Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 308 | 309 | (Page 310) | 311 | 312 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa bunduki mbili pamoja na mali kadhaa kufuatia operesheni tokomeza uhalifu inayoendeshwa na Jeshi la Polisi mkoani Hapo.
  Kamanda Boaz akiwaonesha waandishi wa habari, bunduki mbili, ya kulia ni Shotgun Greener, ambayo imekatwa kitako pamoja na nyingine aina ya shotgun (ya kushoto), namba za usajili 68022, ambazo zinaaminika zimekuwa zikitumika katika matukio kadhaa ya ujambazi mkoani humo.
  Baadhi ya vito vya thamani vilivyokamatwa katika operesheni hiyo zikiwemo bunduki hizo mbili .
  Baadhi ya vito hivyo vikiwa vimetandazwa mezani katika makao makuu ya jeshi la polisi mkoani kilimanjaro.


  Kamanda Boaz akiwaonesha waandishi wa habari, bunduki mbili, ya kulia ni Shotgun Greener, ambayo imekatwa kitako pamoja na nyingine aina ya shotgun (ya kushoto), namba za usajili 68022, ambazo zinaaminika zimekuwa zikitumika katika matukio kadhaa ya ujambazi mkoani humo.
  Bunduki aina ya shotgun Greener ambayo imekatwa kitako huku ikiwa imefungwa 'hirizi' kitu kinachoofanana na gruneti (iliyoning'inia) ambayo ilikamatwa jana katika operesheni tokomeza uhalifu inayoondeshwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro.
  Sehemu ya mali zilizokamatwa katika kamatakamata hiyo.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

  0 0

   Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya kukanusha uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) na kulia kwake n Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
    Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa tarifa ya kukanusha taarifa za uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kuanzia kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) , Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
    Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kuanzia kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) , Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
    Rais wa Bongo Movie Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura (katikati) akizugumza katika mkutanona waandishi wa habari kukanusha taarifa ya uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. 
    Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu akiteta jambo na Wastara Juma mara baada ya mkutano huo.
  Wastara Juma akihojiwa na Timzoo Karugira wa Azam TV. Picha na Cathbert Angelo wa Kajunason Blog.
  ---
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
  WASANII tasnia ya filamu Tanzania ambao wanaunda umoja unaofahamikakama Bongo Movie wameomba kutohusishwa na masuala ya kisiasa katika shughuli zao.
  Hayo yalisemwa na Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere kutokana na hsia za kuhusishwa kwao katika mambo ya siasa mara baada ya kushiriki katika uzinduzi wa filamu ya “I love Mwanza” ambayo ilizinduliwa na wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Utalii, Lazaro Nyalandu.
  Steve alisema kuwa wao kama wakuu wa tasnia ya Filamu nchini, hawana mamlaka ya kumtenga mtukatika shughuli zao zaidi ya kumshirikisha mtu yoyote awe mkulima, mfanyabiashara, mwanasiasi bila kujali wa chama gani.
  “Membe na Nyalandu wameshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, wewe subiri uzinduzi mwingine kama utapata nafasi ya kualikwa, lengo letu kubwa ni kuenea sanaa ambayo imezoeleka zaidi mkoani Dar es Salaam, ni mafanikio kwetu,” alisema Steve.
  Alisema kuwa kitendo cha kuinadi filamu hiyo mbele ya halaiki ya watu kwenye siku ya uzinduzi wake kilikuwa ni cha kawaida tu kwa sababu hata katika katika nyumba za ibada mambo haya hufanyika, tulifanya wazi bila kificho kwa sababu halikua jambo la haramu ukizingatia ni jambo lililokuwa lina lengo la kusaidia maendeleo y asana nchini katika kukuza kipato cha wasanii wa nchini Tanzania.
  Mwenyekiti wa Wasanii wa Filam Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura alisema kuwa Membe hakuwa na shughuli nyingine tofauti na zaidi ya uzinduzi wa filamu.

  “Ukweli ni huu katika uzinduzi wa filamu ya Ilove Mwanza ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe ndiyo alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Membe ametokea kuisapoti Bongo Movie siyo dhambi hivyo viongozi wengine wajitokeze kusapoti wasanii kama jinsi alivyo Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, alisema Anitha.
  “Tume sikitishwa sana na kusingiziwa mambo ya uongo ambayo hayana ukweli ndani yake na kuhusishwa na masuala ya kisiasa,” alifafanua.

  0 0

   
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kushoto) akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka (katikati) na Mkurugenzi Mstaafu wa TIC na pia Balozi wa heshima wa Botswana hapa nchini, Eng. Emmanuel Ole Naiko wakati wa kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na China lililomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Sekta binafsi nchini imekaribisha wawekezaji kutoka China kuwekeza nchini kwa faida ya pande zote mbili.Akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na China Jumatano wiki hii jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF),Bw. Godfrey Simbeye alisema taasisi hiyo inakaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo katika juhudi za kufikia maendeleo endelevu hapa nchini.
  “Sisi kama sekta binafsi tunasisitiza uwekezaji mzuri unaolenga kuiendeleza Tanzania...tunawakaribisha wawekezaji hawa kuja kufanya kazi hapa,” alisema.Kongamano hilo lilishirikisha kampuni zaidi ya 100 kutoka China na kampuni zaidi ya 120 za kitanzania.Hadi sasa China imesajili miradi 522 TIC yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 2.4 ambayo inatarajiwa kuzalisha ajira 77,335.
  Hata hivyo, Bw. Simbeye aliwaambia waandishi kuwa uwekezaji huo bado ni mdogo ukilinganisha na ukubwa wa uchumi wa taifa hilo.“Tunahitaji uwekezaji wao ufikie dola za kimarekani bilioni 5 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo,” alisema.Alisema sekta binafsi inapenda waje kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda na siyo kutumia fursa waliyopewa na watanzania kuja kuuza tu bidhaa zao.
  Pia alisema wanapokuja kuwekeza ni vema wakatumia fursa hiyo kuwasaidia watanzania kupata ujuzi na teknolojia kupitia miradi ya ushirikiano (ubia) ili taifa liweze kupiga hatua. Alisema taasisi hiyo iko tayari kushirikiana na wawekezaji hao kutoa msaada na mwongozo wowote utakaohitajika ili kuendeleza miradi watakayotaka kuanzisha hapa nchini.
  “Tunazidi kupigania mazingira bora ya biashara ambayo yanaendelea kuboreshwa hivyo wawekezaji wa ndani na nje wachangamkie fursa zilizopo,” alisema.Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi alisema Tanzania imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya biashara ambayo yanavutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza  kwa faifa ya nchi na wawekezaji.“Mazingira yetu ya kufanya biashara yameboreshwa sana na tunaendelea na juhudi kuyaboresha zaidi,” alisema.
  Alisema katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Tanzania inaendelea kupambana na changamoto zinazokabili mazingira ya kufanya biashara.Alisema changamoto hizo ni pamoja na kuzidi kuboresha mazingira ya uanzishaji biashara na upatikanaji wa ardhi ili wawekezaji wasitumie muda mwingi.
  “Maeneo mengi hayajapimwa hapa nchini,hivyo serikali inaendelea kulifanyia kazi jambo hilo ili wawekezaji wasipate usumbufu wa ardhi ya kuwkeza,”alisema.Pia serikali inaendelea kupunguza mianya ya rushwa ambayohuongeza gharama za kufanya biashara na kuwakatiza wawekezaji kuja kuwekeza.
  Alisema TNBC kama chombo kinachokutanisha sekta binafsi na umma kinaendelea kuangalia kero na maeneo yanayofanya mazingira ya biashara na uwekezaji kutokwenda vyema ili kuibadilisha Tanzania.
  Kongamano hilo la siku tatu lilofunguliwa na Makamu wa Rais wa China Bw, Li Yuanchao liliandaliwa na TIC kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Baraza la Biashara China Afrika (CABC) na kudhaminiwa na Stanbic Bank Tanzania.

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

   Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutanomkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmKatibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungumkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu .
   Katibu Mkuu Ofisi Rais, Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.

   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue  (haypo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue  (haypo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.


  Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. Solanus Nyimbi akiongea kwa niaba ya Wakurugenzi Rasilimaliwatu Serikalini baada ya ufunguzi wa mkutano  mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.
  Sekretarieti ikichukua michango wakati wa mkutano  mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

  0 0

  IMG-20140625-WA0044
  Mkurugenzi  Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42)  unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB)uliyofanyika  jijini Arusha
  ======= ======= 
  Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota maji.
   
  Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi  Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42)  unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.
   
  Alisema kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.
   
  Alifafanua  kuwa, halmashauri za wilaya pamoja na serikali za vijiji wamekuwa wakitoza kodi mbalimbali kwa vifaa vya ujenzi kama kifusi, mchanga,kokoto,na maji.
   
  Mfugale alisema kuwa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha-holili ni sehemu ya mradi wa kimataifa unaojulikana kwa jina la Holili/Taveta –Voi unaounganisha nchi yetu na nchi jirani ya Kenya utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 223.
   
  Alisema kuwa, awamu ya kwanza ni kuijenga kwa njia nne sehemu ya barabara kutoka Sakina –Tengeru (km 14.1) na Arusha bypass (km 42) kwa fedha za mkopo kutoka ADB .
   
  Aliongeza kuwa, sehemu ya pili ni kuendeleza ujenzi wa njia nne kutoka Tengeru hadi Usa river (km 8.2) na ukarabati wa sehemu ya barabara iliyobaki hadi Holili baada ya kupata fedha.
   
  Naye Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa  alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya hali ya hewa ambayo imekuwa ikichangia mradi kukamilika kwa wakati na ucheleweshaji wa ulipwaji wa fedha za wakandarasi .
   
  Alisema kuwa, wao kama benki ya maendeleo ya Afrika wataendelea kutafuta hela kwa ajili ya maendeleo kwani ni fursa nzuri wao kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo.(jamiiblog Pamela  Mollel)

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal. akipata maelezo juu ya athari za utumiaji wa madawa ya kulevya kutoka kwa Msanii Rehema Charamila (RC) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Akionyeshwa baadhi madawa ya kulevya na Mkemia Daraja la kwanza Alois Ngonyani, alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya.


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Msanii Rehema Charamila kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya.


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Msanii Masanja Mkandamizaji kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya.
   Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa mbeya na baadhi ya Vijana walioathirika kutokana na kumia madawa ya kulevya wakiwa katika maandamano kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya.
  (Picha na OMR)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wanafunzi wa shule mbalimbali za Mkoa wa Mbeya baada ya kuhutubia kwenye ya maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya yaliyoadhimishwa kitaifa leo Juni 26-2014 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mkoani mbeya. 

  0 0

   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni Milton Lazaro (katikati) akipeana mkono na  Meneja wa Kanda wa Interair, Angelo Cossi  mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya shirika la ATCL na shirika la Interair la Afrika ya Kusini, yatakayowezesha kuwepo na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na Johannesburg Afrika ya Kusini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL Bw. Juma Boma (kushoto). . 
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni Milton Lazaro (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam jana kutangaza makubaliano yaliyosainiwa kati ya shirika lake na shirika la Interair la Afrika ya Kusini, yatakayowezesha kuwepo na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na Johannesburg Afrika ya Kusini. Wakishuhudia kushuto ni Meneja wa Kanda wa Interair, Angelo Cossi na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL Bw. Juma Boma (kushoto)

  =======  ====== ========
  SHIRIKA la Ndege la Taifa la Air Tanzania (ATCL) limesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Interair ya Afrika Kusini, itakayowezesha shirika hilo kuwa na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika ya Kusini ikiwa ni kama ratiba ya mwanzo.

  Taarifa hiyo imetolewa siku chache tu baada ya mashirika hayo mawili kusaini makubaliano ya kufungua soko la kitanzania kwa Interair na kulifufua soko la Afrika ya Kusini kwa shirika la Ndege la Air Tanzania kwa kupitia safari zitakazofanyika siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa, ikiwezeshwa na ushirikiano huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya ATCL jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro alisema ushirikiano huo na Interair ni sehemu ya mkakati madhubuti wa kuboresha shirika hilo, kama siyo kwa safari za moja kwa moja basi kupitia ushirikiano wa aina hiyo, ili kuweza kurejesha huduma za shirika hilo katika njia zote lililokuwa likiruka, likianzia Afrika ya Kusini.  

  “Kwa kutumia ndege za Interair, abiria wetu sasa watakuwa na uwezo wa kusafiri kwenda na kutoka Johannesburg katika siku zifuatazo; itawasili jijini Dar es Salaam kila Jumatatu na kuondoka kwenda Johannesburg Jumanne, kuwasili Dar es Salaam Jumatano na kuondoka siku hiyo hiyo, kuwasili Dar es Salaam Ijumaa na kuondoka kwenda Johannesburg siku ya Jumamosi,” alisema.

  Kapt. Lazaro alibainisha kuwa mashirika hayo mawili sasa yanatoa fursa kwa wasafiri kutoka nchi hizo mbili kuyafikia masoko, wanaotaka kutumia na kupata uzoefu wa siku kuu za kipekee wanazo kuwa wakizisoma kuhusu Afrika ya Kusini au Tanzania, na pia kutoa fursa za ongezeko la ushirikiano wa kibiashara na kidiplomasia.

  “Kwa kupitia makubaliano haya mapya, tuna uhakika kuwa ratiba itakidhi haja kwa wasafiri wote katika sehemu hizi mbili, na kutoa chanzo cha mapato kitakacho changia katika ukuaji wa shirika la Air Tanzania, Sekta ya Utalii Tanzania na uchumi wetu wa ndani,” alisema Kapt. Lazaro. Aliongeza kuwa ATCL katika siku za usoni itatanua safari zake mpaka Arusha, Zanzibar, Mwanza, Mbeya, Comoros na baadae katika maeneo mengine yote inayofanyia shughuli zake. 

  Kwa upande wake, Meneja Interair wa Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Angelo Cossi, alisema: “Ushirikiano na Air Tanzania ni muungano nzuri kwa sababu ya faida itakayopatikana ambayo itafaidisha mashirika haya mawili. 

  “Shirika la Interair la Afrika ya Kusini ni moja kati ya mashirika ya ndege nchini Afrika ya Kusini yanayomilikiwa kibinafsi yenye mafanikio. Shiriki hili, mwanachama wa Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (I.A.T.A), na Chama cha Mashirika ya Ndege Afrika (AFRAA) limejiimarisha kama moja kati ya mashirika makubwa katika ukanda. Ushirikiano na Air Tanzania utawapatia wateja wa Interair, njia mpya bora ya kusafiri kwenda Tanzania na kutoka Tanzania, Johannesburg inakuwa karibu zaidi na ni ya rahisi kufika kwa wateja wa Air Tanzania,” alisema.

  Alisema Interair ya Afrika ya Kusini ambayo ina makao yake makuu Johannesburg, Afrika ya Kusini, kwa sasa ina ndege aina za Boeing 727, 737 na 767, ambazo zinatoa huduma ndani ya Afrika na katika visiwa vya Bahari ya Indi. Alikuwa na matarajio kwamba ushirikiano huo utausaidia shirika lake kutengeneza jina thabiti katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

  0 0

   Launch of the College of Business Education (CBE) and University of East Finland (UEF) HUB for SADC member states at CBE by H.E. Ambassador of Finland to Tanzania, Sinikka Antila (left). Second left is Permanent Secretary Ministry of Industry and Trade, Uledi Musa, followed by CBE Governing Body Chairperson, Prof. Mathew Luhanga,  Prof Erkki Sutinen from UEF and Prof Emanuel Mjema, Rector CBE, respectively.
   Guest of Honour, Permanent Secretary, Minostry of Industry and Trade, Uledi Musa (seated centre) in a group photo with organizers and invites guests of the occasion.
   College of Business Education (CBE) Rector, Prof Emanuel Mjema.
   College of Business Education and PhD candidates from CBE, Godfrey Ambrose and William Gomera with their supervisor, Dr Mikki Apiola, from University of East Finland, during the launch of the CBE PhD Studies Hub for SADC member states.  
   A participant commenting on the presentations done by the Doctorate candidates
   College of Business Education (CBE) Lecturer, William Mwakyusa gives a comment to PhD candidates after presentation of their research papers during the CBE PhD studies Hub for SADC member states in collaboration with University of East Finland.
  Ezra Nisaki, one of CBE lecturers and PhD candidates responds to questions after presentations during the launch. Others from left are; Godfrey Ambrose, Alsa Kapinga , William Gomera and Nasibu Mramba .


  The College of Business Education (CBE) in collaboration with the University of Eastern Finland (UEF)has launched the first International Multidisciplinary PhD Programme in Education Technology and Learning Environments (IMPDET-LE) Hub for East Africa and SADC member states.

  The ICT based education is strongly supported by the Government, as was assured by Permanent Secretary at the Ministry for Industries and Trade, Uledi Musa who officiated the event on behalf of the Minister, which was organized jointly by the College of Business Education (CBE) and University of East Finland member states on behalf of the Minister.

  “The government is in the process of establishing an online program called National Business Portal (NBP), which will allow for on line registration of businesses without the need of a physical visit toBusiness Registrations and Licensing Agency (BRELA) offices.

  According to Musa, the country’s investment in information technology allows fore reduction of youth unemployment and he is optimistic that at this pace Tanzania will lead and become in ICT consultant for countries in the region.
  “Currently Tanzania is the second country in the world in terms of applying electronic system in money transactions…hence there is a need for youths to look for more opportunities resulted from the sector,’’ he said.

  The Permanent Secretary also challenged academicians to write inspiring articles which bring hope to the citizens and they should aim to encourage policy makers to arrive at constructive and positive decisions.

  Concerning the Doctorate Hub launched, Uledi Musa promised that the government will provide all support needed for its development. Speaking during the occasion, Chairman of the CBE Governing Board, Prof Mathew Luhanga, said thatalready five College lecturers have started doctoral training on-site at CBE.

  “The project will last four years, during which the first batch of five faculty members is expected to graduate from UEF. The studies emphasize both local and international academic and business co-operation and the faculty members are expected to form a computer science research group as one of their outcomes”, he said.

  The event was attended by Ambassador of Finland to Tanzania, H. E. SinikkaAntila,ProfessorProfessorErkkiSutinenand Doctors JarkkoSuhonen and MikkoApiola, fromUniversity of East Finland who supervise the five PhD candidates in the country, while their lectures are conducted from Finland via Skype.

  Ambassador of Finland to Tanzania said that as a country of about five million people, Finland stands to be an innovative nation which also imparts their knowledge to Tanzania in various development projects involving health, agriculture and ICT for the past 25 years. She also commented CBE for financing the project and said that, “ …this type of co-creation is the best type of development co-operation we can have.”

  Rector of CBE, Professor Emanuel Mjema commented on the studies and their importance to the community, since now one can obtain a Doctorate Degree on local issues rather than those of a country of studies, as happens in many cases. Some of the studies include usage of ICT for street vendors, women entrepreneurs and in obtaining rural information.

  0 0

  eketaji.Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania. 
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.
  Washiriki Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam. Washiriki Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.

  SERIKALI imesema kitendo cha baadhi ya makabila kuendeleza mila za kuwakeketa wanawake na watoto ni ukatili mkubwa ambao umekuwa na madhara kiafya kwa anayetendewa. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba alipokuwa akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji nchini Tanzania unaofanyika kwa siku mbili katika Mkumbi wa Mikutano wa Kunduchi Hoteli. 

   Waziri Simba alisema ukeketaji ni udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike na umekuwa ukihatarisha maisha ya wahusika kwa matokeo ya vifo, vilema na maradhi kama vile fistula na magonjwa mengine hivyo kutaka kila mmoja kuungana kuupinga. Alisema kwa upande wa Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inatokomeza mila hizo pamoja na ukatili mwingine wa kijinsia. 

   “Wengi hapa ni mashaidi wa madhara ya ukeketeji ikiwemo vifo, vilema na maradhi kama vile, fistula na mengineyo. Serikali inalaani na kukemea ukatili huu unaomdhalilisha mwanamke na kumletea madhara makubwa,” alisema Waziri Simba. Aidha alisema ili kupambana na hali Serikali imesaini mikataba mbalimbali ya kukabiliana na ubaguzi anuai hasa kwa wanawake na pia kuanzisha Dawati la Jinsia kila sekta kukabiliana na vitendo vya kikatili nchini. “…Serikali iliandaa na inatekeleza mpango wa taifa wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (2001-2015) na mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji (2001-2015)…,” alisisitiza Waziri Simba.


   Aliongeza pamoja na hayo na juhudi mbalimbali za Serikali ukatili huo kwa wanawake na watoto hauwezi kuzuiliwa kwa sheria na mipango ya serikali hivyo kuitaka jamii pamoja na wadau wengine kuunganisha nguvu kupambana na vitendo hivyo hapa nchini. “….Suala la kutokomeza ukatili wa kijinsia, halitakwisha kwa kutegemea Serikali au sheria peke yake. Ni jukumu letu wadau wote kwa pamoja kukemea na kupiga vita kwa nguvu zote, kutoa elimu dhidi ya ukatili, huduma kwa wahanga na kuhakikisha wanaotenda na kubariki vitendo hivi wanachukuliwa hatua,” alisema.

   Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Mwakilishi wa UNFPA Tanzania, Mariam Khan alisema licha ya juhudi zinazofanywa kupambana na ukeketaji nchini, kila mwaka vipindi vya ukeketaji bado wasichana na watoto wanaokeketwa wamekuwa wakipoteza maisha bila sababu ya msingi kutokana na madhara ya ukeketaji jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa. Aliwataka washiriki kwa pamoja kujadiliana nini cha kufanya ili kukomesha ukatili huo unaoendelea kushamiri nchini na kuahidi kuwa UNFPA itaendelea kuunga mkono juhudi za mapambano hayo kwa kutoa mafunzo na kuwezesha shughuli za mapambano hayo.

   Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Nsoka alisema mkutano huo umewashirikisha wakuu wa mikoa, viongozi wa dini, wawakilishi wa madawati ya jinsia na wadau wengine kutoka mikoa yenye vitendo vya ukeketaji pamoja na asasi zinazopambana na ukeketaji. Aliongeza kuwa mkutano huo utafanyika kwa siku mbili ambapo wajumbe, watapeana uzoefu na kufanya majadiliano ya kina kabla ya kuibuka na mpango kazi wa nini kifanyike kutokomeza vitendo vya ukeketaji nchini. Mkutano huo ulioratibiwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) umefadhiliwa na Shirika la UNFPA, Tanzania. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
  Mwakilishi kutoka Asasi ya NAFGEM inayofanya kazi mikoa ya Manyara na Arusha akielezea namna shirika hilo linalofanya kazi. 
  Mwakilishi kutoka Asasi ya NAFGEM inayofanya kazi mikoa ya Manyara na Arusha akielezea namna shirika hilo linalofanya kazi kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania. Mkaguzi wa Polisi, kutoka Dawati la Jinsia na Watoto, Tarime-Rorya, Saumu Ngoma akizungumza na wanahabari namna dawati hilo linavyoshiriki kupambana na vitendo vya kikatili ukiwemo ukeketaji. 
  Mkaguzi wa Polisi, kutoka Dawati la Jinsia na Watoto, Tarime-Rorya, Saumu Ngoma akizungumza na wanahabari namna dawati hilo linavyoshiriki kupambana na vitendo vya kikatili ukiwemo 

  0 0

  Watumishi waliostaafu katika Ofisi ya Makamu wa Rais wametakiwa kuendelea na moyo wa kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na uhifadhi wa mazingira.

  Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano),  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastaafu wapatao 12 wa kada ya maafisa katika ofisi hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.

  Mheshimiwa Samia alisema wastaafu hao wanapaswa kuendelea na moyo huo kwani jukumu la kuudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira ni la kila mmoja katika jamii.

  “Natambua kwamba ninyi nyote mliostaafu na mtakao staafu ni mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii kuhusu majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais yanayohusu kuudumisha Muungano wetu pamoja na kuhifadhi mazingira,” alisema Waziri Samia na kuongeza

  “Natarajia mtakuwa mfano katika kuendeleza jitihada za kudhibiti uharibifu wa mazingira katika jamii inayowazunguka.”

  Aidha, aliwaasa  wastaafu hao kushirikiana na Asasi na Taasisi mbalimbali zilizoko kwenye maeneo yao ili kupitisha mawazo ambayo yatasaidia kuwaletea wananchi maendeleo 

   “Kupitia mawazo yenu Taasisi kama hizi zitaweza kujenga uwezo zaidi katika masuala ya maendeleo ya jamii hususan fursa za ajira kwa vijana wetu,” alisema

  Kwa wale wanaoendelea na utumishi wa umma Waziri Samia aliwataka waige mfano kwa watumishi waliostaafu na kuendelea kujenga tabia ya uadilifu, uaminifu na uchapakazi.

  Wastaafu hao walipatiwa zawadi ya jiko la gesi kila mmoja jambo ambalo Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete alipokuwa akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi alisema ofisi iliandaa zawadi hiyo ili  wastaafu hao wakawe mabalozi wazuri wa kuhimiza matumizi ya jiko la gesi na hivyo kusaidia katika suala zima la uhifadhi wa mazingira.

  0 0
 • 06/27/14--02:47: Article 11


 • 0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal (kulia) wakipeana maneno ya mwisho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa ishara ya kuagana baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita. 

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akimpa mkono wa shukurani Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara kabla ya kuanza safari yake ya kurudi nchini kwake.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

   Kikundi cha ngoma kikicheza mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (hayupo pichani) wakati wa kumuaga baada ya kukamilisha ziara yake ya siku sita nchini Tanzania.


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiwapungua mkono baadhi ya viongozi pamoja na wananchi waliokuja kumugaga katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha ziara yake nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiwa amekumbatiana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal ikiwa ishara ya kuagana mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita nchini Tanzania.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiondoka kuelekea kupanda ndege ya Qatar Airways kwa ajili ya kurudi kwao China. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.


  0 0

  1
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwenye hoteli ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo asubuhi hii wakati wa seina inayojadili masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio ya mfuko huo, malengo na Changamoto zake katika kufanikisha huduma ya afya kwa jamii, ambapo uwigo wa walengwa katika huduma hizo umeongezeka kutoka kaya 120 mwaka 2009 na kufikia kaya 668.474 mwaka 2014 sawa na wanufaika milioni 4.01 na mpaka sasa mfuko huo unafanya kazi na Halmashauri za wilaya 129 katika nchi nzima kati ya Halmashauri 168 zilizopo lakini pia tayari Halmashauri 20 kati ya hizo zimeshahamasishwa na zitaingia katika mpango huo siyo muda mrefu, .(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-BAGAMOYO)2Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji akitoa mada katika semina hiyo juu ya uchangiaji wa huduma za mfuko wa bima ya afya kulia ni Raphael Mwamoto Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti na katikati ni Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF)3


  5John Bwire Mkurugenzi wa kampuni ya Raia Mwema na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbalzinazotolewa katika semina hiyo6Kulia ni Mhariri Dany Mwaijega na wenzake wakifuatilia majadiliano ya semina hiyo78910Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri mtendaji wa New Habari Bw. Absalom Kibanda akizungumza katika semina hiyo inayofanyika mjini Bagamoyo anayefuata ni Abdalla Majura kutoka ABM Radio.11Mhariri wa Gazeti la Mawio Jabir Idrissa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano katika semina hiyo12Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee na viongozi wengine wa mfuko huo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi mjini Bagamoyo.13Wahariri mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kufungua semina hiyo14Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi na Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wakiwa katika picha ya pamoja.15Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi katikati ni Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma na Anna Mziray Meneja wa Msoko na elimu kwa umma wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao  na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana. 
   Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua ndani ya Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.

   Pichani baadhi ya Screen zikionyesha picha mbalimbali za matukio yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC lililopatikana kwa msaada wa Serikali ya China.

   : Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Bw. Clement Mshana mara baada ya gari hilo kukabidhiwa na kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia matangazo la TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana.


   Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi vinavyorushwa na Startimes alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
   Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China jana jijini Dar es Salaam.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akijadiliana na jambp na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw. Jack Zhou.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja (OB Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa hotuba wakati wa hafla fupi ya makabidhiano na uzinduzi wa gari la kurushia matangazo(OB Van) la Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)  leo katika viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

  : Katikati Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwa na wake Makamu wa Rais wa China Li Yunchao kushoto kwa Waziri Fenella katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na wafanyakazi wa TBC na Startimes. Picha na Frank Shija. WHVUM  0 0
 • 06/27/14--09:08: KAAZI KWELI KWELI


 • 0 0

   Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke  akizungumza na wadau mbalimbali  wakati wa kujadili Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo leo jijini Dar es salaam. Mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kukusanya takwimu sahihi zinazokidhi viwango vya ndani na vile vya kimataifa.
   Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) nchini Tanzania Bi. Diana Tampelman  akizungumza na waandishi wa habari kupongeza  hatua iliyofikiwa katika kukamilisha Mpango mkakati wa Takwimu za Kilimo nchini Tanzania  na kueleza  kuwa hatua hiyo inaendana na  Mpango wa Dunia  ulioanzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kuboresha takwimu za kilimo maeneo ya vijijini.
   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Kijadili Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
  ======= ==== =====
   

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  inakamilisha  Mpango mkakati  wa Takwimu za Kilimo wa mwaka 2014/15  mpaka 2018/19  utakaoiwezesha Ofisi  hiyo kuendesha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za kilimo nchini kila baada ya miaka 5.

  Akizungumza wakati wa mkutano uliohusisha wadau mbalimbali wa kupitia  na kujadili rasimu ya mwisho ya mpango huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kukusanya takwimu sahihi zinazokidhi viwango vya ndani na vile vya kimataifa.

  Amesema  mpango mkakati huo unalenga kuboresha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za kilimo  hapa nchini  kwa kujenga mfumo mmoja wa utoaji wa takwimu za Kilimo kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuliko ilivyo sasa na kubainisha kuwa taarifa zote za shughuli za kilimo nchini zitaingizwa kwenye mfumo wa serikali.

  “Hapa tumekutana wadau mbalimbali kutoka  serikalini kwa maana ya wizara husika  na  wawakilishi kutoka mashirika ya maendeleo, lengo letu ni kupitia na kujadili rasimu hii ya mwisho itakayotuwezesha kujenga uwezo wa ndani wa  ukusanyaji wa takwimu za kilimo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa’’ Amesema

  Amefafanua  kuwa mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bara na ile ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar kupata takwimu za shughuli zote za kilimo kuanzia wazalishaji wenyewe, hali ya kilimo, mazao, masoko pia kutoa mwelekeo wa nini kifanyike kuboresha sekta hizo kupitia takwimu zitakazokusanywa.

  Aidha, amesema kuwa vipaumbele vya mpango huo vimeshaainishwa na kuwekwa mbele ya wadau ili kuwezesha upatikanaji wa nyenzo na uwezo wa kutekeleza mpango huo.

  Kuhusu kufanikisha  mpango huo Bw. Oyuke  amesema kuwa jopo la taifa la wataalam  limeundwa likihusisha wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na ile ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, Wizara husika za Kilimo, Chakula na Ushirika,Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Maliasili na Utalii pamoja na wataam kutoka mashirika ya maendeleo.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani(FAO) nchini Tanzania Bi. Diana Tampelman  amepongeza  hatua iliyofikiwa katika kukamilisha Mpango mkakati huo nchini Tanzania  na kueleza  kuwa hatua hiyo inaendana na  Mpango wa Dunia  ulioanzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kuboresha takwimu za kilimo maeneo ya vijijini.

  “Tunapongeza hatua hizi na tutaongeza nguvu zetu katika mpango huu ili kupata uhalisia wa shughuli za kilimo Tanzania kuhusu nani kazalisha nini na kwa kiwango gani ingawa watu wanaweza kushindwa kuona umuhimu wake lakini tunajua kuwa taarifa hizi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi” Amesema Diana.

  Naye mtaalam kutoka Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Bw. Mzee Mohammed Mzee akiwasilisha mada kuhusu Hali ya Takwimu za kilimo nchini amesema kuwa kwa kipindi kirefu takwimu za kilimo zimekuwa zikipatikana kupitia Wizara na Taasisi zenye dhamana ya usimamizi wa sekta ya kilimo na kusababisha upatikanaji wa takwimu zinazotofautiana kutokana na njia zilizotumika wakati wa ukusanyaji wa takwimu hizo.

  “Kisheria Ofisi ya Taifa ya Takwimu hapa nchini ndio yenye dhamana ya kukusanya  na kusambaza takwimu, suala la ukusanyaji wa takwimu lina njia zake, kumekuwa na shida ya ya njia za ukusanyaji wa takwimu hizi na wakati mwingine takwimu kutofautiana ,kukamilika kwa mpango mkakati huu kutaliondoa tatizo hili” Amesema.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014
  PICHA NA IKULU

  0 0

   Wakishindana  katika mchezo wa kuvutana kamba.
   Wafanyakzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na familia zao wakiwa kwenye foleni ya kupata msosi wakati wa hafla ya Siku ya Familia ya TBL,  kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Hoteli ya Bahari Beach, Kunduchi, Dar es Salaam.
   Badhi ya viongozi wa TBL wakistarehe  huku wakibadishana mawazo.
   Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Magese (kulia), akimkabidhi mtoto Said Shaban zawadi baada ya kuwa mmoja wa washindi wa mbio za watoto wakati wa hafla ya Siku ya Familia ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo, katika ufukwe wa Bahari ya Hindi karibu, Kunduchi, Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Mauzo wa TBO Kanda ya Kusini, James Bokela.
   Bendi ya Mashujaa iktoa burudani murwa.

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, akijisajili kushirikia kwenye tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014, kama ishara ya kuzindua tovuti hiyo, shughuli iliyofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi na Msemaji wa Wizara Nurdin Chamuya.


   Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo

  Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na hadhiri wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Wazara hiyo kuzungumza na kuzindua tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Kuhusu Tabia Nchi  ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea leo Juni 27, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea leo Juni 27, 2014.

  PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 308 | 309 | (Page 310) | 311 | 312 | .... | 1898 | newer