Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 249 | 250 | (Page 251) | 252 | 253 | .... | 1896 | newer

  0 0


  UTAMADUNI huu ulioanza wa waamini licha ya kusali, pia wakaenda kusherehekea sikukuu hizi za kiroho ni mgeni na mzuri kwa kuwa unawajenga watu kiroho, na kuwaepushia uwezekano wa kutumbukia katika matatizo kwa kwenda katika maeneo mbalimbali ya sterehe; Amesema Askofu Method Kilaini.

  Mhashamu Kilaini ambaye ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, ameyasema hayo alipozungumza na Gazeti hili kuhusu Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika katika jiji la Dar es Salaam, Aprili 20 mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Pasaka.

  Mwaka huu Sikukuu ya Pasaka inaangukia Jumapili ya Aprili 20, Tamasha la Pasaka linatarajiwa kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini kwa siku tofauti  kuanzia Siku hiyo ya Pasaka. Akifafanua faida za Tamasha la Pasaka na mengine ya kidini kama Tamasha la Krismasi, Mhashamu Kilaini amesema yanasaidia kuifanya dini isiishie kanisani pekee kwa siku za sikukuu mfano Pasaka na Krismasi, badala yake kuifanya iende hata katika maeneo ya starehe yanayozingatia usafi wa kimwili na kiroho.

  “…Wakienda kwenye matamasha kama hili la Krismasi, watu waanze kwa sala, maombi na hata mahubiri kidogo ili waendeleze moyo wa kumpenda Bwana (Yesu Kristo) maana katika matamasha kama haya, hakuna ulevi, uzinzi wala ufuska,” amesema Mhashamu Kilaini.Akaongeza, “Utamaduni huu wa kusherehekea siku za Sikukuu katika Jina la Bwana katika matamasha ni mpya, lakini pia ni mzuri maana unawaondoa watu katika vishawishi vya kuhangaikia katika mambo yanayowatia hatarini kimwili na kiroho na kulazimisha matumizi ya pesa yasiyo ya lazima….”

  Amesema ili kushirikishana neema na baraka katika matamasha kama hilo la Pasaka, ni vema waamini wakajitokeza na kwenda kwa pamoja kama familia ili wafurahie kwa kufahamiana vema zaidi na Wakristo wenzao. Hata hivyo amesema katika sikukuu kama hizi, ni vema pia kuzingatia suala la usalama wa familia kwa kuhakikisha kuna ulinzi ili kuepusha uwezekano wa kufanyika vitendo vya kihalifu. “…Kwa yule anayependa kukaa na familia yake nyumbani, akae nyumbani, badala ya kwenda katika baa na sehemu nyingine zinazohatarisha imani, amani na usalama wake,” amesema. Tamasha hilo linatarajiwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwamo waimbaji maarufu wa muziki wa Injili toka ndani na nje ya nchi.

  Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa Tamasha la Pasaka mwaka 2014 imekuwa ikiendesha upigaji kura kwa njia ya ujumbe mfupi za maandishi za simu za mkononi (sms) ili waumini na wapenzi wa Tamasha la Pasaka wamchague mgeni rasmi, waimbaji wanaotaka watumbize katika tamasha hilo pamoja na mikoa wanayoitaka. Zoezi la upigaji kura linaendelea.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama amenukuliwa na vyombo vya habari akiutaarifu umma kuwa, kupitia upigaji kura huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete anaendelea kuongoza kwa kura za kuwa mgeni rasmi katika Tamasha hilo zilizofikia milioni 6.9 idadi ambayo haijafikiwa na kiongozi mwingine yeyote.

  Habari zinasema katika kura hizo, Rais Kikwete anafuatiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima. Kwa upande wa muziki wa Injili, waimbaji kadhaa wamekwishachomoza miongoni mwao wakiwa ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Voice Acapela na Sarah Kiare kutoka Kenya.

  Hivi karibuni, waimbaji Rose Muhando na John Lisu wamewashukuru mashabiki wa Tamasha la Pasaka kwa kuwapigia kura nyingi zilizowahakikishia kushiriki katika Tamasha hilo. Mchuano mkali kumpata mgeni rasmi kwa upigaji kura huo ulikuwa hasa baina ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Regnald Mengi, Mwangalizi Mkuu wa WAPO Mission International Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekolo maarufu kama “Mzee wa Upako”.

  0 0


  kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani
  ======  =====  =====
  Na Edwin Moshi, Njombe
  Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  imesema kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi, ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki

  Tukio hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta mkoani Mbeya

  Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo na chanzo bado hakijafahamika

  0 0   Nadhir (kushoto) akimkabidhi hundi,   Rehane Jaffer (kulia) yenye thamani ya sh 500,000.
  =====  ==== =====

  Na Andrew Chale

  KAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za   
  majumbani na ofisini ya Home 
  Shopping Centre (HSC) imemzawadia 
  mshindi wake wa kwanza 
  wa ‘pendezesha nyumba na HSC’ 
  ,Rehane Jaffer hundi ya sh 500,000.


  Shindano hilo linaendeshwa  
  kwenye mtandao wa kijamii wa 
  Facebook na limepewa jina la 
  ‘Give a Way’. 
  Hundi hiyo ilikabidhiwa jijini 
  Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, 
  Meneja Mauzo na Masoko wa HSC, 
  Nadhir Mubarak Bahayan ambaye 
  aliwataka watanzania kushiriki 
  shindano hilo ambalo kila Ijumaa 
  watakuwa wakijishindia sh. 
  500,000.

  “Wateja wetu wa HSC,  
  wanatakiwa kujiunga kwenye 
  mtandao wetu wa facebook na 
  kisha kututumia picha walizopamba
  ndani ya nyumba zao zitokanazo 
  na bidha a zetu,” alisema Nadhir.

  Alisema shindano hilo litaendeshwa 
  kwa mwezi mzima wa
  Machi. Mshindi huyo aliipongeza 
  HSC kwa shindano hio na kusema
  ni faraja kwake na familia yake. 
  Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa
  kwa  muda wa mwezi mzima wa Machi 
  huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza 
  washindi na kukabidhiwa hundi 
  siku inayofuata.

  Nadhir aliwataka wateja wao 
  kuwa natabia ya kutembea kwenye
  mtandao wa HSC,  na kushiriki 

  0 0

   Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga, na Mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya habari Frank Mvungi 
   Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda  katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga  
  Mhandisi wa mradi wa  magadi soda  Godfrey Mahundi akitoa ufafanuzi kuhusu makadirio ya gharama za mradi huo ambao unakadiriwa kutumia  kiasi cha dola za kimarekani milioni 500. Katikati ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba na wa mwisho ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga.PICHA ZOTE  NA. Georgina Misama-MAELEZO.
  ========    ==========  ========
  Frank Mvungi-MAELEZO.


  IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni  mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni  480 kwa mwaka.


  Hayo yamesemwa na  Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Ngapemba alisema hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini hayo katika Bonde la Engaruka  Wilayani Monduli mkoani Arusha.

  Alizitaja faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na fedha za kigeni kutokana  na mauzo ya madini hayo nje ya nchi. Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.

  Ngapemba  alibainisha kuwa madini ya magadi soda yanatumika viwandani  katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza  karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.


  Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu  tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda. Alisema kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata ni kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.

  “Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo”, alisema Ngapemba na kuongeza:


  Alisema kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014.  
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya, wakati alipotembelea banda la Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi  mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kulia ni Mkuu wa Maendeleo ya Biasara na Habari, Linda Byaba.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kushoto ni Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya (kulia) ni Mkuu wa Maendeleo ya Biasara na Habari, Linda Byaba
     Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia ukumbini humo. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka ukumbini baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Makamu  Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Phillip Mangula, ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, mara baada ya kufungua mkutano huo leo kweny Ukumbi wa Mwalimu Nyerere.  

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo wakati wa kumkabidhi  Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Rashid Seif Suleiman (Mwenye Kanzu)Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha na Nafisa M. Ali-WMM
  Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

  Na Nafisa M. Ali –WMM    
        17/03/2014
  Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 leo imekabidhi rasmi Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa  Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Akikabidhi Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema kazi hiyo waliyopewa wameweza kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na walikuwa huru bila ya kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi yoyote.

  Aidha alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi wa Zanzibar. Hata hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa kuifanya kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi hiyo na majukumu mengine walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi hiyo walitakiwa kuikabidhi kesho na badala yake wameweza kuikabidhi leo.

  Aidha mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo. Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi walizingatia uhalisia wa kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu.

  Aidha alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia. Hata hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa mujibu wa taratibu zilizopo. Aidha aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala Serikali.

  Naye Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki  itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika. Bodi hiyo ya Wajumbe watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Baharini kifungu no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 iliyotokea Miezi miwili iliyopita katika Mkondo wa Nungwi ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja.
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   mshindi wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa akiwa na mke wake Robby Mgimwa wakifurahia hati aliyokabidhiwa ya kuwa mbunge.
   Godfrey Mgimwa akiwa anafurahia ushindi katikati Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijiji mama Mtavilalo.

  0 0

   

  Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mfano wa hundimwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo wakati wa halfa ya Tuzo za Mwanamakuka 2014 ambapo Airtel Tanzania ni moja kati ya Wadhamini wa tuzo hizo,  Bi Leil Mwambungu aliibuka na kutangazwa mshindi wa mwanamakuka 2014. Akishuhudia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha (wakwanza kulia), Hafla ya mwanamakuka ilifanyika jana katika ukumbi wa Escape 1 mikocheni Dar es salaam. 

   Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kulia) akimpongeza mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika halfa ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam
  mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika hafla ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam, pichani kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha

  ========  ========  =========
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imekabithi waandaaji wa Tuzo za mwanamakuka The Unity of Women Friends kiasi cha million tano pesa taslimu wakati wa halfa ya  tuzo za mwanamakuka 2014 zilizofanyika jijini Dar es saalam mwisho wa wiki
  Tuzo hizi za mwanamakuka 2014 ziliwashirikiasha washindi 10 wa mwaka 2012 na mwaka 2013 ambapo washindi hawa walifatiliwa biashara zao na kuchaguliwa mshindi mmoja aliyefanya vizuri na kutumia vyema zawadi aliyoshinda katika kuendeleza biashara zao ambapo bi Leila Mwambungu aliyekuwa mshindi wa pili mwaka Jana kuibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
  Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema”  Tunayofuraha kuwa  wadhamini  wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa miaka mitatu mfululizo kwa sasa na kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa wanawake kupitia tuzo hizi. tunafurahi kuona jinsi kina mama hawa wajasiriamali walioshinda miaka iliyopita wakifanya vizuri katika biashara zao.
  Na sisi Airtel leo tunakabithi kiasi cha kiasi cha shilingi milioni tano kama mchango wetu kwa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka 2014. Tunaamini kiasi hichi cha fedha kitaweza kuwawezesha waaandawaji wa tuzo hizi kufanikisha halfa hii na kuwafikia wanawake na kuwawezesha  kutanua mitaji yao na hatimae kuongeza kipato na faida zaidi na kujikwamua kiuchumi”.
  “Tutaendelea kushirikiana na The unity of Women Friends ili kuhakikisha tunaweza kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini” aliongeza Matinde.
  Kwa upande wake mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu Alisema “naona fahari na furaha kuwa mshindi wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka huu, napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi kwa kuniona kupitia juhudi ninazoziweka katika kazi zangu na biashara zangu. Mpaka sasa nimeweza kuajiri watanzania kupitia biashara zangu na  Kiasi hii nilichozawadiwa leo kitanisaidia sana kukuza mtaji. 

  Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza  katika biashara zao,  haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
  Naye mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema Tuzo hizi za Mwanamakuka zinaendelea kukua na kuziboresha zaidi,   kwa mwaka huu lengo letu lilikuwa ni kuwawezesha wachache kwa kuwafatilia washindi wetu 10 wamiaka iliyopita na kuona jinsi gani biashara zao zinavyoenda na kumzawadia anayefanya vizuri zaidi. Lengo ni kuendelea kuwahamasisha na kufatilia mafanikio yao kwa karibu.
  vilevule tukiangalia miaka iliyopita tuliweza kuwashirikisha wanawake tu katika sherehe za tuzo hizi lakini kwa mwaka huu tumeamua kushirikisha familia kwa kuandaa bonanza ambapo wakinababa na watoto kwa pamoja tunasherehekea mafanikio haya, na kusherehekea siku ya wanawake duaniani huku tukienzi juhudi za wanawake jasiri nchini na kuwazawadia
  Tunashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi miaka mitatu kwa sasa na tunaamini kuwa bado wataendelea kutoa mchango wao na kushirikiana nasi na kutuunga mkono kwa miaka mengine ijayo na kuhakikisha lengo letu la kumwinua mwanamke wa kitanzania linafikiwa. Alisema Shamo

  Kwa mwaka huu Tuzo hizi zilishirikisha washindi waliopatikana miaka iliyopita ambapo kati yao pamoja na Tatu  Ngao, Mwananne Msekalile, Sikudhani Daudi, Nasra, Aziz, Khalid, Leila Mwambungu, Selestina Renatus, Maajab Yusufu na Agnes Daudi  ambapo Bi Leila Mwambungu Ameibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014

  0 0


  ALLY MWAZOA PROMOTA
  WADAU wa mchezo wa masumbwi nchini Tanzania wamejitokeza kuwa walinzi wa mapambano yaliyo andaliwa na promota Ally Mwazoa yatakayoanza march 29, april 26 na mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba  akizungumzia mpambano wa Japhert Kaseba na Thomas mashali mpambano ambao umebakiza siku chache tu ili ufanyike

  Mwazoa aliwashukulu wadau hawo ambao wamejitokeza kwa ajili ya ulinzi wa ali ya juu utakaofanyika siku hiyo kwa mabondia na wadauwenyewe kukubali kulipa kiingilio na kufanya ulinzi wa kila kona katika ukumbi huo
  ambapo klabu mbalimbali za ngumi kutoka Temeke Ilala Kinondoni na Tanga pamoja na mikoa ya jirani na wadau wamejitokeza kuthibiti fujo mbalimbali ambazo zitajitokeza siku hiyo pia wale ambao wamedhamilia kufanya fujo siku hiyo kutakuwa naaskari kanzu mbalimbali hivyo watapata kipondo cha ali ya juu pamoja na kutupwa lupango

  Mwazoa aliongeza kwa kusema siku hiyo kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa kila upande wa ukumbi huo ili kuona matukio mbalimbali ya nje na ndani yatakayokuwa yakiendelea ili kuthibiti vitendo vya uhuzwaji wa tiketi feki na kuingia kiolela na kusababisha asara kwa promota na washiliki katika tukio zima

  aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi makali ambapo bondia Haji Juma atavaana na Juma Fundi wakati Fred Sayuni atapambana na Rajabu Mahoja na Zuber Kitandula atamenyana na Issa Omar wakati Bakari Dunda ataoneshana ubabe na Baina Mazola

         Mwazoa

  aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka  Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
  Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
  pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

  0 0

  MUIMBAJI wa muziki wa Injili raia wa Zambia, Ephraim Sekeleti naye amepata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili 20 jijini Dar es Salaam.

  Sekeleti ni mmoja wa waimbaji wa muda mrefu katika tamasha hilo amekubali kushiriki kwa sababu ana kiu ya kufikisha ujumbe wake kwa Watanzania.


  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama taratibu za kuwapata waimbaji mbalimbali watakaoshiriki katika tamasha hilo linaendelea. Msama alisema muimbaji raia wa Kidemokrasia ya Kongo, Faraja Ntaboba naye pia amechomoza kushiriki tamasha hilo ili kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu.


  Rebecca Malope ni miongoni mwa wasanii kutoka nje ya Tanzania watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu ambaye naye amethibitisha kuwepo kwenye tamasha hilo. Waimbaji wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na kwaya ya Kwetu Pazuri wote wa Tanzania.


   Aidha Msama alifafanua kuwa tamasha hilo linatarajia kuanza Aprili 20 jijini Dar es Salaam wakati siku inayofuata litafanyika mkoani Morogoro huku mikoa mingine ikiendelea kupigiwa kura.


  0 0

    NA ZAMARADI KAWAWA MAELEZO, DODOMA

  Kamati ya Maridhiano ya Bunge Maalum la KATIBA waridhia Jaji Joseph Warioba kuwasilisha bungeni Rasimu ya KATIBA kwa masaa 4 Jumanne, Machi 18, 2014

  Wabunge aw Bunge Maalum la Katiba wametakiwa kuhudhuria kikao cha bunge Hilo kesho Jumanne Saa Tatu asubuhi kwa shughuli za kuapishwa kwa wabunge 30 na kumsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba akiwasilisha rasimu ya KATIBA kwa muda wa masaa 4.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kikao cha maridhiano kilichohudhuriwa NA takriban viongozi aw vyama vya upinzani vya CUF, Chadema, NCCR NA wajumbe wengine kilichomalizika takriban saa 3.30 usiku, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Samuel Sitta amesema Jumatano kutakuwa na semina ya wabunge kuhusu kanuni za bunge Hilo.

  Amesema wamekubaliana kuwa semina ya wabunge Hao kuhusu historia ya Tanzania NA Zanzibar iliyokuwa ihutubiwe NA wataalam Sita toka pande mbili za Muungano imefutwa ili kuzuia Watu wasitoe hisia zao zitakazoweza kubadili misimamo ya wabunge.

  Aidha, Mheshimiwa Sita amesema kutakuwa NA semina ambapo mshauri aw Rais aw Kenya BW. Abdulkadeer NA Seneta Amos Wako watawasilisha mada kuhusu uzoefu wa Kenya katika kuandaa Katiba.

  Amesema wajumbe aw Kamati ya maridhiano wamekubaliana kuwa Rais Jakaya Kikwete atalihutubia bunge Hilo SIku ya Ijumaa saa 10 jioni kwa kuwa yeye ni sehemu muhimu ya bunge Hilo.

  0 0

   Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzania Bw. Yasunori Onishi (kulia) akielezea kuhusu watalaam wa kujitolea kutoka nchini Japan  walivyofanya kazi hapa nchini katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
   Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wake hapa nchini, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. 
   Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akitoa zawadi kwa Mtaalamu wa kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu kutoka Japan Bw.  Jun Tsuda (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita wa kujitolea kutoka nchini Japani iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzanian Bw. Yasunori Onishi.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kulia) akitoa ufafanuzi wa maswali kutoka kwa waandishi wa habari baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
  Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani (kushoto) akijibu maswali ya Mwandishi wa Habari wa gazeti la  Daily News Bi. Hilda Mhagama baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.

  0 0


            
          
      REPUBLIC OF RWANDA
      Higher Education in Science & Technology Critical for Africa’s Future, say Rwanda's President Kagame, WB's Makhtar Diop

  KIGALI, March 17, 2014 – At a high-level forum in the Rwandan capital, H.E. President Kagame, President of Rwanda and World Bank Vice President for Africa Makhtar Diop highlighted Africa’s urgent need for larger numbers of scientists, engineers, and technicians who can meet the growing market demand for such expertise and contribute to development and shared prosperity in their countries.

  Themed “Accelerating Africa’s Aspirations,” the forum on Higher Education for Science, Technology and Innovation was co-hosted by the Government of Rwanda, a champion of science and technology, and the World Bank, one of Africa’s largest development partners in higher education. The forum aimed to boost science, technology, and engineering capability as a key driver of economic growth and job creation.

  The governments represented at the forum (Ethiopia, Mozambique, Rwanda, Senegal and Uganda), private sector participants and development partners issued a communiqué to the effect that they would invest strategically in science, technology, and engineering education to accelerate Africa’s progress into a developed, knowledge-based society within a generation.
    
  H.E. President Paul Kagame said: "I welcome the commitment to strengthen and mobilise resources for building capacity in science and technology, in our pursuit of Africa’s socio-economic transformation. Our collective commitment must be followed by concrete action to drive innovation for the development of our people and our continent."

  Makhtar Diop, the World Bank’s Vice President for Africa, who delivered the keynote address, said:
  “To be more competitive, expand trade, and remove barriers to entering new markets, Africa must expand knowledge and expertise in science and technology. Let us set some bold targets: that we will see a doubling of the share of university students graduating from African universities with degrees in mathematics, science and technology by 2025. The time has never been more auspicious to focus on higher education, particularly in science, technology and mathematics.”

  In the concluding communiqué, countries present committed to collaborate with development partners and the private sector to support Africa’s socioeconomic transformation with strategic actions to reform tertiary education systems; increase the share of students in science, technology and engineering; and improve the quality of learning and research. 

  They also committed to use growing foreign direct investment flows to build greater technological capability, to enroll more women in science and technology disciplines, and to strengthen science and mathematics education at all levels.

  The forum highlighted the importance of setting up regional centers of excellence in various disciplines such as agriculture, biotechnology, health, water and sanitation, and ICTs. 

  “Regional partnerships help universities to pool their resources, achieve economies of scale, set up joint facilities and standards, and most importantly, share knowledge and expertise,” Diop noted, “Beyond the borders of the continent, we need to tap the vast experience of Brazil, China, India, and Korea.”  


  0 0

  Kamera za usalama zikimwonyesha rubani wa ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777, Zaharie Ahmed Shah,  kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.
  Michoro inayoonyesha njia ambayo ndege hiyo huenda ilipitia kwenda kusikojulikana.
  Mwanafunzi, Firman Siregar, akiwa na wazazi wake, ni mmoja wa abiria 239 waliokuwa katika  ndege hiyo yenye orodha ya safari namba  Flight MH370.
  Rubani Zaharie Ahmad Shah.
  Nyendo za ndege hizo zinavyokisiwa na wataalam.
  Mwandishi wa habari akichukua picha nyumba ya  rubani Fariq Abdul Hamid eneo la Shah Alam, karibu na Kuala Lumpur.
  Maafisa nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege hiyo kutoweka.
  Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, au goodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
  Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
  Juhudi za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.
  CHANZO: PICHA DAILYMAIL / HABARI BBC SWAHILI

  0 0

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama  akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Boma mara baada ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto 200 wa shule za msingi tano za wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam jana. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), na kufadhiliwa na kampuni ya Msama Promotions. 
   Baadhi ya watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Ilala wakionesha vipaji vya kucheza ngoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),na kufadhiliwa na Kampuni ya Msama Promotions . Jumla ya watoto 200 wamenufaika na mafunzo hayo.
    Mmoja wa wanafunzi akionesha mitindo ya mavazi.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buguruni Visiwi wakionesha mitindo mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa hafla hiyo.
   Mtoto Mariam Yusuf akisimulia hadithi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto wa shule za msiongi kutoka Manispaa ya Ilala. 
   Mtoto Mariam akionesha kipaji chake.
   Watoto wakicheza maigizo.
   Baadhi ya watoto wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana wakiwa katika hafla hio.
   Msama akiagana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana.
  DAR ES SALAAM, Tanzania

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama amepongeza hatua ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuanzisha mafunzo maalumu kwa watoto wa shule za msingi.
   
  Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo maalumu
  yanayolenga kuwajenga watoto katika fani ya sanaa na kushirikisha watoto wapatao 200 kutoka shule tano za wilaya ya Ilala, Msama alisema ni jambo zuri kuandaa vipaji vya kesho.
   
  “Mafunzo haya yataweza kuwajenga watoto wetu ambao ndio taifa la kesho, pia kupunguza tatizo la watoto kujiingiza katika mambo mabaya kama matumizi ya bangi, dawa za ulevya, hivyo kuwa mzigo na janga kwa taifa,” alisema Msama.
   
  Shule zilizonufaika na mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Msama kupitia
  kampuni yake ya Msama Promotions, waratibu wa Matamasha ya Pasaka na Krismas, ni Buguruni Moto, Buguruni Visiwi, Ilala Boma, Uhuru Wasichana na Msimbazi.
   
  Aidha, Msama alihimiza umuhimu wa somo la sanaa shuleni akitaka lipewe msisitizo mkubwa katika kuandaa vijana bora ambao hata kama wakifeli masomo mengine, wanaweza kuwa wasanii bora. “Somo hili la sanaa mashuleni lipewe uzito unaostaili kama masomo mengine kwa sababu, mtoto akifeli masomo mengine, fani ya sanaa yaweza kuwa msaada kwake,” alisema.
   
  Msama aliwashauri pia Basata kuyapeleka mafunzo hayo hadi mikoani na
  kupendekeza kwa hatua ya awali waanzie katika mikoa ya Pwani na Morogoro, akiamini kuna vipaji vingi vya sanaa.
   
  Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema mafunzo hayo yaliyoanza Machi 1, wanafunzi walikuwa wakifanya mazoezi ya sanaa katika fani utambaji, hadithi, ngoma za asili na maigizo katika maeneo ya shule zao chini ya usimamizi wa walimu wao na waratibu kutoka Basata.

  Mngereza alimshukuru mgeni rasmi Msama kwa kudhamini mafunzo hayo
  akisema amefanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu ya sanaa katika maisha ya kila siku.
   
  “Msama ameonesha wazi kuwa yeye ni mdau na mfurukutwa wa sanaa,
  aliyepania kuendeleza sekta ya utamaduni hasa sanaa kwa kuibua vipaji vya
  watoto,” alisema.

  0 0

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto) na Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha Msata,Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa Lugoba,Chalinze.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akiambatana na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chalinze (CCM),Saleh Mpwimbwi (kushoto) pamoja na Msafara wake wakielekea kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakishiriki kwenye dua ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kisomo cha kumuombea Marehemu ambaye ni Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman (alieketi nyuma ya mgombe) mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Adelaide cha Jijini Adelaide nchini Australia Alec Gilbert (wa tatu kushoto), akitoa maelezo ya namna ya ujenzi na uendeshaji. Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC, Mkurugenzi Mwendeshaji na Maofisa wawili wapo nchini Australia katika ziara ya mafunzo ambapo mbali na kutembelea Kituo cha Adelaide pia watatembelea Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Melbourne kilichopo katika Jijini la Melbourne chini Australia.

  0 0  0 0

   Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake. Kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia).
   Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa akisisitiza jambo wakati wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake.
   Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa (Wapili kulia, aliyenyanyua mikono) akiwaonesha eneo litakapokuwepo Hospitali mpya ya rufaa mkoani humo wakati wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika kujionea maendeleo ya maandalizi ya awali ya ujenzi wa hospitali hiyo.
   Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdallah Komba (aliyeinama) akiwaelekeza namna ya hospitali ya rufaa ya mkoa huo itakavyokuwa wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea mradi huo.
  Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza wakati timu yake ilipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya awali ya ujenzi wa hospitali hiyo.
  =======  =======  =========
  MTWARA KUJIVUNIA HOSPITALI YA RUFAA
  Na Saidi Mkabakuli
  Wakazi wa mikoa ya kusini ikiwemo Mtwara, Lindi, na Ruvuma inatarajiwa kupata hospitali ya kisasa ya rufaa itakayojengwa katika eneo la Mikindani, nje kidogo ya mkoa wa Mtwara katika lengo la kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unakuwa shirikishi na kuendelea kuboresha huduma za jamii hususan na afya katika mikoa hiyo.
  Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya katika mkoa huo.
  “Mradi wa hospitali ya Rufaa ya Mtwara umelenga kutoa huduma za rufaa kwa kanda ya kusini hususan mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma, hospitali hii itakapokamilika inategemewa kuchukua wagonjwa wa nje na ndani watakaohudumiwa kwenye vitengo mbalimbali vinavyojitosheleza kwa vifaa na wataalamu, “ alisema Dkt. Maarifa. Kwa mujibu wa taarifa za awali mradi ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2012/13 kwa fedha za Serikali zinazotolewa kupitia ngazi ya wizara ambapo mpaka sasa ujenzi wa uzio kuzunguka eneo hilo umekamilika.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa suala la afya kwa wakazi wa mikoa ya kusini, na akatoa wito kwa uongozi wa mkoa kuzingatia na kusimamia matumizi sahihi ya fedha za serikali katika mradi huo.
  “Madhumuni ya mradi ni mazuri hivyo mkoa kupitia wizara kuweka msukumo kwa kuhakikisha mradi unakamilika na kutelezwa kwani utachangia kuboresha huduma za afya katika maeneo ya kusini na kupunguzia wananchi mzigo wa gharama kwa kufuata hospitali zilizo mbali na mikoa yao,” alisema Bibi Mwanri ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Huduma za Jamii na Maendeleo ya Idadi ya Watu.
  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) eneo la afya ni kipaumbele cha nne cha mkakati kwa lengo la kuongeza maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi ambapo Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu hasa katika elimu ya juu na vyuo vya huduma za afya na uongezaji ubora na upatikanaji wa huduma hizo katika kujenga nguvu kazi itakayoleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
  Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  0 0

  DSC_0496

  Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai, akiendesha Ibada bya Misa maalum ya Shukrani kufuatia kifo cha Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma (100), aliyeaga dunia Ijumaa ya tarehe 17 January,2014 katika hospitali ya Mount Ukombozi na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 19 January, 2014 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
  DSC_0486
  Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikishiriki misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika mwishoni mwa Juma jijni Dar.
  DSC_0491DSC_0551
  Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai akimrithisha kiti alichopenda kukaa marehemu wakati wa ibada za Jumapili kanisani hapo mmoja wa watoto wa Mzee Arnold Nkhoma Bw. Amos Nkhoma.
  DSC_0554
  Baadhi ya wajukuu na vitukuu wa Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma, wakiwa kwenye misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika jijini Dar.
  DSC_0562
  Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikitoka kanisani mara baada ya misa maalum.
  DSC_0595
  Babu wakiwa na mmoja wa vitukuu wa Marehemu Mzee Arnold Nkhoma.
  DSC_0607
  Michael Nkhoma, ndiyo mtoto mkubwa wa marehemu, akiongea na mdogo wake Amos Nkhoma. Kulia ni Aidan Nkhoma.
  DSC_0626
  Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na baba yake mkubwa Michael Nkhoma,(kushoto) na Mzee Aidan Nkhoma.
  DSC_0608
  Mama na Mwana wakijichukua taswira.
  DSC_0642
  Familia ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma wakiwasha mishumaa kwenye kaburi la Mzee Arnold Nkhoma mara baada ya misa maalum ya shukrani iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
  DSC_0664
  Mmoja wa vitukuu wa Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma akiweka shada la maua kwenye kaburi la babu yake.
  Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.AMEN.
  DSC_0679
  Ndugu, jamaa na marafiki walipojumuika nyumbani kwa nyumbani kwa Profesa Alice Nkhoma Wamunza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya chakula cha mchana.
  DSC_0750
  Profesa Alice Nkhoma Wamunza, akiongoza ndugu, jamaa na marafiki kwenye chakula mchana baada ya misa ya shukrani ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma.
  Kwa picha zaidi ingiahapa

older | 1 | .... | 249 | 250 | (Page 251) | 252 | 253 | .... | 1896 | newer