Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 262 | 263 | (Page 264) | 265 | 266 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Utawala na Masoko kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Stanley Mahembe akiwatambulisha wageni walioketi meza kuu (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini, mafunzo hayo yamefungwa jana Mkoani Morogoro. 
   Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwahutubia Wasimamizi na Wadadisi (hawapo pichani) muda mchache kabla ya kufunga mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini, mafunzo hayo yamefungwa jana Mkoani Morogoro. 
   Baadhi ya Wasimamizi na Wadadisi wa Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi hilo jana Mkoani Morogoro.
  Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Serikali pamoja na Wasimamizi wa Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini mara baada ya kufunga mafunzo ya zoezi hilo jana Mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

  0 0

   Magari Mapya aina ya Toyota  Yakiwa Manispaa ya Kinondoni leo mara baada ya kukabidhiwa
   Mwonekano wa moja ya gari mpya zilizonunuliwa na manispaa ya kinondoni
   Gari mpya aina ya Landcruiser ikiwa Ofisi ya manispaa ya Kinondoni
   Mstahiki Meya Yussuph Mwenda akiongea na Vyombo vya habari Leo mara baada ya kukabidhiwa magari hayo
  Meya wa Kinondoni Yussuph Mwenda akikabidhi funguo kwa mmoja wa madereva.

  Manispaa ya Kinondoni imenunua magari kumi (10) hard top na double cabin, Magari hayo yanayo gharimu kiasi cha Tshs. 779 milioni ikiwa ni mapato ya chanzo cha ndani ili kuboresha huduma za Mipango miji, elimu, ustawi wa jamii, afya, mapato pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo . Magari haya yatasaidia sana kuleta maendeleo na vilevile kukuza mapato ya ndani. kwa pamoja tunajenga lipa kodi kwa maendeleo ya Kinondoni (tuulize info@kinondonimc.go.tz)

  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kundi la Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya Uingereza walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu kuendesha mfano wa mtambo wa kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari kuu (KCA Deutag Dart Drilling Simulator and Well Enginering System) alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. 

  Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi. Nyuma yake ni ujumbe alioongozana nao ikiwa ni pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo (wa pili kulia) Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya katika Wizara za mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Dorah Msechu.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo wakisindikizwa na Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 alikotembelea akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.PICHA NA IKULU.

  0 0

   Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali WOINSO, Bi. Janeth Sebastian (katikati) akifafanua jambo juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Shirika lake wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msaidizi wake Bi. Namsifu Singo na kushoto ni Katibu wake Bi. Consolota Simon.

   Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali WOINSO, Bi. Janeth Sebastian (kulia) akijibu maswali toka kwa waandishi wa Habari (hawako pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza toka kushoto ni Mweka Hazina Philipina Raymond na katikati ni Katibu wa Shirika hilo Bi. Consolata Simon.

   Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano wakisikiliza kwa makini maelezo toka kwa mtoa mada ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali WOINSO, Bi. Janeth Sebastian (hayupo pichani).
  PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO


  =======  ====== =======
  Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

  SHIRIKA lisilo la Kiserikali Women in Society (WOINSO) linatarajia kuzindua mpango wa Elimu juu ya athari ya magonjwa ya ngono, utoaji mimba na mahusiano mashuleni kwa shule za msingi darasa la sita na la saba.

  Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bi. Janeth Sebastian wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Habari Maelezo uliopo jijini Dar es Salaam.

  Bi. Janeth amesema kuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Shirika lake linazindua mpango huo Kiwilaya na baadae wanatarajia kuzindua pia katika Wilaya ya Ilala na Temeke ikiwemo na mikoa mingine kama Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Songea.

  Bi. Janeth ameongeza kuwa Elimu itakayotolewa juu ya athari ya magonjwa ya ngono, utoaji mimba na mahusiano mashuleni kwa shule za msingi darasa la sita na la saba na Daktari Mwelimishaji italenga kuwapa uelewa wanafunzi na kuwafanya wajitambue kwa yale watakayofundishwa na hivyo kuwaepusha vijana hao na athari mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza kwao.

  “Elimu hiyo watakyopewa wanafunzi wa darasa la Sita na Saba itawawezesha kuwafanya wajitambue kwa yale watakayofundishwa na hivyo kuwaepusha vijana hao na athari kama vile magonjwa yatokanayo na ngono, utoaji mimba unaosababisha vifo na ugumba na mahusiano kabla ya wakati”. Alisema Bi. Janeth.

  Aidha, Bi. Janeth amewasisitiza wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kuhudhuria Uzinduzi rasmi utakaofanyika ukumbi wa Shekina Garden uliopo Mbezi Beach Makonde jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 3/04/2014 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Meh. Yusuph Mwenda.

  WOINSO ni Shirika lisilo la Kiserikali lililosajiliwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto kwa namba00NGO/00006564 mwaka 2013. Kabla ya usajili mkubwa lilikuwa linaelimisha kwa usajili maalumu na limefanya kazi tokea mwaka 2011 ambapo makao yake makuu yapo Dar es Salaam.

  0 0

    Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita Bi Felistus Joseph (wa kwanza kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam kuhusu mikakati ya Kamati hiyo katika kulinda amani, kuzuia uhalifu na kupinga ubaguzi hapa Nchini. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Farida Khalfan na mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.

   Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Farida Khalfan akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) nafasi ya vyombo vya Habari katika kuzuia mauaji ya Kimbari. Kushoto ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita Bi Felistus Joseph
  1.     Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya kuzuia Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita.  Picha zote Na. Georgina Misama-MAELEZO

  0 0


   Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia) akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma  kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba  baada ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) na Mwanasheri Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud Othaman(kulia). 
    Mwanasheri Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud Othaman(kulia) akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma  kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba  baada ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia). 
   Wajumbe wa Kamati namba mbili wakimsikiliza Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (hayupo pichani) wakati anatoa ufafanuzi leo mjini Dodoma  kuhusu hati ya Muungano baada ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ali Mzee Ali (kushoto) akiwafafanulia wajumbe wenzake Kamati namba mbili leo mjini Dodoma kuhusu wazee walioshuhudia utiaji wa saini hati ya Muungano kwa upande wa Bara na Visiwani. Kulia ni Mjumbe mwezie Asha Bakari Makame. 
   Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) akizungumza na wajumbe wa Kamati namba Sita (6) ya Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati akitembelea Kamati mbalimbali kujionea maendeleo ya uchambuzi wa vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya kwa sura ya Kwanza na Sita. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stephen Massato Wassira(katikati) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Maua Abeid Daftari(kushoto).Picha na Bunge la Maalum la Katiba.
  0 0

  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akikata utepe kuzindua kitabu cha ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi uliofanyika leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akikata utepe kuzindua kitabu cha ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi uliofanyika leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akiongoza wageni waalikwa kuonyesha kitabu cha utafiti mara baada ya kumaliza kuzindua.
  Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano huo wa kutangaza ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi.
  Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano huo wa kutangaza ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi.
  Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano huo wa kutangaza ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi.
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akizungumza katikamkutano na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuzindua ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi iliyotolewa na taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT). Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe na Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Slyvia Meku.
  Waandishi wa habari waliohudhuria katikamkutano na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuzindua ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi iliyotolewa na taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT).
  Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe akikazia jambo.
  Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Slyvia Meku akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi utafiti huo ulivyofanyika na kupata matokeo. Mkutano huo ulifanyika leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu.
  ---
  Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imethibitisha kuwa watu takribani watu milioni 3.3 ni kwa kutumia huduma za kibenki, kulingana na matokeo ya FinScope 2013 utafiti uliofanywa na Financial Sector Deepening Trust (FSDT ).

  Hayo yamesemwa na jijini Dar es Salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof Benno Ndulu , wakati akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa utafiti wa ripoti ya FinScope Tanzania 2013; habari zilizomo katika utafiti huu thamani ni muhimu kwa ajili yetu maendeleo ya kiuchumi. Utafiti huu wa FinScope ni wa tatu tangu mwaka 2006.

  Hata hivyo, alisema nusu ya Watanzania wote watu wazima - watu milioni 12 - sasa kutumia simu zao kwa kuondoa , kupokea na kuokoa fedha, au kulipa bili. Wanaume na wanawake katika maeneo ya mijini na vijijini katika nchi nzima na upatikanaji wa haraka kwa aina mbalimbali ya huduma za kifedha katika bonyeza ya kifungo chache .

   Alisema hii ni mapinduzi ya utulivu ambayo ni kuwa na madhara makubwa kwa mazingira ya fedha katika Tanzania . Mtandao wa simu operators kuendelea kufanya kazi na baadhi ya benki yetu ya kibiashara na kuendeleza bidhaa na huduma iliyoundwa na kukutana kutarajia kuongezeka kwa mahitaji katika muongo ujao.

  Mkurugenzi wa Ufundi wa FSDT, Sosthene Kewe alisema zaidi ya nusu ya watu katika nchi kutumia huduma rasmi za kifedha, ikiwa ni pamoja na akiba na mikopo vikundi vidogo , maduka, ugavi mikopo na wakopeshaji fedha , ambayo bado ni mkubwa sana muhimu kwa nchi na mara nyingi pamoja na huduma nyingine.

  " Ingawa hakuna miongoni mwao pia umewekwa au inasimamiwa na taasisi rasmi za fedha, akiba na mikopo ya vikundi inamilikiwa na kuendeshwa na watu ambao matumizi yao . Hii , kama vile bidhaa na huduma ambayo ni makini kulengwa kwa soko yao, inaweza kuelezea umaarufu wao "alisema.
  Alisema matokeo ya utafiti inaonyesha kuna ongezeko la kuingizwa fedha na ufahamu juu ya huduma za benki za Mkono, ambapo zaidi ya watu 6.6m katika nchi kwa kutumia simu za kibenki.

  0 0

  Wananchi wakiwa wamejikinga jua na picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete.9Mwanamuziki Hafsa Kazinja akiimba na wananchi katika mkutano wa kampeni katika kijiji cha Madesa.10Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza na akina mama katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Madesa kata ya Msata.11Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Kihangaiko.12Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM akicheza pamoja na Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati akimnadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lugoba leo.13Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana mkoa wa Simiyu Bw. Njalu Silanga wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Lugoba.14Mbunge wa Shinanga mjini na Naibu Waziri wa Madini Mh. Steven Masele akimuombea kura Bw. Ridhiwani Kikwete katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lugoba leo.15Wananchi wakinyoosha mikono yao juu kama ishara ya kumkubali mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete.2Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM ndugu Ridhiwani Kikwete akiangalia bendera ya Chama cha kampeni wa CUF iliyokabidhiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Msata mara baada ya kujiunga na CCM katika kijiji cha Pongwe Msungula kwenye mkutano wa chama cha Mapinduzi.

  0 0

   
   Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akifanya ukaguzi wa vitabu na nyaraka za taarifa mbalimbali kwa ajili ya wasomaji , pembeni yake ni Mkutubi msaidizi wa maktabaa hiyo Ndg. Judith Lugongo, ukaguzi huo ulifanyika mapema Leo hii wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba mkoa wa Dodoma.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akikagua jengo la maktaba mkoa wa Dodoma kujionea mfumo wa vifaa vinavyotumika kutolea elimu na taarifa mbalimbali kwa njia ya video na sauti,  zoezi hili la ukaguzi lilifanyika mapema leo kwenye viwanja vya maktaba ya Dodoma wakati wa maadhimisho  ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba
   Watumishi wa maktaba ya mkoa Dodoma wakiwa tayari kupokea wananchi wenye mahitaji mbalimbali ya huduma za maktaba kwa ajili ya kuwapa maelekezo ya namna ya kupata taarifa na huduma nyingine mbalimbali mapema leo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba ya Dodoma.
    Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akikagua nyaraka na vitabu mbalimbali wakati akitembelea mabanda ya maonesho  ya vitabu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba Nchini, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba ya mkoa.


   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akipata ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa kutafsiri taarifa za vitabu na nyaraka mbalimbali katika lugha za watu wenye mahitaji maalumu/wenye ulemavu wa kuona (nukta nundu) Mwl. Charles Mtimatuku mapema wakati anatembelea mabanda ya maonesho wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini  mkoani Dodoma. Huduma za maktaba nchini zimepiga hatua kiasi cha kuzalisha taarifa na nyaraka mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu.
  Baadhi ya walimu na wanafunzi shule za Dodoma waliojitokeza kwenye viwanja vya maktaba ya mkoa Dodoma kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini wakifuatilia salamu za mkuu wa mkoa Dodoma mapem leo.

  NA JOHN BANDA

  0 0

  Meneja Mradi wa Asasi ya Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA), Agnes Hanti akiongea wakati wa mafunzo kwa wadau wa Habari nchini juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari hasa katika haki ya kukuza demokrasia kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo Aprili 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mradi wa Asasi ya Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA), Agnes Hanti akiongea wakati wa mafunzo kwa wadau wa Habari nchini (hawapo pichani) juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari hasa katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Msaidizi wa OSIEA, Mburu Gitu (Kulia).
  Meneja Mradi wa Asasi ya Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA), Agnes Hanti akiongea na waandishi wa habari wakati wa majadiliano.
  Waandishi wa Habari na wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Chuo Cha Uandishi wa Habari za Kibiashara (EABMTI), Bi. Rosemary Mwakitwange akifafanua changamoto mbali mbali zinazowakabili wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
  Waandishi wa Habari na wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Waandishi wa Habari na wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  ---
  Asasi isiyo kuwa ya kiserikali ya OSIEA imesema kazikubwa inahitajika kufanyika ili kulinda Uhuru wa kujieleza na kujitegemea kwa vyombo vya habari nchini Tanzania. Wito huo unatokana na kuongezeka kwa vitendo vya kufungia vyombo vya habari na kuongezeka kwa matukio ya kuwadhuru waandishi wa habari pamoja na kuingiliwa kwa Uhuru wa wahariri na wanasiasa na wafanyabiashara.

  Mwaka jana serikali ili yafungia magazeti binafsi ya Mwananchi na Mtanzania kwa siku 14 na 90 kwa tuhuma za kuchapisha habari zenye uchochezi ambazo serikali ilidai zinahatarisha usalama wa taifa na zinatishia uvunjifu wa amani na umoja.Gazeti jingine la Mwanahalisi liliamriwa kufungwa tangu mwezi Julai2012 na halijafunguliwa mpaka sasa. Sheria ya magazeti inaipa serikali mamlaka makubwa ya kukandamiza vyombo vya habari. Hatua zote hizo zinakwenda kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu ambazo Tanzania imeridhia.

  Pamoja ukweli kuwa vyombo vya habari binafsi vinaongezeka tangia mwaka 1990 lakini Uhuru wa wahariri wa vyombo hivyo bado una maswali mengi kuhusiana na baadhi ya vyombo kutumika kutanga biashara na kuwasaida wengine kisiasa. OSIEA inaitaka serikali na vyombo vya usalama kuheshimu Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na kuacha kuwanyanyasa waandishi wa habari. Waandishi wa habari lazima waweze kuzungumza na kuandika bila ya kuwepo kwa vizuizi vyovyote. OSIEA pia inaitaka serikali kuwasilisha Bungeni muswaada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utaweka mazingira bora ya Uhuru wa vyombo vya habari.

  Wakati Tanzania ikiwa katika maandalizi ya kupata katiba mpya, tunahitaji kukumbuka kuwa Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari ni kitu cha muhimu kwa ajili ya kusambaza taarifa kwa jamii. Sio tu haki ya jamii kupokea taarifa bali bila kuwa na Uhuru haitakuwa na maana yoyote kwa serikali yao. Uwezo wa kupata taarifa utawezesha kukua kwa demokrasia, kuongeza msisismko wa mijadala ya kitaifa kutoa taarifa zitakazoongeza uwajibikaji. Uhuru wa kupata habari una mchango mkubwa katika mchakato wa kupata Katiba mpya.
  Licha ya kwamba Tanzania inakuza uchumi wake wa wakati lakini kusahau Uhuru wa vyombo vya habari kunaweza kukapunguza ufanisi wa ukuaji wa uchumi. Vyombo vya habari huru vinaweza kukuza kuimarisha jamii na kuvutia wawekezaji.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shares a light moment with Swaziland King Mswati III shortly before the commencement of the Fourth European Union and Africa Summit held in Brussels Belgium this afternoon. The summit will illustrate how EU-Africa relations have evolved over the past years, will highlight the results achieved by the continental Partnership and will frame cooperation for the years to come.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets German leader Chancellor Angela Merkel during the Fourth European Union and Africa Summit held in Brussels Belgium this afternoon. President Kikwete arrived in Brussels today for a two days working visit.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete greets French President Francois Hollande at the beginning of the EU Africa Summit held in the Belgium Capital Brussels this afternoon.Photos by Freddy Maro 

  0 0

  Timu nzima ya Tanzania Movie Talents kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza kwaajili ya shindano la kutafuta Vipaji vya Uigizaji Tanzania ambapo shindano hili litaanzia katika Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa Mwanza Kuanzia tarehe 5 April 2014 mahali ni Isamilo Lodge.
  Mdau Karimu Muhidin Michuzi na Baadhi ya vijana wa kazi katika timu ya kusaka vipaji wakiwa tayari kwa safari ya Mwanza.
  Mabasi yakiwa tayari kwa safari ya Mwanza.

  Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Limited imeondoka leo jijini Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Mwanza kwaajili ya kuendesha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania ambapo Kwa kuanza shindano hili litaanzia Mkoani Mwanza Katika Kanda ya Ziwa.

  Usaili wa Kutafuta vipaji utafanyika mnamo tarehe 5 mwezi huu katika ukumbi wa Isamilo lodge ambapo vijana wengi wanaomba kuhudhuria kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao.

  Zoezi la kusaka Vipaji katika Kanda ya ziwa utafanyika kwa Siku nne kuanzia tarehe 5 mwezi huu na pia kwa kanda ya Ziwa Usaili utafanyika katika Mikoa Miwili ya Kigoma na Mwanza. Proin Promotions Limited imeamua kusaka vipaji ili kuweza kuinua tasnia ya filamu nchini.

  0 0

  DSC_0546
  Mwenyekiti wa huduma za jamii manispaa ya Ilala, Angelina Nyalembeka akitoa ufafanuzi kuhusiana na kero za wadudu aina ya Kunguni katika shule hiyo ambapo amesema mwaka jana walipulizia dawa kwenye mabweni yote ya wanafunzi na haraka iwezekanavyo ataliwasilisha kero hiyo kwenye vikao vya Manispaa na kupatiwa ufumbuzi na wanafunzi waweza kukaa kwa amani bila usumbufu.
  DSC_0572
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa, akizungumza na waalimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu, kabla ya kukabidhi madawati kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  DSC_0527
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu wakifuatilia risala ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.
  DSC_0622
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha tatu ambaye ni mlemavu Voster Peter wakati akikabidhi madawati shuleni hapo.
  DSC_0482
  Baadhi ya viongozi wa Kata ya Pugu, Gongo la Mboto na Upanga Magharibi waliohdhuria hafla hiyo.
  DSC_0626
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahi jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi, wakati hafla fupi ya kukabidhi madawati 107 kwa shule hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa huduma za jamii manispaa ya Ilala, Angelina Nyalembeka akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela.
  DSC_0631
  Sasa mtajinafasi wakati wa masomo darasani si ndio..? Mstahiki Meya Jerry Silaa akimuuliza mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Pugu alipokuwa akikabidhi madawati.
  DSC_0638
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ulongoni, Bi. Sikitiko Salehe,( wa pili kulia) akipokea moja ya madawati kati ya 93 kwa niaba ya shule yake kutoka kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa ikiwa ni zao la matunda ya Mayor's Ball 2013 iliyoweka kipaumbele kwenye elimu kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule ya sekondari Pugu jijini Dar.
  DSC_0645
  Wanafunzi wa Shule ya sekondari Pugu wakionyesha nyuso za furaha isiyo na kifani walipokabidhiwa madawati 107 na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
  DSC_0661
  Mstahiki Meya Jerry Silaa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali Kata za Gongo la Mboto na Pugu.


  DSC_0669
  DSC_0674
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa shule ya sekondari Pugu mara baada ya kukabidhi madawati 107 kwa shule hiyo.
  DSC_0678
  Kaka mkuu wa shule ya Sekondari Pugu, Nicetas Ndekubali Ndeng'asso, akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
  DSC_0692
  Kaka mkuu wa shule ya Sekondari Pugu, Nicetas Ndekubali Ndeng'asso akipeana mkono na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
  DSC_0701
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiondoka shuleni hapa mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi madawati kwa shule hizo za sekondari za manispaa ya Ilala.
  DSC_0490
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi akielezea furaha yake ya kupokea madawati 107 yaliyotolewa na mpango wa Mayor's Ball 2013 kupitia kampeni ya "Dawati ni Elimu" chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
  DSC_0521
  Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, akiwasilisha kero ya shule ya Sekondari Pugu kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhusiana na wadudu aina ya Kunguni kwenye mabweni ya wanafunzi shuleni hapo ambapo imekuwa kero kubwa wakati wa kulala na kuwasababisha usumbufu.
  DSC_0524
  Sehemu ya madawati kati ya 300 yaliyotolewa na mpango wa Mayor's Ball 2013 kupitia kampeni yake ya "Dawati ni Elimu" inayolenga kutatua uhaba wa madawati kwa shule zilizomo ndani ya Manispaa ya Ilala.
  DSC_0428
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akiwasili kwenye shule ya sekondari Pugu kwa ajili ya kukabidhi madawati 300 kwa shule tatu zilizopo manispaa ya Ilala na kulakiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jovinus Mutabuzi.(Picha zote na Zainul Mzige).

  .Ni katika Mpango wa “Mayor’s Ball” “Dawati ni Elimu, Kalisha mmoja, boresha Elimu”.

  Na Zainul Mzige
  “Kiongozi hapaswi kutegemea nguvu za Serikali kufanya shughuli za maendeleo” Hayo ni maneno ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa katika hafla ya kukabidhi madawati kwa shule tatu za sekondari zilizopo Manispaa ya Ilala iliyofanyika Shule ya sekondari Pugu.

  Katika hafla hii, jumla ya madawati 300 yenye thamani ya shilingi milioni 45 za kitanzania yaligawiwa kwa shule 3 zilizopo manispaa ya Ilala ambazo ni Shule ya sekondari Pugu (107), Shule ya sekondari Ulongoni (93) na Shule ya sekondari Jangwani (100) kupitia jitihada zake za kuanzisha mpango wa Mayor’s Ball 2013 ulioanza mwaka jana kupitia kampeni ya “Dawati ni Elimu, Kalisha mmoja, boresha Elimu”.

  Bwana Silaa alitoa pongezi na shukrani za dhati kwa wote waliotimiza ahadi zao katika kufanikisha zoezi zima la ununuzi wa madawati mapya na kufanikisha kampeni yenye lengo la kuinua viwango vya elimu ya sekondari na msingi Tanzania. Pia, alichukua nafasi kuwaomba wadau waendelea kujitokeza kuchangia elimu kwani ni mara ya kwanza kwa jambo hili la “Mayor’s Ball” kufanyika nchini.
  DSC_0431
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akisaini kitabu cha wageni katika shule ya sekondari Pugu mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
  “naomba nitumie nafasi kuwapongeza wadau wote walioitikia wito huu na naomba kutoa rai kwa wale wote walioahidi kutimiza ahadi zao ili kufanikisha lengo la kampeni hii iliyobeba kauli mbiu ya Dawati ni Elimu kalisha mmoja, boresha elimu”, alisema Mstahiki meya Jerry Silaa.

  Katika hotuba yake, amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii hasa baada ya kuwaboreshea mazingira ya kusomea kwa msaada wa madawati mapya na ya kisasa.

  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Imelda Samjela, ameiomba serikali kuu kuiangalia shule ya Sekondari Pugu kwa jicho la pili kutokana na hadhi yake ya kutoa viongozi nchini na kuifanya iwe na hadhi ya kimataifa. Shule ya sekondari Pugu inajivunia sifa ya kuwa shule iliyozaa viongozi shupavuTanzania akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Bi. Imelda aliongeza kuwa kila mwaka tunapoadhimisha Maisha ya Mwalimu Nyerere basi kufanyike jambo aidha kupaka rangi na kusafisha mazingira ya shule hiyo iliyobeba historia ya Taifa la Tanzania. Diwani pia alitoa wito wa kuweka fungu la fedha za kukarabati majengo ya shule hiyo pamoja na kutokomeza kero ya Kunguni shuleni.
  DSC_0446
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi(mwenye suti nyeusi) akizungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa. wengine pichani ni wakuu wa shule za sekondari Ulongoni na Jangwani waliojuika katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati. Kunguni wamekuwa ni kero kubwa kwa wanafunzi hasa wakati wakulala. Alitoa angalizo hili kwa mwenyekiti wa huduma za jamii.

  Akitoa ufafanuzi wa suala la ukarabati wa majengo ya shule hiyo, Mwenyekiti wa huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, Bi. Angelina Nalembeka amesema kuwa Manispaa ilishatoa shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ukarabati na wanampango endelevu wa kufanya hivyo kila mwaka. Mpango huu si tu kwa shule ya Pugu bali kwa shule nyingine pia zinazoizunguka manispaa ya Ilala.

  Mwenyekiti huyo pia alithibitisha kufanyika kwa zoezi la awali la kutokomeza Kunguni shuleni kwa kunyunyiza dawa na kuwepo kwa mpango endelevu wa kunyunyiza dawa ili kuondoa kabisa kero hiyo ya Kunguni shuleni.
  DSC_0456
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akipitia moja ya mafaili ya taarifa za shule hiyo.
  “Mheshimiwa Diwani amefuatilia suala lenu la Pugu kwa umakini na taarifa zake tunazo katika Halmashauri. Mwalimu mkuu atakuwa shahidi na tumeshakuja kupiga dawa na bado mwaka huu tutakuja kupiga dawa tena kuondoa Kunguni” alisema Mwenyekiti, Huduma za Jamii.
  Aidha, Mwenyekiti wa huduma za Jamii Manispaa ya Ilala aliongeza kuwa suala ya kero la Maji liko kwenye utatuzi kamati yake ya manispaa yake ilishatembelea shuleni hapo na kuona kero hiyo.

  Amempongeza Mstahiki Meya kwa juhudi zake za kutatua tatizo la madawati na ameomba wengine pia ambao ni viongozi wakubwa serikalini waliosoma shuleni hapo wakumbuke walipotoka na kusaidia kuiweka katika hali nzuri.
  DSC_0479
  Meza kuu ikipokea heshima ya ukaribisho kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Pugu (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Kaimu Diwani wa Upanga Magharibi, Bi. Jokha Lemki, Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, Mstahiki Meya, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabazi na Mwenyekiti wa Hudama za Jamii Manispaa ya Ilala, Angelina Malembeka.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na baadhi ya viongozi wa chama Wilaya ya Kalambo,wakikatiza kwenye Ofisi ya CHADEMA,ambayo inadaiwa imefungwa miaka mitatu 3 sasa kwa kushindwa kulipia pango.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia tofali ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akibeba tofali aliyoifyatua,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo
   Wajumbe wakifurahia jambo mara baada ya Ndugu Kinana kuzungumza jambo mbele yao.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe nyumbani kwa Mjumbe wa shina No.1,Bwa.Apolinali Kwidikwa,katika kata ya Kateka,wilayani Kalambo mkoani Rukwa mapema jana jioni.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Matai,katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa mapema jana jioni.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Kinana akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Kasanga Wilayani Kalambo jana jioni,kabla ya kufanya mkutano wa hadhara na kuzunguma na wananchi hao mambo mbalimbali ikiwemo Afya,maji,Elimu.Barabara na mengineyo.
   Baadhi ya Wanachi wa kijiji cha Kasanga wilayani Kalambo wakifuatilia mkutano. 
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Balozi Ally Karume akihutubia mbele ya wananchi wa kijiji cha Kasanga,Wilayani Kalambo mkoani Rukwa mapema jana,wakati wa mkutano wa hadhara.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akila kiapo na  Sehemu ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi,ambapo Wanachama wapya 266 wamejiunga na chama hicho katika kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
   Sehemu ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi na Ndugu Kinana wakila kiapo.Wanachama wapya 266 wamejiunga na chama hicho katika kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizawadiwa zawadi kutoka kwa akina mama wa kata ya Kasanga,iliopo ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Kasanga,iliopo ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa mapema jana jioni.Kinana bado yupo Mkoani Rukwa na ziara yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi mbalimbali,ikiwemo na kusikiliza kero za wananchi. 
  Baadhi ya akina mama wakazi wa kata ya Kasanga wilayani kalambo wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo utatuzi wa masuala ya  Afya,Elimu,Barabara na maji.
  Waendesha bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuelekea kijiji cha Matai,Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa ya hali ya kisiasa katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa mapema jana.

  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka na Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti kulia), akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), anayemsaidia ni Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi. Wanaoshudia ni Mkuu wa Mahusiano wa TBL, Bw. Stephen Kilindo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Dkt. Asenga Severin. 
   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akijaribu kufungua koki ya bomba la maji, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, kilichojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL,  Ilala, Bw. Godrack Kalebi na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu.
   (mwenye suti), akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvuti, Bi. Aghata Senga, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). kulia ni Mkuu wa Mahusiano na sheria wa TBL, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL kanda ya Ilala, Bw. Godrack Kalebi (wa pili kulia) na Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka (mwenye kilemba kushoto). 
   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akijaribu kufungua koki ya bomba la maji, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, kilichojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL,  Ilala, Bw. Godrack Kalebi na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu.
   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akimshika mkono wa pongezi Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), wakati wakielekea kuzindua mradi wa maji katika zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, ulichojengwa na TBL. Kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo.


  0 0

  DSC_0716

  Na. Mwandishi wetu.
  Makampuni matatu makubwa yaliyo ndani ya MeTL Group hivi majuzi yamefanikiwa kutwaa tuzo za Rais za Watengenezaji Bidhaa kwa mwaka 2013.

  Makampuni hayo ni: East Coast Oils & Fats Ltd ya Kurasini ambayo hutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia pamoja na bidhaa nyingine.
  Afritex Limited ambayo hutengeneza Khanga, Vitenge na bidhaa zifananazo; na 21st Century Textiles ambayo ni kampuni kubwa na ya kisasa Afrika Mashariki na kati inayotengeneza bidhaa kama khanga, vitenge, vikoi, mashuka, nguo za kimasai n.k.

  Tuzo ya Rais ya Watengenezaji wa Bidhaa ni tuzo ambayo hutolewa kwa makampuni mbali mbali nchini Tanzania yanayojihusisha na utengenezwaji wa bidhaa. Ubora wa bidhaa ndio hufanya kampuni kushinda tuzo hiyo.
  DSC_0722DSC_0723DSC_0724

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ukaguzi maalum wa maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es salaam kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219.
  Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge akitoa ufafanuzi kwa waandishi kuhusu hatua zinazochukuliwa na TFDA kuhakikisha usalama wa vyakula na Dawa nchini .TFDA imekuwa ikiongeza nguvu katika kukabiliana na bidhaa zisizokidhi viwango kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za udhibiti kwa kukagua, kukamata na kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wanaokiuka sheria.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo (kulia) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika ukaguzi maalum kwenye maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es salaam zikiuzwa kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219. Wengine ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge, na Meneja wa Ukaguzi wa Chakula wa TFDA kanda ya Mashariki Bw. Emmanuel Alphonce.
  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) akiwaonesha waandishi wa habari baadhi ya bidhaa zilizokamatwa na mamlaka hiyo zikiwemo chumvi, vinywaji, maziwa ya watoto ambazo hazijasajiliwa na mamlaka hiyo kufuatia ukaguzi maalum uliofanyika katika jiji la Dar es salaam.
  Maziwa ya watoto aina ya SMA 1,2 na 3, Promil Gold, S-26 Gold, Nursoy, Progress Gold, Cow &Gate, Isomil 2 na Infacare Soya , Nutrikids na Aptimil 1 yaliyokamatwa ambayo hayajasajiliwa na TFDA .
  Vinywaji baridi ambavyo havikusajiliwa na TFDA vilivyokamatwa kufuatia ukaguzi maalum katika jiji la Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa. 

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the President of the European Commission Jose Manuel Barroso at his Office in Brussels Belgium this morning. President Kikwete was in Brussels where he attended the 4th EU Africa Summit under the theme, ”Investing in People, prosperity and peace”.(photo by Freddy Maro).

  0 0

  Viongozi wa Nchi za Kiafrika katika Makao Makuu ya AU. Jumla ya nchi 34 kati ya 54 wanachama hai wa AU ni wanachama Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
  Wajumbe wa Bodi na Sekretarieti ya APRM (Tanzania) wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt. Jakaya Kikwete. Kushoto kwa Rais ni Mwenyekiti wa APRM, Prof. Hassa Mlawa na kulia ni Katibu Mtendaji wa APRM, Bibi Rehema Twalib. 
  ========  ======  =======
  APRM, MKAKATI MARIDHAWA KUDUMISHA UTAWALA BORA NA UCHUMI

  Na Saidi Mkabakuli.

  Wasomi na wanafalsafa waliobobea toka vizazi na vizazi wamekuwa wakiamini kwenye usawa na haki. Kwa mtazamo wa sasa, imani hii ni msingi wa maendeleo wa kijamii na kiuchumi kwa taifa lolote linaloamini katika demokrasia.

  Hatahivyo, licha ya upana wa kitafsiri na mitazamo na mapokeo ya msamiati huu unaotokana na maneno ya Kigiriki, dêmos lenye maana ya watu (people) na kratos lenye maana ya nguvu (power) au tawala (rule) yenye kumaanisha utawala wa watu; misingi yake inachagizwa na Dola kufuata kwa vitendo utawala wa haki na sheria.

  Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi duniani kwa miaka mingi imekuwa mfuasi wa dhana hii na ikifanya jitihada nyingi za kuboresha licha ya changamoto zinazokinzana na jitihada hizi. Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ufuasi wake kwa demokrasia na hasa suala zima la utawala bora, sio tu ilianzisha wizara maalum kwa ajili ya kusimamia utawala bora pia ilijiunga na Mpango wa Kujipima kwa kutumia vigezo vya Utawala Bora (APRM) kwa kuwasilisha rasmi maombi ya kujiunga na mpango huu tarehe 26 Mei, 2004 na kukubaliwa rasmi tarehe 8 Julai 2004, wakati wa Kikao cha Tano cha Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika.

  APRM ni mpango wa hiari, uliobuniwa na viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, kuziwezesha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, kujitathmini katika utendaji wa shughuli za serikali na shughuli zao nyingine kwa ujumla. Aidha mpango huu unalenga kuzipa nchi wanachama, fursa ya kujifunza kutokana na uzoefu na mafanikio ya nchi zingine za Kiafrika, na hivyo kuziwezesha nchi husika kuiga sera na mbinu muafaka zilizoleta mafanikio hayo kwa manufaa ya nchi zao. Kwa ujumla, ombi la kufanyiwa tathmini linapofanywa, linaashiria nchi husika kukubali kufuata misingi ya utawala bora katika uendeshaji wa siasa na shughuli za kiuchumi na wakati huohuo, kukubali kufanyiwa tathmini na Viongozi Wenza wa nchi za Kiafrika.

  Hadi sasa nchi 34 kati ya 54 wanachama wa Umoja wa Afrika zimejiunga na mpango wa APRM. Mpango huo unahusisha uhakiki katika vipindi mbalimbali (periodic reviews) wa sera, kanuni na taratibu za utendaji zilizozoeleka (practice) ili kubaini maendeleo yaliyopatikana katika kutekeleza malengo yaliyokubaliwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na utawala wa pamoja wa kibiashara kama ilivyoainishwa kwenye Tamko la Demokrasia, Siasa, Uchumi na Utawala wa Pamoja.

  Chimbuko la APRM ni Mpango Mpya wa Maendeleo ya Afrika (New Partnership for Africa’s Development-NEPAD), ambao unalenga kuliondoa bara la Afrika kutoka kwenye lindi la umaskini, na kuleta maendeleo. NEPAD imeunganisha mipango ya maendeleo iliyobuniwa chini ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, (OAU), na kuainisha ukosekanaji wa utawala bora kama mojawapo ya vikwazo dhidi ya maendeleo yanayolikabili bara la Afrika. Hivyo, ili kukabiliana na kikwazo hiki, viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika (UA) walitoa Tamko Kuhusu Demokrasia, Siasa, Uchumi na Uongozi Bora katika nyanja za uchumi na mashirika ya kibiashara. Tamko hilo pia linaainisha mkakati wa kufanikisha azma hii, kupitia demokrasia na utawala bora.

  Lengo la msingi la APRM ni kuhimiza utumiaji wa sera, viwango na miendeno inayokubalika kitaalamu ili kujenga utengamano wa kisiasa, ukuaji chanya wa uchumi, maendeleo endelevu na kuharakisha ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda na hatimaye bara zima. Pia, APRM inatoa fursa ya kuchangia katika kudumisha utengamano, kuleta maendeleo pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kikanda kwa njia ya kubadilishana uzoefu na kuiga mifano bora ikiwa ni pamoja na kutambua udhaifu na kutathmini mahitaji ya kuongeza uwezo wa serikali na nchi.


  Kwa kutambua umuhimu wa utawala bora, Mipango na mikakati mingi ya kimaendeleo na ile ya kupambana na umaskini imekuwa ikijumuisha kipengele cha utawala bora kama moja ya misingi ya kufikia malengo. Kwa mfano, moja ya misingi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV) 2025, kati ya misingi minne ya utekelezaji, unahimiza uimarishaji wa utawala bora na uongozi wa haki na kisheria ikiwa ni pamoja na jamii kukataa rushwa, kuimarisha mifumo ya uongozi na utawala ili kuweza kufikia malengo makuu ya Dira hiyo.
  Pia, kwa upande wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA) I&II, sifa na misingi yake ni pamoja na Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Mapato; Kuboresha maisha ya watu na Ustawi wa Jamii; na Utawala bora na uwajibikaji. Suala kuu la msingi linalojitokeza katika kila Mkakati ni Utawala bora na uwajibikaji. Dhana hii ni msingi madhubuti katika kutekeleza mikakati hii yenye mkondo wa kiuchumi na mingine mingi inayotekelezwa na Serikali. Hivyo basi, umuhimu wa APRM katika mustakabali wa ustawi wa jamii ni chanya, kwa kuwa nchi inapata faida ya kujitathmini pale inapokosea. Hivi karibuni Katibu Mtendaji wa Mpango huu (APRM) nchini Tanzania, Bibi Rehema Twalib alitoa taarifa kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri katika utawala bora Barani Afrika.

  Akizungumzia umuhimu wa APRM katika kufikia lengo la msingi la mikakati hii, Bibi Twalib anasema kuwa ni muhimu kudumisha utengamano, ili kuleta maendeleo pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kikanda kama njia ya kubadilishana uzoefu ili kuiga mifano mizuri kutoka nchi zilizopiga hatua kiuchumi.

  Kwa mujibu wa Bibi Twalib, Tanzania imepata mafanikio katika maeneo ya Usimamizi wa Uchumi, Maendeleo ya Uchumi-Jamii Demokrasia na Utawala Bora, Siasa, Uendeshaji wa Kampuni na Masuala Mtambuka kama Afya.

  Bibi Twalib alisema kuwa Tanzania kupitia APRM, imefanya tathmini yake katika maeneo hayo na kuwasilisha ripoti yake mbele ya wakuu wa nchi wanachama na kujadiliwa. Akizungumzia mikakati iliyopo katika kuhakikisha kuwa malengo ya APRM yanakuwa chachu ya kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo kwa jamii ya Kitanzania.

  Bibi Twalib aliongeza kuwa APRM kupitia Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inaendelea kuendesha tathmini ya utendaji wake na vyombo vyake kwa uwazi, ukweli na umakini, kulingana na vigezo vilivyowekwa kwenye Mpango wa Kujipima kwa kutumia Vigezo vya Utawala Bora.

  “Kwa kutambua umuhimu katika kuimarisha utawala bora, Sekretarieti inaendelea kutekeleza Mpango kazi wa kitaifa wa kujitathmini katika masuala ya utawala bora (African Peer Review Mechanism - National Plan of Action, APRM-NPoA),” aliongeza Bibi Twalib.
  Kwa mujibu wa APRM-NpoA, moja kati ya manufaa ya ya utekelezaji wa Mpango huu ni kubaini mambo mazuri juu ya utawala bora nchini Tanzania hali inayoongezea imani (confidence) wawekezaji toka nje ya nchi na wabia wa maendeleo. Hili moja ya mafanikio ya APRM, maana kwa mujibu wa takwimu kutoka Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) mpaka kufikia mwezi Desemba, 2013 kilifanikiwa kusajili miradi 9,442.
  Hatahivyo, suala la kushirikisha wananchi ni suala lisiloepukika, ambapo, Bibi Twalib anahimiza suala la nafasi ya wananchi katika Mchakato huu. Bibi Twalib anasema kuwa, kwa kuwa APRM ina njema ya kupanua wigo wa demokrasia, na kuwapa wananchi kauli katika maamuzi yanayohusu mustakabali ya nchi yao.

  “APRM Tanzania inategemea kuwa wananchi watatumia kikamilifu, nafasi inayotolewa ili kutoa tathmini yao ya kweli, kuhusu yale wanayoyaona kuwa ni mapungufu ya utendaji serikalini na mapungufu ya utawala bora nchini kwa ujumla, ili kuiwezesha serikali nayo kuyabaini mapungufu hayo na kuyachukulia hatua muafaka” anasihi Bibi Twalib.

  Anaongeza kuwa ikiwa wananchi watatumia vyema fursa hizi vizuri, ndipo malengo ya kuanzishwa kwa Mchakato huu yatakapotekelezwa na kuwezesha kutimia malengo na misingi ya mikakati ya Serikali ya kuivusha Tanzania kutoka dimbwi la umaskini.

  0 0

   Skimu ya Maji ya Kabambe iliyojengwa  katika Wilaya ya Monduli kata ya Majengo kuwasaidia wakulima kupata maji kwa ajili ya kilimo cha Mahindi, Ndizi na Mbogamboga, ikiwa ni sehemu ya miradi inayoratibiwa na ASDP na kusimamiwa na wadau wa maendeleo IFAD .

   1.    Mojawapo ya Shamba la Nyanya linalotumia Skimu ya Maji ya Kabambe inayoratibiwa na Miradi ya ASDP katika Wilaya ya Monduli.  

   1.    Shamba la Mbogamboga la Wakulima wa Monduli wanaotumia  Skimu ya Maji ya Kabambe  ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya miradi ya ASDP inayosimamiwa na wadau wa maendeleo IFAD

  1.    Afisa Miradi wa IFAD nchini Dkt. Mwatima Juma pamoja na waratibu wa miradi mbalimbali akitoa maelezo kwa wakulima (Kulia) wanaotumia Skimu ya Maji ya Kabambe iliyopo katika jinsi ya kujipanga katika kilimo na kutunza chanzo cha Skimu hiyo iliyopo katika Wilaya ya Monduli katika kata ya Majengo Mkoani Arusha.


older | 1 | .... | 262 | 263 | (Page 264) | 265 | 266 | .... | 1898 | newer