Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 251 | 252 | (Page 253) | 254 | 255 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Katikati)akizindua tawi jipya la Benki ya KCB Shariah Lililopo barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam, litakalotoa  huduma kwa kuzingatia maadili ya kiislamu,ambapo watapata mikoipo isiyokuwa na riba .Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania  Moezz Mir, wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa benki hiyo Dr.Edmund Mndolwa na wakwanza Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Shariah wa benki hiyo Uzairu Athuman. 
  Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Katikati)akimkabdhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni kumi,Mwenyekiti wa yatima group trust fund Winfrida Lubanza kwaajili ya kuendeleza kilimo cha kisasa wakati wa uzinduzi tawi jipya la Benki ya KCB Shariah Lililopo barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.kushoto ni ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Dr.Edmund Mndolwa na  watatu toka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania  Moezz Mir.  

  0 0
 • 03/19/14--07:29: Article 5


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana akimuinua Mkono Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM,zilizofanyika leo Machi 19, 2014 kwenye Viwanja vya Polisi Chalinze,Mkoani Pwani.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakiwapungia mkono wananchi wa Jimbo la Chalinze na WanaCCM waliofika kwa wingi kwenye Uzinduzi wa Kampeni za CCM,zilizofanyika leo Machi 19, 2014 kwenye Viwanja vya Polisi Chalinze,Mkoani Pwani. 
   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi na wanaCCM wa Jimbo la Chalinze wakati akiwahutubia kwenye Uzinduzi wa Kampeni za CCM,zilizofanyika leo Machi 19, 2014 kwenye Viwanja vya Polisi Chalinze,Mkoani Pwani
   Mjumbe wa NEC na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akijumuina na WanaCCM wa Jimbo la Chalinze huku akiwa amebeba bango la Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza wakati akifungua warsha kwa wataalamu wa kilimo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo. 
  Mwezeshaji kutoka shirika ka TAHA Bw. Isaac Ndamanhyilu akizungumza kwenye warsha hiyo. 
  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wataalamu wa kilimo wa kata na vijiji vya wilaya ya Makete. 
  Wataalamu wakifuatilia mafunzo hayo. 
   Mwezeshaji Manfred Bitala akiwawezesha washiriki wa warsha hiyo.
  Na Edwin Moshi, Globu ya jamii Makete
  Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imedhamiria kuinua kilimo cha matofaa maarufu kama apples, ili kiweze kuinua uchumi wa wakulima pamoja na wilaya kwa ujumla

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amesema wilaya imeanza kutekeleza agizo la rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara wilayani hapo kuwa ni lazima kilimo cha apple kiwe cha biashara wilayani Makete

  Mh. Matiro amesema mafunzo watakayopatiwa maafisa hao wa kilimo, wanatakiwa kuyafuata na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kata na vijiji vyao ili mabadiliko yaanze kuonekana na ndiyo maana halmashauri imeshirikiana na shirika la TAHA kuwapatia mafunzo ya namna ya kuboresha kilimo hicho katika maeneo wanayotoka

  Amesema kwa kuwa jambo hili halihitaji masihara anatarajia kuona mabadiliko mara moja pindi mafunzo hayo yatakapo malizika kwa kwenda kuwaelekeza wakulima kitu cha kufanya ili apples zizalishwe kwa wingi na kwa ubora unaohitajika kwani hilo linawezekana kwa mujibu wa utafiti ambao umefanyika wilayani hapo

  Mh. Matiro amesisitiza pia badala ya wananchi kupanda miti mingi ya mbao kwa sasa wanatakiwa wabadilike na wapande miti ya matunda hasa apples kwa kufuata elimu ya wataalamu hao wa kilimo ambayo wamepatiwa katika mafunzo hayo 

  Kwa upande wake Bw. Isaac Ndamanhyilu kutoka shirika la Tanzania Hoticultural Association maarufu kama TAHA ambao ni watoaji wa mafunzo hayo, amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuongeza uzalishaji wa apples pamoja na uuzaji wa matunda hayo

  Amesema kwa wilaya ya Makete imekuwa ikizalisha matunda hayo kwa wingi lakini hakuna kumbukumbu zinazoonesha kama uzalishaji huo upo Makete, na pia hakuna taarifa zinazoonesha kama wilaya hii ni miongoni mwa maeneo ndani ya Tanzania yanayozalisha apples

  Bw. Ndamanhyilu amesema kufuatia kukosekana kwa kumbukumbu hizo, ndiyo maana wameamua kushirikiana na halmashauri kuhakikisha elimu inatolewa kwa mabwana shamba na mabibi shamba na wao wawaongoze wakulima kulima kilimo cha kisasa ili matunda hayo yazalishwe kwa wingi na yenye ubora unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa

  "Kulikuwa kuna maonesho fulani jijini Arusha, na mgeni rasmi alikuwa Rais Kikwete na alibahatika kuona apples pale, na alipoambiwa kuwa zinazalishwa Makete kwa kweli alishangaa, na ndiyo maana alisema atafika Makete kujionea, na kweli alifika na amesisitiza kilimo hiki kiwe cha biashara na ndio maana tunatoa hii elimu kwenu" alisema

  Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amewaasa mabwana na mabibi shamba hao kubadilika kwani wapo baadhi ya wataalamu hao wamekuwa wakihubiri elimu bila kufanya kwa vitendo jambo linalowakatisha tamaa wakulima

  "Yaani wakati mwingine ukiliangalia shamba la mabwana na mabibi shamba nia aibu, yaani unakuta shamba la mkulima linaubora kuliko la ninyi wataalam, sasa hii inakatisha tamaa, lazima ninyi muwe mfano wa kuigwa" alisema Bitala

  Amesema wao wananafasi kubwa ya kuibadilisha hii nchi kutoka hapa ilipo na kuonekana mabadiliko makubwa na yenye tija katika sekta ya kilimo kama kila mmoja ataamua kufanya kazi yake ipasavyo

  Katika mafunzo hayo wamefundishwa mambo mengi ikiwemo dalili na aina za magonjwa yanayoshambulia matunda, na namna ya kulima na kupata mazao mazuri zaidi ya ilivyo sasa

  0 0

  Na Edwin Moshi, Makete.

  Jehi la polisi wilaya ya Makete mkoani Njombe linamshikilia Bw. Sadick Sanga (28) mkazi wa kijiji cha Unyangogo kata ya Iniho wilayani hapa, kwa tuhuma za kumuua kikatili Bibi Meluti Mbwilo (70) ambaye ni mama yake wa kambo

  Tukio hilo limetokea Machi 14 mwaka huu ambapo mtuhumiwa alitenda mauaji hayo kwa kumkatakata na panga kichwani na miguuni wakati marehemu akiwa jikoni kwake

  Akizungumzia tukio hilo Afisa upelelezi wilaya ya Makete ambaye pia ni kaimu OCD, Bw. Gosbert Komba amesema kuwa baada ya wananchi kugundua mauaji hayo, walimkamata mtuhumiwa na kisha wakatoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo walifika mara moja na kumtia mbaroni mtuhumiwa

  Amesema mtuhumiwa alikamatwa na kielelezo ambacho ni panga analodaiwa kulitumia kutekeleza mauaji hayo na kwa sasa anashikiliwa na jeshi hilo na atapandishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kujibu mashitaka yanayomkabili

  Bw. Komba amekiri vitendo vya mauaji ya kikatili kuendelea kushamiri wilayani Makete ambapo ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume na sheria za nchi

  Amesema mauaji hayo yanahusishwa na imani za kishirikina hivyo, kutokana na wazee wengi kuonekana wana macho mekundu hivyo watu kuwadhania kuwa ni wachawi hivyo kuwataka wananchi kuondokana na dhana hiyo potofu

  "Unajua maeneo mengi hapa wilayani watu wanapikia kuni, na kuni zinatoa moshi, hawatumii gesi ama umeme huko vijijini, hivyo uwezekano wa watu kuwa na macho mekundu ni mkubwa kutokana na moshi unaotokana na kuni wakati wa kupika, haimaanishi macho mekundu yao eti ni wachawi" alisema Komba

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Binti wa Mfalme wa Sweden HRH Crown Princess Victoria Lugrid Alice Desiree alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Mach 19, 2014 Princess Victoria, ambaye ameambatana na Waziri wa Biashara wa Sweden. Bi Ewa Björling, yuko nchini kwa ziara ya siku tatu.

  0 0

  Napenda kuwajulisha kwamba uzinduzi wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2014 utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi 2014 saa 5.00 kamili asubuhi katika hotel ya JB Belmont ukumbi wa savannah. 

  awali uzinduzi huu ulikuwa ufanyike sambamba na semina ya mawakala, lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu, imebidi semina isogezwe mbele hadi tarehe 25 Machi 2014. 

  Mawakala waliopo jijini DSM na wale wenye nafasi mnakaribishwa kuhudhuria uzinduzi huu. 

  natanguliza shukrani.

  HIDAN .O. RICCO.
  PRO.

  0 0

   Viongozi wakuu wa kampuni ya Smart Telecom,Afrika Masharikii wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi waliojipatia zawadi kupitia mtandao huo,baada ya kushiriki kwenye kampeni ya GIVE US A NAME iliofanyika hivi karibuni.
   Pichani kati ni Balozi wa Kampuni hiyo ya simu iliyozinduliwa leo jijini Dar,Msanii wa maigizo ya vichekesho atambulikae kwa jina la Hemed Maliyaga a.k.a Mkwere Orijini akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Telecom,Afrika Mashariki,Abdullatif Bouziani (shoto) na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham wakiwa katika picha ya pamoja.
   Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom,Afrika Mashariki,Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar,kulia kwake ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham 
  Pazia likishushwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kampuni hiyo ya simu za mikononi-Smart."lets talk.
   Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom,Afrika Mashariki,Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar


  IPS kukuza ujasiliamali wa jamii katika mawasiliano ya simu Burundi, Uganda na Tanzania


  Machi 19, 2014 Shirika la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya viwanda chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED),jana wametangaza kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini ya kampuni iitwayo SMART. 

  Jina la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED kukuza huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda, lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja


  Mtandao wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni washirika wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika shirika la Tcell linaloongoza katika kutoa huduma Tajikistan. 

  IPS pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee waliowekeza SEACOM submarine cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao ushirika wa IPS ndani ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya ushirikiano wa makampuni ya simu Nepal na Cambodia  na kuwafanya wawe waongozaji katika soko hili.


  Kuzinduliwa kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi wa sauti ambao utatoa fursa nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika Mashariki. AKFED imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance Group, National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.


  “Kazi zetu katika mawasiliano kwa njia ya simu hasa Roshan-Asia ya kati ni kuboresha uwekezaji wa jamii katika miundombinu ya jamii, huduma za afya na elimu. Pia kutengeneza biashara yenye mafanikio katika soko ili tuweze kujitofautisha na washindani wengine, Tunatazamia kuwa uwekezaji katika kampuni dada ya AKDN utakua umeenea katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka 100” alisema Lutaf Kassam Meneja wa IPS


  SMART itaingia katika masoko haya ikiwa na dhamira ya embrance tamaduni za ndani ili kuboresha jamii wanakofanyia kazi.mfano mzuri wa dhamiri hii ni njia ambayo jina la kampuni lilivyochaguliwa. Kampeni ya Tupe Jina ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2013 ikiwahamasisha watu wa Afrika Mashariki kupendekeza na kulipigia kura jina la kampuni.

   Kampeni hiyo iliwavutia zaidi ya watu 70,000 na majina tofautitofauti yalipendekezwa na kupigiwa kura. Mwisho kampeni ililipata jina la SMART ikikusudia kuangalia uvumbuzi wa mawazo katika soko la Afrika Mashariki.


  0 0

  Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Omar Kigoda akiongea ofisini kwake jijini Dar es Salaam na ujumbe kutoka kampuni ya Ujerumani ya Helma Dungemittel ambayo ina mpango wa kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia. Pembeni yake ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bi. Janet Mbene pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Oliver Mehl.
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Omar Kigoda akisisitiza jambo.
  Ujumbe kutoka kampuni ya Ujerumani ya Helma Dungemittel ukimsikiliza waziri.
   Wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakifuatilia mkutano huo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ujerumani ya Helma Dungemittel, Bw. Oliver Mehl akitoa maelezo juu ya ujio wao na kuelezea mambo watakayoyafanya.

  0 0

  Afisa Habari wa Wizara ya Viwanda na Uchukuzi, Nicodemas Mushi (kulia) akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam kuelezea tamko la serikali kuanza ukaguzi wa leseni za biashara. Pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uhamasishaji Biashara na Masoko, Mashingo Christopher.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uhamasishaji Biashara na Masoko, Mashingo Christopher (kati) akikazia tamko la serikali juu ya ukaguzi wa leseni za biashara. Pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Viwanda na Uchukuzi, Nicodemas Mushi (kushoto) na Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Frank Mvungi.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
  Serikali ilirejesha utaratibu wa kupata leseni ya biashara kwa kulipia kuanzia 1/7/2013. Wizara ilitoa kipindi cha miezi 6 kwa wafanyabiashara waliokuwa na leseni zisizo na ukomo kuhuisha leseni zao. Kipindi hicho cha miezi 6 kiliishia 31/12/2013. 

  Na kama tulivyowatangazia Umma, wale waliochelewa kufanya hivyo walipata leseni zao kwa kulipa ada na adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Leseni Namba 25 ya 1972 kifungu cha 11(a) na (b). Ukaguzi: (Kifungu na 17 cha Sheria Na 25 ya 1972) Ukaguzi unafanyika ili kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa mujibu wa Sheria na taratibu za nchi. 

  Kama alivyoagiza KMWVB, kwamba Mamlaka za Leseni zifanye ukaguzi wa kina katika maeneo yao, tunapenda kusisitiza kuwa ukaguzi huu ufanyike kati ya mwezi wa Aprili na Mei. Wito kwa wananchi Wananchi kufuata Sheria na taratibu za nchi, kwani kufanya hivyo ni alama ya maendeleo. Kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu, ni kwa jinsi gani watu hao wanafuata taratibu.

  0 0  Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela kushoto akikabidhi vifaa mbalimbali vya mchezo wa ngumi kwa kocha wa klab ya Msisiri Daudi Muhunzi ikiwa ni uboreshwaji wa klab hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni Dar es salaam  wa pili kulia ni Ally Moja na Rashid Kipaga Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

  =======  ========
  Msanii wa filamu za bongo Yusuph Mlela ameibukia katika mchezo wa masumbwi nchini kwa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo wa ngumi

  kama vile Glove,Clip bandeji,Proctecta,GumShit kwa klabu ya msisili iliyopo kinondoni Dar es salaam akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa hivyo Mlela alisema nimevutiwa na vijana wenzangu jinsi wanavyojituma kufanya mazoezi hivyo nikaamua kujitolea kidogo nilicho nacho kwa ajili ya kuendereza mchezo huu wa masumbwi

  katika kata yangu ambapo mimi naishi karibu na maeneo haya hivyowalivyo niomba nichangie nikawa sina jinsi kwa kuwa na mimi mwenyewe siku moja moja nitakuwa nakuja kufanya mazoezi hapa hapa nawaomba wadau wengine wenye uwezo zaidi yangu ata ambao wapo kama mimi wasaidie vijana kwa ajili ya kujiendeleza na mchezo huu waupendao

  Nae kocha wa mchezo wa ngumi katika Klabu ya Msisiri Daudi Muhunzi alitoa shuklani zake kwa Mlela kuwakumbuka vijana wenzie ambao walikuwa na huaba wa vifaa vya ngumi kwani yeye amekuwa kama mkombozi katika kata hiyo

  aliongeza kwa kusema tunaomba wadau wengine waje watusaidie vifaa mbalimbali kama punch bag,pad na maswala ya hudhamini wa  muda mrefu   kwa ajili ya kuendereza gym hii ambayo tunaitumia kwa kuchangia kidogo .

  0 0

  Meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd,s Miss Tanzania 2014kulia ni   mkurugenzi wa kamåuni ya LINO International Hashi Lundenga ambao ni waandaaji wa mashindano hayo na kushoto ni  Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
   Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International Hashi Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
   Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kwenye uzinduzi jijini Dar Es Salaam.

  0 0

   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo.
   Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyevaa fulana nyeusi) akihoji uimara wa sehemu ya kutulia ndege wakati walipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
   Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mhandisi Mugasa Mlondo akitoa maelezo juu uimara na ubora wa uwanja wake wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo. Picha na Saidi Mkabakuli.

  ========  =========  ======
  UWANJA WA NDEGE MTWARA KUIMARISHWA ZAIDI

  Na Saidi Mkabakuli.

  Serikali imesema kuwa kuna haja ya kuuimarisha Uwanja wa Ndege wa Mtwara ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za huduma, hasa kufuatia kugundulika kwa gesi mkoani humo, hali inayochochea mahitaji makubwa ya kuutumia uwanja huo.

  Hayo yamebainishwa mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  wakati ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja wa huo.

  Bibi Mwanri alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini na mikakati mbalimbali itakayopelekea kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara ili kuweza kuhudumia uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni mbali mbali ya ndani na nje ya nchi mkoani humo. Aliongeza: “Tathmini ya awali inaonesha kuwa miradi mingi ipo mkoani Mtwara kufuatia kugundulika kwa gesi hivyo kuna haja ya dhati ya kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara kwa lengo la kutoa huduma za uhakika wakati huu wa mfumuko wa kiuchumi mkoani Mtwara,” alisema Bibi Mwanri.

  Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara ambaye alikuwa kiongozi mwenza wa ukaguzi, alisema kuwa kuna haja ya dhati ya kuwekeza katika uwanja huo ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara kufuatia wawekezaji wengi kuendelea kumiminika na kuwekeza mkoani humo.

  “Uwanja wa ndege wa Mtwara una fursa za nyingi za kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, hakika ni lango la biashara hasa kipindi hiki cha uchumi wa gesi mkoani Mtwara, hivyo uendelezaji wa uwanja huu ni jambo lisilo epukika,” alisema Prof. Rutasitara.
  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),  Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.
  Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.
  Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  0 0

  IMAG0466

  Mzee Bakari (mwenye shati ya bluu) wa Kijiji cha Madanga wilaya ya Pangani, akipongeza Kituo cha Redio cha Pangani FM kuendeleza Kiswahili kupitia kipindi cha Lugha ya Kiswahili.
  Na.Mwandishi wetu,

  Kikundi cha Wazee cha MWEHU katika kijiji cha Madanga wilayani Pangani kimeipongeza redio ya Pangani FM kwa kueleza Kiswahili kupitia kipindi kinachorushwa hewani na kituo hicho.

  Wakichangia majadiliano ya kikundi kufuatilia usikivu wa vipindi vya kituo hicho, zoezi linalofanywa kwa pamoja na Redio Pangani FM kwa kushirkiana na Shirika la Kimataifa la UNESCO, wazee hao wamesema wanafurahishwa sana na kipindi cha LUGHA YA KISWAHILI kinachorushwa hewani kila Alhamisi jioni na kurudiwa Jumamosi mchana.

  “Kile kipindi cha Kiswahili kinanikosha sana kwa sababu Kiswahili kinachozungumzwa na vijana wa sasa sio Kiswahili kizuri kwa mfano ‘kasheshe, mkwara’… tofauti na Kiswahili tulichosoma cha Hekaya za Abunuwasi kinapendeza sana. Nakipenda kipindi cha Kiswahili kiendelee sana kwa sababu kinaendeleza utashi wa lugha ya taifa”, alisema mzee aliyejitaja kwa jina moja la Mzee Bakari.

  Wamesema Kiswahili kinachozungumzwa hivi sasa na kizazi kipya kinapotosha kwa kuingiza na kuondoa baadhi ya maneno, matamshi mabaya kiasi kwamba kinaondoa maana nzima ya kukuza Kiswahili na kuienzi kama lugha ya taifa.
  IMAG0463
  Mzee Mwehu (koti la suti) wa kikundi cha wazee cha MWEHU kijiji cha Madanga, Pangani akitoa mapendekezo yake ya kuanzishwa kipindi cha wazee chenye lengo la kuibua matatizo yanayowasibu.

  Pamoja na kukisifu kipindi cha Kiswahili, wazee hao pia wamempongeza mtayarishaji wa kipindi hicho kwa kusema kwamba yuko makini na umahiri mkubwa katika utayarishaji na utangazaji wake.
  Vipindi vingine visivyosifiwa ni pamoja na kipindi cha Urithi wa Pangani, Muziki, Michezo na Taarifa ya Habari.

  Zoezi la ufuatiliaji na tathmini ni miongoni mwa utekelezaji wa mradi wa kuzipa uwezo Redio 9 za Jamii za kutumia TEHAMA kutayarisha vipindi vya afya, kilimo na elimu ili kutoa taarifa ya maeneo hayo kwa urahisi na wingi, unaotekelezwa na UNESCO kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA).

  Hata hivyo wazee hao wamependekeza kuanzishwa kwa kipindi cha wazee jambo ambalo wanasema kuonekana kusahaulika kwa kuwa wana urithi wa mambo mengi yenye busara ambayo ni hazina kwa maendeleo ya wanajamii wa Pangani.

  “Mimi masikitiko yangu ni kutokosekana kwa kipindi cha wazee. Tuna matatizo yetu mengi yanayotusibu lakini hakuna pa kuyasemea. Kwa mfano tuna tatizo la maji hapa, tumefuatilia kwa viongozi lakini tunazungushwa tu.

  Laiti tungeyazungumza haya kupitia kipindi chetu, tungefikisha ujumbe”, alisema mzee maarufu kwa jina la MWEHU.
  IMAG0470
  Mzee Hadhrina Hatibu Msiagi wa kijiji cha Madanga akizungumza na Mtangazaji wa Pangani FM, Bi. Maajabu Ali kuhusu umuhimu wa kuwa na msemaji mahiri wa historia za kale za Pangani wakati wa zoezi la ufuatiliaji na tathmini lilioendeshwa kwa pamoja na Redio Pangani na UNESCO hivi karibuni.

  Kwa upande wa kipindi cha Urithi wa Pangani, wamependekeza kuboreshwa kwa kipindi hicho kwa kumtafuta msemaji anayeijua kwa kina historia ya kale ya Pangani kinyume cha ilivyo sasa.
  Wamesema Pangani ina utajiri wa historia ya kale lakini anayekiendesha kuzungumzia historia ya kale ya jana hivyo kuwanyima wanajamii haki ya kujua na ukweli wa chimbuko lao.

  “Kuna mambo mengi ya kale ya Pangani, lakini siyo yanayozungumzwa, yanayozungumzwa ni ya jana kwa hiyo tunataka wapatikane watu wazee wanaozijua habari hizo”, alisema Mzee Hadhrina Hatibu Msiagi.
  Kijiji cha Madanga ni miongoni mwa vijiji kongwe vya kwanza kuanzishwa ndani ya wilaya ya Pangani, kilichoanzishwa karne ya 17. Vijiji vingine ni Mwera, Pangani na Bushiri.
  SAM_0015
  Kikundi cha Wazee cha MWEHU wakiwa katika picha ya pamoja na wanaoendesha zoezi la ufuatiliaji na tathmini ya vipindi vya Pangani FM kijijini Madanga.

  0 0

   Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
   Bi Severa joseph akitoa maelezo ya aina ya dawa zinazotumika kwa akina mama wajawazito katika kituo cha afya Kaloleni cha jijini arusha kwa baadhi ya washiriki wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani.
  Dr Anna Kimaro mganga wa zamu wa kituo cha afya Kaloleni aliyebeba faili kwapani akiwa na wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani YWCA walipo tembelea katika kituo hicho jijini arusha.
   Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha wakipata maelezo ya kina kutoka kwa moja ya wafanyakazi wa kituo hicho.

  0 0

   • CCM bado inaamini katika Muundo wa Serikali mbili
   • CCM ina amini Muungano huu muhimu unadumishwa na kuimarishwa
   • Muundo tulionao uboreshwe
   • Tutangulize mbele Uzalendo na maslahi ya kweli ya nchi yetu.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti CCM Makao Makuu Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo alizungumzia imani ya CCM katika muundo wa serikali mbili.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza  baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Lumumba jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Machi 2014.
   ========  ======  =======
   Juzi tarehe 18/03/2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha kwenye Bunge maalum la Katiba rasimu ya pili ya katiba.

   Toka awasilishe rasimu ile bungeni , kumekuwa na maombi mengi sana ya kutaka kujua kama msimamo wa CCM juu ya baadhi ya mambo hasa muundo wa muungano bado ni uleule.

   Kwasababu ya maombi hayo CCM imeona bora kueleza kwa mara nyingine tena msimamo na imani ya CCM juu ya swala zima la Muungano na muundo wake.

   Kimsingi CCM ndio waasisi wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. CCM inamasilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.

   Bado CCM inaamini changamoto za Muungano huu suluhisho lake sio kubadili muundo wa Muungano bali ni kuufanyia maboresho muundo wa muungano tulionao wa serikali mbili. Hivyo basi CCM bado inaamini muundo bora kwasasa utakao dumisha muungano wetu ni muundo wa SERIKALI MBILI.

   Kwakuwa kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi, kuisha kwa kazi yao ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya Tume sio mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo bali ni mwanzo wa awamu nyingine ya mjadala mpana na maboresho kama sio marekebisho ya kuondoa mapungufu kwenye rasimu iliyowasilishwa.

   Mwanzo wa awamu hii nyingine ni furusa nzuri ya kupima kama kweli yaliyomo kwenye rasimu na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yana akisi maoni ya Watanzania walio wengi.

   CCM   ina amini awamu mbili zilizobaki kwakuwa zinahusisha wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge maalum la Katiba, na hatimaye itawahusisha wananchi wenyewe moja kwa moja kupitia kura yao, zitatumika vizuri kutupa ni nini hasa matakwa ya Watanzania juu ya Katiba waitakayo na sio maoni au matakwa ya wachache.

   Wakati haya yote yakiendelea CCM bado tunaamini Muungano huu ni muhimu ukadumishwa na kuimarishwa. CCM tunaaamini ili Muungano huu udumu njia pekee kwasasa ni kufanya marekebisho kwenye Muundo wa serikali mbili ili ujibu vizuri zaidi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kukidhi mazingira ya sasa.

   Tunawaomba wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi hiki. Ni vizuri Watanzania tukavumiliana,tukashindana kwa hoja tukitanguliza mbele uzalendo na masilahi ya kweli ya nchi yetu.
   KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

   Imetolewa na;-
   Nape Moses Nnauye
   Katibu wa Itikadi na Uenezi 

  0 0   Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam
  Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusiana na masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini. Pamoja nae ni Ofisa Mwandamizi Habari, elimu na mawasiliano, Veneranda Malima. 
   *********
   1.0     UTANGULIZI

   Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi majukumu yake Julai 2005. Bodi ina majukumu makuu mawili; kwanza ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa ajili ya masomo ya Shahada au Stashahada ya juu. 
  Jukumu la pili ni kukusanya marejesho ya mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994.

  2.0        UTOAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
   Tangu kuanzishwa kwake, Bodi imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya Wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla Bodi haijaanzishwa. Mwaka 2005/2006 Bodi ilipoanza kazi ilitoa mikopo kwa Wanafunzi 42,729 wa elimu ya juu kwa kutumia bajeti shilingi Bilioni 56.1.

  Idadi ya Wanafunzi wa elimu ya juu wanaopewa mikopo imeendelea kuongezeka kutoka  wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi Wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013. Hii ni sawa na ongezeko la wastani wa 10.4% kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS 56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS 306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.

  Kwa mwaka wa masomo 2013/2014, jumla ya wanafunzi 95,178wamenufaika na mikopo hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2014 ambao mikopo ya kiasi cha TZS 223,977,042,853.00 imekwishalipwa.  Mwaka
  Idadi ya Wanafunzi Waliokopeshwa
  Ongezeko
  (%)
  Kiasi kilichoko-peshwa
  (Tshs Bilioni)
  Ongezeko
  (%)
  2004/05 (Na Wizara)

  16,345

  -

  9.9

  -
  2005/2006
  42,729
  161.4
  56.1
  467
  2006/2007
  47,554
  11.3
  76.1
  35.7
  2007/2008 
  55,687
  17.1
  110.8
  45.6
  2008/2009
  58,798
  5.6
  139.0

  25.5
  2009/2010
  72,035
  18.4
  237.8
  28.7
  2010/2011
  92,791
  28.8
  230.0
  24.5
  2011/2012
  94,533
  2.0
  311
  35.0
  2012/2013
  97,348
  2.9
  335.2
  7.2

  0 0

    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani,Mwishehe Shaban Mlawa akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye kijiji cha Misakazi,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014
    Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akitambulishwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwidu,Mzee Mohamed Said kwa Bw. Chomiki kutoka jamii ya Wafugaji mwenye makazi katika kijiji hicho,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014.
   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mzee Ally Mohamed Meta mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kampeni kwenye Kijiji cha Misakazi,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014.
   Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Sam wa Ukweli akitoa burudani kwa wananchi wakazi wa kijiji cha Misakazi,Kata ya Ubena ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 20, 2014


  0 0

  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule, (aliyeshika vitabu) akifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo tofauti tofauti kutoka kampuni ya  simu ya Airtel jana. katikati ni Ofisa Masoko wa kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga na Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Mbeya Priscus Kimario.  
   Ofisa Masoko wa kampuni ya simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga, akionesha vitabu kabla ya kumkabidhi mkuu wa shule ya Sekondari ya  Mbeya, Magreth Haule (kushoto) wakati walipofika shuleni hapo kutoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
   Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa shule hiyo  kwa maofisa wa kampuni ya Simu ya Airtel mara baada ya kupokea msaada wa vitabu zaidi ya 200 vya masomo tofauti tofauti kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne jana. (katikati) ni Ofisa Masoko wa kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga na Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Mbeya Priscus Kimario.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule (kushoto) akikabidhiwa msaada wa Vitabu vya masomo tofauti tofauti jana kutoka kwa Ofisa Masoko wa kampuni ya simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga, (katikati) vitabu hivyo vilivyotolewa msaada na kampuni hiyo.
   ========  ======  =======
  AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE ZA SEKONDARI MBEYA

  Kampuni ya simu ya Airtel chini ya mradi wa shule yetu imetoa msaada wa vitabu  vyenye thamani ya takriban shilingi milioni 2 kwa shule ya sekondari ya Mbeya.

  Makadhiano ya vitabu yameshuhudiwa na jumuiya nzima ya Shule yenye zaidi ya watu takribani 1365 wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine waliokusanyika kwa shauku ya kupokea vitabu hivyo ikichagizwa na kauli mbiu ya Airtel Baba lao.

  Afisa Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini, Jonas Mmbaga amesema “lengo la kutoa msaada huo ni kutekeleza azma ya kuendeleza ushirikiano na jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kukuza taaluma mashuleni. Chini ya mpango wa shule yetu tumeweza kuzifikia shule mbalimbali nchini na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari mbeya.


  Mbaga alisema Vitabu hivi ni vya masomo ya sayansi vikiwemo vya Hisabati, Kemia, Fizikia, na Biolojia, kwa ajili ya  kidato cha kwanza hadi cha nne. Na tumeichagua shule ya Sekondari Mbeya ili kuwakilisha shule nyingine zilizopo mkoani Mbeya.

  “Tunaahidi kuendelea kuzifikia shule nyingi zaidi mkoani hapa na mikoa ya jirani kupitia mpango wetu maalum wa shule yetu ambao ni endelevu uliodumu zaidi ya miaka 7 mpaka sasa.  Tuaamini kwa kujikita kwenye sekta ya elimu tunaendeleza ushirikaino wetu na serikali chini ya wizara ya elimu kusaidia kutatua changamoto zilizopo husasani ya vitabu mashuleni na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini”.aliongoza Mmbaga

  Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbeya Bi Magreth Haule alisema” Nawashukuru sana Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa shuleni hapa huu ni uthibitisho kuwa Airtel wapo karibu na jamii hasa katika kuendeleza sekta ya elimu. Msaada huu ni mchango mkubwa na ni changamoto kwa wanafunzi na walimu kuongeza juhudi katika kuhakikisha tunakuza kiwango cha elimu shuleni hapa. Tunaahidi kuvitumia vizuri vitabu hivi kwa manufaa ya wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla

  Nao Wanafunzi  Revina Florence, Denis Michael na Happy Mwaisengela kwa nyakati tofauti na kwa niaba ya wenzao wameipomgeza kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada huo na kwamba vitabu hivyo vitachochea hamasa za wanafunzi kuongeza bidii katika masomo ili kufikia lengo lililokusudiwa.

  Vitabu hivyo ni mwendelezo wa shughuli za huduma kwa jamii zinazotelewa na Airtel kupitia mradi maalumu wa Shule yetu unaoziwezesha shule mbalimbali kutapa vitabu vya ada na kiada, mpaka sasa shule zaidi ya 900 zimeshafaidika na mpango huu


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Fatma Abubakar Mwassa akikata utepe kuzindua rasmi tawi la AccessBank Tabora mnamo tarehe 15th March 2014. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Masoko mkuu mwandamizi wa benki hiyo Ndugu Muganyizi Bisheko akifatiwa na muwakilishi wa uongozi wa AccessBank Ndugu Emmanuel Venance. Waliosimama kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tabora mh. Suleiman Kumchaya akifatiwa na Meneja wa Tawi hilo ndugu Enosy Ndobeji.
  Meneja wa Tawi la AccessBank Tabora ndugu Enosy Ndobeji akitoa neon la shukrani kwa walioudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi hilo. Kushoto kwake ni Afisa Masoko mkuu mwandamizi wa Benki hiyo ndugu Muganyizi Bisheko na aliekaa kulia ni Mwakilishi wa uongozi wa Benki hiyo ndugu Emmanuel Venance.  Wafanyakazi wa AccessBank tawi la Tabora wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hili iliyofanyika tarehe 15th March 2014.

older | 1 | .... | 251 | 252 | (Page 253) | 254 | 255 | .... | 1897 | newer