Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 297 | 298 | (Page 299) | 300 | 301 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Gari la Waziri wa  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka likiwa katika kituo cha polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kugonga punda June 11,2014.
  Waziri wa  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Bukoba kwenda Dodoma kugonga mnyama punda katika kijiji cha Wendele Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga. 

  Walioshuhudia tukio hilo walisema lilitokea jana majira ya saa 11  jioni ambapo gari lenye namba za usajili STK 5857mali ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi lililokuwa likiendeshwa na dereva Linusi Eliasi (42) liligonga mnyama punda aliyekatiza ghafla barabarani.

  Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyang'a,Bw Benson Mpesya amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa Waziri Tibaijuka alipata mshtuko baada ya ajali hiyo na ofisi ya mkuu wa wilaya Kahama ilimpatia usafiri mwingine kwa ajili ya kuendelea na safari ili kuhudhuria vikao vya bunge kufuatia gari lake kuharibika. 
  Waziri wa  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
  Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya  ya Kahama Benson Mpesya amesema waziri  Tibaijuka hakuumia katika ajali hiyo na leo  ameendelea na vikao vya bunge mkoani Dodoma.

  Akielezea zaidi kuhusu ajali hiyo ,Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya amesema  Waziri Tibaijuka alikuwa na baadhi ya wanafamilia wake katika gari hilo wakitoka Bukoba kwenda Dodoma kwa ajili ya kuwahi shughuli za Bunge zinazoendelea.

  Kamanda Kihenya amesema  baada ya kufika katika eneo hilo alikatisha punda katikati ya barabara na katika harakati za dereva kumkwepa ndipo gari hilo lilipomgonga na kisha mnyama huyo kufa papo hapo.

  Kihenya alisema kuwa katika ajali hiyo hakuna mtu aliyeumia ila kuna baadhi ya watu waliopata majeraha madogo madogo ikiwa ni pamoja na waziri huyo aliyepata mshtuko kidogo lakini baadaye hali yake iliendelea vizuri.


  Hata hivyo katika  hali ya mshangao wa watu waliomiminika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya kumjulia hali waziri na kumpa pole lakini Waziri huyo na msafara wake walikuwa wakipatiwa matibabu na wauguzi katika Hoteli moja iliyopo pembeni mwa hospitali ya Wilaya Kahama.

  0 0

  Baadhi ya washiriki watumishi kutoka katika serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushoto Bw. Fred Manyika,katikati Bi. Emelda Adam na Bw. Abdul Mhinte wakifuatilia mazungumzo wakati wa  mkutano wa kundi la Africa katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaoendela mjini Bonn Ujerumani leo (Picha na Evelyn Mkokoi).

  0 0

  NDUGU MDAU MICHUZI TV SASA IPO HEWANI. 
  JIUNGE HARAKA UPATE MAMBO MOTOMTO!!
  TUNAANZIA  NA WATEJA WA VODACOM, AMBAO WANAKARIBISHWA KUPIGA  *149*01#  KISHA CHAGUA NAMBA 4 SIMU.tv (MPYA) 
  HALAFU NENDA  NAMBA 1. Habari (BURE), 
  BAADA YA HAPO 
  CHAGUA NAMBA 5 Michuzi TV (BURE) KISHA KUBALI...
  UNAKUWA UMESHAJISAJILI KWA HUDUMA HII MPYA. 
  LIBENEKE OYE!

  0 0

  MKURUGENZI wa Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda, amesema kwamba mwenye uwezo wa kupunguza makali ya mwimbaji Nassib Abdul Diamond ni Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’ pekee.
  Msanii Diamond, pichani.
  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mhonda alisema hiyo inatokana na ubora wa wasanii hao, pamoja na aina yao inayovitia kuwasikiliza.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda pichani.

  Alisema Diamond ni msanii mkali ambaye kwa mtindo wake huenda akakosa mpinzani, kama Mb Dog atazidi kushuka thamani yake kisanaa.
  Msanii Mb Dog, pichani.
  “Kila nikimuangalia Diamond Napata shauku ya kuona makali ya Mb Dog yanarudi kwasababu ndio anayeweza kuleta ushindani kwa mwimbaji huyo anayetamba na mtindo wake wa Ngololo.

  “Mb Dog ana ladha nzuri, sambamba na uimbaji wake unaovutia bila kusahau ubunifu pia katika tungo zake, hivyo kwa kiasi kikubwa yeye ndio mpinzani wa kweli wa Diamond na si mwingine,” alisema.

  Mb Dog kwa sasa anatamba na wimbo wake Mbona Umenuna, akiimba kwa hisia kubwa, huku akiwa na shauku ya kurudi makali yake ya zamani.

  0 0

  Baadhi ya washiriki wa redds miss iringa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi katika ukumbi wanakofanyia mazoezi hotel ya Gentle Hill iliyoko mkoani Iringa. 

  Na Denis Mlowe,Iringa
   
  HATIMAYE kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama lilivyopangwa mwanzoni na Tanzania Daima kuwa la kwanza kuripoti kuhusiana kutoweka kwa shindano hilo.
   
  Waandaji wa Redds Miss Tanzania chini ya Lino Agency Hashim Lundenga baaada ya kugundua hilo wamempatia kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo na kwasasa Redds Miss Iringa imepata mratibu mwingine ambaye ni kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini uongozi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mjini Iringa.
   
  Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana Mkurugenz wa kampuni hiyo, Victor Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
   
  Alisema kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
   
  Chakudika alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
   
  “Kwa kweli baada ya mratibu wa kwanza kukimbia kutokana na gharama za uandaaji niliamua kuchukua jukumu hilo kulikomboa shindano hilo lifanyike na warembo wengi wamejitokeza kushiriki miss iringa” alisema Chakudika.
   
  Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini hapa. Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance wa mjini Iringa.

  Aliwataja wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class, Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini shindano hilo.

  0 0

  Baadhi ya wanaharakati ngazi ya jamii wakielezea mafanikio ya utafiti wa kiragibishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika maeneo yao ulivyokuwa chachu ya baadhi ya mabadiliko kwenye mkutano jijini Dar es Salaam.  
  Baadhi ya wanaharakati ngazi ya jamii wakielezea mafanikio ya utafiti wa kiraghbishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika maeneo yao ulivyokuwa chachu ya baadhi ya mabadiliko kwenye mkutano jijini Dar es SalaamBi. Marjorie Mbilinyi mwanachama wa TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika semina hiyo. 
  Bi. Marjorie Mbilinyi mwanachama wa TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika semina hiyoBaadhi ya washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada.Baadhi ya washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiraghbishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada.Baadhi ya washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada.Baadhi ya washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada.Mmoja wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiraghbishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na asasi binafsi.Mmoja wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiraghbishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na asasi binafsi.Baadhi ya wanaharakati ngazi ya jamii wakielezea mafanikio ya utafiti wa kiragibishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika maeneo yao ulivyokuwa chachu ya baadhi ya mabadiliko kwenye mkutano jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanaharakati ngazi ya jamii wakielezea mafanikio ya utafiti wa kiragibishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika maeneo yao ulivyokuwa chachu ya baadhi ya mabadiliko kwenye mkutano jijini Dar es Salaam.

  WANAHARAKATI ngazi ya jamii kutoka mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wamesema utafiti wa kiraghbishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika maeneo yao unaleta mafanikio kwani changamoto zinazoibuliwa katika maeneo ya utafiti baadhi zimeaza kufanyiwa kazi.

  Kuanzia Machi 9 hadi 31, mwaka huu TGNP Mtandao iliendesha utafiti wa kiragibishi kwa kuishirikisha jamii katika kata tano za Mondo (Shinyanga), Tembela (Mbeya), Kiroka (Morogoro), Nyamaraga (Mara) na Kata ya Mabibo ya jijini Dar es Salaam ambapo jamii iliibua kero katika maeneo yao na kupaza sauti kwa mamlaka husika kuchochea mabadiliko.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam mwanaharakati ngazi ya jamii, Leah Peter kutoka Kata ya Mondo, Wilaya ya Kishapu kwa niaba ya wenzake alisema kero lilizoibuliwa katika utafiti baadhi zimeanza kushughulikiwa na mamlaka husika.

  Bi. Peter alisema eneo lao wakati unaendeshwa utafiti wananchi walilalamikia kitendo cha wajawazito wanaohudumiwa katika Zahanati ya Mondo, wilayani Kishapu kulipishwa shilingi 500 kulipia kadi ambayo imeandikwa 'haiuzwi' kitendo ambacho kwa sasa hakifanyiki tena baada ya kupaza sauti.
  Mmoja wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na asasi binafsi. 
  Mmoja wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na asasi binafsi.Mmoja wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiraghbishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na asasi binafsi. 
  Mmoja wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na asasi binafsi.

  "...Eneo letu awali wajawazito katika Zahanati ya Mondo tulikuwa tukidaiwa shilingi 500 kulipia kadi ya kliniki ambayo ina maandishi ya 'haiuzwi' kitendo hiki kwa sasa hakifanyiki tena na kila muhudumu wa zahanati hiyo kawa mlinzi wa mwenzake hili tunajivunia," alisema Bi. Peter.

  Alisema mabadiliko mengine ni pamoja na mikutano ya mapoto na matumizi ya vijiji kufanyika jambao ambalo walililalamikia wananchi kuwa lilikuwa halifanyiki, alisema huduma za maji ambazo ni kero eneo hilo kwa sasa halmashauri imeleta shirika linaloendelea na maandalizi ya kuchimba visima vya maji katika shule za msingi Kabila na Buganika. Alisema na Shule ya Msingi Mwigumbi imepata madawati jambo ambalo lilikuwa kero.

  Kwa upande wake Bi. Neofita Kunambi kutoka Mtaa wa Azimio Mabibo jijini Dar es Salaam alisema kero ya ngoza maarufu kwa jina la 'vigodoro' zimepigwa marufuku eneo lao baada ya kulalamikiwa, huku amri ya wajawazito wanaojifungulia katika Hospitali ya Parestina kutakiwa kwenda na ndoo ya kubeba kondo la uzazi ikipigwa marufuku jambo ambalo liliibuka katika utafiti ragibishi eneo hilo.

  Aidha alisema wanajamii eneo hilo pia walilalamikia kupanda kwa bei za maji huku kila muuzaji akiuza bei atakayo kero ambayo imeanza kusikika kwani sasa bei zimepungua tofauti na ilivyokuwa awali. "...Maji eneo letu kila muuzaji alikuwa na bei yake lakini sasa imeshuka waliokuwa wakiuza miambili ndoo sasa wanauza 100, hili pia lililalamikiwa na wananchi kwenye utafiti," alisema Bi. Kunambi.

  Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya mafanikio ya utafiti huo Kata ya Nyamaraga mkoani Mara imefanikiwa kupaza sauti kupinga zoezi la bomoabomoa iliyotaka kutekelezwa eneo hilo bila wahusika kulipwa haki zao, huku wananchi wa Kata ya Mondo Kishapu kuandamana wakati wa ziara ya Waziri wa Maji eneo hilo kudai maji safi na salama.

  Taarifa ilifafanua kuwa Kata ya Kiroka utafiti umesaidia watendaji wa huduma ya afya kuwajibika na kuwasikiliza wananchi na suala la kero ya upatikanaji wa dawa imebadilika tofauti na ilivyokuwa awali. TGNP Mtandao imewakutanisha baadhi ya wanaharakati ngazi ya jamii kutuka maeneo ya utafiti jijini Dar es Salaa ili kwa pamoja kutathimini matokeo ya utafiti huo na kuwashirikisha kutoa mapendekezo na mikakati ya kufanya kwa jamii ili kuchochea mabadiliko zaidi.

  0 0

  Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa na mabanda yao katika soko la Karume wakiwa na nyuso za majonzi mara baada ya mabanda yao kuteketezwa kwa moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya mali za wafanyabiashara hao.
   Baadhi ya Wafanyabiashara na wakazi wa Jiji la Dar wakiwa katika soko la karume kujionea hali ilivyokuwa mara baada ya moto kuteketeza  kila kitu.
   Moto ukiendelea Kuunguza mabati na vitu mbalimbali katika Soko hilo la Karume, Jijini Dar Es Salaam
   Askari wa Kikosi cha Zima Moto akiendelea na Zoezi la kuzima Moto katika Soko la Karume lililoteketea kwa Moto ambao chanzo chake hakijulikani bado
   
  Mmoja wa mfanyabiashara katika soko hilo hakikusanya mabati yake mara baada ya kuteketea kwa moto katika Soko la Karume
  Wafanyabiashara wakikukasanya mabaki ya mabati mara baada ya mabanda yao kuteketea kwa moto uliowaka tokea usiku wa kuamkia leo katika Soko hilo la Karume.
  Mfanyabiashara akiamisha baadhi ya mali alizoweza kuziokoa mara baada ya moto mkubwa kuteketeza soko la Karume.
  Masanduku ya chuma yakiwa yameungua kabisa na moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya Soko la Karume.
  Wakazi wa Jiji la Dar Wakishuhudia jinsi kikosi cha Zimamoto kikiendelea na zoezi la Uzimaji wa moto huo ambao umeendelea kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko hilo.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0


  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb)Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.
   Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) pamoja na Naibu wake, Bw. Maduka Kessy wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa Taarifa ya Hali yaUchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15. Picha zote na Thomas Nyindo,Afisa Habari Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
   Wageni wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb) ambao ni baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 naMpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.


  0 0

   Baadhi ya wandishi wa habari  kutoka Afrika Kusini wakipiga picha Simba waliotulia chini ya mti katika Pori la Akiba la Selous
   Simba wakiwa wamepumzika chini ya mti katika Pori la A Kiba ka Selous
  Mwongoza watalii Bw. Mohammed Kabouru akitoka maelezo kwa wandishi wa habari wa Afrika Kusini kuhusu kaburi na historia ya marehemu Selous Mwingereza ambaye jina lake ndilo asili ya pori hilo akiba maarufu hapa nchini na Afrka.


  Na: Geofrey Tengeneza - Selous.

  Kundi la wandshi wa habari tisa kutoka vyombo vya habari vya Serikali na binafsi nchini Afrika Kusini wametembelea Pori la Akiba la Selous na kufurahishwa na vivutio vllivyomo katika pori hilo wakiwemo wanyama kama Simba, tembo,  twiga, na ndege wa aina mbali mbali.


  Wandishi hao walivutiwa na kufurahia sana kuwaona hasa Simba na tembo kiasi cha  miongoni mwao Kulikiri kuwa  ni mara yao kwanza kuwaona wanyama hao kwa macho yao wakiwa katika maisha yao ya asili msituni kudaikuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaona katika televisheni na filamu tu.

  “Nimefurahi sana na mwki umenisisimka sana kuona Simba na tembo kwa mara ya kwanza kwa macho yangu katika historia ya maisha yangu” alisema Bwana Yolisa Mkele, mwandishi wa habari kutoka gazeti la the Times. Aidha walivutiwa sana na ziara ya boti katika mto Rufiji ambapo walifanikiwa kuona idadi kubwa ya kiboko na mamba walioko katika mto huo.


  Katika ziara hiyo ya Selous wandishi hao walitembelea na kuona kaburi la Mwingereza Kapteni  F.C Selous aliyekuwa akiishi na kufanya shughuli za uwindaji katika eneo hili kabla ya kuuawa na Wajerumani katika vita ya kwanza ya dunia na kuzikwa katika eneo hili lililopewa jina lake kama kumbukumbu na heshima kwake.


  Ziara hii ya kundi la wandishi wa habari imeandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania-TTB  kwa kushirikiana na Hoteli ya Serena na Shirika la ndege la Fast jet kwa lengo la kitangaza Tanzania nchini Afrika Kusini . Wandishi hawa wako nchini kwa ziara ya siku tatu ya kujionea vivutio vya utalii vya Tanzania  hususan vilvyoko katiia pori la akiba la Selous na Zanzibar.


  Wakati huo huo wandishi wa habari watano kutoka vituo vya televisheni vya nchi za Ufalme za Kiarabu wanatembelea pia pori la akiba la Selous baada ya ziara yao katika hifadhi ya Taifa  ya Serengeti kabla ya kuelekea Zanzibar.  Ziara ya wandishi hao imeandaliwa  na Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa lengo hilo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika nchi za falme za kiarabu.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi akifungua Mkutano wa siku mbili wa Jumuiya ya Africa Mashariki wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa kwa Mamlaka za udhibiti wa bidhaa hizo kwa Nchi wanachama.
    Mratibu wa Mradi wa Usajili wa Chakula na Dawa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. John Patrick (aliesimama) akitoa maelezo kuhusiana na Mradi huo katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar.
   Afisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bi. Hidaya Juma Hamad akielezea changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa kazi za Bodi hiyo, (kusho) ni Meneja Operesheni wa Mradi wa Usajili wa chakula na Dawa wa nchi za Afrika Mashariki Apolo Muhaiwira.
  Mrajis Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhani Othman Simai akijibu  masuali aliyoulizwa na wajumbe wa Mkutano huo, (kushoto) Mwenyekiti wa Mkutano Dkt. Jamala Adam Taib.

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi (wakatikati) waliokaa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Africa Mashariki wa tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

  0 0

   The Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Agriculture, Food Security and Cooperatives Eng. Raphael Daluti (centre) launches documents on Making the Case for Ecological Agriculture today in Dar es salaam.Left is Dr. Vandana Shiva, Award winning authour and environmental activist and Mr. Jordan Gama Chief Executive Officer of Tanzania Organic Agriculture Movement (TAOM).
   Mr. Pius Paulini, one of the member of the Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) an Organisation for farmers and good practice of Agro-ecology  based in Morogoro region display some of their products during the 2014 International Year of Family Farming workshop in Dar es salaam.

  TANZANIA AND THE 2014 INTERNATIONAL YEAR OF FAMILY FARMING.

  By. Aron Msigwa - Dar es salaam.
   12/6/2014.

  The United Nations General Assembly declared 2014 the International Year of Family Farming (IYFF) at its 66th session to highlight the important of global role family and smallholders farmers have contributed in eradicating hunger and poverty, providing food security and nutrition, improving livelihoods, achieving sustainable development and building resilience especially in rural areas.

  The UN goal for the International Year of Family Farming is to reposition family farming at the center of agricultural, environmental and social policies in the national agenda by identifying gaps and opportunities to promote a  shift towards a more equal and balanced development.

  Family farming contributes a lot to the global food security. It is estimated that family farming accounts to 80% of total food produced globally.
  In Tanzania about 74% of its population is employed in agriculture and majority are small holder farmers who have enabled the sector to account for 24.7% of the GDP and about 34% of foreign export earnings.

  The government of Tanzania has embarked on range of strategies and programs that aim at increasing agriculture production and productivity. Some of the programs include; Agriculture sector Development Program (ASDP), The Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan (TAFSIP) and the Big Result Now (BRN). For all programs and strategies smallholders and family farmers are at the center.

  0 0

   Daktari Bingwa wa upasuaji Dk. Muganyizi Kairuki akizungumza wakati wa semina ya upasuaji kwa njia  matobo Laparoscopia uliofanyika LIVE katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliwashirikisha madakatari wa ndani na nje ya nchi.
   Daktari Bingwa wa upasuaji kutoka Afrka Kusini, Prof. Zacharia Koto (wa pili kulia), akisaidiana na daktari bingwa wa upasuaji kutoka Namibia Dk. S. Kaikai (kulia) na Dk. Muganyizi Kairuki wakimfanyia operesheni ya kuondoa mawe tumboni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki, wakati wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Madaktari wakiwa kazini.
   Madaktari wakishauriana jambo wakati wa operesheni.
   Madktari wakiwa kazini.
   Dk. Sunil Popat kutoka India akifanya operesheni ya matobo Laparoscopia Live.
   Kutoka kushoto ni Dk. Ali Mwanga wa Muhimbili, Dk. Steven Mbata wa Kairuki Hospitali, Dk. Brown Ndofor wa Namibia Dk. Sunil Popat wa India na Sister Salvata Kulaya wa Kairuki Hospitali.
   Chumba cha upasuaji kikiwa na vifaa vya kisasa.
    Kutoka kushoto ni Dk. Jerome Mtiramweni wa HKMU, Dk. Brown Dafor wa Namibia, Dk. Sunil Popat wa India na Sister Salvata Kulaya wa Kairuki Hospitali.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni, akizungumza wakati wa semina ya upasuaji wa matobo Laparoscopia uliofanyika LIVE katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Dk. Muganyizi Kairuki (kushoto) akiwaonyesha madaktari vifaa vinavyotumika wakati wa kufanyia operesheni ya matobo Laparoscopia, madaktari waliohudhuria kwa mafunzo vitendo namna ya kutumia vifaa hivyo.  
  Professa Esther Mwaikambo akichangia mada wakati wa semina hiyo.
   Professa Zacharia Koto (kushoto), akipokea ngao kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni
   Dk. Paul Kisanga wa Selian Hospitali Arusha, akipokea cheti kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni.
  Baadhi ya madaktari wakiwa katika picha ya pamoja.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo kwa vitendo Laparoscopia.

  0 0


  Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz, Mchungaji Deo Lubala wa Kanisa la Word Alive pamoja na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
  Mchungaji Abel Orgenes (wa kwanza kulia) wa Kanisa la International Evangelism akiendelea kufafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. 
  Mchungaji Deo Lubala (katikati) wa Kanisa la Word Alive akiongea machache na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mkesha utakaofanywa na Huduma ya AFLEWO ambao utakuwa wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Anayefuatia kulia ni Mchungaji Fred Okello wa Kanisa la Upper Room Ministries Tz na mwenyeji wao Mchugaji Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste.
  Huduma ya AFLEWO imeandaa mkesha wa kusifu na kuabudu na maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania. Waimbaji zaidi ya hamsini kutoka makanisa mbali mbali watakuwa kwenye jukwaa moja wakisifu Mungu. Waumini na Wachungaji na maaskofu watakusanyika kumsifu na kumuomba Mngu kwa ajili ya taifa la Tanzania hasa kwa ajili ya mchakato wa katiba na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2015.

  Mkesha huu maalum utafanyika kesho Ijumaa Juni 13, 2014 katika kanisa la City Christian Center, Upanga jijini Dar es Salaam (CCC) lililoko karibu na Chuo Kikuu cha Mzumbe. Kutakuwa hakuna kiingilio, watu wote mnakaribishwa kusifu na kuabudu.

  0 0

      Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa kongamano
      Makamu wa Rais, Dr Bilal akizungumza

   Wageni waalikwa katika kongamano.

  Dubai, United Arab Emirates-Katika kile kinachoonekana ni hatua kubwa katika kuelekea kutengeneza fursa kwenye sekta ya uendelezaji wa makazi, Shirika la Nyumba la Taifa limeweka historia kwenye soko la kimataifa na kufanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya kongamano la uwekezaji hapa Dubai ambalo limefanikiwa kufikia lengo lake la kuonyesha fursa zilizopo kwenye sekta ya ujenzi kwa makampuni makubwa ya ujenzi yaliyopo Mashariki ya Kati na kwingineko.

                               

  Tukio hili la kipekee na kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Gharib Bilal na lilihudhuriwa na makampuni makubwa ya ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambayo yamehusika na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira na Dubai Mall.


  Makampuni mengine yaliyohudhuria kutoka ukanda wa Guba kama Qatar na Bahrain pamoja na nchi nyingine kama Korea, Sweden na Romania yameonyesha kuwepo kwa nia ya makampuni makubwa kuwekeza kwenye sekta ya makazi Tanzania.  Malengo ya Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa;


  Kongamano la Wawekezaji Wa Sekta ya Makazi Tanzania ni sehemu ya lengo kuu la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu, ambaye kwa sasa analiongoza shirika hilo kubwa Afrika Mashariki. Kipindi cha Msechu kwenye uongozi kimeonyesha mabadiliko na ubunifu mkubwa kwenye uendelezaji wa sekta ya makazi nchini.


  Mchechu anasema lengo kuu la kongamano hili ni hatua kubwa kuelekea mkakati wa kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni sehemu pekee likija swala la uwekezaji na urudishaji wa faida kwenye sekta ya makazi.


  ‘Tanzania inatoa fursa ya pekee linapokuja swala la uwekezaji kwenye sekta ya makazi barani Afrika na hii ni kutokana na uwazi pamoja na utulivu wa kisiasa na amani inayopatikana nchini, uchumi unaokua pamoja na ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali’ anasema Mchechu.


  ‘Tukio hili la kihistoria ni sehemu tu ya mpango kamili wa kuifahamisha dunia kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta ya makazi zinazopatikana nchini’ alisema Mchechu.


  Mchechu anaamini kuwa huu ni muda mwafaka kwa wawekezaji kuitazama Tanzania na Afrika kwa ujumla. ‘Zamani ilikuwa ni hatari kwa wawekezaji kuwekeza Afrika na Tanzania, lakini kwa uchumi wa leo, ni hatari kutokuwekeza Tanzania’ alisema Mchechu.


  Kati ya miradi iliyoonyeshwa kwa wawekezaji ni pamoja na miradi mitatu ambayo itaendelezwa kwa kwa kipindi cha miaka 5. Hii inajumuisha miradi miwili ya kuendeleza Arusha inayoitwa Safari City na USA River ambayo kwa pamoja itakuwa na jumla ya nyumba 8000, pamoja na mradi mwingine wa kuendeleza makazi Dar es Salaam utakaofahamika kama Salama Creek Satellite City ambao utakuwa na jumla ya nyumba 9,500.


  Miradi hii yote iko tayari kwa maana ya kuwa vibali vyote vya mradi vimepatikana na kinachotakiwa ni kuwekeza tu, na ndio maana kongamano hili lilikuwa muhimu kwa ajili ya kupata uwekezaji unaotakiwa.
  Serikali inatimiza wajibu wake;


  Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dr Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wageni waalikwa alielezea namna serikali yake imefanya kazi kubwa kwa miaka michache iliyopita kuhakikisha inatengeneza fursa katika sekta ya makazi, ambapo mabadiliko makubwa yalikuwa katika maeneo matatu makuu ambayo sasa yamekuwa sheria. Maeneo hayo ni pamoja na mikopo ya nyumba, uanzishwaji wa kampuni ya kusaidia kuwezesha mikopo ya nyumba (TMRC),pamoja na upitishaji wa sheria ya Condominium ambazo kwa hakika zimechangia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya makazi.


  ‘Tanzania kwa sasa inashuhudia mafanikio makubwa kwenye sekta ya makazi, huku kukiwa kuna upungufu wa jumla ya nyumba milioni 3.8 na upungufu huo unakua kwa kiasi cha makazi 200,000 kwa mwaka, ambayo kwa hakika inatoa changamoto kubwa kwa Tanzania lakini ni fursa kubwa kwa wawekezaji’ alisema Bilal.


  Naye Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na wageni waalikwa alisisitiza namna sekta ya makazi ilivyoimarika nchini Tanzania.


  ‘Sekta ya makazi ndio sekta inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania na tunakaraibisha wawekezaji kutoka nchi za falme za Kiarabu’ alisema Mbarouk.


  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa George B. Simbachawene, anasema msingi mkuu wa kukua kwa sekta ya makazi ni ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi ambao unaruhusu uwekezaji na ukuaji mzima wa sekta.


  ‘Ushirikiano baina ya sekta binafsi na serikali ni muhimu kwa ukuaji wa sekta ya makazi. Tukio kama hili linaruhusu wawekezaji kutoka nchi za falme za Kiarabu kuona fursa zilizopo Tanzania na kuzitumia’ anasema Simbachawene.


  Kiwango cha Uwekezaji ni kipi?


  Mchechu anasema kongamano la hili linalenga kufikia wawekezaji wenye uwezo wa kuanzia dola milioni 20 hadi dola nusu bilioni.


  ‘Tunajua uwezo wa uwekezaji unaotakiwa hauwezi kufikiwa kwa usiku mmoja na ndio maana miradi yetu mingi ni zaidi ya miaka 5 hadi 7, lakini tuna miradi ambayo inaanzia dola milioni kumi hadi dola milioni mia, kwahiyo kiasi chochote ambacho mwekezaji atakuwa nacho kati ya kiwango hicho tuna fursa za kuwekeza’ anasema Mchechu.  Watanzania Wanaowekeza Tanzania:


  Mchechu anasema kutafuta wawekezaji hakuishii tu kwa wale walio nje ya Tanzania bali hata kwa Watanzania, na kwa kuanza kutakuwa na kongamano mwisho wa mwezi huu litakalofanyika Dar es Salaam ambalo litajumuisha wawekezaji walio nchini wanaotaka kuendeleza nchi yao.


  ‘Hatujasawahau dada na kaka zetu nyumbani Tanzania, wengi wao wana nafasi kubwa ya kuwekeza katika miradi ya uendelezaji wa sekta ya makazi nchi, na tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo pia’ anasisitza Mchechu.


  Ushirikiano na Wadau:


  Kongamano hili limefanyika kwa ushirikiano kati ya Balozi wa Tanzania Dubai, Mheshimiwa Omary Mjenga pamoja na Balozi Maalumu wa Mambo ya Kiuchumi, Bwana Cleophas Ruhumbika, ambao walishughulikia taratibu za kongamano pamoja na kualika makampuni ya uwekezaji ya Dubai.


  "Tuna furaha kubwa kufanya kazi bega kwa bega na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye tukio hili la kihistoria’ anasema Mjenga. ‘ Sehemu kubwa ya kazi yetu hapa Dubai ni kuwezesha fursa kwa Tanzania ambayo inaendana na wajibu wetu hapa. Pia tuna furaha kubwa kuwa tukio limekuwa la mafanikio makubwa na nina hakika kuwa fursa zaidi za wawekezaji kuja Tanzania zitazidi kufunguka’ anamalizia Mjenga.
  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala Ndugu Theresia Mbando (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (wa nne) nje ya jengo la Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kupokea maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi za Dar es Salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa huo tarehe 12.6.2014.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam wakiwa wamebeba mabango yenye picha na ujumbe mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar zilizofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mchezo wa sarakasi iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar wakati wa sherehe ya uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya E & D, Ndugu Demere Kitunga (kushoto) wakati wakielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya sherehe za uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Theresia Mbando mara baada ya kuzindua rasmi Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa terehe 12.6.2014.
  Baadhi ya watoto walioshiriki uzinduzi wa tamasha la vitabu mkoani Dar es Salaam wakiwa wanasoma baadhi ya vitabu na majarida ya watoto wakati wa sherehe hizo kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha moja ya kijarida cha hadithi kwa ajili ya watoto alichokichagua kwa ajili ya kuwasomea hadithi watoto wakati akizindua rasmi Tamasha la vitabu vya watoto kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa hapa Dar Es Salaam tarehe 12.6.2014.
  Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wakati wa uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Makumbusho terehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mtoto Edda Kasika kutoka Shule ya Msingi Maktaba tuzo kwa kushika nafasi ya pili katika uandishi wa insha katika Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha la vitabu kwa watoto tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi washindi wa insha na mchapishaji wa vitabu bora vya watoto na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua rasmi tamasha la vitabu vya watoto wa shule tarehe 12.6.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia maonyesho ya vitabu, vijarida na kazi mbalimbali zilizokuwa zikionyeshwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.7.2014.

  0 0

   Warembo wanaogombania Miss Manyara 2014
  Warembo wanaogombania Miss Manyara 2014 wakiwa wanacheza mmoja ya wimbo watakaoucheza katika siku ya mashindano ikiwa ni moja ya sehemu ya mazoezi. Picha na Woinde Shizza.

  Na Woinde Shizza, Manyara 
   Kinyanganyiro cha kugombea Redd's Miss Manyara 2014, kinatarajia kufanyika kesho Jumamosi Juni 14 mwaka huu katika ukumbi wa CCM Mkoa, mjini Babati, ambapo warembo 10 wanatarajia kuchuana. 

   Mkurugenzi wa Mirerani Entertainment, Akon Clement ambaye ni Mratibu wa mashindano hayo alisema mgeni rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mary Nagu. 

   Akon alisema msanii maarufu wa kizazi kipya, Bob Junior kutoka jijini Dar es salaam anatarajiwa kutoa burudani kali wakati akisindikiza michuano hiyo ambapo pia wasanii chipukizi kutoka mjini Babati watashiriki kunogesha. 

   Aliwataja wanyange hao wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kuwa ni Miss Mirerani 2014 Amina Omary, Miss Mirerani namba mbili Catherine Emmanuel na Miss Mirerani namba tatu Happy William. 
  Wengine ni Fatuma Salim, Betha Fredrick, Rose Evason, Edna Mushi, Hosiana John, Mary Ruta na Flora Godlizen, ambao ni warembo walioshinda kwenye mashindano ya wilaya za Babati, Hanang' na Mbulu, alisema Clement. 

   Aliwataja wadhamini wa mashindano hayo ni kampuni ya Tanzania Breweries (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd's Original, Open University, Manyara Computer, mireranitanzanite.blogspot.com,libeneke la kaskazini blog na Active Classic Fashion. 

  Mratibu huyo alisema kuwa wadhamini wengine wa shindano hilo ni TanzaniteOne, Assey Printing company, Trimus Saloon, Kifaru Agrovet, Winners Hotel, Sarafina Lodge na Kimweri Sport Wear.

  0 0

   Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu discussing with the former French President H.E Giscard d’Estaing who is a Patron of the Tanzania Wildlife Conservation Foundation during the  fundraising dinner in Paris last night. 
   Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (MP) meets Mr. John Jackson, Chairman of the US Conservation Force during the fundraising dinner organized by Wildlife foundation of Tanzania in Paris. Looking on from left are the Director General of Tanzania National Parks Mr. Allan Kijazi and Director General of National Museum Professor Audax Mabulla.
   Former French President H.E Giscard d’Estaing who is the  Patron of  the Wildlife Conservation Foundation of Tanzania delivering a speech during the  fundraising dinner in Paris last night. 
   Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu presenting his remarks to the invited guests at the fundraising dinner in Paris. 
   Various wildlife pictures were auctioned during the Wildlife Conservation Foundation of Tanzania fundraising dinner in Paris.

  Over 500 Million Tanzanian shillings was raised during the recent Wildlife Conservation Foundation of Tanzania annual fundraising dinner last night in Paris, France. 

  Speaking during the function, Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu thanked the foundation for their passion in wildlife conservation over the past 10 years since the foundation was formed as they have contributed much to the wildlife sector through their donations in terms of vehicles, equipment and supplies to various protected areas in the country. 

   Hon. Lazaro Nyalandu said that a major review of the law has been made to enable establishment of the Tanzania Wildlife Authority, which will be a solution to various conservation challenges facing some of the protected areas particularly the poaching crisis. 

  He told the invited guests that government would work closely with other stakeholders and international community to ensure that illegal wildlife trade is stopped for the betterment of the wildlife sector in the country. 
   On his side, former French President H.E. Giscard d’Estaing  who is the Patron of the Tanzania Wildlife Conservation Foundation of Tanzania, thanked the participants for their financial commitments and pledges towards conservation sector and assured them that the raised funds will be used for the intended purpose of conserving wildlife sector in the country. 
   Over 170 participants attended this year’s fundraising dinner from various parts of the world who have a passion in wildlife biodiversity conservation.
  For more photos CLICK HERE

  0 0  0 0

  Baadhi ya Watu wakitazama ajali ya magari mawili kama yaonekanavyo pichani,iliyotokea mapema leo eneo la Moroco-Posta jijini Dar,katika ajali hiyo ambayo chanzo chake hakikufahamika mara moja,mtu mmoja alijeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha.
  Mama ambaye jina lake halikufahamika mara moja moja aliyekuwa kwenye gari lenye usajili wa namba T679 CKC,akipewa huduma ya kwanza mara baada ya kupoteza fahamu
  Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani
  Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani,huku abiria wake mmoja akiwa amepoteza fahamu,kama aonekavyo kwa mbali
  Majeruhi akipewa huduma ya kwanza na mmoja wa akina mama aliyekuwa akifanya usafi kando kando ya barabara mapema leo asubuhi,katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha. 

older | 1 | .... | 297 | 298 | (Page 299) | 300 | 301 | .... | 1898 | newer