Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

INTRODUCING BRAND NEW VIDEO_ MY GAL _PREZZO


Wamiliki wa Vyombo vya habari watakiwa kuheshimu taaluma ya habari

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akizungumza na Baadhi ya Wafanyakazi wa chumba cha habari cha Clouds Media wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari kwenye Vyombo vya habari. Kulia ni Mhariri Mkuu wa Clouds Media Joyce Shebe na Kushoto ni Mhariri wa Habari za Michezo Shaffih Dauda.
Mhariri Mkuu wa Clouds Media Joyce Shebe akieleza jambo wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari kwenye Kituo hicho katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene na Kushoto ni Mhariri wa Habari za Michezo Shaffih Dauda.
 Mhariri wa Picha wa Clouds Media Joachim Kanyopa akimueleza jamabo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari kwenye Vyombo vya habari.
Mtaalam wa Sauti na Taa wa Clouds Media Cyprian Kisheto akimueleza jamabo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari kwenye Vyombo vya habari.
===========    ========  =========
Na Jovina Bujulu-MAELEZO.

Wamiliki wa Vyombo vya habari nchini wametakiwa kutumia waandishi wa habari wenye Taaluma ya habari ili kuweza kuilinda taaluma hiyo. Wito huo umetolewa na Mkurungenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene wakati wa Ziara ya Kikazi aliyoifanya katika Kituo cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.

Mwambene Alisema kuwa kumekuwa kukiongeza kwa wimbi la wanahabarti wasio na taalum hali inayosababisha kudharaulika kwa taalum hiyo.

“me napenda kuwaasa wamiliki wa vyombo vya habari kuendelea kusisitiza uajiri wa watu wenye taalum husika na wale waliosomea masuala haya ya uandishi wa habari ikiwa ni njia ya kuimarisha na kuilinda taaluma hii” Alisema Mwambene.

Akizungumzia kuhusu waandishi wasio uwezo Mhariri Mkuu wa habari Bi. Joyce Shebe alisema kuwa baadhi ya vyuo vya habari nchini vimekuwa vikizalisha waandishi wasiokidhi viwango. Aidha aliongeza kuwa ofisi yao imekuwa na utaratibu wa kuwaendeleza wafanyakazi kwa lengo la kuwajendgea uwezo wa utendaji kazi katika Tasnia ya Habari nchini.

Ili kuhakikisha Tasnia ya Habari inakuwa wadau wa habari nchini wameombwa kuendelea kuishauri serikali katika masuala mbalimbali yatakayosaidia kuimarisha Tasnia hiyo.

MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU MKOA WA NJOMBE YAFANA, MKUU WA MKOA ATILIA MKAZO SUALA LA ELIMU

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akihutubia mamia ya wananchi waliofurika viwanja vya mabehewani wilayani Makete mkoani Njombe katika maadhimisho ya wiki ya elimu kimkoa.(Picha/habari na Edwin Moshi, Makete)
Licha ya serikali kuendelea kutatua changamoto lukuki katika sekta ya elimu nchini, wadau wa elimu mkoani Njombe wametakiwa kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake, ili kuinua kiwango cha elimu mkoani humo kwa kuwa ni agizo la serikali hasa katika mkakati wa matokeo makubwa sasa (BRN)

Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi ameyasema hayo wilayani Makete mkoani hapa katika maadhimisho ya wiki ya elimu kimkoa na kusema kwamba ushirikiano wa pamoja kila mtu kwa nafasi yake kutasaidia kuzidi kuinua kiwango cha elimu kwa mkoa wake

Mh. Msangi amesema suala la kuongeza kiwango cha ufaulu ni la kila mmoja hivyo kuagiza maafisa elimu wilaya zote za mkoa huo kupita kwenye kila shule za sekondari na msingi kubaini changamoto zinazopelekea wanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani yao, na kuwashirikisha wazazi kwa kufanya nao kikao na baada ya hapo watagundua changamoto nyingi ambazo wataweza kuzitatua na zile zilizozidi uwezo wao watazipeleka sehemu husika ili zitatuliwe

"Nyie maafisa elimu wa wilaya zote, nawaagiza tembeleeni shule zenu hasa zile zinazofanya vibaya, mtagundua changamoto nyingi sana, pia muwashirikishe wazazi kwa kufanya nao kikao na muandike kwenye muhtasari maana mwisho wa mwezi huu nitaihitaji ili nione kama mmetekeleza, nawahakikishieni mtagundua mambo mengi sana huko" amesema Msangi

Amesema kwa sasa wanafunzi 538 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu bado hawajaripoti hivyo kutoa agizo kuwa wanafunzi hao watafutwe popote walipo ili waripoti shuleni tayari kwa masomo
 Mwanafunzi Noela Msinangila akisoma risala.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake mkoani Njombe, Noela Msinangila amesema wanaipongeza serikali kwa kuongeza idadi ya waalimu kila mwaka, kuongeza vitabu, kujenga mabweni pamoja na nyumba za waalimu huku wakiomba serikali kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa, kuongeza idadi ya waalimu wa sayansi na hisabati, pamoja na kuwasaidia wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Naye afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro amesema mkoa wa Njombe umejipanga vilivyo katika kuinua kiwango cha elimu siku hadi siku kulingana na mipango iliyowekwa ikiwemo kuhskikisha wanafunzi wanasomea katika mazingira mazuri
 Afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro akisoma taarifa ya elimu kimkoa.

Bw. Nyasiro amesema kwa sasa watahakikisha shule zote katika mkoa huo zitatoa chakula kwa wanafunzi wake kwa kuwa itasaidia wanafunzi hao kuzingatia masomo ipasavyo wawapo darasani, pamoja na kutoa zawadi kwa shule 10 za sekondari na msingi zinazofanya vizuri kimkoa kama motisha katika kuinua elimu

Katika maadhimisho pamoja na mambo mengine zimetolewa zawadi kwa shule 10 za sekondari na msingi zilizofanya vizuri pamoja na halmashauri 3 zilizoongoza kielimu

Msama Promotions yatangaza Viingilio Tamasha la Pasaka

$
0
0
Sehemu ya Umati wa watu uliohudhuria tamasha la pasaka mwaka jana katika uwanja wa Taifa.

KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, mwishoni mwa wiki iliyopita ilitangaza viingilio vya tamasha hilo litakalofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, viti vya kawaida ni shilingi 5000 na watoto 2000.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama viti maalum ni shilingi 20,000 wakati VIP  ni shilingi 10,000.Msama alisema hivi sasa wanaendelea na mchakato wa kufanikisha zoezi la mgeni rasmi katika tamasha hilo kwani hivi karibuni watakamilisha zoezi la upigaji kura kumchagua. Msama alisema mchakato wa kuelekea katika tamasha hilo litakalofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 20 na baadaye mikoa mingine saba hapa nchini.

Aidha Msama alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujiandaa na tamasha hilo ipasavyo kwani lina mlengo wa kurudisha mapato yanayopatikana na kuyapeleka katika maeneo matatu ambayo yanawahusu, yatima, walemavu na wajane.

Msama alisema mipangilio yake ya kuwawezesha wenye uhitaji maalum ni kuwajengea kituo kitakachokuwa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambacho kitajulikana kama Jakaya Mrisho Kikwete, rafiki wa wasiojiweza.

KATIBU MKUU WA CCM,AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KIGOMA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM;Ndugu Kinana na Wananchi wakishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo  linalenga kusaidia katika kuhifadhi mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine katika ghala hilo utawasaidia  pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo  linalenga kusaidia katika kuhifadhi mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine katika ghala hilo utawasaidia  pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akifafanua jambo kwa Wananchi (hawapo pichani) walipokwenda kukagua kushiriki na kukagua ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.
Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Nkungwe wakifuatilia yaliyokuwa yanazungumwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Nkungwe,kuhusiana na tatizo la ufumbuzi wa mradi wa maji.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Nkungwe kuhusiana na mradi wa maji unaojengwa,ambao kwa sasa umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.
Ujenzi wa tanki hilo la maji kama lionekanavyo pichani.
Katibu Mkuu Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigoma vijijini.
Ndugu Kinana (wa tatu kulia),akishiriki kufukia mabomba ya mradi wa maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigima vijijini.Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kusaidia vijiji zaidi ya 30.
Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi mbalimbali (hawapo Pichani),wakati alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nkungwe kukagua mradi wa maji ambao umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha. Kinana amewaahidi wananachi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili mradi huo ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mjumbe wa NEC,Balozi Ally Karume akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kukagua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigoma vijijini.Mradi huo umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha,lakini pia Kinana amewahidi wananchi kulitafutia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na hatimaye mradi huo kukamilika na kuwasiadia wananchi mbalimbali wa maeneo hayo.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe, Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Baadhi ya Wanakijiji cha Mahembe wakiwa kwenye mkutano huo wa hadhara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopatiwa umeme na maji katika wilaya ya Kigoma Vijijini. Kikiwemo Kijiji cha Mahembe ambacho tayari kimepata umeme.
Mkutano wa hadhara ukiendelea kwenye kijiji cha Mahembe,Kigoma vijiji ambapo wananchi wengi walijitokeza kusikiliza yaliyokuwa yakisemwa kwenye mkutano huo.
Vijana wa bodaboda wakiwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na wanachama mbalimbali wa CCM,alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizunguma na baadhi ya Mabalozi mbalimbali wa CCM (hawapo pichani),kwenye kikao chao cha ndani,kilichofanyika katika ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .

Baadhi ya Mabalozi mbalimbali wa CCM,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Nduguu Kinana alipozungumza nao kwenye kikao chao cha ndani,kilichofanyika katika ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa emeongozana na Viongozi wengine wa CCM,Mkoa na Wilaya katika kukagua mradi wa  wajasiliamali wa Kilimo,ndani ya kijiji cha Kidahwe Kigoma Vijijini mkoani Kigoma.

DAKIKA 90 ZA DUNIA: Maadhimisho ya Kwibuka20, Washington DC

$
0
0
 Wiki kama hii, miaka 20 iliyopita, nchi ya Rwanda ilishuhudia kuanza kwa mauaji ambayo kwa siku 99 zilizofuata, yaliacha historia mbaya na ambayo itaendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.

Ndani ya siku 100, watu wanaokadiriwa kufika milioni 1 waliuawa katika mauaji ya kimbari.
Miaka 20 baadaye (mwaka huu), dunia nzima imeungana na Rwanda kukumbuka kile ambacho wengi wanaona kuwa kilitokea na kuachwa kuendelea kutokana na Jumuiya ya kimataifa kutoingilia kati na kutoa msaada muafaka kwa wakati muafaka.

Kumekuwa na matukio mbalimbali kukumbuka mauaji ya kimbari ya Rwanda ambayo yamefanyika duniani kote, Kutoka Kigali Rwanda mpaka hapa Dar-Es Salaam na hata huko Washington DC.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Aprili 12, 2014

IFC and CRDB Bank sign landmark $75 million loan agreement, commit to support SME and agribusiness sectors in Tanzania

$
0
0
Dr. Charles Stephen Kimei, Managing Director of CRDB Bank Group, speaks during a landmark $75 million loan agreement signing ceremony with the International Finance Corporation (IFC) aimed at providing support to small businesses, particularly those owned by women, as well as to farmers and agribusiness in Tanzania held at the IFC headquarters in Washington DC on Friday April 11, 2014 in the sidelines of  the World Bank-IMF Spring Meeting.
The IFC, a member of the World Bank Group, on Friday April 11, 2014 signed a landmark $75 million loan agreement with the CRDB Bank that will help provide much needed support to small businesses, particularly those owned by women, as well as to farmers and agribusiness in Tanzania.  In Tanzania, there is a significant financing gap for SMEs, and women-owned businesses are particularly disadvantaged with only 15% reporting having access to a bank loan. 

 Access to finance is critical to helping them to grow their businesses and contribute to economic development. IFC and CRDB Bank will partner to focus on undeserved SME and retail market segments, as well as agribusiness producers and exporters. 

 Jean Philippe Prosper, IFC Vice President for Sub-Saharan Africa, said: “IFC is committed to partner with CRDB Bank to reach out to undeserved communities in Tanzania. This is the beginning of IFC’s collaboration with CRDB Bank and we hope to work more closely to support economic development and promote job creation in the country.” 

 “Working with IFC, we intend to strengthen our reach to SMEs and further promote agri commodity export. As a market leader in Tanzania, we have a mandate to support these market segments and are grateful to launch the collaboration with IFC,” said Dr. Charles Stephen Kimei, Managing Director of CRDB Bank Group. 

 The investment will promote financing for women-owned businesses, as well for farmers, capitalizing on CRDB Bank’s position as a leader in financial inclusion in Tanzania. IFC also plans to provide advisory services in the field of trade and warehouse financing to strengthen CRDB’s operations. 

 The signing ceremony took place in Washington DC during the World Bank-IMF Spring Meeting and was observed by the Finance Minister Hon. Saada Mkuya Salum, and other top officials from Tanzania's finance sector.

 The comprehensive investment package consists of a $40 million loan targeting SMEs, particularly those owned by women, including $6 million through IFC’s Global SME Finance Facility; a $10 million trade line through IFC’s Global Trade Finance Program and $25 million through IFC’s Global Warehouse Finance Program to support the agricultural commodity business, including $10 million from the Global Agriculture and Food Security Program’s (GAFSP) private sector window.
Dr. Charles Stephen Kimei, Managing Director of CRDB Bank Group (second left), and Mr. Jean Philippe Prosper, IFC Vice President for Sub-Saharan Africa, signing the landmark $75 million loan agreement at the IFC headquarters in Washington DC on Friday April 11, 2014 witnessed by the Chairman of the board of Directors Mr Martin  J. Mmari (left) and IFC's  Principal Operations Officer, Ms. Wendy Teleki (second right), and the Head of Blended Finance Ms. Kruskaia Sierra Escalante.
 Dr. Charles Stephen Kimei, Managing Director of CRDB Bank Group (second left), and Mr. Jean Philippe Prosper, IFC Vice President for Sub-Saharan Africa, shake hands after signing the landmark $75 million loan agreement at the IFC headquarters in Washington DC on Friday April 11, 2014


 Finance Minister Hon. Saada Mkuya Salum, speaks after the signing ceremony, flanked by  the Chairman of the board of Directors Mr Martin  J. Mmari (third left),  Dr. Charles Stephen Kimei, Managing Director of CRDB Bank Group (second right), IFC's Senior Investment Officer - Financial Markets, Mr Kariuki Thande (right) and CRDB's Deputy Managing Director  Mr. Saugata Bandyopadhyay (left)

Finance Minister Hon. Saada Mkuya Salum, the Chairman of the board of Directors Mr Martin  J. Mmari (third left),  listen to Dr. Charles Stephen Kimei, Managing Director of CRDB Bank Group (second right). Right is  IFC's Senior Investment Officer - Financial Markets, Mr Kariuki Thande (right) and CRDB's Deputy Managing Director  Mr. Saugata Bandyopadhyay (left)
Tanzania Government officials, CRDB top brass in a Group photo with IFC's officials after the signing ceremony.
For more photos CLICK HERE


KUFUATIA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR,DARAJA LA MAPINGA LABOMOKA.

$
0
0
Kufuatia mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar, Daraja la Boko lililopo Barabara ya Bagamoyo limebomoka na kufunga mawasiliano!

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ATEMBELEA MJI WA KIHISTORIA WA UJIJI,AKUTANA NA WAVUVI WADOGO WADOGO ZIWA TANGANYIKA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana nawananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake ya siku 5, Mwanga, Manispaa ya Kigoma, ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiingia kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Mjumbe wa NEC CCM kutoka Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kigoma leo. ambapo alisisitiza wananchi kuunga mkono Muungano wa Serikali mbili.

 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara huku akiponda vyama vya upinzani kwa tabia yao ya kila mara kupiga kelele bila kusaidia ujenzi wa miradi ya maendeleo nchini.
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamejifunika kwa nguo ili wasilowe na mvua wakati Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Kinana (wa pili kulia) na viongozi wengine wa CCM wakiwa jukwaani wakinyeshewa mvua sambamba na wananchi wakati wa mkutano huo wa hadhara. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa NEC CCM, Balozi Ali Abeid Karume, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaborou na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Peter Serukamba.
 Ndugu Kinana akihutubia huku mvua kubwa ikinyesha wakati wa mkutano huo
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamejikinga mvua kwa viti huku wakiendelea kumsikiliza Ndugu Kinana
Kinana na viongozi wengine wakiondoka baada ya mkutano kumalizika huku wakiwa wamelowa chapachapa kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM (tatu kulia),Ndugu Kinana pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM,Mkoa na Wilaya wakipata maelezo mafupi kuhusiana na historia ya mnara huo,ambao Dr.Livingstone na Henry M.Stanley walikutana kwa mara ya kwanza katika mji wa Kihistoria wa Ujiji mkoani Kigoma katika suala zima la kusambaza dini na kupambana na biashara ya Utumwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mama Mawazo Rashid Mawala mkazi wa Ujiji Kigoma ,Katibu Mkuu alikuwa akitembea kwenye njia (route) iliyotumika na Watumwa ambapo kuna miembe yenye umri zaidi ya miaka 150,miembe kama hii inapatikana sehemu ya ya Tabora na Bagamoyo. 
 Sehemu ya njia (route) kama ionekanavyo pichani ndani mji wa kihistoria Ujiji mkoani Kigoma,iliyotumika kusafirishia Watumwa kwenda sehemu mbalimbali,katika njia hiyo kuna miembe inayoelezwa ina umri zaidi ya miaka 150 tangu kupandwa kwake,na inaelezwa inapatikana sehemu ya Tabaro na Bagamoyo.  
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Masoud Mwinyi Chande kwenye mnara wa kumbukumbu ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Inaelezwa kuwa Nyumba hiyo Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.Kulia ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba,Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,pamoja na Mwenyekiti wa CCM-Kigoma Ndugu Amani Kabouru.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akielekezwa sehemu ya Chumba na mlango ndani ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Nyumba hiyo inasemekana Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa,wakiwasilia kwenye Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma na kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria yaliyomo ndani ya jengo hilo. 
 Mmoja wa wakazi wa eneo la Kibiri,ambalo liko ufukweni kabisa mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma,akibandika mabango yake yenye ujumbe wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,alipokwenda kutembelea eneo hilo na kusikiliza kero mbalimbali za wavuvi wadogo wadogo.
 Baadhi akina Mama ambao ni wafanyabiasha wa samaki na dakaa pamoja na uvuvi wakiwa wamekusanyika wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa ajili ya kuwazisilisha kero zao mbalimbali ikiwemo tozo za kodi na ushuru mkubwa ikilinganishwa na kipato chao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma bango lenye ujumbe wa kulalamikia kodi kubwa  wanazotozwa wavuvi wadogowadogo wa Kibirizi,Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibirizi mkoani Kigoma ambao wanakilio cha kutozwa kodi kubwa, kuvamiwa na majambazi wakati wa shughuli zao za uvuvi.
 Katibu Mkuu,Ndugu Kinana akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Ofisi mpya ya CCM,kata ya KIbirizi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza kwenye kikao cha Mabaraza ya Jumuiya zote (CCM) katika ukumbi wa Kibo Peak Club,Wilaya ya Kigoma mjini mkoani humo,ambapo Kinana walizungumza mambo mbalimbali ya kutekeleza na kuhimiza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010,pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.
Pichani Kati ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (shoto) wakati wakielekea kutazama Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma,kulia ni a Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye.

VIDEO: RAY C: NEW SONG TEASER: LEGENDARY MUSIC-STUDIO

$
0
0
Ray C akiwa ndani ya Legendary Music Studio akirekodi moja kati ya nyimbo zake Mpya. It was a good experience working with such a Big Tanzanian and East African Female Artist. Stay tuned for more good music from Legendary Music-Tanzania stay tuned kwa Ujio Mpya wa Ray C.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 30 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE WILAYANI MONDULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameketi na wajane wa hayati Edward Moringe Sokoine pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa katika misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.
Mhe. Rais akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim nae akiweka shada la maua.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa nae akiweka shada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Dk Mukangala Aipongeza NSSF Kuviunganisha Vyombo vya Habari

$
0
0
Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kikombe mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa. Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kikombe mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa.Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 4 baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa. Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 4 baada ya timu hiyo kuibuka mabingwaNaibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu. Wengine ni viongozi wajuu wa NSSF wakishuhudia. Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu. Wengine ni viongozi wajuu wa NSSF wakishuhudia.Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited akionesha kitita cha shilingi milioni 4 na Nusu mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu. Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited akionesha kitita cha shilingi milioni 4 na Nusu mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu.Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited akionesha kombe juu mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi. Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited akionesha kombe juu mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmiBaadhi ya wachezaji wa Business Times Limited wakishangilia kikombe na kitita cha shilingi milioni 4 na Nusu mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu.  Baadhi ya wachezaji wa Business Times Limited wakishangilia kikombe na kitita cha shilingi milioni 4 na Nusu mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu.


Nahodha wa Timu ya Mwananchi kulia akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi, kikombe hicho ni cha mshindi wa nne. Nahodha wa Timu ya Mwananchi kulia akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi, kikombe hicho ni cha mshindi wa nne.[/caption] [caption id="attachment_45117" align="aligncenter" width="452"]Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Abubakar Rajabu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Abubakar Rajabu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.[/caption] [caption id="attachment_45110" align="aligncenter" width="640"]Mwakilishi wa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akitembelea banda la NSSF lililopo kwenye mashindano hayo kupata maelezo anuai. Mwakilishi wa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akitembelea banda la NSSF lililopo kwenye mashindano hayo kupata maelezo anuai.[/caption] [caption id="attachment_45108" align="aligncenter" width="640"]Meza kuu ikifuatilia mechi anuai za fainali ya Mashindani ya 11 ya NSSF yanayoshirikisha vyombo vya habari anuai katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete kwa wasichana. Meza kuu ikifuatilia mechi anuai za fainali ya Mashindani ya 11 ya NSSF yanayoshirikisha vyombo vya habari anuai katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete kwa wasichana.[/caption] [caption id="attachment_45112" align="aligncenter" width="480"]Baadhi ya wachezaji wa timu ya Changamoto wakipata picha na kikombe chao cha mshindi wa pili mpira wa miguu. Baadhi ya wachezaji wa timu ya Changamoto wakipata picha na kikombe chao cha mshindi wa pili mpira wa miguu.[/caption] [caption id="attachment_45109" align="aligncenter" width="413"]Mechi ya fainali kati ya Business Times Limited na Habari ya Zanzibar mpira wa pete ikiendelea. Mechi ya fainali kati ya Business Times Limited na Habari ya Zanzibar mpira wa pete ikiendelea.[/caption] [caption id="attachment_45107" align="aligncenter" width="640"]Meza kuu ikifuatilia mechi za fainali ya Timu ya mpira wa pete kutoka Habari, Zanzibar ikipata picha ya ukumbusho. Meza kuu ikifuatilia mechi za fainali ya Timu ya mpira wa pete kutoka Habari, Zanzibar ikipata picha ya ukumbusho.[/caption] [caption id="attachment_45120" align="aligncenter" width="640"]Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited (wenye jezi bluuu) ya  wakilisha Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited (wenye jezi bluuu) ya wakilisha[/caption] WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuviunganisha vyombo vya habari anuai nchini Tanzania kupitia tasnia ya michezo. Dk. Mukangala ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia kwa niaba ya waziri, alipokuwa akifunga rasmi Mashindani ya 11 ya NSSF yanayoshirikisha vyombo vya habari anuai katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete kwa wasichana. Dk. Mukangala alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa yakivikutanisha vyombo anuai vya habari kutoka Tanzania Bara na Visiwani hivyo kujenga uhusiano mzuri kwa washiriki kupitia michezo, huku yakiimarisha uhusiano kati ya vyombo hivyo na shirika la NSSF ambalo hudhamini mashindano hayo kila mwaka kwa muda wa miaka 11 mfululizo hivi sasa. "...Hakuna ubishi kwamba miaka 11 sio michache kwa kuendesha mashindano kama haya, lakini kwa sababu uongozi wa NSSF unaheshimu na kukubali nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha jamii ni wazi kwamba mtaendelea kutenga bajeti ya mashindano haya kila mwaka," alisema Dk. Mukangala. Aidha aliwapongeza washindi wa mwaka huu kwa jitihada na nidhamu ya mchezo waliozionesha hadi kufanikiwa kutwaa ushindi, hivyo kuwataka wanahabari wote kuendelea kuyatumia mashindano hayo kwa kujenga mahusiano mazuri na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Mwaka huu timu ya Kampuni ya Bussnes Times Limited (BTL) imefanikiwa kutwaa kombe la mpira wa miguu na kuzawadiwa fedha shilingi milioni nne na nusu baada ya kuishindilia Changamoto mabao matatu kwa mtungi, nafasi ya pili ilichukuliwa na timu ya Changamoto na kujinyakulia kikombe pamoja na kitita cha shilingi milioni tatu na nusu. Mshindi wa tatu mpira wa miguu imeibuka timu ya wenyeji wa mashindano hayo NSSF baada ya kuifunga timu ya Mwananchi, hata hivyo NSSF walichukua kikombe na kusamehe kitita chao cha shilingi milioni 2 kilichokabidhiwa mshindi wa nne, yaani Timu ya Mwananchi. Neema ya mashindano hayo mwaka huu iliiangukia kampuni ya BTL ambapo kwa upande wa mpira wa Pete pia timu ya wasichana ya kampuni hiyo ilifanikiwa kutwaa ubingwa na kukabidhiwa kombe na fedha shilingi milioni 4, nafasi ya mshindi wa pili imechukuliwa na timu ya Habari kutoka Zanzibar na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni tatu na nusu. Washindi wa tatu mpira wa pete imeibuka timu ya NSSF ambao walitwaa kombe bila fedha ambazo zilichukuliwa na mshindi wa nne (Mwananchi). Kikombe cha nidhamu kimenyakuliwa na timu ya Tumaini wamiliki wa Redio na TV Tumaini pamoja na gazeti la Tumaini Letu. Jumla ya timu 20 za mpira wa miguu na 18 za mpira wa pete zimeshiriki mashindano hayo kwa mwaka huu idadi ambayo inazidi kuongezeka kila mwaka tangu kuanza kwa mashindano hayo. Hafla ya kufunga mashindano hayo iliyofanyika katika viwanja vya Sigara (TCC) jijini Dar es Salaam pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Abubakar Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau viongozi waandamizi wa shirika la NSSF pamoja na wageni mbalimbali waalikwa.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AWASILI SALAMA MKOA WA KATAVI USIKU HUU AKITOKEA KIGOMA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo,Kinana umepotewa ziwa la Tanganyika,jambo amabalo si la kweli na la kizushi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaaf Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,na Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake (hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye bandari ya Karema mkoani humo usiku huu.Kinana ameongoza na Katibu Wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanal Issa Machibya,Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Kigoma ndugu Kabouru na wengineo.
 Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.



















SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAINGIA SIKU YA PILI MKOANI DODOMA, MCHUJO KUANZA KESHO

$
0
0
Mmoja wa washiriki wa Shindano la kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania, lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) Bw  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kwa zoezi la usaili katika shindano la TMT.
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya Kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji wakiwa katika mstari tayari kwa kupewa fomu ya usaili ili kuweza kushiriki kwenye shindano la TMT.
 Baadhi ya washiriki waliofika katika ukumbi wa African Dream kwaajili ya usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya shindano hilo ambalo kwasasa linaendelea Katika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma.
Kundi la kwanza likiwa tayari kwaajili ya kupewa namba za ushiriki mara baada ya kumaliza zoezi zima la kujaza fomu za ushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Mkoani Dodoma leo ikiwa inawakilisha Kanda ya Kati.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.

Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.
Shindano la Tanzania Movie Talents leo limeingia siku ya pili ya usaili mkoani Dodoma, Kanda ya Kati ikiwa na washiriki waliojitokeza zaidi ya 600. Shindano hili limeibua hisia za Watu wengi kutokana na Umahiri wake na kuwa shindano la kwanza kutokea Afrika Mashariki na Kati huku maandalizi yake yakiwa yamefanyika kwa umakini wa hali ya juu huku Majaji wa Shindano hilo wakitokea kuwa Vivutio vikubwa kwa washiriki hao kutokana na jinsi wanavyotoa Uamuzi.

Washiriki zaidi ya 600 wameweza kujitokeza kushiriki shindano hili ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na mpaka sasa zoezi hili limeingia siku ya pili ambapo timu ya TMT imeendelea kusaili vijana waliojitokeza.

Safari ya Mchujo wa shindano hili kwa kanda ya kati ambapo shindano hili linafanyika mkoani Dodoma utaanza kufanyika kesho Jumatatu ili kuweza kupata washindi watatu bora ambao kila mmoja atajiondokea na Kitita cha Shilingi laki tano (500,000) kwa kila mshindi na baadae kujiunga na washindi wengine wa kanda zilizobakia Kwaajili ya fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na kupelekea Mshindi kujinyakulia zawadi kubwa kabisa ya Kitita cha pesa za Kitanzania Milioni 50 (50,000,000/=) na vilevile washindi kumi bora katika fainali hiyo watakuwa chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions na watafanya kazi ya pamoja na hatimaye kazi yao kuweza kuuzwa nchini nzima na wao kunufaika na kazi hiyo.

Shindano hili linaloendelea kufanyika mkoani Dodoma linatarajiwa kumalizika mnamo Jumanne ya 15 April 2014 na siku hiyohiyo Washindi watatu watatangazwa. Baada ya shindano hili kumalizika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma, shindano litaelekea Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya kwaajili ya vijana kuweza kuitumia fursa hii kwaajili ya kuonyesha Uwezo na vipaji vyao katika Kuigiza.

Katika Shindano hili vijana wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuitumia fursa hii na hatimaye kuweza kuonyesha vipaji vyao kwa maana huu ndio muda wao. Hakuna viingilio katika shindano hili na fomu zinapatikana bila gharama yoyote ile.

JAMII IMETAKIWA KUTUMIA VYAKULA VINAVYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA KUBORESHA AFYA ZA FAMILA ZAO

$
0
0
DSC_0494
Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole, akiendesha mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi uliopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Na Mwandishi wetu.

Wito huo umetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole katika semina ya siku nne kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii iliyomalizika mwishoni mwa katika ukumbi wa Kartasi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kidole alisema kuwa ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia vyakula vile vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri vyakula vya msaada kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.

Hayo yamezungumzwa katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa Msaada wa Dharura yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio jamii yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa mada ya Usalama wa Chakula nchini.
DSC_0482
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada wa chakula kwa wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika maeneo husika.

Aidha Kidole amesema kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ni nafaka ambayo hayawezi kuboresha afya zao. Katika halmashauri za mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula, viongozi wa ngazi husika hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao mengi yanayohimili hali ya hewa husika na kwa wakati mwafaka ili kupunguza tatizo la upungufu wa chakula katika maeneo yao. Ni kwa namna hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa chakula cha msaada na badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.


DSC_0534
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa Redio jamii ya namna ya kuandaa jedwali maalum kwa ajili ya kuibua masuala katika utayarishaji wa vipindi kwenye mafunzo ya siku 4 yaliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
DSC_0468
Msimamizi wa huduma za hali ya hewa kwa jamii kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Hellen Msemo, akitoa mafunzo ya namna ya kuripoti taarifa sahihi za hali ya hewa kwa jamii kwa jamii na kuwaasa kuepuka upotoshaji wa taarifa za uongo kutoka kwenye vyombo visivyohusika zaidi ya mamlaka hiyo.
DSC_0431
Baadhi ya waandishi na watangazaji wa redio za jamii nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO ambayo yamemalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
DSC_0506
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pambazuko FM, Goodluck Msowoya, akielezea uzoefu wake kwa washiriki wenzake wakati wa mafunzo hayo ambapo amewataka kuwa na uthubutu kwa manufaa ya jamii.
DSC_0444
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pangani FM, Mwajabu Ali akiwasilisha kazi ya vikundi wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
DSC_0433
Mafunzo yakiendelea.
DSC_0545
Washiriki wakiwa katika vikundi kazi.

JAMII IMETAKIWA KUTUMIA VYAKULA VINAVYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA KUBORESHA AFYA ZA FAMILA ZAO

$
0
0
DSC_0494
Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole, akiendesha mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi uliopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Na Mwandishi wetu.

Wito huo umetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole katika semina ya siku nne kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii iliyomalizika mwishoni mwa katika ukumbi wa Kartasi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kidole alisema kuwa ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia vyakula vile vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri vyakula vya msaada kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.

Hayo yamezungumzwa katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa Msaada wa Dharura yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio jamii yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa mada ya Usalama wa Chakula nchini.
DSC_0482
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada wa chakula kwa wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika maeneo husika.

Aidha Kidole amesema kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ni nafaka ambayo hayawezi kuboresha afya zao. Katika halmashauri za mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula, viongozi wa ngazi husika hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao mengi yanayohimili hali ya hewa husika na kwa wakati mwafaka ili kupunguza tatizo la upungufu wa chakula katika maeneo yao. Ni kwa namna hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa chakula cha msaada na badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.


DSC_0534
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa Redio jamii ya namna ya kuandaa jedwali maalum kwa ajili ya kuibua masuala katika utayarishaji wa vipindi kwenye mafunzo ya siku 4 yaliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
DSC_0468
Msimamizi wa huduma za hali ya hewa kwa jamii kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Hellen Msemo, akitoa mafunzo ya namna ya kuripoti taarifa sahihi za hali ya hewa kwa jamii kwa jamii na kuwaasa kuepuka upotoshaji wa taarifa za uongo kutoka kwenye vyombo visivyohusika zaidi ya mamlaka hiyo.
DSC_0431
Baadhi ya waandishi na watangazaji wa redio za jamii nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO ambayo yamemalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
DSC_0506
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pambazuko FM, Goodluck Msowoya, akielezea uzoefu wake kwa washiriki wenzake wakati wa mafunzo hayo ambapo amewataka kuwa na uthubutu kwa manufaa ya jamii.
DSC_0444
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pangani FM, Mwajabu Ali akiwasilisha kazi ya vikundi wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
DSC_0433
Mafunzo yakiendelea.
DSC_0545
Washiriki wakiwa katika vikundi kazi.

NITETEE FOUNDATION YAZINDULIWA RASMI JIJINI MWANZA KUTETEA WANAWAKE NA WATOTO WANAOSHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU TANZANIA.

$
0
0
 Mtoto Veronica ambae ni mmoja ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu walioibuliwa na taasisi ya Nitetee akitoa ushuhuda wa maisha yake yeye na wadogo zake baada ya baba yao kufungwa jela kwa kesi ya mauaji na kasha mama yao kuwakimbia na kwenda kwa mwanaume mwengine. Kwa mujibu wa Veronica anasema baba yao amefungwa kwa kusingiziwa kwani siku mauaji hayo yakitokea baba yake alikuwa ndani anaumwa, na tukio hilo limezima ndoto zote za maisha yake na wadogo zake.

 1.   Meya wa Jiji la Mwanza Mh. Stanislaus Mabula (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) na kumpongeza Mkurugenzi wa Nitetee Foundation kwa moyo wake wa kujitoa katika kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum. Mh meya aliahidi kufanya kazi na taasisi hiyo katika lengo la kutetea watu wengi Zaidi ambae nae alichangia magodoro sita. Katikati ni Mshehereshaji wa hafla hiyo ambae ni Mtangazaji wa kituo cha Start TV Bi. Ivona Kamonte na msanii H-Baba.

 Baadhi ya misaada iliyoletwa na wageni waalikwa katika kusaidia familia zaidi ya 25 zilizo katika mazingira magumu chini ya taasisi ya Nitetee.

  Kina mama wa jiji la Mwanza walihudhuria hafla ya uzinduzi wa jiji la Nitetee Foundation katika Hoteli ya New Mwanza.

1.   Mama Tizeba (kulia), Mke wa Naibu Waziri wa Uchukuzi ambae alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Nitetee wakifungua kwa pamoja pazia na Bi Flora Lauwo (kushoto), Mkurugenzi na Muasisi wa Nitetee Foundation kuashiria uzindizu rasmi wa taasisi hiyo katika hafla iliyofajiaka Jumapili Jioni katika Ukumbi wa New Mwanza Hotel, jijini Mwanza.



Nguvu imeongezeka katika jitihada za kusaidia jamii ya wanaoishi mazingira magumu hapa nchini baada ya kuzinduliwa taasisi inayojishughulisha na kutoa misaada ya kibinaadamu kwa wanawake na watoto walio kwenye mahitaji makubwa hasa jamii ya vijijini na nje ya miji, inayojulikana kama NITETEE FOUNDATION toka jijini Mwanza. 
 Shirika hilo la maendeleo kwa ajili ya wanawake na watoto nchini Tanzania lilizinduliwa usiku wa Jumapili na mgeni rasmi ambae alikuwa ni mke wa Naibu Waziri wa Uchukuzi Mama Charles Tizeba katika ukumbi wa New Mwanza Hotel, iliyopo jijini Mwanza. 
Tukio hilo la aina yake lilipendezeshwa na wenyeji wa mkoa wa Mwanza pamoja na watu maarufu kadhaa, viongozi wa vyama na jiji la Mwanza akiwemo Stanislaus Mabula, Mwanamuziki Stara Thomas na H-Baba, Katibu CCM mkoa wa Mwanza Bi Joyce Masunga. 
Akiongea na wageni walihudhuria katika uzinduzi huo Mgeni rasmi ambae ni Mke wa Waziri wa Uchukuzi Mama Charles Tizeba aliwasihi wanawake nchini kutunza familia zao na kutowaacha wakaitwa watoto wa mitaani. 
 “Wimbi hili la watoto mpaka hii leo hata wengine kufikia hatua ya kuwaita watoto wa mtaa kana kwamba wanazaliwa na mitaa tuna uwezo wa kuliondoa endapo tu, wakina mama tutasimamia kwanza misingi ya walezi, ama wazee wetu kwa kurudisha dhana ya ‘MTOTO WA MWENZIO NI WAKO PIA” alisema mama Tizeba na kuhoji “haya maneno ya sugar mamy, sugar dady, sijui vidumu, wamama haya maneno yanatoka wapi?”
 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa NITETEE Foundation Bi. Flora Lauwo amesema kwamba Taasisi ya NITETEE imekuwa ikifanya shughuli zake za kuwasaidia watoto kutoka familia zenye kipato cha chini vijijini na pembezoni mwa mji ili waweze kupata fursa ya kupata elimu pamoja na wanawake kupata fursa za kujikwamua kiuchumi. “Malengo yetu ni kutoa na kuongeza kasi ya maendeleo hapa nchini hasa katika sekta ya elimu. 

Hivyo basi miradi yetu italenga kuhamasisha jamii ya kipato cha chini ambao hawawezi kuwapatia elimu watoto wao hasa maeneo ya vijijini na pembezeno mwa miji na kupunduzo matatizo ya moja kwa moja kwa jamii hizi pamoja na matatizo ya saikolojia wanazokumbana nazo watoto, vijana pamoja na wanawake” alisema Mkurugenzi wa Nitetee Bi. Flora .
 “Lengo la Ntetee ni kufikia jamii zote za Tanzania nzima, kwa kuanza tumeanza moja kwa moja kwenye ngazi ya familia ambapo tunamgusa mototo na mama ama mlezi ambaye anasimamia kuleta ustawi wa mtoto huyu, tutahangaika kwanza kubaini hizo familia zenye kusongwa na uduni wa maisha usio na msaada, baada ya kujiridhisha tutaambatana na familia hizo kushirikisha watanzania wengine kuona uhitaji huo ili kuweza kusaidia kwa namna Mungu anavyotuwezesha watu wake.” aliongeza Bi. Flora.

 Bi Flora alimalizia kwa kusema kwamba “Kwa kuanzia taasisi hii mpaka sasa tumetembelea familia 25 zote za kutoka hapa jijini mwanza, kati ya hizo familia baada ya kuridhia, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kutoa msaada ambao tulishirikiana na marafiki wachache tuliokuwa tukizungumza nao juu ya hizo familia na kutoa mahitaji muhimu naya karibu kwa kadri tulivyoweza kwa baadhi tu ya hizo familia” .

MKURUGENZI ALEX MSAMA ANAENDELEA VIZURI

$
0
0

Minister for Finance and CNN talk Investment and Entrepreneurship as Tanzania Union Celebrations Approach

$
0
0

Hon. Saada Mkuya Salum, Minister for Finance (centre) and Tanzania's Ambassador to the United States Hon Liberata Mulamula (right) with CNN International's Producer Brian MacBride at the Tanzania embassy in the US in Washington DC
Hon. Saada Mkuya Salum, Minister for Finance prepares for the interview with CNN International's  Producer Brian MacBride
Hon. Saada Mkuya Salum, Minister for Finance during the interview with CNN International's Producer Brian MacBride.

Hon. Saada Mkuya Salum, Tanzania's Minister for Finance. engages with CNN International on the role that the Government is playing in creating an environment that is conducive for investment in support of  Small and Medium Enterprises (SME's) and Start Ups. 

Central to the interview held at the Tanzania embassy in Washington DC in the US, was CNN's quest to know how Tanzania differentiates itself from other African countries in terms of fostering entrepreneurship and facilitating investment in support of innovation. Tanzania Start Up, an initiative of  the Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) was cited as an example of how The Government is working to incubate Start Ups. 

The Minister also alluded to how the Investment promotion agencies in Zanzibar and Mainland were working to improve the investment climate including publishing procedures and costs. The CNN interview was negotiated in London by the Tanzania Investment Centre (TIC). 

Content was provided by COSTECH and DAR Technohama. The tentative date for airing of the interview is May 2014 on CNN International's "Africa Start Up" Programme.

Huduma ya Airtel Money "Hatoki Mtu Hapa" yapokelewa vyema na watanzania

$
0
0
Wateja wa Airtel wameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia bidhaa na huduma zake husisani huduma ya Airtel Money kuwa ni bora na salama nchini

Huduma hii ijulikanayo kama "Hatoki Mtu Hapa" inawawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bila makato kwa kununua kifurushi cha wiki au cha mwenzi cha Bure Pack na pia kuwawezesha wateja kutuma pesa kwa nusu gharama ukilinganisha na ziwango vinavyotozwa sokoni. Ambapo kwa sasa Airtel ndio kampuni inayotoza viwango vya chini vya miamala ya pesa nchini.

Wakiongelea kuhusu huduma za Airtel, wateja wa Airtel jiji Dar es saalam walisema" tunafurahishwa na hufuma ya Airtel money kwani inatuhakikishia usalama wa pesa zetu

"huduma ya Airtel Money inamgusa kila mtanzania kwani kutuma na kupokea pesa ni kitu kisichokwepeka katika maisha yetu ya kila siku, na kama tunavyofahamu si salama sana kutembea na kiasi kikubwa cha pesa mfukoni, huduma ya Airtel Money ni mkombozi wa huduma za kifedha na usalama wa pesa zetu katika maisha ya sasa. Pamoja na huduma hii kutoa usalama pia inatoza viwango vya gharama zaidi yaani Nusu gharama inaleta unafuu na kutupatia ziada ambayo inatuwezesha kutumia pesa hizo kufanya mambo mengine ya muhimu" alisema Finora Fokasi mmoja wa wateja wa Airtel Money.

Kwa upande wake baadhi ya mawakala wa Airtel Money walithibitisha kuwa 'Hatoki mtu hapa' imepokelewa vizuri na wateja kwani tumeona ongezeko la wateja katika vituo vyetu wakija kufanya miamala ya pesa . Hii nikutokana na ukweli kwamba mteja ambaye angetozwa shilingi 7000 kutoa pesa kupitia mitandao mingine sasa kwa kupitia huduma ya Airtel Money "Hatoki Mtu Hapa" anatozwa shilingi 3500, niwazi kabisa kuwa punguzo la bei limekuwa kivutio hivyo kuongeza idadi ya wateja wa Airtel Money"alisema Paulo Msangi Mkazi
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images