Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

KAMPENI ZA CCM JIMBO LA CHALINZE,ZAENDELEA LEO KATA YA LUGOBA

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makombe,Kata ya Lugoba leo Machi 25,2014,wakati wa muendelezo wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani).
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa kijiji cha Makombe,Kata ya Lugoba leo Machi 25,2014,ikiwa ni muendelezo wa Kampeni zake.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnauye wakishiriki kucheza muziki pamoja na wananchi wa Kijiji cha Kinzagu,Kata ya Lugoba leo Machi 25,2014.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnauye akishiriki kuruka juu pamoja na Wamasai ambao ni wakazi wa Kijiji cha Kinzugi,Kata la Lugoba ndani ya Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani.

GLOBAL WOMAN OF THE YEAR 2013

UZINDUZI WA MCHAKATO WA KUANZISHA TIKA (TIBA KWA KADI) KATIKA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE

$
0
0
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kufungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia). 
 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (Kulia) akiongea wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (Katikati) katika ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (katikati) akifungua kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika mfumo wa afya ya Jamii mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
 Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini. 
 Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini. 
Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini. 
 Mwenyekiti wa Kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Korogwe, Tanga (CHMT), Bw. Salim Bori (Kushoto) akijadili jambo wakati wa kikao cha majadiliano. Pembeni ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Bima ya Afya, Singida Bw. Issaya Shekifu akiwapa uzoefu jinsi wao walivyofanikiwa kwenye mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya CHF kwenda kwenye TIKA na Jinsi CHF inavyofanya vizuri wilayani Iramba kwa kauli mbiu ya "Kuku mmoja CHF na matibabu mwaka mzima. 
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (katikati) akijadiliana jambo na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia). Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Eastern Africa Business & Pleasure Networking Event” on Friday 28th March 2014 at Utalii College

$
0
0
unknown.jpeg


“Eastern Africa Business & Pleasure Networking Event” on Friday 28th March 2014 at Utalii College

Eastern Africa Professionals & Business Network (EAPBN) is a “Network” of “Positive Minded People” who believe that Africans can be successful & change for better. We believe we can make ourselves successful by using “the power of our brains” and also by “creating good businesses and social networks”.
The true Integration of East African Community will only happen when integration has already taken place at professional, business; social & grassroots level. This EAPBN network is about GIVING other than RECEIVING. There are lots to be done and we must utilize all resources to be successful. We believe that we are the source of positive development by giving out and not receiving. We also believe there is power in sharing.

Since 1st December 2013; EAPBN in collaboration with ConsNet Group has partnered with TBC1 to prepare and broadcast the “Wake-Up and Change” Motivational TV Programs which are aired for 1 hour at TBC1 every Sunday from 9.00 PM to 10.00 PM and repeated on Wednesdays from 2.00 PM to 3.00 PM.

The key objectives of these TV Talk Show Programs are as follows: to change people’s mentality on how to look into issues positively, motivate and inspire them; to provide answers to key common issues which needs solutions; to encourage people to take action and change instead of complaining and pointing fingers to each other as they customarily do; and also to provide a forum for positive changes discussions etc.
From the received feedback, the program has proved to have a positive impact across the East Africa countries and would now like to hold a regular networking event featuring the live “motivational talks” of various subjects to fulfil the demand.

In implementing its key objectives in fostering cooperation among the people of East Africa and other countries, EAPBN in collaboration with Consnet Group Limited would like to seek INVITE you for the: Weekly Business & Pleasure Networking Event featuring the Motivational Talks. The first talk is about: HOW TO BE SUCCESSFUL IN BUSINESS & WEALTH BUILDING. We plan the event to have an International Status.

The talks will be presented by two Motivational Speakers; Entrepreneurs; Business Owners & Consultants. The talks will be hosted by Sanctus Mtsimbe, the presenter of “Wake-Up & Change” Motivational TV Program and Rose Ndauka an Actress and has been planned to take place on Friday28th March 2014; from 6.30 PM. We plan the event to be repeating weekly every Thursday’s at Utalii College along Shaaban Robert/Samora Avenue.

The arranged music entertainment will feature international music, classics; jazz; slows; zouk, oldies with Leah Muddy  the former winner of Bongo Star Search accompanied by Wake-Up Dancers. The entrance fees will be TZS 35,000/= Per Person which will include audience one drink and bites.  Impressive dresses are encouraged. We have invited professionals and business people from Tanzania and all over East Africa and other countries to attend and we request and encourage you to invite your friends and other colleagues currently in Dar Es Salaam.

In this event Ladies  are strongly encouraged to attend to leverage business opportunities. All the participants are requested to bring their business cards to facilitate easy networking.

For tickets & confirmations call: +255 755 285 023 (amka@consnet.co.tz).

SITTA ATANGAZA MAJINA YA WENYEVITI NA MAKAMU WENYEVITI KAMATI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

$
0
0
N a Magreth Kinabo ,Dodoma
 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo (jana), ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.
 
 Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo  baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika  (jana) Machi 24 , mwaka  2014 mjini  Dodoma .
 
Mwenyekiti ametangaza majina haya baada ya kuunda kamati hizo  jana kwa mujibu wa kanuni ya 54 (1) ya kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014 ambazo zimetungwa chini ya kifungu cha 26 (1) cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83, ambazo zinataja kuundwa kwa kamati 12 za Bunge Maalum.  
 
Wenyeviti na makamu wenyeviti waliochaguliwa katika kamati hizo ni pamoja na  Kamati  ya Uandishi ambayo Mwenyekiti   amechaguliwa Mhe. Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni  Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni  Prof. Makame  Mbalawa
 
Wengine waliochaguliwa  katika Kamati Na. 2  ni  Shamsi Vuai Nahodha ambapo Makamu wake ni  Shamsa Mwangunga, Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni  Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma Mussa Juma.
 
Mhe. Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni  Christopher  Ole-Sendeka, Makamu wake ni  Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni  Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni  Assumpter  Mshama.
 
Waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti ni Stephen Wassira na Makamu wake ni  Dkt. Maua Daftari, Kamati Na. 7  Mwenyekiti  Brig. Hassan Ngwilizi  ,Makamu wake  Waride BakariJabu, Kamati Na. 8 Mwenyekiti   ni Job Ndugai,Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.
 
Hali kadharika Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh, Makamu wake Wiliam  Ngeleja, Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna  Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin, Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni  Anne  Malecela, Makamu wake  Hamad  Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti  niwake  Paul  Kimiti na Makamu wake ni  Thuwaybah E. Kisasi.
 
Aidha, kwa uchaguzi huo, Mhe. Sitta  alitangaza wajumbe wa Kamati ya  Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba ambao  ni wenyekiti wote wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua kwa mujibu wa Kanuni.
 
Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni pamoja na Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na Hamoud Abuu Juma. Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na kujitoa katika nafasi hiyo hivyo kufanya nafasi za uteuzi kuwa nne badala ya Tano .
 

WIZARA YA BISHARA ZANZIBAR YAPATA MSAADA KUTOKA WIZARA YA BIASHARA SMT

$
0
0
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Funguo ya Gari Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael,kushoto ni Elizabeth Lukaza Mchambuzi wa Shirika la UNDP Tanzania.Hafla imefanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Vifaa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael katika hafla iliyofanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael kulia akitoa neno la Shukran baada ya Makabidhiano ya Gari na Vifaa kwa Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula.

=========  =======  ======

Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Wizara ya Biashara na Viwanda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Gari na Vifaa vya Ofisini kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Wizarani Malindi mjini Unguja.

Msaada huo uliofadhiliwa na Shirika la Biashara la Dunia WTO ulitolewa ili kuijengea uwezo Wizara ya Biashara ya Zanzibar katika kukabiliana na majukumu yake ya kila siku.

Akikabidhi Msaada huo Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Bara Edward Sungula kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael amesema Suala la Biashara ya Kimataifa ni la Muungano hivyo Serikali mbili lazima zishirikiane na kusaidiana katika kutekeleza majukumu yao.

Amesema Msaada huo ni utekelezaji wa Mradi wa “Capacity Building for Trade Development and Integration Project” ambao una lengo la kuzijengea uwezo Serikali katika kutekeleza misaada chini ya utaratibu wa “AID FOR TRADE”.

 Ameongeza kuwa msaada huo ni mwanzo wa kudumisha ushirikiano katika kutekeleza mradi huo na njia ya kuendeleza kudumisha Muungano uliopo baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael ameishukuru Wizara hiyo juu ya Msaaada huo na kuongeza kuwa utachochea ufanisi katika majukumu yao.

Katika kutekeleza Mradi huo wa kukuza Sekta ya Biashara Tanzania Bara na Zanzibar Mradi umeanza kwa kununua Vifaa ambavyo ni pamoja na Gari mbili, Komputa, Projekta na Mashine ya Kuprintia.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

TANZANIA'S BUSINESS MOGUL MOHAMMED DEWJI ON INVESTING LOCALLY

$
0
0
Untitled 00
According to the World Bank, Tanzania's economy has been growing steadily for the last decade.One of the companies that has benefitted most from that growth is Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL).

Meeting the day-to-day needs of ordinary consumers, it makes products that range from cashew nuts to toothpaste, bicycles to soap.

And they are all gradually being united under one brand called "Mo" - named after the company's chief executive, Mohammed Dewji. The BBC's Lucy Hooker met up with him in Dar es Salaam.
To see the video click here http://www.bbc.com/news/world-africa-26692518

GLOBAL WOMAN OF THE YEAR 2013

$
0
0

Tuzo za The Woman Of The Year zinatarajiwa kutolewa Jumamosi wiki hii Machi 29, mjini Dodoma kuanzia saa 1:30 usiku ndani ya Ukumbi wa The African Dream. Hafla hii ni kwa wageni waalikwa na waheshimiwa wajumbe wa Bunge la Katiba, mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
P1130382
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza katika viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga kwenye warsha ya siku moja iliyokutanisha shule 10 za sekondari, vyuo na walimu kutoka katika shule na vyuo hivyo vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema Umoja wa Mataifa(UN) unalipa suala la elimu kipaumbele sana kwa wanafunzi hivyo kuwataka wanafunzi kuwa na malengo katika maisha yao kwa kusoma kwa bidii,kuepuka vishawishi vinavyopelekea kupata ujauzito wakiwa wanafunzi tena chini ya umri wa miaka 18.

Afisa habari huyo pia aLItumia fursa hiyo kuwatahadharisha wanafunzi wa kike kuepuka ngono kwani kwa mujibu wa utafiti wao takwimu zinaonesha kuwa vijana wa kike wenye umri wa miaka 15-19 wana uhusiano wa kingono na wanaume wanaowazidi miaka juu zaidi ya umri wao hivyo kuwepo kwa hatari ya kuambukizwa VVU na Mimba za utotoni.Kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra Manjerenga.(Picha zote na Malunde1 blog ya Shinyanga)
100_5397
Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Busurwa, Uhuru, Mazinge, Buluba, Chamaguha, Kizumbi, wakimsikiliza Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania (UNIC) Bi Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) ambaye alisema kwa mujibu wa sensa yao mwaka 2012 asilimia 65 ya Watanzania wote vijana wenye umri wa miaka chini ya 24,lakini pia asilimia 40 ya vijana wa kike wenye miaka chini ya 18 wanapata mimba za utotoni na wengine kuolewa katika umri huo.Aliongeza kuwa asilimia 23 ya vijana umri wa miaka 15-19 wameanza kuzaa na katika umri huo kati ya vijana wanne basi mmoja anaolewa ama kupata mimba.
P1130388
Wanafunzi wa vyuo vya VETA, MUCCOBS, Shycom , waliohudhuria katika warsha hiyo ya Umoja wa Mataifa wakimskiliza Afisa habari kutoka UN, (hayupopichani) ambaye aliwataka kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Umoja wa mataifa hapa nchini,lakini pia kuwaomba wazazi na walezi wa wanafunzi kujenga tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuwasaidia ili kuwafanya wapende elimu ili kufikia malengo ya Millenia.
100_5396
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) alisema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 52 ya vijana wa kike umri wa miaka 18-14 wameanza kufanya ngono na na asilimia 7 kwa wenye miaka 15-19 wanafanya ngono na wanaume wanaowazidi umri miaka 10 zaidi ,huku vijana wa kiume wakidaiwa kuanza kufanya ngono wakiwa na umri wa miaka 20, akatumia fursa hiyo kuwataka vijana kuepuka ngono kwani wakindekeza ngono UKIMWI upo na hawataweza kutimiza ndoto zao hivyo. Alisema Umoja wa Mataifa haupo tayari kuendelea kuona vijana hawatimizi malengo yao.
P1130428
Mjumbe wa asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Bw. Innocent akizungumzia kuhusu klabu za Umoja wa Mataifa katika shule za sekondari na vyuoni ambapo alisema miongoni mwa faida ukiwa mwanachama wa klabu hizo ni kupata taarifa nyingi tena kwa wakati kutoka UN kuwa karibu na umoja wa mataifa, kuhudhuria mikutano ya UN, kupata nafasi ya kusaidia jamii lakini pia kuwajengea uwezo wa aina mbalimbali kama vile kuongea mbele za watu,kuandaa ripoti,kupata vyeti n.k
P1130436
Walimu na wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika eneo la viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga ambapo maafisa kutoka Umoja wa Mataifa walieleza kazi za Umoja wa Mataifa na wakatumia muda fursa hiyo kuitaka jamii kubadilika na kuhamasisha jamii kufuata uzazi wa mpango ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kupiga vita suala la vifo vya akina mama wajawazito na watoto,mimba za utotoni ambapo watoto wa kike milioni 7.5 miaka chini ya 18 wanazaa kila mwaka.
P1130444
Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA), Bw.Moses Mongo akizungumza katika warsha eneo la Mazingira Senta mjini Shinyanga ambapo alisema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1964 kote duniani na ndiyo taasisi pekee hapa nchini yenye klabu nyingi yenye lengo la kuwaunganisha watu wa chini na Umoja wa Mataifa. Alisema hivi karibuni wamefungua tawi la taasisi hiyo mkoani Shinyanga na mwenyeki wake ni Bwana Ezra Manjerenga. Mosea Mongo alitumia fursa hiyo pia kuwataka wanafunzi na wanajamii kwa ujumla kubadilika na kwamba mabadiliko yanaanza kwa kutenda na wafanye kazi kwa malengo ili kuleta mabadiliko katika jamii.
P1130455
Bi Usia Nkhoma Ledama akieleza kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa hususani malengo ya millenia kama vile kuhamasisha Afya ya Uzazi, Haki za Binadamu, kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi, umaskini, kuhamasisha Amani na Chakula kwa wenye njaa. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Anna rose Nyamubi ambaye alikuwa mgeni rasmi.
P1130452
Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Annarose Nyamubi katika warsha hiyo iliyokutanisha shule 10 za sekondari na vyuo vitatu vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga. Katikati ni Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Harriet Macha na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Anna rose Nyamubi.
P1130457
Mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Anna rose Nyamubi, ambaye ni mdau wa maendeleo na mwanafamilia wa Umoja wa Mataifa (siku za nyuma aliwahi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa katika shirika la UNICEF), alisema nchi ya Tanzania inatekeleza malengo ya millenia kupitia ilani ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi wake hususani katika kupunguza umaskini.
Katika hatua nyingine Bi. Nyamubi aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa mataifa. Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kuwa serikali inawajali vijana hivyo kuwataka kusoma kwa malengo kwani bila elimu dunia itawaacha na kuwataka kuacha kutegemea wazazi wao kwamba watarithi mali.
Aidha Nyamubi alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi ambao hawajapeleka watoto wao kidato cha kwanza wawapeke haraka kabla ya kuwachukulia hatua.
P1130353
Mapema kabla ya warsha Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha ambapo alisema lengo la ziara yao ni kuhamasisha uanzishwaji wa klabu za Umoja wa Mataifa na kutoa elimu kuhusu shughuli za Umoja wa Mataifa ambapo huwa wanatembelea shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali kuwaelimisha kuhusu ajenda za Umoja wa Mataifa.
P1130376
Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA), Bw. Moses Mongo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema shule hiyo ni miongoni mwa shule chache zilizopata bahati kutembelea na Umoja wa mataifa na kuwataja miongoni mwa watu ambao ni mazao ya klabu za Umoja wa Mataifa kuwa ni Zitto Kabwe na John Mnyika.Alisema klabu za Umoja wa Mataifa zinawajengea wanachama wake ujasiri pamoja na kuwafundisha mambo mbalimbali kama vile elimu ya ujasiriamali.
P1130361
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Chamaguha wakinyoosha mikono kwamba wako tayari kuwa na klabu ya Umoja wa mataifa katika shule yao baada ya kuridhishwa na maelezo kutoka Umoja wa Mataifa hapa nchini wakiongozwa na Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa Tanzania (UNIC)Bi. Usia Nkhoma Ledama.
P1130367
Awali katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga ,ambako maafisa wa Umoja wa Mataifa walifanya ziara yao, Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UNIC) Bi. Harriet Macha akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambao wamedhamiria kuanzisha klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule hiyo ambayo itaundwa na wanafunzi kuanzia 10 na kuendelea .Hapo anaonesha vitabu na vipeperushi mbalimbali vinavyohusu Umoja wa Mataifa ambao ulianzishwa mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia.Hivi sasa Umoja wa Mataifa una nchi wanachama 193 duniani kote na nchi 3 pekee siyo nchi wanachama wa Umoja huo, nchi hizo ni Taiwan,Cossovo na Vatican.
100_5382
Ni katika ofisi ya walimu katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga,muda mchache tu baada ya maafisa kutoka Umoja wa mataifa kuwasili katika shule hiyo kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo. Aliyesimama ni kaimu mkuu wa shule hiyo bwana Malongo Maganga akiwakaribisha wageni hao ambapo aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuwafikia na kufurahishwa na mpango wake kuhusu elimu ya uzazi wa mpango kwa wanafunzi kwani itawasaidia kuongeza uelewa na kujilinda zaidi ili kutimiza malengo yao.Alisema jamii inaamini kuwa elimu hiyo ni kwa ajili ya akina mama pekee.

Aidha mwalimu Maganga alisema tayari shule yake imefungua faili kwa ajili ya klabu ya Umoja wa Mataifa kwa wanafunzi wa shule hiyo.(Picha zote na Malunde1 blog ya Shinyanga)

ASILIMIA 25 YA WANAWAKE WAKO HATARINI KUPATA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa T-Marc Tanzania Diana Kisaka akizungumza na wadau kuhusu majukumu ya T-Marc.
 Mkurugenzi Mtendaji wa T-Marc Tanzania Diana Kisaka akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu, mgeni rasmi wa uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu huduma za uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi uliondaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya T- Marc Tanzania katika mkutano na wadau mbalimbali wa afya mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Veta.
 Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu huduma za uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi uliondaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya T- Marc Tanzania katika mkutano na wadau mbalimbali wa afya mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Veta. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu
========  =======  ========
ASILIMIA 25 YA WANAWAKE WAKO HATARINI KUPATA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI.

Na Denis Mlowe,Iringa

IMEBAINIKA asilimia 25 ya wanawake nchini Tanzania wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Saratani ya shingo ya Uzazi katika maisha na kusababisha vifo kwa wanawake nchini.

Kwa mujibu wa takwimu asilimia 80 ya wagonjwa wanaogundulika na aina hii ya saratani hugundulika katika hatua kubwa ya ugonjwa ambapo hakuna tiba wala kinga.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu huduma za uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi uliondaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya T- Marc Tanzania katika mkutano na wadau mbalimbali wa afya mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Veta.

Alisema asilimia kubwa ya wanawake nchini Tanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuangalia afya zao na kupima saratani ya shingo ya uzazi kuweza kubaini kama wameathirika na kupata matibabu mapema.

Wamoja alisema takwimu kutoka taasisi ya Saratani ya Ocean Road inaonyesha kati ya wagonjwa wa saratani wanaopelekwa katika taasisi hiyo kila mwaka zaidi ya wagonjwa 5000 wanatatizo la saratani ya shingo ya kizazi.

“Kwa kutambua hilo serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii inafanya juhudi mbalimbali katika kupambana na saratani ya mlango wa uzazi kwa wanawake kwa sababu saratani ya mlango wa kizazi inatibika ila tu ili iweze kutibika ni muhimu kwanza igundulike katika hatua zake za awali” alisema Ayoub

Aliongeza kuwa wataalamu wa mambo ya saratani wamegundua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya saratani ya mlango wa kizazi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Alisema kutokana na tatizo la saratani ya mlango wa kizazi mkoani Iringa serikali imewataka wadau mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono ili kuhakikisha wanawake wanakuwa salama kutokana na tatizo hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa T- Marc Tanzania,Diana Kisaka alisema kuwa kila mwaka wanawake 6000 hugundulika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi Tanzania.

Alisema wanawake 4000 wa kitanzania hufa kila mwaka kutokana na saratani ya mlango wa kizazi sawa na wanawake 11 wanaofariki kila siku nchini kutokana na tatizo hilo.

Kisaka alisema takwimu za hospitali ya Ocean Road zinaonyesha asilimia 40 ya vifo vinatokana na matatizo ya saratani ni wagonjwa saratani ya mlango wa kizazi.

“Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wote wanaokwenda kwenye matatibu ya saratani ya shingo ya uzazi hufanya hivyo wakiwa wamechelewa, hii ina maana kuwa wagonjwa hawa hutafuta huduma za tiba wakati saratani yao tayari imefikia kiwango ambacho haiwezi kutibika” alisema Kisaka.

Alisema  ugonjwa  wa Saratani ni  tatizo kubwa sana ulimwenguni na hasa katika nchi zinazoendelea ambapo takwimu  za kimataifa zinaonyesha kuwa kila mwaka zaidi ya watu  milioni 5 hugundulika kuwa na saratani na kufanya tatizo  hilo  kufikia asilimia 29 huku kati yao hupatikana na saratani ya mlango  wa kizazi na kwa bahati mbaya Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye tatizo kubwa la ugonjwa  huo
 
Alisema moja ya sababu zinazochangia tatizo la saratani ya shingo ya uzazi ni ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu umuhimu wa watu kuchunguza afya zao mara kwa mara, Imani potofu na kukosa taarifa halisi kuhusu saratani na matibabu ya mionzi.

Kisaka alisema kwa kutambua tatizo hilo T-MARC  kama asasi  isiyo kuwa  ya  kiserikali ambayo inajishughulisha na uboreshaji  wa afya ya watanzania  kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara   ya  Afya na  ustawi wa jamii pamoja na wadau mbali mbali wa sekta ya  umma ,sekta binafsi ,wadau wa  kimataifa ,asas za kijamii na watanzania wote kwa ujumla  kwa kuanza  kupambana na tatizo  hilo.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE (DENGUE FEVER)

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI TEMEKE LEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajasiliamali-VICOBA mbalimbali katika mkutano uliofanyika mapema leo asubuhi  ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,katika Wilaya ya Temeke.Kinana aliwapongeza VICOBA hao kwa kuchapa kazi nzuri na kuwa waaminifu katika mazingira yao ya kufanya kazi.Aidha amewataka akina mama na vijana mbalimbali kutobweteka na badala yake wajitume kufanya kazi,katika suala zima la kujipatia maendeleo yao sambamba na kujikwamua na Umaskini.Ndugu Kinana amefanya ziara yake leo ya siku moja ndani ya Wilaya ya Temeke,ikiwa na lengo la Kuimarisha Uhai wa Chama hicho na kuhamaisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtemvu akielezea namna alivyoweza kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali katika kuunda VICOBA kwa ajili ya Maendeleo yao,katika Wilaya ya Temeke mapema leo wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokutana na VICOBA hao alipokuwa kwenye ziara yake ya siku moja wilayani humo.
Wana-VICOBA wakifuatilia mkutano 
 Meneja Mradi wa kiwanda cha kuzalisha gesi kilichopo kata ya Mtoni,Bwa.Richard Matari akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipotembelea mradi huo na kujionea hali halisi ya eneo hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi huo wa kuzalisha gesi na changamoto zake,Kiwanda hicho mpaka sasa hakifanyi kazi kutokanana kukumbwa na changamoto mbali mbali na kupelekea kusimama kutofanya kazi mpaka sasa. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Mkuu wa Mkoa,Mh.Meck Sadicky wakikagua mitambo ya kuzalisha gesi inayotokana na taka taka,kilicho Mtoni,wilayani Temeke.Kinana yuko ziarani wilayani humo kwa siku moja.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtevu akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa,Mh.Meck Sadicky nje ya ofisi za CCM,wilaya ya Temeke mapema leo asubuhi wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipoanza ziara yake wilayani humo.
 Katibu Mkuu wa CCM,akiwasili kwenye ofisi za CCM,wilaya ya Temeke mapema leo,ambapo alikutana na kamati ya siasa ya wilaya na kupewa taarifa kamili ya hali ya kisiasa ya wilaya hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipunga mkono kwa wananchi waliokuwa pembeni (hawaonekani pichani)  mapema leo asubuhi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar,Ramadhan Madabiba wakiwa ndani ya bajaji (hawaonekani),wakielekea kwenye mkutano mfupi wa kukutana na wajasiliamali-VICOBA,ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,wilayani Temeke.Kinana yupo wilayani humo kwa ziara ya siku moja.
 Baadhi ya akina mama mbalimbali waliojiunga kwenye VICOBA wakishangilia jambo,wakati wa mkutano mfupi uliowakutanisha na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,ambaye alizungumza nao na kuwatia moyo katika juhudi zao mbalimbali za kupambana na kujikwamua na lindi la umaskini.Kinana aliwaasa VICOBA hao kutobweteka na badala yake wafanye kazi kwa bidii na kujitegemea bila ya kusubiri ajira. 
 Mkutano ukiendelea
 Mwakilishi wa VICOBA wilaya ya Temeke,Mariam Temela akisoma hotuba yake fupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo asubuhi  katika Wilaya ya Temeke wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15 uliojumuisha VICOBA mbalimbali (hawapo pichani). 
 Mwakilishi wa VICOBA wilaya ya Temeke,Mariam Temela akikabidhi hotuba yake fupi aliyoisoma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo asubuhi  katika Wilaya ya Temeke wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15 uliojumuisha VICOBA mbalimbali. 

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA YA NJE WA UJERUMANI DKT FRANK-WALTER STEIMEIER IKULU LEO

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo ya faragha (tete-a-tete ) huko Ikulu tarehe 25.03.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe wakipiga  picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na ujumbe aliofuatana nao wakati wakipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na baadhi  ya viongozi aliofuatana nao wakati walipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonyesha wageni wake jengo la ikulu sehemu iliyojengwa na Wajerumani (jengo halionekani pichani) mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dkt. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani Mheshimiwa Phillip Marmon na  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah Msechu.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu kwa mazungumzo  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier. Waziri huyo aliwasili nchini tarehe 25.3.2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.PICHA NA JOHN  LUKUWI.

WASANII WA BONGO MOVIE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA MABIBO BEER WATEMBELEA HOSPITALI YA MWANANYAMALA LEO NA KUTOA MISAADA KWA WAGONJWA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax, Mama Benadetha Rugemalila akikabidhi baadhi ya misaada kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi wakati Kampuni ya Mabibo Beer wakishirikiana na Wasanii wa Bongo movie walipotembelea Hospitali ya Mwanyamala ikiwa wanaadhimisha miaka mitatu ya Kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa Mabibo beer na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala mara baada ya wasanii wa bongo movie na Kampuni ya Bia ya Mabibo kutembelea na kukabidhi misaada katika hospitali ya Mwananyamala mapema leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila(kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada katika Hospitali ya Mwananyamala leo, Katikati ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Tanzania.
 Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi (kulia) akitoa maelekezo kwa Wasanii wa bongo movie pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila (pili kulia) ambao ndio wauzaji na wasambazaji wa Vinywaji vya Windhoek na Climax wakati walipotembelea Hospitali ya Mwananyamala leo kwaajili ya kutoa Misaada mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movies huku Kampuni ya Mabibo Beer ikiwa wadhamini wakuu wa Bongo Movie.
 Wasanii wa bongo movie wakielekea kwenye wodi za wagonjwa katika hospitali ya mwananyamala mapema leo kwaajili ya kutoa misaada kwa wagonjwa wakati bongo movie wakiadhimisha kilele cha Miaka 3 tokea kuanzishwa kwake.
 Bi Sada Abasi (kushoto) akipokea misaada kutoka kwa mmoja wa wasanii wa bongo movie ambao walitembelea hospitali ya Mwanyamala leo ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Msanii wa Bongo Movie Sandra (kulia) akikabidhi misaada kwa mmoja wa wagonjwa waliopo kwenye Hospitali ya Mwananyamala wakati wasanii wa bongo movie kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo Beer wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo.
 Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bw Steve Nyerere (kushoto) akisisitiza jambo kwa Wasanii wa Bonngo movie wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.
 Jackline Wolper (katikati) akimsaidia Mmoja wa wagonjwa waliopo kwenye hospitali ya Mwananyamala wakati wasanii wa bongo movie walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo.
 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na Waandishi wa habari wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo na kukabidhi misaada ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
 Shamsa Ford akiongea na Waandishi wa Habari.
............................................
Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa Vinywaji vya Windhoek na Climax kwa kushirikiana na Wasanii wa Bongo Movie leo wametembelea hospitali ya Mwananyamala ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie ambapo Kampuni ya Mabibo Beer wakiwa wadhamini wakuu wa Bongo Movie kwenye kilele cha Kuadhimisha Miaka Mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.

Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw Steve Nyerere Wameweza Kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala ikiwa wanadhimisha Miaka mitatu ya Kuzaliwa Kwa Bongo Movie.

Misaada iliyotolewa leo na Wasanii wa Bongo Movie kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo Beer ni Mabeseni ya Kuoshea watoto wadogo, pampers, sabuni na mafuta ya kujipaka.

Kampuni ya Mabibo Beer ndio wadhamini wakuu wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kudhaliwa kwa klabu ya Bongo Movie ambapo kilele chake kitafanyika katika Ukumbi wa Arcade East 24 uliopo Mikocheni ambapo kutafanyika bonge la Sherehe huku FM Academia, Banana Zoro Band, na Msanii Shilole watatoa Bonge la Burudani

Benki ya NBC yakabidhi zawadi ya gari kwa mshindi wa kampeni ya Weka Upewe

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi Mzinga Melu (kushoto) akikabidhi zawadi ya gari jipya aina ya Suzuki Swift kwa Bi. Mary Malifedha Popote mkazi wa Kigoma, aliyeibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe iliyokuwa ikiendeshwa na NBC. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow, Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale. Gari hilo lina thamani ya dola za kimarekani 17,000.  
 Mshindi wa gari wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Mary Malifedha Popote akifungua mlango wa gari lake baada ya kukabidhiwa. Nyuma yake ni    Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. Mzinga Melu.
Mshindi wa gari wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Mary Malifedha Popote akiwasha gari lake jipya aina ya Suzuki Swift tayari kwa safari ya kwenda Kigoma. 
=======  =====  ======
NBC HANDS OVER THE WEKA UPEWE GRAND PRIZE
MD’s Talking Points.
  
We are handing over the WEKA UPEWE Grand prize to our winner.
The draw was done in February and Ms Mary Malifedha Popote from Kigoma emerged the grand winner.

It took more than 3 weeks to hand over the prize as we have to make sure that we have all the ownership documents done and arrange bringing the winner to Dar es Salaam to receive her prize.

Ms. Mary Malifedha Popote closed the number of winners to 13 making us feel excited being able to change 13 Tanzanians’ lives. All the other prizes have been handed over to the winners and today we are handing over the car to the owner. We believeit will change her life through solving her transport issues or even uses the car as a means of extra income to support her families.

The NBC Weka Upewe campaign was intended to benefit all customers who have Malengo savings accounts and for any customer who will open a new fixed deposit.  Any NBC customer who deposited any amount starting from TZS 50,000 into his/her NBC Malengo account, or anyone who opens a Malengo account and or Fixed Deposit account with NBC and deposit TZS 50,000 or TZS 1,000,000 or more respectively got an opportunity of winning a generator, a motorbike or  a brand new car won today.
   

MGOMBEA WA AFP CHALINZE RAMADHANI MGAYA AJINADI KWA WANANCHI

$
0
0
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha AFP, Ramadhani Mgaya akinadiwa na  Mkurugenzi wa habari na uenezi wa AFP kitaifa, Mwalami Uwesu wakati wa kampeni za mgombea huyo katika ebneo la sokoni Chalinze mjini Kata ya Bwilingu Chalinze.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha AFP, Ramadhani Mgayaakijinadi kwa wananchi wa jimbo la Chalinze wakati wa kampeni zake za kuwania Ubunge jimboni humo.

BENKI YA NIC ARUSHA YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO WA SHULE MAALUM YA DYMPHNA ILIYOPO SAKINA KWA IDD

$
0
0
 Meneja wa benki ya NIC Mbuche Mgawa  wa nne kulia akipokea maelezo kutoka kwa bibi Mary Robert Kaswende meneja wa kituo cha Dymphna Special school iliyopo sakina kwa idd mara baaada ya kuwasili shuleni hapo.

 Watoto wa shule maalum ya Dymphna wakiwasikiliza wageni ambao ni wafanyakazi wa benki ya NIC
 Watoto wa shule hiyo wakiwa wamebeba bango la kutoa shukrani kwa benki ya NIC
Watoto wa shule hiyo wakiwa wamebeba bango la kutoa shukrani kwa benki ya NIC, na BENKI YA NIC wakiwa pamoja na misaada waliyobeba na watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara ya kuwatembelea kituo hichon ambvacho ni maaalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo.

SERIKALI YA UJERUMANI KUTUMIA EURO MILIONI 10 KUKARABATI RELI YA KATI

$
0
0
DSC_0072
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Membe alilisisitiza kwamba ziara ya Waziri mpya wa mambo ya nje kutoka Ujerumani ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa sababu amekuja na wawekezaji 65 kutoka maeneo mbalimbali.

Amesema kuwa ukarabati wa reli ya kati ni muhimu katika kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili kwa maslahi ya watu wao. “reli ya kati kama mnavyojua ilijengwa na Wajerumani mwaka 1913 na kwa sasa ina miaka karibu mia moja na kitu,” aliongeza Waziri Membe.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Steinmeier amesema kuwa nchi yake itaendelea kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na Tanzania katika jitihada za kuharakisha maendeleo ya nchi na watu wake. Amesema kuwa serikali ya Ujerumani imeamua kukarabati reli ya kati katika jitihada za kukumbuka na kudumisha historia ya muda mrefu kati ya nchi hizo mbili. “najisikia furaha na faraja kuona nchi yaTanzania inapiga hatua mbele kimaendeleo baada ya uhuru wake,” amesema
DSC_0096
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa kihistoria na kiuchumi kati ya Tanzania na Ujerumani jijini Dar es Salaam.
DSC_0112
Baadhi ya wageni waalikwa na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani nchini.
DSC_0043
Sehemu ya waandishi wa habari nchini pamoja na waandishi kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo leo jijini Dar.
DSC_0116
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akiuliza swali wakati wa mkutano huo.


DSC_0122
Waziri Membe na mgeni wake wakiondoka kwenye chumba cha mkutano kuelekea Ikulu kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
DSC_0001
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini, Dkt Frank-Walter Steinmeier wakiwasili kwenye chumba cha mkutano kuzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa MObog).

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
SERIKALI ya Ujerumani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imeahidi kutumia zaidi ya Euro milioni 10 kukarabati reli ya kati (Central Line Railway). MOblog inaripoti.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini, Dkt Frank-Walter Steinmeier, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe amesema serikali ya Ujerumani imekubali kwa dhati kabisa kukarabati reli ya kati kwa manufaa ya Tanzania na nchi jirani.

“kwa sasa siwezi kusema ukarabati utaanza lini na jina la mwekezaji kwa sababu mazungumzo yanaendelea lakini kwa hakika kabisa tumeshakubaliana kwenye jambo la ukarabati wa reli ya kati,” amesema Waziri Membe.

Amesema reli ya kati itapunguza matumizi ya barabara kwa mizigo na barabara za nchi zitakuwa salama na kuongeza tija katika Nyanja za biashara kupitia soko la pamoja Afrika Mashariki na kati.

MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya jana Mjini Matai. 

Katika salamu zake za ufunguzi alizitaka halmashauri Mkoani Rukwa kuhakikisha kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyake vyote vya maamuzi, Aidha alizitaka Halmashauri ziandae utaratibu wa kuzitambua familia zisizo na uwezo wa kuchangia na zitenge fedha kutoka katika vyanzo vyake ili kuzilipia familia hizo na kuhakikisha kuwa hakuna mkazi wa Halmashauri husika anapoteza maisha kwa kukosa fedha za kuchangia katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mwanachama wa mfuko huo anatakiwa kuchangia Tsh 10,000/= kwa mwaka ambao ni mchango wa kaya moja isiyozidi watu sita.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Filbert Ngaponda (Mwana wa Magreth) akiwatambulisha washiriki wa Mkutano huo wakiwepo watendaji wa Serikali na madiwani wa halmashauri hiyo pamoja na wageni mbalimbali waalikwa ambao ni wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (CHF).  
Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo (NHIF) wakiwa katika Mkutano wa kujadili umuhimu wa wa huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na kuangalia namna ya kuzindua rasmi mpango wa kuchangia kabla ya kuugua katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia washiriki wa mkutano huo.


Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Hamza Temba wa pili kushoto akiwa na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NHIF) Mkoa wa Rukwa mara baada ya Mkutano huo.
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Rukwa wakijadili jambo kuhusiana na huduma za mfuko huko. Kulia ni Ramadhan Juma Ofisa Habari Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo, Hamza Temba Ofisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na Ndugu Mussa Hajj Chewa Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo
Picha ya Pamoja ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, viongozi wa Serikali, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Watumishi wa ofisi hiyo Mkoa wa Rukwa.  (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII YA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE YAPITISHA MPANGO WA TIBA KWA KADI

$
0
0

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (Kulia) akichangia mada wakati wa wa kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). 

Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kuendesha kikao hicho, Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi (katikati) na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).

Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi akiendesha kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). 

Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) wakati wa kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). 

Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kuendesha kikao hicho, Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).



 Mwenyekiti wa Vibindo, Gaston Kikuwi akiongoza ni Wajumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) kutoa pongezi wa waheshimiwa madiwani kuweza kupokea kwa mikono miwili mpango wa Tiba Kwa Kadi (TIKA).
Wajumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Wajumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Waheshimwa Madiwani wakifuatilia kwa makini kikao hicho, toka kulia ni Diwani wa Kata ya Kwamsisi, Mheshimiwa Nassoro Hassan, Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Mji Korogwe, Mheshimiwa Neema Isack pamoja na Diwani wa Kata ya Magunga, Mheshimiwa Mariam Ngonyani (Mama Maji Marefu).
Mratibu wa Ukimwi (CHAC) wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT), akichangia mada. 

Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Mji Korogwe, Mheshimiwa Neema Isack akitoa msimamo wake katika mada iliyokuwa ikijadiliwa.
Diwani wa Kata ya Kwamsisi, Mheshimiwa Nassoro Hassan akiongea machache wakati akichangia mada. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale.
Diwani wa Kata ya Kwamsisi, Mheshimiwa Nassoro Hassan akiongea machache wakati kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni Afisa Matekelezo na Uratibu wa Bima ya Afya, Singida Bw. Issaya Shekifu (kushoto) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Mwenyekiti wa Vibindo, Gaston Kikuwi akijadili jambo na Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Mji Korogwe, Mheshimiwa Neema Isack.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images