Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 267 | 268 | (Page 269) | 270 | 271 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia nishati, Mhe. Charles Kitwanga katikati akisisitiza jambo wakati wa kikao na Mameneja wa Tanesco wa wilaya katika Mikoa ya Mtwara na Lindi (hawapo pichani).  Pamoja nae ni watendaji wakuu wa Tanesco Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kikao hicho kilijadili maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha umeme vijijini kupitia REA na namna ya kuvifikia vijiji ambavyo havijafikiwa katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya pili. 

   Baadhi ya Mameneja wa Tanesco wa Wilaya katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati nayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga  (hayupo pichani) wakati wa kikao. Mhe. Kitwanga alisisitiza ubunifu na kuhakikisha mameneja hao wanapunguza tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika Mikoa hiyo.

   Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme cha Tanesco- Mtwara  Mhandisi Didas Maleko ( wa pili kulia) akimwongoza Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Kitwanga kuangalia mitambo inayozalisha umeme katika kituo hicho. Kwa mujibu wa maelezo ya Maleko, kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha kiasi cha megawati 18. 
   Mhe. Naibu Waziri akitoka kuangalia maendeleo ya ujenzi wa bomba katika eneo la Somanga. Nyuma linaloonekana ni sehemu ya bomba la gesi la nchi 36 ambalo linaelekea  Dar es Salaam katika eneo la Kinyerezi likitokea Mtwara. 
  Msimamizi wa Kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia cha Somanga  Mhandisi .
  ========  =======  ======
  Wananchi Changamkieni Mradi wa REA – Kitwanga


  Na Asteria Muhozya, Mtwara

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga, amewataka wananchi waliopo katika vijiji vinavyopitiwa na Mradi wa kuunganisha Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme vijijini (REA) kuchangamkia fursa hiyo wakati ambao mradi huo unatekelezwa kwa kuwa gharama zake ni nafuu.


  Mhe. Kitwanga aliyasema hayo jana wakati wa kikao chake na Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Wilaya za Lindi na Mtwara  waliokutana kwa lengo la kujadili maendeleo ya mradi wa kuunganisha umeme  Vijijini katika Wilaya za mikoa hiyo unaosimamiwa na REA, ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuvifikia vijijii ambavyo bado havijafikiwa na mradi huo awamu ya pili.


  Aliongeza kuwa, wananchi walioko katika maeneo ya vijiji ambapo mradi wa REA awamu ya pili unatekelezwa, wanapaswa kuitumia fursa hiyo vizuri kwa kuwa gharama kubwa za kuunganisha umeme zimebebwa na serikali kwa kipindi hicho na endapo mradi huo utakapokamilika watatakiwa kulipa gaharama zote kama kawaida.


  Aidha, alizitaja gharama  hizo kwa kipindi cha utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya pili  kuwa ni kiasi cha shilingi 27,000/- ikiwa ni gharama ya kuunganishwa  ambayo ni  VAT  na gharama za fomu kiasi  cha shilingi 5000/-  


  Katika hatua nyingine Mhe. Kitwanga aliwataka Mameneja wa Tanesco kuhakikisha wanapunguza tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara  na kuhakikisha wanaweka mipango endelevu ya upatikanaji wa nishati hiyo kutokana na kwamba mikoa hiyo inatarajia kuwa na uwekezaji mkubwa vikiwemo viwanda vya sementi.


  Aidha, aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu na kuongeza kasi ya utendaji katika shughuli zao ili kurejesha imani ya wananchi kuhusu shirika hilo kwa kuzingatia kwamba, nishati hasa umeme ina mchango mkubwa katika shughuli zote za kiuchumi na maendeleo ya taifa.


  “ Lazima tuibadilishe Tanesco. Wananchi wanatakiwa waishangae tanesco kwa huduma nzuri na si vinginevyo. Sitaki umeme ukatike hovyo hovyo. Vaeni viatu mlivyopewa .Taswira ya tanesco lazima ibadilike”. Aliongeza Kitwanga.


  Halikadhalika, aliwataka mameneja hao kuhakikisha wanakusanya madeni kutoka kwa wadaiwa wote zikiwemo taasisi za serikali na watu binafsi ili kuwezesha shirika hilo kujiendesha na kuendelea kutoa huduma kwa wananachi. Hivyo, amewataka wateja wote wanaodaiwa na  shirika hilo kuhakikisha wanalipa madeni yao ili shirika hilo liendee kutoa huduma stahiki.


  Wakati huo huo, Meneja  Mwandamizi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahenge Mugaya alieleza kuwa, tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika mikoa hiyo linaweza kuzuilika na kuongeza kuwa, tayari  zoezi la kubadilisha nguzo mbovu limeanza na kuwekwa mpya. Vilevile, aliongeza kuwa, katika kukamilisha zoezi hilo, tayari watumishi zaidi wameongezwa kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya shughulli ya kubadilisha nguzo hizo.


  Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kituo cha Tanesco- Mtwara cha kuzalisha umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara , Mhandisi Didas Maleko,  wakati akitoa taarifa ya uzalishaji  umeme katika kituo hicho alieleza kuwa, kituo hicho kinazalisha  kiasi cha megawati 18 kutoka katika mashine tisa ambapo kila machine inazalisha kiasi cha megawati 2.

  .

  Katika hatua nyignine Mhe. Kitwanga alitembelea eneo la  wazi la makutano ya bomba la gesi la inchi 16  kutoka Songosongo na lile la inchi 36 linalotoka Mtwara kwenda Kinyerezi Dar es Salaam katika eneo la Somangafungu ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. Aidha, alitembelea kituo cha  kuzalisha umeme unaotokana na gesi asilia kilichopo Somangafungu ,kituo ambacho kina uwezo wa kuzalisha megawati 7.5. 


  0 0

  Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) wakiendelea na Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Mkutnao huo umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka (kushoto) akizungumza kwenye Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko,Mitaji na Dhamana (CMSA),Nasama Masinda akieleza jambo wakati Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA),Oaitse Ramasedi (wa tatu kushoto) akiongoma Mkutano huo unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa
   Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi.
   Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa
   Huu ni upande wa kutokea Mwenge kuelekea Posta ambapo Bajaji haziruhusiwi kuvuka hapo kuelekea Posta.


   Baadhi ya Madereva wa Bajaji na Boda boda wakijadiliana Juu ya swala hilo la kuzuiliwa kuelekea Posta

   Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa

    Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa  kwenda Posta wakitokea Mwenge
   Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa Mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.

  Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake  kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufanikiwa kuwanasa wengi.

  Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.

  "Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo"Hiace" pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa"  alimalizia kwa kusema "Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali" alisema Polisi huyo.

  Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo. 

  Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.

  Picha na Dar es salaam yetu

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani, Mhe. Martin O'Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania katika masuala ya uchumi, jamii na siasa. Mhe. Membe alipata fursa ya kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye upokeaji Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa Mwaka 2013.
  Mhe. Gavana O'Malley akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula
  Mhe. Waziri Membe akitoa salamu maalum kwa wajumbe kabla ya mkutano kuanza. Pembeni ni Mhe. Gavana O'Malley.
  Mhe. Membe akizungumza huku Gavana O'Malley akimsikiliza.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


   BONDIA KUTOKA THAILAND SUKKASEM KOKIETYONGYUTH
  BONDIA KUTOKA THAILAND SUKKASEM KOKIETYONGYUTH KUSHOTO AKIPOKEWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO KATIKATI NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' NA AGAPETER MNAZALETI
  BONDIA KUTOKA THAILAND SUKKASEM KOKIETYONGYUTH KULIA AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA PROMOTA MUSSA KOVA NA RAIS WA PST EMANUEL MLUNDWA NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
  BAADHI YA WADAU WALIOJITOKEZA KUWAPOKEA MABONDIA WAKIWA WANAZUNGUMZA 

  BONDIA KUTOKA THAILAND SUKKASEM KOKIETYONGYUTH
  BONDIA KUTOKA THAILAND SUKKASEM KOKIETYONGYUTH KUSHOTO AKIPOKEWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO KATIKATI NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' NA AGAPETER MNAZALETI
  Bondia kutoka Thailand Skkasem Kokietyongyuth kushoto na kocha wake Panyapari Ehot mwingine ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wakiwasili nchini kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Miyeyusho litakalofanyika P.T.A Sabasaba April 12 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia kutoka Thailand Skkasem Kokietyongyuth kushoto na kocha wake Panyapari Ehot mwingine ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wakiwasili nchini kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Miyeyusho litakalofanyika P.T.A Sabasaba April 12 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


  BONDIA KUTOKA THAILAND SUKKASEM KOKIETYONGYUTH AKIWASILI NCHINI KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE WA aPRIL 12 KATIKA UKUMBI WA PTA SABASABA
  Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Panyapari Ehot akitafuta zawadi mbalimbali kwa ajili  ya kuwapatia wenyeji wake waliompokea

  0 0  0 0

  Country Director, AMREF, Dr. Festus Illako cutting the ribbon during the AMREF Health Africa launch new identity. The frame Ceremony held yesterday April 10, 2014 AMREF office in Dar es Salaam, Tanzania.
  Country Director, AMREF, Dr. Festus Illako with Amref Health Africa staff during the new identity launch
  ---
  AMREF, the leading international African organisation in health today rebranded to Amref Health Africa after 57 years as the African Medical and Research Foundation.

  A key reason for the rebrand is to ensure that our name more accurately reflects the nature and scope of our work, which has grown beyond research and provision of basic medical services to strengthening of health systems through training and capacity building and strategic programming in areas such as maternal and child health, HIV, Water and Sanitation, TB and Malaria, and clinical and diagnostics services.

  “Our new name exemplifies our commitment to improving health in Africa through a wide a range of critical programmes and services so that we can achieve lasting health change for the people of Kenya and Africa in general,” said Director General Dr Teguest Guerma.

  Although we are rebranding, our focus remains the same: communities continue to be the primary beneficiaries of our work. Our rebrand will in effect put us in a more strategic position to continue working with our partners and aligning ourselves as an African-led and Africa-based health organisation seeking to meet the needs of the most vulnerable populations on the continent.

  Since 1957, Amref Health Africa has been providing health services to the most vulnerable communities, working in partnership with a cross-section of stakeholders including governments. With seven offices in Africa and 10 in Europe and North America, Amref Health Africa reaches over 30 countries with its work and has impacted the lives of millions of people living in hard-to-reach parts of Africa.

  0 0

   Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa  Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi ambapo naye alialikwa kuhudhuria hafla hii
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akifurahia baada ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi ambapo naye alialikwa kuhudhuria hafla hii

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akimshukuru Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adefuye baada ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akifurahia Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akimpa Naibu Spika Mhe Job Ndugai  Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.

   Naibu Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko Washington kwa zaiara ya kikazi akifurahia Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
  Kiongozi wa kwaya iliyotumbuiza katika hafla hiyo akiimba atika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, akiwa na Balozi Liberata Mulamula (kushoto)  baada ya sherehe  ya  kupokea  Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014. Picha na IkuluT

  0 0


  Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga akiongea na waandishi wa Habari(Hawapo pichani) mikakati ya kupunguza ajali za Barabarani ikiwemo kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kuendelea kununua vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kupunguza tatizo la ajali nchini,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga akiwaonyesha waandishi wa Habari(Hawapo pichani) vipima mwendo vya magari, Kushoto ni Kipima mwendo cha kisasa kinachotumiwa na jeshi hilo na kulia ni kipima mwendo cha zamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga akiwaonyesha waandishi wa Habari(Hawapo pichani) kitabu cha mwongozo cha askari kwa usalama barabara juu ya yale wanayopaswa kufanya na yale wanayokatazwa wawapo kazini, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia Kipima mwendo cha kisasa kinachotumiwa na askari wa usalama barabara, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano mkutano wa kikosi cha usalama barabarani, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Hassan Silayo)
  ========   =========
  Na Frank Mvungi


  Serikali yajipanga kuondoa ajali za barabarani hapa nchini kwa kushirikiana  na wananchi.

  Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama  Barabarani  Mohamed Mpinga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Akieleza kamanda Mpinga amesema kwa sasa kikosi cha usalama barabarani kinashirikiana na vituo vya redio vipatavyo 70 vilivyopo takribani katika mikoa yote hapa nchini.

  Akifafanua alisema kikosi chake kimekuwa kikiendesha vipindi vya Televisheni na pia kuendelea kutoa elimu mashuleni ili kuwajengea wananchi uelewa kuhusu sheria za barabarani.

  Kamanda Mpinga alisema mchakato wa kuanza kuweka nukta kwenye leseni (point system) kwa madereva watakaovunja sheria za usalama barabarani upo katika hatua za mwisho na tayari umeridhiwa na Wizara ya Katiba na Sheria.

  Pia Kikosi cha Usalama barabarani kimeongeza matumizi ya Tehama kudhibiti ulevi na mwendokasi ikiwa ni sambamba na kuhifadhi takwimu za matukio ya uvunjaji wa sheria kwa njia ya kielektroniki.alisema Kamanda  Mpinga.

  Kamanda Mpinga alisema Kikosi chake kimekwishatoa mwongozo wa utendaji utakaotumika na askari wa Kikosi cha usalama barabarani ukiwa na lengo la kuweka kiwango cha utendaji kinachofanana na chenye tija.

  Kamanda mpinga alibainisha kuwa Kikosi chake kimekuwa kikitoa elimu kwa madereva wa Bodaboda kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo waendesha bodaboda 4000 wameshapatiwa mafunzo.

  Katika hatua nyingine Kamanda Mpinga amesema Kikosi chake kimekuwa kikifanya utambuzi wa maeneo hatarishi (Black spot areas) kwa kutumia takwimu za matukio ya ajali za barabarani.


  Kikosi cha usalama barabarani kimeboresha taratibu za ukaguzi wa magari kwenye barabara kuu ili kudhibiti madereva wasiozingatia sheria  na kanuni za usalama barabarani.

  0 0

  Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay akimjulia hali mmoja wa akinamama aliyejifungua katika wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kibiti leo. Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay akimjulia hali mmoja wa akinamama aliyejifungua katika wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kibiti leo.Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay akitambulishwa kwa baadhi ya wahudumu katika wodi ya wazazi kwenye Kituo cha Afya Kibiti leo alipotembelea kuangalia mwenendo wa utoaji huduma za dharura katika kituo hicho. Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay akitambulishwa kwa baadhi ya wahudumu katika wodi ya wazazi kwenye Kituo cha Afya Kibiti leo alipotembelea kuangalia mwenendo wa utoaji huduma za dharura katika kituo hichod="attachment_45028Jengo ambalo ni chumba cha upasuaji linalotoa huduma za dharura kwa wajawazito katika Kituo cha Afya Kibiti. Jengo ambalo ni chumba cha upasuaji linalotoa huduma za dharura kwa wajawazito katika Kituo cha Afya Kibiti.[/caption] Mmoja wa akinamama aliyepatiwa huduma za uzazi katika Kituo cha Afya Kibiti kinachotoa huduma za dharura kwa akinamama wajawazito akizungumzia msaada wa huduma hiyo kwa wajawazito. Mmoja wa akinamama aliyepatiwa huduma za uzazi katika Kituo cha Afya Kibiti kinachotoa huduma za dharura kwa akinamama wajawazito akizungumzia msaada wa huduma hiyo kwa wajawazito.Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibiti, Chagi Jonas Lymo akizungumza na mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV alipotembelea kituo hicho pamoja na Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance). Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibiti, Chagi Jonas Lymo akizungumza na mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV alipotembelea kituo hicho pamoja na Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance).Baadhi ya akinamama wakipatiwa huduma katika kituo cha afya Kibiti leo. Baadhi ya akinamama wakipatiwa huduma katika kituo cha afya Kibiti leo.

  Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay (kulia) akizungumza na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibiti, Chagi Jonas Lymo katika kituo hicho leo Kibiti. Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay (kulia) akizungumza na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibiti, Chagi Jonas Lymo katika kituo hicho leo Kibiti.[/caption] MGANGA Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibiti, Chagi Jonas Lymo amesema uwepo wa huduma za dharura kwa wajawazito katika kituo hicho cha afya umesaidia kiasi kikubwa katika uokoaji wa maisha ya mamamjamzito pamoja na vifo vya watoto eneo hilo. Lymo ametoa kauli hiyo leo mjini Kibiti alipokuwa akizungumza na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa (The White Ribbon Alliance), Rose Mlay pamoja na Mkurugenzi wa World Lung Foundation walipotembelea kituo hicho kuangalia namna kinavyotoa huduma kwa wananchi na changamoto zake. Akizungumza zaidi, Lymo alisema tangu Kituo cha Afya cha Kibiti kuanza kutoa huduma za dharura kimekuwa msaada mkubwa kwa akinamama wajawazito eneo hilo na kwa sasa idadi ya akinamama wanaojifungulia eneo hilo imeongezeka mara tatu zaidi tofauti na ilivyo kuwa awali jambo ambalo unaonesha wamevutiwa na huduma hiyo muhimu kwa wajawazito. Alisema kwa sasa kituo hicho kinafanya upasuaji kwa matatizo yote ya uzazi kwa wajawazito, ikiwemo kutoa huduma za kuongezewa damu kwa wajawazito wenye mahitaji jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya mama mjamzito pamoja na mtoto mtarajiwa. "...Awali tulikuwa hatutoi huduma za upasuaji kwa akinamama wajawazito...tulikuwa hatuna chumba cha upasuaji hivyo tulitoa huduma za uzazi za kawaida, na ilipotokea matatizo kwa mjamzito tulimshauri kwenda ama kwenye hospitali ya Mchukwi (ya kulipia) ambayo ipo umbali wa takribani kilometa 15 au kwenda kwenye Hospitali ya Wilaya Utete ambayo ni kilometa 84 kutoka hapa," alisema. "...Baada ya kuanzisha huduma za upasuaji kwa akinamama wajawazito, akinamama waliokuja kujifungulia hapa waliongezeka..., mwezi wa kwanza tu wa kuanza kutoa huduma hizi wakinamama waliongezeka kutoka idadi ya wagonjwa 35 kwa mwezi waliongezeka hadi kufikia zaidi ya akinamama 100 kwa mwezi," alisema Lymo. Alisema kwa mwezi uliopita (Machi) jumla ya wajawazito 135 walifika kupata huduma za uzazi kiasi ambacho kwa sasa ni kikubwa na kinazidi uwezo wa kituo, jambo ambalo alishauri ipo haja ya kituo hicho kuongezewa mahitaji anuai ili kwenda sambamba na ongezeko la wateja wake kwa sasa. Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe nchini, Bi. Rose Mlay alisema serikali ikiamua kwa kushirikiana na wadau wengine inaweza kumaliza matatizo ya vifo kwa wajawazito pamoja na watoto kwa kusogeza huduma za dharura katika vituo vya afya ambavyo vingi vipo karibu na wananchi. "...Inawezekana kabisa kupambana na vifo vya akinamama wajawazito pamoja na watoto endapo Serikali ikijipanga na kuamua vituo vya afya viwekewe bajeti ya kutosha na hatimaye kuweza kutoa huduma za dharura kwa akinamama wajawazito na watoto," alisema Bi. Mlay. World Lung Foundation ndiyo taasisi iliyokiwezesha kituo cha Afya cha Kibiti kuweza kutoa huduma za dharura kwa akinamama wajawazito. Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi wa World Lung Foundation, Dk. Nguke Mwakatundu alisema taasisi hiyo imevisaidia jumla ya vituo 10 vya afya kutoa huduma za dharura pamoja na kuziwezesha hospitali nyingine tano katika nyanja tofauti kwenye utoaji huduma za afya. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengene wakiangalia jinsi watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mto Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi. Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka wa Tanzania na Burundi, alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma,Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
   Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya biashara upande wa Burundi. 
   Watu wote hao wakisubiri kuvushwa kwenye mto huo Malagalasi,kwa kimtumbwi kimoja ama kubebwa kama baadhi ya picha zinavyoonyesha
  Baadhi ya Wanahabari pichani Kulia Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania na Bwana Jongo kutoka gazeti la Uhuru wakionja joto ya kuvushwa kwenye mto wa Malagalasi ambao ndio sehemu ya mpaka kati ya Burundi na Tanzania.Kuonja adha hiyo hulipia kiasi cha fedha shilingi 500 mpaka 1000 kama nauli.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo kwa msisitizo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius walipokwenda kukagua  mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
  Msanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni kutoka Burundi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kibande, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
  Mbunge wa Jimbo la Manyovu wilaya ya Buhingwe,Mh.Albert Obama Ntabaliba akizungumza na Wanakijiji cha Kibande,kwenye mkutano wa hadhara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kibande,kwenye mkutano wa hadhara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD,Mkoa wa Makamba nchini Burundi,Bwa.Nishimwe Zen,kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
  Wanachama waliohamia chama cha CCM wakionesha kadi zao ambazo walimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,na kukabidhiwa kadi mpya za CCM.
  Sehemu ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM,wapatao zaidi ya 300 wakila kiapomara baada ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
  Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu wakishangilia jambo wakati katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu .
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Kamati ya Siasa Wilaya ya Buhingwe na kupata taarifa mbalimbali za maendeleo.
  Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius pamoja na Afisa Mipango,Charles Mduma wakitoa ufafanuzi mfupi kwa Waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya Maendeleo ya Wilya ya Buhingwe iliyotolewa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Manyovu-Wilaya ya Buhigwe.Mh Albert Obama,mara baada ya kumaliza kikao cha siasa cha wilaya 
  Baadhi ya Wakazi wa Buhigwe wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowasili wilayani humo mkoani Kigoma.
  Ndugu Kinana akizungumza jambo na baadhi ya Wananchi wa Buhingwe huku wakimsilikiza kwa makini.

  0 0

  Hatimaye kikosi kazi cha Proin Promotions Limited kimeshawasili mkoani Dodoma tayari kwa Kazi ya Kusaka vipaji vya kuigiza Katika Kanda ya Kati ambayo inawakilishwa na Mkoa wa Dodoma. Shindano hili linaendelea ambapo awali lilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza na hatimaye kupatikana kwa washindi watatu wa kanda ya Ziwa huku wakisubiri washindi wa Kanda nyingine kupatikana Kwaajili ya fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na mshindi mmoja kuibuka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.

  Timu nzima ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu na waendeshaji wa Shindano hili tayari wapo sawa kwa shughuli hiyo katika kanda ya kati. Zoezi la kusaka Vipaji vya Kuigiza katika Kanda ya Kati itafanyika Mkoani Dodoma ambapo litaanza tarehe 12 Aprili 2014 katika Ukumbi wa African Dreamz uliopo Area C Mjini Dodoma.

  Mpaka Sasa kanda zilizobakia ni Kanda ya Juu Kusini  ambapo Mkoa utakaowakilisha ni Mbeya, Kanda ya Kusini  usaili utafanyika Mkoani Mtwara, Kanda Pwani usaili utafanyika Mkoa Dar Es Salaam na Kanda ya Kaskazini usaili utafanyika katika Mkoa wa Arusha huku Mkoa wa Kigoma ukipewa upendeleo wa kuiwakilisha Kanda ya Ziwa tena ambapo tayari zoezi hilo ndipo lilipoanzia Mkoani Mwanza.

  Kabla ya Usaili wa kusaka Vipaji vya Kuigiza Kuanza Siku ya Ijumaa kutakuwa na Promotion Party itakayofanyika Katika Ukumbi wa Disco wa 84 kuanzia saa tatu usiku na kuendelea Wakazi wa Kanda ya Kati wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuonyesha Vipaji vyao na kuitumia fursa hii katika kukuza vipaji vyao

  0 0

  http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/10580-sikiliza-kipindi-cha-soko-la-habari-kariakoo.html#.U0dqX1dQ7U4

  0 0

   Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akikabidhi kompyuta 5 kwa Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba kwa ajili ya shule ya sekondari ya Pangani wakati wa makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo leo mjini Kibaha ambapo pia mwakilishi huyo alikabidhi kiasi cha fedha Taslimu  shilingi milioni 10,000,000 kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabala katika shule hiyo.katikati ni Mkuu wa shule hiyo Inocencia Mfuru(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBAHA)
   Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni 10,000,000 kwa Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara katika shule hiyo katikati ni Mkuu wa shule hiyo Inocencia Mfuru
   Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya makabidhiano.
   Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba wa tatu kutoka kushoto akiwa pamoja na wanafunzi wawakilishi wakati wa makabidhiano hayo, kutoka kulia ni Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises,Mkuu wa shule hiyo Inocencia Mfuru na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Jenipher Omolo.


   Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba pamoja na wawakilishi wa kampuni za RAN IT Solution na Lugumi Enterprises pamoja na wakuu wa shule ya Sekondari Pangani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo.
   Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Pangani wilayani Kibaha wakibeba kompyuta kwa ajili ya kukamilisha kazi ya makabidhiano shuleni hapo leo.
    Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akipokea cheti cha kutambuliwa rasmi kwa mchango wa kampuni hizo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba.
   Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano.

   Baadhi ya wanafunzi wakihojiwa na mwandishi wa habari Faraja Kihongole kutoka kituo cha Televisheni cha Chanel Ten.
   Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprisesna ,Ellygood Sangawe Meneja wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa wakitembelea maabara ya shule hiyo.
   Mkuu wa shule ya sekondari ya Pangani ya Kibaha  Inocencia Mfuru akitoa maelezo kwa wageni hao wakati walipokuwa wakitembelea maabara.
  Baadhi ya majengo ya shule ya Sekondari Pangani.

  0 0

  Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
   Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba kushoto ni bondia Gavad Zohrehvand wa Iran .  Baadhi ya Waandishi wa habari wakipata taswira mbalimbali za mabondia wakati wa kupima uzito.


  Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi katikati ni Promota Jay Msangi 
  Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mustafa Doto utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam .


  Na Mwandishi Wetu

  Mpambano huo wa raundi kumi utasindikizwa na mabondia Fransic Cheka na 
  bondia Gavad Zohrehvand wa Iran atakaecheza raundi 8
  mbali na mapambano hayo kutakuwa na mpambano mwingine utakaowakutanisha mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atakae pambana na Mustafa Doto mpambano wa Raundi sita pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi yatakayosindikiza mchezo huo
  katika ukumbi wa PAT Sabasaba Dar es salaam  

  Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
  Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
  pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

  0 0

  Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Mwenyekiti wa Bongo Movie(Steve Nyerere) na Single Mtambalike wakiwa pembeni ya Mkurugenzi wa Msama Promotions Limited Bw Alex Msama kwa ajili ya kumpa pole na kumfariji mara baada ya kupata ajali wakati akitokea Dar Es Salaam kuja Dodoma, ajali iliyotokea Ipagala Mwisho Kilometa chache tu kufika Dodoma Mjini.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.

  Mkurugenzi wa Msama Promotion, Bw Alex Msama amepata ajali leo, eneo la Ipagala mwisho wakati akitoka Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Dodoma, ajali hiyo imemuhusisha Dereva wa Bodaboda na gari la Bw Msama kugongana, Katika Ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.

  Akiongea na Mtandao wa Lukaza Blog, shuhuda ambae hakupenda jina lake kutajwa alisema "Gari la Bwa Msama lilikua likitoka Njia ya Morogoro Dodoma akielekea Dodoma Mjini wakati akiwa anaendesha gari, kuna bodaboda alikuwa akitokea Mjini Dodoma mara akaingia barabarani bila kuangalia mbele yake ndipo alipogongana na gari la Bw Msama".

  Mara baada ya ajali hiyo kutokea ,walifanikiwa kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupata Matibabu zaidi. Baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma walipokelewa vizuri na kupelekwa chumba cha X-ray kwaajili ya kuangaliwa na mara baada ya kumalizika kwa vipimo vya X-ray walipelekwa Wodi namba moja kwa ajili ya uangalizi wa madaktari na manesi.

  Hali ya wagonjwa wote inaendelea kuwa nzuri mara baada ya kupatiwa matibabu ya haraka na kupatiwa vipimo. Wagonjwa wote wamelazwa Wodi namba 1 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

  0 0

  Waziri Mkuu mstaafu na. Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akitembelea eneo la daraja la mto Kirurumo huko Mto wa Mbu lililoathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Balozi wa Canada nchini,Mh. Alexandre Leveque ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini,Mh.Alexandre Leveque ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa SAGCOT Fund Balozi Ami Mpungwe baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salam leo.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa watoto wa Marehemu Edward Sokoine aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Namelok Sokoine (MB) na Joseph Sokoine ambaye ni Afisa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Canada, kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine, yatakayoadhimishwa kesho April 12. Rais Jakaya Kikwete ataongoza maadhimisho hayo pamoja na marais na mawaziri wakuu wastaafu.
  Kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine.

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akionyesha simu ya Aina ya Samsung S5 mara baada ya kuzindua ofa itakayowawezesha wateja wake kununua simu hiyo na kujipatia vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe inayowawezesha wateja wake kununua simu ya kisasa ya aina Samsung S5 na kupata vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

  Akiongea wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” leo tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo inawawezesha kununua simu ya Samsung S5 na kupata dakika 1500 bure , SMS 5000 kutuma mitandao yote pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi katika mitandao kama vile facebook na twitter kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G yenye kasi zaidi. 

  Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya Samsaung S5”.

  Simu hii ya Samsung S5 inapatikana katika maduka ya Airtel yaliyopo Moroco, Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka yote ya Samsung pamoja na maduka yanayouza simu za smart phones yaliyoko nchi nzima.

  Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde

older | 1 | .... | 267 | 268 | (Page 269) | 270 | 271 | .... | 1897 | newer