Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

TAZAMA TUKIO LA RISASI ZA MOTO NA MABOMU HUKO NZEGA,DKT KIGWANGALA ALIVYOKAMATWA NA WACHIMBAJI WADOGO WA NZEGA WALIVYOTAWANYWA NA POLISI

$
0
0
Hivi ndivyo Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dkt Hamis Kiwangala(mwenye shati jeupe) alivyokamatwa wakati wa maandamano ya wachimbaji wadogo machimbo ya Mwashina wilayani Nzega mkoani Tabora,huku wananchi wakikimbia hovyo kwani polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya.
Polisi wakikabiliana na wachimbaji wadogo wa madini wilayaniNzega

Pichani ni mmoja kati ya waandamanaji hao aliyekuwa karibu na Dkt Kigwangala akiwa chini baada ya kujeruhiwa na polisi
Mlipuko wa mabomu kwa mbali

Awali mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kigwangala akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini  hao katika kijiji cha Nzega Ndogo kabla ya maandamano
Maandamano baada ya mkutano wa Dkt Kigwangala kuelekea eneo la machimbo ya Mwashina wilayani NZega.

Jeshi  la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora  jana limemkamata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt. Hamis Kigwangalla aliyekuwa kwenye maandamano ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ya kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited.


Kabla ya hapo mbunge huyo alifanya mkutano mkubwa wa hadhara na wachimbaji hao katika kijiji cha Nzega Ndogo wilayani humo ambapo alielezwa matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na kamishna wa madini nchini Bw. Paulo masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao wadogo kwenye eneo hilo.

Katika mkutano huo wachimbaji hao walidai ni vema serikali iangalie haki zao zilizotumika kwenye uendeshaji na uchimbaji wa mashimo hayo kuliko kuwafungia bila kujali ingawa eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa Resolute  lakini wao ndiyo wamiliki wa ardhi hiyo.

Hata hivyo katika hoja hiyo mbunge huyo aliwataka wachimbaji hao kudai haki yao kwa kufuata taratibu zinazostahili bila kujali tofauti zao kisiasa, kikabila na kidini na badala yake wawe kitu kimoja.

Baada ya kauli hiyo mbunge huyo aliwaambia wachimbaji hao wadogo kuwa haki yao iko mikononi mwao hivyo ni uamuzi wao wa kudai haki yao na yeye kama mwakilishi wao yuko nyuma yao mpaka pale haki yao itakapopatikana.

Wachimbaji hao walimwomba mbunge huyo kuambatana nao kwenye maandamano ya amani kutoka kijiji cha Nzega Ndogo kwenda Mwashina yalipo machimbo yaliyofukiwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu kujionea hali halisi ya kufukiwa kwa eneo hilo na ikiwezekana kufanya mkutano mwingine wa hadhara kijijini hapo.

Kufuata hali hiyo wachimbaji hao walianza maandamano ambayo yaliungwa mkono na mbunge huyo hadi kijiji cha Mkwajuni kabla ya kufika Mwashina ambapo polisi waliibuka na kuyasambaratisha maandamano hayo kwa mabomu ya machozi na risasi za moto.

Katika  na purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.

Awali askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.

Kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda alipopigiwa simu na waandishi wa habari alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na maandamano hayo, kukamatwa kwa mbunge huyo wa jimbo la Nzega na kutumika kwa risasi za moto na mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo.

Tayari Dkt Kigwangala ametoka polisi usiku wa kumkia leo

 Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora

walichokisema Mh.Stephen Wasira na Mh. Asha Mtwangi Juu ya Hotuba ya Rais.

REBECCA MALOPE KUWAINUA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0
BAADA ya kuweka historia  katika Tamasha la Pasaka la mwaka 2012, malkia wa muziki wa injili wa Afrika Kusini, Rebecca Malope anatarajia kuuinua umati wa mashabiki wa muziki huo, jijini la Mwanza Aprili 4 mwaka huu.

Nguli huyo wa Injili anayekubalika Afrika na bara la Ulaya anatarajia mwaka huu kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka katika mkoa huo ambapo kamati ya maaandalizi imeshakamilisha taratibu zote za kumleta mwimbaji huyo. Kurejea mara ya pili  katika tamasha hilo inaonesha jinsi anavyokubalika, Malope ambaye alianza muziki wa injili akiwa na umri wa miaka 18, kipaji chake cha uimbaji kimekubalika Tanzania na yeye kuipenda nchi hii na kuja kuwapa raha ya neno la Mungu kupitia nyimbo zake.

Imezoeleka kuwa waimbaji kutoka nchi hiyo, wamekuwa waakiishia katika jiji la Dar es Salaam, ambapo kamati ya maandalizi inayoongozwa na mwenyekiti wake, Alex Msama iliona umuhimu wa waimbaji kutoka nje kufika katika mikoa mingine ambako wameanza na mkoa wa Mwanza ambao Malope anatarajia kufanya mambo makubwa.
Ni nafasi ya pekee kwa wakazi wa jiji la Mwanza ya kupata fursa ya kusikiliza neno la mungu kupitia nyimbo za mwimbaji huyo nguli, hivyo wajitokeze kwa wingi kupata jumbe nzuri za neno la Mungu kupitia kwa Malope na waimbaji wengine kutoka sehemu mbalimbali.

Rebecca Malope ambaye ni kipenzi cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na rais wa sasa Jacob Zuma, amepitia tabu na changamoto nyingi katika maisha yake na amekuwa mwimbaji wa kimataifa na amefanikiwa kufanya maonyesho takribani nchi nyingi za Ulaya na Afrika kwa ujumla. Historia ya Rebecca Malope Mwimbaji huyo mkongwe alizaliwa 1968 katika kijiji cha Lekazi karibu na mji wa Nelsprut, Mpumalanga nchini Afrika kusini. 

Historia ya mwimbaji huyu nguli wa muziki wa injili ambayo si nzuri kimaisha ambapo Malope hakuendelea katika elimu na ni mambo machache yanayofahamika kuhusiana na enzi za utoto wake.  Akiwa na umri mdogo Malope alipata ugonjwa uliopelekea kutoweza kutembea na madaktari walidhani asingeweza kutembea tena katika maisha yake.  Familia yake ilikuwa masikini kwa kiasi kikubwa na ndipo yeye na dada yake Cynthia waliamua kukimbilia katika jiji la Johannesburg kitongoji cha Evaton kwa ajili ya kutafuta kazi kwa ajili ya kujikimu na maisha. 

Mwaka 1986 Malope akiwa na miaka 21 alishiriki kwenye mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji yaliyojulikana kama ‘Shell Road to Fame’ lakini hakufanikiwa kufika mbali.  Malope hakukata tamaa ndipo mwaka uliofuata alishiriki tena na kuibuka mshindi na wimbo wa ‘Shine on’ ushindi huo ulimsogeza mbali zaidi kimuziki na ndipo alipokutanishwa na muandaaji mashuhuri Sizwe Zako na akapata meneja wake wa kwanza akijulikana kwa jina la Peter Tladi.  Albamu yake ya kwanza ilikuwa na nyimbo za kidunia, albamu hiyo ambayo haikufanya vizuri sokoni na ndipo alipoamua kujiingiza moja kwa moja kwenye muziki wa injili. .

Alipata ushirikiano mkubwa kutoka redio mbalimbali kwa nyimbo zake za injili kitu ambacho hakikuwa kawaida Afrika Kusini.  Mwaka 1990 Rebecca alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike wa Afrika Kusini na mwaka 1993 ilikadiriwa watu zaidi ya milioni moja walimpigia kura kama mwanamuziki bora wa kike kwenye Coca Cola Full Blast Music Award Music Show na alishinda kwa mwaka huo na 1994 pia. Kwenye mauzo, Album zake zote kumi za kwanza ziliingia kwenye hadhi ya dhahabu. 

Katika kipindi chote nakala zaidi ya milioni 2 zilikuwa zimeshauzwa sokoni. Mwaka 1995 kwenye CD yake ya ‘Shwele Baba’ nakala zaidi ya milioni moja ziliuzwa ndani ya wiki tatu toka uzinduzi wake na hii iliweka rekodi ya aina yake katika historia ya soko la muziki Afrika Kusini. Mwaka 1996 haukuwa mwaka mzuri kwa Rebecca kwani alimpoteza baba yake mzazi, kaka yake na dada yake. Wote walifariki katika mazingira ya kutatanisha wakifuatana. 

Lakini hili halikumfanya Rebecca kukata tamaa na kuacha huduma bali alisonga mbele na kazi hiyo akijipa moyo na kuamini ni mpango kutoka kwa Mungu mwenyewe na hataacha kumtumikia.  Rebecca anasema siri ya mafanikio yake ni kujituma, kuwa na malengo na kufanya kazi kwa bidii akimshirikisha Mungu hayo ndiyo yaliyomfanya kutawazwa Malkia wa muziki wa injili Afrika huku wengi wakimfananisha na marehemu Brenda Fassie.  

 Kati ya mwaka 1995 na 2004 Rebecca amezunguka ulimwenguni akiwa na bendi ya Pure Magic akimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.  Mwaka 2003 Malope alitunukiwa udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Natal kwa mchango wake mkubwa kwa jamii na muziki nchini Afrika kusini na Desemba mwaka huo huo alishinda tuzo ya Kora kwa upande wa mwanamuziki bora wa Injili. 

Licha ya kuwa mwimbaji Mwaka 2004 Malope alianzisha kipindi chake katika luninga kikiitwa ‘Gospel time’ ambacho kinafanya vizuri hadi sasa.  Februari 25 mwaka jana  Malope alirekodi nyimbo za ‘live’ katika jiji la Pretoria hiyo ikiwa ni albamu ya 32. Baadhi ya Tuzo ambazo Dkt. Rebecca Malope amewahi kutunikiwa ni 1994 mwimbaji bora, 1997 albamu bora sokoni iliyoitwa ‘Uzube Nam’, 1998 muimbaji bora wa nyimbo za injili Afrika na albamu bora katika mauzo iliyoitwa ‘Angingedwa’. 

Nyingine ni 1999 muimbaji bora wa kike na muimbaji bora wa injili Afrika kupitia albamu ya ‘Somlandela’, 2002 msanii bora wa nyimbo za injili akishinda na wimbo wa ‘Sabel Uyabizwa’, 2003 msanii bora Afrika kupitia wimbo wake wa ‘Iyahamba Lenqola’ na 2004 msanii bora wa mwaka kwa wimbo wa ‘Hlala Nami’. 

NAIBU WAZIRI JANETH MBENE AFUNGUA MAFUNZO YA WADADISI WA ZOEZI LA SENSA YA VIWANDA

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu Sensa ya Viwanda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani Morogoro.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Eliya Ntandu akizungumza kwa niaba ya Makatibu Tawala wa mikoa yote nchini wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu Sensa ya Viwanda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene akiwahutubia wadadisi na wasimamizi kabla ya kufungua rasmi mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
 Baadhi ya wadadisi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani Morogoro.


======  ======  ======

NAIBU WAZIRI JANETH MBENE AFUNGUA MAFUNZO YA WADADISI WA ZOEZI LA SENSA YA VIWANDA
Na Veronica Kazimoto
Morogoro.

Wamiliki wa viwanda nchini wameagizwa kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa kutosha wakati wadadisi watakapofika katika ofisi zao kuwahoji kwa ajili ya kupata takwimu za viwanda vyao. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi na wasimamisi wa zoezi la Sensa ya Viwanda iliyofanyika leo mkoani Mororgoro, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (Mb) amesema ni muhimu wamiliki wa viwanda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi kwa kuwa takwimu zitakazopatikana kutokana na Sensa hiyo zitatumika katika kupanga shughuli mbalimbali za maendeleo.  

“Nichukue Fursa hii kuwaagiza wenye viwanda wote nchini kuona kuwa zoezi hili ni lao na ni jukumu lao kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na pia waone kuwa zoezi hili ni kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla.” Amesema Naibu Waziri Mbene.

Naibu Waziri Mbene amefafanua kuwa, zoezi hili la Sensa ya Viwanda lisichukuliwe kama njia ya Serikali kutaka kujua mapato au faida wanayopata wenye viwanda kwa lengo la kukusanya kodi bali ni kuisaidia Serikali kubaini mabadiliko ya muundo wa sekta ya viwanda, mchango wake kwenye pato la taifa na hatimaye kufanya maamuzi sahihi ya kisera.

Aidha ametoa wito kwa wadadisi wote wanaoshiriki katika mafunzo ya Sensa ya Viwanda kufuatilia na kuzingatia kwa makini mafunzo yote yatakayotolewa na wakufunzi ili lengo la kupata takwimu sahihi za viwanda liweze kufanikiwa. Awali akitoa maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa  amesema takwimu zitakazokusanywa katika Sensa hiyo zitahusu viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Dkt. Chuwa amefafanua kuwa katika sensa hiyo baadhi ya taarifa zitakazokusanywa ni pamoja na anuani na mahali viwanda vilipo, aina ya umiliki, utaifa wa mmiliki, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa zinazozalishwa na idadi ya wafanyakazi.

Taarifa nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaji, gharama za uzalishaji na mapato mangineyo. Mafunzo ya zoezi la Sensa ya Viwanda yamelenga vijana wapatao 175 ambao watafanya kazi ya kukusanya takwimu zinazohusu sekta ya viwanda hapa nchini kwa muda wa miezi miwili kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2014.  

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, SAAZ SULULA, AKAGUA MIRADI YA HIFADHI YA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA

$
0
0
Safari ya msafara wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula mwishoni mwa juma katika kukagua miradi inayofadhiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na wahisani wengine katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa haikuwa rahisi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya barabara kutokana na mvua kubwa kunyesha na hivyo kupelekea magari ya mizigo inayokwenda nchi jirani za Burundi na DRC kupitia bandari ya kasanga kukwama na kuziba njia. Juhudi za ziada kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mkandarasi anaejenga barabara hiyo ya Sumbawanga - Kasanga kwa kiwango cha lami zilisaidia katika kuhakikisha magari yote yaliyokwama pamoja na msafara wa katibu Mkuu yanavuka salama.   
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia)Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula akizungumza na mhudumu wa afya katika wadi ya wazazi Samazi juu ya huduma na mahitaji ya kituo hicho kipya ambacho kinategemewa kuanza kazi siku za hivi karibuni.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake wakikagua vitanda kwa ajili ya wanafunzi pamoja na daharia katika shule ya  Sekondari Kasanga  Mkoani Rukwa. Mradi huo wa daharia (bweni) ni kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika Shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula katika Wilaya yake kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la samaki la Kirando linalofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa Ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuonyesha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula (wa pili kushoto) sehemu inapojengwa gati kwa ajili ya kushushia samaki na abiria katika soko hilo pamoja na eneo linalojengwa kwa ajili ya kukaushia samaki wabichi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake katika kukagua ujenzi wa miundombinu inayoendelea kujengwa katika soko la samaki la Kirando Wilayani Nkasi Mkaoni Rukwa mwishoni mwa juma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula akitoa baadhi ya maelekezo kwa mkandarasi wa Soko la Samaki la Kirando ambae pia anajenga Gati linaloonekana kwa ajili ya kuunganisha huduma katika soko hilo na bidhaa za samaki zinazotoka  ziwani (Ziwa Tanganyika).  
Gati linaloendelea kujengwa kwa ajili yakuhudumia soko hilo la samaki la Kirando wilayani Nkasi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com)

KINANA AMWOMBEA KURA RIDHIWANI KIKWETE KATIKA KATA ZA UBENA ZOMOZI LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwa amemuinua mkono Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete ikiwa ni ishara ya kumnadi kwa wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ubena Zomozi huku akishangilia kwa shangwe,leo Machi 24,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akimwaga sera zake kwa Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa amesimama kusikiliza kwa makini sera za  Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alizokuwa akitoa kwa Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi wakifatilia kwa makini sera za Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete huku wakiwa wamejikinga kwa mvua kwa kutumia viti,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi wakiwa wamejikinga kwa mvua chini ya paa la moja ya Nyumba zilizopo kwenye Kata hiyo wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.

HUDUMA BORA YA MASAJI JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Wewe  ni  mkaazi  wa  Dar  Es  salaam ? 
Unahitaji  huduma  bora  ya  masaji  au  escort ? Kama  jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema sana  kwako.
DAR   MOBILE   MASSAGE  AND  ESCORT  SERVICES   AGENCY    ( DAR  ESCORT )  ni  kampuni  inayo  husika  na  kutoa  huduma   YA  MASAJI   na  ESCORT  kwa  watu  mbalimbali.

Wahudumu  wetu  ni  wadada  maridadi, open minded  na  wenye  uzoefu   mkubwa  sana  katika  utoaji  wa  huduma  ya  masaji  za  aina zote   pamoja  na  huduma  ya  escort  kwa  watu  wa  aina  zote. 

Tunatoa  mobile  services. Huduma  zetu  ni  bora  sana.

Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu  :  0766101669.
Tembelea   blogu  yetu  :  http://www.darescort.blogspot.com

Facebook  :  www.facebook.com/darescort.

Ukurasa  wetu  wa  facebook  :     DarEscortServices

Wizara ya Kilimo na Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Mimea,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Fabian Nkondo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaelimisha wananchi kuhusu maboresho katika Sekta ya  Kilimo ili kuleta Tija.
 Msemaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Richard Kasuga akiwaeleza waandishi wa habari  kuhusu tahadhari ya kutokea viwavi jeshi hapa nchini hivyo wananchi kutakiwa kuchukua tahadhari. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya habari Maelezo na kushoto ni  Mkurugenzi Msidizi Afya ya Mimea,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Fabian Nkondo.
 
 Afisa habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaeleza  waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam  kuhusu  waombaji kazi kujiandaa vyema ili kukidhi vigezo  vya usaili, na kushoto ni  Afisa Udhibiti na Ubora  wa Sekretarieti hiyo  bw. Chistopher  Liganga. 
Afisa habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya nakala ya maombi ya ajira isiyokidhi vigezo hali inayosababisha waombaji wengi wenye sifa kushindwa kupata ajira Serikalini. Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi na kushoto ni  Afisa Udhibiti na Ubora  wa Sekretarieti hiyo  bw. Chistopher  Liganga.

TAZAMA ORODHA YA MAWAKALA WA REDDS MISS TANZANIA 2014

Maisha ya 'Geto' Changamoto kwa Wanafunzi Sekondari za Kata Tanga

$
0
0
UJENZI wa Sekondari za Kata katika mikoa mbalimbali umesogeza huduma za elimu kwa baadhi ya maeneo. Ipo mikoa ambayo awali ilikuwa na shule chache za sekondari hali ambayo ilifanya wanafunzi wachache kupata fursa ya kujiunga na sekondari. Kwa sasa hali si hivyo tena, mikoa mingi imeongeza idadi ya shule hizo licha ya changamoto kibao inazozikabili shule hizi.

Zipo baadhi ya shule za sekondari zimejengwa mbali kidogo na makazi ya wahitaji kitendo ambacho huwalazimu wanafunzi kutembea muda mrefu asubuhi wakielekea shuleni na baadaye jioni wakirejea nyumbani, hali ambayo ni changamoto kwa wengi wao.

Hata hivyo baadhi ya maeneo shule hizo zimejengwa mbali zaidi na makazi ya watu kutokana na kile kuhudumia vijiji ama vitatu hadi vinne, na hazina mabweni jambo ambalo wanafunzi wanashindwa kuvumilia umbali uliopo kutoka kijiji kimoja hadi kingine hivyo kutafuta mbinu mbadala ya kusogea jirani na shule wanazokuwa wamepangiwa.

Wanafunzi wanaamua kutafuta vyumba vilivyopo jirani na maeneo ya shule walizopangiwa na hivyo kupanga (kukodi chumba). Wenyewe vyumba hivi huviita mageto. Vyumba hivi huwa vidogo na vingine mithili ya vibanda, ambapo bei huwa ya chini zaidi kwa mwezi. Wanafunzi wengine huamua kujikusanya wawili ama zaidi na kuishi pamoja kwenye geto ili kupunguza gharama.

Mkoa wa Tanga katika Wilaya ya Lushoto baadhi ya maeneo aina hii ya maisha ya wanafunzi ni kitu cha kawaida. Wanafunzi wameamua kupanga kwenye mageto (vyumba mitaani) na kuishi kwa makundi huku wakikabiliwa na changamoto lukuki zinazohatarisha safari yao ya elimu ya sekondari.

Mbwambo Conrad ni Mkazi wa Kata ya Bungu wilayani Lushoto, eneo ambalo lina idadi kubwa ya wanafunzi waliopanga kutoka vijiji vya mbali huku wakihudhuria masomo yao ya sekondari. Anasema eneo hilo kuna wanafunzi wengi ambao wametoka vijiji vya mbali na wamepanga jirsni na shule kwenye kata hiyo kuhudhuria masomo. 

Anasema wanafunzi hao wamepangiwa na wazazi wao ili waweze kuhudhuria masomo yao kuepuka umbali wanaotoka kwenye vijiji vyao. "Wanafunzi hawa wamepanga katika baadi ya vyumba na wanaishi kwa tabu sana...wengi wanaingia katika majaribu kutokana na aina ya maisha wanayoishi," anasema Mzee Conrad.

Anasema wavulana wengi huishia kuwa wahuni maana uangalizi wa wazazi hawana, mara nyingi utawakuta wamekaa vikundi kwa vikundi nyakati za jioni hadi usiku unaweza kufikiri sio wanafunzi. Wanachelewa kulala muda mwingi wanazunguka kwenye majumba ya sinema (vibanda vinavyo onesha picha za video) hivyo wanaishi kwa kujitawala utazani si wanafunzi.

Willson N'gwamizi ni Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Muungui wilayani Lushoto, anasema licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali katika shule hiyo suala la wanafunzi kuishi kwenye mageto ni changamoto kubwa kwa shule kwani linaathiri maendeleo ya shule kitaaluma. Anasema wanafunzi hulazimika kuishi katika vyumba hivyo vya kupanga kutokana na shule nyingi za kata zilizojengwa kutokuwa na mabweni huku zikichukua wanafunzi kutoka vijiji vya mbali.

"...Kifupi suala la wanafunzi kuishi katika mageto linaathiri maendeleo ya shule kitaaluma...wanafunzi hawa wanapoishi huko hukosa usimamizi wa wazazi na wengine hata hela ya kumudu maisha hayo huwa ni tatizo maana wanatoka vijiji vya mbali na uwezo wa familia zao wakati mwingine hushindwa kuwatimizia mahitaji yote," anasema N'gwamizi.

Anasema kutokana na uhuru huo wa kukaa kwenye mageto wanafunzi wengine hutoroka na kwenda kufanya vibarua kwenye mashamba ya chai na sehemu nyingine wasichana nao huwa huru zaidi kitendo ambacho hushindwa kukabiliana na changamoto za vishawishi mitaani.

"Ukizunguka katika baadhi ya kata unaweza kukuta wanafunzi wa kidato cha pili wamepanga kwenye chumba kimoja, ndani ya chumba hicho wapo wawili hadi watatu...wengine wanatoka katika familia duni hawapewi mahitaji ya kutosha, wengine hujikuta wanashawishika na kuingia mitaani na kujikuta wanakatizwa masomo kwa kutiwa ujauzito," anasema.

"Kwa kweli mageto ni tatizo, wapo baadhi ya walimu hujitahidi kuwafuatilia huko wanakoishi ili kuhakikisha wanajenga nidhamu ya kiuanafunzi, hata hivyo zoezi hili bado ni changamoto maana na walimu wamejikuta wakikaa mbali na shule kutokana na ukosefu wa nyumba za walimu jambo ambalo ni tatizo pia...," anasema mwalimu huyo.

Suala la ukosefu wa mabweni kwa shule za kata na kuwalazimu wanafunzi kupanga mitaani (mageto) halipo kwa wilaya ya Lushoto pekee. Wilaya ya Handeni nayo inakabiliwa na changamoto hiyo ya wanafunzi kupanga uswahilini wenyewe karibu na shule walizopangiwa. 

Ester Frank ni mmoja wa wanafunzi wa sekondari za kata wilayani Handeni anasema changamoto kwa wanafunzi kukaa kwenye mageto ni kubwa hasa wa kike. Anasema wengi wanakosa uangalizi na usimamizi hivyo kujikuta wanajiingiza kwenye vishawishi hivyo kuishia kupata mimba na kukatizwa masomo yao. "...Usema kweli mageto yanatuathiri wanafunzi hapa wilayani Lushoto," anasema mwanafunzi huyo.

Afidha Said ni mkazi wa Kijiji cha Kidereko, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Said anasema katika mahojiano na mwandishi wa makala haya kijijini Kidereko wilayani Handeni, aliyekuwa akifuatilia vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo hufanyiwa baadhi ya wanafunzi na wanawake eneo hilo kwa ushirikiano na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa). Anasema matukio ya mimba kwa wanafunzi eneo hilo si kwamba hulazimishwa kimahusiano, bali huingia wenyewe katika mahusiano kingono kutokana na mazingira halisi.

Anasema ukiachilia mbali uduni wa kipato kwa familia nyingi eneo hilo, ambao wengi ndio wazazi/walezi wa wanafunzi, shule nyingi za kata Wilaya ya Handeni zipo mbali na makazi ya wanafunzi. Zimejengwa hivyo ili kuweza kuhudumia vijiji vingi, ambavyo pia kuna umbali mkubwa kutoka kijiji kimoja hadi kingine.

Wapo wanafunzi ambao hulazimika kutembea kilometa 12 hadi 20 kwenda na kurudi shuleni kila siku jambo ambalo linawaumiza wengi, hivyo kulazimika ama kutafuta urahisi wa kupata usafiri hasa kwa wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali au kulazimika kupanga katika mageto jirani na shule walizopangiwa. kwa usafiri maarufu ambao hutumika na jamii maeneo mengi ya vijiji hivi ni pikipiki (bodaboda), ambao wazazi hawawezi kuumudu kwa wanafunzi wao kutokana na gharama za juu.

Mmoja wa walimu katika moja ya shule za kata wilaya ya Handeni (jina tunalihifadhi kwa kuwa si msemaji) anasema shule yao inawanafunzi wanatoka katika vijiji kama Kidereko ambacho ni takribani kilomita 6 kwenda na Kijiji cha Bangu ambacho ni karibu kilomita 10 kwenda tu. Anasema umbali kama huu ukiuunganisha mwanafunzi analazimika kwenda na kurudi kila siku unakuta ni tatizo.

Anasema na wengi wanatoka katika familia duni unakuta hawapewi chochote wanapotoka nyumbani kama matumizi ya siku (kula), sasa katika hali kama hii inakuwa tabu. Wapo ambao wanaamua kukata tamaa ya kuendelea na shule hivyo kujiingiza katika mambo ambayo yanawaharibu kitabia kabisa.

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wananchi Januari 7, 2013 mjini Igunga aliwahi kusema kuwa serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto za elimu. "Kwa upande wa elimu tumeendelea kupata mafanikio katika kupunguza tatizo la upungufu wa walimu wa shule za msingi na sekondari. Mwaka huu (2013) tuliajiri walimu 28,666. Kwa ajili hiyo upungufu wa walimu ni 57,755 kati yao  20,625 wa shule za msingi na 37,130 wa shule za Sekondari.  

Rais Kikwete anasema kwa mwaka 2014 Serikali itaajiri walimu wapya 36,100 kati yao 18,100 wa shule za msingi na 18,000 wa sekondari. Kufanya hivyo kutafanya pengo lililopo liwe dogo zaidi. Kwa upande wa shule za sekondari, tatizo la walimu wa masomo ya sanaa tunakaribia kulimaliza. Changamoto yetu kubwa itakuwa kwa walimu wa masomo ya sayansi.

Rais Kikwete anasema upungufu ni walimu 26,998 na uwezo wa vyuo vya ualimu nchini ni kutoa walimu wa sayansi 2,300 kwa mwaka. Anaongeza kuwa mapema mwaka 2014 Serikali itakutana na wadau wa elimu nchini kujadiliana juu ya mkakati wa haraka wa kulikabili tatizo hilo.

Hata hivyo licha ya juhudi hizi kwa upande wa changamoto ya walimu hasa kwa shule za kata kuna haja ya Serikali kuangali namna ya kulipa kipaumbele suala la kupambana na changamoto za umbali wa shule za kata na makazi ya wananchi na kuhakikisha ujenzi wa mabweni ili kupunguza adha wanazopata wanafunzi wa kike na kiume kutokana na changamoto hiyo inamalizima kama si kupungua kwa kiasi fulani. Tukiamua tunaweza kukabiliana na changamoto hizi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TAMWA

KKKT: Nawaita waumini Tamasha la Pasaka

$
0
0
KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mkoa wa Morogoro limetoa wito kwa jamii kuungana na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama katika kipindi hiki cha Pasaka kutumia kidogo ambacho Mungu amewajalia kuwakumbuka wenye mahitaji maalum kama vile walemavu, wajane na yatima.Wito huo umetolewa na Mchungaji Raymond Dunia wa kanisa hilo akiwa na nia ya kuwakumbusha Wakristo kuwa na moyo wa kujitolea hasa kwa wenye mahitaji maalum.
 
Anasema kuwa lengo la Msama kusaidia jamii kupitia matamasha  ya nyimbo za injili ni lengo zuri kwa kipindi hiki cha Pasaka,  kwani ni wakati wa ukombozi kwa waliokandamizwa, Pasaka ni furaha kwa walio wahitaji, pia  Pasaka ni amani kwa watu wenye mashaka ya maisha yao.
 
Anaongeza kwa kusema kuwa kupitia matamasha ya nyimbo za injili watu wengi wanaokolewa, hivyo ni njia mojawapo ya kusababisha watu waokolewe.“Wapo watu wenye mipango bora ya kusaidia jamii, lakini wanapofanikiwa wanajihudumia wenyewe. Msama awe mfano mwema katika kuisaidia jamii ili kutimiza lengo la Kristo aliyesema, “Wenye afya hawahitaji tabibu ila walio hawawezi,”” alisema.
 
Hata hivyo mchungaji Dunia amesema kuwa wapo wanaotumia fedha nyingi kwa kuandaa sherehe katika sikukuu ya Pasaka huku wengine wakihangaika kutafuta angalau mlo mmoja wa siku, hata katika kipindi cha sikukuu kama hiyo, lakini wakumbuke kuwa ni vyema kwenda kuwatia moyo kuwafariji wale wanaolea wenye uhitaji maalum vituoni.
 
Aliongeza kwa kumtia moyo Msama aendelee na moyo  huo wa imani wa kuwasaidia wasiojiweza kwa kuwa anayetoa atazidishiwa mara dufu, kwa kuwa yeye yu miongoni mwa wachache wenye moyo wa kusaidia wahitaji hao.
 
Anatoa wito kwa mashabiki na waumini wajitokeze kwa wingi kuhudhuria matamasha hayo kwa kuwa kupitia nyimbo za injili watabarikiwa na hata kujifunza neno la Mungu. Pia aliwapongeza waimbaji wa nyimbo za injili kwa kuwa wao wamekuwa ni njia nyingine ya kutangaza neno la Mungu na kupitia wao watu wengi wanaokolewa. Hivyo wajue kuwa wao pia ni kioo cha jamii, jamii inahitaji kujifunza kutoka kwao
.
Matamasha hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika mikoa tofauti yamekuwa ni moja ya njia pekee ya kupunguza uhalifu na kuongeza kipato cha wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo ya karibu na yanapofanyika matamasha hayo.Hata hivyo Msama ana nia ya kujenga kituo cha kusaidia wahitaji hao ambacho kitasaidia maeneo mbalimbali  kama kuwasaidia wahitaji  wenye kipaji cha uimbaji.
 
Pamoja na hayo  Msama anaiomba jamii, ikae tayari kusubiri matamasha hayo yanayosubiriwa kwa hamu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na mashabiki wa nyimbo za injili kujitokeza  kwa wingi kwa kipindi hicho cha matamasha ili kuweza kumsapoti kutimiza lengo lake la kusaidia wahitaji hao.

MHE.RAIS AWATAKA VIONGOZI MKOANI TANGA KUSIMAMIA WATOTO KWENDA SHULE

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
MHE.RAIS AWATAKA VIONGOZI MKOANI TANGA KUSIMAMIA
WATOTO KWENDA SHULE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule, wanakwenda shule bila kukosa hata kama hawana uwezo wa kumudu mahitaji maalum ya shule.

Rais amesema hayo Wilayani Korogwe wakati akipokea taarifa ya Wilaya iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw. Mrisho Gambo.

Katika taarifa yake kwa Rais, Bw. Gambo ameelezea hali ya mdondoko wa wanafunzi Wilayani mwake na kuelezea kuwa unasababishwa na utoro, mimba, vifo na wazazi kukosa mahitaji muhimu kwa watoto wao.

Ndipo Rais Kikwete akasema kuwa "Ni lazima warudi shule ni, na viongozi mtafute namna ya kuwasaidia, msiwaache bure, muwatafutie na muwapatie hayo mahitaji maalum wanayotakiwa kuwa nayo" Rais amesema na kusikitishwa na taarifa hizo ambazo amewaagiza viongozi wa Wilaya kuwatafuta watoto hao walipo na wale wasio na mahitaji maalum ambayo baadhi yake ni sare za shule, kuhakikisha kuwa uongozi wa Halmashauri husika zinawatimizia hayo mahitaji na kuwapa watoto fursa ya kuwa shuleni.

Taarifa za Wilaya zinaonesha kuwa Mwaka 2011 jumla ya watoto 63,918 waliandikishwa shule na Kati yao watoto 492 hawakuhudhuria shule kwa sababu mbalimbali.

Rais pia amezitaka Wilaya kuweka mkakati wa kutengeneza madawati kwa ajili ya shule zao, kuwa na nyumba za walimu, ujenzi wa madarasa,  maabara na vitabu.

Rais Kikwete yuko Mkoani Tanga kwa ajili ya shughuli za kikazi na kukagua miradi ya maendeleo, kuangalia utekelezaji wa ahadi na Ilani ya Chama.

Mara baada ya kuwasili Mkoani Tanga siku ya Jumapili tarehe 23 Machi, 2014, Rais ameweka jiwe la Msingi la ujenzi wa bwawa la Maji, Mkata Wilayani Handeni na kuzindua ujenzi wa barabara ya Handeni-Korogwe na Handeni-Mkata ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama za serikali kwa asilimia Mia moja.

Katika siku yake ya pili katika Wilaya ya Korogwe, pamoja na mambo mengine Rais amezindua barabara ya Korogwe - Mumbara na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara ya shule ya Sekondari Madago kabla hajahutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Mombo.

Ziara ya Rais Mkoani Tanga itakuwa kwa awamu mbili ambapo awamu hii ya kwanza atatembelea Wilaya za Handeni, Korogwe, Muheza na Tanga Mjini na awamu ya pili itahusisha Wilaya za Kilindi, Lushoto, Mkinga na Pangani.


Imetolewa na;

 Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Mkoani Tanga.



25 Machi,2014

WATENDAJI DAR WAASWA KUSHIRIKIANA ILI KUWEKA JIJI KATIKA HALI YA USAFI

$
0
0
DSC_1151
Meneja Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande (mwenye suti ya damu ya mzee) akinyoosha kidole kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (wa pili kulia) sehemu korofi za kutiririsha maji machafu barabara ya Morogoro kati kati ya jiji.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania.

WATENDAJI wa Mamlaka za Maji Safi na Taka, Manispaa, Halmashauri, Wakala wa Barabara na Mabasi yaendayo kasi wameshauri kuwa na utaratibu wa kuwasiliana na kushirikiana kwa pamoja ili kuleta tija katika usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu, kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo amesema kuwa tatizo la jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa mkoa hawana mawasiliano ya kutosha katika utendaji kazi wa kila siku.

Shayo alizungumza hayo kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya kugagua hali ya usafi katika maeneo kadhaa pamoja na kuangalia maeneo korofi katika kutitirisha maji machafu kwenye mitaro kadhaa kati kati ya jiji.

“tatizo kubwa katika jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa jiji, manispaa, wakala wa barabara, Tanesco na mamlaka za maji safi na taka kutokuwa na utaratibu wa kuwasiliana katika utendaji kazi wa kila siku katika kuboresha usombaji wa taka kwenye jiji la Dar,” amesema Shayo
DSC_1173
Meneja Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande akiwaonyesha baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick na Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu baadhi ya mashimo (Potholes) ambayo ni hatari kwa wananchi watembea kwa miguu baada ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.

Shayo alilisisitiza kwamba katika utendaji kazi wa jiji kama la Dar inahitajika ushirikiano wa dhati kati ya wadau wa kusomba taka na watendaji wa manispaa pamoja na jiji ili kuweka mkoa wa Dar es Salaam katika hali safi wakati wote.

Amesema kuwa ingawaje tatizo kubwa la uchafu linasababishwa na miundombinu mibovu ya barabara na maji hasa kuelekea katika dampo kuu la mkoa sehemu ya Pugu Kinyamwezi, Gongo la Mboto.

Shayo ambaye kampuni yake inajishughulisha na usombaji wa taka ngumu na nyepesi katika mkoa wa Dar es Salaam amesema kwamba mamlaka zinazohusika kwa kushirikiana na wadau lazima watoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi taka.
“sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi. inahitajika kampuni ya ujenzi yenye uwezo wa kuboresha miundombinu ya barabara kuelekea kwenye dampo ili kupunguza foleni ya magari ya taka na kuongeza tija ya kazi katika eneo husika,” aliongeza
DSC_1231
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick akiongoza msafara wa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika kuangalia hali ya usafi na miundombinu ya maji na barabara jijini Dar.


Kwa upande wake, Minael Mshanga Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, amesema jiji limejipanga kufanya ukarabati wa miundombinu ya barabara kuelekea dampo ili kuongeza kasi ya magari yanayokwenda kumwaga taka katika dampo hilo.
“hivi tupo katika hatua za mwisho na tumempata mkandarasi wa kuja kujenga na kutengeneza miundombinu ya barabara kuelekea katika dampo pamoja na kutengeneza mataa katika eneo husika ili kazi ya kutupa taka ifanyike usiku na mchana,” amesema Mshanga
Aliongeza kwamba jiji lina mpango wa kuanza kushirikiana kwa karibu na wakandarasi wazalendo katika kuleta ufanisi wa usombaji taka ili kuzuia magonjwa ya mlipuko katika mkoa wa Dar es Salaam.
DSC_1240
Mbunge wa Ilala, Hassan Zungu akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick wakati wa ziara ya ghafla ya kugagua hali ya miundombinu ya maji na barabara kati kati ya jiji la Dar.
DSC_1310
Baadhi ya magari ya wakazi wa jiji yakipita kwa taabu katika madimbwi na mashimo ya maji machafu kati kati ya jiji la Dar es Salaam.
DSC_1337
Viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakijadili moja ya sehemu korofi kati kati ya jiji karibu na Haidery Plaza ambapo kipindi cha mvua maji taka yaliyochanganyikana na kinyesi yanatuama kwa kipindi kirefu ambapo hakuna mfereji wala mtaro wa maji machafu.
DSC_1350
Mashimo ya miaka nenda rudi yasiyopatiwa ufumbuzi lakini baada ya ziara yatarekebishwa.
DSC_1402
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa ushauri kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midala (mwenye tai nyeusi).
DSC_0468
Kaimu Mkuu wa Idara ya Udhibiti taka kutoka jiji, Enezael Ayo (kushoto) akifafanua jinsi magari ya taka yanavyomwaga taka katika dampo kuu la Pugu Kinyamwezi jijini Dar wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar.
DSC_0477
Mkurugenzi Mtendaji wa Tirima Enterprises, Robert Ngeleshi akizungumza changamoto na matatizo ya mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar ambao waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo.
DSC_0514
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akielezea jambo kwa mkuu wa mkoa wakati wa kuhitimisha ziara hiyo katika maeneo ya dampo Pugu Kinyamwezi.
DSC_0531
Moja ya Bull dozer linalorekebisha barabara likiwa limeharibika kutokana na miundombinu mibovu katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
DSC_0553
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Minael Mshanga (kulia kwa Mkuu wa Mkoa) akitoa ufafanuzi wa matatizo na changamoto za usombaji na utupaji taka katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
DSC_0560
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akiagana na wakandarasi wa usombaji taka na watendaji wa jiji. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa kwa shangwe na Wanachama mbalimbali wa chama hicho mapema leo asubuhi alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Ilala,ambapo alizungumza machache na  kamati ya siasa ya Wilaya na baadae kuanza ziara rasmi wilaya ya Ilala.
 Pichani kulia ni Mwenyekiti Mkoa wa CCM,Dar Es salaam Ndugu Ramadhan Madabida akizungumza jambo mbele ya kamati ya Siasa ya mkoa (hawapo pichani) mapema leo,kwenye ofisi Kuu za CCM mkoa,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana (pichani kushoto) anaanza rasmi ziara ya siku nne mkoani humo,ambapo atatembelea wilaya ya Ilala (ambayo ameianza leo),Temeke na Kinondoni. Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuimarisha chama cha CCM na kuhamasisha na kutenda utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,sambamba na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pichani kulia ni Mwenyekiti Mkoa wa CCM,Dar Es salaam Ndugu Ramadhan Madabida akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana taarifa ya hali ya kisiasa mkoani Dar es salaam,mapema leo mara baada ya kufanyika kikao kifupi cha kuanza ziara ya siku ya nne mkoani humo
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao kifupi mbele ya kamati ya Siasa ya mkoa mapema leo,kwenye ofisi Kuu za CCM mkoa.Ndugu Kinana anaanza rasmi ziara ya siku nne mkoani humo,ambapo atatembelea wilaya ya Ilala (ambayo ameianza leo),Temeke na Kinondoni. Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuimarisha chama cha CCM na kuhamasisha na kutenda utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,sambamba na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Baadhi ya Wananchi wakiutazama msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (haupo pichani),ulipokuwa ukiwasili kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Ilala

BANDARI MTWARA YAJIDHATITI KUONGEZA UWEZO WA KUHUDUMIA MIZIGO Na Saidi Mkabakuli.

$
0
0
 Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella (Kuliai) akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake kukagua kukagua mirdai ya maendeleo Bandari hapo. Kutoka kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof. Longinus Rutasitara (Wakwanza Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Katikati).
 Afisa Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Kushoto) akitoa maelezo ya uendelezaji wa maeneo ya Bandari hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara Bandarini hapo. 
 Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea eneo la Bandari ya Mtwara ambapo panapotarajiwa kuongezwa magati.
 Shehena ya korosho ikiendelea kupakiwa katika makontena tayari kusafirishwa. Picha na Saidi Mkabakuli
 Afisa Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Wambele Kushoto) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango eneo jipya (halionekani) ambalo Bandari hiyo imeliongeza ili kuboresha ufanisi bandarini hapo.
Ujenzi wa eneo la kuhifadhia saruji ukiendelea.
========  =======  ======
BANDARI MTWARA YAJIDHATITI KUONGEZA UWEZO WA KUHUDUMIA MIZIGO.

Na Saidi Mkabakuli.

Mamlaka ya Bandari Tanzania, kupitia Bandari yake ya Mtwara inajidhatiti katika kuongezea uwezo wa kuhudumia mizigo iingiayo na itokayo mkoani humo kupitia bandari hiyo kufuatia kuongezeka kwa shughuli za biashara mkoani Mtwara.

Akizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella amesema kwamba hatua hii inachagizwa na mkakati wa  kukabiliana na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za huduma mkoani Mtwara.

Aliongeza kuwa mkakati huu unajumuisha upanuzi wa eneo la bandari hiyo kutoka hekta 70 zilizokuwa zikimilikiwa na Bandari tangu kuanzishwa kwake mwaka 1950 hadi kufikia hekta zaidi ya 2600 pamoja na upanuzi wa magati manne ya kuhudumia meli bandari hapo. “Upanuzi huu utaongeza kasi yetu ya kuhudumia mizigo toka tani za ujazo 270 za sasa hadi kufikia tani za ujazo 400 kwa mwaka hii itatuongezea ufanisi katika kuhudumia watumiaji wa Bandari yetu, hasa kufuatia kugundulika kwa gesi mkoani Mtwara,” alisema Bw. Bohella.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri ambaye ni mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi hiyo, alisema kuwa kuna haja ya dhati ya kuwekeza katika Bandari hiyo ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara kufuatia wawekezaji wengi kuendelea kumiminika na kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizomo mkoani humo.

“Bandari ya Mtwara ina fursa za nyingi za kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, hasa katika kipindi hiki cha uchumi wa gesi mkoani Mtwara, hivyo uendelezaji wa upanuzi wa bandari hii ni suala la kimkakati,” alisema Bibi Mwanri.

Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),  Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.

Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.

Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AKAMILISHA ZIARA YAKE WILAYA YA ILALA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye mradi wa ujenzi wa tanki la maji katika eneo la Tabata Kimanga, akiwa katika ziara ya siku moja katika wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadik
 Kinana akipanda juu kukagua ujenzi wa tanki hilo la maji ambalo lina uwezo wa lita 200,000
Kinana akishuka baada ya kukagua tanki hilo litakalohudumia wakazi wa Tabata,zaidi ya Elfu 20 Tabata Kisiwani na Tabata Kimanga
Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabiba wakishuka baada ya kinana kukagua tankii hilo
Kinana akikagua soko la Tabata Kisiwani wakati wa ziara hiyo
Bango la kumkaribisha Kinana alipotembelea viwanja vya Kidongo Chekundu, Ilala kuona mradi wa viwanja vya michezo kwenye eneo hilo.
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili viwanja vya Kidongo Chekundu wilayani Ilala
Mbune wa Ilala Mussa Zungu akizungumzia mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo kwenye eneo la Kidongo chekundu, wilayani Ilala
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akizungumzia mradi huo mbele ya Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpongeza Silaa baada ya kuzungumzia mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo Kidongochekundu.

BIDHAA YA TreSSa YAZINDULIWA JIJINI MWANZA

$
0
0


Meneja masoko wa bidhaa za TreSSa, Manoj Kumar akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa za TreSSa uliofanyika katika Hoteli ya Goldcrest jijini Mwanza jana.  Kulia ni Meneja wa bidhaa za TreSSa, Dorith Godfrey.
Balozi wa TreSSa, Eligiva Meena akipozi na kuonesha unywele wake ulivyo stawi.
Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akielezea furaha yake ya ujio wa bidhaa hiyo jijini Mwanza na namna itakavyoongeza ajira ya vijana hasa watoto wakike watakao kua wakiiuza.
Johan Vanden Heevevol akitoa maelezo ya bidhaa ya TreSSa.
Waalikwa wakifuatilia maelezo ya bidhaa hiyo ya TreSSa
Mwana dada Olever Nazareth mkazi wa malimbe jijini Mwanza akiwekwa dawa ya TreSSa na mhudumu wa salon.


Olever Nazareth akionesha vile unywele wake unavyomeremeta baada ya kutumia dawa ya TreSSa.
Olever Nazareth (kushoto) akiwa na Aziza Ismail kutoka Chuo Kikuu cha St Augustino (SAUT) cha jijini Mwanza baada ya kusetiwa nywele zao na dawa ya TreSSa.
Zawadi zilitolewa kwa washindi wa bahati nasibu.
Msanii Sara Kaisi 'Shaa' akitoa burudani ya sugua gaga ukumbini.
Meneja wa bidhaa za TreSSa, Dorith Godfrey akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Mwanza.

Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto) akizungumza jambo na Meneja masoko wa bidhaa za TreSSa, Manoj Kumar wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo ya Tressa inayozalishwa na Kampuni ya Chemi cotex mkoani Mwanza jana.
Waalikwa katika uzinduzi huo wakisakata rumba

CHUO CHA VETA CHATAMBULISHA MRADI WA USHIRIKIANO KATI YAKE NA UJERUMANI UJULIKANAO KAMA "GERMAN DUAL SYSTEM APPRENTICESHIP" LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akizungumzia juu ya mradi ambao German wameshirikiana na Chuo cha VETA nchini katika kuhakikisha wanaboresha maswala ya elimu ya vitendo Tanzania. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru.
 Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutambulisha mradi wa ushirikiano kati ya Vyuo vya Ujerumani na VETA kwa wanafunzi wa Tanzania.
 Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akiongea na waandishi wa habari wakati alipowatembeza kwenye moja ya karakana ambayo inatoa masomo kwa vitendo yaliyo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship" iliyopo katika Chuo Cha VETA kilichopo Chang'ombe jijini Dar Es Salaam.
 Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akiwaonyesha moja ya magari yaliyotolewa na Kampuni ya Noble Motors kwaajili ya Mafunzo ya Vitendo yaliyo chini ya Mradi wa "German Dual System Apprenticeship" kwa wanafunzi wa Chuo Cha VETA.
 Wanafunzi wa Chuo Cha VETA wakiwa katika mafunzo kwa vitendo ambayo yapo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship" ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo na kuunganishwa na makampuni ambao wanafunzi hao hupelekwa kwaajili ya mafunzo zaidi
Moja ya gari lililotolewa na Kampuni ya Noble Motor kwaajili ya mafunzo kwa vitendo yaliyo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship"
Moja ya gari lililotolewa na Kampuni ya Scania Tanzania kwaajili ya mafunzo kwa vitendo yaliyo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship"
 Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam, Bi Benadetha Nduguru akiongea na waandishi wa habari wakati walipotembezwa kwenye moja ya karakana inayotumika kwaajili ya Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"
Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuwatembeza waandishi wa habari na wageni waalikwa kwenye karakana zilizo chini ya Mradi wa "German Dual System Apprenticeship" ambapo Ujerumani na Chuo Cha VETA wameshirikiana katika mradi huo.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Redd's Original yawapiga msasa waandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2014

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa shindano la Redds Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza na mawakala wa shindano hilo Dar es Salaam jana katika semina ya seku mbili. Katikati ni Redd's Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa na Mshindi wa pili, Latifa Mohamed. Shindano la Miss Tanzania linadhaminiwa na Kinywaji cha Redd's Original.
 
 Baadhi ya mawakala wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakiwa  katika semina ya siku mbili juu ya namna ya ufanyanyaji wa mashindano hayo mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Shindano la Miss Tanzania linadhaminiwa na Kinywaji cha Redd's Original.
========  ======  ====
MAWAKALA wa mashindano ya urembo nchini wametakiwa kutafuta washiriki wenye vigezo kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu na hatimaye kupata mshindi wa kitaifa “Redd’s Miss Tanzania 2014” atakayeipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye fainali za dunia.
Akizungumza katika semina ya mawakala hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Regency iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Lino Agency International, Hashim Lundenga, aliwataka kusaka washiriki bila ya kuwanyanyapaa wasichana kutokana na maumbile yao.
Lundenga alisema kuwa mawakala hawapaswi kutoa maamuzi ya washiriki wakati wa mchakato wa kutafuta warembo na jukumu la kufanya hivyo litabaki kwa majaji.
Mkurugenzi huyo alisema pia mawakala wanaume wanatakiwa kuwa makini katika mchakato huo wa awali na kuhakikisha wanaendeleza maadili ya Kitanzania na kufanikisha sanaa hiyo inazidi kufanikiwa.
“Si vizuri kuwakataa wasichana wanaotaka kushiriki kwa sababu eti wafupi au sabau nyingine…kufanya hivyo si sahihi, pia huu ni wakati mwingine kwa mawakala wanaume kuhakikisha mnavivuka  viunzi kwa wasichana wanaojiandaa kuwaweka mtegoni,” alisema Lundenga.
Aliwataka mawakala hao pia kuhakikisha wanafanya mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kusaka udhamini wa kufanikisha mashindano yao ambayo yanaania ngazi ya vitongoji, wilaya, mikoa na kanda.
“Kuhusiana na zawadi pia mnatakiwa kuwa na makubaliano na washiriki kulingana na uwezo wako wakala…hata kama uko tayari kutoa jiko waeleze hivyo,” Lundenga aliongeza.
Aliwaeleza pia mawakala hao kwamba mdhamini mkuu wa mashindano hayo ni Redd’s Original ambayo imeahidi kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500.

Happiness Watimanywa ndiye mrembo anayetetea taji la taifa na mshindi wa pili, Latifa Mohammed pia walikuwepo jana katika semina hiyo inayotarajiwa kumalizika leo.

AFRICAN BARRICK GOLD MINING WADHAMINI TIBA YA UPASUAJI BURE KWA KICHWA, MGONGO NA MISHIPA YA FAHAMU KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA

$
0
0
Daktari Bingwa wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu Dr. Othman W. Kiloloma kutoka hospitali ya Muhimbili amesema kuwa timu ya madaktari saba imewasili kutoka Muhimbili  ikiwa na daktari bingwa 1 wa usingizi wakiwa na vifaa vyote muhimu ili kuungana na madaktari Bingwa wa upasuaji Bugando kwaajili ya kuweka kambi ya tiba mkoani Mwanza.  
Dr. Othman W. Kiloloma ameongeza kuwa dhana ya kuweka kambi Mwanza imekuja ikiwa ni hatua ya kujaribu kupunguza vifo na usumbufu unaowakumba watu wenye maradhi hayo pindi wanapohitaji tiba ambapo wengi wameshindwa kupata huduma mapema kutokana na kushindwa kuzimudu gharama kwa magonjwa hayo ambayo kila kukicha idadi ya watu wenye matatizo ya Ubongo na Mishipa ya fahamu inaongezeka. Ameishukuru sana African Barrick Gold kwa kudhamini mpango huo. 
Kama upasuaji utahitaji kufanyika masaa 24 tuko tayari kwa hilo, nia ni kuwahudumia wale wote watakao jiandikisha kuwa wanamatatizo na wanahitaji tiba.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa mpango huo wa tiba, Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula amewataka wananchi wote wenye matatizo kujitokeza kwani ni nadra sana kupata tiba kama hiyo bure bila malipo, naye akisema kuwa ni mmoja katiya waathirika wa matatizo hayo ambapo ni hivi karibuni tu! naye ametoka kufanyiwa upasuaji wa matatizo ya mgongo katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili. Pia amewashukuru sana Madaktari hao bingwa kwa kuliona tatizo na kulitafutia ufumbuzi sambamba na kuwashukuru Kampuni ya ABG waliodhamini mpango huo. 
Sehemu ya madaktari Bingwa watakao husika na zoezi hilo la tiba itakayo tolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando.
"Mpaka sasa tumeandaa wagonjwa 33, ambao wanahitaji oparesheni, leo kuna wagonjwa 12 ambao wamepangiwa oparesheni, watoto ni wa8 na watu wazima ni wa4". Miongoni mwao kuna wagonjwa wenye matatizo makubwa wawili, mmoja anausaa kwenye ubongo, mwingine damu imeingia kichwani" alisema Dr. Gerlard ambaye ni Bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC ambao ni wenyeji). 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bugando (BMC) Prof. Charles Majinge, Meneja Mahusiano na jamii wa Kampuni ya ABG  Steve Kisake, mgeni rasmi Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na kulia ni mmoja kati ya madaktari bingwa wakisikiliza maelezo na ufafanuzi wa jinsi zoezi litakavyo fanyika.
Ni mmoja kati ya akinamama waliojitokeza kwa kuwaleta watoto wao kufanyiwa upasuaji wa mishipa na mgongo.
Ni uvimbe wa mmoja kati ya watoto wanao subiri tiba. Kila la kheri Mwenyezi Mungu awaongoze na mfanikishe kwa wale wote wanaopata tiba na wale wanao subiri tiba.
Ni mtoto ambaye anasubiri kupatiwa tiba kwa tatizo la kichwa kujaa maji kwa tiba ya bure itakayo tolewa na madaktari bingwa wa upasuaji toka MOI na BMC akiwa katika ward ya Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza. Kila la kheri Mwenyezi Mungu awaongoze na mfanikishe kwa wale wote wanaopata tiba na wale wanao subiri tiba.
Tatizo la kichwa.
Tatizo la uvimbe kwenye mgongo.
Baadhi ya akinamama wakiwa na watoto wao katika ward wakisubiri kupatiwa tiba kwa matatizo mbalimbali yanayo hitaji upasuaji unaofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji toka MOI wakishirikiana na mabigwa wa upasuaji wa BMC, ni katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Dr. Othman W. Kiloloma akitoa ufafanuzi katika kusanyiko la uzinduzi wa tiba ya bure kwa maradhi ya Kichwa, Mgongo na Mishipa uliofanyika ukumbi wa mikutano kitengo cha Satatani Bugando jijini Mwanza.



HALI IKIWA TETE KANDA YA ZIWA NAKO WODI ZA MOI ZIMEFURIKA.
MWANZA.
LICHA ya kuwa na Madaktari bingwa wa upasuaji wa kichwa wasiozidi watano tu nchini, wodi za kitengo cha upasuaji wa kichwa na mifupa cha Hospitali ya Rufaa ya Taifa Mhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam, zimefurika wagonjwa.

Mratibu wa jopo la madakatari bingwa saba wa MOI walioweka kambi maalum ya matibabu ya mgongo na upasuaji kichwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) jijini Mwanza, Dkt Othman Kiloloma, amesema hali hiyo ni moja ya changamoto kubwa inayokikabili kitengo hicho.

Amedai, kutokana na kusubiri matibabu hayo kwa muda mrefu, baadhi ya wagonjwa wa nje ya Dar es salaam huishiwa fedha za kujikimu na hata nauli, hivyo Madkatari hao kulazimika kuwasaidiwa nauli za kuwarudisha makwao.

Dkt Kiloloma alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Matibabu ya mgongo na upasuaji kichwa unaofanywa na wataalam hao hapa, kwa kushirikiana na madakatari bingwa wa BMC.  

Matibabu hayo yanayotolewa bure kwa ufadhili wa kampuni ya African Barrick Gold katika hospitali ya Bugando, yalianza juzi (Machi 24) na yataendelea hadi Machi 28 mwaka huu ambapo wagonjwa zaidi 33 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa vichwa na kutibiwa migongo.

“Wodi zetu zimejaa wagonjwa wetu wanasubiri kwa muda mrefu, ukituletea mgonjwa atalala wapi wakati wamejaa hadi kwenye makorido lakini hatuwezi kuwafukuza.” Alieleza Dkt Kiloloma wakati akionyesha picha za wagonjwa waliolazwa MOI, walivyofurika.

Alisema kupeleka wagonjwa wa aina hiyo Dar ni gharama kubwa hivyo ndiyo maana jopo hilo kwa ufadhili wa kampuni hiyo ya uchimbaji madini nchini, limeweka kambi Bugando ili kuwasaidia wagonjwa waliopo kanda ya ziwa ambao ingebidi wapelekwe Mhimbili au nje ya nchi kwa matibabu hayo.

“Kati ya Madaktari saba tuliotoka MOI kuja Mwanza kuungana na wenetu wa Bugando kusaidia wangonjwa wa Kanda hii ya ziwa, mabingwa wa upasuaji wa kichwa tupo watatu. Tanzania nzima ina mabingwa wa Upasuaji kichwa wasiozidi watano, hivyo wawili ndio wamebaki Dar.” Alieleza bingwa huyo na kudai upungufu wa wataalamu hao ni changamoto kubwa inayolikabili taifa.

Alieleza kwamba kukamilika kwa jengo la ghorofa nane linalojengwa MOI kutasaidia kuondoa mlundikano wa wagonjwa ambao sasa wanakosa pa kulala licha ya wengine kuwa nje ya wodi wakisubiri matibabu.  

“Tunapasua wagonjwa 600 kwa mwezi lakini kutokana na kusubiri matibabu kwa muda mrefu kidogo, baadhi au wauguzi wao huishiwa fedha za kujikimu na kulazimika kuwasaidia nauli ya kurudi kwao, wengine (akina mama) hukuta waume zao walisha oa wanawake wengine.” Alidai.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images