Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA MKOANI DODOMA.

$
0
0
 Wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waki kagua moja ya Mradi  uanao tekelezwa na ( CDA) Miradi hii nikatika   mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).
 Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu Dkt : Florens M Turuka  wa (katikati)  akitoa  maelekezo kwa Wakurugenzi wa OWM walipo tembelea eneo la mradi wa Makaburi ya Viongozi  katika eneo la  Mlimani .
Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa  (CDA) Bw: Pascal Muragiri  akitoa maelezo ya mradi wa Barabara unaotekelezwa na CDA kwa msaada  wa  Benki  ya Dunia   wanao wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu OWM Mkoani Dodoma
======  ====== =====
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA  TAASISI ZILIZO CHINNI YA OFISI YA WAZIRI MKUU MKOANI DODODMA LEO 12  Mai 2014
 
(Na  Mwandishi Ofisi ya Waziri Mkuu)
Uongozi wa ngazi ya juu wa Ofisi ya Maziri Mkuu watembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo inayo simamaiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Dkt: Florens M. Turuka  amesema lengo la kutembelea miradi ni kujionea mwenywe yeye na Wakurugenzi na wakuu wa Taasisi ili kuweza kujiridhisha na mana ya uwendelezaji wa Miradi hiyo inayao simamiwa na Serikali.
 
Miongoni mwa miradi iliyo tenmbelewa ni  Mradi wa Makaburi ya viongozi  ambapo mradi huu uko katiaka hatua za Mwisho za kukamilisha kuwalipa fidia wakazi wa eneo husiaka ili kupisha mradi huo uendelee .
 
Aidha pamoja na mradi wa makaburi pia waliweza kutembelea miradi ya upimaji viwanja vya makazi  na eneo la uwekezaji katiaka eneo la Njedengwa  njekidogo ya Manispaa ya Dododm unao tekelezwa na Mamlaka ya Uastawishaji Makao Makuu Dododma (CDA)
 
Naye kaimu Mkurugengenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji  Makao Mkuu Dododma (CDA) Bw: Pascal  Murugiri  amesema mradi wa Njedengwa  umegarimu jumla ya ya kiasi cha Shilingi Bilioni 15 ikiwa kama mkopo kutoka benki hivyo nifursa sasa kwa wananchi  kuja (CDA) na kujipatia viwanja amabavyo viko tayari vikiwa na  huduma zote za msingi kama Barabara za lami Umeme na Maji.

RUCO MABINGWA WA POOL VYUO VIKUU WAPONGEZWA

$
0
0
Nahodha wa timu ya Pool ya chuo kikuu cha Ruco , Said Mohamed akimkabidhi mgeni rasmi kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi kikombe cha ubingwa wa mchezo huo baada kuandaliwa hafla ya kuwakaribisha iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hill  juzi kushoto ni meneja mauzo wa tbl mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma Raymond Degera.

Na Denis Mlowe,iringa

WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCO) cha mkoani Iringa nchini wameshauriwa kuundeleza mchezo wa Pool sambamba na kufanya vema katika masomo yao na kuwapongeza kwa kuuletea sifa mkoa wa Iringa katika mchezo huo kwa vyuo vikuu.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, ACP Ramadhani Mungi katika hafla ya kuwapongeza  mabingwa wa mchezo huo kitaifa katika ngazi ya vyuo vikuu uliondaliwa na kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha safari Lager na chuo cha RUCO kuchukua ubingwa kwa mara ya kwanza iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hill.

Mungi alisema wanafunzi wengi wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na kubanwa na mambo ya burudani na michezo na kuwapongeza vijana hao kuwa na ratiba nzuri ya masomo na michezo hadi kufanikiwa kuchukua ubingwa wa vyuo vikuu kitaifa.

“Naupongeza sana uongozi wa chuo cha ruco kwa kuweka ratiba nzuri ya vipindi na michezo, utaratibu wa kujua ni wakati gani wa kusoma, wakati gani wa kufanya mazoezi hivyo bila uongozi wa chuo hicho msingefikia hapo na ndio chanzo hadi nyie kuchukua ubingwa huu na kuuletea sifa mkoa wa Iringa nawapongeza uongozi wa chuo cha ruco na vijana wangu” alisema Mungi

Alisema kuwa mchezo wa pool unazidi kukua kwa kasi kubwa nchini na lakini viongozi wake wanatakiwa kuwa makini na vijana wanaoweza kuharibu sifa ya mchezo huo hasa kwa vijana wanaofanya pool kama kijiwe cha kuvutia bangi.

Aliongeza asilimia kubwa ya vijana wanajiajiri kwa kuppitia michezo hivyo juhudi kubwa inatakiwa kuwekwa kuweza kuwawezesha vijana kuingia katika sekta ya michezo kwa kuwa ni ajira tosha katika maisha ya sasa.

Mungi alisema kupitia michezo hata uhalifu huwa unapungua kwa kuwa wengi wamekuwa wakijishughulisha hasa katika tasnia ya burudani kwa kuwa  hata wao wanapenda kujishughulisha katika michezo.

“Katika burudani uhalifu huo unapungua kwani wahalifu nao wanapenda kuburudika kwa hiyo tujitahidi sana kushughulikia michezo na burudani kuweza kupunguza uhalifu, mfano mmoja ni kuwa kuna tamasha kubwa liliwahi kufanyika hapa mkoani iringa katika kuripoti matukio siku ya pili kwa kweli polisi kulikuwa hakuna tukio lolote la uhalifu siku hiyo kwa kuwa wahalifu hao walikwenda nao kuburudika siku hiyo” alisema na kuwafanya wageni waalikwa kucheka .

Aliitaka serikali kuwa jirani na sekta ya michezo yote na kuiboresha kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana ambao asilimia kubwa hawana ajira na kuongeza kuwa michezo uleta afya ya akili na afya ya mwili hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kufanya mazoezi.

Mungi alivitaka vijiwe vyote vya mchezo wa pool kujiepusha na kuuza na kununua madawa ya kulevya na kuahidi kufanya msako mkali kwa kila kijiwe cha mchezo huo wanaojihusisha na biashara hiyo kwa kuwa vinajulikana na jeshi la polisi.
 
Alivitaja vijiwe vinavyojihusisaha na biashara hiyo kwa kigezo cha mchezo wa pool kuwa ni Mashine tatu, Ipogoro, Kihesa na Mlandege ndio vinaongoza kwa biashara hiyo inayoharibu sifa ya mchezo wa Pool.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya mchezo wa Pool kutoka Ruco, Said Mohamed aliutaka uongozi wa chuo hicho kuwapa ushirikiano katika kuundeleza mchezo huo kwa kuwaandalia ratibu nzuri ya mazoezi na muda wa masomo.

Alisema kupitia mchezo huo wamefanikiwa kukitangaza chuo kitaifa na kimataifa hivyo ni jukumu la chuo sasa kuweka kipaumbele katika michezo mingine kuweza kukiletea sifa chuo na mkoa kwa ujumla.

Aliupongeza uongozi wa Tbl kuptia kinywaji cha Safari Lager kwa kudhamini mchezo huo na kuongeza soko la ajira kupitia michezo na kuutaka kuendelea  kudhamini mchezo huo.

Naye meneja mauzo mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma Raymonda Degera aliwapongeza mabingwa hao na aliwataka kuongeza juhudi na maarifa ilikuweza kuuchukua tena mwakani katika mashindano mengine ya vyuo vikuu nchini wa mchezo wa pool

KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR

$
0
0
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu shughuli za Mkutano wa 16 wa Baraza la Nane la Wawakilishi utakaoanza tarehe 14 Mei 2014 katika Ukumbi wa Baraza hilo Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa gaazeti la Daly News Issa Yussuf akiuliza maswali katika mkutano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad alipokutana na waandishi wa Habari kuzungumzia shughuli za Mkutano wa 16 wa Baraza la Nane la Wawakilishi utakaoanza tarehe 14 Mei 2014 katika Ukumbi wa Baraza hilo Mbweni nje ya mji wa Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR. 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MKUU WA UNDP BIBI HELLEN CLARK

$
0
0
 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya ukumbusho na  na Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bibi Hellen Clark na ujumbe wake aliyemtembelea leo Mei 13, 2014 Ikulu jijini Dar es salaam

Mlimbwende Jokate Mwegelo awataka wahitimu wa vyuo vikuu kujiajiri

$
0
0
Mbunifu wa mitindo na Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
Mbunifu wa mitindo na Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006,Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyoandaa kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
Jokate Mwegelo akiwa na mshindi wa shindano la ubunifu, Jacqueline Rimoi ambaye alimzawadia sh, 300,000 kwa kutengeneza tangazo la kunadi bidhaa za kidoti kwenye ukumbi wa Nkrumah.

Mbunifu wa mitindo na Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 ametoa wito kwa wanafunzi wanao hitimu vyuo vikuu nchini kujihusisha na ujasiliamali na kutumia vilivyo vipaji vyao katika kupambana na soko la ajira.

Joketi alitoa wito huo juzi wakati akitoa mada ya jins ya kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu katika kongamano la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lijulikanao kwa jina la 2014 Market Forum.

Alisema kuwa pamoja na yeye kusomea mambo ya siasa na kuhitimu digrii yake chuoni hapo, mpaka sasa hajaweza kufanyia jambo lolote taaluma hiyo zaidi ya kujiajiri kupitia kampuni yake ya Kidoti Tanzania Limited ambayo inamuingizia fedha.

Alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na ugumu wa soko la ajira na kutokana na kuamua kujiajiri kwa njia mbadala (vipaji) vyake.

“Wakati nasoma, lengo langu kubwa lilikuwa ni kuwa mwanasiasa, nilimaliza hapa hapa Chuo Kikuu na baadaye nilishauliwa nichukua ‘masters’, nilianza kusoma, hata hivyo nilihairisha masomo hayo baada ya kuamua kuanza kuwa mbunifu na mwaka 2013 nilizindua bidhaa yangu ya nywele na nguo zijulikanazo kwa jina la ‘kidoti brand’ na sasa nimeingiza sokoni kandambili aina ya kidoti,” alisema Jokate.

Alisema kuwa alifanya utafiti wa kina ili kuteka soko la bidhaa zake na mpaka sasa anazidi kubuni aina nyingine za mitindo ya nywele, nguo, kandambili na bidhaa nyingine.

“Tusitegemee ajira kutokana na kile tulichokisomea, tunatakiwa kuwa wabunifu na kutumia vipaji vyetu, ukiweka nia tafanikiwa pamoja na ugumu wa kupata mtaji na mambo mengine, kwa kufanya hivyo utaweza kumpa ajira mtu aliyesoma zaidi yako, ipo mifano mingi duniani na matajiri wengi hawana elimu ya kutosha, ila wamekuwa wabunifu na sasa wameajiri wataalam ambao ni wasomi, hata hivyo soko la ajira ni dogo na wachache ndiyo wanabahatika kupata kazi,” alisema.

Alisema kuwa kwa sasa lengo lake kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea pamoja na kupata ushindani mkubwa katika soko kutokana na wingi wa bidhaa kama zake.

TAARIFA YA UTEUZI WA BODI MPYA YA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII (SSRA)

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watakiwa kutumia muda wa kujadili masuala muhimu kwa wananchi na taifa kwa ujumla

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo- Zanzibar     
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wametakiwa kutumia muda wao katika kikao kijacho cha Bajeti  kujadili masuala yalio kuwa muhimu kwa wananchi  na Taifa kwa ujumla  na waepukane na masuala yanayo husiana na bunge la katiba, kwani masuala yake yanajadiliwa katika  Bunge  maalum la katiba.
Hayo yamesemwa leo huko Baraza la Wawakilishi na Katibu wa Baraza hilo Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa na mazungumzo na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusu muwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka  2014/2015 ambayo inatarajiwa kusomwa kesho katika Baraza hilo.
Amesema ameonavyema  kutoa wito  huo kufuatia baadhi ya wajumbe wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano katika kikao kinachoendelea hivi sasa kuzungumzia masuala ya Bunge la Katiba ndani ya Bunge hilo jambo ambalo si pahala pake na halitasaidia chochote.
“Ni muhimu sana kwa wajumbe kujuwa wajibu wao na  wanachopaswa  kufanya wakiwa  ndani ya Baraza   la Wakilishi na waepukane na mawazo ya Bunge la katiba”, alisema Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
Aidha aliwataka wawakilishi  watumie nafasi zao vyema si kwa kumridhisha   mtu au chama  kwani  wakifanya hivyo watakuwa hawatendei haki  wananchi wao walio wachagua majimboni.
Alishauri  michango na  majadiliano yao ilenge  zaidi katika kuisaidia Serikali na wananchi wao kwani hicho ndicho kinacho hitajika na kuleta mustakabali mzuri kwa Taifa.  
“Baraza la Wawakilishi halina opposition ndio maana hata wajumbe wake wamechanganyika hivyo hatutarajii kutokea malumbano yasiyo na tija”, alisema Yahya.
Katibu huyo alizitaja shughuli za mkutano huo wa 16 wa Baraza la nane kuwa ni pamoja na  kujibiwa masuala 90 yaliyoulizwa na wajumbe  na kupitisha bajeti za Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanibar.
Aidha Miswada ya sheria miwili  itasomwa  ambayo ni mswada wa sheria ya Fedha  na mswada wa sheria ya matumizi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 2014/2015.
Alisema hakutakuwa na shuhuli yoyete itakayofanywa Barazani hapo  mpaka bajeti hiyo itakapomalizika tarehe 30 Julai.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR LEO.

Barnaba Ney na Vanesa Wasisitiza mawifi wajipangeeeeeee


Sekta ya Utamaduni kudumisha Ushirikiano baina ya Tanzania na China

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga(kulia) akiteta jambo na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Liu Dong walipotembelea ofisi za Wizara hiyo kuwatambulisha wasanii wa kikundi cha sanaa cha Yunnan Arts Troupe kutoka China leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Micherzo Prof. Hermas Mwansoko akielezea jambo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wasanii wa kikundi cha Yunnan Arts Troupe kutoka China leo jijoni Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Sihaba Nkinga na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Lui Dong.
 Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Lui Dong (Kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga alipotembelea ofisini kwake  leo jijini Dar es Salaam. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Kiutamaduni Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Chija hapa nchini Bw/. Lui Dong walipotembelea ofisi za Wizara ya habari leo jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga(mwenye suti ya rangi ya maziwa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa kundi la YunnanArts Troupe kutoka China pamoja na maafisa kutoka Ubalozi wa China nhini Tanzanaia. Picha na Frank Shija,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WHVUM

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI UYUI,KESHO KUUNGURUMA WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui  ambapo aliwaambia wananchi hao Kilimo cha Tumbaku kiondoe umasikini na si kuongeza umasikini kwa mkulima.

Wakulima wa Tumbaku kata ya Ufuluma wamelalamikia kulazimishwa na viongozi wa vyama vya ushirika kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ,hata kama sio wanachama.Kinana amewataka wakulima hao kutokukubali kusumbuliwa kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ambavyo baadhi yake vimejaa walaghai na wanyonyaji wa wakulima hao.


Amesema kuwa Wakulima wa zao hilo la tumbaku wamekuwa wakifanya kazi kubwa na ngumu,lakini hawafaidika na jasho la kazi yao,kutokana na kuanzishwa kwa vyama vingi vya ushirika ambavyo vipo kwa faida ya wajanja wachache,hivyo wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa vyama vya ushirika.


Nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa aliongeza kuwa mnamo mwaka 2012 wakulima wa Tumbaku waliibiwa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 16,kama vile haitoshi mnamo mwaka 2013 wakulima hao waliibiwa kiasi cha fedha shilingi bilioni 12 na umoja wa vyama vya ushirika,akabainisha kuwa kufuatia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha kwa wakulima,mwaka huu tumbaku haitatolewa kienyeji kwa vyama hivyo mpaka wahakikishiwe fedha zao zitalipwaje.



Akabainisha kuwa imefika wakati wakulima wa Tumbaku wajitegee,wawe huru na kuamua ni wapi wauze tumbaku yao na kwa bei waitakayo ni si kupangiwa na vyama vya ushirika,akaongeza kwa kusema kuwa Wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa Vyama vya ushirika. 

Kinana amemaliza ziara yake wilayani Uyui leo  na kesho ataunguruma wilayani Sikonge mkoani Tabora. 
 Wakazi wa Ufuluma wakishangilia na wengine wakifuatilia jambo kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kata hiyo ya Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora. 
Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Ndugu Shaffin Mamlo Sumar akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora.

 Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma mapema leo jioni katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
 Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Ufuluma,Wilayani Uyui mkoani Tabora.

 Sehemu ya baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao jioni ya leo mkoani Tabora
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  akizungumza na Sehemu ya baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali mkoani Tabora jioni ya leo,ambapo Walimu waliwasilisha changamoto zao mbalimbali,na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyajibu papo kwa papo na mengine aliahidi kuyafanyia kazi na mengine aliyapatia majibu mapema iwezekanavyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Mh Lucy Mayenga wakijiandaa kuingia kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Mh Lucy Mayenga akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye Ofisi yake wilayani humo.Kinana amekuwa wilayani humo kwa ziara ya kutekeleza  na kuhimiza Ilani ya CCM,kukagua maendeleo ya Miradi mbalimbali na kusikiliza kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Mh Lucy Mayenga akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo Pichani),kwenye makao Makuu ya wilaya hiyo katika kijiji cha Isikizya mkoani Tabora. 
 Wapiganaji wakiwa kazini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ,Halmashauri ya wilaya ya Uyui imejenga nyumba nane kwa ajili ya watumishi wake.
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uyui huku akipokea maelezo ya mradi wa ujenzi kutoka kwa Mhandisi wa Wilaya Ndugu Stephen Nyanda.

 Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mapema leo.
 Kinana akikagua Mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi,wilayani Uyui
 Kinana akipewa maelezo juu ya mradi wa chanzo cha maji,katika kijiji cha Isikizya,wilayani Uyui.



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiweka kibao cha kumbukumbu kuonyesha mti alioupanda kwenye shule ya sekondari Lolangulu piaKatibu Mkuu alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara  kwenye sekondari hiyo iliyopo kata ya Ilolangulu wilayani Uyui mkoa wa Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Uyui uliofanyika kata ya Ulolangulu. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa moja ya kifaa cha maabara na mwalimu wa Fizikia,Mahugila Chandarua wakati akipita kukagua  maabara ya shule ya sekondari ya Kata ya Ndono,wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Katika mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa  Sasa wilaya ya Uyui imekamilisha maabara katika shule za kata tano na zingine sita kukamilishwa mwaka ujao wa fedha.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ukarabati wa Zahanati ya Ufuluma katika kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui,mkoani Tabora 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisomewa taarifa na  Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Tabora Ndugu Erasto Chilambo ,Shirika la Nyumba la Taifa linajenga nyumba 50 katika wilaya ya Uyui.

MKUU WA MKOA WA TABORA,FATMA MWASA AZUNGUMZIA MAFANIKIO MAKUBWA YA WILAYA MPYA YA UYUI

Rais Kikwete afungua Mkutano mkuu wa NSSf jijini Arusha leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuga yake ya Ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.katika hotuba yake,Rais Kikwete ameitaka Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuhakikisha inawafikia wananchi wengi ambao bado hajapata ufahamu mzuri wa umuhimu wa kujiwekea akiba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi Tuzo ya Utoaji wa Huduma bora za Mafao iliyoipata NSSF,kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza mapema leo asubuhi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akiwasi Utekelezaji wa Maazimio ya Shirika wakati Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi mfano wa kadi ya Uanachama wa NSSF,kwa mwanachama mpya aliejiunga na Mpango wa Wakulima,Bi. Amina Salehe Sakali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi mfano wa kadi ya Uanachama wa NSSF,kwa mwanachama mpya aliejiunga na Mpango wa Madini,Bw. Emmanuel Ismael.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF  Bwana Crescentius Magori akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  katika viwanja vya AICC mjini Arusha ambapo alifungua mkutano Mkuu wa wadau wa NSSF leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo muda mfupi baada ya kuwasili katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC mjini Arusha leo ambapo alifungua mkutano wa nne wa wadau wa NSSF.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mages Mulongo, Naibu Waziri wa TAMISEMI Kassim Majaliwa, Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Bwana Abubakar Rajabu na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NSSF Bwana Crescentius Magori Picha na Freddy Maro.

Mantra yasaini makubaliano na Serikali kupiga vita ujangili wa ndovu

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Chris Sattler, Afisa Mtendaji Mkuu wa Uranium One, (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambao inairuhusu kampuni ya uchimbaji madini ya urani ya Mantra Tanzania kuwekeza dola za Kimarekani 800,000 katika mwaka 2014 itakayo tumika katika shughuli za kupambana na ujangili katika mbuga za wanyanya nchini Tanzania. Aliyesimama ni Galina Molchanova, Makamu wa Rais wa kamapuni ya Mantra Tanzania. Hafla hiyo fupi ilifanyika sambamba na mkutano wa siku mbili wa Wanyamapori uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
=========  ========
Mantra yasaini makubaliano na Serikali kupiga vita ujangili wa ndovu
·         Yawekeza dola za kimarekani 800,000 mwaka 2014 katika vita dhidi ya ujangili.

Dar es Salaam, Tanzania – KAMPUNI ya Mantra Tanzania na Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Wildlife Division) wamesaini mkataba wa makubaliano, ambao umelenga kwa pande zote mbili kushirikiana katika kupiga vita ujangili wa tembo katika eneo la kusini mwa hifadhi ya wanyamapori ya Selous. Katika makubaliano hayo, kampuni ya Mantra Tanzania itawekeza Dola za Kimarekani laki nane ($ 800,000) katika mwaka 2014 katika kampeni dhidi ya ujangili nchini. 

Makubaliano hayo yalisainiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Uranium One Inc Bw. Chris Sattler kwa niaba ya Mantra Tanzania (kampuni dada ya Uranium One ambayo inasimamia mradi wa Mto Mkuju, mgodi mkubwa duniani wa uranium katika ukanda wa kusini wa nchi). Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika sambamba na mkutano wa siku mbili wa Wanyamapori uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

“Ujangili wa ndovu umefikia hatua mbaya katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous na kampuni ya Mantra imejipanga kikamilifu kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na tatizo hili,” alisema Bw. Sattler. Aliongeza, “Makubaliano haya yanaturuhusu kushirikiana na Idara ya Wanyamapori, kuandaa na kuutekeleza mpango wa kupiga vita ujangili ili kuwaokoa ndovu waliopo katika hifadhi ya Selous. Napenda kumshukuru Waziri Nyalandu kwa uongozi wake katika suala hili la msingi. Najua wote tunamatumaini kuwa mpango huu utasaidia kuonyesha njia  kwa makampuni binafsi na ya umma kushirikiana katika kuhifadhi wanyamapori Tanzania na Afrika.”

Kwa upande wake, Waziri Nyalandu alisema serikali ya Tanzania, ambayo inaunga mkono Mradi wa Mto Mkuju, itajitahidi kuhakikisha kwamba masuala mengine yaliyosalia kusainiwa yatasainiwa ikiwa ni pamoja na Makubaliano ya Uchimbaji Madini na uendelezaji wa migodi (Mining Development Agreement -MDA-) inatekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha unaoishia mwezi Juni.

 “Jitihada zinazoambatana na hati hii ya kulinda na kutusaidia kupambana na ujangili katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous na pia kupiga hatua zaidi na kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania zitakuwa na maana mara baada ya kusaini MDA. Nategemea kushirikiana na wenzangu toka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Fedha kuhakikisha kuwa tunayafanyia kazi utaratibu zilizobakia ili mradi huo uanze  uzalishaji. “Kwa kusaini makubaliano haya, ninaonyesha njia ya kuwa ni suala linalowezekana kwa seka binafsi na ya umma kufanyakazi kwa pamoja ili kufikia lengo linalokusudiwa,” alisema Nyalandu.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, kamati maalum itakayojumuisha wawakilishi wawili kutoka Mantra na wengine wawili kutoka katika Idara ya Wanyamapori itaundwa. Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuandaa, kutekeleza na kuufanyia tathmini mpango huo wa kupiga vita ujangili, na pia kwa ajili ya kuwasiliana na wadau mbali mbali, ikiwa ni pamoja na wawakilishi toka katika ngazi zote za serikali, jamii, makundi ya wawindaji na mashirika yasiyo yakiserikali.

Mkataba huo umejikita zaidi katika kuuendeleza mpango wa vita dhidi ya ujangili, ambao kampuni ya Mantra Tanzania ulishauanza mwaka 2013. Chini ya mpango huu, wahitimu 20 kutoka Chuo cha Mafunzo ya Uaskari wanyamapori cha hifadhi ya Selous wataingizwa katika kitengo cha kampuni ya Mantra cha kupiga vita ujangili. Makubaliano hayo yanaeleza kuwa askari watabaki kuwa wafanyakazi wa hifadhi ya Selous na kurudishwa katika hifadhi baada ya miezi 12 ya kufanya kazi. Wakati kitengo cha kupiga vita ujangili cha Mantra, askari watapatiwa hifadhi karibu na Mradi wa Mto Mkuju na kufanya patroo katika eneo lenye kilometa za mraba 20,000 kuzunguka eneo la mradi.

Mantra itawapatia askari hao mavazi, vifaa na vyombo vya usafiri, pamoja na mafunzo maalum katika mawasiliano, usalama, utafutaji uelekeo na mbinu za kukabiliani na ujangili. Kufanya uchunguzi kwa kutumia ndege maalum inaandaliwa na majaribio ya kutumia magari maalum yenye kamera zitumikazo usiku GPS navigation na video transmitters vimeshakamilishwa. Kufuatana na kufuata taratibu na ruhusa zinazotakiwa, shughuli hizi za ulinzi, zinazounga mkono vita dhidi ya ujangili vitaundwa na kuanza kazi.
Shughuli za Mantra za kupiga vita ujangili pia zitaenda pamoja na mitandao ya ukusanyaji taarifa ya jamii, ambayo itasaidia katika kukusanya, kuchambua na kutoa taarifa juu ya shughuli za ujangili.

WAZIRI FENELLA AKUTANA NA MMILIKI WA STARTIMES

$
0
0

Star1
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kushoto) akielezea jambo kwa Mmiliku wa Startimes Bw. I MR. Pang alipotembelea ofini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.Star3.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga wakati wa kikao chao na mmiliki wa Startime Bw.Pang (kushoto) alipotembelea ofoini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.Star4. (1)Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akiwa katika kikao na mmiliki wa Kampuni ya Star Media Bw. Pang (wa pili kushoto) alipotembelea ofini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Startimes Bw. William Lan, Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assa Mwambene na Mwakilishi wa Startimes nchini Bw. Jack Zhou.
Picha zote na Frank Shija
Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM

RAIS KIKWETE AHUDHURIA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI ILIYOANDALIWA NA NSSF JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab wakati wakiingia Ukumbini tayari kwa kushiriki chakula cha jioni na Wadau mbali mbali wa NSSF wanaohudhulia Mkutano wa Nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF.Tafrija hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi tuzo kwa Makampuni na Mashirika mbali mbali ambayo idadi kubwa ya wafanyakazi wake ni wanachama NSSF,wakati wa tafrija ya Chakula cha jioni iliyofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha leo. 
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini,Mzee King Kikii a.k.a Mzee wa Kitambaa cheupe akizikonga vilivyo nyoyo za Mashabiki wake wakati wa hafla hiyo.
Rais Kikwete pia alijumuika na Wadau wa NSSF kuyarudi mangoma ya Kitambaa cheupe.


MABONDIA SAID MBELWA NA KARAMA NYILAWILA WATAMBIANA KUPAMBANA MEI 24 MANZESE

$
0
0
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony Rutta.
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese.
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Said Mbelwa na Karama Nyilawila wametambiana kila mmoja kuibuka mbabe katika mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Univers Boxing Oganaization UBO  mpambano utakaofanyika katika ukuimbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam

likiwa linasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST mpambano huo utakao onesha kuwa nani mbabe wa uzani wa kg 76 ubingwa wa UBO akizungumzia mpambano huo Katibu mkuu wa shilikisho la ngumi za kulipwa nchini Antony Rutta amesema kuwa mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi nchini ukuiwa na mabondia wote wamecheza ngumi za kitaifa na kimataifa yani ndani na nje ya nchi

akitolea mfano bondia Said Mbelwa ndie bondia pekee ambaye anaenda nje ya nchi kucheza ngumi na kumaliza raundi zote 12 walizo pangiwa ingawa anapigwa kwa pointi ambapo mabondia wengi wa Tanzania wakienda nje wanapigwa K,O mbaya sana ambazo zinawatia mpaka itrafu katika baadhi ya maeneo

akimzungumzia Nyilawila ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa uzani huo wa WBF ambaye alichukua mkanda huo nje ya nchi jambo ambalo kubwa sana duniani kumpiga mzungu nyumbani kwao si mchezo hivyo mabondia wote hawa wana sifa zinazo lingana

nae bondia Mbelwa aliongeza kwa kusema kuwa mimi nipo fiti hivyo mashabiki waje kwa wingi kuangalia ngumi ambazo zitahacha historia kubwa katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwa kipigo nitakachompa Karam


Nae bondia Nyilawila alitamba kwa kukimbiwa na Thomasi Mashali ambaye alikuwa acheze nae ata hivyo bondia huyo amepata ajali ya gari na zamu yake atacheza Mbelwa uchu wangu mkubwa ni Mashali huyu wamemuonea bule kunipa mimi nita hakikisha namchakaza bila huruma ata chembe.


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile gem ya fransic Miyeyusho vs Mohamed Matumla 'Sneak jr'  mpambano ulivuta hisia za wapenzi wengi wa ngumi nchini 

PSPF YATOA MSAADA WA MADAWATI 100 KWA SHULE ZA MSINGI

$
0
0
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Pensheni kwa watumishi (PSPF)Mkoa wa Iringa, Baraka Jumanne akizungumza na waalimu wa Shule za Msingi tatu Mufindi Kaskazini(hawapo pichani) kabla ya kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na mfuko huo.
Afisa Mfawidhi PSPF Iringa,Bakari Jumanne akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Mufindi Evarista Kalalu Madawati miamoja kwa ajili ya Shule za Msingi Mjimwema, Mamba na Nyamalala yenye thamani ya sh. milioni 5 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Mufindi.
Baadhi ya madawati yakiwa ndani ya lori kabla ya kukabidhiwa kwa shule za msingi 3 za Mufindi Kaskazini.(picha zote na Denis Mlowe).

MKUTANO WA NNE WA WADAU WA NSSF WAENDELEA KWA SIKU YA PILI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akisisitiza jambo wakati wa kujibu baadhi ya maswali ya Wadau wa NSSF wanaohudhulia Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza rasmi jana na kuendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kikao cha kwanza siku ya leo,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) la Nchini Kenya,Adan Mohamed  akiongoza kikao hicho leo kwenye Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza rasmi jana na kuendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Mipango,Uwekezaji na Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yacoub Kidula akiwasilisha mada yake iliyohusu mambo ya Uwekezaji,kwenye Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza rasmi jana na kuendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akichangia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa kwenye Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza rasmi jana na kuendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kikao cha Pili kwa siku ya leo cha Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Prof. Mussa Assad akizungumza jambo wakati akiweka sawa taratibu za uchangiaji katika kikao cha Mkutano huo, unaoendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mwenyekiti Mpya wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA),Juma Ally Muhimbi akifatilia mada mbali mbali zinazoendelea kutolewa kwenye Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF ulioanza rasmi jana na kuendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.


JESHI LA POLISI LAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM (PICHA YAKE YATOLEWA HADHARANI) ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI

MKURUGENZI MKAZI WA OXFAM TANZANIA JANE FOSTER ATEMBELEA KIJIJI CHA MAISHA PLUS NA KUJIONEA KAZI ZA UJASILIAMALI

$
0
0
 Wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus ambao ni Vijana wa Maisha Plus pamoja na Mama shujaa wa Chakula wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster ambaye hayupo 
 Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster, Mkamiti Mgawe wa Oxfam na Babu kutoka kijiji cha Maisha Plus Rajabu Msumi  wakiongea na washiriki wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula.
 Mkamiti Mgawe wa tatu kutoka kushoto akimtambulisha Markia wa Kijiji cha Maisha Plus kwa Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster
 Mkurugenzi  wa Maisha Plus akioneshwa Shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus
 Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa moja ya jiko lililotengenezwa na Akina mama Shujaa wa Chakula pamoja na Vijana wa Maisha Plus.
 Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa moja ya Ghala la kienyeji na imara kwa ajili ya kuhifadhia vyakula.
 Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa shamba linalotumia kilimo hai na cha kisasa katika kijiji cha Maisha Plus ambapo wahusika wa shughuli hizo na uangalizi wa Shamba hilo ni Mama Shujaa wa Chakula na Vijana washiriki wa Maisha Plus
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster  akiendelea na ziara yake ndani ya kijiji cha Maisha Plus na kujionea mambo mbalimbali yanayo endelea Kijijini hapo.

**********************************

Chereko na vifijo vilitawala katika kijiji cha Maisha Plus kuonyesha furaha kwa kuwa  Katika siku hii kijiji kilitembelewa na Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongozana na mfanyakazi wa Oxfam Mkamiti Mgawe ili  kujionea miradi mbalimbali waliyobuni wanakijiji cha Maisha Plus.

Mkurugenzi alifurahishwa sana na kazi zilizofanywa kwa usatadi na umahiri wa hali ya juu na kujionea hazina za vipaji vya wanakijiji hao. Oxfam Tanzania ni moja ya wadhamini na wadau wakuu wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula 2014. 

Miradi iliyotembelewa ni pamoja ya utengenezaji wa batiki, sabuni, kikapu cha ajabu, bustani ya kuhama, jiko la gesi, aina mbalimbali za majiko ya udongo wa mfinyanzi, ufugaji bora wa kuku na nyuki, bustani za mboga na shamba linalotumia kilimo hai na kilimo cha kisasa. 


Chereko na vifijo vilitawala katika kijiji cha Maisha Plus kuonyesha furaha waliyonayo na pia kusherehekea siku ya mama duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 11 Mei. Katika siku hii kijiji kilitembelewa na Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongozana na mfanyakazi wa Oxfam Mkamiti Mgawe kujionea miradi mbalimbali waliyobuni wanakijiji cha Maisha Plus. 

Mkurugenzi alifurahishwa sana na kazi zilizofanywa kwa usatadi na umahiri wa hali ya juu na kujionea hazina za vipaji vya wanakijiji hao. 

Oxfam Tanzania ni moja ya wadhamini na wadau wakuu wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula 2014. Miradi iliyotembelewa ni pamoja ya utengenezaji wa batiki, sabuni, kikapu cha ajabu, bustani ya kuhama, jiko la gesi, aina mbalimbali za majiko ya udongo wa mfinyanzi, ufugaji bora wa kuku na nyuki, bustani za mboga na shamba linalotumia kilimo hai na kilimo cha kisasa.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images