Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

ZANZIBALICIOUS KUWAKOMBOA WANAWAKE

$
0
0
DSC_0271
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe akisaini kitabu cha wageni cha Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious kwenye sherehe za uzinduzi wa Umoja huo zilizofanyika mwishoni mwa juma kwenye Hoteli ya Ocean View Beach Resort mjini Unguja.(Picha zote na Zainul Mzige).
=======  =======  ======
UMOJA wa Wanawake wa Zanzibarlicious umeamua kuwakomboa wanawake kutoka katika utumwa wa kiuchumi kwa kuwawezesha kwa kuwapa ujuzi na maarifa ili kujikwamua kwenye umasikini.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Umul-kulthum Ansel wakati wa uzinduzi wa umoja huo kwenye sherehe zilizofanyika mwishoni mwa juma katika Hoteli ya Ocean View Beach Resort mjini Unguja. Alisema lengo la kuwakwamua wanawake ni kutokana na kuonekana wao na watoto ni waathirika wakuu wa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ulimwenguni hasa katika bara la Afrika.

“Umoja huu umeundwa kwa lengo la kuwashajihisha,kuwahamasisha ,kuwaunganisha na kuwaendeleza wanawake kwa kuwapa ujuzi na maarifa ili waweze kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuleta maendeleo,”alisema.
DSC_0284
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya picha na kazi mbalimbali walizofanya kwa jamii mara baada ya kuwasili mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy).

Alisema malengo ya umoja huo ulioanzishwa mwaka 2011 na kusajiliwa mwaka jana ni kumuendeleza na kumuwezesha mwanamke kiuchumi,kijamii na kimwenendo.
Alisema umoja huo umekuwa ukitoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vya wanawake na kuwawezesha kubuni biashara ndogondogo na jinsi ya kuweza kutafuta mitaji kutoka taasisi mbalimbali za kitaifa. “Pia tunatoa ushauri nasaha kwa masuala ya familia, waathirika wa virusi vya Ukimwi na Dawa za Kulevya,”alieleza Mwenyekiti huyo.
DSC_0289
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe akitizama picha mbalimbali zinazoonyesha kazi walizofanya Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious kwa jamii inayowazunguka visiwani humo.

Vilevile Zanzibaliciuos inatoa ushauri wa kisheria katika masuala ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kuwakutanisha wanawake kutoka sehemu mbalimbali kupitia maonesho ya kibiashara na kwenye sherehe za kitaifa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwanaidi Salehe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema masuala ya wanawake yapo chini yake hivyo atahakikisha anawasaidia kwa kila namna.

Katibu Mkuu huyo ambaye alichangia Sh milioni moja kusaidia umoja huo alisisitiza kuwa “lazima tuzipiganie haki zetu wanawake, tuelimishane na tupendane na tuanze kwa watoto wetu wa kike tuwape mafunzo bora na kuwalinda wasijiingize kwenye vitendo viovu kama kuepuka dawa za Kulevya”.
DSC_0302
Wageni waalikwa wakiipokea meza kuu.
DSC_0311
Meza kuu katika nafasi yao kutoka kushoto ni Mkurugenzi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa FAWE, Bi. Khadija Ally Mohamed, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy), mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji, Bi. Fatma Gharib Bilal.
DSC_0318
Mshehereshaji kwenye uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Fauziat Abood.


DSC_0360
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy), akisoma risala yake mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0379
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe akitoa baraka zake kwenye uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious mjini Unguja.
DSC_0371
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson akiteta jambo na mjumbe wa Umoja huo Bi. Sheha Hilal.
DSC_0323
Pichani juu na chini Baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Zanzibalicious na wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mwenyekiti wa Umoja huo kwenye sherehe za uzinduzi wa kukata na shoka uliofanyika kwenye hoteli ya Ocean View Beach Resort mjini Unguja.
DSC_0327
DSC_0328
DSC_0393
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious mjini Unguja.
DSC_0002
Cake maalum katika kusheherekea uzinduzi wa Zanzibalicious Women Group.
DSC_0405
Mgeni rasmi Bi. Mwanaidi Salehe akikata cake maalum iliyoandaliwa kusindikiza uzinduzi wa Umoja huo.
DSC_0410
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy), akimlisha kipande cha cake mgeni rasmi kama ishara ya kumshukuru kwa kushiriki nao katika uzinduzi wa Umoja huo.
DSC_0417
Mgeni rasmi Bi. Mwanaidi Salehe akimlisha cake mdau wa masuala ya wanawake Bi. Mariam Abdallah.
DSC_0419
Mshehereshaji Bi. Fauziat Abood akianzisha mnada kwa wageni waalikwa kwa kuuza kipande cha cake kwa shilingi 10,000/= kwa ajili ya kuchangia Umoja huo ambao Wanawake wa Umoja huo wamekuwa wakijichangisha fedha kutoka mfukoni mwao kwa ajili ya kuisadia jamii hususan wanawake na waathirika wa Madawa ya Kulevya.
DSC_0434
Kina baba nao walihamasika kuunga mkono zoezi hilo ambapo walilishwa vipande vya cake na mgeni rasmi Bi. Mwanaidi Salehe.
DSC_0439
DSC_0442
DSC_0452
Mmoja wa wadhaminiwa sherehe hizo kutoka kampuni ya FAITH Tours and Safaris akilishwa kipande cha cake na mgeni rasmi.
DSC_0456
Burudani kutoka COCONUT BAND ambayo ndio habari ya mujini visiwani Unguja chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wake Bw. Raymond.
DSC_0485
Mshehereshaji Bi. Fauziat Abood akikteta jambo na mwimbaji taarab mkongwe Bi. Zuhura Shaabani.
DSC_0503
Mjumbe wa Umoja na Wanawake wa Zanzibalicious Sheha Hilal na Makamu mwenyekiti wa Umoja huo Evelyne Wilson wakimwaga manoti kwa mwimbaji mkongwe wa taarab mjini Unguja Bi. Zuhura Shaabani alipokuwa akitoa burudani kwa wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Umoja huo.
DSC_0588
Uliwaidia ule wasaa wa mahanjumaati yaliyoandaliwa na hoteli ya Ocean View Beach Resort kwa wageni waalikwa.
DSC_0565
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji Zanzibar, Bi. Fatma Gharib Bilal akiongoza meza kuu kupata Dinner kwenye sherehe za uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious.
DSC_0619
DSC_0618
Wageni waalikwa wakijisave msosi wa nguvu, chezea Unguja wewe kwa kukaangiza....!!!
DSC_0631
It's Dinner time... ndani ya hoteli ya Ocean View Beach Resort.
DSC_0641
Mshereshaji Bi. Fauziat Abood akiendesha harambee ya kutunisha mfuko wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicous kwa kunadi vitu mbalimbali kwa wageni waalikwa.
DSC_0660
Makamu Mwemyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson akizunguka kwenye meza za wageni waliohidhuria sherehe za uzinduzi wa umoja huo kunadi vitu mbalimbali.
DSC_0666
Mnada ukiendelea.
DSC_0672
Hili litamfaa mke wa wangu, zuri.....! Mambo ya LVD mjini Unguja....Baba akionekana kuvutiwa na pochi lililotengenezwa na kitenge wakati wa mnada.
DSC_0680
Madam Ummy nae akinadi T-shirt kwa mdau wa Fisherman Tours.
DSC_0691
Mr. Otembo aalinunua T-shirts hizo kwa Tshs 200,000/= katika kuchangia jitihada za Umoja huo kuwafikia jamii visiwani Unguja.
DSC_0464
Pichani juu na chini wageni waalikwa wakibadilishana mawazo na kufurahi wakati wa sherehe za uzinduzi wa Zanzibalicious Women Group.
DSC_0542
DSC_0535
Walipendezaje...!!
DSC_0540
DSC_0536
DSC_0529
DSC_0528
DSC_0723
Makamu mwenyekiti akitoa utambulisho wa Wanawake wanaounda Umoja wa Zanzibalicious kwa wageni waalikwa.
DSC_0790
Mgeni rasmi na meza kuu kwenye picha ya pamoja na Zanzibalicious Women Group.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI WAENDELEA KUKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
 Meneja Mauzo eneo la Moshi mjini Fredrick Chambega (kulia) akimkabidhi zawadi ya king’amuzi mmoja wa washindi wa wiki wa promosheni ya Winda Safari YA Brazili na Serengeti Pasian Shirima (kulia) katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Kilimanjaro, promosheni hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Orest Mmbaga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy tab mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti Elly Kisanga (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiani mkoani Kilimanjaro

MKOTYA ASHIRIKI KUZINDUA KATIBA YA CHA WATU WALIO NA MRIJO

$
0
0
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania Jumamosi, Khamis Mkotya, mwenye shati la Kitenge, akishiriki kikamilifu kuzindua Katiba ya Chama Cha Watu Mrijo wilayani Chemba, mkoani Dodoma, wanaoishi jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu wa Chama hicho, Yasin Kimwaga. 
 Khamis Mkotya katikati, wakati kushoto kwake ni Shaaban Ng’oka na kulia ni Katibu, Yassin Kimwaga.
Khamis Mkotya katikati akizungumza katika uzinduzi wa Katiba hiyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Chemba.
Tunahitaji maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kwa wale wanaoungana kama watu wa Mrijo. Ndivyo anavyoonekana kusema Khamis Mkotya alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa Katiba ya Chama cha Watu wa Mrijo Wilaya ya Chemba wanaoishi Dar es Salaam juzi, akiwa kama mgeni rasmi. Kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho, Shaaban Ng’oka na kulia ni Katibu, Yassin Kimwaga.

MAJANGILI 6 YAKAMATWA NA MENO YA TEMBO 53 YENYE JUMLA YA KILO 169.7

$
0
0
DSCF3201Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha juu ya kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7 na majangili sita
DSCF3202Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Sheluteteakifurahia jambo na wanahabari jijini Arusha
DSCF3199
DSCF3198Wanahabari wa vyombo mbalimbali wakifatilia jambo kutoka kwa Waziri wa maliasili na utalii

Na Pamela Mollel,Arusha
Wizara ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu pamoj na majangili sita katika wilaya ya manyoni mkoani singida
 
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo
 
Waziri Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu
 
Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana
 
Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasata wauwaji wa tembe 26,huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyama pori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama
 
Pia alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyama pori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo
Wizara ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu pamoj na majangili sita katika wilaya ya manyoni mkoani singida
 
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo
 
Waziri Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu
 
Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana
 
Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasata wauwaji wa tembe 26,huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyama pori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama
 
Pia alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyama pori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA TANZANIA, JIJINI DAR

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa Moja ya kitabu cha kuhifadhi kumbukumbu chenye picha ya Baba wa Rais Jakaya Kikwete, Mrisho Kikwete, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa baadhi ya vitabu na Ofisa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mture Educational Publishers Ltd, Bupe Mwasaga, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Mkutubi wa Jiji, Lusekelo Mwalugelo, Gazeti la Mambo Leo la Mwaka 1923 ambalo ni moja kati ya magazeti ya zamani, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo wakiisomea vitabu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.

 Baadhi ya wadau waliohudhuria sherehe hizo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunukia cheti Mama Kaunga kwa kutambua mchango wa, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.

10:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Katalogi ya Kieletriniki, wakati wa  sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Picha ya pamoja na Wadau waliotunukiwa vyeti.

kibonzo cha Nathan Mpangala

Jumuiya ya Watanzania nchini Malaysia yapata Uongozi wao

$
0
0
Jumamosi ya tarehe 29 March 2014, watanzania waishio na wasomao Malaysia walikutana katika Ubalozi wa Tanzania na kuunda Jumuiya mpya ya Watanzania wanaoishi South East Asia.

Uongozi wa Wana Jumuiya hiyo ambao kwa kuanzia ni Watanzania waliopo Malaysia wakiwa na Balozi Mpya wa Tanzania,Dr. Aziz Ponary Mlima (katikati) na maafisa wa Ubalozi. Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Katibu Mkuu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Elimu, Waziri wa Jamiii, Utamaduni na Starehe ikiwa pamoja na Wadhamini wawili.

Picha nyingine ni Watanzania wote kwa pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Malaysia.

Jumuiya hiyo ilianzishwa Mwishoni mwa wiki,ambayo inajulikana kama " Tanzanian Diaspora in South East Asia" ambayo itakuwa inawashirikisha Watanzania wote katika nchi za Malaysia, Indonesia, Thailand, Philippines, Brunei, Laos na Cambodia.

Picha zaidi zinaweza kuonekana kwenye Ukurasa wa Facebook


Watanzania kutoka maeneo hayo wanaombwa kujiunga ili tuweze kutambuana na itakapokuwa lazima kusaidiana.

Kwa niaba ya Tanzanian Diaspora South East Asia.

SERIKALI YAWAPONGEZA WADAU WA SANAA ZA MONYESHO

$
0
0
Na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM

Serikali imewapongeza wahisani wa maendeleo kwa kufadhili na kukuza sanaa ambao wamekuwa wachangiaji muhimu wa kuendeleza na kukuza uchumi na kupunguza umasikini miongoni mwa wasanii na Taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga alipokuwa akizindua programu ya “kujenga fursa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho iliyoratibiwa na asasi isiyo ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la Nafasi Arts space hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Sihaba amesema kuwa kuanzishwa kwa dhana ya Programu hii kunatoa fursa ya kujipatia kipato na kuongeza ujuzi ambao utapanua wigo wa ubunifu kwa wasanii na kuongeza mahusiano baina yao na wasanii wengine, ikiwemo kupanua soko la bidhaa zao.

“Nachukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza kwa dhati Nafasi Art Space kwa uamuzi huu mahususi mlioufanya wa kuratibu uanzishwaji wa Programu ya kuibua fursa kwa wasanii wa Sanaa za Maonyesho Tanzania.” Alisema Bi. Sihaba

Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sanaa imekuwa ikifanya juhudi za kutosha kuinua viwango vya sanaa nchini kwa kuanzisha programu za kitaifa na kimataifa.

Aidha Bi. Sihaba alisema kuwa programu kama hizi zitasaidia kubadilishana habari, ujuzi, mikakati na ubunifu  miongoni mwa wasanii kitaifa na kimataifa.
 

Airtel yasaidia Afya ya Uzazi kupitia kampeni ya Wazazi Nipendeni

$
0
0
 Airtel Tanzania imetangaza kuendelea kushirikiana na M-Heath Tanzania katika Kampeni ya Wazazi nipendeni baada ya kuwa na ushirikiano wa mwaka mmoja wenye mafanikio  makubwa  katika  kuwasaidia kina mama wajawazito na watoto wachanga
Akiongea kuhusu mpango huo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema”  katika kutambua umuhimu na changamoto zinazoikumba sekta ya Afya ya uzazi, Airtel tumeonelea ni vyema tukashirikia na wenzetu wa M- Health katika kuwawezesha kina mama wajawazito kupata takarifa za afya ya uzazi kirahisi. Katika mwaka wa kwanza wa ushirikiano huu program hii imeweza kufanya vizuri kiasi cha kuchaguliwa kuwa huduma bora ya mobile heath katika kategori namba 1 ya Tuzo za Connected Life zinazotolewa na Global mobile Awards kila mwaka
Aliongeza kwa kusema wanawake nchini Tanzania wapo katika hatari ya vifo vya uzazi kwa uwiano wa 38:1 yaani kati ya wanawake 38 basi yuko  1 katika hiyo hatari na kila mwaka Tanzania inakumbwa na  vifo vya watoto wachanga vyenye idadi ya kiasi cha watoto 48,100 ikiwa ni ya 10 kwa ukubwa duniani. Huduma ya ujumbe mfupi wa simu inawapatia watanzania , kina mama wajawazito na wamama wenye watoto wachanga hadi umri wa wiki 16 taarifa za afya kwa lugha ya Kiswahili bure yaani bila makato yoyote.
Airtel tunaahidi kuendelea kusaidia kampaini hii kwa kuendelea kuwawezesha wateja wetu waweze kupata huduma hii bure wakati wote na kuhakikisha tunachangia kikamilifu katika kutoa elimu na hatimae kusaidia kuboresha afya ya uzazi nchini.
Akiongea kwa niaba ya M- Health Tanzaania Mkurugenzi wa Mradi Janita Ferentinos alisema” tunapenda kuwashukuru sana Airtel kwa msaada wao mkubwa katika kuiwezesha kampaini hii kufanya vizuri. Ushirikiano wetu umetuwezesha kuwafikia watu wengi  waliojiandikisha.  Kwa watanzania wengi wanatumia huduma ya ujumbe mfupi zaidi , kwa kuondoa gharama na kufanya bure kumewezesha zaidi ya watanzania milioni 8 Tanzania kuweza kupata taarifa za msingi za afya ambazo zinaokoa maisha yao. Na ushirikiano huu umekuwa wa mafanikio kiasi cha mradi huu wa wazazi nipendeni kupewa Tuzo kama moja kati ya mpango bora wa M- Health duniani.

MKUU wa Mkoa wa Geita azindua mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA)

$
0
0
 1.       Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula akifungua mkutano wa wadau mkoani Geita unatakaojadili mchakato wa uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA).

  Katibu Tawala wa Mkoa  Severine Kahitwa akieleza umuhimu wa kuwa na utaratibu wa TIKA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.

Wadau wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo.

Sehemu ya wadau wakisikiliza maagizo kutoka kwa mgeni rasmi ya namna ya kujadiliana katika mkutano huo.

  Mkutano huo pia haukuwanyima fursa ya kuelewa kinachozungumzwa ndani ya kikao hicho walemavu wa kusikia, mbele ni mkalimani wa walemavu hao John Mukube.

  Mkuu wa Mkoa Magalula Said Magalula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya kundi maalum ambalo nalo limeshiriki mkutano huo.

 Wadau wakiwa makini kusikiliza mada zilizowasilishwa kwa ajili ya uanzishwaji wa TIKA mjini Geita.

 Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimshukuru mgeni rasmi kwa hotuba nzuri.



MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APANDA MTI KUADHIMISHA SIKU YA KUPANDA MITI KITAIFA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akipanda mti wa Mwembe nje ya Ofisi yake mpya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya kupanda miti.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wakati akizungumza nao.Picha na OMR 

Mwelekeo wa Kimbunga cha “HELLEN” na hali ya Mvua

Exim Bank increases its footprints in Comoros

$
0
0
 The press and other attendees witnessing the launch of Exim Bank Tanzania branch in Domoni (Anjouan) at the weekend. The bank’s fourth branch to be opened in Comoros Islands. (Photo by our correspondent)
Governor of Anjouan Mr. Anissi Chamsidine (standing) who was the guest of honour speaks during the launch of Exim Bank Tanzania branch in Domoni (Anjouan) at the weekend. Sitting from right is Ganesh Kumar, Country-Head-Exim Bank Comoros, Mr. Ahmed Jaffer, Chief of Staff, Anjouan Island and Mr. Nassim Alloui Houmadi, Head of Council of Ministers. It was the bank’s fourth branch to be opened in Comoros Islands. (Photo by our correspondent)

=========  =========  ==========
By Correspondent, Comoros. 

EXIM Bank Tanzania has continued to widen its reach to customers abroad by opening its 4th branch in Domoni (Anjouan), a move that aimed at taking the bank’s services closer to its customers in Comoros Islands.  

Speaking during the inauguration ceremony in Domoni at the weekend, the guest of honour, Governor of Anjouan Mr. Anissi Chamsidine, congratulated Exim Bank’s effort to bringing its innovative services closer to the people of Domoni and reaching the unbanked communities. 

“I would like to applaud Exim Bank for its efforts to bringing its banking services closer to the people of Domoni. The bank’s customer-friendly approach and innovation in the services offered have been remarkable and should be an example for other banks to emulate,” said Governor Anissi.

He said the creation of the Domoni Branch, will allow the Exim Bank in Comoros to possess a financial services platform closer to its market and clients in the country as a whole.

Governor Anissi reiterated that the branch would enable the entire population of Domoni to access quality banking facilities, which include inward and outward remittances and access to credits at reasonable rates.

“With this branch, it means the services have been brought closer to the people of Domoni, this will be the opportunity for them to access quality services the bank offers. I would like to urge Domoni people to use this opportunity by opening-up accounts with the bank which will ensure safety of their money and they will also enjoy other services offered by the bank,” he added. 

On his part, the bank’s Country Head, Mr. Ganesh Kumar said that Exim Bank would soon be expanding its reach to the people of Comores, by opening satellite offices, extension counters and will install more ATMs and point of sales machines  in various places.

He said that, Exim Bank is also committed to bring in the best of technology to the benefit of the Comorian people and stated that, Exim Bank would roll out new technology products in the near future. 


Exim bank opened the first branch in the Island at Moroni in 2007, with branches being followed in Mitsamudu (Anjouan) and Moheli, covering all the islands of the Archipelago.

NI SHIDAAAA...!

Msama Promotions kuwapiga msasa waimbaji watakaoshiriki tamasha la pasaka

$
0
0
 KAMPUNI ya Msama Promotions ambayo ndio waandaaji wa Tamasha la Pasaka, hivi karibuni  wanatarajia kuandaa semina kwa ajili ya waimbaji walioteuliwa kuimba katika tamasha hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Bwa.Alex Msama alisema kuwa semina hii ni kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye tamasha la KrismasI lilofanyika mwaka jana katika mikoa kadhaa hapa nchini.

“Lengo la semina hii ni kuboresha Tamasha la Pasaka ili tamasha lijalo makosa yaliyofanyika yasijirudie na tamasha la mwaka huu litakuwa la kihistoria kuliko matamasha yote yaliyopita,” alisema Mang’era.
Mang’era alisema katika semina hiyo kabla ya tamasha la Pasaka, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) litahusika katika utoaji wa elimu hiyo sambamba na kampuni waandaaji wa Tamasha.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tamasha la Pasaka mwaka huu litakuwa ‘live’ kwa Dar es Salaam na pia kutakuwa na ushindani kati ya waimbaji wa Tanzania na waimbaji wa nchi za nje, lengo likiwa ni kujifunza jinsi wenzao wanvyofanya kazi zao za muziki  wa Injili.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA YAKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA BARABARA WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ali Mohammed Kessy,walipokuwa wakitembea kwa miguu kufuatia msafara huo kukumbana na changamoto ya barabara mapema jana jioni katikati ya Msitu wa hifadhi ya wilaya ya Nkasi.Ndugu Kinana na Msafara wake ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha Mwampemba kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 100,lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12 kwenda na kurudi kutokana na ubovu wa barabara.Ndugu Kinana yuko Mkoani Rukwa,Katavi na Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha CCM,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero mbalimbali za wananchi
 Ndugu Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara wake uweze kuendelea na safari.
 Sehemu korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao uweze kupita,lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
 Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanahabari aliokuwa ameambatana nao kwenye msafara wake,baada ya magari kunasa kutokana tatizo la barabara
 Wanahabari waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakiwa hoi kabisa,wakisubiri kudra za Mwenyezi Mungu,msafara wa magari yao yanasuliwe na kuendelea na safari.Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu,Ndugu Kinana.
 Hali ilikuwa tete mnoo,kipande cha kilometa mia kinapitika kwa zaidi ya masaa sita,kutoka kijiji kimoja kwenda kingine.
 Ilikuwa ni shughuli nzito katika msafara wa Ndugu Kinana,barabara ni mbovu kupita maelezo
 Kila mmoja akipumua kivyake,baada ya kuvuka salama sehemu korofi ya barabara.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (alinaerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa mawe,ili msafara uweze kupita
 Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi ya barabara kwa miguu,huku madera wakipiga hesabu zao namna ya kupita.
Mchuma ukipita sehemu korofi ya barabara kwa mbinde.

TBL YAIBUKA MSHINDI WA PILI TUZO ZA MZALISHAJI BORA WA MWAKA 2013

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi kombe  kwa mshindi wa pili wa tuzo wa mzalishaji bora wa mwaka 2013, kwa  Mkurugenzi wa Huduma ya Makampuni na Masuala ya Sheria wa kampuni ya Bia ya TBL, Stephen  Kilindo wakati wa hafla ya makabidhiano ya tuzo hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia)  wakati wa kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa  makampuni ya IPP ambayo ilikuwa mdhamini mkuu wa hafla hiyo.
Rais  Jakaya Kikwete akipiga picha na Watendaji Wakuu wa kampuni ya Bia TBL mara baada ya kuwakanidhi tuzo ya  mzalishaji bora wa mwaka 2013 inayotolewa na CTI.
 Watendaji wakuu wa TBL wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mzalishaji bora wa mwaka 2013 inayotolewa na CTI.

CALL FOR PROPOSALS.

$
0
0
Tanzania Financial Services for Underserved Settlements (TAFSUS) is a Local Finance Facility which provides credit enhancement to Community Driven Settlement Upgrading Projects in the form of Guarantee or bridge finance. 

TAFSUS is a not-for-profit organization registered on 27th January 2009 with registration No 69478 as a Company limited by guarantee, located within TAWLAT offices, NIC Life House, 5th Floor at the Sokoine Drive/Ohio Avenue.

The Objectives of TAFSUS are:
·         To bring together key players involved in cities and national level settlement upgrading strategies to address the challenge of financing;
·         To catalyze the integration of commercial finance into settlement upgrading;
·         To provide mechanisms to blend different forms of funding to maximize affordability for the poor;
·         To provide a financial mechanism to support the implementation of city-based settlement upgrading strategies; and
·         To advocate for sound policies, enforcement of laws and proactive planning to prevent further growth/generation of unplanned areas.
TAFSUS is looking at supporting community initiatives through development of Bankable projects to access funds from commercial financial institutions with leverage of community contribution and Government subsidy. TAFSUS also offers technical support for developing and upgrading projects which include low cost housing, accesses to portable water and titling of properties in informal settlements.

TAFSUS has currently entered into Agreement with Azania Bank Limited to provide Credit Guarantee Facility to finance upgrading of unplanned settlements.

TAFSUS  now invites Associations, NGOs, Registered Communities or Groups to submit brief Concept Notes of maximum of 3 pages indicating name of organisation, nature of project, location, problem to be solved, beneficiaries, estimation of revenue and expenditures, Project costs and any other aspects that they feel should be known to enhance the acceptability of the project (Technical and Financial).

Budget Limit
The value of the Project per applying Organization, Group, community or individual differs depending on type of Project according to the guideline below:
Ø  Access to improved water supply; TZs. 30-100 Million per Project
Ø  Access to improved sanitation; TZs. 30-100 Million per Project
Ø  Housing Improvement; TZs. 1,000,000-5,800,000 per individual
Ø  Formalization of ownership; TZs. 500,000-4,800,000 per individual
Submission of the Concept Note

Mode of submission should be in hard copy and soft copy to;
TAFSUS Manager,
Tanzania Financial Services for Underserved Settlements,
P O Box 79603
Dar es Salaam- Tanzania

Tel No.  +255 222120285


KINANA ATEMBELEA WANANCHI PEMBEZONI MWA WILAYA YA NKASI, AKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA UBOVU WA BARABARA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwafurahia vijana aliowakuta wakifanya kazi katika kijiji cha Wampembe kilichopo kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi. Vijana hao wanafanyakazi katika sekta ya afya na ujenzi.Pichani kulia ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka,Injinia wa maji wilaya ya Nkasi,Bwa.Simon Sadala,Fundi Mkuu Ujenzi,Bwa.Athanael Rwamlema na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nkasi,Bwa.Kimulika Galikunga.
Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa akipata maalezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho cha afya kuyoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka.Kituo hicho kimejengwa kwa msaada mkubwa wa Africare kwa kushirikiana na Plan International,ambacho ni maalum kwa ajili ya afya mama na watoto na upasuaji
Sehemu ya jengo la kituo cha Afya kikiendelea na ujenzi katika kijiji cha Mwampembe,wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo.
Pichani Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Wampembe, jana,Aprili Mosi, 2014. Na zinazoendelea ni picha zaidi za ziara hiyo na changamoto hizo alizokumbana nazo kama zilizvyopigwa na Bashir Nkoromo aliyeko kwenye ziara hiyo. 

Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana jana, aliendelea na ziara yake katika mkoa wa Rukwa, kwa kutembelea wananchi walioko pembezoni mwa mkoa huo, ambapo alifika hadi katika Kata ya Wampembe iliyopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilaya ya Nkasi iliyomo kata hiyo.

 Katika safari iliyomchukua zaidi ya saa tisa, Kinana na msafara wake alikumbana na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara kutoka Namanyere hadi kwenye vijiji vya kata hiyo kutona na magari kunasa mara kwa mara kwenye tope na makorongo,kwa kuwa barabara haijapata kufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu.

 Kufuatia kujionea changamoto hiyo, Kinana amewambia wananchi wa vijiji vya Wampembe na Ntemba, kuwa ataishauri serikali kuifanya barabara hiyo iwe chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) badala ya sasa ambapo ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na hivyo kuwa vigumu kupatikana fedha za kutosha kujenga barabara hiyo. 
Kinana akizungumza na wananchi saa mbili usiku, baada ya kuzuia msafara wake eneo la  kijiji cha Ntemba kaya ya Kate akitoka Kata ya Wampemba kwenda Sumbawanga mjini.

CCM ITASHINDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 94 UCHAGUZI CHALINZE

$
0
0
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images