Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 298 | 299 | (Page 300) | 301 | 302 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Bertha Mollel – Arusha.
  Shirikisho la kandada nchini Tanzania (TFF) limeingilia kati kuokoa mashindano ya vijana ukanda wa maziwa makuu ambayo yalikuwa hatihati kufanyika na sasa yataendeshwa kwa kushirikiana na waratibu wa mashindano hayo Rollingstone Sports academy ya mjini Arusha chini ya mwamvuli wa mtandao wa taasisi za za soka la vijana afrika mashariki na kati ECAYFA.

  Mashindano hayo ya wazi hufanyika kila mwaka mkoani Arusha mwaka huu yatafanyika jijini dar es salaam na kushirikisha timu za vijana za under 20 na under 14 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, ,Zanzibar, na jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC) na yatafanyika wiki ya kwanza ya mwezi julay.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi wa rollingstone football academy ally mtumwa masoud alisema mashindano hayo yalikuwa katika hatihati ya kufanyika au kutofanyika baada ya TFF kuchelewa kutoa kibali cha kuendesha mashindano hayo kwani taasisi hiyo iliandika barua ya kuomba kibali tangu mwezi wa pili lakini hawakupatiwa kibali kwa wakati.

  Mtumwa alisema kuwa kufuatia kuchelewa kwa kibali hicho walishindwa kufanya maandalizi ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta wafadhili na kualika timu hususani zile zinazotoka nje ya nchi  hali iliyosababisha kufikiria kuyasogeza mbele au kutofanyika kabisa kwa mashindano hayo.

  Hata hivyo baada ya kufuatilia TFF walikiri kupokea barua hiyo na kusema sababu zilizochangia kutofanyiwa kazi kwa barua hiyo ni piikapilika za TFF kuhama ofisi kupisha ukarabati wa ofisi za karume lakini kwa kujua umuhimu na ukubwa wa mashindano hayo waliamua yafanyike kwa ushiriano wa pamoja na Rolly store kwa sharti la mashindano kufanyika jijini dare s salaam ili waweze kushuhudia.

  Hii itakuwa mara ya pili kwa mashindano hayo ya 14 kufanyika nje ya Arusha kwani mwaka 2012 yalifanyika nchini Burundi na utakuwa mwanzo wa mashindano hayo kuzunguka katika mikoa na nchi mbalimbali ambazo zitakuwa tayari kuandaa na kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuhudumia malazi na chakula kwa timu zinazotoka nje ya nchi.

  TFF, rollingstone na ECAYFA wameunda kamati ya maadalizi itakayokuwa chini ya uratibu wa afisa uhusiano na mawasiliano wa rollingstone Wilbrode Alfonce na tayari nchi wanachama wa CAYFA na taasisi za sika nchini Tanzania zimeshatumiwa barua za mialiko huku baadhi ya nchi kama burundi ,Kenya na DRC zikionyesha nia ya kushiriki.

  0 0
 • 06/13/14--08:07: PUKU YAJA NYUMBANI RASMI


 • Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU,Bwa.Meck Mbwana akizungumza kuhusiana na bidhaa hiyo,mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar.
  Pichani wa pili kulia ni Mwanamitindo Millen Magese ambaye ni balozi wa bidhaa ya PUKU akiwa na waanzilishi wa bidhaa hiyo ya PUKU mara baada kuzungumza na Wanahabari jijini Dar leo

  ===============

  WATUMIAJI wa simu za kisasa za Smart Phone wametakiwa kutumia chaji za Puku kuchajia simu zao ili kujihakikishia usalama wake.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa chaji hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU alisema kuwa chaji hizo kwa sasa zinapatikana hapa nchini.


  Alisema kuwa ni chaji ambazo zinahifadhi umeme kwa muda mrefu ambao unakuja kutumiwa kuchajia simu hasa pale ambapo panakuwa hakuna umeme. Aliongeza kuwa bei yake kwa sasa ni kuanzia 160,000 kutokana na ubora wake na pamoja na namna ambavyo inasaidia.

  "Mimi ni mtanzania kutoka Tanga na nilisoma hapa hapa ila nilielekea Marekani kusoma na ninaishi huko na nimebuni hii chaji kwa lengo la kusaidia watu mbalimbali ambao wanakuwa wakisumbuliwa na tatizo la kuchajia simu zao pale ambapo panakuwa hakuna umeme wa uhakika"alisema Meck Mbwana ambaye ni mvumbuzi na mkurugenzi mtendaji wa PUKU.


  Aliongeza kuwa " kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za smart phone huku watumiaji wakilalama kuwa wanakosa uhakika wa umeme wa kuzihudumia sasa hii bidhaa itasaidia".


  Aliongeza kuwa kwa sasa zinapatikana hapa nchini na aliwataja wahusika wakubwa kuwa ni pamoja na Ed Kavishe-mshirika mwenza, Joseph sikare – Rais Tanzania huku Mwanamitindo Millen Magese akiwa ni mshirika mwenza na balozi wao.  Kwa upande wake Millen aliwataka wananchi kutumia bidhaa hiyo kwa kuwa mbali na kuwa ni ubora bali pia ni bidhaa ya watanzania wenyewe.

  Tayari PUKU wameshajikita na uchangiaji wa huduma kwa jamii ambapo asilimia kadhaa ya mauzo itaelekezwa kwenye kampeni ya uelewa wa hali ya endometriosis na ujenzi wa hospital kwa ajili ya magonjwa yanayowasumbua akina mama. 

  Mbali na udhamini wa kampeni ya endometriosis PUKU watachangia ujenzi wa madarasa mawili yaliyoko chini ya mradi wa Millen Magese Foundation yanayojengwa huko Mtwara ambapo mpaka sasa madarasa matatu yameshakamilika.

  0 0

   Mtaalam wa kutoa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami (kushoto) akimtoa damu Meneja Mwandamizi Tawi la Samora la Benki ya Exim Nancy Huggins, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Duniani inayofanyika kila mwaka ifikapo Juni 14
   Mtaalam wa kutoa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami (kushoto) akimtoa damu Afisa wa Benki ya Exim Daniel Lukuba, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Duniani inayofanyika kila mwaka ifikapo Juni 14.
   Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakichangia damu wakati wa kampeni ya Benki hiyo ya kuchangia Damu ili kuokoa maisha ya kina mama, inayofanyika kila mwaka katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Duniani inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Juni 14. 
   Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Bi Anita Goshashy (Kushoto) akichukuliwa vipimo kabla ya kuchangia damu. Benki hiyo inaendesha kampeni ya kuchangia damu kila mwaka katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Duniani inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Juni 14. 
   Mtaalam wa kutoa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami (kushoto) akimtoa damu mmoja kati ya wafanyakazi wa Benki ya Exim, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Duniani inayofanyika kila mwaka ifikapo Juni 14.
  Wafanyakazi wa Benki ya Exim katika picha ya pamoja wakati wa kampeni ya uchangiaji damu inayofanywa na Benki hiyo kila mwaka ili kuadhimisha Siku ya Uchangiaji Damu Duniani inayofanyika kila ifikapo Juni 14

  0 0

  TANZANIAONE3

  Chairman, Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Ami Mpungwe (Photo by Library).

  0 0


  13/06…Regional retailer, Nakumatt Holdings, has kicked off a clearance sale campaign in Dar es salaam Tanzania, as it prepares to formally assume business at the former Shoprite locations in the country.

  The 50% Sale at Nakumatt Mlimani City, flagship store located at Mlimani Mall in Dar es Salaam, today attracted an overwhelming crowd of shoppers hoping to catch a bargain.

  According to Nakumatt Holdings, Managing Director, Mr. Atul Shah, the clearance sale shopping bonanza will be undertaken throughout this weekend to facilitate a stock clearance process.

  “Nakumatt has sealed an assets buyout agreement with Shoprite and we are undertaking this immensely popular sale to clear current stock holds ahead of a rebrand and reopening of the three stores,” Shah explained.

  “Through this sale, we are also evaluating the variety and demand for some of the items to ensure that we optimize the stockholding based on customer demands here in Tanzania,”

  At the end of this week, Shah further confirmed that Nakumatt will be briefly closing down the three stores to facilitate stores refurbishment process.

  The process expected to last a month will thereafter facilitate the reopening of the three stores under the Nakumatt banner and management, which will give an opportunity for all customers to experience the renowned Nakumatt courtesy.

  In Tanzania, Nakumatt operates a single store in Moshi and will be effectively raising its branch network to 49 up from the current 46 across East Africa.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  OFISI YA RAIS,

  MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA


  RATIBA YA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM, TAREHE 16 JUNI 2014


  MUDA

  TUKIO

  MHUSIKA

  02.00-03.30

  Burudani

  MC

  03.30-04.00

  Waalikwa Kuingia Uwanjani

  MC/Wageni Waalikwa

  04.00-04.15

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kuingia Uwanjani

  MC/ Kamati ya Mapokezi

  04.15-04.30

  Mgeni Rasmi Mhe. Waziri wa Nchi, OR MUU Celina O. Kombani (Mb) kuwasili

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

  04.30-05.15

  Mgeni Rasmi Kupokea Maandamano

  MC

  05.15-05.30

  Burudani

  MC

  05.30-05.35

  Kumkaribisha Mgeni Rasmi Mhe. Waziri wa Nchi, OR MUU Celina O. Kombani (Mb).

  MC/Katibu Mkuu Utumishi

  05.35-06.00

  Mgeni Rasmi Kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2014

  MC/ Mhe. Waziri wa Nchi, OR MUU Celina O. Kombani (Mb).

  06.00-06.05

  Kutoa Neno la shukrani kwa Mgeni rasmi

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

  06.05-06.20

  Burudani

  MC/Kikundi cha Ngoma

  06.20 na kuendelea

  Mgeni rasmi kutembelea mabanda ya Maonesho

  MC/ Katibu Mkuu Utumishi

  06.20 -06.50

  Burudani

  MC/Kikundi
  0 0

   Mwenyekiti wa kamati ya kituo cha afya Mlandizi, bw Makamba Mwaluka (watatu kushoto), akiwakaribisha wageni kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kufanya ziara katika wodi ya akina mama na watoto Kituo cha Afya Wilayani Mlandizi. Juni 12,2014 na kukabidhi mashuka kwenye kituo hicho (kulia kwake), Muendeshaji shughuli mama Gaudensia Ndegea (katikati kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Michael John, na Mjumbe wa bodi NHIF, bwana Charlse Kajege.  
   Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamoto (kulia), akiwakaribisha wageni aliyoambatana nao kutoka katika mfuko huo(wakwanza kulia), Mjumbe wa bodi NHIF, Charlse Kajege, Mjumbe wa bodi wa NHIF Dr. Hashim Mohamed, Diwani wa Mlandizi  mama Ndessi, Mkurugenzi wa Matibabu na Huduma za kiufundi  Dr. Frank Lekey
   Mjumbe wa bodi wa NHIF Dr. Hashim Mohamed(kushoto), akikabidhi mashuka kwa mgeni rasmi, diwani wa Mlandizi  mama Ndessi baada ya kufanya ziara katika katika wodi ya akina mama na watoto Kituo cha Afya Wilayani Mlandizi na kukabidhi mashuka kwenye kituo hicho.
   Mjumbe wa bodi aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa bodi ya NHIF Dr. Hashim Mohamed (katikati), akisisitiza jambo mara baada ya kumaliza ziara hiyo wilayani Mlandizi.
   Wajumbe wa bodi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ndugu Charlse Kajege na Dr. Mohamed Hashim wakiwa na diwani wa Mlandizi Mama Dessi       wakitandika moja ya mashuka yaliyotolewa na NHIF.katika wodi ya akina mama na watoto Kituo cha Afya Wilayani Mlandizi.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti,Raphael Mwamoto(kushoto), akimtambulisha Mkurugenzi wa huduma za utabibu na ufundi  Dr. Frank Lekey ambaye waliambatana katika ziara hiyo wilayani mlandizi.


  0 0

  Hapa ndipo mwili wa Marehemu George Tyson ulipozikwa mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.George Tyson ambaye alikuwa ni mmoja wa Waongozaji filamu mahiri hapa nchini Tanzania,alifarika kwa ajali ya gari wakati akitokea mkoani Dodoma kikazi akirejea jijini Dar.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.Amin.
  Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
  Ndugu na jamaa mbalimbali wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu George Tysombani kwako,katika kijiji cha Siaya nchini Kenya.
  Baadhi ya Ndgu na Jamaa mbalimbali wakiwa kwenye maombolezo ya mwisho ya mazishi ya marehemu George Tyson mapema leo mchana,nyumbani kwao
  Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
  Mdau Felix akizungumza jambo na kuwashukuru Watanzania wote na wengineo walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kuhakikisha mpendwa wao,ambaye Mwenyezi Mungu kampenda zaida anaenda kuishi kwenye nyumba yake ya milele.
  Watoto wa marehemu George Tyson wakiwa katika picha ya pamoja.
  Nyumba ya milele ya marehemu George Tyson kabla ya kulazwa.Picha kwa hisani kubwa ya Mdau William Mtitu kutoka kijiji cha Siaya,nchini Kenya.

  0 0

  1a
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akifungua semina ya wenyeviti, Makatibu na Makatibu Wenezi wa CCM wilaya ya Ludewa3aMwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndugu Stanley Kolimba akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai ili kufungua rasmi semina hiyo ya kimafunzo kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa. 6a
  Matson Chizii Mkurugenzi wa Uchaguzi Mstaafu CCM kulia akinyanya mkono juu wakati washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo maalum wa CCM 16a

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali wakati wa Tamasha la Uzalendo na uzinduzi wa Video ya Wimbo Maalum wa Mika 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazoendelea hivi sasa katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jioni hii. Picha na Freddy Maro
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendi na uzinduzi wa Video ya wimbo Maalum wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini dodoma leo jioni.

  0 0

  DSC_0002
  Jukwaa litakalotumika kwa masuala ya burudani kuanzia leo Juni 14 hadi 22 ndani ya Ngome Kongwe katika ukumbi wa Mambo Club linavyoonekana muda huu kwenye hatua ya mwisho kuelekea ufunguzi rasmi saa moja jioni.(Picha na Zainul Mzige modewjiblog)
  Opening Night: Mandela: Long Walk to Freedom
  June 14th 20:20 Old Fort Ampitheatre
  Opening Night Concert:
  June 14th Mambo Club
  Tamaduni Music (Tanzania) followed by BODY, MIND & SOUL (Malawi)
  DSC_0003
  Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Andrew Chale akiwa kwenye ukumbi wa Mambo Club - Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. Kulia ni baadhi ya raia wa kigeni wakivinjari kwenye viunga hivyo.
  DSC_0009
  Sehemu maalum itakayokuwa ikitoa huduma wa chakula na vinywaji.
  DSC_0022
  Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (mwenye t-shirt ya blue) akiongoza baadhi ya wasanii kuelekea jukwaani kwa ajili ya mkutano mfupi na waandishi wa habari waliowasili mchana huu.
  DSC_0034
  Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa “Has T” akiwatambulisha wasanii watakaotoa burudani leo kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za Majahazi ZIFF kwenye mkutano mfupi na waandishi wa habari (hawapo pichani).
  DSC_0042
  DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto Rico(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna atakavyosugua sahani za muziki usiku wa leo. Wengine ni wanamuziki wa kundi la BODY, MIND & SOUL kutoka Malawi.
  DSC_0075
  Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwatambulisha wasanii watakaotoa burudani kwenye ufunguzi wa tamasha hilo.
  DSC_0044
  Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa “Has T”, Andrew Chale kutoka Tanzania Daima, Festo Polea kutoka Mtanzania pamoja na Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala wasikiliza vionjo kutoka kwa wasanii wakati wa utambulisho.
  DSC_0092
  Picha ya pamoja na Ma-DJ's na wasanii watakaotoa burudani leo kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014.

  0 0

  MAKAMU  Mwenyekiti wa Umoja  wa Makanisa ambaye pia ni Katibu wa PCT  jijini Mwanza, Askofu Zenobius Isaya, anatarajia kuwaongoza Maaskofu na Wachungaji mbalimbali katika ufunguzi wa duka la Msama Promotions jijini Mwanza litakalofunguliwa Juni 17.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama Maaskofu hao sambamba na wachungaji wataweka wakfu kwa dua maalum itakayoongozwa na kiongozi huyo wa juu wa kiroho jijini humo.

  Msama amesema shughuli za kuweka wakfu duka hilo linasindikizwa na shangwe na furaha kutoka kwa wadau mbalimbali jijini humo ambao watashiriki katika ufunguzi huo.

  Aidha, Msama alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha ufunguzi wa duka hilo ambalo ni mkombozi wa wizi wa kazi za sanaa, hasa nyimbo za Injili Tanzania.

  “Kwa kuwa nawajali wananchi, naomba wajitokeze kwa wingi kujipatia kazi halisi na kuondokana na wizi wanaofanyiwa na wachache wasioitakia mema tasnia ya sanaa hapa nchini,” amesema Msama.

  Aliongeza kuwa huo ni mwanzo wa maendeleo ya kudhibiti kazi za sanaa, baada ya Mwanza anatarajia kupanua wigo kwa kufungua maduka katika mikoa mingine.

  0 0


  Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Iraq Hudu 'Mkumwena' wakipeleka mwili kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam kwa ajili ya kumuhifadhi.
  Baadhi ya waombelezaji wakitia udongo katika kaburi la marehemu Iraq Hudu wakati wa maziko yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam .
  Mashekhe wakisoma duwa kabla ya kwenda kuzika
  Baadhi ya waombelezaji na mabondia wakiwa nyumbani kwa marehemu Iraq Hudu kutoka kushoto ni bondia Adwer George, Rashidi Matumla, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yasini Abdallah na Mwenyekiti wa Shiwata Cassim Twalibu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
  Meneja wa bendi ya msondo ngoma Said Kibiriti akisalimiana na mabondia
  Baadhi ya waombelezaji waliojitokeza
  Mtangazaji Maulid Baraka Kitenge akizungumza na mabondia mbalimbali wakati wa msiba wa bondia Iraq Hudu.

  Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Maulid Baraka Kitenge akisalimiana na bondia mkongwe ambaye kwa sasa ni kocha wa MKoa wa Tanga katika wilaya ya Muheza Chales Muhilu 'Spins'
  Bondia Marehemu Iraq Hudu 'Kimbunga' kulia enzi za uhai wake katikati ni marehemu bondia Papa Upanga
  Bondia Iraq Hudu' Kimbunga kulia akipambana na Stanley Mabesi katika mpambano wao
  IRAQ HUDU
  WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
  WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
  Mmoja wa waombelezaji kulia akimpa pole bondia Chuku Duso katika msiba wa bondia Iraq Hudu
  Ibrahimu Kamwe na Said Chaku
  wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi
  WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU


  WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KWENYE KABURI LA MAREHEMU IRAQ HUDU
  WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU
  WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

   

  1w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akifunga rasmi mafunzo ya kikazi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya 2010 na masuala ya Itikadi kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa wakiwemo Wenyeviti, Makatibu na Makatibu wenezi wa wilaya hiyo yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es salaam kwenye hoteli ya JB. Belmont, yakindaliwa na Mbunge Makini na Machachari wa jmbo la Ludewa Mh. Deo Filikunjombe, Viongozi hao wa CCM wilaya ya Ludewa walianza na ziara ya kikazi iliyoanzia Bungeni Mjini Dodoma, Chuo Kikuuu cha UDM na Makao makuu ya CCM mjini humo ambapo walikutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula na kuzungumza naye akiwapa nasaha nyingi kuhusu maadili ya uongozi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)2w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha kuhudhuria semina hiyo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Ndugu Stanley Kolimba.3w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo hayo Eliud Shemauya Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa.4w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo hayoHonolatus Pilimini Mgaya Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa.5w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo hayo Rosemary Lwiva Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe.6w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akikabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo hayoviongozi mbalimbali wa kata CCM wilaya ya Ludewa.7w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo hayoviongozi mbalimbali wa kata CCM wilaya ya Ludewa.8w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh. Deo Filikunjombe ambaye ndiye aliyeandaa ziara hiyo na semina ya kimafunzo kwa viongozi mbalimbali wa kata CCM wilaya ya Ludewa. 


  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akipiga picha na viongozi mbalimbali wa kata CCM wilaya ya Ludewa mara baada ya kufunga mafunzo hayo11w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akimsikiliza Mh. Deo Filikunjombe wakati alipokuwa akimueleza jambo mara baada ya kupiga picha.15w
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akisalimiana na Rosemary Lwiva Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe mara baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika, katikati ni Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh. Deo Filikunjombe.16w
  Mbunge wa jimbo la Ludewa akizungumza na viongozi hao wa Chama cha Mapinduzi kutoka Wilaya ya Ludewa ambao aliwaandalia ziara ya kimafunzo ya kikazi na kiitikadi ndani ya Chama kabla ya kufungwa kwa semina hiyo leo.

  0 0

  DSC_0213
  Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisoma hotuba wakati akizindua rasmi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za Majahazi (ZIFF) linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.
  DSC_0344
  Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimtambulisha mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (kulia) kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi.
  DSC_0348
  Mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed akikambidhi zawadi ya kifurushi cha Internet ya mwaka mzima mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi .
  DSC_0157
  Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya wageni alipowasili kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la ZIFF Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mahmoud Thabit Kombo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
  DSC_0159
  Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto ambayo ilifungua tamasha hilo la 17 la ZIFF usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar.
  DSC_0158
  Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby wakati wa tamasha hilo.
  DSC_0164
  Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.


  DSC_0174
  DSC_0386
  Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akimkaribisha mgeni Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwenye jukwaa.
  DSC_0391
  Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto akielekea jukwaani wakati wa ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF 2014.
  DSC_0395
  Picha juu na chini Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto, akizungumzia changamoto mbalimbali na mafanikio aliyoyapata baada ya kushiriki kwenye filamu hiyo.
  DSC_0409
  DSC_0414
  Mmoja wa wageni waalikwa akimpongeza mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwa kazi nzuri aliyofanya kupitia filamu yake.
  DSC_0351
  Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akimshukuru mwakilishi wa Com-net mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo kwa zawadi hiyo.
  DSC_0332
  Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby akizungumzia udhamini wao wa miaka 10 kwenye tamasha hilo ambapo kwa sasa lina mwaka wa tatu.
  DSC_0490
  Meza kuu ikifuatilia filamu ya "Long Walk to Freedom" inayozungumzia maisha ya MANDELA wakati wa ukombozi wa mtu mweusi kutoka kwa makaburu.
  DSC_0375
  Mwigizaji Terry Pheto akifurahia jambo wakati wa kutazama filamu yake.
  DSC_0342
  Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
  DSC_0370
  Picha juu na chini wakazi wa Zanzibar na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wakitazama filamu ya "Long Walk to Freedom kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF.
  DSC_0317
  DSC_0316
  DSC_0431
  Mwigizaji Terry Pheto akipozi na mmoja wa ushers waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye tamasha hilo.
  DSC_0574
  Mdau Lucy (wa pili kushoto) katika pozi na picha yake kwenye viunga vya Ngome Kongwe wakitoa huduma ya vinywaji.

  0 0

   Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Helkopta kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  (hayupo pichani) kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu.Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Idd Mfunda (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helkopta Charter (EA) Ltd Bw. Peter Achammer wakitiliana saini katika hati za makabidhiano ya Helkopta moja iliyotolewa kama msaada na Taasisi ya Howard G. Buffet Foundation ya nchini Marekani.Wanaoshuhudia zoezi hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (aliyesimama kushoto) na Balozi wa Marekani hapa nchini Mark Childress

   Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akionyesha ufunguo wa Helkopta mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helcopter Charter (EA), Peter Achammer kwa niaba ya Mfuko wa Howard G. Buffet ambapo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za mmiliki wa Mfuko huo alizozitoka kwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara katika Mbuga za wanyama hapa nchini hivi karibuni.Wa pili kulia ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress naWaziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa .

   Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amepanda Helkopta ambayo alikabidhiwa kama msaada kutoka Mfuko wa Howard G. Buffet kwa ajili ya kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na ujangili.

  Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiteta jambo na  Wawakilishi wa Bunge .katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Helkopta kwa ajili kupambana na ujangili nchini Mh. James Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Maliasili na Mazingira (katikati) na Mhe. Mch. Peter Msigwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

   Meneja Mipango na Mikakati wa Howard G. Buffet Foundation Tanzania Chapter Bi. Ellen Mutalemwa akitoa rai wakati wa hafla ya kukabidhi Helkopta moja ambayo ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Mfuko huo alipomtembelea Rais Kikwete hivi karibuni. Helkopta hiyo imetolewa ili kusaidi juhudi za Serikali katika kupambana na ujangali katika hifadhi za Taifa.

  0 0

   Baadhi ya Wana Njia Panda wakifanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Amana jana jijini Dar es Salaam.  
   : Mmoja wa Wana Njia Panda Andrew Kwingwa kwa kushirikiana na Mfanaya usafi wa kampuni ya Care Sanitation yenye jukumu la kufanya usafi katika Hospitali ya Amana, Bi. Anna Mkonda wakimwaka takataka katika jaa la kuhifadhi taka la Hospitali ya Aman kabla ya kupelekwa Dampo.

   : :Mwakilishi wa Kampuni ya Grace Products watengenezaji wa Vipodozi na bidhaa za usafi kwa kutumia mimea asili Bi. Happiness Tibaijuka akikabidhi msaada wa kwa u Afisa Afya wa Hospitali hiyo Bw. Ally Kasembe (kushoto).Grace Product wametoa msaada wa Sabuni za kuogea, mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto, sabuni za kusafishia choo, pamoja na Lotion.

  Wana Njia Panda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaa jana. Picha na Frank Shija, WHVM.
   Mtangazaji wa Kipindi cha Redio cha Njia Panda kinachorushwa na Clouds FM Dkt. Isack Maro akizungumza na mwandishi wa habari wa Zanznbar Media Bi. Sophia Kingimali wakatika wa zoezi la usafi katika Hospilali ya Amana iliyopo Ilala, jana jijini Dar es Salaam. Wananjiapanda wamejitolea kufanya shughuli za usafi katika Hospitali hiyo ikiwa ni kutoa mchango wao kwa jamii inayowazunguka.

   Afisa Afya wa Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam Ally Kasembe akizungumza na mwandishi wa habari wa Zanznbar Media Bi. Sophia Kingimali wakatika wa zoezi la usafi katika Hospilali hiyo ambapo Wasikilizaji na wapenzi wa Kipindi cha Redio cha Njia Panda kinachorushwa hewani na Clouds FM walifika Hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya usafi wa mazingira yanayoizunguka Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.

   Mwakilishi wa Kampuni ya Grace Products watengenezaji wa Vipodozi na bidhaa za usafi kwa kutumia mimea asili Bi. Happiness Tibaijuka akifafanu jambo kw mwambdishi wa habari Bi. Sophia Kingimali wakati wa zoezi la usafi wa Mazingira katika Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokewa na wenyeji wake wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia.
   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa Bolivia, Evo Morales, walipokutana kabla ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, jana Juni 14, 2014. Katikati ni Mkalimani wa Rais wa Bolivia. 

  Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meya wa Jiji la Santa Cruz,  Percy Fernandez, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Kushoto ni Mama Zakhia Bilal.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Bolivia, Evo Morales, baada ya mazungumzo yao yalioyofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, jana Juni 14, 2014.


  Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Mwenyeji wake Rais Evo Morales, Rais wa Bolivia baada ya kufanya mazungumzo saa chache kabla ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia. 

  Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania ni inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo. Picha na OMR

  0 0

   Division Manager of the French Development Agency Mr. Jean-Luc Francois (left) and Project Manager of Biodiversity Agriculture and Rural Development of the French Development Agency Ms. Karen Collin de Verdiere speaking to Tanzanian delegation recently in Paris.
   Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (MP) (right) and the Tanzanian Ambassador to France H.E. Mrs. Begum Taj listening to officials from the French Development Agency recently in Paris.
  Discussions going on between the Tanzanian delegation led by the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (MP) and officials from the French Development Agency recently in Paris.  Photos  by Pascal Shelutete.

  ==========  ========
  French Development Agency is considering providing a reasonably financial support that will help biodiversity protection in the country’s protected areas.

   The Division Manager of AFD Mr. Jean-Luc Francois said this when he met with the Tanzanian delegation in France led by the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (MP) in Paris. 

  Jean-Luc said that they have already spent 260 Million Euros in the country in the areas of water and sanitation as well as energy projects and they are now looking in to expanding their financial support in biodiversity conservation. 

  He said that promoting conservation is among their main objectives whereby they are supposed to make sure that they protect, restore and manage ecosystems and share the benefits of the protected areas with the local communities around protected areas. 

  On his part, Hon. Lazaro Nyalandu (MP) urged AFD to consider supporting the conservation sector and pointed out areas such as the Ruaha-Rungwa ecosystem as among the priority areas for support on biodiversity conservation. 

  He said financial support from AFD is highly needed now than ever because of the poaching crisis, which is now a global agenda for conservationists, and that strengthening of partnerships between France and Tanzania would also support to encounter the crisis. 

  Currently, AFD has provided grant worth 0.8 Million Euros to a FISONG Project in Manyara region which is being implemented by a French NGO (IGF  Foundation) in collaboration with Babati District Game Office; Burunge Wildlife Management Area. The project has an overall goal of Sustaining Wildlife Movements in Northern Tanzania particularly the two corridors of Tarangire-Manyara and Tarangire-Simanjiro.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Kimara Baruti kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mbele ya ofisi za TRA Kimara Baruti ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa tatizo kuwabwa la foleni linadhoofisha uchumi hivyo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi mara moja,pia alisema atazungumza na viongozi wa ngazi za juu wa CCM kuwapa kipaumbele wakazi wa Ubungo na Kawe waweze kupata maji mwanzoni katika miradi ya maji inayokuja.
   Baadhi ya Wana CCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti.
   Baadhi ya Wana CCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye alipohutubia wakazi wa Kimara Baruti leo.
   Hamida Issa Selemani akielezea umati wa wakazi wa Kimara uamuzi wake wa kujiunga na CCM baada ya kuchoshwa na siasa chafu za chama cha  CUF.Hamida alishakuwa Diwani na Kaimu Katibu wa CUF Wilaya ya Biharamulo na mgombea Ubunge wa CUF jimbo la Biharamulo Magharibi
   Rashid Idd aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Biharamulo akimpa mkono Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye baada ya kutangaza kujiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti.
    Rashid Idd aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Biharamulo pamoja na Hamida Issa Selemani na wanachama wengine zaidi ya 420 wakila kiapo cha kuwa wanachama watiifu wa CCM Jumuiya ya Wazazi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiondoka eneo la mkutano akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiagana na wakazi wa Kimara Baruti mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara .
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akicheza bao na Bi Agustina Batromeo mara baada ya kuzindua shina namba 770 la wacheza bao Kimara Baruti.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipandisha Bendera ya Chama baada ya kufungua shina la wakereketwa wa CCM Gereji Butcher. Zaidi ya mashina manne ya Jumuiya ya Wazazi CCM yamefunguliwa leo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi katika kata ya Kimara.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipokelewa kishujaa baada ya kuwasili eneo la mkutano Kimara Baruti,mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kimara ,wilaya ya Kinondoni.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwapungia wananchi mkono wakati akiwasili eneo la mkutano kwenye viwanja vya mbele ya ofisi za TRA kimara Baruti.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipiga Gitaa kabala ya kupanda jukwaani kuhutubia wakazi wa Kimara Baruti.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Ramadhani Madabida kabla ya kupanda jukwaani na kuhutubia wakazi wa Kimara Baruti. (Picha na Adam Mzee)

older | 1 | .... | 298 | 299 | (Page 300) | 301 | 302 | .... | 1898 | newer