Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 250 | 251 | (Page 252) | 253 | 254 | .... | 1897 | newer

  0 0

  NA Zamaradi Kawawa, Maelezo Dodoma.

  Mwenyekiti aw Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba ameliambia bunge Maalum la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma kuwa Rasimu ya Katiba mpya inapendekeza Mawaziri wasitokane na wabunge.

  Amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye bunge kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya bunge Hilo kunalifanya bunge kushindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya bunge Hilo.

  Amesema Mawaziri watateuliwa na Rais NA kuthibitishwa na bunge . Aidha , rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .

  Rais Mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa kiti hicho aliyeshindwa na Shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja.

  Jaji Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo NA ukomo wa wabunge wa miaka 15 ya kukalia kiti hicho mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki wa ubunge na kuimarisha uwajibikaji.

  Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa NA vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.

  Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu Waziri NA wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.

  0 0

  Mwenyekiti wa  Benki ya  Covenant  Balozi Salome Sijaona  akimkabidhi  mratibu wa uhamasishaji wa vikundi vya Wilaya ya Temeke Bi.Tukae Kondo ufunguo wa pikipiki baada ya kuwapatia mikopo wajasiliamali mbalimbali.Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi imewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo na mitaji. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.

   Mkurugenzi Mtendaji wa  benki ya Covenat  Sabetha Mwambenja, akiwasisitizia  jambo juu  ya kurejesha mikopo baadhi ya wajasiriamali waliopata mikopo  ya pikipiki  iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasilia mali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo . Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Balozi Salome Sijaona
  Mwenyekiti wa  Benki ya  Covenant  Balozi Salome Sijaona  akimkabidhi  Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano cha  Yombo Vituka cha jijini Dar es Salaam,Charles Rweyemamu  ufunguo wa gari aina ya basi lenye thamani ya shilingi Milioni 45 .Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.

   Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant  Sabetha Mwambenja akiongea na Waandishi wa habari  juu ya benki hiyo kutoa mikopo kwa wajasiliamali wadogo  nchini  ili waweze kujikwamua  kimaisha kwa kuwapatia mitaji  ambayo ilijumuisha  Basi la abiria ,pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.


  0 0  0 0

   kushoto Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Fatma Ally, akiwa na Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe wakizindua kisima cha maji.

   Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe, pamoja naMkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Fatma Ally wote kwa pamoja wakifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya maji.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvumi makulu Mkoani Dodoma.
   Muonekano wa kisima kichozinduliwa.
   Kulia Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe (katikati),Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Fatma Ally, na kushoto Afisa Tarafa Chamwino Mvumi Mohamed Mfaki akielekea kuzindua bomba la maji.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akipanda mti.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe akisalimiana na Mkurugenzi ya Halmashauri Wilaya Chamwino Mkoani Dodoma Adrian Jungu.baada ya kuwasili kuzindua mradi mkubwa wa maji wenye uwezo wa kuwahudumia wakazi zaidi ya elfu 13 uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 300.kilichopo katika kijiji cha Mvumi makulu Mkoani Dodoma
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akiongea na wana kijiji wa Mvumi makulu Mkoani Dodoma.PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE,DODOMA


  0 0

   Mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili Omari Mikidadi (47) kutoka Mbagala jijini Dar es Salaam akipokea zawadi ya simu ya kisasa aina ya Samsung Gallaxy tablet kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Erick Tafisa(kulia), wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam. 
   Meneja Promosheni wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Davis Kambi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili Alex Sylvester(34) kutoka Zanzibar, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.
  Meneja Promosheni wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Davis Kambi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili  Rogers Isdory (29) kutoka Tabata, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

   

  Mwandishi Wetu, Dar es alaam
  WASHIRIKI wa shindano la Maisha Plus ambayo kwa mwaka 2014 inatambulika kwa jina la Maisha Plus Rekebisha, kutoka nchini Kenya, Rwanda,Uganda na Burundi tayari wameshawasili nchini na jana wameelekea wako mkoani Morogoro kushiriki shughuli za kijamii.

  Mratibu wa onyesho hilo, Ally Masoud Kipanya amesema hili ni kundi la tatu kushiriki shughuli za kijamii, ambapo kundi la kwanza lilikuwa Iringa, kisha la pili likaenda Zanzibar na hili la tatu linaenda Morogoro kushiriki shughuli za kijamii, huku lengo kubwa likiwa ni kubadilisha maisha ya wanajamii wa huko.

  "Hii ndio sababu Maisha Plus ya mwaka huu inaitwa Maisha Plus Rekebisha, ambapo lengo kuu ni kuangalia matatizo ya eneo husika na kuangalia jinsi ya kutatua, na sio kulalamika, tunataka kurekebisha wananchi wenye fikra za kusubiri kufanyiwa, kuwa wepesi wa maamuzi na kutatua matatizo waliyonayo", alisema Masoud

  “Wananchi wengi hulalamikia serikali juu ya maswala mbalimbali ambayo hata wao wenyewe wanaweza kuyarekebisha bila kusubiri kufanyiwa”,alisema.

  Washiriki kutoka nchi jirani ni walio mkoani Morogoro kwa sasa ni Loveness Asantely ,Mary Sidi(kutoka Kenya), Borandanginye Aurore, Mvano Ciza, na Abdou Karim(kutoka Burundi), Aminata Siira(kutoka Uganda), Uwamahoro Fatima, Ngabozinza Khalid, na Ngabozinza Daniel (kutoka Rwanda)

  Kupitia Maisha Plus Rekebisha mwaka huu, wananchi watapata elimu juu ya kuepukana na mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo magonjwa kama malaria, kipindupindu, homa ya manjano na mengineyo.

  Washiriki wote kwa ujumla kutoka nchi za jirani wanatakiwa kuwa 12 nambili,waliofika nchini ni 10 wawili wanaotambulika kwa majina Said Rashid (Uganda) na Caron Abisai (Kenya) bado hawajafika.

  0 0


  Hadidu rejea
   
  1)      Kuchunguza uendeshaji wa mkataba wa kuzalisha Umeme kati ya kampuni ya IPTL na TANESCO
   
  2)      Kuchunguza kama wakati escrow inafunguliwa kampuni ya mechmar ilikuwa inamiliki IPTL, kama ilikuwa imefilisiwa na kama ilikuwa imehamisha umiliki wake kwa kampuni ya PAP.
   
  3)      Kuchunguza na kuthibitisha ushahidi wa kampuni ya PAP kununua kampuni ya mechmar na kumiliki IPTL
   
  4)      Kuchunguza chanzo cha mgogoro kuhusu tozo kati ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha ushahidi wowote kuwa mgogoro uliamuliwa kwa faida ya IPTL
   
  5)      Kuchunguza kama ilikuwa sahihi kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kusamehe kodi ya VAT ya jumla ya tshs 26 bilioni kutokana na tozo ya capacity charges na TRA wachukue hatua gani kuhakikisha kodi hiyo inakusanywa
   
  6)      Kuchunguza kiwango cha fedha kilichopaswa kuwemo katika akaunti ya escrow, kiwango gani kilikuwepo wakati IPTL wanalipwa na kiwango gani kitapaswa kulipwa zaidi kutoka tanesco
   
  7)      Kuchunguza madai ya benki ya standard chartered kwa tanesco na madai mengine yeyote yanayohusiana na mkataba wa kuzalisha Umeme wa IPTL na iwapo Serikali imejihadhari na uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa, nafasi na heshima ya nchi katika kuheshimu mikataba ya kimataifa na ya uwekezaji.
   
  8)      Kuchunguza iwapo Wizara ya Nishati na madini ambayo ni mhusika Mkuu wa akaunti ya tegeta escrow ilifanya 'due diligence' ya kutosha kabla ya kuingia makubaliano ya kutoa fedha zilizopo akaunti ya tegeta escrow. Kupata Maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na madini ni kwa nini aliagiza ukaguzi maalum wakati yeye ni mhusika Mkuu kwenye mchakato mzima na ilhali akijua PAC tayari imeanza mchakato wa ukaguzi.
   
  9)      Kutoa mapendekezo ya njia bora za kisheria kulinda Taifa kutoingia hasara zaidi katika mkataba wa IPTL chini ya wamiliki wapya
   
  10)   Kutoa ushauri kwa kamati ya PAC juu ya mapendekezo ya hatua ambazo Bunge linapaswa kuchukua kuhusu matokeo ya ukaguzi huu maalumu
   
  Imetolewa na;
  KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)

  0 0

  Picha ya Kikundi, baadhi ya members wa UWF na  washindi wa miaka ya nyuma pamoja na Mshindi mpya wa Mwaka 2014 wakiwa katika picha ya pamoja.
  Bi Jane Matinde, Ofisa wa maosiano wa Airtel, akikabidhi hundi ya udhamini ya million tano, kwa mwenyekiti wa UWF, Unity Of Women Friends Bi.Mariam Shamo,mwishoni Kulia ni Mkurugenzi wa benki ya Wanawake,Bi Magreth Chacha.Hafla hiyo iliofana kwa kiasi kikubwa ilifanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape One,Mikocheni jijini Dar mwishoni mwa wiki.
  Mshindi wa Awards 2014,Bi.Leila Mwambungu aangua kilio baada ya kutangazwa mshindi wa Tuzo ya Mwanamakuka.
  Maryam Shamo, Mwenyekiti wa UWF na Meneja mradi wa Mwanamakuka, kulia na Mkurugenzi MKuu wa Benki ya Wanawake Tanzania,Bi.Magreth Chacha wakimkabidhi tuzo Mshindi wa mwaka 2014,Bi.Leila Mwambungu. 
  Bi Magreth Chacha, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania,ambaye ni Mdhamini na Mdau mkubwa wa UWF katika kuwaongoza Washindi wa mwanamakuka katika kufikia malengo yao,akizungumza machache kwenye hafla hiyo.
   Mdhamini wa mradi wa Somki- Somesha Mtoto wa Kike top 15, Mr. Chriss Wade, akimkabidhi mmoja wa wahitimu aliyefanya vizuri katika mitihani yake ya kidato cha nne.
  Picha Ya Pamoja, baadhi ya wanafunzi wanaonufaika na mradi wa Somesha Mtoto wa Kike, wakiwa na Members wa UWF na Mfadhili.

  Dr.Vicensia Shule, mtaalam wa mambo ya ubunifu, akitoa mada kwa wanamakuka jinsi ya kuwa wabunifu kwenye kazi zao za mikono.
  Mwana kikundi wa UWF ambaye pia ni Meneja mradi wa Somesha Mtoto Wa kike (SOMKI), Bi Belinda Ngowi, akielezea mafanikio makubwa ya mradi huo, haswa kwenye matokeo ya kidato cha nne wahitimu wote wamefanikiwa kupata daraja la kwanza na la pili.
  Mwenyekiti wa UWF, Maryam Shamo akisema machache kuhusiana na mradi wa Mwanamakuka 2014.

  0 0

   Mbunge a Jimbo la Mchinga,Mh. Said Mtanda (kulia) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014,wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (wa pili kushoto walioketi).Picha na Othman Michuzi,Chalinze.

   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.Katika Mikutano yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo,Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo.
  Wananchi wa Kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na wanakijiji wa Kijiji cha Msigi Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze  Machi 18,2014.

  0 0

   
  Exim Bank Tanzania Manager Corporate Relationship Justin Wambali (left) speaks to a customer who visited the bank’s pavilion during the four-day exhibition in line with Tanzania Israel Business and Investment Forum (TIBIF) held at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam on Monday.
  =======  =======  =======
  Exim Bank urges more people to access financial services
  By Staff Reporter

  THE Exim Bank Tanzania Manager – Corporate Relationship Justin Wambali has called upon Tanzanians to access financial services since it is a safe way of saving money for their future development. 

  He was speaking during the opening day of a four-day Tanzania Israel Business and Investment Forum (TIBIF) exhibitions held at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam. 

  Wambali explained that, Tanzanians need to start accessing financial services and save money in a safely manner as until recently, few Tanzanians have access to financial services.

  According to Finscope 2009 survey only 56 percent of Tanzanians have access to banking services which is not good for an economy such as Tanzania’s. That’s why we use a platform like this to speak directly to people who still don’t have bank accounts to do so for their own betterment. 

  “Apart from that, Business and Investment Forums of this nature are very crucial to us as we get the chance to interact with different people, our esteemed customers and hence understanding their queries directly from them.”  Mr Wambali added “This is also used to showcase our different products.”

  Mr Wambali as well emphasized on how Exim Bank believes that ‘Innovation is Life’ and therefore in the process of achieving their goal of becoming the most preferred bank in the banking sector in Tanzania, they tend to put in the market new innovative products.  
    
  He reiterated that the TIBIF forum which was opened by the Vice President of the United Republic of Tanzania, Dr. Mohammed Gharib Bilal will engage many business investment institutions operating in Agriculture, Mining, Financial services, Education, Infrastructure (Roads, Water), Construction/Property/Housing, and therefore the bank will have such a great chance to showcase its variety of products.  

  “This forum has brought together more than 500 business, investors, policymakers, industry leaders and decision makers from various enterprises and institutions of all sizes, therefore we also see this as platform where the Exim Bank Tanzania can increase its connections with different people in and outside the country,” Wambali added. 
    

  0 0

   Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania, Juma Boma (wa pili kulia) akipanda ndege mpya aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe. Shirika hilo limeanza safari zake kwenda Mbeya ambapo itaruka mara nne kwa wiki.
   Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma akipokea maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 iliyotumika  kuzindua safari za kati ya Dar es Salaam na Songwe. Nyuma yake ni kaimu mkurugenzi wa ufundi, Patrick Itule. Shirika hilo litakuwa linaruka mara nne kwa wiki kwenda Mbeya. 
   Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma, akibadilishana mawazo na Kaimu mkurugenzi wa ufundi wa shirika hilo, Patrick Itule, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 inayotumika katika uzinduzi wa safiri kati ya Dar es S alaam na Mbeya. Shirika hilo litakuwa likifanya safari zake mara nne kwa wiki kwenda Mbeya, safari ya lisaa limoja tu.
   Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL), Shabani Mtambalike (kulia), akimkaribisha Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa ATCL, Juma Boma (wa pili kulia) na kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe Jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.
   Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma (wa pili kulia, Kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule (wa tatu kulia) na Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika hilo Shabani Mtambalike (kulia) wakishangilia, pamoja na wageni wengine, kuwasili kwa ndege ya ATC katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe  jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.
   Kaimu mkurugenzi wa  biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania Juma Boma akikata keki kama ishara ya kuzindua safari za ndege ya ATCL kati ya Dar Es Salaam na Mbeya, hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Songwe siku ya Jumatatu mchana. Shirika hilo la ndege lilitumia ndegeyake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki
   Abiria wakiwa ndani ya ndege mpya ya Air Tanzania aina ya CRJ-200 muda mfipi kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa  Songwe wakitokea Dar es Salaam. 
  Abiria wakipanda ndege ya Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe wakielekea Dar es Salaa. Safari hizi zitafanyika mara nne ndani ya wiki.
  ========  ========    =========
  ATCL yaanza safari za kwenda Mbeya  

  Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Jumatatu hii lilizindua safari zake za kwenda Mbeya kupitia uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Songwe likitumia ndege yake mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ya Canada aina ya CRJ – 200.

  Safari hiyo inayochukua kadri ya saa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya itakayofanyika siku nne kwa wiki; Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili, ililakiwa na abiria na wafanyabiashara wanaosafiria kutoka Mbeya kwenda katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

  Akizungumza katika uzinduzi wa kihistoria uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara/Masoko wa shirika hilo Bw. Juma Boma alisema Air Tanzania imerudi kwa kishindo katika mji ambao ni kitovu cha biashara kwa mikoa ya nyanda za juu kusini na inayotumika kama njia ya kuiunganisha Tanzania na nchi za Kusini mwa  Afrika, ili kupunguza adha ya usafirina kuiunganisha sehemu ya Kusini mwa Tanzania na mikoa mingine.

  “Safari ya Air Tanzania kwenda Mbeya iliyosubiriwa kwa muda mrefu imeanza rasmi leo hii. Kwa kutumia ndege yetu mpya, tunatoa usafiri wa haraka na salama, tukiiunganisha Mbeya na mikoa mingine. Kwa saa moja tu, abiria wetu wanauhakika wa kutua uwanja wa ndege wa Songwe kutokea Dar es Salaam.

  “Tumezingatia masuala yote ya kiuchumi ili kupanga nauli tuliyoanza nayo ambayo ni kiasi cha shilingi 150,000 kwa tiketi ya kwenda na shilingi 260,000 kwa tiketi ya kwenda na kurudi,” alisema,” Bw. Boma.

  Alisema uzinduzi wa njia ya Mbeya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati madhubuti wa upanuzi wa shirika, ambao umelenga katika kuzirejesha safari zote za ndani na za kimataifa na kufungua njia nyingine mpya.

  Boma alisema kuwa kutokana na mkakati wao ujulikanao kama go-green utalipelekea shirika hilo la ndege la taifa kuongeza toleo jipya ya ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 78 mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, shirika hilo litaongeza idadi ya safari zake katika njia zake kuu na kuongeza safari za kimataifa.

  “Kupitia upanuzi wa safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondokea Dar ukiwa ni saa 11 jioni na kutokea Mwanza  ni saa moja usiku. Tutakuwa tukienda mwanza mara nne kwa wiki.

   Tutakuwa pia tukisafiri kwenda Moroni nchini Comoro katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Vile vile tunatarajia kufungua njia ya Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.

  Alibainisha kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria wanaoshindwa kutokea wakati wa safari na wale wanaobadilisha ratiba ya safari zao, na kusema kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana na dharura mbali mbali kabla ya safari.

  Mmoja kati ya abiria aliyesafiria katika ndege hiyo kwenda Mbeya, Deogratius Nyanshile aliipongeza Air Tanzania kwa maamuzi yake na kutoa wito kwa watanzania kuliunga mkono shirika kwa kusafiria na Air Tanzania.

  “Nawaasa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kanda ya kusini kwa ujumla, kuitumia fursa hii kikamilifu iliyotolewa na shirika la Ndege la Air Tanzania,” alisema Nyanshile. Ndege hiyo ya taifa, ambayo ilisimamisha huduma zake katika mkoa huo kwa sababu ya ubovu wa uwanja wa ndege wa zamani wa Mbeya, imerejesha safari hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.

  Ikitumia ndege yake aina ya  Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa shirika hilo linasafiri katika zaidi ya sehemu naneTanzania ikiwa ni pamoja na Mtwara, Mwanza,  Tabora,Kigoma, Dar es Salaam, Bujumbura, Mbeya na kwendaMoroni nchini Comoro.

  0 0


  Maandalizi ya mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge kupitia CCM jimbo la Chalinze yaendelea vizuri ambapo jioni ya leo Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajiwa kuhutubia wakazi wa Chalinze na Vitongoji vyake pamoja na kumnadi mgombea wa ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.

   Barabara Kuu iendayo mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha ikiwa imependeza kwa bendera za CCM ,ambapo masaa machache yajayo kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za ubunge CCM.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mratibu wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze akisoma vichwa vya habari vya magazeti ya leo kwenye moja ya vibanda vya magazeti Chalinze huku sehemu kubwa ya maeneo yote yakiwa yamebandikwa mabango yenye picha za mgombea kiti cha ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
   Mratibu wa Kampeni za Ubunge CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye akibadilisha na Kamanda wa Vijana wilaya ya Bagamoyo Ndugu Haidary Mohamed wakati wa kukagua hatua za mwisho za maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa Kampeni.
   Shumina Sharif Kiongozi wa kampeni kata ya Msata na Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa akiwa na mratibu wa kampeni za ubunge za CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni jimbo la Chalinze.
  Mratibu wa Kmapeni za Chalinze CCM Nape Nnauye akijadiliana jambo na maofisa wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM jimbo la Chalinze.

  0 0

   Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga akizungumza na wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema leo.
    Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga akizungumza na wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema leo.
  Sahihi halali ya Mwigulu Nchemba ambayo iko tofauti ya waraka uliosambazwa.
  =======  ======  ========
  Na Denis Mlowe,Iringa

  KATIBU wa CCM Mkoa wa Iringa Hassani Mtenga amekanusha chama hicho kuhusishwa na waraka aliodai umesambazwa na Chadema ukihusu mchanganuo wa matumizi ya Sh Milioni 560 katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga.

  Alisema propaganda za kisiasa za wapinzani ndio chanzo cha waraka huo kusambaa na kuwaonyesha waandishi wa habari sahihi kamili ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Mwigulu Nchemba anayesemekana alisaini waraka huo.

  "Kwanza kuna kosa hawa wenzetu wanafanya, waraka huo una anwani ya Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa lakini chini unaonekana umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba, sahihi ambayo imegushiwa,” alisema Mtenga


  Katika waraka huo wenye kichwa cha habari kinachosema ‘Malipo ya kamati mbalimbali kwenye ushindi wa jimbo la Kalenga, umeidhinisha fedha hizo zitolewe kwa viongozi mbalimbali kama walivyoomba oili zitumike katika kampeni za jimbo.


  Waraka huo unaonyesha kuwa CCM wametumia kiasi cha shilingi milioni 560 kwa ajili ya timu ya ushindi wiki hii ya mwisho ya kampeni, fedha hizo zimetumwa kutokana na tathimini yenu kuwa ni hali mbaya kwetu kwa barua yenu yenye  kumb Namba  CCM/IR/VOL11/096.

  “Hakikisha kiwango hiki kinwafikia  walengwa wote wafuatao kwa uwiao tuliokubaliana kulingana na maeneo yao na wao wazigawe kwa mabalozi wetu kwenye kila kitongoji na kata apewe Balozi Sh850,000, Mama Galinoma Sh Milioni 80, Mama Ray (Ulanda) Sh Milioni 60, wenyeviti wa kata wa CCM kila mmoja Sh Milioni 20, makatibu wa kata kila mmoja Sh Milioni 8, makatibu wenezi CCM kila mmoja Sh Milioni 14 na Kamati ya ushindi Nzihi Sh Milioni 108,” sehemu ya waraka huo inasema.

  Mtenga alisema lengo la kusambazwa kwa waraka huo lilikuwa kuwaaminisha wapiga kura wa Kalenga kwamba kuna fedha zimetolewa na CCM kwa ajili yao lakini zimeliwa na watu wanaotajwa katika waraka huo.

  Alisema kuna kila dalili kwamba waraka huo uliandaliwa na Chadema kwa lengo la kuwarubuni wananchi wa jimbo la Kalenga wakose imani na CCM.

  Wakati huo huo CCM kimempa siku 7 Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Iringa, OCD Sifael Pyuza kuwataka radhi kwa madai ya kuwadhalilisha katika ofisi za chama hicho mkoani hapa baada ya kuwafanyia uchunguzi bila kuwa na kibali maalum.

  Kamanda Pyuza anatuhumiwa na chama hicho kukihusisha na mchezo mchafu wa siasa kwa kuficha watu ndani ya jengo la ofisi yake waliokuja katika uchaguzi mdogo wa Kalenga uliofanyika machi 16 na ccm kuibuka kidedea.

  Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliyasema  hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuwa , Machi 16 mwaka huu kamanda huyo alituma makechero wa jeshi hilo katika ofisi za CCM za mkoa wa Iringa waliotumia mabavu kupekua ofisi moja baada ya nyingine bila kuwa na kibali halali.

  Alimtaka kamanda huyo kuwaomba radhi baada ya tuhuma yake dhidi yao kubainika haina ukweli.

  na chama cha mapinduzi hakiwezi kukaa kimya kwa udhalilishaji huu uliofanywa na mkuu wa upelelezi wa wilaya kwa sababu jambo hilo ni sawa na kukiingiza chama cha mapinduzi katika kashfa ya mchezo mchafu wa kisiasa.

  Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na madai ya chama hicho lakini yupo tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi.

  0 0


    Ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma ukiendeleo kwa kasi hapa ni maeneo ya Manispaa katika kata ya Mtwivila maeneo ya Mwang'ingo wakiendelea na ujenzi wa Daraja.(picha na Denis Mlowe)

  0 0  Video mpya ya Msanii Kadja yule Dada aliyeimba Maumivu.
  Amekuja tena na Audio na Video yake mpya. Kazi imefenywa na Legendary Music-Tanzania. Tunaomba Support yako sana kwa ku share na watu wengine. Pia usisite kutupa Maoni yako ili kuweka kufika mbali zaidi.

  0 0  0 0
 • 03/19/14--06:30: Matukio Bungeni leo.

 • Mjumbe wa Bunge Maalum, Evod Mmanda akifafanua kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Bunge wa Maalum ambaye pia ni Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi  akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kushoto) wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
  Waziri wa Katiba na Sheria ,Dk. Rose Asha Migiro akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ,Januari Makamba wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum Dk.  Tulie Akson  akifafanua kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.(Picha na Magreth Kinabo)

  0 0


   Na Magreth Kinabo

  Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge Maalum Machi 21, mwaka huu mjini Dodoma.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa bunge hilo,  Yahya Khamis Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa ofisi za Bunge mjini Dodoma.

  “Kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21 ,mwaka 2014 saa 10:jioni, ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na kuketi katika  maeneo watakayoelekezwa saa 9:00 alasiri,” alisema Katibu huyo.

  Aidha Katibu huyo alisema ratiba ya shughuli hiyo itaanza na kikao cha Bunge saa 9:10 na baadae kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea Rais .

   Aliongeza kuwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, Rais Kikwete atapokewa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Naibu Katibu wa Bunge Maalum, ambapo baadae ataelekea katika jukwaa maalum kwa ajili ya kupokea salamu za heshima na kukagua Gwaride Maalum ambalo limeandaliwa na jeshi la polisi.

  Baada ya shughuli zote kufanyika katika viwanja vya Bunge kumalizika, utaratibu umewekwa  kwa viongozi kuingia Bungeni kwa maandamano maalum.

  Viongozi watakaohusika katika maandamano hayo ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ,Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na hatimaye   Rais Kikwete ambaye atafuatana na Mwenyekiti wa bunge hilo.

  Katibu huyo aliwataja viongozi wegine walioalikwa kuwa ni viongozi wa kitaifa na watendaji wakuu kutoka pande zote Muungano, viongozi wa kitaifa wastaafu,ambao ni marais wastaafu kutoka pande zote za muungano, mawaziri wakuu wastaafu, waziri kiongozimstaafu na maspika wastaafu.

  Viongozi wengine ni mama Maria Nyerere, Mama Shadia Karume na Mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya  Mabadiliko ya Katiba.

  Wageni wengine walioalikwa katika utaratibu huo ni taasisi za dini, zisizozakiserikali, tansia  ya habari, vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu, vyama vya watu wenye ulemavu, wafanyakazi,wafugaji,wavuvi, wakulima na wawakilishi kutoka sekta binafsi.


  Kwa  mujibu wa ratiba ya shughuli hiyo Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia bunge hilo kwa muda wa saa moja. Hivyo shughuli hizo zitakamilika majira ya saa 12:00jioni.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtwisha ndoo ya maji Bi. Amina Rajab, mkazi wa Wilayani Mpwapwa, baada ya kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Maji wa Wilaya ya Mpwapwa, Shadrack Matemba (wa pili kulia) wakati alipotembelea moja ya chanzo cha maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kulia kwa Makamu ni Mama Asha Bilal na Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji sikiliza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kushoto kwa Makamu ni Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe,(kushoto) ni Mama Asha Bilal
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wagogo wakati alipokuwa akiwasili katika sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.
   Baadhi ya wananchi wa Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akiwahutubia.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.Picha na OMR

older | 1 | .... | 250 | 251 | (Page 252) | 253 | 254 | .... | 1897 | newer