Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

HALMSHAURI YA WILAYA IRINGA YAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO YATIMA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akipanda mti katika shule ya msingi Igula katika Tarafa ya ismani
 Wafanyakazi wa shirika la Restless Tanzania, Mwadawa na Amne wakitoa maelekezo kwa Mkurugenzi bg wa  Halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka juu ya shughuli za shirika hilo. 
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo Nyumbani kilichoko Ismani.


TATHMINI YA ARDHI YA BANDARI MPYA YA MBEGANI YAKAMILIKA

$
0
0
 Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Timu yaUkaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wawakilishi wa wanavijiji vya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani na Timu ya Uthamini wa Ardhi wa eneo la mradi. Waliokaa viti vya mbele ni viongozi wa Timu ya ukaguzi, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kulia) na Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia). Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
 Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) akizungumza katika mkutano huo.
 Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema (Kulia) akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Pande, Bw. Ubezi Kondo (Kulia aliyesimama) akizungumza wakati Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipopita kijijini hapo kujua hali ya zoezi la tathmini ya ardhi kwa ajili ya mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani. Kulia kwake ni Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri na Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Pande, Bw. Ubezi Kondo (Kushoto) akionesha eneo itakapokuwepo Bandari Mpya ya Mbegani. Wanaotazama ni Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia), Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema (Wapili Kulia) na Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia).
 Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia) akitoa maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani katika eneo itakapokuwepo bandari hiyo. Wanaomsilikiliza ni Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Picha na Saidi Mkabakuli
========  =========  ========
TATHMINI YA ARDHI YA BANDARI MPYA YA MBEGANI YAKAMILIKA
Na Saidi Mkabakuli
Tathmini iliyokuwa ikifanyika katika kutimiza ndoto ya kuwa na Bandari mpya ya Mbegani kufikia mwaka 2017 na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) imekamilika kwa takribani asilimia 90 ya eneo zima la mradi huo.  
Hayo yamedhihirishwa na Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja naTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo.
Mhandisi Mrema alisema kuwa mpaka sasa jumla ya kaya 1100 kutoka vitongoji vya Bisibisi, Mji Mpya, Mlingotini na Pande vimeshafanyiwa tathmini, ambapo makadirio ya awali yanaonesha jumla ya shilingi bilioni 23 zinatarajiwa kulipwa kupisha mradi.
“Mpaka sasa takribani asilimia 90 ya eneo la mradi ambalo ni sawa na hekta 2000 limeshakamilika, ambapo kwa mujibu wa mapendekezo ya tathmini tunatarajia malipo kufanyika kufikia mwezi Juni mwaka huu,” alisema Mhandisi Mrema.
Akizungumza katika mkutano huo, mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  alisema kuwa kuna haja ya kuhakikisha fidia kwa wanavijiji hao inalipwa kwa wakati ili kuondoa usumbufu wa kusubiri malipo ya kwa muda mrefu hali itakayochochea kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi.
“Nawaomba muhakikishe malipo yanafanywa kwa wakati ili kuwaondoshea usumbufu wananchi ili kulinda heshima ya Serikali na kuondosha kero ya kusubiri ya kusubiri kwa muda mrefu,” alisema Bibi Mwanri ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Huduma za Jamii na Maendeleo ya Idadi ya Watu.
Akijibu hoja ya ushirikishwaji wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Pande, Bw. Ubezi Kondo alisema kuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakishirikishwa katika kila hatua ya uthamini huo. Aliongeza kuwa hali hii imewaongezea hamasa ya kuupisha mradi huo ili kutimiza ndoto ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ya kujenga Bandari hiyo pamoja na ahadi aliyoitoa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1968.
“Kwa hakika tunaukubali mradi huu kwa mikono miwili ili kutimiza ndoto na ahadi za Rais Kikwete na ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1968 wakati akifungua Chuo cha Mbegani ambapo aliahidi kuwa atahakikisha kunajengwa Bandari ya kisasa Mbegani,” alisema Bw. Kondo.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara ambaye ni kiongozi mwenza wa ukaguzi huo, uwekezaji katika Bandari mpya ya Mbegani unatoa fursa za kimkakati katika kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16).
“Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) unaweka bayana kuwa uwekezaji wa Bandari ni mojawapo ya maeneo ya kipaumbele na kimkakati ambapo kukamilika kwa ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani Bagamoyo kunatarajiwa kupunguza msongamano wa meli katika bandari ya Dar es Salaam,” alisema Prof. Rutasitara.
Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

NYUMBA ZA JESHI LA POLISI ZILIZOPO CHUMBAGENI ZATEKETEA KWA MOTO TANGA

$
0
0


Jana mchana nyumba za Askari wa jeshi la polisi zilizopo eneo la chumbageni nyuma ya kituo cha polisi kikuu cha chumbani jijini Tanga zaungua moto.



Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh.Halima Dendegu akiwasili katika eneo la ajali.
Mh.Halima Dendegu akishuhudia ajali ya moto katika nyumba za polisi chumbageni,jijini Tanga hapo jana 
Wananchi wakishuhudia na kusaidia vikosi vya zimamoto katika uzimaji moto huo.
Baadhi ya vitu vilivyookolewa katika ajali ya moto. Picha kwa hisani ya Tanga kunani(TK)

WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA SIKU YA UTEPE MWEUPE TANZANIA MKOANI RUKWA

$
0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa katika zoezi la ukaguzi wa mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu na huduma za mama wajawazito na watoto wachanga katika maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe Tanzania yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa katika Tarafa ya Mtowisa. Dkt. Seif Rashid alimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambae awali alikubali kushiriki maadhimisho hayo ambapo amekabiliwa na majukumu mengine ya kitaifa. Kushoto kwa Dkt. Seif Rashid ni Mratibu wa Taifa wa Utepe mweupe Mama Rose Mlay. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni "WAJIBIKA MAMA AISHI"
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akihutubia katika maadhimisho hayo ambapo aliwapongeza wadau wote wanaopigania na kusaidia afya ya mama na watoto na kuahidi kutoa kipaombele katika bajeti kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto nchini. Aidha amezitaka Halmashauri nchini kutoa kipaombele kwa kuongeza bajeti zao katika kuhudumia afya ya mama wajawazito na watoto wachanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa salamu za Mkoa wa Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya katika Maadhimisho hayo ya kitaifa. Katika Salamu hizo alisema zipo changamoto nyingi  katika sekta ya afya zinazohitaji ufumbuzi wa haraka ikiwemo upungufu wa watoa huduma, vifaa tiba, dawa, magari ya kubebea wagonjwa, vituo vya kutolea huduma za afya na vingine kuwa mbali na maeneo ya wananchi kwa baadhi ya maeneo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akifafanua baadhi ya mambo katika sekta ya afya Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akikabidhi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid maoni na maombi ya wakazi wa Wilaya yake katika kuimarisha sekta ya afya katika Wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
Maadhimisho hayo yalitawaliwa na hali ya hewa ya mvua ambayo hata hivyo haikuathiri mwenendo mzima wa ratiba iliyopangwa, baadhi ya wananchi walilazimika kutumia miamvuli na wengine kuonyesha uzalendo mkubwa na kuamua kunyeshewa hadi kukamilisha maadhimisho hayo, hata hivyo mvua hiyo ilikatika karibu na kufikia mwishoni mwa maadhimisho hayo.
Bi Adrianne Strong ambae nae ni mdau wa afya ya mama wajawazito na watoto wachanga akitoa salam zake na kujitambulisha. Hivi karibuni Bi Adriane Stong kwa kushirikiana na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani walitoa msaada wa boti na life jacket kwa ajili ya kusaidia huduma za afya ya mama wajawazito na wagonjwa mwambao wa Ziwa Rukwa.
Balozi wa Utepe Mweupe Tanzania ambae pia ni mwanamuziki Sara Thomas akijumuika na wanawake wengine kuimba wimbo wa kuihimiza Serikali na wananchi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanaokoa maisha ya mama wajawazito na watoto wachanga.
Zoezi la uchangiaji wa damu salama lilikua likifanyika katika kila Wilaya za Mkoa wa Rukwa katika wiki ya maadhimisho hayo ya utepe mweupe ambapo chupa za damu zaidi ya alfu moja zilichangiwa na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

MISS TABORA 2012 ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO NA KUFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA

$
0
0
Mrembo Sarah Paul aliposhiriki furaha yake ya siku ya kuzaliwa na watoto wa kituo cha TZ 820 FPTC NG'AMBO STUDENT CENTER - Kilichopo Tabora.
Kila mmoja alipata nafasi ya kufurahia keki iliyoandaliwa maalumu kwa watoto hao.
Baadhi ya vitu alivyowaandalia watoto hao na kuvikabidhi kwenye shirika hilo.
Sarah Paul, mshindi wa shindano la urembo la Redds Miss Tabora 2012, ambaye pia mwaka jana alishiriki katika shindano hilo hadi kufikia fainali za Miss Tanzania.
****
Leo katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa amefanikiwa kuwatembelea watoto wanakusanywa na kanisa la FPCT NG'AMBO wanaopewa msaada na Shirika la Compassion International Tanzania na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hawa wanakusanywa kwa lengo la kuwatoa na kuwakomboa umaskini wa kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho na kuwawezesha waje wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na kujitegemea.

Pia huwalipia ada, huwauguza na kuwapeleka hosipitali wanapoumwa, huwafundisha ujasiriamali n.k Aliyasema  Suleiman H. Halletu mkurugenzi wa kituo kinachoitwa TZ 820 FPCT NG'AMBO STUDENT CENTER na kuongeza kuwa wana watoto 254 katika kituo chao.


Mrembo huyo akiongea na watoto
Richard, mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha SAUT (SAUT-TABORA) AMUCTA anayesomea Mahusiano ya Umma na Masoko akiongea na watoto.
Miss Pauline (Mshindi namba 3 wa chuo cha Utumishi wa Umma-Tabora) akiongea na watoto.
Sarah akikata keki na watoto.
Suleiman H. Halletu (Mkurugenzi wa kituo) akishukuru baada ya kupokea zawadi za mrembo Sarah kwaajili ya watoto.
Team nzima iliyomsindikiza mrembo katika hafla hiyo fupi. Kutoka kulia ni Marry, Richard, Miss Zennah (Miss Singida 2012/13), Miss Pauline, Miss Sarah (MissTabora2012), Miss Lilian (Mshindi No2 TPSC 2013), na Annah Henry (Afisa Ugani)

BREAKING NEWZZZZZ:Matokeo ya Awali yasiyo rasmi kutoka vituo mbalimbali uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga.

$
0
0
  
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wafuasi wa chama hicho usiku huu,kwenye Ofisi za CCM mkoa,huku wakisubiri matokeo rasmi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda wowote kuanzia sasa.
TOSA no.1 
CCM 98 ,Chadema 20, CHAUSTA 0
Ipamba no2. CCM 104, Chadema 10,CHAUSTA 0
Isakulilo CCM 83,Chadema 8,CHAUSTA 0

Kilindi A CCM 69 ,Chadema 23, CHAUSTA 0
Ofisi ya Kijiji(Kilindi) CCM 117, Chadema 53, CHAUSTA0
Zahanati  CCM 117,Chadema 67, CHAUSTA 1
Ifunda
Kivalali A CCM 99 Chadema 19 CHAUSTA 0
Kivalali B CCM 109 Chadema 14, CHAUSTA 1
Muwimbi CCM164, Chadema 22 CHAUSTA 0

Mahanzi CCM 130 Chadema 46 CHAUSTA 0
Ikungwe A CCM 131 Chadema 23 CHAUSTA 0
Ikungwe B CCM 216 Chadema 13 CHAUSTA 0
Magunga CCM 184 ,Chadema 4 CHAUSTA1
Wasa CCM 149,Chadema 15 CHAUSTA 0
Usengelidete CCM 260,Chadema 46,CHAUSTA O
 KAMANDA WA UVCC MKOA WA IRINGA  SALIM ASAS AKICHEZA  KWA SHANGWE  VIWANJA  VYA CCM MKOA KUSHEREKEA  USHINDO  WA  CCM KALENGA

Matokeo ya Awali yasiyo rasmi baadhi ya vituo  inaongoza kwa mbali.

AJIRA MPYA YA WAKUFUNZI WA VYUO VYA UALIMU NA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI ZA MAZOEZI MWAKA 2013/14

RIDHIWANI KIKWETE ADHAMIRIA KUWAKOMBOA WANA CHALINZE

$
0
0

Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Kwamsanja,wakati alipofika kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwaomba kura katika Uchaguzi huo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa Wanachalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang'ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 16,2014.


Mtandao wa Wanawake na Katiba Walipongeza Bunge la Katiba Kuonesha Usawa wa Jinsia

$
0
0
Na Thehabari.com

MTANDAO wa Wanawake na Katiba wenye mashirika zaidi ya 50 yanayotetea haki za wanawake katika Katiba mpya, umelipongeza mchakato na matokeo ya  uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Bunge Maalum la Katiba (Mwenyekiti na Makamu wake) ambao umezingatia usawa wa jinsia.

Kauli hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao kwa niaba ya Mtandao wa Wanawake na Katiba jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa licha ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Mwaka 2012 haikuanisha kuwa uchaguzi wa uongozi wa Bunge hili uzingatie usawa wa jinsia bunge hilo limeona umuhimu huo.

“…Tumetambua busara na hekima za wajumbe za kuonyesha nia ya kujenga msingi wa usawa wa jinsia katika uongozi na vyombo vya maamuzi nchini. Kwetu sisi, hili si suala la uwepo wa mwanamume na mwanamke katika uenyeketi  wa Bunge Maalumu tu, bali pia ni ukomavu wa kipekee wa wajumbe katika kuuona ukweli kuwa suala la kuimarisha sauti za wanawake na wanaume ni nyeti sana, haswa wakati wa ujenzi wa maridhiano muhimu kikatiba,” alisema Liundi.

Tunawapongeza waliochaguliwa ambao ni Mhe. Samweli Sitta (Mwenyekiti) na Mhe.  Samia Hassan Suluhu (Makamu Mwenyekiti) kwa kuaminiwa katika nyadhifa hizo muhimu.  Mtandao wa Wanawake na Katiba  unatambua uwezo wao katika utendaji na una matumaini makubwa kuwa pamoja na mengine mengi watakayoyasimamia, watatoa uongozi ulio imara na wenye weledi wakati wakiongoza Bunge hili katika kujadili na kupitisha misingi muhimu itakoyopelekea katika ujenzi wa usawa wa kijinsia nchini.

Alisema mtandao huo unategemea kuona usawa wa jinsia ndani ya Katiba mpya, ambao sio ule tu wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika  ngazi mbalimbali, lakini pia usawa ulio na nia ya kujenga misingi ya kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi walio wengi na haswa wanawake nchini.

“…Kwa mtazamo huu, tunatarajia kuwa busara za Wenyeviti hawa na washauri wao zitatumika pia kuzingatia usawa wa kijinsia  katika Kamati zitakozoundwa pamoja na kuwa kuzingatia ustadi na uzoefu wa wanakamati unahitajika. Nia kubwa ikiwa kuona wanawake kwa wanaume watatoa sauti zao kuhakikisha na kulinda, pamoja na mengine, uzingatiwaji wa usawa wa jjinsia katika vifungu vyote vya Katiba mpya.

Aidha alifafanua kuwa Mtandao wa Wanawake na Katiba, unawapongeza wajumbe wote wanawake kwa umoja wao, mshikamano na ushirikiano imara, ambao umeleta mafanikio makubwa katika michakato inayoendelea huko Dodoma kwenye Bunge Maalumu.
“…Huu ni mwanzo wenye kuonyesha mifano mizuri, na ambao tunapenda  kuuona ukiendelezwa na kusimamiwa imara wakati wote Bunge Maalumu litakapokuwa likifanya kazi yake ya kuchambua na kupitisha vifungu mbalimbali vya Katiba,” alimalizia Bi. Liundi.

Kamati ya PAC yakutana na Benki Kuu ya Tanzanzia (BoT)

$
0
0
Kamati ya PAC Leo (jana), imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.

Kamati imeamua kwamba;

1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya tegeta escrow.

2) TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.

Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.

PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.

PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.

Imetolewa na 

Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014

Wananchi Rukwa Waunga mkono Serikali Kutenga Bajeti Maalum Kukabiliana Vifo vya Uzazi

$
0
0
Daktari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, John William Gurisha akitoa takwimu za afya ya Uzazi Mkoani Rukwa katika maadhimisho hayo. Daktari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, John William Gurisha akitoa takwimu za afya ya Uzazi Mkoani Rukwa katika maadhimisho hayo.Washiriki anuai kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha za matukio. Washiriki anuai kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha za matukioBaadhi ya washiriki wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya Utepe Mweupe. Baadhi ya washiriki wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya Utepe MweupeMkurugenzi Mkazi wa Shirika la Evidence for Action Tanzania, Craig John Ferla, kupitia kampeni ya Mama Ye akichangia damu.Zaidi ya chupa 970 za damu zilipatikana katika maadhimisho ya wiki ya utepe mweupe. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Evidence for Action Tanzania, Craig John Ferla, kupitia kampeni ya Mama Ye akichangia damu.Zaidi ya chupa 970 za damu zilipatikana katika maadhimisho ya wiki ya utepe mweupe.

  ZAIDI ya wananchi 16,828 wa Mkoa wa Rukwa wamesaini ombi la haki (petition), wakiiomba Serikali kutenga bajeti mahususi ili kuviinua vituo vya afya nchini viweze kutoa huduma za dharura kwa za uzazi ikiwemo upasuaji, damu salama, vifaa vya kutosha na wafanyakazi wenye ujuzi. Taarifa hiyo imetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay jana mjini hapa mbele ya mgeni rasmi wa siku ya Utepe Mweupe ambaye ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda. 

 “Lengo ni kuhakikisha bajeti ya kutosha inatengwa na Serikali Kuu pamoja halmashauri ili kuhakikisha kuwa angalau asilimia 50 ya vituo vya afya nchini vinatoa huduma za dharura za uzazi,” alisema Mlay. Kwa Upande wake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika ujumbe wake ameziagiza mara moja halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya kutosha ili kuimarisha vituo vya afya viweze kutoa huduma za dharura za uzazi ikiwamo upasuaji lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

 Tamko hilo lipo katika hotuba ya Waziri Pinda iliyosomwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akimwakilisha Waziri Mkuu. Katika maelezo yake Waziri Pinda alisema vifo vya mama na mtoto baado ni changamoto nchini hivyo Serikali ina kila sababu ya kukabiliana na changamoto hiyo. 

 Aliongeza kuwepo kwa huduma hizo na watalaamu kwenye vituo vya afya na hospitali nchini, ni njia pekee itakayosaidia kupunguza vifo hivyo. “Kila mwaka karibu wanawake milioni sita hupoteza maisha ulimwenguni kote wakati wa kujifungua, asilimia 50 ya wanawake hawa wanatoka kusini mwa Jangwa la Sahara na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizo kwenye ukanda huu."

Boniface Makulilo azungumzia maisha katika jeshi la Marekani kwenye kipindi cha NJE-NDANI

$
0
0
Boniface Makulilo alipokuwa katika Jeshi la Maji la Marekani (Navy)
Mtanzania Boniface Makulilo ametumikia Jeshi la Maji (NAVY) hapa Marekani kwa miaka miwili na sasa ni mwanajeshi mstaafu (Veteran). Amezungumza na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kuhusu maisha yake ya jeshini na namna ambavyo watu toka nje ya nchi wanaweza kunufaika na mafao yaliyopo jeshini. Ameeleza mengi ya manufaa ambayo wengi hatuyajui kuhusu maisha katika jeshi hilo.
Karibu uungane nasi
NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

Viongozi wa Barclays Africa Group walivyotembelea nchini.

$
0
0
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Malawi nchini, Bi.  Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga wakati wa mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa Kundi la Barclays  Afrika (the Group),  wakitembelea nchini, jijini  Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Ofisa Mkuu Vihatarishi (Risk) wa Barclays Afrika, Anil Hinduja.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kulia) akisalimiana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi & Cotex, Lakshmi Narayan wakati wa  mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa Barclays  Afrika, wakitembelea jijini  Dar es Salaam. Katikati ni baadhi ya maofisa wa NBC, Daniel Kaila (wa pili kushoto) na Azza Ernest Mnzava.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Huduma  Rejareja za Kibenki wa NBC, Mussa Jallow  katika mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa  Barclays  Afrika, wakitembelea nchini.. Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr Hussein Kassim na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi & Cotex, Lakshmi Narayan.   
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu (kushoto) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika mkutano huo jijini Dar esd Salaam.
 Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC Tanzania, Maharage Chande (kulia), akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nyanza Mines, Mukesh Mamlani  wakati wa mkutano huo  jijini  Dar es Salaam.  Katikati ni baadhi ya maofisa wa NBC, Godfrey Nderingo (wa pili kushoto) na Cletus Shirima. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) akiwa na wageni wengine katika mkutano huo. Kundi la Barclays Afrika ‘the Group’, limetokana na kuunganishwa kwa Kundi la ABSA ya Afrika Kusini (ABSA Group Ltd) na sehemu kubwa ya shughuli za Benki ya Barclays barani Afrika hapo Juni 31, 2013. ABSA (sasa the Group) ikimiliki asilimia 55 ya hisa ndani ya NBC, serikali ya Tanzania asilimia 30  zinazobaki zikimilikiwa na mashirika ya fedha ya kimataifa.      

WAANDISHI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI KWENYE KURIPOTI BUNGE LA KATIBA

$
0
0
DSC_0641
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan akifungua warsha ya siku moja kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya nafasi ya watetezi wa Haki za Binadamu katika Katiba mpya.

.waambiwa waache kamari ya majongoo kuhusu serikali mbili ama tatu
.watetezi wa haki za binadamu, waandishi watoswa kwenye rasimu ya Katiba

Na Damas Makangale, Dodoma, MOblog
WAANDISHI na Wahariri wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kuweka mbele maslahi ya taifa wakati wa kuripoti Bunge maalum la katiba. MOblog inaripoti.

Akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya watetezi wa haki za binadamu na asasi za kirai katika katiba mpya jijini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa kuzingatia weledi wa fani yao na maadili ya uandishi.

“waandishi wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa kuweka mbele maslahi ya taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta suluhu, amani, mshikamano na utulivu,” amesema.
DSC_0650
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Ndg. Onesmo Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la wabunge wa katiba na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa haki za binadamu katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku moja uliofanyika mjini Dodoma.

Amesema waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao wanaweza kushauri na kushirikiana na serikali na mamlaka zingine kupatikana kwa katiba mpya yenye tunu za taifa, Sululu aliongeza kwa kuweka hoja zao kwa ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta mshikamano na ushirikiano wa kitaifa katika kudumisha amani na haki za binadamu nchini. Amesema kwamba kupitia bunge la katiba wanahabari ni kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi na kuelimisha umma jinsi sheria na haki za binadamu zinavyoweza kulinda na katiba ya nchi.
DSC_0627
Mwezeshaji, Mwandishi wa Habari, Mwanasheria, msomi na mjumbe wa Bunge la Katiba Ali Uki akizungumza kwenye warsha hiyo.

“waandishi kwa kutumia nafasi yao wanaweza kushauri kwa kurekebishwa baadhi ya sheria, vifungu ili kuweza kulinda haki za binadamu nchini kwa kupitia bunge maalum la katiba,” aliongeza. Alisisitiza Mhe Sululu kwamba bunge la katiba halijadili kuhusu ama serikali mbili au tatu kwa sababu kuna mambo mengi kwenye rasimu ya katiba yakujadiliwa.

“kwa jinsi mnavyoripoti kuhusu serikali mbili ama tatu ni kama mchezo wa kamari ya majongoo jamani katiba siyo muungano tu,” amesema. Kwa upande, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo olengurumwa amesema ingawaje kwenye rasimu ya katiba hawajatambua watetezi wa haki za binadamu bali wataendelea kushauriana na wajumbe kupata mwafaka wa jambo hilo.
DSC_0629
Meza kuu, Ndg. Onesmo Olengurumwa akiwa na Mgeni rasmi Samia Suluhu Hassani kwenye warsha hiyo.

“Rasimu ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama zilivyoanishwa kikatiba,” amesema

Olengurumwa aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia haijatambua wasaidizi wa kisheria wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa msaada mkubwa kisheria kwenye ngazi za vijijini. Amesema ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua mjadala wa katiba ili misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya utetezi wa haki za binadamu nchini.

Olengurumwa amesema waandishi wa habari kama vile watetezi wa haki za binadamu maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na katiba ya nchi ili kujenga mazingira mazuri ya haki za binadamu nchini. Hivi karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa Serikali tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika. Mjadala wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma.

wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten hivi karibuni.
DSC_0637
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Nyamsenda amesema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume hiyo, ambayo haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu rasimu ambayo haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya wananchi na maoni yao.


Takwimu za Tume
Akifafanua zaidi, Nyamsenda anasema takwimu zinazotajwa kwamba asilimia 61 ya Watanzania Bara wanataka Serikali tatu, asilimia 60 ya Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba si za kweli. “Tume ya Warioba imetoa takwimu kuwa, watu waliotoa maoni kwa jumla ni 333,537. Kati yao, waliogusia Muungano ni 77,000, kwa hiyo 256,537 hawakugusia Muungano,” anasema na kuongeza:
“Ukiwagawanya katika Bara utakuta ni watu wapatao 36,000 na Visiwani watu 38,000. Kati ya waliozungumzia muungano. Kwa Zanzibar watu 19,000 hawakugusia muundo na watu 10,400 ndiyo waligusia Muungano wa Mkataba.”
Anaendelea kufafanua: “Waliozungumzia Serikali mbili ni 6,460 sawa na asilimia 34. Kwa hiyo ni wachache kuliko waliozungumzia Serikali ya Mkataba ambao nao ni wachache kuliko wale ambao hawakugusia kabisa suala la muungano. Ni sawa na tone la maji katika bahari,” amesema.
DSC_0656
Benedict Ishabakaki, Afisa Usalama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu akishiriki mkutano huo.
Anaendelea kufafanua kuwa waliotoa maoni kuhusu Serikali ya Mkataba na Serikali tatu, ni wachache huku wengi wakiwa Bara.
“Kama jumla ya watu waliotoa maoni ya Katiba ni 333,537, huwezi ukachukua watu 16,000 waliotaka Serikali tatu ukawaziba wengi ambao hawakutaka,” anasema na kuongeza:
“Ukijumlisha watu wanaotaka Serikali moja na mbili ambao ni 16,475, utaona ni wengi kuliko wanaotaka Serikali tatu ambao ni 16,470.”
Anasema watu hao wakiwekwa katika kundi ambalo halikugusia kabisa muundo wa muungano, ni watu 287,537 sawa na asilimia 86.
DSC_0647
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya siku moja.

FAIDIKA: Kuchukua mikopo ya biashara bila elimu ya ujasiriamali ni hatari

$
0
0

 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate to Margaret Yohana, an entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days " NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam end of the week. Left is co-author and project coordinator, Dr Ellen Otaru Okoedion.
 An entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam end of the week, Helen Makuru (left) is congratulated by VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi shortly before receiving her certificate from FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore.
 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate to Famasa Disabled Group Chairperson, Lillian Kabaliki, who was part of entrepreneurs  who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Center is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi.
 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate to an entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days "NAWEZA, a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend, Fatuma Miringa. Center is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi.
 FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore (center) speaks to a group of entrepreneurs from marginalized groups and local Tanzanians from the streets, who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Left is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi and right is Andrew Okallo, Project designer. 
  Director for Small Industries and Small and Medium Enterprises (SMEs) at the Ministry of Industry and Trade, Consolata Ishebabi, speaks to a group of entrepreneurs from marginalized groups and local Tanzanians from the streets, who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Left is VIBINDO Society Chairman Graston Kikuwi and right Emanuel Mwakyusa co-author of the training manual and moderator. 
One of the entrepreneurs (fourth right) who attended a two days"NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend, being congratulated by the seminar moderators, organizers and sponsors.   

======  ======  ======

FAIDIKA: Kuchukua mikopo ya biashara bila elimu ya ujasiriamali ni hatari   
Na Mwandishi Wetu.

Wajasiriamali wakitanzania wameonywa dhidi ya tabia ya kuchukua mikopo bila kuwa na elimu sahihi ya kuziendesha biashara zao, lakini badala yake wanapaswa pia kupata elimu ya ujasiriamali kama wanahitaji kuziendeleza biashara zao.

Wataalam wameonya kuwa mikopo bila ya kuwa na ujuzi wa uendesheji biashara unaweza sababisha biashara kufanya vibaya, mtaji kufa kabisa na kupelekea mkopaji kubaki na madeni makubwa.

Akizungumza wakati wa warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na FAIDIKA kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupata mafunzo ya usimamizi wa biashara na fedha iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na wa kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi alisema biashara za kitanzania zinashindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa elimu ya usimamizi bora na uongozi wa biashara.

“Watanzania wengi wajasiriamali wanadhani kuwa na mtaji wa kutosha ni njia pekee ya kufanikiwa katika biashara. Hili ni wazo potofu. Wengi uchukua mikopo baada ya hapo biashara zao ushindwa kukua na wanajikuta katika madeni makubwa,” alisema.

Aliwaasa wajasiriamali kujenga utamaduni wa kutafuta mafunzo fasaha kabla ya kuwekeza sana katika biashara ambazo hawazifahamu kiundani.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore alisema ikiwa ni kama mchango wa kampuni yake kwenye ustawi wa jamii ya kitanzania, FAIDIKA imetanua wigo wa elimu ya ujasiriamali mpaka kwa jamii ya kitanzania isiyokuwa na uwezo, kupitia warsha ya mafunzo ya usimamizi wa biashara na uhamasishaji ijulikanayo kama ‘FAIDIKA FREE Financial Empowerment, ikiwa na kauli mbiu ya ‘NAWEZA’.

Warsha hiyo pia iliyoambatana na uzinduzi wa kitabu cha mafunzo kilichoandikwa na wataalam watatu wa mafunzo ya biashara, imeanzia jijini Dar es Salaam na itaendelea katika mikoa mingine.   

“Mpango huu umelenga katika kukuza na kutekeleza mbinu za ukuzaji uchumi kwa watu wa hali ya chini kama walemavu na watu waishio katika mazingira magumu kupitia mikopo midogo midogo na elimu ya ujasiriamali na itafanyika kama warsha ya siku mbili itakayojumuisha masuala yote ya jinsi gani ya kuanzisha, kuendesha biashara na pia jinsi ya kutumia teknolojia hususani ya simu za mokoni ili kuboresha biashara,” alisema.

Bi Moore alisema kuwa mwishoni mwa warsha, washiriki wataweza kutambua ni biashara ya aina gani wanataka kuifanya, kuandika mchanganuo wa biashara, kufanya mahesabu ya awali na kuweza kubadilisha maisha yao. 

"Haya ni majaribio ya awali ya elimu kwa umma na utafanyika katika mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha, ikilenga jumla ya washiriki 300 kutoka katika makundi matatu: Wanawake wa Tanzania asilimia 34, watu wenye ulemavu asilimia 32 na watu wa kawaida mitaani asilimia 34," alisema.

Kwa hatua nyingine, Ofisa mtendaji mkuu huyo wa FAIDIKA alidokeza kuwa, mbali na kuwakopesha waajiriwa kama ilivyokuwa desturi yao, taasisi yake ya fedha hivi karibuni itaanza kutoa mikopo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati, taasisi ndogo za fedha, kukopesha kwenye biashara, na itakuwa ikifanyakazi kwa ukaribu na watu wanaojituma, waaminifu na kujiamini kuwa wanaweza kama ilivyo kauli mbiu yao ya ‘NAWEZA’.

Bi Moore alibainisha kuwa wajasiriamali watakaopata mafunzo hayo pia wataingia katika shindano la uandishi wa mchanganuo wa biashara, ambapo mshindi atapokea zawadi ya pesa taslim itakayokuwa kama mtaji kwa mchanganuo huo wa biashara ulioshinda.

Kwa niaba ya washiriki wote wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kundi la wajasiriamali walemavu (FAMASA disabled group), Lillian Kabalika, aliipongeza FAIDIKA kwa kutambua umuhimu wa kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali bure.

“Tunatoa pongezi kwa wazo hili. Tunawaomba FAIDIKA wasiishie kuwapatia mafunzo watu wasiojiweza peke yake, lakini pia wawasaidia katika kuyafanyia kazi yale waliojifunza. Na pia nawaomba waendelee na elimu hii ili watu wengi walio na ulemavu watambue kuwa ulemavu si kushindwa na kila kitu na wanaweza kuondoka mitaani na kuacha kuomba omba na kuanza kujitegemea na hata kuweza kutengeneza ajira zaidi na kuwaajiri wale wasiokuwa na ajira,” alisema. 

NYUMBA INAPANGISHWA MBEZI BEACH BEI POA KABISA

$
0
0
DSC_0842
Nyumba yenye vyumba vitatu kikiwemo Master Bedroom inapangishwa Maeneo ya Mbezi Beach, Barabara ya Muafaka nyuma ya Art Gallery almaarufu kama Jogoo.
Nyumba hii inauzio pamoja na geti.
Kama utapenda kupangisha unaweza kupiga namba 0754-367995 , 0777-967995 na 0763-114544
DSC_0835
Huu ni monekano wa Sitting room.
DSC_0838
Na hapa ni Dinning room.

MATOKEO YA JUMLA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA:CCM YASHINDA KWA KISHINDO

$
0
0

Mgombea Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa  akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho jana usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko kwenye jimbo hilo la Kalenga. 
=======  =====  =======
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga Iringa vijijini yametangazwa rasmi jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha CCM kilipata jumla ya kura 22962,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5853 na chama cha CHAUSTA kilipata kura 150.Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia 79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo.

ZE KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA NA BUNGE LA KATIBA

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watumishi Bw. George D. Yambesi, katikati, akiendesha mkutano wa Baraza, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAB Mkwizu na kushoto ni Katibu Bi. Lilian Denis.
Sehemu yaWajumbe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba akitoa mchango wake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu Bw. Emmanuel Mlaya akitoa mchano wake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Utumishi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watumishi akisikiliza hoja wakati wa mkutano, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAb Mkwizu
Mmoja wa wajumbe Suleiman Mafele anayetarajia kustaafu, kulia, akimuaga Katibu wa Baraza la Watumishi wa Ofisi ya Rais , menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Lily Denis, katikati, kushoto ni Bw. Festus Mbwiro.

FILAMU YA KITENDAWILI KUTOKA PROIN PROMOTIONS IPO SOKONI SASA

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images