Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 309 | 310 | (Page 311) | 312 | 313 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyata International Convention Centre hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya. Kushoto kwa Rais Kenyata ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Mheshimiwa Kyriakos Gerentopoulos. Ujumbe wa Tanzania ulishirikisha pia Mhe. Janet Mbene (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (aliyevaa gauni la kijani).

   Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara akimshukuru Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre jijini Nairobi, Kenya.  Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), na Rais wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika, Carribean na Pacific akiongoza Mkutano wa 99 wa Baraza hilo la Mawaziri. Kushoto kwake ni Mheshimiwa Adan Abdulla Mohamed, Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya akifuatilia mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre, Nairobi Kenya.

  0 0


   Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifatilia mada mjini Dodoma leo.
  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga  kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa  za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi hiyo.

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
  “Mpaka sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha taarifa za watumishi wao  wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu” alisema Bw.Robert.

  Alisema, mwajiri atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi kwa wakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja. Aidha,Bw. Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa 18 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

  Bw.Robert alifafanua kuwa ili kufanikisha zoezi la urejeshaji  mikopo kutoka kwa wadaiwa,  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatunga sheria na mifumo  mbalimbali ya kuwadhibiti wadaiwa hao. “Tunatengeneza sheria ambazo zitawazuia wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kupata hati ya kusafiria nje ya nchi au kibali cha kusafiri hadi atakapowasiliana na Bodi.”

  Pia,alisema mhitimu atakayeshindwa kulipa mkopo taarifa zake zitatangazwa kwenye vyombo vya habari na kwenye taasisi za mikopo ili asipate huduma yoyote ya kifedha.

  Naye, Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Dk. Veronica Nyahende amewataka wahitimu wa elimu ya juu nchini kutumia elimu waliyonayo kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa. Alisema changamoto ya kurejesha mikopo  ni kubwa kwa upande wa wahitimu wa elimu ya juu ambao hawana kazi ama hawajajiajiri.

  “Changamoto iliyopo ni wahitimu kushindwa kulipa mikopo hiyo kutokana na kuwa na kipato cha chini ama kukosa ajira.” Alisema Bodi imeingia mkataba na kampuni zitakazokusanya mikopo kwa walionufaika na mikopo hiyo na kushindwa kuilipa .  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iko katika mchakato wa kuelimisha umma na watendaji wakuu Serikalini ili kuhakikisha wanawasilisha taarifa za watumishi wao wanaodaiwa mikopo hiyo.

  0 0
 • 06/28/14--04:05: KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA
 •  Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akitambulishwa na Mbunge wa  Hanang na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Ukezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary (kulia) kwa Wananchi kutoka jimbo hilo waliotembelea Bunge mjini Dodoma Junu 27 kwa mwaliko wa mbunge wao.
    Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge  kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma juni 27, 2014. Kutoka kushoto ni Martha Mlata wa Viti Maalum,Tundu Lissu wa Singida Masharikina na Felister Bura wa Viti Maalum. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu).
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiteta na Mbunge wa Mbinga Magharibi Cpt. John Komba, Bungeni Mjini Dodoma Juni 27, 2014.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge Samuel Sita wa Urambo Masharikiambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki (katikati) na  Mbunge wa Tabora mjini Aden Rage kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Juni 27, 2014.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako Rais alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria).
    Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) akifafanunua jambo kwa Rais Kikwete walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako, Rais Kikwete alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria).
  Picha ya pamoja.Picha na Ikulu

  Rais Kikwete aliwapongeza sana watafiti hao pamoja na taasisi ya IHI kwa kuiletea sifa Tanzania katika fani ya utafiti nje ya nchi.Watafiti hao wako Equatorial Guinea (EG) kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi wa utafiti wa chanjo ya malaria iitwayo PfSPZ na kuwafunza wenzetu kuhusu maarifa ya fani hii ya utafiti wa chanjo ya malaria.

   IHI ni shirika la utafiti lenye kufanya tafiti za afya nchini Tanzania lenye uzoefu wa miaka zaidi ya miaka hamsini. Mfano mmoja wa mafanikio yake ni utafiti uliopelekea vyandarua vyenye dawa kutumika kama moja wapo ya njia za kujikinga na malaria nchini Tanzania. Tunafanya kazi pamoja madaktari na wataalamu kutoka Wizara ya Afya ya EG, shirika lisilo la kiserikali la Marekani liitwalo MCDI (Medical Care Development International) na Sanaria ambao ndio watengenezaji wa chanjo hiyo ya malaria.

  Mradi huu wa utafiti  unagharamiwa na serikali ya EG pamoja na sekta binafsi za mafuta. Mradi huu wa miaka mitano una lengo la kuchunguza kuhusu uwezo wa chanjo hiyo kukinga dhidi ya ugonjwa wa malaria. Ushirikano huu ni mmoja ya mfano wa mashirikano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kutafuta njia bora za kukinga maradhi katika jamii. Vilevile ni moja ya kielelezo kizuri cha jinsi gani nchi za kusini zinaweza kushirikiana katika taaluma mbali mbali (south south corporation).

  Tumepata fursa ya kukutana na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshima Jakaya Mrisho Kikwete Malabo na kumueleza kuhusu kazi tunayofanya na changamoto mbalimbali zinazotukuta pamoja na kutoa ombi kwa mheshimiwa Rais kusahilisha mashirikano kati ya nchi mbili za Tanzania na Equatorial Guinea kupitia Wizara za Afya na Tume za Sayansi na technologia za nchi hizi mbili. Hili litafanya utelekelezaji wa mashirikiano hayo kuwa bora zaidi kwa lengo la kunufaisha nchi zote mbili.

  Mashirikiano haya ni fursa ya watanzania kuwafunza wenzao pamoja na wao kujifunza kutokana na mashirikiano hayo. Utafiti huo pia utasaidia juhudi za kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kufanya tafiti zenye lengo la kutafuta chanjo bora ya malaria pamoja na njia bora za kusambaza chanjo hiyo kwa nchi zote mbili kama itakuwa ni yenye mafanikio.

  0 0

   Mgombea wa nafasi ya urais Evans Aveva, akiwa na Mlinzi wake 'Board Guard' (nyuma) akijinadi kwa wanachama, wakati wa mkutano wake wa kampeni za mwisho na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo kesho, kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuiongoza Klabu ya Simba kwa kipindi kijacho cha miaka minne. Hitimisho hilo la kampeni zake limefanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
   Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, akimnadi mgombea Urais Evans Aveva.
   Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
   Baadhi ya wanachama wa Simba waliohudhuria mkutano huo.
   Baadhi ya wazee wa Simba waliohudhuria mkutano huo.


   Meza kuu....
  ***********************
  *Amwaga sera kabambe, kula sahani moja na mafisadi, makomandoo


  Na Majuto Omary

  WAKATI Kampeni za uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba zikifungwa rasmi leo kuelekea zoezi kamili la uchaguzi huo linalotarajia kufanyika kesho (Jumapili) kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, mgombea anayepigiwa ‘chapuo’ kubwa na wanachama wa klabu hiyo katika nafasi ya Urais, Evans Aveva amemaliza kampeni zake kwa kishindo na kutoa ahadi ya kula sambamba na Makomandoo na mafisadi wanaoihujumu klabu hiyo.


  Mbali ya ahadi hiyo, Aveva pia amesema, iwapo atapewa ridhaa ya kuiongoza Simba, atarudisha heshima ya klabu hiyo kwa kutwaa ubingwa na kushiriki mashindano ya kimataifa kwa kusajili wachezaji bora wazawa wenye uwezo na kuongeza wageni iwapo watahitajika baada ya kukosa mzawa wa kumudu nafasi husika. 
  Akizungumza katika mkutano wake wa mwisho uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency Kulimanjaro, Aveva alisema kuwa atatumia vyombo vya sheria kupambana na wauzaji bidhaa za klabu hiyo wanaotumia nembo ya Simba ili kukusanya mapato ya klabu kwa ajili ya kutumika katika maendeleo ya klabu.


  Aidha, Aveva alisema kuwa katika kuhakikisha anaondoa mianya hiyo, atatumia matawi ili kukamata bidhaa hizo na lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuweka utaratibu ambao utaiwezesha klabu hiyo kujikusanyia mapato na kuweza kujitegemea.

  “Bidhaa zenye nembo ya klabu zinauzwa kiholela na kufaidisha wachache huku klabu ikiendelea kuwa tegemezi, mimi sitavumilia hali hiyo na nitahakikisha nakula nao sahani moja ili kuokoa klabu,” alisema Aveva.

  Alisema kuwa uongozi wake utakuwa wa kushirikisha zaidi Matawi na ataunda kamati mbali mbali ili kuweza kufanikisha mpango mkakati wake wa kuendeleza klabu.

  “Sitaweza kufanya kila kitu mimi, nitaunda kamati ambazo zitawajibika katika kamati ya utendaji na kufanya majukumu hayo, lengo kubwa ni kufikia lengo na kuhodhi madaraka, nitafanya hivyo kwa maendeleo ya klabu na wala si vinginevyo,” alisema.


  Pia alisema kuwa atasajili wachezaji ambao wataiwezesha timu hiyo kufanya vyema katika ligi na kurejesha hadhi na heshima yake ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

  Uchaguzi huo utashirikisha jumla ya wagombea 27 ambapo mbali na Aveva, nafasi hiyo pia inagombewa na Andrew Tupa. Wagombea  wengine ni Swedi Mkwabi, Bundala Kabulwa , Geofrey Nyange na  Jamhuri Kihwelo ambao wanagombea nafasi ya makamu Rais.


  Wanaowania ujumbe ni Said Tulliy,  Yasini Mwete, Ally Suru,  Rodney Chiduo,  Said Pamba,  Ally Chaurembo , Abdulhamid Mshangama , Chano Almasi,  Damian Manembe,  Ibrahim Masoud, Kajuna Noor,  Hamisi Mkoma,  Alfred Elia na Saidi Kubenea.

  Wagombea wengine ni Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid Abdallah na Collin Frisch. Wagombea kwa upande wa wanawake ni Asha Muhaji, Amina Poyo na Jasmine Badour.

  0 0

   Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila akijaribu kusukuma moja kati ya viti 33 vilivyotolewa na asasi ya MUVIMA kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Mufindi. Anayefurahi katikati ni mkurugenzi mwenza wa MUVIMA, Albert Chalamila akipongezwa na Katibu wa Afya wa Wilaya hiyo, Atupekisye Mwakifamba
  Albert Chalamila na baadhi ya wanahabari wakiangalia hali ilivyo ndani ya wodi ya wazazi ya hospitali hiyo; hapa wanaonekana baadhi ya wajawazito wanaolala chini kutokana na ukosefu wa vitanda

  Na Denis Mlowe,Mufindi  ASASI ya Mufindi Vijana kwa Maendeleo (MUVIMA) imetoa msaada kwa hospitali ya wilaya ya Mufindi yenye matatizo mbalimbali  kwa lengo la kusaidia kutoa huduma bora kwa kutoa viti 33 vya kubeba wagonjwa.

  Akikabidhi msaada huo hivi karibuni Kaimu Mkurugenzi wa MUVIMA, Albert Chalamila alisema asasi yao imeguswa na kero mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na kwa kuanzia ililazimika kutafuta viti hivyo kwa lengo la kusaidia hospitali hiyo yenye matatizo mbalimbali  yanayofifisha utoaji wa huduma bora za afya, zikiwemo zile za wajawazito na watoto,


  Alisema kwa msaada wa asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia waliomba msaada huo baada kuomba msaada wa vitanda kwa ajili ya hospitali hiyo hivyo vitanda 23 vimekwishawasili bandari ya Dar es Salaam na tumeanza na viti vya kubeba wagonjwa.


  Alisema Mkurugenzi Mkuu wa MUVIMA, Cosato Chumi anaendelea na utaratibu wa kuvitoa vitanda hivyo bandarini na mara baada ya shughuli hiyo kukamilika vitakavifdhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo.  Kaimu Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila kwamba vitapunguza adha waliyokuwa wanapata watoa huduma wa hospitali hiyo ya kupokea na kubeba mikononi, wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.


   Akishukuru kwa msaada huo, Dk Mlimbila alisema hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa vifaa tiba na dawa na akalitaja eneo lenye tatizo zaidi kuwa ni lile la huduma kwa mjamzito na watoto.

  Alisema katika kuboresha huduma za uzazi, jengo lenye uwezo wa kulaza wajawazito zaidi ya 100 na lenye chumba cha upasuaji na kile cha kuhifadhia watoto wanaozaliwa kabla ya muda lilijengwa katika hospitali hiyo ambayo awali ilikuwa ikitumia jengo lenye uwezo wa kuweka vitanda 27 tu.


  Alisema msaada uliotolewa na MUVIMA una umuhimu mkubwa katika hospitali hiyo kwani utarahisisha huduma za ubebaji wagonjwa kutoka eneo moja hadi lingine na utapunguza idadi ya wajawazito wanaolala chini baada ya vitanda vilivyoahidiwa kuwasili.


  Naye Katibu wa Afya wa wilaya hiyo, Atupakisye Mwakifamba aliwataka MUVIMA na wadau wengi kujitokeza kuzimaliza kero za utoaji huduma zinazoikabili hospitali hiyo na vituo vingine vingi vya huduma wilayani humo.

   Mwakifamba alisema pamoja na wilaya hiyo kuwa na idadi ya kuridhisha ya watoa huduma wenye ujuzi, inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa tiba, dawa na magari ya kubeba wagonjwa.
  0 0

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo (kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( wa pili kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
  ·Ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano nchini kuingia mkataba wa ushirikiano na Apple.

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma bora na nafuu leo imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi ya Apple.Airtel imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano nchini Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu huo jijini Dar es Saalam Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema” leo tunazindua  simu ya iPhone 5s na kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa mwezi. Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kutumbelea maduka yetu na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi, Beatrice Singano alisema “Uzinduzi huu leo utato fulsa kwa wateja wetu  kupata uzoefu tofauti wa huduma zetu na kuwawezesha  kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH on, huduma ambayo imezinduliwa ili kuwawezesha wateja wetu kupata internet yenye kasi zaidi bila kikomo kupitia mtandao wa Airtel”

  “Simu hii ya iPhone 5s itawawezesha wateja wetu pia kupiga picha, kutuma video na kuwaunganisha na marafiki na familia . Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ofa hii ya simu ya iPhone 5s tembelea tovuti yawww.apple.com/phone “aliongeza mmbando.
  <

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo.Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea. Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani). Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani)Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.

   KITUO cha Usuluhishi (CRC) kinachofanya kazi chini ya Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) kimejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kinapambana na matumizi ya pombe kupindukia kwa jamii suala ambalo limezidisha vitendo vya ukatili wa jinsia unaofanywa na watumiaji pombe kupindukia. 
   Akizungumza na wahariri wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka alisema utafiti uliofanywa na Shirika la IOGT International unaonesha kuwa kiwango cha unywaji pombe jijini Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake huku ikibainika kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya vitendo vya ukatili na matumizi ya pombe kupita kiasi. 

   Bi. Soka alisema takwimu zinaonesha kuwa wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha vipigo, kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77, huku kiwango cha ukatili kwa wanawake ambao waume ama wenzi wao hawanywi pombe ni asilimia 33. "...Utafiti uliofanywa na shirika la IOGT International unaonyesha kwamba kiwango cha unywaji pombe katika jiji la Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake...lakini takwimu kutokana na utafiti wa Demographia na Afya Tanzania (TDHS) 2010...unaonesha wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha kipigo/kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77," alisema. 

  Aidha aliviomba vyombo vya habari kushirikiana na TAMWA kutoa elimu kwa jamii kupunguza matumizi ya pombe kupindukia kwani licha ya ukatili huo familia pia zimekuwa zikiathirika kiuchumi juu ya matumizi ya pombe huku baadhi ya watoto wakikosa huduma za msingi kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao ni walevi kupindukia. Alisema TAMWA inatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaosababishwa na pombe huku lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha maisha ya wanawake na watoto yanaboreshwa kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia. 

  Hata hivyo alisema tayari chama hicho kimeanza kufanya utafiti mwingine katika Wilaya ya Kinondoni kuangalia madhara yanayotokana na unywaji wa pombe kupindukia ili kuangalia hali halisi ya matumizi ya pombe eneo hilo na madhara ambayo yamekuwa yakitokana na matumizi hayo. Alisema malengo mengine ya mradi ni pamoja na kuboresha maisha ya wanawake na watoto kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe katika wilaya ya Kinondoni na pia kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa pombe kupindukia. 

   Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA aliongeza kuwa mapambano hayo pia yatasaidia, kukabiliana na matumizi ya pombe na kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake unaotokana na matumizi ya pombe, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na ukatili unaosababishwa na unywaji wa pombe dhidi ya wanawake na watoto. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Malabo Equtorial Guinea ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) uliomalizika jana.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange Picha na Freddy Maro

  0 0
 • 06/29/14--01:08: SSebo ajiunga E fm

 • Mtangazaji maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a Ssebo amejiunga na Radio ya E FM ambayo imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo
  nchini.

  Ssebo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo
  hewani.    "Mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM",alisema Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika
  Radioni hapo.

  0 0

   Millard Ayo akipokea Tuzo ya Mtangazaji wa Radio wa kiume anayependwa mara baada ya kuibuka mshindi katika kipengele hiko
   Akiwashukuru Wadau waliompigia kura na kumpa sapoti
   Salim Kikeke kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC akiwashukuru wadau wake waliomuwezesha kushinda Tuzo 
  King Majuto akifurahi mara baada ya kuppokea Tuzo yake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kipengele cha Msanii Bora anayependwa wa Kiume.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili nchini Rose Muhando ameibuka na wimbo mpya uitwao Facebook. 

  Akizungumzia  wimbo huo, Rose amesema  ana imani wimbo huo utakuwa kivutio kikubwa kwa jamii hasa vijana kwa sababu una ujumbe mzuri ambao utagusa wengi.

  “Sitaki kuwaambia nimeimba nini, lakini Facebook ni wimbo mzuri na mashabiki wangu naamini wanatambua kwamba mimi si mtu wa masihara ninapotunga kazi zangu,” alitamba mwimbaji huyo.

  Alieleza kuwa wimbo huo utakuwa katika albamu yake mpya iitwayo Kamata Pindo la Yesu anayotarajia kuizindua jijini Dar es Salaam katika siku itakayotangazwa wakati wowote kuanzia leo.Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu msanii huyo ni pamoja na Mteule Uwe Macho, Nipe Uvumilivu, Yesu Nakupenda, Akina Mama, Nakuuliza Shetani, Yerusalemu, Mwambieni Mungu na Nakaza Mwendo.

  Pia nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni Kitimutimu, Imani, Onjeni, Sikilizeni Enyi Makahaba, Mungu Wangu, Moyo Wangu, Najitoa Sasa, Hey Mbona Watenda Dhambi na Wapendwa.

  Nyingine ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Nyimbo hizo zipo katika albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa na Utamu wa Yesu.

  Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya katika albamu ya Vua Kiatu.


  0 0
 • 06/29/14--01:20: Article 0


 • 0 0


  Kiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi akiwapatia maelezo mbalimbali kwa watu waliotembelea kanisa hilo wakati wa siku ya wazi kwa ajili ya watu mbalimbali kuangalia shughuli zinazofanywa na kanisa hilo
  Baadhi ya watu waliotembelea kanisa hili wakipata maelekezo mbalimbali
  Mwakilishi wa Darasa la Mkono msaidizi wa akina mama Happy Ayubu akitoa maelezo kwa watu waliotembelea kanisa hilo
  Baadhi ya watu waliotembelea kanisa hili wakipata maelekezo mbalimbali.

  Mhumini waKanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho Framers Ngosha akijibu maswali ya watu waliojitokeza katika siku hiyo


  Kiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi 'kulia' akionesha vitabu vinavyotumika kwa ajili ya mafunzo kushoto ni Rais wa tawi la Mbezi Beach, Malabi Kyubi
  Rais wa tawi la Mbezi Beach, Malabi Kyubi akitoa maelezo
  Baadhi ya watu mbalimbali waliotembelea katika kanisa hilo lililopo Mbezi Beach
  Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba wakati wa siku ya wazi kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali iliyofanyika katika kanisa lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam


  Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba wakati wa siku ya wazi kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali iliyofanyika katika kanisa lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
  watu waliotembelea wakipata mahelezo mbalimbali
  Baadhi ya watu waliotembelea katisa hilo

  0 0

   Muonekano wa TMT House ambayo washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents wameweka kambi rasmi kuanzia jana Usiku kwa mchakato wa kuwania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane
   Mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwizago akiingia rasmi kambini hapo jana wakati wakitokea kwenye matembezi. Washiriki wote 20 ambao ni washindi kutoka Kanda sita za Tanzania sasa wapo kambini kwaajili ya kujifua ili kuwania kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.
   Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la TMT wakiingia kambini hapo jana Usiku
   Washiriki wakiwa ndani ya Nyumba ya TMT tayari kwa kambi
  Washiriki wakipewa maelekezo mara baada ya kuwasili kambini hapo jana.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions - Dar Es Salaam.
  Washiriki 20 kutoka Kanda sita za Tanzania wameingia rasmi kambini hapo Jana mara baada ya kumaliza zoezi la Kupima Afya, kutembezwa sehemu mbalimbali za Jiji la Dar pamoja na Ofisi za Global Publishers.

  Washiriki hao watakaa kambini kwa Siku 64 ambapo wataanza rasmi kufundishwa Hapo kesho siku ya Jumatatu na walimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo ambapo baadae sasa baadae zoezi la kuanza kuwapigia kura washiriki hao litaanza na hatimaye watanzania ndio watakuwa majaji kwa washiriki hao ambapo mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 atapatikana katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

  Zoezi la Upigaji kura litaanza mapema wiki ijayo ambapo washiriki wote watakuwa tayari washapewa namba za ushiriki na hatimaye watanzania kuweza kuwachagua washiriki wanaowaona wana vipaji.
  Zoezi hili la kupiga kura litapelekea Washiriki wawili kuondolewa kila wiki katika Kambi ya TMT ambapo pona yao ni kutoka kwa Watanzania ambao ndio watakuwa majaji kwa kuwapigia kura.

  Vilevile Mara baada ya washindi hawa wa kanda kuingia kambini Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa kila siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku na Kurudiwa kila Siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa tano usiku kupitia Runinga ya ITV.

  Tunawaomba watanzania kuendelea kutizama vipindi vyetu kwani vimekuwa na mvuto wa hali ya juu sana lakini pia kuendelea kuwawezesha 
   Washiriki wanaowaona wana vipaji ili kuwa ushindi. Namba za washiriki zitaanza kuonekana katika Kipindi chetu kijacho ambapo Sasa watanzania wataanza kuwapigia kura kwenda namba 15678
  Na ili kuweza Kufahamu taarifa zaidi za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678.

  0 0

  Wanachama wa Simba wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Klabu ya Simba katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande)
  Wagombea wa nafasi ya Urais katika Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) na Andrew Tupa na wakipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Hassan Dalali akipiga kura.
   Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage wakipiga kura.
   Rais wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage akiagana na mgombea wa Urais wa Simba, Evans Aveva (katikati).
   Wagombea wakitafakari.

   

   Wanachama wakihakiki kadi zao.
  Mgombea wa Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akizungumza na baadhi ya wanachama kabla ya uchaguzi.
  Mgombea akiomba kura......Tukiwezeshwa tunaweza.
   Mgombea akijinadi.
   Mgombea wa nafasi ya Kamati ya Utendaji wa Simba, Asha Muhaji akijinadi mbele ya wapiga kura.
   Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiwa Rais aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
   Ibrahim Masoud Maesto akijinadi.
   Mbunge wa Mtwara, Mohamed Murji, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
   Tunaomba kura zenu..............
   Nitaleta Maendeleo mkinichagua mimi..........................
   Simba Oyeeeeeee......................
   Jamhuri Kihwelo akielekea kujinadi kwa wanachama wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Simba.
   Jamhuri Kihwelo 'Julio' akiomba kura.
   Wagombea wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Andrew Tupa, Evans Aveva.
   Wagombea wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Andrew Tupa (kupara), Swed Nkwabi,  Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Evans Aveva.
   Jamhuri Kihwelo 'Julio'akimwaga sera zake.
    Jamhuri Kihwelo 'Julio'akimwaga sera zake.
    Jamhuri Kihwelo 'Julio'
   Kaburu akijinadi kwa wapiga kura.
  Jamhuri Kihwelo 'Julio' akiteta na Evans Aveva.
   Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba, Amin Bakhressa.
   Evans Aveva akijadiliana jambo na Hans Pope.
   Mgombea wa nafasi ya Urais, Andrew Tupa akijinadi.
   Mgombea wa nafasi ya Urais, Evans Aveva akijinadi.
   Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba, Amin Bakhressa akionesha fomu za uchaguzi.
   Mmeona hakuna kitu humu....
   Asha Muhaji akipiga kura.


  0 0

   Afisa Michango wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gloria Maboya, (Kulia), akiwapatia taarifa za michango, wanachama wa PPF, waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyeshjo ya 38 ya biashara ya kimagtaifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
   Afisa Michango wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gloria Maboya, (Kushoto), akitoa elimu kuhusu Mfuko huo, kwa mwanachama huyu aliyetembelea banda la PPF lililoko viwanja vya Maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
   Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (Kushoto), akimkabidhi Mwnanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, taarifa yake ya michango alipotembelea banda ya PPF, kwenye siku ya pili ya Maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
  Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku Magawa (Kushoto), akimfafanulia Mwanachama wa Mfuko huo, kuhusiana na michango yake, alipotembelea banda la PPF, kwenye siku ya pili ya Maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF, lililoko kwenye viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam. PPF inashiriki maionyesho ya 38 ya biashara ya mwaka huu 2014 na inawakaribisha wananchi wote kujonea na kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo


  0 0

   Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma kutoka kwa Meneja Utawala Msaidizi wa kampuni ya Tanzania – China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) Bw. Israel Mkojera. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Mlingi E. Mkucha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama wa NDC Bw. Ramson Mwilangali (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (wa pili kushoto), Erasmus Masumbuko, Tume ya Mipango (wa tatu Kushoto).
   Viongozi pamoja na Maofisa kutoka Tume ya Mipango wakiangalia sehemu ambayo makaa ya mawe yanaonekana juu ya ardhi. Kulia ni mhandisi wa madini kutoka kampuni ya TCIMRL. Kampuni hii ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania, na kampuni ya Sichuang Hongda Group Limited ya China. 
   Sehemu ambayo makaa ya mawe yanaoneka kwa juu katika uhalisia wake.
  Shimo hili lilichimbwa mwaka 1956 kwa ajili ya utafiti kuangalia tabaka za makaa ya mawe katika eneo hilo la Mchuchuma.

  0 0

  Bi Rusi akikabidhiwa zawadi yake.

  Mashindano ya kumtafuta Bibi bomba mwaka 2014 yalifanyika Mikocheni katika ukumbi wa Saadani Parking national hotel jijini Dar es salaam , mgeni rasmi alikuwa Bi.Anna Kilango. Aliyefanikiwa kuibuka mshindi usiku huo ni Bi Rusi Manfred ambaye alijipatia zawadi ya shilingi milioni kumi za kitanzania na kiwanja chenye thamani ya shilingi Milioni tano.

  Mashabiki wakimshangilia Mshindi

  Bi Rusi akiwa ameshikiria Hati ya kiwanja kama
  moja ya zawadi yake.

  Mkurugenzi wa Tanzania Women's Bank (TWB) Bi Margareth Chacha  akitoa pongezi zake. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  DSC_0125
  Meneja wa kituo cha Sengerema FM Redio, Ndg. Felician Ncheye, akitoa nasaha za ukaribisho kwa washiriki wa mradi wa SHUGA na mgeni rasmi. Katikati ni Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu na Kulia ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  Na Mwandishi wetu, SENGEREMA - MWANZA
  Redio za jamii nchini zimeaswa kutumika vizuri katika kuelimisha kamii juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia vipindi vya redio. Hamasa hiyo imetolewa na Ndg Geofrey Mabu ambaye ni mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS wakati akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya ujulikanao kama SHUGA, unaotekelezwa na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana Shirika la Mfuko wa Watoto (UNICEF) inayofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani Mwanza.

  Mabu amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo malengo yake yakizingatiwa na kutekelezwa kama ilivyopangwa utasaidia kufikia malengo ya serikali ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi Zero.
  DSC_0129
  Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.

  Amesema kuwa redio za jamii ni kiungo muhimu katika kuelimisha jamii na kuwa kama zitatumika vizuri kusambaza elimu ya UKIMWI kupitia vipindi vyake zitasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali kupitia TACAIDS.
  Vile vile ameziomba redio zitakazoshiriki katika mradi huu, kutumia vizuri fursa hii waliyoipata kuhakikisha wanafanikisha malengo ya mradi kwa kiwango cha juu kwa kufanya hivyo pia watakuwa wamelinusuru taifa na janga hili la UKIMWI.
  DSC_0069
  Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa maelezo kuhusu madhumuni ya warsha inayohusisha mradi wa SHUGA.

  Awali Mkufunzi wa Radio za jamii kutoka shirika la UNESCO Bi Rose Mwalimu akitoa ufafanuzi wa malengo ya semina hiyo, amesema kuwa mradi huu wa SHUGA unalenga kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa vijana hapa nchini kupitia vipindi vya mchezo wa redio kubadili tabia.

  Amezitaja redio 10 zinazoshiriki katika mradi huu nchini Tanzania kuwa ni FADECO Redio ya Karagwe mkoani Kagera, ORS ya Manyara, Sengerema FM mkoani Mwanza, Pangani FM ya mkoani Tanga na Kahama FM kutoka Shinyanga. Nyingine ni Kitulo FM ya Makete Njombe, Kyela FM ya Mbeya, Nuru FM kutoka Iringa, Pambazuko FM Ifakara na Kwanza Jamii Redio FM kutoka Njombe.
  DSC_0269
  Afisa Mipango VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias akitoa mada kuhusu VIjana, Balehe na Mahusiano ya Ngono wakati warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.
  DSC_0103
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi.
  DSC_0238
  DSC_0261
  Mshiriki kutoka Kahama FM Redio, Makunga Peter akiuliza jambo kutoka kwa mkufunzi (hayuko pichani).
  DSC_0192
  Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akitoa mada kuhusu kiwango cha Maambukizi ya VVU kwa Vijana na hali ya Afya ya Uzazi Salama wakati wa mafunzo hayo.
   
  DSC_0212
  DSC_0251
  Mshiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA kutoka Sengerema FM Redio, Peter Marlesa akijenga hoja kuhusu viashiria hatarishi vya maambukizi ya VVU kwa vijana.
  DSC_0279
  Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi wa SHUGA wakiwa katika vikundi kazi.
  DSC_0289
  DSC_0169
  Mgeni rasmi Ndg Geofrey Mabu wa TACAIDS, wakufunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.

older | 1 | .... | 309 | 310 | (Page 311) | 312 | 313 | .... | 1897 | newer