho, Idda alisema matarajio ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mtanzania wa kwanza kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro katika umri mdogo kwa kupitia njia ngumu huenda sasa yakatimia.


  Idda, alisema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuupanda mlima huo kama njia ya kuthibitisha uzalendo wake ambapo pia anaamini kwa kufanya hivyo atakuwa ametoa hamasa kwa watanzania wengine hususani wanawake kutembelea vivutio vya ndani.


  Alisema ameamua kufuata nyayo za Baba yake ambaye tayari kwa sasa anajiandaa kuweka rekodi ya kuwa mtanzania na mwafrika wa kwanza kupanda vilele saba virefu katika mabara yalioko duniani ambayo hadi sasa ameshapanda vilele vinne.


  "Nimekuwa nawaza juu ya azma yangu ya kuwa wa kwanza, nimekuwa nikimuona Baba akipanda milima nikawa natamani sana kufanya hivyo, nimechagua Njia hii ngumu kuliko zote kwa sababu nataka kuwaonesha watanzania wenzangu kwamba tunaweza na sio kuwaachia wageni pekee," alisema Idda.


  Akizungumzia hatua ya Binti yake huyo  Baba mzazi wa Idda ,Respicious Baitwa aliishauri serikali kupitia wizara ya elimu kuweka msisitizo kwa wanafunzi mashuleni na vyuoni kutembelea hifadhi za taifa ili kujionea vivuito mbalimbali sanjari na kuwajengea hali ya uzalendo wa kupenda vitu vya
  nyumbani.


  Alisema ipo haja kwa serikali kupitia wizara ya elimu kuelekeza nguvu kwenye shule za msingii na vyuo kuwahamasisha wanafunzi kupanda mlima kilimanjaro kwa lengo la kuongeza hamasa ya watanzania kujitokeza kufanya utalii wa ndani.


  "Sekta ya Utalii ina kazi kubwa sana ya kufanya, sio sekta hii tu hata Wizara ya elimu nadhani ni muda mwafaka sasa inatakiwa kujipanga na kuanza kuhamasisha wanafunzi mashuleni kupenda kutembelea vivutio vyetu, ipo haja ya kuongeza katika mnasomo mashuleni somo la utalii wa ndani na sio kuzungumza tu kwebnye vyombo vya habari," alisema Baitwa.


  Kwa upande wake, LightnessSebastian, ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Mmbee iliyopo wilaya ya Mwanga, ameiomba wizara ya elimu kuongeza somo la utalii wa ndani katika mitaala ya elimu kwa lengo la kuwapa wanafunzi uelewaa wa utalii wa ndani

  0 0

  Wananchi wengi hawana matarajio makubwa ya watoto kujifunza shuleni
  Wazazi watathmini ujuzi wa watoto japo ni wa chini ila kwa usahihi.
  na wala hawaoneshi kudai kubadili hali hii katika siku zijazo

  Mwananchi 1 tu kati ya 10 ndiye anayefikiri kuwa watoto wengi wanaomaliza darasa la 2 wana uwezo wa kusoma na kufanya hisabati wa darasa hilo hilo (ngazi ya darasa la 2). Mbaya zaidi, wananchi 3 tu kati ya 10 (31%) wanafikiri kuwa watoto hawa wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma na kuhesabu kwenye ngazi yao; ikimaanisha kuwa wananchi hawana matumaini kama kweli mfumo wa elimu utawafundisha watoto ujuzi na stadi wanazotakiwa kupata wakiwa shuleni.

  Matokeo haya yalitolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Nini kinaendelea kwenye shule zetu? Wananchi watafakari juu ya hali ya elimu. Muhtasari huu umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa ambao unauwakilishi wa kaya zote Tanzania Bara.

  Muhtasari huu unachunguza hali ya shule zetu, ufundishaji na ujifunzaji pamoja na ushiriki wa wazazi kwenye elimu ya watoto wao. Licha ya matarajio ya chini kwenye mfumo wa elimu, wazazi mara nyingi hutimiza wajibu wao kuhamasisha na kusimamia ujifunzaji. Wanafunzi 7 kati ya 10 waliripoti kuwa wazazi wao hupitia na kukagua madaftari yao mara kwa mara.

  Walimu wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanajifunza shuleni. Hata hivyo, hawawezi kufanya kazi hii kama walimu wenyewe hawaingii darasani. Wanafunzi 3 kati ya 10 walithibitisha kuwa mwalimu wao muhimu aliingia darasani vipindi vyote siku iliyopita. Wanafunzi 4 kati ya 10 (38%) waliripoti kuwa mwalimu wao hakuingia darasani siku nzima, na wanafunzi 3 kati ya 10 (28%) walisema kuwa, mwalimu aliingia baadhi ya vipindi tu vya siku hiyo.

  Sauti za Wananchi iliuliza pia maswali kuhusu hali ya mazingira ya shule. Karibu wanafunzi wote (99%) wanafundishwa wakiwa madarasani, siyo nje, na wanafunzi 9 kati ya 10 (91%) hukaa kwenye fomu au dawati shuleni. Hata hivyo, ni nusu tu ya idadi ya wanafunzi (49%) waliosema hupewa chakula shuleni. Ingawa kukosekana kwa viti na madarasa kuna uwezekano wa kuathiri viwango vya kujifunza, watoto wanapokuwa na njaa wanakuwa na uwezo mdogo kupokea na kumiliki maarifa mapya.

  Njia nyingine ambayo watoto huhifadhi maarifa ni kupitia kazi za masomo kufanyia nyumbani. Kazi hizi za masomo nyumbani husaidia wanafunzi kukumbuka na kupitia upya masomo ya siku hiyo na kufanya mazoezi elimishi ya yale waliyojifunza akiwa mwenyewe. Hata hivyo, wanafunzi 7 kati ya 10 (69%) waliripoti kuwa ni mara chache sana (au hawapewi kabisa) kazi za masomo za kufanyia nyumbani. Wakipewa kazi za masomo nyumbani, wanafunzi walisema kuwa mara nyingi kazi hizo husahihishwa.

  Hivi karibuni Tanzania ilizindua Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mpango huo umeiweka sekta ya elimu kuwa moja ya vipaumbele vyake muhimu. Sauti za Wananchi iligundua kuwa ni mtu 1 tu kati ya 7 (16%) ndiye aliyewahi kusikia kuhusu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

  Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Utafiti wa Serikali na utafiti wetu (Uwezo) umeonesha kuwa watoto wako shuleni lakini hawajifunzi. Utafiti huu pia umegundua hali ya kutisha- theluthi mbili ya walimu hawaingii madarasani kwa siku nzima au baadhi ya vipindi. Hali mbaya ya mfumo wetu wa elimu sasa ni jambo la kawaida kiasi kwamba wazazi hawatarajii kama watoto watajifunza stadi wanaopaswa kujua. Kama tutaendelea katika hali hii, tutakuwa na kesho isiyo na mafanikio. Ingawa mpango kama BRN unatafuta kuinua ubora wa elimu, haiko wazi masuala gani ni kipaumbele muhimu kwa hali ya sasa."

  "Kila shilingi inayotumika kwenye elimu inaweza kutumika mara moja tu. Kama raia wa nchi hii tunapaswa kudai kuwa sera zote za elimu, jitihada, vitendo na hatua kwa uaminifu kabisa zijikite kuboresha matokeo ya kujifunza. Bila kufanya hivyo, hakuna uhakika kwamba thamani ya fedha itapatikana. Kwa maneno mengine, watunga sera wanapaswa kutumia ushahidi kuwashawishi walipa kodi, Washirika wa sekta na wanasiasa kuwa fedha za kodi zinatumika kwenye sera zinazoleta manufaa na ambazo "zinanunua" matokeo ya kujifunza.”

older | 1 | .... | 310 | 311 | (Page 312) | 313 | 314 | .... | 1898 | newer