Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Basata wabariki Tamasha la Pasaka

$
0
0
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa kibali kwa ajili ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa kutokana na kupata kibali hicho maandalizi rasmi sasa yameanza. “Nilikuwa Napata tabu hata kuanza kuhangaikia ukumbi ambao tutafanyia tamasha maana mwaka jana tulifanyia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa bado hatujaamua tutafanyia wapi kwa sababu ilikuwa hatuna kibali.

“Lakini hatua ya Basata kutupatia kibali inamaanisha tumepata baraka, hivyo tuendelee na mambo mengine ya maandalizi,” alisema Msama. Alisema wamepanga siku yenyewe ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam na siku inayofuata bado wanaangalia wafanye wapi kwani mikoa mbalimbali imeomba ipewe uenyeji.


“Vipo vigezo tutaviangalia kwa wanaotaka tuwapelelekee, kama vitakuwa sawa basi tamasha litafanyika kwa watakaotimiza, lakini kwa sasa Jumatatu ya Pasaka bado hatujaamua wapi twende,” alisema Msama katika taarifa hiyo.


Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.


Rais kikwete katika mkutano wa SADC nchini Msumbiji

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji wakiwa katika mkutano wa wakuu wa ncho za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC jijini Maputo Msumbiji jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) na Mwenyeji Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakati wa kikao cha SADC jijini Maputo jana(picha na Freddy Maro).

Shida ya maji Handeni yatikisa Jeshi la Kujenga Taifa

$
0
0

Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa

Na Mashaka Mhando, Handeni.

SHIDA ya maji Wilayani Handeni imeingia sura mpya baada ya jeshi la kujenga Taifa kutangaza hali ya hatari baina yake na wananchi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni jeshi hilo kuchoshwa na mvutano wa mara kwa mara uliyopo wa kugombea upatikanaji wa huduma hiyo.

Tahadhari hiyo ilitolewa na Mkuu wa kikosi cha 835 KJ- Mgambo JKT kilichopo wilayani hapa, Meja Mohamed Mketto wakati akisoma taarifa ya kikosi hicho kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa katika sherehe za kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi yaliyopewa jina la “Vijana op Sensa 2012” yaliyofanyika jana katika uwanja wa kikosi hicho uliyopo kijiji cha Mgambo Wilayani Handeni.

Meja Mketto ambaye alikuwa akieleza miongoni mwa changamoto za kikosi hicho alidai kuwa ni pamoja na tatizo la maji ambalo linakiingiza kikosi hicho kwenye mgogoro baina yake na wananchi na kufikia hatua ya malumbano yanayohatarisha usalama na amani iliyokuwepo.

Alimueleza Mkuu huyo wa Mkoa kwamba yamekuwepo malumbano ya muda mrefu kati ya kikosi na jamii inayokizunguuka kuhusu matumizi ya bomba la maji linalotumiwa na kikosi hicho ambapo wakati mwingine wananchi hulihujumu kwa kulitoboa na hivyo kusababisha huduma hiyo kukosekana kabisa.

Alidai kuwa kikosi hicho kinapata huduma hiyo kutoka mradi wa HTM ambayo pia si ya uhakika na hivyo wakati mwingine wanalazimika kutembea hadi kijiji cha Hale umbali wa kilometa 54 kutoka kikosini hapo.

Hata hivyo kutokana na hali hiyo uongozi wa kikosi hicho ulitahadharisha kuwa endapo hali hiyo itaachwa iendelee bila kushughulikiwa na mamlaka zinazohusika kuna hatari ya kuzuka mgogoro mkubwa usiyo wa lazima unaoweza kuathiri amani na maelewano.

Alieleza jitihada zinazofanywa katika kuondokana na kero hiyo kuwa ni pamoja na kuchimba visima virefu kikosini hapo hata hivyo alisema kuwa jitihada hizo zinagonga mwamba kwa kuwa havitoi maji hasa wakati wa kiangazi.Habari zaidi ingia http://handenikwetu.blogspot.com

MASHINDANO YA BODABODA CUP KINONDONI YAZIDI KUSHIKA KASI, TEGETA YAPIGWA 3-0 NA KAWE

$
0
0
k6
Mchezaji wa timu ya waendesha Bodaboda kutoka Tegeta akiwania mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Waendesha Bodaboda kutoka Kawe katika mashindano ya ligi ya Bodaboda Cup inayoendeshwa na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ambapo timu ya Kawe imeifunga timu ya Tegeta kwa magoli 3-0 kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo.

Mashindano hayo yanashirikisha timu mkoa wa kipolizi wa Kinondoni ambazo zinatoka katika maeneo ya Kimara, Kawe, Tegeta, Mabibo na Ubungo wachezaji wakiwa ni waendesha Booda, awamu ya kwanza ya ligi hiyo ilikuwa na timu 32 na sasa ni awamu ya pili ambapo timu 16 zinashindana ili kupata timu 8 zitakazoshiriki Ligi ya Nane Bora na hatimaye kupata mshindi wa mashindano hayo ya Kinondoni Bodaboda Cup ambaye atapata zawadi nono.

Lengo la Mashindano hayo ni kuwakutanisha waendesha Bodaboda wote wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ili waweze kufahamiana wao kwa wao, lakini pia ili jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liweze kuwaelimisha juu ya sheria za usalama Barabarani na Ulinzi Shirikishi kwa jamii.
k9
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Agatha Isack akikagua timu kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
k10
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Agatha Isack akikagua timu kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
k11
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Agatha Isack akimtakia uchezeshaji mwema mshika kibendera wa kushoto Hamis Pondamali kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
k1
Timu ya Kawe ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo na kupata mawaidha mawili matatu.
k2
Kikosi cha timu ya Tegeta kikiwa katika picha ya pamoja kalba ya kuanza kwa mchezo huo timu hiyo imefungwa magoli 3-0 na timu ya Kawe.
k3
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
k5
Wachezaji wa timu za Kawe na Tegeta wakiwania mpira uliojuu wakati wa mchezo uliokutanisha timu hizo leo kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam
k8
Kutoka kulia ni Aghata Isack Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Esther Ngaja Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Refarii wa mchezo huo Geofrey Mwamboneke, Mshika Kibendera Hamis Pondamali, Mshika Kibendera Mwanahamisi Matiku, ASP. Emilian Kamuhanda Insp.Soud Ramadhan na Mratibu wa kombe hilo Ernest Mbaga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers leo,
k7 Mashabiki wakijikinga na jua huku wakifuatilia mchezo huo.

rais kikwete awasili Dodoma leo kwa vikao vya CCM

$
0
0
 Vijana wa CCM wakimvika skafu Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete muda mfupi baada ya kuwasili mjini Dodoma kongoza kukao cha Halmashauri kuu ya CCM taifa.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu  Abdulrahman Kinana muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma ambapo ataongoza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM taifa.

Rais Kikwete amkabidhi Mlemavu Bajaji mjini Dodoma

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bajaji mpya mlemavu wa miguu ambaye ni mfanyakazi wa TANROADS Bi.Sarah Nalingigwa Nkumbo huko ikulu mjini Dodoma leo asubuhi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli.Wapili kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni mkurugenzi Mkuu wa TANROADS Injinia Patrick Mfugale. Bi. Sarah ambaye ni Mfanyakazi wa TANROADS mkoani Singida alikabidhiwa Bajaji hiyo ikiwa ni ahadi ya Rais alipokuwa akifungua Barabara ya Manyoni- Itigi.(picha na Freddy Maro)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Februari 10, 2013 amekabidhi pikipiki aina ya bajaj kwa mama mmoja mlemavu, Mama Sarah Mkumbo Nalingigwa katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo mjini Dodoma.

Mama Nalingigwa ni mtumishi wa Wakala wa Barabara nchini – TANROADS- katika Mkoa wa Singida na shughuli ya leo imehudhuriwa pia na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mufugale na Mama Salma Kikwete.

Shughuli ya makabidhiano ya leo, inatimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa kwa Mama Nalingigwa wakati alipokutana naye miongoni mwa wananchi waliohudhuria sherehe ya utiaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi=Chaya mjini Itigi, Mkoa wa Singida Novemba mwaka jana.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo, Rais Kikwete amemwambia mama huyo: “Nimefurahi kwamba nimeweza kutimiza ahadi yangu. Hii ndiyo faraja yangu kwamba sasa utaweza kufanya kazi zako kwa urahisi zaidi, utaweza kutembea kwa urahisi zaidi na kufika kazini na kurejea nyumbani kwa namna ya haraka zaidi.”

Naye Mama Nalingigwa amewwambia Rais Kikwete: “Wewe ni kiongozi shupavu, kiongozi hodari na mpiganaji anayemjali kila mtu. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akujalia ili uendelee kuwaona wengine wenye mahitaji kama ya kwangu.”

Ameongeza mama huyo ambaye amefanya kazi Wizara ya Ujenzi kwa miaka 30 iliyopita: “Kwa kuniwezesha kiasi hiki, umenipa uwezo wa kufanya kazi kwa namna bora zaidi., Ni vyema kuwa viongozi wengine wakaiga mfano wako wa kujali watu walioko chini yako.”

Amesisitiza: “ Sisi walemavu tuna mahitaji mengi na hivyo naomba unedelea kutuangalia kwa jicho la huruma na kutupunguzia vikwazo vya maisha kila nafasi inapojitokeza.”

MSAMA ATANGAZA UZINDUZI WA TAMASHA LA PASAKA 2013

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki wakati akitangaza uzinduzi wa tamasha hilo la Pasaka kwa mwaka huu wa 20 13 litakaloanza kufanyika hapa nchini hivi karibuni.

======= ======   ========    =========

Tamasha la Pasaka kuhamasisha amani na pendo

Na Mwandishi Wetu

WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka mwaka 2013 wameibuka na kaulimbiu inayohamasisha amani na upendo kwa jamii.  Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wanashukuru kwamba sasa wamepata kibali cha kufanya tamasha hilo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Alisema tamasha la mwaka huu litakuwa zaidi katika kuhubiri amani kwa jamii na kusisitiza kuwa dhamira yao ni kuhakikisha Watanzania wanazidisha upendo na mshikamano uliokuwepo. Alisema tamasha hilo litafanyika Machi 31 katika ukumbi ambao utatangazwa hivi karibuni na kuwa wana matumaini mambo yatakuwa mazuri kuliko tamasha la mwaka jana lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 “Hatua ya Basata kutupatia kibali inamaanisha tumepata baraka, hivyo tuendelee na mambo mengine ya maandalizi, nasi tunasema mambo mwaka huu yatakuwa mazuri zaidi,” alisema Msama. Alisema wamepanga siku yenyewe ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam na siku inayofuata bado wanaangalia wafanye wapi kwani mikoa mbalimbali imeomba ipewe uenyeji.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration. Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Neno La Leo: Ukimwona Tajiri, Tamani Kuwa Kama Yeye, Ukimwona Masikini...

$
0
0

Ndugu zangu,

Leo asubuhi nikiwa kwenye jogging hapa Iringa nilikutana na picha ya watu wazima wawili; wote wameshika baiskeli. Hawaendeshi, wanazikokota. 

Mmoja anapandisha, mwingine anashuka. Jua la asubuhi lilikuwa likichomoza. Anayeshuka anapigwa na jua usoni, anayepanda, mgongoni.

Niliipiga picha ile. Kisha nikaendelea kufanya jogging huku nikitafakari kuhusu maisha. Kuwa katika dunia hii, kama ilivyokuwa kwa watu wale wawili; kuna kupanda na kushuka.

Kuna masikini na matajiri. Masikini anaweza kuwa tajiri na tajiri anaweza kurudi kwenye umasikini. Hakuna aliyezaliwa kuwa masikini daima na kinyume chake. Ni mazingira tu. Kama mwanadamu, ukisema mimi siwezi hutaweza, na kinyume chake. 

Na wengi walioshinda katika maisha humu duniani wana historia ya kushindwa pia. Wengine wamepata kushindwa mara nyingi, lakini, hawakukata tamaa. Walianguka, wakasimama kuendelea kupambana.

Ndio, katika dunia hii, mwanadamu unatakiwa upambane mpaka pumzi yako ya mwisho. Kwenye Uchina ya kale kulikuwa na mwanafalsafa kwa jina la Comfucius. Katika mafundisho yake mengi aliyopata kumpa mwanafunzi wake Tzu Kung, mojawapo linahusu dhana ya utajiri na mahusiano yake na umasikini. 

Comfucius anasema; ukimwona mtu tajiri(aliyefanikiwa kimaisha),basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe.

Kwa mwanafalsafa Comfucius, dhana ya utajiri haikuwa na maana kuwa na mali pekee, bali, pamoja nazo, ni uwezo wa mtu kuishi maisha adilifu na yenye fadhila (virtues). Na katika fadhila zote, ile ya unyenyekevu na ukweli ndio chanzo cha fadhila nyingine zote.

Umasikini vilevile, yumkini unaweza kuwa na maana ya kukosa mali na uadilifu. Ndio, mwanadamu waweza kuwa na mali lakini ukakosa uadilifu. Ni dhahiri, katika hali hiyo, hata mwenye mali naye ni masikini sana. 

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765

UTARATIBU wa upimaji wa Mabasi na Malori watajwa kuwa kero kwa soko la pamoja la biashara afrika mashariki.!

$
0
0

UTARATIBU wa upimaji wa Mabasi  na Malori katika mizani umetajwa kuwa chanzo kitakachoichelewesha Tanzania kufikia maendeleo ya haraka mara pale Soko la pamoja la Biashara kwa nchi za Afrika mashariki litakapoanzishwa.
 
Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Shakur Wahad, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam juzi, kuhusu matatizo waliyokutana nayo katika mizani wakati  wakiingia nchini kushiriki michezo ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki na Kati, inayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
 
Akizungumzia kuhusu matatizo Wahad alisema wanashangazwa na utaratibu huo wa upimaji wa magari katika mizani kuwepo hapa nchini tofauti na nchi zinngine za Afrika Mashariki, huku wakilalamikia kutozwa kiasi cha  zaidi ya sh. milioni 3 katika mizani kama faini baada ya  basi la Chuo hicho walililokuwa wakisafiria  kuonekana kuzidi uzito zaidi ya viwango vilivyowekwa.
 
“Kama Tanzania itataka kufika mahali ikajivunia kimaendeleo inapaswa kulitazama eneo hilo, tumetoka Uganda, tumepita Kenya hatuja kutana na kikwazo chochote hadi tulipoingia Namanga kwa upande wa Tanzania ndipo balaa lilipoanza, hii ni kikwazo kwa maendeleo ya Tanzania ikizingatiwa kuna mipango ya kuingia katika soko la pamoja” alisema Wahad.
Wahad alisema wakiwa katika  mizani hiyo ya Namanga, basi lao lilitozwa faini kwa kuzidisha uzito, na baadae tatizo kama hilo liliwakuta tena  walipofika  mizani iliyopo njia  panda ya Himo Mkoani Kilimanjaro na kisha katika mizani ya Mkata iliyopo mkoani Pwani.
 
Aidha alisema matatizo hayo waliyokutana nayo, yanatokana na wao kutofahamu juu ya uwepo wa utaratibu wa upimaji katika mizani jambo lililowafanya waamini kuwa safari yao ilikuwa salama pasipo tatizo lolote hususani linalohusiana na masuala ya matumizi sahihi na sheria za barabara.
 
Wahad alisema  anaamini Tanzania ina fursa nyingi za kimaendeleo na kwamba ili iweze kujihakikishia inatimiza ndoto zake kuendelea kukua kiuchumi, ni vyema ikatazama maeneo muhimu yanayochangia kukua kukua kwa uchumi huo ikiwemo njia ya usafirishaji hasa  barabara.
 
Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Msemaji wa Wizara ya Ujenzi Martin Ntemo, alisema Wizara inalifuatilia suala hilo ili kufahamu undani wa tatizo walilokutana nalo wanafunzi hao katika mizani na kisha atalitolea ufafanuzi baadae.
 
 “Kiasi fulani nimesikia taarifa kuhusiana na suala hilo, lakini naomba nipe muda ili niweze kulifuatilia kwa ajili ya kupata taarifa kamili halafu nitakujulisha kila kitu juu ya kilichokuwa kimetokea” alisema Ntemo.
 
Akizungumzia kuhusu utaribu wa upimaji mabasi katika mizani  hapa nchini Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Enea Mrutu, alisema Tanzania inapaswa kujifunza kutoka katika nchi zingine kama kweli ina nia ya kuboresha sekta ya usafiri.
 
Alisema inashangaza kuona utaratibu huo kuwepo hapa Tanzania pekee dhidi ya nchi zote  Duniani, suala alilosema ni vyema kama litatazamwa upya  kwa lengo la kuondoa dosari zilizopo  kabla ya kuungana na wenzetu wanachama wa nchi za  Afrika Mashariki katika soko la pamoja la kibiashara.

watanzania waungana na Iran kusherehekea miaka 34 ya mafanikio

$
0
0

WATANZANIA jana wameungana na Jamhuri ya  Kiislam ya Iran katika kusherehekea miaka 34 ya mafanikio tangu  mapinduzi yaliongozwa na Kiongozi wa Kidini, Ayatollah Khomen yakumuondoa madarakani Mfalme Shah Pahlavi mwaka 1979.
 
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana, na Balozi wa Iran nchini Mehdi Agha Jafari, katika sherehe hizo ambazo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje, akiwemo Rais wa awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi.
 
Alisema Wairan wanajivunia mapinduzi hayo kwani yamekuwa chachu ya misingi ya haki katika jamii ambapo pia yameweza kuifanya nchi hiyo kupiga hatua kimaendeleo hadi kutambulika kimataifa.
 
Jafari alisema mafanikio yaliopatikana baada ya mapinduzi hayo ni katika sekta za viwanda, afya, Teknolojia na upande wa kilimo. Aliongeza kuwa nchi hiyo hivi sasa imefanikiwa kuzalisha awataalam wake, ambao wamefanikiwa kurusha vyombo vya kisayansi kwenda anga za juu.
 
“Hivi sasa nchi yetu inaviwanda vya kutengeneza dawa mbalimbali ikiwemo za binadamu pia upande wa kilimo hatuko nyuma tunazalisha zana za kilimo haya ndio mafanikio ya mapinduzi”alisema Jafari.
 
Aidha, nchi hiyo iliingia katika mapambano dhidi ya utawala wa Mfalme Shahah kwa zaidi ya miaka 20 kutokana na dhuluma, kujilimbikizia mali katika familia yake, kuua tamaduni za Wairan huku akiruhusu tamaduni za nchi za magharibi ambazo ni kinyume na nchi  hiyo.
 
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha, akizungumza kwa niaba ya Waziri Berdard Membe ambaye yuko Dodoma kwa majukumu muhimu, alisema Tanzania itaendeleza ushirikiano na nchi hiyo, kwani ushirikiano wa nchi hizo mbili una historia ndefu hususan  kwa upande wa Zanzibar.
 
Vilevile wanaishurukuru nchi hiyo kwa misaada kwenye maeneo mbalimbli nchini yakiwemo ya Afya, kilimo, kielimu na mengine.
 

Kufutwa kwa #POAC: #AnnaMakinda adhibitiwe au tusahau Uwajibikaji nchini

$
0
0


Katika mkutano wa Kumi wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Spika wa Bunge ndugu Anna Makinda alitangaza mabadiliko kadhaa ya muundo wa Bunge katika Kamati mbalimbali za Bunge. Moja ya maamuzi ya Spika yalikuwa ni kufutwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ambayo inajulikana kifupi kama POAC. Maamuzi haya yameleta sintofahamu kwa wananchi wengi na wafuatiliaji wa masuala ya Bunge na Uwajibikaji katika nchi yetu. 

Ni muhimu tufahamu uundwaji wa POAC ulitokana na misingi gani na kwamba Uamuzi wa Spika unarudisha nyuma maendeleo makubwa ya kujenga Bunge imara na lenye meno. Maamuzi ya Spika ni kinyume cha kanuni za Bunge, sheria ya Ukaguzi na Katiba ya nchi. Maamuzi ya Spika yanavuruga Bunge,ni ya hovyo na yanapaswa kupingwa na kila mdau wa Uwajibikaji nchini.
 
Baada ya Tanzania kuingia kwenye zoezi la Ubinafsishaji, mashirika mengi ya Umma yaliuzwa na mengine kufa kabisa. Wakati huo kulikuwa na chombo kinaitwa SCOPO (Standing Committee on Parastatal Organisations) kwa madhumuni ya kusimamia uendeshaji wa Mashirika ya Umma. Bunge lilikuwa na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na kamati hiyo ilifutwa mwaka 1997 kufuatia hatua za ubanifsishaji na ukweli kwamba Mashirika ya Umma hayatakuwapo na hivyo hapakuwa na haja ya kuwapo kwa kamati hiyo. Mwenyekiti wa mwisho wa Kamati hiyo alikuwa ni Mzee William Shellukindo wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga.
 
Mwaka 2007, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alifanya mkutano wa Uwajibikaji na kueleza Taifa kuwa kimsingi Mashirika ya Umma bado yapo na mahesabu yao, kwa kuwa hayaangaliwi, ni mabaya sana nafedha za umma zinapotea. Pia alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 143(5) inamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoa taarifa za Ukaguzi za Mashirika ya Umma (Public Authorities and Other Bodies). 

Hivyo aliomba Bunge liunde Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ili liweze kupokea, kujadili na kutoa maelekezo kuhusu mahesabu ya Mashirika ya Umma na kusimamia ufanisi wa Mashirika ya Umma. Vile vile alishauri Kamati hiyo isimamie sera ya  Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma. Spika wa Bunge wa wakati huo, kupitia Kamati aliyoiunda chini ya Job Ndugai (wajumbe wengine walikuwa dkt Willibrod Slaa, Beatrice Shelukindo, Hamad Rashid Mohammed na Nimrod Mkono) wakaunda Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kanuni za Bunge za Mwaka 2007. Kamati ya POAC iliundwa rasmi mwaka 2008 mwezi Februari. Nilipewa dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamati hii. Sababu za kuanzishwa kwa kamati ya POAC bado zipo na kimsingi sababu hizo ni za maana sana sasa kuliko ilivyokuwa kabla.
 
Majukumu ya POAC yaliainishwa na sehemu ya tatu ya nyongeza ya nane ya Kanuni za Bunge toleo la mwaka 2007, kanuni ya 115 (13)(a-e). Majukumu hayo ni pamoja na kushughulikia mahesabu yaliyokaguliwa ya Mashirika ya Umma, kuainisha maeneo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Umma, kutathmini ufanisi wa Mashirika ya Umma na kufuatilia utekelezwaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya Umma. Kuanzia mwaka 2008 Mdhibiti na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa taarifa za mahesabu ya mashirika kama Katiba ya nchi inavyomtaka na sheria ya ukaguzi ya mwaka 2008. Sheria hii imeitaja kamati ya POAC kama moja ya kamati zenye majukumu ya kuwasilisha Bungeni taarifa ya mwaka ya mahesabu ya Mashirika ya Umma.
 
Katika kipindi cha miaka mitano POAC imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa umahiri na kwa kweli kwa uwazi sana kuliko kamati nyingine zote za Bunge. Taarifa ya mwisho ya POAC katika Bunge iliyowasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge, mwezi Aprili mwaka 2012 ulipelekea kutolewa kwa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ambayo ilisababisha mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri. Hatua hii ilikuwa ni hatua muhimu sana katika kuweka mizizi ya utamaduni wa uwajibikaji nchini kwetu. 

Wakati Kamati inajiandaa na Taarifa yake ya Mwaka 2012 kwenye Mkutano wa Kumi na Moja, Spika ameivunja. Ikumbukwe maagizo ya mwisho ya Kamati ya POAC yalikuwa ni kuzuia mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mikopo kwa Serikali bila ya kuwapo kwa mikataba. Hivi sasa Serikali imekopa zaidi ya shilingi 1.2 trilioni kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa ajili ya miradi mbalimbali, mikopo hiyo ya fedha za wafanyakazi haina mikataba yeyote na POAC iliona hatari ya fedha za wafanyakazi kupotea na kuleta madhara makubwa kwa wastaafu nchini.
 
Katika maelezo yake Spika amesema nchi nyingine duniani hazina kamati kama ya POAC. Nadhani waliomshauri Spika waliamua kumdanganya na yeye akadanganyika. Nchi zote za Afrika Mashariki zina Kamati ya kusimamia Mashirika ya Umma. Kenya inaitwa Public Investments Committee, Uganda inaitwa State Corporations Committee na hata nchi nyingine kama India ambazo zinafuata utamaduni wa kibunge kama wetu wanayo na wanaita Public undertakings Committee. Nchini Afrika Kusini sio tu kuna Kamati ya Mashirika ya Umma bali pia kuna Wizara inayosimamia Mashirika ya Umma (Ministry of Public Entreprises). Kimsingi Kamati ya POAC ilipaswa kuongezewa nguvu zaidi ili kufikia uwezekaji wa Serikali kwenye makampuni binafsi badala ya kuifuta. Uwezekaji wa Serikali kwenye makampuni kama BP, AirTel, Kilombero Sugar, SonGas nk hauna uangalizi wowote.
 
Uamuzi wa Spika wa Bunge kuifuta Kamati ya POAC ni uamuzi unaorudisha nyuma juhudi za nchi kujenga asasi za uwajibikaji, ni kinyume cha sheria ya ukaguzi wa umma inayotaja Kamati tatu za Bunge za kusimamia fedha za Umma na ni kinyume cha Katiba ya nchi. Spika wa Bunge anasema kazi za Kamati ya POAC zitafanywa na Kamati ya PAC; Tanzania ina jumla ya Mashirika ya Umma 258 yenye thamani ya shilingi trilioni 10.2 mpaka mwezi Juni mwaka 2012, hata kamati ya POAC ilikuwa haiwezi kushughulikia Mashirika yote ya Umma katika mwaka mmoja, PAC itawezaje kusimamia Wizara za Serikali, 

Mikoa na wakala za Serikali na wakati huo huo Mashirika ya Umma 258? Kwa vyovyote vile Taifa linarudi miaka ya kabla ya 2008 ambapo Mashirika ya Umma yalikuwa kichaka cha kuiba fedha za Umma. Hivi karibuni Kamati ya POAC iligundua mtindo wa Wizara za Serikali kupeleka fedha Serikali kwenye Mashirika na kutumia kifisadi ili kukwepa ukaguzi kwenye Wizara (Wizara ya Utalii ilipeleka zaidi ya shilingi 600 milioni Bodi ya Utalii mwaka 2010/2011). Ikumbukwe pia wizi wa EPA, MEREMETA na hata uuzaji holela wa baadhi ya mali za Serikali kupitia ubinafsishaji ulifanyika nyakati ambazo Bunge halina kamati inayosimamia Mashirika ya Umma.
 
Kwa vyovyote vile Spika wa Bunge amedhihirisha namna ambavyo anafanya maamuzi bila kuzingatia maslahi ya nchi wala kuzingatia historia ya uwajibikaji katika nchi. Namna mijadala ya Bunge inavyoendeshwa, namna anavyobeba ajenda za Serikali katika kujenga Bunge kibogoyo na namna anavyofanya maamuzi kwa kukurupuka, inahitaji hatua za kuokoa misingi ya uwajibikaji wa nchi. Ni lazima Spika wa Bunge adhibitiwe kwa kuondolewa katika nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Spika lazima ajue kwamba Mamlaka yapo kwa wananchi na yeye ni msimamizi tu wa vikao vya Baraza la wananchi liitwalo Bunge. Anna Makinda lazima adhibitiwe, vinginevyo nchi yetu itaumia.

TASAF YATUA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0


Na Mwandishi Maalum

  Mfuko wa Maendeleo ya  Jamii (TASAF) umeelezwa kama mfano halisi unaoweza kuigwa  na jumuiya ya kimataifa hususani katika eneo la   uwezeshaji  wa kipato kwa  wananchi maskini,dhana ya ushirikishwaji, upunguzaji wa umaskini , upatikanaji wa ajira na ulinzi wa Jamii.

“ tunaweza  kujifunza mengi kutoka TASAF ni mfuko ambao unafanya kazi kubwa na nzuri, nimekwenda Tanzania nimejionea mwenye. Wakati mwingine ili kufahamu  lipi linawezekana, na lipi haliwezekani, ni jambo jema sana kama ukienda na kushuhudia mwenyewe badala ya kusoma au kusikia kutoka  kwa watu wengine”

Hiyo ilikuwa ni kauli ya  Bw. Mawutor Ablo, Mkurugenzi wa  Ulinzi wa Jamii, Wizara ya Ajira na Ustawi wa jamii nchini Ghana. Bw. Ablo alikuwa mmoja wa wana-jopo watano waliokuwa wakichangia  majadiliano ya mada iliyohusu “ Mwelekeo wa Jamii katika Ajenda ya Kimataifa ya  Maendeleo baada ya  mwaka 2015.

Majadiliano hayo ni sehemu ya   mada kadhaa zinazohusu  Mkutano wa 51 wa Kimisheni ya Maendeleo ya Jamii, mkutano huu wa wiki moja  ambao maudhui yake ni “ kukuza uwezeshaji wa watu katika kufanikisha uondoaji wa umaskini, ushirikiano wa kijamii, ajira kamili na zenye tija”,  unafanyika hapa  Makao  Makuu ya Umoja wa  Mataifa ukiwashirikisha mawaziri, wanazuoni, watafiti wa masuala ya kijamii  na taasisi zisizo za kiserikali.

Bw. Mawutor Ablo amekwenda mbali zaidi kwa kusema tunapojadiliana kuhusu kile tunachotakiwa kufanya baada ya 2015, miradi kama ya TASAF inatakiwa kuchukuliwa kama sehemu ya mafaniko na mfano wa kuigwa. Wala hatuna sababu ya kwenda mbali, mifano hai na yenye mafanikio ipo”. akasisitiza.

Kauli hiyo ya Bwa. Ablo iliungwa mkono na mwana-jopo mwingine, Dkt. Timo Voipio ambaye ni Mshauri  Mwandamizi  kuhusu Sera ya Jamii  na Kazi za  Heshima katika  Wizara ya Mambo ya Nje ya  Norway. Yeye alieleza kwamba licha ya kwamba tafiti zake nyingi kuhusu maendeleo ya jamii amezifanyia Afrika, lakini pia  ameishi Tanzania kwa miaka kadhaa na  amejionea mwenyewe kazi nzuri inayofanywa na TASAF.

“ inawezekana kabisa kuwa na sera za ulinzi wa jamii, uwezeshaji wao,  kuwapunguzia makali ya umaskini na kubwa zaidi ushirikishwaji katika maamuzi ya mambo yanayowahusu”. Nimeyaona haya kupitia TASAF, inawezekana kukawa na ugumu katika kubadili  mfumo wa maisha  hususani kwa  mwananchi maskini ambaye amezoea  kulima muhogo ukamwambia alime mahindiaina” akasema Dkt. Voipio.


Lakini  hili inawezekana kwa kupitia miradi kama ya  TASAF ambayo inasisitiza sana ushirishwaji wa wananchi wenyewe” kwa mujibu wa  Dkt. Timo Voipio Akizungumzia kuhusu viashiria vya maendeleo ya binadamu, bila ya kuingia kwa udani,  Dkt. Voipio anasema Tanzania na Kenya kama nchi jirani zina ushindani Fulani linapokuja suala la viashiria zima la viashiria hivyo kila nchi ikijitahidi kuipiku nyingine. Ushidani ambazo anasema anaamini unafanyika katika nchi nyingi majirani.

Naye mshiriki mwingine wa majadiliano hayo,  Bwa, Stephen Pursey, ambaye ni Mkurugenzi wa Muunganiko wa Sera na mshauri wa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kazi duniani ( ILO) yeye alibainisha kwamba suala la  upatikanaji wa ajira ni jambo ambalo limekuwa likizungumzwa na kujadiliwa na kila mtu achia mbali serikali.

Hata hivyo anasema ingawa  ukosefu wa ajira  ni tatizo linaloendelea duniani kote. Bado anaamini kuwa ajira zinaweza kutengenezwa  kupitia ubunifu wa sera na kuwajibika. Akasema bado anakumbuka kauli ya Bado  Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa ambaye katika mikutano  ya  Kamisheni.kuhusu Athari za Utadawazi katika Jamii,alivyokuwa  akielezea namna alivyokuwa akiwabana mawaziri wake wanapowasilisha maandiko yao katika Baraza la  Mawaziri

“ Mkapa alikuwa akitueleza kwamba kila waziri aliyekuwa anawasilisha  mpango wake katika Baraza la Mawaziri alikuwa akimuuliza ni ajira ngapi zitazalishwa kutoka na mpango au mradi unaowasilishwa”.

Ni  wazi kwamba ufuatiliaji wa aina hii uliwafanya mawaziri husika kuhakikisha kwamba suala la ajira lilikuwa linapewa uzito wa peke yake, na hili ni jambo ambalo linaweza kuwa mfano wa kuigwa   kama kweli tunataka kupunguza tatizo la ajira hususani kwa vijana” akasisitiza Bw. Stephen Pursey.

Akasema ajira  au uwezeshaji wa kipato si lazima ziwe kazi za maofisini tu. Hata kwa kuwapatia wanakijiji tenda ya kutengeneza madawati  kwaajili ya shule yao, au ujenzi wa barabra ya  eneo lao, tayari unakuwa umewapatia ajira na kipato hataka kama ajira hiyo ni ya muda lakini tayari  umewawezesha.

Kama hilo halitoshi, Mtaalamu huyo kutoka ILO alikwenda mbali zaidi kwa   kusisitiza haja na umuhimu wa kuwa na vipaumbele vinavyotekelezeka. Anasema  haiwezekani  kuwa na vipaumbele vingi, tafsri ya kuwa na vipaumbele vingi  iwe katika eneo lolote lile, maana yake ni moja tu huna kipaumbele.

Akaongeza kwamba watu wanajua  nini wanataka hata kama watu hao ni maskini, wanajua nini wanataka wakati gani, mahali gani na kwa mazingira gani, kwa  hiyo tunapotafakari  nini kifanyike  baada ya 2015 lazima pia tuheshimu matakwa ya watu, wao wanajua nini wanataka badala ya kuwapandikizia au kuwaamulia.

Muhimili wa Maendeleo ya Jamii, ni kati ya mihimili mitatu inayounda maendeleo endelevu na  ambayo Jumuiya ya Kimataifa imekuwa  ikiyafanyia kazi  katika nyanja mbalimbali  hususani kupitia utekelezaji wa   Malengo ya Maendeleo ya Millenia na mkazo mkubwa  ukiwa katika kupunguza au kuondoa umaskini,  kupungua pengo  kati ya walio nacho na wasio nacho, utafutaji wa vyanzo  vya ajira hususani kwa vijana, ulinzi wa jamii, elimu, hifadhi ya mazingira na ukuaji wa uchumi.
Kupitia mkutano huu wa Kamisheni ya  Maendeleo ya Jamii washiriki  wanajadiliana na kukusanya mawazo ambayo yatachangia katika maadalizi ya sera ya Jamii na kuchangia mwelekeo vipaumbele vya nini kifanyike baada ya mwaka 2015, mwaka ambao  utekelezaji wa  Malengo  Nane ya  Maendeleo ya Millenia  utafikia   ukingoni.

TOVUTI YA USHAURI NA MABORESHO KWA WANANDOA YAZINDULIWA DAR.

$
0
0


Heshima kwenu Wadau.

Wakati mwingine wanandoa upitia kwenye wakati mgumu katika mauhusiano yao,mambo yanaweza kuonekana kuwa ya  kuchosha kukera na kukwaza, yaweza kuwa kwasababu ya mabishano yatokanayo na  wivu,kiburi,fedha,mapenzi na sababu nyingine nyingi kitu ambacho upelekea amani kutoweka ndani ya Ndoa na mapenzi kupotea kabisa.Pamoja na hayo yote kutokea  bado wanandoa wanayo nafasi ya kurekebisha mapungufu yao na kurejeasha amani na upendo katika ndoa zao.Hili linaweza kufanyika kwa njia mbali mbali moja wapo ikiwa Retreat.

Couples Consult Tupo kwaajili ya kuwaandalia wanandoa(Couples Retreat) Mazingira muafaka  ya kuzungumza tofauti zao na kujenga upya ndoa zao kwa ushauri kutoka kwa wataalamu kwa mambo ya kifamilia,kiafya,kimahusiano,kiujasiriamali na kiuchumi.Kwa maelezo zaidi tembelea tofuti yetu:www.coupleconsult.comtunapatikana pia kwenye facebook:http://www.facebook.com/pages/Couples-Retreat-Consult/281753185281342 na Twitter:https://twitter.com/CouplesC.
Karibu sana

Rais Kikwete afungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu mjini Dodoma

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akielekeza jambo wakati wa ufunguzi wa Semina maalum kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa iliyofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa White House makao makuu leo.Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM bara Pius Msekwa.Wengine katika picha ni Rais Wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(Wapili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana(wanne kushoto), na kulia ni Makamu Mwenyekiti CCm Bara Ndugu Philip Mangula
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM taifa wakihudhuria semina maalum iliyofunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White House,Makao makuu ya CCM mjini Dodoma.Picha na Freddy Maro.

Mwenyekiti wa CCM ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa White House uliopo katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.Rais Kikwete amefungua na kuongoza semina kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa ambayo pamoja na mambo mengine itachagua wajume wa Kamati kuu.

WHEN LOOKING AT YOU, BENEDIKT

$
0
0


HAPPY 2ND BIRTHDAY


My dearest son, Benedikt Fulbright Makulilo,

Guess what Benedikt? It is another February 10th. On every change of calendar year, such day is very significant and special to you. It was on February 10th 2011 at 5:42pm Pacific Time when you were born. Today February 10th 2013 you have turned 2 years old. 

Celebration is not because of the change in date/number rather is the significant changes you have been through in growing as a person, how you have been influential to your mother and I as parents, spouses and persons. But above all, it all about you – you are such a big Blessing from God, and in every way your mother and I have to celebrate the Blessing. It is indicated in the Holy Bible, “…Children are a gift from God; they are real blessing…” (Psalm 127:3)


When looking at you, Benedikt I see your entire future largely depends on me. My behaviors, teachings, love, what I do, how I do and so forth have great impact in your childhood upbringing and will impact your future positively or negatively. As a father, I have been so proud to have my father as my father – in every way I thank him and my mother for their hard work as parents. I would like you not to regret in any way for me to be your father, so I have to make it the best of it as it is written “Train a child in the way he should go, and when he is old he will not turn from it” Proverbs 22:6. It is a huge task as a father to make everything right, but remember I am still a human being. I have my own strengths and weaknesses, learn from me, correct me in a respectful manner, and challenge me in appropriate ways. I have also to learn so many from you; it is a mutual thing between us. 

I will try my best not provoke you to anger as we are given special wisdom in the Bible “Fathers, do not provoke your children to anger, but bring them up in the discipline and instruction of the Lord” (Ephesians 4:6). Benedikt remember to have respect not only to your parents but also to everybody and not because of financial status rather because they are human beings. In Exodus 20:12 you have been told to have respect to your parents “Honor your father and your mother, so that you may live long in the land of the Lord your God is giving you”. In respect, both your mother Marie and I have been respecting you, and will continue to respect you – so do you.


In your first birthday I wrote you a letter. Your mother and I promised you a very special gift. We promised you at one point we are going to start a scholarship fund under your name. We have fulfilled the promise by starting The Benedikt Fulbright Makulilo Scholarship. It is your scholarship; you are in charge of it. But for now because of your age, we will help you on setting up most of things and as time goes on other things which you would like to include will be added in your scholarship fund. The scholarship will be helping poor children in Africa mainly Tanzania to support their dreams through education (books, uniforms, fees, stationeries etc.)


Since January 2013 I have been donating plasma at Octapharma Plasma. In donating plasma one becomes somebody’s hero for life. Plasma helps patients who suffer from variety of illness including burns, shock, infection, trauma, and breathing disorders. The Octapharma Plasma provides small amount of money in each donation as thank you for generosity of donors in life-saving therapies. All the money I have been receiving through Plasma Debit Card I direct donate to your scholarship. On this special day – your birthday, I donate $200 (Two hundred US Dollars) to The Benedikt Fulbright Makulilo Scholarship so that you can also help other children to reach their dreams. I will continue donating plasma and at the same time all the money I will be donating to your scholarship.




Benedikt, as your father I am very much proud of you. You have been insisting on your birthday what you want…..you have been saying you want Donuts with sprinkles as well as getting into the bus and trolley tour. I am definitely going to give you bus and trolley tour. Your mother has already made arrangements for special donut with sprinkles as you requested. It is written, “If a son shall ask for bread for any of you that is a father, will he give him a stone? Or if he asks a fish, will he for a fish give him a serpent? (Luke 11:11). The answer is definitely no; a father will neither give his son a stone nor serpent in place of bread or fish respectively. So apart from what you requested for your birthday, your mother Marie and I will take you to SeaWorld San Diego to experience Shamu show and other attractions.


Your mother has been extremely helpful and the rock of our family in taking care of you and me. She has been outstanding and her love to us is unexplainable. She is amazing. Please continue to be a good boy especially when I will be going away for a little while as part of my job.


HAPPY 2ND BIRTHDAY

I love you so much, son

It’s your loving Baba


Ernest Boniface Makulilo


roma afunika tamasha la tabasamu na Tigo jioni ya leo.

$
0
0


Bofya video hiyo hapo juu kuona ROMA alivyoitikisa Cocobeach jioni ya leo.
Msanii nyota wa muziki wa hip hop hapa nchini ajulikanae kwa jina la Kisanii ROMA,akitumbuiza jukwaani,mbele ya umati wa watu  mapema jioni ya leo ambapo kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imezindua kauli mbiu yake mpya iitwayo "Tabasamu,upo na Tigo na kuchana na ile ya zamani iliyokuwa ikiitwa 'Jielezee mwenyewe',tamasha hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa limefanyika kwenye fukwe za Coco Beach,jijini Dar  na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.Tamasha hilo limeratibiwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd. 
Mshabiki wakijiachia vilivyo mara baada ya msaani wa hip hop Roma kupanda jukwaani na kuwasha moto vilivyo,ama kwa hakika Coco beach palikuwa hapatoshi kabisa.
Msanii nyota wa muziki wa Bongofleva kutoka kundi la TMK Wanaume Halisi Sir Juma Nature sambamba na wasanii wenzake wakizikonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliofika mapema jioni ya leo kwenye fukwe za Coco beach,ambapo kampuni ya simu za mikononi ya Tigo imezindua kauli mbiu yake mpya iitwayo "Tabasamu,upo na Tigo na kuchana na ile ya zamani iliyokuwa ikiitwa 'Jielezee mwenyewe',tamasha hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa limefanyika kwenye fukwe za Coco Beach,jijini Dar  na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.Tamasha hilo limeratibiwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd. 
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo
Msanii wa kizazi kipya kutoka THT,ajulikanae kwa jina la Rachael akitumbuiza mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia uzinduzi wa kauli mmpya ya kampuni ya Tigo kwa wateja wake.
Naitwa Mr Blue kijana machachari sana awapo jukwaani,pichani akiwarusha wakazi wa jiji la Dar na viotongoji vyake waliofika kulishuhudia tamasha hilo likirindima jioni ya leo kwenye fukwe za Coco beach.

Pichani juu ni kikundi cha wasanii wa muziki  wa kizazi kipya kutoka TMK Orijino likiongozwa na Mh Themba sambamba na Chege wakilishambulia jukwaa namna ya kipekee kabisa.
Ma-Mc wakiwa kazini
Shemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha hilo lililofanyika kwenye fukwe za Coco Beach,jijini Dar.

KINYWAJI CHA BAILEYS KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL) CHAFANIKISHA BOOKERS PARTY KATIKA HOTELI YA SEA CLIFF JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 BAADHI YA WAGENI WALIOHUDHURIA BOOKERS PARTY WAKIFURAHIA KINYWAJI CHA BAILEYS NA KEKI ZILIZOTENGENEZWA KWA KUTUMIA KINYWAJI HICHO KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL)
MENEJA MASOKO WA DSTV  FURAHA SAMALU AKIFURAHIA KINYWAJI CHA BAILEYS NA KEKI ILIYOTENGENEZWA KWA KINYWAJI HICHO KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI(SBL) KATIKA BOOKERS PARTY ILIYOFANYIKA SEE CLIFF MWISHONI MWA WIKI.
  MENEJA MAUZO NA MASOKO KUTOKA HOTELI YA SEE CLIFF JEAN FRANCOIS VARET AKIKABIDHI ZAWADI YA BAILEYS KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KWA MFANYAKAZI  WA DSTV GABRIEL ERINEST KATIKA BOOKERS PARTY ILIYOFANYIKA HOTEL YA SEE CLIFF MWISHON MWA WIKI
MABALOZI WA KINYWAJI CHA BAILEYS KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL) WAKITOA UFAFANUZI KUHUSU KINYWAJI HICHO  KWA WAGENI WALIOHUDHURIA BOOKERS PARTY ILIYOFANYIKA KATIKA HOTELI YA SEA CLIFF JIJINI DAR ES SA

Azania Bank donates 5m/- to support 2013 Breast Cancer Campaign

$
0
0
 The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya (left) hands over a 5m/- dummy cheque to the Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee (right) being support for the 2013 Breast Cancer Awareness Campaign organized by the hospital. 
 The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya (left) hands over a 5m/- cheque to the Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee (right) being support for the 2013 Breast Cancer Awareness Campaign organized by the hospital.
 The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya briefs reporters at the weekend on the bank’s donation to the 2013 Breast Cancer Awareness campaign by Aga Khan Health Service. Centre is the Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee and the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left). 
 The Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya shares a light moment with Zain from Aga Khan Hospital
The Aga Khan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee (left) explains a point to the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (right) shortly after the event
============  ======== ========

Azania Bank donates 5m/- to support 2013 Breast Cancer Campaign

By Staff Reporter.
                                                                                      
AZANIA Bank Limited has donated 5 million shillings to Agha Khan Health Services that will help boost this year’s breast cancer awareness drive in a bid to create public awareness on the fatal disease.

Speaking during a handover ceremony at the bank's headquarters in Dar es Salaam, Azania Bank Director in the Managing Director's office (Treasury Management and Business Development) Godwin Seiya, said the bank is committed to support various social programs as part of its Corporate Social Responsibility (CSR) and in the course of giving back a certain percentage of the Bank earnings to the society they work with.

Mr. Seiya noted that his bank has decided to support the campaign to sensitize women and the public in general to make routine tests at least once a year, with the view of minimizing risks for many women who are potential future victims.  "Records indicate that up to 1.5 million women have breast cancer problems. Tanzania accounts for 1,307 of the breast cancer victims. We at Azania Bank believe that the only way to minimize the risk is through public sensitization.

"We believe with proper information dissemination, victims of breast cancer   can seek early medication thus increasing their chances of living. We are today donating five million shillings to support this year’s Breast Cancer awareness campaign," he said. The Aghakhan Hospital Medical Director Dr. Jaffer Dharsee during the event said the campaign targets to screen up to 5000 women throughout the country this year.

He said last year’s campaign that was held in Dar es Salaam, Mtwara, Dodoma and Lindi cost upto $ 100,000 (Tsh 160m) and reached 3000 women in the four regions. “We will continue with the campaign this year and our target is screening 5000 women across the country this year. We will also bring on board cervical cancer screening this year. We call upon various corporate companies to render support to the campaign,” he said.

Safari za ndege ya ATCL kwenda Mtwara zaanza

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho, akizungumuza na wageni waalikwa, abiria waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja na maofisa wa uwanja wa ndege la Mtwara (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoani Mtwara , mara tu baada ya kutua ndege hiyo uwanjani hapo mwishoni mwa wiki.
 Meya wa Mtwara Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoani Mtwara, akizungumuza na wageni waalikwa, abiria waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja na maofisa wa uwanja wa ndege la Mtwara (hawapo pichani) mara tu baada ya kutua ndege hiyo uwanjani hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho na kulia ni Meneja Rasilimali watu na Utawala, Bi. Halima Nabalang’anya. Picha na mwandishi wetu.  
Baadhi ya abiria waliopanda dege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), wakitembea kuelekea katika chumba cha kupumzikia abirai, wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za shirila hilo mkoani Mtwara iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
======  ======  ========
Safari za ndege ya ATCL kwenda Mtwara zaanza

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) mwishoni mwa wiki lilizindua upya safari zake za moja kwa moja za Dar es Salaam-Mtwara na kuahidi kuongeza idadi ya safari hizo na kutoza nauli nafuu.

Akizungumza baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho alisema kuwa kurejeshwa kwa huduma za usafiri wa anga na shirika hilo la taifa mjini Mtwara ni chachu ya mapinduzi makubwa katika usafiri wa anga mjini hapo kwa kuhakikisha kuwa abiria wanapata huduma bora na za kiushindani.

"Nataka kuwahakikishia wakazi wa Mtwara kwamba ndege yao ya taifa imekuja kuwahudumia watu wa mkoa huu. Kwa kuanzia, tutaruka Mtwara mara nne katika wiki; ikiwa ni siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili, lakini tutaendelea kufanya marekebisho ya safari kutegemeana na mahitaji. Abiria watarajie ATCL kuwapatia huduma  ambazo ni salama na za gharama nafuu, "alisema.

Mwanamvua alieleza kuwa shirika hilo litatoza shilingi 199,000 / - kwa tiketi ya kwenda na kurudi, na kuahidi kuwa shirika hilo litafanyia kazi suala la kupunguza gharama za usafiri zaidi ili kuwawezesha wasafiri wanaoenda na kutoka Mtwara kuona faida za kutumia usafiri wa anga.

Kwa upande wake, Meya wa Mtwara Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema baada ya ndege ya taifa kurejesha huduma zake mkoani Mtwara, wakati wa shirika moja la ndege kutawala utoaji huduma mkoani hapo na kulazimisha abiria kulipa nauli za juu, sasa umekwisha.

“Ninafuraha kuona shirika la ndege la taifa likiwa limerejesha huduma zake mkoani Mtwara. Kwa muda mrefu sasa usafiri wa anga hapa Mtwara imekuwa ikitawaliwa na shirika moja tu la ndege. Ukweli ni kwamba, pasikuwepo na ushindani, suala la bei mara nyingi ni changamoto kwa walaji/wateja. Abiria wa kwenda na kutoka Mtwara wamekuwa wakilipa nauli za juu. Ila kwa kuwa tuna ATCL sasa na Kaimu Mgurugenzi wa Biashara ametuakikishia, wakazi wa Mtwara na wageni wetu watapata fursa ya kufurahia usafiri wa anga ulio salama na wa gharama nafuu,” alisema Shilingi.

Meya huyo alisema kuwa idadi ya abiria wanaokwenda Mtwara imekuwa ikiongezeka sana katika siku za karibuni, kwa sababu Mtwara imekuwa na sura ya kibiashara baada ya ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia na kuwa mkoa unaozalishaji zao la korosho kwa wingi hapa nchini.

“Wawekezaji wengi wanaendelea kumiminika katika mkoa wetu, na hivi karibuni Mtwara itakuwa na muonekano tofauti kabisa. Ushawishi huu wa kuwekeza mkoani Mtwara umeongeza idadi ya abiria wanaosafiri na ndege. Nina uhakika ATCL itaona ongezeko la abiria mapema na kulifanya shirika kuongeza idadi ya safari zake mapema,” alisema.      
          
Shirika hilo litatumia ndege yake aina ya Dash 8-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, wakati huu wa mwanzoni, lakini uongozi umebainisha kuwa pale idadi ya abiria itakapoongezeka kuzidi uwezo wa Dash 8, watatumia ndege yao aina ya Boeing.

Urejeshwaji wa safari za Mtwara umekuja ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya shirika hilo pia kurejesha safari za Kigoma baada ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kigoma kumalizika.

MASHABIKI WA SOKA ZANZIBAR WALIVYOFURAHIA FAINALI AFCON 2013 KUPITIA DStv

$
0
0
Picha moja ni sawa na maneno elfu moja. Sehemu ya umati wa mashabiki wa soka Zanzibar wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali kati ya Nigeria na Burkina Faso wakati wa special screening ya fainali hiyo iliyowezeshwa na DStv ndani ya Gymkhana Club.
Experience The Spirit Of Africa- wadau wa soka ndani ya kiota cha Mtoni Marine wakiwa wenye tabasamu wakati wa fainali ya AFCON 2013.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa makini mtanange wa fainali ndani ya Mtoni Marine.Uwapo Zanzibar na unataka kuangalia michezo kama huu wa fainali ya AFCON 2013, Mtoni Marine ni sehemu inayohusika. Kila kona pametapakaa TV Screen ambazo zote, Live bila chenga hurusha matukio ya michezo kupitia DStv, wakongwe wa digitali.

Kwa zaidi ya wiki tatu zilizopita, kuanzia tarehe 19 Januari 2013 mpaka 10 Februari 2013 mashabiki wa soka barani Afrika na duniani kote walikuwa hawabanduki katika viti vyao au sofa kwa ajili ya kutizama mashindano makubwa kabisa ya soka barani Afrika ya kuwania Kombe la Mataifa Ya Afrika mashindano ambayo kwa kizungu yanajulikana kama Orange Africa Cup Of Nations. 

Wenyeji wa mashindano ya mwaka huu walikuwa Afrika Kusini. Jumla ya mechi 32 zilichezwa na zote zilionyeshwa Live bila chenga kupitia channels za SuperSport zinazopatikana kupitia DStv, wakongwe wa digitali. Wakati wa fainali, DStv kupitia kampuni mama ya MultiChoice Tanzania walijumuika na mashabiki wa soka na wadau mbalimbali visiwani Zanzibar katika viota vya Gymkhana Club na Mtoni Marine. 

Huko palikuwa na special screening ya mchezo huo wa fainali ambapo Nigeria waliibuka mabingwa (kwa mara ya tatu sasa) baada ya kuwalaza Burkina Faso kwa goli 1-0. Kwa mapana na marefu umekuwa msimu wa kufurahi na marafiki na pia kutizama jinsi ambavyo kabumbu linazidi kutamba kama mchezo unaopendwa zaidi sio tu Afrika bali duniani kote.

Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu(kushoto) akiwa na wakurugenzi wa Island Promotions, Adelina Ngalo(katikati) na Ameir Kombo.
Macho yote katika screen. Mchezo wa fainali unaendelea-Gymkana Club.
Mkurugenzi wa Island Promotions,Ameir Kombo, akisaidia zoezi la maswali na majibu kuhusiana na michuano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa Afrika-AFCON 2013. Kushoto kwake ni Mohamed kutoka IBS-, mahali ambapo unaweza kupata huduma za aina zote zinazohusiana na DStv.
Mbali na kufurahia Soka, mashabiki mbalimbali walijishindia zawadi mbalimbali kutoka DStv.
Ni SuperSport, Ni Zanzibar, Ni DStv.
Sehemu ya umati wa mashabiki wa soka waliofurika kushuhudia Live mchezo wa fainali ya AFCON 2013.
Baadhi ya washindi wa zawadi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na DStv wakati wa special screening ya fainali ya Africa Cup Of Nations wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa DStv akiwemo Meneja Masoko wa MultiChoice,Furaha Samalu.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images