Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 263 | 264 | (Page 265) | 266 | 267 | .... | 1898 | newer

  0 0

   
  Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhisina na uzinduzi wa upimaji macho utakao fanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam. Kushoto ni Mratibu mradi huo Violet Shirima.
   Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akionesha miwani itakayozinduliwa.
  ********
  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa utoaji wa huduma ya macho bure, itakayofanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam.

  Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema wameamua kutoa huduma hiyo bure kwa sababu inakadiriwa, watanzania Milioni 3.5 wameathirika na ugonjwa wa macho wengi wao ni  wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.

  Alisema huduma hiyo itaanza kutolewa leo hadi Aprili 11 mwaka huu jijini Dr es Salaam, kuhamasisha watu kuwa na desturi ya kupima macho mara nyingi zaidi.

   ‘’Tumeandaa miwani za aina 12 ambazo saizi zote zinapatikana na tutaziuza kwa bei nafuu kuliko wanavyouza mawakala wengine’’ alisema Mashayo.

  Aliongeza kuwa Taasisi hiyo inatoa huduma katika mikoa nane ambayo ni Mbeya, Mwanza, Mtwara, Singida, Iringa, Dodoma, Songea na Lindi. 

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu faida za Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato yatokanayo na Simu unaojulikana kama Telecommunication Traffic Monitoring System (TTMS). Mtambo huo unaweza kutambua mawasiliano ya udanganyifu katika mitandao na namba za ulaghai zinazotumika kwenye mawasiliano ya kimataifa kinyume cha sheria. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi. 

   Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  uliofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la Mkutano huo ni kuelezea mtambo wa TTMS unavyodhibiti udanganyifu katika mitandao ya simu za kimataifa. PICHA ZOTE NA FATMA SALUM- MAELEZO
   Naibu Mkurugenzi anayehusika na usimamizi wa Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato ya Simu (TTMS) kutoka TCRA, Mhandisi Sunday Richard akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jinsi mtambo huo unavyofanya kazi ya kudhibiti udanganyifu katika mitandao ya simu za kimataifa zinazoingia hapa nchini

  0 0
  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw.  Ridhiwani Wema akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo piuchani) kuhusu taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu au makampuni binafsi kuhusiana na maudhui ya Tamko la Serikali lililoziagiza wakala binafsi  wa Huduma za Ajira  kuwasilisha upya maombi ya usajili wa uwakala kwa Kamishna wa Kazi.

   Afisa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Themistocles Rumboyo akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa hadi kufikia Februari mwaka huu jumla ya maombi 56 ya makampuni ya huduma za ajira nchini yamewasilishwa kwa Kamishna wa Kazi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.

  Afisa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Omari Sama akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua taratibu za kusajili wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini. Kulia ni  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema. PICHA ZOTE NA FRANK MVUNGI- MAELEZO

  0 0

   Uwanja wa mabembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika matengenezo,ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara leo ya kuona maendeleo ya ujenzi huo.
   
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,atembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja.

  =======  ===== =====
  Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar        .

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein  ameagiza kufanyika mazungumzo  kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na Wizara ya Ardhi,Makaazi Maji na Nishati ili kupatikana Hati miliki katika  eneo la Ujenzi wa Mnara  wa Mapinduzi katika eneo la Michezani Mjini Zanzibar.

  Hayo ameyasema leo alipofanya ziara maalum kuangalia hatua ya ujenzi wa  Mnara huo na Kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo unaosimamiwa na  Mfuko huo.   Amesema kupatiwa hati miliki ya eneo la Michezani ni suala la kukaa pamoja taasisi hizo husika kwani eneo hilo linamilikiwa na Serikali na sio la mtu binafsi. 

  “Nendeni mkazungumze na watu wa Ardhi mkubaliane halafu nijue mulipofikia  haya yote ni maeneo ya Serikali,”alisema Dkt. Shein. Alisisitiza  kwamba  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuliendeleza eneo hilo la Michezani kwa kujenga Mnara utakao kuwa na  Maduka na Mikahawa hivyo kuna haja  kukaa na wafanya biashara wa eneo hilo kufanya mazungumzo na kuwatafutia maeneo mengine ya kuendeleza biashara zao.

  “Wafanya biashara wanapenda maeneo mazuri, sidhani kama watakataa kupatiwa sehemu nyengine ili kuendeleza biashara zao,”aliongeza Rais wa Zanzibar. Aidha Dkt. Shein alifurahishwa na hatua iliofikiwa katika ujenzi wa majengo hayo na kusema kiwanja cha Kariakoo kinapaswa kuwa cha kisasa na bora kwani kitatoa huduma nyingi za kibiashara kitakapo malizika.  

  Hata hivyo alisema  kiwanja cha Kariakoo kimezungukwa na majirani hivyo upo umuhimu  kukaa na majirani hao kwa mazungumzo ili kupatikana usalama wa eneo hilo. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Abdulwakil Haji Hafidh alisema kuwa kiwanja cha Kariakoo hadi sasa kimeshagharimu shilingi bilioni 10 na mpaka kitakapomalizika kitagharimu shilingi bilioni 13.5 za Tanzania.

  Alisema kiwanja hicho kinatarajiwa kutoa huduma kuanzia mwakani kwani  hatua kubwa ya ujenzi imekamilika na vifaa vingi vimeshawasili na vinasubiri  kufungwa. Abdulwakili alisema kuwa kiwanja hicho kitakuwa na huduma zote muhimu  kwa binaadamu ikiwemo maduka, mikahawa na maeneo ya kupambia maharusi na burudani nyengine. Aliongeza kuwa  ujenzi wa kiwanja  hicho utakapo kamilika  wataunda bodi maalu  itakayojitegemea  kukiendesha.

  Wakati huo huo Dkt. Ali Muhamed Shein alitembelea eneo la Skuli ya Sekondari ya Lumumba na kukemea tabia ya kuvamia eneo hilo kwa kuchimbwa mchanga na kuligeuza kuwa gereji.
  Amesema Serikali inampango wa kulizungushia uzio na  matayarisho yake yamekamilika na  karibuni tenda ya ujenzi itatangazwa ili kuirejeshea skuli hiyo hadhi yake ya zamani.

  0 0

   
  Warembo 17 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumtafuta Redds Miss Tabata 2014. Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Da West Park kila siku kuanzia saa nane mchana.

  Kapinga aliwataja warembo waliojitokeza kuwania taji hilo kuwa ni Ester Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18),  Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
  Wengine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21),  Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22) na Faudhia Hamisi (21).
  Warembo hao wanafundishwa na Neema Mchaki, Pasilida Mandali na mcheza shoo wa kiume maarufu nchini Bokilo.
   
  Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu. Anayeshikilia taji la Miss Tabata Dorice Mollel ambaye pia ni Miss Ilala.
  Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

  0 0

  Serikali inalenga kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya shilingi trioni 6 hadi kufikia mwaka 2015/16 ikiwa ni sehemu ya ukamilishwaji wa mkakati wa “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

  Katika mkutano wake na wamiliki wa magazeti tando, msemaji mkuu wa wizara ya Fedha, Bi Ingiahedi Mduma alibainisha kuwa kuna vyanzo vingi vya fedha ambavyo wizara yake imedhamiria kuvitumia lakini kwa hii ambayo wanatarajia kushirikisha sekta binafsi ipo miradi mitatu mikuu ambayo inatarajiwa kutoa muongozo.

  Bi mduma aliitaja miradi hiyo ya awali kuanza kutekelezwa kwa ubia ni ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze, uendeshaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, na ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi III. 

  Amesema ukiachana na miradi hii, Wizara ya Fedha inaendelea kutekeleza jukumu la kutafuta na kutoa fedha za kugharamia shughuli za BRN zilizoibuliwa katika maabara zote sita za Elimu, Maji, Kilimo, Uchukuzi, Nishati na utafutaji na mapato ya serikali.

  Bi Mduma ameelezea pia kwamba katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 Wizara ya Fedha imefanikiwa kutekeleza kiashiria hiki kwa kutoa fedha za maendeleo za ndani kwenye Wizara zinazotekeleza shughuli za BRN.

  Amesema jumla ya shilingi Bilioni 590.5 zimetolewa katika kuhakikisha kwamba maabara hizi zinaweza kujitegemea katika miradi yake.

  Akitaja viwango nvya fedha ambavyo wizara imetoa, Bi Mduma alisema miradi ya Elimu imepewa jumla ya shilingi bilioni 8.3, Miradi ya Maji imepewa shilingi bilioni 86.0, Miradi ya Kilimo shilingi bilioni 10.2, Miradi ya Uchukuzi shilingi bilioni 146.6 na Miradi ya Nishati imepewa jumla ya shilingi bilioni 339.4.

  0 0

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  

  Kampuni ya Royal Hanskoning DHV ya Nchini Uholanzi inayoendelea na Utafiti wa kujua Maeneo ambayo yanafaa kujengwa Bandari imegundua Maeneo ya Fumba, Mangapwani na Maruhubi ni maeneo muhimu ambayo yanaweza kujengwa bandari za kisasa.

  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Elzinga Theun amesema hatua za awali za utafiti wao zinaonesha maeneo hayo ya Kisiwa cha Unguja ni mazuri kwa Ujenzi wa Babandari kutokana na kuwa na kina kizuri cha maji na kukosekana kwa mawimbi Makali.

  Theun ameyasema hayo leo katika Semina ya kujadili maendeleo ya Sekta ya Bandari iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar. Amefahamisha kuwa katika Tafiti zao wamegunduwa kuwa maeneo ya Mashariki ya Kisiwa cha Unguja yana changamoto nyingi za Ujenzi wa Bandari ikiwemo ile ya Mawimbi makali ya bahari jambo ambalo linaweza kuleta shida.

  Aidha Mkurugenzi Theun ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutafuta mbinu za kuitanua Bandari ya Malindi ili iweze kuhimili mahitaji yaliyopo.  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dkt Juma Malik Akili amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kufikiria namna ya kuitanua Bandari ya Malindi ili kuhakikisha inakidhi Viwango vinavyotakiwa.

  Amesema kabla ya kuanza Ujenzi wa Bandari Mpya ya Maruhubi Serikali inatafuta eneo la kuweka Makontena zaidi ya Laki mbili kwa mwaka ifikapo mwaka 2017 badala ya uwezo wa kuweka Makontena Elfu 60 uliopo sasa.

  Dkt Akili amesema hatua hiyo itaisaidia Zanzibar kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya Bandari na kuufanya uchumi wa Zanzibar kukua kwa kiwango kikubwa. Utafiti huo unaofanywa na Kampuni ya Royal Hanskoning DHV ya Nchini Uholanzi wa kuchunguza maeneo mazuri ya kujenga Bandari katika Visiwa vya Unguja na Pemba unatarajiwa kugharimu Jumla ya Pounds Laki 1.5 za Uengereza ambapo gharama hizo zimetolewa na Serikali ya Uholanzi.

  0 0

   Wananchi wakimuangalia mgambo wa Manispaa ya Ilala wakati akichukua magazeti katika moja ya meza Posta mpya jijini Dar es Salaam Aprili 3, 2014 Mkoa wa Dar es Salaam upo katika operesheni kabambe ya kusafisha jiji hilo kwa kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara ndogo ndogo maeneo yasioruhusiwa wilaya zake zote za Ilala, Temeke na Kinondoni.
   Mgambo wa Manispaa ya Ilala akiwa amebeba magazeti.
   Mgambo wa Manispaa ya Ilala akiwa amebeba magazeti wakivunja moja ya toroli la Kampuni ya TSN katika operesheni safisha jiji maeneo ya Posta mpya Dar es Salaam. Operesheni hiyo inafanyika mkoa wa Dar es Salaam kwa kuzihusisha wilaya zake zote za Ilala, Temeke na Kinondoni.
   Mgambo wakiondoa kibanda cha Kampuni ya Simu Tigo.
   Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.
   Eneo la Posta Mpya .
   Wafanya biashara wa Stendi ya Daladala Mwenge jijini Dar es Salaam wakiwa hawana lakufanya wakiangalia zoezi la bomoa bomoa likiendelea.
   Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON .


  0 0

  Mabasi yaliyokuwa yamebeba timu nzima ya Proin Promotions Limited yakiwa yamewasili Mkoani Mwanza Usiku huu.
  Baadhi ya Timu ya Wafanyakazi Kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ndio waendeshaji na wasimamiaji wa Mashindano ya Kusaka Vipaji vya uigizaji Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents wakiwa wanashuka katika Moja ya Basi lililokuwa limebeba wafanyakazi na timu nzima ya Proin Promotions Limited mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza Usiku huu.

  Timu nzima ya Proin Promotions Limited imewasili salama usiku huu katika Jiji la Mwanza ikitokea Mkoani Dar Es Salaam, tayari kwa kuanza zoezi la Kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania, Zoezi hilo limeanzia Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa Mwanza ambapo mashindano hayo yataanza tarehe 5 aprili.

  Mashindano haya yatafanyika Mkoani Mwanza kwa siku Tatu kuanzia tarehe 5 hadi 9 mshindi wa kwanza atakayepatikana atajinyakulia kitita cha Shilingi laki tano.

  Tunaomba Vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza na Vitongoji vyake waweze kujitokeza kwaajili ya kuonyesha vipaji vyao ili kuweza kuendelea ujuzi na vipaji vyao vya kuigiza Tanzania na kukuza tasnia ya filamu Nchini.

  0 0

  hamisi2
  Learning to walk: Hamisi and his prosthesis.
  What happens when a community pulls together to help one of their own? MOblog has followed the remarkable story of a young Tanzanian boy called Hamisi.

  Hamisi is a young Tanzanian boy who has suffered for a long time from Plexiform Neurofibromatosis, a disease which causes large and restricting tumors. Hamisi developed an enormous growth on his right leg which was incredibly heavy. Due to the weight he was unable to walk and had to crawl on all fours and drag his heavy leg behind him. His leg which grew to a monstrous size, weighed the young boy down, preventing him from playing and enjoying a normal childhood.
  hamisi 4
  Hamisi's leg before the operation
  Hamisi grew up in Tanzania with his father. Despite the desire, his father was unable to afford the expensive healthcare to ease Hamisi’s suffering. But through the kindness of others the community rallied together and through their efforts they were able to raise enough money to send Hamisi for an operation which would change his life forever.

  In February 2014 Hamisi and his father nervously boarded a plane bound for Coimbatore in Southern India. It was here that he was greeted by an expert team of plastic surgeons at Ganga Hospital who were about to change his life.

  Hamisi underwent extensive surgery where the surgeons removed the entire leg below the knee which weighed a staggering 5kgs. They hoped that removing the weight would allow him to move freer and feel lighter; it will also help his father to carry him when he is unable to walk. People suffering from Plexiform Neurofibromatosis tend to heal slowly and there can be complications so doctors were concerned that he may not make a full recovery. Hamisi is obviously a fighter at heart and defied the odds and recovered quickly and the doctors were able to remove some more of the leg around the knee in a second operation.
  hamisi 3
  Hamisi with his father and the surgeon who amputated his leg.
  After the operation Hamisi was fitted with prosthesis. Special prosthesis was made exclusively for him; both for the amputated limb and special shoes for the other leg but then came the hardest part. For many days he was sent to a training centre where he had to learn to walk with a walker. He needed very aggressive physiotherapy and walking training but doctors knew that they were pushed for time as he had a flight booked back to Tanzania after a couple of weeks. They worked overtime and fast to get him fit to walk and by the time he got on a plane he could take 30 steps with walker.
  hamisi 1
  Lots of smiles from Hamisi after the operation was a success.
  On the 29th March 2014, Hamisi returned to Tanzania a changed boy. His father has been trained in his physiotherapy so he can continue to build his strength. Both father and son are overwhelmed and so happy with the outcome of the operation which has made both their lives so much easier. A few months ago Hamisi’s future looked bleak but now thanks to the help of many people he faces a brighter, freer, independent future.

  It just goes to show a little kindness can go a long way.
  We, MO Blog team, would like to express our sincere appreciation to Miss Hoyce Temu for her outstanding support to our communities through her TV Program “Mimi na Tanzania” Or “Me and Tanzania.” Recently, she has mobilized our fellow Tanzanians to contribute to the treatment of a Tanzanian boy, Hamis, who was suffering from unknown illness. Miss Hoyce Temu you are an inspiration and your heart reflects Tanzanian spirit. You are Tanzanian for Tanzanians.

  0 0

  Katika karne iliyopita, wasomi mbali mbali wakiwepo wanauchumi, pamoja na wataalamu wa maswala ya kijamii waligundua umuhimu wa rasilimali watu katika kukua kwa uchumi wa dunia. Kuwepo kwa elimu bora, na ujuzi katika nafsi ya binadamu huwasaidia watu kujitengenezea vipato vikubwa. Tanzania inahitaji idadi kubwa ya rasilimali watu ili iweze kupiga hatua kubwa za kiuchumi.

  Kuwepo kwa mali asili kama madini, mafuta na gesi asilia kwa kiwango kikubwa imekuwa laana kwa mataifa kwani yamekuwa vyanzo vya unyanyasaji wa kijamii na umasikini uliopitiliza kwa jamii zisizokuwa na rasilimali watu ya kutosha ili kuzisimamia na kuziendeleza.


  Baada ya vita vya pili vya dunia, Ujerumani ilikuwa katika wakati mgumu wa kujinyanyua kiuchumi. Miundombinu mingi iliharibiwa kipindi cha vita. Na Ili kujinyanyua kutoka katika uharibufu mkubwa uliosabishwa na vita,  serikali ya Ujerumani ilibuni mfumo wa elimu ambayo ilielekeza juhudi zake katika kutayarisha rasilimali watu. Elimu ilipewa kipaumbele; Ilifanywa kuwa ya bure na ya lazima kwa kila mjerumani. Mfumo huu wa elimu ulifanywa kuwa wa vitendo zaidi na lazima kwa kila mtoto mwenye umri wa miaka tano hadi kumi na tisa, huku kila mwanafunzi akipewa nafasi kuchagua cha kujifunza kutokana na uwezo wake lengo kubwa ikiwa ni kutayarisha rasilimali watu.

  Jitihada hizi za serikali ya Ujerumani ilizaa matunda makubwa ambayo yaliitwa miujiza ya kiuchumi. Leo, uchumi wa Ujerumani ndio uchumi mkubwa zaidi katika bara la Ulaya, na pia ndio mdhamini mkubwa wa mataifa taabani kiuchumi kama Ugiriki, Hispania nk. Ujerumani ni moja ya mataifa yaliyo juu zaidi kwenye maswala ya uhandisi inaongoza kwa uhandisi. Ujerumani inaongoza kwa uzalishaji wa viwanda ikiuza nje ya nchi bidhaa yenye thamani ya dola za kimarekani trillion 1.52 kwa mwaka 2012 tu. Haya ni mafanikio yaliyotokana na kuipa elimu kipaumbele, pamoja na matumizi ya rasilimali watu zilizoko ndani na nje ya nchi.


  Mataifa yasiyokuwa na mali asili nayo yameonyesha ubunifu wa hali ya juu. Israel kwa mfano, ni taifa dogo lenye rasilimali chache, huku ikizungukwa na maadui ambao lengo lao kubwa ni kuliangamiza. Ikiwa imezingirwa na maadui kila kona pamoja na kukosa rasilimali za asili, Israel imelazimika kutumia rasilimali watu ili isiangamizwe kijeshi na kiuchumi.


  Licha ya kujitengenezea baadhi ya taasisi bora za kielimu na utafiti duniani, Israel iligeukia wataalamu wenye asili ya kiyahudi waliotapakaa katika kila pembe ya dunia, ikiwapa uraia watu wote wanaotaka kurudi nchini humo. Leo Israel ndio moja ya nchi iliyoendelea zaidi kiteknolojia. Vyuo vikuu vya Israel vimezalisha wataalamu wa kila aina ambao  wanasaidia nchi hiyo kujiendeleza kiuchumi na kujilinda kijeshi.


  Baada yakugundua kwamba hatma yake haikuwa nzuri kiuchumi na kijamii, Singapore, nchi ndogo barani Asia ilianzisha mapinduzi ya miundombinu , viwanda, mawasiliano, na ya kielimu ili iweze kustahimili mabadiliko ya kiuchumi ya baadae. Leo, Singapore ni nchi ya nne duniani kwenye maswala ya kifedha na mmoja wa magwiji katika masoko yanayochipukia. Korea kusini nayo haina tofauti na Singapore, kwani ilikuwa masikini zaidi ya Kenya mwaka 1960. Leo hii Korea ya Kusini ina uchumi wenye thamani ya dola za kimarekani trillion 1.56 ambayo ni mara 47 ya Kenya. Hii yote imetokana na jitihada zake za kuzalisha rasilimali watu.


  Marekani imekuwa ni taifa lenye nguvu zaidi ya nchi yoyote ile duniani kiuchumi, kiteknolojia na kijeshi. Kwa kipindi kirefu sasa. Mapinduzi ya viwanda ya karne ya 19 iliisukuma nchi hiyo kutumia kila mbinu ; Marekani ilitumia rasilimali zake zote ikiwemo rasilimali watu. Mafanikio ya taifa hili kubwa duniani hayakuwa ya kubahatisha, yametokana na kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa, na pia kujivunia kile wanachokifanya.


  Wamarekani wamewekeza kwenye elimu kwa kiwango kikubwa. Wameanzisha vyuo vikuu vya elimu na utafiti bora kuliko zote duniani. Sera zao za uhamiaji zimekuwa kivutio kwa wataalamu bora kutoka  kila pembe ya dunia ili tu watu wenye vipaji waendelee kusadia taifa hili kuendelea kuongoza kiuchumi. Hazina kubwa ya Tanzania imetapakaa ulimwenguni. Wataalamu mbali mbali wenye asili ya kitanzania wametapaa kila pembe ya dunia wakitafuta maisha huku wakichangia maendeleo ya mataifa mengine kutokana na kukosa uhuru wa kuchangia nchi yao ya kuzaliwa.


  Wataalamu wenye asili ya Kitanzania wapo katika taasisi kubwa za kitafiti nchini marekani na mataifa mengine makubwa; wapo kwenye mashirika makubwa ya kifedha, wapo kwenye taasisi kubwa za afya nk. Mifano ni mingi ambayo siwezi kuielezea yote kwa leo, ila lengo langu ni kuielemisha jamii yetu kuhusiana na umuhimu wa watanzania waishio ughaibuni


  Ushindani mkubwa wa kiuchumi katika eneo la maziwa makuu ni msukumo tosha kwa Tanzania kutumia kila mbinu inayoweza kuwa mstari wa mbele tukizingatia kwamba, Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika yenye utajiri mkubwa; kwani imebarikiwa na kila aina ya rasilimali muhimu ambazo zingesaidia kuharakisha maendeleo yake. Ugunduzi wa gesi asilia na mafuta, madini pamoja na mbuga zake za wanyama ni rasilimali adimu na  muhimu kulikwamua taifa kutoka katika wimbi la umasikini.


  Kinachohitajika ni rasilimali watu; Kinachohitajika ni wataalamu wenye asili ya kitanzania waliopo ndani na nje ya nchi kushirikiana ili kuleta maendeleo ya haraka. Lazima watu wote wenye asili ya Kitanzania wapewe haki yao ya kikatiba pamoja na nafasi ya kushiriki kulijenga taifa, kijamii, kiuchumui na kisiasa


  Kamwe Tanzania haiwezi na haitaweza kuendelea ikitegemea wageni. Watakaoleta maendeleo na mabadiliko makubwa ni watanzania wenyewe. Mipaka ya dunia imefunguka katika hii karne ya ishirni na moja. Badala ya kukumbatia misaada inayotudhalilisha na wageni wanaoiba rasilimali zetu, tutumie hazina kubwa tuliyonayo ya  rasilimali watu, ili tuweze kujikwamua kutoka katika wimbi la umasikini.


  Wataalamu wa kitanzania waliotapakaa duniani, wanastahili haki ya kurudi kwenye ardhi yao ya kuzaliwa bila vikwazo vya aina yoyote. Katika kuandaa katiba mpya ya Tanzania, tusifanye kosa la kuwafungia nje ndugu zetu walio ughaibuni  kwa kuwa na  vibali vya kuishi na kusafiri. Ikumbukwe kwamba,  pamoja na kuwa na vibali hivyo, bado asili zao na mioyo yao itabaki Tanzania. Tusiruhusu historia ituhukumu hasa katika kipindi hiki ambapo ushindani wa maendeleo ya kiuchumi unazidi kuongezeka duniani

  Mungu Ibariki Tanzania

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Waalimu wa shule ya sekondari Ilemba,Sumbawanga Vijijini,alipokwenda kukagua ujenzi wa bweni la wasichana wa shule hiyo,iliopo nje ya kilometa 104 kutoka Sumbawanga Mjini.
  Sehemu ya bweni hilo la Wasichana,ujenzi wake ukiendelea.
  Ndugu Kinana akipokea taarifa ya Shule ya Sekondari ya Ilemba kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Bwa.Abeid Missana.Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 237 inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya Sayansi,Nyumba za walimu na idadi ya waalimu waliopo.
  Kinana akishiriki ujenzi wa jengo hilo la Bweni la wasichana shule ya sekondari ya Ilemba.
  Katibu Mkuu wa CCM,akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama Wilaya na Mkoa wakielekea kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya,kilichopo kata ya Ilemba;Sumbawanga Vijijini
  Kinana akipitishwa kukagua ujenzi wa zahanati hiyo na Ofisa Mtendaji wa Kijiji,Kata ya  Ilemba,Bwa.Desdei Kayola (pichani kati)
  Muonekano wa ujenzi wa kituo hicho cha afya,kata ya Ilemba ambacho kikikamilika kitaokoa maisha ya idadi kubwa ya watu,ambayo inapotea kutokana na uduni wa huduma ya afya iliyopo sasa,hivyo kituo hicho kitatatua changamoto zilizopo za huduma ya afya.
  Kinana akikagua ujenzi wa kituo cha Polisi kata Ilemba,Sumbawanga vijijini.
   Kinana akishiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi wa kituo hicho


  Wananchi wa kata ya Ilemba wakiwa na mabango Wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Kinana
  Wananchi wa Kijiji cha Ilemba wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Ilemba.
  Baadhi ya Wanachama wapya wapato 300 kutoka kata ya Ilemba, waliojiunga na chama cha CCM,wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa.
  Wananchi wa kijiji cha Ilango,Kata ya Ilemba,Sumbawanga vijijini wakimpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa aina yake alipokuwa akiwasili kijijini hapo ambapo pia aliongea na kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo na kuyafanyia kazi.


  0 0

  Ndege ya Shirika la ndege la Air Tanzania aina ya CRJ-200, yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ikiwa imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya hivi karibuni 
  =====  =======  ===
  SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania limeweka rekodi ya ongezeko la abiria kwa asilimia 57 wiki chake baada ya kupokea  ndege ya kukodi yenye uwezo wa kubeba abiria 50 aina ya CRJ-200 pamoja kuiongezea uwezo wa kuruka kwa wakati kwa asilimia 98.

  Aidha, shirika hilo limeweza kutoa nauli maalum kwa sikukuu za Pasaka kwa abiria wa mkoani Mtwara ambao kwa sasa watakuwa wakilipa shilingi 250,000/- ikijumuisha kodi zote, kwa tiketi ya kwenda na kurudi.

  Hayo yalidhihirishwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Air Tanzania (ATCL), Kapteni Milton Lazaro, wakati akitathmini utendaji wa kipindi kifupi wa ndege hiyo iliyokodishwa pamoja na kuangalia mchango wake wakibiashara katika shirika hilo.

  Kapt. Lazaro alisema kwa ujumla, ujio wa ndege ya CRJ-200 mapema mwezi Machi mwaka huu umesaidia kuboresha utendaji na kufikia kiwango cha juu, hali inayoipa uongozi wa shirika sababu za kujivunia kwa maamuzi yao ya kukodisha ndege hiyo.

  “Inabidi nikubali kuwa ndege imepokelewa vizuri na wateja wetu. Ndani ya wiki chache tu ikiwa inafanyakazi, tumepata ongezeko kubwa la abiria wetu na huduma zetu zimeweza kuaminika zaidi na wateja wetu wengi. Kwa maana hiyo, matokeo yamekuwa ni mazuri sana,” alisema Kapt. Lazaro.

  Alibainisha kuwa kinyume na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vikidai kwambandege iliyokodishwa ya CRJ-200 ni mzigo kwa shirika ikilinganishwa na ndege yake aina yaBombardier Dash-8, ndege hiyo mbali na kuimarisha utendaji wa ATCL, pia imeisaidia shirika kuokoa fedha na muda.

  “Hatutajitendea haki sisi wenyewe au kwa waliyotukodishia ndege hiyo kama tukiruhusu sisi wenyewe tujiingize kwenye mjadala wa muundo wa gharama au mchango wake wa kimapato, kwa muda huu mfupi. Inatosheleza kusema kuwa lengo letu la kukodisha ndege hii ambalo lilikuwa ni kubwa kuliko mengine limefanikiwa,” Ofisa Mtendaji huyo mkuu alisema.

  Kapt. Lazaro aliongeza kuwa, kuongezeka kwa idadi ya abiria wanaosafiri na Air Tanzania kumetokana na ukweli kuwa muda inayotumia ndege ya CRJ-200 kusafiri umekuwa mchache zaidi ukilinganisha na ndege nyinginezo zinazosafiri njia hizo, kwa hivyo uokoa muda wa abiria na pia abiria wengi ufurahia huduma za ATCL wakiwa safarini.

  “Mbali na muda mfupi wa kusafiri, ndege hiyo imeboresha zaidi utendaji wa shirika kwa asilimia 98. Ujio wa ndege hii umerudisha imani miongoni mwa abiria wetu ambao sasa wanauhakika wa kusafiria kwa kufuata muda uliyopangwa,” alisema.

  Hivi karibuni shirika hilo la ndege la Air Tanzania lilizindua safari za kwenda katika mkoa wa Mbeya kwa kupitia uwanja mpya wa kimataifa wa ndege wa Songwe ikitumia ndege yake ya CRJ-200.

  Dakika 58 za safari kati ya Dar es Salaam na Mbeya, ambayo imepangwa kuwa siku nne kwa wiki; Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili, imepokelewa vizuri na abiria na wafanyabiashara wanaosafiri toka Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam.

  Taarifa za awali kutoka katika shirika hilo zilisema kuwa abiria sasa watafurahia safari za kila siku za kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, mara nne kwa wiki kwenda Mbeya na itakuwa inasafiri kwenda Comoro katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi.

  Shirika hilo pia limefuta adhabu zinazotozwa kwa abiria wanaoshindwa kusafiri na wale wanaobadilisha safari zao, ili kuwasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada pale wanapopatwa na dharura kabla ya kusafiri.
  “Hatuamini kabisa katika kuwaadhibu abiria wetu wapendwa,” alisema Kapt. Lazaro.

  Mkakati wa utanuzi wa shirika hilo la ndege la taifa ni pamoja na kufungua njia ya Tabora – Mpanda pamoja na kurejesha njia zake zote za zamani.
  Kwa sasa ATCL inasafiri katika maeneo 8 nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Mtwara, Mwanza, Tabora, Kigoma, Dar es Salaam, Mbeya, Bujumbura na Moroni nchini Comoro.

  0 0

  Wanachaso wakiwa katika picha ya pamoja
   Katibu Mwenezi wa Chaso Iringa, Michael Noel akizungumza kushoto kwake ni mwenyekiti wa chaso mkoa wa Iringa Thimotheo Mkanyia.
   baadhi ya viongozi wa chaso kutoka katika vyuo vikuu vilivyoko mkoa wa Iringa wakiwa katika ofisi za chama hicho.

  ========  ========  ========
  CHASO IRINGA WATOA TAMKO KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA

  Na Denis Mlowe.

  JUMUIYA ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Wanachadema Mkoa wa Iringa (CHASO) wamelaani vikali mwenendo mbovu wa Bunge Maalum la Katiba katika kuendesha na kujadili rasimu ya katiba tangu lilipoanza kwa kuendesha malumbano kila kwenye kikao na wakati mwingine wajumbe kuzomeana na kuacha kujadili mambo ya msingi yanayowagharimu Watanzania mamilioni ya Fedha.

  Wakitoa msimamo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Chaso zilizoko Tumaini katika kata ya Kihesa jana, Katibu Mwenezi wa Chaso Iringa, Michael Noel alisema bunge la katiba limepoteza imani kwa wananchi na wamekuwa wakilipwa posho kwa kodi zetu, wanataka watupatie katiba ya msimamo wa chama cha mapinduzi.

  Alisema kuwa chaso haiko tayari kuona mawazo ya wananchi katika rasimu ya katiba yanapotoshwa kwa misingi ya faida ya chama kimoja hivyo wako tayari kuandamana nchini nzima endapo ccm watapitisha katiba yenye msingi ya maslahi ya chama chao.

  Alifafanua kuwa wajumbe wa vyama vya siasa vya upinzani wamekuwa wakibaguliwa na wakati mwingine kutosikilizwa hoja zao hata kama za msingi kwa kuwa hawafungamani na chama cha mapinduzi.

  “ Hata wenyeviti wa kamati nyingi za bunge hilo ni wa ccm kitu kinachowasaidia kuchakachua kanuni ili kuwarahisishia kutekeleza dhamira yao ya kubadilisha vifungu vya rasimu hasa mfumo wa muungano ambao umependekezwa na tume kupitia maoni ya wananchi” alisema Noel

  Aliongeza kuwa kuna tuhuma za rushwa zinazosikika kila kukicha lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa wajumbe wanaotuhumiwa na tuhuma zote hizi ni dhidi ya wajumbe wa ccm wakiwamo mawaziri wa serikali na kuhoji wanafanya hivyo kwa dhamira ipi?

  Noel alisema wajumbe wa bunge hilo wanatakiwa kutambua kuwa waamuzi wa mwisho ni wananchi hivyo ccm isitumie hila kuwachagulia katiba waitakayo kwa maslahi ya chama hicho na kuongeza watahamasisha wananchi popote walipo waikatae kama rasimu hiyo itachakachuliwa na kubeba msimamo wa ccm uliotangazwa na katibu mwenezi Nape Nnauye.

  Alisisitiza kuwa maoni ya wananchi yazingatiwe na hawako tayari kuona chama tawala wakipuuza na kujiona wao wana hisa juu ya mfumo wanaoutaka.

  “Chama cha Mapinduzi kisijidanganye kuwa mchakato huu wakiuvuruga tutaendelea kuitumia katiba iliyopo iliyosababisha taifa makovu makubwa yanayoendelea kututafuna bali watasababisha taifa kuingia katika machafuko ambayo kama busara ikitumika tunaamini katiba mpya itapatikana kwa utulivu na amani.” Alisema Noel

  Alisema msimamo wa chaso kuunga mkono mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya katiba ambayo maoni yake yametolewa na wananchi walio wengi.

  Aidha Noel amesema wamesikitishwa na hotuba aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati akifungua bunge maalum kwa kuendeleza msimamo wa ccm kwa kutaka mawaziri watokane na wabunge.

  Akifafanua alisema hotuba ya Kikwete ni kupigiria msimamo wa ccm na kukejeli maoni ya wananchi ambao ndio waliomuweka madarakani kunaashiria usaliti mkubwa kwa wananchi walioamua namna mfumo mzuri wa kuendesha nchi.
   
  “Itambulike kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya CCM lakini Tanzania na maisha ya watu wake siyo mali ya CCM, hivyo kitendo cha kuwalazimisha wananchi juu ya hatima ya nchi yao kinachofanywa na CCM hakikubaliki. Kama tunataka katiba bora lazima ibebe maoni na matarajio ya wananchi na ndio maana tuanaza na maneno ‘Sisi wananchi’ na sasa kama CCM haikubaliani na maoni ya wananchi maana yake katiba ianze na maneno ‘Sisi CCM’ kitu ambacho hakikubaliki” alisema Noel

  Noel alisema kazi ya bunge maalum la katiba siyo kubadilisha bali ni kuboresha kwamba mambo gani yanapaswa kuingizwa ama kutolewa ndani ya mfumo wenyewe na kutolea mfano mambo ya muungano na yasiyo ya muungano na vyanzo vya mapato.


  0 0


  Kundi maarufu la muziki wa Kwaito la nchini Afrika kusini, Mafikizolo linatarajia kutua mchana huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya onesho moja tu linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City, kesho, Jumamosi Aprili 5 mwaka huu.

  Mafikizolo imekuwa na rekodi nzuri ya kushinda kwenye tuzo mbalimbali za muziki, kutokana na kupiga muziki na kucheza kwa umahiri, hasa mtindo wao maarufu wa Kwaito.

  Kundi hilo linaloundwa na wasanii wawili(Nhlanhla Nciza na Tebogo Madingoane pichani juu), kwa sasa linalotamba na vibao kama "Khona" na "Happiness", watawasili nchini kesho mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

  Akiongea na gazeti hili, mratibu wa onyesho hilo Vinny Magere kutoka kampuni ya Juegacassa, amesema Mafikizollo, wanatarajia kufanya onesho moja tu maalum na la kihistoria litakalodumu kwa muda wa saa nne.

  Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kundi hili kufika nchini, tangu kuachia wimbo wao wa "Khona", wimbo ambao umesababisha kundi hilo kujizolea umaarufu mkubwa kwenye kumbi za starehe, na hata katika vituo mbali mbali vya redio.

  Mafikizolo kwa sasa wanashikilia taji la kundi bora la mwaka, kwa mujibu wa tuzo za muziki za SAMA (South African Music Awards), huku wakiongozwa kwa kutajwa mara nyingi  kwenye tuzo za Ulaya kama kundi bora la muziki kutoka Afrika.

  Kundi hilo maarufu kuliko yote yaliyowahi kutokea kusini mwa Afrika liliwahi kutamba pia miaka ya nyuma na nyimbo kama "Ndihamba Nawe", "Ndixolele", "Sebenza", "Ndashata" na "Ndizolila".

  Onesho la hilo, linatarajiwa kuanza saa moja usiku ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 20,000 kwa watakaolipa kabla ya onyesho, huku mlangoni watalipia shilingi 35,000 za kitanzania.

  Kundi hilo mwaka huu, limeingia katika vipengele vinne kwenye kinyanga’anyiro kikubwa cha tuzo za SAMA.

  Katika kinyang’anyiro hicho chenye vipengele 28, kundi hilo limepata nafasi ya kuwania vipengele vinne, ambavyo ni Kolabo Bora ya Mwaka, albam Bora ya Pop ya Mwaka, albam ya Mwaka kupitia albam ya Reunited, na kundi  bora la Mwaka.

  Kwa mujibu wa tovuti ya destinyconnect, hafla ya ugawaji tuzo hizo itafanyika nchini humo Aprili 28 mwaka huu.

  Kundi hili lilianza shughuli za kimuziki tangu miaka ya 1990, albamu yao ya kwanza walitoa mwaka 1996. Tangu hapo wameshatoa albamu sita, baada ya kutoa albamu yao ya tano mwaka 2003 "Kwela". 

  Kundi lilianza kutetereka na baadaye mwaka 2013 waliungana tena na kutoa albamu ya sita iliyoitwa "Reunited" na kutoa singo yao ya kwanza "Khona" wimbo ambao umewatambulisha upya.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro.
  Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu(Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo
  ======  ====== =======
  Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya  shule yetu  imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo  ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika masomo ya sayansi  kwa shule ya  sekondari ya MOTAMBURU   iliyopo  Kata ya tarakea  wilaya ya  Rombo mkoani Kilimanjaro.

  Akizungumzia msaada huo  Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala   alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni  ikiwemo  vitabu vya kiada na ziada   kwa upande wa masomo ya sayansi  ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900 katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".

  "Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala

  Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo  ambaye ndio  alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi za makabidhiano hayo ,alipokea msaada wa vitabu  na kuukabidhi  kwa uongozi wa shule baada ya kukabidhiwa na meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini ambapo amewashukuru airtel kwa msaada huo ambao amesema  umekuja wakati muafaka  huku akiwakumbusha wadau wengine kuiga mfano wa Airtell Katika kuchangia maswala muhimu ndani ya sekta ya elimu hususani katika maeneo ya vijijini.

  Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya shule kwa mkuu wa wilaya  mkuu wa shule ya  sekondari MOTAMBURU Abel Masuki  ameishukuru airtel Tanzania kwa msaada huo ambao wamesema Airtel imeonyesha kuwa mfano mkubwa kwa makampuni mengi kwa kuungana na serikali kutekeleza sera  ya  elimu ya kuwaelimisha watanzania wengi  hasa walio  maskini kuwaondolea ujinga lakini pia akatoa changamoto ya vifaa vya maabara.


  0 0

   Jeneza likiwa na  mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maarumu.
  Waumini na viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati wakilishusha Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika ya Kusini kanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
  Wachungaji na makasisi wa Kaanisa la Anglican Dayosisi ya Kati wakiwa wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo.
    Waumini wa kanisa la Anglican wakiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu walipokuwa wakifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo kanda ya Dodoma  aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika ya Kusini.
   Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ibada maaumu ya kuuombea mwili liyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu Afrika ya Kusini.
   Ndani ya kanisa la Roho mtakatifu waumini wakifuatila ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita akiwa kwenye matibabu.
  Baadhi ya Viongozi wa Serekali wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Waumini wa kanisa hilo wakiwa ndani ya hema lilijengwa katika eneo la makaburi ya kuzikia viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati ambapo walikuwa wakiandaa sehemu ya kuuzikia mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo unaotarjiwa kuzikwa kesho Jumamosi.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

  0 0


  Kikosi cha TSN Boys
  TIMU ya soka ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika Kombe la NSSF kwa Vyombo vya Habari 2014.

  Mechi hiyo itakayochezwa saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani mshindi atasonga mbele katika hatua ya robo fainali zitakazoanza Jumatatu ijayo.

  TSN imetinga hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na wapinzani wao, Mlimani Media kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali. Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa mabao 9-0.

  Mwananchi ni mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi nyingine kesho ni kati ya Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande wa netiboli, itakuwa ni mechi za robo fainali kati ya Business Times dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wenyeji NSSF dhidi ya Tumaini Media.


  TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu"  ameahidi kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000.   "Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.  Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo. 


  Katika mechi za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo Leo walitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh Mohammed.

  Bao la Jambo Leo lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto ilisonga mbele baada ya kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya sare ya bao 1-1. Free Media na New Habari zilisonga mbele kama timu bora mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo mazuri (best looser).

  Katika netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari Zanzibar kwa kufungwa mabao 19-15, wakati IPP iliizamisha Global Publishers kwa
  mabao 27-8.

  0 0

   Msanii wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) akikumbatiana na Mmoja wa Mashabiki wa Filamu zake katika Eneo la Nyegezi Mwanza Jioni ya Leo wakati wasanii wa filamu Tanzania walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents litakaloanza kesho Mkoani Mwanza, Mahali ni Isamilo Lodge
  Baadhi ya Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakiwa wamekusanyika kwaajili ya kuwashuhudia wasanii wa filamu Tanzania waliofika katika Viwanja hivyo vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya Kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania litakaloanzia Jijini Mwanza.
   Kijana Mmoja wa Kike ambaye jina lake halikuweza kupatikana haraka akionyesha jinsi ya kushtua Kijoti joti wakati wasanii wa filamu Tanzania Walipofika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni ya leo
   Msanii wa Vichekesho Joti akimchagua mmoja wa wakazi wa Nyegezi Mwanza kwaajili ya Kupewa zawadi kutoka kwake
   Lulu akiongea na wakazi wa Nyegezi Mwanza wakati walipotembelea Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni ya Leo
   Baadhi ya wakazi wa Nyegezi wakinyoosha vidole kwaajili ya kuchaguliwa kujibu swali ambapo mshindi alijishindia Zawadi ya Kopi moja wapo ya Filamu ya Msanii Lulu
   Lulu akimkabidhi Zawadi ya Filamu yake ya Foolish Age kijana ambae alipatia kumtaja jina lake halisi wakati wasanii hao walipotembelea viwanja vya Nyegezi Mwanza 
   Picha ya Pamoja na Mshindi wa zawadi ya Filamu
   Msanii Rich Rich akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya Leo
   Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere ambe pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya leo wakati wasanii walipotembelea viwanja vya stendi ya nyegezi kwaajili ya Kutambulisha na kuwahamasisha vijana na wazee kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuonyesha Vipaji vyao Vya kuigiza katika Shindano la Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo linaanza rasmi Kesho jijini Mwanza mahali ni Isamilo Lodge
  Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakichungulia kwenye gari walilopanda wasanii wa kuigiza Tanzania ambao walifika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya kuhamasisha vijana kwa wazee kuweza kujitokeza kwa wingi Hapo Kesho katika Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo litafanyika Isamilo Lodge kuanzia Saa Moja asubuhi na Hakuna Kiingilio.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

older | 1 | .... | 263 | 264 | (Page 265) | 266 | 267 | .... | 1898 | newer