Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Mahojiano ya moja kwa moja na msanii Anna Mwalagho kuhusu Tamasha lijalo

$
0
0
Anna Mwalagho.
Photo Credits Anna Mwalagho Facebook page
 Karibu katika mahojiano mafupi na ya moja kwa moja kati ya msanii Anna Mwalagho na Kwanza Production kwenye kipindi cha NJE-NDANI Jumamosi Juni 14, 2014.Amezungumzia tamasha kubwa linaloendelea ambalo atatumbuiza pamoja na kikundi chake kwa siku tatu

Tamasha hilo linaandaliwa kwa ushirikiano wa watu wa Oman na maktaba ya sanaa za waAfrika hapa Washington DC
Karibu usikilize

Article 12

$
0
0
Ticket zinapatikana- Beauty Point- Mayfair plaza,  Seki land of fashio- opposite Shoppers plaza, Bang! magazine office- Mikocheni B- opposite East Africa International school. Kiki shop oysterbay, Total Bonjour shops- Mlimani city, Morocco, city centre and Mbezi. Or call 0754844578 to book your ticket. Wahi sasa upate ticket yako

KITWANGA ATEMBELEA BWAWA LA MTERA

$
0
0
 Kaimu Meneja wa Bwawa  la Kuzalisha Umeme la Mtera, Mhandisi Steven Mfumbusa akimweleza jambo Naibu Waziri Nishati na Madini  anayeshughulikia  Nishati  Mhe. Charles Kitwanga alipotembelea Bwawa hilo ili kuangalia mwenendo wa maji katika Bwawa hilo. 
Naibu Waziri Nishati na Madini Mhe. Charles Kitwanga katikati akiongea jambo wakati Uongozi wa Bwawa ulipowasilisha  taarifa kuhusu Bwawa la Mtera. Anayefuatia kulia kwake ni Meneja Mwandamizi Kanda ya Kati Mhandisi Godwin Mzava na anayefuatia ni Meneja Uzalishaji TANESCO, Mhandisi Costa Rubagumwa.
  Mhandisi Mwandamizi masuala ya uendeshaji katika Bwawa la Mtera, Mhandisi Julius Chomora akimweleza Naibu Waziri Nishati  Mhe. Charles Kitwanga namna mtambo  wa uendeshaji unavyofanya kazi. Anayefuatia ni Mhandisi Nishati Mwandamizi Wizara ya Nishati na Madini Salum Inegeja.
 Kaimu Meneja wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mtera, Mhandisi Steven akimwonesha Mhe. Charles Kitwanga moja ya “Transfoma ‘’ iliyopo katika eneo la Bwawa la Mtera.


======== ==========
NAIBU WAZIRI KITWANGA ATEMBELEA BWAWA LA MTERA

Na Asteria Muhozya, Mtera.

Naibu Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Mhe. Charles Kitwanga amefanya ziara ya kutembelea Bwawa la kuzalisha Umeme la Mtera mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuangalia mwenendo wa maji katika bwawa hilo. 


Wakati akizungumza na watendaji wa Bwawa hilo, Kitwanga amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa Bwawa la Mtera linaendelea kuwa na kiasi cha maji ya kutosha wakati wote ili kuweza kuzalisha umeme wa kutosha.


“Lazima muhakikishe bwawa hili linakuwa na maji ya kutosha wakati wote. Hakikisheni kuwa vyanzo vya maji ya bwawa hili vinakuwa endelevu”. Amesisitiza Kitwanga.


Aidha, ameongeza kuwa, uzalishaji umeme kwa njia ya maji ni muhimu kutokana na gharama zake kuwa nafuu ikilinganishwa na gharama za kuzalisha umeme unatokana na gesi au vyanzo vingine. Hivyo, amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao jirani na vyanzo vya maji kuhakikisha wanavilinda kwa ajili ya maendeleo na manufaa ya taifa.


Katika hatua nyingine amewataka watendaji hao kufikiria vyanzo vingine vya kuzalisha umeme mbali na gesi badala ya kusubiri rasilimali ya gesi pekee kuweza kuzalisha umeme. “Tukumbuke gesi inaweza kuisha, lakini kuna vyanzo vingine vingi ambavyo vinaweza kwenda sambamba na gesi, lazima tuwe wabunifu”. Ameongeza.

Aidha ameeleza kuwa, wananchi wana matarajio makubwa na nishati ya umeme hivyo, amewataka watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuwatumikia watanzania huku wakitanguliza uzalendo.

VIJANA WA KIMASAI WAENDELEA KUDUMISHA MILA NA DESTURI

$
0
0
 Mgeni rasmi Mhe. Peter Toima Kiroya wa pili kushoto mkazi wa Manyara Wilayani Simanjiro ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akiwaongoza vijana wa kimasai kundi la Korianga kuingia kwenye boma kwa ajili ya kushiriki sherehe ya unywaji wa maziwa ikiwa ni mojawapo ya hatua ya makuzi  kwa vijana jana mkoani Manyara,  wapili kulia ni Mke wa Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya.

 Mgeni rasmi Mhe. Peter Toima ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akipokea Kiyabuyu cha maziwa kutoka kwa Mkewe Bi. Filomena Toima Kiroya kama ishara ya kuwaonyesha vijana waliohitimu hatua moja ya makuzi katika sherehe za unywaji wa maziwa Mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro
 Mmoja wa vijana wa kimasai kundi la Korianga akipokea kibuyu cha maziwa kutoka kwa mke wake kama ishara kuwa kuanzia sasa anaruhusiwa kunywa maziwa katika boma lake bila ya kujificha kama alivyokuwa akifanya kabla ya kuingia katika hatua hiyo ya makuzi kwa vijana wa kimasai.

 :Bw. Onesmo Toima akinywa maziwa yaliyomo katika kibuyu baada ya kuvuka hatua ya malezi iitwayo Sporio na kuingia hatua ya Korianga katika sherehe za unywaji wa maziwa zilizofanyika jana Mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Venerose Mtenga akitoa hotuba wakati wa Sherehe za unywaji wa maziwa kwa vijana wa kimasai kama hatua mojawapo ya malezi kwa vijana, kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mhe. Peter Toima Kiroya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Venerose Mtenga aliyekaa kulia katika picha ya pamoja na vijana wa kundi la Korianga, watatu kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mhe. Peter Toima Kiroya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma na wapili kulia ni Mke wa Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya. (Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM)

MAONESHO YA 15 YA WAJASIRIAMALI SEKTA ISIYO RASMI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NCHINI KIGALI RWANDA

$
0
0
Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya wajasiriamali wa sekta isiyo rasmi ya Jumuhiya ya Afrika Mashariki; yajulikanayo kama Nguvu Kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kufanyika Kigali Rwanda,Novemba 30 hadi Desemba 7 mwaka huu. Kulia ni  Afisa Kazi Mwandamizi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Sara Daudi.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasirimali Tanzania, Joseph Rweyemamu (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari, leo jijini Dar e s Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  yajulikanayo kama Nguvu kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kuanza 30 hadi Desemba 7 mwaka huu. Kushoto ni  Afisa Kazi Mwandamizi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Sara Daudi.
Mratibu wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania, Boniverntura Ferdinand (katika), akiwaeleza umuhimu wa dawa asilia wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  yajulikanayo kama Nguvu kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kuanza Novemba 30 hadi Desemba 7 mwaka huu, kulia ni  Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema na kushoto ni Mweka Hazina wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Tanzania, Jumbe Ngutto. Picha na Lorietha(Laurence-Maelezo)

JAPAN YATOA BILIONI 24 KUSAIDIA BAJETI YA SERIKALI

$
0
0
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania, hafla hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada.

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa kushoto) akiongea na waandishi wa habari pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani) wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada.

Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada akiongea na waandishi wa habari pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani) wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania katika hafla ilifanyika leo mjini Dodoma.

  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) nchini Yasunori Onioshi akiahidi shirika lake kuendelea kushirikiana na Serilkali ya Tanzania katika masuala mbalimbali yamaendeleo nchini, leo mjini Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari pamoja, Maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Ubalozi wa Japani wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha  Saada Mkuya Salum wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania katika hafla ilifanyika leo mjini Dodoma.


(Picha na habari na Ingiahedi Mduma na Eleuteri Mangi-Wizara ya Fedha)

======  =======  =====
Serikali ya Tanzania imepokea shilingi bilioni 24.1 kutoka Serikali ya Japani kwa ajili ya shughuli za maendeleo hapa  nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini , Waziri  wa Fedha Sada Salum Mkuya aliishukuru Serikali ya Japani kwa kuwa na  ushirikiano mzuri na Tanzania.
“Mkopo huu utachangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2014/2015, na fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Maji, Elimu na Afya” alisema Waziri Mkuya.
                                             
Mkuya aliishukuru Serikali ya Japani kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa ambayo imeleta mafanikio makubwa Tanzania.
Alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ,misaada hiyo imesaidia kupunguza umaskini na kuongeza kipato kwa wananchi.
                                                                                     
Akijibu swali kuhusu fedha hizo za mikopo kuchelewa kufika, Waziri Mkuya alisema kuwa changamoto kubwa ambayo Serikali imekuwa ikiipata ni kutokana na taratibu  za sera za nchi husika ambapo kila nchi wana sera zao.
Kwa upande wake Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada alisema kuwa msaada huo unahusiana na ushirikiano wa pamoja na Benki ya Dunia katika mkopo wa kumi na moja wa kusaidia kupunguza umaskini ambao umekuwa ukitolewa tangu mwaka 2001.
Mikopo hiyo imekuwa ikitolewa kwa masharti ya mkataba wa mkopo nafuu wa riba ya asilimia 0.01 kwa Serikali  hapa nchini.
Balozi Okada alisema kuwa nchi yake imekuwa ikitoa mikopo mabalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania katika kupunguza umaskini ambapo misaada hiyo imekuwa ikitumika kufuatana na GBS hapa Tanzanaia kwa kutoa fedha moja kwa moja ambazo zinalenga kuharakisha juhudi za kupunguza umasikini hususani MKUKUTA.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) nchini Yasunori Onioshi alisema kuwa shirika lake litaendelea kushirikiana na Serilkali ya Tanzania katika kusaidia bajeti yake kwani Tanzania inakua kwa haraka na mahitaji yake yanaendelea kuongezeka kila mara.
Makampuni ya Kijapani yanayofanya kazi na Serikali ya Tanzania ni pamoja na Kampuni ya Sigara (TCC) inayomilikiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Tumbaku ya Kijapani, Panasonic Energy Tanzania na JICA.
Hali ya hewa ya Dodoma ni baridi na majadiliano kuhusu Bajeti ya Serikali yameanza na yanaendelea.
Imetolewa na:
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
16/06/2014

MAKAMU WA RAIS WA CHINA,LI YUANCHAO KUTUA NCHINI

$
0
0
  Balozi wa China nchini,Lu Youging(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Watu wa China Mhe. Li Yuanchao katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China ,Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo . 
 Balozi wa China nchini,Lu Youging(kulia) akizungumza na waandishi wa habarikuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Watu wa China Mhe. Li Yuanchao katikaukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo jijini Dares Salaam. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China ,Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo na kulia ni  First  Secretary  kutoka  ubalozi  wa China ,Ren Zhihong .
 Balozi wa China nchini,Lu Youging(kulia) akizungumza na waandishi wa habarikuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Watu wa China Mhe. Li Yuanchao katikaukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China ,Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo na watatu kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiruikiano wa Kimataifa.
 Picha namba 0272 ni Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi wa China nchini,Lu Youging.Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo

Maandalizi ya mkutano wa kimataifa kuhusu matunda ya teknolojia mpya ya upashanaji wa habari yaja.

$
0
0
 Mhadhiri Mwandamizi katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) Charles Irigo(katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano wa kimataifa kuhusu matunda ya teknolojia mpya ya upashanaji wa habari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari(MAELEZO). Kulia ni Mhariri wa Mlimani media Hamis Dambaya na kushoto ni Mhariri wa Mlimani Media,Amini  Mgeni.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhadhiri Mwandamizi katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habar na Mawasiliano ya Umma(SJMC) Charles Irigo. (Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo).

TFDA katika Wiki ya Utumishi wa Umma

$
0
0



Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imeendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya vipodozi vyenye viambato sumu kwa jamii ikiwa watanzania hawataacha kuvitumia kwa hiari yao. Elimu hiyo inatolewa katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Vijana wa Babati wapata Mafunzo kuhusu upatikanaji wa Mikopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akisalimiana na Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole alipomtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akizungumza na Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole ofisini kwake kabla ya kukutana na Vijana kwa ajili ya Mafunzo yanayohusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akitoa mada kwa wanamafunzo (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole na katikati ni Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga.
Bw. Petro Benedict kutoka Kikundi cha Ebenezer Group akichangia mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati (hawapo pichani) kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati (hawapo pichani) kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati. (Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini – WHVUM)  
===== =====
Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM

Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati waaswa kuzingatia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 ili kuweza kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Babati na hivyo kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga wakati wa Mafunzo kwa Vijana kuhusu upatikanaji wa Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yaliyofanyika leo Mjini Babati.

Akitoa mada kuhusu Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Bibi Mtenga amewataka vijana kujitambua na kujua kuwa wao ni rasilimali muhimu na mchango mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na Kijamii hivyo kuithamini Sera ya Vijana inayomtambua kijana kuwa ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 na kutumia fursa hiyo kupata haki zao kama vijana.

Aidha Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga amewataka Vijana wa Babati kuweka jitihada katika uandikaji wa miradi yao kwa kuzingatia muongozo wa utoaji fedha za mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi endelevu ambayo itakuwa na sifa za kupata mikopo hiyo kupitia SACCOS ya vijana ya Halmashauri hiyo.

Kwa upande Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole amewataka Vijana wa Babati kutumia fursa hiyo ya kipekee ya kutembelewa na maofisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kupewa mafunzo ya kuwajengea uwezo mzuri wa kuendesha shughuli zao za uzalishaji mali kwa ufanisi kwani huu ni muda muafaka kwa Vijana kuendeleza vikundi vyao na kuweza kuimarisha SACCOS ya vijana kwa maendeleo yao na Mji wa Babati.

Nao vijana walioshiriki mafunzo hayo wameitaka Serikali kupitia Idara ya Vijana kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanakuwa endelevu na yanawafikia   vijana nchini kote ili kuwawezesha vijana kufahamu umuhimu wa Mfuko huo, upatikanaji wa fedha, pamoja na sifa za upatikanaji wa fedha kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

MAMA SALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA OFISI YA TEWO SACCOS-TEMEKE

$
0
0

IMG_0244
IMG_0093Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea Tuzo maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa TEWO Saccos  Ndugu Sophia Kinega. Mama Salma alipewa Tuzo hiyo kwa ajili ya ushirikiano wake na Saccos hiyo katika kuchangia kwa kiasi kikubwa ujenzi  wa jengo la ofisi ya TEWO Saccos.IMG_0130Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wanachama wa TEWO Saccos, mwana Vicoba na wananchi wa wilaya ya Temeke waliohudhuria sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za TEWO Saccos huko Temeke tarehe 17.6.2014.IMG_0144Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti  Ndugu Yusuf Manji kilichotolewa na TEWO Saccos  kwa watu na makampuni mbalimbali yaliyoshiriki katika kuchangia ujenzi wa jengo la TEWO Saccos huko Temeke tarehe 17.6.2014.IMG_0183Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti (Certificate of Appreciation) Ndugu Philomena Marijani, Afisa kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, kilichotolewa na TEWO Saccos kwa ajili ya kuwashukuru watu na Taasisi mbalimbali zilizochangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa ofisi za Saccos hiyo huko Temeke tarehe 17.6.2014.IMG_0219Mwakilishi wa Kampuni ya Mabasi ya Usafiri Dar es Salaam, UDA, Ndugu Simon Bulenganiya akikabidhi  mfano wa hundi ya sh 30,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya TEWO Saccos kwa Mwenyekiti wa Saccos hiyo Ndugu Sophia Kinega wakati wa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi terehe 17.6.2014.IMG_0233Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya TEWO Saccos wakati wa sherehe ya kuweka jiwe la msingi huko Temeke tarehe 17.6.2014.
IMG_0266Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TEWO Saccos na wale wa serikali waliohudhuria sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la SACCOS hiyo tarehe17.6.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI .

"WOMEN WITH ATTITUDE" SINEMA YENYE LADHA YA SHUGHULI KUONYESHWA NGOME KONGWE LEO

$
0
0
DSC_0166
Mtanzania mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya "Woman with Altitude" iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

UNAWEZA kudhani kamba kila aliyefanikiwa amezaliwa na kijiko cha fedha, yaani amezaliwa katika eneo lenye hali shwari na kitanda chake ni mayai ya dhahabu, kumbe sivyo kabisa. Hili linajadliwa kwa undani katika sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with Atitude.

Sinema hii ambayo inaoneshwa katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutambua kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa migogoro inayowakuta na kwa kupitia elimu.

Women with Altitude inazunguka katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini. Baada ya kufanikiwa kupanda mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal waliamua kupanda milima mingine nmirefu katika mabara mbalimbali wakiwa na lengo la kutoa ushawishi kwa wanawake na wasichana duniani kote kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni magumu na hayawezekani.
DSC_0162 
Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na documentary iliyopewa jina la “Women with Altitude” ambapo ndani yake wameshirikishwa wasichana wa kitanzania wawili na imefadhiliwa na shirika hilo itakayooyeshwa leo jioni ndani ya viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF 2014.

Machi 2013,wanawake hao walipata ushosti kutoka kwa wanawake wa Kiafrika wane akiwemo muigizaji wa Afrika kusini Hlubi Mboya,ambaye anatambulika sana kwa kuigiza nafasi ya mtu anayeishi na VVU kama Nandipha kwenye Isidingo kupanda mlima mlima mkubwa wa bara la Afrika, Mlima Kilimanjaro.
Tofauti ya utamaduni na mazingira kwa wanawake wote 11 ilikuwa pia ni ishara ya matatizo waliyokumbana nayo katika maisha yao.

Filamu hii ya Women with attitude inaonesha matatizo ya wanawake hao 11 waliokuwa wakikumbana nayo katika maisha yao yote, na nafasi ya elimu katika kuwasaidia kufika pale walipo kwa leo.

Wanawake hawa wanaonekana wakikabiliana na Mlima Kilimanjaro, wakiangalia maisha ya wenzao na kuwashawishi katika kutokata tama na badala yake kutumia changamoto kuleta maisha yenye hadhi ya aina yake.
Ofisa habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumza katika mahojiano alisema kwamba taarifa iliyomo ndani ya sinema hiyo ni ujumbe tosha kwa vijana na wanawake kuhusu ukweli wa maisha na namna ya kuyabadili.
  DSC_0098
Baadhi ya wasanii na waigizaji filamu wanaohudhuria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.

AJALI MBAYA YA GARI NA PIKI PIKI BARABARA YA CHALINZE SEGERA

$
0
0

Mwendesha pikipiki na abiria (majina hayakutambulika) wakiwa wamelala chini katika barabara ya Chalinze Segera karibu na Kabuku baada ya kugongwa na gari ndogo yenye usajili namba T818 BNS leo mchana. Mpiga picha wa tukio hili alienda kutoa taarifa ya ajali kiTuo cha polisi cha Kabuku ambapo Polisi walienda kutoa msaada wa kukimbiza majeruhi hospitali pamoja na kupima ajali. (Picha kwa hisani ya Rodney Thadeus)

NEWS ALERT: MUME WA FROLA MBASHA APANDISHWA KIZIMBANI kWA KESI YA UBAKAJI

$
0
0





Na Mwene Said 


MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha (pichani wakiwa, amefikishwa katika Maha kwenye shughuli zao siku za nyuma) kama ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.



Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.



Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.



Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).



Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). 



 Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .


Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.



Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.



Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.


IPTL yapiga jeki ujenzi wa kituo cha polisi cha Mbweni- Malindi

$
0
0
 Meneja Mkuu wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi la Tanzania, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Bw. Harbinder Sethi (kushoto), wakati akipokea hundi ya shilingi milioni 10 iliyotolewa na IPTL kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbweni-Malindi. Katikati ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum la kipolisi Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova.
Meneja Mkuu wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi la Tanzania, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 Kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Bw. Harbinder Sethi (kushoto) iliyotolewa na kampuni yake kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbweni-Malindi.  Katikati ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum la Kipolisi Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova.
======  ========
KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imepiga jeki mradi wa ujenzi wa kituo cha polisi cha Mbweni Malindi kwa kuchangia zaidi ya silingi milioni 10, ikiwa na lengo la kuyafanya maeneo hayo kuwa maeneo salama kibiashara.

Wakati akikabidhi mchango huo kwa maafisa wa polisi kanda maalum la kipolisi Dar es Salaam katika eneo la ujenzi mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Harbinder Sethi alisema kampuni yake imeitikia wito wa kusaidia ujenzi huo sababu inaamini kuwa usalama thabiti utasaidia maendeleo ya haraka kiuchumi katika eneo husika. 
  
“IPTL inaelewa kuwa ili kupata maendeleo thabiti ya kiuchumi katika sehemu yoyote ile, ni lazima eneo hilo liwe na usalama wa kutosha. Utakapo boresha usalama, wawekezaji wataleta fedha  sababu watakuwa na uhakika kuwa fedha zitakuwa salama. “Ongezeko la uwekezaji katika jamii pia litabadilisha hali ya kiuchumi na maisha ya watu. 

Hii ndiyo maana tumetenga sehemu ya pato letu ili kusaidia miradi mbali mbali ya kijamii ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia miradi ya kijamii inayotuzunguka,” alisema.

Bw. Sethi alisema kuwa IPTL imejikita katika kusaidia miradi mbali mbali yenye chachu kubwa ya kuwaletea watu maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Akipokea hundi hiyo kwa niaba ya Jeshi la Polisi, Meneja Mkuu wa Utawala na Rasilimali katika Jeshi la Polisi la Tanzania, Kamishna wa Polisi, Thobias Andengenye alisema mchango huo utasaidia kukamilisha mradi huo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700. “Kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa mchango huu.

Ninaamini kwamba baada ya mradi huu kukamilika na kuzinduliwa, uwepo wa polisi utasaidia kuboresha hali ya usalama katika eneo hili la Mbweni. Kama mnavyofahamu, hakuna maendeleo ya kiuchumi yanayoweza patikana katika eneo lisilokuwa na usalama. Tunakushukuruni sana,” alisema. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho cha polisi, Reeves Mutalemwa alisema maombi ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi yalitumwa na wakazi wa Mbweni ambao pia wamekuwa wakichangia katika mradi.


WITO WATOLEWA KWA WATANZANIA KUTUNZA ARDHI NA UDONGO KWA MATUMIZI ENDELEVU YA KILIMO NA MIFUGO

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Henry Kapufi wakisikiliza maelekezo juu ya ufugaji nyuki kutoka kwa mmoja wa wafugaji(hayupo pichani)  katika  kijiji cha  mabilioni wilayani Same katika siku ya kupambana na kuenea kwa  hali ya jangwa na ukame duniani.

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipanda mti wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa duniani zilizofanyika katika kijiji cha mabilioni wiayani Same.

: Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akihutubia katika siku ya kupambana na kuenea kwa  hali ya jangwa na ukame duniani. Kitaifa maadhimisho ya siku hiyo yamefanyika katika kijiji cha mabilioni Tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.

 Sehemu ya umati wa Wananchi waliojitokeza katika kuadhimisha siku ya  kupambana na kuenea kwa  hali ya jangwa na ukame duniani iliyofanyika kitaifa katika kijiji cha mabilioni wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.

 Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akiongea na wananchi katika maadhimisho hayo .

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya msanja sanjari na kikundi cha wakinamama wa kijiji cha mabilioni wilayani Same katika maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
=======  =======  ======
Wito umetolewa  na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwaimu kwa jamii ya Umma wa Tanzania kutunza ardhi na udongo kwa ajili ya matumizi endelevu na kuifanya ardhi iwe na uwezo wa kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo na kutoa huduma zingine muhimu ili kuepuka hali ya jangwa na ukame kwa kizazi cha sasa na kijacho na pia kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.


Mheshimiwa Mwalimu amesema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani. Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika katika kijiji cha Mabilioni tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.  

Aliongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa robo ya dunia ambayo ni zaidi ya hekta bilioni 3.6 inatishiwa na janga la kuenea kwa hali ya ukame na jangwa. Hivyo basi alisema ni wajibu wa kila mmoja  kulinda ardhi ili iweze kuleta manufaa baadaye sababu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunasababisha matatizo ya kiuchumi,kimazingira na kijamii . 

Vivyo hivyo kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunapelekea ardhi kupunguza uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula na kuongeza umaskini . Mwisho alitoa wito kwa Hamashauri zote Nchini kuunda kamati za Mazingira kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Wilaya. 

Pia aliomba vyombo vya habari Nchini kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuchukua njia thabiti za kupambana na kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni Ardhi  ni mustakabali wa maisha, tuilinde dhidi ya uharibifu. 

KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA YAONDOLEWA KATIKA ORODHA HATARISHI YA UNESCO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmoud Mgimwa akipongezwa na mmoja wa wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa UNESCO jijini Doha, Qatar kufuatia hatua ya Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kuondolewa katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kutoweka na kurudishiwa hadhi yake ya awali ya urithi wa dunia. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Tarishi Kibenga (kati) na Mkurugenzi wa Malikale Bw. Donatius Kamamba.
Ujumbe wa Tanzania unaohudhuria Mkutano wa UNESCO jijini Doha, Qatar ukiwa katika ukumbi wa mkutano. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Malikale Bw. Donatius Kamamba, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Tarishi Kibenga, Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Mahmoud Mgimwa na Mjumbe wa Tanzania katika Kamisheni ya UNESCO Profesa Mohamed Sheya.
=======  ======  ======

MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM


PRESS STATEMENT

Tanzania’s Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songo Mnara removed from UNESCO List of World Heritage in Danger

The World Heritage Committee meeting in Doha (Qatar) has found that management and safeguarding of the Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songo Mnara in the United Republic of Tanzania have improved to the point where the site can be removed from the List of World Heritage in Danger.


Located on two islands close to each other just off the Tanzanian coast about 300km south of Dar es Salaam, Kilwa Kisiwani and Songo Mnara were Swahili trading cities. Their prosperity was based on control of Indian Ocean trade with Arabia, India and China, particularly between the 13th and 16th centuries, when gold and ivory from the hinterland was traded for silver, carnelians, perfumes, Persian faience and Chinese porcelain.


The site was inscribed on the List of World Heritage in Danger in 2004, because of deterioration and decay leading to the collapse of the historical and archaeological structures for which the property was inscribed.


The 38th session of the World Heritage Committee began on 15 June and will continue through to 25 June, under the Chair of Sheikha Al Mayassa Bint Hamad Bin Khalifa Al Thani.


Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songo Mnara are the remains of two great East African ports admired by early European explorers and are situated on two small islands near the coast. From the 13th to the 16th century, the merchants of Kilwa dealt in gold, silver, pearls, perfumes, Arabian crockery, Persian earthenware and Chinese porcelain; much of the trade in the Indian Ocean thus passed through their hands.


Issued by the Spokesperson

Ministry of Natural Resources and Tourism

17thJune, 2014



TBL YAPATA TUZO YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema (kushoto) akimkabidhi tuzo ya cheti Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu, kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika utunzaji wa mazingira nchini, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Dorris Malulu akifurahia TBL kupata tuzo ya utunzaji mazingira nchini

MISS TANGA 2014 WATEMBELEA MWAMBAO FM

$
0
0
  Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamesimama mbele ya basi lao muda mfupi baada ya kutoka kutembelea kituo cha redio Mwambao Fm jijini Tanga.
  Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamesima mbele ya hoteli ya Tanga Beach Resort ambako wameweka kambi yao kwa wiki ya pili sasa wakijiandaa na shindano hilo litakalofanyika jumamosi hii 21/06/2014 Mkonge Hotel.
Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamelizunguka gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo.
=======  =======  =======
Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 jana walitembelea kituo cha matangazo cha redio Mwambao Fm cha jijini Tanga kujionea jinsi kituo hicho kinavyorusha matangazo yake.

Wakiwa katika kituo hicho, warembeo hao walipata fursa ya kuzungumzia shindano hilo huku kila mmoja akitamba kuibuka mshindi siku ya jumamosi ya tarehe 21/06/2014 ndani ya Mkonge Hotel kuanzia saa moja usiku.

Baadaye leo washiriki hao watatembelea kituo cha redio cha Breeze Fm pia cha jijini Tanga na kesho wanataraji kwenda kutoa msaada katika moja ya vituo vya kulea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Shindano hili limedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Redd's, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm. Malkia wa mipasho Afrika Mashariki, Bi Hadija Omary Kopa ndiye atakayetoa burudani siku hiyo

IJUMAAA PALE ECAPE ONE LIVE

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images