Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46339 articles
Browse latest View live

WAZIRI NYALANDU AKABIDHIWA MAGARI YA KUSAIDIA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MAJANGILI WA MAUAJI YA TEMBO

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu, akisainiana mkataba wa makabidhiano wa magari matatu aina ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa na Makamu wa Rais Dkt Bilal, jana limemalizika leo Mei 10, 2014. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhri, Job Ndugai (kulia) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa
 Wakibadilishana nyaraka za mkataba huo baada ya kutiliana saini. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, wakiwa katika Kongamano hilo, lililomalizika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar Es salaam.

Rais Kikwete akutana na Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola jijini Luanda leo

$
0
0
 Rais wa Angola Mhe. Jose Eduardo Dos Santo akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda na kufanya naye mazungumzo leo. Rais Kikwete alikuwa nchini Angola kwa ziara ya kikazi ya siku moja
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na mazungumzo na Rais wa Angola Mhe. Jose Eduardo Dos Santo  katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda leo. .Rais Kikwete alikuwa nchini Angola kwa ziara ya kikazi ya siku moja
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akibadilishana mawazo  na Rais wa Angola  Mhe. Jose Eduardo Dos Santo  katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda wakati akihitimisha  ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na Rais wa Angola  Mhe. Jose Eduardo Dos Santo  katika ikulu ya nchi hiyo jijini Luanda wakati akihitimisha  ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo.Picha na Freddy Maro

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO NA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA WILAYANI NZEGA LEO

$
0
0
Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana akipita kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la mapokezi la wagonjwa wa nje (OPD),hospitali ya wilaya ya Nzega,mapema leo mchana,katika ziara yake anayoendelea nayo yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali sambamba na wananchi,ikiwemo pia kusikiliza kero za wananchi zinazowakabili na kuzitafutia majibu.

Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Mbunge wa jimbo la Nzega,Mh.Hamisi Kingwangalla wakishiriki katika ujenzi wa jengo la mapokezi la wagonjwa wa nje (OPD),hospitali ya wilaya ya Nzega,wakati Ndugu Kinana alipokagua ujenzi wa jengo hilo katika ziara yake anayoendelea nayo yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali sambamba na wananchi,ikiwemo pia kusikiliza kero za wananchi zinazowakabili na kuzitafutia majibu.

Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa jambo kwenye simu na mfuasi wa chama cha CCM,mapema leo,wakati Ndugu kinana alipokwenda kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata katika kijiji cha Nkiniziwa,Wilayanni Nzenga mkoani Tabora. 

Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata katika kijiji cha Nkiniziwa,Wilayani Nzenga mkoani Tabora. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani shoto na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakimsikiliza mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Kampala,Amos Kashindye namna ya kutumia moja ya kifaa cha maabara,mara baada ya kuitembelea shule hiyo ya kata na kukagua maabara ya sayansi na fizikia katika shule hiyo.

Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Ndala katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Taifa,wilayani Nzega mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua moja ya barabara zinazojengwa mjni Nzega kwa kiwango cha lami,kushoto kwake ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye na pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh,Fatma Mwasa.

Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiyapokea baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini wilayani Nzega,wakiomba Serikali na chama cha CCM,kuwasaidia vijana hao wachimbaji wadogo wadogo kupewa maeneo yao ya kuchimba madini bila kubugudhiwa na mengineyo
Sehemu ya Wananchama na wafuasi wa chama cha CCM,wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Nape Nnauye akiwahubia Sehemu ya Wananchana na wafuasi wa chama cha CCM,katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Baadhi ya Baiskeli zilizotolewa na Mjumbe wa Mkutano Halmashauri kuu CCM Taifa,Ndugu Hussein Bashe kwa ajili ya kuwakabidhi viongozi wa mbalimbali wa chama hicho katika suala zima la kurahisha utendaji wao wa kazi. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahubia baadhi ya Wananchana na wafuasi wa chama cha CCM,katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Sehemu ya Wananchama na wafuasi wa chama cha CCM,wakimsikiliza Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akizungumza jambo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika jioni ya leo Nzega Mjini.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimpongeza Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM,Taifa,Ndugu Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi piki piki tatu kwa jumuiya za Chama,na Baiskeli 163 kwa ajili ya matawi yote ya CCM ya Wilaya ya Nzega kupitia mradi wao wa kuimarisha chama,pia alitoa baiskeli 37 kwa Jumuiya ya UVCCM wilayani humo,Pia alikabidhi kiasi cha shilingi Milioni mbili kwa kikundi cha Boda boda na milioni mbili kwa kikundi cha Mamalishe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimpongeza Mbunge wa Nzega,Mh.Hamisi Kingwangalla mara baada ya kukabidhi mashine ya kutotolea vifaranga kwa kikundi cha vijana.

Rais Kikwete atembelea kiwanda cha saruji kikubwa zaidi duniani cha Dangote, Nigeria

$
0
0
. Ni kile kinachomilikiwa na mwekezaji anayejenga kiwanda cha saruji Mtwara 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametumia siku nzima ya  Ijumaa, Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Bwana Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mjini Mtwara.
Akiandamana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Abdallah Kigoda, kwa siku nzima, Rais Kikwete ametembelea kiwanda hicho cha Saruji cha Dangote kilichoko katika eneo la Obajana, Jimbo la Kogi, kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos. 
Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria Kongamano ya Uchumi Duniani-Afrika (WEFA) mwaka huu aliamua kutumia siku yake ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini humo, kwa kutembelea uwekezaji mkubwa wa mwekezaji ambaye ameanza ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Mtwara ambacho kitakuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote katika Tanzania, kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani za kimetriki milioni tatu kwa mwaka. 
 Rais Kikwete ambaye alipokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kiwanda hicho na Bwana Dangote mwenyewe, na kuanza ziara yake kwa kutembelea machimbo ya kiwanda hicho ambayo yako kilomita tisa kutoka kiwandani ambako malighafi ya kiwanda hicho husafirishwa kwa madaraja na mikada maalum hadi kiwandani. 
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kwa sasa Kiwanda cha Obajana kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa sasa kwa mwaka na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja na kuwa baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka ifikapo mwakani 2015. 
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilicho kwenye eneo la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika. 
Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka. Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilichoanza kujengwa mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006 na hatimaye kuzinduliwa na Rais Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria. 
“Mheshimiwa Rais, ili kuelewa vizuri mchango wa kiuchumi na kijamii za kiwanda hiki na viwanda vyetu vingine katika maeneo mengine ya Nigeria, unahitaji kukumbuka kuwa kabla ya kuanza kujenga kiwanda hiki, Nigeria nzima ilikuwa na uwezo za kuwazalisha tani za kimetriki za saruji milioni1.5 tu, wakati huo chini ya miaka 10 iliyopita. 
"Tunataka kufikia hatua ya kuhakikisha kuwa eneo la Afrika Magharibi na hata Bara letu la Afrika linaacha kabisa kuagiza saruji nje ya Bara letu. Na tutafikia huko.” 
Mbali na Kiwanda cha Obajana, Kampuni ya Saruji ya Dangote inazalisha saruji katika maeneo mengine mawili ya Nigeria ambalo uzalishaji wa jumla wa maeneo hayo matatu ni tani za metriki 20.25 kwa mwaka. Amesema Bwana Dangote kuwa ili kuweza kuwa na uhakika wa umeme, uongozi wa kiwanda hicho uliamua kuzalisha umeme wake kwa ajili ya kiwanda hicho kwa kujenga, miongoni mwa hatua nyingine, bomba ya kilomita 92 la kusafirisha gesi kutoka Ajaokuta hadi kwenye kiwanda hicho. 
Alipoulizwa na Rais Kikwete kama wanategemea kwa namna yoyote umeme wa taifa, Bwana Dangote alijibu kwa furaha, “hatujaunganishwa kwenye gridi ya taifa na tunadhani hili ni jambo zuri kwa sababu hatua tulizochukua zinatuhakikishia umeme wakati wote na kwa kiwango ambacho tunakihitaji. Tunatumia gesi ama diseli yetu wenyewe. Na wala siyo umeme tu, hata miundombinu ya eneo hilo kiliwemo daraja hili kubwa linalonganisha eneo la machimbi na kiwanda, tumejenga sisi Mheshimiwa Rais.” 
 Bwana Dangote amesema kuwa mbali na kujenga miundombinu ya umeme wake, kiwanda hicho pia kimejenga bwawa lake lenyewe kwa ajili ya huduma ya maji kusaidia uzalishaji wa saruji bila kutegemea huduma ya maji ya Serikali. 
Aidha, bwawa hilo linatoa huduma ya maji kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho. Mbali na shughuli za kiwanda, Kampuni ya Bwana Dangote inashiriki kwa karibu sana shughuli za jamii inayozunguka kiwanda ambacho kwa sasa imeanzishwa miji midogo saba katika eneo lililokuwa pori lenye nyumba 50 za wenyeji tu kabla ya shughuli za kiwanda hicho kuanzishwa. 
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inatoa shughuli za elimu, maji na umeme kwa wananchi ambao wanazunguka kiwanda ambacho tokea kuanzishwa kwake limevutia mabenki 13 ambayo yameanzishwa matawi yake katika eneo la kiwanda. 
“Mheshimiwa Rais, mbali na nyumba za wafanyakazi, tunawajengea hata nyumba za kuishi wananchi wanaozunguka eneo hili ambao wanatuunga mkono sana.” Mbali na kutoa huduma nyingine za kijamii, Kampuni ya Saruji ya Dangote inajenga taasisi kubwa ya elimu ya Dangote Academy ambayo itatoa elimu na mafunzo ya kiufundi kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa kiwanda hicho na watoto wa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
 Ili kuhakikisha kuwa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kwa kasi kubwa zaidi, Bwana Dangote ameagiza kiasi cha malori 6,000 kutoka China kusaidia ujenzi na pia amechukua uamuzi usiokuwa wa kawaida wa kuagiza maelfu ya vibarua kutoka nchi hiyo hiyo ya China kushiriki katika ujenzi huo na kuumaliza kwa haraka. 
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inafanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa Rais Kikwete anakifungua kiwanda cha saruji cha Mtwara kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka ujao. 
Mbali na Nigeria na Tanzania, Bwana Dangote ana viwanda ama anajenga viwanda vya saruji ama na shughuli za saruji katika nchi 14 za Afrika ikiwamo Ethiopia, Zambia, Mozambique, Kenya, Senegal na Sierra Leone, Afrika Kusini, Congo (Brazzaville), Cameroun, Ghana, Liberia na Ivory Coast. 
Mbali na shughuli za uzalishaji wa saruji, Bwana Dangote ambaye anakubaliwa kuwa tajiri mkubwa zaidi katika Afrika kwa thamani ya dola za Marekani bilioni 25 yeye na kampuni yake ya Dangote Group pia ina shughuli za uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa chumvi, utengenezaji wa magunia, uzalishaji maji, uzalishaji wa vyakula vya aina mbali mbali, uzalishaji wa mafuta ya kupikia, utengenezaji wa nyanya. 
Kwa sasa anaendelea na ujenzi wa kiwanda cha mbolea na kile cha kuzalisha bidhaa za petrol na kemikali. Kampuni ya Saruji ya Dangote – Dangote Cement- ndiyo kampuni kubwa kuliko zote katika Afrika Magharibi kwa sasa ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 22.7 kwa tathmini ya mwaka huu baada ya kuongeza thamani yake kutoka dola za Matrekani bilioni14.5 za mwaka jana. Mwishoni mwa ziara hiyo yenye mafanikio makubwa, Rais Kikwete aliondoka Obajana kurejea nyumbani kupitia Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Luanda, Angola ambako jana Jumamosi  alikutana na marais wa nchi hizo kabla ya kurejea nyumbani.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye machimbo ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.

KIPINDI CHA KWANZA CHA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS KURUSHWA HEWANI TAREHE 17 MAY 2014.KATIKA KITUO CHA RUNINGA CHA ITV

TGNP Mtandao ya Chambua Bajeti na Wahariri wa Vyombo vya Habari

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwasilisha mada kwa wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari leo. Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwasilisha mada kwa wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari leoMmoja wa wachambuzi wa sera wa TGNP Mtandao, Agnes Lukaya akiwasilisha matokeo ya tafiti mbalimbali za TGNP zilizofanywa kwa jamii. Mmoja wa wachambuzi wa sera wa TGNP Mtandao, Agnes Lukaya akiwasilisha matokeo ya tafiti mbalimbali za TGNP zilizofanywa kwa jamii.Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Usu Mallya (kushoto) akiwasilisha mada yake kwa wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wa TGNP na wahariri hao.   Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Usu Mallya (kushoto) akiwasilisha mada yake kwa wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wa TGNP na wahariri hao.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa na wataalamu wa masuala ya uchambuzi wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa na wataalamu wa masuala ya uchambuzi wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia.Juu ni baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa na wataalamu wa masuala ya uchambuzi wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia.
Juu ni baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa na wataalamu wa masuala ya uchambuzi wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia.
IMG_0240
Mada ikiwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao
TGNP Mtandao ya Chambua Bajeti na Wahariri wa Vyombo vya Habari  Juu ni wahariri wakifuatilia mada anuai katika mkutano huo. Juu ni wahariri wakichangia mada anuai katika mkutano huo.Uwasilishaji mada kwa hisia! Mmoja wa wadau wa TGNP akiendesha mjadala mara baada ya mada kwenye mkutano huo. Uwasilishaji mada kwa hisia! Mmoja wa wadau wa TGNP akiendesha mjadala mara baada ya mada kwenye mkutano huo.Mkutano wa TGNP na wahariri wa habari kuzungumzia uchambuzi wa bajeti kwa muktadha wa kijinsia. Mkutano wa TGNP na wahariri wa habari kuzungumzia uchambuzi wa bajeti kwa muktadha wa kijinsia.

MSAMA PROMOTIONS KUFUNGUA MADUKA MANNE KATIKA MAJIJI MAKUBWA YA KUUZA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
DSC_8730Na Mwandishi Wetu
IKIWA na lengo la kudhibiti wizi wa kazi za Sanaa hapa nchini, Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kufungua maduka katika majiji manne hapa nchini baada ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama maduka hayo yatakuwa katika majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na mkoani Dodoma ambayo yatakuwa yakiuza kazi halisi za wasanii.

Msama alisema kwa kuanzia wataanza na jiji la Mwanza, ambako wanatarajia kuweka duka katika mitaa ya Nyerere na Libert jijini humo.

Aidha Msama alisema mashabiki wengi wanauziwa DVD feki nyingi ambazo wanauziwa kati ya shilingi 1000-1500 ambazo zinadumu wii mbili wakati kazi halisi wanaziuza kwa bei ya jumla shilingi 2000 na rejareja shilingi 3000.

Msama alisema kwa jiji la Dar es Salaam, kampuni yake ina maduka katika maeneo ya Kariakoo mtaa wa Msimbazi naMasasi  lingine lipo Posta Mpya mtaa wa Mkwepu

MWIMBAJI NYOTA WA MUZIKI WA INJILI ROSE MUHANDO KUZINDUA KAMATA PINDO MIKOA 10

$
0
0
rose-muhando-post
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Rose Muhando anatarajia kuzindua albamu yake ya  Kamati Pindo yenye nyimbo nane atakayoifanya kwenye mikoa zaidi ya 10 ya Tanzania bara, uzinduzi utakaofanyika Agosti mwaka huu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama awali uzinduzi wa albamu hiyo ulikuwa ufanyike kabla ya Tamasha la Pasaka lilimalizika Mei 4 jijini Mwanza, kutokana na unyeti wake wameonelea kufanikisha baada ya tamasha.

Msama alisema uzinduzi wa albam hiyo utakuwa ni wa Kimataifa kwa sababu utashirikisha waimbaji mbalimbali kutoka nje ya Tanzania, hivi sasa taratibu za uzinduzi huo zinafanyika. “Katika uzinduzi huo, Rose Muhando ataimba live nyimbo zake zote tangu alipoanza kazi ya uinjilishaji, hasa kwa nyimbo zake kama Mteule uwe macho, Nibebe na nyinginezo ambazo atapiga live siku hiyo,” alisema Msama.

Albam hiyo ya Kamata Pindo la Yesu  imefanikishwa na kampuni ya Msama Promotions ikiwa  ina nyimbo ambazo ni Facebook, Wewe Waweza, Nibariki, Kwema, Muongo, Usiniache, Bwana Niongoze na iliyobeba albam  ambayo ni Kamata Pindo la Yesu.

Rose Muhando anatamba na albam zake nyingine zilizofanya vizuri ambazo ni pamoja na Mteule uwe Macho, Nibebe, Utamu wa Yesu, Jipange Sawasawa, Mungu anacheka na y a sasa ambayo ni Kamata Pindo la Yesu.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI NZEGA LEO,KESHO NDANI YA WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, wakati wa mwendelezo wa ziara hiyo ndani ya  Mkoa wa Tabora.Kinana amemaliza ziara yake katika Wilaya ya Igunga na Nzega na kesho kuhamia wilayani Uyui,katika suala zima la kuimarisha chama,kutekeleza na kuhimiza maendeleo ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010,sambamban a kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuni kwa namna moja ama nyingine,zira hiyo itakuwa ni ya siku kumi ndani ya mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya  Bukene, wilayani Nzega leo. 

Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo cha utii cha chama hicho, baada ya kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega leo.
Katibu wa NEC,Uenezi siasa na Itikadi,Nape Nnayue akiwahutubia wakazi wa Bukene,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, mkoani Tabora.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya  Bukene, wilayani Nzega leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiwapungia mikono wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega leo.
Kinana akishiriki kufyatua tofali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matofali wa akina mama wa CCM Wilaya ya Nzega. Mradi huo umefadhiliwa na Mbunge wa Viti MaalumMkoa wa Tabora, Munde Tambwe (pichani kushoto), katika eneo la Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega leo.
 Kinana akiwa na Mohamed Kashindye mmiliki wa shamba la kumwagilia la mpunga  alipoombwa kwenda kulikagua,katika Jimbo la Bukene, wilayani Nzega. Mkulima huyo alimuomba Kinana kufanya hivyo licha ya shamba lake kutokuwemo kwenye ratiba ya ziara ya kiongozi huyo. Kinana alikubali kukagua shamba hilo na kumpongeza Kashindye kwa kilimo hicho.
 Kinana akishuka kwenye tanki  alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, wilayani Nzega leo.
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka Nzega, Samweli Buyigi alipokuwa akikagua chujio la maji mjini Nzega leo
Wananchi wakifautilia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Itobo,jimbo la Bukene wilani Nzega mkoani Tabora.
 Vijana wakitumbuiza kwa ngoma ya zeze walipokuwa wakimlaki Kinana katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Itobo. 

 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo.
 Sehemu ya umati wa watu uliofurika kwenye mkutano wa CCM Kata ya Bukene .
Kinana akihutubia katika mkutano huo na kukemea kitendo cha wana Ukawa kuwatukana vingozi waasisi wa muungano.
Kinana akikagua mradi wa maji ndani ya jimbo la Bukene,wilayani Nzega mkoani Tabora.

Rais Kikwete awasalimu watoto mapacha DRC

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia watoto mapacha waliokuwa wanasubiri kupata matibabu katika Hospitali ya Ngaliema iliyopo jijini Kinshasa jana.Rais Kikwete alikwenda hospitalini hapo kumjulia hali balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mh.,Antony Ngereza Cheche anayetibiwa hospitalini hapo(picha na Freddy Maro)

Benki ya Exim yaisaidia wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala

$
0
0
Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni Wafanyakazi wa Benki ya Exim.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Picha na Mpiga Picha Wetu. 
  Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Wakwanza Kushoto)  na Meneja Msaidizi Msoko mwenzake Bi Violet Bikoche (Wapili Kushoto) wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua mara baada ya kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani
 Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni Wafanyakazi wa Benki ya Exim.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani.
Katibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bi. Erica Mbutu (wakwanza kushoto) na Meneja Msaidizi Msoko wa Benki ya Exim, Bi Violet Bikoche (Wapili Kushoto) wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua mara baada ya kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.  Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani.
Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Sr. Tuswege Mwamwaja (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania mara baada ya Benki hiyo kukabidhi magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani.
=====  =====  ======
BENKI ya Exim ya Tanzania imeadhimisha Sikukuu ya Mama Duniani kwa kuchangia magodoro 60 katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam katika kutoa heshima kwa kinamama wote na kuunga mkono jitihada za kuboresha afya ya uzazi nchini.  

Kwa sasa, Hospitali ya Mwananyamala ambayo ni hospitali kubwa ya rufaa jijini Dar es Salaam inatoa huduma kwa wakinamama wanaotarajia kujifungua zaidi ya 3100 kwa mwezi, ikiwa na vitanda 136 tu katika wodi hiyo ya wazazi.


Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magodoro hayo hospitali hapo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Msaidizi Masoko Bi Anita Goshashy alisema mchango huo ni moja kati ya utekelezaji wa shughuli za benki yake zinazolenga kuisaidia jamii inayoizunguka.


 “Mwaka jana, Benki ya Exim imeweza kufikia faida ya shilingi bilioni 20, na tumekuwa na utamaduni wa kurejesha kile tukipatacho toka kwa jamii. Sasa, leo hii tuko hapa Mwananyamala kukabidhi vitu hivi, ikiwa kama njia ya kutambua mchango wa kina mama zetu na kuonyesha jinsi gani tunaisaidia jamii inayotuzunguka kama benki,” alisema Bi. Goshashy, aliongeza kuwa benki itaendelea kuipiga jeki jamii hususani katika sekta ya Afya, Mazingira na Elimu.


Bi. Goshashy alisisitiza kuwa, “Leo hii tunakabidhi magodoro haya ili kuweza kusaidia kuboresha uzazi uliosalama. Kina mama wengi wanaotarajia kujigfungua ufariki wakati wakijifungua. Mchango wetu leo utasaidia katika katika kuboresha hali hiyo hapa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.


Jitihada zetu hazitaishia hapa tutaendelea kufanyakazi karibu na jamii inayotuzunguka.” Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani aliipongeza Benki ya Exim kwa msaada huo, na kuongeza kuwa msaada umewafikia kwa wakati muafaka na kuziasa taasisi nyingine za kifedha na makampuni mengine nchini kuiga mfano huo.


“Kwa niaba ya Jamii ya Hospitali ya Mwananyamala, Ningependa kuelezea shukrani zangu za dhati kwa hatua nzuri mliyoichukua kuweza kutusaidia vitanda hivi ambavyo vitatumika kwa wakinamama ambao tunawathamini kwa kiasi kikubwa maishani mwetu. Mchango huu utasaidia Jamii ya Mwananyamala kwa kiaasi kikubwa  sana,” alisema Dkt. Ngonyani.


Dkt Ngonyani alisema kuwa kadri ya serikali inapojitahidi kuzipatia vifaa vituo vya afya, jitihada haziwezi kutoshereza mahitaji yote kwa ujumla katika hospitali hizi, ndiyo maana kuna haja ya wadau wengine, hususani makampuni kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo na kuweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini.


“Nawapongeza kwa utekelezaji wenu mzuri wa sera yenu ya kufanya shughuli za kijamii. Ombi langu kwa benki ni kwamba bado tunakumbana na changamoto nyingi kama hospitali ya rufaa, Nawaasa msichoke kutupatia michango yenu katika sekta hii nyeti iokoayo maisha ya watu wetu,” Dkt. Ngonyani aliongeza.


MAMA TUNU PINDA AOMBA WATU NA MASHIRIKA MBALIMBALI KUSAIDIA KUCHANGIA KATIKA KUENDELEZA ELIMU KWA WATOTO NA VIJANA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALIBINO)

$
0
0
Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda akipokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda na anaye shuhudia ni Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi msaada huo wa vitabu ni kwaajili ya kusaidia Elimu kwa watoto na vijana wenye ulemavu wa ngozi (ALIBINO) sherehe hiyo ya makabidhiano imefanyika katika makazi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam.
picha ya pamoja
 Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda (pichani kati) akizungumza na Wanahabari kabla ya ya kupokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda (pichani kulia) na kushoto ni  Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi ..

THT yatoa vitabu kwa maktaba ya walemavu wa ngozi Kanda ya Ziwa

Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) imetoa vitabu vya Sayansi, Sanaa na Hesabu kwa maktaba ya walemavu wa ngozi inayotarajiwa kujengwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya New Millennium Group.


Vitabu hivyo vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 35 vimetolewa kwa lengo la kusaidia kukuza elimu Tanzania hasa kwa jamii ya walemavu wa ngozi, ikiwa ni mchango wa THT kwa huduma za jamii.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja Mkuu wa Nyumba ya Vipaji Tanzania, Mwita Mwaikenda alisema taasisi yake iliona changamoto ya vitabu baada ya taasisi ya New Millennium Group kutembelea vituo vya maalbino vya kanda ya ziwa mwanzoni mwa mwaka huu.


‘Msaada huu wa vitabu sisi kama THT tumeutoa ili kuiwezesha maktaba ya walemavu kupata vitabu vya kujisomea na hivyo kujiongezea maarifa baina yao’ alisema Mwita. Kwa upande wake Mlezi wa Taasisi ya New Millenium Group, Mama Tunu Pinda, alisema wanaishukuru THT kwa msaada huo ambao alisema ni muhimu sana kwa ajili ya lengo lao la kusaidia kuiwezesha kielimu jamii ya watoto wenye ulemavu wa ngozi.

‘Hakika msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha lengo la kuanzisha maktaba kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, na tunaaamini msaada huu utawapa changamoto wadau wengine kusaidia kukamilisha maktaba hii ya kwanza kabisa kuhudumia watu wenye ulemavu wa ngozi’ alisema Mama Pinda.



Naye Mwenyekiti wa New Millennium Group, Mama Germina Lukuvi anasema pamoja na vituo hivyo kuwa na sehemu ya malazi kwa maalbino bado kumekuwa na changamoto ya sehemu za kujisomea na New Millennium Group itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.

RAIS KIKWETE NA MKEWE WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA BALOZI WA MALAWI MAREHEMU MHE. FLOSSIE ASEKANAO CHIDYAONGA JIONI HII DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa  heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia na maafisa wa ubalozi wa Malawi  alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AUNGANA NA WAUGUZI KUSHEREHEKEA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Baadhi ya Wauguzi wakila kiapo cha uaminifu na kutunza siri za wagonjwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha leo.
Baadhi ya wauguzi waliohudhuria sherehe za siku ya wauguzi duniani wakifuatilia kwa makini Hotuba ya mgeni rasmi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Arusha leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia waanguzi   na wananchi kwenye sherehe za waauguzi duniani ambazo kitaifa zimefanyika Mjini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MFUKO WA UBUNIFU NA MAENDELEO YA WATU (HDIF)

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu, unaosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu, unaosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Eng. George Mulamula, wakati alipowasili kuzindua  Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu, unaosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
   Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa na baadhi ya viongozi wa Costech, baada ya uzinduzi huo. Picha na OMR

NANI KUIBUKA NA MILIONI 20 KATIKA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014?

$
0
0


Wafuatao ni washiriki wa mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao sasa wapo kijijini Maisha Plus wakiwania zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tzshs. Milioni 20.


MS 01: Elinuru M. Pallangyo - Arusha
MS 02: Dorothy D. Pallangyo - Arusha
MS 03: Leah D. Mnyambugwe - Dodoma
MS 06: Martina G. Chitete - Iringa
MS 08: Grace G. Mahumbuka - Kagera
MS 10: Zinaida J. Kijeri - Kigoma
MS 11: Upendo M. Msuya - Kilimanjaro
MS 12: Neema U. Kivugo - Manyara
MS 15: Elizabeth Simon - Morogoro
MS 16: Joyce N. Hassan - Mtwara
MS 17: Bahati Muriga - Mwanza
MS 18: Thereza Kitinga - Mwanza
MS 20: Santina Mapile - Njombe
MS 21: Mary A. Ndasi - Rukwa
MS 22: Fredina M. Said - Shinyanga
MS 23: Esther Kulwa - Simiyu
MS 24: Mary J. Mwanga - Singida
MS 25: Doricus M. Shumbi - Singida
MS 27: Kuruthum R. Mwengele - Tanga

Kumpigia kura mshiriki umpendae, andika namba yake mfano MS 00 kisha tuma kwenda +255689666662 au mtandaoni kupitia: http://voting.maishaplus.tv/index.php/voting/mamashujaa

Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake. INALIPA.


DAR YAZIZIMA KUFUATIA KIFO CHA BALOZI FLOSSIE GOMILE CHIDYAONGA

$
0
0
DSC_0051
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi Haji Makame, akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili kuhudhuria misa maalum ya kumwombea aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini, Mh Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
DSC_0063
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi Haji Makame akibadilishana mawazo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dk Ishaya Samaila Majanbu (kushoto).
DSC_0099
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule na kulakiwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
DSC_0106
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisubiri kwenda kutia saini kitabu cha maombolezo kabla ya kuanza kwa ibada maalum ukumbini hapo. Kushoto ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
DSC_0110
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisaini kwa huzuni Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini, Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 mei 2014. Kulia ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
DSC_0116DSC_0123
Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila wakilia kwa uchugu pamoja na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole wakati wa misa maalum ya kumwombea aliyekuwa balozi wa Malawi nchini Tanzania Mh. Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.


DSC_0124DSC_0131
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisalimiana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole. Katikati ni Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila.
DSC_0138
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole (mwenye mtandio mweupe) akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania nje ya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
DSC_0146
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga ukiingizwa kwenye ukumbi tayari kuanza kwa ibada maalum na kutoa heshima za mwisho.
DSC_0167
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0169
Mchungaji akiongoza ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0184
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bi. Tonia Kandiero (kushoto) akiwa na baadhi ya mabalozi pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania wakati wa ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossi Chidyaonga iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
DSC_0186DSC_0189DSC_0191
Nyuso za simanzi zikiwa zimetawala ukumbini hapo.
DSC_0192DSC_0194DSC_0197
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria ibada msiba wa Balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0198DSC_0203
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard K. Membe (Mb) akiwa mwenye huzuni kubwa kwenye misa ya kumwombea marehemu Balozi Flossie Chidyaonga.
DSC_0206
Familia ya karibu ya marehemu ikiongozwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini, Mh. Chisiza (kulia).
DSC_0219
Huzuni, simanzi na majonzi vilitawala ukumbini hapo.
DSC_0221
DSC_0222
DSC_0264
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa karibu wa familia ya marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho.
DSC_0277
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa mkono wa pole familia ya balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0284
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
DSC_0289
DSC_0299
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero, akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
DSC_0308
Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga, akishindwa kujizuia wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
DSC_0318
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh. Filiberto Sebregondi, akitoa heshima zake za mwisho.
DSC_0324
DSC_0327
DSC_0333
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole, akitoa pole kwa wafiwa.
DSC_0382
DSC_0387
DSC_0394
DSC_0380
DSC_0410
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu,(wa tatu kulia) , Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga (wa pili kulia) wakati wa misa maalum ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
DSC_0407

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMNUSURU MBUNGE WA IGALULA MFUTAKAMBA BAADA YA WANANCHI WAKE KUMJIA JUU

$
0
0
Wakazi wa Kata ya Kizengi wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akizungumza nao,mara baada ya kuweka jiwe la msingi na  kuzindua Ofisi ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kata ya Kizengi,Wilayani Uyui mkoani Tabora,wakati wa ziara yake iliyoendelea mkoani humo.Kinana amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi ili kuchukua hatua na kuzishughulikia,aidha katika ziara hiyo Kinana pia ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

Ndugu Kinana amehutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano hadhara uliofanyika katika Kata ya Loya,ambapo kuliibuka sintofahamu ya baadhi ya mambo ikiwemo Mbunge wa Jimbo Igalula, Mhandisi  Athuman Mfutakamba kutokuwa na tabia ya kuwatembelea wananchi wake na kujua matatizo waliyonayo, hali iliyosababisha Wananchi wamzomee alipopanda jukwaani kuhutubia na kujibu maswali aliyoulizwa  ambapo ilibidi Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuingilia kati na kurejesha hali ya utulivu na kumtaka Mbunge wa jimbo hilo Mh,Athumani Mfutakamba kuwa na tabia ya kuwatembelea wananchi wake.

Aidha kauli hiyo imekuja,kufuatia Wananchi kulalamika wazi kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kutokubali utendaji kazi wa Mbunge huyo.Wananchi hao waliweka wazi kuwa Mbunge huyo amekuwa akipiga porojo tu kwa mambo mengi ,badala ya kuwasikiliza na kutatua matatizo yanayowakabili amekuwa akiingia mitini.

Wananchi hao wakatolea mfano wa  Zahanati ya Kata hiyo ambayo haina jokofu la kuhifadhia chanjo za watoto na Dawa,kwamba aliahidi kulishughulikia lakini hakuna utekelezaji uliofanyika hadi sasa,kama vile haitoshi Wananchi hao wakoangeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa Mbunge huyo aliwaahidi kuwaletea mnara wa mawasiliano ya simu za mikononi kwa muda wa siku 100,ambalo ndio tatizo kubwa kwa kata hiyo ya Loya,lakini hakulitekeleza mpaka sasa.

Hata hivyo katika kuweka mambo sawa kwa Mbunge huyo,katibu Mkuu wa CCM,Ndugu kinana aliwaeleza wananchi kuwa atawasaidia kufuatilia suala hilo la mawasiliano,na pia amewaahidi kuwanunulia jokofu hilo kwa wananchi wa Kata ya Loya wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye,akiwahutubia wakazi wa Kata ya Kizengi waliojitokeza kwa wingi,Wilayani Uyui mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Igalula,Mh.Athuman Mfutakamba,akieleza maendeleo ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa na chama cha CCM,kufuata Ilani ya chama hicho,katika Lijiji cha Loya,Wilayani Uyui mkoni Tabora.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kizengi wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya chama hicho na kuzungumza na wananchi.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Loya,Wilaya ya Uyui.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani) akisomewa taarifa fupi mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba mbili za waalimu wa Shule ya Sekondari Lutende,Wilayani Uyui mkoani Tabora.
Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Miyenze,ambapo paalibulika na hoja ya mgogolo mkubwa wa wafugaji na Wahifadhi uliodumu kwa muda mrefu.



Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi kenyew Ofisi ya CCM,kata ya Loya wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi na Mbunge wa Jimbo la Igalula,Athumani Mfutakamba, wakisalimiana na  baadhi ya vijana wa michezo mara walipowasili katika kata ya Loya,kwa ajili ya mkutano wa hadhara na wananchi.



Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Loya,katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo,Wilayani Uyui mkoni Tabora.
Katibu wa NEC,Itikadi Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akihutubia Wananchi,katika kijiji cha Loya,Wilayani Uyui mkoni Tabora.
Vijana wa Sungusungu wakicheza wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika kata ya Kizengi,wilayani Uyui kuweka na kuzindua Ofisi ya chama hicho na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Vijana wa Sungusungu na Baadhi ya Wazee wa Kata ya Kizengi wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake walipokuwa wakiwasili katika kata ya Kizengi,wilayani Uyui kuweka na kuzindua Ofisi ya chama hicho na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

BALOZI WA FINLAND NCHINI SINIKKA ANTILA AMTEMBELEA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO OFISINI KWAKE LEO

$
0
0
 Balozi wa Finland  Nchini Sinikka Antila akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kuwasili.

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akisisitiza jambo katika kikao hicho. Kati ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Finland katika masuala ya teknolojia,  uendelezaji wa rasilimaliwatu na usimamizi wa fedha

Balozi wa Finland Nchini Sinikka Antila (kulia) akizungumzia jinsi  nchi ya Finland ilivyopiga hatua kimaendeleo hususani katika sekta ya nishati pamoja na utayari wa nchi hiyo kushirikiana na nchi  ya Tanzania katika kuimarisha sekta za nishati na madini.

MUAKILISHI WA JIMBO LA KWAMTIPURA AHUTUBIA WANACCM JIMBONI KWAKE.

$
0
0
 Muakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma akiwahutubia wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali katika Mkutano wa hadhara kuhusiana na Mchakato wa Bunge la katiba huko katika jimbo la kwamtipura Zanzibar.
 Wanachama wa CCM wakishangilia na kuonesha ishara ya vidole viwili wakimaanisha Serikali Mbili wakati wa Mkutano uliohutubiwa na Muakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma huko katika Uwanja wa mpira wa Mkele Zanzibar. 
 Muakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan Juma akisoma baadhi ya Vifungu vilivyo muhimu kutoka katika Rasimu ya katiba alipowahutubia Wananchi na wana CCM wa Jimbo la Kwamtipura Zanzibar.



Muakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan Juma akipeana mikono na wananchi na viongozi wa CCM waJimbo la Kwamtipura baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara Mkele Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
Viewing all 46339 articles
Browse latest View live




Latest Images