Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

Airtel Divas watoa msaada kwa wanawake wasiojiweza

0
0
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (kushoto), huku akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Happy John wakikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa kikundi hicho, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA), kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Divas. 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (wa pili kulia), akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA ) cha Kinondoni, kabla ya kuzindua rasmi Kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). Kushoto ni mwanachama wa Swauta, Adelina Mluge.
  Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Airtel Divas, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). 
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (kushoto), akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia), baada ya kutembelea bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kabla ya kuzindua rasmi Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
 Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, wakilisakata rhumba, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kikundi hicho, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro, akifurahia zawadi ya kitenge baada ya kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba (kulia), katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Picha ya Pamoja

========  ========
Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel ujulikanao kama Airtel Divas umejitoa kuwasaidia na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA )  kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao wa Airtel walifanya uzinduzi rasmi wa Airtel Divas  na kualika kikundi cha SWAUTA kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wafanyakazi wa Airtel na kuwawezesha kupata fedha kwaajili ya kuwa na banda lao katika maonyesho ya 38 ya kimataifa  ya SABASABA.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja Rasilimali watu Sophia Melamali alisema” tunayofuraha kuzindua rasmi Airtel Divas mpango maalumu wenye lengo la kuwainua na kuwahamasisha wanawake na wafanyakazi wa Airtel kuzifikia ndoto zao. Kama tunavyofahamu wanawake wanayo majukumu makubwa ya familia na kazi,  hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kugawa muda wao kwa ufanisi. kwa kupitia Airtel Divas tunashirikiana kwa pamoja kupeana ujuzi na mawazo ya namna ya kupambana na changamoto hizi na kufikia mafanikio katika malengo tuliyojiwekea.

Sambamba na hilo tunawahamasisha wanawake kushiriki katika kujitolea na kutoa msaada kwa jamii na ndo maana leo tumewaalika kina mama hawa wenye ulemavu na kuwapa nafasi ya kuuza bidhaa zao na kiasi cha pesa watakachopata leo tutakiongeza mara mbili na kuwawezesha kupata fedha za kutosha kulipia banda katika maonyesho ya sabasaba. Tunaamini kwa kufanya hivi tutawawezesha kukuza biashara yao. Natoa wito kwa watanzania watakaopata nafasi ya kwenda kwenye maonyesho haya wapate nafasi ya kuwatembelea na kuwaaunga mkono pia.

Akiongea mara baada ya kukabithia msaada huo mwenyekiti Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania SWAUTA bi Stella Jairosi Alisema, Tunawashukuru Airtel kwa kutuwezesha kupata banda zuri liliopo eneo zuri katika maonyesho ya Sabsaba, kwa miaka 8 sasa tumekuwa tukishiriki katika maonyesho haya lakini hatukuwahi kuwa na banda letu wenyewe. Kupitia msaada huu kutoka Airtel kutatupatia mwanya wa kuonyesha bidhaa zetu na kupata mwaya wa kuuza kwa soko la ndani na la nje na pia kutatusaidia kuuza bidhaa zetu kwa kiasi kikubwa na kuongeza pato letu na hivyo kuendeleza miradi ambayo hatukuweza kuifanya kutokana na uhaba wa fedha.

Kwa upande wake mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro alisema“ nimejisikia furaha kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya leo na napenda kuwapongeza sana Airtel Divas kwa kujitolea kusaidia jamii kupitia shughuli hizi za huduma kwa jamii wakiwemo wa mama hawa wa kikundi cha walemavu nawahamasisha muendelee na juhudi hizi.Pamoja na hayo pia nachukua nafais hii kuwahimisha Airtel Divas kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha uwezo wao katika maeneo yao ya kazi ili waweze kupata nafasi nyeti katika Uongozi

MUME WA FLORA MBASHA APEWA DHAMANA

0
0
Mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akipelekwa mahabusu ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar....Emmanuel Mbasha akifungiwa ndani ya mahabusu.…
Mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akipelekwa mahabusu ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar.
...Emmanuel Mbasha akifungiwa ndani ya mahabusu.
...Askari Magereza akifunga mlango wa mahabusu.
...Emmanuel Mbasha akielekea kizimbani.
MUME wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) anayekabiliwa na kesi ya ubakaji amepewa dhamana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar baada ya kutimiza masharti.
Mbasha amefikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Keko alikopelekwa Juni 17 mwaka huu akikabiliwa na kesi ya kumbaka shemeji yake.
Mbasha baada ya kutolewa kwenye mahabusu ndogo ya mahakamani hapo alionekana mnyonge na aliyechoka hali iliyosababisha simanzi kwa ndugu na jamaa zake waliokusanyika mahakamani hapo.
Baada ya kesi hiyo kutajwa, rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa mtuhumiwa huyo, Mwahimu Juma walifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana.
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)

PRIMIA YA AFRIKA YA "HALF OF A YELLOW SUN" YAFANYIKA ZANZIBAR

0
0
Half of a Yellow Sun FILM TIE IN B PB.inddDSC_0234
Dairekta wa filamu ya Half of a Yellow Sun, Biyi Bandele akizungumza na wadau wa sinema kabla sinema yake hajafanyiwa Primia ya Afrika mjini Zanzibar. Kushoto ni mratibu wa majaji ZIFF, Fabrizio Colombo kutoka Italia.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
TANZANIA imebahatika kufanya Primia ya Afrika kwa sinema ya Half of a Yellow Sun , miezi miwili tu baada ya sinema hiyo kuzuiwa kimtindo nchini Nigeria ambako mtengenezaji ndiko nyumbani kwake. Sinema hiyo ilioneshwa jana katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe.

Sinema hiyo ambayo imefanyiwa kazi kwa miaka 6 ni miongoni mwa sinema ndefu bora tatu ambazo zipo katika mashindano kwenye tamasha la filamu la Kimataifa la Zanzibar, ZIFF.Sinema nyingine zenye ubora mkubwa na ambazo zimevutia wapenzi wengi wa sinema ni The Thorn of The Rose kutoka Guinea Bissau na Mandela:Long walk to Freedom ya Afrika Kusini.

Pamoja na ugumu wa masuala mbalimbali yanayozungumzwa katika filamu za The Thorn of The Rose na Half of a Yellow Sun watu wa Zanzibar wakiwemo madairekta, maprojuza na waigizaji wa ngazi za kimataifa 30 kutoka nchi 14 mbalimbali walizikubali filamu hizo.

Filamu iliyoleta kizaazaa kikubwa cha fikira ni The Thorn of the Rose. Sinema hii ya aksheni yenye mapenzi yenye vurugu, rushwa , utendaji mbovu wa wanasiasa na vyombo vya dola na imani kuhusu mzimu uliofanyiwa vibaya ukiwa dunia kutopumzika mpaka mambo yamerekebishwa si ajabu ikatwaa tuzo kwa jinsi ilivyotulia.

Muigizaji wa sinema hii Ady de Batista kutoka Guinnea Bassau alikuwepo kushuhudia namna ambavyo wapenzi wa sinema wanavyoipokea sinema yake hiyo yenye ukakasi maeneo mengine, hasa ubakaji uliokuwa unafanywa na ofisa wa polisi cha mdada mhusika hadi kifo chake.
DSC_0015
Wasanii mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa katika moja ya mikutano ya wasanii na waandishi wa habari kwenye tamasha linaloendelea la nchi za majahazi ZIFF mjini Zanzibar.(Picha zote na zainul Mzige wa Mo blog).

Sinema ya Half of a Yellow Sun, inayotambulika kimataifa na kufanya vyema katika mabara mengine, ilkioneshwa kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika nchini Tanzania katika onesho la Jumatano wiki hii Ngome Kongwe.

Sinema hiyo iliyotokana na kitabu chenye jina kama hilo cha mwaka 2006 iliyoandikwa na kuongozwa na Biyi Bandele inaonesha namna gani dairekta huyo amekomaa katika miaka yake 20 ya utengenezaji wa sinema.

Sinema hiyo ambayo ilizuiwa kuoneshwa Nigeria miezi miwili iliyopita katika kile ilichodai bodi ya sensa ya nchi huyo kutoona mahali sinema hiyo inaweza kufiti katika viwango cha uonekanaji na dai la kuwa inaweza kuchochea ghasia, ni moja ya sinema iliyoangalia kwa undani vurugu za Biafra na maisha kuendelea ndani ya vurugu hizo. Ikiwa imetumia miaka sita kutengenezwa sinema hiyo ni moja ya sinema tunazoweza kusema kwamba ni babu kubwa kutokana na simulizi lake na uigizaji ukiongozwa na kinara wake Thandie Newton.

Pamoja na kwamba Bandele amekuwa akilaumiwa kwa kumweka Newton katika kinara cha uigizaji katika simulizi hilo anasema kwamba hiyo si kweli kwani anaona kwamba kazi na maamuzi yake yamekuwa mema na ya maana zaidi kuliko kipindi chochote cha kazi yake kama dairekta.
Pamoja na kuonesha sinema tamasha la 17 la filamu la ZIFF pia limeendelea na program zake nyingine kama watoto na wanawake na soko la wanawake mwaka huu limefanya vyema zaidi.

UNICEF Launches Tanzania Music Video to Prompt Action to End Violence against Children

0
0
UNICEF Launches Tanzania Music Video to Prompt Action to End Violence against Children Dar es Salaam, Tanzania, 19 June 2014 - UNICEF today launched a creative video initiative in support of the #ENDviolence movement, designed to reinforce the growing global momentum to end violence against children. This includes connecting with, and engaging parents and care givers to tackle violence against children and find solutions to prevent and end it in their own communities. 

The video features the single ‘Our Navigation’ from the UK-based electronic music band Four Tet’s latest record, ‘Beautiful Rewind’, on Text Records. The release is part of UNICEF’s ground breaking #ENDviolence initiative, a global movement to raise awareness and spark local action to combat violence against children by making violence more visible. 

UNICEF’s newly-appointed National Ambassadors for Tanzania’s #ENDviolence initiative, hip-hop star Ambwene Yessayah, better known as AY, and former Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu, helped to launch the video. AY and Faraja, who have an impressive following in the country, featured in the video to highlight the important role of young people in the national response to violence against children. "Acting in this video is very meaningful for me. 

I am a mother and I expect children to be protected by each one of us. Violence is everywhere. It happens in Tanzania, and across the globe, at all levels of society. Ending violence is everyone’s business. Silence is not acceptable. I am committed to keep using my voice to ensure that we all speak out and put an end to violence against children," Faraja Kotta Nyalandu said.

MIRADI YA MAENDELEO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE YAENDELEA KUKAGULIWA

0
0
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango wa Halamashauri ya Wilaya ya Rungwe wakikagua tenki la maji katika kata ya Kyimo
Jengo la hostel ya wasichana katika shule ya sekondari ya Lupoto, linaendelea kujengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe


Wajumbe wa Kamati ya fedha wakiwa pamoja mbele ya jengo la Shule inayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Ikuti.

Kwa Picha na habari zaidi bofya 

WARSHA YA KUJENGA UWEZO WA MUZIKI NA SARAKASI KWA WATOTO NA VIJANA YATOLEWA

0
0

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Center Bw.Mgunga Mwamnyenyelwa kilichopo mburahati kwa jongo wilaya ya kinondoni Dar es salaam, akizungumzia juu ya kituo hicho kinavyo fanya kazi na sababu za kuwakusanya watoto hao katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuwajengea uelewa zaidi na kuwafundisha vitu mbalimbali kama Ngoma, Sarakasi, ushonaji ili baadae waweze kuja kujitegemea wenyewe.

Meneja mradi wa Fit For Life Habiba Issa akielezea kwa kina juu ya Mradi huo pamoja na malengo yake

Daniela Titze International Relation Fit For Life
 Mani kutoka Ujerumani na ambaye pia ni Mwalimu wa Ngoma ya Brazil Samba Rege akielezea mafanikio na jinsi mafunzo yanavyo endelea.
Kikundi cha ngoma ndani ya kituo cha Baba watoto pamoja na wanafuzi waki achia burudani ya muziki aina ya Samba Rege
Mwalimu Daudi akiwa ana piga ngoma aina ya Samba Rege
Moja ya mambo yanayo fanywa katika kituo cha baba watoto utengenezaji wa maleba(costumes)
Vijana wakiwa katika mazoezi
Vijana wakifanya mafunzo ya serekasi katika kituo cha Baba watoto center

Kituo cha kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu cha Baba watoto center kupitia mradi wa FIT for –LIFE kinacho endesha mafunzo ya sanaa kwa watoto walio kati ya umri wamiaka 10 hadi 15 mpaka 25 aina ya mafunzo yanayo tolewa na pamoja na sarakasi ,muziki wa aina ya samba rage,kituo hicho kilichopo wilayani kinondoni  ambapo mradi huo ni wamiaka mitatu kutoka mwaka  2013 hadi mwaka  2016

Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyo andaliwa kwaajiri kuwafundisha vijana ambao nimaalumu kwaajili ya kuwa waalimu watakao weza kuwafundisha wanafunzi  katika kituo hicho mkurugenzi mtendaji wa kituo Ndugu Mgunga Mwamnyenyelwa ameeleza jinsi kituo hichokilivyo weza kuanzishwa katika maeneo ya mburahati  na wakazi wa maeneo hayo kuweza kufaidika na kituo hicho ,vilevile ameeleza changamoto wanazo kumbana nazo katika kituo hicho,

Mradi huo wa FFL unao fadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) ambao unaendeshwa  kwa hisani ya Goethe-Institute kama msimamizi mkuu amapo meneja wa mradi Habiba Issa ameeleza jinsi mradi huo unavyo endeshwa ikiwa lengo la mradi huu ni kuendeleza kukuza kwa vipaji kwa vijana na kuweza kujipatia fura mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa mwalimu katika sehemu tofauttofauti za mradi huo

Aidha meneja huyo bi. Habiba Issa amesema kuwa wameamua kuanzisha mrahi huu wa ili kuweza kuwasaidia vijana hususani walio maliza katika viwango mbalimbali vya elimu kwani wameweza kuwaandalia mazingira mazuri ya kujifunza uselemala,utengenezaji wa  maleba (costomes)kwaajili ya sanaa,uandaaji wa jukwaa(stage desgn) na matumizi ya mfumo wa sauti na mwanga katika maonyesho ya sanaa.

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Bw.Mgunga na Meneja Mradi wa FIT For the Fit Habiba Issa wameweza kutoa rai kwa wazazi na vijana mbalimbali waewez kutumia fursa zinazo onekana hata kufikia malengo yao waliweza kutoa mifano mbalimbali ambapo waliweza kuwataja wahitimu wallio hitimu na kuweza kuwa waalimu na wengine kutoka nne ya nchi ikiwa ni idadi ya zaidi ya wanafunzi 5 ambao waliweza kwenda nchini idia na nchi jirani,kwa wazazi wawe na moyo wa kuwaleta watoto ili waweze kupata elimu ya sanaa mbalimbali waache zana potofu ya kuwa sanaani uhuni usio kuwa na faida hayo yamesemwa na viongozi hao wa mradi huu.

WAZIRI HAWA GHASIA AZINDUA KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Henry Mambo akiwakaribisha washiriki pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia(huyumo katika picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano la miaka 50 ya muungano katika utumishi wa umma ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere katika  leo, jijini Dar es Salaam.

 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Hawa Ghasia (hayumo katika picha), wakati wa ufunguzi wa kongamano la miaka 50 ya Muungano katika utumishi wa umma, katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam, leo .

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma,katika  ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere leo jijini Dar es Salaam, kongamano hilo la siku mbili linaambatana na maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Watumishi wa umma na washiriki  wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma wakimfuatilia kwa makini mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Hawa Ghasia (hayumo katika picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere  leo, jijini Dar es Salaam. 

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Miaka 50 katika  Utumishi wa Umma baada ya kufungua rasmi kongamano hilo la siku mbili Juni 19 na 20 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere, jijini Dar es Salaam. Lengo la kongamano ni kujadili maada mbalimbali zinazohusu utumishi wa umma. (Picha na Lorietha Laurence).

=========  ========  =======
Na Ismail Ngayonga

Maelezo

Dar es Salaam

19. Juni, 2014

SERIKALI imewataka wananchi kuzingatia taratibu za kimsingi  zinazopaswa kufuatwa na mteja wakati wa ufuatiaji na utoaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na watoa huduma katika sekta ya Utumishi wa Umma nchini.


Rai hiyo imetolewa leo tarehe (19. Juni, 2014) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia wakati alipokuwa akifungua kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam. Waziri Ghasia alisema katika utoaji wa huduma za umma, mwananchi ambaye ndiye mteja mkuu katika utumishi wa umma ana wajibu wa kuwasilisha taarifa muhimu zitakazoombwa na mtoa huduma wa sekta ya umma, na mwananchi atapaswa kuziwasilisha kama sehemu ya udhibitisho wa kutolewa kwa huduma husika.

“Kwa mfano mwananchi anayehitaji huduma ya cheti cha kuzaliwa kwa mtoto wake atapaswa kuwasilisha kadi ya hospitali, ambayo itaombwa na mhudumu wa afya, hivyo ni wajibu wa wananchi kutimiza kigezo hicho kama sharti la msingi la kupatiwa huduma hiyo” alisema Waziri Ghasia.


Akifafanua zaidi alisema ni dhahiri zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya umma na zipo zinazofanyiwa kazi na baadhi yake zinazohitaji ushirikishwaji wa wadau na kwa kulitambua suala hilo  Serikali iliandaa kongamano hilo ili kuisaidia kutekeleza mipango yake kwa ufanisi kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.


Aidha Waziri Ghasia alisema katika kipindi cha miaka 50 ya utumishi wa Muungano, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuimarisha sekta ya utumishi wa umma ikiwemo ubunifu wa Sera mbalimbali zinazotekelezwa kupitia kamati za mashauriano baina ya pande mbili za Muungano.


Waziri Ghasia aliongeza kuwa zipo changamoto mbalimbali za kimaendeleo zinazolikabili taifa, ambapo kwa kiasi kikubwa utatuzi wake unategemea namna sekta ya utumishi wa umma ilivyojipanga na kutekeleza wajibu wake.


“Sekta binafsi, Asasi za Kiraia na Sekta isiyo rasmi ni sekta muhimu kwa maendeleo ya Taifa kuweza kukaa pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu katika maeneo yetu, na zote kwa pamoja zina mchango mkubwa kwa kuwa zinasaidia kuwasilisha mawazo ya jamii Serikalini” alisema Waziri Ghasia.


Aliongeza kuwa mwaka 2011 Serikali ilibuni sera ya ushirikiano baina yake na sekta binafsi yaani Private Partnership Policy iliyopitishwa mwaka 2010 na kufuatiwa na sheria ya kutekeleza sera hiyo na kwa upande wa Asasi za kiraia upo mwongozo wa kushirikiana na asasi hizo uliotolewa mwaka 2012.


Akizungumzia suala la maadili katika utumishi wa Umma, Waziri Ghasia alisema wapo baadhi ya watumishi wanaokiuka maadili ya kazi ingawa si wote, kwani kwa sasa Serikali inatafakari changamoto na mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka 50 ya utumishi wa Umma nchini.


Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu alisema maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni maonesho ya wazi na yanahudhuriwa na wananchi wote yanayotoa fursa kwa watoa huduma a,bao ni taasisi za umma kukutana moja kwa moja na wateja na wananchi kwa upande mwingine.

“Utaratibu huu unatumika kuelimisha na kuonesha aina ya huduma zinazotolewa na watumishi wa umma kwa wananchi” alisema Mkwizu.

WATOTO MFANANO KUKARIMIWA NGOME KONGWE

0
0
DSC_0147
Mwenyekiti na mwasisi wa kikundi cha kujitolea kinachowalea watoto wenye mfanano wa kikundi cha Trabajo Voluntario, Marisa Yussuf Himid akionyesha bango wakati maandalizi ya shughuli hiyo.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

ZAIDI ya watoto mfanano 50 na familia zao wanatarajiwa kujumuika na watu wengine katika viwanja vya Ngome Kongwe kwa mashamushamu ya kuonesha upendo na kushuhudia mateso yanayowapata watoto hao.

Taasisi isiyo ya kiserikali ya kujitolea ya mjini Zanzibar ya Trabajo Voluntario, (Voluntary Work) inakutanisha watoto hao wakishirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF).

Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa Trabajo Voluntario, Marissa Himid Yusuf taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 ili kusaidia watoto mfanano, lengo lao kubwa la kuwakusanya hapo ni kuwaonesha upendo na pia kujadili maslahi yao.

Alisema kwa sasa watoto wengi wenye hali ya ufanano hawatimiziwi haki zao msingi ikiwemo ulinzi na wala hakuna sera inayohakikisha kwamba wanalindwa na wanapewa haki nyingine kama watoto wengine hasa elimu itakayowawezesha kuwa na kitu cha kufanya katika maihs ayao.

Alisema katika maelezo yake kwamba kuna simulizi za kutisha kuhusu watoto hao na kwamba wapo baadhi ya wanwake wapo tayari kutoa nushuhuda wa yaliyotokea katika famulia zao baada ya watoto walionao kubainika kwamba wana tatizo la mfanano.

Alisema pamoja na ushuhuda huo mkusanyiko huo umelenga pia kukemea maovu wanayofanyiwa watoto hao na watu wazima kwamkusanyiko huo ni kuelimishana kuhusu watoto hao na kuhimiza ushiriki wa serikali na jamii kuhakikisha usalama wao na kupata haki yao ya msingi ya kupendwa na kulindwa.
DSC_0136
Alisema pamoja na kuwapo kwa haja ya sera zinazotekelezeka ili kutoa ulinzi kwa watoto na familia zao, ipo haja kw ajumuia kuondoa unyanyapaa dhidi yao. Kwa kusanyiko hilo la Ijumaa tunategemea wananchi watakuja kujifunza kuondokana na unyanyapaa na pia kufanya kampeni ya kuondoa hali hiyo miongoni mwa jamii.

Marisa Yussuf Himid, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya TrabajoVoluntario, alisema mamlaka zinaozhusika zinaonekana kukimbia jukumu la kulea watoto hao ambao wana manufaa makubwa katika jamii wakielekezwa na kujua.

Aidha alitumia wasaa kuiomba serikali na mamlaka zake kuangalia suala la kunyan yaswa kwa watoto hawa, kufuatilia na kuwafikisha kizimbani wale wote wanaowatesa watoto hao kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwabaka, kuwanajisi na hata kuwalawiti. Aidha ametaka shule kutumika kufunza watoto hawa ambao elimu yao huchukua muda mrefu.

Kwa mujibu wa Marissa mgeni rasmi atakuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya ulemevu, AbedaAbdallah Rashid, ambaye atazungumza.
Aidha balozi wa watoto mfanano Fareed Kubanda, atazungumza wakati wa kufunga kusanyiko hilo.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA KICHOCHO LEO

0
0
 Mkuu wa Divishen ya Elimu Zanzibar Maalim. Ahmed Abdul-majid ambae ni Mgeni rasmin siku ya Kichocho Zanzibar, akihutibia wananchi na wanafunzi waliofika katika hafla hiyo huko Skuli ya Mwera Wilaya ya Kati Unguja ambapo kunasadikiwa kuwa na wingi wa Koa wambukizao Kichocho
  Wanafunzi wakionyesha picha jinsi ya maambukizi ya Kichocho yanavyopatikana. 
 Sehemu ya wanafunzi waliofika katika sherehe ya siku ya Kichocho inayoadhimishwa kila mwaka hapa Zanzibar. 
 Aina za Konokono wanaoambukiza Kichocho na wale wasio ambukiza.
Sehemu wanaopenda kukaa Konokono wanaoambukiza Kichocho. Mto wa Mwera Wilaya ya Kati Unguja.

AJALI YA ROLI YATOKEA ENEO LA KINYEREZI/UKONGA NA KUNG'OA DARAJA

0
0
 Lori likiwa limedondoka pamoja na Daraja Eneo la Majumba sita
 Wakazi wa Eneo hilo wakitazama ajali hiyo iliyotokea jioni ya leo
 Kama Unavyoona Roli limeng'oa daraja na kudondoka hivy njia haipitiki

WANAFUNZI DAR WAVUTIWA NA SHUGHULI ZA NISHATI NA MADINI

0
0
 Kamishna Msaidizi wa Madini, Uratibu, Mhandisi John Shija  akiwaeleza  wanafunzi  namna shughuli za  uchimbaji madini zinavyofanyika nchini  wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika Maonesho  ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja , Jijini Dar es Salaam 

  Mtaalamu wa madini ya Vito vya Rangi na Almas Bibi Teddy Goliama kutoka Kitengo cha Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini, akiwaeleza wanafunzi kuhusu aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara.  Anayesikiliza wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Uratibu, Mhandisi John Shija.

Mhandisi  Mwandamizi  Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) akitoa ufafanuzi kuhusu namna Shirika hilo linavyofanya kazi kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Taasisi hiyo.

1.  Afisa Habari kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Yisambi Shiwa, akiwaonesha baadhi ya madini yanayopatikana nchini wanafunzi waliotembelea banda la TMAA.

========  =======
Wanafunzi Dar es Salaam Wavutiwa na Shughuli za Nishati na Madini

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Baadhi ya Wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari mbalimbali Jijini Dar es Salaam wametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini yake kutaka kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na zinazofanyika.


Wakati wanafunzi hao walipotembelea Wizara na Taasisi zake, wameoneshwa kuvutiwa na kutaka kufahamu kuhusu namna shughuli za uchimbaji madini nchini zinavyofanyika, kutaka kufahamu aina za madini yenye thamani kubwa na  madini yenye uzito mkubwa.


Vilevile, wanafunzi hao wametaka kuelimishwa kuhusu shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi zinazofanyika nchini ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu vyuo mbalimbali vinavyotoa mafunzo kuhusu masuala ya gesi, mafuta na madini.


Aidha, wengi wao walipenda kuona madini ghafi ya Tanzanite yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na kufahamu aina zote za madini yaliyopo chini. Wanafunzi hao wamepata nafasi ya kupata majibu kuhusu masuala mbalimbali waliyouliza kutoka kwa waatalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi waliopo katika maonesho hayo.


Xxxxxxx    xxxxxxx     xxxxxxxx



ZANZIBAR YAPANIA KUMALIZA MARADHI YA KICHOCHO

0
0
 Naibu Waziri wa Afya Zanzinzibar Dkt. Sira Ubwa Mamboya akifungua Mkutano wa kufanya tathmini mafanikio ya changamoto za mradi wa miaka mitano wa kutokomeza maradhi ya Kichocho Zanzibar (kushoto) Prof. David Rollinson Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya wanyama, na (kulia) Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Juma Rajab. 
 Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa kutathmini mafanikio ya changamoto za mradi wa miaka mitano wa kutokomeza maradhi ya Kichocho Zanzibar uliofanyika Juni 17 katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
  Prof. David Rollinson Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya wanyama na, akielezea hatari za ugonjwa wa Kichocho na athari zake katika Mkutano huo.


Mgeni rasmin Naibu Waziri wa Afya Zanzinzibar Dkt. Sira Ubwa Mamboya katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano huo, huko Zanzibar Ocean View Hotel Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo ZNZ).
======  ======= =======
NGUVU za pamoja kati ya Wizara ya Afya Zanzibar, Nchi Washirika wa Maendeleo na Taasisi ya SCORE yenye makao makuu yake jijini Georgia Marekani, zimesaidia kupunguza kasi ya maradhi ya kichocho Unguja na Pemba.


Aidha mafanikio hayo yameelezewa kuwa yametokana na mkakati madhubuti uliowekwa na wizara hiyo kuhakikisha inatokomeza kabisa maradhi hayo yanayowaathiri kwa kiasi kikubwa watoto wenye umri kati ya miaka 7 na 14.


Akifungua mkutano wa kufanyia tathmini mafanikio ya changamoto za mradi wa miaka mitano wa kutokomeza maradhi hayo nchini Zanzibar huko hoteli ya Zanzibar Ocean View, Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya, amesema ufanisi huo usingepatikana bila ya ushirikiano kati ya pande hizo.


Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya Juma Duni Haji, Dk. Sira amesema mpango huo ulihitaji nyenzo za kitaalamu na fedha nyingi, ambazo Serikali ya Zanzibar isingeweza kumudu kwa wakati muafaka bila kushirikisha wadau mbalimbali wa kimataifa.


Amesema chini ya uongozi wa Profesa Dan Colley wa Chuo Kikuu cha Georgia, utafiti ulifanyika kwa mafanikio ili kubaini ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa kichocho nchini.


Mapema akiwasilisha ripoti ya utafiti wa Kitengo cha Maradhi Yasiyopewa Kipaumbele Dk. Khalfan Mohammed, amesema kwa sasa mradi huo wa miaka mitano ambao umetimiza miaka miwili, unahusisha shehia 90 (Pemba 45, Unguja 45).


MAREHEMU EDWARD KAHURANANGA KUZIKWA KESHO IJUMAA NYUMBANI KWAKE VIKINDU JIJINI DAR

0
0


Mwandishi na mtangazaji wa habari wa siku nyingi, Bwana Edward Kahurananga, amefariki dunia hapo juzi tarehe  17/6/2014 baada ya kuugua na kulazwa kwa muda mfupi.


Marehemu Edward Kahurananga alizaliwa tarehe 25 Desemba, 1949 katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma. Alihitimu elimu ya Sekondari mwaka 1968 katika Sekondari ya Livingstone iliyoko mkoani Kigoma.


Katika uhai wake alisoma vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari ndani na nje ya nchi. Mwaka 1970 aliajiriwa na Radio Tanzania Dar es Salaam kama Mtangazaji Msaidizi daraja la III. Alifanya kazi katika ngazi  mbalimbali katika mikoa katika mikoa kadhaa nchini chini ya Radio Tanzania Dar es Salaam .


Baadaye aliteuliwa kuwa  Mhariri wa Habari Mkuu wa Radio Tanzania Dar es Salaam kabla haijaunganishwa na Televisheni ya Taifa kuunda TvT ambayo baadaye ilibadilishwa kuwa TBC.  Mwaka 2004, Marehemu Edward Kahurananga alihamishiwa Idara ya Habari-MAELEZO kama Afisa Habari Mkuu.Wakati ule Idara ya Habari ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.  


Tarehe 25 Desemba, 2009, Edward Kahurananga alistaafu kazi kwa mujibu wa kanuni za Utumishi wa Umma wakati huo Idara ikiwa imehamishiwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


Edward Kahurananga alianza kuugua akiwa Mwanza na kulazwa katika hospitali ya Bugando lakini akahamishiwa hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ambapo amefia tarehe 17 Juni, 2014 wakati wakiendelea kujaribu kuokoa maisha yake.Atazikwa kesho (Ijumaa) tarehe 20 Juni, 2014 nyumbani kwake Vikindu jijini Dar es Salaam.


MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

AMINA

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YASHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI MNAZI MMOJA.

0
0

Usikose kusikiliza kipindi cha NJE-NDANI Jumamosi hii

0
0
Haika Lawere akiwa tayari kwa mahojiano na Kwanza Production ya Washington DC
 Katika NJE-NDANI ya Kwanza Production na Border Radio wiki hii, mbali na habari kuhusu Afrika, utasikia mahojiano yangu na Haika Lawere.

Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mbezi Garden Hotel ya Dar Es Salaam Tanzania,Amekuwa mkarimu sana kujiunga nami hapa Maryland USA kuzungumza mengi kuhusu maisha na ujasiriamali.
Haika Lawere akizungumza na wanawake kwenye tukio la wanawake waTanzania Washington DC
Photo Credits: IskaJojo Studios 
Usikose kujiunga nami Mubelwa Bandio jumamosi katika kipindi cha NJE NDANI kuanzia saa sita mpaka saa nane mchana kupitia www.kwanzaproduction.com ama www.bordermediagroup.com

2 DAYS TO GO....

0
0
Peace and Blessing of Allah be with you,

Alhamdulillah, we are set for another Ramadhan with another Welcoming Ramadhan Conference 1435H.

Tanzania Muslim Professionals Association (TAMPRO) is again bringing to you the 6th Welcoming Ramadhan Conferences 1435H that will be held on 22nd June, 2014 at Julius Nyerere International Convention Centre - Shaban Robert Street Posta/Gymkhan Area.


The Conference will bring together more than 600 Practitioners, Scholars and Experts to discuss and share their knowledge and experience on the Islamic principles, instruments and issues related to Raising Muslim Youth in today's world through the 1435H theme of“Our Youth, Our Future”.

Professor Mohamed Badamana From Nairobi University - https://profiles.uonbi.ac.ke/badamana/content/prof-badamana-mohamedSheikh Mussa Kundecha, Amir The Supreme Council of Islamic Organizations - Baraza Kuu, Brother Ali Masoud aka Masoud Kipanya http://www.kipanya.de/aboutcartoonist.htm will lead the presentations to inspire the fruitful discussion on 1. Challenges of raising the Muslim Youth in Today's Rapid Changing world, 2. The Qur'an, The Country Constitution and The Future of Muslim Youth 3. Muslim Youth, Media and Globalization, respectively.

The participation contribution is TZS 30,000 per person ( Lunch and Other Goodies Inclusive).

Days are numbered Book your Sit NOW,
Kindly call 0712588375 OR 0686666686.

BARAZA LA WAZEE KANISA LA MORAVIAN TABATA LAWATOA HOFU WAUMINI, LAKANUSHA TAARIFA YA KUZUILIWA KWA IBADA.

0
0
 Wakili wa kujitegemea wa Baraza la wazee wa kanisa la Moravian Usharika wa Tabata Bw. Benjamin Mwakambe akiongea na waandishi wa habari kuhusu amri ya iliyotolewa na mahakama kuzuia Bodi ya wadhamini wa kanisa la Moravian Kanda ya Kusini kusimamisha huduma za kiroho na kijamii katika eneo hilo. Wengine ni Mzee Kiongozi wa Usharika huo Bw.Ernest Isakwisa(kulia) na Hamphrey Mgema (kushoto)
Baadhi ya Wazee wa Kanisa la Moravian usharika wa Tabata wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari.
=======  ======== ======
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
19/6/2014.Dar es salaam.

Uongozi wa Baraza la wazee wa Kanisa la Moravian usharika wa Tabata jijini Dar es salaam umekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa huduma za kiroho na kijamii katika ushirika huo zimesimamishwa kufuatia mgogoro wa uongozi wa usharika huo kupelekwa mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa niaba ya Baraza la wazee wa usharika wa Moravian Tabata Mzee Kiongozi, Bw. Humphrey  Mgema amesema kuwa  usharika huo ambao uko chini ya jimbo la Mashariki linaloongozwa na Mwenyekiti,Mchungaji Dkt.Clement Fumbo umekuwa katika mgogoro wa uongozi kwa zaidi ya miaka 2 na uongozi wa jimbo la Kusini linaloongozwa  na Askofu Lusekelo Mwakafwela.

 Amesema tofauti za uongozi na hasa baraza la wazee wa usharika huo  kutokubaliana na baadhi ya maagizo ya askofu Mwakafwela na Bodi ya Wadhamini kuhusu umiliki na uangalizi wa usharika huo vimesababisha Bodi hiyo kwenda mahakamani kuzuia kufanyika kwa shughuli zozote katika eneo la usharika huo. 

“Yapo mambo mengi ambayo ni kiini cha mgogoro huu lakini jambo kubwa ni hatua tuliyoichukua ya kutokubaliana na baadhi ya maagizo yake ambayo yalionekana kutolinufaisha kanisa na hasa madai ya Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Moravian kanda ya kusini kututaka sisi tutamke wazi kuwa wao ndio wamiliki halali wa kanisa hilo” Amesema.

Ameeleza kuwa tamko la maaskofu lililotolewa na mwangalizi wa Kanisa la Moravian jimbo la Kusini askofu Lusekelo Mwakafwela katika ushirika wa Kinondoni kuzuia ibada na shughuli za kijamii katika usharika wa kanisa hilo eneo la Tabata halikubaliki na kuongeza kuwa limeleta athari kwa washirika wa kanisa hilo zaidi ya 700 na kuwafanya baadhi yao kushindwa kuhudhuria ibada.

Aidha,amesema  kufuatia mgogoro huo kushindwa kupatiwa ufumbuzi katika ngazi za juu za kanisa hilo na hatua iliyochukuliwa ya kuwapeleka mahakamani wao kama baraza la wazee wameamua kuadai haki yao kupitia Wakili wa kujitegemea Bw. Benjamin Mwakambe.

 Amesema kuwa licha ya baadhi ya mashauri kuendelea kusikilizwa mara mahakama imetoa Amri kuwa shughuli za ibada na kijamii katika usharika huo ziendelee kama kawaida.

Kwa upande wake wakili wa kujitegemea wa Baraza la wazee wa kanisa hilo Bw. Benjamin Mwakambe amefafanua kuwa hukumu ya mahakama iko wazi na kuongeza kuwa maombi ya Bodi ya wadhamini yalikataliwa mahakamani.

“Mahakama imeshaamua katika masuala haya kuwa ile jamii iachwe na wala isibugudhiwe na mtu yeyote na kama kuna usumbufu wa aina yoyote utakaofanywa dhidi yao ni wazi watakuwa wamedharau amri ya mahakama”

NEC kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

0
0
 Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) wakati wa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini, kulia ni Mkurugenzi wa uchaguzi toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Julius Mallaba.

 Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini. 
 Baaadhi ya wakuu wa Idara toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.

 Waandishi wa habari wakifanya kazi yao kwa umakini wakati Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini. 
Baadhi ya wahariri wakimfuatilia mtoa mada  kwa makini toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Julius Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.


Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO.


====== ===== =====
NEC kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Na: Frank Shija, Maelezo



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarijia kuanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mapema mwezi Septemba 2014, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na upikaji wa Kura za Maoni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Damian Lubuva wakati akifungua Mkutano wa NEC na Wahariri wa Vyombo vya Habari, leo jijini Dar es Salaam. Jaji Lubuva amebainisha kuwa uborehasji wa Daftari la Wapiga kura litatumia mfumo mpya wa Kiteknolojia ujulikanao kama Biometric Voter Registration (BVR) ambapo katika mfumo huo taarifa za mtu za Kibiolojia au tabia ya mwanadamu zitachukuliwa na kuifadhiwa kwenye kanzi data ya Wapiga Kura. 

Katika mfumo huo wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na Kadi za Mpiga Kura watatakiwa kuandikishwa upya ili kupata Daftari sahihi linaloaminika zaidi kwa ajili ya upigaji Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Uamuzi wa kutumia mfumo huo mpya wa kuandikisha wapiga kura umefikiwa baada ya kubaini kasoro mbalimbali zilizokuwepo kutokana nma kutumia mfumo wa zamani wa Optical Mark Recognition (OMR) hadi kupelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kupigia kelele mfumo huo, Aliongeza kuwa kutumiika kwa mfumo wa BRV kutasaidi kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo ikiwemo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.

“Ndugu zangu wahariri ni ukweli ulio dhahiri kwamba matumizi ya OMR yalisababisha kwa kiasi kikubwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa na kasoro,zilizopelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake. Hivyo ni mategemeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa matumizi ya BVR yatapunguza au kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo”. Alisema Jaji Lubuva.


Aidha Jaji Lubuva alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kutoa ushirikiano kwa NEC ilikufanikisha zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura kwa kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi ili waapate uekewa wa mfumo huu mpya utakaomtumika katika zoezi hilo, na kutoa hamasa wajitokeze katika viotuo vya kujiandikishia.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba amesema kuwa maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja na kufanya uhakiki wa vituo vya kujiandikishia ambapo jumla ya vituo 40,015 vimeainishwa kutoka vituo 24,919 vilivyokuwepo awali.


Malaba aliongeza kuwa ongezeko hilo la vituo limetokana na kushusha zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kutoka ngazi ya Kata, na sasa utafanyika kuanzia ngazi ya Vitongoj,Vijijii na Mitaa ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wananchi.


Malaba aliongeza kuwa Tume inatarijia kupokea vifaa kwa ajili ya zoezi hilo mapema mwezi Aguosti 2014 kwa aijili ya  kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura, na kuongeza kuwa vifaa vichache vitawasili mapema mwezi julai kufanikisha mafunzo kwa watendaji watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura.


Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linatarijiwa kuanza mwezi septemba 2014 ambapo kila kituo cha kujiandikisha kinakadiriwa kutumia siku 14 hadi zoezi kukamilika , na jumla ya takribani shilingi Bilioni 293 zinatarajiwa kutumika katika zoezi hilo.



WAZIRI LAZARO NYALANDU AONGOZA MATEMBEZI YA KUPIGA VITA UJANGILI WA TEMBO.

0
0
  1. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MB) akipokewa na Bi. Raabia Hawa, Mratibu wa matembezi ya kupiga vita ujangili wa tembo yaliyoanzia Hifadhi ya Taifa Arusha na yanatarajiwa kumalizikia Nairobi, Kenya tarehe 28 mwezi huu.
Matembezi yakaanza katika nyika eneo la Sanya Juu
Wageni hawa nao kutoka Australia walishiriki matembezi hayo
Mwendo ulipokolea na makoto yalivuliwa ili kuwa na wepesi zaidi.
Watembeaji wakipumzika kidogo kabla ya kuendelea na matembezi.
Kundi kubwa la nyuki liliwafanya watembeaji kuinama kwa muda kupisha nyuki wapite.
Bi. Raabia Hawa akifuta machozi baada ya kuguswa na hotuba ya Waziri Nyalandu kuhusu askari aliyepoteza maisha yake katika Pori la Akiba la Maswa kwa kuuwawa na  Majangili.
Watembeaji katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu. 
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

TCRA YATOA ONYO KWA WANAOTUMIA MITANDAO KUCHAFUA WENGINE

0
0
Dr. Raynold Mtungahema
Na Yusuph Kileo
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa na mkono wa sheria.
Onyo hilo limetolewa jana mjini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, Dkt, Raynold Mtungahema, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha chafu zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye mitandao.

Nilipata kufafanua yakua mtandao au kifaa chochote cha digitali kinapotumiwa visivyo kinaweza kupelekea mtumiaji kujikuta akifanya uhalifu mtandao. Mifano katika hili nilipata kueleza, pale mtumiaji anapotumia mtandao kutukana, kutishia na kudhalilisha wengine mitandaoni anakua amefanya kinachoitwa "Cyberbullying" ambacho ufafanuzi wa hili unaweza kusomeka "HAPA"
Kwa nchi za magharibi wamekuwa na kampeni mbali mbali zinazo hamasisha kutokomeza aina hii ya uhalifu mtandao ambapo takwimu za ITU za mwaka 2013 zilionyesha takriban nusu ya wenye umri kati ya miaka 13 - 17 wamekua wana athirikazaidi na "Cyberbullying".

Kwa Tanzania hapakua na tofauti, Mitandao imekua ikitumika kusambaza taarifa za uongo, chuki na kudhalilisha wengine na hata baadhi kutishia wengine kupitia mitandao (Simu pamoja na Komputa) kitu ambacho ni hatari sana kwa usalama wa taifa lolote. Hili lilipelekea TCRA kuja na kampeni ya "Futa delete kabisa" inayo hamasisha kutosambaza jumbe za chuki, matusi au uongo ili kulinda amani ya Tanzania.
Aidha, hapo jana Katika muendelezo wa kuhakiki kunakuwa na matumizi salama ya mitandao Dr. Mtungahema amesema, matumizi ya mitandao ambayo sio sahihi ni kosa la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na akawataka  wanaochafuliwa kupitia mitandao wafungue majalada polisi na mamlaka hiyo itasaidia kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Alisema mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika kuchafua anaishi uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya matumizi yasiyo sahihi  ambayo hayaruhusiwi.
Mtungahema,  amesema  atakaebainika anatumia mtandao kumchafua mtu mwingine huyo amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwa kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa mtuhumiwa atakaepatikana na hatia.
Aliongeza kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari wahusika wameshatiwa mbaroni  na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu mamlaka hiyo itaarifiwe.

Nchi wanachama wa Jumuia  ya Afrika Mashariki zimeaanza kikao cha siku nne  jijini Arusha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO, Dakta   Fracis Wangusi, amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa haraka.
Wangusi ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya, amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka mtandao wa analojia kwenda digital na  matumizi ya visumbusi kwa ajili ya luninga.
Aliongeza kuwa sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya kuwepo gharama kubwa za matumizi, usambazaji barua na vifurushi kunakofanywa na mashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao haujapangiliwa, matumizi ya  vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka ya internet.
Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images