Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 269 | 270 | (Page 271) | 272 | 273 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Hawa Ladha meneja miradi Serengeti breweries, Bw Evans Mlelwa meneja mawasiliano serengeti breweries na Bw Joseph Mkirikiti Mkuu wa Wilaya Songea wakizindua miradi ya maji Songea iliyogharimu zaidi ya millioni 140 hivi karibuni.
  Kampuni ya Bia ya  Serengeti Breweries kupitia mpango wake wa kusaidia jamii,imekabidhi rasmi mradi wa maji uliopo katika Kituo cha afya cha  Mletele  na kituo cha afya cha Tanga vilivyopo mjini Songea. Mradi huo umezinduliwa rasmi na Mkuu wa  Wilaya Mh. Joseph Mkirikiti ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo 

  Mradi huo wa maji ambao umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 140 za kitanzania unatarajia kukidhi mahitaji ya watu zaidi ya 100,000  wanaohudumiwa na vituo hiyo na jamii inayovizunguka.. Miradi hii kwa kiasi kikubwa utapunguza mfumuko wa magonjwa na vilevile vifo vya watoto na kina mama wajawazito. 

  Mradi wa Hospitali ya Mletele unajumuisha kisima , pampu ya maji ya solar na matanki ya kuhifadhia maji ya lita elfu kumi, na mradi wa Na mradi wa maji wa Hospitali ya Tanga  unajumuisha kisim na pampu ya maji ya solar. Visima hivi viwili vinaweza kutoa  lita 72,000 kwa siku. 

  Akiongea katika hafla fupi hospitalini Mletele , Bw. Mkirikiti amesema “ Nafarijika sana kuona hospitali hii sasa imepata suluhisho la tatizo la maji walilokuwa nalo hapo awali. Ningependa kuwashukuru sana Serengeti Breweries kwa juhudi zao katika kusaidia shughuli za kijamii na hasa katika upatikanaji wa maji safi na salama na hasa katika hospitali zetu.” 

  Kampuni ya Bia ya Serengeti wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama na tayari wamewezesha miradi mbalimbali ya maji kama vile Iringa – Hospitali ya Frelimo, Moshi – Hospitali ya Mawenzi, Dares salaam – Hospitali ya Temeke na ule wa Mkuranga na Sekou Toure mwanza.

  Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti , Bwana Evans Mlelwa , amesema “Suala la kuisaidia jamii kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti limepewa kipaumbele na uzito wa hali ya juu na hasa katika kusaidia upatikanaji wa maji safisalama  na pia endelevu.

  Serengetti Breweries inatambua umuhimu wa maji kwa binadamu na pia mchango wa maji katika maendeleo ya nchi, kiuchumi na kijamii. Tutahakikisha tunaendelea kuwekeza katika miradi ya maji kwa ajili ya jamii inayotuzunguka ili kuongeza ari ya uwajibikaji kwa maendeleo ya taifa letu na kwa ustawi wa kila mmoja wetu”,ameongeza Bw. Mlelwa.

  “Kampuni ya Bia ya Serengeti na EABL Foundation mpaka sasa tumeshawekeza zaidi ya milioni 500 za kitanzania , katika maeneo mbalimbali ambapo zaidi ya watu 450,000 wanafaidika na miradi hiyo”.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Muhidini Maalimu Ngurumo


  “ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Muhidini Maalimu Ngurumo ambaye mchango wake katika muziki wa dansi ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” 
  Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.  Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


  Imetolewa na

  Godfrey Mngereza

  Kaimu Katibu Mtendaji


  Baraza la Sanaa la taifa.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe, sehemu ya Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, wakati Makamu alipofanya ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo Aprili 13, 2014. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wanaosimamia shughuli ya daraja hilo, baada ya kuwasili eneo hilo leo
   Sehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika kutoka mita 25 na  sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia hiyo.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
   Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja
   Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
   07:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo, katika eneo la Daraja la Mpiji, linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, leo Aprili 13, 2014. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Picha na OMR

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Joel Bendera akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya Uongozi Bora wakati wa sherehe za Tuzo za Urugulu kwa mwaka 2014 zilizofanyika Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TLTC wakifurahia tuzo ya Mshindi wa jumla kwa utoaji wa misaada kwa Jamii mkoani wakati wa Sherehe za Tuzo za Urugulu mwaka 2014 zilizofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dk Joel Bendera akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania (TLTC) ambayo ilitwaa tuzo ya Mshindi wa jumla kwa utoaji wa misaada kwa Jamii mkoani humo wakati wa Sherehe za Tuzo za Urugulu mwaka 2014 zilizofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki.
   Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania (TLTC), Richard Sinamtwa akiwa amenyanyua juu kombe la Mshindi wa jumla kwa utoaji wa misaada kwa Jamii mkoani Morogoro wakati wa Sherehe za Tuzo za Urugulu mwaka 2014 zilizofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Joel Bendera(kulia) akimkabidhi Kombe, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania (TLTC), Richard Sinamtwa kampuni tuzo ya Mshindi wa jumla kwa utoaji wa misaada kwa Jamii mkoani wakati wa Sherehe za Tuzo za Urugulu mwaka 2014 zilizofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki

  0 0

  Rais mstaafu wa awamu wa tatu Mh Benjamin Mkapa leo(jumatatu) amefanya ziara kumtembelea Shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori la African wildlife foundation wilayani Monduli.

  Mzee Mkapa ni Makamu mwenyekiti wa shirika hilo lenye makao yake mjini Washington Marekani.picha mbalimbali zinamuonesha waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimuongoza Rais Mkapa kuzuru shule hiyo.
  Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa (katikati) akimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati alipotembelea Shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Wanyama pori la African Wildlife Foundation,wilayani Monduli.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa wakati walipokuwa kwenye moja ya madarasa ya shule hiyo.
  Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.

  0 0

  Miss Ilala 2013, Doris Mollel ijumaa ya wiki iliyopita alitembelea shule ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam na kukabidhi vitabu 50 za hadithi kwa wanafunzi wa shule hiyo katika harakati zake binafsi za kuwajengea wanafunzi na watoto utamaduni na tabia ya kujisomea kwenye umri mdogo.

  Miss Ilala huyo wa mwaka 2013 alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi kujisomea kama ufunguo wa maisha yao ya baadaye.
  Img_4177
  Miss Ilala 2013, Doris Mollel, akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembea shule hiyo ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam.
  Img_4227
  Doris Mollel akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo ya msingi ya Pugu muda mfupi baada ya kukabidhi vitabu hivyo.
  Img_4285
  Img_4273
  Miss Ilala 2013, Doris Mollel akimkabidhi vitabu Mwalimu Josephine Matiku kwenye hafla rasmi ya makabidhiano shule hapo ijumaa iliyopita jijini Dar.
  Img_4236
  Miss Ilala 2013, Doris Mollel akipozi na walimu wa shule hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu.
  Img_4265
  Miss Ilala 2013, Doris Mollel katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Pugu.
  Img_4294

  0 0

  PIA HALMASHAURI KUU YA TAWI YAMSIMAMISHA KAZI
  KATIBU WA TAWI BI. MARIAM  MUNGULA:

  Mwenyekiti wa CCM UK Ndugu Maina Ang’iela Owino jana ametangaza rasmi nia yake ya kujiuzulu Uongozi wa CCM Tawi la UK baada ya kutumikia toka mwaka 2007.
  Ndugu Owino alitoa uamuzi huo wa hiari wakati akifungua rasmi kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la UK kilichokaa jana Jumamosi tarehe 12/04/2014 katika jiji la Reading, Berkshire, Uingereza.

  Ndugu Owino aliwakumbusha wajumbe kuwa awali aliomba kukitumikia Chama kwa muhula mmoja wa uongozi na alitaja kumbukumbu ya vikao vya Chama vilivyomuomba aendelee kukisimamia Chama hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wakuu wapya wa Tawi mwezi septemba 2012 jijini Manchester. Ndugu Owino aliwakumbusha mafanikio waliyopata katika muda wa uongozi wake ikijumuisha harakati za kufungua mashina hadi 15 katika miji na Jiji mbalimbali; Kuhamasisha na kujenga mtandao wa kuanzisha Jumuiya ya kwanza ya Watanzania hapa UK na Kuwashirikisha wanaCCM kuanzisha miradi ya kujitegema ikiwepo ari ya kumiliki jengo la CCM UK.

  Alikumbusha pia juhudi na msukumo wa kutaka CCM Taifa kuanzisha dawati rasmi la matawi ya nje na kuyapa uwakilishi wa kudumu katika vikao vya juu vya CCM Taifa. Pia kupigania Sera ya CCM ya Diaspora iboreshwe kwa Kuanzisha Kituo Maalum cha Diaspora nchini Tanzania ili serikali iwashirikishe na kuratibu hoja na haja za wana Diaspora.

  Aidha aliwataka wajumbe kutoa ushirikiano wa wazi kwa Idara ya uenezi ambayo kwa sasa inajenga Website ya kisasa na Online TV itakayowapa wanaCCM uhuru wa kutoa maoni na hoja zao bila uwoga lakini kwa nidhamu na kufungua soko la kutangaza bidhaa za Tanzania.

  Ndugu Owino alisema wanaCCM hujenga umoja wa kweli na hawaogopi kusingiziwa au kusemwa vibaya na hivyo wasiogope changamoto mbalimbali wakati wanatekeleza Mapinduzi ya umma na kukijenga Chama hapa Uingereza.

  Ndugu Owino aliiomba Halmashauri Kuu ya Tawi ishirikiane na Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Tawi kufanya maandalizi na kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wakati wowote kuanzia sasa ili wanaCCM wote wawe huru kumchagua kiongozi atakaye sukuma CCM UK toka hapa tulipofikia.

  Wakati huohuo Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi la UK jana iliazimia kwa pamoja kumsimamisha Katibu wake wa Tawi Mariam Mungula baada ya majadiliano ya kina ya kutokuridhishwa kabisa na utendaji na uratibu wake wa kazi. Kikao hicho kilipeleka shauri lake kwa Kamati ya Maadili na Usalama ili apate haki ya kujitetea ni kwa nini asiachishwe moja kwa moja kazi yake za Ukatibu wa CCM UK. Ndugu Leybab Mdegela anakaimu nafasi yake kuanzia jana 12/04/2014.
  Kikao kiliendelea na hoja zake za kuboresha Chama hapa UK na kuweka mikakati yenye mawazo chanya katika kukisaidia chama katika mikakati kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wote wa Tanzania.

  Imetolewa na Abraham Sangiwa  
  Idara ya Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya CCM UK.  
  13/04/2014.

  0 0


  0 0

  Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa soko la Samaki (Mwalo),ambao imeelezwa kuwa utapunguza umaskini kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo imeelezwa kuwa mradi huo wa soko na kuhifadhia samaki umechelewa kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda ulipangwa kwenye mkataba,Kinana amewahidi Wananchi kuwa atalifuatilia tatizoo hilo na kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyoahidiwa.Eneo hilo la kisasa kabisa litatumika kuongeza thamani ya samaki. 
   Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,akiuliza swali la zahanati na ,Elimu na Barabara kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana (pichani kulia),alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa Samaki (Mwalo). 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirikii ujenzi wa mradi wa soko la samaki (Mwalo),katika kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,
   Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na eneo la soko hilo la kukaushia samaki na dagaa
   Ndugu Kinana akikaribisha kwa balozi.
   Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakiwa wameketi kwa balozi wa shina namba 2,tawi la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani Katavi.
    Ndugu Kinana akizungumza na wajumbe wa shina namba 2 (hawapo pichani),tawi la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani Katavi.
   Wajumbe wa tawi la Ikolasto wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.(hayupo pichani). 
  Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, akijibu na kutoa taarifa  mbalimbali kuhusiana na jimbo lake katika suala zima la kutekeleza na kuhumiza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,mbele ya wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
   Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo,katika mkutano wa hadhara,Kinana alijikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa kata ya Kirema, Ikola na Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa,kumekuwepo na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Serikali.Kinana amesema chama chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu na umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi kwa kuwajibika ipasavyo.

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiowaonesha waandishi wa habari hati halisi ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)


  0 0


  0 0

  Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za kitanzania.
  Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
  Washiriki wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa muswada (script) kwaajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo wao kwa majaji.
  Msanii wa Vichekesho Joti akihojiana na Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents mara baada ya kutoka kwa majaji, shindano limeingia hatua ya pili leo kwa kuchagua washiriki 30 ambao watatafutwa washiriki 15 bora hapo kesho.

  Mshiriki namba 00554 akihojiwa na msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho ambapo watapatikana washindi kumi na tano bora na hatimaye kupata washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano za kitanzania
   
  Baadhi ya washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakibadilishana mawazo mara baada ya kupatikana kwa washiriki 30 ambao wataendelea na mashindano hapo kesho kwaajili ya kupata washiriki 15 bora.
   Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akiwa amenyongonyea mara baada ya safari yake katika mashindano kuishia leo kutokana na kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya tatu hapo kesho.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions - Dodoma
  Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
  Leo Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya Kati na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=).
  Mpaka sasa washiriki 30 wameshapatikana kwa kanda ya Kati na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya Kati katika fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania (50,000,000/=).

  Katika Washindi 30 waliopatikana leo, washiriki wawili wameweza kuonyesha vipaji vyao huku washiriki hao wakiwa ni ndugu kabisa, washiriki hao ni babu na mjukuu wake wa kike ambao wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya tatu kesho ambapo washindi wa Kanda ya Kati watapatikana.

  Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho Kanda ya Kati Mkoani Dodoma na hatimaye kuhamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya na usaili wa Kanda ya Juu Kusini utaanza tarehe 19 April 2014 saa 1 asubuhi na wakazi wa Kanda ya Juu Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina gharama yoyote ile.

  0 0


  Berlin,Ujerumani,
  Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu  wa uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za muunganno wa Tanzania mjini Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014 kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.

  Watanzania wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.

  Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo. Pia milango ipo wazi kwa wadau na wale wote wanaohitaji ushauri juu ya kuwekeza au kuchangia maendeleo ya jamii nyumbani Tanzania.

  Pia pata kuwepo na vyakula vya kitanzania

  KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE

  UMOJA NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU

  UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
  MUNGU IBARIKI TANZANIA


  0 0

  1. Wewe  ni  mjasiria mali  ?  Unahitaji  fedha  kwa  ajili  ya   kupanua huduma  yako  ?
  2. Wewe  ni  mfanya  biashara  au  mmiliki wa  kampuni  ? Unahitaji fedha  kwa  ajili  ya  kukuza  mtaji  wako na  kupanua  biashara  yako  ?
  3. Wewe  ni  Taasisi  isiyokuwa  ya  kiserikali ?  unahitaji  fedha  kwa ajili  ya  kuendesha  miradi  na  program  mbalimbali  ?
  4. Wewe  ni  mtayarishaji  wa  filamu  au  kiongozi  wa  kundi  la maigizo ?  Unataka  kutayarisha  filamu  au  tamthiliya  lakini unashindwa  kwa  sababu  ya  ukosefu  wa  fedha  za  gharama  za utayarishaji ?
  Kama  jibu  ni  ndio basi  hii  ni  habari njema  sana  kwako. 
  FUNDRAISING  SOLUTION  & General  Enterprises  ni  kampuni  inayo jihusisha  na  kutoa  huduma  ya  kuzisaidia  taasisi, kampuni  na  watu binafsi (wafanyabiashara  & wajasiriamali ), ku –raise  funds  kwa  ajili ya  kufanikisha  miradi  na  program  mbalimbali  zinazo  hitaji  fedha.
  Tunakaribisha maombi  kutoka  kwa  wajasiriamali, wafanyabiashara,wamiliki  wa  kampuni,watayarishaji  wa  filamu, wamiliki wa  makundi  ya  maigizo, taasisi  zisizo  kuwa  za  kiserikali  na  watu binafsi  wanao  hitaji  kuf-raise  funds  kwa  ajili  ya kufanikisha miradi  na  program  mbalimbali.

  Tunao  wataalamu  walio  bobea na wenye  uzoefu  mkubwa  katika    suala la   kuraise  funds  kwa  ajili  ya  miradi  na  program  mbalimbali.
  Tunaptikana  Mikocheni  jijini  Dar  Es  salaam.
  Tuma  maombi yako  kwenda  : fundraisingtanzania@gmail.com 

  Kwa  maelezo  zaidi, tembelea : http://www.fundraisingtanzania.blogspot.com

  0 0
 • 04/14/14--21:28: Shiwata wamlilia Gurumo

 • MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)Umepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi nchini na aliyekuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Muhidin Maalim Gurumo "Kamanda"aliyefariki Jumapili katika hospitali ya Muhimbili.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa wamepokea kwa majonzi makubwa na kusema kuwa pengo lake haliwezi kuzibika haraka kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kutunga, kuimba na kuongoza wanamuziki wenzake.

  Alisema marehemu Gurumo hakuwa mtu wa kukata tamaa kuendeleza muziki wa dansi kwani aliwahi kuwafundisha wanamuzi wanaotamba katika bendi mbalimbali ikiwemo Msondo Ngoma..

  "Kutoka miaka ya sitini Gurumo alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki akiwa na NUTA, JUWATA,Safari Sound,Sikinde na Msondo ambayo aliastaafu kabla ya kifo chake"alisema Taalib.

  Wakati wa uhai wake, Gurumo alikuwa mwanachama wa SHIWATA na alikuwa kiunganishi cha wanamuziki wa Msondo Ngoma kushiriki kuunda kijiji cha wasanii Mkuranga mkoa wa Pwani na kubariki jitihada za kuwakomboa wasanii wa fani mbalimbali kujikomboa kiuchumi..

  Marehemu Gurumo alitarajiwa kuzikwa jana Jumanne nyumbani kwao Masaki wilaya Kisarawe mkoa wa Pwani.

  0 0


  Habarini Bloggers, Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa kuwa Blog ya Kijiwe Cha Wasomi iliyokuwa na makazi yake Wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma, sasa itahamia Mtwara mjini.

  (Gas City). Hii ni kutokana na majukumu mengine ya kitaifa yanayofanywa na mwongozaji wa blog hii. Bado hatujajua ni eneo gani tutaweka ofisi zetu mkoani Mtwara, lakini nitawataarifu mara baada ya kukamilisha taratibu zote.
  Pamoja na mabadiliko haya, utendaji wa blog hauta athiriwa.
  Karibuni sana Gas City.

  Elly Marimbocho,

  Admin Kijiwe Cha Wasomi


  0 0
 • 04/14/14--21:36: Article 1


 • 0 0


  0 0

    

  1 
  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama katikati akiwa katika picha ya pamoja na baba yake mzazi Mzee Mwita na mmoja wa waratibu wa tamasha la pasaka Bw. wakati walipofika katika hospitali ya muhimbili ili kumjulia hali kutokana na majeraha na maumivu ya ajali aliyoipata wiki iliyopita wakati akielekea mkoani Dodoma kwa shughuli zake, watu wengi wamemtembelea hospitalini hapo leo akiwemo Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT ,Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa kutoka Mbweni jijini Dar es salaam.(FULLSHANGWE NA KIKOSIKAZI CHAKE TUNAKUTAKIA AFYA NJEMA MUNGU AKUPONYE HARAKA UREJEE KATIKA KAZI YA KUMTUMIKIA MUNGU)2Alex Msama akifungua mlango wa chumba chake alimolazwa ili kusalimiana na baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo.3Alex Msama akitoka nje ya chumba chake alimolazwa ili kusalimiana na baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo.4Alex Msama akifelezea jambo kwa baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo.6Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT akimsalimia Alex Msama wakati aliomtembelea hospitalini hapo kumjulia hali.7Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT akisoma neno takatifu la kumtia faraja Bw. Alex Msama ili aendelee na kazi ya mungu wakati aliomtembelea hospitalini hapo.8 Watoto yatima cha Mwandaliwa kutoka Mbweni jijini Dar es salaam wakimjulia hali Bw. Alex Msama wakati walipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili na kumjulia hali leo9Watoto yatima cha Mwandaliwa kutoka Mbweni jijini Dar es salaam wakimuombea dua Bw. Alex Msama wakati walipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili na kumjulia hali leo10Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akimjulia hali Bw. Alex Msama wakati alipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili leo

  0 0

  Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Omary Matulana akihutubia kwenye Baraza kuu la Vijana la kazi la mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika siku ya Jumapili Aprili 13, 2014.

older | 1 | .... | 269 | 270 | (Page 271) | 272 | 273 | .... | 1897 | newer