Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 254 | 255 | (Page 256) | 257 | 258 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel (kushoto) akishikana mikono na Mkurugrenzi wa Kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman baada ya kuzindua  Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo Wilayani  Bagamoyo, Pwani .  Anayeangalia ni,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali.

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman. 
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali alizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo iliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani .  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala, Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel na Mkurugenzi wa 4Beli, Giulbert Herman.
  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf  Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo katika uzinduzi wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 4Beli, Deogratius Soka (kulia) akisoma hotuba wakati wa uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
  Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi. 

  0 0


   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Kamanda wa vijana UVCCM Bw Agrey Marealle Akila kiapo cha utii kwa CCM wakati wa kusimkwa kuwa Kamanda wa vijana wa CCM wilayani humo mbele ya mgeni rasimi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Bw Agrey Marealle akiwa amekalishwa kwenye kigoda huku akiwa na ngao na mkuki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa vijana UVCCM wilayani humo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
   Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimvalisha kofia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle kuwa Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani humo Mjini katika halya iliyofanyika viwanja vya CCM katab ya Njoro.
  Mkamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimkabidhi mkuki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle katika hafla ya kumsimika kuwa Kamanda wa Vijana wa UVCCM wilayani humo katika sherehe ya kumsimika iliyofayika katika viwanja vya CCM kata ya njoromjini humo.
  =======  =======  =======
  Marealle apewa tena Ukamanda wa Vijana wa CCM Moshi Mjini
  *Ahimiza mshikamano kwa wanaCCM

  MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kupitia Moshi  Mjini, mkoani Kilimanjaro, Aggrey Marealle, amesema mshikamano   miongoni mwa wanachama wa chama hicho ndiyo pekee utakaopelekea chama    hicho kufanya vyema katika chaguzi zijazo.  Bw. Marealle aliyasema hayo juzi mjini Moshi, wakati wa hafla ya
  kusimikwa kwake kama kamanda wa vijana wa umoja wa vijana wa CCM,
  (UVCCM), wa wilaya ya Moshi Mjini  kwa kipindi cha pili cha miaka
  mitano, hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa tawi la wakereketwa
  la Marealle lililopo Kata ya Bondeni, Moshi Mjini.

  "Changamoto kubwa ambayo CCM imekuwa ikikumbana nayo nyakati za
  kuelekea chaguzi mbali mbali ni kutokuwa na mshikamano jambo ambalo
  mara nyingi hutokana na makundi ndani ya chama, ni vyema tukaepuka
  hili na msamiati wetu mpya uwe ni mshikamano, hapa tutashinda",
  alisema.

  Aidha alitoa wito kwa wananchi hususan wanachama wa CCM kutokutumia
  changamoto za kimaisha walizonazo kama sehemu ya maamuzi katika 
  kuchagua viongozi na mstakabali mwingine wa kisiasa.

  Katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la wakereketwa, Bw. Marealle
  alisema kada ya vijana ni nguzo ya Taifa ambayo haina budi kulindwa
  kwa kuhakikisha maswala yanayowahusu yanapewa kipaumbele ili wasikate 
  tamaa.

  Akihutubia katika hafla hiyo ambayo ilienda sanjari na kusimikwa
  makamanda wapya wa UVCCM Kata zote za Moshi Mjini, Makamu Mwenyekiti    
  wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, alisema kuwa kazi kubwa ya makamanda wa    
  vijana wa CCM ni kuwaunganisha vijana, kubaini kero zao na  
  kuzishughulikia kwa wakati.

  Bi Mhita alielezea kazi zingine kuwa ni pamoja na kuwasaidia vijana
  kupata ajira za zikiwemo zile za kujiajiri wenyewe pamoja na kutoa
  ushauri kwa vijana unaohusiana na mwelekeo wa kisiasa na kimaisha kwa
  ujumla.

  "Kwa kufanya hivi mtakuwa mnaweka nguzo imara ya Taifa kwa ajili ya
  miaka mingi ijayo", alisema na kutoa wito kwa vijana kuwa tayari
  kupokea ushauri watakaopata kutoka kwa makamanda hao wapya wa vijana.

  Aidha aliwaasa vijana kuiepusha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja
  na anasa zilizopitiliza ambapo alisema mambo hayo yanachangia kwa
  kiasi kikubwa kupunguza ari na nguvu kazi ya Taifa.

  0 0
 • 03/23/14--04:14: Article 3
 • KIKOSI CHA UOKOAJI TANAPA CHAMNASUA MTALII ALIYEKWAMA KILELENI MAWENZI KILIMANJARO

  Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.

  Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia njia maalum ya uokoaji na kufika katika Lango Kuu la Marangu saa nne na nusu usiku.

  Hali ya hewa ilisababisha helikopta maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa kuwa mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.
  Hivi sasa mtalii huyo pamoja na muongoza wageni wake bado wapo chini ya uangalizi wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours iliyomleta mgeni huyo.

  Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza sababu zilizowafanya kuchepuka njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.

  Imetolewana Idara ya Mawasiliano
  Hifadhiza Taifa Tanzania
  23.03.2014

  0 0


  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) na kuwaasa kutumia kalamu vizuri hasa katika kipindi hiki cha uandaaji wa katiba mpya kwa maslahi ya Taifa, kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
  Mhadhiri katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dkt. Ayoub Rioba akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) na kueleza kuhusu umuhimu wa Vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uandaaji wa katiba mpya, Kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwalimu Bashiru Ally akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) na kuwaasa kutumia nyenzo zote ikiwamo Rasimu ya Katiba, Hotuba ya Mh. Rais Jakaya Kikwete hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika upatikanaji wa katiba mpya. kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari  ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa habari Hawapo Pichani) na kuwaasa wananchi kuwa na umoja hasa katika kipindi hiki cha upatikanaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya Taifa na Wananchi kwa Ujumla. kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari                      ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
  (Picha na Hassan Silayo)

  0 0

    Mtaalamu wa Hali ya Hewa Bw. Hassan Khatib Ame akitoa ufafanuzi wa kitu kwa wanafunzi wa Skuli ya Kombeni walipotembelea Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa iliopo ndani ya Uwanja wa ndege wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyo adhimishwa leo.
   Afisa Usalama wa Anga Bw. Rashid Omar Mselem akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani kuhusiana na usalama wa Anga na Hali ya Hewa pindi inapokuwa mbaya, katika kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani.
   Wanafunzi wakipata maelezo juu ya upimaji wa Hali ya Hewa kwa Mtaalamu wa Hali ya Hewa Bw. Khamis A. Salum. 
   Wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mtabiri wa Hali ya Hewa (hayupo pichani) Bw. Hafidhi Juma Bakari walipofika ofisini kwake Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo march 23/2014.
   Mtabiri wa Hali ya Hewa Bw. Hafidhi Juma Bakari akifafanua kitu kwa wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani walipofika ofisini kwake kwa ziara ya kimasomo na kusherehekea siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoadhimishwa leo Duniani kote. 
   Mkurugenzi Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar Bw. Muhammed Khamis Ngwali (wakatikati) waliosimama akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani.
  Mkurugenzi Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar Bw. Muhammed Khamis akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwenye picha ya pamoja katika kusherehekea siku ya Hali ya Hewa Duniani. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  ======  =======  ========
  Na Miza Kona   - Maelezo Zanzibar            

  Wanafunzi wa vyuo na sekondari wameitaka jamii kuwa na mwamko wa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa pamoja na kutembelea vituo hivyo ili kuweza kujua na kupata taarifa za mwenendo wa hali ya hewa Nchini.

  Kauli hiyo wameitoa leo huko katika ofisi za Mamlaka hiyo ziliopo Uwanja wa Ndege Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani, wamesema jamii imekuwa haina mwamko mzuri katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa nchini.

  Wamesema kuwa kila siku jamii inatakiwa kujua na kufuatilia taarifa hizo ili kuweza kufahamu hali ya hewa ilivyo ili kuepukana na majanga na matatizo yanaweza kutokea ambapo mamlaka hiyo hutoa taarifa. Aidha wanafunzi hao wamewataka wanafuzi wenzao kutembelea katika vituo vya Mamlaka hiyo kwenda kusoma kwa vitendo na kuona shughuli hizo zinavyotolewa.

  Wanafunzi hao wametembelea sehemu mbali mbali na kuona jinsi shuguli za kituo hicho zinavyofanyika ikiwepo sehemu ya usalama wa Anga, kipima joto, kipima mvua, kipima upepo, pamoja  utabiri wa hali ya hewa.


  Wakitoa maelezo kwa wanafunzi maafisa mbali mbali wa Mamlaka hiyo wamesema kuwa huduma nyingi zinazoendeshwa nchini huwa zinashirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa taarifa za hali ya hewa ili kuendesha kazi zake.
  Wamefahamisha Mamlaka ya Hali ya Hewa hushirkiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege jinsi ya kuingia kutoka kwa ndege nchini na namna ya kuwasiliana katika uendeshaji shughuli wa zake.
  Aidha wamefahamisha kuwa Mamlaka hutoa taarifa zake kwa kutumia vipimo mbali mbali viliopo nchini vikiwemo kipima ju, kipima upepo pamoja na kipima mvua na kutoa taarifa jamii jinsi ya hali ya hewa ilivo na itakavyokuwa nchini.    

  Nae  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mohammed Khamis Ngwali , amesema vijana wanatakiwa kubadilika na kuchukua tahadhari za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kizazi kijacho kiweze kufaidi dunia yenye mazingira bora.

  Hata hivyo  Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana katika kujihisha na  masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa na hatua za kuchukua katika kipindi cha hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

  Amesema hatua hii muhimu ikichukuliwa na vijana italeta ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho kwa kujenga jamii iliyo imara baadae pamoja na kuokoa dunia  kwenye majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini.

   Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 23 Machi, kauli mbiu ya mwaka huu ni ushirikishwaji wa vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizindua mradi wa maji kwenye kijijicha Chididimo manispaa ya Dodoma leo, wengine ni wajumbe wa chombo huru cha watumiaji maji kijijini hapo.
   Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasha mashine ya kusukuma maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo manispaa ya dodoma muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo.
    Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akizungumza na  viongozi pamoja na  wananchi wa kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma kuulinda na kuutunza mradi wa maji kijijini hapo muda mfupi mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuuzindua mradi huo leo.
    Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) na katibu tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge wakifungua na kukinga maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi huo mapema leo hii. Wanaoshuhudia ni wananchi wa kijiji cha Chididimo.
    Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akimtwika ndoo ya maji mdala Morleni Mwaluko mmoja wa wanakijiji cha chididimo, maji hayo safi kwa  sasa yanapatikana kwa urahisi na kwa karibu  kijijini hapo baada ya kukamilika kwa  mradi wa maji wa kijiji hicho, mkuu wa MKOA dodoma amezindua mradi huo mapema leo hii.
   Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Chididimo waliojitokeza kumlaki alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji kijijini hapo, mapema leo hii.
   Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi(kushoto) akipokea taarifa ya mradi wa maji kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma kama inavyowasilishwa kwake na mhandisi Mohamed Khali ( Kulia)  kutoka idara ya maji manispaa ya Dodoma wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika leo.
   Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (aliyeshika kibuyu katikati) akiimba na kuserebuka nyimbo za asili ya kigogo pamoja na akinamama wa kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma kusherehekea muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua mradi wa maji kijijini hapo leo.

  0 0

  KUNA njia nyingi ya kumtukuza, kumuabudu na kupata Neema ya Mungu ambayo ni kwenda kanisani na kusali na njia ya nyimbo ambayo mtu unaweza kupata Baraka kubwa kutokana na nyimbo za injili zinazoimbwa na waimbaji mbalimbali wa muziki huo; amesema Mama Tunu Pinda.

  Mama Pinda ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda, ameyasema hayo alipozungumza na Hekaheka kuhusu Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 20 mwaka huu ambayo itakuwa  ni Sikukuu ya Pasaka inayoadhimishwa na Wakristo Duniani kote kwa Kufufuka Yesu Kristo mwana wa Mungu.

  Akielezea faida za kwenda kwenye Tamasha la Pasaka, Mama Pinda anasema ni kwa ajili ya kwenda kusikiliza nyimbo mbalimbali zitakazokuwa zikiimbwa na waimbaji wa nyimbo za injili ambako unaweza kupata Baraka na kuachana na matendo yasiyompendeza Mungu na hatimaye kutenda dhambi.Tamasha hilo ambalo huandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam kwa siku hiyo ya Pasaka na hatimaye katika Mikoa mingine saba ya Tanzania Bara.

   “...Mwaka juzi nilipokuja kwenye Tamasha la Pasaka kulikuwa kuna watu wengi wa kila rika wazee, vijana na hata watoto wadogo hali hiyo ilidhihirisha ni kwa namna gani Watanzania wanapenda nyimbo za injili ambazo ninaamini wanapata Neema ya Mungu, alisema Mama Pinda.Akaongeza, “Utamaduni huu wa kusherehekea Sikukuu za kidini kama vile Pasaka kwa kwenda katika matamasha ya nyimbo za injili ni mzuri kwa sababu unawaondoa watu katika vishawishi na kuwafanya kuwa karibu zaidi na uwepo wa Mungu,…”

  Amesema ili kupata Neema ya Mungu ni vyema watu wengi zaidi wakajitokeza siku hiyo ya Tamasha la Pasaka kwa Dar es salaam na mikoa mingine ambayo Tamasha litafika ili kuweza kujizolea baraka za Mungu kupitia nyimbo za injili ambazo zitaimbwa na waimbaji wa ndani na nje ya nchi; huku akisisitiza kuwa endapo atapata nafasi kwa mwaka huu atahudhuria tamasha hilo. Hata hivyo alisema nyimbo za injili ni burudani lakini kwa upande mwingine ni sehemu ya ibada ambayo msikilizaji anapokea Baraka na mafundisho ya biblia kupitia nyimbo hizo; lakini pia zinasaidia kutokutenda dhambi kwa kwenda katika starehe ambazo hazimpendezi Mungu.

  “…Sikuku ya Pasaka inaadhimishwa kwa Kufufuka kwa Yesu Kristu ambayo ni alama ya ushindi kwa wanadamu, hivyo ni busara kwa Wakristo wote kuhakikisha tunaacha dhambi na kuyashika yale yote aliyotuachia Yesu Kristo, ambayo ni Upendo na Amani bila kusahau kuiombea nchi yetu. 

  Tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kuwashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi, lengo kuu ni kuweza kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea yatima, akinamama wajane na wengine wenye uhitaji maalum.

  Hata hivyo Mama Pinda aliwataka Watanzania kuwa na Moyo wa kujitoa kwa watu wahitaji ambao wanahitaji misaada mbalimbali na hawana mtu wa kuwasaidia. “…Unaweza kukuta familia moja mtoto anakula chakula mpaka anazasa na kutupwa, lakini familia nyingine mtoto hana chakula na analala njaa; hivyo ni jukumu letu sote kusaidiana kama binadamu, tusiiachie serikali kila kitu ifanye,” alisema Mama Pinda.

  Akaongeza kuwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, ni mfano mzuri wa kuigwa na  watu wenye uwezo kuwasaidia wahitaji, kwa kufanya hivyo watapata Baraka na kuongezewa zaidi.

  0 0

   .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Bwawa la Maji la Mkata wiklayni Handeni leo
  Chipukizi wa Mkoa wa Tanga wakimkaribisha kwa maua Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika tarafa ya Mkata, wilayani Handeni mkoa wa Tanga, Rais Kikwete yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi .
   -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Msomela wakatia  a lipokwenda kukabidhi madume bora ya ng’ombe kwa wafugaji leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madume bora ya ng’ombe na kasha kuwakabidhi baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Msomela wilayni Handeni leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mmoja wa wafugaji mwenye asili ya kimasai bwana Shayo Lahoda aliyegawiwa dume bora la ng’ombe katika kijiji cha Msomela wilayani handeni leo 
   .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na ngoma za utamaduni baada ya kuzindua Bwawa la Maji la Mkata wiklayni Handeni leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Bwawa la maji la Mkata muda mfupi baada ya kulizindua huko Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga leo asubuhi.Rais Kikwete yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

  0 0


  Mdau Ernest Makulilo ambaye huandika kuhusu masuala ya Scolarship HAPA na pia kutoa video za suala hili HAPA
  UNATAKA SCOLARSHIP? Unajua pa kuzipata? Unajua namna ya kuzipata? Masharti yake je? Makosa yanayofanywa na wengi? Tofauti ya Scholarships za Undergraduate na Graduates wazijua? Yapi ya kuchunga wakati wa kutafuta scholarships? Boniface Makulilo ambaye amenufaika na scholarship hizi na kuandika kuzihusu kwa miaka ipatayo sita anaungana na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kujadili hili. Kuna mengi mema ya kujifunza. KARIBU NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

  0 0

  Russell Hobbs, today, launched its Tanzanian distribution outlet at Viva Towers Dar es salaam. Russell Hobbs, the number one small appliances brand in the United Kingdom, is a brand that is known for its quality and unique functional design. 

  It is strong in all the categories in which it operates, such as beverage, cooking, food preparation, house wares, personal care and others. It is therefore able to offer a quality, branded family of products which other competitors are not always able to. This will be the world’s first exclusive Russell Hobbs concept store. 

  “The move to open in Tanzania is driven by it’s fast growing economy which is quickly making investors realize it’s potential as a hub for East Africa. The port facilities are an added benefit and the road infrastructure gives ample access to neighbouring countries.” said Alan Coward, Chief Executive Officer of HOLB (Pty) Ltd .
  In addition, Marion Kearns, Marketing Executive of HOLB(Pty) Ltd said that, the Growth in the country’s infrastructure and government investment therein make Tanzania a strategic location for investment and business development.

  And further noted that “The work ethic and diligence of the Tanzanian people make it a natural target for future expansion for HOLB.”

   

  The relationship between JD Pharmacy, which is the leading provider of pharmaceuticals in Tanzania, and HOLB (Pty) Ltd will create major opportunities for all the stakeholders such employees, suppliers, government and consumers.

   “We perceive an exciting epoch with HOLB in bringing the Russell Hobbs brand to Tanzania. Our clientele are the lifeline of our business and we are committed to provide outstanding service to our customers.” commented Kiran Pattni, Chief Executive Officer of JD Pharmacy.

  Home of Living Brands (Pty) Ltd is an African Company with its head office based in Johannesburg, and is a wholly-owned subsidiary of the Bidvest Group Limited. HOLB is a consumer brands company which has leading world brands either under licence or with direct ownership, which it markets along with its chosen business partners to consumers in Africa, the JD Pharmacy in Tanzania


  Home of Living Brands Limited is a focused group specializing in the sales and marketing of branded household durables. Whereby their vast range of quality products consists of the best known local and international brands, so you always know that you're getting world-class products.

  Russell Hobbs which was Founded in Great Britain in 1952 by Bill Russell and Peter Hobbs, the brand led the way by introducing products which offer real consumer benefits and technological advancements to make life in the home easier and more enjoyable, also has presence in South Africa, Namibia, Botswana, Zambia, Zimbabwe, Mauritius, Tanzania, Kenya, Ghana, Nigeria, Ivory Coast and Angola.


  In attendance of the event from Home of Living Brands (Pty) Ltd (HOLB) was: Alan Coward -Chief Executive Officer; Murray Crow - Managing Director; Erwin Minnie - Africa Sales Manager; Marion Kearns - Marketing Executive; and Michele Snyders – Exports Operations Manager. Attending from JD Pharmacy, the official Tanzanian distributors for HOLB: Kiran Pattni - Chief Executive Officer; and Sanjay Patadia - Managing Director. Also in attendance were store owners and management from Tanzania Retailers, HOLB (Pty) Ltd distributors from various African countries, VIP Guests and select media. 


  0 0

   The Exim Bank Tanzania Mbeya Assistant Branch Manager Patric Nalascow (first right) and Mbeya Branch Officer Israel Augustine (second right) speak to Architects and Quantity Surveyors Registration Board (AQSRB) Board Chairman Dr. Arch Ambwene Mwakyusa (first left) flanked by  Chunya District Commissioner mr Deodatus Kinawiro (second left) when they visited the bank’s pavilion during the 21st Continuing Professional Development (CPD) seminar held at Mkapa Conference Centre in Mbeya region over the weekend. 
   The Exim Bank Mbeya Branch Manager Iddy Mwacha (second left) shakes hands with with Chunya District Commissioner Deodatus Kinawiro (right) who represented Mbeya Regional Commissioner Abbas Kandoro. Looking on is Architect Henry Mwaloka (first left) during the 21st Continuing Professional Development (CPD) seminar held at Mkapa Conference Centre in Mbeya region over the weekend. 
  From left  Quantinty Surveyor  Mwanaidi Daffa, Exim Bank Mbeya Branch Manager Iddy Mwacha, Architects and Quantity Surveyors Registration Board (AQSRB) Board Chairman Dr. Arch Ambwene Mwakyusa, Chunya District Commissioner Deodatus Kinawiro who represent Regional Commissioner, Exim Bank Mbeya Branch Officer Israel Augustine and Assistant Exim Bank Mbeya Branch Manager  Patric nalascow and Architect Henry Mwaloka in a group photo during the 21st Continuing Professional Development (CPD) seminar held at Mkapa Conference Centre in Mbeya region over the weekend.
  =========  ======= =======
  Modern construction technology key to industry transformation says AQSRB
  By Our Correspondent, Mbeya.

  Architects and Quantity Surveyors Registration Board (AQSRB) sees the use of modern construction technology as a sure answer to many challenges that are currently facing Tanzania infrastructure development sector.

  The board has now embarked on a drive to encourage architects, contractors, quantity surveyors and other stakeholders in the construction industry to uphold the use modern technology in their work in a move aimed at improving quality of infrastructure developed in the country.

  Speaking during the 21st Continuing Professional Development (CPD) seminar which was sponsored by Exim Bank Tanzania and held at Mkapa Conference Centre in Mbeya region over the weekend, AQSRB Board Chairman Dr. Arch Ambwene Mwakyusa said the board having acknowledged the challenges that Tanzania construction industry has been facing, which includes collapse of buildings under construction and completed ones, it thinks that the use of modern constructions technology will greatly control and improve the quality of work done. 

  Dr. Arch Mwakyusa said that emphasis is currently made on the use of modern technologies such as Building Information Modeling especially for Architects and Quantity Surveyors and Green Building Concept, with a focus to help improve the quality of buildings in the country. 

  “We have vehemently addressed the significance of using building information modeling and green building concept for both architects and quantity surveyors because we believe through these technologies, we will be able to improve the quality of our buildings in the country,” said Dr. Arch Mwakyusa. 

  He said that the seminar brought together more than 350 participants all over the country and others from the neighbouring countries such as Kenya, Uganda, Burundi and Rwanda. 

  “With all the participants on board, we have also managed to use this platform well to share business ideas, experience, perspective, insight and latest technology issues. This opportunity also helps us in developing healthy and positive associations among the participants,” added Dr. Arch. Mwakyusa. 

  On his part, Exim Bank Tanzania Mbeya Branch Manager Iddy Mwacha said the bank decided to support the AQSRB 21st Continuing Professional Development (CPD) seminar, because it was a great platform for the bank to build relationship particularly with stakeholders in the construction sector for the good of the country. 

  “We agreed to support and of course participate as exhibitor in the AQSRB 21st Continuing Professional Development (CPD) seminar because participants in this seminar are the stakeholders who hold the key to transformation and improvement of infrastructure in the country. With improved infrastructure, even the banks will have a better platform to do their business. Better infrastructure in a country always acts as a catalyst to fast economic growth.   


  “As a bank, we also support our customers to finance construction of their homes or any other infrastructure, easily and without stressing themselves to think where and how they will fund the project. Through our mortgage finance facility, we offer different tailored solutions to our customers. In that regard, we saw that this seminar was a better platform to showcase our mortgage product to allow stakeholders in the construction sector to understand it better and may advice their clients where to run to incase they need financial support,” Mr. Mwacha added. 

  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiongea na wafanyakazi wakituo cha Afya  Tunduma mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho na TBL.
  Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

  Kituo cha Afya Tunduma

  Kampuni ya Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.

  Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

  Malulu amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  Naye Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza  tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya Zambia.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  amesema kuwa watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho .

  Aidha Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo  mbinu  ya maji. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.


  0 0

   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kifuleta,Kata ya Mbwewe jana Machi 23,2013 
   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini,Mzee Rajab Seif Kabeilwa ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mzee Mrisho Kikwete ambaye ni Babu yake,wakati alipokwenda kumsalimia kijijini kwake,Pongwe Kiona jana Machi 23,2013.
  Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akizindua shina CCM la vijana wa boda boda katika kijiji cha Pongwe Kiona, jana Machi 23,2013.

  0 0

  Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.
  Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao. 
  Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya). 
  Mkuu wa Kijiji... Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe. 
  Wageni waalikwa. 
  Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea... ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48. 
  Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa. 
  Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.  Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi... washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka... wengine walitamani kughairi kuendelea na safari. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe... Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo. 

  Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi... Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

  0 0


  DSC_0400
  Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na mawakala wa Redio Jamii nchini. 
  DSC_0043
  Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akisisitiza jambo katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya.

  Na. mwandishi wetu, Pangani.
  Mawakala wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari .

  Wakitoa tathmini ya maendeleo ya mradi katika warsha inayowapa uwezo wa kuweka kumbukumbu za kazi zao na vyanzo vya habari kwa kutumia Tehama iliyofanyika Pangani, washiriki hao wamesema mafanikio hayo siyo tu katika taaluma bali pia yamewajenga na kuwaimarisha kimaisha.

  Mmoja wa washiriki hao alisema, “kusema ukweli natoa shukrani zangu kwa SIDA na UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwa sababu mimi binafsi nimeweza kununua kompyuta pakato (laptop) kwa ajili ya kuendeleza niliyoyapa kwa vitendo, na niko mbioni kununua simu za kisasa aina ya ‘tablet’,” alisema Sospether Rugemarila kutoka Fadeco FM redio.
  DSC_0105
  Sehemu ya washiriki wakifutilia kwa umakini mafunzo hayo.
  Katika kipindi cha miaka miwili cha mradi huo, mafunzo mbalimbali yametolewa kwa mawakala wa redio jamii kama vile matumizi ya mtandao katika kutafuta habari, mbinu mbalimbali za kupeleka taarifa na vipindi vya redio kupitia mtandao, matumizi ya simu aina ya ‘smartphone’ katika kuripoti taarifa maalum au majanga na matumizi ya mitandano ya kijamii kwa lengo la kuwasiliana, kushirikiana na kubadilishana mawazo, taarifa na vipindi vya redio.

  “Sisi baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya simu aina ya “smartphone” tulifungua akaunti ya pamoja ya Facebook kwa jina na UMMAREJA kama ulingo wetu wa kubadilishana mawazo, taarifa na masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wetu kama mawakala,” alisema mwenyekiti wa umoja huo Msuli Mwaijengo kutoka Kyela FM redio.
  DSC_0281
  Sospeter Rugemarila wa FADECO FM Redio, akizungumzia mafanikio aliyoyapata kutokana na mafunzo ya kuzipa uwezo Redio Jamii matumizi ya Teknolojia mpya katika kukuza upatikanaji na upashaji habari vijijini.
  Sabina Nestory ni miongoni mwa mawakala ambao walikuwa na uwezo mdogo sana kabla ya mafunzo haya kuanza. 

  Lakini ila anapohudhuria mafunzo mapya na kiwango chake pia kimekuwa kikiongezeka kiasi cha kumfanya aone umuhimu wa kununua simu aina ya ‘smartphone’ ambayo anasema itamrahirishia kutafuta na kutuma taarifa mbalimbali kwa niaba ya chama cha Umoja wa Wanawake katika Habari na Mawasiliano Sengerema (WAHAMASE) unaomiliki kituo cha Sengerema FM redio.

  “Mimi nilipohudhuria mafunzo ya Tehama Ifakara nilikwenda moja kwa moja dukani kununua simu ya ‘smartphone’ ili nione inafanyaje kazi, ninayo, bado naisoma huku nikiendelea kuitumia kwa kuripoti matukio mbalimbali ya vijijini hususan ya maendeleo”.
  DSC_0290
  Peter Marlesa wa Sengerema FM Redio, akielezea jinsi alivyofanikisha kutayarisha makala na vipindi mbalimbali zikiwemo habari za Mahakama na migogoro vijijini.


  Mafunzo hayo yameweza kuwapandisha ngazi baadhi ya mawakala kuwa wafanyakazi vituoni baada ya kuonyesha umahiri na ujasiri katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku kama ilivyofanyika Mtegani FM redio, Makunduchi Zanzibar na Sengerema FM, Sengerema Mwanza. Peter Marlesa ni miongoni mwa waliobahatika kupanda ngazi kutokana na umahiri na ubunifu wake katika kuandaa vipindi mbalimbali kwa kujituma.

  “Baadhi ya mambo niliyofaidika na mradi ni utayarishaji wa vipindi vya makala ya redio, jarida, vipindi vinavyohusu makundi maalum, habari za mahakamani na migogoro na taarifa za habari. Ni mara ya kwanza katika kituo chetu kuandika habari za mahakamani na maeneo tata vijijini.”

  Kwa mara ya kwanza warsha hii ya kuwapa uwezo wa kuweka kumbukumbu imewakutanisha mawakala 25 kutoka redio tisa ambazo ziko kwenye mradi wa kuzipa uwezo redio jamii matumizi ya Tehama ulioanza mwaka 2012 ambao baada ya hitimisho watapitiwa vyeti vya ushiriki. Redio hizo ni Fadeco, Kahama, Kyela, Micheweni, Mtegani, Orkonerei, Pambazuko, Pangani na Sengerema.
  DSC_0112
  Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa maelekezo jinsi ya kufanya mazoezi kwa vitendo.
  DSC_0347
  Sabina Nestory wa Sengerema FM Redio, akionyesha Smart Phone yake aliyoinunua wakati wa mafunzo ili kufanikisha mafunzo ya matumizi ya simu na habari kwa vitendo.
  DSC_0268
  Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama kutoka UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiewaelekeza jambo washiriki namna ya kuhifadhi habari kwa kutumia simu yenye uwezo mkubwa (Tablet).
  DSC_0084
  Programme Assistant wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka UNESCO, Rosemary Lyamba, akitoa maelekezo kwa washiriki katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
  DSC_0178
  Picha juu na chini ni washiriki wa warsha hiyo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya TABLET.
  DSC_0064
  DSC_0263
  Washiriki wakiwa kwenye kazi za vikundi.

  0 0
 • 03/24/14--01:23: Article 13


 • 0 0

  KUNA njia nyingi ya kumtukuza, kumuabudu na kupata Neema ya Mungu ambayo ni kwenda kanisani na kusali na njia ya nyimbo ambayo mtu unaweza kupata Baraka kubwa kutokana na nyimbo za injili zinazoimbwa na waimbaji mbalimbali wa muziki huo; amesema Mama Tunu Pinda.

  Mama Pinda ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda, ameyasema hayo alipozungumza na Hekaheka kuhusu Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 20 mwaka huu ambayo itakuwa  ni Sikukuu ya Pasaka inayoadhimishwa na Wakristo Duniani kote kwa Kufufuka Yesu Kristo mwana wa Mungu.

  Akielezea faida za kwenda kwenye Tamasha la Pasaka, Mama Pinda anasema ni kwa ajili ya kwenda kusikiliza nyimbo mbalimbali zitakazokuwa zikiimbwa na waimbaji wa nyimbo za injili ambako unaweza kupata Baraka na kuachana na matendo yasiyompendeza Mungu na hatimaye kutenda dhambi.Tamasha hilo ambalo huandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam kwa siku hiyo ya Pasaka na hatimaye katika Mikoa mingine saba ya Tanzania Bara.

   “...Mwaka juzi nilipokuja kwenye Tamasha la Pasaka kulikuwa kuna watu wengi wa kila rika wazee, vijana na hata watoto wadogo hali hiyo ilidhihirisha ni kwa namna gani Watanzania wanapenda nyimbo za injili ambazo ninaamini wanapata Neema ya Mungu, alisema Mama Pinda.Akaongeza, “Utamaduni huu wa kusherehekea Sikukuu za kidini kama vile Pasaka kwa kwenda katika matamasha ya nyimbo za injili ni mzuri kwa sababu unawaondoa watu katika vishawishi na kuwafanya kuwa karibu zaidi na uwepo wa Mungu,…”

  Amesema ili kupata Neema ya Mungu ni vyema watu wengi zaidi wakajitokeza siku hiyo ya Tamasha la Pasaka kwa Dar es salaam na mikoa mingine ambayo Tamasha litafika ili kuweza kujizolea baraka za Mungu kupitia nyimbo za injili ambazo zitaimbwa na waimbaji wa ndani na nje ya nchi; huku akisisitiza kuwa endapo atapata nafasi kwa mwaka huu atahudhuria tamasha hilo. Hata hivyo alisema nyimbo za injili ni burudani lakini kwa upande mwingine ni sehemu ya ibada ambayo msikilizaji anapokea Baraka na mafundisho ya biblia kupitia nyimbo hizo; lakini pia zinasaidia kutokutenda dhambi kwa kwenda katika starehe ambazo hazimpendezi Mungu.

  “…Sikuku ya Pasaka inaadhimishwa kwa Kufufuka kwa Yesu Kristu ambayo ni alama ya ushindi kwa wanadamu, hivyo ni busara kwa Wakristo wote kuhakikisha tunaacha dhambi na kuyashika yale yote aliyotuachia Yesu Kristo, ambayo ni Upendo na Amani bila kusahau kuiombea nchi yetu. 

  Tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kuwashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi, lengo kuu ni kuweza kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea yatima, akinamama wajane na wengine wenye uhitaji maalum.

  Hata hivyo Mama Pinda aliwataka Watanzania kuwa na Moyo wa kujitoa kwa watu wahitaji ambao wanahitaji misaada mbalimbali na hawana mtu wa kuwasaidia. “…Unaweza kukuta familia moja mtoto anakula chakula mpaka anazasa na kutupwa, lakini familia nyingine mtoto hana chakula na analala njaa; hivyo ni jukumu letu sote kusaidiana kama binadamu, tusiiachie serikali kila kitu ifanye,” alisema Mama Pinda.

  Akaongeza kuwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, ni mfano mzuri wa kuigwa na  watu wenye uwezo kuwasaidia wahitaji, kwa kufanya hivyo watapata Baraka na kuongezewa zaidi.

  0 0

  Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
  Bondia Iddi Bonge kushoto akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika mpambanio huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge' mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam

  mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na filimbi

  Bonge alipiga ngumi ya kwanza na kumfanya 'Shoka ya Bucha ' kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba ya uzito wa juu

  mara baada ya mpambano huo bondia Iddi Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu

  katika mpambano huo uliosindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally Jagalaga uku Amani Bariki ' Manny Chuga' akimsambaratisha kwa TKO ya raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma bondia  Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya raundi ya nne

  Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa.

  Bondia Amani Bariki 'Manny chuga' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Selemani Moto wakati wa mpambano wao Many chuga alishinda kwa TKO ya raundi ya nne.
  Bondia Kasimu Gamboo kulia akipambana na mohamed babeshi wakati wa mpambano wao Ganmboo alishinda kwa k,o ya raundi ya tatu ya mpambano huo .
  Refarii Omari Yazidu akimwinua mkono juu Bondia Kassim Gamboo.

  bONDIA aLi Bugingo kushoto akioneshabna umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Mandula mandula alishinda kwa pointi

  Bondia Fadhili Majia kulia akimtupia konde Juma Selemani wakati wa mpambano waio uliofanyika manzese majia alishinda kwa k,o ya raundi ya tatu
  Bondia iddi bonge akiwa ulingoni

  0 0


   picha ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo, katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti  wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo.
   Mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm

  Na Woinde Shizza,Arusha  Jumla ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti  wilayani Arumeru  kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani  wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo mwenyekiti wa   vijana wa  CHADEMA wa kata hiyo .

  tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.  Akiongea wakati wa kurudisha  kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya CCM,Mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa   ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.  Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani CHADEMA  ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli  ambayo inatakiwa iwenacho kama chama  Alisema kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi  na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atakaeweza kukisemea chama  .  Aidha alibainisha kuwa katika kata yao  tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi  bila kufanya maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa  Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi  ya kata yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.  Kwa upande wake  katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa  wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika ofisi ya mkurugenzi  kufuatilia swala hili.  Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka  na kata yao haitapata viongozi wazuri.  Aliongeza kuwa haiwezekani kuchagua viomgozi waizi maana mwisho wa siku wanaoumia ni wao wananchi kwani viongozi wao watakula fedha zao na wao wataendelea kufaidi huku wao wakiwa wanaendelea kuumia ukuwengine watoto wao wakilala njaa.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kukata utepe kuifungua rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko mkoani Tanga.
   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye koti jeusi katikati) akiwa na baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kuifungua rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko mkoani Tanga.

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyenyoosha mkono) akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anayempongeza kiongozi wa kikundi cha ngoma ya Selo baada ya kutumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mkata – Handeni - Korogwe. Anayeangalia (kulia) ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Handeni Dkt. Abdallah Kigoda.
  Sehemu ya barabara ya Handeni – Mkata.


  RAIS KIKWETE AZIFUNGUA BARABARA ZA MKATA – HANDENI NA KOROGWE – HANDENI MKOANI TANGA.
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wakazi wa Handeni na maeneo inakopita barabara ya Mkata – Handeni na Korogwe – Handeni kutumia ipasavyo fursa ya kupatikana kwa barabara hizo za lami kuyaboresha maisha yao.
   
  Rais Kikwete alitoa rai hiyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara  inayoinganisha Makao Makuu ya Wilaya ya Handeni na barabara kuu ya Tanga - Dar es Salaam kupitia Mkata na upande mwingine kuunganisha na barabara kuu ya Tanga – Moshi – Arusha kwa upande wa Korogwe.
   
  Mhe. Rais ameelezea kuwa lengo la Serikali ni kuona kwamba, barabara ya Mkata hadi Handeni inaendelezwa hadi Kondoa kupitia Kiberashi kwani kufunguka kwa ukanda huu kutakuwa ni chachu kubwa ya kuinua shughuli nyingi za kiuchumi hasa kwa sekta ya kilimo katika maeneo hayo inakopita barabara hiyo.
   
  Akiwasilisha tarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale alielezea kuwa barabara ya Mkata - Handeni ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ina urefu wa kilometa 53.2 ikiwa imejengwa na Mkandarasi Sinohydro Corporation Ltd kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya Shilingi bilioni 57.3.  Eng. Mfugale alibainisha kuwa mkataba wa mradi huu ulisainiwa mwezi June 2009 na kazi zikakammilika mwezi Novemba 2012 baada kutatua changamoto ambazo zilikuwa zinakwamisha kukamilika kwa muradi huo mapema zaidi kama ilivyokuwa imepangwa kimkataba.
   
  Ufunguzi wa barabara hiyo umeenda sambamba na ufunguzi wa barabara ya Korogwe hadi Handeni ambayo vile vile imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
   
  Akitoa tarifa kuhusu miradi huo wa Korogwe – Handeni, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale alielezea kuwa Mkandarasi Sinohydro Corporation Ltd ndiye pia iliyeijenga barabara hiyo ambayo ina urefu wa kilometa 65. Mkataba wa Mradi huu ulisainiwa mwezi June 2009 na kazi zikakamilika mwezi June 2013 na imejengwa kwa ghrama ya Shilingi bilioni 63.2. Kiasi cha Shilingi bilioni 3.3 kimelipwa kama fidia kwa wale waliofuatwa na barabara hiyo katika baadhi ya maeneo.
   
  Naye Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielezea baadhi ya faida zitakazopatikana kutokana na kujengwa kwa barabara hizo alibainisha kuwa barabara ya kutokea Korogwe hadi Handeni ndiyo barabara itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari katika barabara  kuu ya TANZAM hasa kwa wasafiri na wasafirishaji wanaotokea maeneo ya Iringa, Mikumi na mengineyo katika ukanda huo.

  Waziri Magufuli alifafanua kwa kwa kupitia Mikumi, Kilosa, Turiani, Mziha hadi Handeni na kuelekea Korogwe au Mkata mkoani Tanga kunapunguza zaidi ya kilometa 120 tofauti na kuzungukia Morogoro na Chalenze.

  “Hivi sasa mtu anayetokea Iringa analazimika kupitia Mikumi na Morogoro mjini hadi Chalinze ndipo aelekee Tanga, mzunguko ambao ni mrefu kulinganisha na barabara hii ya kupitia Mikumi, Kilosa Magole, Mziha hadi Handeni” alisistiza Waziri Magufuli.

  Kwa upande mwingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliwafahamisha wananchi waliohudhuria kwa wingi katika sherehe hizo kuwa, tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika kwa barabara inayoanzia Handeni kuelekea Kiberashi hadi Kwamtoro mkoani Dodoma.

  Rais Kiwete aliabinisha kuwa hatua hiyo pia imefikiwa kwa barabara ya Handeni, Mziha, Dumila, Kilosa hadi Mikumi. “Hatua inayofuata ni kutafuta fedha za kujenga maeneo katika sehemu hizo ambayo bado hayajapata makandarasi” alifafanua zaidi Rais Kikwete.  

  Hata hivyo Mhe. Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaasa wasafirishaji kuzingatia masuala ya usalama barabarani kwa kupakia mizigo kulingana na viwango vilivyowekwa kisheria. Alielezea kuwa moja ya adui wakuu waharibifu wa barabara ni uzidishaji wa mizigo kupita viwango vilivyowekwa kisheria.

  Mheshimiwa Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo pia ataweka jiwela msingi kuzindua ujenzi wa barabara ya Korogwe – Mkumbara.


older | 1 | .... | 254 | 255 | (Page 256) | 257 | 258 | .... | 1897 | newer