Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia,wakazi wa Sikonge katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,wilayani Sikonge mkoani Tabora jioni ya leo,Kinana alizungumzia matatizo makubwa yanayowakumba wakulima wa zao la Tumbaku huku akionesha kabrasha la taarifa ya ukaguzi na uchunguzi wa chama cha Ushirika cha WETCO LTD,ambalo linaeleza namna wakulima wa Tumbaku walivyoibiwa mamilioni ya fedha.
Aidha,Wananchi wa Sikonge wameulalamikia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha uliofanywa na viongozi wa vyama vya ushirika,Kufutia taarifa ya ukaguzi na uchunguzi katika vyama hivyo vya ishilika,inaelezwa kuwa kiasi cha fedha milioni 28 zimefujwa,na kwamba wamekuwa wakicheleweshewa malipo ya fedha zao na pia kutolipwa kwa wakati,jambo ambalo limekuwa likiwakera wakulima hao na kuwarudisha nyuma katika suala zima la maendeleo.
Kinana aliongeza kusema kuwa vyama vya ushirika vimeanzishwa kwa wingi na wajanja wachache kwa ajili ya kujinufaisha wao na kuwanyona na kuwadhuruma wakulima wa Tumbaku,hivyo Kinana alisema kuwa amekisikia kilio cha wakulima hao,na ameahidi kuyafikisha malalamiko hayo kwa Rais Jakaya Kikwete na hatimaye kupatiwa ufumbuzi.
Wakazi wa mji wa Sikonge wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa CCM,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Sikonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM,mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye,akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Sikonge waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM,Wilayani humo mkoani Tabora jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Sikonge,Said Mkumba kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakumba wakulima wa zao la Tumbaku wilayani Sikonge mkoani Tabora,ambapo inaelezwa kuwa wakulima hao wamekuwa wakilaghaiwa,kudhulumiwa na kunyonywa na vyama vya ushirika.
Mbunge wa jimbo la Sikonge,Said Mkumba akiwahutubia wananchi wa sikonge jioni ya leo
Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba sita za kuishi vijana wa PathFinder Green City Wilayani Sikonge mkoani Tabora
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongezana na Mkuu wa Mkoa,Mh,Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye wakikagua mradi wa ufugaji kuku wa asili ikiwa ni sehemu ya mradi wa Vijana wa Path Finder Green City,Wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipeana mkono na Mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha PathFinder Green City,mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo madawati kutoka Shirika la Viwanda vidogo vidogo (SIDO),vyenye thamani ya shilingi milioni 15
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kwenda kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Mazinge wilayani Sikonge,kituo hicho kitakuwa kinatoa huduma mbalimbali kama vile wagonjwa wa nje,kuhudumia Wazazi na watoto,waja wazito,sehemu ya kuhifadhia maiti,Wodi ya Wanaume na nyinginezo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akielekezwa na vijana hao namna ya kuchambua tumbaku,na kupanga kulingana na ubora wake,katika ghala la kuhifadhia tumbaku hiyo,ambao pia ni mradi maalum wa vijana wapatao 70 katika kijiji cha PathFinder Green City,wilayani Sikonge,mkoani Tabora.
Mkufunzi wa Kilimo cha Tumbaku kutoka kampuni ya TLTC,Goodluck Mmasi akifafanua namna ya uhifadhi tumbaku kwenye maghala na namna inavyochambuliwa,Mradi huo ni wa Vijana wa PathFinder Green City,ambao wamekuwa wakijituma kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo na za ujenzi pia katika suala zima la kujikwamua na umasikini.
Kinana akishiriki ujenzi wa majengo sita ya mradi wa Vijana wa Pathfinder Green City kwa ajili ya kuishi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Vijana wa PathFinder Green City,katika kata ya Pangale Wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Vijana wa kijiji cha Path Finder Green City wakiimba mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndgu Kinana mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho na kukagua miradi mbalimbali,ikiwemo ya ufugaji nyuki,ulimaji wa zao la tumbaku,ufugaji wa kuku,ufundi aina mbalimbali,Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa.
Kinana akikagua jengo la Karakana la Mradi wa Vijana wa PathFinder Green City,katika kata ya Pangale wilayani Sikonge mkoani tabora jioni ya leo.
Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na mradi wa ufugaji nyuki wa vijana wa PathFinder Green City,katika kata ya Pangale wilayani Sikonge mkoani Tabora
Sehemu ya mradi wa Vijana wa Ufugaji Nyuki katika kijiji cha Path Finder Green City kilichopo katika kata ya Pangale,wilayani Sikonge mkoani Tabora,Vijana hao wana jumla ya Mizinga ya nyuki 600 maalum kwa ufugaji nyuki.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa leo na vijana wa chipukizi katika wilaya ya Sikonge akitokea wilayani Uyui kwa ziara ya siku 10 mkoani Tabora