Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 24 | 25 | (Page 26) | 27 | 28 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Habari zilizotufikia hivio punde kutoka Jijini Arusha zinaarifu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Ask Thomas Laizer amefariki dunia.

  Taarifa hizo zinadai kuwa Ask. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha. Jana Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea  na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.

  Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu. Pinda alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

  Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye.

  Awali ilisemekana kuwa Askofu Laizer amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika Selian kutaka kumwona, lakini jana ilidhihirika kuwa, amelazwa hospitalini hapo.

   FK Blog inatoa pole kwa Waumini na washarika wote wa KKKT nchini kote kufuatia msiba huo mzito ulilolikumba Kanisa la Kilutheri hasa wakati huu ambao kuna mgongano kati ya waumini na Viongozi wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.Habari kwa hisani ya FK Blog.

  0 0  MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.

  Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.

  Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
  Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
  Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.Picha zaidi ingia Gsengo Blog.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambukisho cha Taifa katika hafla ilkiyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi mke wa Rais Mama Salma Kikwete kitambulisho chake cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo huku Rais Kikwete akishuhudia.Kushot o Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa kitambulkisho cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kitambilisho cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu.

   Rais Kikwete akimkabidhi Kada wa CCM Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kitambulisho cha taifa.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Dkt. Alex Malasusa kiongozi wa kanisa la KKKT kitambulisho cha taifa.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Elihad kitambulkisho cha taifa.

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akimkabidhi Mwenyekiti wa CUF Professa Ibrahim Lipumba kitambukisho cha taifa.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau kitambulisho cha taifa leo katika viwanja vya Karimjee.
  Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimkabidhi mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio kitambulisho cha taifa.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw.William Erio mara baada ya kupokea Kitambulisho cha Taifa
  Baadhi ya wageni walioudhuria sherehe za uzinduzi wa Vitambulisho vya Taifa kutoka kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN Bw.Gabriel Nderumaki,Mkurugenzi Mkuu wa NSSF DKt.Ramadhani Dau,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw.William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.Emanuel Humba .Picha  na Freddy Maro  wa Ikulu.

  0 0  0 0

  Mwimbaji wa bendi ya Mashauz Classic, Hashimu Said 'Mzee wa majanga akiimba wakati wa onesho lao lililofanyika katika bustani ya Magomeni Dar es salaam jana .
  Mwimbaji wa bendi ya Mashauzi Classic, Rukia Jumaa kulia akiimba wakati wa onesho lao lililofanyika katika bushati ya Magomeni Dar es salaam jana kushoto ni Mpiga gita la Solo wa bendi hiyo Jumanne Ulaya .
  Mwimbaji wa bendi ya Mashauz Classic, Hashimu Said 'Mzee wa Majanga' akiimba kwa hisia wakati wa onesho la bendi hiyo lililofanyika katika bustani ya Magomeni Dar es salaam jana nyimbo anayoimba ni tukio la kweli lililomtokea na kumfanya atunge nyimbo inayokwenda kwa jina la 'Mimi Mwanaume Bonge la Bwana' baada ya kuchomewa moto kila kitu cha ndani pamoja na nguo zake zote na mke wake wa ndoa  baada ya kuhitarafiana.

  Mwimbaji wa bendi ya Mashauz Classc, Rukia Jumaa akiimba wakati wa onesho la bendi hiyo.

  Mwimbaji wa bendi ya Mashauz Classic, Hashimu Said 'Mzee wa Majanga' akiimba kwa isia wakati wa onesho la bendi hiyo lililofanyika katika bustani ya Magomeni Dar es salaam jana nyimbo anayoimba ni tukio la kweli lililomtokea na kumfanya atunge nyimbo inayokwenda kwa jina la 'Mimi Mwanaume Bonge la Bwana' baada ya kuchomewa moto kila kitu cha ndani pamoja na nguo zake zote na mke wake wa ndoa Picha na www.burudan.blogspot.com

  0 0


  0 0
 • 02/07/13--22:12: tangazo kwa umma.

 • MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

  TANGAZO KWA UMMA

  KITENGO CHA HUDUMA KWA WATEJA.


  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwatangazia Wateja na Watumiaji wote wa Bandari kwamba imeanzisha Kitengo Maalum cha Huduma kwa Wateja kitakachopokea malalamiko, kero, taarifa, maoni, ushauri juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.


  Kuanzishwa kwa Kitengo hiki ni moja kati ya Mikakati ya Mamlaka ya kuboresha huduma zake na kuondoa kero kwa Wateja na Watumiaji wa Bandari.


  Kwa huduma ya haraka tafadhali piga namba zifuatazo;

  0754 292998

  0756 849868

  0788 888801

  0789 334398


  Namba hizi pia zinapatikana kwenye mtandao wa TPA   

  MENEJIMENTI.


  0 0


  Mahojiano maalum na Mkurugenzi Mkuu wa Alliance One - Mark Mason kuhusu

  kilimo na uwekezaji wa tumbaku nchini

                                           
    Mkurugenzi Mkuu wa Alliance One Tobacco Tanzania Ltd. (AOTTL) Bw. Mark Mason


  Mwandishi: Mara zote watu wakisikiapo Alliance One Tobacco Tanzania wanadhania ni kampuni inayozalisha sigara, ambayo si kweli; je Alliance One inajishughulisha na nini hasa?


  Mark Mason: Alliance One Tobacco Tanzania (AOTTL) ni moja kati ya makampuni matatu yanayonunua bidhaa ya tumbaku nchini Tanzania iliyo chini ya mwamvuli ya kampuni ya kimataifa Alliance One International (AOI) yenye makao makuu North Carolina, nchini Marekani. AOTTL ilianza kazi nchini Tanzania mwaka 2005 baada ya kuunganishwa kwa makampuni ya kimataifa DIMON Incorporated na Standard Commercial Corporation (STANCOM) zote kutoka Marekani.


  Shughuli inayofanya Alliance One Tobacco Tanzania ni kununua tumbaku, kuiandaa kiwandani na kuiuza ndani na nje ya nchi kwa makampuni yanoyotengeneza sigara. AOTTL inanunua kati ya kilo milioni 30 mpaka 50 za tumbaku kutoka kwa wakulima 182 waliokuwa na mikataba na Shirika la Wakulima wadogo wadogo kutoka sehemu 8 tofauti zinazolima tumbaku nchini Tanzania ikiwemo Tabora, Urambo, Kahama, Manyoni, Iringa, Kigoma, Songea na Mara. AOTTL inazalisha aina mbili za tumbaku zenye majina yakitaalam Flue Cured Virgina (FCV) na Dark Fire Cured (DFC).


  Mwandishi: Ni kitu gani kinachofanya Tanzania iwe na mazingira bora ya kufanya biashara tofauti na nchi zingine?


  Mark Mason: Uwekezaji mkubwa wa kampuni yetu nchini Tanzania ipo Kingolwira, Morogoro ambapo tumewekeza dola za kimarekani milioni 50 sawa sawa ma bilioni 50 zakitanzania. Kushamiri kwa uwekezaji huu wa Alliance One ni matokeo ya sera nzuri za uwekezaji  na mazingira bora yakufanya biashara inayowezeshwa na serikali ya Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania maarufu kama TIC.                                                                           


  Mwandishi: Hivi karibuni utafiti uliofanywa na taasisi ya wanauchumi wakujitegemea NKC kwa dhamana ya taasisi ya Tumbaku kwa nchi za kusini mwa Afrika (Tisa), imetangaza thamani ya sekta ya tumbaku kuwa dola bilioni 10 kwa kusini mwa jangwa ya sahara. Kampuni yenu inapokeaje taarifa hizi, hususani wakati huu ambapo tume yakukumbana na tumbaku (FCTC) inafanya jitihada ya kufungia kilimo na biashara ya tumbaku duniani?  


  Mark Mason: Alliance One ilijishirikisha kikamilifu katika utafiti huu na inakaribisha kwa furaha kubwa hizi taarifa kwa sababu ni mara ya kwanza kwa tafiti ya thamani ya tumbaku kufanywa katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara. Utafiti huu wa TISA inatusaidia kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu  wa sekta ya tumbaku, sio kwa jumla ya uchumi wetu tu bali kwa nchi zinazo lima tumbaku pia. Matokeo ya utafiti huu yanaweza kutumika na wadau mbali mbali kama serikali (kwa ajili yakutunga sera na mipango), mamlaka za udhibiti, mamlaka za kukusanya mapato na watoa huduma mbali mbali.


  Kuhusiana na sera ya FCTC kufungia tumbaku, utafiti huu utasaidia wadau mbali mbali wa FCTC wanaolima tumbaku kuweka sera ambazo zitafanikisha maamuzi sahihi kwa ajili ya kulima tumbaku.


  Mwandishi: Je nini athari ya kusimamisha kilimo cha na kuuza tumbaku kama FCTC itafanikiwa kupitisha sera hiyo?  Mark Mason: FCTC ikifanikiwa katika kampeni yake ya kuzuia tumbaku duniani, athari zake katika uchumi wa Tanzania yatakuwa kama yafuatayo; Maisha ya wakulima 100,000 na familia zao zitaathiriwa sana kwa sababu hakuna zao mbadala uliopatikana mpaka sasa. Pili, kwa uchumi wa Tanzania, fedha za kigeni kutokana na mauzo ya tumbaku yatasimama. Pia mapato ya serikali kutokana na tumbaku na bidhaa za tumbaku yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 157 nazo zitayumba. Hii ni kwa sababu katika miaka mitatu iliyopita tumbaku ndio imekuwa ikiongoza katika zao linalopatisha nchi yetu fedha za kigeni kwa kusafirishwa nje.


  Kutokana na takwimu za Benki Kuu ya Tanzania katika ripoti ya Septemba 2012, mauzo ya tumbaku nje ya nchi kufikia Agosti 2012 yalifikia dola milioni 307.3. Maisha na maendeleo ya wafanyakazi na wategemezi takribani 790,000 sawa sawa na asilimia 1.5 ya idadi ya watu ambao wananufaika moja kwa moja na kutegemea mlolongo wa thamani na mapato ya zao la tumbaku nao wataathirika. 

  Mwandishi: Kama FCTC wapo sahihi, je kuna uwezekano wakupata mbadala wa zao la tumbaku kama zao la biashara linaloongoza kwa kuuzwa nje ya nchi Tanzania?


  Mark Mason: Mpaka sasa kumekuwa na mazao mbadala machache sana zinazotajwa na kuhakikishwa kuweza kuchukua nafasi yakulimwa katika mashamba ya tumbaku yaliyopo sasa. Mapendekezo yameshatolewa kwa sektretarieti ya FCTC  na wadau wa tumbaku kuwa utafiti zaidi juu ya mazao mbadala yanabidi yafanyike.

    

  Mwaandishi: Inavyoonekana, watu wengi wanafahamu athari za kiafya zaidi zinazoletwa na tumbaku kuliko manufaa inayoleta kiuchumi, je unadhani elimu imetolewa vya kutosha ili watu waweze kuelewa mchango wa zao hili kiuchumi katika taifa letu?


  Mark Mason: Ndio, jitihada zimefanyika kujaribu kuwafahamisha watu kuhusiana na manufaa ya tumbaku katika uchumi wetu kupitia vyombo vya habari, warsha na mikutano mbali mbali. Kwa mfano, mwaka 2012 Alliance One ilifanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana mambo kadha wa kadha ya sekta hii ikiwemo umuhimu wa tumbaku katika uchumi wa Tanzania.


  Mwandishi: Inavyoonekana, wakulima wa tumbaku ndio wadau wakubwa wa Alliance One, je mnawejengea vipi mazingira bora ya kazi kwenye kilimo na kupata masoko ya mazao yao?


  Mark Mason: Alliance One imeingia mkataba wa miaka mitatu yakununua tumbaku kutoka kwa wakulima waliojiunga na mashirika ya wakulima wadogo wadogo. Kupitia mikataba hii wakulima wana uhakika wa kupata soko la tumbaku yao. Alliance One inawapatia huduma mbali mbali pia wakulima hawa ikiwemo; Mikopo kwa waakulima kupitia mikataba ya mikopo na benki zinazokopesha inayohakikiashia benki marejesho ya mkopo kwa sababu mkulima anakuwa ana uhakika na kuuza tumbaku yake kutokana na soko la Alliance One. Alliance One pia inatoa huduma za kuandaa mipango ya mauzo na masoko kwa wakulima na uratibu huo kupitia wakala wake anayitwa asasi ya wafanyabiashara wa tumbaku Tanzania (ATTT).


  Pia, Wadau wa tumbaku kupitia baraza la tumbaku pia wameanzisha mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda miti inayozingatia mkulima kutumia miti kwa nidhamu kwa ajili ya kuandaa tumbaku na matumizi ya nyumbani kuanzia msimu 2012/2013. Kupitia mpango huu, wakulima watahitajika kupanda miti katika mashamba yao na kutakuwa na ukaguzi kila mwaka na kutegemeana na matokeo ya ukaguzi, Alliance One itarudisha gharama zote za mbegu, kupanda na kuotesha miti.


  Mwandishi: Umesema kampuni yako imekuwa ikifanya kazi kwa muda sasa nchini Tanzania. Je ni faida gani kubwa iliyoiletea jamii ya watanzania mpaka sasa?


  Mark Mason: Kama nilivyotamka mwanzo, biashara ya AOTTL nchini Tanzania ni ya kununua tumbaku, kuiandaa kiwandani na kuiuza. Kwa kufanya haya, biashara ya AOTTL inafaida mbali mbali katika jamii ya watanzania kama ifuatavyo; Uwezeshwaji wakiuchumi wa wakulima wapatao 38,000 pamoa na familia na jamii inayowazunguka katika mahali wanapolimia. Pili, kutoa ajira kwa watanzania wapatao 300 kama waajiriwa kamili na 2,500 kama vibarua wakati wa misimu ya kilimo. Tatu, AOTTL pia imeweza kusambaza aina ya teknolojia kwa wakulima iliyowawezesha kuongeza mavuno kutoka kilo 1060 kwa hekari moja 2005 mpaka kilo 1390 mwaka 2012. La mwisho, kupitia malipo yetu ya kodi baraza la wilaya, serikali za mikoa na serikali kuu zimeweza pia kutoa huduma za kijamii kama elimu, maji na afya, pamoja na kuboresha hadhi ya miundombinu kama barabara.    


  Mwandishi: Mbali na kutoa nafasi za ajira na kuwawezesha watu kiuchumi, je kuna mkakati wowote wa misaada kwa jamii mliowahi kutoa?


  Mark Mason: AOTTL  imejikita kuboresha hali ya maisha ya jamii za wakulima wa tumbaku kupitia mpango maalum wa kutoa misaada inayolenga katika elimu, afya na maendeleo ya kijamii. Kila mwaka AOTTL inatoa bajeti ya dola laki moja na ishirini sawia na shilingi milioni 192 ambayo inagawiwa kwa watu au vikundi vya maendeleo wanaotuomba misaada hii kupitia barua rasmi zinazopitiwa na kamati husika na kutolewa kwa njia ya vitu. Baadhi ya misaada ambayo tumejikita nayo ni kujenga madarasa, kugawa madawati, kutoa vitabu na kulipia karo za wanafunzi wanohitaji msaada. Pia tunajenga kliniki na kuwasaidia watoto yatima.    


  Pamoja na hayo, mpango wetu wa kutoa msaada pia inaambatana na programu maalum ya wafanyakazi katika kilimo yenye malengo mbali mbali katika sekta ya utendaji kazi wa kilimo cha tumbaku kama ifuatazo; kufuta utumikwishaji wa watoto katika kilimo, kulinda maslahi ya mapata na masaa ya kazi kwa mfanyakazi, kupatiwa mazingira salama ya kazi, kushirikishwa kwa haki katika shughuli za kilimo, kufutwa kwa utendaji kazi wa kulazimishwa yaani “Forced labour”,  kuwajengea uhuru wa kujiunga na mashirika ama asasi za kilimo na tumbaku na mwisho ni kuhakikisha sheria za kazi zinafuatwa.


  Mwandishi: Je, Alliance One inamipango gani ya baadae nchini Tanzania?


  Mark Mason: Sekta ya tumbaku nchini Tanzania inategemewa kuwa na mwonekano mzuri sana mbele ya safari kwa sababu  tutabakia kuwa washindani imara na kuendelea kuboresha maslahi kwa wakulima. Kwahiyo mipango yetu ya baadaye inajumuisha; kuendeleza kukuza kwa nafasi ya Tanzania katika soko la duniani huku tukizingatia gharama na ubora tukijilinganisah na nchi zingine, kuendelea kuimarisha maisha ya wakulima, kuendelea kuwekeza katika sehemu za masoko ili kuweza kumnufaisha mkulima kwa kumpunguzia siku za kufanya kazi zinazotakiwa kuzalisha mazao, pamoja na kuongeza namna bora ya uzalishaji na kufuta vitendo haramu katika kilimo tuikizingatia sheria za kazi, kuongeza uwekezaji katika kiwanda na ufanisi ili kuweza kuwasaidia wakulima katika kilimo cha tumbaku na kupunguza gharama kubwa katika zoezi la kupanda miti na hatimaye kuendelea kuuza tumbaku iliyobora na kwa bei yenye ushindani ili kuweza kupata mwendelezo wa masoko duniani.


  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Seneta, Stive King, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc nchini Marekani, Feb 6, 2013.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washngton Dc, Feb 6, 2013.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washngton Dc, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Feb 6, 2013, katika Hoteli ya Omni Shoreham.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc, baada ya mazungumzo yao alipowasili jijini humo kuanza ziara yake ya siku nne, iliyomalizika jana Feb 7, 2013. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa tano kutoka kushoto) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mahadhi Juma Maalim. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 

  0 0

   Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Mtwara,Lindi na Pwani. Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha makumbusho,Makumbusho ya Taifa, Pugu sekondari,maeneo mengine ni ufukwe wa kigamboni, soko la kimataifa la magogoni, uwanja wa taifa, J.K.Nyerere Air Port, Soko la kariakoo, mashule ya sekondari na msingi, pia watatembelea manispaa za ilala, temeke na kinondoni ambapo watakutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa, na wabunge katika majimbo ya mikoa hiyo.

  0 0

  1Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Devota Mdachi kushoto na maafisa wengine wakiwa katika maonyesho ya Utalii ya FITUR ambayo ni ya tatu kwa Duniani yaliyofanyika kuanzia Januari 30 mpaka Februari 3 mwaka huu nchini Madrid nchini Hispania na kushirkisha Bodi ya Utalii (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ya Ngorongoro (NCAA) na makampuni zaidi ya sita ya utalii kutoka nchini Tanzania katikati ni Esther Solomon (Senior Tourist Information Officer,(TTB) , Israel Naman ({Principal Conservation Officer, (NCAA) na Maria Kirombo (Park Warden, Arusha National Park).
  2Devota Mdach kushoto, Maria Kirombo and Esther Solomon wakiwa katika banda la Tanzania nchini Hispania kwenye maonyesho ya utalii ya FITUR.
  3
  Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Youssou Ndour Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini Senegal ambaye pia ni mwanamuziki maarufu duniani wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho hayo , Youssou Ndour amewahi kufanya ziara ya kimuziki mara tatu nchini Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini mwake.

  0 0


  by / Thursday, February 7th, 2013

  Social networks are becoming popular gateways for customers seeking help or updates in crisis situations. And socially devoted brands are tapping into them.

  These social networks such as Facebook provide a better alternative to busy call centers and may inadvertently, through one post, respond to multiple customers sharing the same problem.

  According to SocialBakers‘ Socially Devoted study for October to December 2012, brands on Facebook are responding faster to questions from their fans. What previously took brands an average of 21 hours to respond to fans toward the end of June, decreased to 19.5 hours during Q3 of 2012.

  The latest report released today reveals that brands on Facebook have shortened their average response times to 13.7 hours. But which brands respond faster?
  This table below ranks Egyptian telecom giant, Mobinil 3rd amongst the top 10 fastest responding socially devoted brands on Facebook with a response rate of 96.24% and response time of 18 minutes. Quite impressive!

  Also, you would notice that Tanzania’s leading telecom operator, Tigo is ranked 8th with an 87.30% response rate and 28 minutes response time.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo.Rais Kikwete yupo nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC.Picha na Freddy Maro.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji katika ikulu ya jijini Maputo leo.Rais Kikwete yupo nchini Msumbiji kuhudhuria kikao cha viongozi wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC
   Akisindikizwa na mwenyeji wake
  Akiagana na mwenyeji wake

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa leo, Alhamisi, Februari 7, 2013, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Mkuu Dkt. Alex Malasusa kuombeleza kifo cha Askofu Thomas O. Laizer wa Jimbo la Kaskazini Kati Arusha la KKKT aliyeaga dunia jioni ya leo.

  Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Askofu Mkuu Malasusa: “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Askofu Thomas Laizer ambaye nimejulishwa kuwa ameaga dunia muda mfupi uliopita, jioni ya leo, katika Hospitali ya Rufaa ya Selian, Arusha.”
  “Askofu Thomas Laizer ametutoka lakini tutaendelea kumkumbuka kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi wa kiroho wa Watanzania na ambaye wakati huo alitafuta namna bora zaidi ya kuwatumikia waumini wake. Daima takumbukwa kama kiongozi ambaye alitumia vipaji vyake vyote kuwatumikia waumini wake na wote waliokuwa chini yake.”
  Ameongeza Rais kikwete: “Kufuatia msiba huu mkubwa, nakutumia wewe Baba Askofu Mkuu Alex Malasusa salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kukupa pole ya msiba huu na kupitia kwako kuwapa pole nyingi maaskofu na viongozi wenzako katika KKKT pamoja na waumini wote wa Kanisa kwa kuondokewa na kiongozi mwenzao na muumini mwenzao.”
  Aidha, Rais Kikwete ameongeza, “Pia kupitia kwako Baba Askofu Mkuu, natuma salamu nyingi za moyoni mwangu kwa familia na wana-ndugu wa Marehemu Thomas Laizer.  Naungana nao katika kuomboleza. 

  Naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Baba, Babu na mhimili wa familia. Nawaombea subira ili waweze kuvuka kipindi hiki kwa sababu yote ni Mapenzi ya Mungu. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Thomas Laizer. Amen.”

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  IKULU
  DAR ES SALAAM

  07 Februari, 2013


  0 0


  0 0
  0 0


  Kama jibu  kwa taarifa za kupotosha za hivi karibuni kutoka kwa vyombo vya habari, Bodi ya fastjet ingependa kuchukua fursa hii kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli na za kuchafua zilizotolewa na Don Smith wa fly540 Kenya. 
  Kampuni, kwa msisitizo mkubwa, inakataa madai yaliyotolewa na Don Smith kuhusu  wazo la ununuzi wa hisa ndani ya Fly540 Kenya pamoja na madai mengine mengi yaliyofanywa kupitia vyombo vya habari katika majuma ya hivi karibuni.


  Akitoa kauli kuhusu madai ya hivi karibuni, mweyekiti wa fastjet David Lenigas alisema:  “fastjet imenuia kufanya biashara zake katika hali ya uwazi, isiyofichika na ya kihalali kwa ujumla wake, kupitia itifaki zinazotakiwa. Kampuni hii haina nia ya kuendelea kukanusha madai ya uongo kupitia vyombo vya habari lakini itachukua hatua za kisheria kuhusu madai mengine zaidi kama hayo.”

  “fastjet imemlipa Don Smith na wenzake zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 6 kwa ajili ya hisa zake kwenye  Fly540 na nembo nyingine za kibiashara zinazohusiana na hiyo, na sasa kwa ari kubwa itachukua hatua kuhakikisha kuwa mikataba yake imetekelezwa.”


  “Kampuni haitavumilia mikakati yoyote ya ulaghai na isiyo ya wazi. Masuala yaliyotungwa na Don Smith nchini Kenya hayatadhuru mpango wa jumla wa fastjet wa kuwa kampuni ya kwanza ya safari za ndege kwa Afrika nzima yenye gharama za chini”


   “Nafasi ya kampuni nchini Kenya, ambayo ni  sehemu ndogo tu ya upanuaji wetu, imeshawekwa salama kupitia mkataba wa makubaliano na Jetlink uliotangazwa wiki iliyopita. Tunahisi kuwa Jetlink, ambayo tayari ina ithibati ya  IOSA, ni mshirika mzuri zaidi wa fastjet ukizingatia viwango vyetu vya usalama na uaminikaji. Baada ya kufanya mapitio ya kina, tulitambua kuwa Jetlink itaweza kuipa fastjet msingi wa kudumu wa kuanzia kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa miundombinu na ithibati yake ya kiwango cha kutoa huduma na kusimamia ndege nyingi kubwa za kisasa”.


  “Afrika ina karibu asilimia 4% ya abiria wa safari za anga duniani lakini kwa bahati mbaya kwa sasa ndiyo yenye asilimia 25% ya ajali za ndege duniani. Dhima yetu ya kuleta usafiri salama kwa watu wa Afrika inahitaji viwango vya juu na uzingatiaji wa kila mara kuhakikisha kuwa haya yanatekelezwa.”


  Mkurugenzi mkuu wa fastjet Ed Winter aliongeza:


   “Pale ambapo madeni ya kihistoria yaliyoendelea kuongezwa na Don Smith na Fly540 yamekuja kuwa wazi baada ya umiliki, fastjet inafanya kazi kwa karibu na wadai wake ili kufikia muafaka unaoridhisha kwa pande zote zinazohusika. Hatukubaliani na viwango vya gharama ambavyo vimekuwa vikitamkwa katika vyombo vya habari hivi karibuni, na pale viwango vinavyodaiwa vinapotambulika, msivichukulie kwa umakini kuhusiana na biashara kwa ujumla. Masuala haya yaliyojitenga hayadhuru utendaji wa siku hadi siku wa fastjet au utendaji wowote wetu katika Angola au Ghana ambao wanasafirisha chini ya nembo nyingine ya Afrika ya Fly540”   “fastjet itachukua hatua kurejesha madeni haya ambayo hayawekwi wazi na mengine yoyote yaliyomo chini ya waranti zilizotolewa na Don Smith na wenzake katika makubaliano yao ya kuuza hisa zao ndani ya Fly 540 Kenya na kuiuzia fastjet mwezi Juni mwaka jana”


  Timu ya menejimenti ya fastjet inabaki kuwa ya wanaharakati wakubwa wa maendeleo ya kampuni, kujenga mafanikio yake Tanzania na ukuaji kuelekea kuweka demokrasia katika usafiri wa anga wa Afrika na kuwa shirika la kwanza  la usafiri wa anga barani Africa lenye gharama za chini


   “Kwa sasa, tunaendelea kufanya kazi na mamlaka zinazohusika katika mataifa mengine Afrika kupanua mtandao wa fastjet”


  0 0


  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com.

  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka, wanashudia katikati ni Promota wa mpambano huo, Kaike Silaju na Makamu wa Rais wa PST, Aga Peter .

  0 0   Mwili wa Marehemu Dereva kwa Mbele ukiwa Umekandamizwa na Lori lililo beba Mbao izo.
   Huu ni Mguu wa Dereva ambaye amekandamizwa na Gari hilo.

   Hivi Ndivyo Gari hili lililo beba Mbao limeanguka .older | 1 | .... | 24 | 25 | (Page 26) | 27 | 28 | .... | 1896 | newer