Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 23 | 24 | (Page 25) | 26 | 27 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza(kulia)akimkabidhi Abella Tarimo, Meneja biashara wa Vodacom Tanzania zawadi ya ngao na cheti kwa kuwa mfanyakazi bora katika kuunganisha idara zote kwa wakati na utendaji kazi kiufanisi. Anaeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wateja Harrieth Lwakatare.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Masoko Vodacom Tanzania wakiwa wameshikilia hundi yao yenye thamani ya $ 5,000 mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Rene Meza (wa pili kulia)kwa kuibuka wafanyakazi bora kwa mwaka 2012/13.
  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza,akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo hayupo pichani akiongea nao wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria  leo  Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria  leo  Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini 
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi  Mhe Fakihi Jundu, Jaji January Msofe, Spika Anne Makinda, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Mathias Chikawe na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Mecky Sadik leo Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
   :Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mchungaji Christopher Mtikila leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Kushoto ni Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman
   Viongozi wa dini ya Kihindu wakielekea kwenye kipaza sauti ili kuomba dua leo Februari 6, 2013 wakati wa  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Viongozi wa dini za Kiislamu na Kiktristo pia walishiriki kwenye maadhimisho hayo.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama ya Rufaa leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wakuu wastaafu na viongozi wengine leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu  Rais wa Mawakili leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.Picha na IKULU.

  0 0   Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akitangaza washindi wa promosheni ya Amka millionea kwa mwenzi wa Februari ambapo wateja 40 wameamka mamilione, kulia ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde
   Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa promosheni ya Amka millionea mara baada ya kujaza fomu za uhakiki wa ushindi wa promosheni hiyo.
   Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akiwaelekeza washindi wa Amka millionea namna ya kujaza fomu zao uthibitisho wa ushindi mara baada ya kutangazwa washindi wa promosheni hiyo kwa mwenzi huu wa pili

  Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiwaelekeza washindi wa Amka millionea namna ya kujaza fomu zao uthibitisho wa ushindi mara baada ya kutangazwa washindi wa promosheni hiyo kwa mwenzi huu wa pili
  ===============  ============  ===============

  ·         Hawa ni washindi wa Amka Millionea wa tarehe 1 hadi 4 ya mwenzi wa February 2013
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washindi wa promosheni ya Amka millionea na kuwazawadia wateja wake mamilioni ya pesa taslimu.

  Akiwataja washindi hao wakati wa hafla fupi ya utambulisho iliyofanyika Airtel meneja uhusiano wa Airtel Jackson mmbanso  alisema “promosheni inaendelea hivyo bado waeja endleeeni kushiriki, jinsi ya kushiriki Tuma memdo SHINDA au MILIONEA kwenda namba 15595 .Kuna zaidi ya ,ilioni 150 zimebaki kwaajili ya wateja kujishindia hadi itakapofika mwisho wa promosheni  hii.

  Promosheni ya amkamilionea leo tunawatangaza washindi wa dar es salaam wa droo ya jana ambao ni Emmanuel Johnson Mndeme, Salima Mzee Hassan, Jamali Mohammed Kahema, Veronica Rogarian Mrema, EliHuruma Tamilwai Kihiyo, Dini Kaikai Saidi, Simon Revocatus Siyantemi, Nikatus Malimi Francis, Joseph James Nguruko, Neno Kamilifu Ntetema, Adnan Ayub Khan, Bearthas Byabato Nshekanabo, Salum Lenjima Mshindo, Florence Josephine Mwahali na Said Shabani Wamba.

  Wengine walioibuka washindi kutoka mikoani ni Novatus Lenard Majura kutoka mkoa wa Kagera, AbdulAbbas Hatibu Joshua, Frederick Nelson Shirima, Joseph Peter Bombo, Sapuro Lemkishoi Mollel, Gadi Paul Shami kutoka Arusha , wengine ni Zena Mohammed Kilongo na Juma Julius Milaji kutoka Tabora, Gervas Bryson Kaiba, Ester Samson Makubo, Dickson Msenda Kamla kutoka Mwanza, Joseph Raphael Malya, Nicodemus Bandaja Kisahan kutoka Kilimanjaro, Ramadhani Chande Mkwango na Fabian Kulwa Nkwabi kutoka Lindi, Christa Masudi Ng'uso kutoka Mtwara Zaituni Juma Luena kutoka Iringa, Yahya Issa Nasoro na Rajab Hassan Mapezi kutoka Tanga, Anna Steven Mtuka kutoka Rukwa, Dominic Gerald Ndimbo kutoka Ruvuma, Maria Leonsi Gilo kutoka Manyara, Jacob Filemon Kashililika kutoka Mbeya, Paulo Thomas Tungu Zina kutoka Shinyanga na mwisho ni Alex Emmanuel Mbugi kutoka Morogoro.

  Hii ni maalum kwaajili ya wateja wote wa Airtel nchi nzima hivyo tunawashauri wale wote ambao ni wateja wa Airtel au wanatamani kuijiunga na Airtel wahamie sasa ili wafurahie kuamka mamilionea


  0 0

  images

  Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

   Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kabisa kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.

  Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.
  Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.

  0 0
 • 02/06/13--13:45: VALENTINE CONTEST NAPOLI


 • 0 0


   Bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight) Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana walio chini ya miaka 25 uzito wa Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.

  IBF imeamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia kwa vijana baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,

  Mabondia wengi wa Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.

  Kama Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Dong King, Bob Arum na wengine wengi. Nafasi kama hii inaipa nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya kujitangaza kibiashara na utalii kwani dunia inaiona kuwa kati ya nchi zinazotoa mabingwa wa dunia.

  Kama Shauri atashinda taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu historia ya ngumi nchini kuweza kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya manne duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO na WBA.

  Shiriksiho la Ngumi la Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina makao yake makuu ya kuhudumia bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ndilo lililomtafutia Shauri nafasi aliyopata.

  IBF/Africa inawahamasisha Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao pamoja na makampuni mbalimbali bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia Shauri ufadhili wa kuweza kuligombea taji hili.

  Mungu mbariki bondia Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amen.

  Imetolewa na:

  UTAWALA

  Shiriklisho la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa)

  Dar-Es-Salaam, Tanzania

  0 0


  Pichani katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za wanawake wenye Mafanikio Tanzania bi. Sadaka Gandi akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na mchakato mzima wa tuzo hizo, kulia Raisi wa tuzo hizo bi. Irene Kiwia na kushoto ni bi. Esther Shayo mratibu.
  Pichani kulia ni Raisi wa tuzo hizo Irene Kiwia akielezea jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na tuzo hizo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013, zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.

  Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.

  "TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa si tu kibinafsi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na  michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufariji na kuridhisha sana.”


  Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi naTeknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.


  Bi SadakaGandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteuawa na wake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili watuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wamabadiliko katika jamii zao.


  Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "


  Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu yaMtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello – Kamishna waTume ya Hakiza Binadamu naUtawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga-Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi.Ludovicka Tarimo–Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlakaya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.


  Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwana Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, WatuwaMarekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.

  0 0

   Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki akisoma hotuba katika maadhimisho ya miaka 14 ya Kumbukumbu ya siku ya Muasisi wa Shirika Hayati Prof. Hubert Kairuki. Alisema kuwa Tangu Muasisi huyo amefariki Februari 6, 1999, shirika lao limejiwekea utaratibu wa kumuenzi kwa kutenda yale mambo muhimu aliyokuwa akiyathamini wakati wa uhai wake. 

  Hayati Prof. Hubert Kairuki alithamini jitihada za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kuongeza idadi ya rasilimali watu kwenye fani za udaktari na uuguzi katika sekta ya afya. Ni katika jitihada hizo ndiyo aliamua kutoa mchango wake kwa kuanzisha shule ya Wauguzi ya Mikocheni (Mikocheni School of Nursing) na baadae kuanzisha Chuo Kikuu cha Tiba.

  Aliongeza katika maadhimisho ya kumuenzi mwasisi huyo, shirika lao kwa mwaka 2013 wameamua kijikita katika mambo matatu; Kutoa elimu ya Afya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni. Pili, kutoa zawadi ya madawati yapatao 50 kwa shule hiyo ya msingi Mikocheni yenye thamani ya shilingi milioni 4,500,000/=. 

  Tatu, Shirika kupitia chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki limetayarisha mhadhara kwa jamii 'Public Lecture' ambayo itatolewa na mwananzuoni Mtaalam Bingwa katika Afya ya jamii Prof. Theonesta Mutabingwa ambapo umelenga kutoa somo la matibabu ya ugonjwa wa malaria kwa wanawake wajawazito.

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akipokea zawadi ya madawati kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuk.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph Mwenda akitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki mara baada ya kukabidhi zawadi hizo za madawati.
  Wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni wakiimba wimbo kuwakaribisha wageni.
   Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki (kushoto) akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.


   Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph Mwenda akiongea  machache katika halfa hiyo. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akitoa shukrani zake.
   Wanahabari nao hawakuwa nyuma kunasa tukio.
   Wanafunzi wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kwa madawati hayo.
  Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairukia akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugombana (kushoto) na

  0 0


  Turner, 73, has lived in the Zurich suburb of Kuesnacht since the mid-1990s and speaks fluent German.

  The local Zuerichsee-Zeitung newspaper claimed on its website the local council announced its decision to grant Turner citizenship in an official notice published in Friday's edition.

  The decision still demands formal approval from state and federal authorities.
  Turner told a local German newspaper: "I'm very happy in Switzerland and I feel at home here. I cannot imagine a better place to live."

  Her agent revealed to Zuerichsee-Zeitung that Turner wanted to "clarify her situation"."Tina Turner will therefore also give back her US citizenship," she was quoted as saying.

  Needless to say that Tina Turner's move has sparked rumors she is following in Gerard Depardieu's footsteps, who  renounced his French citizenship because of the country's high taxes. (Depardieu was promptly offered Russian citizenship by President Vladimir Putin).

  Forbes explains of Turner's move: "There's little to suggest taxes motivate the decision, and Swiss rates are high." The mayor of Tina's hometown in Brownsville, Tennessee, admitted he was shocked at the news.

  "Tina Turner - as she has gotten worldwide fame - has never forgotten her roots," Mayor Jo Matherne revealed to Fox. "We've been in recent contact with some of her people talking about some projects we have in Brownsville."

  "I think anytime a person, whether they're world-renowned or the most meek and mild, makes the decision to change their citizenship we need to step back and think what causes that decision," Matherne added.

  What do you think of Tina Turner's swap?

  0 0


  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akizindua rasmi gari ya Nissan Patrol aina ya Y62 leo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo wa gari hiyo mpya ambayo ni Four Wheel Drive yenye uwezo wa kubeba watu 8 na yenye nguvu ya 5.6L V8 injini yenye spidi ya 240 ni ya pekee duniani kuzinduliwa na Tanzania inakuwa ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na kati kuingia baada ya Congo DRC, Angola na Ghana. Bw. Mcintosh amesisitiza kwamba gari hii inaviburudisho pamoja na Tv katika hali ya kumsaidia dereva kwenye safari ndefu.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya CFAO Motors na wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Wayne Mcintosh (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.

  Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors Tharaia Ahmed (wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa.

  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akiendesha bahati nasibu ya kwenda kushuhudia fainali na Michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika inayofanyika nchini Afrika kusini kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo.

  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akitangaza washindi wawili watakaoenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya AFCON.


  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa shindano la bahati nasibu Group Manager wa DELFINA Bw. Sajjad Dharamsi atakayeenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya michuano ya AFCON 2013. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
  Bw. Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa pili wa Kampuni ya Wambi Lube Oil Distributor Bw. Omari Omari.
  Peer Educator wa CFAO Motors Maria Petro (kulia) akimpongeza Bw. Omari Omari kwa kushinda droo ya kwenda kutizama fainali za AFCON 2013 nchini Afrika Kusini iliyoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Nissan Patrol Y62. Katikati ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
  Afisa Mauzo wa CFAO Motors Magdalena Mpeku akitoa maelezo ya gari mpya aina ya Nissan Patrol Y62 kwa baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.

  Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akizungumza na mmoja wa wateja wakati wa uzinduzi wa gari aina ya Nissan Patrol Y62 makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar.

  Wageni waalikwa wakila na kunywa wakati wa hafla hiyo.
  Warembo waliokuwa wakikaribisha wageni wakipozi kwenye gari hiyo mpya aina ya Nissan Patrol Y62. 

  0 0
 • 02/07/13--03:37: mambo ya kpzzz....!


 • 0 0

  Michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa upande wa soka(AFCON 2013) inaelekea ukingoni. Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa michezo ya nusu fainali ambapo Nigeria walikuwa wanaumana na Mali na kisha Ghana wakavaana na Burkina Faso. 

   Katika mchezo wa kwanza Nigeria walifanikiwa kuingia katika fainali kwa kuichabanga vibaya timu ya Mali kwa jumla ya magoli 4-1 kabla ya baadae Ghana kutupwa nje ya mashindano ya mwaka huu kwa kuchapwa kwa mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya 1-1 katika dakika za kawaida na 30 za nyongeza. Jijini Dar-es-salaam, mashabiki wa soka wameendelea kufurahia michuano ya AFCON 2013 sehemu mbalimbali kupitia SuperSport Channels ambazo zinapatikana Live na pia katika High Definition(HD) kupitia DStv. Mojawapo ya sehemu hizo ni viota vya Samaki Samaki jijini Dar-es-salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha mauzo DStv wakiongozwa na Meneja Mauzo, Salum Salum(mwenye t-shirt ya Blue) walikuwepo tayari kabisa kufurahi pamoja na wateja na mashabiki wa soka na pia kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wateja na mashabiki hao.
  Ukimuuliza shabiki yeyote wa soka atakwambia kwamba soka ina raha yake unapotizama na marafiki. Lakini....soka ina raha ya kipekee unapoitazama kwenye kiwango cha High Definition(HD). Ni DStv pekee wanaokuwezesha kupata raha hiyo.
  Cartoonist wa siku nyingi,Fred Halla alikuwa na mengi ya kuuliza lakini pia kusifia na kufurahia michuano ya AFCON 2013 kupitia DStv.
  Soka, mijadala, kinywaji...AFCON 2013 ina mengi. Samaki Samaki-Mlimani City.
  Baada ya kazi, ni AFCON 2013 kupitia DStv pekee!
  Unapozungumzia michezo,unazungumzia SuperSport.Unapozungumzia SuperSport unazungumzia DStv.
  Meneja Mauzo wa DStv,Salum Salum, amenidokeza kwamba Jumapili ijayo(tarehe 10 Feb) siku ya Fainali ya AFCON 2013 patakuwa na shughuli maalumu ya kumaliza msimu wa AFCON 2013 katika viota vya Samaki Samaki na sehemu zinginezo. Mashabiki watashinda zawadi mbalimbali na watapata kujua mengi zaidi kuhusu DStv ambao ni wakongwe wa digitali. Usikose kutizama fainali ambayo itakuwa kati ya Nigeria(Super Eagles) na Burkina Faso.

  Ili kujua mengi zaidi yanayojiri kwenye luninga yako,Jiunge na ukurasa wa Facebook wa DStv Tanzania kwa kubonyeza hapa.

  0 0


  ·         Wateja kupata salio mara mbili kila anapotuma pesa kupitia Airtel Money
  ·         Ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi nzima

  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpaya ya Airtel Money ambapo wateja wakel watapata muda wa maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kwa kutuma  pesa na kupata wateja muda wa maongezi kulingana na ada ya makato pale wanapotoa pesa  kwa kupita huduma ya  Airtel money.

  Akizungumza kuhusu promosheni hiyo, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando alisema” Tumewawezesha wateja wetu kutumia huduma ya Airtel money na kufanya miamala mbalimbali ya pesa huku tukisogeza huduma za kifedha karibu na makazi na sehemu zao za  kazi , leo tunayofuraha kuwazawadia wateja  wetu waliojisajili nchini nzima muda wa maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kutuma pesa kupitia Airtel money na pia tunawapa muda wa maongezi kulingana na ada watakayotozwa kutoa pesa pale watakapo toa pesa kupitia Airtel money. Bonus hii ya muda wa maongezi itatumika  kupiga simu Airtel kwenda Airtel siku nzima , kwa siku nzima hadi saa sita usiku.”

  “Tunaendelea kuboresha huduma yetu ya Airtel money na kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha hasa katika maeneo yenye changamoto ya huduma za kibenki. kwa kupitia mtandao wetu mpana ulioenea zaidi tuna wawezesha watanzania nchni nzima hasa wa maeneo ya vijijini kupata huduma za fedha zilizo salama , nafuu na gharama nafuu kupitia Airtel Money.

  Promosheni hii ya pata muda wa maongezi itaondoa Kampeni ya  bure,  na kuanzia sasa wateja wa Airtel watazawadia muda wa maongezi kila wanapotuma na kupokea pesa kupitia huduma ya Airtel Money”. Aliongeza Mmbando.

  Airtel bado inaendelea kutoa huduma za mawasiliano za simu zenye ubora na gharama nafuu , kwa sasa wateja wa Airtel wa malipo ya Awali wanatuma ujumbe mfupi was ms kwa shilingi moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125na kupiga simu kwa senti 10 mara baada ya dakika mbili za mwanzo.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Mazingira, Seneta,Robert D. Hormats, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc Marekani, jana Feb 6, 2013.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo jana Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo leo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR 

  0 0


  Kampuni ya bia ya Serengeti imezidi kukonga nyoyo za wapenzi wa bia jijini Dar Es Salaam  kupitia kinywaji  chake cha Tusker Lite . Kinywaji hicho cha ukweli  kilizinduliwa  mwezi Novemba mwaka jana . Tusker Lite ina wanga kidogo  na ladha halisi  ya kuburudisha. Kwa mujibu wa matukio yanayoendelea  katika baa mbalimbali jijini,  wapenzi wa bia wamepata fursa ya kuzungumza na mabalozi wa kinywaji hicho na  kukiri  kuwa Tusker Lite ina ladha murua na kukubali kuwa Tusker Lite ni Lite ya ukweli .

  0 0    Baadhi ya watoto wa Kijiji cha Matumaini wakiangalia zawadi walizopelekewa leo Februari 7, 2013 na Mama Tunu Pinda wakati alipotembelea kijiji hicho

   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akiwa amembeba mtoto Consolatha kwenye shule ya awali ya Kijiji cha Matumaini kinacholea watoto yatima eneo la Kisasa, Dodoma leo mchana Februari 7, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, wilaya ya Dodoma Mjini, Bi. Fatuma Mwenda na (kushoto) ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo, Bi Salome Kiwaya. (Picha na Irene Bwire – OWM).
   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Sista Rosaria Gargiulo wa Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu alipowasili kwenye Kijiji cha Matumaini kinacholea watoto yatima eneo la Kisasa, Dodoma leo mchana Februari 7, 2013. Katikati ni Padre Vincent Boselli anayesimamia mradi wa kijiji hicho.
   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Cyprian (doto) mmojawapo wa mapacha wanaolelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013. Pacha mwingine (kulwa) Christian)  amebebwa na Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Dodoma, Bi Salome Kiwaya.  Kushoto ni Pd. Vincent Boselli akielezea jinsi watoto hao wenye miezi mitatu walivyofikishwa kituoni hapo wakitokea Morogoro.
    Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Elizabeth (mwenye miezi saba) anayelelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimwangalia mtoto wa kiume aliyezaliwa leo saa 11 alfajiri (Februari 7, 2013) na Bi. Fatma Mohammed kwenye kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini. Bi. Fatma ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nzuguni, alisema atamwita mtoto huyo Pinda kwa sababu mama Pinda amekuwa mtu wa kwanza kumjulia hali..

  Neema Ntandu (wa tatu kushoto) ambaye ni mmojawapo wa watoto watatu waliokuwepo wakati Kijiji cha Matumaini kikianzishwa mwaka 2002, akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Bikira Maria, Mama Tunu Pinda ambayo imetengenezwa na watoto wa kijiji hicho wakati Mama Pinda alipotembelea kijiji hicho leo mchana, Februari 7, 2013

  0 0  WABUNIFU ZAIDI YA KUMI KUONYESHA UBUNIFU WAO KATIKA JUKWAA MOJA.KUFANYIKA IJUMAA YA TAREHE 15/O2/2013, MBWENI RUINS.

  Onyesho kubwa la mavazi Afrika Mashariki na kati la Swahili Fashion Week, limepanga kufanya onyesho kubwa visiwani Zanzibar katika Hoteli ya Mbweni Ruins siku ya Ijumaa ya tarehe 15/02/2013 ambapo wabunifu nguli kutoka Tanzania bara na Visiwani wamethibitisha kwa shauku na hamu kubwa ya kuacha kumbukumbu  nzuri ndani ya usiku huo wa onyesho la mitindo katika visiwa hivyo vya marashi ya karafuu.

  Tukio hili la Swahili Fashion Week Zanzibar litawaleta kwa pamoja zaidi ya wabunifu kumi kutoka ndani ya nchi kuonyesha ubunifu na umahiri wao katika tasnia ya sanaa ya ubunifu na kuongeza kasi ya maendeleo ya tasnia ya mitindo nchini Tanzania huku ikitangaza dhana nzima ya kujali vitu vinavyotengenezwa Afrika (Promote Made in Africa Concept)

  “Maandalizi yameshika kasi, tuko tayari kupeleka ladha ya Swahili Fashion Week katika visiwa vya Zanzibar, Kama inavyofahamika kwamba watu wengi watakuwa visiwani humo kufuatilia Sauti za Busara, huu ni mwezi wa burudani na vitu vizuri kwa watu wote Zanzibar, timu ya Swahili Fashion Week inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba inatibu kiu ya wapenzi wote wa Swahili Fashion Week na wadau wa maswala ya Ubunifu na Mitindo Zanzibar” Alisema Mustafa Hassanali muanzilishi na muandaaji wa Swahili Fashion Week.

  “Kupeleka Swahili Fashion Week kwa mashabiki waliopo visiwani Zanzibar, ni kuendeleza utamaduni wetu wa kuwa tukio bora la burudani na biashara katika tasnia ya mitindo, tukio hili la Zanzibar litawashirikisha wabunifu nguli toka bara na visiwani kuonyesha ubunifu na ladha tofauti za kiutamaduni, na wapenzi wa ubunifu na mitindo kupata ladha kutoka kwa wabunifu wa ndani ikiwa ni kama sehemu ya kuongeza familia yetu ya mitindo na ushirikiano baina ya wabunifu wa bara na visiwani” Aliongezea Hassanali

  Baadhi ya wabunifu watakaoshiriki ni Asia Idarous (Mshindi wa tuzo ya Humanitarian katika tuzo za SFW 2012), Dominick Godfrey, Subira Wahure, Ailinda Sawe, (Mshindi wa tuzo ya Origin Africa, SFW 2012), Martin Kadinda (Mbunifu Bora wa Nguo za Kiume, SFW 2012), Sarah Masenga (Mbunifu Bora Chipukizi, SFW 2011), Gabriel Mollel (Mbunifu Bora wa Mwaka na Mbunifu Mvumbuzi wa mwaka, SFW 2012), Subira Wahure, Jamila Vera Swai, Salim Ali, Ahmed Abdul pamoja na mshindi wa tuzo ya Mbunifu Anaechipukia wa SFW 2012, Lucky Creation.   

  “Swahili Fashion Week Zanzibar ni onyesho rasmi na la kwanza kufanyika visiwani humo, Swahili Fashion Week ilishafanya onyesho la mitindo mkoani Arusha mwaka 2011 na mipango ni kufanya maonyesho mbalimbali katika miji mikubwa hapa Tanzania” Alimalizia Meneja Uhusiano wa Swahili Fashion Week, Hassan Mrope.

  Onyesho limepangwa kuanza mapema ambapo kuanzia saa moja usiku milango itakuwa wazi. Tiketi za onyesho hili zinapatikana katika Hoteli ya Mbweni Ruins na Hotspot Bistro. Onyesho hili la Swahili Fashion Week Visiwani Zanzibar limedhaminiwa na Mbweni Ruins, ZG Tours, Daja Salon & Spa, Vayle Springs Clouds TV, Coconut Fm na 361 Degrees.

  Swahili Fashion Week mpaka sasa ndio ni tukio kubwa la mitindo Afrika ya Mashariki na Kati. Ni mwaka wa sita sasa, Swahili Fashion Week ni jukwaa la wabunifu wa mitindo na vito vya urembo kutoka nchini zinazoongea Kiswahili na Bara la Afrika kwa ujumla kuonyesha vipaji vyao, kutangaza ubunifu wao na kutengeneza mtandao na wadau duniani. Dhamira kubwa ni kuweka mkazo katika ukanda huu kwamba ubunifu ni tasnia inayotengeza vyanzo vya mapato huku ikitangaza bidhaa zinazotengenezwa Afrika “Promoting Made in Africa concept”.

  0 0  0 0  0 0


  Sauti za Busara inaleta watu pamoja, licha ya kwamba  kuna tamaduni tofauti, siasa na dini, lakini kupitia muziki unaondosha mipaka iliyopo.


  Mkurugenzi wa Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud amesema kwamba muziki ndio njia pekee ya kujenga au kuleta amani. “Nafikiri umoja kwa Waafrika ni lazima, na kujenga umoja kwa Afrika ni kitu cha lazima, lakini ni rahisi katika kiwango cha mtu na mtu, kuliko katika tasnia ya siasa”. Alisema Mahmoud. Aidha Bwana Mahmoud anaamini kwamba hali hiyo imepelekea kusaidia Busara Promotion kuandaa ratiba ya  kuonesha filamu ambazo zitafikisha ujumbe wa umoja na mshikamano kwa Waafrika  kwa sauti na kueleweka. 

  “Kwa kuwaleta watu pamoja kusheherekea katika tukio linaloheshimu mchanganyiko wa tamaduni na uhuru kwa kujieleza, lakini pia Sauti za Busara inasaidia kuleta demokrasia na uwazi,.kwa lengo la kuinua  jamii. Naamini kwamba tamasha la Suti za Busara lina jukumu la kulinda au kuendeleza amani na umoja Zanzibar, kukuza uelewa wa muingiliano wa tamaduni na kuuheshimu”. Alisema Mahmoud.

  Mwaka huu tamasha la Sauti za Busara linaleta watu pamoja kwa muda wa siku tatu katika kufurahia filamu ndefu zinazohusiana na muziki wa Afrika. Filamu hizo ni ‘Omar Sosa's Souvenirs from  Africa’, ‘Benda Bilili!’, and ‘United States of Africa: Beyond Hip Hop’. Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions  Bi. Rebecca Corey amesema filamu zote tatu zinatoa nafasi nyingine  kwa watazamaji kuona thamani ya utajiri na mchanganyiko wa muziki wa Afrika, na kuchangia kuwapo kwa mabadiliko chanya katika jamii ambayo ni urithi katika muziki. 

  “ Filamu tatu za mafunzo zilizochaguliwa mwaka huu zinahusu aina  tofauti za muziki, ikiwemo Jazz,  Rumba ya Congo na Hip hop, lakini zote kwa pamoja zina maudhui yanayofanana.  Ambapo ujumbe katika muziki  unaodosha mipaka, unajenga amani na mazungumzo, na unasisitiza utu wa mtu”. Alisema Corey.

  Nae Mkurugenzi wa tamasha Ndugu Mahmoud, amesema kwamba wamekuwa wakifanyakazi kwa upana na kuangalia mahitaji ya watu, huku wakiendeleza muziki, pia kuheshimu dini na tamaduni. Amesema atahakikisha kwamba muziki haupigwi wakati wa sala, na wasanii wote wamesaini mikataba ambayo inawataka kuvaa vivazi vya heshima na kutokwenda kinyume na maadili ya wazanzibar. Kwa upande mwingine alipatwa na mshangao anapofikiri hali aliyoiona nchini Mali,  kumekuwa na kutoheshimu wanamuziki kwa muda mrefu. Mahmoud amesema anajisikia vibaya kuona msanii kama Khaira Arby, ambae atafanya onesho katika tamasha la mwaka huu akiwa anasumbuliwa na kutothaminiwa nchuni mwake.

  Mahmoud amesema Busara Promotions imekuwa akikumbana na changamoto katika masuala ya udhibiti, kutokana na baadhi ya viongozi wa siasa wakiwa hawafurahii baadhi ya maonesho ya wasanii kama Comrade Fasto kutoka Zimbabwe na Didier Awadi kutoka Senegal. Wasanii hawa wamekuwa wakizungumzia masuala ya rushwa katika siasa na kutokuwepo kwa haki. Sauti za Burasa maana yake  Sound of Wisdom, kwa hiyo tunaona ni jukumu letu kuandaa jukwaa kwa wasanii kama hawa ambao wanatoa ujumbe muhimu  unaogusa na kuingia katika mioyo ya watu, na ni tofauti na siasa.  

  Pata taarifa zaidi za tamasha kwenye www.busaramusic.org. Sauti za Busara zitafanyika mji mkongwe wa Zanziba kuanzia tarehe 14 mpaka tarehe 17 mwezi wa Februari 2013.


  *Shukrani za pekee kwa wadhamini wa  Sauti za Busara ambao ni: Norwegian Embassy, Hivos, Goethe Institut, Grand Malt, Embassy of the United States, Precision Air, Memories, Zanzibar Unique, Diamond Trust Bank, ChemiCotex, Azam Marine, Embassy of France and more


older | 1 | .... | 23 | 24 | (Page 25) | 26 | 27 | .... | 1897 | newer