Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

JAMII YAASWA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilolo Ulbad Wampemba akizungumza na watoto na wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika kiwalaya yalifanyika katika ofisi za kijiji cha Ilamba kata ya Dabaga tarafa ya Kilolo mkoani Iringa.
 Baadhi ya watoto waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wakifatalia hotuba mbalimbali za viongozi walihudhuria sherehe hizo. Maadhimisho hayo kiwalaya yalifanyika katika ofisi za kijiji cha Ilamba kata ya Dabaga tarafa ya Kilolo mkoani Iringa.
 Watoto wa shule ya msingi Ilamba wakiimba wimbo maalum wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika.
 Watoto wa shule ya msingi Ilambawa wakionyesha baadhi ya mabango yenye ujumbe maalum za haki za watoto.
 Baadhi ya wakuu wa idara katika wilaya ya Kilolo wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akimkabidhi zawadi Blessing Kikoti mwanafunzi wa darasa la nne aliyefanya vizuri katika masomo yake kwa kuwa wa kwanza katika masomo.
Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akihutubia.(picha zote na Denis Mlowe)
 
Na Denis Mlowe,Iringa
 
JAMII imetakiwa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, kwa kuwapatia elimu iliyo bora na kuwapa upendo na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali kuwasaidia.
 
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Ilamba kata ya Dabaga tarafa ya Kilolo.
 
Guninita alisema jamii imekuwa ikiitupia lawama serikali mara kwa mara bila kutambua kuwa jukumu la kuwalea na kuwasaidia ni jukumu la kila mmoja katika jamii tunayoishi kwa lengo la kuwapatia elimu itakayowakomboa katika mazingira magumu.
 
Alisema jamii inatakiwa kupanga mikakati kabambe ya kuwaepusha watoto na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia au unyanyasaji wa aina yoyote katika maisha yao ya kila siku kwa kuwa nao wanahaki ya kuishi.
 
Aidha aliitaka jamii kuacha mila na tamaduni zilizopo katika jamii ambazo zinamnyima motto haki ya kupata elimu na kusababisha baadhi ya watoto kukimbilia mitaani kwa kuwa mila hizo zinakiuka misingi ya haki za msingi za mtoto.
 
"Ni kweli wilaya ya Kilolo ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo wilayani mwetu kama wanaoishi Amani Center ni jukumu la kila mmoja wetu kuwasaidia na kuwapatia elimu iliyo bora na kuwaondoa katika mazingira yasiyofaa katika jamii” alisema Guninita

Katika taarifa iliyosomwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Kilolo Issa Mohamed alisema jamii inatakiwa kuondokana na mila ambazo zinawazuia watoto kupata elimu au kuendelea na masomo kama vile ndoa za utotoni, ukeketaji na kusomesha watoto wa kiume.
 
“Wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuendelea na mila zenye madhara ambazo zinawasababisha watoto kutoendelea na masomo au kutoende shule kabisa kwa kufanya hivyo ni kukiuka haki ya msingi za watoto kwani watoto wana haki ya kulindwa na kupewa huduma zote za msingi ikiwemo elimu bora.” Alisema Mohamed
 
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo"

TUMETOKA MBALI: WAZO LA 'MJENGWABLOG' LILIZALIWA KWENYE MAZUNGUMZO HAYA NA ANKAL MUHIDIN MICHUZI.

$
0
0
Ankal akiwa na Mdau Maggid Mjengwa.

Ndugu zangu, 

Septemba kumi, 2006 nilikutana na ndugu na kaka yangu Muhidin Issa Michuzi pale Food World Restaurant, Maktaba Street, Dar es Salaam.

Kaka Michuzi na mimi tulizungumza kwa kirefu juu ya masuala ya kublogu. Wakati huo blogu ilikuwa ni kitu kipya sana hapa nyumbani. Na hakika hapa nyumbani alianza Muhidin Michuzi kuwa na blogu ya habari na picha. Mimi ni kati ya wachache tuliofuatia kwa hapa nyumbani.

Kwenye mazungumzo yetu pale Food World, nilimwambia Michuzi niwe nachangia kwenye Michuzi blog kwa kumtumia picha na habari kutoka vijijini, ni kwa vile nimekuwa nikiishi Iringa na kufanya kazi za vijijini tangu 2004. 

Michuzi aliniangalia na kusema; " Maggid, mimi nafikiri nawe uwe na blogu yako mwenyewe yenye kutoa zaidi taswira za maisha ya vijijini".

Michuzi na mimi tumefahamiana tangu miaka ya 80 mwishoni. Kilichotuunganisha na Michuzi tangu wakati huo ni picha, kama Michuzi, nami pia nimekuwa na mapenzi makubwa na picha tangu utotoni.

Michuzi aliufahamu uwezo wangu, na ndio maana akaona bora niongeze nguvu kwa kuanzisha blogu yangu mwenyewe.

Na ndipo hapo ' Mjengwablog' kama wazo l a ' blogu kama kijiji' likazaliwa, na Jumanne ya Septemba 19, 2006, ndipo picha ya kwanza na maelezo iliingizwa kwenye Mjengwablog. Naam, nimeratibu shughuli za ' Mjengwablog' kama ' Kijiji' tangu 2006. Ndio sababu ya kuitwa ' Mwenyekiti'. Ina maana ya ' Mwenyekiti' wa Kijiji cha ' Mjengwablog'!

Na profile picture yangu ya kwanza kwenye Mjengwablog ilikuwa nimetinga shati hilo hilo nililovaa nikiwa na Michuzi ( Pichani).

Hakika, nyingine ni kumbukumbu muhimu sana katika kuandika historia ya chimbuko la blogu Tanzania. Kuna umuhimu wa kuweka kumbukumbu hizi katika maandishi ili yasaidie vizazi vijavyo.

Maggid Mjengwa,
0754 678 252

MAAMBUKIZI YA VVU KITAIFA KWA WANAWAKE NI ASILIMIA 6.2 NA WANAUME NI ASILIMIA 3.8.

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Terezia Mmbando (kulia) akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi katika jiji la Dar es salaam kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho alipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ziara yake ya siku nne.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akitoa tathmini ya hali ya maambukizi ya VVU katika jiji la Dar es salaam na hatua zinazochuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukabiliana na janga hilo mara baada ya kupokea ugeni kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye pia ni diwani wa kata ya Gongolamboto akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho  kwa kuhusu hatua iliyofikiwa na mikakati ya manispaa ya Ilala katika kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (kulia) na Diwani wa Viti maalum Ilala Mh.Batuli Mziya (katikati) wakati wa ziara ya viongozi wa TACAIDS kata ya Gongolamboto.
Mmoja wa wanachama wa Asasi ya Vijana ya St. Camilus inayojihusisha na utoaji wa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa vijana kupitia sanaa mbalimbali Bi. Aquila Mawenya akisoma taarifa ya utendaji kazi wa asasi hiyo kwa  Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho alipokutana na wanachama wa Asasi hiyo Kiwalani jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (katikati) akiwa na baadhi ya wanachama Asasi ya Vijana ya St. Camilus inayojihusisha na utoaji wa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa vijana kupitia sanaa mbalimbali alipowatembela eneo la Kiwalani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya viongozi wa manispaa ya Ilala wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mh. Jerry Silaa (katikati) wakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho (wa tatu kutoka kulia) alipotembelea Kata ya Gongolamboto kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.
Picha na 10. Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akikutana na vijana wa kata ya Vingunguti wa Asasi ya Watoto na Vijana –CAFLO. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho  akizungumza na viongozi na wakazi wa kata ya Gongolamboto jijini Dar es salaam alipotembelea eneo hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.
Katibu wa mtandao wa Vikoba vya watu wanaoishi na VVU (IDINEPA VICOBA) kata ya Kiwalani Bw. Shaban Mwasa Wamikole akimkabidhi risala ya kikundi hicho  Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho alipokutana na wanachama wa kikundi hicho katika kata ya Kiwalani jijini Dar es salaam.
==== =======
MAAMBUKIZI YA VVU JIJINI DAR ES SALAAM YAPUNGUA.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
18/6/2014. Dar es salaam.

Licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali za udhibiti wa maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Jiji la Dar es salaam limefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 9.8 za mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 6.9 kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali zikiwemo za uundaji wa kamati shirikishi za mkoa kudhibiti maambukizi hayo. 

Hayo yamebainishwa  katika taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi iliyotolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Terezia Mmbando kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho alipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo.

Akisoma taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Bi. Mmbando ameeleza kuwa janga la Ukimwi ni tatizo la dunia nzima na limekuwa kikwazo cha maendeleo ya jamii hapa nchini na kuongeza kuwa jitihada za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi jijini Dar es salaam zimechukuliwa kupunguza maambukizi ikiwa ni pamoja na uanzishaji rasmi wa kamati za kuratibu na kusimamia shughuli za kudhibiti Ukimwi kuanzia ngazi ya mkoa, halmashauri, ngazi ya kata na mtaa.

Amesema jiji la Dar es salaam linakabiliwa na changamoto ya ongezeko la kubwa la watu ikilinganishwa na mikoa  mingine hali inayochangia mwingiliano wa tamaduni, shughulim mbalimbali, masuala ya kijamii,kimila na kiuchumi na kuongeza kuwa kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi 2012 idadi ya watu imefikia  4,364,54, wanaume wakiwa 2,125,786 na wanawake 2,238,755 sawa na ongezeko la asilimia 5 kwa mwaka.

Hali ya VVU na Ukimwi mkoa wa Dar es salaam.
Hali ya maambukizi ya Ukimwi katika jiji la Dar es salaam kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuhusu viashiria vya Ukimwi na Malaria mwaka 2011/2012 inaonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kitaifa ni wastani wa asilimia 5.1 ambapo maambukizi kwa wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8.

Sababu za maambukizi.
Miongoni mwa sababu zinazochangia kuendelea kuwepo kwa maambukizi mapya ya VVU katika mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na kasi ya ukuaji wa jiji na shughuli za kibiashara hali inayosababisha mwingiliano wa watu na mahusiano ya kimapenzi pia baadhi ya wakazi kutobadili tabia licha ya kupatiwa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ya ugonjwa huo.

Sababu nyingine ni hali ngumu ya uchumi hususani maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa wakazi wa kipato cha chini,kuongezeka kwa vitendo vya ngono isiyo salama hususani maeneo yenye nyumba nyingi za kulala wageni, kumbi za starehe, madangulo na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi ya madereva wa magari ya masafa marefu.

Aidha, ngoma za usiku zinazokesha  hasa maeneo ya pembezoni mwa jiji zinazoambatana na unywaji wa pombe kupita kiasi  na uwepo wa makundi maalum ya watu wanaofanya biashara ya ngono na wale wanaotumia dawa za kulevya hali inayowafanya washindwe kutoa maamuzi sahihi ya kujikinga na VVU ni miongoni mwa sababu zinazochangia maambukizi mapya ya VVU.

Hatua zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi.
Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri za manispaa na wadau mbalimbali pamoja na mambo mengine umeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU,kuhamasisha upimaji wa hiari wa VVU pia kuongeza nguvu katika mapambano ya kuzuia maabukizi kutoka mama kwenda kwa mtoto kupitia kliniki za afya ya uzazi. 

Hatua nyingine ni utoaji wa huduma za tiba na virutubisho kwa wagonjwa, kuwahudumia watoto yatima na wale wanaoishi mazingira hatarishi pia kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kuhamasisha uundaji wa vikundi vya ujasiriamali kwa wanaoishi na VVU ili waweze kumudu gharama za maisha na uundaji wa vikundi vya sanaa vya vijana kwa ajili ya kutoa elimu ya VVU na Ukimwi kwa vijana walio katika mazingira hatarishi ya maambukizi katika jiji la Dar es salaam.

WASHINDI WA CHEMSHA BONGO YA BRAZIL WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatano, Phillip Nkini (kulia) akimkabidhi Said Muhammed Muba zawadi yake ya dekoda na dishi.
Ofisa Mauzo wa Azam TV, Shah Seffu Mrisho (kulia)  akimkabidhi Allen John Muhuma zawadi ya TV na dekoda.
Ofisa Usambazaji wa Global, Benjamin Mwanambuu (kushoto) akiwa katika pozi na washindi Allen na Said pamoja na Nkini na Shah.
Washindi wa Chemsha Bongo ya Brazil, Said Muhammed Muba (kushoto) na Allen John Muhuma wakiwapozi na zawadi zao.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Innocent Mafuru (kulia) akipozi na washindi wa Chemsha Bongo ya Brazil. Kushoto ni Benjamin Mwanambuu na Ofisa Matukio na Mitandao ya Kijamii wa Azam TV, Irada Mtonga (katikati).
Allen John Muhuma akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani).
Ofisa Usambazaji wa Global, Benjamin Mwanambuu akielezea jinsi ya kushiriki Chemsha Bongo ya Brazil inayoendeshwa na magazeti ya Championi kwa udhamini wa Azam TV.
Said Mohammed Muba akipozi na dekoda yake.
Washindi hao baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

WASHINDI wa Chemsha Bongo ya Brazil ambayo inadhaminiwa na Azam TV, Allen John Muhuma na Said Mohammed Muba, wamekabidhiwa zawadi zao leo kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar.

Washindi hao ambao walifanikiwa kujibu ipasavyo maswali kwenye swali la Chemsha Bongo lililokuwa kwenye magazeti ya Championi ya wiki iliyopita, wamejishidia TV, dekoda ya Azam na dishi.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao walisema kuwa hii ni faraja kubwa sana kwao kwa kuwa wameweza kuboreshewa maisha yao na Championi. “Ukweli hii ni faraja kubwa sana kwangu na familia yangu, nimejisikia vizuri sana na kamwe sitaacha kushiriki kwenye kila toleo,” alisema Muba. Kwa upande wake Muhuma, alisema awali aliamini kuwa kuna watu huwa wanaandaliwa kwa ajili ya kushinda zawadi hizi.

“Hili limenifanya niamini kuwa Chemsha Bongo hizi ni za kweli, nimefarijika sana na niahidi kuwa nitashiriki kila siku na naamini nitashinda tena.” Ukitaka kushiriki Chemsha Bongo hii jibu swali ambalo lipo kwenye gazeti la Championi kisha tuma jibu lako kwenda namba 15564, hapo utakuwa umeingia moja kwa moja kama mshindani.

WARSHA YA TASAF ILIVYOZINDULIWA LEO NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS,MH.MOHAMMED ABOUD,ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akifunguwa Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania, ilioandaliwa na TASAF Taifa. Iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mkurugenzi Uratibu wa Shughuliza Serekali Zanzibar, Ndg Issa Ibrahim Mahmoud, akitiwa maelezo ya Ufunguzi wa Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania unaotekelezwa na TASAF, uliofanyika katika ukumbib mdogo wa Baraza la Wawakilishi Chukwani. Kushoto kwake Mkurugenzi wa Program wa TASAF Ndg Amadius Kamagenge akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud. Mohammed.



WASHIRIKI wa Warsha ya Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi wa Program wa Tasaf Ndg. Amadius  Kamangenge, akitowa maelezo ya Mradi TASAF.wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Yaliofanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Program wa TASAF Ndg Amadius Kamagenge, akitowa maelezo ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Ujenzi  ambayo pia itawanufaisha walengwa  wa mpango wa kunusuru kayacmasikini Tanzania.
Maofisa wa Mradi wa TASAF Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa semina ya Utekelezaji wa Mradi Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Ujenzi  ambayo pia itawanufaisha walengwa  wa mpango wa kunusuru kayacmasikini Tanzania. Wakati Waziri Aboud akifungua semina hiyo katika ukumbi mdogo wa baraza la wawakilishi chukwani Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Ndg. Ahmad Kassim, akitowa maelezo ya mafanikio ya Mradi wa Tasaf Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Mradi wa (PWP) .
Maafisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania TASAF,kutoka kushoto Ndg. Abass Saleh, Bi .Mary Kiula na Ndg. Geofrey Nyamwihula, wakijadiliana jambo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Warsha ya Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania, ilioandaliwa na TASAF Taifa. Iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akiwa katika picha na Maofisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) baada ya ufunguzi wa  Warsha ya Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania, ilioandaliwa na TASAF Taifa. Iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Washindi Promosheni Shinda Ki-Brazil na Mwanaspoti wazawadiwa

$
0
0


Washindi wa bahatinasibu ya Shinda Ki-Brazili na Mwanaspoti,Issa Rashid (wapili kushoto) na Michael Msumba (wapili kulia) wakipokea zawazi zao kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mult Choice ( Dstv ) Barbara Kambogi (kulia) na Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi,Edward Uisso.

======== ======= ========

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kupitia gazetilake la michezo la Mwanaspoti kwa kushirikiana na DSTV wamekabidhi zawadi za washindi wa kwanza wa ptomosheni ya Shinda Ki-Brazil iliyozinduliwa wiki iliyopita.

Washindi walizawadiwa ni Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla ambao walizawadiwa ving'amuzi na vifurushi vyake huku Jackson Fredrick wa Mwanza akikabidhiwa jozi ya jezi yenye jezi 16.

Mbali ya kukabidhi zawadi hizo, promisheni hiyo pia iliendesha droo na kupata washindi wapya. Washindi wa vingamuzi vya DSTV pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa mwezi mmoja (Compact Plus) waliopatikana ni Sharifu Migui (34) ambaye ni Fundi Magari, John Kilalago (39) ambaye ni Mlinzi, Mahmud Salum (54) ambaye ni Mtaalamu wa Takwimu wakati mshindi wa jozi moja ya jezi(ina jezi 16) ni Bariki Massawe(38) ambaye kazi yake ni mfanyabiashara.

Migui ambaye ni mkazi wa Mikumi Morogoro alisema, " Ninafuraha kushinda kwenye shindano hilo. Ni kitu rahisi kupata kama mtu unashiriki kwani unakuwa umejijengea nafasi ya kutosha endapo ninashiriki na mimi nimeshiriki mara nyingi ."

Massawe ambaye ni mkazi wa Tabata Kinyerezi alisema," Nimefurahi kushinda jezi baada ya kushiriki kwenye promosheni bomba ya Mwanaspoti. Jezi hizo nitatoa zawadi kwa timu yangu ya maveterani inayoitwa Kinyerezi Veteran FC."

Afisa Masoko wa Kampuni ya MCL, Edward Uisso, amesema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 24 za DSTV zilizounganishwa na kifurushi cha Compact Plus kwa muda wa mwezi mmoja, seti nne za jezi pamoja na fedha taslimu zinazotolewa kila siku mpaka shindano litakapomalizika.

Promosheni hiyo ambayo ilifunguliwa Juni 2 itafungwa Julai 13 siku ya mwisho ya fainali hizo.Ili kuendelea kushiriki, wasomaji wa Mwanaspoti watatakiwa kutuma namba zitakazopatikana kwenye ukurasa huu wa tatu wa gazeti la Mwanaspoti kwenda namba 15551.

Kwa mujibu wa vigezo na masharti ya promosheni hiyo, kila nakala ya gazeti la Mwanaspoti itakuwa na namba mbili za ushiriki zenye tarakimu nane kila moja.

Mshiriki ana hiari ya kutuma namba yoyote kati ya hizo kushinda aina moja ya zawadi, au akipenda anaweza kutuma namba zote mbili ili kujishindia aina zote mbili za zawadi.

Namba moja imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za binafsi. Namba ya pili imetambulishwa kwa herufi T na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za timu.

WASHINDI WA UTC WAREJEA TOKA BRAZIL.

$
0
0
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo akiwaongoza washindi wa tiketi ya Winda SAFARI YA Brazil na Serengeti mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere. Nyuma ni Bi Juliana Joseph Masawe(mshindi)
 Mshindi wa tiketi ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili nchini huku akiahidi kushiriki katika kila promosheni zitakazokuwa zikichezeshwa na kampuni ya SBL.
 Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha akihojiwa na waandishi mara baada ya kurejea nchini. Bw. Shayo alielekea nchini Brazil baada ya kushinda tiketi kupitia kampuni ya bia ya Serengeti. Shayo aliambatana na washindi wawili katika ziara ya utembelea vivutio mbalimbali.
 Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro akieleza kwa kufuraha juu ya mambo mazuri aliyoyaona nchini Brazil huku akiwashukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kumwezesha kula bata kiasi ambacho hakutegemea maishani mwake.
Pilikapilika za washindi mara baada ya kuwasili nchini kutokea Brazil kula bata baada ya ushindi kupitia kampeni ya Winda Tiketi ya Brazil na Serengeti iliyokuwa ikichezeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Lager. Kulia ni Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam, Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro (katikati) pamoja na kushoto ni mwenyeji wa washindi hao Bw. Allan Chonjo Meneja Masoko wa kampuni ya Serengeti.

Ni baada ya kutembelea vivutio mbalimbali nchini Brazil

17/06/2014, Washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti waliokwea pipa wiki iliyopita kuelekea nchini Brazil kutembelea vivutio mbalimbali wamerejea kwa shangwe kubwa baada ya kuyaona maisha mapya ya bara jingine. Ziara yao ilichukua siku tano nchini Brazil huku washindi hao wakila bata katika vivutio mbalimbali nchini Brazil.


Washindi wa tiketi hizo Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro, Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam pamoja na Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha wamerejea nchini wakiwa na mwenyeji wao Bw Allan Chonjo ambaye ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Washindi hao walijishindia tiketi hizo baada ya kutumia bia ya Serengeti na kufungua chini ya kizibo ili kushinda na hivyo walijipatia tiketi za kwenda nchini Brazil kutembelea vivutio mbalimbali.


Juliana Joseph Masawe amewapongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwa wakweli na kuwajali wateja wao. “Sitasahau starehe nilizoziona nchini Brazil. Siku tano zimakuwa kama siku mbili. Nilitamani kukaa mwezi. Najivunia kutumia bia ya Serengeti kwani imenionjesha maisha tofauti kabisa. Mwanzo nilijihisi uoga kwani sikuwahi kupanda ndege lakini kupitia bia ya Serengeti nimepanda ndege, nimetembelea vivutio mbalimbali, nimeona makanisa makubwa mno sijawahi kuona, mashamba makubwa ya mpunga na mihogo pia nimekutana na watu wapya kabisa katika maisha yangu”.  


Nae Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha  alishindwa kujizuia kwa furaha wakati akihojiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere “Sio siri najiona mpya kabisa sikutegemea kufika nchini Brazil katika maisha yangu, kila promosheni itakayotolewa na Kampuni ya bia ya Serengeti  lazima nitashiriki kwa sababu hawana upendeleo kabisa kama ni mshindi basi utapewa kile unachostahili. Kampuni ya bia ya Serengeti imenifanya niwe na kitu cha kuhadidhia maisha yangu yote, naamini familia yangu itafurahi zaidi nikiwapa habari za nchini Brazil.


Mwenyeji wa washindi hao Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti  Bw. Allan Chonjo amewashukuru sana washinidi kwa kuichagua bia ya Seregeti na kushiriki katika promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti. “Ninaamini mmefurahia ushindi wenu. Bila shaka mtakuwa mabalozi wa bia ya Serengeti kila mtakapokuwa. Promosheni hii ililenga kawashukuru wateja wetu kwa kuichagua bia ya Serengeti kuwa kinywaji chao. Tumerudisha fadhida kwa wateja wetu kama shukrani kwao kwani bila wao sisi tusingeweza kusonga mbele”.

WATU WAWILI WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA WAKIWA KWENYE JARIBIO LA KUTAKA KUPOA FEDHA KWA MTEJA BENKI YA NMB

$
0
0
Watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa wakiwa katika jaribio la kupora fedha kwa mmoja wa wateja ndani ya benki ya NMB tawi la uwanja wa ndege, Dar es Salaam wakiwa na pikipiki aina ya Boxer. Watuhumiwa hao wameuawa na wananchi wenye hasira, huku polisi kanda ya Dar-es-Salaam wakiwashikilia watu watatu, miongoni mwao akiwemo mganga aliyekuwa akiwatibu kwa nguvu za giza na kudai kuwapa nguvu

ESCAPE ONE FULL KUJIBWENDENGA KILA IJUMAA

INNOCENT NGANYAGWA KUTUMBUIZA TAMASHA LA ZIFF 2014 USIKU HUU NDANI YA UKUMBI WA MAMBO CLUB, NGOME KONGWE

$
0
0
DSC_0276
Mwanamuziki Mkongwe wa Rege nchini, Innocent Nganyagwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na show yake kwenye tamasha la ZIFF 2014 usiku wa leo ndani ya ukumbi wa Mambo Club kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.Kushoto Mtaalamu wa masuala ya habari ZIFF, Bw. Dave Ojay.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
DSC_0094
Baadhi ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari wanaohuduria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.

BAADA ya kutoa demo katika mkutano wake na waandishi wa habari, mkali wa rege nchini Innocent Nganyagwa ameahidi kuporomosha muziki mzito katika ukumbi wa mambo klabu leo usiku.

Katika demo ambapo alipiga verse ya gila, mkali huyo aliwataka wazanzibari kuingia kwa wingi kuona sweet reggae baada ya mfumo wa Babylion wa ukombozi kumalizika.

Anasema kwamba wapenzi wake watarajie vitu vipya kuonesha kwamba yeye hajalala kwa miaka yote hata baada ya kuonekana kuwa nje kwa miaka 9.Nganygwa mwenye tuzo tano za nyumbani na albamu nne katika mikono amesema kwamba kimya chake kilitokana nba kuamua kusuka kizazi kipya cha rege kupitia kampuni yake ya Reggae Production.

Akizungumza kuhusu muziki wake alisema kwamba yeye anapiga muziki wa rege lakini si kwa mtazamo wa Jimmy Clief,Bob marley na Burning Spear ; ni muziki wenye utamaduni wa nyumbani na hivyo kwua na rege yenye utambulisho wa Tanzania.

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa Shisha.

$
0
0
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana wadogo mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara. Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavitaji wa sigara.

UHAMIAJI WAKANUSHA JUU YA MHAMIAJI ALIYEDAIWA KUTOROSHWA

$
0
0
IMG-20140618-WA0007
Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba akikanusha vikali taarifa za  aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
IMG-20140618-WA0006
Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
IMG-20140618-WA0008
Waandishi wa habari wakiwa kazini

Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa za  aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa na kueleza kuwa mtu huyo alipatiwa notice ya kuondoka nchi ambapo Juni 10 mwaka huu aliamriwa kuondoka nchi Juni 13 huku akisindikizwa hadi mpaka wa Namanga na si uwanja wa Kia kama ilivyoelezwa.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari amesema kuwa Maofisa wa Uhamiaji walimkamata Jaques na kumpatia notice ya kuamriwa kuondoka nchini na si kutoroshwa na kufafanua kua uamuzi huo ulizingatia taratibu zote za kisheria.

Nanomba alisema kuwa Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Afrika kusini  na alikua mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambao tumewaita na kuwaonya.

Afisa huyo amesema kuwa hawamzuii Mwajiri yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya nchi na hivyo kuwataka waajiri wahakikishe kuwa watu hao wana kibali cha kufanya kazi nchi vinginevyo watachuliwa hatua kali na kuongeza kuwa hadi sasa wamewachukulia hatua waajiri watano.

Kwa kipindi cha Januari hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku nchi ya Kenya ikiwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao nchini.

Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13,Ethiopia wanne,Kongo 4,Ghana 4,dachi 3,Marekani mmoja na kutoka nchi nyingine
Pia  wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa nchini.

(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

WADAU WA SEKTA YA MAWASILIANO WAKUTANA ARUSHA

$
0
0
IMG-20140618-WA0010
Mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi ambaye pia ni  mkurugenzi mkuu  wa tume ya mawasiliano nchini Kenya
IMG-20140618-WA0004
 Mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Uganda Patrick Mwesigwa
IMG-20140618-WA0001
 Mkurugenzi wa  Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema
IMG-20140618-WA0005
Balozi Joseph  Bangurambona wa Burundi akiongea juu ya mkutano huo
IMG-20140618-WA0002
IMG-20140618-WA0003
Wadau wakifuatilia mkutano leo jijini Arusha
IMG-20140618-WA0009
IMG-20140618-WA0011
Kulia Pamela Mollel wa jamiiblog na Jusline Marcko wa gazeti la Siha Leo.
IMG-20140618-WA0012

Wadau  zaidi ya mia moja kutoka taasisi za mamlaka ya mawasiliano Afrika Mashariki (EACO} wamekutana jijini Arusha ili kuangalia namna ya kuweza kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo muhimu ya mawasiliano.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi  ambaye pia ni  mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Kenya alisema kuwa mkutano huo unalenga kujadili  changamoto zilizobainishwa na wadau wa sekta hiyo kuhusu vikwazo ambavyo vinakwamisha mbalimbali  usambazaji wa mawasiliano kwa nchi hizo.
 
Wangusi alisema kuwa  sekta ya mawasiliano ina vitengo mbalimbali ikiwemo posta,mawasiliano ya simu na utangazaji na mitandao ya kijamii(internet) ambayo bado inakabiliwa na changamoto nyingi  zinazohitaji juhudi za wadau wa sekta hiyo ili kuwafikia watumiaji.
 
Aidha alibainisha kuwa huduma ya posta bado inakabiliwa na changamoto ya anuani makazi ili kuwawezesha watumiaji  wanaoutumia huduma hiyo iweze kuwafikia kwa haraka kama zilivyo huduma nyingine.
 
Hata hivyo wangusi aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa ni mawasiliano ya huduma za simu katika nchi za Afrika mashariki ambapo mbali na watoa huduma kupata faida kubwa lakini pia wanawatoza watumiaji gharama kubwa hivyo kupelekea watumiaji kutoka nchi moja hadi nyingine kushindwa kumudu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema alisema lengo ni kuangalia kuwa mawasiliano yanawafikia watumiaji  na kufaidi huduma hiyo ya simu,internet,utangazaji na maswala ya posta.


(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

WANANCHI WAMGOMBEA AMINA MAIGE ANAYETUHUMIWAA KUMNG'ATA MSICHANA WA KAZI WAKATI AKIPELEKWA KIZIMBANI

WASHINDI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KWA KANDA YA PWANI WAPATIKANA NA KUKABIDHIWA VITITA VYAO PAPO HAPO

$
0
0
 Majaji wakiwa kazini katika Shindano lililofanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza.Picha na Maktaba.

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions, Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Kwa KAnda ya Pwani limemalizika leo Mkoani Dar Es Salaam mara baada ya washindi watano watakaoiwakilisha Kanda hii katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane kupatikana katika Ukumbi wa Makumbusho na hatimaye washindi hao Kukabidhiwa shilingi laki tano taslimu.

Shindano hili lilianza tarehe 30 Mei 2014 na kusimama kwa Muda kutokana na Msiba wa George Tyson ambae alikuwa ni mzazi mwenza wa jaji Yvonne Cherry au Monalisa. Katika Kuungana nae katika kipindi kigumu alichopitia Timu nzima ya TMT ilibidi kusimamisha Shindao hilo Kwa Muda hadi pale Msiba kumalizika, na Baada ya Msiba kumalizika Shindano hili liliendelea tena mnamo tarehe 15 June 2014 na kufikia tamati leo kwa Washindi watano Kupatikana.

Kanda ya Pwani inahusisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar Es Salaam ambapo takribani washiriki 300 waliweza kujitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili kwa Kanda ya Pwani. Washindi watano waliopatikana katika Kanda ya Pwani wataungana na Washindi wengine kutoka Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini ambao walishapatikana kwaajili ya kuingia kambini ambapo wawakilishi hao wa kanda hizo watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu wa Sanaa wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na hatimaye wataendelea na mchujo ambapo Mshindi mmoja ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.

Vilevile vipindi vya Shindano hili vinarushwa katika kituo cha runinga cha ITV siku ya Jumamosi saa 4 Usiku na Marudio yake ni Saa 10 Jioni siku ya Jumapili na Jumatano ni saa 5 usiku. Na Jumamosi ya Wiki kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa muda ule ule wa Saa 4 Usiku siku ya Jumamosi na marudio yake siku ya Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 usiku.
Washindi wa Kanda zote wanatarajia kuwasili katika Nyumba ya TMT hivi karibuni kwaajili ya Kuanza kambi kwaajili ya safari ya kuwania Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Vilevile katika Fainali hiyo washindi kumi bora watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano hili na hatimaye wataweza kufanya kazi ya pamoja na hatimaye kunufaika na Kazi hiyo.

Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) lilianza safari zake za kusaka Vipaji katika Kanda ya Ziwa na kuendelea na zoezi hilo kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini na hatimaye safari hizo zimefikia tamati leo mara baada ya washindi watano kupatikana kutoka Kanda ya Pwani.

Shiwata kugawa mashamba kwa wanachama wake

$
0
0

 MTANDAO WA WASANII TANZANIA   (SHIWATA)
Umeamua kutoa ofa ya kugawa shamba lake la ekari 500 lililoko Mkuranga mkoa wa Pwani kwa wanachama wake wenye uwezo wakulima mazao mbalimbali yatakayochangia kupunguza uhaba wa chakula nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Mtandao wa SHIWATA, Cassim Taalib kwa vyombo vya habari inasema wanachama watakaogaiwa shamba hilo ni wale walio hai waliolipia ada zao watapaswa kutoa sh. 200,000 kulipia ekari moja atakayopewa.

Alisema kuratibu mpango huo SHIWATA imeitisha mkutano wa wanachama wote Jumamosi Juni 21,2014 kwenye ukumbi wa Splendid Ilala ili kujadili mambo mbalimbali katika kijiji cha wasanii Mkuranga ambacho mpaka sasa kimejenga na kukabidhi nyumba 66 kwa wanachama wake kati ya 265 wanaojenga nyumba zao kwa njia ya kuchangishana.

"Ujenzi wa nyumba za kisasa katika kijiji chetu cha Mwanzega Mkuranga chenye ukubwa wa hekari 300 unaendelea tunatarajia kukabidhi nyumba 40 Desemba mwaka huu katika sherehe kubwa ambayo tunatarajia kumpata mgeni rasmi kutoka ngazi za juu" alisema Mwenyekiti.

Alisema shiwata inawataka wanachama wote ambao hawakuwahi kwenda kuona au kukabidhiwa viwanja au nyumba zao kutokana na sababu mbalimbali wafike na kadi zao ofisini Ilala Bungoni Chuo cha Splendid kabla ya Jumatano Juni 19, 2014 ili wakakabidhiwe nyumba zao na kiwanja vyao Jumamosi Juni 21, 2014 saa 2 asubuhi kwa nauli ya sh. 10,000 ya kwenda na kurudi.

Aliwatoa wasiwasi wanachama waliokuwa wanahofia kuwekeza katika ujenzi wa nyumba kuwa mpango wa kupimia wasanii nyumba zao ili wapate fursa ya kukopa kutoka benki mbalimbali za hapa nchini umeanza kushirikiana na Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya Mkuranga ikifuatiwa na ujenzi wa barabara, uvutaji wa umeme na uchimbaji visima vya kisasa unafanyiwa kazi.

Aliwahimiza wanachama wanaochangia ujenzi wa nyumba zao kukamilisha michango hiyo ili wakabidhiwe nyumba zao kukamilisha malengo ya kuwasaidia wasanii kujikwamua kiuchumi.

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) ulianzishwa mwaka 2004 na kusajiliwa na baraza la sanaa tanzania shiwata mwaka 2005 pia imesajiliwa na brella kwa shughuli za kiuchumi ikiwa na dira ya kuwakomboa wasanii kuwa na maisha bora kupitia mtandao huu ifikapo mwaka 2015.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda 0715/0752 222677.

Benki ya Exim yatoa milioni kumi kupiga jeki miradi ya wazee

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Risks na Compliance wa Benki ya Exim, David Lusala (wapili kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa Mweka Hazina wa Tushikamane Pamoja Foundation (TPF), Ana Rupia (wapili kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa benki hiyo kupiga jeki miradi ya TPF ya kuwasaidia wazee wasiojiweza. Wakishuhudia ni Meneja wa Fedha Mwandamizi wa Benki ya Exim, Issa Hamisi (katikati) na Meneja Masoko Msaidizi wa Benki hiyo Anita Goshashy
Mkuu wa Kitengo cha Risks na Compliance wa Benki ya Exim, David Lusala (wapili kushoto) akionyesha hundi ya shilingi milioni 10  baada ya kukabidhi hundi hiyo kwa Mweka Hazina wa Tushikamane Pamoja Foundation (TPF), Ana Rupia (wapili kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa benki hiyo kupiga jeki miradi ya TPF ya kuwasaidia wazee wasiojiweza. Wakishuhudia ni Meneja wa Fedha Mwandamizi wa Benki ya Exim, Issa Hamisi (kulia) na Meneja Masoko Msaidizi wa Benki hiyo Anita Goshashy (kushoto).

BENKI ya Exim Tanzania imekabidhi hundi ya shilingi milioni kumi kwa taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) ikiwa na lengo la kusaidia wazee wasiojiweza wanaoishi katika kaya zaidi ya 40 jijini Dar es Salaam.
Taasisi hiyo ambayo kwa sasa inasambaza chakula na vitu binafsi kwa kaya 40 jijini Dar es Salaam kila mwezi pia utekeleza miradi mbali mbali ambayo ni pamoja na matibabu kwa kundi hilo maalum.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Risks na Compliance wa Benki ya Exim, David Lusala alisema kuwa benki inajua umuhimu wa kuchangia sehemu ya pato lake kwa jamii, kwa njia ya miradi ambayo inabadilisha au kuboresha viwango vya kijamii na kiuchumi kwa jamii.

"Benki ya Exim imekuwa makini sana katika kusaidia jamii ianyoizunguka. Kama sehemu ya shughuli zetu za kijamii, leo tunakabidhi shilingi milioni 10 kwa taasisi ya TPF ili kupiga jeki miradi yao iliyoanzishwa ili kusaidia wazee wasiojiweza na jamii kwa ujumla.

"Nauasa uongozi wa TPF  kuhakikisha kuwa fedha hizi tulizochangia zinaelekezwa kwenye matumizi yaliyokusudiwa ili kuwawezesha watu wasiojiweza kufaidika na shughuli zenu zenye malengo mazuri ya kuboresha maisha yao," alisema Bw Lusala.

Alibainisha kuwa benki ya Exim itaendelea kuelekeza fedha zake katika kusaidia miradi ambayo ni chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini ili kusaidia kuboresha hali ya maisha ya jamii.
Kwa upande wake, Mweka Hazina wa Tushikamane Pamoja Foundation, Bi. Ana Rupia ameipongeza Benki ya Exim kwa msaada wake na kusema kuwa fedha hizo zilizopokelewa na TPF zitaelekezwa katika miradi ambayo tayari iliyoundwa kwa lengo la kuwasaidia wazee wasiojiweza.

"Tuna mpango wa kujenga nyumba kwa ajili ya wazee katika kata ya Kwembe, Wilayani Kinondoni ambayo itakuwa kama makazi ya wazee wasiojiweza. Nyumba hiyo itatoa urahisi wa wazee hao kupata huduma za matibabu, usimamizi wa karibu na huduma nyingine za kiubinadamu kwa walengwa.

"Sasa tunasubiri kibali cha ujenzi kabla ya kuanza kazi ya ujenzi rasmi. Tunaishukuru Benki ya Exim kwa msaada wao na nazisihi taasisi nyingine kuiga mfano huu mzuri wa kuigwa,” Bi Rupia alisema.

MUCCoBS YAWAKUTANISHA WANATAALUMA NA WAAJIRI KATIKA CAREER DAY.

$
0
0
Baadhi ya wananfunzi katika chuo kikuu cha Ushirika na Biashara Moshi(MUCCoBS)wakiwa katika ukumbi wa Nyerere kufuatilia Career Day iliyofanyika chuoni hapo.
Wanafunzi wanaochukua taaluma mbalimbali walipata nafasi ya kuwaeleza waajiri nini wanaweza kufanya pindi watapato nafasi ya kuajiri wa katika taasisi ,kampuni na mashirika mablimbali.

Baadhi ya wanafunzi wa taaluma mbalimbali walioshiriki kutoa mada katika siku ya Career iliyofanyika chuoni hapo.
Baadhi ya waajiri.
Wawakilishi wa kampuni ya Marenga Investment ya mjini Moshi.
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu taaluma ya Meneja rasilimali watu ,Rusma Ndosi akitoa maelezo kuhusuana na taaluma yake hiyo na kwa nini ni muhimu kwa waajiri kuchukua wananfunzi katika chuo hicho.
Wanafunzi wanaochukua taaluma mbalimbali walipata nafasi ya kuwaeleza waajiri nini wanaweza kufanya pindi watapato nafasi ya kuajiri wa katika taasisi ,kampuni na mashirika mablimbali.

Mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Marenga Jonas Mshiu akizungumza na wananfunzi wa Chuo kikuu cha Ushirika na Biashara ,MUCCoBS wakati wa siku ya Career Day.
Wanafunzi wanaochukua taaluma mbalimbali walipata nafasi ya kuwaeleza waajiri nini wanaweza kufanya pindi watapato nafasi ya kuajiri wa katika taasisi ,kampuni na mashirika mablimbali.

Kampuni ya Fast Jet iliwakilishwa na kiongozi wa timu ya Mauzo wa Fast Jet kanda ya kaskazini Neema David.
Kwa upande wa wanahabari Fadhili Athumani wa kampuni ya New Habari alipata kuzungumzia nafasi ya waandishi wa habari katika kufanikisha malego ya wanataaluma.
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya siku ya Career katika chuo kikuu cha Ushirika na Biashara ,MUCCoBS wakiwa katika pozi la picha.
Washiri katika siku ya Career katika picha ya pamoja.

Kamati ya maandalizi ya Career Day.
Mshauri wa wanafunzi chuo kikuu cha Ushirika na Biashara Moshi ,Mr Machimu akiteta jambo na baadhi ya wakufunzi. 
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

NGUMI KUPIGWA ULONGONI B JUNI 21 GONGOLAMBOTO

$
0
0
 Bondia Said Uwezo kushoto akifundishwa jinsi ya kutupa makonde na Shujaa Keyakeya wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Thobias Adaut katika ukumbi wa Swai pub ulongoni 'B' gongolamboto picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Abdallah Mbela kushoto akipiga ngumi kwa Said Uwezo wakati wa mazoezi ya kujianda kupambana juni 21 Uwzo atapambana na Thobias Adaut katika ukumbi wa swai pub ulongoni 'B'  gongolamboto

MASHINDANO YA NGALAWA YANOGESHA TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014 VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
DSC_0217
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya resi za Ngalawa wakijiandaa tayari kwa kuanza mashindano hayo katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF 2014 linaloendelea visiwani Zanzibar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Ripota , Zanzibar.

NGALAWA zote 11 zilizoingia majini kukamilisha mzunguko wa saa mbili wa resi za ngalawa mjini Zanzibar zilimarisha mashamshamu hayo bila najali na timu tatu zilipewa zawadi za ushindi. Resi za Ngalawa kama zinavyojulikana ni utamaduni halisi wa visiwa vya pemba na Unguja na ni sehemu ya tamasha kubwa la filamu la kimataifa la Zanzibar ambalo linaendelea visiwani hapa.

Kwa wale waliozaliwa maeneo ya bara, resi hizi zilikuwa kivutio kikubwa kwao kutokana na maandalizi yanayofanywa kabla ya kuingia majini na dau kunyanuliwa.

Wakati dau limenyanyuliwa, maji yamekuwa yakichotwa ama ndani ya Ngalawa au nje katika bahari kumwagia tanga katika hali inayoelezwa kuliimarisha katika ukinzani wa upepo.

“mbio za Ngalawa ni kipimo kikubwa cha Uzanzibari wetu na kila mwaka ZIFF huhitimisha utashi wake wa kuwa na tamasha la nchi za jahazi kwa kuwa na mbio za ngalawa” alisema mshehereshaji Muslim Nassoro Abdalla katika shamrashamra zilizofanyika ufukweni kandoani mwa hoteli ya Tembo.
DSC_0235
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (mwenye t-shirt ya njano) akupiliza Kipenga kuashiria kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za Hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.

Muslim ambaye alisema kwamba mwaka huu walitaka kuwa na mbio za timu 20 (ngalawa) walishindwa kuhitimisha ndoto hiyo kutokana na masuala nje ya uwezo wa ZIFF.

Ili kukamilisha vyema mbio hizo kunatakiwa kuwa na boti za kutosha za uokozi kama kutatokea ajali. Mwaka juzi kulitokea ajali ambayo hata boti ilipofanya uokozi nayo ikazidiwa na kulazimisha watu kukwama mpaka jioni walipopata boti nyingine kutoka Bandarini.

Wakati wa mbio za resi ambazo washindi wa kwanza ni timu iliyokuwa ikiongozwa na Hatibu Suleiman waliokuwa ndani ya ngalawa Ipo Siku, ngoma mbalimbali za asili zilipigwa ufukoni kama hamasa huku watu wakisubiri marejeo ya ngalawa hizo.
DSC_0241
Baadhi ya Ngalawa zinazoshiriki mashindano hayo zikianza kukata mawimbi.

Mbio hizo ambazo zilianzishwa na mbunge wa Kiembesamaki na Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mahmoud Thabiti Kombo mshindi wake wa pili alikuwa ni timu ya haji Hassan (kama nadhodha) ndani ya ngalawa Kipanga. Aidha Hassan Simai na wenzake waliokuwa katika ngalawa iliyoitwa peace of Love walikuwa washindi wa tatu.

Timu ya ngalawa ambayo inahitaji ujuzi katika utekaji tanga , kulirekebisha na kubalansi ngalawa inahitaji watu wapatao watano na si chini ya watatu.
Tamasha la filamu linaendelea mjini hapa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya utunzi, utengenezaji wa filamu na uhakiki wake.
DSC_0262
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakishuhudia mashindano hayo.
DSC_0280DSC_0266 Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ( wa pili kulia) akiwa meza kuu na mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo Mohammed DSC_0299DSC_0268
Burudani ya Ngoma kutoka Nungwi ikitumbuiza wakati wa mashindano hayo.
DSC_0314
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akionyesha moja ya zawadi t-shirt kwa watoa burudani waliokuwa wakishindana kucheza ngoma za asili.
DSC_0286
Mkazi wa Nungwi na Stone town (mwenye kaptura) wakishindana kutoa burudani ya ngoma za asili za visiwani humo wakati wa mashindano hayo.
DSC_0325
Mshehereshaji wa tamasha la ZIFF 2014, Muslim Nassor akimuonyesha moja ya zawadi (haipo pichani) mkazi wa Stone town aliyekuwa akisherehesha wakati wa mashindano ya Ngalawa kwenye fukwe za hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
DSC_0581
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa tatu nahodha wa resi za Ngalawa iliyopewa jina la " Peace of life" M, Bw. Hassan Simai.
DSC_0586
Mshindi wa tatu nahodha wa resi za Ngalawa, "Peace of life" Bw. Hassan Simai katika picha ya pamoja na mdhamini wa Ngalawa yao iliyopewa jina la " Peace of life" Mkurugenzi mtendaji wa Zanlink, Bw. Sanjay Raja.
DSC_0593
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili nahodha wa resi za Ngalawa iliyopewa jina la "Kipanga" Haji Hassan. Katikati ni mdhamini wa Ngalawa ya Kipanga, Bi. Latifa Mohamed Omar kutoka Zan Air.
DSC_0594
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa nahodha mashindano ya resi za Ngalawa, Bw. Khatib Suleiman katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF linaloendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.
DSC_0598
mshindi wa kwanza wa mashindano ya resi za Ngalawa, Bw. Khatib Suleiman (kushoto) akipongezwa na mdhamini wake mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (katikati). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live


Latest Images