Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Waandishi 37 watunukiwa tuzo za maoni yao kuhusu kuboresha utoaji huduma

$
0
0

Twaweza, kama sehemu ya kazi zake kwenye Mpango wa kuendesha shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), imetoa tuzo za kompyuta (aina ya laptops) na taa zinazotumia nishati ya jua kwa waandishi 37 kutokana na mawazo yao juu ya namna Serikali na wananchi wanavyoweza kuboresha utoaji huduma kwenye sekta za elimu, afya na maji.


Shindano hili la kutafuta maoni ya wananchi lilizinduliwa kwa ushirikiano wa Twaweza pamoja na Serikali ya Tanzania mwezi Desemba 2012. Twaweza iliisaidia Serikali kukusanya maoni haya kwa kusambaza taarifu kuhusu shindano hili na maelezo yake kwenye vijitabu takriban milioni tano vyenye kueleweka kiurahisi na pia ilipitia na kuchambua maoni yaliyowasilishwa.

Kati ya maoni 250 yaliyopokelewa, 12 bora walizawadiwa kompyuta na maoni 25 yaliyofuatia walipewa pongezi kubwa na taa zinazotumia nishati ya jua. Majina ya washindi hao ni:

Washindi 12 bora zaidi: Rahma Chanzi, Yavan N. Eslon, Amani Frank, Kingstone W. Kahumuza, Sarah Lucas Kisusange, Castory Luoga, Noely Sosimaria Mapunda, Allen Richard Materu, Abdul Walter Moshi, Einoth Justine Ngotoroi, Editha M. Tairo na Godwin Waziri.

Washindi 25 waliofuatia: waliopata pongezi na taa inayoitumia nishati ya jua ni- Godfrey Baraka, Sande John, KenethKammu , Gabriel Erick Mvingira, Fatuma M. Athumani, Joseph Mathew Buyende, Rachel Philip Bwathondi, Johanita Chimwanga, Christina K. Christopher, William Gabriel Lugis Benjamin John, Specioza Joseph Kalekwa, Kelvin CosmasMacha, Kaliro M. Magoro, Emmanuel Deus Malimi, Filipo Faraja Maliwa, Mariamu Omary Mcholo, Simon Sabaya Mollel, Dorcus Ayoub Mollel, Mary Richard Msukwa, Dativa Mugashe, Abubakar Khasim Mweli, Erick Rwelamila, Vincent Deo Simba na Hedwiga Medard Tairo.

 Baadhi ya mawazo yaliyoshinda yalikuwa pamoja na:
·         Uwepo wa gazeti maalum linalochapishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwajulisha wanafunzi, walimu, wazazi na watu wengine kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu na takwimu muhimu kama vile viwango vya kufaulu mitihani, mitaala na matukio mengine muhimu.
·         Upungufu wa wafanyakazi wa afya nchini Tanzania kwa sehemu unaweza kuhusishwa na ukosefu wa wanafunzi waliosomea masomo ya sayansi. Ili kukabiliana na tatizo hili Serikali inapaswa kuanzisha mfumo wa motisha, kama vile kutoa zawadi, ili kuvutia wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.

Zawadi zilitolewa kwenye mkutano ulioitishwa na Serikali ya Tanzania ili kushauriana na wadau juu ya rasimu ya pili ya Mpango wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP).. Mgeni rasmi, Mheshimiwa George Mkuchika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Utawala Bora, aliwazawadia wanafunzi vyeti na tuzo zao.

OGP ni jitihada ya kimataifa inayolenga kuziongoza Serikali kuwajibika zaidi kwa wananchi kwa kukuza uwazi, kuwawezesha wananchi, kupambana na rushwa, na kutumia teknolojia mpya kuimarisha utawala. Hadi sasa, ni mataifa 64 yaliojiunga na OGP, Tanzania ikiwa mmoja wapo.

Mpango Kazi wa  kwanza  wa OGP kwa Tanzania inapatikana hapa: http://bit.ly/1mZCPj4. Mpango huu umeweka kipaumbele kwenye utoaji huduma na upatikanaji wa taarifa kama nguzo muhimu kwenye harakati za Tanzania kuelekea Serikali wazi. Mpango Kazi wa pili wa Tanzania kwa sasa uko hatua za mwisho kukamilishwa kufuatia mashauriano na wadau mbalimbali.

Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Mawazo mapya yanatoka sehemu mbali mbali na shindano hili lilikuwa ni njia moja ya kuibua michango mipya kutoka kwa vijana. Huu ndiyo moyo wa OGP; kutambua kuwa serikali haina ukiritimba juu ya ufumbuzi wa changamoto zetu kuu na huitaji kutoa nafasi na fursa kwa wengine kuchangia mawazo."

Grand Malt yadhamini tamasha la filamu Mtwara

$
0
0
Meneja masoko wa Tbl Fimbo Buttala katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzunduliwa kwa tamasha kubwa la Filamu litakalofanyika mkoani Mtwara ambapo litashirikisha jumla ya wasanii arobaini nchini,kulia ni mratibu wa tamasha hilo Musa Kisoki na mwakilishi wa Bongo Muvie Shashim kambi 
========  =======   =======
KAMPUNI ya Bia Nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt kimetangaza kudhamini tamasha la wazi la  filamu ‘Tanzania Open Festival’ litakalofanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu mkoani Mtwara. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia sikukuu ya Eid Pili hadi Agosti 5 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana , Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah, alisema kuwa tamasha la mwaka huu  litafanyika mkoani Mtwara kwenye viwanja vya Mashujaa na hii imetokana na muonekano mkubwa uliopatikana mwaka jana.

Butallah alisema kuwa  lengo la kudhamini tamasha hili ni kutoka nafasi kwa mashabiki wa sanaa ya filamu nchini kushuhudia kazi zilizoandaliwa na wasanii wa hapa nchini. Butallah alisema kuwa wanaamini kufanyika kwa tamasha hili kunasaidia kukuza filamu za wasanii hao ambao wanapata ajira kupitia kazi wanazozifanya ambazo pia huburudisha jamii. Alisema tamasha hili linasaidia kutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kubadilishana mawazo na wadau ambao wananunua kazi zao.

“Tamasha hili tunaamini litatoa nafasi na kwa wapenzi wa Bongo Movie wa mkoa wa Mtwara na jirani kuona filamu zetu za kitanzania,” alisema Butallah. Alisema kwamba kwa kushirikiana na kampuni ya Sophia Records , TBL itahakikisha filamu za wasanii wa Kitanzania zinajulikana na kupata soko ndani na nje ya nchi.

Mratibu wa tamasha hilo, Mussa Kisocky, wanawashukuru wadhamini kwa sababu wamesaidia kulikuza na kufikisha ujumbe wa walengwa. Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni Amani na Upendo na wakiwa huko wasanii wanapata nafasi ya kutembelea shughuli mbalimbali za kijamii.

Alieleza kwamba mwaka huu wanatarajia kutoa vyandarua na magodoro kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto ya hospitali ya mkoa huo. “Ni chombo kinachowakusanya wasanii na wananchi wanaoona kazi zao,” alisema Kisocky. 

Mwakilishi kutoka Bongo Movie, Athumani Kambi, mbali na kupata nafasi ya kukutana na mashabiki wao, pia hukutana na wasanii chipukizi na kuwaelekeza njia sahihi ya kujiendeleza na kukuza vipaji vyao. Grand Malt inadhamini tamasha hili kwa mara ya tatu mfululizo ambapo mwaka juzi lilifanyika jijini Tanga na mwaka jana lilikuwa Mwanza.

NBS YAENDESHA SEMINA KUHUSU CHAPISHO LA TAARIFA ZA MSINGI ZA KIDEMOGRAFIA, KIJAMII NA KIUCHUMI KATIKA HOTELI YA PEACOCK

$
0
0
1
Mwandishi wa TBC Elisha Elia akizungumza na Mwandishi Mwanafunzi wa TBC Bi Laura Pylvanainen wakati wa semina hiyo.

Airtel yawezesha mafunzo kwa wafanyakazi wa Afya kijiji cha Mbola Tabora

$
0
0
 Wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora wakijaribu namna ya kutumia simu zao mara baada ya mafunzo ambapo Airtel inawawezesha kutumia simu zao kutoa huduma za Afya chini ya mradi wa millennium village. 
 Akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora namna ya kutumia huduma ya mawasiliao ya simu kutoa huduma za kiafya Ambapo Airtel imewapatia wafanyakazi hao huduma ya internet , message na simu bure na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia maeneo mengi zaidi.
Mfanyakazi wa huduma za afya bi Amina Wakasuvi akitoa huduma kwa moja ya familia katika kijiji cha mbola mkoani Tabora  ambapo Airtel chini ya mradi wa millennium village imewawezesha wafanyakazi hao kutumia mtandao wa mawasiliano kutoa huduma za Afya.
=======  =======  =======
·         Airtel yajikita kuboresha mazingara ya jamii  vijijini
Tabora Junanne 10 Juni 2014, wafanyakazi wa afya wa kijiji cha mbola mkoni Tabora wametoa shukrani zao kwa Airtel kufatia technologia ya huduma ya mawasiliano inayoyowawezesha kutoa huduma za afya kwa wigo mpana na kuwafikia wakazi wengi zaidi.

Wafanyakazi hao wa afya walipata mafunzo ya namna ya kutumia technologia ya huduma ya afya kupitia simu iitwayo COMCARE, iliyoanzisha kwa msaada wa Dagiba  inapatikana kupitia simu za smart phone zenye application maalumu inayowawezesha wafanyakazi wa afya kukusanya takwimu za wagonjwa na kutuma repoti kwenye vituo vya afya.

Akiongea wakati wa mafunzo mmoja wa wafanyakazi wa afya Ms Amina Wakasuvi alisema” Tekinologia hii mpya  ya kisasa itatuwezesha kufatilia kazi zinazofanywa na wafanyakazi wa afya wakiwa katika maeneo mbalimbali na wafanyakazi hao wataweza kutuma repoti zao kwa wakati kila siku kupitia mtandao wa Airtel. Hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa ubunifu huu na huduma ya vifurushi vya internet vya bure vinavyotuwezesha kufanya kazi zetu kwa wakati.

Akionge wakati wa tukio hilo Meneja huduma kwa jamii bi Hawa Bayumi alisema” kwa miaka mitatu sasa Airtel imewekeza katika kuleta mapinduzi ya kupatikana kwa  huduma kwa jamii husasani katika maeno ya vijiji vya Tabora  kwa kushiriki katika mradi wa  Millennium village kama mtowaji mkuu wa huduma za mawasiliano. 

Katika mradi huu Airtel inatoa njia ya mawasiliano kwa kuwezesha jamii inayoishi katika maeneo ya pembezoni kupata huduma za Afya. Wafanyakazi wa afya katika maeneo hayo wameunganishwa na mtandao wa kisasa unaowapatia huduma ya internet na simu na kurahisisha kazi zao pindi wakiwa kazini. Sasa wafanyakazi hawa wanaweza kukusanya takwimu kwa kutumia simu na pia kuwawezesha wagonjwa walioko vijijini kuongea na madakitari specialist walioko mjini na kupata huduma za afya kupitia simu za mkononi”.

Bayumi aliongeza mpaka sasa tumeiwezesha miradi mitatu kupata huduma ya kupiga simu, ujumbe mfupi na vifurushi vya internet bure, Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuwaleta watanzania karibu na huduma muhimu za jamii kupitia technologia ya mawasiliano.

Akiongea kuhusu mradi huo, Mkurugnzi wa mradi wa Millennium Village Dr. Gerson Nyadzi alisema “ Mtandao wa 3G wa Airtel umetuwezesha kwa kiasi kikubwa  kufikia maeneo ya vijijini  ambapo huduma ni duni na haba. Kuanzia mradi huu uanzishwe  kumekuwa na ongezeko la 85% la  upatikanaji wa huduma muhimu za afya hapa Mbola. Kwa kuongeza mradi wa Child count katika techonologia ya huduma za afya ya CommCare kutawezesha zaidi ya wakazia 97% kupata huduma za afya kupitia watoa huduma wetu wa afya wenye vyenzo hizi muhimu za kutendea kazi.

MWENYEKITI CHADEMA AHAMIA CCM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa Vijijini,Seleman Kiponda  akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa.
 Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa Vijijini,Seleman Kiponda  akikabidhi bendera ya Chadema kwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa.
 Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa Vijijini,Seleman Kiponda  akizungumza nia yake ya kuhamia CCM.

diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa akimkabidhi bendera ya CCM aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema kata ya Ihimbo katika jimbo la Kilolo Selemani Kipondi.

 Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akizungumza wakati wa kumkaribisha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo,Seleman Kiponda baada ya kuhamia CCM katika ofisi za ccm mkoa wa Iringa.

Na Denis Mlowe,Iringa

 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ihimbo jimbo la Kilolo  mkoani Iringa,Selemani Kiponda ameamua kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukosa ushirikiano na uongozi wa juu.
 
Kiponda alifikia uamuzi huo juzi kwa kile alichosema amekuwa kiongozi wa chadema kwa  miaka minne na ameweza kushawishi wakazi wengi katika maeneo mbalimbali katika kata ya Ihimbo kujiunga na  chama hicho lakini hawajawahi kupata ushirikiano kutoka uongozi wa juu wa chama wa mkoa hadi taifa.
 
“Nilijiunga na Chadema mwaka 1993 wakati ndio kwanza upinzani umeingia nchini na nimekuwa kiongozi kwa miaka zaidi ya minne lakini hakuna ushirikiano kutoka uongozi wangu hivyo nimerudi ccm kwa kuwa ndio chama changu ambacho kwa kweli nilikuwapo tangu enzi za Tanu na hivyo kwa hiari yangu nimeamua kurudi ndani ya chama makini na chenye sera zenye kueleweka” alisema Kiponda”
 
Aidha alisema kuwa hatua ya yeye  kurudi CCM imetokana na maendeleo yanayofanywa na diwani wa kata hiyo Hezron Nganyagwa pamoja na mbunge wa jimbo la kilolo profesa Peter Msola kwa kuwa ushirikiano umekuwa mkubwa kuliko ambavyo sikutegemea uwepo kwa kuwa nilikuwa chama cha upinzani.
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema Kiponda amefanya maamuzi sahihi ya kurudi CCM kwa kuwa muda mrefu amekuwa Chadema hivyo ameona tofauti iliyoko miongoni mwa vyam hivyo pinzani.
 
Mtenga alisema kuwa viongozi na wanachama wa CCM  wataendeleza ushirikiano katika kuwarudisha wanachama wa Chadema wengine waliobaki Ihimbo kwa kuwa kimefanikiwa kuwaunganisha wananchi katika kujiletea maendeleo kutokana na uongozi imara wa chama hicho.
 
Naye diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa aliahidi kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo kama ilivyokuwa mwanzo walipokuwa wakishirikiana ingawa walikuwa wapinzani.
 
Kurudi kwa kiongozi huyo kunaongeza idadi ya wanachama  wanne waliohama Chadema hadi sasa wakiwemo Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje, Zawadi Waziri Shombe ambaye alikuwa ni mjumbe wa oparesheni ya M4C Nyanda za Juu Kusini, pamoja na Bernado Lugenge.

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE TAMASHA LA KWANZA LA VITABU VYA HADITHI KWA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI

$
0
0
DSC_0481
Baadhi ya watoto wa shule za msingi jijini Dar wakifanya mazoezi ya maigizo kwa ajili ya tamasha la kesho kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
DSC_0533
WANAFUNZI wa shule za Msingi nchini, wameshauriwa kuwa na mazoea ya kusoma vitabu kwa lengo la kuwa wagunduzi wa vitu mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Soma, Demere Kitunga wakati wa maandalizi ya tamasha la kwanza la vitabu vya hadithi kwa watoto wa Shule za msingi.

Kitunga amesema kuwa tamasha hilo ni moja ya michakato ya kuwataka watoto kupenda kusoma vitabu hasa vitabu vya hadithi kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii.

"Ugunduzi wa jambo fulani unaanzia katika kusoma hivyo watoto wakiwa wanania ya kusoma vitabu mbalimbali hususani vya hadithi wataweza kuongeza uwelewa fulani katika fikra zao,"amesema Kitunga
Aidha amesema kuwa tamasha hilo linatarajia kuanza kesho hadi juni 14 mwaka huu katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini ,ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
DSC_0590
Mmoja wa watoto akionyesha kipaji chake wakati wa mazoezi kwa vitendo kupitia hadithi mbalimbali walizosoma kutoka kwenye vitabu.
Kitunga amesema kuwa Taasisi hiyo hadi sasa imeweza kusambaza vitabu katika Shule mbalimbali za Msingi pamoja na klabu za kujisomea zikiwemo Kurasini ,maktaba pamoja na Chang'ombe.

Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na maigizo ambayo yatafanywa kwa kutumia hadithi zilizokuwa katika vitabu hii yote kwa lengo la kukuza utamaduni wa watoto kusoma vitabu.

WAKULIMA WADOGO WAASWA KEPUKA MATUMIZI YA KEMIKALI ZENYE ATHARI KWA MAZINGIRA NA AFYA.

$
0
0

  Mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa wakulima wadogo ambao wanazalisha 70% ya chakula kinachotumiwa duniani kote walivyo na wajibu wa kuiepusha jamii na matumizi ya vyakula vinavyozalishwa na kuhifadhiwa na kemikali za viwandani zenye madhara kwa afya.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania Bw. Jordan Augustino (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa kimataifa wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kilimo utakaofanyika June 12 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es salaam ambapo washiriki wa mkutano huo watabadilishana uzoefu kuhusu mchango wa wakulima wadogo katika sekta ya kilimo.
  Mratibu wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) kutoka Ethiopia Dkt. Million Belay akiongea na waandishi wa habari kuhusu  umuhimu wa kilimo kinachoendana na mazingira halisi barani Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kitabu kinachoelezea shughuli mbalimbali za binadamu zinavyoathiri uharibifu wa mazingira ya asili duniani. Kulia ni Muhamasishaji na mtetezi wa uhifadhi wa Mazingira kutoka Greenpeace Bw. Glen Tyler.

=======  ====== ======
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.


Wito umetolewa kwa wakulima wadogo kote nchini kuzingatia kilimo salama kinachohimiza matumizi ya mbolea za asili ili kupata mazao bora na salama kwa afya ya jamii na kuepuka kutumia kemikali zenye athari kwa uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam mshindi wa tuzo mbalimbali na mwanaharakati wa mazingira duniani Dkt.Vandana Shiva kutoka nchini India amesema kuwa wakulima wadogo ambao wanazalisha 70% ya chakula kinachotumiwa duniani wanao wajibu wa kuiepusha jamii na matumizi ya vyakula vinavyozalishwa na kuhifadhiwa na kemikali za viwandani zenye madhara kwa afya.



Dkt. Vandana ambaye yuko nchini Tanzania kuungana na wadau wengine wa kutetea kilimo salama na rafiki wa mazingira wanaohudhuria  mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kilimo ameeleza kuwa yeye pamoja na wadau wengine wanaendelea kuhamasisha wakulima duniani kote kupitia programu zinazohimiza kilimo kinachoshabihiana na mazingira ya asili na uhifadhi wa mazingira kwa chakula salama barani Afrika.

Amesema kuwa yeye pamoja na wadau wengine wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) wanaamini kuwa chakula bora na salama ni kile kinachozalishwa kutokana na ardhi na si vinginevyo na kuongeza kuwa kilimo kinachohimiza matumizi ya mbegu na mbolea za viwandani licha ya kuwa na gharama kubwa za uzalishaji kina athari na madhara kwa afya na viumbe wengine wakiwemo nyuki na vipepeo.

“Ninao ushahidi wa kutosha unaoonesha madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya madawa makali na kemikali za viwandani kwa afya ya binadamu na viumbe wengine wa asili ambayo kama tusipochukua tahadhari mapema dunia itakua si mahali salama pa kuishi” amesema. Kwa upande wake Mratibu wa Muungano huru wa watetezi wa Kilimo Hai na Chakula Salama Barani Afrika (AFSA) kutoka Ethiopia Dkt. Million Belay amesisitiza kuwa kilimo kinachoendana na mazingira halisi ndicho kitakacholifanya bara la Afrika kujitosheleza kwa chakula.

 Amesema wao kama muungano na watetezi wa kilimo kinachozingatia uhifadhi wa mazingira wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali na tayari baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo Ghana,Ethiopia,Tanzania na Msumbiji zimechaguliwa katika mpango huo wenye lengo la kuwafanya wananchi wake kujitosheleza kwa chakula .

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania Bw. Jordan Augustino ameeleza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika June 12 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es salaam ambapo washiriki wa mkutano huo watabadilishana uzoefu kuhusu mchango wa wakulima wadogo katika sekta ya kilimo.

VURUGU ZA WAMACHINGA MWANZA MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA ZAIDI YA SAA 3, BIASHARA ZAFUNGWA KABISA.


WAHISANI WA MAENDELEO KUTOKA MAREKANI WAZINDUA MIONGOZO YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MAAMBUKIZI ZANZIBAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magonjwa unaosimamiwa na Shirika la Afya la Kimataifa la Jhpiego Dkt. Albert Komba (alisimama) akitoa maelezo katika uzinduzi wa Miongozo ya kitaifa ya kukinga na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
  Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akizundua vitabu viwili vya miongozo ya Kitaifa ya kukinga  na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa katika Hospitali na sehemu za  kutolea huduma za Afya katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Dkt. Jamala Adam Taib akionyesha vitabu  vya miongozo ya Kitaifa ya kukinga na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa katika Hospitali na sehemu za kutolea huduma za Afya.
 Meneja Mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magonjwa Zanzibar Bi. Asma Ramadhan Khamis akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa Mradi huo.
Picha ya pamoja ya watendaji wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wizara  hiyo (wa kati kati) waliokaa Dkt. Jamala Adam Taib na viongozi wa Shirika la Jhpiego baada ya uzinduzi wa miongozo ya Kitaifa ya kukinga na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
=======  ========
NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO.
                   
Wizara ya  Afya kwa kushirikiana na wahisani wa Maendeleo kutoka Marekani na Shirika la Afya la Kimataifa la Jhpiego imezindua miongozo miwili ya Kitaifa katika kukinga na kudhibiti kuenea kwa mambukizi ya magonjwa katika Hospitali na sehemu za kutolea huduma za afya Zanzibar.

Miongozo iliyozinduliwa ni wakuboresha viwango katika Hospitali na vituo vya afya ili kuzuia na kudhibiti maambukizo  na  ule unaobainisha vigenzo vya tathmini ili hospitali ziweze kutambuliwa na kupewa tunzo zitakazobainisha jitihada za vituo katika kufikia viwango vya ubora vya kitaifa.

 Akizindua miongozo hiyo katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya Dkt. Jmala Adam Taib amewataka madaktari na wafanyakazi wa vituo vya afya kubadilika katika kutoa huduma ili kupunguza maabukizi ya magonjwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa.

“Imebainika kati ya wagonjwa 100 wanaofikishwa katika Hospitali na vituo vya afya Unguja na Pemba, 15 kati yao wanapata magonjwa mengine  mapya wakiwa sehemu hizo jambo ambalo linaongeza gharama za matibabu kwa wagonjwa hao,”alisema Dkt. Jamala.

Ameshauri kuanzisha utaratibu utakaohakikisha maeneo ya kutolea huduma za afya  zinakinga na kudhibiti kiwango cha maambukizi ya magonjwa ili kuwalinda wananchi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma salama na za kiwango cha juu.

“Miongozo hii isaidie kuzifanya Hospitali zetu ziwe sehemu za wagonjwa kwenda kupata huduma na sio kuishia kupata maambukizi mapya na kuwaongezea mzigo na madhara zaidi,” alisisitiza kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya.

Amesema kitu muhimu kwa wafanyakazi ni kushirikiana katika kuzitunza na kuziendeleza nyenzo zilizopo katika Hospitali na vituo vya afya  na kuzifanyia matengenezo ambazo haziko katika hali nzuri ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Dkt. Jamala ameongeza kuwa miongozo hiyo pia itasaidia kuwalinda watoa huduma na jamii nzima katika hatari ya kupata maambukizo wakati wakiwasaidia wagonjwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizo ya magonjwa unaosimamiwa na  Shirika la Jhpiego Dkt. Albert Komba ameahidi  Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya ili kuhakikisha kiwango cha maambukizo mahospitalini kinapungua.

Amewashauri wataalamu wa Afya na wafanyakazi wa Hospitali na vituo vya Afya  kutekeleza wajibu wao na kuunga mkono mpango huo  kwa vitendo na Shirika la Jhpiego litaendelea kuwajengea uwezo ili  uweze kufanikiwa.

Dkt. Albert amesema Hospitali na vituo vya Afya vya Tanzania Bara vilivyoanzisha mpango huo zimepata mafanikio makubwa na ameeleza matumaini yake kwamba Zanzibar itanufaiki zaidi katika mpango huo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Wanne wanyakua zawadi ya Shinda Ki-Brazil na Mwanaspoti

$
0
0
Meneja Kasoko wa Mwananchi Communications Ltd (MCL) wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen  na Mwanaspoti, Bernard Mukasa akizungumza kwa njia ya simu katika ofisi za MCL  jijini Dar es Salaam jana na mmoja wa washindi wa bahati nasibu ya Shinda Ki-Brazil ambaye ni fundi umeme, Issa Rashid Ndingo mkazi wa Kigogo aliyeshinda king’amuzi cha DSTV. Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na gazeti la Mwanaspoti. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo nchini, Mrisho Millao.  Pcha na Rafael Lubava
===========  ============

Wasomaji wanne wa gazeti la Mwanaspoti jana Jumatano walitangazwa kuwa washindi wa kwanza wa promosheni ya Shinda Ki-Brazil na Mwanaspoti baada ya kunyakuwa zawadi mbalimbali zikiwemo vingamuzi vya Dstv pamoja na jezi.


Washindi hao wamenyakua zawadi hizo baada ya kutuma neno namba zitakazopatikana kwenye ukurasa wa tatu wa gazeti la Mwanaspoti kwenda kwenye namba 15551.Namba moja imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za binafsi. Namba ya pili imetambulishwa kwa herufi T na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za timu. 

Washindi wa vingamuzi vya Dstv pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa mwezi mmoja (Compact Plus) ni  Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla. Kwa upande mwingine aliyejishindia Jozi moja ya jezi (ina jezi 16), Jackson Fredrick wa Mwanza. 

Namenga (54) ambaye ni Afisa Mstaafu wa Jeshi na pia mkazi wa Mbagala alisema, " Nina furaha sana, nitaendelea kushiriki kwani naamini nitapata zawadi zingine."


Ndingo (42) ambaye ni mkazi wa Kigogo alisema, " Nawashukuru sana Mwanaspoti, nina uhakika wa kuona Kombe la dunia." 
Chengulla (25) ambaye ni mkazi wa Songea mjini, " Jamani someni Mwanaspoti mfaidi kama mimi, nimebahatika kwasababu nimeshiriki kwa kipindi kidogo na kushinda."


Fredrick (28) ambaye ni mwalimu alisema, " Nimefurahi kushinda jezi za kwenye promosheni hii, zawadi hii ni kwa wanafunzi wangu wa timu ya shule ya Sekondari ya Mamaye iliyopo Misungwi, Mwanza." 

Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi, Bernard Mukasa alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 27 za Dstv zilizounganishwa na kifurushi cha compact plus kwa muda wa mwezi mmoja, jozi tano za jezi pamoja na fedha taslim zinazotolewa kila siku mpaka shindano litakapomalizika.

Promosheni hii imeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications LTD (MCL) kupitia gazeti lake la Mwanaspoti kwa kushirikiana na kampuni ya  Multchoice Tanzania (Dstv) ikiwa na lengo la kuwaunganisha wadau wa soka nchini katika kufurahia mlolongo wote wa matukio ya michuano ya Kombe la Dunia huko Brazil.


Promosheni  hiyo ambayo ilifunguliwa rasmi  Juni 2   itafungwa Julai 12 siku ya mwisho ya mashindano hayo ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Brazil. 

TASAF yaendesha Warsha elekezi kwa watekelezaji wa PSSN.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF- Ladislaus Mwamanga amewataka watumishi wa Mfuko huo kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kufanya kazi ili mpango wa kunusuru kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi kuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na serikali.

Mwamanga ametoa kauli hiyo mkoani Mtwara wakati akifungua warsha elekezi ya siku mbili kwa maafisa ushauri,ufuatiliaji,wahasibu  na waratibu wa mikoa na wilaya ikiwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa mradi wa TASAF awamu ya tatu katika halmashauri 22 ambazo zimeanza utekelezaji wa mpango huo.



Halikadhalika Mwamanga amewataka kushirikiana,kuwa makini  na kutokiuka taratibu na matumizi ya fedha za mpango huo na kufuata miongozo sahihi ya kazi kwa sababu serikali imeona njia pekee ya kuwakomboa watu waliosahaulika ni kuwaingiza katika mpango.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati waliokaa) na wakurugenzi wengine wa TASAF Wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waratibu wa mikoa wa mamlaka ya eneo la utekelezaji wa halamashauri 22 baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili mjini Mtwara

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akifungua Warsha elekezi  ya siku mbili kwa maafisa ushauri na ufuatiliaji, waratibu wa mikoa, waratibu na wahasibu wa mamlaka ya eneo la utekelezaji wa halamashauri 22 nchini inayofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha SAUT Mjini Mtwara

 Mkurugenzi wa mpango wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akitoa maelezo juu ya mpango wa kuzinusuru kaya masikini na zilizo katika mazingira hatarishi katika warsha hiyo

 Washiriki wa warsha hiyo wakiwa wamenyoosha mikono juu kama ishara ya kukubaliana na jambo wakati Mkurugenzi mkuu wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo

 Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa makini uwasilishi wa moja kati ya mada ilyokuwa ikiwasilishwa. 

 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa makini uwasilishi wa moja kati ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, na wakurugenzi wengine toka TASAF Makao Makuu wakiwa kwenye picha ya pamoja  na waratibuwa  mamlaka ya eneo la utekelezaji wa Halamashauri 22 nchini (waliyosimama) Mjini Mtwara 

DCI MNGULU KUONGOZA TIMU YA WAPELELEZI KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WIZI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA MKOANI TABORA

$
0
0

 Na Allan Ntana wa Globu 
ya Jamii, Tabora 
MKUU wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Ernest Mangu ameteua timu ya askari polisi wataochunguza tuhuma za wizi wa fedha za wakulima wa zao la tumbaku katika vyama vya ushirika vya wakulima hao mkoani Tabora. 

 IGP Mangu amemteua Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu (pichani) ambaye ni Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai hapa nchini kuongoza timu. 
 Timu hiyo ya upelelezi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam tayari imewasili mkoani hapa kuanza kazi ya kuchunguza ubadhirifu huo unaofanyika katika vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku. 
 Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani hapa Kamishna Mngulu alisema timu imeundwa kutokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la tarehe 7/6/2014 alipokuwa ziarani mkoani hapa baada ya kuguswa na kilio cha wizi mkubwa wa fedha za wakulima wa tumbaku. 
 Mngulu alisema timu hiyo ni maalumu na imekuja mahsusi kwa ajili ya kuchunguza wizi wanaofanyiwa wakulima wa tumbaku kupitia vyama vya msingi mkoani hapa Alifafanua kuwa timu hiyo inaanza kazi mara moja kwa kuchunguza chama kimoja hadi kingine ili kubaini wizi na hujuma zote zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika ambazo zimekuwa kero kwa wakulima wa zao hilo katika mkoa wa Tabora. 
 ‘Natoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kutoa ushirikiano kwa timu hii mara watakapohitahika ili kuwezesha mafanikio ya kazi hii kwa wakati mwafaka, kazi hii ni ngumu lakini tutaifanikisha kwa ushirikiano wa wananchi na wadu wengine, aliongeza.

WADAU WA SHUGHULI ZA UZALISHAJI NA UTAFUTAJI GESI,MAFUTA WATOA MAONI RASIMU YA SERA YA PETROLI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( Wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha  ya pamoja na  Wadau wa  shughuli za   utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta  mara baada ya kufungua warsha hiyo. Picha na Asteria Muhozya.
 Mmoja wa wadau wa shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi akitoa maoni yake kuhusu namna ya kuboresha rasimu ya Sera ya Petroli. Wanaofuatia ni baadhi ya wadau kutoka  Kampuni mbalimbali zinazofanya shughuli hizo nchini.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) akifuatilia kwa karibu wadau wakitoa  maoni wakati wa warsha ya  wadau wanaoshughulika na   shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao  yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli. 

Wa Kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme Mhandisi Innocent Luoga, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi  Nishati, anayeshughulikia  Petroli  Mhandisi Stanley Marisa na wa kwanza kulia ni Mjiolojia Mwandamizi  Wizara ya Nishati na Madini,  Adam Zuberi.

 Washiriki katika warsha ya  wadau wanaoshughulika na   shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao  yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli

RAIS KIKWETE AWASILI DODOMA LEO

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete Akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM wa mkoa wa Dodoma MzeePancras Ndejembi  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo Juni 11, 2014.  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA NAIBU MABALOZI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Naibu Mabalozi wawili.Walioteuliwa ni Bw. Robert Kahendaguza (pichani kushoto) anayekuwa Naibu Balozi, Ubalozi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, na Bw. Msafiri Marwa (pichani chini) anayekuwa Naibu Balozi wa Tanzania London, Uingereza.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kahendaguza alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.

Uteuzi huu unaanza tarehe 25 Mei, 2014.

IMETOLEWA NA:

KATIBU MKUU

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,

DAR ES SALAAM

JUNI 11, 2014

GODOWN LINAUZWA BAHARI BEACH

$
0
0

Godown linauzwa bahari beach.Linauzwa kuna ofisi na nyumba ya kuishi two in one.
 mawasiliano barua pepe mwijo70jojo@yahoo.co.uk.Simu 0786666708.

Ngoma Africa Band watikisa mji wa Dortmund,Ujerumani

$
0
0
 Si wengine bali ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ukipenda waite viumbe wa ajabu "Anunnaki alien" au watoto wa mbwa, ambao walifanikiwa kutingisha jukwaa tena siku ya jumamosi 7 Juni 2014 mjini Dortmund,Ujerumani.katika onyesho la Challenge Festival liloandaliwa na umoja wa Wakameruni nchini Ujerumani. Wasikilize FFU Ughaibuni at www.ngoma-africa.com
 Kamanda Ras Makunja akiongoza mashambulizi
 Hapo ni supu ya mawe kwa kwenda mbele. Kamanda awapo jukwaani anacheka lakini hakuna masikhara kabisa katika gwaride
 Sehemu ya nyomi ya wadau katika onesho la FFU Ughaibuni
 Ras Makunja akikipa ishara kikosi chake wakati wa Sebene la nguvu


TANZANIA YAASWA KUJIFUNZA KUFUATIA KUKATAZWA MATUMIZI YA WINDOW 8 CHINA

$
0
0
Katika wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na China , Serikali ya Marekani inailaumu china kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni zake na biashara nyingine huku china nayo ikiilaumu marekani taarifa juu ya hili inaweza kusomeka "HAPA" .


Uchina baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo na hili linaweza kusomeka kwa kirefu na viambatanishi vingine "HAPA"


Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS China Operating System kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .


Kwan nchi za ulaya suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita , lakini umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya .


Kitu kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .



Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote .


Suala la serikali ya China lituamshe na tuanze harakati za kuangalia maslahi makubwa ya taifa wakati wa manunuzi na matumizi ya vifaa na program mbalimbali toka nchi za nje , program hizi na vifaa vyake vinaweza kutumika kwa urahisi kuhamisha taarifa na chochote kile au kufanya uhalifu bila mnunuzi au mtumiaji kujua .


Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni , ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .


Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani .

Huduma ya Push for Change yazinduliwa Tanzania

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Media Mobile, Freddie Manento akizingumza katika uzinduzi wa Kitengo cha Push For Change ambacho kinajihususisha zaidi na utoaji taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii.Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka.
 Miss Tanzania 1999 ambaye kwa sasa anafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (UN) kitengo cha mawasiliano akiwa na wageni wengine waalikwa katika uzinduzi wa Kitengo cha Push For Change ambacho kinajihususisha zaidi na utoaji taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii.Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka.
 Gonzaga Rugambwa (kushoto) wa Push for Change akitoa maelezo kwa baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa uzinduzi wa Kitengo cha Push For Change ambacho kinajihususisha zaidi na utoaji taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii.Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka.
 Mtaalam wa Mahesabu, Sam Awuku kutoka African Institute for Mathematical Science, akiteta jambo na Hoyce Temu wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Push For Change ambacho kinajihususisha zaidi na utoaji taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii.Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka.
Mmoja wa wageni waalikwa akijiunga na ya Push For Change
ambayo ina jihususisha zaidi na utoaji taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii.Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka.

=======  ======  =====
Kampuni ya Push Media Mobile Limited imeanzisha kitengo maalum cha kuhudumia taasisi za Kijamii kupata taarifa mbalimbali kijulikanacho kwa jina la Push for Change.

Kwa kupitia huduma hiyo, taaasisi za kijamii sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali kwa kupitia njia za mawasiliano na pamoja na simu za mkononi. Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka.

Mbali ya kupata taarifa na huduma, kwa kupitia programu ya Push For Change, taasisi za kijamii pia zinaweza kuunganishwa na washiriki wengine wa hapa hapa nchini na nje ya nchi kwa njia mbali mbali za mawasiliano pamoja na simu za mkononi.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na taasisi zaidi ya 62 zikiwemo za umoja wa mataifa,  Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile Limited, Freddie Manento alisema kuwa lengo la kuanzisha huduma hiyo ni kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii (non-profit organization) na kuyaunganisha na taasisi nyingine za aina hiyo duniani kupitia teknolojia ya kisasa.

Manento alisema kuwa sekta ya mawasiliano duniani imekuwa na inaendelea kupanuka na kuwafanya wao kubuni njia mbalimbali ambazo zintaweza kuunganisha jamii katika kupata taarifa kama za uchumi, biashara, afya, michezo na burudani, savei, elimu na kilimo, utaliii na nyinginezo.

“Mtandao wa simu ya mkononi umefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini na bara la Afrika, umerahisisha sana upatikanaji wa taarifa, tena kwa bei nafuu, takwimu zinaonyesha kuwa mpaka sasa kuna watumiaji simu za mkononi milioni 761 ambao wanaweza kupata taarifa katika mazingira mazuri na hata wanaoishi katika mazingira magumu, hivyo progamu hii itawafikia watu wengi zaidi na kwa haraka zaidi,” alisema Manento.

“Tumetumia teknolojia ya kisasa katika kufanikisha huduma hii kuiwezesha jamii kwa haraka zaidi kutokana na ushirikiano na wadau wetu mbali mbali katika huduma ya kijamii nchini na nje ya mipaka ya nchi, taarifa hizi zinaweza kupatikana kwa njia ya redio na televisheni mbali ya njia nyingine za mawasiliano,” aliongeza.

MIKONO SPEAKERS YAANDAA SEMINA MAALUM YA UONGOZI BORA

$
0
0
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy,Brian Tracy kutoka nchini Marekani,akizungumza jambo mapema leo asubuhi katika moja ya ukumbi wa Serena Hotel,jijini Dar kuhusiana na semina maalum ya uongozi bora ilioandaliwa na Mikono Speakers iliyomuhusisha nguli huyo wa masuala ya uongozi na kutoka nchini Marekani na Azim Jamal pichani kulia ambaye ni  mwanzilishi na Mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.Wa pili kutoka kulia  ni Wakurugenzi wa Mikono Speakers ambao ndio waandaji wa semina hiyo maalum ya Uongozi na kushoto ni  (Deogratius Kilawe na Themi Rwegasira.

====== ======  ======= 
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Mikono Speakers wanakuletea semina maalum ya Ufanisi bora katika Uongozi itakayoongozwa na Nguli wa masuala ya uongozi na maendeleo, Brian Tracy kutoka nchini Marekani na Azim Jamal kutoka nchini Canada. Semina hii maalum chini ya nguli hao wenye kuheshimika duniani ni fursa ya kipekee kwa wa-Tanzania kujifunza na kuboresha vipaji vyao vya uongozi katika biashara na taasisi zao mbalimbali. Semina hii ya siku moja itafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam tarehe 13 ya Mwezi Juni, 2014.


Akiongelea kuhusu umuhimu wa Semina hii kwa umma wa Tanzania, mkurugenzi mkuu wa Mikono Speakers, ndugu Deogratius Kilawe aligusia kuhusu kukosekana kwa wa-Tanzania katika eneo la juu, hususani katika nyanja ya uongozi. 

“Kama ukiangalia katika makampuni makubwa na taasisi mbalimbali hapa nchini, hasa maeneo ya uchimbaji madini, mawasiliano, huduma na taasisi za kifedha utaona kuwa ni wa-Tanzania wazawa wachache tu ndio wako katika ngazi za juu za uongozi. Ni asilimia nne tu, (4%) ya viongozi hao ni wazawa, na asilimia tisini na sita (96%) iliyobakia ni wageni.


Hali hii inabidi kubadilika kama kweli wa-Tanzania wanataka kuchukua hatamu ya uongozi na maendeleo yao,” alisema ndugu Kilawe. Semina hii inayoletwa na Mikono Speakers ni moja ya hatua na fursa za kuwafanya wa-Tanzania kuwa viongozi bora. Semina hii ambayo itaongozwa na nguli ambao wamefanya kazi na makampuni makubwa duniani, tuna imani itawawezesha wa-Tanzania kupata ujuzi wa kipekee katika kuboresha utendaji wao katika biashara, taasisi za umma na kijamii kwa ujumla,” aliongeza bwana Kilawe.


Semina hii inawalenga wale walio katika uongozi katika sekta binafsi, sekta za umma na taasisi za kijamii, kama makampuni ya umma, viongozi wa kiserikali, wabunge, wakufunzi na wote walio katika eneo la uongozi. Ni matarajio kwamba wadau mbalimbali kutoka makampuni makubwa, na makampuni ya kimataifa na taasisi ndogo na kubwa, wakiwamo na viongozi wakubwa wa kiserikali watahudhuria semina hii ya kipekee. Pia wananchi wote wanahimishwa kushiriki, haswa wale wenye kupenda kufahamu masuala ya uongozi.  


Semina hii inadhaminiwa na:


·         National Housing Corporation

·         The Citizen Newspaper

·         Dar Es Salaam Serena Hotel

·         Julius Nyerere International Convention Centre

·         Raha

·         Montage Ltd

·         Dephics Company Ltd

·         Rodizio Brazilian Grill

·         Dar City Promotions

·         Prime Advertising

·         Clouds FM

·         Man Magazine

·         Jamii Forums

·         Issa Michuzi Blog





Kuhusu waendesha Semina hii.


Brian Tracy

Brian Tracy ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy, kampuni inayayojihusisha na kutoa mafunzo kuendeleza watu na taasisi mbalimbali. Lengo la ndugu Tracy ni kuendeleza na kusaidia walengwa kufikia malengo binafsi na a kibiashara mapema zaidi.


Brian Tracy amesaidia zaidi ya makampuni 1000, na kuongea na watu zaidi ya milioni tano katika nchi arobaini (40) duniani. Ndugu Tracy amesoma, kufanya utafiti, na kuandika matoleo mbalimbali katika Nyanja za Uchumi, Biashara, Falsafa an Saikolojia. Ameandika zaidi ya vitabu 45 ambavyo vimetafsiriwa katika lugha mablimbali.


Azim Jamal


Azim Jamal ni mwazilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.


Ni mwandishi wa vitabu mbalimbali, vikiwamo “The Corporate Sufi”, “Business, Balance & Beyond” na pia ni mwandishi mwenza wa “The Power of Giving”. Ameshika nafasi ya kwanza katika mtadao wa Amazon wa mauzo ya vitabu mara mbili, 2005, na 2008, na pia ameshika nafasi hiyo katika kampuni ya Barnes & Noble. 

Barnes & Noble ni muungano wa maduka makubwa zaidi duniani, yakimiliki  maduka yapatao 3000. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha 10. Azim ana shahada tatu za mahesabu, na baada ya kufanya kazi na wakimbizi wa Afghanistan alibadilisha taaluma yake kutoka “mahesabu kwa biashara” kwenda “mahesabu kwa maisha” baada ya kuona maswaibu wayapatayo wakimbizi hao ambayo yalimgusa sana.

Ametoa ukufunzi kwa wamiliki wa makampuni ambayo ni ya thamani ya mabilioni ya dola. Wateja wake ni pamoja na “Fortune 500”, wanamichezo maarufu, na mengine mengi. Kwa kawaida katika mihadhara yake amekua akipata wastani wa alama 9+ chini ya kumi. 

Ujumbe wake wenye kuvutia, kutoa hamasa, na wakati mwingine wenye mtizamo tofauti umeonwa na zaidi ya hadhira ya watu milioni moja katika nchi 26. Ujumbe wake kupitia vyombo vya habari umesikiwa na watu wapatao milioni 5. Amezaliwa Tanzania na anaongea Kiswahili.  



Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images