Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46338 articles
Browse latest View live

MATUKIO MBALIMBALI KUELEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO KUFANYIKA.

$
0
0
Msemaji wa Serikali  Bw. Assah Mwambene akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
========  ======  ==========
MATUKIO MBALIMBALI KUELEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO KUFANYIKA.

Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
14/3/2014, Dar es salaam.

SERIKALI imetoa wito kwa wananchi na vyombo vya habari kushiriki katika shughuli na matukio  mbalimbali ya  maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 ya Muungano  yanayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 26,April 2014,  siku ya maadhimisho ya sherehe hizo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam, Msemaji wa Serikali  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu ambayo ni ya kipekee yanaongozwa na kauli mbiu isemayo Utanzania wetu ni Muungano Wetu, Tuulinde, Tuuimarishe na Kuudumisha  yanaambatana na matukio mbalimbali yanayozihusisha wizara na taasisi mbalimbali za Muungano.

Amesema wizara na taasisi hizo zitashirikiana na vyombo vya habari kutoa  elimu kwa wananchi  kuhusu  mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi chote cha uhai wa Muungano ikiwemo umoja, amani na mshikamano. 

“Sisi tumeungana miaka 50 iliyopita,huu ni muungano pekee uliobaki Afrika wa kupigiwa mfano na unaoendelea kudumu haya ni mafanikio makubwa “ amesema.

Ameeleza kuwa katika  kipindi chote cha muungano watanzania wamebaki kuwa wamoja kwa kuhakikisha kuwa Muungano unalindwa , kuenziwa na kudumishwa  na kizazi cha sasa na vile vitakavyofuata na kuongeza kuwa mwananchi anawajibu wa kuyalinda mafanikio hayo.

“Watanzania  tuna kitu cha  kusherehekea kwa sababu  miaka 50 ya Muungano kwa sababu tumebaki kuwa wamoja. Tanzania ni nchi moja ni lazima wananchi waliohusika kuunda Muungano huu tuendelee kuwakumbuka na ni sehemu ya sherehe hii”

Aidha amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana  baadhi ya watu wamekuwa wakibeza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chote cha Muungano kwa kulaumu na hata kutumia vyombo vya habari kuharibu taswira ya mafanikio hayo jambo ambalo halina msingi wala ukweli wowote kutokana na matunda  yanayoonekana sasa ya kuwafanya watanzania kuendelea kuwa wamoja.

Ameeleza kuwa vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kuendelea kueleza mambo makubwa yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika ndani na nje ya nchi na kufafanua kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa wa masuala mbalimbali katika Nyanja ya ushirikiano.

Amesema Tanzania imekuwa na ushirikiano na mataifa mbalimbali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na nchi nyingine jambo linaloonyesha ukomavu wa Muungano na utayari wa ushirikiano wa Tanzania na mataifa mengine.

“Ukiangalia sisi tuna miundombinu ya reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA inayokwenda nchi ya Zambia hii yote, miradi hii ni mikubwa iliyojengwa kwa ushirikiano  hili tu linaonyesha kuwa sisi tuna uzoefu mkubwa katika masuala ya muungano hasa kufanya kazi kwa pamoja  katika masuala haya ya Muungano”

Amesema Tanzania inaendelea kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ya kiuchumi kwa kushirikiana na mataifa jirani ikiwemo mkataba wa ujenzi wa reli uliosainiwa hivi karibuni kati ya Tanzania na Burundi.

Kuhusu  wizara na taasisi za muungano zitakazoshirikiana na vyombo vya habari kutoa taarifa kwa umma kuhusu  masuala mbalimbali kuhusu taasisi na wizara husika kuanzia mwezi huu  amesema ni pamoja na Wizara ya Kazi na Utumishi wa Umma na Ofsi ya Makamu wa Rais Zanzibar, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tume ya uchaguzi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Nyingine ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar,Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu.

Wizara na Taasisi nyingine ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Katiba na Sheria, Taasisi za Wizara ya Fedha (Muungano) za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bodi ya Mikopo ya Nje, Benki Kuu ya Tanzania, Taasisi ya Kupambana na Fedha Haramu na Mamlaka ya Bima.

Aidha amesema kuwa kuelekea kilele cha sherehe hizo kutakuwa na fainali tamasha kubwa linalohusisha vikundi mbalimbali vya muziki na taarabu ambapo rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi atakuwa mgeni rasmi katika eneo la viwanja vya Mnazi mmoja pia kutakuwa na kongamano kuhusu Muungano wa Bara la Afrika ambalo litafanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu mstafu  Dkt. Salim Ahmed Salim. 

Matukio mengine ni pamoja  na fainali  za kongamano  la wazi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  litakalofanyika Zanzibar tarehe 19 mwezi huu,Hotuba na  zoezi la utoaji wa nishani litakalofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete na mkesha mkubwa wa miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam na viwanja vya Mwaisla, Zanzibar. 


RAIS KIKWETE KATIKA PICHA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA NDANI NA NJE YA NCHI IKULU LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongea kwa furaha na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe John Sitta, Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe Samia Suluhu Hassan Katibu wake Mhe yahaya Khamis Hamad  na naibu katibu Dkt Thomas Kashilia  na Mawaziri Mhe John Lukuwi na Mhe Aboud baada ya zoezi la kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum lililofanyika Ikulu ndogo mjini Dodoma leo Machi 14, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Wastaafu Mhe Olesegun Obasanjo wa Nigeria, Festus Mogae wa  Botswana, Mzee Benjamin William Mkapa, na (walioketi kulia kwa Rais) Mhe Pedro Pires Rais Mstaafu wa Cape Verde, Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Mhe Joachim Chisano wa Msumbiji na Rais wa Benki ya Afrika Dkt Donald Kaberuka. PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AWASILI KALENGA LEO,AMNADI MGOMBEA UBUNGE WA CCM KWA KISHINDO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba wakimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.

Kinana amewataka wakazi wa Kalenga kumpigia kura za kutosha na hatimae kuibuka mshindi kwa maendeleo ya jimbo hilo,hapo siku ya jumapili ambapo uchaguzi utanfanyika.Uchaguzi unafanyika ndani ya jimbo hilo kuziba nafasi ya aliyekuwaMbunge wajimbo hilo kwa tiketi ya  CCM,Marehemu William Mgimwa.
 Katibu Mkuu wa CCm,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Magulilwa mapema leo jioni wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama,alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge kupitia chama hicho,Ndugu Godfreya Mgimwa kwa wananchi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa akijinadi kwa wakazi wa kijiji cha Magulilwa,kata ya Magulilwa Iringa Vijijini wakati wa mkutano wa kampeni  za lala salama,amapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16,siku ya jumapili.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.
 Wananchi wa kijiji cha Magulilwa wakishangilia jambo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo katika kijiji cha Magulilwa,kata ya Magulilwa,Iringa Vijijini.

 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Magulilwa akisoma moja ya gazeti la kila siku wakati mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi,ukiendelea jioni ya leo.
Pichani Kulia ni  Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akifarijiana na Mbunge wa jimbo la Mwibara,Mh.Kangi Lugora mara baada ya MKutano wa kampeni kumalizika jioni ya leo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe akiagana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kumlaiza mkutano wa hadhara wa Kampeni,kwa ajili ya kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika jioni ya leo kwenye kijiji cha Magulilwa,Iringa vijijini,pichani kati ni Mbunge wa jimbo la Mwibala,Mh Kangi Lugora akisikiliza.

MISA YA SHUKRANI

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ALIVYOUNGURUMA JIMBONI KALENGA

RIDHIWANI AANZA HARAKATI ZA KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE

$
0
0
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Steven Kazidi (kushoto) akimuinua mkono juu kwa ishara ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo jana Machi 14,2014. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akinong'onezwa jambo na Mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Matipwili (Jina lake halikuweza fahamika mara moja).
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wanakijiji wakazi wa Kijiji cha Mkange,Saadani Wilayani Bagamoyo waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza huku wengi wakiahidi kumpa kura zao pindi itakapofika siku ya Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo.

PICHA ZA AJALI YA BASI LA JAPANESE WILAYANI MAKETE NJOMBE

$
0
0
 Basi la kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe likiwa limetumbukia mtoni mpakani mwa kata ya Lupalilo na tandala wilayani Makete mkoani Njombe, zaidi tazama picha zifuatazo hapa chini.
Katika ajali hii, abiria wameumia na kutibiwa katika hospitali ya Ikonda, hakuna abiria aliyefariki na kwa mujibu wa abiria waliokuwemo kwenye basi hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kukutana na gari jingine kwenye daraja hili jembamba hivyo katika harakati za kumpisha mwenzake ili wasigongane uso kwa uso, ndipo basi hili lilipopoteza uelekeo na kutumbukia mtoni. Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe kuja Makete mjini.

DROO YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YACHEZESHWA KIAINA YAKE JIJINI DAR.

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti ilyofanyika jana katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili aliyepatikana wiki  iliyopita, Deusdedit Kahwa akielezea furaha yake kwa wana habari katika droo ya tano ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo.
  Mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili Deusdedit Kahwa akibonyeza kitufe kuchezesha droo ya tano ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti.

TANZANIA HOSTS HIGH-LEVEL DIALOGUE ON ECONOMIC INTEGRATION

$
0
0
The former president of Tanzania, Benjamin Mkapa (L) speaking to media in Dar es Salaam after finishing the High-level Dialogue which was organised by The Mandela Institute for Development Studies (MINDS) based in Johannesburg. (R) is the founder and Executive Chairman of MINDS, Dr. Nkosana Moyo. Picture by Cathbert Kajuna.
---
The former president of Tanzania, Benjamin Mkapa yesterday (14th March 2014) hosted various African thought leaders from trade, industry, political, civil society, consultants plus six former heads of state in an informal dialogue that discussed the pace of economic development in the continent.

Speaking to media in Dar es Salaam Mr. Mkapa said the one day High-level Dialogue was organised by The Mandela Institute for Development Studies (MINDS) based in Johannesburg and sought to address ways in which to make interaction between different sector leaderships more efficacious for African Development within countries and across the continent.

“We fully appreciate the fact that economic integration is a major driver of the development process in our countrys. We discussed at length various factors that drive this process forward. This is a totally informal dialogue by people that are concerned and interested in the pace of integration in Africa from obstacles, how we can overcome them and achievements we seek to find,” said Mr Mkapa.

Among those who took part in the closed door dialogue included six former Head of State and Government, namely former Presidents Joachim Chissano of Mozambique, Thabo Mbeki of South Africa, Festus Mogae of Botswana, Olusegun Obasanjo of Nigeria, Pedro Pires of Cape Verde, and Benjamin Mkapa of Tanzania.

They were joined by the President of the African Development Bank, Dr. Donald Kaberuka plus forty other distinguished invitees - former civil servants, CEOs, academics and some civic society thought leaders from various regions of the continent.

According to the founder and Executive Chairman of MINDS, Dr. Nkosana Moyo, the institution is an ‘Pan-African Think Tank’ born out of the realisation that Africa’s development efforts have a tardy impact, and that the dialogues can help Africa take ownership.

“The MINDS think tank was set up with the aim of creating a space/ platform to give sector leaders an opportunity to meet amongst ourselves and discuss issues of relevance to the development of the continent to identify any obstacles that are present and try to work out possible solutions to those obstacles,” Dr. Moyo said.

“In terms of the people that are invited to the dialogues, we include politicians, civil servants, private sector, civil society, women and youth. These stakeholders are involved in identifying obstacles to Africa’s economic development, trying to formulate response to the same and lobbying those currently running the continent to try and getting those policies formulated which are responsive to implementation of possible solutions,” he elaborated.

“Some of the issues addressed just to name a few, was the philosophy of economic integration since the Lagos plan of action, how far has been achieved since then to now, is the spirit still there? What can be done to give more momentum? We also went into the concept of development corridors in Africa for instance Maputo, Mtwara corridor, north- south corridor e.t.c. What state are they in, is the implementation vigorous enough, to what can be done to step that forward,” explained former Tanzanian president Benjamin Mkapa.

MINDS received explicit endorsement by the late President Mandela as its founding in 2010. He said:- It is my hope that the Mandela Institute for Development Studies ( MINDS) will make a real difference in the resolution of the challenges that confront Africa through vibrant and robust debate, interrogating current paradigms and offering new approaches.

Ms Graca Machel, Mr Ali A. Mufuruki and Ms Sarah Mankaer serve on the Board of MINDS. It has an Advisory Board comprising Dr. Kaberuka, Dr. Ngozi Okonjo-Eweala, Mr Francis Daniel, and Mr Ayed Nouredinne.

DAKIKA 90 ZA DUNIA: Mfungwa aliyekuwa akisubiria KIFO aachiwa huru

$
0
0
Picha iliyopigwa na mwanasheria wake, ikimuonyesha Bwn Ford, siku ya kwanza kama mtu huru baada ya miaka 30 jela kwa kosa ambalo hakufanya. Photo Credits: theatlantic.com
Wiki hii, mmoja wa wafungwa nchini Marekani, ambaye alikuwa kwenye orodha ya wanaosubiri kunyongwa kutokana na kuhukumiwa kifo kwa mauaji  aliyotuhumiwa kufanya mwaka 1984 aliachiwa huru baada ya Jaji kukubali kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa ni yeye aliyeshiriki mauaji hayo.

Sasa, mfungwa huyu atalipwa dola 25,000 kwa kila mwaka aliotumikia kifungo hicho, lakini, kwa mujibu wa sheria ya Louisiana, kiwango cha juu anachoweza kulipwa ni dola 250,000,Ina maana, atalipwa kwa miaka 10 tu kati ya 30 aliyokaa gerezani
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Machi 15, 2014

Maisha Plus kurudi tena hewani TBC 1 leo!

$
0
0
Baada ya kusimamishwa kwa takriban wiki moja, vipindi vya Televisheni vya shindano la Maisha Plus, vinatarajiwa kurudi tena hewani leo saa tatu usiku, kupitia kituo cha televisheni kile kile, TBC1.


Akizungumza mapema asubuhi hii katika mkutano na wanahabari, Mratibu wa shindano hilo ambalo mwaka huu limepewa jina la Maisha Plus Rekebisha, Ally Masoud `Kipanya', amesema baada ya kukaa chini na uongozi wa televisheni hiyo, wamekubaliana kimsingi kutangaza ratiba itakayokuwa rasmi ambayo haitabadilika kama ilivyokuwa awali.

Kipanya amesema ratiba ya vipindi itaanza upya na ratiba itakuwa kwamba, siku za ijumaa na jumamosi, vipindi vitaoneshwa kuanzia saa tatu usiku lakini siku zote za wiki zilizobaki, kipindi kitakuwa kinaruka saa nne na dakika tano usiku.


Alisema vipindi hivyo vitaonyesha hatua za awali ambazo ni usaili na mpaka kupatikana kwa washiriki 30 waliobahatika kuingia kijijini.
“Tutaanza kuwaonyesha kipindi chetu kuanzia leo hii saa tatu usiku, kipindi kitaanza kwa kuonyesha hatua za mwanzo kabisa za mashindano haya,” alisema Kipanya.

Alifafanua akisema kuwa vipindi 10 vya mwanzo vitaonyesha mchakato mzima wa upatikanaji wa vijana 18 kutoka Tanzania watakao ungana na vijana wengine 12 kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi zitakazotoa washiriki watatu kwa kila nchi.

Usaili wa mwaka huu ulikuwa tofauti na miaka mingine ambapo orodha ya washiriki 40 ilitengenezwa na ikagawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza lilikwenda mkoani iringa kuishi kwenye vijiji vya huko na kushiriki shughuli za kijamii.

Kundi la Pili litaenda visiwani Zanzibar ambalo pia litashiriki utamaduni wa kila siku wa kimaisha wa visiwani humo ambapo ni washiriki tisa tu katika kila kundi watachukuliwa na watachujwa kutokana na jinsi walivyoyamudu maisha ya huko.

“Vijana wakiwa huko katika vijiji vya kweli watakuwa wakishiriki shughuli za kilimo, usafi, za kiafya na nyinginezo kabla hawajaingia katika kijiji cha Maisha Plus”, alifafanua Kipanya.


Baada ya kundi la kwanza na la pili kutoa washiriki tisa kila kundi, washiriki 18 watakuwa wameshapatikana, na sasa nchi za zikishapata washiriki wake 12, idadi ya washiriki 30 itaingia kijijini cha Maisha Plus katikati ya mwezi huu.

ANGALIA PICHA MTIBWA SUGAR WATOKA SARE YA BILA KUFUNGANA NA YANGA

$
0
0

Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Iliyoanza Leo Dhidi Ya  Yanga.
Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema 
Kikosi cha Timu ya  Yanga Kilichoanza Leo : Kutoka Kushoto Didier Kavumbangu, Haroub Canavaro,Khamis Kiiza,Oscar Joshua,Frank Domayo,Simon Msuva, Juma Abdul,Nizar Khalifan,Mbeleni Juma Kaseja. 









Ligi Kuu Tanzania Bara Imendelea Leo Ambapo Katiak uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kulikuwa na Mchezo Mkali Dhidi ya Wenyeji Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogogo Dhidi ya Mabingwa Watetezi  Yanga ya Dar es Salaam .


 Katika Mchezo Huo Hadi Dakika 90 za Mchezo Zinamalizika Matokeo Timu Hizo Zmetoka sare ya Bila Kufungana.Mchezo Ulikuwa Mkali na wakukamiana Pamoja na Hali ya Uwanja Kutokuwa nzuri kutoka na Mvua Zianzoendelea Kunyesha Mkoani Hapa.




Timu ya   Yanga walitengeneza Nafasi Nyingi za Kufunga lakini walishindwa Kuzitumia .Wachezaji Emanuel Okwi na Didie Kavumbangu walipata nafasi za kufunga katika dakika ya 80 na 88 lakini awalishindwa kufunga, Yanga walifanya Mabadiliko katika Dakika ya 65 Alitoka Nizar Khalifan  na Kuingia Said Dilunga,Dk78 Alitoka Khamis Kiiza na Kuingia  Husein Javu. 
Mtibwa Sugar Walipata Pigo katika Dakika ya 70 Ambapo Mshambuliaji Wao Abdalah Juma  Alionyeshwa Kadi Nyekundu kwa Kumchezea Rafu mbaya.






 Mashabiki wa Timu ya  Yanga waliojitokeza kwa Wingi katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani morogoro
Benchi la Timu ya Soka ya Mtibwa ya Morogoro  Lilkiongzwa na Kocha wa Timu Hiyo  Meky Mexime Wa Kwanza Kushoto..
Makocha wa  Yanga 
Mashabiki waliojitokeza kwa Wingi Katika Uwanja w Jamhuri Mkaoni Morogoro Leo Katika Mcheza Kati ya Yanga Dhidi ya Mtibwa Sugar 
Mshambuliaji wa Timu ya  Yanga Emanuel Okwi akitafuta Mbinu za Kufunga katika Lango la Timu ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro.
Moja ya Purukushani katika Lango la Timu ya  Yanga Katika Mchezo Uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro  
Mchezaji wa  Yanga Simon Msuva Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Timu ya Mtibwa Sugar Paul Ngalema 


KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA LEO

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama hicho,Ndugu Godfery Mgimwa,wakati wa mkutano wa kufunga kampeni katika jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mkoani Iringa.Uchaguzi wa jimbo la Kalenga unafanyika kesho siku ya jumapili,Machi 16,kuziba pengo la aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,Waziri wa Fedha na Uchumi,Marehemu Dk.William Mgimwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia Wananchi wakati wa kufunga Kampeni za Uchaguzi wa jimbo hilo jioni ya leo,katika kijiji cha Kidamali,kata ya Nzihi Iringa vijijini.
 Mkutano wa kufunga kampeni ukiendelea kwenye kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi jioni ya leo.
  Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Godfrey Mgimwa akimtambulisha mke wake,Bi.Robby Mgimwa kwa wananchi wa kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,ambako kumefanyika mkutano wa kumfunga kampeni jioni ya leo.



  Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa akiwa amebebwa juu juu na Wafuasi wa chama hicho,mara baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa kufunga kampeni za cha hicho,zilizofanyika katika kijiji cha Kidamali,Kata ya Nzihi,Iringa vijijini.
 Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe akihutubia mbele ya wananchi katika suala zima la kumuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM,Jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kidamali Kata ya Nzihi Iringa vijini. 
Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Bi Robi Mgimwa akiwa amepiga magoti mbele ya wananchi waliokuwa wamefika kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za chama hizo,akimuombea kura mumewe ili ashinde.
 Wakina dada wakifuatilia mkutano huo 
 Wadau nao walikuwepo.
  Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya lala salama ya CCM,jioni ya leo kwenye kijiji cha Kidamali,kata ya Nzihi Iringa Vijijini. 
 Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali kwenye mkutano huo wa kampeni.
 Wakazi wa kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi wakishangilia jambo.
 Niabu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akimnadi na kumwombea kura mgombea wa Ubunge wa CCM,jimbo la Kalenga,Ndugu Godfreya Mgimwa katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,katika mbio za kufunga mkutao wa Kampeni jioni ya leo
 Mke wa Mgombea,Bi Robby Mgimwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kushoto ni Katibu wa CCM mkoa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mhadhiri wa chuo cha Tumaini  na Mtangazaji wa Radio One na ITV,Godfrey Gondwe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Kidamali,Kata ya Nzihi,Iringa Vijijini jioni ya leo,kabla ya kuhutubia kufunga kampeni za chama hicho,kupisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo keshoi katika jimbo la Kalenga.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa wakiwapungia mikono wananchi jioni ya leo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho.

JUMUIYA YA FAWE YAFANYA MKUTANO MKUU WA NANE ZANZIBAR

$
0
0
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akizindua Tovuti (WEBSITE) ya Jumiya inayosaidia maendeleo ya Elimu kwa wanawake (FAWE) Zanzibar katika ukumbi wa Chuo  Kikuu cha Taifa  Zanzibar SUZA Mjini Zanzibar (kulia) Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Khadija Ali Mohamed.
 Baadhi ya wanachama wa Jumuiya inayosaidia maendeleo ya Elimu kwa wanawake (FAWE) wakitizama Tovuti yao mara baada ya kuzinduliwa na Mama Mwanamwema Shein.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdallah Mzee Abdallah akitoa shukurani kwa Jumuiya ya (FAWE) kwa kuwasaidia watoto wa kike kielumu (kushoto) Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Khadija Ali Mohamed.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akizungumza na wanachama na wananchi wa Jumuiya ya (FAWE) hawapo pichani katika Mkutano Mkuu wa 8 wa Jumuiya hiyo pamoja na kuzindua Tovuti yao katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Mjini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimkabidhi cheti Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Khadija Ali Mohamed wakiwa ni waanzilishi wa Jumuiya ya (FAWE) Zanzibar.
Afisa Miradi wa Jumuiya ya (FAWE) Bi. Arafa Yahya Saleh (wakatikati) akiwa na baadhi ya wanawake waliosaidiwa kielimu na Jumuiya ya hiyo. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA HARAKATI ZA KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE

$
0
0
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014, wakati akiwasili kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa wakazi wa Kijiji cha Miono,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano ya Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.
Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi (kulia) akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kabla ya kumpatia kipaza sauti ili aweze kuzungumza na wanakijiji wa Kimange.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BREAKING NEWWZZZZ:MBUNGE WA CHADEMA AKAMATWA NA JESHI LA POLSI IRINGA AKITUHUMIWA KUGAWA FEDHA KWA WANANCHI

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili,ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
 Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
 Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji 
Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.

MO aapishwa rasmi Bungeni

$
0
0
IMG_9709
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Singida mjini, Ndg. Mohammed Dewji ( wa pili kushoto) akiteta jambo na baadhi ya Wajumbe wenzake wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo wakati wa sherehe fupi za kuapishwa kwa wajumbe hao.
IMG_9729
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Singida mjini, Ndg. Mohammed Dewji akielekea kula kiapo cha kulitumikia Taifa Bunge la Katiba.
IMG_9731
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Mohammed Dewji akila kiapo mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Samwel Sitta mjini Dodoma.
IMG_9739
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Mohammed Dewji, akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Samwel Sitta mjini Dodoma.
IMG_9741
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Samwel Sitta , akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Mohammed Dewji.

RAIS KIKWETE AONANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA AFRIKA KUSINI MHE MAITE NKOANA-MISHAMBANE LEO IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
 :Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.PICHA NA IKULU

UPIGAJI KURA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA WAENDELEA KWA UTULIVU MKUBWA.

$
0
0
 Baadhi ya Wanakijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini mkoani Iringa wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kupiga kura kumchagua Mbunge wamtakae wa jimbo hilo la Kalenga.Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo unafanyika leo,ambapo vyama Vitatu;CCM,CHADEMA na CHAUSTA vikiwa vimesimamisha wagombea wake katika uchaguzi huo unaotokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,pia Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa.Aidha Wagombea wa Chadema Grace Tendega na wa CCM,Godfrey Mgimwa ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kuchuana na hatimaye mmoja wao kuibuka kinara kwa kupigiwa kura na Wananchi,huku mgombea wa CHAUSTA,Richard Minja akipewa nafasi ndogo kutokana na maandalizi hafifu ya ushiriki wake.
 Baadhi ya akina Mama waliojitokeza kupiga kura mapema leo asubuhi katika kijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini wakitazama majina yao kwenye ukuta tayari kwa kutumia haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi wamtakae kwa kupiga kura
 Mmoja wakazi wa kijiji cha Mangalali,kata ya Ulanda akiwa ndani ya chumba cha kupigia kura akisubiri kupiga kura mapema leo asubui.
Wakazi wa kijiji cha Mangalali,kata ya Ulanda jimbo la Kalenga,wakiwa nje ya chumba cha kupigia kura mapema leo asubuhi.Kwa ujumla katika kata kadhaa ambako Globu ya Jamii imepita kumekuwepo na utulivu mkubwa,wapiga kura wamejitokeza kadiri ya uwezo wao bila kubugudhiwa na hali ya namna yoyote,huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa likiwa limejipanga vyema kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika uchaguzi huo Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga.

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM TOKA KWA RAIS ZUMA WA AFRIKA KUSINI LEO IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone:255-22-2114512, 2116898

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

              P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 
TAARIFA KWA UMMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.


Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.


Mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mheshimiwa Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete. 


Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

16 Machi,2013 


Viewing all 46338 articles
Browse latest View live




Latest Images