Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 26 | 27 | (Page 28) | 29 | 30 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Vanessa Mdee hugs a fan
   Vanessa Mdee's fans watch her perform
   Vanessa Mdee, Heineken Country Manager - Uche Unigwe, Eskado Bird

  ========  ======= ======
  Vanessa Mdee serenades fans at Heineken House


  Tanzania's newest hit maker, Vanessa Mdee, had a great opportunity this weekend to thank some of her supporters and friends at a meet and greet event organized by Heineken Tanzania at their offices in Dar es Salaam.


  At the meet and greet which was attended by many of Bongo's top celebrities, Vanessa entertained the audience by singing her current smash hit single, Closer, as well as a medley of other songs in which she has had guest appearances. She also gave the guests a short history of her musical career.


  In addition to Vanessa Mdee's performance the fans in attendance also had the great pleasure of having all the B Hitz group performing their recent release-'Press Play', followed by a surprise appearance from another Bongo flavor artist, Channel O and Kora Award nominee, C Pwaa performing his song, 'Mmmh',Speaking of Vanessa, Heineken Country Manager, Mr. Uche Unigwe, said Vanessa is a brand Heineken is proud to be associated with.

  'We at Heineken are very happy to host Vanessa tonight. Vanessa has been a huge supporter of Heineken since we started marketing efforts in Tanzania one year ago and tonight's meet and greet is a great opportunity for us to give back and say thank you to Vanessa for all of her support" said Unigwe.


  0 0


  Bendi ya Akudo Impact wazee wa masauti ,siku ya Jumapili tarehe 17, Februari 2013, itatoa burudani katika shindano la Taifa la kumsaka Mrembo wa Utalii mwenye kipaji kati ya warembo 40 waliopo kambini Ikondelelo Lodge wakijiandaa kushiriki Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 zitakazo fanyika mwisho wa mwezi huu katika Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

  Katika shindano hilo la Vipaji , ambalo litafanyika katika Ukimbi wa Jeshi wa Msasani Beach Club Jumapili kuanzia saa nane mchana ,pamoja na Bendi hiyo ya Akudo Impact , wasanii wengine watakao tumbuiza ni pamoja na mwanamuziki wa kimataifa Che Mundugwao, Msanii mdogo chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Geneous na burudani za ngoma za asili kutoka katika kundi kongwe la Kaole  Sanaa Group wakiomgozwa na mwana dada mahili katika uchezaji wa ngoma za asili Mariam Kweji aka kalunde wa Bongo Movie.


  Shindano hilo la Vipaji ni moja ya mashindano ya awali ya kuwania tuzo mbalimbali kabla ya Fainali kuu,ambapo washiriki wote watashindana kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila mbalimbali ya mikoa wanayo iwakilisha. Mikoa hiyo na majina ya washiriki katika mabano ni  Arusha (Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera 1(Elline Bwire),  Kagera2 (Jania Abdul), Kagera 3(Mulky Uda),  Kilimanjaro (Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni), Manyara (Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija Said),Tanga (Sarafina Jackson), Ruvuma 2 (Leah Makange), Tabora (Magreth Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma (Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani (Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange).

  Wakizungumzia kwa nyakati tofauti shindano hilo la Vipaji,Rais wa Miss Tourism Tanzania International Organisation ,wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo , alisema kuwa mandalizi karibu yote yamekamilika kuanzia ngazi za warembo hadi burudani za bendi, ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya. Hili litakuwa ni tukio kubwa na la kihistoria kuwahi kufanyika Tanzania ambapo Utalii, Urembo na Utamaduni wa ngoma za asili vitaonyeshwa kwa pamoja jukwaani, lakini kivutio cha pekee ni jinsi mabinti wa kizazi kipya tena warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na vyuo Vikuu watakavyo onyesha maajabu ya kusakata ngoma za asili kwa umahili mkubwa na wa pekee.

  Shindano la Miss Utalii Tanzania mwaka huu limedhaminiwa na wadhamini mbalimbali wakiwemo Coca Cola Kwanza Limited, Daja Salon, Mtwana Catering Services Enterprises, Zizzu Fashion, Global Publishers, Ikondelelo Lodge, Clouds Media Group, Tone Multimedia Group,Valley Spring na www.misstourismorganisation.blogspot.com.

  Katika Shindano hili viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo 5,000 kwa viti vya kawaida, 10,000 kwa V.I.P 2, na 30,000 kwa V.I.P 1 pamoja na Chakula.
  Asante,
  Erasto G. Chipungahelo
  Rais

  0 0


   Mabondia Omary Ramadhani kushoto na Deo Njiku wakitunishiana misuri baada ya kusaini mkataba kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  ===========  =======  ======
  MABONDIA Deo Njiku wa Morogoro na Omary Ramadhani wataingia uringoni  February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese 14 kuwania Ubingwa wa Tanzania PST 

  Mpambano huo wa aina yake unatarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana kila mtu kuwa na rekodi nzuri mpambano uho utakaosindikizwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya  Godfrey Silver na Adam Yahya ambapo mipambano hiyo itakuwa ya raundi kumiHuku kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' atampandisha kwa mara ya kwanza bondia wake mpya Iddy Mnyeke kuvaana na Sadiki Momba mpambano utakaopigwa kwa raundi nne

  Mgeni rasmi siku hiyo anatsrahjiwa kuwa ni Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela atakaewafisha mikanda ya ubingwa

  Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.  michezo

  ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.  

  Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.  

  Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada na Mtandao wa Vodacom Tanzania Bw.Charles Matondane akiongea kwenye simu na mmoja wa washindi aliejishindia shilingi Milioni 5 katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu na Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Abdallah Hemedy.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (kushoto)akionesha moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya"MAHELA"aliejishindia kitita cha shilingi Milioni 5 katika promosheni hiyo inayoendelea kuchezeshwa na kampuni hiyo,katikati ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy,anaeongea kwa simu ni  Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada na Mtandao wa Vodacom Tanzania Bw.Charles Matondane.

  0 0

  Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini  wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.


  Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.

  Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu. Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.

  Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE,YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.  Kutokana na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia.

  Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.  Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45),Sadick Yahaya(40),Yasin Rajab(56),Vicent Damon(22),wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita.

  Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.  Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.

  Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.

  Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.

  Habari picha kwa hisani ya Gsengo Blog.

  0 0


  Naomba msaada wakoLeo nimepoteza wallet yangu majira ya saa tano na nusu asubuhi. 

  Sina hakika sana ni wapi lakini mara ya mwisho nimesihika nikiweka mafuta pale Total Petrol Station ya Mlimani City. Niliweka mafuta kisha nikalipa pesa. Nilipowaomba risiti yule muhudumu akaniomba nisogee mbele kidogo ningoje waniletee risiti maana kulikua na magari mengi kidogo yanatangoja huduma , hivyo nilisogeza mbele kidogo kisha nikapaki na ili kuokoa muda, nilishuka kumfuata aliyekua ananiletea risiti ili kuichukua. 

  Sasa ninahisi nilipotoa pesa sikurudisha wallet mfukoni bali niliiweka juu ya mapaja na hivyo niliposhuka huenda niliingausha chini na sikugundua. Nimekuja kugundua tayari niko Ukonga nilipokuwa nakwenda. Nimejaribu kufuatilia sijaipata hadi sasa hivi. Ndani ya wallet kulikua na pesa si, vitambulisho, mastercards za bank tatu, leseni yangu ya udereva, kadi ya bima ya afya (green card), kitambulisho cha kazi na vitu vingine nisivyovikumbuka kwa haraka.

  Business cards zilikua zimeniishia hivyo sina uhakika kama kuna kitu kilichokua na mawasiliano ya namna ya kunipata kama vile namba za simu. Kitambulisho changu cha kazi kinaonesha kuwa ni mwajirwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mlimani.

  Kwa atakayekuwa ameikota ninaomba na ninatanguliza shukurani zangu kwa kunisaidia kunipa vilivyomo.

  Namba zangu za simu kwa ajili ya mawasiliano ni:  0782 581941 au 0 713 581941  au 0756 581941

  ASATENI.

  Mathew Mndeme (MM)
  Department of Computer Science and Engineering 
  University of Dar es Salaam
  P.O. Box 35062, Dar es Salaam.
  Phone: +255 (0) 782 581941 / 713 581941 / 756 581941

  0 0

  Digital World Training Centre ni Kituo kipya kabisa na chenye hadhi ya juu,kinachotoa huduma kama za mafunzo ya Computer Introduction,Accounting Packages,Office Packages,Internet na Web Designing.

  Tupo jijini Tanga , Custom Road near TANESCO Ufundi.

  Kwa mawasiliano zaidi tupigie kwa namba zetu zifuatazo.

   +255 655 33 13 74
   +255 784 33 13 74
   +255 767 33 13 74


  0 0


     Meneja masoko wa vinywaji vikali kutoka kampuni ya bia ya Serengeti  Emillian Rwejuna akiwaelezea wanahabari jinsi kampeni hiyo inayofanyika katika supermarket mbalimbali huku akionyesha baadhi ya zawadi ambazo wapenzi wa Baileys wanapata.
   Mteja wa Baileys akijaribu bahati yake katika msimu wa valentine ndani ya supermarket ya Shoppers Plaza. 
   Katika picha ya pamoja Thomas Michelis akiwa na mke wake baada ya kumkabidhi ua kutoka Baileys ishara ya upendo
   Thomas Michelis akisoma kipeperushi na kupata maelekezo kutoka kwa balozi wa kinywaji cha baileys katika supermarket ya Shoppers Plaza, kuhusu kinywaji hicho na zawadi zinazotolewa  katika msimu huu wa Valentine

  Kampuni ya bia ya Serengeti inaendelea kufanya kampeni maalumu kwa msimu wa valentine kwa wapenzi wa kinywaji cha Baileys kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao zawadi hizo zinatolewa katika supermarket za Mlimani City, Uchumi na Shoppers Plaza kwa wale watakaonunua baileys wanapata t-shirt, maua, chupa ya Baileys na kubwa zaidi ni kupata bahati ya kula chakula cha jioni katika mgahawa wa kisasa wa Akemi uliopo  jijini  Dar es Salaam.

  0 0


   Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa kuendelea na semina, leo kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa semina iliyoanza jana, na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk. Sheni na Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo  ukumbini na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo.
   Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
   Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta.
   Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na kuweka kumbukumbu ya mijadala inayozungumzwa kwenye mkutano huo
   HII UNAONAJE?  Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na Mzee Mtandika.
   TUKIFANYA HIVI MAMBO YATANYOOKA AU SIYO? Inaelekea ndivyo Dk. Asha-Rose Migiro alivyokuwa akisema kumwambia Nape katika mazungumzo yao ukumbi kabla ya kikao.
   Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe kwenye kikao hicho.
  Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kikao kuanza.Picha kwa hisani ya Bashir Nkoromo.

  0 0

    Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid akikabidhi zawadi ya trophy kwa Dkt. Yakiya kwa kutambua mchango 
    Dkt. Yakiya akiwa amepozi na zawadi yake,pichani kati ni  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbalawa, 
    Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Dkt. Yakiya Amano akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa
   Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, akimkaribisha Dkt. Yakiya ili atoe hotuba yake
   Wageni waalikwa wakimsikiliza Dkt. Yakiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA katika ukumbi wa TFDA Makao makuu
    Mchunguzi wa Chakula katika maabara Bw. Rajab Mziray akitoa maelezo kwa Dkt. Yakiya na wageni wengine katika maabara ya chakula 
    Mtaalamu wa uchunguzi wa dawa Bw. Yonah Hebron akitoa maelezo kuhusu uchunguzi wa dawa  katika maabara ya TFDA kwa Dkt. Yakiya na wageni wengine
  Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akimwongoza Dkt. Yakiya pamoja na wageni wengine kuelekea maabara ya TFDA

  ======== =====  ==========

  Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Atomik Dr. Yukiya Amano kwa TFDA

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Atomik (IAEA), Dkt. Yukiya Amano, amesifu kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika udhibiti wa bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba katika Tanzania kwa lengo la kulinda afya ya wananchi.

  Dkt. Yakiya Amano ambaye yupo katika ziara ya siku mbili nchini Tanzania, ametembelea TFDA kwa lengo la kujionea na kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayodhaminiwa na IAEA katika maabara ya TFDA.

  Katika maelezo ya utangulizi, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alieleza kuwa hadi sasa TFDA imekuwa ikitekeleza miradi miwili ya IAEA. Miradi hiyo ni URT 5024 ambao ulianza 2005 - 2009 ambapo TFDA ilipatiwa USD. 241,892 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara na ukujengewa uwezo kwa wataalam wa Maabara. Kufuatia kujengewa uwezo na shirika la  IAEA, hivi sasa TFDA inachunguza sumu kuvu, kemikali za melamine na madini tembo kwa wastani wa sampuli  za 1000 kutoka 30 za mwaka 2008/09.

  Sillo aliendelea kueleza kuwa, Mradi mwingine unaodhaminiwa na IAEA unajulikana kama RAF 5067 ulianza  Agosti 2012 utamalizika 2015 ambapo unajumuisha nchi 13 za Afrika ikiwepo Tanzania. Kupitia mradi huu, TFDA hadi sasa imepatiwa kifaa kiitwacho CHARM II cha thamani ya USD 55,015 na kemikali za thamani ya USD 6,637.

  Akihutubia watumishi wa TFDA na viongozi wengine walioshiriki katika ziara hiyo, Dkt. Yakiya Amano aliwaeleza kuwa hivi sasa kumekuwepo na  ukuaji wa uchumi, idadi ya watu imeongezeka na mahitaji wa watu yameongezeka na hivyo kusababisha uwepo wa bidhaa nyingi katika soko lakini hata hivyo suala la usalama na ubora wa bidhaa za chakula na dawa havitaweza kuachwa bila udhibiti, hivyo udhibiti lazima uende sambamba na mabadiliko yanayotokea.

  Dkt. Yakiya ameahidi kuendelea kushirikiana na TFDA katika kuhakikisha masuala ya udhibiti wa Usalama na Ubora wa bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi na vifaa tiba yanapewa kipaumbele kwa lengo la kulinda wananchi.

  Naye Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Rashid, katika hotuba yake ya kumkaribisha Mkurugenzi wa IAEA amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Washirika wa maendeleo na TFDA na kusema kuwa mafanikio ya TFDA katika kulinda afya za wananchi yamechangiwa na wadau wa kimaendeleo ikiwa ni pamoja na IAEA.

  Baada ya kutembelea Maabara ya TFDA, Dkt. Yakiya ameahidi kuisaidia TFDA katika kulipia gaharama za ufundi (USD 25,000) kwa mtaalam kutoka Kenya pamoja na ununuzi wa kifaa cha kupimia mabaki ya viuatilifu katika uchunguzi wa Chakula.

  0 0


  Hoyce Temu akimpa mkono wa pole mke wa Marehemu Daudi Mwangosi alipoitembelea familia hiyo kuifariji.

  Mwanaharakati wa kijamii Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania amefanya ziara mkoani Iringa na kupitia nyumbani kwa familia ya mwandishi aliyeuawa Daudi Mwangosi na kuwajulia hali. Hoyce Temu kwa pamoja na kundi zima la waandaaji wa kipindi cha mimi ni Tanzania waliwasili katika nyumba ya mjane huyo Bi. Itika Mwangosi kumsabahi na kutaka kujua anaendeleaje na maisha kila siku.
  Hoyce Temu akimfariji mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi alipoitembelea familia hiyo mkoani Iringa.

  Ziara hiyo nyumbani hapo ni kwa nia nzuri ya kutaka kujua jinsi anavyokabiliana na changamoto za kila siku za maisha pamoja na watoto wake wanne. Walizungumza mengi yakiwemo yale yanayomkwaza Bi. Itika Mwangosi na jitihada anazofanya ili kujikwamua. Aidha Bi. Temu akiwa amewapakata watoto wa marehemu aliifariji familia hiyo akiwataka kutokata tamaa na kuwa Mungu yupo na kwa kuwa watanzania ni wamoja mambo yatakwenda sawa.
  Hoyce Temu akiwapa kumbatio la upendo watoto wa marehemu Daudi Mwangosi.
  Bi. Itika Mwangosi akionyesha uso wa matumaini baada ya kupewa maeneo ya faraja na Hoyce Temu.

  Amezungumza na watoto kuhusu kwenda shule na kutaka kujua wanasoma shule gani na iko umbali gani kutoka nyumbani. Pamoja na mambo mengine Hoyce Temu kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania amewasihi watanzania wenye moyo wa ukarimu kumsaidia Mjane huyo ambaye hana ajira kwa hivyo ni vigumu kupata kipato cha kujitosheleza yeye na wanawe kwa mahitaji muhimu ya kila siku.
  Watoto wa Marehemu wakionyesha matumaini mapya baada ya kufarijiwa na Hoyce Temu.

  Mtanzania mwenye ufariji kwa familia hiyo anaweza kutuma kiasi chochote cha fedha kwenye namba inayomilikiwa na mjane huyo Mama Itika Mwangosi kupitia mtandao wa M-Pesa: 0767670739 ili msaada huo uwafikie walengwa.

  0 0


   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler. 

  Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Craters na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki

  Katika picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
   

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Craters  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
  Vikundi vya ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kama vinavyoonekana.
  Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB
  Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
  Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
  Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla hiyo.
  Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
  Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.
  Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.


  Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
  Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David Kafulila.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.
  Mama Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.
  Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema  kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB)  Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
  Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi  katika hafla hiyo, kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
  Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
  Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
  Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
   Balozi wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid(katikati),Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kulia) Mkurugenzi wa Shirika la Switchboard Ali Block wakionesha mabango ikiwa ni inshara ya uzinduzi wa kuwawezesha wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure,huduma hiyo inatolewa na  Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Switchboard ili kurahisisha huduma za kiafya mahosipitalini.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid (kushoto)Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (katikati)pamoja na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim,wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwawezesha wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure huduma hiyo inatolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Switchboard  ili kurahisisha huduma za Afya mahosipitalini.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  Marehemu Mzee Wilfred Mahendeka Mtaki

  Ndugu Sospeter E Mtaki wa Kimara King’ong’o jijini Dar es Salaam, anasikitika kuwatangazia kifo cha baba yake Mzazi, Mzee Wilfred Mahendeka Mtaki kilichotokea Jumatatu, Februari 11, 2013 jijini Dar es Salaam.

  Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa motto wa Marehemu Kimara King’ong’o. Misa ya kumwombea Marehemu itafanyika Alhamisi Februari 14 kuanzia saa 5 asubuhi Katika Kanisa la Mt. Marie Clare Michungwani.

  Heshima za mwisho zitaanza saa 7 mchana na baade safari ya kuelekea kijijini kwake Kisorya-wilayani Bunda itaanza.

  Bwana Alitoa na Bwana ametwaa- Jina lake Lihimidiwe.

  0 0


  UN Secretary-General, Mr Ban Ki-Moon,  message for International Year of 
  Water Cooperation 2013 
  New York, 11 February 2013

  Your Excellency Mr. Pascal Canfin, Minister for Development, Ministry of Foreign Affairs, France; Your Excellency Mr. Hamrokhon Zarifi, Minister of Foreign Affairs, Republic of Tajikistan; Ms. Irina Bokova, Director-General of UNESCO; Mr. Michel Jarraud, Secretary-General, World Meteorological Organization, and Chairperson, UN-Water; Excellencies, Ladies and gentlemen, 

  I am pleased to greet all participants at the inaugural event of the International Year of Water Cooperation. 

  Water is central to the well-being of people and the planet. 
  We need it for health, food security and economic progress. 
  Water holds the key to sustainable development. 
  We must work together to protect and carefully manage this fragile, finite resource. 

  Each year brings new pressures on water. 
  Growing populations.  Climate change. 
  One-third of the world’s people already live in countries with moderate to high water stress. Competition is growing between farmers and herders; industry and agriculture; town and country. 

  Upstream and downstream, and across borders, we need to cooperate for the benefit of all – now and in the future.  The United Nations General Assembly has designated 2013 the International Year of Water Cooperation. 

  Let us harness the best technologies and share the best practices to get more crop per drop.   Let us promote water rights, waste less and design intelligent policies so all users get a fair share. 

  Let us invest in water. 

  Water is life.  0 0  0 0

    Mmoja wa wageni waliohudhuria sherehe hiyo akisubiri kwa hamu glasi yenye kinywaji cha Johnnie Walker kutoka kwa mmoja wa mabalozi wa kinywaji hicho kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
    Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon akifurahia  kinywaji cha Johnnie Walker akiwa pamoja na mmoja wa mabalozi wa kinywaji hicho.
    Baadhi ya wageni waliohudhuria “Pre Valentine Mask Party” wakipata maelekezo kutoka kwa mabalozi wa kinywaji cha Johnnie Walker kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti iliyofanyika Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon akijadili jambo kuhusu kinywaji cha Johnnie Walker na mabalozi wa kinyaji hicho katika “Pre Valentine Mask Party” iliyofanyika Golden Tulip ambapo kampuni hiyo ilidhamini hafla hiyo kupitia kinywaji chake cha Johnnie Walker.

  0 0


  Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM. 

  Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-

  Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara

  1. Ndugu Pindi Chana
  2. Ndugu Adam Kimbisa
  3. Ndugu William Lukuvi
  4. Dokta Emmanuel Nchimbi
  5. Ndugu Jerry Slaa
  6. Profesa Anna Tibaijuka
  7. Ndugu Stephen Wassira

  Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
  1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
  2. Ndugu Hussein Mwinyi
  3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
  4. Dokta Salim Ahmed Salim
  5. Ndugu Maua Daftari.
  6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
  7. Ndugu Hadija H. Aboud

  0 0

   Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel, Awaichi Mawalla katikati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara ya wasanii walioshiriki shindano la kuimba la Epiq BSS mkoani Dodoma Ijumaa hii ( kushoto  kwake)  Nsami Nkwabi na mwengine ni Walter Chilambo  mshindi wa EBSS 2012 

  Mshiriki wa shindano la Epiq BSS, Nsami Nkwabi, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, anayetazama kushoto ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla. Kulia ni mshiriki mwingine, Norman Severino

  ====  ======  ======  ====  EPIQ STARS KUBURUDISHA DODOMA IJUMAA HII.


  Dar es Salaam, 12/2/2013: Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel leo imetangaza uzinduzi wa ziara za mikoani kwa wasanii walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search ambapo ziara hiyo itaanzia Dodoma ijumaa hii kwenye ukumbi wa Maisha Club ikifuatiwa na Dar es Salaam.


  Ziara hiyo itajumuisha vijana walioingia kumi bora, akiwamo Menina Atick, Nsami Nkwabi, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.


  Katika ziara hiyo pia, ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2006, wapenzi wa muziki watapata fursa ya kumshuhudia mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo ambaye atakuwa akizundua wimbo wake siku hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Afsa biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema dhumuni kubwa la ziara hiyo ni kuwajengea vijana hao msingi katika kazi yao ya muziki baada ya shindano la Epiq BSS kuisha.

   ‘Lengo letu kuu la kudhamini Epiq BSS haikuwa kumpa mshindi zawadi, la hasha, bali tulikuwa na mpango madhubuti wa kubadilisha maisha ya vijana hawa kupitia vipaji vyao’ alisema Khan.  ‘Lakini pia dhumuni la Zantel ni kuonyesha kuwa kwa kufanya uwekezaji sahihi kila kitu kinawezekana, na hakika hilo litajionyesha kwa vijana hawa ambao kwa mara ya kwanza toka mashindano ya BSS yaanzishwe hawajawahi kusaidiwa kwa kiasi hiki’ alisisitiza Khan. Kwa upande wao washiriki watakaokuwa kwenye ziara hiyo wameishukuru kampuni ya Zantel kwa kuwasaidia kurekodi nyimbo zao, kuzitangaza na sasa ziara hii.

   ‘Hakika Zantel wameonyesha utofauti na makampuni mengine, kwani makampuni mengi hupotea baada ya kumalizika kwa shindano au tukio husika, ila Zantel wamekuwa nasi baada ya kuisha mashindano wakihakikisha tunarekodi nyimbo zetu na kuzitangaza, tunashukuru sana kwa hilo’ alisema Nsami Nkwabi, mmoja wa washiriki watakaokuwepo kwenye ziara hiyo. Ziara hii pia itawapa fursa kubwa Zantel na washiriki kutoa shukrani kwa mashabiki wa mziki waliowaunga mkono wakati wa mashindano.

  Kwa upande wake mshindi wa Epiq BSS alisema mashabiki watarajie burudani kali kutoka kwake,‘ nimejipanga sana kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania kuwa hawakukokosea kunipigia kura niwe mshindi’ alisema Walter. Wasanii wengine watakaotoa burudani kwenye ziara hii ni Barnaba, Ben Paul, Linah na Ali Nipishe. 


  0 0  Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo. 

  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kuwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati kuu ya CCM ilkiyofanyika katika viwanja vya Makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waliokuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA.Kushoto anayevaa kofia ya CCM ni aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mtela Mwampamba na kulia ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA Bi Juliana Shonza.Weninge katika picha ni Katibu mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman Kinana(kulia) na kushoto ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula.(picha na Freddy Maro).

older | 1 | .... | 26 | 27 | (Page 28) | 29 | 30 | .... | 1898 | newer